Riwaya: KISASI

Riwaya: KISASI

Sehemu ya Nne

Kwa Mary Robert.2010
“Ulemavu wa fikra mgando tulizonazo juu ya
maisha na juu yetu wenyewe huzaa mawazo
mpauko yasiyoakisi umuhimu na umaana wa utu
wetu na malengo yetu, kuna muda tunafikiri kuwa
watu wa aina fulani ndio wawezao kufanya mambo
ya maana na yenye maendeleo kwa wao wenyewe,
na sisi kujiweka nyuma kwa miakisio ya ubovu wa
uteuzi wa fikra sahihi dhidi ya fikra mtambuka.
Tunawaza zaidi kuliko kufikiri juu ya hatima ya
uzio wa upeo wetu na malengo yetu. Akili zetu
hutuongoza katika mwambao wa kukata tamaa na
kutojikubali. Tunahangaikiwa kuona kuliko
kutazama na kuyafanya ya mwisho kuwa ya
kwanza. Sisi ni zao la umakini hafifu wenye
kichefuchefu cha kutambua tunapotaka kwenda na
njia tupitayo. Ukungu wa fikra potofu huyasonga
mawazo machachu tuliyonayo juu ya yale
tuyaamaniyo kwenye maisha ya wengine.
MABADILIKO NI WEWE,,WEWE NI SERIKALI YA
AKILI YAKO.” HII NI SEHEMU YA NNE.”
Ni saa sita na nusu usiku bado sauti ya yule dada
ilikuwa ikisikika ikihadithia,,mawazo yalikijaa
kichwa changu kwakuwa sikujua majibu ya
maswali mengi niliyokuwa nayo, kibaya zaidi ni
kuhusu huyu Patrick, mkojo ulikuwa umenibana na
sikutaka kutoka nje kwakuwa nilihisi kukosa baadhi
ya sehemu, hivyo niliibana miguu yangu vizuri ili
kuuzuia, muda kidogo nilisikia mtangazaji akisema
kuwa ni mda wa matangazo hapo ndiyo
nilikurupuka na kwenda chooni, niliporeje Pamela
alikuwa anaendelea kusimulia ule mkasa.

***PAMELA***
Ule mlio wa bunduki uliuumiza sana moyo wangu
hasa nilipoona Patrick akidondoka, nilisikia tena
mlio mwingine na hapo nikatazama huku na kule
kuangalia ni nini kimetokea, nilikimbia bila kujali
kuwa na mimi ningeweza kupigwa na risasi,
nilipofika pale Parick alikuwa chini, nikapiga haraka
simu pale hospitali na ndani ya dakika tatu gari
ilikuwa imefika tukampakia na kumpeleka hospitali.
Hakuwa na jeraha lolote.

*****
“Ni mshtuko tu na inabidi tumchome sindano ya
usingizi apate masaa mengi ya kupumzika,
utamuhudumia wewe kwa ukaribu zaidi” alikuwa ni
dokta Anderson akinieleza hayo baada ya kutoka
kwenye kile chumba Patrick alichokuwa
amewekwa. Sikujibu chochote bali nilitoka na
kwenda kuchukua mabomba ya sindano
nikamchoma kwa haraka sana na kuondoka
kuelekea nyumbani kwangu, nilichukua bastola
yangu na kwenda mpaka kule ufukweni,
nilizunguka kote na pembeni ya vile vichaka lakini
sikuona mtu yeyote, nilisogea mpaka pale mbele
karibu na Patrick alipokuwa ameanguka na
nilipotazama wenye mti niliona ile risasi ikiwa
imepenya kwenye ule mti, nilichukua kichuma
kidogo nikahangaika mpaka nikaichomoa ile risasi.
“ngriiiii,,,ngriiii” ulikuwa mlio wasimu ukiita ndani
ya simu yangu.
“Habari yako Pamela” aliongea yule mtu baada ya
kupokea simu.
“Nzuri Felicity habari ya kwako mpenzi”
tulisalimiana lakini sikuwa na maneno mengi sana
ya kusema.
“upo kwako? Nataka kuja hapo nina shida”
nilimuliza huku nikionekana mwenye haraka.
“ndio njoo,,kuna tatizo gani?” aliniuliza lakini kabla
hata sijamjibu nilikuwa nimeshakata simu na
kuanza kukimbia kuelekea nyumbani, niliwasha gari
na kuelekea kwa Felicity ambapo ni mwendo wa
dakika kumi na tano toka kwangu, nilikuwa na
mawazo sana na nilikuwa nimeshachoka kwa
kufikiri ni nani anataka kumuua Patrick na kwanini,
nilihisi kama pengine Patrick alikuwa kwenye
matatizo makubwa na sasa alitakiwa kuuwawa ila
sikujua nani muhusika na kwanini afe.

***
“karibu Pamela” Felly alinikaribisha na hapo
niliingia mpaka ndani kwake, alienda kunichukulia
juice kitu ambacho niliona kama ni kupoteza muda
ila sikuweza kumwambia aache kakuwa
hakuniambia kama anaenda kuleta juice.
“karibu Pamela” alinikabidhi ile juice huku
akinitazama usoni.
“kunanini Pamela?” aliniuliza.
“unakumbuka nilikuambia nina boyfriend sasa hivi
ila nikakuelezea kuhusu ile ajali yake na kila kitu?”
nilimuuliza kwanza.
“Ndio nakumbuka” aliitika huku macho yakiwa
yamemtoka, nilijua kuwa aliwaza moyoni pengine
Patrick amefariki hivyo sikumuacha akae na
mafikirio hayo kichwani mwake hata kwa sekunde
moja kwakuwa sikutaka yeyote awaze hayo.
“Leo kama lisaa limoja lililopita amekoswa na
risasi kule ufukweni na amepoteza fahamu, sijui ni
nani kafanya hivyo lakini naamini wewe unaweza
kunisaidia kufanya hivyo” nilimtazama kwa makini
huku kijasho chembamba kikinitoka.
“umefanikiwa kuipata hiyo risasi” aliniuliza.
“ndiyo ninayo hapa” niliitoa ile risasi na
kumkabidhi.
“sawa nipe muda nitakujibu kesho nitakachokuwa
nimekigundua” nilinyanyuka nikamkumbatia na
kuondoka.
Felicity alikuwa ni rafiki yangu wa siku nyingi toka
nikisoma shahada ya kwanza tulisoma chuo
kimoja, na nilipokwenda kusoma shahada ya pili
naye pia tulisoma nae lakini yeye alisoma mambo
ya uchunguzi wa kisayansi wa makosa ya jinai
(criminal and forensic investigation), baada ya
kumaliza shahada ya pili aliajiriwa kwenye
maabara ya mkemia mkuu na baadaye alikwenda
kitengo cha polisi wa upelelezi, hivyo ni mtu
ambaye ni mtaalamu sana wa kufanya uchunguzi
wa mambo hayo, nilikuwa na shahuku sana ya
kutaka kujua.

KESHO YAKE.

“pipii,,,pipiiii” zilikuwa honi za gari, nilikurupuka
toka usingizini na kuchukua shati la Patrick
lililokuwa limetundikwa ukutani kisha nikalivaa na
kuchingulia dirishani. Niliona gari kule nje
nikagundua alikuwa ni Felly, hata sikuhangaika
kufungwa shati nikatoka vilevile nikiwa nimelivaa
huku nikiwa na chupi tu, nilisogea pale getini na
kufungua geti kisha aliingia.
“hey unakuwa kichaa au ni nini” aliniuliza huku
akicheka. Alikuwa amependeza, Felly alikuwa ni
mzuri ila sikuzote alikuwa akijiweka katika namna
ambayo wanaumea wengi waliogopa kumfata,
alikuwa ni mrefu na mara zote alikuwa akivaa nguo
zake za upelelezi na kuweka bastola yake kiunoni,
alikuwa ni msichana lakini ningeweza
kumfananisha na nikita au Angelina Jolie kwenye
Salt, au Nina Myer kwenye 24 au Anny Walker
kwenye Covert affairs, alikuwa ni mtu wa mazoezi
na mwalimu wa karate katika chuo cha polisi pia,
hayo yaliwafanya wanaume wengi sana
wamuogope, japo mwanaume mmoja tu alifanikiwa
kuuteka moyo wake lakini alifariki akiwa vitani
nchini Iraq kwahiyo mar azote amekuwa
akishindwa kutafuta mtu mwingine kwakuwa
anashindwa kumsahau yule aliyekuwa nae.
“Felly acha tu mpenzi, nakosa usingizi sasa yani
nimepata usingizi asubuhi hii” nilimwambia huku
nikitangulia ndani.
“mimi sikai nataka unipeleke hapo ulipoitoa hii
risasi” aliniambia huku ameshikilia kiuno na
kuyatazama makalio yangu.
“Hey stop that, have you become a Lesb?”(hey
acha, umekuwa msagaji) nilimwambia huku
nikivuta shati langu na kuingia ndani.
“hahaa you are”(wewe ndiye msagaji) alicheka na
mimi niliingia ndani nikavaa suruali na kutoka nje
kisha tuliteremka kuelekea ufukweni.
Nikamuonyesha ile sehemu.
“sasa kama risasi imekuja hapa inamaana imepita
mkono wa kulia wa Patrick kwa futi sita toka
alipokuwepo, na itakuwa imetoka mita miamoja
mbele yake kwenye kale kamsitu pale, sasa hii
inamaana kama angekuwa anataka kumuua Patrick
basi risasi isingepita mbali hivyo, na isingepigwa
mara ya pili na isionekane kujia upande huu. Lakini
pia kama alipanga kumuua Patrick basi huyo mtu
atakuwa sio muuaji anayejua kuua na atakuwa ni
mwanamke, kwakuwa risasi inapotoka inatoka na
mtetemo hivyo kama mkono sio imara basi lazima
iyumbe na isifike pale inapotakiwa kufika, hivyo
muhalifu wetu hapa kama alikuwa hana shida ya
kuua atakuwa ni mwanaume au mwanamke ila
kama alidhamiria kumduru Patrick atakuwa ni
mwanamke ambaye ni laini na muoga.” Alimaliza
kuniambia Felicity na kunishika mkono kisha
tuliondoka na kurudi nyumbani. Akili yangu ilijua
wazi kabisa hapa itakuwa ni Mary, nilikuwa siwezi
hata kuongea.
“unahisi anaweza kuwa ni nani” aliniuliza Felly
“sihisi chochote, au pengine atakuwa ni Mary yule
mpenzi wake aliyemtelekeza huku” nilimuambia
hayo huku nikiwa ninahasira kweli.
“inawezekanaje wakati alishaondoka” Felly
aliniuliza na hata hivyo sikuwa nina uhakika na
nilichokiongea lakini hiyo ilikuwa ni fikirio langu ka
kwanza.
“Sielewi Felly ila fanya uwezavyo umgundue huyo
mtu aliyefanya hivyo, hata kama hakuwa na nia ya
kumdhuru Patrick lakini nataka kumjua”.
Tuliachana yeye akaelekea kazini na mimi
nilijiandaa kuondoka kwenda kazini. Nilipofika
nilimkuta Patrick amesharudi katika hali ya
kawaida na sasa alikuwa nje ya hospitali.
“vipi unajisikiaje Patrick” nilimuuliza kwa shauku
nikitaka kusikia tu sauti yake.
“niko salama, nimekumis” ooh aliongea maneno
yaliyonipa sana faraja aisee, Patrick alikuwa si mtu
hata wa kucheka kwa dakika moja toka arudishe
fahamu alikuwa ni mtu wa kukaa kimya tu na
kutabasamu kwa mbali.
“oooh Patrick nimekumis pia mpenzi wangu”
nilimshika kichwa kwa mikono yangu miwili na
kupeleka ulimi wangu mdomoni mwake bila hata ya
uwoga.
“inabidi nimtafute mtu aliyenyuma ya haya yote
Pamela hivyo nitahitaji kurudi Tanzania” kauli hii
ilinivuruga akili na moyo kwakuwa sasa hii
haikuwa tena nzuri kwangu. Nilimuachia pale na
kunyanyuka nikizunguka huku na kule kama chizi
huku machozi yakinitoka, ilikuwa ni ngumu kwangu
kwakuwa sikuwa na namna ya kumuachia Patrick
asiondoke.
“Pamela, najua hii ni ngumu kwako, natambua
hisia zako kwangu lakini nakosa Amani kuishi bila
kujua sababu iliyopelekea mimi kukaa kitandani,
nataka kujua kila kitu ili nafsi yangu utulie, nataka
kufahamu hatma ya mali zangu zote
nilizozisumbukia” Alinikumbatia kwa nyuma
akapitisha mikono yake kiunoni mwangu na
kuikutanisha kwa mbele.
“ni mapema mno Patrick, mimi ni daktari wako,
bado ugonjwa wako haujaisha kabisa” nilimuambia
huku nilimtoa mikono yake na kumgeukia kisha
nilimshika mashavu yake na kumwambia katika
sauti ya upole ambayo hata hivyo haikumshawishi.
“nitakuwa salama usijali” aliniambia hivyo na
kuondoka pale kisha alisogea mbele kidogo na
kugeuka akinitazama.
“Pamela, kukaa hivi bila kazi wala chochote ni
shida kwangu, mimi sina cha kufanya hapa, ni bora
niende kujua nini kimetokea” aliniambia huku
akionekana kujizuia asitoe machozi.
“nimehangaika sana katika maisha yangu Pamela,
nimehangaika kufika nilipokuwa nimefika, nilikesha
usiku na mchana nikihangaika kila nchi kutafuta
maisha, haiwezekani vikapotea tu kirahisi hivi”
aliongea huku machozi yakimtoka.
“Patrick naelewa hayo ila yupo mtu atatusaidia
kujua hayo tukiwa hapa, na utajua kila kitu na
wakati huo utakuwa ukifanya kazi hapa nchini
nimeshaongea na dokta Anderson na amesema
anaanza kukutafutia kwanza kibali cha kukaa hapa
na cha kufanya kazi, kisha tutaanza kufatilia upate
kazi hapa” nilimuambia huku nikijitahidi kuongea
kwa sauti ambayo angeweza kuielewa vizuri na
kumshawishi.
“nitakaa huku hadi lini?” aliuliza
“sijui hadi lini lakini ni hadi upone kabisa na sumu
iwe imeondoka mwilini, Patrick nakuhitaji, siko
tayari kukupoteza, huwezi kwenda Tanzania kama
hujui kila kitu kuhusu safari yako, huwezi kwenda
Tanzania ukiwa na milioni 15 tu na ukategemea
utafanya kila kitu, hapana ni lazima uwe
umejipanga na uwe unajua utaanzia wapi na
utaishia wapi, bado hatujajua nani alikufanyia
hivyo na kwaiyo unaweza ukaenda nso ukaisha
kabisa, nina rafiki yangu anaweza akasaidia”
nilimuambia na kumuona akiwa kimya nikajua
dhahiri ameshanielewa.
“nataka kuonana na huyo rafiki yako kwanza
nimuambie vitu vya kunisaidia kufatilia” aliniambia
huku akinitazama kwa jicho kali usoni.
“usijali ila kwasasa anafatilia ni nani alikufyatulia
risasi pale ufukweni” nilimueleza huku nikimshika
mkono kuelekea kule hospitalini, alikuwa na
mawazo sana, nilimpeleka mpaka hospitalini
kwangu na kumchukulia dawa kisha alikunywa na
hapo nilisaini na kuondoka naye mpaka nyumbani,
aliingia kuoga na mimi nianza kumuandalia
chakula, alipomaliza alikaa sebuleni huku
akionekana kuwa na hasira sana, nilipomaliza kula
mimi nilikwenda kuoga na nilipotoka nilikuja mpaka
sebuleni nikiwa na kitaulo kifupi ila nilishtuka
kumkuta mtu pale.
“hee, umekuja saa ngapi wewe” nilishtuka na
kujifunika na pazia.
“hahaa,,nimefika mda sio mrefu na ninaondoka
muda sio mrefu, hivyo njoo hapa tuelezane kwanza
kisha utafanya kazi zako nyingine” nilitoka na kile
kijitaulo mpaka pale sebuleni.
“Patrick usiniangalie” nilimtania huku nikicheka,
nilikwenda mpaka pale akanivuta na kunipakata.
“Patrick huyu anaitwa Felicity, ni rafiki yangu,
Felicity huyu ni mpenzi wangu anaitwa Patrick,
najua hamjawahi kukutana ila kipindi yuko
hospitali Felicity aliwahi kuja mara kadhaa
kukuangalia” niliwatambulisha kila mmoja kwa
mwenzio.
“nashukuru sana kukufahamu Felicity” walishikana
mkono na kama kawaida ya Felly huwa hapendagi
kupoteza muda.
“Nimefanya uchunguzi na nimeichunguza ile risasi,
sasa nataka nikuonyesheni kitu hapa” aliwasha
‘projector’ aliyokuwa ameiweka pale mezani kisha
akawasha na laptop yake na kuanza kuelezea.
“Risasi ile uliyoiokota pale inaitwa 2.34 mm rimfire,
inatengenezwa uswis na ina milimita 2.3, bastola
yake ina 6.1 milimita ni rimedrife, imesajiliwa kwa
namba 23kyt45, mwaka jana, ilipigwa kwenye kona
ya nyuzi 75 toka upande wa kulia wa alipokuwa
Patrick, hii inaonyesha kuwa kama mpigaji alikuwa
ni mzoefu wa kutumia bastola basi angeweza
kumlenga kama mkono usingecheza. Lakini
kwakuwa ulicheza na kupiga futi sita kushoto kwa
Patrick inamaana alikuwa amelegeza mkono hivyo
mtu kama huyu atakuwa ameshtuka kiwiko cha
mkono wake, pia niliende pale eneo la tukio jana
baada ya kuachana na wewe pale,,nilikuta kuna
miguu ya viatu visivyo na soli na inaonekana
aliyepiga aliegemea mti na nywele zake zilibaki
kwenye zilishika kwenye magome ya miti na hivyo
kuacha nywele kidogo pale ambazo nilichukua na
kwenda kuangalia DNA, hivyo baada ya uchunguzi
wote nimegundua kuwa aliyefyatua risasi ni NANCY
ROVELT”
“WHAAAAT”
NINI KITATOKEA?? ENDELEA KUFATILIA
 
Ni kama mnawasiliana...weka hii....ngoja etc!
Nikutoe tu wasiwasi mkuu hakuna cha mawasiliano wala nini, interest zikioana mtajikuta mnashea kila mmoja alichonacho. Wewe na wengine tujali zaidi burudani hayo mengine si yetu kuyafuatilia hata tungekua kampuni moja as long as tunapata burudani yanini kufuatilia mengineyo?
 
Sehemu ya Tano

Kwa Mary Robert.2010
“Hakuna haja ya kukata tamaa na kujiona kuwa huna thamani katika mapenzi yako kwakuwa tu kila mahusiano uanzishayo hayawi na mwisho
mzuri au ulioutarajia, maisha ya mapenzi ni maisha dhalimu muda mwingine. Unaweza
kukutana na mtu sahihi katika muda usio sahihi,na unaweza kukutana na aliyesahihi katika muda usio sahihi. Unachotakiwa kufanya si kukata tamaa bali kuwa makini na muda na unaokutana nao. Kila mtu anapacha wake hapa duniani,inapotokea umekutana na pacha wa mtu, ndipo shida na matatizo huanzia hapo. ATAKUJA MTU KATIKA MAISHA YAKO ATAKAYEKUFANYA UGUNDUE KWANINI HUKUDUMU NA ULIOACHANA NAO” HII NI SEHEMU YA TANO.


Msisimko wa simulizi ile uliufanya uso wangu upauke kama kipande cha muogo wa kiangazi,niligundua kuwa baridi lilikuwa likipenya kwenye lile dirisha dogo la chumba changu na kunifanya nikakamae, lakini hiyo haikunifanya nichoke kusikiliza, tayari yule msichana Felicity ambaye ni mpelelezi alikuwa ameshagundua kuwa Nancy ndiye aliyefyatua ile risasi, moyoni nikajiuliza
kwanini Nancy afanye hivyo, lakini sikuwa na jibu.
Nilifunga lile dirisha vizuri na kuchomeka makaratasi ili lisifunguke tena na kupitisha baridi
kisha nikachukua ‘headphones’ zangu na
kuchomeka kwenye redio kisha nikaweka masikioni ili nipate kusikia kwa ukaribu zaidi. Na sasa Pamela alikuwa na kibarua kizito cha kueleza Nancy ni nani. Ikawa hivi;

***PAMELA***

“Hapana Nancy hawezi kufanya hivyo, hanasababu ya kufanya hivyo” nilitokwa na machozi
kila nilipokuwa nikimtetea, nilimpenda sana Nancy
japo nilimpenda sana Patrick kuliko mtu yeyote.
“Nancy ni nani” aliuliza Patrick huku akinitazama
kwa jicho kali, sikuwa na la kumjibu kwakuwa
ilitakiwa nitumie mda mrefu kumuelezea kuhusu
Nancy ili anielewa na awe tayari kuyapokea yale
nitakayomwambia.
“Nancy ndiye aliyetenda hili na si mtu mwingine
Pamela” alidakia Felly kabla sijamjibu Patrick swali
lake, nilikuwa nikimtazama Felly na hapo alifungua
tena ile laptop yake na kuendelea kuelezea;
“Nilikuambia mapema kuwa kama mpigaji alikuwa
ni mtu mwenye uzoefu wa kushika bastola basi
asingiweza kumkosa Patrick kwa ile kona aliyokaa
(huku akielekeza kwenye projekta), na kama
angemkosa au kucheza mkono kidogo basi
ingemchubua mkono wake wa kushoto, lakini
haikuwa hivyo badala yake ilipita futi 6 toka
alipokuwa Patrick, kwa maneno mengine mtu huyo
mkono wake ulicheza kutokana na ule mtikisiko wa
risasi ilipokuwa inatoka. Sasa kama ulicheza na
kama alikuwa sio mzoefu basi inamaana mkono
ulishtuka, na kama ulishtuka basi ni wazi kuwa
lazima atakuwa ameufunga mkono kwa sasa”
alivuta pumzi na kufungua tena sehemu nyingine
kisha aliendelea.
“hii hapa ni picha iliyopatikana kwenye kamera za
zahanati ya Hilton, mita mia saba hamsini kutoka
hapa, ilikuwa ni picha iliyonaswa lisaa limoja
baada ya tukiohilo kutokea, itazame kwa makini
huyu ni Nancy, alikwenda siku hiyo akiwa
ameushikilia mkono, na alifungwa bandeji mkononi,
sasa ukiangalia alifungwa mkono wa kushoto hii
inamaana kuwa Nancy anatumia mkono wa
kushoto, baada ya mimi kufatilia juu ya faili la
Nancy katika zahanati hiyo nilikuta limeandikwa
kuwa alianguka kwenye ngazi. Kwenye siku ya
tukio Nancy hakwenda kazini, alikuwa nyumbani
siku nzima kwakuwa siku hiyo haikuwa siku ya
kazi, hii inamaana kuwa kama Nancy alikuwa
hayupo kazini basi angekuwa ameanguka kwenye
ngazi za nyumbani kwake, lakini pia nyumbani
kwake yeye hakuna ngazi fupi wala ndefu hivyo ni
ngumu sana kwa yeye kuwa ameanguka kwenye
ngazi” aliongea Felicity na mimi nilikosa namna ya
kumtetea tena Nancy, ilikuwa wazi kuwa yeye
ndiye aliyehusika.
“Kwahiyo unataka tuliweke vipi hili jambo,
uchunguzi wote nimeufanya kwa siri bila
kushirikisha ofisi hivyo nasubiri uniambie nini cha
kufanya” Felicity aliniweka katika wakati mgumu
sana wa kufanya maamuzi.
“Naomba tuongee nje Felly” nilijivuta pale na
kufungwa taulo langu vizuri kisha nilitoka nje na
Felly nae alitoka.
“Tushughulike na hili swala nje ya ofisi yako,
unajua dhahiri kujaribu kuua ni kosa kubwa sana,
nipe muda niongee na Nancy juu ya hili, sitakuwa
tayari kumuona Nancy akienda jela Felly” niliongea
na Felly huku machozi yakinitoka. Nilifahamu kuwa
nilimuumiza sana Nancy kwa kumwambia kuwa
nisingeweza tena kuwa na yeye kwakuwa
nilimpenda sana Patrick, mimi na Nancy
tulipendana sana na naelewa kuwa alifanya vile
kwakuwa hakuwa tayari kunipoteza. Nancy alikuwa
mtu mzuri sana na mpaka kufikia kufanya vile
inaonyesha kiasi gani alishindwa kuvumilia
maumivu ya nilichomwambia, hivyo huo ulikuwa
muda wangu wa kumfanya aachane na anachotaka
kukifanya.
****
Kazi kubwa niliyokuwa nayo ilikuwa kumueleza
Patrick ukweli wa kila jambo, nilimkwepa sana
lakini kila mara aliponitazama usoni niliona kabisa
deni nililokuwa nalo kwake na sasa niliona ipo haja
ya kumuambia ukweli.
“Patrick nadhani sasa ni wakati muafaka wa
kukueleza kila kitu kuhusu mimi na pia kuhusu
Nancy” nilimwambia huku nikitazama chini kwa
aibu.
“Am listening”(nakusikiliza) alinijibu na kukaa
sawa akinitazama, nilianza kumueleza historia
yangu yote ya kipindi cha nyuma toka udogo
wangu ila nilipofika kwenye kuelezea kuhusu mimi
na Nancy nilisita kwanza nilijiuliza Patrick
atanichukuliaje.
“Nancy ni nani na kwanini atake kuniua” aliniuliza
huku akiwa amenishika mikono yangu kama ishara
ya upole.
“Baada ya hayo yote kunitokea, niliwachukia sana
wanaume, sikuwa na hisia na wanaume. Mbali na
dokta Anderson kujitahidi kunisihi nisahau kila kitu
lakini haikuwa rahisi, hivyo nikiwa kazini kama
daktari kipindi cha mwanzoni, alikuja mgonjwa
aliyekuwa na ugonjwa wa kutokwa na damu
mfululizo, nilitakiwa kumfanyia uchunguzi lakini
nilikuja kugundua kuna dawa alikuwa akimeza
ndizo zilimletea tatizo hilo, hivyo nikalazimika
kumpangia kliniki ili kumpa ushauri nasaha na
kumfanya aachane na zile dawa, nikiwa kwenye
kliniki siku moja yule mgonjwa alikuja na tulikuwa
tumejifungia ofisini kwangu akawa amelala
kitandani kavua nguo zote ili nimfanyie uchunguzi,
alinishika mkono wangu na kuupeleka kwenye uke
wake akawa kama ananisugulia, nilipata msisimko
wa ajabu na siku hiyo ndipo niligundua kuwa
nilikuwa na hisia na mwanamke mwenzangu,
sikuipenda ile tabia lakini taratibu nilizoea na hati
maye nilimfanya yule Mgonjwa kuwa mpenzi
wangu, na ndiye huyu Nancy, nilimpenda sana na
nlijitoa kwake, nikilala kwake na yeye akilala
kwangu na kufanya mambo yote kama wapenzi,
malengo yetu ya yalikuwa motomoto na wote
tulijaliana katika kila hali, siku zote Nancy alikuwa
akinipenda na kuvutiwa na mwili wangu, vivyo hivyo na mimi nilimpenda sana na nilivutiwa na kili
kilichokuwa katika mwili wake” nilivuta pumzi kidogo na kumtazama Patrick aliyekuwa ametoa macho kama vile anaota;
“hali ilikuja kuwa tofauti wewe ulipoletwa pale hospitali, haswa pale Mary alipokuacha na kuondoka zake, nilikuwa nikikuhudumia kwa karibu sana na sikuwa na mtu mwingine wa kumwangalia kwa ukaribu bali wewe tu, nilianza kukupenda taratibu na hisia zangu juu ya Nancy zilianza kupotea na nilianza kumkwepa, nilikuwa nataka kuanza maisha mapya hasa kwakuwa kupitia wewe niliona Tumaini jipya tena hapo hisia juu ya wanawake wenzangu zilikatika kwakuwa haikuwa utamaduni wangu, nilifahamu kuwa nilichokifanya kilikuwa ni kosa hata mbele za mungu lakini sikuwa nikifikiria sawia, hivyo nilitaka kulibadilisha
hilo kwa kuanza tena upya kila kile nilichokuwa nikikiamini, hivyo siku moja asubuhi nilimuita Nancy nyumbani kwangu na hapo nilikuwa na nia ya kumueleza kubadilisha kwangu mawazo juu ya hisia zangu kwake”

******
Ilikuwa majira ya saa nne asubuhi nikiwa najiandaa kwenda kazini, jana yake nilikuwa nimempigia simu Nancy kuwa ningetaka kuongea nae na hapo ilikuwa ni wiki mbili toka mara ya mwisho nilipoonana nae. Wakati niko chumbani nikipaka mafuta mlango ulifunguliwa na Nancy aliingia moja kwa moja bila ya kupiga hodi, alianza kunishikashika na kunibusu kila sehemu huku mikono yake akiipitisha kwenye sehemu zangu za siri, sikuwa na hamu ya kufanya alichotaka lakini kwakuwa nilikuwa ninatafuta njia rahisi ya kumuambia ili anielewa nilijilazimisha na kuanza kumshikashika na yeye, tulianza kufanya tulichokuwa tukikifanya na baada ya kumaliza tulikwenda kuoga na baada ya hapo, Nancy alichukua nguo yangu ya ndani na kuanza kunivalisha, ndipo nilipomshika mkono nakumuomba tuongee.
“Kuna kitu nataka kukuambia Nancy” nilimvuta na kumkalisha chini wakati huo wote tukiwa watupu, alipandisha miguu yake kitandani na kuweka kichwa chake kwenye mapaja yangu na kunitazama.
“Nancy kwenye maisha kuna muda kila mtu
hufanya mambo fulani kwasababu, kila mtu hujikuta katika mkondo mbovu kwasababu tu alitaka mwenyewe au maisha yalimchagulia namna ya kuishi, lakini hayo yote huwa ni matokeo ya bahati mbaya ambayo kuna muda kwa uzembe wetu au kwa kuyaamini yale tusiyoyasimamia tunajikuta tukiyatenda yasiyo mema, nimegundua nilipojikwaa Nancy na ninataka nirudi nyuma nianze upya, sifurahishwi tena na mahusiano tuliyonayo kwani huu sio utamaduni wa mwanamke, hisia zangu kwako zimeyeyuka mfano wa theluji ichemshwayo, nakupenda lakini sitaki tena tuendelee hivi” alinyanyuka baada ya kusikia maneno yale na kuamua kukaa huku akilia.
“haiwezekani mpenzi, siku zote tumekuwa pamoja leo hii unataka uniache kwa kusingizia huna hisia na mimi? Niambie ni nini unataka nikufanyie,unataka nini mpenzi wangu na mimi nitafanya,niambie tafadhali” Nancy aliongea huku akilia kama mtoto, nilimuonea huruma sana lakini huo ulikuwa msimamo wangu na nilikuwa tayari kuusimamia mda wowote.
“sitaki chochote Nancy, umekuwa mtu mzuri sana kwangu na umenionyesha mapenzi ya kweli na mimi nashukuru sana kwa hilo lakini kwasasa yupo ambaye inanibidi niwe naye” nilimueleza kwakujikaza lakini huo ndio ulikuwa ukweli wangu.
“ni nani huyo” aliuliza.
“ni Patrick, yule mgonjwa ninayemuhudumia pale hospitali.
“yani unaniacha kisa yule mfu? Nini kimekupata Pamela,,eehh, unahitajika kupumzisha akili mpenzi,yani yule mtu amekaa miaka na miaka hajaamika,mtu anayetegemea kufa muda wowote ndo akuchanganye kisi hicho kweli?” kabla hajamaliza kuongea tayari alikuwa ameshanichefua kumuita Patrick mfu.
“ishia hapohapo Nancy, vaa nguo zako ondoka sitaki kukuona, nampenda sana huyo unayemuita mfu, hivyo nakuomba wewe uondoke hapa”
nilimsukuma na kuchukua nguo zangu kisha nilikwenda kuvalia nguo sebuleni.
“Pamela naomba unisamehe sikuwa na maana ya kukuudhi mpenzi wangu, naomba unielewe”
alinifata huku akinishika na kujaribu kunituliza.
“Nimekuelewa Nancy ila mimi na wewe basi, sitaki tena usagaji, siko tayari tena na nina uhakika kama wazazi wangu wangekuwa hai wangeniua kwa hili, nampenda Patrick huo ndio ukweli mpya ambao inabidi mimi na wewe tuwe nao kichwani na tujue kuwa mambo yameishia hapo” nilimuambia hivyo na kuondoka pale sebuleni nikamuacha akilia, nilichukua vitu vyangu na nilipofika pale sebuleni nilisimama na kumtazama.
“Nancy hakuna jinsi inabidi ukubaliane na hilo nililokuambia kwakuwa hakuna suluhu zaidi ya wewe kukubali, tafadhali nyanyuka tuondoke nataka nifunge nyumba yangu. Hapo ndo ilikuwa mwisho wa mapenzi yangu na Nancy.

***********
Yalikuwa matarajio yangu kuwa Patrick angekuwa mkali na pengine angeweza hata kutaka kuondoka na kuniacha lakini hali ilikuwa tofauti kabisa,baada ya kumueleza ukweli wa kila jambo Patrick alinivuta na kunikumbatia.
“usijali kila mtu anahistoria mbaya katika maisha yake, lakini ikitokea ukajua unapokosea na kuamua kujirudi na kujirekebisha basi hiyo ni faraja ndani ya moyo wa kila mmoja aliyechukizwa na tabia yako ya awali, hivyo usiwe na hofu, nenda kanisani katubu zambi zako na mungu atakusaidia, ila ipo haja ya kuongea taratibu na Nancy, na mimi ndiye nitakwenda kuongea nae” nilishtuka kwakuwa sikutegemea awe mpole kiasi kile lakini kilichonichaosha ni pale aliposema kuwa anataka kuongea na Nancy.

**SIKU MBILI MBELE**
Jioni tukiwa tumetoka matembezini Felicity alinipigia simu na kunitaarifu kuwa alikuwa ameshakamilisha uchunguzi kuhusu ajali aliyoipata Patrick miaka zaidi ya sita iliyopita, hivyo aliniambia twende mimi na Patrick nyumbani kwake kwakuwa ndiko kuna vifaa anavyoweza kutumia kutuelezea.
Tuliondoka hadi kwa Felicity na tulipofika kwake alitukaribisha kisha tukakaa kwa muda kidogo wakati yeye akiwa ndani na baadaye alituchukua na kutupeleka kwenye chumba fulani kama darasa dogo kisha aliwasha kompyuta kubwa iliyokuwaukutani na kama kawaida yake alianza kuelezea.
“nilianzankufanya uchunguzi juu ya ile ajali kwa kufatilia wale trafiki waliokuwa wakifatilia ile kesi,sikuile wakati ile ajali inatokea inaonekana njiani kulikuwa na ile gari iliyosababisha ajali kwa zaidi ya masaa mawili ikifanya doria njia ile, mazingira ya ajali yanaonyesha kuwa ile ilikuwa ajali ya kupangwa, swali ni je nani alipanga ajali hiyo? Na majibu ni kwamba, toka Patrick aje huku kulikuwa na mawasiliano yakifanyika kwenye mgahawa wa Roshan uliopo chini ya hoteli aliyofikia,mawasiliano hayo yalikuwa yakifanywa kati ya mtu anayeitwa George mwenye namba yenye code namba +255 ambayo ni ya nchini Tanzania na Mary ambaye ndiye mkeo uliyekuwa naye.Mawasiliano hayo ambayo tumefanikiwa kuyapata yalikuwa yakifanyika kila siku kati ya saa 9:45 na10:34 usiku. Mawasiliano hayo yalikuwa ya aina nyingi, kuna siku walifanya mawasiliano ya simu na kuna kipindi waliwasiliana kupitia barua pepe.Maongezi hayakuwa wazi kwakuwa walikuwa wakiongea katika lugha ambayo waliijua wao wenyewe, lakini tulichofanikiwa kukijua ni kwamba mawasiliano haya kila mara yalitaja kampuni iitwayo PATRIMARY, na pia kuna barua pepe moja ilikuwa ikiuliza aina ya jina jipya ambalo lingefaa kuwa mbadala wa lile la mwanzo, na katika majibu ya Mary pamoja na mambo mengi anamtaarifu George kuwa jina mbadala ni GEOMARY. Baada ya siku tatu toka wafanye mawasiliano hayo, George alituma ujumbe kwenye simu ya Mary akimtaarifu kuwa tayari ameshafanikiwa kubadilisha na akamwambia sasa anaweza kuingia kwenye tovuti ya www.geomary.co.tz kuangalia kama mambo yote yalikuwa sawa, tulichogundua ni kwamba wakati huu walikuwa wakiandaa tovuti kwaajili ya kazi waliyokuwa waifanye baadaye. Siku ya tukio la ajali magazeti ya nchini Tanzania yaliripoti juu ya ajali ile na waliambiwa kuwa hali ilikuwa mbaya
sana, lakini baada ya Mary kuondoka huku na alipofika Tanzania aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kuelezea kuwa mumewe alifariki na
kupotelea baharini wakati wakiwa wanamuhamisha kutoka Fiji kwenda Suva ambapo ndege yao ilipata
ajali na kuangukia baharini ila yeye Mary alipona.Waandishi walilipwa ili kuandika habari hiyo na baada ya wiki mtu anayeitwa wakili Mrutu
aliwasilisha maombi mahakamani akiiomba
mahakama ipokee wosia wa marehemu yaani
Patrick alioandika na kuuweka kwa huyo
mwanasheria juu ya nani amiliki mali za
marehemu. Wosia uliwataja watu wawili tu ambao ni Mary na George, na baada ya mahakama kupokea waliamuru wahusika wapewe mali zile.Majina ya kampuni na mali nyingine yalibadilishwa,na cha kushangaza miezi 9 mbele Mary alijifungua,upelelezi unaonyesha George alifunga ndoa na Mary miezi michache baadaye, hii inamaana kuwa
mimba hii Mary aliipata siku alivyokuwa ameshukaTanzania.”
“unasemaje? Mimba?” nilimuona Patrick akishtuka kwa kuhamaki.


NINI SABABU YA YOTE HAYAAAA???.........JE UPI
MWISHO WA PATRICK NA PAMELA?
KWANINI FELICITY ANAJITOLEA SANA KUFANYA
KAZI HII KWA PAMELA??
FATILIA SEHEMU ITAKAYOFUATA
 
Sehemu ya Sita

Kwa Mary Robert.2010
“Kwa mwanamke kuwa na furaha katika mapenzi
unahitaji kupata mtu mnayependana,,mtu
atakayejali sana furaha yako kuliko yake,,mtu
atakayekuwa wa mwisho kukufanya ulie,,mtu
ambaye atakupa kila unachostahili, atakayejitolea
muda wa maisha yake kuishi na wewe kama
mkewe,,mkweli, muaminifu,,mtu asiye na tamaa,
mtu makini katika kufikiri na ajuaye anachohitaji
mwanamke,,mtu pekee ambaye atajisikia fahari
kuwa na wewe popote na kulitetea penzi lenu kwa
namna yoyote ile,,MWANAUME ANAYEKUPENDA
KULIKO WEWE UNAVYOMPEDA. Hawapatikani
kirahisi ila tu ni KAMA WEWE NAWE UTAKUWA
UNAVIGEZO UVITAKAVYO….KUWA SEHEMU YA
MABADILIKO UYATAKAYO” HII NI SEHEMU YA SITA ANDIKA HIVI

Simulizi ilikuwa imeushika moyo wangu kiasi fulani,
mara ghafla nikiwa bado nasikiliza, niliona giza
nene na kimya cha hali ya juu kilitanda, sauti
niliyokuwa nikiisikia ilikuwa ni ya magari tu
yaliyokuwa yakisikika kwa mbali sana huko
barabarani.
“aaaahhh hii nchi hii” nilijisemea moyoni na kubaki
nikitafakari mwenyewe juu ya yale niliyoyasikia,
nilishangaa sana juu ya alichokifanya Mary lakini
bado nilikuwa na maswali mengi sana ambayo
sikuwa na majibu nayo.
“huooooooo” niliropoka kama mwehu vile nilioona
taa zinawaka tena, haraka niliwasha kile kiredio na
kuchomeka headphones ili nilisikilize, nilipoweka
masikioni nilikuta
Patrick akisimulia.


***PATRICK***

Nilikuwa nimelowa kwa hofu na kutokuamini ukweli
wa mambo yaliyokuwa yanatokea hapo, haikuwa
rahisi kuamini kuwa msichana niliyempenda kwa
maisha yangu yote leo hii alikuwa ndiye adui
wangu, pengine ni ndoto, hilo lilikuwa ni jambo
pekee nililowaza ambalo halikuwa kweli, vitu
vilikuwa vinatokea na ukweli ulikuwa umejulikana.
Swali kubwa nililojiuliza ni kwanini basi Mary
afanye hivyo wakati tayari alikuwa ni tajiri pia na
mwenye pesa nyingi.
“Patrick” nilishtuka toka katika msongo wa
mawazo na kukurupuka.
“Naam” ilikuwa sauti ya Felly.
“Usiwaze sana kila kitu kitajulika na kila mtu
aliyeshiriki kukufanyia chochote atafahamika,
nitakusaidia kwenye kila hatua, lakini nakuomba
sana usiende nchini kwenu hivi karibuni mpaka
mipango yote iwe imefahamika, tutahakikisha
unaondoka hapa ukiwa unajua kila kitu” aliongea
Felly huku akinitazama.
“ asante sana Felly, mungu atakulipa” nilimwambia
na yeye alinisogelea na kunikumbatia.

**WIKI TATU MBELE**

“Majina yako kamili ni nani” aliuliza yule dada
mwenye asili ya Asia.
“Patrick Mfangavo” nilimjibu huku nikimtazama
kwa makini.
“unatatizo lolote kaka, naona kama hauko sawa?”
aliniuliza kama vile aliisoma akili yangu.
“Hapana niko sawa” nilimjibu huku nikitabasamu
kama njia ya kumuonyesha kuwa tuko pamoja.
“Unakumbuka nimekuuliza maswali mangapi?”
aliniuliza huku akinitazama usoni bila chembe ya
aibu. Niliwaza kwa muda na kujibu japo sikuwa na
uhakika wa jibu.
“matano” nilimjibu na hapo alitizama chini kisha
alipoinua macho alinisemesha tena.
“Kaka naweza kujitolea muda wangu kukusaidia
wakati mwingine kama leo hujisikii vizuri, hizi fomu
ni za uhamiaji, zinahitajika kujazwa kila kitu kwa
usahihi ila kwa hali uliyokuwa nayo hatutaweza
kuelewana sana hapa” alinisemesha kwa upole
sana lakini nilisisitiza kuwa nilikuwa sawa.
“Nimekuuliza maswali nane na umejibu yote ila
maswali matatu umekosea, moja ni nchi
uliyozaliwa, mbili ni muda wako uliokaa Fiji na tatu
ni kama umeoa au la” aliniambia na mimi
niligundua kuwa ni kweli kabisa kuwa nimekosea.
Sikuongea chochote nilinyanyuka na kuondoka.
Nilimpigia simu Pamela kuwa nitachelewa siku
hiyo kwakuwa nilitaka kuwa mwenyewe, nilipofika
nje niliingia kwenye gari na kisha nilianza
kuendesha kuelekea nisipopajua, sikuwa na leseni
lakini nilipewa ruhusa ya kuendesha huku
wakinitengenezea leseni nyingine. Umbali wa
kilomita kumi nilikuta sehemu kuna uwanja wa
mpira na watu walikuwa wakitizama mpira pale,
ilikuwa ni majira ya saa 12 jioni na mimi nikaamua
kuungana na wale watu kutazama mpira ule
mpaka saa moja jioni nilipogeuza na kwenda
kwenye hoteli maarufu iliyoko juu ya mlima wa
Penvisk, nilinunua pombe chupa kubwa na kuinywa
kisha nilipanda juu kabisa ya hoteli hiyo ambapo
ulikuwa ukisimama unaona Fiji yote. Mandhari
yakuvutia ya eneo lile ilinifanya nikumbuke sana
hotel ya Ngurdoto iliyopo nchini Tanzania, katika
kipindi cha mwanzo kabisa cha mapenzi yangu na
Mary tulienda katika hii hoteli kutembea na tulikaa
kwa muda wa siku nne kabla ya kurejea jijini, ni
siku hii ambapo Mary alinieleza mipango yake
mingi ya kimaisha, lakini moja ya mpango wake
mkubwa ulikuwa ni kufunga ndoa na mimi, hii
ilinitoa mchozi sana nilipoikumbuka. Lilikuwa ni
pigo kubwa sana kwa Mary kuniacha peke yangu
tena bila kujua ninini sababu ya kufanya hivyo.
Nilisimama pale na kulia sana.
“maisha hayanyooki siku zote, unatakiwa uwe
imara mda wote kukabiliana na kila linalotokea
pale litakapotokea” ilikuwa sauti ya msichana,
ilinishtua nikaangalia pembeni yangu alikuwa
amesimama msichana mwenye umbo dogo
aliyekuwa naye akitizama kule nilikokuwa
nikiangalia mimi, hakugeuka kuniangalia kama
nilikuwa namuangalia.
“Wewe ni nani?” nilimuuliza kabla ya yeye kugeuza
kichwa na kunitazama.
“Naitwa Khajat Kapur” alinitajia jina lake na kunipa
mkono huku akitabasamu, nilipomtazama vizuri
alikuwa yule afisa uhamiaji aliyekuwa akinihudumia
muda wa mchana.
“Umekuja kufanya nini hapa”nilimuuliza huku
nikiendelea kutazama mbele na yeye akiwa
ameegemea chuma nililokuwa nimeweka mikono.
“Nimekuja kutembea tu, hii ni sehemu ambayo
watu wengi wajisikiao upweke huja na kukaa”
aliongea hayo na kimya kidogo kilitanda kisha
alianza kuongea tena.
“Kwanini unataka nafasi ya kufanya kazi Fiji”
alianza kuongea tena.
“kwani ni vibaya” nilimuuliza kwa mshtuko.
“sio vibaya nimeuliza tu” alinitazama kisha alitoka
pale na kutembea mpaka mbele kulikokuwa na kiti
kisha aliketi na kuniita.
“Nataka kukupa kazi” aliniambia huku akinitazama
usoni.
“Sihitaji kazi” nilimjibu huku nikiwa naketi kwenye
kiti.
“vizuri ila uwe na uhakika kuwa hauhitaji kazi”
aliniambia na kunyanyuka ili aondoke ila
nilimkamata mkono na kumsukuma mpaka ukutani
kisha nilimkaba huku nikimlazimisha aniambie
anataka nini kwangu.
“utaniumiza, tafadhali niachie” aliongea sauti ya
kinyonge kisha nilimuachia.
“Patrick unahitajika kubadilika kabisa, hii ni Fiji,
huwezi kufanya kazi na watu wa huku kama
utakuwa huna namna ya kujua kuishi nao.
Punguza hasira na upunguze mawazo, kila kitu
kitakuwa sawa.
“wewe ni nani?” nilimuuliza tena.
“mimi ni rafiki yake na Felly, yule dada aliyekuleta
ofisini kwangu mchana wa leo” alinijibu na hapo
nguvu ziliniishia kwakuwa nilihisi sikuwa
nimemtendea haki kuwa mkali kwake.
“samahani” nilimuambia huku nikinyanyuka na
kurudi kule nilikokuwa nimesimama mwanzoni,
nilisimama pale bado machozi yakinitoka na
sikujua kwanini, alikuja taratibu na kunifata pale
kisha alisimama pembeni yangu kisha alinitazama
na kunishika bega.
“kuna mwisho wa kila jambo Patrick” aliniambia na
kunipa bahasha kisha aliondoka. Niliitazama ile
bahasha lakini sikuwa nafahamu nini kilichopo
ndani, nilitoka mpaka kwenye taa na kufungua,
nilichokikuta ilikuwa ni furaha yangu kubwa.
Nilishuka mpaka kwenye lift nikaingia ndani lakini
nilipofika pale chini sikumuona. Nilirudi kwenye
gari yangu na kuingia ndani kisha nilitazama zile
karatasi vizuri, zilikuwa ni ruhusa ya mimi kufanya
kazi kama nilivyokuwa nimeomba, niliwasha gari
na kuendesha kwa haraka sana na baada ya muda
fulani nilikuwa nimefika nyumbani.
“Ulikuwa wapi Patrick, umenifanya nikae na
wasiwasi muda wote” aliongea Pamela ambaye
nilikuwa nimemkuta pale nje akiwa amekaa.
“lakini sinilikuambia kuwa nitachelewa kurudi”
nilimuambua huku nimemshika mashavu yake na
kumbusu, kisha nilimkumbatia na kukumbuka
kipindi nikiwa na Mary.
“Twende ndani Pamela” nilinyanyua ile glas yake
ya mvinyo na kuondoka nayo ndani.
“Tukaoge” aliniambia huku akitabasamu na mimi
nilivua nguo na kwenda kuoga nae.

**MWEZI MMOJA MBELE**

Tayari nilishaanza kufanya kazi kwenye kampuni
ya ANDERSON CONSULTANCY baada ya
kufanikiwa kuifungua anuani yangu ya barua pepe
na kuchukua vyeti vyangu nilivyokuwa nimewahi
kumtumia mtu, nilifanya kazi kama afisa
maendeleo na mshauri wa mambo ya ujasiriamali.

*******
“Halooo,,Haloooo, Halooo, mbona huongei,,haloo”
sikuweza kuongea nilijikuta machozi yakinitoka,
nilikata simu na kuanza kulia nikiwa pale ofisini,
ilikuwa ni sauti yake kabisa, ile namba ilikuwa ni
ya ofisi yao niliitoa kwenye ile tovuti aliyoitamka
wakati akiwasiliana na yule jamaa.
“Hey Mbona unalia Patrick” nilishtushwa na sauti
hiyo na alikuwa ni Felly.
“hamna niko sawa” nilimuambia huku nikifuta
machozi.
“hauko sawa Patrick, umepiga simu kwa Mary si
ndio” aliniuliza na sikuwa na namna ya
kumdanganya bali kukaa tu kimya. Alinichukua
pale na kuniomba akaninunulie chakula cha
mchana na mimi nilikubali tukaondoka pale na
kuelekea kwenye mgahawa uliokuwa karibu na
pale kazini.
“Patrick kuna mtu anaitwa Drew Barrymore aliwahi
kusema, ‘nafikiri furaha ndiyo humfanya mtu kuwa
mzuri, watu wenye furaha ni wazuri, Patrick maisha
ni leo, kesho ni majaaliwa. Unatakiwa ufanya
maamuzi ya kukufanya uwe na furaha sasa hivi,
unatakiwa uanze upya na ukubali kuwa mambo
yametokea na sasa uangalie mbele zaidi. Utalia
kila siku na utajikuta upo palepale katika maisha
yako. Fanya uamuzi sasa na uwe na furaha
Patrick” yalikuwa maneno ya msingi na ya
kunifariji yaliyotoka kinywani mwa Felly, sikuwa na
la kusema zaidi ya kulia.
“Uko sahihi Felly nitafanya hivyo” nilimjibu na
kukumbuka kitu fulani.
“Naomba unielekeze nyumbani kwa Nancy”
nilimuomba huku nikishika mikono yake miwili kwa
maana kuwa sikutaka anikatalie.
“sawa, anuani yake ni MDSK 234 Pentagone street,
nakuomba uwe makini, kama aliweza kukuvizia
akajaribu kukuua hatashindwa kukufyatulia risasi”
niliitikia na kumshukuru.

**JIONI YAKE**

Baada ya saa za kazi niliondoka mpaka kule
nilipoelekezwa na baada ya kufika pale kwa Nancy
niligonga mlango na hapo niliruhusiwa na
mfanyakazi wake kisha niliingia na nilipofika
sebuleni nilikutana nae uso kwa uso.
“habari yako Nancy” nilimsalimia lakini hakujibu
badala yake alianza kutetemeka lakini baada ya
mabishano ya muda mrefu sana nilifanikiwa
kumtuliza na tulikaa chini tukaongea.
“Nancy najua jinsi unavyompenda sana Pamela,
nafahamu sana mahusiano yenu na Pamela
amenieleza kila kitu lakini tafadhali nakuomba
sana, heshimu maamuzi yake na pia mimi sina
uadui na wewe, mimi sijakufanya chochote, huna
sababu ya kuniwinda kama njiwa, nina mengi sana
yanayonisibu na roho ya subira kwasasa sina ndio
maana nakuomba uache kuniwinda, umenikosa na
risasi, leo pengine ningekuwa marehemu lakini
nashukuru kuwa niko hai, hivyo kaa mbali na mimi,
nakuonya tu kwakuwa mimi sio mtu mzuri sana
kwa sasa” baada ya kumuambia maneno hayo nili
nyanyuka na kutoka nje kisha niliondoka kurudi,
nikiwa njiani kwa zaidi ya kilomita moja niliona
kuna gari ilikuwa ikinifatilia, nilikatiza na kupaki
sehemu kisha nayo ilikuja na kupaki, nilipotazama
ndani ya ile gari alikuwa ni Pamela alinipa ishara
ya kwamba nimfate na hapo niliingia tena kwenye
gari na kumfata nyuma mpaka tulipofika
nyumbani. Tuliingia ndani na tulipofika tu
hakukuwa na maongezi Pamela alinishika na
kuanza kunibusu huku na kule alifanya hivyo na
baada ya kumaliza alinipa makaratasi aliyokuwa
ameshikilia mkononi, niliyachukua na kuyasoma
kwa makini nikahisi kuchanganyikiwa,
“hii ni nini Pamela” nilimuuliza huku nikimtazama.
“nina mimba ya wiki tatu Patrick” aliniambia huku
akirukaruka. Ilikuwa furaha kwake ila kwangu
ilikuwa ni tofauti, sikuzijua hisia zangu kwake,
sikujua ni nini nilitaka kutoka kwake.
“Patrick najua kabisa akili yako haijatulia najua
pengine hukulitegemea hili, ila usijali nitalea
mimba na mtoto pia, usijali mana naona umekosa
raha” furaha yake iliisha ghafla na kuniambia hayo
huku akiondoka na machozi yakimtoka. Lilikuwa ni
jambo la kunishtua nililokosa maamuzi nalo,
ilitokea haraka sana na sikulitegemea hasa kwa
wakati kama ule.
Nilimfata Pamela ili niweze kuongea naye lakini
hakuwa tayari kuongea, alikuwa ameshakasirika na
mlango wa chumbani ulifungwa.
Nilirudi mpaka sebuleni na kuamua kukaa pale
mpaka usingizi uliponipitia.

*****
Kesho yake asubuhi Pamela alitoka chumbani na
kunipita nikiwa pale sebuleni lakini nilimzuia na
kumuomba niongee nae.
“Patrick umeniudhi sana” aliniambia hukua akilia.
“najua Pamela, nafahamu kuwa natakiwa
kusimama kama mwanaume, lakini pia unatakiwa
ujue kuwa kwasasa siko sawa kabisa, akili yangu
haijatulia na nina mengi ninayoyafikiria, lakini
nitakuwa bega kwa bega kuhakikisha kuwa tunalea
mtoto huyo, nisamehe sana kwa nilichofanya”
nilimuomba msamaha kwa unyenyekevu na yeye
alisogea na kunikumbatia.
“basi Patrick nenda kaoge kisha tuongozane”
niltoka pale na kwenda kujiandaa na baada ya
muda mfupi nilikuwa tayari na kurudi mpaka
sebuleni nikamkuta Pamela na Felly.
“mambo Patrick” Felly alinisalimia huku
akitabasamu, alikuwa amevaa sare zake za kazi
zilizomfanya aonekane mzuri na mwenye
kupendeza japo ile bastola aliyokua ameiweka
kiunoni ilimfanya aogopeke, mwili wake mzuri
uliokuwa umeenda hewani kama wasichana wa
Kinyarwanda ulimfanya aonekane mkakamavu na
asiyeweza kuzoeleka, alikuwa amebana nywele
zake na kuvaa kofia iliyoruhusu nywele zake
kutokeza vizuri na kuupamba uso wake.
“safi umependeza” nilimjibu na kushindwa kujizuia
kumsalimia.
“asante, mimi nimekuja kuna kitu nataka
kuwafahamisha kuhusu uchunguzi ninaoendelea
nao kuhusu Mary” alituambia na wote tulikaa
kimya ili kumsikiliza.
“okey tunakusikiliza” nilikuwa wakwaza kudakia.
“ tuanzie pale tulipoishia” alianza kuwasha
kompyuta yake na kisha alianza kuelezea.
“Kipindi Mary alipotoka na kwenda Tanzania na
kufanikiwa yeye na George kubadilisha jina la
kampuni na baadaye walifunga ndoa kabla ya Mary
kugundulika kuwa anamimba, taarifa zilizoandikwa
kwenye magazeti kipindi kile zilikuwa nyingi sana
lakini kati ya hizo ni taarifa juu ya maisha ya Mary
baada ya kufika nchini Tanzania, kuna muandishi
mmoja wa gazeti la kingereza alimuhoji Mary juu
ya maisha baada ya kufiwa na mumewe,
inaonekana dhahiri kuwa Mary alieleza kuwa
mumewe amedariki. Sehemu ya mahojiano hayo
inasomeka hivi;
Mwandishi: Maisha yako bila mumeo unayaonaje.
Mary: (analia) ni magumu sana, mimi na mume
wangu tulikuwa zaidi ya marafiki, tulikuwa ni
wapenzi na mapatna katika biashara zetu, yeye
ndiye aliyekuwa kioo katika maisha yangu na yeye
ndiye alikuwa kila kitu, lakini kuna muda lazima
mambo yatokee ili mipango mingine ifanyike.
Mwandishi: je ni juhudi gani ulizifanya baada ya
ndege ile kudondoka baharini iliyokuwa imembeba
mumeo ambaye muda mrefu nyuma tulielezwa
kuwa alipata ajali akiwa huko.
Mary: nikishirikiana na mamlaka za kule nilifanya
utaratibu wa kumtafuta lakini walisema kwa hali
ya baharini si rahisi kumuona.
Mwisho wa kunukuu,,sasa angalia mahojiano
mengine aliyofanya na kituo kimoja cha radio,
aliulizwa hivi;
Mtangazaji: Unawezaje kuendesha biashara zako
mwenyewe kwa sasa.
Mary: ni ngumu sana bila mume wangu , lakini
kuna muda lazima mambo yatokee ili mipango
mingine ifanyike. Lakini mume wangu alikuwa mtu
wa kuchukua tahadhari siku zote, hivyo aliacha
utaratibu wa namna mambo yatakavyokuwa iwapo
atakuwa amefariki.
Mtangazaji: ni kwanini umeamua kuolewa mapema
hivi tena na mtu wa karibu kabisa wa mumeo?
Mary: Yalikuwa maelekezo ya marehemu mume
wangu kuwa niolewe na mwanaume ambaye
niliyeolewa naye sasa” Felly alimaliza kuelezea
hayo na mimi nilianza kujisikia kizunguzungu lakini
sikuweza kufanya chochote zaidi ya kumsikiliza.
“hapa kuna kauli inajirudia mara kwa mara kwenye
karibu mahojiano matano aliyowahi kufanyiwa
maneno hayo ni ‘lakini kuna muda lazima mambo
yatokee ili mipango mingine ifanyike’, haya
maneno amekuwa akilitumia mara kwa mara. Pia
kuna mahojiano ambayo huyo George amehojiwa
na yalikuwa hivi;
Mwandishi: marehemu alikuwa mtu wako wa
karibu sana, vipi uendeshaji wa miradi yake bila
yeye na ukiwa kama mume mpya sasa wa mke wa
marehemu unajisikiaje kwamba marehemu alipenda
wewe uwe mume wa mke wake iwapo siku moja
itatokea amefariki.
George: ni pigo kubwa sana lakini najitahidi sana
kufanya yote aliyoelekeza kwenye maandiko
machache aliyoyaacha, na mimi kuwa mume wa
mke wa marehemu naona ni njia ya kumuenzi
ndugu yangu.
Sasa kwa nilivyopitia kila kitu kuhusu mahojiano
haya yote na kila aina ya ushahidi uliojitokeza
nilikuja kugundua kuwa mlipofunga ndoa kisha
mkaja huku ndipo hili jina la George lilipoibuka,
huyu mtu alienda kuomba mahakamani kubadilisha
jina lake na baada ya muda fulani jina lilikuwa
limebadilishwa, na muda wa dakika tano atakuwa
akiongea na kipindi cha business times
kinachorushwa na SECURE TV ya nchini Tanzania
kupitia satellite yeye akiwa kama mmoja wa
wamiliki wa makampuni makubwa ya kibiashara”
hofu ilinitanda kutokana na yale aliyoyaongea Felly
lakini haraka nilishika rimot na kuanza kupekua
mpaka nilipoipata ile stesheni kisha mahojiano
yalianza kuonekana, nilipotumbua macho
mtangazaji alimtangaza mkurugenzi wa kampuni
ya GEOMARY, niliisogelea kwa karibu sana TV na
ndipo nilipogundua kuwa alikuwa ni MARK..
“Ohh hii haiwezekani” nilinyong’onyea huku
nikijisemea na hapo Felly alianza kuongea tena.
“inawezekana na imeshawezekana,,Mdogo wako
Mark alikuwa ndiye George aliyeshiriki kwenye kila
hatua, alibadilisha jina ili kuficha kila kilichotokea,
mpango huu unaonekana ni wa muda mrefu sana
lakini bado sijajua madhumuni ni nini na nini
maana ya maneno aliyoyasema Mary”

JEEEEEEEE NINI KITAFUTAAAAAAAAAAAAAAA??
 
Sehemu ya Saba

Kwa Mary Robert.2010
“Kitu pekee kidogo na cha thamani unachoweza
kufanya katika maisha yako ni kutafuta nini
unachokitumainia, na kikubwa unachoweza kufanya
ni kuishi ndani ya matumaini hayo. Sio tu
kuyakubali kwa mbali ila kuyaishi kwa undani
wake. Matumaini yanaweza kuwa nguvu kubwa
yenye msukumo. Inawezekana kabisa kusiwe na
miujiza ndani yake, ila ujuapo unachotumainia
sana na ukakikumbatia kama mwanga ndani yako
basi unaweza kutenda jambo na kuyafanya mambo
yatokee kama miujiza…yafanye matumaini yako yaishi..JUKUMU MOJA WAPO LA BINADAMU NI KUFIKIRI KWA NIABA YAKE MWENYEWE” HII NI SEHEMU YA SABA.

**PATRICK**

Nilikuwa nimechanganyikiwa kabisa lakini kitu
pekee kilichonipa ahueni ni matumaini. Nilikuwa
bado nina matumaini ya kuishi na kupata vitu
vyangu kwa gharama ya damu ya mtu au kwa
gharama yeyote ile. Niliendelea kuangalia kile
kipindi jinsi ambayo Mark alijitutumua kuelezea juu
ya kampuni hiyo ambayo yeye ni mkurugenzi.
Sikujua ilikuwaje mpaka ikatokea hayo yaliyotokea.
Nilichokuwa nakumbuka ni kwamba mimi na Mark
tulikubaliana sawia kabisa kuwa hakuwa na
mahusiano na Mary na kwamba Mary hakuwa
anampenda. Nilikuwa sijui kama walikuwa na
mpango mwingine wowote juu yangu. Haikuwa
rahisi hata kuamini kuwa mambo yalikuwa
yakitokea sasa,
“Kampuni yangu imepiga hatua kwasasa na mimi
pamoja na mke wangu tunategemea baada ya yeye
kujifungua hivi karibuni tutaanza kufungua matawi
mapya huko Kenya na Burundi pamoja na
kuboresha matawi yetu hapa nchini. Hii itakuwa ni
hatua kubwa kwetu lakini pia kwa huduma zetu
kama kampuni ya GEOMARY, lakini hatua kubwa
sana kwangu pia katika kuyafanya mambo
yatokee. Kubadilisha taswira na muonekanao wa
yaliyofichika juu ya mafanikio ndiyo nguzo na
shabaha ya maisha yangu sikuzote katika kuleta
kwa ukaribu yale niliyopanga kwa muda mrefu”.
Hayo yalikuwa maneno ya Mark pale alipokuwa
akielezea juu ya mipango ya kampuni yake.
“hapohapo, embu angalia hapo inarekodi bado”
alidakia Felly aliyekuwa akirekodi yale
mazungumzo pale kwenye TV na Pamela
alimwambia ndiyo ilikuwa inarekodi. Tuliendelea
kuangalia kile kipindi na sasa Mark aliambiwa
aseme chochote anachotaka kuifahamisha dunia.
Alisema hivi.
“Katika kufanikiwa lazima vijana wajipange vyema,
kila mtu ananafasi ya kuwa vile atakavyo, haijalishi
njia atumiayo ilimradi upo ukweli wa kila jambo
basi mafanikio huja tu pale unapoamua kufanya
mambo magumu kuwa mepesi, unapoamua
kulitazama jua kwa ukali wake na kufumbua
macho pale usiku unapokujia, kufanya
yasiyotarajiwa na kuwa na roho yenye uwezo wa
kujaribu jambo jipya siku zote. Usiogope lawama
kama unataka kufanikiwa, hayo ndiyo
yaliyoniwezesha kufika nilipo. Vyombo vya habari
ni muhimu sana.” Alimaliza na hapo walishikana na
mtangazaji,,,mahojiano haya yalifanyika kwa lugha
ya kingereza, baada ya yale mahojiano kuisha
Felly alikwenda kwenye kile kifaa cha kurekodi na
kuichezesha tena kisha alishika rimoti na
kutuambia tusikilize kwa makini upya.
“sikiliza alichokisema hapa ‘Hii itakuwa ni hatua
kubwa kwetu’, anamaanisha nini hapa? Ukisikiliza
kwa masikio na mtazamo wa kawaida utaona
kama vile ni maneno ya kawaida ila hii ni ishara
ya jambo fulani, kati ya Mary na Mark kuna mmoja
atakuwa si mtu wa kawaida” aliongea Felly huku
akijaribu kurudia yale maneno tena.
“Ni hatua kubwa kwa maana ya kwamba, biashara
yao inakuwa na mtaji pia unakuwa” nilijaribu kutoa
yale niliyoyafikiria lakini hata hivyo Felly
hakuyasikiliza badala yake aliichezesha tena yale
maneno na kuniambia nitazame vidole vya Mark
na midomo yake alivyokuwa akitamka maneno
yake,,alikuwa akisugua vidole na midomo yake
ilionekana kama vile ilikuwa ikieleza kwa
kutetemeka kwa mbali pale alipoikuza ile picha.
“hii inamaana Mark hana uhakika na maana halisi
ya maneno anayoyasema, kuna kitu anamaanisha,
kama ingekuwa anamaana hiyo ambayo Patrick
umeisema basi asingesema tena mbeleni kuwa
‘lakini hatua kubwa sana kwangu pia katika
kuyafanya mambo yatokee’, hapa anamaana kuwa
kuna mipango miwili, tazama mshipa wa damu wa
kichwa wa upande wa kulia alipokuwa akitamka
maneno hayo, utagundua ulikuwa umetokeza sana
kuliko alipokuwa akitamka akiwa anasema ni hatua
kubwa kwao, hii inamaana maneno ya pili aliyatoa
kwa hisia za hasira” aliongezea Felly huku
akiendelea kuichambua ile video, alikuwa makini
kweli na mimi sikuwa na la kuongea.
“Sikiliza tena hapa anasema ‘haijalishi njia
atumiayo ilimradi upo ukweli wa kila jambo basi
mafanikio huja tu pale unapoamua kufanya mambo
magumu kuwa mepesi’ hapa inamaana
anahalalisha njia aliyoitumia kuwa tajiri, hili jambo
walipanga muda ila inaonekana Mark anampango
wake mwingine zaidi ya huo wa pamoja, kwenye
sentensi hii ameongea mambo yasiyo na uhusiano
ila ni katika kufikisha ujumbe, anasema anasema
‘ilimradi upo ukweli wa kila jambo’ alaf anasema
bas mafanikio huja tu pale,,,,anaendelea, ukweli ni
upi hapo anaousema je kuna uhusiano gani kati ya
hayo aliyoyasema?” nilikuwa nimeshachoka mwili
na roho mpaka dakika hii, mambo kwangu
yalikuwa ni kawaida ila kwa aliyokuwa akiniambia
yalikuwa mambo mazito na ya kuchosha. Nilijaribu
kurudisha akili yangu nyuma japo kujua ni wapi
Mary au Mark aliwahi kufanya jambo la kunitia
wasiwasi lakini sikuona.
“sikiliza hapa alivyosema tena ‘unapoamua
kulitazama jua kwa ukali wake na kufumbua
macho pale usiku unapokujia’ alikuwa anamaana
si rahisi kulitazama jua au kufumba macho usiku
wakati unatembea,,hii ni ishara kuwa unatakiwa
kufanya yale usiyoweza yanayoweza kukuletea
matatizo,,anakoleza kauli hii anaposema ‘Usiogope
lawama kama unataka kufanikiwa, hayo ndiyo
yaliyoniwezesha kufika nilipo’, ukiunganisha
maneno yake yote hayo na neno la mwisho kuwa
vyombo vya habari ni muhimu utajua kuwa
anamaanisha, alifanya dhuluma kwakuwa
hakuogopa, na alitumia vyombo vya habari
kurekebisha ukweli wa jambo husika” alimaliza
kuongea na kisha alikaa akinisikiliza kama nilikuwa
nina lolote la kusema.
“Nahitaji kurudi Tanzania” niliwaambia kwa kauli
iliyojaa mchosho.
“Patrick, huendi popote mpaka niwe na uhakika na
usalama wako” aliongea Pamela kwa sauti iliyojaa
kujiamini na kuondoka pale sebuleni kuelekea
chumbani.
“Patrick bado tupo nusu ya safari, tunatakiwa
kujua mambo mengi sana kabla ya wewe kupanga
chochote, kila siku unaona kabisa kunaibuka jipya,
uchunguzi wa jambo hautakiwi kutolewa uamuzi
mpaka pale ambapo kila kitu kitakuwa kimesemwa,
kila kitu kitakapokuwa wazi ndipo hapo
tutakapojaribu kutafuta mbinu utakazozitumia ili
uweze kufanikisha kurudisha kila kitu chako, Mark
na Mary ni matajiri wakubwa kwasasa waliojizatiti
na wenye kukubalika, hivyo huwezi kwenda
kichwakichwa tu na mambo yakawa sawa, nina
utaalamu na haya mambo nipe nafasi nikusaidie.

**MWEZI MOJA MBELE**

Mimba ya Pamela ilishaanza kujitokeza kwa mbali
na sasa nilianza kuwa namsaidia baadhi ya vitu
ikiwa ndio ushauri wa daktari.
Jioni ya siku ya jumatano nikiwa niko nyumbani
Pamela alikuja na kunieleza kuwa amepata dharura
inabidi asafiri kwenda India kwaajili ya kusoma
kozi ya mwezi mmoja ambayo angekuja kuifanyia
kazi pale. Ilikuwa ni taarifa ya ghafla na ilibidi
nikubaliane naye tu sikuwa na jinsi wala namna ya
kuzuia yale yasitokee, nisingeweza kuondoka naye
kwakuwa bado nilihitajika kazini na hakukuwa na
mtu yoyote wa kufanya kazi zangu.

*****
Jioni ya siku hiyo nikiwa na dokta Anderson
tulimsindikiza Pamela uwanja wa ndege na
alipanda ndege na kuondoka, tulipotoka pale mimi
pamoja na mzee Anderson na mkewe tulikwenda
kwenye mgahawa mmoja na kupata msosi wa
jioni;
“Patrick lazima sasa ujifunze kuanza upya mambo
yako, lazima ukubali kuwa mambo yametokea na
usonge mbele zaidi, hiyo ndio njia pekee ya
kukusaidia wewe kuwa mpya tena kifikra”
aliniambia mama Anderson huku akionyesha
kuhuzunishwa sana na namna nilivyokuwa na
mawazo.
“ni kweli mama ila ni ngumu sana kusahau”
“najua ni ngumu lakini kila lenye ugumu lina
suluhisho ndani yake”
“mama kipindi naanza maisha nilikuwa
nimejiwekea misingi ya kuishi na namna ya kuishi,
nilikuwa najua nguzo za kuishi na wapi nitapita,
nilishatimiza robotatu ya ndoto zangu nilipokutana
na Mary, na nilimuamini sana lakini haya
yanayotokea sasa hivi yote naona kama ndoto”
“Maisha ni mazuri sana ukipata wa kukupenda,
mimi nilianza mapenzi na Sara miaka 30 iliyopita,
moja kati ya wanawake ambao sikuwahi
kuwaamini kabisa alikuwa Sara na hilo alikuwa
analijua, alikuwa ni mchezaji wa kasino, alikuwa ni
mwanamke ambaye kila mtu anamshika na
kumfanya chochote, nilimpenda siku ya kwanza
nilipokwenda kasino, kipindi hicho nilikuwa daktari
kwenye hospitali moja Australia, nilimchukua na
kumueleza nia yangu yakuwa naye, haikuwa rahisi
sana kumpata lakini baada ya kumfata sana na
kumuonyesha nia yangu ya dhati ya kutaka
kumtoa kwenye ile hali yake alikubali, niliishi naye
kwa mashaka makubwa sana, nilikuwa sifichi pesa
zangu bali nilikuwa nikiziweka sehemu anapojua ili
nijue kama atachukua au la, lakini kwa mwaka
mzima hajawahi kufanya chochote zaidi ya
kwamba alikuwa mlevi wa kupindukia, nilijua
namna ya kumbadilisha, nikampeleka chuo
akasoma na alipata shahada yake ya kwanza ya
udaktari, nikamuweka karibu sana na mimi, baada
ya mwaka toka amalize masomo tukafunga ndoa
na akajifungua mtoto wetu wa kike. Maisha
yakianza japo bado nilikuwa simuamini sana, lakini
muda ulivyokwenda nilianza kumuamini na kiukweli
nilikuwa nimejifunza kabisa kuwa mwanamke
anaweza kuwa anafanya kazi yoyote ila kazi yake
au vile alivyo haitakuwa utambulisho sahihi wa
namna ambavyo atakuwa mwema au mkaidi kwa
mumewe. Kipindi cha nyuma nilikuwa mchumba
tuliyekuwa tunaimba kwaya kanisa moja huko
SUVA, alikuwa ni msichana bikra na aliniambia
nimsubiri nisiwe na haraka, tulijuana toka utoto
wetu na wazazi walijua vizuri mahusiano yetu,
lakini yule binti alikufa kwa kutoa mimba ambayo
haikuwa yangu, nilipoteza matumain kabisa lakini
nilikuja kugundua kuwa kazi kubwa moja wapo
niliyonayo ilikuwa ni kufikiri kwa niaba ya furaha
yangu, nilifanya hivyo na nikamuamini tena Sara
na sasa ni mke wangu kwa miaka mingi sana.
Nakuambia haya nikiwa na maana kwamba sasa
hivi unanafasi ya kuyatengeneza upya maisha yako
bila kuingia tena kwenye matatizo, umempata
Pamela, msichana ambaye nimemlea na nina
mfahamu kama mtu makini na asiye na tama,
Pamela anaweza kukuonyesha mwanzo mpya
kama hutaangalia tena kuhusu yaliyotokea”
aliongea hayo na mimi nilitingisha kichwa
kuonyesha kuwa nakubaliana naye japo haikuwa
kweli, sikuwa tayari kuwa na roho nyepesi namna
hiyo ya kuacha mambo yatokee kama hivyo,
nilikaa na kuwa sikiliza kwa muda mrefu ila wao
hawakujua kuwa sikuwa pale kabisa, akili yangu
ilikuwa inapiga mahesabu makubwa kwa jambo
kubwa ambalo nilikuwa natafuta mwanzo wangu
tu.
Akili na mawazo yangu yalikuwa yakimuwaza
Mary,sikujua adhabu gani nimpe itakayoendana na
kile alichokifanya,mda mwingine niliona kama Mary
hakuwa na kosa maana yeye ni binadamu,ni kati
ya wasichana warembo ambao walipanga kuwa na
maendeleo na maisha yao toka utotoni,kuishi na
mimi katika hali ambayo nilikuwa nayo kungempa
usumbufu mkubwa pengine na aibu mbele ya
wasichana wenzake,lakini upande mwingine wa
moyo wangu uliniambia Mary hakunipenda kweli
toka awali na kama alinipenda asingeniacha
ugenini alaf aje kutangaza kuwa nimekufa,,kitu cha
mwisho duniani ambacho nilitaka kuamini ni kuwa
Mary alikuwa hanipendi toka awali,niliamini kabisa
alikuwa akinipenda lakini hali yangu haikumruhusu
yeye kuwa na mimi,kuamini huko kulikatishwa na
kumbukumbu ya ahadi tuliyowekeana pale kanisani
kuwa tutapendana katika shida na raha. Lakini
kikubwa ni kwanini alikimbilia kubadili jina la
kampuni yangu na kwanini basi alikuwa haraka
sana ya kutaka kuzaa na Mark.
“Patrick vumilia tengeneza kwanza maisha”
aliniambia mama Anderson mda mfupi kabla ya
wao kuondoka na kuniacha pale nikinywa ule
mvinyo niliokuwa nimeuagiza, kwenye mida ya saa
4 usiku nikiwa pale, nilishtuka baada ya mtu kuja
na kunifumba macho, niliishika ile mikono
nikagundua ilikuwa ni ya mwanamke, lakini sikujua
ni nani mpaka aliponiachia.
“Mambo Patrick” alinisalimu huku akinitazama kwa
makini usoni.
“Safi tu habari yako” na mimi nilizidi kumkodolea
macho.
“Salama, kwanini unapenda kukaa peke yako
Patrick” aliniuliza huku akisogeza kiti karibu yangu.
“Hapana sikuwa mwenyewe, nilikuwa na watu
hapa ila wameondoka muda sio mrefu sana, lakini
pia ni kweli napenda kukaa mwenyewe hiyo
inanifanya nipate muda mwingi sana wa kujifunza”
alikuwa akinitazama huku akichezesha nyusi zake.
“muhudumuu” alimuita muhudumu na alipokuja
alimuagiza pombe kali.
“Khajat kwanini unapenda kunywa pombe na dini
yako hairuhusu” nilimuuliza huku nikimtazama, na
yeye kwa tabasamu zito alisogea karibu tena na
mimi.
“Dini yetu hairuhusu mambo mengi sana, hata aina
za mavazi wengi tunayovaa hayaruhusiwi, kufanya
mapenzi kabla ya ndoa pia hairuhusiwi,
haturuhusiwi kusuka rasta, kutengeneza nyuso zetu
kwa vitu bandia, kuna mengi sana ambayo
ukiyafanya haina tofauti sana na kufanya mengine”
alinijibu na wakati huo ile chupa ya MCdowell
ilikuwa imeshafika aliifungua huku akinitazama na
kuweka kisha alikunywa pafu mbili kubwa na
kunitazama huku akitabasamu.
“sasa kama unajua mengi yanakatazwa kwanini
unafanya?” niliendelea kumuuliza lakini hakuwa
anajibu moja kwa moja.
“aah ni kama wewe tu unavyofanya mapenzi na
Pamela wakati hamjafunga ndoa na unajua ni
dhambi” alinijibu kiufupi kisha wote tulicheka,
alinimiminia kisha tuligonga glasi na kuendelea
kunywa.
“Ujue wengi hawajui ukweli wangu, mimi
nimechukua jina la mama yangu, ila kiukweli mimi
ni mpagani, sina dini wala sina imani yoyote,
nilichukua jina hili ili nizidi kumchukia mama
yangu, namchukia sana ndo mana naishi maisha
haya unayoniona, niko kama mwanaume, ninaishi
maisha ya uhuru usio na mipaka, nafanya kazi kwa
bidii na mimi ni mbinafsi kuliko binadamu
yoyote,,hahaa ila usiniulize kwanini namchukia
mama yangu kwakuwa sitakujibu” nilikuwa
nashangaa tu kusikia hayo, nilianza kugundua
taratibu kuwa kila binadamu anahadithi yake ya
maisha yake ya kusikitisha na pengine ya
kukatisha tamaa ila tunatofautiana namna ya
kuzikabili huzuni zetu, kila mmoja aliwahi kupitia
jambo gumu lililomkatisha tamaa lakini wengi
waliteseka na kukubali matokeo ya jambo hilo na
baadaye walisonga mbele.
Tulikaaa pale tukanywa na kupiga hadithi mpaka
saa nane usiku kisha nilirejea nyumbani.
“ngriii,,,,ngriii” nilikuwa bado nimelala na
niliposhtuliwa na ule mlio wa simu niligundua kuwa
kulikuwa kumekucha.
“Haloo” niliitikia kwa ile sauti iliyojaa usingizi.
“ndio, habari yako”
“nzuri za kwako Pamela”
“salama, yani Patrick nikiondoka ndo unalala
mpaka muda wa kazini huu mpenzi, sasa
utakunywa chai muda gani mpenzi” ilikuwa sauti
ya Pamela ikiendelea kunisemesha na hapo
nilinyanyuka na kwenda bafuni kuweka mswaki
dawa.
“kazini wataniandalia,,leo nimepitiliza usingizi
mama, nilichelewa kulala jana” nilimweleza na
kushtuka kuwa natengeneza swali lingine la wapi
nilikuwepo mpaka nikashindwa kulala mapema.
“ulienda kunywa pombe tena Patrick” nilikaa kimya
baada ya swali hilo.
“yeah, kidogo tu” nilimjibu huku nikiweka mswaki
mdomoni.
“unatakiwa upunguze Patrick” aliniambia hivyo na
baada ya mazungumzo kidogo tuliagana na mimi
niliamua kuelekea bafuni.

**MWEZI MMOJA NA WIKI MOJA MBELE**

Siku za kurudi Pamela zilikuwa zimefika lakini
hakuwa amerudi kwakuwa alisema wameongezewa
muda kidogo ili kumalizia baadhi ya vipindi. Siku
zote kila jioni nilikuwa nikienda kwa Felly
ilimkupata chakula cha jioni na kuoiga story
nyingine nia ikiwa nikumfanya aweze kuharakisha
sana uchunguzi juu ya swala langu.
Jioni ya siku hiyo nilipotoka kazini Felly alinipita
na kuniambia twende nyumbani kwake, tulienda na
tulipofika alibadilisha nguo na kuingia jikoni na
mimi nilienda kumsaidia, tulipika vizuri na chakula
kilipokuwa tayari Felly alikwenda kuoga na mimi
nilikuwa pale sebuleni nikimsubiri.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Felly alikuja
akiwa na taulo tu, iliyokuwa fupi kabisa na
kuruhusu mabaja yake yote mpaka juu kuonekana,
inawezekana kwa utamaduni wa kule ilikuwa ni
sawa ila haikuwa sawa kwangu na yeye alifanya
vile makusudi, alikuja mpaka mbele ya tv na
kuinamba akirekebisha kebo hali iliyoacha kila kitu
chake nje.
“Felly unafanya nini?” nilimuuliza huku nikijizuia
kumuangalia lakini haikuwa rahisikuacha
kumuangalia, alikuwa amejazia mapaja yake
yasiyokuwa na mikunjo kutokana na mazoezi
aliyokuwa akiyafanya mara kwa mara, alikuwa na
mapaja mazuri japo hayakuyafikia yale ya Pamela.
Alikuwa ni mzuri sana ndani ya lile taulo na urefu
wake ulimfanya azidi kuonekana mrembo kama vile
twiga.
“nimefanyaje kwani Patrick” aliniuliza huku
akinyanyuka na kunifata pale kwenye kochi.
“huoni..uuu…uu…livyo vaa” nilishikwa na
kigugumizi hasa alipokuwa amenisogelea na
kuachia lile taulo.
“Hey, Felly acha bhana, si sawa hivi”
nilimkatazama na wakati huo alishafika na
kufungua shati langu kisha kupenyeza mikono yake
na kuanza kucheza na kila alichokikuta.
“Felly tafadhali acha” nilizidi kumsihi lakini alikuwa
amedhamiria na hivyo alikuwa amebibana katika
namna ambavyo nisingeweza kufanya chochote,
hali ilizidi kuwa mbaya baada ya yeye kupenyeza
mikono ndani ya suruali yangu na mimi nilijikuta nimeshakutanisha mdomo wangu na wake na kuanza kupeleka mrejesho kwa matendo yake.
“Felly” wote tulishtuka na kutazama mlangoni, aibu ilinipata na kila kitu nilihisi kimepooza.
“Patrick, kweli ndo unachonifanyia?” alikuwa ni Pamela.
“Ahh Pamela” sikuwa na la kusema hasa kwakuwa alikuwa sikuwa na cha kujitetea.
“Felly kweli jamani” aliongea huku akilia lakini Felly
hakuonekana kujali sana.
Pamela aliondoka pale na kwa jazba na kuwasha
gari lake kisha alitimka na kuondoka.
“Felly tumefanya nini sasa” nilimuuliza Felly ambaye bado alikuwa uchi akiwa amelala pale kwenye kochi.
“hahaa, usijali Patrick kila kitu kitakuwa sawa” aliongea hayo na mimi nilimrushia lile taulo lake ili
ajifunike.
“Kula Patrick kisha nenda kamfate Pamela” aliniambia huku akicheka, nilikuwa nimechanganyikiwa na nilikasirika sana kwa
kilichotokea, sikutaka kabisa maisha yangu yote ya
sasa kumuona Pamela akiwa na majonzi.
Sikuweza tena kula nitoka nje na kuondoka mpaka
kule nikamkuta Pamela akilia.
“Pamela samahani nipe mda nijieleze” nilijaribu
kumbembeleza lakini hakusikia kitu chochote.
“sitaki uongee chochote, wewe niliyekuhudumia
kwa miaka yote katika hali ngumu leo unanifanyia
hivi? Patrick! Aliongea huku akilia, nilimbembeleza
lakini haikuzaa matunda.
“chukua kila kitu chako humu ndani na uondoke,
nimekuambia ondoka kabla akili yangu
haijabadilika, ni bora ningekuwa na Nancy kuliko
wewe, nilikuona ni mwanaume pekee kumbe wewe
ni wale wale” aliongea hayo na kwenda ndani
akachukua mabegi yangu na kunitupia pale
sebuleni.
“Nimekuambia toka” nilikuwa sina jinsi zaidi ya
kuinamba niokote mabegi yangu lakini nilikutana
na mguu ukiokanyaga lile begi nisilinyanyue.
“Pamela huna haja ya kumfukuza Patrick” Felly
alimwambia Pamela na hapo niliona kama yeye
ndiye alikuja kuharibu kabisa.
“Felly na wewe ondoka kwangu” niliona jicho la
hasira likimtoka Pamela na hapo sikuelewa nini
kilikuwa kitokee.
“Pamela, mchumba wangu hakufa vitani kama
ilivyosemekana, alikufa kwa kulipiwa na bomu
nililomuwekea mimi ndani ya begi lake lililokuwa
na vitu vingine wakati akiondoka kwenda Iraq, siku
hiyo wakati anaondoka nilitegesha bomu hilo kwa
masaa ambayo yangemkuta akiwa Iraq, hii ni
kwakuwa nilimpenda sana, na hiyo ndiyo sababu
pia sina mwanaume hadi leo, nilimpenda na
nitampenda daima. Nilimuhangaikia maisha yake
yote,nilimtoa kwenye kuvuta unga mpaka
nikamsomesha na kumtafutia nafasi jeshini ila
alikosea kitu kimoja tu, HAKUJUA MIMI NI WAAINA GANI, alikufa na mimi ndiye nilimuua na nilimuua kwakuwa ALIFANYA MAPENZI NA WEWE,nyumba yangu ina kamera nyingi kila sehemu na
siku ya tukio mlilewa na mlifanya mapenzi chumbani kwangu na juu ya kitanda changu,nafahamu kuwa hukuwa unampenda ila alikunywesha pombe na wewe ukawa tayari kufanya mapenzi na yeye, sababu ya kukuacha
wewe ni kwakuwa ulirubuniwa tu na hukuwa na nia, lakini nilitaka ujifunze, na ndio maana
uliponitumia ujumbe kuwa ulikuwa umeshafika
uwanja wa ndege nilikuambia ukifika kwako uje
kwangu haraka. Patrick amerubuniwa na mimi
lakini nia yangu ilikuwa ni kukufundisha kuwa kuna
muda kila mtu huumia kwa tendo analofanyiwa na
mtu anayemtegemea, siku hiyo uliacha nguo yako
ya ndani asubuhi baada ya kuamka ukiwa
chumbani kwangu, hii hapa chukua”

ITAKUWAJEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!!!!!!!!
!!!!!!!!???????
 
Kama kaka nawe iko kwa promo tafadhari twambie mapema Wapi vitabu vinapatikana no hill turn mpendwa
Sijui kitabu chake kunauzwa wapi, mimi nna soft copy tu mkuu na jipange kuipata hadi mwisho hapa hapa
 
Sehemu ya Nane
Kwa Mary Robert.2010
“UKOSEFU WA FIKRA HURU NDIO UZAAO UTUMWA
WA MAWAZO NA MATAZAMIO HAFIFU,,KIJANA
MWENYE FIKRA MPAUKO HUWA NA MAWAZO
MGANDO NA MITAZAMO MDEBWEDO, HUFIKIRI
KWA LUGHA FULANI NA KUTENDA KWA
UTAMADUNI WENYE KILEMA CHA UTASHI...HUWAZA KWA KWENDA MBELE YAKE NA
KUTENDA KWA YALIYONYUMA YAKE,,,UKUBWA WA
UBOVU WAKE NI MKONDO HASI WA AYAAMINIYO..HUFIKIRI KWA FIKRA TATA ZA
WENGINE NA KUPAMBANUA KWA MAWAZO
MTAMBUKA YA WASIOJIKUBALI,,MUHIMU KWAKE
NI JIONI KILA IANZAPO ASUBUHI. AHUENI YA
MAISHA YAKE NI MKONO UNYOOSHWAO ILI
KUMBEBA NA SIO KUMUONYESHA NJIA”…..HII NI
SEHEMU YA NANE.

**PATRICK**

Pamoja na Felly kujitokeza pale na kueleza nia
yake ya kufanya hivyo bado hiyo haikuwa sababu
ya mimi kusamehewa. Pamela alikuwa mkali sana
na hakutaka kunisamehe hata kwa asilimia moja.
“Ondoka nyumbani kwangu Patrick, ondoka sitaki
kukuona hapa” aliongea Pamela huku akilia na
kwikwi zikimbana.
“Sikufanya chochote Pamela, naomba nielewe”
nilimsihi huku nikimpigia magoti lakini hakutaka
kunielewa. Felly alikuwa bado yuko pale
akimtazama Pamela alichokuwa anakifanya.
“Ulivyotoka na mchumba wangu ulifikiria nini
Pamela mbona unashindwa kuelewa hili ambalo
Patrick hakufanya?” Felly alijaribu kujielezea lakini
hiyo haikusaidia kitu. Haikuwa rahisi kabisa kwa
Pamela kuelewa.
“Felly hili halikuhusu, kaa mbali na mimi. Kama
ilitokea kipindi hicho ni kwakuwa mchumba wako
alikuwa ameninywesha pombe. Sikufurahia hata
mimi na ndio maana namchukia hadi leo. Kama
ulikuwa unajaribu kulipa kisasi sina shaka na hilo
na wala sina shaka na wewe. Ulitakiwa uniulize
kwanza ilikuwaje. Mchumba wako alinibaka kwa
tafsiri nyepesi na sio kwamba nilimvulia nguo.
Hivyo kama na wewe umembaka Patrick basi
ondoka naye kabisa mimi simuhitaji tena hata kwa
sekunde moja” yalikuwa maneno ya Pamela
kwenda kwa Felly. Sikuelewa vizuri kilichokuwa
kikiendelea pale lakini pia sikutaka kuwa sababu
ya mnyukano ule wa maneno.
“Sikiliza nikuambie rafiki yangu mpenzi Pamela.
Siku uliyofanya mapenzi na mchumba nilikuwa
nimeenda kwenye operesheni ya kijeshi nchini
Korea, siku ile ilikuwa ni siku yangu ya kuzaliwa na
nilirudi nikiwa na furaha sana kwakuwa nilijua
nitakuja kuutumia muda wangu na yeye siku hiyo
baada ya kuwa nje ya nyumbani kwa zaidi ya
miezi miwili. Nilimkosa sana kwa kipindi chote
hicho. Lakini nilipofika nyumbani siku ile hakuwa
sawa, alikuwa hata hakumbuki kama siku hiyo
ilikuwa ni siku yangu ya kuzaliwa, hilo halikuwa ni
shida sana kwangu. Lakini shida ilikuja kuanza
nilipohitaji kufanya nae mapenzi siku ile, hakuwa
kwenye hali ya kufanya mapenzi kabisa kwakuwa
alikuwa amechoka na alionekana kutokuwa na
hamu ya kufanya hivyo hiyo ilinifanya nifanye
uchunguzi ni kwanini imekuwa hivi, nilimfahamu
sana mchumba wangu kwahiyo anapokuwa hayuko
katika hali fulani huwa najua kuna kitu katikati
yetu. Nilimuuliza kwanini amechoka sana lakini
alinijibu bila kunitazama usoni, hii ilimaanisha
kuwa kuna kitu hakuwa anakisema. Hivyo
kwakuwa yeye hakuwa anaijua vizuri nyumba
yangu ilikuwa rahisi sana mimi kuujua ukweli kama
alikuwa anadanganya. Nilikwenda kwenye kamera
za pale ndani na kutazama yaliyotokea kwa kipindi
hicho, nilikuta matukio ya wiki mbili nzima ambayo
mliitumia wewe na mchumba wangu. Mlifanya
mapenzi siku ya kwanza ambapo mlikunywa
pombe mkalewa na hamkujielewa wote, mkalala
kwenye kitanda changu na mkafanya yenu. Alikuja
kukuomba msamaha kwa kilichotokea siku mbili
mbele na wewe ukamwambia haina shida.
Mkaendelea kuwa mnakuja na kushinda kwangu,
hiyo haikuwa shida sana kwangu, shida ilikuja pale
ambapo mlifanya mapenzi tena usiku wa kuamkia
siku ambayo nilikuwa nikirudi nyumbani, usiku wa
kuamkia siku yangu ya kuzaliwa. Mlikuwa kwangu
na mlikuwa mnakunywa kama kawaida yenu, lakini
wakati wewe ukinywa mchumba wangu alikuwa
akicheza kujifanya kuwa amelewa lakini kumbe
hakuwa amelewa bali alitaka tu ulewe afanye
mapenzi na wewe. Na alifanikiwa. Kilichonifanya
nimchukie yeye na sio wewe ni kwakuwa baada ya
kosa la kwanza ulimwambia hujapenda na si sawa
kwakuwa mimi ni rafiki yako. Na pia siku ya tukio
la mwisho ulimwambia kuwa hata kama mkilewa
vipi kila mtu aiangalie akili yake. Hii haikuwa mara
yake ya kwanza na ndio mana niliamua kumfanya
asiwepo tena duniani. Hivyo si kwamba ulibakwa,
hapana, ili ubakwe lazima uwe hujapata nafasi ya
kuepuka kubakwa. Ila wewe ulifanya mapenzi naye
kwakuwa ulikuwa na nafasi ya kuepuka kwa
kutokunywa naye pombe tena. Hujabakwa ila
ulishawishiwa” aliongea Felly huku akizunguka pale
sebuleni.
“Hivyo umeamua kulipa kisasi?” Pamela aliuliza.
“Sijui kama ni kisasi lakini nilitaka kupata nafasi ya
kutoa lililo moyoni mwangu kwa muda mrefu sasa,
nilitaka uumie japo kwa dakika mbili tu kama mimi
nilivyoumia kwa miaka sasa, ni kisasi kidogo sana
hicho kisichokuwa na uhalisia ndani yake. Patrick
ni mwanaume ambaye sio tu anakupenda ila si
mwepesi sana kukusahau. Nilifanya makusudi na
kwakulazimisha kwakuwa nilijua upo karibu na
kwangu, hivyo nimefurahi kwamba umeumia kiasi
na sasa tunaweza kuanza upya. Ila jua sijafanya
chochote na Patrick” alimaliza kuyasema hayo na
kuondoka zake. Pamela alikaa chini na kulia sana
na nilipomfata kuongea naye hakutaka nimguse.
“Patrick msimamo wangu bado ni mmoja, ondoka,
sikuamini wewe wala Felly. Ondoka kabisa
kwakuwa umeniumiza sana”. Sikuwa na namna
zaidi ya kuingia ndani na kukusanya kila
kilichokuwa changu, nilibeba nguo zangu na kila
kitu kisha nilimfata pale sebuleni nikambusu na
kuondoka mpaka Villa Hotel ambapo nilipanga
chumba.

*****
Maisha bila Pamela hayakuwa rahisi kabisa, kwani
sikuweza kuonana naye wala kupata taarifa yeyote
juu ya mimba yake ambayo kwasasa ilibaki muda
mchache sana ajifungue. Nilikuwa nikienda kazini
lakini mara nyingi sana nilikuwa nikiwaza juu ya
hatima ya maisha yangu.

****
“Hallo” ulikuwa ujumbe wa simu toka kwa Khajat.
“nambie” nilimjibu kwa neno hilo.
“Safi, sijakuona muda mrefu sana, kuna tatizo
lolote?” aliniuliza lakini sikuwa na kikubwa sana
cha kumjibu.
“Hapana hakuna tatizo” nilimjibu na yeye alinitumia
tena ujumbe wa mwisho.
“Tukutane Cambria jioni hii, upande wa kasino”
alimaliza kwa ujumbe huo na mimi nilikubaliana
naye.

****
Jioni ya siku hiyo nilikwenda Cambria kukutana na
Khajat. Nilfika mpaka sehemu aliyonielekeza lakini
sikumkumkuta hivyo ikanibidi nikae tu nikimsubiri.
Nilinunua kinywaji na kuamua kuketi sehemu ya
peke yangu nikitafakari yaliyokuwa yakitokea
kwenye maisha yangu. Niliwaza sana juu ya
hatima ya mtoto wangu ambaye atazaliwa hivi
karibuni lakini sikupata jibu.
“Hey, acha kuwaza Patrick maisha ni leo na jana
iliyopita, hatuijui kesho yetu hivyo mbali na
kuiwaza kesho inayotuumiza inatubidi tuiishi kwa
furaha leo iwapo faraja” aliongea Khajat baada ya
kufika. Khajati alikuwa ni msichana mwenye umbo
dogo lakini mrembo sana, nilikuwa kila nikimuona
namfananisha na msichana Kalinda Sharma
aliyeingiza kama mpelelezi binafsi kwenye filamu
ya THE GOOD WIFE aliyekuwa rafiki wa karibu wa
Alicia Florick mkewe na Peter Florick. Khajat
alikuwa ni mchangamfu sana lakini aliyetumia
ucheshi wake kuficha udhaifu wake wa kimapenzi,
hakutaka kupenda wala kuingia kwenye mapenzi
kwakuwa tu na yeye hakuwapenda sana wanaume
ila alijitahidi kumfanya kila mwanaume rafiki yake
mkubwa wanayeheshimiana ili kuzuia hisia za
mapenzi kuingia ndani ya moyo wa yeyote kati
yao.
“mh! Asante sana Khajat, huwa siku zote wewe ni
mtu wa matumaini” nilimueleza hayo baada ya
yeye kumaliza.
“karibu tena, vipi mchumba wako anaendeleaje”
aliniuliza huku akibugia ile pombe kali iliyokuwa
kwenye glasi yake.
“aaahh,” nilivuta pumzi nikakosa cha kusema lakini
kabla sijanyanyua tena mdomo na kuongea Khajat
alikuwa ameshaanza kuongea tena.
“Usijali nafahamu kila kitu. Patrick usijione huna
bahati, maisha yana mengi ambayo ni msamiati
kwenye fikra zetu. Majibu sahihi kwa msamiati
ambao huujui ni kubahatisha jibu la swali ambalo
hujalisikia. Hivyo unachotakiwa kufanya ni
kuiambia imani yako itawale utashi wako”.
Sikuyaelewa maneno yake lakini nilikuwa nikijiuliza
juu ya busara yake.
“huwa unatoa wapi maneno hayo Khajat”.
Nilimuuliza huku nikimtizama usoni.
“Nimepitia mengi sana Patrick, mengi sana mazito.
Tuondoke” alininyanyua pale na kunishika mkono
kisha tulielekea kwenye chumba kimoja ndani ya
ile kasino kisha nilimshuhudia akivua nguo zote na
kupaki na nguo ya ndani tu
“Unafanya nini Khajat” nilimuuliza huku macho
yakinitoka kama panya aliebanwa na mlango.
“Nataka nikuonyeshe kitu fulani kwenye mwili
wangu” aligeuka na kunipa mgongo, alikuwa na
alama za mikwaruzo mikubwa kwenye mwili wake
kama vile alichomwa na kitu au kuchapwa sana na
waya tena mfululizo.
“ni nini hicho Khajat” nilimuuliza na kumsogelea
kisha nilizishika zile alama ili nijue ni nini kile lakini
sikuweza kupata jibu la haraka.
“Huu ni unyama niliofanyiwa miaka mingi iliyopita,
hii ni sababu ya mimi kumchukia mama yangu
mzazi” Alivaa nguo zake na kuniambia turudi
tulikokuwa. Nilikuwa nimepigwa na butwaa na
shauku ya kutakaka kujua tatizo ni nini.
“Utajua kila kitu siku moja Patrick, nilitaka
kukuonyesha tu kuwa kuna watu wanamatatizo
mengi sana lakini hawawezi kuyaonysha au kuwa
na huzuni maishani mwao. Nimeishi miaka mingi
na hata dada yangu hajui kilichonitokea baada ya
yeye kutoroka nyumbani akiwa na miaka mitano,
alikimbia haya yaliyonikuta mimi. Lakini leo hii
nataka unisindikize sehemu nikakufundishe kitu,
hivyo malizia kwanza hicho kinywaji alafu
tuondoke” alimaliza kuongea na kunyanyuka kisha
na mimi nilimalizia kile kinywaji na kunyanyuka
kuondoka naye, tulipofika nje aliingia kwenye gari
yake na mimi niliingia kisha aliliondoa gari kwa
kasi sana.
Kilomita 15 mbele alilipaki gari pembeni na
kunigeukia.
“Patrick umefanyiwa ubaya si ndio” aliniuliza kwa
macho makali.
“Ndio, Mary amenifanyia ubaya sana” nilimjibu
huku na mimi nikimtizama.
“Unataka kumfanya nini? Aliniuliza huku
akinitazama.
“Sijui hata ninachotaka kufanya” nilimjibu
kiunyonge kwakuwa ni kweli sikujua cha kufanya
japo nilijua nataka kulipa kisasi.
“Wakati shemeji yangu amemsaliti dada yangu,
nilimuuliza dada yangu swali hilo na alinipa jibu
kama lako, lakini nilimuambia kama anataka kulipa
kisasi basi ni lazima kwanza achimbe makaburi
mawili, moja lake na lingine la shemeji yangu.
Katika kulipiza kisasi unaweza kukuta adui yako
ananguvu kuliko wewe hivyo lazima ujitolee, ama
yeye aingie kwenye kaburi lake au wewe uingie.
Unapolipa kisasi hutakiwi kuwa na chakupoteza.
Mara unapoanza mbio za kulipa kisasi basi jua
kabisa hakuna kusimamal. Hutakiwi kumuogopa
adui yako bali kuiamini na kuiabudu hasira yako.
Sababu ya kwanini mimi sina dini ni kwakuwa
sikutaka kubanwa na amri yoyote ile nitakapokuwa
tayari kulipa kisasi. Kuwa na moyo wa uvumilivu
na ujasiri wa nafsi nikufundishe maisha” aliongea
hivyo huku machozi yakimchuruzika na kuwasha
gari, alikanyaga mafuta kwa kasi sana na
kuondoka.
Njia nzima alikuwa akinieleza mambo ambayo
sikuyaelewa sana kwakuwa nilikuwa nawaza juu
yake kuwa yeye ni mtu wa aina gani, mshale
kwenye sehemu ya kuonysha mwendo kasi ulikuwa
unasoma 240 kwa maana kuwa zilikuwa zimebaki
20 tu kumaliza mwendo wote wa gari. Ilikuwa ni
kasi ya ajabu sana na machozi yalikuwa yakimtoka
sana.
“Niliisubiri siku hii kwa muda mrefu sana wa
maisha yangu, nilipoteza furaha yangu kwa muda
mrefu na kuishi nikiwa na furaha ya kughushi kwa
siku zote za maisha yangu, kwakuwa mtu mmoja
tu aliamua mimi niishi hivyo”. Aliongea huku akilia.
“kuna nini kwani Khajat?” nilimuuliza tena huku
nikimsihi apunguze spidi ya gari.
“Umeona zile alama mgongoni mwangu, yule
aliyenifanyia leo hii nataka na yeye apate uchungu
wa kile nilichopata mimi. Sitaki kumuona tena
katika maisha yangu. Nimevumilia lakini sina
namna ya kutafuta Amani yangu zaidi ya
kumfanya asiishi”. Aliongea huku akizidisha spidi.
“Sasa kwanini umenichukua mimi” nilimuuliza huku
nikimgeukia. Roho yangu iliingia woga kiasi na
hasa ukizingatia sikuwa na ujuzi na mambo ya
kijasusi kama yale.
“Nakufundisha jinsi ya kuishi na maadui zako,
kwenye maisha usiogope kutafuta furaha yako kwa
damu ya yule anayeikatisha, tofauti ya mimi na
wewe ni kwamba wewe una dini na mimi sina, ila
naamini wewe una mungu ambaye ndiye
aliyeniumba mimi lakini kwenye kisasi huwa
namuomba mungu anisaidie niwaone adui zangu
wakitaabika kama mimi” aliongea hayo na hapo
alisimamisha gari kwa ghafla.
“Patrick utakuwa mtu wa kudhulumiwa kwa siku
zote za maisha yako. Kuwa mwanaume. Huwezi
kulipa kisasi kama huna roho ngumu. Hakuna haja
ya kumchekea mtu aliyetaka kukudhuru. Maana
halisi ya kulipa kisasi ni kumfundisha adui yako
njia bora aliyotakiwa kwenda” aliongezea tena
maneno hayo lakini bado nilikuwa na uoga ndani
yangu.
“Lakini kuua ni dhambi” nilimueleza lakini bado
hakuelewa akawasha gari na tukaendelea tena na
safari.
“Hakuna anayeweza kuiua roho, dini yako ndivyo
isemavyo. Anayeua roho ni yeye tu aliyeiumba.
Ninachofanya mimi ni kuua mwili, iwe dhambi au
thawabu hilo silijui kwakuwa sifahamu chochote
kuhusu maisha ya kusadikika, siishi kwa kusadiki,
naishi kwa uhalisia wa kile nikionacho. Historia ya
maisha yangu ni uhalisia tosha wa roho mbaya za
watu wanaoishi dunia hii, na ili yasimtokee
mwingine basi kila mbegu ileteyo madhara na
itafukiwa”
Tulifika eno la msituni na hapo tulishuka kisha
aliniongoza njia kwenda kwenye shimbo lenye urefu
wa futi sita lililokuwa limechimbwa pale msituni
kisha aliniambia nisubiri pale na nilipomuangalia
niliona akitoa kitu kwenye buti la gari yake.
Kwakuwa ilikuwa ni usiku sikuona vizuri lakini
alipofika pale ndio niligundua alikuwa ni mtu
aliyefungwa mikono yote.
“Ni nini unafanya Khajat” nilimuuliza na
hakuniambia kitu zaidi ya kunipa jicho kali
lililonifanya nikae kimya. Alimfungua kitambaa yule
mama aliyeonekana kuwa na asili ya kihindi au
kiarabu kisha alimuegemesha kwenye mti na
kuanza kumuangalia huku machozi yakimtoka. Yule
mama alikuwa amechakaa kwa majeraha mwili
mzima yaliyoonyesha kuwa alikuwa amepigwa na
kufungwa bandeji.
“Mama siku uliyotenda kosa kubwa sana kwenye
maisha yako, ni siku uliyoacha kuitoa mimba
niliyokuwepo mimi. Umekuwa muda mwingi sana
ukiniambia kuwa ulinizaa kwa makosa, umenitesa
kama mimi si mtoto wako, umenidumbukiza chooni
nikaokolewa, ukaona haitoshi ukanifanya mfungwa
katika umri mdogo na kunipiga sana kama sikuwa
mwanao. Hiyo haikutosha, ukanipeleka mahabusu
kwakosa ambalo silijui, nikabakwa mpaka kizazi
kikatoka. Nilipotoka ukaona haitoshi wakati nataka
kutoroka kwako ukanikamata na kuanza kunitesa
tena, yote haya ni kwasababu ulimchukia sana
baba ambaye naye ulimuua. Umenitesa sana lakini
sikujua kwanini. Mara zote nilikosa pa kwenda
kushitaki maana kila sehemu nilijulikana kama
mtoto mtukutu, leo hii nataka uniambie sababu ya
kunitesa tena nikiwa kwenye umri mdogo vile”.
Nilishangaa kwa yale aliyokuwa akiongea Khajat.
“Wewe sio mwanangu. Wewe ni mtoto wa
mwanamke mmoja aitwaye Khajat, alikuwa ni
mwanamke katili sana. Alitembea na mume wangu
ambaye ndiye yule uliyedhani kuwa ni baba yako.
Baada ya kumuambia kuhusu swala la yeye
kutembea na mume wangu hakunielewa, aliendelea
kupoteza Amani ya nyumba yangu. Taratibu mume
wangu akawa hanisikii tena, akaamua kuhama na
nyumba. Mimi na mume wangu tulitoka mbali
sana, toka kipindi cha shule hadi tulipofikia
kuoana. Lakini mama yako alikuwa haelewi,
alimfanya mume wangu awe dhaifu na hakuona
huruma yoyote. Kuna muda nilimfata mume wangu
nyumbani kwa mama yako lakini niliishia kupigwa
kama mbwa. Hakunionea huruma kama
mwanamke mwenzake, hiyo haikutosha kabisa
alikuja na kuchukua kila kitu changu. Akaondoka
nacho wakaniacha nikiwa sina chochote.
Wakanisingizia kuwafanyia fujo na mahakama
ikanihukumu kwenda jela mwaka mmoja.
Nilipotoka nilikwenda kwao kumuomba mume
wangu tuanze maisha mapya lakini haikuwa hivyo,
alinipiga sana siku hiyo kwa shinikizo la mama
yako. Nakumbuka mama yako alinipiga na kiti
tumboni. Niliumwa na tumbo kwa muda mrefu
sana, niliishi kwa maumivu makali na hapo ndipo
mama yako aliponichukua niishi nao pale kwakuwa
walihofia ningekufa. Mama yako alikuwa ni nesi,
hivyo alikataa nisipelekwe hospitali na kwakuwa
mume wangu hakuwa na usemi kwake alikubali,
sikuwa naweza kutembea hivyo sikuweza kwenda
popote. Siku moja mama yako alikuja na daktari
ambaye ni kaka yake na akamwambia anitoe kizazi
kwakuwa nilikuwa naumwa sana. Walifanya hivyo
na hapo hali ilikuwa mbaya zaidi. Wakati huo
mama yako alikuwa na ujauzito wa miezi nane.
Baadaye ulipozaliwa na mimi nilikuwa nimepata
nafuu. Niliamua kumuua mama yako kwa sumu na
kabla hajafa nilimueleza wazi kuwa huko
atakapokuwa atashuhudia mwanae akiyapitia
magumu niliyoyapitia mimi. Hiyo ilikua ahadi yangu
na ndiyo maana niliamua kukutesa nikiamini kuwa
huko aliko anaona. Nilimuua mume wangu pia
kama njia ya kumaliza hisia zangu” yule mama
alihadithia mkasa ulionifanya nione mwili wangu
ukitetemeka.
“Kaburi la mama yangu liko wapi” aliuliza Khajat
kwa sauti kavu.
“Lipo Bombay huko India” alijibu hivyo na hapo
Khajat alimuuliza eneo lilipo na yeye alitaja.
Alikuwa akiomba msamaha na kumuambia Khajat
amsamehe lakini haikusaidia, Khajati aliondoka na
kwenda kwenye gari na aliporudi alirudi na mtungi
mdogo sana wa gesi wenye kidude cha kupachika
puani na mdomoni. Kisha alimvalisha na kuifunga
vizuri ile gesi, kisha alinigeukia na kunitazama.
“Nilikuambia unapoanza mbio za kisasi hakuna
kusimama, wala kurudi nyuma, hata ikitokea silaha
ya kulipia kisasi imedondoka we songa mbele
utapata namna nyingine. Ukirudi nyuma au
kuyumbishwa na historia uchwara utajikuta
umesahau njia ya malipizi” aliniambia huku akiwa
amenikazia macho na kumgeukia tena yule mama.
“Ubaya wa kisasi ni kwamba, mzunguko wake
huwa mrefu sana, ungeamua kuishi na mimi vizuri
bila kunidhuru ungekuwa salama leo, nisingelipiza
na mimi. Lazima kuwe na mtu wa kumaliza kisasi
kwa kukubali kukaa bila kulipa kisasi ili kisiendelee,
lakini mtu huyo hawezi kuwa mimi. HIYO GESI
KIDOGO ITAKAPOISHA NADHANI ITAMAANISHA
MWISHO WAKO PIA. Kwaheri” alimsukumia kwenye
lile shimbo na kuanza kufukia mpka lilipofunga
kabisa na hapo alienda kuleta gari na kupita juu ya
lile shimo mara nyingi zaidi mpaka alipohakikisha
kuwa udongo umekuwa mgumu.
“Ingia kwenye gari tuondoke Patrick”

JEEEEEEEEEEEEEE NINI KITAFATA KWA
PATRICK???
 
Mi imeniacha hoi kwenye kusahau nguo ya ndani. Gamba shusha vitu
 

SEHEMU YA TISA


“KITU KIKUBWA KINACHOTUOGOPESHA SI
KWAMBA TUNA MAPUNGUFU AU KWAMBA
HATUJAKAMILIKA. WOGA WETU MKUBWA NI
KWAKUWA TUNA NGUVU KUPITA KAWAIDA.
HUO NI MWANGA WETU, NA WALA SIO GIZA
LINALOTUOGOPESHA MDA WOTE. MUDA
MWINGINE TUNAJIULIZA ‘MIMI NI NANI
MPAKA NIWE MWENYE KIPAJI, NGUVU,
MWEREVU AU MWENYE AKILI NYINGI?’ LAKINI
TUNASAHAU KUJIULIZA KWANI ‘MIMI NI NANI
MPAKA NISIWE VYOTE HIVYO?’. MAISHA NI
KWA WALE WAAMINIO UZURI WA NDOTO ZAO,
NI KWA WALE WAOTAO NA KUFANYA JUHUDI
YA KUZIBADILI NDOTO ZAO KUWA KWELI.
Unaweza kama Ukiamua,,WEWE NDO WA
KUJIPANGIA MAMBO MENGI UYATAKAYO. Hii nisehemu ya TISA

Inawezekanaje mtu amfukie mwenzake akiwa mzima, tena mama yake,,,looh! Nikajiuliza mara mbili mbili lakini sikuelewa kabisa huyu Khajat alikuwa mtu wa aina gani, nilijaribu sana kufikiria huyu msichana ni wa aina gani lakini bado akili yangu ilirudi nyuma tena na kutafakari iweje msichana wa aina hiyo japo sijamuona awe na roho ya kiume namna ile. Nilitulia nikimsikiliza Patrick wakati akiendelea kusimulia.

**PATRICK**

Niliganda, nilikuwa nimetumbua macho nisijue nini cha kufanya kwakweli. Sikuelewa nini fundisho pale, sikujua ni kwa vipi mtu anaweza kuwa mnyama vile. Khajat alikuwa na macho
makavu kabisa. Hakuwa akicheka wala
hakusomeka usoni mwake.
“Patrick wewe ni mwanaume au mwanamke?”
aliniuliza huku akinitazama kwa hasira.
“Kwanini unaniuliza swali la kipuuzi hivyo”
nilimuuliza huku nikimtazama usoni.
“Kwanini unakuwa muoga kiasi hicho hasa kwa
kitu ambacho hufanyi wewe” aliongea huku
akilia, nilielewa kabisa uchungu aliousikia, lakini
hiyo haikunizuia mimi kushangaa kitendo kile
cha kinyama kilichotendwa na mwanamke.
Nilimvuta na kumkumbatia kwani alikuwa
amezidisha kulia. Sikutaka kumuonyesha kabisa
kuwa yeye ni mnyama kwa kiasi kile ambacho
kilikuwa ni ukweli. Tangu nizaliwe hii ndio mara
ya kwanza naona kitu cha ajabu vile. Ilikuwa ni
kitu ambacho ningekuja kumsimulia hata mtoto
wangu. Haikuwa kawaida kabisa kwakweli, ni
kitu ambacho hata msikilizaji wa simulizi hii
atakubali kuwa si kawaida.
“Patrick niliteswa sana, niliteseka katika umri
ambao nilitakiwa kupata upendo. Sikuwa na
hatia lakini nilibakwa na kuteswa nikiwa na
umri wa mtoto. Nilianza kuingiliwa kimwili hata
kabla sijaota maziwa kifuani mwangu. Nilikuwa
mdogo sana lakini nilikomazwa. Nililia usiku na
mchana lakini sikusikilizwa na huyu mwanamke.
Kwanini alinitesa kwa makosa ya mama yangu?
Je hastahili leo kulipa kwa ubaya alionifanyia?
hii ni adhabu yake na adhabu ni malipo halali
kwa mkosaji, hata mimi niko tayari sasa kwa
kupewa adhabu kama itabidi kupewa” aliongea
huku akiendelea kuongea. Hakika sikuwa na la
kusema wala kufanya, nilibaki nikiwa
nimemkumbatia huku moyo wangu ukitafuta
neno la kumwambia lakini sikulipata. Bado
nilikuwa nikitafakari hasa ni nini anajisikia yule
aliyewekwa ndani ya lile shimo.
“Patrick, kitu kilichonifanya niwe hai mpaka leo
ni hii siku, nilikuwa nikimuomba mungu aniweke hadi siku hii ya leo ili niweze kumaliza lililo moyoni mwangu” aliniambia na kujiachilia toka
kwangu kisha aliondoka na kuingia kwenye gari.
Nilikuwa bado mimi nimesimama pale kwenye ile sehemu aliyofukiwa yule mama. Machozi yalinitoka nilipolitazama lile kaburi. Nilikuwa namuogopa sana Khajat kwa sasa, hakuwa mtu wa kawaida. Ni bora adhabu ya dada yake Felly aliyompa mchumba wake kuliko adhabu hii ya kumfukia mtu akiwa hai.
“Tuondoke Patrick”. Nilisikia sauti ya Khajat ikisemesha, nilipogeuka alikuwa ameshawasha gari tayari akinisubiri. Taratibu niliingia kwenye gari huku akili yangu ikiwa imechanganyikiwa kwa niliyoyaona. Khajati akawasha gari na tukaondoka.
“Nipeleke hotelini nikapumzike Khajat”.
Nilimweleza huku nikivuta pumzi, lakini
nilishangazwa na yeye kuipita hoteli niliyofikia na kuendelea na safari.
“Khajat nimekuambia unishushe hotelini”.
Nilimueleza hayo lakini alikataa mimi kwenda kulala hotelini.
“Huwezo kwenda kulala hotelini wakati mimi nina nyumba kubwa, hivyo utalala kwangu Patrick”. Aliongea hayo na kuzidi kukanyaga mafuta.
“Hey Khajat embu acha masihara, mimi
nitaendaje kulala kwako?”. Nilimuuliza hayo lakini hata hivyo hakuonekana kujali swali langu.
“Patrick hatuna cha kujadili hapo” aliongea hayo
na muda huo tayari tulikuwa tumefika kwake.
Tulishuka akaingia ndani na kisha alinionyesha
chumba cha kulala mimi na yeye alitoka nje ila
kwa mbali nilimsikia akiongea na simu;
“Kwahiyo amesema hawezi kutoa ni la kwake?”
aliongea hivyo kisha alikaa kimya akisikiliza
mtu wa upande wa pili wa simu na kuanza tena
kuongea.
“Nipe niongee nae” alisema tena na hapo
nilimsikia akifoka tena.
“Mpe huyo kijana hilo begi, unataka maelekezo
ya aina gani ndo utoe. Acha upuuzi. Taarifa
zote alizokupa hazikutoshi mpaka utake nini
zaidi, nikikata simu nategemea huyo kijana awe
ameshaondoka hapo na hilo begi, kinyume cha
hapo anza kuandika upya barua ya kuomba kazi
sehemu nyingine”. Alimaliza na kukata simu
kisha alipiga tena simu nyingine ambayo
alikuwa akiongea kwa upole.
“Habari yako kipenzi”. Aliongea na kunyamaza
kidogo.
“Hapana unajua shughuli ni nyingi sana lakini
nilikuona siku moja na kitumbo chako sema
nilikuwa kwenye gari na wewe ulikuwa uneingia
ofisini kwako, hahaa” aliongea na kutoa kicheko
kilichoonyesha kabisa kuwa alikuwa
akijilazimisha.
“Hapana siumwi ila nataka kuonana na wewe
kesho, nina shida ya kitu fulani nilitaka
tuongee”. Mh! Niliguna nakusogea mlangoni
nijue alikuwa anaongea na nani.
“hapana sio ugonjwa, ni mamabo tu ya
kawaida”. Alimaliza na kilichofuata ilikuwa ni
salamu ya usiku mwema. Niliyatafakari maneno
machache aliyokuwa ameongea na hii simu ya
pili aliyopiga nikagundua wazi alikuwa
anaongea na Pamela,,uuf nilichoka, sikujua
angeongea nae nini.
Nilioga na nilipomaliza tayari chakula kilikuwa
tayari na Khajat alikuja kunigongea kisha
nilishuka na kwenda mezani. Alikuwa amevaa
nguo yake nzuri ya kulalia lakini usoni
alionekana kama mtu ambaye hakuwa tayari
kulala.
“Khajat unafikiria nini”. Nilimuuliza kwakuwa
hakuwa anakula vizuri.
“Nahisi yule mwanamke nimemuwahisha sana,
alitakiwa ateseke sana kabla ya kufukiwa kama
vile”. Mh! Macho yalinitoka kweli, niliogopa
kuona huyu ni mtu wa aina gani ambaye
pamoja na adhabu kubwa isiyo ya kibinadamu
aliyompa yule mwanamke lakini yeye bado
hakuridhika, alikuwa bado na hasira ya kufanya
makubwa zaidi.
“Khajat!!” nilijikuta nikiita na kushangaa.
“Patrick, mimi nina roho mbaya kuliko shetani.
Mtu akinifanya niumie na kujuta kuzaliwa huwa
lazima nimfanye ajute na yeye kukutana na
mimi. Niliteseka na kuumia kama wao
wanavyoumia”. Mh! Hata kama lakini sio kuwa
mkatili hivyo, nilijisemea moyoni.
“Naelewa, lakini achana na hayo mambo
kwasasa, umeshamaliza kulipa kisasi sasa acha
kuwaza zaidi”. Nilijitahidi kumuonysha kuwa lile
jambo lilikuwa la kawaida japo hata kwenye
macho yangu yeye mwenyewe aliona kuwa
nilikuwa nina uwoga. Sio kwamba mimi sikuwa
katili, hapana, ni kwakuwa tu mimi sikuwa katili
wa kiasi kile.
“Kesho nataka kwenda kuongea na Pamela
kuhusu wewe na yeye. Nafahamu kwanini dada
yangu alifanya hivyo. Felly ni mtu muungwana
sana, ana huruma na sikuzote Felly amekuwa
akimpenda sana Pamela ila aliumizwa tu na
namna ambavyo Pamela alifanya”. Aliongea na
kunyanyuka kabla sijasema chochote, alikwenda
akafungua mlango na kijana mmoja aliingia.
“Ukiwa unatumwa kitu, uwe unajua na namna
ya kujieleza, sio unalegeza mdomo na kuogopa
kuongea, wewe ni askari wa aina gani
unaletewa Kiswahili kirefu na mtumishi wa
kawaida unalegea. Weka begi hapo chakula
kipo pale kama unataka kula kama huli basi
kesho, makabrasha yote niyakute mezani
kwangu saa moja asubuhi, kinyume cha hapo
kila kazi kesho utafanya mwenyewe”. Aliongea
mfululizo na huyo jamaa alisimama kwa
ukakamavu kweli.
“Sawa mkuu”. Yule jamaa alijibu nakufunga
malango kisha aliondoka.
“Patrick ukimaliza nenda kapumizike, mimi niko
‘TV ROOM’ naangalia filam” aliongea hayo huku
akiendelea kupanda ngazi kuelekea juu. Nyumba
yake ilikuwa ni ndogo lakini ilikuwa ni ghorofa
iliyobuniwa vizuri na kusanifiwa vizuri.

******
Ilikuwa asubuhi tulivu sana, haikuwa ni siku ya
kazi. Niliamka mapema sana na kuambua
kwenda na Khajat mazoezi, tulikimbia umbali
kwa kilomita kumi toka pale nyumbani kwake,
na huko tulikuta sehemu yenye kama msitu
mdogo hivi. Kulikuwa na kambi ya jeshi.
“Usiogope Patrick, lazima ujifunze mambo
mengi sana yatakayokusaidia baadaye”.
Sikumuelewa Khajat alichoniambia lakini
sikuhangaika kumuuliza kwakuwa
nilishamfahamu kuwa yeye huwa hatoagi
ufafanuzi kwa maneno bali kwa matendo, hivyo
nilijikaza na kuingia kwenye ile kambi.
“Oooh Kapten Janeth, habari”. Alimsalimia dada
mmoja aliyeonekana kuwa na yeye alikuwa
kwenye mazoezi ndani ya lile jengo kubwa
lililokuwa kama linatisha hivi.
“Salama mwalimu wa mafunzo, hahaa”
walicheka na kukumbatiana, nilichotambua kwa
haraka ni kuwa yule dada na Khajat walikuwa ni
marafiki wa siku nyingi waliosoma shule moja,
na pia niligundua Khajat ni mwalimu, sikujua ni
mwalimu wa nini lakini nilivuta subira kidogo ili
nijue ukweli wa kila kitu.
“Huyu anaitwa Patrick, ni mpenzi wangu,,Patrick
huyu ni mwanafunzi wangu, ni rafiki yangu na
pia ni mtu wa karibu sana baada ya Felly”.
Aliongea hayo na mimi sikutaka kuonyesha
mshangao kutambulishwa kama mpenzi
kwakuwa nilijua atakuwa amesema hivyo
kwasababu yoyote nzuri aliona inafaa.
“Nashukuru kukufahamu Patrick”. Janeth alinipa
mkono na mimi nilimsalimu na hapo tulianza
kuondoka kuelekea upande wa pili wa lile jengo.
“Ulimaliza salama?” Janeth alimuuliza Khajat.
“Yeah, nilifanikiwa lakini bado nahisi ile adhabu haikumfaa sana”. Aliongea Khajat.
“Ulimpa adhabu gani?”. Aliuliza Janeth.
“XT3 na KM3”. Alitaja vitu ambavyo
sikuvifahamu lakini sikutaka kushangaa.
“He! Khajat, wewe!”. Janeth alishangaa na kusimama.
“Janeth katika mapambano, silaha yoyote
inaweza kufanyakazi nzuri dhidi ya adui iwapo tu utakuwa umejua lengo la mapigano, hiyo ndiyo kanuni niliyowafundisha”. Aliongea na
kumshika mkono Janeth ikiwa ni ishara ya kumwambia waondoke.
“Lakini kwa mtu wa kawaida tena dhaifu kama yule huwezi kutumia hata 1 au 2 wala huwezi tumia XT au KM, du! Khajat, nimekuogopa aisee, sijawahi kuona hata mtu akifanyiwa hayo
kwakweli”. Aliongea Janeth na hiyo ilinipa moyo
na kujioa kumbe sio muoga kwani hata Janeth
mwenyewe alikuwa akishangaa.
“Nafurahi kuona unashangaa, hii inamaana
nimejitahidi kulipa kisasi kitakatifu”. Aliongea
hayo Khajat na Janeth alikaa kimya kama
aliyepigwa na butwaa. Tulikuwa tumeshafika
kwenye chumba chenye silaha na hapo
alichukua bunduki moja ndefu na mimi alinipa
bastola ndogo na kuanza kunifundhisha namna
ya kushika na kupiga. Tulifanya zoezi hilo kwa
muda wa lisaa limoja kisha tulitoka nje na
tulipofika pale aliondoka na kuniacha nikiwa na
Janeth tukiongea.
“Janeth XT3 ndio nini?”. Nilimuuliza Janeth
wakati Khajat hayupo, ila kabla hajanijibu
nilisikia sauti ya Khajat ikijibu swali lile, alikuwa yuko nyuma yangu tayari na alianza kunielezea.
“XT3 inasimama badala ya ‘xtreme Torture namba tatu’ hii ni kutesa kulikopitiliza, kwenye mafunzo ya kijeshi, hii hupewa gaidi asiyetaka kutaja sehemu ambapo kitu cha kudhuru watu kipo na kinahatarisha uhai wa watu kwa wakati huo na ni cha haraka, adhabu za hapa ni kama
kuchoma sindano ya maumivu makali, kuchoma
mishipa kwa bisibisi, kumchoma mtu kwa moto
wa gesi, kukata vidole au kung’oa kucha,
kukata sehemu yenye nyama na kuchomeka
waya zenye shoti ya umeme. Kama jambo si la
haraka unatumia XT1 ambayo huwa ni kumpiga,
kumtishia kuwaumiza awapendao, kumpiga
shoti za kawaida au kumpiga sehemu
zinazomletea maumivu, kama anachelewa
kusema na jambo ni la hatari kidogo unatumia
XT2 inayojumuisha, kuua mtu mwingine mbele
yake ili kumletea woga, kumuingizia waya puani
na kuzidi kuusukuma kama haongei,
kumuwekea kitambaa usoni na kumimina maji
huku ukikibana ili maji yaingie puani na
kumfanya asipumue, kumvisha mfuko wa lastiki
kufunika uso wake ili ashindwe kuvuta pumzi na
mengine. Umeridhika?” aliniuliza na sikuwa na
cha kusema kwakuwa maswali yalizidi kuwa
mengi.
“KM3 inasimama badala ya ‘Kilingi method
namba tatu’ hii ni mbinu ya kuua. Kwenye hii
wanafanyiwa watu kama magaidi, walioua watu
wengi sana, watu kama kina Osama na
wengine, inajumuisha, kuua kwa kumfukia mtu
akiwa mzima huku umemfunga gesi ilia pate
maumivu makali kabla hajafa, kuna kumfunga
jiwe na kumtosa baharini akiwa mzima, kuna
kumkata kiungo kimoja baada ya kingine huku
ukimtundikia drip ya damu na kumpiga sindano
ya kumpa nguvu ili asife haraka, kuna
kumchoma sindano ya kumfanya aoze na
kutoka wadudu akiwa mzima, tuishie hapo”.
Alimaliza na kumuambia Janeth ampe usafiri ili
turudi kwa gari. Niliogopa sana, maswali
niliyokuwa nayo ni juu ya ualimu wa Khajat,
ilikuwaje Khajat alikuja Fiji na kupata kazi,
Khajat alikuwa ni afisa uhamiaji iweje sasa awe
ni mtu anayejua mambo ya kijeshi, je Khajat
alimfundisha Janeth wapi, yalikuwa ni baadhi tu
ya maswali mengi yaliyokisumbua kichwa
changu. Sikuwa na muda wa kuuliza lolote
kwakuwa hakuonyeshe kutaka maswali.
“Ngriii,,,ngriii”. Mlio wa simu yangu ulisikika
ukiita, nilipoitazama alikuwa ni Pamela.
“haloo” niliipokea kisha niliitikia.
“Habari Pamela” ilikuwa salamu iliyofuata kabla
ya yeye kuongea. Sauti yake ilikuwa ya
kinyonge sana, alionekana hakuwa na raha
kabisa na hiyo ilinifanya nijisikie
kunyong’onyea.
“Salama mpenzi, nahisi kukumis Patrick,
naomba urudi nyumbani, sitaki tuongelee tena
hilo jambo nimeelewa na sitaki ukae mbali na
mimi” aliongea bila kung’ata maneno.
“Nimekumis pia Pamela, nitarudi nyumbani”
nilimueleza huku Khajat akionekana
kutabasamu. Niliongea nae kidogo na kukata
simu.
“Inapendeza sana kama ameamua yaishe,
unajua nyie mmejaliwa maisha sasa, mnakaribia
kupata mtoto. Mnatakiwa muwe karibu sana
pamoja.” Aliongea Khajat huku akitabasamu.
Niliona jinsi ambavyo aliyatamani yale maisha
lakini alionekana bado alikuwa na kitu cha
kutekeleza.
“Ndio, ila nina changamoto kubwa sana ndani
yangu”. Nilimueleza hayo lakini hata hivyo
hakujibu zaidi ya kucheka tu na kukanyaga
mafuta, baada ya dakika chache tulifika
nyumbani, nilikwenda kuoga na yeye pia na
baada ya muda mfupi tulikutana tena mezani
kwaajili ya chai.
“Khajat…..” nilitaka kuongea lakini nilikatishwa
na kudakia kwake.
“Nataka kujua umejua wapi mambo yale na
wewe ni nani. Ndo swali ulilotaka kuuliza si
ndio?” aliniuliza huku akinitazama kwa
kutabasamu.
“Ndio” nilimjibu huku nikijiweka tayari kwa
kumsikiliza.
“Nilipotoroka kule Bombay, nilikuja huku
kumfata Felly, nilikuwa mtoto wa miaka 9,
nilikuwa naitwa Roshan, ila mimi nilibadili na
kujiita Khajat ambalo ni jina la yule mwanamke
niliyemfukia, lengo likiwa ni jina hilo
linikumbushe jukumu la kulipa kisasi
nililojiwekea siku ikifika. Baada ya kuja huku
nilianza shule na nilikuwa kila ninachokifanya
nakifanya kwa hasira sana na hiyo ilinisaidia
kufanya mambo mengi kwa makini na usahihi,
nilipomaliza elimu ya sekondari, Felly alikuwa
tayari ni mpelelezi, hivyo aliniuliza ninachotaka
kufanya au nataka kwenda chuo. Nikaamua
kwenda chuo cha jeshi na huko nikajifunza
mambo mengi, baadaye waliona juhudi yangu
na nikachaguliwa kujiunga na mafunzo zaidi ya
kijeshi na baadaye walinipeleka Cuba kwenda
kusoma shahada ya sayansi ya kijeshi na
mambo ya ujasusi. Niliporudi nilikuwa mwalimu
kwenye chuo cha kijeshi, ni hayo”. Alimaliza
kuongea na kunywa funda moja la chai.
“Sasa ilikuwaje tena ukawa kwenye idara ya
uhamiaji?” nilimuuliza tena kwakuwa sasa
alionekana akijali mimi kumfahamu.
“Huku uhamiaji nilikuja kwakuwa sikutaka
kwenda kwenye operesheni za kivita, nia yangu
ni ili nisijekufa huko kabla aliyecheza na maisha
yangu hajawajibika kwa makosa yake, hivyo
nilichagua kuja uhamiaji ila kwa kitengo cha
jeshi cha kudhibiti uingiaji wa magaidi na
madawa ya kulevya, wakati huo nilikuwa
nikijipanga kwa kilichotokea”. Aliongea na
mpaka hapo nilikuwa nimebakiwa na swali moja
tu.
“Sasa kama huyu Bi Khajat alikuwa India,
ilikuwaje wewe ukampata na kumtesea huku au
ilikuwaje yeye kuwa huku, au ulimfata?”
nilimuuliza kisha alicheka na kuanza tena
kuongea.
“Nilianza mawasiliano na Bi Khajat mika 6
iliyopita kwa njia ya mtandao, tulikuwa marafiki
lakini muda wote hakujua kama ni mimi na hata
picha nilizokuwa nikimtumia zilikuwa ni za
mama mmoja marehemu. Tulijadili mambo
mengi sana na baadaye nilimwambia aje
kunitembelea na yeye alikubali kuja. Nilimtumia
barua ya mwaliko na niliwasiliana na uhamiaji
wa kule nao walimkamilishia kila kitu. Niliingia
gharama za kumtumia tikiti ya ndege na pesa
nyingine kwaajili yake, hivyo kama mwezi hivi
uliopita alipanda ndege na kuja alipofika pale
uwanja wa ndege nilikwenda kumpokea
nikimueleza kuwa mimi ni mtoto wa huyo
mama aliyekuwa anawasiliana naye na
nilitumwa kumchukua. Hakuwa amenijua hivyo
nilimchukua mpaka nyumbani kwangu hapa na
nilimuhudumia kila kitu alipotulia ndipo
nilimueleza ukweli mimi ni nani na mambo
mengine yalifata.” Aliongea huku akionyesha
kufurahishwa zaidi na jinsi alivyomkamata.
“Mh! Aisee, hiyo nimeipenda, mimi sina swali
lingine kwakweli ila nataka Pamela
akishajifungua nirudi kwanza nchini kwangu
nikajue mambo yanaendaje kule, nahisi si sawa
mimi nikiendelea kuvumilia dhuluma hii.”
Niliongea huku nikitazama juu.
“Najua inavyokuuma ila kila kitu kitakuwa
sawa. Kila mtu atalipa kwa kadiri alivyofanya.”
Alisisitiza Khajat na hapo tulimaliza chai na
safari ya mimi kurudi kwa Pamela ilianza.
Baada ya muda nilikuwa nimeshafika na
kupokelewa na Pamela.
“Oooh Patrick, nisamehe mpenzi kwa
kutokukuelewa mapema.” Alinikimbilia na
kunikumbatia. Nilikuwa njia panda kwa mambo
mengi sana, kwanza sikujua ni upi mwisho
wangu au malengo yangu na Pamela, sikujua
nini kitafata baada ya yeye kujifungua. Sikujua
nampenda au vipi, sikuwa naelewa maana ya
chochote kilichokuwa kikitokea.
“Hapana Pamela, kosa lilikuwa langu na
ulikuwa na haki ya kuchukia na kunipa adhabu
ndogo uliyonipa”. Niliongea nae na kisha
tuliingia ndani.

***ITAENDELEA
 
Back
Top Bottom