Riwaya magnum22

Riwaya magnum22

Leo weekend natamani tuende na dozi mchana na jion bando langu linaexpire mchana kama atakae guswa ni nunulie 0758844240
 
MAGNUM 22

Sehemu 19


FREETOWN
ALFAJIRI YA SAA kumi na moja, Kamanda Amata aliwasili katika jiji la Freetown, alifurahia zaidi kufika muda huu kwa sababu maalum, kwanza alikuwa na uhakika kuwa hakuna mtu mbaya anayemuona na pia alijua wazi kuwa kama mambo yatakwenda vizuri basi siku hiyohiyo angeweza kufika anakokutaka. Katika kijitabu cha kumbukumbu alichpewa na marehemu Inocent kule katika kaburi la halaiki kulikuwa na ramani ya kufika mpaka katika jumba linalokusudiwa kuwa Martin Guter na timu yake hujificha kila baada ya uhalifu.
Nje ya uwanja huo akachukua gari la kukodi na kumtaka dereva kumfikisha katika hoteli ile ile aliyofikia mwanzo, hoteli ya Swizz Spirit. Katika meza ya mapokezi akapokelewa bila tatizo lolote na kupatiwa chumba anachostahili. Ndani ya chumba chake hicho, Amata alijikuta anashikwa na hasira ghafla akiwa ndani ya chumba hicho, akamkumbuka mwanamke ambaye alimhadaa kimapenzi na kumtumbukiza kwenye hatari kubwa.
“Naanza na yeye!” akajisemea huku akiuweka mkanda wa suruali yake kitandani nay eye kuingia maliwato. Baada ya kuoga na kujipulizia manukato akajitupa kitandani japo apate usingizi wa saa mbili au tatu hivi.
* * *
Majira ya saa nne asubuhi, Amata akatoka ndani ya hoteli hiyo akapita mlango wa nyuma na kujikuta kwenye maegesho ya magari, hapo akachukua taksi na kuelekea nyumbani kwa yule mwanamke. Hakuwa amesahau njia, alimwongoza yule dereva mpaka mbele kabisa ya ile nyumba. Nyumba hii ndogo lakini ya kisasa ilikuwa imejitenga na nyingine, ilikuwa imezungukwa na maua mengi na miti kadhaa ya kuifanya iwe kivulini. Akamlipa dereva taksi na kumtazama akiondoka kutoka katika uwanja wa nyumba hiyo, kisha akaigeukia na kuutazama mlango mkubwa. Nje ya nyumba hiyo kulikuwa na gari moja la kisasa sana, Aston Martin.
Bila shaka kuna kibopa anayejifaidia! Akawaza na kujiweka tayari kuikabili nyumba hiyo, akazikwea ngazi na kuufikia mlango, akachukua funguo yake na kuipachika tunduni, hakupata shida; mzunguko wa kwanza, wa pili, kitasa kimeachia, akajitoma ndani. Sebule ileile ikamkaribisha, akatazama mandhari yake, haikuwa imebadilishwa, jicho lake likaugonga mlango wa chumbani. Akauendea na kuuskuma taratibu, naam, hakukosea, aliyemtaka alikuwa kajilaza kitandani kama embe dodo, akiwa hana hata kipande cha nguo maungoni mwake. Maji yaliyokuwa yakitiririka yalisikika kutoka mlango wa bafuni. Akapiga hatua nyingine kadhaa na kukifikia kitanda hicho huku tayari mkononi bastola ‘Berreta’ ikiwa tayari.
“Nimekupata!” akasema, na kumfanya mwanamke yule kushtuka, Amata akazunguka kitanda mpa upande wa miguu na kusimama akimtazama mwanamke huyo akijikusanya na kujisitiri kwa shuka.
“You have died!!!” akapiga kelele akimaanisha kuwa mtu huyo alishakufa.
“Yes! I have died and now, I have risen!!!” Amata akamwambia. Akiwa katika hali hiyo hisia zake zikampa taarifa kuwa mlango wa bafuni unafunguliwa, akageuka haraka na kutazama.
“Tulia! Njoo uungane na mkeo hapa!” akamwambia kwa Kifaransa safi kisichoghoshiwa.
“Lakini si-si-na hatia…” akajitetea mwanamke huyo mwenye asili ya kihindi. Kwa macho ya haraka haraka, alionekana wazi kuwa na umri mdogo kuliko hata mwanamke aliyelala naye.
“Ndiyo, hauna hatia, ila tu hujui kuwa umelala na jambazi, ambalo linalaghai wanaume na kisha kuita watu wake wakuue…” Amata akasema. Yule kijana akamtazama mwanamke wake na kumtolea macho.
“Unaona hajibu? Anajua kazi yake…”
“Mimi si jambaziiiii!!!!” yule mwanamke akasema kwa sauti.
“Kimya!” Amata akamkemea huku akiwa kakunja sura isiyo na chembe ya huruma, “Nataka unipeleke mguu kwa mguu kwa wale majambazi wako,” akamwambia.
“Sipajui wanapoishi na wala siwajui watu wale….” Kajibu huku akibubujikwa na mchozi.
“Hupajui kivipi? Wakati wewe ndiwe uliyewaita waniue, ulifikiri huwa nakufa kirahisi? Basi sikufa na sasa nimekuja kwa ajili yenu washenzi nyinyi!”
“Mimi siwajui….”
“Haya nambie ilikuwaje wakanikuta hapa kama si mbinu zako….” Amata akamtaka mwanamke huyo kumpa habari yote. Yule mwanamke akaeleza kila kitu kuanzia A mpaka Z.
“Kwa hiyo ulinisaliti kama Yuda alivyomsaliti Yesu, ukaniwekea na ua waridi kitandani, ukinidanganya kuwa wekundu wa ua lile ni rangi ya upendo kumbe ni damu itakayomwagika, dah!”
“Sammaahhaanni sana!” yule mwanamke akaomba msamaha na kushuka kitandani akiwa uchi, akapiga magoti na kuishika miguu ya Amata akilia. Kamanda si kwamba alikuwa akisikiliza sauti hiyo ya kuomba msamaha bali umbo malidhawa la mwanamke huyo, lenye utamu wa kila namna na wenye kumpendeza kila mwanaume rijali, mwii ambao haujakobolewa, upon a uasili wake wa kutoka tumboni mwa mamaye. Akajikuta anameza mate hata kama hakutaka.
“Sasa, mguu huu mimi na wewe mpaka walipo, kwa kuwa wewe ulishuhudia kifo changu sasa nataka ukashuhudie vifo vyao…” Amata akamwambia huku akiiweka bastola yake kiunoni.
“Nipo tayari,” akaitikia mwanamke yule kisha akasimama na kuliendea kabati, akachukua suruali yake ya jinzi la kuvutika na kujitwalia, fulana kisha raba nyepesi, akachukua na kiburungutu cha pesa, akakisunda kwenye sidiria. Dakika kumi, akawa tayari kwa safari hiyo ambayo hata hakuijua ni wapi anapelekwa.
“Hey!” akamshtua yule kijana, akamtazama, “Lete funguo ya gari, ukae hapa ole wako uondoke na ole wako umwambie mtu kuhusu haya… nikukute hapa baada ya saa kadhaa, lala jifunike, mkeo atarudi uendelee kumndondomola,” akamliza kusema na kijana huyo akaiendea suruali yake na kuto funguo, akampatia Amata pasi na kunena lolote.
Amata na yule mwanamke wakaingia garini, hakika lilikuwa gari la kisasa sana, tangu aanze kuendesha magari hakuwahi kukaa kwenye gari la starehe kama hili, zaidi ni kuliona kwenye filamu za 007.
* * *
Hali ya hewa ilikuwa baridi na mvua za hapa na pale zikiendelea kunyesha, Kamandal Almata aliendelea kuendesha gari lile kwa kasi huku akiwa anaambaa sambamba na Mto Lofa. Simu yake iliyokuwa akimwongoza kwa kutumia mfumo wa GPS. Akaambaaambaa na barabara hiyo na kuanza kupanda milima mikali.
‘SILENT ROCK VILLA’ maandishi katika kibao yakamkaribisha, kichwani mwake akalikumbuka jina hilo kutoka kwenye kijitabu cha kumbukumbu cha Innocent ila kwa wakati ule hakuyaelewa kutokana na kwamba hayakuwa pamoja n ale ramani.
“Sasa huku tunaenda wapi?” akauliza abiria wake.
“We tulia si nimekwambia utashuhudia rafiki zako wanavyokufa!”
“Mh!” akaguna wakati Amata akiegesha gari juu kabisa ya kilima cha piali ambapo aliiona ile nyumba vizuri kabisa. Akatazama saa yake, saa saba mchana, akashuka na kusimama nje, baridi ilikuwa kali na yule mwanamke akamfuata na kusimama kando.
“Tunatakiwa twende pale,” akamwambia yule mwanamke ambaye mpaka dakika hii hakumjua jina lake.

Nimewahi sana! Muda mzuri ni jioni, no! sasa hivi…! Akajisemea moyoni na kuchukua kama sekunde kumi au kumi natano hivi kushirikisha mwili wake.
Naenda! Akakamilisha maamuzi na kuingia garini na yule mwanmke naye akaingia, Amata akawasha gari na kuigeuza, akaanza kuteremka mlima ule alioupanda mwanzo.
“Uwe tayari ni wakati wa mapigano makali, ama wao washinde au sisi tushinde,” akamwambia huku akibadilisha gia na kuteremka kwa kasi. Haikuwachukua muda mrefu, wakawa karibu sana na jumba lile, Amata akapinda kulia na kuingiza gari vichakani akalizima.
“Vipi, Mbona porini?” akaulizwa.
“Ndiyo tunaegesha gari hapa kisha tunakwenda ndani ya hilo jumba, au we unabaki?” Amata akamjibu.
“Nani abaki! We si umesema unataka nishuhudie hao jamaa wanavyokufa, twende wote,” yule mwanamke akajibu wakati Amata akikata baadhi ya matawi ya miti na kulundika kulificha lile gari. Dakika kumi na tano baadae, tayari akafanikiwa kulifanya lisionekane. Yeye na huyo mwanamke wakaanza kutembea taratibu kupita pori kwa poori kulielekea jumba hilo. Baada ya hatua chache wakakutana na ukuta mkubwa kama wa gereza, akautazama kuanzia juu mpaka chini. Akampa ishara mwanamke huyo na kuanza kutembea kuufuata ukuta huo mpaka walipokaribia lango kuu. Akampa ishara ya kusimama naye akafanya ivyo.
“Kaa nyuma yangu daima, usitoke!” Amata akamwambia kwa kunong’ona. Akatoa bastol kiunoni mwake na kuiweka tayari kwa kazi, magazine aliyoipachika haikuwa na risasi za moto, basi vitu kama vijishale vidogo vyenye urefu kadiri ya inchi moja ambavyo vina dawa ya usingizi inayoweza kukulaza kwa takribani saa tatu. Hatua nyingine kama kumi hivi zikamfikisha katika lango la kuiingia ngome hiyo, mbele yake kulikuwa na round about kubwa iliyojawa maua kedekede. Kwa jicho la haraka hakuona kamera yoyote ya usalama. Akajitokeza tayari kuuvamia mlango ule mkubwa wenye nakshi za kuvuti na kupambwa na maandishi yaleyale kama aliyoyaona kule kwenye njia panda. Aliapoanza tu kuuendea akasikia muungurumo wa gari ukitokea barabara kuu, akarudi nyuma na kuchuchumaa kwenye maua marefu, na yule mwanadada akafanya vivyo hivyo.
Sekunde thelathini gari moja jeusi likawasili ndani yake kulikuwa na jamaa Mwafrika akilindesha, lile lango likafunguka na taratibu. Amata hakutaka kuipoteza nafasi hiyo, kutoka alipokuwa yeye na ule mlango ni kama mita kumi hivi, akapiga hesabu ya haraka haraka ni jinsi gani anaweza kuingia pamoja na gari lile, akapata jibu. Kwa haraka akainguka na kuvuta hatua kwa kukimbia mpaka katika mlango wa lile gari, akau8fungua na kuketi kiti cha abiria huku tayari bastola ikiwa mbavuni mwa dereva. Yule mwanamke naye akafungua mlango wa nyuma na kuketi.
“Lala chini!” Amata akamwambia mwanamke huyo kisha akamwamuru dereva aendeshe kuingia ndani naye taratibu akaendesha na kuvuka lango hilo. Kama alitegemea kujikuta kwenye uwa au maegesho ya magari basi alikosea sana, gari lile liliingia katika sebule kubwa ya kupitab taratibu mapa katika moja ya kuta nayo ikafunguka kwa kwenda juu, likaingiamo. Mbele kidogo likasimama na yule dereva akamtazama Amata kwa woga.
“Unataka nini?” akamuuliza.
“Martin Gupter?” Amata akajibu.
“Gupter?” yule dereva akauliza
“Ndiyo…”
“Mbona simfahamu!” akashangaa.
“Humfahamu au unataka nitumie nguvu ndio unambie ukweli?” Amata akamwambia huku tayari keshamkunja shati lake. Yule dereva akaanza kutetemeka kwa woga.
“Hamkuwa na wageni wowote ndani ya jumba hili?” akamtupia swali kwa kuligeuza, “Wazungu watatu, mmoja mwanamke na wawili wanaume…” akaongeza kusema.
“Kulikuwa na watatu kama usemavyo, mmoja alikwishaondoka na wawili ndo sasa nimetoka kuwapeleka Uwanja wa Ndege,” akamwambia Amata.
“Wanakwenda wapi?”
“Aaaa mi sijui na wala sitakiwi kujua mimi hapa ni dereva tu, na wageni wa mzee sitakiwi kuwahoji chochote!”
Kamanda Amata akafyatua bastola na kile kishale kikamdunga jamaa shingoni, sekunde kumi tu akaanza kukodoa macho kama fundi saa anayetafuta skurubu. Amata akashuka na kufuatiwa na yule mwanamke, akapita katika uwazi mwingine na kujikuta katika ukumbi mkubwa ambao katikati kuna bwawa kubwa la kuogelea. Akalizunguka mpaka upande wa pili, akakwea ngazi na kufika ghorofa ya kwanza. Muda wote huu hakukutana na upinzani wowote, hapa akakutana na mlango mkubwa wa mbao, akakitazama kitasa na kugundua kuwa anaweza kucheza nacho, akachukua funguo yake na kuitumbukiza.
‘Twiiip! Twiiip! Twiiip! Twiiip!’ kelele kali za hatari zikasikika, Amata akajua amebugi, amefanya makosa, hakuna jinsi ya kuyasahihisha. Akamvuta yule mwanadada na kuingia naye kwenye uwazi mmoja ambao ndani yake kulikuwa na mtungi mkubwa wa maua, wakajificha nyuma yake na kusubiri. Mara watu wawili wakawasili, mmoja wao akachukua funguo yake na kuitumbukiza katika tundu, ile kengele ya hatari haikulia tena. Mambo yote haya amata alikuwa akiyashuhudia kwa macho yake.
Kumbe kuna funguo maalum! Akawaza. Alipowaona jamaa hao wanatoka, akajitokeza haraka na kuruka hewani, miguu yake ikatawanyika na kumtandika mmoja ambaye alisukumwa na kujikuta kingo za sakafu zikishindwa kumhimili, hivyo akadondoka vibaya na kutumbukia katika bwawa. Huyu mwingine alijibamiza ukutani akarudi wima na kukutana na kishale cha Amata, naye hakuchukua hata dakika akabebwa na usingizi.
“Chukua funguo!” Amata akamwambia yule mwanadada, naye kwa haraka akachukua, Amata akatazama huku na kule, hakuna shida. Akachukua funguo ule na kuingia ndani ya sebule kubwa, nzuri yenye samani za thamani. Amata akajikuta akitazama huku na huko, hata hakujua ni wapi ashike. Kando kabisa ya sebule hiyo kulikuwa na dirisha kubwa na meza ndogo ya kusomea iliyobeba kabrasha moja tu tena lilionekana kana kwamba limesahaulika, akaliendea huku nyuma yake akifuatwa na yule mwanamke, akalichukua na kulitazama, akasoma mawili matatu, moyo ukaanza kumwenda mbio, akaitazama saa yake.
“Shiiiittt!!!” akang’aka na kuikunja ile karatasi akaitia mfukoni na kuanza kurudi alikotoka. Akiwa anataka kumshika mkono yule mwanamke ili watoke kwenye jumba hilo, akasikia ‘clack’, milango yote ya kutokea nje ikajifunga. Akamwacha mwanamke huyo na kushika kitasa cha kwanza, umefungwa! Akauacha na kuuendea ule wa pili nao umefungwa, kengele za hatari zikagonga kichwani mwake.
“Tumeingia mtegoni,” akamwambia mwanamke huyo aliyekuwa naye.
“Sasa tunafanyaje?”
“Hatuna cha kufanya!”
Ukimya wa sekunde kadhaa ukatawala kati ya wawili hao, yule mwanamke akamsogelea Amata na kumkumbatia huku machozi yakimtoka.
“Kwa hiyo tunakufa?” akauliza.
“Hapana, ukiwa na mimi amini tu kuwa kifo kinaletwa na Mungu na si mwanadamu,” Amata akajibu huku akiliendea dirisha kubwa, akasimama na kuvuta kioo upande, macho yake yakashuhudia kolongo kubwa sana ambalo chini yake kuna mto Lofa uliyofanya mazingira ya kupendeza. Mara akasikia mlango ukifanya ukulele kuwa kuna mtu anafungua.
“Wanakuja!” yule mwanamke akasema.
“Tulia,” akamjibu na kutzama huku na huko kuona jinsi ya kujiokoa, hakuna. Haraka sana, akasukuma kochi na kuuziba mlango ili angalau kuongeza kizingiti kwa watu hao. Amata akaingia chumba kingine na kugundua kuwa ni jiko, hapo akakuta kuna bomba mtepeto ‘hose pipe’, kwa ngumi moja akavunja kioo na kuchukua ule mpira wenye urefu kadiri ya mita hamsini hivi. Aliporudi katika ile sebule tayari jamaa walikwishafungua mlango.
“Kill him!!!!” mmoja alisikika akipiga kelele na mara Kamanda Amata akasikia milio kadhaa ya risasi, akajua zimemkosa. Kwa kasi akawahi lile dirisha na kumkuta yule mwanamke akihaha, akamdaka na kumzungushia mkono wake kiunoni.
“Hold tight!!!” Amata akamwambia mwanamke huyo naye akafanya alivyotakiwa. Amata akachukua bastola ya upande wa pili, yenye risasi za moto. Risasi ya kwanza ikamteremsha kiongozi wao, ya pili ikamvunja mguu mwingine. Amata akiwa kakamata ule mpira kwa mkono mmoja na mwingine bastola huku kabanwa sawia, akatumia nguvu zote na kujirusha katika dirisha, kioo kikatawanyika naye akajirusha nje.
* * *
“Hii ndiyo misheni ya mwisho!” Gupter akamwambia Fredy.
“Na inabidi tuipange kwa umakini wa hali ya juu maana najua kuwa usalama wte wa Afrika utakuwa hapo,” Fredy akamwambia Martin huku akiendelea kunywa mvinyo wake taratibu.
“Kwa uzoefu wangu, kwanza mpaka sasa watakuwa wamebana uwanja wa ndege, na mahotelini pia…”
“Lakini kwa mpango huu wa kushuka hawatatukamata hata kidogo,”
“Yeah!”
Martin Gupter na Fredy walikuwa wakibadilishana mawazo ndani ya ndege wakiwa hewani kuelekea Addis Ababa. Kazi iliyokuwa ikiwasubiri katika jiji hilo ilikuwa ya kufa na kupona lakini walijiamini kutokana na weledi wa kazi yao.
“Hatujawahi kushindwa!” Martin akamwambia Fredy.
“Tutaingia pale usiku lakini mpango wetu ni kama tulivyopanga, Amanda anatusubiri kadiri ya maelekezo tuliyompatia…” Martin akasema.
“Yaani mimi kwa kumdhibiti yule mshenzi wa Tanzania, tumefanya kazi kubwa, hawa wengine takataka tu,” Fredy akasema. Martin akabadili kutoka kutazama muvi kwenye sikirini mbele ya kiti chake na kuweka ramani kutazama ni wapi wapo.
“Tumekaribia, sasa tunafika ukingoni mwa Jangwa la Sahara, dakika kama kumi na tano hivi tutakuwa tumeianza Addis,” Gupter akamwambia Fredy. Freddy akanyanyuka kitini na kuvuta pazia kisha akafuata ujia wa kuelekea chooni. Ndani ya choo hicho alitulia kwa dakika kadhaa, si kwamba alikuwa akijisaidia bali ni moja ya mbinu ambayo walipanga na swahiba wake. Freddy na Martin waling’amua mbinu ambazo dhahiri shahiri zingeweza kutumika na wana usalama kuwanasa. Kati ya hizo ni kuweka makachero katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Bole. Kwa kugundua hivyo wakajipanga kutumia mbinu mbadala kuingia katika jiji hilo.
‘Ngoh! Ngoh! Ngoh!’ Freddy alisikia mlango ukigongwa mara tatu, akaufungua na kutoka chooni.
“Hili ni kwa ajili yako,” Martin akampatia Freddy parachute naye akalivaa. Wakiwa katika harakati hizo, mtumishi wa ndege hiyo akawakuta.
“Hey! What are you doing?” akawauliza wanafanya nini. Martin hakumjibu bali akachomoa kisu kutoka kwenye mguu wake ndani suruali.
“Be silence!” akamuonya kuwa kimya.
“Hatutaki kudhuru mtu ndani ya chombo hiki, sisi tuna kazi zetu na sasa tunataka kuondoka, tuoneshe njia ya siri kuingia katika chumba cha mizigo haraka,” wakamwamuru na huyo dada hakuwa na jinsi akawapitisha katika njia zao wambazo huzitumia kwa kazi zao huku wengine nao wakitahadharishwa kutofanya lolote. Baada ya sekunde chache, yule mwanadada akawaonesha njia ya siri kabisa inayoshuka chini ambako uhifadhiwa mizigo ya wasafiri.
“Please, don’t hijack a plane!” tafadhali msiiteke ndege! Yule mhudumu akawasihi.
“That is not our mission,” hiyo si kazi yetu! Martin akajibu huku akiufunga ule mlango na wao kupotelea chini. Huko wakapenyepenye mpaka usawa wa magurudumu ya nyuma, kwa kutumia vifaa vyao vya siri wakafungua kijimlango ambacho kiliwaruhusu kuona nuru ya nje. Upepo mkali ulianza kuingia ndani na kuleta vurugu. Kengele za hatari zikaanza kufanya fujo ndani ya chumba cha rubani, wakang’amua kuwa kuna hitilafu katika sehemu ya chini ya ndege. Mmoja wao akatumia njia maalumu ndani ya chumba hicho na kuingia katika sehemu ya mizigo, akapita kwa taabu kutokana upepo mkali akafika eneo husika na kutumia nguvu nyingi kudhibiti kijimlango hicho, akafanikiwa japo si kwa kiwango kikubwa. Dakika ishirini na tano baadaye ndege ile kubwa ikafanikiwa kutua salama katika uwanja huo na abiria waliokuwamo wakapiga makofi kumpongeza rubani kwa kuwa amewanusuru maisha yao.
* * *
VILIMA VYA ETONTO – ADDIS ABABA
Amanda Keller aliegesha garile katikati ya msitu Etonto ulio nje kidogo ya jiji hilo maarufu Afrika. Jua tayari lilikuwa likiimaliza safari yake ya siku nzima upande wa Maghalibi wa jiji hilo na kuanza kuliacha giza litawale. Sauti za ndege wazuri zilisikika pia zikiimba na wakirudi makundimakundi kwenye viota vyao ndani ya msitu huu. Akaitazama saa yake, ikamwonesha ni saa kumi na mbili na robo jioni; mara tu baada ya kuushusha mkono wake akasikia muungurumo wa ndege-Ulaya na kuiona ikikatiza anga kuelekea Bole ambako ndiko uliko uwanja mkubwa wa ndege wan chi hiyo. Akafungua mlango na kutoka nje ya gari hilo aina ya Jeep Cherokee. Haikupita hata dakika tano akasikia vishindo nyuma yake, akageuka na kutazama, akaona vitambaa vikubwa vikifunika eneo dogo lenye mzingo wa kama mita nane hivi na miguno ya watu ikasikika. Akakimbia mara moja na kuwasaidia japo kusimama.
“Natumai mmetua salama!” akawaambia.
“Yes, na sasa ni kazi moja tu! Vipi huko Addis, mambo yakoje?” Martin akauliza wakati Fredy akikunja ile miamvuli waliyotumia.
“Addis ni moto, ulinzi kila mahala, kila hoteli, kila baa na kila kilabu cha usiku, patroo za askari mchana na usiku…” Amanda akajbu huku akifungua mlango wa gari tayari kwa safari.
“Bila shaka wanataraji uwepo wetu,”
“Haswaaa, uwanja wa ndege wana usalama wengi wana picha zetu, wanategemea tungeingia kizembe sana ili watunase…” akaeleza.
“Wameula wa chuya kwa uvivu wa kuchagua,” Fredy akasema huku akifunga mkanda na gari lile likaondoka kwa kasi kurudi mjini.
Dakika hamsini na tatu ziliwafikisha katikati ya jiji hilo baada ya kupita vikwazo vingi vya askari na ukaguzi wa hapa na pale lakini hakuna askari hata mmoja aliyewagundua watu hao kutokana na jinsi walivyojibadili hapa na pale. Amanda akaendesha gari mpaka upande wa pili wa jiji hilo huko viungani na kuingia katika nyumba moja ya ukubwa wa wastani iliyozungukwa na miti mkubwa ya maua ya bugamvili na kufanya picha ya kupendeza.
“Makazi yenu yatakuwa hapa!” Amanda akawaambia baada ya kuegesha gari lake mbele ya nyumba hiyo. Wakateremsha mabegi na kuingiza ndani kila mmoja akachukua chumba alichokipenda.
“Hapa ni salama?” Martin akauliza.
“Yeah nimefanya uchunguzi wa kina na kila kitu kipo sawa, hata ulinzi huku si sana kama mjini,” Amanda akawaambia swahiba zake.
“Good!”Martin akajibu na kujitupa kitini.
“Sasa ni kuoga na kulala mengine kesho asubuhi, ratiba ipo vipi Amanda?” Martina akauliza.
“Aaaannh kesho kuanzia majira ya saa tano asubuhi hivi, viongozi wataanza kuingia hapa jijini tayari kwa mkutano wa kesho kutwa. Mpaka sasa katika orodha yangu, wageni wa ndani na nje tayari wametimia wote wanasubiriwa hawa wa juu tu ili kikao kifanyike,” akawaambia.
“Na kila kitu kipo sawa?”
“Kila kitu nimeweka sawa, tusubiri wakati tu, maana kazi yetu ni kesho kutwa baada ya mkutano,”
“Unaonaje, tutafanikiwa au la?”
“Tutafanikiwa tu, ila tu inabidi tuwe na chaguzi mbili za kutekeleza mauaji ama kwa risasi au kwa sumu…”
“Usijali, kwa kuwa hiyo ni kazi yangu nitashughulikia mwenyewe, tukutane kesho hapa kwa chai na mipango mingine, pia lazima tufike uwanja wa ndege ili kuungana na wapenda amani kuwapokea viongozi wetu,” Martin akasema na wengine wakabaki kuangua vicheko.
 
Moto moto hatareeeee!!!

Kulubule fanya utupe cha mwisho kwa usiku huu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom