Riwaya: KISASI

Riwaya: KISASI

SEHEMU YA KUMI

“Maisha hutupa changamoto ili kupima ujasiri wetu na utayari wetu wa kubadilika, katika
muda huo, hakuna nafasi ya kujifanya kwamba hakuna linalotokea au kusema kuwa hauko tayari kuipokea hiyo changamoto.
CHANGAMOTO HAZISUBIRI UTAYARI WAKO.
Maisha hayaangalii nyuma, ni kama sheria mpya inayotungwa juu ya jambo fulani, huwainaanzia pale iliposainiwa. Wiki moja ni zaidi ya
muda wakutosha tunaohitaji ili kuamua kama
tunakubali mwisho wetu tuupanga au
la”Japokuwa unaweza pia kuhutaji kwenda
mbele kwenye maisha yako, lakini unaweza
kukuta umeweka mguu mmoja kwenye ‘break’.
Nini thamani ya maisha kama tunaamua
kwenda mbele kwa mashaka ya kukanyaga
breki. Ili uwe huru, lazima ujifunze kusahau na
kuacha mambo mengine yaende. Acha
kuumizwa na machungu yaende, sahau. Tupa
woga kulee, achana na kuzisumbukia na
kukumbuka maumivu yako ya zamani. Nguvu
unayotumia kujihusisha na maumivu yako na
maisha yako ya zamani ndiyo inayokuvuta
nyuma na kukufanya usisonge mbele. KUBALI
KUANZA UPYA. HII NI SEHEMU YA KUMI.

Basi ndugu mwandishi mimi nilikaa kama
nimepigwa na butwaa hivi. Nilitokea kumpenda
sana Khajat lakini nilimuogopa sana. Ukioa
mwanamke kama huyu unatakiwa kuwa makini
na kila ufanyacho kwakuwa muda wowote na
popote anaweza kukufanya kitu kibaya. Hii
simulizi iliachiwa usiku kucha. Na sasa ilikuwa
inaelekea saa nane za usiku. Bado nilikuwa
macho nikisikiliza redio nione nini kinafuata,
ILIKUWA HIVI.

MWEZI MMOJA MBELE.

***PATRICK****

“Hongera sana Patrick ni mtoto wa kiume,
muda si mrefu tutakuruhusu uingie ndani.”
Ilikuwa kama miujiza vile, alizaliwa mtoto wa
kiume, asante mungu, nilijisemea moyoni nikiwa
pale nje ya kile chumba alichokuwa ameingizwa
Pamela jana usiku.
“Patrick ujue ilishindikana kabisa Pamela
kujifungua kwa njia ya kawaida kwakuwa cevix
zake zilikuwa hazijatanuka vizuri, hivyo ilibidi
tumpasue, kwahiyo mkeo amezaa kwa
uapasuaji.” Ilikuwa sauti ya dokta Anderson
ikinipa taarifa. Khajat na Felly walikuwa
pembeni yangu nao wakisubiri kumuona mtoto
aliyeletwa duniani. Nilikuwa na jukumu sasa la
kulea familia, nilikuwa tayari sasa ni baba wa
mtoto wa kiume.
“Asante sana dokta Anderson, nilipopata taarifa niliona ni vyema kukatisha safari yangu na kurejea tena kumtizama Pamela na mtoto wetu.” Wakati huo nilikuwa nimekatiza safari yangu ya kikazi baada ya kupata taarifa kuwa Pamela alikuwa amepatwa na uchungu wa kujifungua na alipelekwa hospitali. Tulikaa pale nje kwa muda kidogo na walipomaliza mambo yao walituruhusu kuingia.
“Ooooh Pamela, hongera mpenzi, sasa tuko watatu na sio wawili tena” nilimsogelea pale kitandani na kumbusu.
“Asante sana Patrick, hongera na wewe,
nakupenda sana Patrick.” Alisema Pamela, ila
neno ananipenda lilizidi kuniumiza kwakuwa
sikuwa nafahamu hisia zangu juu yake, nilikuwa
nimevurugwa na mambo mengi sana na sikujua
nishike lipi niache lipi.
“Nakupenda pia Pamela.” Niliongea huku
nikionyesha kabisa kuwa nilikuwa na wasiwasi
na nilichokiongea, wakati huo Pamela alikuwa
akinitazama kwa makini sana.
“Usijali Patrick kila kitu kitakuwa sawa mpenzi.”
Alisema Pamela na kunifanya nishangae kwanini
alisema vile, pengine aligundua kabisa kuwa
sikuwa sawa na ile kauli yangu, pengine
aligundua nilichokuwa nikikiwaza.
“Niko sawa mbona Pamela.” Nilijikosha kwa
kujichekesha, lakini alitabasamu akiashiria kuwa
nisimdanganye.
“Alafu embu sogea karibu.” Aliniambia na hapo
nilimsogelea na alinitazama macho yangu kisha
alimwita nesi mmoja aliyekuwa pale ndani ya
chumba kile.
“Lailath naomba ukamcheki Patrick wingi wa damu, naona macho yake ni meupe sana.” Loo!
Alikuwa anajali sana siku zote alikuwa
akihakikisha kuwa afya yangu iko sawa hasa ukizingatia kuwa yeye alikuwa daktari.

******
Tulirudi nyumbani na maisha yaliendelea kama kawaida. Siku zilienda na mwezi ulikatika sasa.
Siku moja nikiwa natoka kazini mchana na kwenda kwenye chakula cha mchana nilikutana na mtu amabye aliponiona alikimbia karibu avunjike mguu.
“Dany, habari yako?” nilimsalimu mtu huyu na baada ya kugeuka na kuniona alishtuka na kuanza kukimbia.
“Mamaaaa,,,mzimuuu” alipiga kelele huku
akikimbia kama mwehu, nilijitahidi kumfata
nyumanyuma lakini kadiri nilivyokuwa nikimfata
ndivyo alivyozidi kukimbia na hapo niliamua kumuacha tu. Niliketi chini na kulia sana kwakuwa kile kilichotokea sio tu kuwa kilinifadhaisha na kuniaibisha lakini kilinipa picha ya ubaya niliofanyiwa.
“Patrick mbona umekaa chini?” nilishtushwa na sauti ya msichana ikiniuliza swali lakini niliponyanyua macho juu alikuwa ni Khajat na nilipotazama kwa mbali nilimuona na Felly nayeye akija upande ule. Nilinyanyuka na kujikung’uta kisha nikazuga kama vile hakuna kilichotokea.
“Nilikuwa nasikia kizunguzungu nikaamua
kukaa hapa kidogo.” Nilijaribu kudanganya ili angalau niepushe maswali zaidi.
“Hapana Patrick huwezi kusema ni
kizunguzungu wakati macho yako yanaonekana kama vile ulikuwa ukilia.
“Kuna kitu kimetokea hapa ila nitakimaliza tu usijali.” Nilimjibu na kujifuta machozi kisha waliongozana na mimi kuelekea ofisini kwangu.
Tulipofika mlangoni tulisimama nje tukiongea maneno mawili matatu lakini nilipotazama kwa ndani kupitia vile vioo sikuona mtu hata mmoja ofisini. Nilishtuka nikatazama vizuri pale mlangoni kile kibao cha mlango kilikuwa kimegeuzwa na kusomeka CLOSED, nikashtuka
nani anayeweza kufungwa ofisi wakati mimi
sipo.
“Patrick rudi nyuma usiusogelee mlango njoo
huku.” Khajat alinivuta mkono na kunisogeza
mpaka lilipokuwa gari lake.
“Felly, kuna uhalifu unafanyika kule ndani.”
Aliongea Khajat na kuniambia niingie ndani ya
gari nitulie. Niliona Felly akifungua gari yake
kule nyuma na kutoa bastola mbili na moja
alimpa Khajat, kisha walikuja tena kwenye gari
na kuniuliza.
“Mlango mwingine wa kuingilia ndani ya ofisi
zenu uko wapi?” aliuliza Felly.
“Hakuna mlango hapo zaidi ya huo, mlango mwingine ni mpaka uzunguke kwenye lile
ghorofa kubwa ukapitie ghorofa ya pili ndio kuna ngazi ya kushuka kutokea chini.”
Nilimueleza hayo Felly lakini kabla hajamaliza kunisikiliza Khajat alidakia.
“Nimeona ndani kuna jamaa wanne na wote
wana silaha, sasa kuna liledirisha pale linaweza kutupelekea kwenye ‘ventilation’ tukapita hivyo
mpaka ndani kisha tutashukia kwenye huo
mlango anaosema Patrick.” Alimwambia Felly na kwa pamoja niliona wakiondoka taratibu,waliingia kwenye kile kidirisha na baada kama ya dakika tano nilisikia mlio wa risasi na watu huku nje walianza kukimbia, nilishuka kwenye
gari na kuanza kukimbilia kule ndani kuangalia kama kuna jinsi naweza kusaidia. Nilipofika karibu na mlango alitoka mmoja wa wale
wahalifu na kuanza kukimbia na mimi nilianza kumkimbiza, nilikimbia na mwendo wa mita mia tatu mbele nilimkaribia na kumpiga mtama kisha alianguka chini, alipokuwa anageuka ajitetee nilishtuka kuona buti likipita mdomoni kwake na kumfanya ateme damu,nilipotazama
ni nani nilitabasamu kwakuwa alikuwa ni Felly.
“hahaa” nilijikuta nikicheka yule jamaa alishikwa akapelekwa mpaka pale ofisini na maaskari walikuwa wameshafika wakawachukua na kuondoka.
“Nyie hamfai kuolewa, hahaa” niliwatania na kuingia ndani ya ofisi walipokuwa wamekusanyika wafanyakazi wote.
“Jamani poleni sana kwa yaliyotokea, kwa kipekee na niaba ya kampuni niwashukuru Felly na Khajat kwa msaada wao mkubwa
uliofanikisha wote hapa kuwa hai lakini kuzuia fedha na mali zetu zisiharibiwe. Kampuni itaangalia namna ya kuonyesha jinsi inavyothamini walichokifanya. Naomba kwasasa wakati nawasiliana na wenzangu wa utawala,kila mtu amalizie kazi zake ndani ya nusu saamfumo mzima wa kompyuta utazimwa na kazi
kwa leo tutakuwa tumemaliza.” Nilimaliza
kuongea na wafanyakazi na hapo mimi pamoja
na kina Khajat tulikuwa pale nje kwaajili ya
kutoa kwanza maelezo ya awali na hatua
nyingine za kipolisi ziliendelea.

**JIONI YAKE**

Tulikuwa nyumbani na wakina Khajat walikuja
kumuona mtoto kama kawaida yao ya kuja kila
jioni kumtembelea Pamela, nilikuwa bado
nikichanganywa na lile swala la pale ofisini
lakini zaidi lilikuwa swala la Dany.
“Jamani, kuna kitu kimetokea leo
kimenifadhaisha sana lakini nahitaji pia msaada
wenu wote wa mawazo na namna yeyote.”
Niliwaambia kabla ya kuendelea.
“Baba Cris na wewe, swala la kazini
siumeshasema jamani na polisi watafatilia.”
Aliongea Pamela aliyekuwa amenogewa na
maongezi waliyokuwa wakiyafanya pale.
Nilinyanyuka na kwenda dirishani nikifikiri nawezaje kuliongelea hivyo na nilipopata namna niligeuka na kuongea nao;
“Sio swala la kazini, ni tukio lililotokea mda mfupi kabla ya tukio la kuvamiwa kwa ofisi.”Niliongea kwa upole na pamela alikaa kimyaanisikilize.
“Ndio lililokufanya ukae pale chini si ndio?”aliuliza Felly.
“Ndio, ndilo lililonifanya nikae pale chini na kulia.” Niliongezea na hapo nilihisi machozi yakinitoka lakini niliyazuia.
“Patrick umelia leo?” aliuliza Pamela.
“Nini kilitokea?” aliuliza Khajat
“Nilimuona kijana mmoja anaitwa Dany, Daniel Mfangavo, huyu ndiye alikuwa ‘bestman’wangu. Huyu ndiye aliyekuwa rafiki yangu wa siku nyingi sana, nilipomuona nilimuita aliitika na kugeuka, nilikwenda kwa furaha na kujaribu kumpa mkono lakini alianza kukimbia huku akisema mimi ni mzimu. Nilijaribu kumfata ili niweze kumuelezea lakini ikashindikana kwakuwa watu walikuwa wakishangaa na
mwishowe nilimuacha akatokomea. Imeniuma sana kwakuwa sasa nimepata picha halisi kuwa huko Tanzania mimi nitakuwa kituko mbele za watu siku wakiniona.” Niliwaeleza hayo huku nikiwa bado na maruweruwe ya kilichotokea pale.
“Kwahiyo ni Mtanzania?” aliuliza Khajat.
“Ndio ni Mtanzania, na itakuwa yupo huku kwa biashara au kikazi labda.” Nilimjibu huku akili yangu bado ikikumbuka tatizo lililotokea. Mimi na Dany tulijuana mda mrefu sana toka kipindi nikiwa kidato cha pili na toka pale tulikuwa marafiki wakubwa sana na tulibahatika hata kuwa ndugu. Maisha yangu na Dany yalikuwa ni
kama mtu na kaka yake. Tuliishi vizuri sana na
mpaka yeye anafikia umri wa kuoa mimi ndiye
nilikuwa msimamizi wa ndoa yake na pale mimi
nilipooa yeye ndiye aliyekuwa msimamizi wa
ndoa yangu. Undugu wangu na Dany ulizidi
hata undugu wangu na Mark ambaye alikuwa ni
ndugu yangu wa damu.
“Kesho asubuhi itanibidi nikafatilie kwenye
makabrasha ya ofisi za uhamiaji na kama kuna
taarifa yoyote basi tutajua alipo na mimi
nitamfata kwaajili kuongea naye na
kumuelimisha kabla ya wewe kuongea naye.”
Aliongea Khajat na mjadala wa hilo ulikuwa
umefungwa mpaka kesho yake. Khajat alikuwa
ni mtu wa vitendo zaidi kuliko maneno, alikuwa
kama dada yake, hakuwa anapenda kuongea
sana juu ya mambo ambayo ipo njia ya kuya fahamu bila nadharia nyingi kuhusishwa.
“Hilo nadhani Khajat atalikamilisha, ila Patrick kuna kitu kingine inabidi ukifahamu na uwe makini sana kuelewa na uwe na moyo mgumu.”Aliongea Felly na hapo macho yalinitoka.
“Njoo ukae mpenzi.” Aliniambia Pamela ambaye alionekana kama kufahamu anachotaka kusema Felly. Mapigo ya moyo yalizidi kunienda mbio,nilijua kabisa Felly huwa anaongea kuhusu Mary tu kwakuwa amekuwa akijielekeza sana katika kufanya Uchukuzi wa namna mbinu za kunihujumu ulivyofanyika. Nilitegemea tena kusikia kuna baya lingine limetokea. Hivyo nilikaza moyo na kwenda kuketi pale karibu na Pamela aliyekuwa amenishikilia vilivyo.
“Baada ya habari kupelekwa na Mary
akishirikiana na Mark kuwa umefariki na mwili wako haujapatikana, taharuki ilitanda ndani ya familia na nje ya familia yako. Hali hiyo ilikuwa mbaya sana hasa kisa kizima na mafanikio uliyoyafikia kuwashika wengi sana. Taharuki hii ilipelekea vifo viwili, cha kwanza ni cha mama yako mzazi aliyefariki kwa shinikizo la damu baada ya kupata taarifa ya kuwa umefariki,alifariki akiwa nyumbani kwenu na kifo kingine ni cha baba yako aliyepooza baada ya kupata ile taarifa. Baba yako alitaka kuagiza uchunguzi binafsi ufanyike juu ya kifo chako lakini kuna siku alikutwa amefariki. Taarifa ya madaktari inayopatikana kwenye tovuti ya hospitali
inayoitwa Regency iliyopo huko Tanzania
inaonyesha kuwa alifariki kwa kukosa hewa.
Lakini kwa maelezo ya Pamela ambaye
nilimuonyesha ile taarifa ya daktari inaonekana
kuna habari zinakosekana kwenye taarifa ile.
Ukiangalia ile taarifa, (akamtuma Pamela ailete
kwenye ngamizi yake, na ilipokuja aliendelea
kuelezea), kuna namba za kurasa hazionekani
sawia. Kwamfano kwenye taarifa inayoonyesha
kuwa alikuwa ameishiwa pumzi na ndio chanzo
cha kifo chake, kwenye kurasa ya 5 ilitakiwa
ifate kurasa ya 6 na 7 ndio ije kurasa ya 8, ila
taarifa ina kurasa namba 1 mpaka 5 kisha
inafata 8 mpaka 9. Hii inamaana kuwa kurasa
ya 6 na 7 imechomolewa. Je kurasa hizo
zinahusu nini? Ndilo lilikuwa swali la msingi
lililonifanya sasa niombe ushauri wa kidaktari
kwa Pamela ili kujua kitu gani kilichomolewa
kwenye hiyo taarifa. Sasa alichoeleza Pamela ni
kwamba kwenye ile kurasa ya tano inaishia kwa
kueleza tu kuwa marehemu aliishiwa pumzi,
lakini kurasa za nyuma hazionyeshi kama
marehemu alikuwa na pumu, au kwamba
alikuwa sehemu isiyokuwa na hewa, hivyo swali
la kujiuliza ni je marehemu alikosa pumzi au
alikoseshwa pumzi? Majibu yote haya mawili
yanaweza kujibiwa kwa njia ya kitaalamu ya
kidaktari, mfano kwenye karatasi
zilizochomolewa Pamela anasema zitakuwa
zinaelezea mazingira ya mgonjwa kukosa hewa,
lakini pia kurasa ya nane ambayo ni
muendelezo wa kurasa zilizochomolewa
zinaonyesha kuwa kuna neno linamalizia na
‘mto’ au ‘kabali’. Hii kwa maneno mengine ni
kwamba hilo tatizo la kukosa hewa linaweza
kuwa limesababishwa na marehemu kubanwa
na mto ambao Pamela anasema ni njia rahisi
ya kumkosesha mtu pumzi ambao kwa dakika
kumi tu humfanya mtu kukosa hewa na kufariki,
kwa maelezo ya Pamela ambayo hata hivyo
yanashabihiana kabisa na sehemu ya taarifa,
anasema kuwa mtu akibanwa na mto usoni na
kwa mkandamizo mkubwa inamfanya mtu
kukosa dakika 1 hadi ya 3 na kuanzia dakika ya
4 mpaka ya saba kitendo cha kukosa hewa
huaribu ubongo na mfumo wa taarifa na
kusababisha hadi mfumo wa hewa huaribika
kabisa na dakika zinazopata huwa ni kupoteza
uhai. Hayo yote ni kweli na yanathibitishwa na
sehemu ya taarifa hiyo iliyochomolewa ambayo
niliipata baadaye ikitoka kwa mtu anayejiita
dokta Muya kwenda kwa Mary na pia kutoka
kwa Mary kwenda kwa Mark na baadaye kutoka
kwa Mark kwenda kwa mtu mwingine
anayeitwa Paul, taarifa hiyo ilionyesha kuwa ni
kweli mzee wako alifariki kwa kukoseshwa
hewa na alikutwa pingili zake za uti wa mgongo
za shingoni zinazounganisha na fuvu la kichwa
zikiwa haziko sawa, hii inamaana kuwa
kulikuwa na kujitetea wakati akizibwa pua na
mdomo na kwakuwa mkandamizo ulikuwa
mkubwa ilisababisha shingo yake kucheza na
ndio moja ya vitu vilivyoharakisha kifo chake.
Taarifa hiyo toka kwa dokta kwenda kwa Mary
ilikuwa imeambatana na ujumbe uliosema
‘tayari imeondolewa kwenye mfumo wa
kompyuta na kijana anasubiri pesa yake’,
ujumbe huo ulijibiwa na Mary kwenda kwa
dokta Muya kuwa ‘malipo nimeyafanya muda
sio mrefu, shilingi laki 5 utampa na shilingi
milioni moja utaweka vocha’. Baada ya kufanya
mawasiliano hayo, Mary alipokea ujumbe toka
kwa Mark ambaye hati yake ya kusafiria
inaonyesha hakuwa Tanzania wakati huo,
ujumbe ulikuwa ukisema ‘umefanya kazi nzuri
beb, namalizia kufanya packaging ya kontena
moja la mwisho kisha wakishapakia mimi
nitarudi na British Airways kesho’. Baada ya
ujumbe huo Mary siku hiyohiyo alimtumia
ujumbe huyo mtu anayeitwa Paul, ujumbe huo
ulisomeka ‘kazi ya taarifa imekwisha na tayari
milioni moja imetumwa kwako na secretary
wangu, sasa nataka kazi ya yule P.I uikamilishe
leo, waambie na kina Jof na malipo yao ya laki
6 kila mmoja yatafanywa leo jioni. Mkimaliza
hiyo hatutaenda Arusha nataka tuanze
kujipanga kwa Master plan, you should all be
set, Buberwa ataleta schematic kisha tutapanga
ni ambush au ni nini.’ Ilimaliza sehemu ya
ujumbe huo, ujumbe huu umezua maswali
mengi moja ikiwa ni hao kina Jof na Paul
wanakazi gani inayoitaji mchoro na mpango.
Hilo nimekosa majibu yake ya kiundani.”
Alimaliza kuongea Felly na wakati huo mimi
nilikuwa nimejawa na hasira na sikujua nilie au
iweje.
“Kwahiyo wazazi wangu wote wawili
wamefariki?” nilijikuta nikiuliza swali ambalo
majibu yake nilikuwa nayo tayari.
“Ndio” alijibu Pamela. Machozi yalinitoka na
nikajihisi kabisa kuwa nilikuwa ninaota.
“Je kwanini walimuua baba yangu?” nilimuuliza
Felly aliyekuwa akinitazama.
“Baba yako alikuwa amemuajiri mtu kufatilia
ukweli wa kifo chako, sasa ilikuwa ni ngumu
sana taarifa kutopatikana kama baba yako
angefatilia ndio mana wakamuua, lakini
mawasiliano ya Mary na Paul yamemtaja yule
mpelelezi binafsi kama ndiye anayefata kwenye
orodha pale waliposema P.I yani Private
Investigator. Na kuna baadhi ya mambo
nimefatilia inaonyesha kuwa Mary anahisa
kwenye kampuni ya Alsad Drilling Company
iliyopo Urusi, hisa hizi alirithishwa na baba
yake, na pia anamiliki kampuni nyingine mbili
Msumbiji na nyingine iko Afrika ya kusini, kazi
za kampuni hizi hazijulikani wazi na pia usajili
wa kampuni hizo una utata kwani inaonekana
kwenye kila nchi imesajiliwa kama kampuni
tanzu ya kampuni inayoitwa Mary and Unique
Supplies lakini kiukweli hakuna kampuni kama
hiyo. Mfano kwenye muongozo wa kampuni ya
Afrika ya kusini kwenye kifungu cha biashara za
kampuni inaonyesha ni kampuni inayohusika na
utoaji wa ushauri kwa wachimbaji wa madini
na mambo ya chemikali za migodini,
inaonekana pia kampuni hii inamakao yake
makuu Pritoria na Maputo, lakini kwenye miji
hiyo hakuna ofisi hata moja inayomilikiwa na
Kampuni hizi. Hii inafanya wasiwasi uwepo juu
ya kazi za Mary.” Aliongea Felly aliyeonekana
kuwa makini sana na kile alichokuwa akikieleza.
“uuf.” Nilishusha pumzi na kumgeukia Pamela
aliyeonekana kuwa mnyonge sana, nilimtazama
na yeye aliangalia chini.
“Nini kingine ambacho sikifahamu hapa Felly.”
Nilimuuliza Felly.
“Ambacho hakifahamiki hapa nadhani ni nia ya
yote haya na huo mpango mkubwa Mary
aliomwambia Paul angeufanya. Haifahamiki
kwanini Mark alishiriki kwenye kusababisha
yote haya, na kingine ambacho hukifahamu ni
kwamba baba yake na Mary alifariki mwezi
uliopita kwa ajali ya gari akiwa anatokea
sehemu inaitwa Arusha. Na huyo Dany
unayemuongelea anamagari yake kumi ya kitalii
aliyoyakodisha kwenye kampuni ya GEOMARY
ambayo inamilikiwa na Mark na Mary, hivyo
kukuona wewe huku kunaweza kupeleka picha
mbaya Tanzania na pengine tutategemea lolote,
lakini kabla ya chochote kutokea sisi tutafanya
namna ya kuwahi. Nimeshafanikisha kutega
mawasiliano yote ya Mary na Mark ya barua
pepe na hapo ni pa kuanzia tu. Khajat atafatilia
ya Dany na tukifanikiwa kumpata yeye ndo
atatusaidia.” Alisema Felly. Nilikaa kimya tu
sikujua cha kusema niliamua kushukuru lakini
nilichokuja pia kugundua kumbe Pamela alikuwa
pia akiwalipa kama motisha ya kufanya kazi
hiyo, nilifarijika lakini kazi kubwa ilikuwa ni je
nini kitafata????

ITAENDELEA
 
Ooooh nashukuru mkuu Willy Gamba 1 kwakuendeleza hii kitu, ntakuepo hapa till the end
 
Last edited by a moderator:
RIWAYA;KISASI
MTUNZI; FRANK MUSHI
SEHEMU YA KUMI NA MOJA

Nimeshafanikisha kutega mawasiliano yote ya
Mary na Mark ya barua pepe na hapo ni pa
kuanzia tu. Khajat atafatilia ya Dany na
tukifanikiwa kumpata yeye ndo atatusaidia.”
Alisema Felly. Nilikaa kimya tu sikujua cha
kusema niliamua kushukuru lakini nilichokuja
pia kugundua kumbe Pamela alikuwa pia
akiwalipa kama motisha ya kufanya kazi hiyo,
nilifarijika lakini kazi kubwa ilikuwa ni je nini
kitafata????
“Unafikiri kuwa kwakuwa hakupendi basi wewe
huna thamani. Unafikiri hivyo kwakuwa tu
hakutaki tena, na kwamba yuko sahihi,
kwakuwa mawazo yake na Hukumu yake juu
yako iko sahihi. Kama amekufukuza na
kukupiga basi wewe ni takataka. Unahisi yeye ni
wako kwakuwa unataka uwe wake. Hapana
usifanye hivyo. Ni neno baya sana kusema ni WAKO. Hasa unavyolitumia kwa mtu unayempenda WEWE. Mapenzi hayatakiwi kuwa
hivyo. Umeshawahi kuona jinsi mawingu
yanavyopenda mlima? Hujizungusha pembeni
yake na kuna wakati huwezi kuuona mlima
kwakuwa tu mawingu yameufunika. Lakini
unajua kuwa ukienda juu ya mlima utaona kilele
chake? Na hii ni kwakuwa mawingu hayafuniki
kilele cha mlima. Kilele cha mlima huonekana
kwa juu kwakuwa mawingu hukiachia,
haikifuniki. Huuacha mlima uweke kichwa chake juu, huru bila kuwa na kitu cha kuuficha juu au kuusonga. HUWEZI KUMILIKI MTU. Huwezi
kupoteza usichokuwa nacho. Kuna muda jifunze kuwa mbinafsi ili kuzuia kuumia na wale uwapendao.” HII NI SEHEMU YA KUMI NAMOJA,

**PATRICK**

Kuna mambo nilikuwa nikiona hayawezkutokea
kwa binadamu wa kawaida. Kuna mambo
mengine niliona ni kama simulizi za kusadikika
na kwamba hayawezi kumtokea mtu kabisa.
Kila mtu ni kipofu wa kesho yake, laiti kama
ningejua nini kitanitokea katika maisha yangu
basi pengine ningetumia uwezo wangu na pesa
zangu zote kuzuia haya yasitokee. Maswali
yalikuwa ni mengi sana, swali kubwa ni kwamba
Mary alikuwa na mpango gani na mimi. Mark
anahusikaje toka mwanzo kabisa wa mapenzi
yangu na Mary. Majibu yalikuwa ni machache
na yasiyo ya kuaminika kabisa kwa maswali
yote niliyojiuliza. Dany angepatikana ndiye
pengine angeweza kunipatia majibu machache
kati ya mengi niliyoyawaza.

*******
Kesho yake asubuhi nilikwenda kazini kama
kawaida na nilipofika pale maaskari na maafisa
upelelezi walikuwa wakinisubiri kwaajili ya
kumalizia upelelezi wa awali. Tulikaa pamoja
na kuzungumza na walipomaliza waliondoka na
mimi niliendelea na kazi.
“Ngriiiiiiiii,,,ngriiiiii.” Simu yangu ilikuwa ikiita na
nilipoitazama nilikuta ni Khajat.
“Hallow Khajat.” Nilimsalimu huku nikitabasamu
kama vile aliniona.
“Hallow Patrick, kuna Maswali nilitaka kukuuliza
kwanza.” Aliongea na kusikika kama alikuwa
akichapa kitu kwenye kompyuta.
“Sawa uliza nakusikiliza.” Nilijiweka tayari
kujibu maswali yake sawia.
“Ulisema Dany anaitwa nani jina lake kamili?”
Aliuliza na kunyamaza kidogo.
“Daniel Mfangavo.” Nilimjibu na yeye alikuwa
kama anaandika.
“Je inawezekana ndio yeye anaitwa Daniel
Fredrick?” aliniuliza tena na mimi nilikaa kwa
muda nikitafakari kama anaweza kuwa yeye.
“Ndio, jina la baba yake ni Fredrick Mfangavo.”
Nilimjibu na yeye aliendelea kuuliza.
“Je unafahamu jina la mke wake?” aliuliza swali
hilo ambalo lilikuwa jepesi kwangu kwakuwa
mke wa Dany alikuwa ni rafiki yangu mkubwa
sana toka kipindi tukiwa sekondari.
“Ndio, anaitwa Catherine Cathbert.” Nilimpa jibu
lakini akaonekana kama kuguna vile.
“Umesema Catherine Cathbert?” aliniuliza tena
na kunyamaza kidogo.
“Ndio, vipi kwani?” nilimuuliza tena. Kwa
vyovyote nilijua kuwa kuna kitu hakipo sawa.
“Subiri kidogo usikate simu.” Aliniambia hayo na
nilisikia kupitia simu kama vile akibonyeza
vitufe vya simu kama ishara ya kwamba
alikuwa akipiga simu, kisha baada ya muda
kidogo nikasikia akiongea kwenye simu.
“Hivi uliniambia umekutana na jina Catherine
Cathbert?” alimuuliza huyo aliyekuwa akiongea naye kwenye simu, ikaonekana kama vile
ameshapata jibu la swali alilouliza na kisha aliendelea.
“Ni mke wa Dany, hivyo endelea kuanzia hapo.”
Alimaliza kuongea na nikasikia akikata simu.
“Patrick.” Alirudi tena kwenye simu tuliyokuwa tukizungumza na kuniita na nilipoitika hakunipa
muda wa kumuuliza chochote bali aliendelea na maswali.
“Dany na Mary walijuana lini?” aliniuliza na
nilikuwa nikisikia kabisa akiandika kwenye kompyuta.
“Aah Dany alimjua Mary wakati nilipoanza
mahusiano na Mary na si kabla ya hapo.”
Nilimjibu na hapo Khajat aliniambia nisubiri kidogo, alipomaliza kuandika aliongea tena.
“Dany anafanya biashara gani?” aliniuliza tena na hapo sikuwa na ushahidi na biashara
anayofanya kwa sasa lakini nikijuacho ni kwamba Dany alikuwa ni meneja wa hoteli kubwa jijini Dar es Salaam na alikuwa akimiliki
kampuni ya utalii ambayo hata hivyo ilikuwa ni
ndogo sana ambayo nilikuwa na mpango wa
kuja kuiunganisha na kampuni yangu
niliyotegemea kufungua hapo baadaye.
“Ni meneja wa hoteli na anamiliki kampuni ya utalii.” Baada ya kumjibu aliendelea tena na maswali.
“Urafiki wenu na Dany ulikuwaje.” Aliuliza swali jingine.
“Alikuwa ndiye mtu ambaye alijua siri zangu zote, kila kitu kwenye maisha yangu yeye ndiye alijua na kila kitu chake aliniambia. Ni rafiki yangu mkubwa na ninayemuamini kama nilivyokuwa nikimwamini mama yangu.” Baada ya hapo Khajat aliniulizwa swali la mwisho.
“Je mpaka sasa kwa walioko Tanzania ni nani unamuamini sana?” sikuwa nimemuelewa vizuri sana.
“Sijakuelewa swali lako.” Nilimuomba alirudie tena swali hilo.
“Kuacha mimi, Pamela na Felly, nani mwingine unamuamini?” lilikuwa swali gumu sana lakini sikuwa na namna zaidi ya kueleza ukweli wa hisia zangu.
“Namuamini sana Dany, ni kwa vile tu hajajua
ukweli kuwa niko hai na nimehujumiwa sana, na
ninajua kama akijua ukweli atatusaidia
kurudisha kila kitu changu.” Nilimueleza hayo
kisha aliniaga na kukata simu.Baada ya muda
kidogo Pamela alikuja pale kazini na alipita
moja kwa moja mpaka ofisini kwangu, nilijiuliza
ni kwanini alikuja ofisini kwa muda ule lakini
nilituliza akili ya kujiuliza baada ya yeye
kunieleza nia yake ya kuja pale.
“Ni mekuja kukuambia kuwa tunaenda na Felly
sehemu fulani hivi kuna rafiki yangu nampeleka
akamuone ilikumsaidia kwaajili ya mambo yake
kisha tutawahi kurudi.” Alineleza hayo lakini
moyoni nilikuwa na wasiwasi sana juu ya
walikokuwa wanatakiwa kwenda.
“Lakini sio hatari huko mnakokwenda Pamela?”
nilimuuliza na kuonyesha dhahiri wasiwasi
wangu kitu kilichoonekana kumvunja moyo.
“Sio hatari Patrick, ingekuwa hatari wala
nisingethubutu kabisa kwenda, najua nimetoka
hospitali muda si mrefu sana na ninatakiwa
nipumzike angalau miezi mitatu lakini huku
tuendako ni muhimu zaidi kwa Felly kukamilisha
uchunguzi wake ili jioni atupe mrejesho wa
alichokuwa akikifanyia uchunguzi.” Alijitahidi
kunishawishi na mimi sikuwa na kitu cha
kupinga. Alikaa pale kidogo na Felly alikuja.
“Hey Patrick najua utakuwa na wasiwasi,
atakuwa sawa ili mradi yuko na mimi,
ananifikisha kwa huyo mtu kisha nitampa
dereva amrudishe.” Aliongea Felly na hapo
waliondoka. Kwenye majira ya saa tisa mchana
kazi zilikuwa zimekwisha na Khajat alikuja
kunifata pale ofisini.
“Patrick nimefanikiwa kujua kujua Dany alipo
sasa nataka twende wote ila utajificha sehemu
nakuwekea hivi vidude masikioni utakuwa
ukisikia nikiongea nae na hata wewe utaweza
kuniambia chochote kama ukitaka, nataka
nimfate kwanza mimi nimjue vizuri kisha
tutaangalia kitu kingine cha kufanya.” Aliongea
Khajat na hapo aliniwekea kidude fulani hivi
kama kifungo na kuongea kisha nilimsikia
kupitia kile kidude, akawasha gari na sasa
tukaondoka mpaka kwenye bar moja maarufu
sana pale Fiji, tulipofika Khajat alishuka na
kuniambia nimfate. Tukaenda mpaka kwenye
sehemu fulani kulikuwa na kona ya kupumzikia
watu na pale tukakutana na dada mwingine
ambaye sikuwa namfahamu.
“Vipi yuko wapi?” Khajat alimuuliza yule dada.
“Nimeshamtengea sehemu ya peke yake yuko
kwenye ile kona pale una muona?” yule dada
akamuonyesha Khajat.
“Patrick, Dany ni mdhaifu wa nini mana kila mtu
anaudhaifu wake.” Aliniuliza Khajat na kunifanya
nicheke.
“Dany anapenda sana wanawake.” Nikamjibu
huku nikiendelea kucheka.
“Najua Dany ni mdhaifu wa wanawake lakini
unajua ni mdhaifu wa sehemu gani ya
mwanamke?” aliuliza tena Khajat na kunifanya
akili yangu irudi nyuma na kukumbuka kipindi
tukiwa shuleni. Kabla ya Dany kuwa na Cathe
alikuwa akimpenda sana msichana mmoja
aliyekuwa akiitwa Anjela, sio kwamba alikuwa
akimpenda sana, hapana alikuwa akimtamani zaidi, kilichokuwa kinamfanya amtamani Anjela ni mapaja yake meupe, na kila mara alikuwa akiniambia hilo. Hata mama yake Dany kabla ya kufariki kipindi Dany akiwa shule ya msingi aliwahi kusema mwanae ni mbaguzi sana hata marafiki huwa anapenda weupe tu. Hivyo ugonjwa wa Dany ni mapaja meupe.
“Anapenda sana mapaja hasa meupe kama
yako.” Nilimjibu Khajat na yeye alicheka kisha aliniambia nimsubiri pale. Akaondoka na yule.msichana na baada kama ya dakika kumi alirejea pale. Alikuwa kapendeza sana ndani ya sketi fupi sana iliyoacha mapaja yake nje.
“Kama hivi.” Aligeuka huku na huko ili
nimtazame.
“hahaa, ndio kama hivyo, umependeza sana.” Nilimwambia Khajat na yeye alicheka na.kukonyeza.
“Sasa, mimi nitaenda kuonana na Dany pale.Wewe utakuwa hapa utasikiliza anayoniambia kama ni ya kweli ama la kama ikitokea nimemuuliza kitu unachokijua, uwe mvumilivu inaweza kuchukua zaidi hata ya masaa 8 kuwa na mazoea nae. Ukiona tumeondoka nitakupa.ishara na wewe utakuwa na huyu dada hapa atakuongoza kila kitu na sehemu ya kwenda,nataka kujua vitu vingi sana kwake hivyo itachukua muda.” Aliongea Khajat.
“Sawa, hilo kwangu mimi sio tatizo.”
Nilimwambia na hapo alianza kufikicha macho yake mpaka yakawa mekundu kabisa.
“Khajati ndo unafanya nini hivyo.” Nilimuuliza kwa mshangao, macho yake yalikuwa mekundu.kama vile alikuwa akilia.
“Hii ni sehemu ya mchezo, nitakie mafanikio basi.” Alicheka wakati akijibu.
“Nakutakia mafanikio mema.” Aliondoka pale na nilimuona akielekea kwenye ile meza aliyokaa Dany. Sikujua alikuwa anataka kufanya lipi na
lipi, sikuelewa kabisa angefanyaje ili kufanikisha hayo aliyoyakusudia. Nilikuwa nimekaa pale nikitamani sana kuongea na Dany, huyu jamaa ni rafiki yangu sana, tulianza wote kutafuta maisha na kutembeza wasifu wetu kila sehemu kabla ya kuamua kujiajiri wenyewe. Mara zote nilikuwa nikikaa kwao na yeye akikaa kwetu.
Dany hakuwa na mama kwakuwa mama yake
alishafariki toka yeye akiwa shule ya msingi
hivyo nyumbani kwao walikuwa watoto wa
kiume tu lakini pia wawili walifariki kwa ajali kipindi tukiwa wakubwa kabisa, hivyo Dany alibaki kuwa peke yake. Hivyo mimi ndiye nilikuwa ndugu yake wa kipekee kabisa.
“Dada unalia nini?” Nilishtuka na kusikia sauti ikiuliza swali hilo. Mh! nikaguna na kutazama
kule alikokuwa Khajat. Nikaona Dany akiwa.karibu naye na Khajat alikuwa ameinama akilia. Sikujua imetokeaje.
“Khajat mbona unalia nini kimetokea.”
Nilimuuliza Khajat kwakuwa nilijua angenisikia
kupitia kile kidude alichoniwekea.
“Niko sawa usijali hakuna tatizo lolote.” Alinijibu
na mimi nilisikia nikamuelewa lakini jibu
alilonipa liliendana na swali alilouliza na Dany
hivyo Dany alidakia.
“Hakuna tatizo wakati unalia dada, nambie nini
tatizo naweza kukusaidia.” Dany alidakia na
kuonyesha nia ya ukaribu.
“Nyie wanaume ni nyoka kabisa, nimempenda
alaf leo anakuja kuniacha pasipo sababu,
kwanini jamani?” Khajat alizidi kulia mpaka
ikabidi mimi nitoe kile kidude nicheke kwanza.
Dany ikabidi aanze kumbembeleza pale mpaka
Khajat akanyamaza. Nikarudisha tena kile
kidude sikioni ili niweze kusikia yanayojiri.
“Usijali maisha ndivyo yalivyo, haimaanishi
mmoja kukufanyia hivyo basi wote ni ndivyo
walivyo. Kuna muda lazima ujifunze kuacha mtu
aondoke kama hataki kukuthamini, ujifunze
kujali zaidi furaha yako kuliko ya mtu asiyejali
ya kwako. Kuna muda lazima mambo fulani
yatokee ili dunia izunguke. Maisha yataenda
kama utajifunza kuwa mbinafsi muda
mwingine.” Aliongea Dany kwa busara ya hali
ya juu.
“Uuf angalau nina jisikia nafuu kwasasa,
naomba muite muhudumu nataka pombe kali.”
Aliongea Khajat na hapo Dany alimuita
muhudumu na kumuagizia amletee pombe kali.
Dany hakuwa mnywaji toka zamani sasa
sikujua itakuwaje hapo kwenye kunywa ila
Khajat alimlazimisha kunywa na muda si muda
niliona wakikumbatiana na kupigana mabusu.
Dany alishaanza kulewa na kuongeaongea.
Muda ulizidi kwenda na mimi nilikaa pale tu
nikisubiri maelekezo yoyote. Nikamuona Khajat
akitoka pale na kuelekea chooni kisha
aliniambia nimfate, muda huo giza lilikuwa
limeshaingia. Nilikwenda mpaka choo cha
wanawake.
“Patrick wewe unatakiwa sasa uende nyumbani,
Felly anakuja hapa utaondoka akishafika, nenda
akae na Pamela.” Aliongea hayo na mimi
sikuwa na pingamizi kwakuwa nilikuwa
nimechoka.
“Sasa na wewe unavyokunywa pombe hivyo
siutashindwa kufanya kazi?” nilimuuliza huku
nikimtazama.
“Hahaaa, hizi kazi nimefanya kwa miaka mingi
sana Patrick, hata ninywe ndoo nzima pale
silewi, atalewa yeye, kwenye ile glasi
ninayotumia nimeweka kidonge cha kukata
kilevi, hivyo mimi pale nakunywa pombe tu
isiyo na kilevi ila yeye ndiye anayekunywa yenye
kilevi ndo mana unamuona hajielewi. Felly
ameshafika fanya uende.” Aliniongelesha na
tuliagana akaondoka, bado aliniambia kuwa
nitamsikia kupitia kile kidude nisikitoe.
Nikaondoka mpaka nyumbani na nikiwa njiani
nilisikia bado Khajat akimsisitiza Dany
wakalale. Kwasauti ya Dany niliyoisikia ni kama
vile alikuwa kalewa sana. Baadaye nilisikia tena
sauti ya Khajat ikimuelekeza Felly namba ya
chumba na hoteli waliyokuwa wakienda na Felly
alimwambia CC2 italetwa kwenye chakula na
muhudumu kisha anajua cha kufanya ili
wafanye kazi kwa ukaribu. Sikuwa nimeelewa ni
nini na mimi ikabidi niingilie.
“Hey CC2 ndo nini nyie watu.” Niliuliza na
nilisikia sauti ya Khajat ikicheka.
“Ni Coca kete mbili, coca ndiyo mmea
unaotumika kutengenezea madawa ya kulevya
ya kokein.” Alinijibu na hata kabla sijauliza
chochote waliendelea na mazungumzo yao na
baada ya muda mfupi sikusikia kitu tena kwa
maana ya kwamba mawasiliano nao yalikatika.
Nilifikia nyumbani na tulikaa na Pamela na
mtoto wetu Cris na hadi tunaenda kulala
hakukuwa na taarifa yoyote toka kwa Khajat
wala Felly na kwakuwa kesho yake haikuwa
siku ya kazi basi wao walikuwa wa kwanza
kufika kwetu asubuhi na kutuchukua mpaka
kwa Felly kwakuwa kule ndio kulikuwa na vifaa
vya uhakika vya kutufanya tuelewe vizuri
watakayokuwa wanatuambia.
“Twendeni kule chini nikatumie ile kompyuta
kubwa.” Aliongea Felly na hapo tulishuka ngazi
na kwenye kwenye chumba kilichokuwa chini ya
ardhi.
“Ataanza kuongea Khajat kisha mimi
nitamalizia.” Aliongea Felly.
“hahaa aanze dogo sio.” Nilitania na wote
walicheka.
“Hahaa, sawa bhana, ila dogo sasa hivi ni
Cris.” Walicheka tena wote na Khajat alianza
kuongea.
“Jana nilianza kazi ya kumtafuta Dany na
nikagundua ameingia nchini kwa biashara,
amekuja kufatilia magari ya kitalii aliyonunu
kwenye kampuni moja iliyoko huku.
Nikabahatika kupata namba yake ya simu
aliyoitumia kumpigia afisa mmoja wa uhamiaji
na ndipo nilipotafuta eneo ambapo ile namba
ipo kwa wakati huo, nikaenda na Patrick mpaka
pale na nilifanikiwa kumpata Dany zaidi ya vile
nilivyotarajia. Baadaye Patrick ulipoondoka
mimi nilikwenda na Dany hotelini na nilifanikiwa
kumuwekea dawa na hapo alilala kabisa. Hivyo
mimi na Felly tulipata muda wa kupekuwa
kompyuta yake na simu na kutambua
mawasiliano yake mengine.” Alimaliza Khajat na
Felly alidakia.
“Katika kutafuta Dany, jana nilikuta mawasiliano
ya barua pepe toka kwa mtu anayeitwa
Catherine kwenda kwa Mary, ujumbe ulikuwa
ukieleza juu ya kuingiza magari yake kwenye
mzunguko wa kampuni yake kama vile walivyo
ahidiana, hii ilikuwa ni mwezi mmoja toka baba
yako afariki, lakini ujumbe huo ulijibiwa na
ulisomeka kama ifuatavyo ‘nakumbuka shem,
tena najua unadai mengi sana na asante kwa
uvumilivu wako, kesho nitamu assign mtu
atakuja kuyaingiza kwenye payroll na wewe
utatuma vijana wako wayalete’ sehemu ya
ujumbe huo ambao ulisomeka hivyo ulikuwa
kwenye anuani ya cathe.co@gmail.com na
uliandikwa kwa mchanganyiko wa lugha ya
kingereza na Kiswahili na Pamela ndiye
aliyetusaidia kutafsiri maneno ya Kiswahili.
Ujumbe huo pia ukajibiwa tena kwa lugha ya
kingereza kuwa ‘thanks, though it was a great
pain but atlist we have accomplished the
mission’ (asante, japokuwa yalikuwa ni
maumivu makubwa lakini angalau
tumekamilisha mpango), swali nililojiuliza
lilikuwa ni huo mpango ulikuwa upi? Na pia
aliyetuma barua pepe hii alikuwa ni nani, je ni
Dany au ni Catherine, jibu lilikuwa ni dogo tu,
kama Cathe ndiye angekuwa ametuma ule
ujumbe basi Mary asingemwita shemeji, hivyo
aliyetuma ule ujumbe alikuwa ni Dany. Baadaye
siku hiyo hiyo ile anuani ya barua pepe ilituma
ujumbe kwa mtu aliyeitwa Paul akimwambia
‘nilitambulishwa kwako na Mary, nimefurahia
kazi yako ya nje na ya ndani. Nategemea
kufanya kazi na wewe ikitokea kuna ulazima’,
ujumbe uliishia hapo na Paul aliujibu. Hapa
kumbuka kuwa Paul ni yule ambaye Mary
alimtumia ujumbe kumwambia juu ya
kukamilika kwa mpango wa kuchomoa zile
karatasi lakini zaidi kumwambia ajiandae kwa
mpango mkubwa utakao fata. Hivyo mpaka
hapa Paul ndiye kijana wa kazi za kihalifu wa
Mary. Kuna wasiliano pia ya Mary kwenda kwa
Paul akimwambia ‘tembea juu ya nyayo za
Mark, subiri ujumbe wenye G na O itakuwa ni
red light and when it turns green, you know
what to do, mind you, this is the master plan,
after this we will be done with all the shit and
you will go back to Al Hamid for the Pritoria
event”(itakuwa ni taa nyekundu, na ikibadilika
kuwa ya kijani, unajua cha kufanya,
nikukumbushe kuwa huu ndo mpango mkubwa,
baada ya hili tutakuwa tumemaliza upuuzi wote
na utarudi kwa Al Hamid kwaajili ya tukio la
Pritoria), huu ulikuwa ujumbe toka kwa Mary
kwenda kwa Paul uliotumwa siku tatu kabla ya
leo, meneno ya Kiswahili tumepata tafsiri toka
google. Pia kwa kipindi cha nyuma kuna ujumbe
ulitoka kwa Dany kwenda kwa Mary na hiki ni
kipindi kile Mary akiwa bado yuko huku, ujumbe
huo ulikuwa ukisomeka ‘Hey Mary, you didn’t
bring me up t speed for two day, is there a
prob? Setup is in place, green code to
you.’ (Hey Mary, hujanipa taarifa kwa siku
mbili, kuna tatizo lolote?, mazingira yako sawa,
unaweza kuendelea) maneno yaliyotumika hapa
ya green code na mengine ni maneno ambayo
hutumiwa na watu wenye mafunzo ya kijeshi au
wapelelezi au majasusi au majambazi wenye
uelewa wa lugha za kijeshi. Hii ikanipa
wasiwasi sana, nikaendelea kutafuta
mawasiliano mengine ambayo yalikuwa kati ya
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Alsad
Drilling Company ya Urusi na Mary
akimuelekeza kuwa atakuwa tayari kununua
hisa zote na kuihamishia kampuni hiyo nchini
Tanzania baada ya kukamilisha mpango wa
kumuondoa mtu ambaye ni kikwazo, ujumbe
unamueleza jinsi alivyofurahishwa na mbinu
aliyompa ya kufungua kampuni Maputo na
Afrika ya kusini ila pia anashukuru kwa zile
sanduku za silaha zilizofanikiwa kumfikia bila
tatizo na hivyo ameimarika na sasa yuko tayari
kwa kazi baada ya vijana wake kumaliza
mafunzo. Hizo ni habari chache tu, lakini kubwa
ni kwamba tunaye Dany hapa ndani.” Felly
alifungua mlango mmoja uliokuwa pale ndani
na nikamuona Dany akiwa amefungwa kwenye
kiti na mdomo wake ukiwa umefungwa pia,
alikuwa na majeraha kiasi usoni.
“Dany!!” nikamsikia Pamela akimwita kwa
mshangao.
“Unamjua?” Nilimuuliza Pamela.
“Huyu ndiye aliyenibaka yeye na ndugu zake
kipindi kile nikiwa nafanya kazi kwao.” Sikujua
cha kusema, Khajat aliufunga ule mlango na
kutugeukia tena.
“Kibaya zaidi ni kwamba leo asubuhi Mary
amemtumia Dany ujumbe kuwa tayari
wameshafanikiwa kumuua MARK usiku wa leo
na sasa wako huru kuendelea na mambo
mengine.” Aliongea Khajat.

ITAENDELEA
 
RIWAYA: KISASI
MTUNZI: FRANK MUSHI

SEHEMU YA KUMI NA MBILI

“Kushindwa kupanga ni kupanga kushindwa.
Kanuni ya mafanikio katika lolote binadamu
afanyalo huwa ni KUWA NA MPANGO THABITI,
mpango hukueleza ni wapi unataka kufika na
kwa kiasi gani. Mipango ya mafanikio yetu
hupangwa na vichwa vyetu pamoja na fikra
tulivu zinazotawala mioyo yetu, ukiwa na
mpango kinachofata ni MKAKATI, hii huwa ni
njia ya utekelezaji wa mpango wako. Ukijua
uendako ni rahisi sana kupata njia ya
kukupeleka huko, hata kama utachelewa kiasi
gani lakini ni rahisi sana kufika huko. Maisha
hayana kanuni maalumu wala haikuhitaji uwe
na elimu kubwa sana ili ufanikiwe katika
maisha, unachotakiwa tu ni kujitambua, kuweka
mipango, kutafuta mkakati, kuweka vipaumbele,
kujiamini na kusimamia unayoyaamini,
UKIMALIZA YOTE HAYO KIKUBWA NI UWE NA
HAMU KUBWA YA KUFANIKIWA INAYOZIDI
WOGA WAKO WA KUSHINDWA. MAISHA
MAZURI NI WEWE TU KUYATAFUTA.” HII NI
SEHEMU YA KUMI NA MBILI

Wengi najua watatokea sana kumpenda Khajat,
kwenye hii simulizi nilitamani sana Khajat
asikike akisimulia, japo sikujua kingereza lakini
nilikuwa nina uhakika sauti yake tu ingenieleza
Khajati ni mtu wa aina gani. Usiku niliuona
mfupi hasa ukizingatia muda huo ilikuwa
ikielekea saa 9 usiku, na kipindi kilikuwa
kinaisha saa kumi na mbili kasoro ili kupisha
idhaa ya Kiswahili ya shirika la utangazaji la
Uingereza. Kwenye sehemu hii ya kumi na moja
ndiyo niliona ni kwa namna gani Khajat alikuwa
si mtu wa mchezo. Pia nikagundua kuwa Felly
ni mpole sana ambaye huongozwa na hisia na
hisia hizo humfanya ashindwe kumtesa mtu.
Lakini bado najiuliza huyu Mary ana mashetani
gani,,unajua nini mwandishi? Patrick aliendelea
kusimulia hivi;

**PATRICK**

Kizunguzungu cha fikra kilinikamata, kila
nililoelezwa pale lilikuwa ni kama mchezo wa
maigizo au ndoto za alinacha, Dany anahusika
kwenye kusuka mpango wa mimi kuuawa?
Haikuwa kitu rahisi sana kukiamini hasa kwa
kuwa Dany alikuwa ni rafiki zaidi ya ndugu.
Alikuwa ni rafiki ambaye kama angekatwa
mikono yote miwili mimi ningeweza kukata
mkono wangu mmoja nimpatie ilimradi tu wote
tuwe na angalau mkono mmoja. Nilijikuta nikilia
sana kwakuwa hata kumuuliza nini kilisababisha
yote hayo ilikuwa ni kitendawili. Toka
tulipokutana shule ya sekondari ya St. Thomas
kula Tabora miaka ile tukiwa kidato cha pili
mimi nikiwa nimehamia pale na kumkuta yeye
akiwa amehamia pia toka shule ya Trust iliyoko
jijini Dar. Siku hiyo ya kwanza tu tukawa
marafiki kama tulijuana miaka mingi, kwakuwa
tulikuwa ni watundu sana ilikuwa rahisi sana
kufahamika, wasichana wote shuleni pale
walitujua hasa kwakuwa tulikuwa wageni lakini
waongeaji kuliko wenyeji. Dany alikuwa na
kipaji cha kuimba, alikuwa na sauti nzuri sana
ya kuimba, mimi nilikuwa na kipaji cha uandishi
wa hadithi na makala za kielimu pamoja na
kuigiza. Tulipofikisha mwezi mmoja toka
tuhamie Dany akiwa na mwezi mmoja na wiki
tulipeleka barua kwa mkuu wa shule juu ya
kuanzisha gazeti la shule ambalo lilikuwa ni
karatasi kubwa ya mita mbili iliyokuwa na
vipande vya makala mbalimbali, hadithi na
katuni pamoja na habari zilizojiri pale chuoni,
mkuu wa shule alituelekeza kuwa tuliandae
alione kwanza na sisi tuliandaa tukawashirikish
a wanafunzi wengine wenye kujua habari za
michezo na wanaofahamu mambo ya sanaa za
muziki wa nje pamoja na mwalimu mmoja wa
sayansi ambaye alikuwa anaandika makala za
afya. Gazeti hili lilikuwa libandikwe kwenye
ubao mkubwa wa matangazo na lingesomwa na
kila mtu ambaye angetaka. Tulifanikiwa katika
hili, tukajulikana sana pale shule na kupendwa
na kila mtu wakituita mapacha. Tulianzisha
kundi la kuhimiza matumizi ya kingereza mda
wote na kuliita English Club, likakua na
tukaanza kupata mialiko toka mashule mengine,
tuliandika muswada (script) kitabu cha THINGS
FALL APART cha Chinua Achebe na kuanza
kufanya mazoezi ya kukiigiza kitabu kile kwa
zaidi ya mwezi, tulishirikisha watu wa vidato
mbalimbali, tukapata udhamini wa bodi ya
shule walioahidi kutuletea kampuni ya
kutengeneza maigizo hayo. Tulifanikiwa kuigiza
na kutolewa kwenye CD ule mkanda ulioitwa
Things Fall Apart ambao baadaye ulitumika
kufundishi kwa karibu shule nyingi za seminari
na mashule mengine. Wazazi wetu wakajuana
na sasa tulikuwa zaidi ya ndugu. Dany kwetu
alikuwa ni kama mtoto wao na vivyo hivyo
mimi kwao. Kwakuwa mama yake na Dany
alifariki kipindi Dany akiwa shule ya msingi hiyo
ilimfanya Dany kuwa mnyonge mda wote lakini
baada ya kukutana na mimi kila kitu kilikuwa
poa. Nilipotenda kosa basi ujue na Dany
alikuwepo, nilipokuwa na majonzi tulikuwa
pamoja, tulitumia pesa pamoja na tulifaidika na
kila tulichokianzisha. Sisi tulikuwa chanzo cha
upendo kwa wanafunzi wengine, tukiwa shuleni
sio tu tulikuwa wabunifu ila tulikuwa njema
sana darasani. Mara zote tulikuwa
tukibadilishana namba mbili na tatu, tulipofika
kidato cha tatu tulibuni kipindi kimoja
tulichokiita jumamosi ya burudani na pia Usiku
wa vipaji. Shuleni ilikuwa ni kusoma kuanzia
jumatatu hadi jumapili, hivyo tulikuwa
tunachoka sana lakini baada ya kukaa na
kutafakari nilimwambia Dany tubuni kitu tukiite
Jumamosi ya burudani, basi tuliandaa andiko
tukapanga kuwa siku ya jumamosi badala ya
kwenda kujisomea usiku basi wanafunzi wote
wakusanyike kwenye ukumbi wa mikutano na
kisha jukwaani kutakuwa na mziki na watu
watapanda kwaajili ya kucheza kwa wale
wanaoweza kucheza, wale wanaoweza kuimba
wataimba, na wale wenye vichekesho na
burudani nyingine watafanya hivyo, Jumamosi
ya burudani ilikuwa inaanza saa 1 jioni na
kuisha saa 4 na nusu usiku. Pia Usiku wa Vipaji
lilikuwa ni tamasha la vipaji vya uigizaji, mitindo
na uimbaji pamoja na vichekesho na uchezaji
ngoma, hii ilikuwa ni kwaajili ya kuendeleza
vipaji vya wale waliokuwa navyo, usiku wa
vipaji ulikuwa ufanyike kila mwisho wa muhula,
yani siku moja kabla ya kwenda nyumbani na
zawadi zingetolewa. Mkuu wa shule alikubali
yote haya. Kikundi chetu cha kingereza
kilitanuka zaidi na kuwa English and Computer
Club, yote haya yalituunganisha kama
wanafunzi. Baada ya kumaliza shule wanafunzi
hawakujizuia kutoa machozi kwa wale
tuliowaacha, tulitengeneza Jarida kubwa lenye
kuonyesha matukio mengi sana tuliyofanya pale
shuleni. Hakika ilikuwa kumbukumbu tosha.
Maisha yaliendelea na kidato cha tano
nilichaguliwa kwenda Benjamini Mkapa na Dany
alichaguliwa kwenda Azania. Mda mwingi
tulisoma pamoja na tulikuwa tunapokezana wiki
hii Dany alikuwa anavaa sare za shule za Benja
na kuja kusoma shuleni kwetu kwakuwa
hakukuwa na ufuatiliaji sana na vivyo hivyo na
mimi. Dany aliwahi kuumwa na kupungukiwa
damu, nilikaa hospitali mwezi mzima sikwenda
shule kuhangaika na ndugu zake. Hayo
yalikuwa maisha yetu na Dany, mtu ambaye
alishiriki kila aina ya maisha yangu, mtu
ambaye nilimuamini na kumpenda kama ndugu
yangu na zaidi hata ya ndugu. Nilichopata
kilikuwa chetu sote na alichopata yeye kilikuwa
chetu sote. Mtu ambaye nilikuwa namthamini
kuliko hata Mark. Hakuna siri ya maisha yangu
ambayo yeye hakuijua, tulitoroka wote shule,
tuliadhibiwa pamoja, alipogombana na
Catherine mimi ndiye niliyekuwa msuluhishi,
mimi nilipogombana Fatima yeye ndiye alikuwa
msuluhishi. Tulichukua wasichana marafiki na
tulikuwa makini kila mmoja kuhakikisha
mwenzake haumizwi. Leo hii huyu Dany
ambaye alijitolea kugharamia safari yangu ya
mapumziko baada ya ndoa yangu na Mary,
safari iliyogharimu zaidi ya milioni 15 ndiye
mmoja wa watu waliopanga kifo changu, Dany
aliyekuwa msimamizi wa ndoa yangu leo hii
ndiye anafanya haya, huyu Dany ambaye nilitoa
pesa yangu ya faida ya miezi minne ya
kampuni yangu kugharamia harusi yake yote
iliyogharimu milioni 55 ndiye yeye adui wangu
wa leo. Alifikiria nini wakati akiyafanya haya?
Nini kilimpata? Hayo ni baadhi tu ya maswali
ambayo ningependa anijibu.
“Patrick!” aliita Khajat.
“Unatakiwa sasa ujikaze, muda wa kufanya
maamuzi ndio huu, muda wa kukaa na kulia au
kutafakari umwekwisha sasa, katika maisha ya
binadamu kuna muda wa kutafakari na muda
wa kutenda. Ukiwa mtu wa kutafakari muda
wote utakuwa unachelewa kwenye kila jambo.
Adui ni adui tu hata awe baba yako.
Akishajigeuza na kuwa adui basi hakuna kufikiri
tena juu yake zaidi ya kutenda kama
ulivyopanga kutenda iwapo ungemkamata adui.
Najua Dany kakuumiza sana, najua pia Pamela
leo na yeye kakutana na adui yake lakini wote
lazima mjifunze kukaza mioyo.” Aliongea Khajat
aliyekuwa tayari ameshafungua mkoba wake na
kuuweka pale mezani, alivaa gloves tayari na
alikuwa ameshikilia kifaa cha kukatia kucha
maarufu kwa lugha ya kigeni kama Nail Cuter.
“Patrick unahitaji kwenda kwenye mazishi ya
ndugu yako?” aliuliza Felly.
“Sidhani kama ipo haja ya mimi kwenda
kumzika, nataka kujua mambo mengi sana
kabla sijarudi Tanzania, nataka kujua kwanini
haya yote yametokea.” Nilimwambia Felly na
wakati huo bado nilikuwa nimekaa nikitazama
ule mlango ambao Dany alikuwapo.
“Felly, tunapoteza muda. Mtu Patrick kama
hautakuwa na roho nyepesi naomba usikae
hapa na Pamela pia. Tunataka kujua vitu vingi
toka kwa Dany na bahati mbaya mimi si mtu
wa kuhoji kwa maneno mengi, hivyo kama kuna
yeyote kati yenu anaogopa damu basi aende
akakae na Cris chumbani.” Aliongea Khajat
huku akiwa na sura yenye kutabasamu.
Alitutazama na Pamela bado alikuwa akilia
lakini alisema yuko tayari kuona damu ya Dany
na hiyo ingempa nafuu kiasi kwa machungu
aliyokuwa akisikia.
“Khajat, unataka kumfanyaje.” Aliuliza Felly.
“Nampa XT 1, itamfaa, nia yangu ni kumfanya
ajute sio kuchukua tu taarifa toka kwake,
nafahamu hata nikimpiga kofi atasema ila
nataka ateseke kwanza kabla ya kumkabidhi
Patrick amfanye atakacho.” Aliongea Khajat
huku akikata kucha na kile kikata kucha.
“Hii ndiyo kazi niliyojitolea maisha yangu
kuisomea na kuifanya kwa moyo. Niliisomea
kwakuwa niligundua kuwa mimi ni kati ya watu
wachache duniani ambao hawata kwenda
mbinguni lakini pia ni kati ya watu wachache
ambao wako tayari kufa muda wowote na hivyo
nafanya lolote kubwa ili nikiwa sipo
nikumbukwe.” Aliongea Khajat na kufungua ule
mlango kisha Dany alitolewa pale kwenye kile
kisehemu alichokuwa amefungwa. Khajat na
Felly wakamfunga kwenye kiti kingine vizuri na
kama mikono pamoja na miguuni na sehemu
nyingine, kisha Khajat alimvua shati na kumtoa
ile Solotape mdomoni.
“Dany, umemuona rafiki yako.” Khajat
alimwambia Dany lakini Dany hakunitazama
usoni.
“Dany nilikukosea nini?” Nilimuuliza huku
machozi yakinitoka lakini bado hakujibu wala
kunitazama.
“Patrick usihangaike kumuuliza, muda ukifika
atajibu yote hata yale ambayo hujamuuliza.”
Aliongea Khajat kwa kujiamini. Muda huo Felly
alikuwa pembeni kimya akiwa anaipekua bado
ile laptop ya Dany.
“Unamjua Pamela? Yule pale uliyeshiriki
kumbaka wewe na ndugu yako na kisha baba
yako naye alimuingilia, na hata alipofukuzwa na
kuitwa Malaya nyie mlichekelea.” Alimuuliza
swali hilo pia hakujibu. Khajat akamrudishia
tena ile solotape mdomoni ili asiweze kuongea
au kutoa sauti.
Dany alikuwa bado ameangalia chini na kila
nilipokuwa nikimtazama nilikumbuka sana
kipindi cha urafiki wetu, hiyo ilinifanya nizidi
kutoa machozi, Khajat alikuwa ametoka kidogo
na aliporudi alikuwa ameshikilia chupa ya
pombe kali na mkono mwingine alikuwa na
Spirit ya kuweka kwenye kidonda, alifungua
mkoba wake na kutoa chupa la damu kisha
alilitundika ukutani na kuvuta ule mrija kisha
akamchoma Dany na kuruhuru damu ianze
kuingia nilimuona Dany akiwa anatetemeka kwa
hofu na wakati huo mimi nilihisi woga wote
umeondoka na hata ningeambiwa nimfanye
chochote kwa wakati huo ningefanya, alikuwa si
rafiki tena. Khajat akamimina ile pombe kali na
kunywa glasi moja kisha alimtazama Pamela
aliyekuwa ametoa macho kusubiri kuona
kilichokuwa kikiendelea.
“Dany najua kuwa uko tayari kusema yote,
lakini muda wa kusema wewe bado haujafika,
hivyo usihangaike kufikiria kuwa sasa ni muda
wa kujibu maswali, hapana huu ni muda wa
majuto.” Khajat alivuta kiti na kukaa karibu
yake kisha alichukua kitambaa na kumfuta
Dany lile jasho kifuani, akamwaga ile pombe
kali iliyokuwa kwenye ile glasi na kuchukua ile
mashine ya kukatia kucha akaanza kumbana
nayo Dany kifuani na kukata nyama
kidogokidogo kama vile alikuwa anakata kucha.
Pamela alishindwa kuvumilia na kuamua
kuondoka pale lakini mimi nilikaa nikishuhudia
jinsi Dany alivyokuwa akiteseka. Nilimtazama
alivyokuwa akilia kama mtoto nikatamani
kumuonea huruma lakini huruma haikuja. Khajat
anaroho ngumu kuliko mtu yeyote niliyewahi
kumuona duniani. Pamoja na damu nyingi
kumtoka Dany lakini Khajat hakuwa anaogopa
kitu, mdomo ulikuwa umevungwa na hakuweza
kuongea chochote japo alizidi kulia. Ile mashine
ya kukata kucha ilikuwa ikifinya na kukata
kinyama kidogo sana kitu kilicholeta maumivu
makali, nilimtazama na taswira ya tulivyokuwa
shule ikanijia. Dany alikuwa amelowa kwa
damu, Felly alikuwa makini kwenye kazi zake na
wala hakuwa na wasiwasi wowote, kwake
ilikuwa ni kama jambo la kawaida sana. Baada
ya kuhakikisha kuwa ile glasi ndogo imejaa vile
vinyama vidogo vya kifuani kwa Dany, Khajat
alinyanyuka na kuchukua kitambaa kisha
akamwagia Spirit kwenye vile vidonda hali
iliyosababisha Dany apige kelele mpaka
kupoteza fahamu. Na baada ya hapo Khajat
alivua zile ‘gloves’ na kumfata Felly pale alipo.
Mimi nilikuwa bado niko pale nikitizama.
“Patrick, hiyo ni adhabu ndogo sana niliyompa
na ni kwakuwa sioni adhabu nyepesi zaidi ya
hiyo. Usihofu hatakufa kwakuwa damu inaingia
mwilini kwake na tulimpima mwanzoni hata
shinikizo la damu wala ugonjwa wowote wa
mwili hivyo sio rahisi afe kabla ya wewe kulipa
kisasi.” Aliongea Khajat huku akinitazama.
“Inabidi kumuhoji sasa, mtengenezee yale maji
umuashe, kuna vitu hapa natakiwa nimuulize
kwanza ili tujue kama Patrick anaweza kusafiri
kwenda Tanzania au la.” Aliongea Felly
akimwambia Khajat na baada ya hapo Khajat
aliondoka kuelekea juu, nilitoka na kumfuata
nyuma.
“Patrick huna moyo wa kiume kabisa, ni bora
ungekuwa muumini wa kanisa. Lakini
sikulaumu ni kwakuwa pengine unaamini sana
dini, lakini nitafanya yote badala yako.”
Aliongea Khajat huku akinitazama.
“Khajat, kuna muda utajua roho yangu ilivyo,
kwasasa nataka kujua kwanza sababu ya kila
jambo. Naelewa kabisa ninachotakiwa kufanya
ila lazima kwanza nijue chanzo cha yote ni nini,
nani alianzisha haya, yalianza lini na
wamepanga kwenda mpaka wapi.” Nilimuambia
Khajat ambaye hata hivyo alinitazama na
kukubaliana na mimi japo alionekana kabisa
kuwa hakuamini maneno yangu.
“Anaweza kuishi kwa muda gani?” nilimuuliza
Khajat.
“hana kitu cha kumfanya afe kwa muda huu, ile
adhabu ni ndogo. Mimi naelewa kanuni za
mateso, yule pale nimeshtua mishipa yake
lakini hiyo sio shida. Damu yake ipo kawaida
kwakuwa inaingia mwilini na tulivyomfunga
mwili wake hauchezi sana, tukimalizana naye
tutamtundikia drip ya maji ilia pate nguvu zaidi.
Atakuwepo mpaka mwisho wewe usijali.”
Alinijibu na tulikuwa tumeshafika juu na
kumkuta Pamela akiwa amelala kwenye kochi.
“Pamela.” Nilimuita na yeye alishtuka.
“Patrick, sitaki kumuangalia yule mbwa,
alininyanyasa sana na kunitesa. Ni kwakuwa
nilikuwa sina wazazi ndio mana aliona mimi
naweza kuwa ni shimo la choo la wao kuweka
uchafu wao na kuondoka si ndio? Waliniumiza
sana, familia nzima waliniigilia bila ridhaa
yangu, walinibaka na kuniita Malaya, kisha
kunipa elfu 45 kwa kazi zote nilizofanya kwa
miezi hiyo? Tena nafukuzwa eti nitawaua watu
mule ndani kwa ukimwi? Yani wao wanibake
alafu mimi ndo niwe wa kuwaambukiza
ukimwi? Kweli jamani?” Pamela alikuwa
akiongea huku akilia kitu kilichomfanya Khajat
atokwe na machozi. Mimi sikuwa na la kusema
nilibaki kumkumbatia tu.
“Pamela, usilie, kila kitu kitalipwa sawa na
maumivu yako.” Aliongea Khajat na kufungua
jokofu kisha alitoa pilipili mbichi kwenye mfuko,
zilikuwa ni zaidi ya pilipili 50 kwenye ule mfuko.
Nilimuacha Pamela pale na kumfata Khajat
aliyekuwa akielekea jikoni.
“Za nini hizo?” nilimuuliza Khajat ambaye tayari
alikuwa ameziweka kwenye mashine ya
kutengenezea juice na kuanza kuzisaga.
“Ni dawa ya kumuamsha.” Aliongea Khajati
huku akiongeza maji kiasi na baada ya dakika 1
ilikuwa imeshakuwa kama juice nzito. Ilikuwa ni
kali kiasi cha kutufanya wote tuliokuwa pale
tukohoe kasoro Khajat peke yake aliyekuwa
kawaida. Alishuka na ile pilipili kwenye kibakuli
kisha tulipofika pale chini alivaa gloves nyingine
mpya na miwani kubwa ya kuzuia ile pilipili
isiingie machoni. Dany alikuwa bado amepoteza
fahamu lakini Khajat alipopeleka lile bakuli
kwenye pua ya Dany alianza kupiga chafya, na
hapo alizinduka. Khajat alichukua ile pilipili na
kuimwaga kwenye vile vidonda vya vya Dany na
hapo alilia mpaka sasa huruma ilinijia. Nilihisi
uchungu aliousikia Dany pale alipokuwa
amekaa na hakuwa na jinsi ya kusema tena.
Khajat aliitoa ile solotape na sasa Dany
aliongea.
“Patrick nisamehe ndugu yangu, nateseka
Patrick naomba mwambie aniache. Khajat
inatosha naomba unisafishe naumia sana.”
Aliongea Dany huku akilia kwa uchungu na
mwili wake kutetemeka.
“Subiri maswali kabla sijakuvuruga zaidi.
Unachotakiwa kusema hapa ni ukweli wa kila
jambo ili ufe ukiwa umesema ukweli na sio
kuomba msamaha na kutaka kuachwa. Elewa
kuwa hapa ulipofika ndo mwisho, mbegu ya
watu wote wanaofanya wengine waishi kwa
tabu duniani ni lazima imalizwe kabisa ili waishi
watu wanaoweza kufata taratibu za
kibinadamu. Kwenye maisha ulikuwa una nafasi
ya kuleta furaha kwa kila aliyekutendea wema,
kama ulishindwa unachostahili ni adhabu
ambayo sio wewe utapanga.” Aliongea Khajat
kwa hasira na kumsindikiza na ngumi nzito ya
sikio iliyomfanya Dany atoe jicho kama vile
aliona pepo.
“Nisamehe Khajat.” Aliongea Dany.
“Nitazame vizuri usoni, unahisi mimi ni mtu wa
kusamehe? Nasamehe makosa ya kawaida ya
kibinadamu ila sio ya kijasusi, Swali la kwanza,
mpango wa kumpoteza Patrick ulianza lini?”
Aliuliza Khajat na Dany alikuwa kimya kama vile
akifikiria. Khajat ahakusubiri alirudi nyuma na
kuchukua ile mashine ya kukatia kucha kisha
alipeleka pale kwenye kidonda na kuvuta tena
nyama kisha kukata, huku akimtazama. Dany
alilia kwa sauti kubwa.
“Ilianza kabla ya Mary kurudi Tanzania.” Alijibu
na hapo nilishtuka ilikuwaje mpaka mpango huo
ukaanza mapema hivyo.
“Nani alisuka mpango huo kabla ya hapo.”
Aliuliza Khajat.
“Alikuwa ni Mary, lakini baadaye nilikuja
kukutanishwa na mtu wa tatu ambaye alikuwa
ni Mchungaji Priscus Mjata, ambaye ndiye
aliyewafungisha ndoa Patrick na Mary na ndiye
mshiriki wa kibiashara wa Mary, Mr. Ruyega
ambaye alikuwa ni dereva wa Patrick na pia
Mark alikuja kuunganishwa baadaye.”
“Mwingine nani?” Khajat aliuliza.
“aahh,,,mhh” Dany alianza tena kung’ata
maneno, alishtuliwa na ngumi nyingine ya uso
iliyofanya damu zianze kumtoka puani, wakati
huo mimi nimesimama kimya nasikiliza tu.
“Na,,,na,,,na mama yake Mark ambaye baadaye
tulikuja kujua kuwa yeye na Mary ndio walikuwa
wanausuka huu mchezo toka siku nyingi.”
“Mama yake Mark!!!!” nilishangaa na kujikuta
nimepigwa na butwaa.

ITAENDELEA!!
 
RIWAYA: KISASI
MTUNZI: FRANK MUSHI
SEHEMU YA KUMI NA TATU
Lisha mbwa wote chakula sawa kwakuwa hujui
yupi atakuokoa wakati wa hatari. Inawezekana
katika kuwalisha mbwa ukawa ukimpendelea
mmoja au hata kuwa pendelea wa aina fulani
tu, lakini katika kuenenda kwako ukakutana na
hatari ukiwa na mbwa wote. Wale uliowalisha
na kuwapendelea wakanenepa na kunawiri
wakakukimbia kwakuwa walikuwa na nguvu za
kukimbia, uliwalisha mpaka wakawa wajinga na
wavivu wa akili yao, hawakujua tena kuwa
wakila wanatakiwa wakulipe kwakuwa walinzi
wako na watetezi wako. Wale ambao
hukuwalisha, hukuwapendelea au kuwajali
wakabaki na wewe wakitamani kukutetea, lakini
wakuwa walikonda kwa upendeleo wako
uliowanyanyapaa na kuwatenga, wakawa
hawana tena nguvu hata ya kukupigania na
kukutetea. UTAKUFA HAPO. Majuto ni mjukuu,
ni mjukuu ambaye hutokea wakati wa dakika za
mwisho kabisa za Tumaini finyu lililobaki
kwenye mishipa ya damu. Kumjua mtu au
kutokumjua hakukupi sababu ya kumdharau au
japo kumuamini sana. Maisha ni kitendawili
ambacho wachache hukitegua kwa wakati
husika. USIMDHARAU MTU KWA KILE
ULICHONACHO AMBACHO YEYE HANA. KILA
MTU NI MUHIMU KWAKO, NI MUDA TU
HAUJAFIKA WA KUONA UMUHIMU WAKE
KWAKO”…………..HII NI SEHEMU YA KUMI NA
TATU.

Ndugu mwandishi, mpaka hapa ilikuwa tayari ni
saa kumi kasoro, ile CD iliendelea kuchezwa na
sauti ya Khajat ikasikika ikisimulia, yeye
alikuwa akisimulia kwa lugha ya kingereza,
lakini kuna msichana ambaye alikuwa akitafsiri
nahisi anaweza kuwa ni Pamela au mtu
mwingine yeyote, masimulizi yake yalikuwa hivi.

**Khajat**

>>MIAKA MINGI ILIYOPITA<<
Kila aina ya binadamu anayedhaniwa kuwepo
duniani ujue yupo. Muda wa maisha ukifika
basi unaweza kubahatika kukutana naye.
Maisha ya ukatili nilijifunza kipindi nikiwa jela
ya watoto, ni siku hiyo nilipoamka na kugundua
kuwa nilikuwa nikionewa. Nikajiuliza sana kosa
langu mimi ni nini mpaka yule mama anifanyie
haya yote, lakini sikujua. Inawezekana labda
nilikuwa mtukutu lakini yawezekanaje mimi
niwe mtukutu kipindi cha udogo wangu tena
wakati namuogopa yule mama kupita ukoma?
Kila siku asubuhi tulikuwa tukienda kupigwa
viboko viwili na yule askari wa kiume, lakini cha
kushangaza sikuzote aliniweka mimi wa
mwisho na wote walivyomaliza kuchapwa mimi
niliachwa bila kuchapwa. Hakuwa ananieleza
sababu ya yeye kuacha kunipa ile adhabu
ambayo ilikuwa ni lazima kwa kila mtoto
kupewa adhabu ile. Siku moja alikuja kunifata
tukiwa ndani na kunitoa nje, niliogopa sana
lakini hiyo haikuwa sababu ya mimi kukataa
kutoka nje.
“Nataka nikupe kazi, na ukifanikisha nitakupa
zawadi itakayokufanya ufurahi maishani.”
Alinieleza huku akijaribu kunishawishi, nilikuwa
mdogo lakini nilikuwa ni muelewa sana na
mwepesi kufikiri.
“Kazi gani.” Nilimuuliza kwa ile sauti yangu ya
kitoto.
“Nataka ukamuue mtu.” Aliniambia hukua
akinitazama kwa macho makali.
“Nani?” nilimuuliza na mimi, yule askari
alishangaa sana kwakuwa alitegemea pengine
ningekataa au ningetetemeka ila haikuwa hivyo,
nilikuwa tayari nimeshachafuka roho.
Nakumbuka nikiwa na miaka mitatu ndo
nilianza kupigwa, nilikuwa mdogo sana lakini
kumbukumbu za kile kipigo zilinijia siku zote za
maisha yangu, nilikuwa silali kwa raha kwakuwa
ndoto zilizidi kujirudia kwenye kichwa changu,
nikiwa na miaka mitano ndipo nilibakwa na
katika miaka hiyo ndipo nilifinywa na mama
sehemu zangu za siri na kupata kidonda,
nilishindwa kwenda shule lakini hiyo haikutosha
akanitafutia kosa na kuamua kunipeleka jela ya
watoto, huko pia kuna kipindi tulichanganywa
pia nikabakwa, nashukuru mungu kile kidonda
kilikuja kupona. Maisha ya jela yalinitengeneza
kuwa mtu mpya kabisa.
“Nataka ukamuue mtoto mwenzake, anayekaa
kitanda cha karibu na wewe, kisha ukitoka
humu ndani nitakupa kiasi kikubwa cha pesa.”
Aliniambia yule askari. Nilimuuliza sababu ya
kumuua lakini alinijibu majibu ambayo sikuwa
naona kama yanasababu yoyote ya kumuua
yule mtoto ambaye naye anapata shida pale
kama mimi, nikamkubalia na kweli akanipa
sumu nikamuwekee na mimi niliipokea lakini
nilizunguka na kumuwekea yeye ile sumu kwa
kuichomokeka kwenye sigara yake, ilikuwa ni
sumu ya unga ambayo nilitakiwa kwenda
kuipaka kwenye mto wa yule mtoto kisha
akivuta ingemfanya aanze kutoka damu puani
akiwa amelala kisha angefariki, hivyo nilikwenda
kupunguza ujazo ya ile sigara yake kisha
nikachomeka ule unga kidogo kwa ndani na
kurudisha majani ya ile sigara kisha alipokuja
kuvuta alianza kutoka damu puani na mpaka
alikufa pale ofisini nikiwa nachungulia. Hiyo
ndiyo siku niliyogundua kuwa nina uwezo
mkubwa sana wa kufanya mambo. Nilipotoka
niliendelea na shule kidogo lakini wakati huo
nilikuwa pia nikifanya kazi na kikundi kidogo
cha majambazi waliokuwa wakinipitisha
madirishani wakati wa kuiba, nilikuwa na akili
shuleni na hakuna mtu ambaye angeamini kuwa
mimi nilikuwa mtu hatari katika udogo wangu.
Nilifanya yote haya kwakuwa nilihitaji pesa za
kugharamia maisha yangu, sikuwa na mtu wa
kunisaidia, mama alikuwa akinitesa sana, kuna
mtoto wa mtaa wa kumi kutoka pale kwetu
alikuwa akiteswa na yeye na wazazi wake wa
kumzaa kwakuwa tu alizaliwa akiwa taahira,
iliniuma kwakuwa kila mra nilikuwa nikipita
wakati natoka Naporill kulekule Bombay
nilikuwa nikimuona akilia, huruma ilinijia na siku
moja usiku nilikwenda kwao nikapita dirishani
na kuingia mpaka kwenye chumba cha wazazi
wake, alikuwepo baba yake akiwa amelala hoi,
nilipitisha kisu kwenye koo lake na kuondoa
maisha yake.Niliua sana katika udogo wangu,
hasa watu wote waliokuwa wakifanya maisha
ya watu kuwa magumu. Hata wale majambazi
waliokuwa wakinituma na kuniingiza dirishani
nilikuja kuwaondoa duniani baadaye. Nilikuwa
hatari sana. Nilipopata pesa ya kuja kwa Felly,
nilikwenda uwanja wa ndege wa Chhatrapati
Shivaji na kuingia upande wa mizigo kisha
nilikuja Fiji. Maisha yangu ya nyuma niliyaacha
Bombay nchini India lakini nilikuja kuyaimarisha
kwakuwa mwema tu kwa kila mtu na mbaya
sana kwa wale wanaowafanya wengine waishi
maisha magumu. Niko tayari hata mimi
kuadhibiwa kwa lolote kama matendo yangu
yatamchukiza yeyote, huo ndo msemo niliokuwa
nikijiambia kila siku. Nilikwenda kwenye shule
ya jeshi, baadaye walinichukua na nilikwenda
mafunzo mbalimbali, lakini kubwa ni mafunzo
ya kutesa na kuua. Sijafundishwa kulenga
mguu, sijafundishwa kulenga kichwa,
nimefundishwa kuua kwa mkono.

**SASA**

Patrick alikuwa ni kinyume cha mimi.
Namaanisha nilikuwa mkatili sana, lakini Patrick
alikuwa ni mpole na mwema sana. Wema wake
sikuuchukia lakini uliniudhi muda mwingine.
Alikuwa na imani za kidini zilizomfanya kuwa
mtu wa kusamehe jambo kubwa lililohitaji
msamaha wa mauti kwa aliyekosa.
“Mama yake Mark alihusikaje kwenye hili?”
nilishtuliwa na sauti ya Felly aliyekuwa bado
akiendelea kumuuliza Mark maswali.
Nilimtazama Patrick alikuwa amekaa akisikiliza
huku machozi yakiendelea kutoka. Nikamtamza
Dany alikuwa anawasiwasi sana kila
nilipomkaribia.
“Mama yake Mark aliambiwa na Mary kipindi
bado akiwa Marekani kuwa kuna mpango wa
kupata pesa nyingi sana kama atakuwa tayari.
Na yeye alisema ndiyo yuko tayari, kipindi hicho
Mary alikuwa Urusi kwenye biashara zake.
Baadaye Mary alinipigia simu na kuniambia
kuhusu mpango wa kupata pesa, nilikubaliana
naye na yeye aliniambia kuwa anakuja Tanzania
ili tuweze kupanga kila kitu. Siku aliyokuja
alianza kwakuniambia kuwa anataka afungue
kampuni ya magazeti, kampuni kubwa ambayo
itakuwa na mtaji mkubwa sana, alaf baadaye
ndio tutafanya huo mpango aliokuwa nao,
tulikuwa na mama yake na Mark. Lakini kesho
yake mama yake na Mark aliniita na kuniambia
kuwa mpango uliopo ni wa kuichukua kampuni
ya Patrick na Mary ameshapanga kila kitu
mpaka kufanikisha kuichukua. Nilikataa lakini
siku hiyo nilipokuwa nataka kwenda kwa Mark
kumwambia, nilipigiwa simu na Mary,
akaniambia niende benki nikatoe pesa kiasi cha
laki nne kisha niende kuonana naye kuna jambo
anataka nimsaidie. Nilimuuliza pesa ni za nini
akasema nifanye hivyo ndo niende kwake.
Sikuwa na wasiwasi, nikaelekea ATM na kutoa
pesa, nikaingia kwenye gari na kuondoka nikiwa
njiani nikakumbuka sikuangalia nilibakiwa na
shilingi ngapi kwenye akaunti yangu kwakuwa
nilitakiwa kuwa na pesa nyingi kwaajili ya
kuagiza mzigo. Nilipoitazama ile karatasi yenye
kuonyesha salio nilikuwa na milioni 45, lakini
ninavyokumbuka akaunti yangu ilikuwa na
milioni 5 tu, hapohapo simu ya Mary ikaingia na
mimi nikapokea, wakati huo nilikuwa
nimeegesha garo pembeni ya barabara.
“Dany usiwe mjinga, tumeletwa duniani ili tuishi
kwa muda mfupi kisha tufe. Mgao wako
umeuona nadhani, nahitaji jibu lako sasa,
utaingia kwenye huu mchakato au ukose pesa
hizo milioni 40 na uhai wako.” Nilisikia sauti ya
Mary upande wa pili wa simu ikiniambia, ghafla
nikatetemeka na sikuwa tayari kuchukua ile
pesa.
“Mary sihitaji pesa yako.” Nilimjibu lakini alikaa
kimya kidogo na kuongea tena.
“Sawa Dany, hakuna mtu anayeweza
kulazimishwa kuchukua pesa hata siku moja,
mimi sina muda huo pia, pesa inatafutwa sasa
ukipewa ukaikataa basi hutakiwi kulazimishwa,
kata simu alaf nitafanya mchakato wa
kuirudisha kwenye akaunti yangu, wakati huo
wewe mpigie simu mkeo mkeo umuage
kwakuwa leo ndo mwisho wa wewe kuvuta
pumzi yako.” Aliniambia hivyo na mimi niliona
masihara, nikacheka lakini kilichofata kilinifanya
nione kuwa sio kawaida.
“Unacheka nini, nimekuambia kata simu Dany
umpigie mke wako, dakika tano zinakutosha
sana kusema yote. Tazama kifuani kwako kisha
uelewe ninachokisema.” Alisisitiza na mimi
nilipotazama kifuani niliona taa nyekundu kama
tochi vile mtu alikuwa akinimulika, sikutaka
kuongea tena nikakata simu na kuwasha gari ili
niondoke lakini sikuweza kwakuwa nilisikia
risasi ikipenya kwenye kioo cha upande wa
kushoto na kabla sijatafakari simu iliita nikaona
ni Mary akipiga, nikapokea.
“Shusha kioo.” Nikasikia sauti ya Mary
ikiniambia hayo, na mimi nikashusha huku
nikitetemeka. Nilipomaliza kushusha aliniambia
niangalie upande wa kulia wa barabara na
nilipoangalia nilimuona akiwa kwenye BMW.
Kisha aliwasha taa na risasi nyingine tena
ilikuja na kupiga upande wangu karibu kabisa
na sikio langu. Niligundua kuwa ile risasi ilitoka
mbele kabisa kama umbali wa mita mia moja
hamsini kutoka pale nilipo. Hivyo nikawa
napanga kurudisha gari nyuma ili nichomoke
kwa kasi lakini sikuweza kwakuwa nyuma
kulikuwa na magari mawili yamepaki pande
mbili za barabara.
“Huna pa kwenda Dany, kifo au ukae kwenye
familia yangu.” Alieleza Mary, sikuwa na namna
ya kufanya zaidi ya kumkubalia, nikakubali
kushirikiana naye. Lakini alichosema kitu cha
kwanza kwa mtu yeyote anayefanya kazi na
yeye ni usiri. Sikujua kama Mary ni mtu mwenye
nguvu vile. Alikuwa ni msichana mzuri lakini
alikuwa na nguvu ya kufanya atakalo. Mfano
kuna siku Mary alimpiga risasi mfanyakazi wake
kwakuwa tu alikuwa anaongea na simu na
kumtajia mtu kuwa bosi wake ni mkali. Hii yote
iliniogopesha na sikuwa na jinsi. Hivyo kwenye
mpango huu tulikuwa watu wanne, mimi Mary,
mama yake na Mark, na Mark ambaye alikuja
kuingizwa baadaye. Sisi tulikuwa wasikilizaji tu
wa mipango ya Mary na tulichotakiwa kufanya
ni kufungwa mkono. Baadaye Mary alinipeleka
mpaka Urusi kwenye kampuni ambayo alikuwa
na hisa nyingi, akanitambulisha kwa watu
ambao wengi walionekana kama majasusi, na
walikuwa wakimuogopa sana. Tukaja mpaka
hapa Fiji kwenye kampuni ya Hawadh Shipping
Agency ambayo ni kampuni pia ambayo yeye
anamiliki asilimia kubwa sana ya ‘share’,
akanikutanisha na Hawadh ambaye ndiye
mwenye kampuni na Gibson ambaye
alinitambulisha kama mkurugenzi wa kampuni
ya Katapila. Nilichokuja kugundua ni kwamba
Mary anaogopeka na anamtandao mkubwa,
lakini sikujua kamwe atawezaje kuchukua mali
za Patrick mpaka siku aliporudi Tanzania na
kudai kuwa Patrick amefariki. Niliamini kabisa
kwa maelezo yake, jinsi alivyoleta zile picha na
habari za kwenye magazeti pamoja na Mark
alivyokuwa akisema. Sikushtuka pia baada ya
baab yake Patrick alipouwawa kwakuwa nilijua
tu ni mpango pengine wa kuficha yote
tuliyopanga. Mary alituaminisha kuwa Patrick
hayuko hai. Nilijua ndio mpango umekamilika
baada ya sasa Mary kuwa mmiliki wa ile
kampuni na mali zote ambazo Patrick aliziacha,
ndio maana hata siku ambayo nilimuona Patrick
nilikimbia.” Aliongea Dany lakini nilihisi kama
kuna kitu natakiwa kukijua zaidi.
“Kwahiyo Mary ana kazi gani hasa?” Felly
aliendelea kumuuliza.
“Kwa kweli sijui, alinikutanisha na watu tu lakini
sikuwahi kumuuliza anafanya kazi gani nyingine
zaidi ya ile ya kampuni ya Patrick na ile ya
majarida anayotoa.” Dany alijitahidi sana
kuongea kwa ile sauti yake iliyojaa maumivu.
“Umesema ulikutana na Hawadh ambaye ni
mmliki wa Hawadh Shipping Agency, je huyo
Hawadhi yukoje?” Felly aliendelea kumuuliza.
“Ni kijana tu wa miaka 35 hivi.” Alijibu Dany.
“Na wewe ulikuja huku kuonana na Hawadhi?”
aliuliza Felly.
“Hapana nilikuja kwa shughuli zangu lakini
nikiwa huku Mary alinipigia simu nionane na
Hawadhi kuna vitu atanipa nimsaidie kuvisaini.”
Alijibu Dany.
“Je unafahamu kuwa Mary husafirisha Biskuti
kuja Australia?” aliuliza Felly.
“Hapana sifahamu.” Alipojibu Felly alinigeukia.
“Umechoka Khajat? Naona nadanganywa na
wewe upo hapa. Dany anaelewa sana juu ya
usafirishaji wa biskuti toka Tanzania unaofanya
na Hawadh Shipping Agency ya Tanzania na
ndiyo kampuni iliyomsaidia kusafirisha hata
magari yake. Hawadh walisafirisha konteza za
futi arobaini za biskuti miezi sita iliyopita na
nyaraka zilizoandikwa ziliandikwa kwa jina na
Priscila Michael, mzigo uliandikwa kuwa ni wa
Hawadh Enterprise, kiwanda mzigo ulipotoka
kinaitwa ni Priscila Food Industrirs, hii kampuni
ni kweli ipo lakini inauwezo mdogo sana,
nataka uniambie nini kinatengenezwa na ni vitu
gani ulikwenda kuweka sahihi.” Aliongea Felly
na mimi nilimsogelea Dany nikiwa nimeshikilia
kisu mkononi. Dany hakuwa tayari kusema,
nilimtsha lakini hakuwa tayari kusema lolote.
“Siwezi kusema chochote, Mary ni mnyama
zaidi ya mnavyodhani. Hakuna kati yenu
atakayemuweza hata kumfikia. Nikisema
chochote hapa basi familia yangu itakuwa
hatarini. Sina cha kuwaambia zaidi ya hicho
nilichosema.” Nilimtazama usoni nikaona ni
kweli hawezi kusema kwakuwa anamuogopa
Dany lakini dawa yake niliijua. Kabla
sijanyanyuka pale, Patrick alikuja na kunipora
kile kisu kisha akamchoma Dany kwenye mkono
lakini aliishia kulia tu, hakuweza kujibu
chochote. Niligundua kuwa Dany anajaribu
kujitoa kama vile ahusiki na kwamba
alilazimishwa.
“Nakuhimiza ujibu swali alilokuuliza Felly kabla
sijatoka hapa.” Nilimwambia Dany lakini
alikuwa kimya tu akilia. Kwa hatua hiyo
inamaana Dany alikuwa ameshayazoe
maumivu. Nilipanda mpaka juu na kuchukua
mashine za kizamani za kusagia nyama yani
zile za kutumia mikono kuzungusha, nilipofika
pale nilimkamata Dany mkono na kuingiza
vidole vyake viwili kisha nilichanganya na
vipande viwili vya nyama ili kuiweka mashinde
sawa na hapo nikaisukuma, Dany alilia sana
kwa uchungu lakini niliisukuma na kuvisaga
nusu kicha niliviweka chumbi iliyomfanya akojoe
kabisa.
“Niendelee?” nilimuuliza huku nikimtazama.
“Hapana, zile kontena hazisafirishi biskuti, ni
unga wa pembe za ndovu ndio zinasagwa na
kuwekwa kama biskuti ili isishtukiwe bandarini.”
Alijibu kwa haraka huku kamasi na machozi
yakimtoka.
“Na Mary kwasasa yuko wapi.” Nilimuuliza na
hapo alikaa kimya lakini nilipompelekea
maishine ile aliongea.
“MARY YUPO KWENYE NDEGE ANAENDA URUSI
AMETOKA TANZANIA LEO NA WIKI IJAYO
ATAKUWA HAPA FIJI.”

ITAENDELEA
 
RIWAYA: KISASI
MTUNZI: Frank Mushi
SEHEMU YA KUMI NA NNE

“Usidhani yanayokutokea sasa, au yale
uliyopitia ndiyo yatakayoonyesha wewe utakuwa
mtu wa aina gani hapo baadaye. Haijalishi
umetoka kwenye familia ya aina gani na wala
haijalishi maisha yako ya sasa yakoje. Lakini
uamuzi wako utakaoufanya sasa juu ya nini
unataka kukitilia mkazo na nini maana ya vitu
fulani kwako, aina ya mafanikio uyatakayo na
jinsi ambavyo utafanya ili kuyafikia ndicho
kitakachokupa mwanga wa mtu wa aina gani
utakuwa. Kila kitu duniani chenye mafanikio
kilianzishwa na mtu mmoja tu. Wazo huwa
kichwani kwa mtu mmoja nayeye
anaposhirikisha wengine bado tunahesabu kuwa
yeye ndiye aliyeleta jambo hilo. Kila mtu
mwenye mafanikio alikuwa na ndoto kabla,
akazichambua ndoto zake na kuziishi huku
akifanya kila njia kuzileta kwenye uhalisia.
WEWE UNANAFASI YA KUFIKA PALE UTAKAPO
KAMA UTAACHA KUJIDHARAU.” Hii ni sehemu
ya KUMI NA NNE.

Ilikuwa sasa ni saa 10 kamili usiku, Khajat
alikuwa amemaliza kusimulia na kuelezea
historia yake mpaka alipofika. Ndugu mwandishi
katika maisha ya kawaida ya binadamu
nilijifunza kumbe kuna muda watu wabaya
wanatengenezwa na matendo ya binadamu
wengine. Khajat alitengenezwa na matendo ya
yule mwanamke aliyefukiwa akiwa hai, ila sasa
Felly alianza kusimulia na yeye. Alikuwa
akiongea kwa lugha ya kingereza lakini
kulikuwako na mtu pembeni akitafsiri. Ilikuwa
hivi;

***FELLY***

>>MIAKA MINGI ILIYOPITA<<
Kwenye maisha nilijifunza kujitegemea toka
nikiwa mtoto kabisa. Kipindi ambacho nilikuwa
binti aliyetakiwa kupata malezi ya wazazi ndiyo
muda ambao nilikuwa mtaani nikitafuta maisha
yangu mwenyewe. Mafanikio katika maisha
niliyapima kwa matendo yangu ya kila siku na
jua lilipozama. Kisichokuua kitakukomaza,
niliamini hivyo na kila jua lilipozama nilipiga
goti na kumwambia mungu nashukuru kwa
pumzi na kama ikikuendeza naomba kesho tena
nivute pumzi. Maisha magumu ya kulelewa na
mama wa kambo baada ya mama yetu kufariki
ndiyo yaliyoniondoa nyumbani. Kipigo
kilichopitiliza kilinifanya mtumwa ndani ya
himaya ya baba yangu, nikaamua kuingia
mtaani wakati huo nikiwa na miaka saba na
Khajat akiwa na mwaka mmoja. Hiyo pia ni
mwaka mmoja toka mama afariki na kumuacha
Khajat akiwa na siku chache. Sikumchukia yule
mwanamke kwakuwa tu hakutuwekea sumu
lakini nililiacha hilo mikononi mwa Khajat
kuamua akikua. Nikiwa na miaka kumi na
kipindi hicho bado nikiwa shuleni nilifanikiwa
kupanda meli ya mizigo na kujificha kwenye
masanduku. Nilikaa siku tatu bila kula, lakini
baadaye nilishindwa na kujitokeza kwa wale
mabaharia. Niliwaeleza kwa nini nilikuwa
naondoka India, walinielewa na nilipewa kazi ya
kupika Mboga kila siku ndani ya ile meli,
walikuwa watu wakarimu sana. Nilitegemea
pengine wangeweza kunibaka lakini haikuwa
hivyo. Baada ya mwezi mmoja tulikuwa
tumefika Australia na meli ilikuwa ikienda kutia
nanga kisiwa cha Fiji. Hivyo na mimi nilifika
mpaka Fiji na kushuka. Nahodha wa ile meli
ambaye nakumbuka alikuwa ni mzungu, akanipa
namba yake ya simu na pesa kiasi fulani kisha
aliniagiza kwenda kwa mama mmoja ambaye ni
dada yake anayeishi SUVA, nilikwenda bila
kusita mpaka kule na yule mwanamke tayari
alikuwa na maelezo juu yangu hivyo alinipokea.
Nilichokuja kugundua kuhusu yule mwanamke ni
kwamba alikuwa haniamini kabisa, alaf pia
alikuwa ni mjane ambaye aliachwa na mumewe
aliyekuwa ni nahodha, mpaka mumewe anafariki
hawakuwa wamebahatika kupata mtoto na
kwenye ile nyumba aliishi peke yake na mbwa
wake. Mara kwa mara alitegesha kiasi kikubwa
sana cha pesa maeneo ambayo alijua kabisa
ningeona. Mara zote hizo nilikuwa nikiona na
kuzichukua kisha nilimpatia. Alikuwa akifanya
majaribio mengi lakini baada ya miezi mitatu
aligundua mimi si aina ya msichana
aliyemtarajia. Nilianzishwa shule na muda wote
huo nilisoma kwa bidii sana. Nilikuwa
nikimuwaza sana Khajat na nilipanga kumfata
siku nikishafanikiwa kuweka maisha sawa.
Nilisoma na kuhitimu vizuri elimu ya sekondari
na baadaye nilijiunga na jeshi kisha nilikwenda
kusoma chuo kikuu, ambapo ndipo nilikutana
kwa mara ya kwanza na Pamela na akawa
rafiki yangu mkubwa, baadaye nilianza
kujitegemea, yule mama alifariki na kuniachia ile
nyumba ambayo nilikuja kuikabidhi kwa kanisa
ili walelee watoto yatima. Nilikuja kusoma
shahada ya pili ya mambo ya upelelezi wa
makosa ya jinai kisha nikawa mwalimu wa
mafunzo ya upelelezi jeshini, wakati huo Khajat
ndio alikuwa amekuja kwangu na kunihadithia
yote yaliyomkuta.
Nilifanya kazi ofisi za jeshi baadaye
nilihamishiwa ofisi za polisi Fiji ambapo
nilikuwa mkuu wa kitengo cha upelelezi na
baadaye nilikwenda Cuba kusomea mambo ya
kivita na uchunguzi wa mauaji. Nilipomaliza
nikapelekwa ofisi ya usalama. Hii yote
iliwezekana kwakuwa yule mama alinitafutia
urai wa Fiji nikiwa bado sekondari, na hata
Khajat alipofika kitu cha kwanza nilianza
kuhangaika ilia pate uraia. Maisha yalikuwa
mazuri, ni kama gari linavyoenda sawia pale
matairi yake yanapokuwa sawa, na inapokuwa
kwenye mteremko, huenda haraka na bila
kuhitaj mafuta mengi, hivyo ndivyo maisha yetu
yalivyoanza kwenda sawia pale ambapo hisia
zetu, akili zetu na maono yetu yalikuwa
yametulia. Sikuwahi kuwa na mwanaume au
kufanya mapenzi mpaka nilipofika miaka 29,
nilikutana na mwanaume aliyeziinua hisia
zangu, alikuwa ni kama teja kwakuwa madawa
ya kulevya yalikuwa yamemuathiri. Sikuwa na
mwanaume kwakuwa sikuona umuhimu wao,
nilikuwa mtu wa mazoezi tu na kufikiria
mafanikio yangu. Nilikuwa mbinafsi na hii
ilikuwa ni njia ya kuzuia kuumizwa. Nilimchukua
yule kijana, nikampeleka kwa daktari ambaye
nilionyeshwa na Pamela, akatibiwa kwa pesa
zangu mpaka akaona kabisa. Nikamleta
nyumbani kwangu, akacheza na mwili wangu
kwa kadiri alivyotaka, nikampa pesa kwa kadiri
alivyotaka. Nilimpenda sana kwakuwa nilijua
wanaume wengi waliniogopa, alitoa bikra yangu
na kumaliza woga wangu. Nikamtafutia kazi
jeshini, nikamuingiza kwenye darasa langu la
karate nililokuwa nikiwafundisha wanajeshi wa
baharini. Akawa ameiva. Nikaanza kuchunguza
mienendo yake nikagundua anawanawake
wengine, sikuwahi kumuuliza, nilijua bado
anahitaji muda wa kubadilika. Lakini hakuwa
anabadilika, nikamuonya mara nyingi akawa
akiitika lakini hakuwa akitekeleza. Ikaniuma
sana lakini bado nilimpa muda nikiamini
angebadilika lakini ilikuwa tofauti, kuna muda
alilala nje akidai yuko kambini lakini nilimfatilia
na kumkuta akifanya mapenzi na mwanamke
mwingine, nilikuwa dirishani siku hiyo,
sikuongea chochote bali nilirudi nyumbani.
Aliporudi kesho yake nilimwambia kuwa
nimemuona na kumuomba ajirekebishe, badala
yake akafoka na kunipiga, nilimtazama tu
kwakuwa nilijua nikisema nimpige na mimi
ningeweza kumuua. Baadaye alianza
kujirekebisha ila bado alikuwa akiendelea na
mambo mengine, siku niliyokuja kugundua
alimlazimisha Pamela kufanya naye mapenzi
tena kwa kumnywesha pombe ndipo niliona huo
ndo uwe mwisho sasa wa wema wangu kwake,
niliiba bomu dogo nikiwa kambi ya jeshi na
kuondoka nalo mpaka nyumbani, kipindi hicho
alikuwa akienda kwenye kulinda Amani Iraq.
Nilikuwa nampangia vitu vyake kwenye begi.
Haikuwa rahisi kwangu lakini niliona kabisa
kuwa sikumuhitaji kwangu na kwenye hii dunia,
hivyo nililishonea lile bomu vizuri kwenye begi
chini na kulitegesha masaa mengi nikijua
kabisa litalipuka akiwa ameshafika. Na ndicho
kilichotokea. Sidhani kama nitakuwa tena na
mwanaume, na hata nikiwa naye najua
nitamuua kinyama siku akifanya upuuzi,
niliamua kuishi kama mwanaume tu lakini
nimekuja kugundua nimekuwa zaidi ya
mwanaume.

>>SASA<<

Dany alitueleza mengi aliyoweza kutueleza
lakini kwenye maelezo yake bado niliona kuna
vitu vingi sana kuhusu Mary bado hatujavijua.
Kikubwa kilichonisumbua kilikuwa ni kwanini
amemfanyia mumewe vile, je ilikuwa ni pesa tu
ama? Lakini hatukujua lolote kabisa. Tuliamua
kumuweka Dany apatiwe matibabu akiwa
palepale kwangu huku tukiendelea kusubiri siku
Mary anayokuja Fiji, tulikaa zaidi ya wiki mbili
lakini Mary hakuwa ametokea wala kupiga
simu.
“Khajat tunafanyaje? Maana naona kama
tumekwamba sehemu.” Nilimuuliza Khajat
wakati huo ikiwa ni wiki ya pili na siku tatu
toka siku Dany aliyosema kuwa Mary angekuja
wiki iliyofuata. Hatukujua lakufanya zaidi lakini
tulikuwa na lengo la kumkamata Mary na
kumfanya chochote ambacho tungekiwaza kwa
muda huo.
“Mfatilie Hawadh umlete hapa nyumbani, yeye
ndiye atatusaidia kujua yaliyobaki.” Aliniambia
Khajat, lakini Hawadh hakuwa mtu wa kawaida.
Alikuwa ni mtu katili sana na aliyejulikana na
kuchukiwa na wengi lakini hiyo haikunipa shida
sana kwakuwa Hawadh anapenda sana
wanawakem na katika kufanya uhalifu au
mauaji au hata upelelezi ni rahisi sana kumpata
mwanaume ambaye anapenda wanawake,
hakuna upelelezi rahisi kama mwanamke
kumpeleleza mwanaume anayependa ngono.
Kanuni kwa watu kama hawa ni tatu tu, mpe
anachotaka kwa kiwango kikubwa ili uivuruge
akili yake, mbili, mfanye akuone wewe ni mtu
wa kawaida ila unayemfaa, tatu weka mihemko
pembeni kisha mpeleke unapotaka wewe.
Ndicho nilichomfanyia Hawadh. Baada ya
kumtafuta kwa siku nzima hatimaye niligundua
alikuwa Kansaz Casino iliyokuwa Vulpatra kama
kilomita 30 kutoka kwangu, nilivaa kama
wahudumu wale wa ile kasino lakini nguo
yangu ilikuwa tofauti kwakuwa niliiweka
mpasuo mpaka juu kabisa na nilipotembea au
kuinama kidogo ilikuwa ikionyesha nguo yangu
ya ndani. Nilipofika pale niligundua alipokuwa
amekaa na alikuwa amekuja na walinzi watatu
waliokuwa wamesimama karibu yake. Haraka
nilimuwahi muhudumu aliyekuwa akimuhudumia
pale na kuchukua vile vinywaji kisha
nilimpelekea, kwa manjonjo kabisa nilimfungulia
na aliponitazama nilijua kabisa alinitamani
nikaondoka na kudondosha funguo niliyokuwa
nimeshika kisha kwa makusudi niliinama
kuiokota na kumpa muda wa kunitamani zaidi.
Niliponyanyuka nilimkonyeza na kama alijua vile
alisimama na kunifuata.
“Binti habari yako.” Tulikuwa tumesimama
kwenye korido wakati akinisemesha.
“Salama, unahitaji nini nikusaidie.” Niliongea
huku nikijiachia kwake na kuondoka, nia yangu
ni yeye ajue tu kuwa sikuwa nafahamu wadhifa
wake na hivyo nilimuona kama mteja wa
kawaida tu ambaye hakuhitajika kupapatikiwa
sana.
“Wewe ni muhudumu mpya hapa?” aliniuliza
huku akinifata.
“Ndio, nimetoka Jorpradigo Casino.” Nilisogea
mbele na kufungua malango wa chumba fulani
na yeye aliingia, bila hiyana nilijifanya kama vile
sikumuona na kuavua nguo zangu zote mpaka
ya ndani mbele yake kisha nilimgeukia, alikuwa
ametoa macho na mdomo ukiwa wazi,
nilichukua nguo nyingine kwenye begi langu
dogo na kuanza kuvaa taratibu huku
nikimtazama, kisha nilimsogelea na kumuomba
alifunge mkanda wa brazia yangu. Alifanya
hivyo lakini nilishamsoma kabisa kuwa alikuwa
ni dhaifu sana. Nilipomaliza alikuwa bado
amesimama pale.
“Unakwenda wapi?” aliniuliza.
“Muda wangu wa kazi umekwisha naelekea
kwangu.” Nilimuambia huku nikimpita na
kwenda kwenye mlango lakini kabla sijafungua,
alinifata na kunisimamisha.
“Naweza kuwa na wewe kwa usiku mzima?”
aliniongelesha huku akionekana kuzidiwa sana.
“Ndio, njoo KLPC 34, SUVA BRIDGE, lisaa limoja
kuanzia sasa. Njoo mwenyewe, sipendi
kulindwalindwa, kama unataka raha waache
walinzi wako nyumbani.” Nilimwambia hayo na
bila kumpa muda wa kujibu niliamua kuondoka,
sikuwa nimempa namba yangu ya simu.
Niliondoka moja kwa moja mpaka nyumbani
nikamweleza Khajat na yeye alikubali kuondoka
na mimi. Tulikwenda mpaka bali na Khajat
alikuwa ameshatega kamera na kila kitu
kwenye hoteli moja iliyokuwa pale, kisha
alipokuja mimi niliingia naye kwenye ile hoteli
baada ya kuhakikisha kuwa alikuwa mwenyewe.
Baada ya kuingia nae nilimuwekea madawa ya
kulevya kwenye kinywaji na alipokunywa tu
alikuwa tayari ameshalewa, madawa
niliyomuwekea yalikuwa ni tofauti sana na yale
mengine ya kulevya, hii ilikuwa ni ya kipolisi
iliyokuwa na nguvu ya kuuharibu ubingo na
kumfanya mtu aseme chochote bila kujijua.
Hivyo baada ya hapo Khajat aliingia kule
chumbani na tulianza kupekua simu yake na
kukuta mawasiliano yake na Mary wiki tatu
zilizopita juu ya kuingia kwa kontena la biskuti
mwezi ujao. Hakukuwa na mawasiliano mengine
kati yake na Mary. Hivyo Khajat alipoingia
ilikuwa ni kumuhoji tu ili kama kuna analolijua
basi atueleze.
“Khajat, hakuna kumtesa huyu.” Nilimuambia
Khajat na yeye alikubali. Nilisema hivyo
kwakuwa kama tungeweza kumfanya chochote
basi ingekuwa ngumu sana kwa sisi kumaliza
tuliyoyaanzisha.
“Hawadhi.” Khajat alimuita kwa sauti ya chini
na yeye aliitika kwa sauti ya chini kama vile
mlevi.
“Mary anakuja lini Fiji.” Khajat alimuuliza lakini
Hawadh hakujibu.
“Hawadh nakuuliza Mary au Priscila analeta lini
lile kontena la biskuti huku Fiji.” Alimuuliza tena
na kwa mbali kabisa Hawadh alianza kujibu.
“Ameshakuja, yuko huku toka jana anamtafuta
Dany.” Alijibu kwa sauti ya kilevi.
“Dany yuko wapi kwani.” Nilimuuliza nikiwa na
nia ya kujua kama anafahamu chochote juu ya
Dany.
“Dany hajaonekana, itakuwa amekimbia na pesa
za mzigo.” Alijibu tena huku akiwa bado
anarembua macho kama vile anasinzia.
“Mary amefikia wapi.” Nilimuuliza tena lakini
hakuonekana kufahamu.
“Sio rahisi kujua Mary anapofikia ila natarajia
kuonana nae siku yoyote akinipigia simu.”
Mpaka hapo hatukuwa tunahitaji tena maelezo
mengine toka kwa Hawadh, nilimpa maji yanye
glucose yaliyomfanya atapike na ile dawa
ikakata akarudi kama kawaida.
“Tumefanya vya kutosha Hawadh mapaka
umelala, sasa naomba tukaoge kisha
tuondoke.” Kwakuwa alikuwa bado hajielewi
vizuri niliharakisha mambo na tukaenda kuoga
kama vile kuna tulichokifanya, baada ya hapo
tulitoka nje. Akaniandikia hundi ya dola elfu 3
na yeye aliondoka kwenda kwake. Tulirudi moja
kwa moja mpaka kwa Pamela na wao walikuwa
bado hawajalala. Tukawachukua na kwenda nao
mpaka kwangu ili wakalale huko. Tulipofika
nyumbani baada ya kufungua tu na kwenda
kule chini aliko Dany ambaye alikuwa tayari
ameanza kurudi katika hali nzuri japo alikuwa
ndani ya sindano ya usingizi, tukasikia sauti ya
simu ya Dany ikiita, tulipoiangalia alikuwa ni
Mary, haraka Pamela alimchoma sindano
nyingine ya kumuamsha, alipoamka tu alikuwa
bado hajakaa sawa. Ujue Khajat ni mtu ambaye
hapendi kucheleweshwa, simu ilikuwa
imeshakatika na sasa ilikuwa ikiita kwa mara
ya pili lakini Dany bado alikuwa na
maruweruwe, Khajat alimpiga ngumi moja ya
uso na akili ya Dany ilikaa sawa, nilimwonea
huruma kwa mara ya kwanza kwani ile ngumi
ilimfanya alie na damu za pua zianze kumtoka.
“Sikiliza Dany, ukijifanya wewe ni mfu hapa,
nitakuzika kabla pumzi yako haijafika mwisho.
Ni lazima ufe ila muda wako bado haujafika
hivyo jiweke kama binadamu.” Khajat
alimsemesha Dany huku akimkazia macho na
Dany alinyamaza kulia na kutingisha kichwa
kama ishara ya kwamba amemuelewa Khajat.
“Sasa Mary anapiga simu hapa, ukionyesha
dalili yoyote ya kumtaarifu kuwa uko sehemu
yenye hatari ujue wakati unakata simu utakuwa
umekata pia koo lako na mkeo atakishuhudia
kichwa chako kikiwa kwenye begi, hivyo
mwambie uko Side Villa Motel, akikuambia
muonane sema sawa. Maneno tofauti na hayo
basi uhesabu kuwa mke wako ni mjane.” Khajat
alimaliza kumtahadharisha na ile simu
ilipokelewa na kuwekwa sauti ya juu ili wote
tusikie.
“Hallo Mary.” Aliitikia Dany.
“Yes Dany, please may I speak to my husband
please?” (Ndio Dany, naweza kuongea na mume
wangu tafadhali?) aliongea Mary kwa sauti ya
kejeli. Nilimtazama Patrick alikuwa amejaa
hasira mpaka machozi yalianza kumtoka.
“I don’t Understand what you talking
about.” (sielewi unachokiongea) Dany alijifanya
kama vile hakuwa anaelewa vizuri alichokuwa
anaongea Mary. Mary alipiga simu na kuongea
kwa lugha ya kingereza kwa makusudi kabisa.
“Dany, am not a kid, hand the phone to
Patrick.”(mimi sio mtoto Dany, mpe Patrick
simu.) Kabla hata Dany hajajishauri Patrick
alikuwa ameshaongea.
“What do you want.” Ilikuwa ni sauti ya Patrick
ikimuliza Mary.
“Patrick mimi si mjinga, na sijafurahia kuwa
kwako hai, ila nakupa mambo mawili uachague
moja, kaburi au uhai. Huyo afisa uhamiaji
anayeitwa Khajat hatakusaidia sana kwakuwa
unahitaji jeshi la watu mia 200 kuniangamiza.
Kaa mbali na njia nipitayo na wewe utaishi kwa
Amani mume wangu. Dunia hii si mapenzi tu,
dunia ina mengi, mwache Dany huru kisha
wewe endelea na maisha yako, usifatilie kuhusu
mimi na umwambia huyo mwanamke wako
Khajat ajali zaidi maisha yake. Hakuna wa
kuangamiza ndoto zangu.” Alimaliza Mary na
hapohapo Khajat alichukua ile simu.
“You don’t know me well Mary.” (Hunijui vizuri
Mary), aliongea Khajat lakini kabla hajaendelea
alikatizwa na kicheko cha Mary.
“Khajat, a senior migration office with no, HA/
MO/2345. You kidnaped Dany three weeks ago,
you drive a black escalade, you are single, 5.5
feet. Is that not you sweatheart?”(Khajat, ni
afisa wa uhamiaji ngazi ya juu, namba yako ni
HA/MO/2345. Ulimteka Dany wiki tatu
zilizopita. Unaendesha gari nyeusi aina ya
escalade, hujaolewa, una urefu wa futi 5.5, je
sio wewe mpenzi?) Aliongea Mary, mimi
nilikuwa kimya.
“Mary, am more that what you have read about
me, the difference between you and me is that,
you take life of the innocent people for you
greed, I serve the life of the innocent people by
taking the life of the guilt one. I don’t need an
army to take you down and slaughter you, I just
need me, and one smart woman. I will catch
you because when you pressed the button to
dial Dany’s number is when you put your life in
jeopardy. So gather you men.”(Mary, mimi ni
zaidi ya yale ulioyasoma kuhusu mimi, tofauti
kati yangu na wewe ni kwamba wewe unaua
watu wasio na hatia kwa uroho wako, ila mimi
naokoa maisha ya watu wasio na hatia kwa
kuua wenye hatia. Sihitaji jeshi kukukamata na
kukuchinja. Najihitaji mimi mwenyewe na
msichana mmoja timamu. Nitakukamata
kwakuwa muda uliompigia Dany simu ndipo
ulipoweka maisha yako hatarini. Kwaiyo
kusanya watu wako) Aliongea Khajat na kukata
simu.

ITAENDELEA!!!
 
RIWAYA: KISASI
MTUNZI: Frank MUSHI
SEHEMU YA KUMI NA TANO

“Kifo ni hatua ya mwisho wa muda wa
binadamu katika dunia, haijalishi ni muda gani
utachukua hapa duniani ila jua tu kwamba ipo
siku na wewe utakufa. Cha kujiuliza ni kitu gani
katika maisha kitakutambulisha baada ya kifo
chako? Ni kitu gani kitamfurahisha muumba
wako pale utakapokuwa ukifanyiwa hesabu ya
mema uliyoyafanya kama shukrani ya pumzi
kwa muumba? Kuna muda wa kila kitu, kuna
starehe za ujana na shida za uzeeni. Kufa
Hakuhitaji uwe mgonjwa au upate ajali, ili ufe
inahitajika SIKU YAKO IWE IMEFIKA. Inaumiza
sana kufiwa na mtu uliyempenda au mtu
aliyewahi kukufanya ucheke ama kujifunza kitu.
Lakini hiyo haitufanyi tusahau kuwa wote
tutakufa. Muda wetu katika dunia hii una
kikomo, na huwa kifo ni mshangao kwetu hasa
afapo mtu ambaye hatukutegemea. Ni kama
kupanda ngazi usiku wa giza nene, ufikapo
sehemu na kudhani kuwa kuna ngazi nyingine
mbele lakini unashangazwa na kujikuta
ukitembea hewani na kuanguka, giza
litakufumba macho na hutaamka tena. KILA
MUDA NI MUDA WA KUJIWEKA SAWA KWA
MUUMBA. TAFUTA KITU CHA KUIFANYA JAMII
YAKO IKUKUMBUKE, TAFUTA KITU CHA
KUMFANYA MUUMBA WAKO AJISIKIE FARAJA
KUKUPOKEA.” ULALE SALAMA NGWEA.HII NI
SEHEMU YA KUMI NA TANO.

**KHAJAT**

Nilikuwa nimeshamaliza na mambo ya kazini na
sasa nilikuwa tayari kwenda kuonana na Felly ili
tupange zaidi juu ya mikakati ya kumuweka
Mary kwenye mikono yetu. Tulikubaliana kabisa
kuwa hakuna kumtoa Dany. Kitendo cha Mary
kumtaka Dany inaonyesha anafahamu mengi
juu ya Mary na sasa ndio alikuwa amefungua
dirisha la mateso ya Dany. Nilikuwa nimeagiza
vifaa zaidi ili Dany aeleze yote anayotakiwa
kueleza. Niliagiza mashine ya kukamulia miwa
ambayo iliwahi kumfanya Gervace Harv kusema
juu ya bomu walilolitega Indovoa karibu kabisa
na soko kubwa la Suva, mashine ile inasehemu
ya kuingiza mua kisha hukamuliwa na makapi
hutupwa pembeni. Baada ya wanajeshi wa Fiji
kushindwa kupata majibu ya maswali yao
kutoka kwa Gervace ambaye alikuwa ni gaidi
aliyetumiwa na nchi za Saudia tuliitwa kikosi
chetu kwaajili ya kwenda kutafuta lile bomu.
Mara zote Gervace alipokuwa akipigwa ili
aseme alikataa na kusema hata mnipige vipi
mimi niko tayari kufa na sitasema chochote.
Nilimuomba mkuu wa kikosi anipe nafasi ya
kuonana na Gervace ila alinikatalia. Nilifikiria
kazi nzito ya kutafuta kitu usichojua kilipo
nikaamua kumtoroka na kwenda kule alikokuwa
amewekwa nikawaomba wale wanajeshi
waliokuwa wanamlinda waniruhusu nionane
naye na wao waliniruhusu, nikaomba ile
mashine ya miwa iliyokuwa karibu na pale
kambini iletwe ndani na wale wanajeshi
waliileta kimya kimya, nilimtazama Gervace
usoni nikamuuliza bomu liko wapi ila hakusema,
alichoniambia ni kwamba baba yake aliuawa na
jeshi kwakuwa tu alitoa siri za wakuu wa jeshi
kufuja mali za ununuzi wa silaha. Lakini
pamoja na kwamba alikuwa akilipa kisasi
alikuwa ameshakosea kutega bomu litakaloua
watu, nilimsihi kwa sauti ya upole lakini
hakusikia. Ile mashine ilipokuja nilimuuliza tena
lakini aliishia kunitemea mate. Nikaukamata
mkono wake na kuuingiza ndani ya ile
mashinekisha nikawasha, ilianza kuminya vidole
vikawa kama chapati na hata haikufika mbali
tayari alikuwa ameshasema bomu lilipo.
Nilikuwa katili sana lakini kama kuna mungu
basi atanisamehe, ila adhabu hii itamkuta Dany
kama ataamua kukaa kimya bila kuusema
ukweli wote bila kuacha chochote. Haijalishi
kwamba yeye sio gaidi au ni mtu wa kawaida
tu, kitendo cha yeye kushiriki kuua na
kudhulumu nguvu ya mtu tayari ni ugaidi
uliostahili adhabu kali ambayo sio kifungo cha
maisha bali maumivu makali na ya muda mrefu
kabla ya kufa.
Nilitoka vizuri nje ya ofisi na nilikwenda mpaka
kwenye gari yangu, nilipofika nilifungua mlango
na kuingia ndani kisha nikawasha gari, ila kabla
sijaingiza gia nikasikia sauti ya mtu ikitaja jina
langu kwenye kiti cha nyuma, nilipogeuka tu
nilikutana na kitu kilichopulizwa usoni kwangu
na hapohapo nilipoteza fahamu. Sikujua ni kitu
gani na ni nani aliyefanya vile. Nikaja kushtuka
nikiwa nimefungwa kila sehemu kwa kamba
ngumu, mbele yangu kulikuwa na mwanamke
ambaye niliweza kuitambua sura yake kwakuwa
niliiona kwenye picha. Alikuwa ni Mary.
“Habari yako Khajat.” Alinisemesha kwa dharau
huku akinitazama machoni, hasira zilinipanda
na nilikuwa nasubiri afanye makosa ya
kunifungua zile kamba. Nilipomtazama usoni
tayari nilikuwa nimeshamsoma kuwa ni mtu
katili mwenye sura ya malaika.
“Unataka nini kwangu.” Nilimuuliza huku
nikiendelea kumtizama usoni.
“Nataka kumuonyesha Patrick kuwa wewe
huwezi chochote, una mpotezea muda wake na
kumuhatarishia maisha yake zaidi.” Aliongea
huku akitabasamu, nilizidi kumtazama usoni ili
kujua ni ipi nia yake.
“Hutapata chochote unachokitaka.”
Nilimsemesha kwa kujiamini na hiyo ilimfanya
acheke kisha aliondoka pale na kurudi tena
akiwa na mikasi, alikuwa na kijana mmoja
ambaye alikuwa ni mzungu aliyejichora mwili
wake. Sikujua alitaka kufanya nini lakini
sikutaka kumuonyesha woga ili asinitawale.
“Mfungue izo kamba.” Alimwambia yule
mzungu na yeye alinisogelea na kutaka
kunifungua kamba.
“Nakushauri kama unataka kufanya chochote
basi usinifungue hapa.” Nilimwambia Mary na
yeye alicheka kisha alinitazama usoni kwa
dakika mbili.
“Khajat, mimi ni zaidi ya hili tabasamu
unaloliona usoni mwangu, Roland mfungue
kamba tuone atafanya nini.” Aliongea Mary na
yule kijana alinifungua kamba, aliponiachia
nilikuwa nimesimama nikimtazama Mary alitaka
kufanya nini;
“Chukua simu mpigia Patrick mwambie amlete
Dany Villa Bridge baada ya nusu saa.”
Aliniambia akiwa ameukunja uso wake kama
vile alikuwa akinitisha, bado nilikuwa sijajua
uwezo wa Mary, lakini pia hakuonekana kama
ni mtu wa kutishwa kirahisi.
“Sipigi simu popote na humpati huyo Dany,
fanya lolote unalotaka, na mimi na wewe
tumemalizana hapa.” Nilimwambia hivyo na
kuondoka, sikufika popote nilipigwa teke
mgongoni lililonifanya nianguke chini,
nilivyojigeuza nikakutana na ngumi nyingine ya
shavu na kiatu kilinikanyaga shingoni, nilikuwa
bado kama nina maruweruwe hivi na
nilivyotazama vizuri nikakuta ni Mary ndiye
aliyenipiga;
“Usinifanye nikakuua mapema.” Aliniambia huku
akinitazama kwa sura yenye kuonyesha kuwa
alikuwa akimaanisha. Nilichokuwa nakifanya sio
kupigana na Mary, nia yangu ilikuwa kuujua
uwezo wa Mary na alikuwa na ujuzi gani
kwenye mambo anayoyafanya. Nilijigeuza vizuri
na kumtazama kisha nilimpelekea ngumi ya uso
iliyomfanya aanguke pembeni, nilikuwa haraka
na kunyanyuka na yeye alikuwa amejibinua
haraka na kukaa sawa, niliitazama miguu yake
alivyoiweka na ngumi alivyokunja nikajua kuwa
Mary alikuwa ni mtaalamu wa karate, kijana
wake wa kizungu alikuja mbio na kutaka
kunivamia ila niliwahi na kuibetua meza
akakutana nayo na hiyo ikamfanya akae chini
kwa maumivu, Mary aliniwahi palepale na kuja
na teke ambalo hata hivyo nilikuwa nimeliona
na kumpisha akutane na ukuta, nilichokifanya
nilimuwahi yule kijana pale chini na kumshika
shingo kisha nikaivunja mbele ya Mary ambaye
alikuwa bado yuko pale chini. Mary alitoa
macho, nikamfata pale alipo na kuzishika
nywele zake kisha nikamnyanyua, wakati
napanga kumpiga ngumi ya tumbo yeye alikuwa
ameshaniwahi na kichwa kilichonipeleka tena
chini na hapo aliniwahi na kunifunga mikono
kwa pingu.
“Nitakuua lakini sio sasa, hivyo usinilazimishe
Khajat.” Aliniambia hivyo huku akininyanyua na
kuniweka kwenye kile kiti. Kisha na yeye aliketi
chini kwakuwa alikuwa tayari amechoka,
alinyanyua simu na kupiga;
“yeah, njoo ndani.” Aliongea maneno machache
tu na hapo alikuja mtu mwingine ndani, wa
sasa hivi alikuwa ni mwafrika ambaye
inaonekana alikuwa ni Mtanzania kwakuwa
lugha waliyoongea ilikuwa inaendana kabisa na
ile ambayo Patrick na Pamela wanayoongeaga.
Hapo walikuwa tayari wamenifunga kwani
sikuelewa walichokuwa wanasema. Lakini
baada ya muda mfupi yule jamaa alionoka na
kurudi na simu yangu, kisha Mary alisogea
karibu yangu na kunisemesha.
“Uko tayari kupiga simu au nipige mimi?”
alinisemesha lakini mimi sikumjibu, alinitazama
huku akitabasamu.
“Ujue Khajat umemuua kijana wangu mmoja,
sijui kwanini unahisi sitaweza kukuua na wewe
hata sasa hivi, sijui kitu gani kinakufanya uone
kuwa ninaweza kuwa na huruma na wewe,mh!
ni hili tabasamu langue e? tabasamu hili limeua
wengi sana, wengi hulitazama juujuu, tabasamu
langu litakuua wewe pia muda ukifika hivyo
kwa sasa chukua simu nifanyie kwanza kazi
yangu.” Alinitazama huku akiendelea
kutabasamu. Alikuwa na tabasamu lililoficha
unyama wake, alionekana mpole lakini alikuwa
muuaji.
“Sipigi simu, usinitishie kufa kwakuwa mimi ni
marehemu siku nyingi sana. Hakuna jipya
unaloweza kunifanya mimi, hakuna maumivu
mapya unayoweza kunipa ambayo sikuwahi
kuyapata kabla, kama unataka kuyaona
machozi yangu hapo sawa ila kama unahitaji
majibu ya maswali yako jua kabisa hapa
hutayapata.” Nilimwambia na yeye alizidi
kunitolea tabasamu. Akachukua mkazi mmoja
uliokuwa pale mezani kisha akanisogelea
taratibu.
“Khajat, nikupe simu upige?” aliniongelesha
tena huku akiniwekea ule mkazi kwenye kidole
changu cha mwisho, ulikuwa ni mkasi wa
kukata vyuma, akauweka katikati ya ukucha
wangu, nilimtazama usoni na kumtemea mate,
kilichofata yalikuwa maumivu makali na jasho,
alikuwa amenikata na niliona sehemu ya kidole
changu ikiwa nusu, kipande alichokikata
kilikuwa kimedondoka chini. Nililia sana
kwakuwa nilisikia maumivu na hapo alichukua
kitambaa anifunge ili kuzuia damu ile isitoke,
nikakataa kufungwa kitambaa ikiwa ni ishara ya
kumuonyesha kuwa sikuwa naogopa kufa,
walinishika mkono kwa nguvu na yule jamaa
aliyekuwa naye alifanikiwa kunifunga mkono ule
na hivyo damu ilikuwa ikitoka kidogo lakini
maumivu niliyasikia mpaka shingoni. Hakuishia
hapo bado alinilazimisha niongee na Patrick
lakini nilimkatalia, nilichojifunza ni kwamba
Mary hakuwa anamjua Felly wala hakuwa na
taarifa kuwa Patrick alikuwa na mtoto huku. Hii
kwa maneno mengine ilionyesha kuwa
intelijensia ya Mary ni dhaifu na hii ilikuwa
nafasi nzuri ya mimi na Felly kumsaka iwapo
ningefanikiwa kutoka nikiwa mzima. Alinipiga
sana lakini baada ya yeye kuchoka aliamua
kutoka nje, nilijifanya nimezimia na alipokuja
alinipiga makofi lakini nilijikaza na kujifanya
nimelegea.
“Itakuwa maumivu yanamfanya mishipa ya
fahamu inaleta shida, mchome sindano ya
diclofenac kisha leta ile drip ya glucose umpe,
tunaondoka hapa baada ya lisaa limoja, ila
wewe utatangulia Villa Bridge na Hasheem,
mkifika pale mtakaa upande wa juu wa daraja
lile mkiwa na silaha, eneo lile halina watu
wanaopitapita, mtakapo muona Dany basi
hapohapo ua mwingine yeyote utakayemuona,
hakikisha kama mkimuona Patrick basi asitoke
kwenye mdomo wa bunduki akiwa hai. Hakuna
kuacha alama, tutafanya kama tulivyofanya ya
Urusi, tupo watatu tu, ni wewe Hasheem na
mimi, yeyote mwingine atakayekuja atakufa,
hata huu mzoga tutaua pale ambapo Dany
atakuwa upande wetu.”alimwambia yule jamaa
wakati huo mimi nilikuwa bado nilikuwa
nimejifanya kama nimezimia. Akachukua simu
yangu na nikamsikia akitafuta namba kisha
alipiga akaweka sauti kubwa ili yule jamaa na
yeye asikie.
“Khajat uko wapi muda wote huo?” sauti ya
Patrick ilisikika, nikatamani sana kuzungumza
na kumuambia asiongee lakini hiyo
haikuwezekana kwakuwa ingeharibu kila kitu.
“Ni Mary hapa, sikiliza Patrick najua
unapafahamu Villa Bridge, nikukute pale ukiwa
na Dany baada ya lisaa limoja, kinyume na
hapo huyu Malaya wako atakufa kwakuwa hata
hivyo amebakiza muda mchache sana kabla
hajafa. Nimesema baada ya lisaa na ninaanza
kuhesabu sasa hivi, ukichelewa dakika moja tu
utakuta kichwa chake pale.” Alimaliza kuongea
na kukata simu kabla hata Patrick hajaongea
chochote kisha akamwambia yule jamaa
anifungue na kunipeleka nje, alinifungua na
kunitoa ile drip, kisha alinibeba na Mary alibeba
bastola yake akawa akimfata yule jamaa
aliyenibeba, nilijilegeza kabisa kama vile
nimezimia kweli, kwakuwa Mary aliponiteka
pale ofisini aliondoka na gari langu basi
alilitumia hilohilo kwenda Villa Bridge,
akamwambia yule jamaa aniweke kwenye buti
ya gari kisha niliwekwa mule na yeye alikuwa
nje nikawa nasikia akiongea na yule jamaa.
“Mna uhakika huyu mwanamke yuko peke
yake?” alimuuliza yule jamaa.
“Ndio bosi, hakuna mtu mwingine
anayeshirikiana naye.” Alijibu na hapo nikawa
pia nimegundua kuwa kumbe alituma watu
kunipeleleza ambao hata hivyo hawakuambulia
kujua mengi zaidi.
“Sawa ila mkifika pale kuweni makini, kuna
kona mbili katika lile daraja, juu kule kwenye
mona ya kwanza ukikaa unaona mashariki mwa
barabara, na kona ya pili unaona pia magharibi
kwa ile barabara, ukikaa kona hii hapa na
unaweza kuwa na uwezo wa kulenga mita mia
tano, hivyo kwa bastola hizi hamuwezi kufikisha
kwenye usawa huo iwapo mtu atatokea kuwa
usawa huo, sasa mtatumia KNT-308 sniper
riffle ambayo inaweza kulenga mita 800,
itakuwa na risasi tatu tu, hatuendi kuvamia,
tunaenda kubadilishana mzigo ila tukiwa na
lengo la kuchukua mizigo yote na kusafisha.
Hivyo risasi chache zikitumika itasaidia zaidi,
kwenye risasi tatu unatakiwa utumie moja
ikiwezekana kwakuwa Patrick ni mtu laini sana,
siwapi risasi nyingi ili kuzuia isijekuwa kama ya
Urusi. Mkiacha mtu akakimbia basi mmoja kati
yenu lazima afe, tangulia mkiwa kwenye nafasi
zenu mniambie nikakuwa kilomita moja karibu.”
Walimaliza kuongea na hapo sikuelewa nifanye
nini, nilisikia Mary akiondoka upende
waliokuwepo na kuja nyuma ya gari, nikajiweka
sawa na alipokuja alikuta bado nimezimia,
akanishika shingoni kisha akafunga buti na
kuingia kwenye gari na kuliwasha. Kule kwenye
buti kulikuwa na kofia yangu ya pikipiki na hapo
niliivaa kabisa tayari kwa lolote, gari ilikuwa
ikikimbia kwa spidi kama 130 hivi, nikawa
nahesabu kwa kukadiria kilomita, ilipofika
sehemu nikafungua mlango wa buti wa chini
kisha nikajitupa na huku Mary akiendelea na
safari, hakuweza kuniona kwakuwa alikuwa
kwenye kasi na mimi nilichokifanya nikukimbilia
sehemu kuliko kuwa na simu za barabarani,
nikampigia simu Felly;
“Felly mko wapi?” nilimuuliza Felly aliyeonekana
kama amechanganyikiwa hivi.
“Oooh Khajat, mzima.” Alinisemesha na
kuonekana kama alisimamisha gari.
“Niko sawa, msiende tena nimefanikiwa
kutoroka ila nataka uje haraka barabara ya
Capricon sasa hivi ili tuwahi mbele ya Mary
tuangalie cha kufanya, uko na nani?” nilimuuliza
wakati huo roho ya hasira imenijaa na nilikuwa
natamani kuona damu ya mtu ikimwagika.
“Niko na Dany kwenye gari na niko mita mia 5
kutoka hapo ulipo.” Nilitazama kwa mbali na
kweli niliona gari kwa mbali sana ikiwa imepaki,
baada ya muda kidogo walikuja pale na
nilimkaba Dany na kuzuia hewa isipite kooni ili
apoteze fahamu kisha nilimfunga mikono na
miguu na kumuingiza kwenye buti.
“Nipe funguo Felly.” Nilimuomba Felly funguo
kwakuwa niliona kama atanichelewesha na yeye
wala hakubisha alinipatia funguo, muda huo
kidole kilikuwa kimeanza kuuma sana kwakuwa
nilikitonesha pale nilipojitupa na maeneo
mengine ya mwili pia yalikuwa yakiniuma lakini
kwa hasira niliyokuwa nayo niliyapuuzia.
“Tunapita porini ndio kuna njia ya mkato,
tukifika mita mia 5 tutaweka gari kichakani na
hapo itabidi tuende kwa mguu na kwakukimbia,
utakwenda kona ya mashariki na mimi
nitakwenda kona ya magharibi kule juu ya
daraja, kila upande una kijana mmoja kwenye
Rifle hivyo unatakiwa uwe makini sana,
ukimshtua na akifyatua risasi tutakuwa
tumeharibu, hatuendi na bastola, utatumia kisu
tu au mkono.” Nilimaliza kutoa maelezo na
Felly alikuwa tayari ameshanielewa, nilivuta
mafuta na kupangua gia, tulipiga msituni na
vichaka vyote tulivilaza chini, kwa mwendo ule
ikatuchukua dakika 25 kuliona daraja kwa
mbali, hakukuwa na dalili yoyote ya gari kwa
mbali na nilipochukua darubini na kutazama juu
ya daraja niliweza kuhakikisha kuwa wapo watu
wawili, walikuwa wamevaa kama wanajeshi na
mmoja alikuwa mashariki na mwingine
magharibi, nilimpa Felly na yeye aliwaangalia
kisha tulianza kukimbia kuelekea kwenye
daraja. Daraja hili ni daraja la treni juu na chini
lilikuwa linapitisha magari, ila mara nyingi
hakukuwa na magari yakipita wala treni
kwakuwa ile barabara ilikuwa imehamishwa kwa
wakati huo. Tulifika mpaka karibu na daraja na
kuamua kuanza kutambaa na tumbo na Felly
alikuwa upande wa pili akifanya hivyo.
Nilifanikiwa kufika nyuma kabisa ya yule jamaa
wa kwanza ambaye ndiye alinibeba kuniingiza
kwenye gari.
“Hey.” Nilimshtua na aliposhtuka na kugeuka
alikutana na kisu kilichopita kwenye koo lake.
Nilimuona Felly akimvizia yule jamaa, na yeye
alimshika bega na alipogeuka alikutana na
ngumi iliyonifanya nicheke japo nilikuwa na
maumivu, ilikuwa ngumi nzuri iliyotua kwenye
pua na kumfanya adondoke kama mzigo.
Hapohapo na simu ya yule mmoja ilianza kuita.
“Hallo, niambieni kama kuko sawa ili nije.”
Aliongea Mary.
“Mary, this is just the beginning, I will catch you
and kill you ASAP, your men are down, get
prepared sweatheart.”(Mary huu ni mwanzo tu,
nitakukamata na nitakuua muda si mrefu,
vijana wako wamekufa, jitayarishe mpenzi)
Nilimwambia na kukata simu.

ITAENDELEA!!!
 
RIWAYA: KISASI
MTUNZI: FRANK MUSHI

SEHEMU YA KUMI NA SITA

“Nitakupenda siku zote. Pale nywele zangu
nyeusi zitakapokuwa nyeupe bado nitakupenda.
Pale ngozi yako laini ya usichana itakapokaliwa
na ngozi iliyojikunja ya uzee bado nitahitaji
kukushika. Pale sura yako itakapokuwa na
makunyanzi unapotabasamu bado nitakupenda,
pale ambapo kila chozi ulilolitoa litakuwa
limeacha alama kwenye sura yako mimi
nitabaki kukupenda. Nitakuthamini daima, yote
ni kwakuwa nilikuwa na wewe wakati wote
ukipitia hayo. Nitashiriki maisha yako,
nitashiriki machozi yako, na nitakupenda mpaka
pale pumzi itakapochoka kuishi ndani yako au
ndani yangu. Nilikupenda kabla na nitakupenda
baada. Pale utakapoamua kwenda na kusema
mimi sio faraja yako nitakuwa tayari
kukuangalia ukiondoka kwakuwa nia yangu ni
wewe uwe na furaha hata bila mimi. Kila mtu
anahitaji faraja na upendo, niko tayari
kukupenda kama nijipendavyo. Siku zote, miaka
yote NITAKUPENDA, na hiyo ni kwakuwa tu
KUKUPENDA WEWE NI AMANI YA MOYO
WANGU.” HII NI SEHEMU YA KUMI NA SITA

**KHAJAT**
Nilikuwa nina hasira sana na Mary kwakuw
alinikata kidole. Toka nimeteswa nikiwa India
hakuna mwanamke amewahi kunitesa au
kunipiga au hata kunidharau, Mary alikuwa
ndiye msichana wa kwanza kunidharau na
kunimudu kwa muda mfupi. Japo sikukaa naye
pale ndani kwa muda mrefu lakini nilikuwa
nimegundua kabisa kuwa Mary sio mtu wa
kawaida. Ni mwanamke ambaye atakuwa na
historia ndefu sana ambayo nilitamani sana
kuijua. Alikuwa ni mwanamke ambaye
anaonekana kabisa kuwa hababaishwi wala
haogopeshwi na kitu lakini pia hakatishwi
tamaa. Mary sio mtu wa kupaniki, sio mtu wa
hasira kama mimi, ilikuwa ngumu sana kujua
kama amekasirika au la kwakuwa alitoa
tabasamu muda wote.
******

SIKU MBILI BAADA YA TUKIO LA KUTEKWA KWANGU.
Nilikuwa nimepewa likizo ya miezi sita
kwakuwa sijawahi kupumzika muda mrefu sana.
Hii ilinifurahisha sana kwakuwa hata Felly
nayeye alikuwa ameomba likizo ya miezi sita na
alipewa. Tulikuwa tuko huru na kazi ambayo
Pamela alikuwa ametuajiri rasmi kumkabili
Mary. Mbali na kwamba tulikuwa tukilipwa
lakini mimi nilijitolea mwenye kwa gharama
zangu kuhangaika na Mary mpaka nihakikishe
kuwa naliona chozi lake na mwisho niwe moja
kati ya watu watakaofanikisha kifo chake.
Patrick alikuwa likizo ya miezi miwili na Pamela
alikuwa kwenye maandalizi ya kuanzisha
hospitali yake ndogo hivyo ni kama wote
tulikuwa huru, maisha yetu tuliishi kama familia.
Cris ambaye ni mtoto wa Pamela na Patrick
alikuwa mzuri sana na Patrick alimuahidi
Pamela kuwa wangefunga ndoa baada ya
mambo yote kuisha. Hiyo ilikuwa ni habari ya
furaha sana, lakini furaha hii ingekamilika kama
Mary angekuwa hayupo duniani.
“Tunaanzia wapi Felly?” nilimuuliza Felly wakati
wa chakula cha jioni ambapo wote wanne
tulikuwa nyumbani kwangu, wakati huo ndio
tulikuwa tunamalizia kula na Felly aliondoka
kwenda kuchomeka ‘projector’ kisha
tulipomaliza alianza kuelezea juu ya uchunguzi
alioufanya kwa siku nne na aliyogundua ili
tuweze kujua zaidi.
“Tuanzie kipindi cha nyuma kidogo mpaka juzi
hapa tulivyokuwa na uhakika kuwa Mary yupo
hapa Fiji. Niliingia kwenye mfumo wa Urusi na
kutafuta kama kwenye vitu vyao kuna jina
linalojulikana kama Mary Robert, nilipata nakala
nyingi sana za matukio ya Mary Robert ambaye
nilihakikisha na kuthibitisha kuwa kweli ni Mary
huyuhuyu, ya kwanza ni Cheti cha kuhitimu
chuo kikuu ambacho Mary alipatiwa na chuo
kikuu cha Altai kilichopo Urusi, hapa Mary
alipewa shahada ya mfumo wa mawasiliano,
ilikuwa mwaka 2003, na kwenye picha ya watu
waliomaliza shahada hiyo ipo hapa lakini
ukiitazama kwa makini sana utaona kabisa hii
picha imepachikwa kwa ujuzi mkubwa, hii inatia
shaka kwakuwa Mary alikuwa Marekani mwaka
1996 akisoma shule ya sekondari huko Tobago.
Lakini pia jina na picha ya Mary inatokea
mwaka 1997 kwenye chuo kikuu cha
Limkokwing huko Malaysia akiwa kati ya
wahitimu wa shahada ya kwanza ya Utawala
wa biashara, kwenye picha ya wahitimu pia
yupo sehemu ya mwisho kabisa, na picha hiyo
sijaielewa pia. Mwaka huohuo kipo cheti cha
Mary akiwa muhitimu wa mafunzo ya kijeshi
kwa watoto wa wanajeshi wa Tobago
yaliyokuwa ya wiki moja huko marekani
yaliyohitimishwa na sherehe ya kupongeza
wanajeshi waliotoka Iran. Mary hakuwa mtoto
wa mwanajeshi wala hakuwa na ndugu
mwanajeshi ila aliweza kuhudhuria mafunzo na
kuhitimu akiwa mwanafunzi bora wa kulenga
shabaha. Hii imenipa wasiwasi mana picha za
wahitimu Mary hakuwepo lakini kuna picha za
mazoezi Mary yupo na ni halisi kabisa. Lakini
pia kuna cheti kingine cha stashahada ya
upelelezi wa makosa ya jinai ambacho Mary
anacho hiki alipata mwaka 1998 chuo kikuu cha
Bradford kilichopo Uingereza. Baadaye
aliaajiriwa na UK Military Academy ambacho ni
chuo cha kijeshi kama mpelelezi, lakini mwaka
huohuo Mary anaonekana tena chuo kikuu cha
Lethoto akiwa ni moja ya wahitimu wa
stashahada ya Uandishi wa habari, na mwaka
uliofuata Mary alifunga ndoa kwenye Kanisa la
St. Petersburg huko Alaska, alifunga na mtu
aliyejulika kama Francisco Domosco, katika
barua pepe iliyotoka kwa Mary kwenda kwa
Domosco wiki mbili kabla ya ndoa yao
alimwambia kuwa hataki sherehe kubwa,
anataka watu wachache tu. Fransic ana Mary
inaonekana walikutana mtandaoni na mara
nyingi waliwahi kuonana. Ila miezi sita baada
ya Mary kufungwa ndoa Domosco alifariki kwa
ajali na hivyo mali zake zilichukuliwa na Mary
ambaye alizifilisi na kuondoka Alaska 2000
mwishoni. Mwaka huo huo Mary alifunga ndoa
na Timoth Mobutu huko Afrika ya kusini, huyu
ni mfanya biashara wa madini, lakini miezi sita
mbele yule jamaa alikufa kwa kupigwa risasi na
Mary alikuwa mrithi wa mali za yule
mwanaume. Hapo Mary alirudi tena Marekani
kwakuwa inaonekana kuna ujumbe wa barua
pepe alioutuma kwa mtu aliyeitwa Derick
aliyekuwa yuko Urusi kumwambia yuko tayari
kuingia kwenye mafunzo, ujumbe huo
haukuonyesha ni mafunzo gani, lakini Derick
alimwambia anaweza kumfanyia mpango wa
kuingia ila sharti ajifunze Kiurusi kwa miezi sita
kwanza, hata hivyo Mary alimjibu sawa, miezi
saba mbele, Mary alimtumia tena yule mtu
ujumbe wa barua pepe akimshukuru kuwa
amefanikiwa ila atafanya kwa miezi mitatu na
kisha atatoroka kwani haitaji kufika mwisho.
Sasa kwenye mazungumzo haya hakuna
mafunzo yaliyotajwa, ila kwenye ujumbe wa
mwisho uliotumwa ulituma kwa kompyuta
yenye anuani ya utambulisho KF5642, hii
kompyuta iliyotumiwa ilikuwa Kazakhstan
upande wa kusini mgharibi mwa Urusi na ni
kaskazini mashariki mwa mji wa Islamabad
Afghanistan. Eneo ilipo kompyuta hiyo kuna
kambi ndogo ya wanajeshi wa kundi la alqaida
sasa ninachojiuliza je alikuwa kwenye hiyo
kambi au la? Lakini majibu sikupata. Mwaka
2001 alimtumia Dany ujumbe wa barua pepe
akimwambia amuandalie vijana wasio na kazi
ila wasomi, wawe ni wale waliotoka JKT na
ambao bado hawajajiriwa na hawajaoa,
alimwambia anataka wawe wenye afya nzuri na
awapime magonjwa yote, wawe imara na wenye
mbavu nene. Ujumbe huu ulitumwa akiwa
Djibouti sehemu inaitwa Arta, wiki mbili mbele
Dany alimtumia majina na picha za vijana hao,
mmoja ni yule ambaye tulimkuta kule Villa
Bridge mwenye asili ya kitanzania. Wengine
picha zao zimetumwa katika namna ambayo
mpaka uwe na vifaa flani ndio uzisafishe
uzione. Kisha wiki hiyo hiyo Mary alitoka
Djibouti na kwenda Tanzania, alipokutana na
vijana wale akamtumia ujumbe mtu anaitwa
Chevinski ujumbe huo ulikuwa ‘Je vais vous
envoyer mes hommes pour la formation que
nous avons parlé, s'il vous plaît raccourcir à
trois mois. tout le paiement a été effectué’,
ujumbe huu ulioandikwa kwa lugha ya Kifaransa
ilikuwa ikimaanisha kuwa ‘ninawaleta vijana
wangu kwako kwaajili ya mafunzo tuliyoongea,
tafadhali fupisha mafunzo na yawe miezi
mitatu. Malipo yote yameshafanyika.’ Huo ndio
ujumbe ambao Mary aliutuma na hapo
inaonekana vijana wale walikwenda Urusi.”
Alimalizia hapo Felly na mimi nilikuwa
nimechoka sana, sikujua kama Mary anaweza
kuwa mtu asikuwa na hadithi moja tu, mambo
mengi sana juu yake inaonekana hatukuwa
tukiyajua, na hiyo pia inaamisha kuwa
itatuchukua muda sana kumuweza Mary lakini
kwangu mimi nitamkamata tu kwakuwa sina
cha kupoteza.
“Hivyo hapo tunatakiwa kufanya nini Felly?”
nilimuuliza Felly ambaye hata yeye alionekana
kama kukata tamaa vile.
“Hapa Dany ndiye ataongea ukweli wa kila kitu,
inaonekana kuna mengi sana ameyaficha
ambayo sisi hatuyajui, tunatakiwa tumjue Mary
kwa uzuri sana na mtandao wake ni upi ili tujue
namna ya kuenenda. Lakini pia Dany ni moja
kati ya watu waliokwenda Urusi kwenye hayo
mafunzo, na baada ya yale mafunzo aliporudi
alikuwa na wale vijana wakaenda mpaka Kabul
ambapo walikutana na mtu anayeitwa
Mahamoud ambaye pia mawasiliano yake ya
barua pepe na Mary yapo ambapo aliambiwa
awape kazi ya kufanya na kama wakishindwa
awaue, lakini hakuna aliyeuawa na wala kazi
waliyopewa haikuelezwa. Na kingine ambacho
hamkijui ni kwamba Mary aliwahi kutembea na
Dany wakiwa Qala-e-Fathullah, eneo hili liko
kaskazini mwa mji wa Kabul na liko karibu
kabisa na Khaje Burga. Na baada ya hayo Dany
aliondoka kurudi Tanzania na Mary alimtumia
ujumbe wa barua pepe akimwambia kuwa
walichokifanya kiwe ndo mwanzo na mwisho ili
wasiharibu kazi na Dany asijiweke pabaya.”
Aliongeza Felly.
“Sasa kama dany alikuwepo kwenye mafunzo
kwanini alimtumia ujumbe Paul, yule muuaji wa
Tanzania na kumwambia nashukuru
kukufahamu na nimetambulishwa kwako na
Mary nategemea tutafanya wote kazi pale
itakapobidi.” Nilimuuliza Felly.
“ule ujumbe haukuwa unaanisha hayo,
nimejaribu kujiuliza pia lakini niliona herufi zake
zikimaanisha kitu kingine, kulikuwa kwenye kila
neno kuna majina ya mahali, mfano kwenye
‘Nashukuru’ ambayo kwa mujibu wa Pamela
maana yake kwa kingereza ni kutoa asante,
neno hilo lilikuwa limeandikwa NashuKuRu,
ukichukua hizo herufi kubwa na ndogo yake
inayofata utapata neno NAKURU, hii ni sehemu
ipo Kenya ambapo Mary alishawahi kumtumia
ujumbe Paul akiwa huko, ukichukua neno lingine
‘kukufahamu’ lilikuwa limeandikwa
KukuFahamU, hii inasimama badala ya KFU,
ambapo niliiona kwenye ujumbe pia toka kwa
Paul kwenda kwa mtu anaitwa Rajab neno hilo
lilikuwa likimaanisha KING FINANCIAL
ASSOCIATION, hii ni taasisi moja ya fedha
iliyopo Nakuru, ambayo ilivamiwa siku nne
baada ya hawa watu kutumiana ujumbe na
kiasi cha pesa kilichoibwa kilikuwa ni dola laki
6.Hivyo maneno mengi waliyokuwa wakiongea
haikumaanisha vile ambavyo wanamaanisha.
Baada ya tukio hilo Mary alimtumia ujumbe mtu
anaitwa Apolo akimwambia amemuwekea pesa
kwenye akaunti namba hii 23456’6753 aliweka
kialama katikati katika namba hizo ionekane ni
makosa, lakini haikuwa makosa hiyo sio
akaunti namba ni namba za kijiografia za eneo
la Iringa huko nchini Tanzania, ukiangalia
kwenye ramani zinazopatikana kwenye satelaiti
utagundua kuwa kwenye namba hizo kuna
benki ya biashara na siku hiyo ambapo ujumbe
huo ulitumwa kesho yake kulikuwa na taarifa
kuwa benki ile ilivamiwa na kiasi cha shilingi za
kitanzania milioni mia 7.” Alieleza Felly lakini
bado nilikuwa naona mambo yanazidi kuwa
mengi sana.
“Patrick unasemaje.” Nilimtazama Patrick
ambaye alionekana kuchoka sana, ilionekana
kabisa alikuwa anajuta kukutana na Mary, lakini
hiyo haiondoi ukweli kwamba alikuwa
amepambana na gaidi.
“Nilitaka kujua, je Mary ni gaidi, jambazi au
nani?” aliuliza Patrick.
“hatujui chochote kuhusu hayo kwakuwa
inaonekana kuna matukio mengi ya kihalifu
ambayo Mary anahusika, kila wanapotumiana
ujumbe kuna jambo zito linalotokea hivyo
hatufahamu kabisa kuhusu mambo mengi
kwakuwa bado taarifa ni nyingi sana.” Alijibiwa
na Felly na hapohapo wakati bado tukiongea
simu yangu iliita, ilikuwa ni namba ya Mary na
hapo sikupokea badala yake niliiacha na Felly
aliingiza kwenye kompyuta ili kujua mahali
ilipopigiwa ile simu tuweze kumpata Mary
iwapo tutajua mnara uliotumiaka. Baada ya
Felly kumaliza kuiingiza niliipokea;
“Khajat huwezi kuitafuta namba yangu
ilipotokea, mimi sio mjinga hivyo, napiga toka
kwenye mkondo usioweza kutafutika, hivyo
usiache kupokea simu yangu ukitegemea
unaweza kunitafuta kwa mtindo huo.” Aliongea
huku akicheka.
“Unahitaji nini wewe mkosaji?” nilimuuliza
swali, lakini alizidi kucheka. Ile hali ya kucheka
ilizidi kuniudhi sana, nilikuwa na hasira na
nilitamani sana kumkamata kwa muda ule.
“Ujue tofauti yako wewe na mimi sio tu kuwa
mimi naua watu wema na wewe unaokoa
maisha yao, hapana, wewe unahasira sana na
unaongozwa na hasira zaidi kuliko utaalamu wa
uyafanyayo, ungekuwa kama dada yako
anayeitwa Felicity basi ingekusaidia, yeye hana
hasira, ni mwoga na woga wake unamsaidia.”
Aliongea kwa dharau huku akiendelea kucheka.
“Mary unajichimbia shimo refu la kujifukia
mwenyewe kila unapozidi kuongea, kata simu.”
Nilimwambia kwa hasira na nilipotaka kukata
simu aliendelea kuongea nikaamua kumsikiliza
kilichomfanya apige simu.
“Nataka kesho saa 2:00 asubuhi umuachie Dany
huru na umpe simu yake ili niwasiliane naye
kwakuwa ninamuhitaji. Ni lazima wewe kufanya
hivyo na sio ombi. Ikifika saa mbili na dakika
moja hujamuachia basi elewa kuwa utakuwa
wewe na dada yako pamoja na Patrick
mmejiingiza kwenye vita itakayogharimu damu
ya mmoja kati yenu, mimi ni binadamu na
ninakikomo cha uvumilivu, nitawavumilia nyie
kukaa na Dany hadi kesho saa 1:55 ila baada
ya hapo muachieni. Hii ni amri, nasisitiza ni
amri.” Aliongea na kabla sijaongea chochote
yeye alikuwa ameshakata simu.
“Vipi Felly umeweza kujua namba ilipotokea?”
nilimuuliza Felly ambaye hata hivyo alikuwa
amekaa kimya akiwaza.
“Hakuna kitu, simu yake haiwezi kufanyiwa
hivyo.” Aliongea Felly.

>>KESHO YAKE<<

Ilikuwa asubuhi ya saa 2:30 bado tulikuwa
hatujamuachia Dany na wala hatukuwa na
mpango wa kumuachia, tulimtoa ndani na
kumuingiza kwenye gari ya Felly ili tumuamishe
toka nyumbani kwa Felly ili akakae kwangu na
siku hiyo ndiyo nilipanga kutumia muda mwingi
na yeye ili nipate kujua majibu ya maswali yote.
“Huyu ni bora kumuweka kwenye buti.” Aliongea
Felly.
“Je akitoroka.” Nilimuuliza Felly japo niliamini
kuwa asingeweza kutoroka lakini ilikuwa kama
ni tahadhari tu. Tulimtoa na kumuingiza kwenye
buti huku tukiwa tumemfunga katika namna
ambayo asingeweza kutoroka hata awe na
mazoezi vipi. Baada ya hapo niliwasha gari na
kuondoka kwa kasi sana. Tukiwa njiani nilisikia
kama kitu kimegonga gari kwa nyuma,
nikasimamisha gari na kuzunguka nyuma lakini
sikuona kitu hivyo nikarudi kwenye gari na
kuodoka, nilipofika nyumbani kwangu niliingiza
gari mpaka karibu na mlangoni na hapo
nilishtushwa na damu zilizoonekana
kuchuruzika toka kwenye buti. Haraka
nikaamua kulifungua lakini nilichoka baada ya
kuona Dany akiwa anavuja damu kichwani,
nilipomtazama vizuri alikuwa na tundu kubwa
lililopenya kichwa chake na kutokezea kwa
nyuma. Wote tulibaki mdomo wazi, nilimgeuza
na kumtazama vizuri alikuwa na tundu la risasi,
ikabidi tufunge ule mlango wa buti na kuanza
kuukagua na ndipo tulipokuta tundu la risasi
moja. Nilipotazama kwenye siti ya gari kwa
nyuma niliona ile risasi ikiwa imejipenyeza
kwenye kiti. Ilikuwa ni risasi ya rifle na hii
ilimaanisha kabisa kuwa alikuwa ni Mary.
Tulichukua ule mwili na kwenda kuuchimbia
mbali sana na pale na kisha tulirejea kwangu
tukiwa wote wanne, Pamela, Patrick, Felly na
mimi, tulikuwa tukitafakari nini cha kufanya na
hapohapo Mary alipiga simu yangu na mimi
nilipokea.
“Khajat, nilikuambia mimi ni binadamu na huwa
uvumilivu wangu una mwisho, sasa nakupa
zoezi lingine, naomba umpe Patrick simu
kwakuwa simu niliyompigia haipatikani.”
Aliniambia kama alikuwa akiniamuru.
“Simpi yeyote simu, ongea unachotaka kuongea
kama huna cha kuongea basi subiri siku
nikikuweka mkononi ili uongee.” Nilimwambia
vile na hapo alizidi kunipandisha hasira.
“Tumia busara ndogo Khajat, mpe Patrick
simu.” Aliongea tena na mimi bado nilizidi
kumkatalia.
“Basi nitakupigia simu baada ya nusu saa,
hakikisha unakuwa na uamuzi wa kumpa simu
Patrick au kumwambia awashe simu yake,
usichukie kipenzi, vita hii itakupelekea kifo
muda ukifika.” Aliongea na kucheka kisha
alikata simu. Tulikuwa kimya wote kila mmoja
akitafakari ni nini tutafanya. Wote walikuwa
wanakaribia kukata tamaa lakini mimi bado
nilikuwa na matumaini. Baada ya nusu saa
simu yangu iliita tena na sasa niliipokea na
kuipandisha sauti ili kila mtu asikie.
“Khajat nadhani uko karibu na Pamela hapo na
Patrick, nataka wasikie kwanza hili kisha
nitatoa maelekezo.” Baada ya kusema hivyo
nilisikia kama mtu akipigwa kofi ambalo
halikuwa kubwa sana kisha tulisikia sauti ya
mtoto ikilia, nilishtuka kwakuwa alivyolia tu
Pamela alianguka na kuzimia, ilikuwa ni sauti
ya mtoto wa Pamela, nilikata kwanza simu na
kumgeukia Patrick.
“Kwani mtoto mlimuacha wapi?” nilimuuliza
Patrick aliyekuwa anahangaika kumpepea
Pamela.
“Tulimuacha nyumbani na mfanyakazi, walinzi
wapo pale.” Alinijibu na mimi nilizima simu
yangu kwanza kisha niliwasha gari na kuondoka
moja kwa moja mpaka kwa Pamela, nilipofika
pale nilikuta walinzi wote wamefungwa kamba
kwenye miti na mfanyakazi wa ndani alikuwa
amefungiwa kwenye kabati la nguo.
“huyo mwanamke amekuja hapa muda gani?”
nilimuuliza yule mfanyakazi aliyekuwa
akitetemeka.
“amekuja asubuhi baada ya bosi kuondoka.”
Alijibu hivyo na wala sikuhangaika tena
kuwahoji, niliondoka mpaka kwangu tena na
sasa nilikuta Pamela ameamka na Patrick pia
alikuwa akimbembeleza kwani alikuwa akilia
kupita kawaida. Felly alikuwa amekaa na hajui
cha kufanya. Nikawasha simu yangu na
kumpigia Mary.
“Nakusikiliza.” Nilimwambia hivyo mara baada
ya yeye kupokea simu.
“Nataka uweke simu ili Patrick asikie.” Aliongea
hayo na mimi niliweka simu sawa ili Patrick na
wote pale wasikie.
“Nakusikia, ongea.” Alisema Patrick na Mary
alianza kuongea.
“Patrick nataka ikifika saa saba mchana leo
uende uwanja wa ndege, ukifika pale yupo
kijana wangu atakupa kila kitu kwaajili ya
kusafiria, utaingia kwenye ndege saa 8 na
ndege hiyo itakupeleka mpa Somalia. Ukifika
Somalia utatafuta gari ndogo yenye namba
SMT5678, ni voxy nyeusi, ukiiona nenda
mwambie dereva akupeleke Jowhaar na hapo
utanikuta, hakuna simu kwenye safari yako
nzima, hakuna kuwasiliana na yeyote,
nikigundua umeenda kinyume na hilo basi jua
kabisa mwanao huwatampata akiwa hai.
Umeelewa?” aliuliza Mary na Patrick aliitika
huku aking’ata meno.
“Nimekuelewa.” Patrick alijibu na kushusha
pumzi.
“Nakupenda sana Patrick kwakuwa wewe ni
msikivu, mpe Khajat simu.” Aliongea Mary na
mimi niliingilia sauti ile.
“Khajat usijaribu kumfata Patrick nyuma
kwakuwa utahatarisha maisha ya Cris, ubishi
wako uzingatie uhai wa huyu mtoto kwakuwa
sitasita kuwaletea kichwa chake kama
nitagundua mnafatilia. Ninawaona kwenye kila
jambo.” Aliongea Mary na mimi nilimkatisha.
“Tutampataje mtoto.” Nilimuuliza lakini moyo
wangu ulikuwa unasononeka sana.
“Mtoto atakuwepo sehemu salama, Patrick
atakaposhuka uwanja wa ndege wa Bender
Qassim basi nitakupigia simu ukamchukue
mtoto sehemu.” Aliongea na kuniuliza kama
nina swali zaidi.
“Nitakuamini vipi kwamba utamleta mtoto?”
nilimuuliza tena.
“Huna chaguo lingine zaidi ya kuniamini,
ukiniona huniamini basi fanya utaratibu
mwingine wa kumpata ila ujue utakuwa
unaweka shingo yake karibu na kisu.” Aliongea
na kukata simu.

ITAENDELEA
 
RIWAYA: KISASI
MTUNZI: FRANK MUSHI
SEHEMU YA KUMI NA SABA

“Watu waliofanikiwa zaidi ni wale walioyajua
matatizo, waliozijua harakati za maisha yao,
waliokumbana na misukosuko na taabu,
waliokutana na kukata tamaa na majaribu lakini
mwisho wa siku waliyakabili na kusonga mbele.
Lolote ambalo haliwezekani leo, unaweza
kulifanya liwezekane kesho, hiyo ni kama tu
utaamua juu ya mustakabali wa njia uipitayo”
HII NI SEHEMU YA KUMI NA SABA

***KHAJAT***
Akili ya Mary ilikuwa inafanya kazi haraka sana,
nilikuwa nimekubali kwa mpaka hapo alipofikia.
Alichokifanya kilikuwa ni mbinu ya kumaliza kila
kitu kwa upande wetu, alikifanya akiwa ana nia
ya kuzima mbio zetu za kumuwajibisha, tusinge
weza kuhangaika tena kama angemuua Patrick
hivyo hiyo ilikuwa kete yake ya mwisho
kuicheza ambayo alijua kabisa ingenyong’onyes
ha juhudi zetu. Sikuwa na lolote kichwani, kwa
mara ya kwanza katika ukubwa wangu nilikaa
chini na kulia, nilimuonea sana huruma Patrick
lakini sikujua nitaweza kumsaidia namna gani.
Kwa vyovyote vile kama Mary ameamua
kumchukua Patrick basi hiyo ilimaanisha kuwa
alikuwa makini kutufatilia na sisi ilikujua kama
kweli Patrick alikwenda mwenyewe. Muda
ulizidi kwenda na saa saba ilikuwa imekaribia.
Kila mtu alikuwa akilia kivyake kasoro Felly tu
aliyekuwa yuko busy kusikiliza tena ile sauti ya
maelekezo ya Mary na kuyaandika pembeni.
Hakuonekana kuwa na chembe ya woga wala
kuhofia juu ya lile litakalokwenda kutokea kwa
Patrick, hiyo ilinipa moyo kiasi na kunifanya na
mimi niwaze zaidi. Sikuwahi kufikiri kuwa
ingefikia huku tulikofikia hasa kwakuwa
mwanzoni ilionekana kama ni kitu kidogo tu,
lakini mpaka sasa hatujajua uwezo halisi wa
Mary japo ameshatuonyesha matukio ambayo
yametutisha kwa kiasi fulani, inaonekana ana
watu kila sehemu na hiyo inamaana ni rahisi
sana kwake kufanya jambo lolote. Umri halisi
pia wa Mary ulinisumbua, japo alikuwa na
miaka isiyozidi 30 lakini alikuwa na uzoefu wa
mambo wa miaka 60, kwa muda mfupi wa
maisha yake ilionekana kabisa Mary aliutumia
sawia kupanga aina ya maisha anayoyataka.
Moyoni nilikuwa nikijiuliza ni nini kimemfanya
Mary awe vile. Nilifahamu na ninajua kabisa
mazingira na matukio yatokeayo kwa binadamu
huchangia kumtengeneza awe mtu wa aina
gani, nisichokuwa na kielewa kwa wakati huo ni
mazingira gani au matukio gani yalimtengeneza
Mary kuwa mtu wa aina ile. Alikuwa ni muuaji
mwenye sura nzuri usiyoweza hata kuitilia
shaka. Urembo wake ungeweza kumvutia tajiri
yoyote duniani kutamani kumpa kasri yake na
roho yake ila umuingizapo ndani basi ni wazi
kuwa umeingiza bomu ambalo ni wazi kabisa
muda wowote litalipuka. Mary anafanya haya
kwanini? Ni swali gumu kujijibu labda yeye tu
ndiye ajuaye. Kumuua Dany ilikuwa ni ujumbe
kwetu kuwa kwake hana mtu muhimu, yeyote
anaweza kuwa muhimu kwa muda tu na
ikitokea hakuna haja tena ya kuwa nae
kutokana na muda basi ni wazi humuondoa
duniani. Hakuwa mwanamke wa mchezo, japo
nilimfahamu muda mfupi lakini nilikuwa
nimemsoma kwa namna hiyo.
*****

Ilikuwa ni saa 6:25 hii ilimaanisha bado dakika
35 kutimia saa aliyoambiwa Patrick awepo
uwanja wa ndege. Bado Patrick alikuwa pale
akimbembeleza Pamela. Felly alinyanyuka pale
alipokuwa amekaa na kutuita wote. Kisha
tulipokuwa tumefika alianza kuongea kwa sauti
iliyoonyesha kukata tamaa.
“Hatuna jinsi hapa, kama tunataka tumpate Cris
basi lazima Patrick aende, lazima tutimize
matakwa ya Mary hasa kwa wakati huu
mgumu.” Aliongea Felly huku akionekana
kulengwa na machozi.
“Lakini pia tutakuwekea kifaa maalim kwenye
saa yako kwa ndani kitakachokuwa
kikituonyesha kila unakoelekea ili tujue.
Nakuahidi hakuna baya litakalokutokea na
unatakiwa uwe jasiri. Kila nafasi ya kutoroka
itakapotokea au nafasi ya kumuua Mary
itakapotokea basi itumie. Unajua kutumia
bastola na bunduki basi ukipata nafasi ya
kuipata itumie. Sisi tuko nyuma yako kwa kila
jambo, ni lazima tutakutoa kwenye hilo banio
alilokuweka na Cris atakuwa salama. Usiogope,
kumbuka unafanya hivi kwaajili ya Cris, huu ndo
muda wa kumfanya Cris aje ajivunie ushujaa
wako baadaye.” Nilimwambia Patrick na yeye
alionyesha kujaa uimara na utayari wa kufanya
hivyo. Patrick alikuwa mtu mzuri sana, alikuwa
ni mtu anayejali sana watu na hii ilikuwa ni
maumivu makubwa sana kwa Pamela.
Hatukuwa na namna ya kufanya zaidi ya
kumuacha akajiandae, tulimuwekea kile kifaa
kilichoonyesha alipo kwa kila hatua aliyopiga,
hii ingetuwezesha kujua sehemu aliyopo. Baada
ya hapo gari ilikuwa tayari na tulimsindikiza
mpaka nje. Alikuwa akijizuia kulia lakini
tulimuona machoni kwamba alikuwa akilia.
Walikumbatiana na Pamela ambaye na yeye
alikuwa akilia kupita maelezo, mimi niliamua
kuwaacha pale nje na kuingia ndani nikitazama
kwa dirishani kwakuwa ilikuwa imeniuma sana.
“Pamela, kama sitarudi, au kama nitakufa
naomba unisaidie kumwambia Cris kuwa baba
anampenda sana, mwambie nilitamani sana
kumuona akiwa mkubwa na mwenye furaha
huku akipata malezi yetu sote, lakini mwambie
kuwa baba aliamua kujitolea ili wewe uishi.”
Aliongea hayo kwa sauti ya uchungu na
kumkumbatia Pamela.
“Utakuwa salama Patrick usiseme hivyo, utarudi
salama mume wangu, tutampata mtoto wetu,
niko tayari kutumia hadi senti ya mwisho ya
pesa zangu kuhakikisha kuwa unakuwa hai.”
Aliongea Pamela huku akizidi kulia, ilikuwa
zimebaki dakika 20 tu na hatukuwa tayari
kuchelewa muda na kusababisha matatizo
mengine. Waliagana na Patrick alimshukuru
sana Felly na hapo Patrick alipanda kwenye gari
na kuondoka, kutoka pale nyumbani mpaka
uwanja wa ndege ilikuwa ni mwendo wa dakika
20 kwa spidi 80, hivyo tulielewa kabisa Patrick
angeweza kufika kwa wakati. Felly na Pamela
walirudi ndani na hapo wote tulikaa kwenye
makochi kila mmoja akigeukia upande wake,
Pamela alikuwa bado akilia lakini Felly
aliendelea kuisikiliza ile sauti ya Mary
alipokuwa akitoa maelekezo, mimi sikuwa
nikiwaza chochote zaidi ya kupangilia kitu cha
kumfanya Mary siku ambayo atajiingiza kwenye
himaya yangu. Nilikaa pale kwenye kochi na
baada ya muda mfupi mimi na Pamela wote
tulipitiwa na usingizi. Nilikuja kushtuliwa na
sauti ya Felly, nilipoitazama saa yangu ya
mkononi ilikuwa ni saa 9 mchana na pale
ukutani alikuwa amebandika makaratasi na
picha nyingi, nikajua kabisa kuna kitu
amegundua, nilitazama pale sikumuona Pamela,
wakati bado nikijinyoosha Pamela aliingia akiwa
na chakula na kila mmoja alipewa mfuko wake,
tulikula na tulipomaliza Felly alianza kuelezea
tena.
“kile kifaa tulichomuwekea Patrick kwenye saa
kitakuwa kimeharibiwa kwakuwa sioni tena
kwenye kompyuta yangu. Alipofika uwanja wa
ndege pale alikaa kama lisaa limoja hivi ndio
hapo sikuona tena alipoelekea.” Aliongea Felly
na hapo nilizidi kuchoka. Kile kifaa ndicho pekee
kingeweza kutuonyesha Patrick anapokwenda
na hiyo ingetusaidia kumtafuta na kumrudisha
akiwa salama.
“Hivyo hatuna namna nyingine ya kujua alipo?”
nilimuuliza Felly.
“Nahisi tunayo ila sina uhakika nayo sana.”
Aliongea Felly na hapo nilikaa makini ili niweze
kumsikiliza.
“Kwenye maelezo yake Mary amesema kuwa
Patrick akifika uwanja wa ndege wa huko
Somalia atapanda voxy nyeusi yenye namba
SMT5678, lakini gai yenye namba hizo sio gari
za Somalia ni gari za Suva, nimejaribu kuingia
kwenye tovuti ya idara ya usajili wa magari ya
Suva na kuwaomba kusajili gari langu kwa
namba hiyo wakaniambia kuwa namba hiyo
tayari ina mtu, na nilipotafuta gari yenye namba
zile kwenye kamera za barabara za Suva
zinazoelekea uwanja wa ndege wa pale mjini
sikuona, ila gari hiyo yenye namba hizo za
usajili zilionekana juzi zikielekea barabara ya
Natovo ambayo ni barabara ya kuja Fiji kupitia
msitu wa Ravo, nilipoitafuta gari hiyo tena
kwenye kamera za uwanja wa ndege wa hapa
kwetu halikuonekana lakini lilionekana leo
asubuhi kwenye kamera za barabarani mitaa ya
bandarini na saa hizi limeonekana uwanja wa
ndege wa Vunesia, uliopo kwenye kisiwa cha
kusini mwa hapa tulipo. Dereva wa gari hilo
aliyejiandikisha pale bandarini ili gari yake
ivushwe anaitwa Johari Qasim, hii inaonyesha
kuwa Patrick hapelekwi Somalia, Patrick
anakwenda Kisiwa cha kadavu kilichopo kusini
mwa hapa tulipo ambacho kukifikia kinachukua
lisaa limoja na nusu tu. Patrick ameambiwa
akifika huko Somalia uwanja wa Bender Qasim
amwambie dereva wa gari hiyo ampeleke
Jowhaar, ni kweli kwamba Jowhaar ni eneo
lililopo Somalia, lakini kwakuwa jina la huyu
dereva linamajina mawili ambayo yote
yanatokea kwenye maelekezo ya Mary basi
hapa tujue kuwa huko ndiko anakopelekwa
Patrick na sio Somalia.” Aliongea felly na muda
sio mrefu simu yangu iliita na alikuwa ni Mary,
nilitazama saa yangu ya mkononi ilikuwa ni saa
10 na dakika ishirini, nikapokea;
“Ndio, unataka nini?” nilimuuliza Mary na yeye
alicheka kabla ya kusema lolote.
“Sina cha kutaka kwako kwakuwa mimi na
wewe tumemalizana, nasubiri muda ukifika
nitakuja kukunyamazisha na mwambie dada
yako nitamtumia barua ya kazi, kama atakuwa
tayari nimuajiri kwa pesa nyingi basi nitafanya
hivyo.” Aliongea huku akicheka na mimi
sikumjibu chochote.
“Okey, sasa sikiliza vizuri, mwambie Pamela
aende Pilmira Hotel, akifika pale aseme
amekuja kwenye chumba namba 548 na
ajitambulishe kama Patronila Mkesi, atapewa
funguo na atamkuta mwanae.” Aliongea Mary
na kutaka kukata simu lakini nilimuwahi.
“Kwanini yeye na sio mimi au mwingine
yeyote.” Nilimuuuliza na kama kawaida
alicheka.
“Yeye ndiye mwenye mtoto, ndio maana
nilimwambia yeye. Ingekuwa mtoto ni wako
basi wewe ndio ungeenda kumchukua, lakini
mmmmhh, unaweza kumsindikiza.” Aliongea
kwa dharau na kuendelea kucheka.
“Kama mtoto umemdhuru nitakukamata na
kukukata vipandevipande.” Nilikuwa na hasira
sana na sikudhani kama atakuwa amemuacha
mtoto akiwa hai.
“Mimi ni mtu wa ahadi, niliahidi nikishampata
Patrick mtoto atakuwa salama hivyo nimetimiza
ahadi yangu kama nitakavyotimiza ahadi
niliyokuahidi ya kukuua.” Aliongea huku
akiendelea kucheka.
“Ni bora ukawahi kuitimiza kabla mimi
sijatimiza ya kwangu.” Nilimwambia na
kumkatia simu. Nilimgeukia Pamela na niliona
dhahiri kuwa alikuwa akitetemeka, hii
inawezekana ni kwakuwa tu alikuwa anahofia
juu ya mtoto wake. Kabla sijafikiria lolote
nilisikia Felly akiongea na simu na muda si
mrefu sana alikata simu na kuingia ndani.
“Khajat nimeongea na rafiki yangu mmoja
anaitwa Babra anafanyakazi kitengo cha
madawa ya kulevya pale uwanja wa ndege
ambapo ndio tunadhani kuwa Patrick atakuwa
amepelekwa, amesema ameliona hilo gari na
alilikagua yeye ni kweli kuna mwanamke, na pia
kuna ndege imetua hapo uwanjani muda si
mrefu sana na kwamba ilitoka Fiji saa nane,
gari hiyo yenye huyo dada wa Kiarabu ilikuwa
inaondoka muda huo ambapo nilikuwa
naondoka naye na ndio anaifatilia, hii inamaana
inawezekana kwamba Patrick alipofika uwanja
wa ndege wa huku alipandishwa kwenye ndege
ya kwenda kisiwa cha kadavu.” Aliongea Felly
kwa haraka haraka huku akiweka visu kwenye
mkoba wake, hiyo ilimaanisha kuwa safari
ilikuwa inaanza lakini bado nilikuwa
sijajiridhisha.
“Sasa tuna uhakika gani kuwa Patrick yuko
huko wakati bado hajaonekana huko.”
Nilimuuliza Felly.
“Kwenye maelezo ya Mary alisema kuwa
atapiga simu kumrudisha mtoto pale
ambapoPatrick atakuwa amefika Somalia, sasa
Somalia na hapa ni zaidi ya siku moja, hapa na
Kadavu ni lisaa limoja na nusu kwa ndege na
amepiga simu muda mfupi baada ya ndege
kutua huko Kadavi, na tayari gari aliyotoa
maelekezo kuwa Patrick akapande ilikuwa
hukohuko, na msichana anayeiendesha gari hiyo
anamajina mawili ambayo yanaendana kabisa
na maneo mawili yenye majina matatu
aliyoyataja Mary. Hii inamaana kuwa ni kwa
asilimia mia moja kuwa Mary yuko Kadavi.”
Aliongea na hapo alikuwa ameshamaliza
kuweka vitu vyake sawa.
“Kwahiyo tunafanyaje?” nilimuuliza huku na
mimi nikifata kisu changu.
“Tunakwenda kumfata mtoto kwanza kisha
mimi na wewe tutakwenda Kadavi, tunafanya
vamizi baridi, hakuna risasi, ni mkono na kisu
au kitu kingine kisicho cha moto.” Aliongea Felly
na hapo tuliondoka mpaka kwenye hoteli
tuliyoelekezwa na tulipofika pale tulimtanguliza
Pamela na yeye aliulizia kama alipoambiwa na
kupewa ufunguo kisha sisi tulikuwa
tumetangulia kule juu, alipokuja alifungua na
tulimkuta Cris akiwa salama kabisa japo
alikuwa na wekundu mguuni ulioonyesha kuwa
lile kofi nililolisikia ilikuwa alipigwa Cris mguuni.
Hatukupoteza muda badala yake tulimrudisha
Pamela na sisi tuliwahi uwanja wa ndege na
kukodi ndege ndogo ya kasi iliyochukua lisaa
limoja.
“Babra umefikia wapi na hiyo gari?” Felly
alimpigia huyo rafiki yake wakati tukiwa
tumeshashuka uwanja wa ndege.
“wameingia kwenye gofu moja liko kilomita
kumi toka hapo uwanjani, kuna kijana hapo
nilimwambia mkifika awape gari, mtapita
barabara ya kwenye Hoolu Park kisha mkifika
Pier mtakuta nimeegesha gari barabarani,
mkishafika hapo tu mimi mtanikuta.” Aliongea
Babra na muda sio mrefu tuliletewa gari na
safari ya kwenda kule ilianza. Nilikuwa
naendesha mimi gari kwakuwa nilihisi nina
haraka kuliko kawaida, tulifanikiwa kufika pale
kwenye eneo alilotuambia na yeye alitokea.
“Sasa kuna geti pale na gari limeingia kule
ndani kabisa, pale getini kuna walinzi wawili,
kule mbele kidogo kuna walinzi wawili na ndani
kule sijaweza kujua, ila tunatakiwa kuhangaika
na hawa kwanza ili tupitie getini kwa hapa
kwanza, hivyo nitajifanya nimeng’atwa na
nyoka na nitakwenda kwa wailinzi pale
nitawaeleza kuwa nyoga bado yupo hapa
kichakani ili watoke pale na nyie mtangoja kule
kwenye kile kichaka pale karibu na geti ambapo
ndipo nitamuelekeza kuwa nyoka yupo, kisha
wakija mtamaliza.” Aliongea Babra na hapo
alivua viatu na kuanza kupita vichakani akienda
kule kwenye kichaka cha upande wa pili ili
atokee kule karibu na geti, na sisi tulikuwa
nyuma tukimfata, alipofika maeneo yale alianza
kulia na kuchechemea kuelekea kule getini na
alipofika pale wale walinzi walimfata;
“Unatatizo gani.” Mmoja wao alimuuliza na
Babra aliyekuwa bado akilia pale chini.
“Nimeng’atwa na nyoka, yuko pale bado ni
mkubwa sana.” Baada ya kuwaambia hivyo
walitoka na kwenda pale kichakani kuangalia
kama huyo nyoka bado yupo na Babra aliwafata
kwa nyuma kisha alipokaribia Babra alichomoa
waya mfukoni na kumrukia mmoja shingoni
kisha alipitisha ule waya kwa nyumba na
kuupitisha kwa nguvu na moja kwa moja ulikata
koo na wakati huo Felly alimkamata yule
mwingine na kukata shingo, kisha wote
tuliondoka mpaka geti la pili kwa kupita upande
kwa upande kwenye maua na tulifanikiwa
kuwaweka chini walinzi wale wawili na mmoja
Babra alimchinja kwa kutumia waya. Hapo
tulifanikiwa kumaliza orodha ya walinzi pale nje
na sasa tulielekea ndani ya lile jengo, Babra
yeye hakuwa muongeaji, alikuwa kama jini, yeye
ni dam utu, anachinja kila anayekutana naye.
Alitangulia yeye kuingia ndani na ndiye
aliyetupanga, baada ya kuvuka mlango
tukakuta walinzi wengine na hapo kama
kawaida kila mtu alikamata wakwake, ila nilizidi
kushangaa jinsi ambavyo Babra alikuwa
akiwachinja kwa waya. Alipochungulia ndani
aliwaona watu wanne na sisi tulipochungulia
tulimuona Patrick akiwa amefungwa na Mary
alikuwa anaongea na simu na kuna mlinzi
mwingine alikuwa pale na yule dada ambaye
kwa mujibu wa Babra ndiye aliyekwenda uwanja
wa ndege, tulivamia na mimi nilimrukia mlinzi
na Felly alimrukia yule dada lakini hakumuua
bali alimzimisha, wakati tumeshawadhibiti hawa
tulishtuka kuona Babra ashamuweka Mary
waya shingoni na sasa alikuwa anataka kuvuta
ndipo Felly alipopiga kelele.
“Babra acha.” Alipaza sauti na Babra aliacha.
“Mary nilikuahidi.” Nilimwambia hayo na hapo
nilimpiga ngumi ya pua iliyomfanya alewe na
kuzimia.
ITAENDELEA
 
RIWAYA: KISASI
MTUNZI: Frank MUSHI

SEHEMU YA KUMI NA NANE

“Umaskini wa fikra ni mbaya zaidi kulikoni
umasikini wa kipato. Fikra sahihi kwa wakati
sahihi ndio njia ya kupata suluhu ya kila
limfikalo mwanadamu.


********KHAJAT**
Nilimshukuru sana Felly kwakuwa umakini wake
umenifanya nijione mtu tena. Hatukukaa sana,
tulipohakikisha kuwa Patrick hana tatizo lolote
tuliamua kumchukua na Mary tayari kwa kurudi
Fiji. Baada ya kuingia kwenye ile ndege ndogo
tuliyokodisha tuliweza kuondoka moja kwa moja
mpaka Fiji bila tatizo lolote na tulifika mpaka
nyumbani.
“Nini kinafuata?” nilimuuliza Felly ambaye mara
zote alionekana kama kuzuia ili nisimfanye
Mary chochote.
“Kwanza lazima Mary arudishe vitu vyote vya
Patrick lazima alipe gharama ya kila kitu, na
kitakachofuata ni kwenda Tanzania kesho
asubuhi.” Aliongea Felly na mimi nilikuwa
nikimtizama kwa mshangao.
“Unaakili vizuri wewe? Tanzania kufanya nini?”
nilimuuliza na yeye wakati huo alikuwa
akitembea kuelekea kule alikokuwa Mary na
Patrick.
“Nataka tupate nyaraka zote za kampuni ya
Patrick alizobadilisha ili kusaidia kurudisha mali
ya Patrick na mambo mengine yatafata.”
Aliniongelesha hayo na hata hivyo sikuwa
nimemuelewa.
“Mengine yapi? Unataka kumuachia huru si
ndio?” nilimuambia na yeye alionekana
kuchoshwa na maswali yangu.
“Khajat yametosha maswali, tukubaliane kwa
pamoja, tumsaidie Patrick arudishe kwanza mali
zake kisha utamfanya chochote utakacho.
Jiandae kesho tunaondoka.” Alimaliza na
hapohapo niliamua kurudi kwenye kochi na
kukaa, muda wote huo Mary alikuwa
amepoteza fahamu bado. Felly aliwaita kina
Patrick na Pamela pale na wote tulikaa kama
kikao kidogo;
“Kila mmoja anisikilize kwa makini, huyu hapo
mnayemuona, anaitwa Babra ni rafiki yangu,
tulikuwa naye jeshini lakini yeye ni mwalimu wa
mafunzo ya kivita pia ni mpelelezi wa kitengo
cha madawa ya kulevya na ugaidi wa uwanja
wa ndege wa huko kidava.” Alitambulisha na
wote tulishukuru kumfahamu. Babra aliendana
sana na mimi na nilipenda jinsi alivyokuwa,
alikuwa ni mshap na sio mzungumzaji sana.
“Kesho tutaondoka kwenda Tanzania,
nimeshafanya mawasiliano na watu wa ndege
na tumepatiwa tayari sehemu za kukaa, ila
sijajua Mary tutaondokaje naye bila kuleta shida
njiani.” Aliongea Felly na hilo wala halikuwa
shida kwangu.
“Hilo sio tatizo, ukimaliza kuongea nitakuwa
tayari nimekuonyesha njia ya kuondoka naye.”
Nilimjibu Felly na yeye alikubali kisha aliendelea
na maelezo.
“Tunakwenda Tanzania kama watalii, kila kitu
kimeshaandaliwa na Babra anawatu wake kule
watakao weka mambo sawa, tunaenda watu
wanne, mimi, Khajat, Patrick na Babra. Pamela
utabaki na Cris na usiogope wapo watu
watakaokulinda muda wote. Kazi ya kwanza
tufikapo Tanzania ni kuhakikisha nyaraka zote
za kampuni zinarudi kwa Patrick, kisha Mary
atalazimika kubadilisha nyaraka zote majina na
kwenda kwenye jina la awali ambalo ni la
Patrick, mashtaka juu yake yatafunguliwa akiwa
nchini Tanzania na sisi tutawatumia watu wa
kule kupenyeza ushahidi wote ili kesi ifike
mwisho kwa haraka. Tunavyoongea hapa tayari
shehena ya biskut ambayo ilitoka Tanzania
imekamatwa na wameitizama na kugundua
ilikuwa ni pembe za ndovu zimesagwa, polisi
wa kimataifa (Interpol) wanatafuta kampuni
iliyotengeneza ule mzigo na hakuna nakala
inayoonekana toka kwa Mary. Hii inamaana
kuwa tunatakiwa kuwahi haraka kabla
hawajagundua kuhusu Mary na kumtafuta.
Taarifa za uhakika zinasema kiwanda cha
biskuti hizo kimeungua moto jana chote na
haieleweki chanzo cha moto, usajili wake pia
una utata. Sisi ndio tuna ushahidi wa yote na ni
juu yetu kufanikisha mambo kwa wakati. Khajat
dada yangu kipenzi kwasasa punguza jazba,
tuhakikishe tunafanikisha haya yote kisha
mengine yatajipanga yenyewe.” Aliongea Felly
na hapo niliona kabisa nia yake ya kumkimbiza
Mary mbali na mikono yangu lakini mimi
nilielewa njia ya kumpata. Nilichomuahidi ni
lazima akipate. Baada ya maelekezo yale kila
mtu alianza kujitayarisha na mimi niliondoka na
kwenda mjini kisha baada ya muda mfupi
nilikuwa tayari nimerudi.
“Unapeleka wapi jeneza wewe Khajat.” Alikuwa
ni Felly akishangaa baada ya kuona nikishusha
jeneza pale nyumbani.
“Mary atakaa humu kwenye jeneza, piga simu
kwa watu wako waambie watuwekee sehemu
ya kusafirisha maiti.” Niliendelea kulishusha lile
jeneza na kumuomba Babra anisaidie tulipeleke
ndani. Nilipoingia nilikutana uso kwa uso na
Mary aliyekuwa tayari amekwisha zinduka.
Alinitazama na mimi nilimsogelea, alionekana
kuchoka lakini hiyo haikunifanya niache kuwa
ha hasira na yeye. Felly aliingia pale na
aliponiona nimesimama mbele ya Mary alikuja
na kusimama mbele yangu na kuniomba
nijiandae kwanza kuongea na Mary.
Walimuweka Mary vizuri na kisha Felly alianza
kumuongelesha. Muda wote huo nilikuwa bado
nikimtazama kwa hasira usoni na yeye alikuwa
akinitazama pia.
“Mary tunakwenda Tanzania kesho, nia ya
safari ni wewe kwenda kurudisha kila kitu
ulichochukua kwa Patrick, tunataka tumalizane
kwa namna hiyo kwa hatua za awali kabisa
kabla hujalipia machozi na maumivu ya kila
mmoja uliyemsababishia usumbufu.” Aliongea
Felly lakini Mary hakujibu chochote badala yake
alikuwa kimya tu akinitizama mimi.
“Mjibu Felly acha kunitazama.” Nilimuambia
hivyo na Mary hakujibu chochote zaidi ya
kunitazama. Niliondoka pale na kwenda
kuchukua waya ule ambao Babra huutumia,
nikaunyoosha vizuri na kurudi nao pale, Mary
alikuwa bado akinitazama tu.
“Mary, sababu ya mimi kukuacha wewe hai
mpaka sasa ni kwakuwa tu kuna mambo inabidi
utimize kabla sijakuaga rasmi, hatua ya kwanza
katika maisha yako ya mwisho ni kusafiri
kwenye jeneza ukiwa hai, hatua ya pili na ya
mwisho utaijua kadiri muda utakavyotutuma.
Hivyo umeelewa tulichokuambia au unahitaji
maumivu ili kuelewa?” nilimuuliza lakini alizidi
kutoa tabasamu. Felly alinitazama kama vile
akinipa ishara ya kwamba nihangaike naye.
Nilimtoboa mkono na ule waya na yeye alikuwa
kimya huku akiguna kwa maumivu kisha
nilikuwa nikimuuliza huku nikiuingiza ule waya
taratibu kwenye mwili wake, zoezi lile huwa
linachana nyama ndani kwa ndani na
kusababisha maumivu makali sana, niliupeleka
na yeye alianza kulia, nilipoufikisha umbali wa
sentimita 30 alianza kuongea.
“Naumia, niache.” Alilia kwa uchungu, ile
ilikuwa ni adhabu ya kumfanya aongee.
“Nia yangu ni wewe uumie, siko hapa
kukufurahisha.” Nilimwambia huku nikiendelea
kuongea. Patrick alikuwa pembeni akimtazama
kwa hasira na wala hakumsemesha kitu.
“Niko tayari kurudisha, niko tayari, tukifika
Tanzania nitafanya mtakalo.” Aliongea hayo na
alipomaliza kuongea nilichomoa ule waya na
kumchoma sindano ya kumpunguzia maumivu.
Alikuwa ametokwa na jasho kama mtoto
mdogo. Kila nilipomtazama nilitamani
nimkatekate kama kachumbari.

******
Mpaka usiku wa saa 8 wote tulikuwa macho,
muda huo ndio Felly alipigiwa simu kuwa nafasi
ya kuweka maiti haitakuwepo kwakuwa tayari
ndege imeshajaa. Tulichanganyikiwa kwakuwa
ndege ilikuwa iondoke saa 11 asubuhi na
mpaka muda huo hatukujua ni wapi
tutamuweka Mary.
“Piga simu waambie watuongeze nafasi moja
kwenye ile sehemu ya peke yetu, Mary
tutaondoka naye akiwa mzima hivihivi.”
Aliongea Babra na hicho ndicho kitu ambacho
niliona hakitawezekana. Tukimfunga pingu
lazima itakuwa ni tatizo tayari kwenye ndege,
tukisema tumuache atembee na sisi kama
kawaida itakuwa tumemuaga bila ya sisi
kutumia akili.
“Babra haitawezekana, ni bora tutafute namna
nyingine au hata kuahirisha safari ili tupate pa
kumuweka.” Felly alimwambia Babra, lakini hata
hivyo Babra alitikisa kichwa akimaanisha
hatuwezi kuahirisha safari, kisha alitoka pale na
kuondoka, nje tulisikia akiwasha gari na
kuondoka kwa kasi sana. Tulikuwa tumechoka
mpaka muda huo, kila mmoja alikuwa
akitafakari ni nini tutafanya, hatukujua Babra
alikoelekea lakini kwa zaidi ya lisaa limoja
alikuwa bado hajarudi.
“Khajat, mbona naona kama tutashindwa kwa
hili?” aliuliza Felly huku akionekana kukata
tamaa.
“Tumsubiri Babra tuone atakuja na mbinu gani.”
Nilimweleza Felly lakini hakuwa tayari
kunisikiliza kuhusu Babra badala yake alizua
kicheko.
“Babra atakuwa amekwenda kuvuta bangi
labda, ujue anamsongo wa mawazo, baba yake
na mama yake waliuwawa kwa kuchinjwa na
waya toka kipindi akiwa mdogo, alishuhudia lile
tukio, sasa ile picha bado huwa inamuijia
kichwani ndio mana katika miaka yote nimekaa
naye sijawahi kuona akicheka, si muongeaji
sana na hajui kumbembeleza mtu, hana mpenzi
na hata siku moja hamnyenyekei mtu. Sasa
sidhani kama anaweza kuwa na njia yoyote.”
Niliguna kwa yale maelezo, na kabla sijauliza
jambo linalofata alikuwa ameingia pale ndani na
kimfuko. Ni kweli alipoingia nilisikia harufu ya
bangi lakini niliamua kukaa kimya tu.
“Vipi umepata njia gani?” nilimuuliza kwa
haraka lakini alitazama saa yake na muda huo
ilikuwa saa 10 kasoro, alivua nguo pale mbele
ya Patrick na sisi bila aibu, na kuondoka
kwenda bafuni, nilitamani sana kucheka lakini
sikuweza. Hatukufungua ule mfuko tulisubiri
mpaka alipokuja, alipewa nguo zake na Felly
kisha alivaa na kutuambia twende kile chumba
ambapo Mary yupo. Alipofika alimfungua zile
kamba na kumchukua kisha alimpeleka bafuni
na kumsimamia aoge.
“Jamani ni saa 10 inaelekea na nusu sasa,
tujiandaeni kuondoka.” Aliongea Babra na sisi
tulimshangaa, lakini yeye hakuonekana kama
kushangazwa na kutokushangaa kwetu. Ilibidi
Felly amuulize kwa lugha kwa lugha ambayo
hata hivyo mimi sikuifahamu;
“conas is féidir linn taisteal léi gan a bheith faoi
deara.” Aliongea Felly na wakati huo Babra
alikuwa akimsikiliza.
“Tá gach rud faoi smacht, ach fan agus a
fheiceáil.” Alijibu na hapo Felly aliondoka pale,
nilimfata Felly na kumuuliza ni lugha gani ile
waliyokuwa wakiongea na yeye alinijibu kuwa
kilikuwa ni ki ‘Irish’, nikamuuliza nini walikuwa
wakiongea na yeye alinyamaza kidogo na
kunitazama.
“Nilimuuliza tutawezaje kuondoka naye bila
kuleta shida? Na yeye akanijibu kuwa nitulie kila
kitu kitakuwa sawa.” Alinijibu Felly na wakati
huo Babra alikuwa amemtoa Mary bafuni na
kumshikilia akiwa uchi, Mary alikuwa na
michubuko kidogo usoni hivyo alimfuta akiwa
amemfunga pingu na kumpaka poda na sasa
alionekana vizuri, tulishangaa kuona akimlaza
Mary pale kitandani na kumfunga mikono huku
na huku na miguu yake pia akaitanua. Mary
aliogopa ni nini alikuwa anafanyiwa, wote
tulibaki midomo wazi, Babra aliondoka pale na
kuchukua ule mfuko aliokuja nao, alimtizama
Mary akiwa katika ile hali ya kupanua miguu
kitu kilichofanya sehemu zake za siri kuwa nje,
alifungua ule mfuko na kuchomoa bomu dogo la
saizi ya mwisho kama kiazi na kulipaka mafuta
kisha alichomoa kipini chake na hapo Felly
alishtuka, Mary alikuwa anatoaka machozi na
alishindwa hata kuongea.
“Babra unafanyaje?” Felly alimuuliza lakini
Babra hakujibu, alimtanua Mary na kuanza
kuliingiza lile bomu taratibu, Mary alipiga kelele
sana lakini Babra hakujali wala kuongea kitu
chochote, alitoa kitu kama uume mmdogo wa
plastiki na kuutumia kusukumiza lile bomu
mpaka alipohakikisha na ule uume umezama
wote, Mary aliendelea kulia na baada ya hapo
Babra alinyanyuka na kumuinua na kuchomoa
ule uume wa plastiki lakini lile bomu lilibakia
ndani.
“Hutapata maumivu yoyote, hilo bomu
limekwenda kukaa kwenye mfuko wa uzazi,
rimoti yake mimi ndio ninayo, hivyo hakuna
atakayekushika wala kukufunga wakati wote
tutakapokuwa safarini kuelekea Tanzania na
hata tutakapofika Tanzania, ila ukijaribu
kuondoka mbele ya uso wangu jua wewe ni
bomu na utalipuka.” Alimaliza kuongea Babra
na Mary alionekana kukubali kushindwa.
Tulikwenda uwanja wa ndege na Mary akiwa
hajafungwa kamba wala pingu, alikuwa na
nidhamu sana, hatukuwa na bastola kwakuwa
hazikuruhusiwa na hasa kwamba tulikuwa
tunasafiri kama watu wa kawaida. Lakini cha
kushangaza tulipofika ndani ya ndege Babra
alitoa vichumachuma vingi kwenye kiatu na
sehemu nyingine za mwili akaviunganisha na
ikatokea bastola, hiyo ilinikumbusha mafunzo
tuliyopewaga kipindi nikiwa jeshini ya namna ya
kuunganisha silaha.
*****
Safari iliyoanza pale Fiji ilitufikisha mpaka Misri
ambapo tulishuka ili kubadilisha ndege. Tafrani
ilianzia pale ambapo baada tu ya kushuka
tuliona watu ambao hatukuwaelewa. Mary
alikuwa bado akionekana kufadhaika sana na
muda wote ule alikuwa akimwangalia Babra.
Nilikuwa makini sana na mimi kumtazama ili
asiondoke mbele ya macho yangu. Wale watu
walikuwa ni wanaume wawili ambao niliwaona.
Walikuwa na asili ya kiarabu na wengine wengi
tu kama sita walikuwa wametapakaa kila kona
ya pale uwanja wa ndege.
“Felly mnaona lakini hapa kuna dalili
nisiyoielewa?” nilimuuliza Felly na yeye
alitazama na kugundua kweli kulikuwa na shida
pale.
“Babra, hawa watu lazima watakuwa na
uhusiano na Mary sasa lazima tujipange vizuri
hapa, kuna uwezekano kabisa kwamba kipo
kilichofanyika kinachoweza kuwa kimewapa
watu wa Mary taarifa. Hapa tusipokuwa makini
tutapotezwa.” Felly alimnong’oneza Babra na
hapo walinichukua na wote tukaenda kwa
pembeni na kumuacha Mary akiwa pale kwenye
viti amekaa kimya. Hakuwa amefungwa popote
lakini lile bomu alililoingiziwa ndani ya mwili
wake ndilo lililomfanya akae kama vile
amefungwa pingu.
“Kila mtu achukue nafasi yake hapa. Hawa
watu hawawezi kufyatua risasi hapa uwanjani,
tumeowaona walipo, hivyo hakikisha kila mtu
anakamata wake kwa kadiri awezavyo. Felly
unakwenda upande wa kulia wa uwanja huu,
Khajat wewe utakwenda upande wa kushoto,
mimi nitakuwa mbele pale. Utaratibu wa hapa
utatofautiana sana na sehemu nyingine zenye
kificho. Hapa ni kimyakimya. Hivyo nashauri ni
bora kutumia waya zaidi kuliko kisu au silaha
nyingine za moto. Hakikisha mtu anakuwa
mbele yako akiwa na yeye anaangalia mbele,
kisha unamuwahi na kumvisha waya na
unavuta kwa nguvu zote ili umnyonge, kisha
akiishiwa nguvu unaivuta waya na mkono
mmoja huku upande mwingine umeachia na hii
itakata shingo bila wasiwasi. Weka mwili
sehemu ambayo haitakuwa na matatizo kwa
muda huu. Kaeni mbali na kamera za uwanja
huu. Kama ukishinda kutumia waya basi tumia
mkono, piga ngumi moja tu itakayomzimisha
mtu ili kusiwe na purukushani zisizo za lazima.”
Aliongea Babra na kutoa waya tatu mfukoni
kisha akatupatia lakini mimi nilimrudishia
kwakuwa niliuamini zaidi mkono wangu, Felly
yeye pia alirudisha na alitaka kutumia zaidi
mkono wake.
“Khe!” nilisikia Babra akishangaa baada ya yeye
kugeuka.
“Mary hayupo pale.” Alitueleza hivyo na tayari
nafsi yangu ilianza kusikia joto tena. Hayupo?!
Nilijiuliza moyoni lakini ukweli ni kwamba Mary
hakuwepo pale na nilipotazama kwa mbali
niliona akitokomea na vijana wawili waliovalia
nguo za kiaskari.
ITAENDELEA
 
RIWAYA: KISASI
MTUNZI: FRANK MUSHI
SEHEMU YA MWISHO -PART 1
“Usilale kwa kujiachia kama bado mafanikio
yanakukimbia. Amka panga namna ya
kuyakabili matatizo yako kwakuwa matatizo
yameshapanga namna ya kukukabili. Amka na
ujiulize utalala mpaka lini na kuamka ukiwa na
hali ile ile na mawazo yaleyale? Jiulize
ulivyokuwa mwaka jana na ulivyo mwaka huu.
Je kwanini hamna tofauti ya mafanikio yako
wakati kuna ongezeko la umri??? GUNDUA
KIPAJI CHAKO…KITUMIE…ELIMU YAKO SI KITU
KAMA ITASHINDWA KUKUTATULIA
CHANGAMOTO ULIZONAZO.”

**BABRA**
Tulikaa pale tukitafakari na kila mtu akiwa
amepigwa na butwaa juu ya kilichotokea,
nikakumbuka juu ya ile rimoti niliyokuwa nayo
ambayo hata hivyo nisingeweza kuitumia pale
kwenye eneo lenye watu wengi. Tulisogea
kando zaidi na tulipogeuka tena nyuma tuliona
polisi watatu wakija upande wetu na sisi
tuliondoka pale na kuanza kutembea haraka
kule mbali na uwanja. Tulipofika mbali kidogo
na pale watu walipokuwepo walituambia wao ni
maafisa wa polisi na kutuamuru tusimame.
Tukasimama na kugeuka, wale ndio tuliowaona
mara ya kwanza pale uwanjani wakiwa
wamevaa nguo za kiraia.
“Nyoosha mikono juu.” Aliongea yule askari
mmoja kwa lugha ya kingereza. Wale wawili
nao walikuja na kuanza kutupekua. Walinikuta
na ile Rimoti na hapo wote walicheka na
kutuambia tulale chini. Wakati tunalala chini
nilimuona Khajat akitutazama kisha alitupa
ishara kwamba tuwarukie wale jamaa ili
kuwadondosha. Kila mmoja alianza kuhesabu
ndani yake moja mpaka tatu kisha tuliwavamia
kwa kasi na kuanguka nao. Hapakuwa na mtu
aliyetuona kwakuwa pale ilikuwa ni mbali
kidogo na uwanja. Tulizungushana nao pale
lakini baada ya kuwapiga sana walilegea. Yule
mmoja aliyekuwa na Khajat alikuwa
ameshauwawa kwa kuvunjwa shingo. Walibaki
wawili na Felly alimnyonga mmoja na kusema
tunayemuhitaji pale ni mmoja tu. Tulimuweka
sana yule jamaa na hapo Khajat alianza
kumuhoji.
“Mko wa ngapi na Mary yuko wapi?” aliuliza
Khajat lakini yule jamaa hakujibu kitu.
Alimuuliza kwa mara ya pili na ya tatu lakini
yule jamaa alikuwa bado tu yupo kimya.
Kilichofata Khajat alichukua ule waya na kuanza
kuuingiza puani kwa yule jamaa.
Aliuchomekana kwa nguvu mpaka damu
zilianza kutoka na yule jamaa aliongea.
“Tuko tisa, watatu ni sisi na wengine sita wako
na Mary kwenye gari ndio wanasubiri tupeleke
rimoti.” Aliongea kwa sauti ya kulia yenye
maumivu ndani yake. Alipomaliza tu kuongea
simu yake ya mkononi iliita, na hapo ndipo
Khajat alipomuonya kuwa akitoa ishara yoyote
ya kwamba amekamatwa atamuua palepale.
“Kama unataka kufa kikatili basi jaribu
kuonyesha hata ishara. Ongea kwa ukakamavu.
Mwambie upo huku ili wakufate na mwambie
kuwa umemkamata mmoja na wengine
wamekimbia.” Alipewa maelekezo hayo na yeye
alisema kama alivyokuwa ameambiwa. Mimi na
Felly tulikuwa tumeondoka na kwenda kukaa
pembeni ya pale tulipokuwa kwa muda ule,
tukajificha vizuri na muda kama wa dakika mbili
tuliona gari nyeusi ikija kwa kasi upande ule.
Yule jamaa alikuwa amemshikia Khajat bastola
kwa nyuma na ile miili mingine ya wale wawili
tulikuwa tumeificha. Ile gari ilipofika walishuka
wale vijana sita na kwenda moja kwa moja pale
aliposhikiliwa Khajat, taratibu mimi na Felly
tulinyata na kulisogelea gari na kufungua
mlango kwa haraka tukakutana na Mary, kabla
hajaongea kitu Felly alikuwa ameshamuwahi na
kumziba mdomo. Kule Khajat likuwa
ameshawabadilikia wale wengine sita na mimi
nilikwenda kuongeza nguvu. Tulifanikiwa japo
kwa tabu sana kuwakabili na kuwaondoa
duniani kisha muda huo ndege tuliyokuwa
tuondoke nayo ndio ilikuwa inatuhitaji ndani.
Tulimchukua Mary na kuondoka mpaka kwenye
ndege bila ya kushtukiwa kuwa kulikuwa na
tukio limefanyika. Tulipofika ndani ya ndege
nilikuwa namtazama Mary kama nilitaka
kumng’ata, alikuwa amenichefua sana na
nilianza kumchukia kwa moyo wote. Nilitamani
yeye ndiye awe aliyemuua baba yangu lakini
haikuwa hivyo.
Kina Felly hawakujua kwanini niliwasaidia kwa
moyo wote. Hawakujua kuwa nilikuwa
nawekeza kwao ili waje kunisaidia katika
mipango yangu ya baadaye. Mpango ambao ni
siri ndani ya moyo wangu, mpango niliouota
kwa muda na kujipanga juu yake kwa zaidi ya
miaka ya nusu ya uhai wangu. Nilikuwa
nimeng’ata meno nikitafakari kwanini Mary
alitaka kumaliza kila kila mtu aliyejitokeza
mbele yake. Nikamwangalia kwa makini sana
lakini aliamua kunitazama pia usoni, alikuwa
haamini ni kwa namna gani ameweza kuzipita
mashine zote za viwanja vya ndege bila
kujulikana kuwa alikuwa na bomu ndani yake.
Hakuna aliyejua, ni mimi tu, ni mimi na mimi
pekee.
Niliamini kila binadamu alikuwa na sababu ya
kumfanya awe vile alivyo, lakini nilitamani zaidi
kujua kwanini Mary alikuwa vile alivyo. Historia
ya maisha yangu ilinichukua na kunifinyanga
ikanifanya kuwa mtu mpya kabisa katika jamii
ya wasio nijua. Nilibadilika kabisa na kuwa mtu
wa kuua na kufanya unyama, lakini huyu Mary
ambaye nimemfahamu kwa muda mfupi tu si
muuaji kama mimi ila ni zaidi ya hivyo.
Msichana mdogo mwenye matukio ya kigaidi,
alikuwa ni mkavu wa macho na fikra na hicho
ndicho kilichonifanya nimuoene kama asiye na
cha kupoteza.
“Mary uko kwenye siku za mwisho kabisa za
uhai wako, unaweza kuelezea historia ya
maisha yako japo tukakuheshimu kwa hilo.”
Nilimsemesha Mary ambaye alikuwa amekaa
pembeni yangu huku jasho dogo likimtoka.
Hakuongea chochote kile bali alinitazama tu
kwa macho yaliyoonyesha kuwa angekuwa na
uwezo wa kunifanya chochote basi pengine
angenigeuza kibiriti. Hakusema chochote kabisa
na mimi nilimuonea huruma nikaamua
kumuacha asiongee chochote.

******
Ilikuwa ni safari ndefu na yenye vikwazo vingi
lakini hatimaye tulifanikiwa kutua uwanja wa
ndege wa Mwalimu Nyerere, ilikuwa ni mara ya
kwanza kukanyaga Tanzania na maelekezo yote
tulitegemea kuyapata toka kwa Patrick na Mary
lakini zaidi mambo ya kiintelijensia tulitegemea
kuyapata toka kwa watu wangu ambao
walikuwa tanzania.
“uvítací” (karibuni) ilikuwa sauti ya Marcus
Diero, kijana wa ubalozi wa Slovakia, alikuwa ni
rafiki yangu wa siku nyingi ambaye nilikutana
naye nchini marekani kwenye mazoezi ya jeshi
la majini yaliyokuwa yakiendeshwa na jeshi la
marekani. Alikuwa ni mpelelezi wa ujasusi wa
Slovakia lakini pia kulikuwa na tetesi kuwa
alichukuliwa na shirika la kijasusi la marekani.
“v&#271;aka”(asante)
“zariadil som všetko, &#269;o pre vás, ako dlho bude
u zostanem tu” (nimewaandalia kila kitu, na je
mtakaa hapa kwa muda gani)
“tak dlho, ako je potreba”(kwa muda wowote
ikaochukua). Tuliondoka na Marcus mpaka
kwenye nyumba moja iliyokuwa kando kidogo
ya mji. Ilikuwa ni nyumba iliyojitenga kidogo na
makazi ya watu na hapo tulikuwa na uhakika
kabisa wa kila kitu kwenda kama
kilivyopangwa. Baada ya kutufikisha yeye
aliondoka na sasa mwenyeji wa kila kitu chetu
alikuwa ni Mary na Patrick, ilikuwa ni usiku wa
saa sita na hatukuwa na muda wa kufanya
lolote zaidi ya kukaa na Mary ili atueleze
tunaanzia wapi na kuishia wapi.
“Mary tuna masaa 72 tu ya kumaliza kila kitu,
tunataka kujua tunaanzaia wapi na tunaishia
wapi.” Khajat alimuuliza Mary huku akimtazama
kwa macho makali. Mary hakuonekana kuogopa
kitu, alikuwa amechoka lakini bado asili ya
kiburi chake ilikuwa imeujaza moyo wake.
“Sijui pa kuanzia, nyie ndio mniambie.” Aliongea
hayo na kunyanyuka huku akitembeatembea
pale ndani. Khajat alimfata na kumpiga kibao
kilichomfanya apepesuke na kuanguka chini,
damu zikaanza kumtoka puani na na Khajat
akamnyanyua kwa roho ya kikatili kisha
akamkalisha kwenye kochi.
“Mary tunataka hati za vitu vya Patrick,
tunataka kila ulichochukua kwa Patrick
kirudishwe kwake”. Aliongea Khajat kwa upole,
wakati huo Patrick alikuwa ameketi kwa mbali
huku akimtazama Mary kwa huruma.
“Naombeni niongee nae labda atanisikiliza.”
Aliongea Patrick kwa upole na unyonge kisha
Khajat alimuacha na hapo Patrick alijisogeza
mpaka pale na kuanza kumfuta zile damu
puani. Mary alianza kulia kwa kwikwi na kuanza
kumtazama Patrick huku akimuomba msamaha,
ghafla wote tulijawa na huruma.
“Nisamehe Patrick”. Aliongea Mary huku
machozi yakizidi kumtoka.
“Nini kimekutokea Mary.” Patrick alimuuliza
Mary.
“Hakuna kilichonitokea ila hukunijua kabla.”
Aliongea Mary lakini wakati bado akiendelea
kuongea pale, simu ya mkononi ya Patrick iliita,
namba ya simu ilionyesha kuwa ilikuwa ni
namba ya simu ya Tanzania, kitu cha
kushangaza ni nani alikuwa anapiga wakati
namba ile ni mpya kabisa na Patrick alinunua
line yake tuliposhuka tu pale uwanja wa ndege.
Khajat aliichukua ile simu na kuileta pale
alipokuwa Patrick, alipoipokea tu sauti
ikasikika.
“Muachieni Mary, nawapa nusu saa vinginevyo
Pamela na mwanae watakufa.” Aliongea yule
mwanaume aliyesikika upande wa pili wa simu.
Mary alishtuka haraka na kunyanyuka, kuja
mpaka pale na kisha alimnyang’anya Patrick ile
simu.
“We ninani unayetaka mimi niachiliwe?”
aliongea Mary na hapo sauti ya upande wa pili
ilisikika ikicheka kwa muda kidogo kisha Mary
alikata simu. Haikuchukua muda simu nyingine
ya iliingia na hapo ilikuwa ni namba ya Pamela.
“Patrick, Patrick wamemchukua mtoto wetu.”
Sauti ya Pamela ilisikika ikiita huku akilia kwa
sauti ya juu. Wote tulijiuliza ni wapi Pamela
alitoa ile namba ya Patrick lakini hatukujua,
kabla Patrick hajaongea kitu ilisikika sauti ya
mwanaume mwingine kwenye ile simu
akiongea.
“Do as u were told and your family will be
safe.” (fanya kama mlivyoambiwa na familia
yako itakuwa salama).

ITAENDELEAAAAA
 
RIWAYA: KISASI
MTUNZI: FRANK MUSHI
SEHEMU YA MWISHO PART 02
“Kuna sababu ya kila kitu kinachotokea kwenye
maisha yako, ingawaje kuna muda kwa upeo
wa fikra zetu au kwa ukungu wa uelewa wetu
mdogo, tunajikuta tukilaani kutokea kwa kitu
hata kama sababu yake inakuwa yenye
manufaa kwetu. Upendo wetu juu ya wengine
hutufumba macho na kutufanya tusahau kuwa
tuna jukumu la kujitazama wenyewe pia pale
wengine wanaposhindwa kujali hisia na machozi
yetu.”
**MARY**
“Sikuamini kama siku moja ningekuja kuishia
hivi. Sikuwahi kufikiri maisha yangu yangekuja
kuwa ya namna hii. Ndoto zangu zilikuwa ni
kufikia sehemu ambayo ningeweza kuionyesha
dunia kuwa kuna wanawake wanaoweza
kufanya mambo yakatokea. Nilitaka kuonyesha
kuwa ndoto ya mtu yeyote ile inaweza
kutimizwa katika namna ambayo yeye
mwenyewe ataamua.” Nilimtazama Patrick na
kusikia machozi yakianza kunitoka tena. Ni
kwasababu yangu leo hii Patrick anataabika na
dunia. Kwa mara ya kwanza kwenye maisha
yangu nilimuonea huruma mwanaume.
“Nisamehe Patrick.” Nilizidi kumsihi lakini
haikusaidia, mwili wangu ulikuwa ukivuja damu,
Patrick alikuwa bado amenishikilia huku akilia
kwa uchungu, nilipomtazama usoni niliona
kabisa kuwa aliumizwa na ile hali yangu.
“Usiondoke Mary, usiondoke tafadhali.” Alizidi
kulia kwa uchungu na mimi sikuweza tena
kujizuia, nilizidi kulia. Picha ile ilinipeleka nyuma
kabisa kipindi ninakutana na Patrick kwa mara
ya kwanza. Nilikuwa nina hisia naye lakini
ndoto na mipango yangu haikuzipa hisia za
mwili wangu nafasi ya kusema akili yangu.
Nilikuwa bado nikitazama juu wakati Patrick
amenibeba na kunirudisha ndani. Haikujulikana
popote ile risasi imetokea wapi, Felly alichukua
vitambaa na kisu na kuja mpaka pale nilipo
kisha aliniweka sana na kuniwekea kipande
kidogo cha mti mdomoni ili aweze kunitoa ile
risasi iliyopiga ubavuni mwangu. Nilisikia
uchungu sana lakini hakukuwa na namna
nyingine ya kufanya zaidi ya kukubali maumivu
yale yakae ndani mishipa yangu ya damu.
Muda wote huo Patrick alikuwa pale pembeni
huku jasho likimtoka. Zoezi lile liliendelea kwa
muda wa dakika kumi na lilimalizika salama
kisha nilifungwa vizuri na ile damu ilikatika.
“Mary, nahitaji kujua kila kitu sasa.” Aliongea
Patrick huku akionekana kuchoka na kila
kilichokuwa kikiendelea pale.
“Nipe simu kwanza.” Nilimuomba simu yake ya
mkononi na hapo alinipatia kisha nilimuomba
apige simu ya mkewe, baada ya sekunde
kadhaa sauti ya mwanaume ilisikika kwenye ile
simu. Hakuwa Pamela tena alikuwa ni yule
mwanaume aliyeteka familia ya Pamela.
“Rajan waachie huru.” Nilimpa maelekezo yule
kijana aliyekuwa upande wa pili na yeye aliitikia
kisha nikakata simu. Felly alikuja mpaka pale
na kuchukua ile simu kisha alipiga tena na
muda sio mrefu niliona akirudi pale na
kumwambia Patrick kuwa mambo
yameshakuwa sawa.
“Mary, nini kimekutokea?” Aliuliza Patrick tena.
“Patrick, mimi nilizaliwa miaka 30 iliyopita…”
Nilianza kumuhadithia Patrick na wale wengine
waliokuwa pale lakini nilikatishwa na sauti ya
Patrick.
“Miaka 30?” Aliuliza kwa mshangao, nilijua
kuwa Patrick hakuwahi kuujua umri wangu
sahihi kwakuwa nilimficha.
“Ndio, nina miaka 30, nilipokuwa na miaka
mitano, nilishuhudia baba yangu akimuua mama
yangu kwa mziba pumzi kwa mto, ni ugomvi
wao wa siku nyingi ndio uliopelekea yote hayo.
Ile picha ilikuwa ikinirudia sana nilipofika umri
wa miaka saba nilimuua baba yangu. Hakuna
aliyefahamu juu ya hilo, kila mtu alidhani ni kifo
cha kawaida tu. Tangu kipindi kile nilivaa roho
ya kinyama. Nilichukuliwa na baba yangu
mdogo na kwenda kuishi naye nchini Marekani,
yeye hakuwa na mke, hakuwa na mtoto hivyo
tuliishi mimi na yeye tu huko Tobargo, nilikuwa
nikienda shule kama kawaida na jirani yetu
kulikuwa na kambi ya jeshi, nilikuwa nikipenda
sana kwenda pale na kuna baadhi ya vijana
nilizoeana nao na hapo nikaanza kuwa nafanya
mazoezi ya wasichana wadogo waliokuwa
kwenye ile kambi. Walinipenda kwakuwa
nilikuwa mwepesi na msikivu. Nikiwa kule
nilibahatika kukutana pia na baba yangu
mkubwa aliyekuwa akiishi Los Angelos.
Mambo hayakuwa mazuri nilipofika miaka 12
kwakuwa baba yangu mdogo alianza kuniingilia
kimwili wakati nikiwa nimelala na muda
mwingine hata kuninyesha pombe na kuniingilia,
hiyo iliniharibu sana lakini, nilikuwa nikitafuta
namna ya kufanya. Miezi sita baada ya
kutimiza miaka 12 ndiyo nilirudi tena Tanzania
nikiwa na baba yangu mdogo, sikujua kuwa
alikuwa na mke wake huku Tanzania. Tulipofika
ndio nilikuja kujuana na mdogo wako Mark.
Tulikuwa marafiki sana na kutaniana kwetu
kulifanya tuwe kama wapenzi watoto.
Wengi walidhani kuwa nilikuwa mtoto wa yule
mama, lakini haikuwa hivyo. Mwanae alikuwa
sehemu nyingine kabisa. Kipindi nikiwa na yule
mama nchini Tanzania, alikuwa akinitesa na
sikuwa na jinsi zaidi ya kuamua kumuwekea
sumu kwenye chakula na ndipo alipokufa na
wengi walijua kuwa yule mwanamke alijiua.
Tulirudi tena Marekani na huko niliendelea na
maisha yangu, lakini kipindi hiki sikuwa
nikisoma tena, nilitoroka kwa baba mdogo na
kwenda kuishi na mtu mwingine aliyekuwa
mwanajeshi wa Marekani. Nia yangu kubwa
ilikuwa ni kujifunza mambo ya kijeshi, huko
nikajiunga na shule ya Lee Hyun aliyekuwa
mwalimu wa mchezo wa Karate, nikafudhu na
kumaliza mikanda yote. Sikujua ni nini nilikuwa
nikiwaza, nilipofika miaka 16 nilianza kusihi
kinyumba na Peterson Anglimayo, huyu alikuwa
ni muuza madawa ya kulevya aliyekuwa akiishi
Toronto, nilifoji vyeti vyangu vya kuzaliwa na
miaka yangu ilionekana kuwa mbele zaidi hivyo
alinioa japo nilionekana kuwa na mwili mdogo,
mwaka mmoja mbele nilimuua Peterson na
kufanikiwa kurithi akaunti yake iliyokuwa na
dola milioni tano. Nilikutana na Hasheem Feisal
ambaye alikuwa ni rafiki wa Peterson na ndiye
aliyeanza kunifundisha mambo yote, nilienda
Urusi na kuanzisha kampuni iliyokuwa ni kivuli
tu lakini ilikuwa njia ya kuficha yetu ya biashara
ya madawa ya kulevya.
Nilirudi kwa baba yangu mdogo tena na
kumuomba msamaha lakini alinielewa ila
aliharibu pale aliponitaka tena kimapenzi na
hapo ndipo nilipouondoa uhai wake. Nilirudi
Tanzania na kufikia kwa baba yangu mkubwa
ambaye ndiye mliyekuwa mkiishi naye karibu
pia. Lakini kipindi hicho nilipata tenda ya
kupeleka pembe za ndovu nchini Australia na
kwingine.
Wakati huo wote jina langu lilikuwa likitokea
kwenye mitandao mingi ya vyuo vikuu kama
muhitimu na msomi mahiri, mfano Shahada ya
mfumo wa mawasiliano niliyopata Altai nchini
Urusi haikuwa ya kweli bali ya kutengeneza,
shahada ya utawala wa biashara niliyopata
Limkokwing haikuwa ya kweli bali ni ya
kughushi japo kweli nipo kwenye majina ya
wahitimu, shahada ya Bradford ni ya kweli
niliisoma mtandaoni. Ni kweli niliajiriwa kwa
miezi michache kama Mpelelezi kwenye shule
ya jeshi nchini Uingereza, nilikuwa nina uraia
wa Uingereza na wa Marekani, shahada ya
Uandishi ni ya kweli nayo nilisoma mtandaoni
na niliipata Lesotho.
Katika maisha yangu baada ya ndoa yangu ile
ya kwanza, nilikuja kufunga ndoa na Fransisco
Domosco huko Alaska, alikuwa ni tajiri, na mimi
nia yangu ilikuwa ni kuja kuwa mwanamke
mwenye mali nyingi za kutosha, miezi sita
baadaye Fransisco aliandika wosia na siku mbili
mbele alipata ajali niliyoitengeneza, alifariki na
nilibahatika kuchukua asilimia 40 ya mali yake
yote. Nilifungua kampuni Msumbiji na nchi
nyingine na wakati huo bado nilikuwa na nina
ndoto za kuwa tajiri kuliko nilivyokuwa wakati
huo. Sikuwa na mapenzi na yeyote, sikuwa na
mzazi wa kumfikiria, nilitazama jinsi watu
walivyoishi kiumasikini nikaona sitaweza kuwa
hivyo, nilijua niko duniani kwaajili ya
kuhakikisha namiliki kila kitu kilicholetwa hapa
duniani. Nilijifunza kuwa ili uwe na uwezo wa
kutosha lazima uwe na roho mbaya. Niliamini
wanaume ni watu ambao kama hutawawahi
wao, basi ipo siku watakuwahi na itakuwa ndio
mwisho wako. Kilichomtokea mama yangu
sikutaka kinitokee mimi, sikutaka kuja
kumnyenyekea mwanaume katika maisha
yangu, nilitaka kutengeneza msingi bora wa
maisha yangu ili nije kuingia kwenye orodha ya
wanawake tajiri duniani.
Nilikuja kuolewa mda mfupi mbeleni na Timoth
Mobutu aliyekuwa mfanyabiashara wa madini
huko Afrika ya kusini, lakini pia nilimuua baada
ya kuhakikisha kuwa kila kitu chake nilijua
kilipokuwa. Hayo ndiyo yalikuwa maisha yangu.
Lakini nilipofika Tanzania tena na kukukuta
nilitokea kuvutiwa na wewe, lakini nilijizuia
kwakuwa nilikuwa na lengo la kutimiza, ni kweli
nilianzisha kampuni nyingine lakini nia yangu ni
kujenga mtazamo wako juu yangu. Hukuwa
tajiri sana hata kunifikia mpaka kwa wakati huo,
lakini tamaa yangu haikuwa na kipimo maalum,
kila kitu kwangu kilichoongeza hata shilingi 50
kwenye mabilioni niliyokuwa nayo kilikuwa ni
muhim. Nilimshirikisha mdogo wako ambaye
naye alionekana kuzimendea mali zako mda
mrefu sana, japo tulifanikiwa na kuwa pamoja
baada ya wewe kuaminika kuwa umekufa lakini
Mark alikuwa mwenye papara, sikuzaa na Mark,
nisingeweza kuzaa naye kwakuwa alikuwa ni
mdogo wako. Mark hajawahi kufanya mapenzi
na mimi. Ni vigumu kuamini lakini huo ndio
ukweli, hata kifo cha Mark kilitokana na
kung’ang’ania vitu nisivyovitaka. Nilijifanya
kuwa mjamzito lakini sikuwa hivyo, mtoto
niliyekuwa naye nilimnunua kwa mtu tu
aliyemuiba toka hospitalini, nia ilikuwa ni
kuficha kila kitu nilichokuwa nikikifanya. Dany
alikuja kwenye mchakato huu baada ya mimi
kuwa na nia ya kufungwa ndoa na wewe, mama
yake na Mark pia alikuwa ndani ya mpango
huo, lakini siku zote faida ndogo haiwezi kuliwa
na walio wengi. Walikufa wote.” Haikuwa
historia nzuri sana kuhadithia lakini sikuwa na
jinsi zaidi ya kumueleza Patrick kila kitu.
Isingeweza kumsaidia chochote lakini ilitosha
kumueleza na kumuondolea maswali mengi
sana aliyokuwa nayo.
Nilimtazama Patrick nikazidi kumuonea huruma,
sikujuta kwa kumuingiza kwenye haya matatizo
yote, lakini kwa mara ya kwanza kwenye
maisha yangu nilipata hisia ambazo sikutaka
kuzizuia juu yake. Nilitamani muda urudi nyuma
nipewe nafasi ya ku kusahihisha makosa yangu
lakini hakukuwa na muda huo. Pale utendapo
kosa ndipo muda wa marekebisho huishapo,
muda wa majuto huja mbele kama matokeo ya
uvivu wako wa kufikiri kutenda mema katika
muda ambao nilikuwa nao. Sikuwa tu nikilipa
kisasi kwa yale niliyokuwa yametokea katika
udogo wangu bali nilikuwa nikitengeneza
misingi imara ya furaha yangu mwenyewe.
Sikufahamu Patrick alipanga kunifanya nini
lakini nilikuwa niko tayari sasa kwa lolote
alilotaka kunifanya. Lile bomu waliloniwekea
lilikuwa likinipa maumivu makali ya tumbo
lakini sikuwa na jinsi. Nimekuwa katili kwa
miaka mingi ya maisha yangu na nimekutana
na watu wengi makatili lakini sikuwahi
kukutana na mtu katili kama Khajat. Kila mtu
anajua kwanini yuko vile alivyo.
“Kwanini ulinichagua mimi Mary, kwanini
usingeniacha niishi maisha yangu tu, kwanini
Mary.” Alizidi kuongea Patrick huku akilia, hapo
alinifanya nizidi kusikia uchungu ndani ya moyo
wangu. Sikuwa na jibu la swali lake,
nilimchagua yeye kwakuwa alikuwa ndiye pekee
ambaye alikuwa anaweza kuzoeleka haraka.
******
Kesho yake asubuhi nikiwa bado sijapelekwa
hospitali nilichukuliwa na Patrick na kuingizwa
kwenye gari ambapo walikuwa pia kina Khajat.
“Hati za mali zangu ziko wapi?” Aliongea
Patrick ambaye alionekana kama amebadilika.
Nilinyamaza kidogo nikitafakari juu ya
kubadilika kwake ghafla lakini nilishtuliwa na
mdomo wa bastola uliokuwa mbele ya paji
langu la uso.
“Sitauliza mara ya pili.” Aliongea hayo na hapo
ndipo nilipomjibu.
“Zipo Mkuranga, kuna sehemu niliweka kila kitu
changu.” Nilimjibu na hapo bado aliendelea
kuninyooshea ile bastola.
“Na huyo aliyeenda kuteka familia yangu ni
nani?” aliuliza kwa hasira.
“Ni mtu ambaye aliwekwa anifatilie nyendo
zangu.” Nilimjibu lakini sikutamani aniulize
swali la pili.
“Aliwekwa na nani.” Aliuliza swali ambalo
sikutaka kabisa aniulize kwakuwa sikuwa tayari
kumjibu. Ingemuumiza au kuona kama mimi ni
mpuuzi zaidi ya alivyokuwa akifikiria sasa hivi.
“Mume wangu.” Nilimjibu kwa kifupi huku
nikiangalia chini, hasira zilinijaa kwakuwa mtu
wa mwisho ambaye nilipanga kuja kumuua kwa
mikono yangu ni Idrisa Eljabr. Alikuwa ni tajiri
wa kiarabu mwenye visima vya mafuta huko
Oman, alinioa kwa ndoa ya lazima na sikuwa na
jinsi, akanifanya mtumwa mpaka pale
nilipoamua kutoroka kwake lakini bado alikuwa
akinisaka kila kona. Nilimuahidi kifo na kama
ningepata nafasi ya kurudi tena kwake basi
ningeweza kumfanya kitu ambacho kingebeba
maumivu ya kila mpuuzi mwenzake aliyewahi
kupata maumivu.
“Una mume tena?” aliuliza kwa mshangao na
hata hivyo sikuwa na la kumjibu, aliwasha gari
kwa kasi na safari ya kuelekea Mkuranga
ilianza. Hakuna aliyeweza kuniuliza chochote au
kuongelea yale niliyokuwa nimehadithia jana
yake. Tulitumia masaa kadhaa na baadaye
tulishuka kwenye shamba kubwa lenye vichaka
na kuanza kuingia ndani kwa mguu. Mpaka
katikati ya lile shamba kulikuwa na kaburi,
hakuwa amezikwa mtu, tulilifukua kwa muda
wa nusu saa, na ndipo tulipokutana na sanduku
lililokuwa na zile hati za kila kitu. Nilitoa na
kumkabidhi Patrick, nilikuwa na moyo mweupe
na nilihisi kupunguza mzigo ndani ya moyo
wangu. Baada ya Patrick kuhakikisha amepata
kila kitu aliniingiza ndani ya gari na tukarudi
mpaka Dar. Usiku wa ile siku nilitolewa lile
bomu kwa mkono. Yalikuwa maumivu makali
makali ambayo sikuyategemea. Siku mbili
mbele nikafunguliwa kesi ya mauaji na makosa
mengine kama 9 hivi. Kesi yangu ilienda kwa
muda wa miaka miwili na kwa muda wote huo
sikuwahi kuona Patrick, nilihukumiwa kifungo
cha maisha jela na sikuwahi kumuona yeyote
aliyekuja kunitembelea.

ITAENDELEA
 
Back
Top Bottom