Riwaya: KISASI

Riwaya: KISASI

RIWAYA: KISASI
NA: FRANK MUSHI
SEHEMU YA MWISHO (FINAL)
“Mtu DHAIFU hawezi KUSAMEHE, kitendo cha
kusamehe ni cha watu JASIRI wenye uwezo wa
kupuuzia machungu nakuamua kuonyesha
kutojali kwao. Ni mpaka utakapo samehe na
kuasahau ndipo utaweza tena kuendelea na
maisha yako. Kwa kushindwa kusamehe
unaweza tengeneza tatizo kubwa kuliko lile
alilotengeneza aliyekukosea.”
HII NI SEHEMU YA MWISHO.
**MWANDISHI**
Yule jamaa aliyenihadithia kuhusu hadithi hii
aliyoisikia kupitia kituo cha radio aliniacha na
maswali mengi sana ambayo nilidhani kuwa ni
muda muafaka wa kuikamilisha hadithi hii kwa
kutafuta kiundani juu ya wahusika kwenye
mkasa huu wa kutisha. Nilifunga safari mpaka
Gereza la Segerea upande wa wanawake ili
niweze kuonana na Mary aliyekuwa akitumikia
kifungo cha maisha gerezani. Safari yangu
haikuzaa matunda baada ya kukuta Mary akiwa
hoi hospitalini, nilibahatika kuruhusiwa kuonana
naye akiwa hospitali huku amefungwa pingu
kila upande wa mikono na miguu yake.
“Mimi ni mwandishi wa habari, nimebahatika
kusikia masimulizi yako ambayo naamini
uliyatoa kwa mwandishi ambaye alikuwa
akikusanya makala kuhusu mkasa wako na
Patrick. Nimebahatika kusikia, japo ni kupitia
kwa mtu juu ya kilichotokea na pande zote mbili
mlitafutwa mkaelezea kilichotokea, lakini
nilitaka kujua hali yako kwa sasa na maisha
yako baada ya yale mambo kuishia, na
unavyojisikia baada ya Patrick kukuacha bila
kukufanya chochote kibaya”. Nilimweleza Mary
nia yangu hiyo, japo alikuwa akionekana kabisa
kuwa alikuwa kwenye dakika za mwisho kabisa
za maisha yake. Alionekana akiongea kwa shida
sana. Nilimgeukia yule askari aliyekuwa karibu
na kile kitanda na kumuomba amfungue mikono
kwani asingeweza kabisa kuwa na hata nguvu
ya kutoroka. Afya yake ilikuwa imedhoofika vya
kutosha, sikuamini kama kweli yule ndiye Mary
niliyemsikia kwenye yale masimulizi ya yule
jamaa. Yule askari alikataa kumfungua huku
akinisisitizia kuwa ilikuwa ni taratibu ya kazi
kuwa lazima afungwe pingu. Nilirudi tena na
kumgeukia Mary, alikuwa akitaka kuniambia
kitu lakini sikuweza kuisikia sauti yake vizuri.
Nikazidi kumsogelea kwa karibu na hapo ndipo
niliposikia sauti yake japo ilikuwa kwa mbali.
“Nenda kwa mkuu wa gereza kuna vitu vyangu
nimeweka kule, mwambie akupatie bahasha ya
kijani, hakikisha unamfikishia ujumbe Patrick,
tafuta namna ya kuwafahamisha watu wengi
zaidi juu ya hali yangu na majuto yangu.”
Aliongea hayo na kabla hata sijatoka Mary
alianza kuhangaika na kurusha miguu huku na
kule, akakata roho mbele ya macho yangu.
*****
Niliondoka mpaka kwa mkuu wa gereza nikiwa
na askari yule aliyekuwepo pale wakati Mary
akinipa maelekezo ya kuchukua hiyo bahasha
ambayo ina ujumbe niliotakiwa kumfikishia
Patrick ambaye hata hivyo sijui alipo wala
sijawahi kukutana nae. Nilibahatika kupata ile
bahasha iliyokuwa nyepesi sana, niliifungua
ndani na kukuta ujumbe mrefu ulionifanya nikae
chini na kuanza kuusoma taratibu kama vile
ulinihusu, ulisomeka hivi;
Mpenzi Patrick, na ulimwengu kwa ujumla,
Nafahamu ya kuwa nimekuwa mnyama wa
kushindwa kusamehewa na hii dunia, sijui kama
naweza kuja kusamehewa na yeyote mwenye
akili timamu. Natamani ningeweza kuumbwa
tena upya nikasawazisha makosa yangu lakini
hakuna tena muda.
Nimeandika huu ujumbe kwako ili kukuambia
sababu ya mwisho ya kwanini nilikuwa hivi
nilivyo. Kila kitu kwenye maisha hutokea kwa
sababu Patrick, lakini katika maisha yangu vitu
vilitokea kwasababu ambayo sikuitaka katika
maisha yangu wala sikuipenda kabisa.
Nilitendewa unyama ulionifanya niwe mtu wa
kuhangaika kila mara hasa pale nilipogundua
kuwa mimi si kitu tena. Nilijidharau kwakuwa
nilifanywa mtu wa kudondoka muda wowote.
Baba yangu alimuua mama yangu nikishuhudia,
lakini chanzo cha ugomvi wao sikukifahamu
mpaka pale nilipofikisha miaka saba. Nilikuwa
mdogo lakini nilikuwa na akili sana,
niliunganisha matukio na kutafuta ushahidi na
ndipo nilipokuja kugundua chanzo cha kifo cha
mama yangu. Aliuawa kwaajili yangu, aliuawa
kwa kitu ambacho hakikuwa cha kweli.
Miaka mingi iliyopita baba yangu alikuwa
akisoma shahada ya udaktari nchini Urusi.
Kuna wakati karibu kabisa na akiwa anamaliza
masomo yake alirudi nyumbani, kwa wakati
wote huo mama yangu alikuwa akimsubiri tu,
walioana na kisha aliondoka na kwenda Urusi
kwa miaka sita, baada ya yeye kurudi ndipo
mama yangu alipopata ujauzito na miezi tisa
mbeleni nilizaliwa. Maisha yalikuwa mazuri
lakini tafrani ilianza pale ambapo nilifikisha
miaka mitatu. Baba yangu alikuwa akimtuhumu
mama kuwa mimi sio mtoto wake na kwamba
mama yangu alikuwa Malaya. Lakini mama
alisisitiza kuwa wakanipime DNA ili iweze
kujulikana ukweli. Aliyeleta maneno ya kwamba
mimi sio mtoto wa baba yangu ni baba yangu
mdogo ambaye alikuja kutembea na mimi
baadaye, ambaye ndiye aliyekuja kuharibu
maisha yangu kabisa. Nilisimuliwa haya na
shuhuda ambaye alifahamu kila kitu na alinipa
njia za kupata ukweli kuhusu kifo cha mama
yangu. Baba zangu wadogo walikuja juu pia na
baadhi ya watu lakini kila mama alipohimiza
kwenda kuangaliwa DNA hawakutaka kabisa.
Nilichomwa sindano ya sumu aina ya
‘dimethylmercury’, hii ni sumu ya kutengenezwa
na binadamu, ni sumu inayoua taratibu na kwa
muda mrefu. Nilichomwa kiasi cha 0.3 Mils na
hichi ndicho kilichonifanya nione hakuna haja ya
kufanya chochote. Nilianza kuumwa lakini
haikuweza kugundulika mapema niliumwa nini.
Baada ya kifo cha mama yangu na hata baada
ya baaba yangu kufa pia niligundua kuwa mzee
wangu alikuwa akifanya tafiti juu ya ile sumu
aliyonichoma. Hapo ndipo nilipogundua ni sumu
ya aina gani nimechomwa. Nilivurugika akili
lakini hakuna yeyote niliyewahi kumwambia.
Katika umri wangu nilianza kuua wanaume
hovyohovyo, lakini hasira yangu haikuwa kwa
wanaume tu, ilikuwa ni kwa kila binadamu na
kiumbe cha dunia hii. Mpaka leo hii nikiandika
ujumbe huu, nimeshaua wanaume zaidi ya 300,
na wanawake wachache, wapo watu ambao nao
niliwachoma sindano ile kwakuwa nilibahatika
kuitafuta mpaka nikaipata. Nia yangu nikuona
kila binadamu akihangaika kama mimi, kila
binadamu akiwa na hofu ya kufa muda wowote.
Lakini katika wote, sikuwahi kukuchoma wewe
tu, japo nakiri kukuchoma sindano iliyopoteza
akili yako kwa muda mrefu. Sio tamaa tu ya
fedha bali roho ya kisasi iliufunga moyo wangu.
Pamoja na pesa nilizokuwa nazo lakini
nilishindwa kabisa kutoa ile sumu mwilini, najua
itaniua siku moja hasa kwakuwa sina tena vile
vidonge vya kupambana nayo na kuniongezea
nguvu. Lakini najuta sana. Najuta yote
niliyoyafanya.
Naomba uniombee kwa mungu, naomba kila
mmoja kwa wakati wake aniombee kwa mungu,
nimefanya mengi mabaya lakini sikuyafanya
kwa raha. Niliyafanya kwa uchungu na nilikuwa
nikilia kila muda ulipopita mbele yangu.
Nisameheni sana, nisamehe sana Pamela,
nisamehe sana Cris, naomba nisameheni wote
mliopata usumbufu kwa mimi kuishi duniani.
Mnisamehe ndugu zangu, niliua baba zangu
wadogo wote na mashangazi zangu kwakuwa
walichangia sana kumnyanyasa mama yangu.
Hakuna aliyefahamu kuwa walikuwa wakiuliwa,
wengi walijua kuwa walikufa kifo cha kawaida
lakini mimi ndiye nijuaye ukweli zaidi wa
yaliyotokea. NISAMEHENI.
NAKUPENDA PATRICK. NIKIFA BASI
TUTAKUTANA MBELE YA HAKI KAMA IKITOKEA
NIKAFIKA HUKO.
Mungu akulinde wewe na familia yako.
AMANI NA SALAMA.
Ni mimi MARY.
*******
Huo ndio uliokuwa ujumbe wa Mary kwa watu
wote na kwa Patrick. Nilihangaika sana kupata
mawasiliano na Patrick lakini mwishoni
nilibahatika kupata namba yake ya simu,
nilimueleza juu ya ule ujumbe na alinitumia
tiketi ya ndege akitaka kuonana na mimi.
Nilisafiri hadi Australia ambapo ndiko anakoishi
kwasasa na mkewe na watoto wake wawili, Cris
na mtoto wao mwingine mdogo aitwaye
Qwinzel. Wanamiliki hospitali maarufu ya
Pamela Mental Clinic, na pia ukumbi mkubwa
wa sinema wa Qwinzel Cinemax huko nchini
Australia, na Patrick kwa sasa ni mhadhiri wa
chuo kikuu cha Swirnbune.

MWISHO.
 
Natumai mmeinjoi, see you another time ila still nipo around
 
Usijali mkuu nitajitahidi

Kaka Asante kwa kuwa mwaminifu!! Maana umeianza na kuimaliza tofauti na wanaokuja kutangaza biashara zao hapa. Mana ni bora mtu aseme kuwa anauza vitabu kuliko hivi wanavyofanya
 
vipi mkuu Willy Gamba1 itakua poa ukitupia `tutarudi na roho zetu' kama ipo
 
Willy shusha yoyote uliyonayo ambayo bado hatujaisoma mana kidi kudi amepotea
 
aisee Willy Gamba 1, story hii niliichukulia poa kumbe bonge la story? kumbe na wapare wamo enhee? iko poa sana. niliichukia kwa kuwa kidi kudi hakumalizia story ya U C H U lkn jana nimejitosa na nimeipenda.

ni kweli tulivyo leo ni matokeo ya mahusiano tuliyokumbana nayo ktk makuzi tetu
 
Kila chenye mwanzo hakikosi kua na mwisho kweli hadith ilikua nzuri na ya kusisimua asante ndugu
 
Back
Top Bottom