RIWAYA: Kikosi cha Pili

RIWAYA: Kikosi cha Pili

[HASHTAG]#Moneytalk[/HASHTAG],kingongoi,billduke,maga junior,bright platnumz,wolf man,popular famous,kiker,i keep ma promise,Emmanuel nemes,donlucchese,shunie,Tumosa,sirbuff,Maxmizer,Nelson nely,Nassib nyika,kichwa kikubwa,#
Nipo mkuu utamu umekolea
 
Hongera kazi nzuri inaeleweka ila usitusahau sana kwa muendelezo
 
Sehemu ya 12*

Wakati vikosi vya askari polisi vikizidi kuweka ulinzi sehemu mbalimbali ili kuhakikisha Zedi Wimba anaingia mikononi mwao,ni wakati huhuo Zedi alikuwa kawapiga chenga ya akili na mwili,.

Baada ya kuchepuka na kuwatoroka askari lengo lake lilifanikiwa na akajikuta yupo Dodoma mjini,pasipo kusubiri akapaki gari lake kwenye gereji ya champion kisha akachukua daladala hadi uwanja wa ndege wa Dodoma,hapo akajitbulisha kwa jina la Zamoyoni akaomba ndege binafsi,akalipia pesa iliohitajika na baada ya utaratibu kukamilika akapaa mwewe kwenda Dar kufanya alioyajua.
*****
Kikao kilikaliwa eneo tofauti na lile la mwanzo,huku mwenyekiti wa kikao kile akiwa mwingi wa wasiwasi na sura ya kupungua morali,akawatazama tena kisha akanena.
"Zedi kaingia zoezini"akaiacha kauli yake ikiambaa kwa wajumbe wake kisha akaendelea
"Zedi hayuko peke yake,na kuna mtu atakuwa kamtuma kufanya jambo hili na bila Shaka ni mwalimu wake kijeshi"
Mjumbe mwingine akadakia
"Meja Salim Komba? inawezekanaje hii? Akatoa swali kwenda kwa wenzie na bila kumwemwesa mkuu wa kikao kile akatoa ufafanuzi,

"kepteni Shayo alikuwa ni mtu wa karibu na Meja Salim,mbali ya kuwa rafiki yake pia alikua ni mwanafunzi wake katika medani ya vita,kubwa zaidi Zedi ni ni rafiki wa wote japo Zedi aliasi jeshi lakini bado anatumia taaluma yake kwa malipo sehemu mbalimbali za Dunia hii."
Akaendela baada ya kupisha ukimya ndani ya dakika moja.

"kilichonifanya niwaite hapa ni kwa sababu mwakilishi wetu Ikulu amenipa taarifa ya kuwa hata Rais anahisi hili jambo la kuuawa wanajeshi wake lina jambo nyuma yake,na ndo maana akatumwa Sajini Mina kuanza upelelezi,sasa sijui tufanyeje ili mambo yaende sawa." akamaliza kuongea bwana yule.

Baada ya ukimya mfupi akakohoa mjumbe mmoja na macho yote yakaelekezwa kwake kumsikiliza

"Mpango Tikisa lazima uitikise Tanzania kisha baada ya raia kutikiswa bungeni nitapeleka hoja ya kumpinga rais ikishindikana nyinyi mtapindua nchi,Ibra mbaya anaendelea kuwafua vijana msituni,lakini hatutaweza kufanya yote hayo kama Zedi atakuwa duniani na Meja Salum ashughulikiwe....

****
Wakati kikao kikiendelea Zedi Wimba alikuwa anatoka maabara ya silaha ya usalama wa taifa Mbezi mwisho.
Huko alikutana na mpenzi wake ambae kimsingi ndie alikuwa mtalam wa silaha.
Alikuwa na jibu la ganda la risasi alilolichukua kutoka Chaya alikofia kepten Shayo.
Jambo moja lilimchanganya ile risasi ilikuwa ina kipenyo cha 18mm na hii ni risasi kubwa sana na inauwezo wa kutembea nusu kilomita au mita hamsini kwa sekunde moja,na inatumika na bunduki ya kudungulia aina ya magnum rifle slig hii ilikuwa ni silaha mpya na hapa kwetu hatukua nayo na wagunduzi wa silaha hii ni wafaransa.
Zedi akaihisi hatari katika nchi hii,.
Wakati akitafakari hayo alikuwa anaikaribia ubungo stendi ya mabasi lengo lake ni kwenda kitunda kulikokuwa na msiba wa kepteni shayo,alipanga kwenda kule akiamini atapata jambo la kumtatulia kitendawili cha matukio haya.

Ni wakati alipokuwa akikunja kona kuifuata barabara ya Tazara,akakumbuka kitu siku anamwokoa Mina alimwibia kijitabu kidogo kilichokuwa kipo kwenye kifua cha mwanadada yule.
Akatafuta maegesho akasimamisha gari aliloazima kwa mpenzi wake.

Akakitafuta kijitabu kile katika mfuko mdogo wa kuhifadhia vitu vyake muhimu,
Hakukawia akakipata,alipokitoa tu kwenye mfuko,akakutana na damu iliokuwa imeganda juu kwenye kijitabu kile cha kumbukumbu,hapo akatafakari kidogo yawezekana hiki kijitabu kilipokonywa mikononi mwa mtu aliekuwa yupo hoi akipigania uhai wake.

Akakifunua na neno la kwanza kukutana nalo juu kabisa ya kijitabu kile ni "MEGA 09" akajua hiyo ilikuwa ni namba ya utambulisho ya kepteni Shayo katika medani za kimkakati vitani.

Akazidi kukifunua akakutana na mambo mengi ya kumbukumbu za maisha ya kepteni shayo.
Punde akakutana na ukurasa mmoja uliokuwa umeandikwa lugha ya fumbo
"Usimwambie mtu kifo"
Kisha akakuta jingine
"Kivu kongo (Goba)"
"saa tatu usiku ngerengere"
"Fire team"

Kisha kukafuatia orodha ya namba zikianza na neno Mega,hii ikimaanisha zilikuwa ni namba utambulisho wa makomando
"Mega 01,G2,Z4,K3"
Kisha kukafuatia na alama ya kuuliza na hakukua na neno lingine zaidi ikabaki ni tafakuri ya nini alichomaanisha kepteni Shayo,hakuona kama ni wakati sahihi wa kutafakari jambo hilo akawahi kwenda Kitunda kwenye mazishi ya rafiki yake Shayo.

Watu wengi walihudhuria msiba ule, Zedi akiwa yupo tofauti kimwenekano alikuwa ni mmoja ya watu waliohudhuria msiba ule.
Alikuwa makini na kila hatua ya mtu msibani pale lengo lilikuwa ni kumtafuta mtu aliemwona kwenye viwanja vya jeshi kambi ya ngerengere siku ya kuaga mwili wa Kepteni Shayo na luteni Koba na dereva private Zedekiah.

Katika pitapita za macho yake akakutanisha macho na mwanamke mmoja aliekuwa kavalia hijabu,walipokutanisha macho Zedi akagundua kariba ya mwanamke yule akatabasamu maana alijua kapata msindikizaji wa nyendo zake.

Baada ya kuuzika mwili wa kepteni shayo kukafuatia heshima ya kijeshi kupiga saluti na mizinga.
Kisha Zedi hakutaka kusubiri zaidi akaenda ilipo gari yake na kuitafuta barabara.
Ni wakati akiwa anaikaribia ukonga akagundua nyuma kuna gari inayomfuata akatabasamu kisha akapanga la kufanya ili akutane na msindikizaji wake...


Asalaam kudo
 
Sehemu ya 13*

Manchester Pub ilikuwa mbele ya gari la Zedi,hakuwa na namna zaidi ya kuifuata pub na kupaki pembeni zilipokuwa gari nyingine,akatulia kidogo na kutazama pembeni kwenye kioo,akaliona gari la lilokuwa linamfuata likipaki pembeni kidogo ya Pub ile,akashuka haraka na kwa mwendo wa kuwahi foleni ya mshahara akaufikia mlango wa kuingilia Pub.Hakuingia akasimama kidogo na kuinama akafunga kamba za viatu vyake,lengo halikuwa hilo alihitaji kuona kama aliekwenye gari lile atashuka ilikuwa hivyo alimuona mtu akishuka na alikuwa ni mwanamke,yeye akazama Pub.

Alienda kaunta na kuagiza maji,wakati alipotaka kulipa yule mwanamke alikuwa kafika na kutoa noti ya elfu tano na kumlipia kisha wakatazamana alikuwa ni koplo Mina mwanamke mzuri ajabu,.Zedi akatabasamu akashuka kitini akamwomba koplo Mina amfuate.

Waliingia ndani ya gari ya Zedi,wakaanza mazungumzo

"Ulinitambuaje wakati nimejitahidi kubadili mwelekeo?"

Koplo Mina hakujibu nae akauliza

"wew ulitambuaje nakuafuata anyway nimefuata kitabu changu"

"kipi"

"Ulichonipokonya kule porini afu huna aibu unaingizaje mikono kifuani kwa mwanamke mwizi wewe"

Zedi akamtazama kwa jicho la kwanini umeniita mwizi,kisha pasipo kumuuliza Mina akawasha gari na kuindoa kwa kasi,koplo Mina akamtazama Zedi kisha pasipo kuongea jambo akaingiza mkono mfukoni na kutoa simu akaweka sikioni akatoa maagizo upande wa pili.
"T685 DLK ipo Manchester pub"kisha akashusha mkono chini na kuitia mfukoni simu yake na kukaa kimya ila Zedi akauvunja ukimya ule
"unaniamini kiasi gani"

"Asilimia sifuri"

"sasa mbona umekubali tuandamane"

"Nataka kitabu ni changu nilikitolea damu kwa wanaharamu wale"

"Nisipo kupa?"

"Itafahamika"

"OK tuachane na hayo hatuna muda wa marumbano,mimi na wewe namba moja tuyajenge mahali flani hapo mbele kisha tusaidiane ila Mimi nikupe wewe ripoti"

Mina hakujibu akakaa kimya na Safari ikaendelea kimya.

****
Ilikuwa ni mida ya jua kuifikia magaribi na mida ni saa kumi na mbili kasoro jioni,ni muda Zedi na Mina walikuwa Mabibo nyumbani kwa mpenzi wake Zedi aliitwa Afsa wakijadili taarifa iliokutwa kwenye kitabu cha kepteni Shayo.

"09 hii ni namba ya Shayo naijua ila hizi code zingine ni ngeni kidogo na hii K3 ni namba ya Luteni Zegera huyu namfahamu hadi kwake tuliwahi kuwa kombania moja ila hawa wengine ni ngumu"

Akadakia Mina
"kinachoniumiza alikuwa anamaanisha nini kuhusu Goba Kivu na kwanini iwe Kongo"

Afsa akadakia
"Hapa jibu laeza kuwa Shayo alikufa akitoka kongo na alishukia kigoma..."
Akaingilia Zedi

"Ok ndoo maana aliandika hapa muda wa kuondoka saa tatu,pia hii ilikuwa ni siri lakini kwanini walikufa watatu na wengine wako wapi,na huyu luteni Koba ni rubani wa jeshi,hii inamaana walikuwa na Safari ya kongo lakini walifuata nini ?"
Hakuna aliejibu Zedi akachukua simu na kumpigia Meja Salimu komba akamweleza alipofikia kisha akampa code za wanajeshi anaohisi walikuwa pamoja na kepten Shayo.
****
Koplo Makame alikuwa katikati ya mji wa Goma alikuwa anaukata mtaa wa Angani akanyoosha na barabara hadi alipofika ilipo kanisa ya waromani akakunja kushoto hadi mtaa wa Lucy lameki hapo akawa anaambaa na mtaa huo hadi akaifikia nyumba kubwa na ya kisasa kuliko zote katika mtaa ule,hapo akapunguza hatua za miguu yake na kwa chati akawa anaitazama nyumba ile mandhari yake kwa nje,akaipita nyumba ile iliokuwa imezungushwa kwa ukuta mrefu na nyaya za umeme,jumba lilikuwa tulivu kama vile halikaliwi na mtu.

Koplo makame alikuwa ameiacha nyumba ile hatua kadhaa ila akagundua hakuwa peke yake kulikuwa na watu wawili nyuma yake,hakuwajali akazidi kusonga mbele akaifikia barabara ya Nyerere,hapo akakunja na kuingia mtaa wa magzabe huko hakwenda kibahati mbaya alienda maeneo yale kwa sababu kulikuwa na utulivu na vichaka vidogo vidogo,japo ni mchana ila hakukua na pilika za watu hivyo akajibanza kwenye moja ya vichaka hivyo kitalaam kabisa.
Punde wakafika watu wawili eneo lile waliongea kiringala huku wakihangaika kuangaza macho yao huku na huko,punde akatokea koplo Makame mbele yao,kwanza mabwana wale walizubaa bila kufanya jambo makame hakuwasemesha akabaki akiwatizama mmoja kati yao akamuuliza kwa kifaransa lugha ambayo haikueleweka mbele ya koplo Makame.
Waliona kama wanadharauliwa kwa kitojibiwa maswali yao na koplo makame kwa wepesi wa ajabu wakamvamia koplo Makame kwa pupa,walikosea Sana hakuwa mzembe kiasi hicho kwa wepesi ule ule akawakwepa watu wale,mmoja kati yao akayumba kisha akajipanga katika mtindo wa kupendeza,Makame akatabasamu nae akajiweka tayari kwa lolote,.
Akamfuata mmoja aliekuwa kasimama kushoto kwake akampiga usawa wa maungio ya goti na kwa kasi ileile akatupia ngumi mparazo iliompata mtu yule kisha akasimama hakutaka kuuweka usiku akapanga kuumaliza mchezo akajiweka mkao wa nyani au monkey style,akateleza chini akakutana na ubavu wa mmoja kati yao aliponyanyuka bwana yule alikuwa mbali na dunia hii akabaki na mmoja aliekuwa anatapatapa kutaka kukimbia akamwahi na kumvunja shingo kisha akatoka pale kama sie yeye aliefanya vile akarudi hadi mtaa wa Angani hapo akasubiri kidogo punde ikaja gari ndogo ya kizamani ikapaki pembeni akadandia ndani akamkuta koplo Ziga bila kusema neno safari ikaanza ila hawakufika mbali mbele yao wakakutana na kizuizi cha gari la kijeshi walikuwa wanajeshi wa kongo wakiwa wamewaelekezea mitutu ya bunduki.


Nb:Chonde chonde ndugu zangu naomba mnisapoti kwa chochote sehemu za nyuma zinaelezea zaidi

0758573660
0658564341
0624155629
 
Sehemu ya 14*


Koplo Ziga aliekuwa dereva wa gari lile aina ya pijot toleo la zamani la mwaka 1992,akasimama kisha kama aliesubiri neno toka kwa koplo Makame akaweka usikivu na macho mbele akilitazama gari lile la wanajeshi wa Demokrasia ya Kongo.

Akamtazama koplo Makame aliekuwa tayari kwa lolote na kwa utulivu kabisa akamuuliza Koplo Makame...

"Tunafanyaje soldier!"

"wapo wangapi kwani"

"Hawafiki saba"

"Ila tusiwatege isije kuwa ni trap hii"

"upo sahihi soldier ngoja waje"

Wakati wakijadili wakaona lile gari likisogea karibu yao na askari waliokuwa kwenye lile gari wakaweka silaha zao tayari kwa lolote.

Akashuka mwanajeshi mmoja aliekuwa na cheo cha sajenti akionekana ndie kiongozi wa kikundi kile,akalifuata gari la lile la Pijot lililobeba makomando wawili wa kitanzania.

Kwa lugha ya kifaransa akamwongelesha koplo Ziga ambae nae alikuwa anaielewa lugha ile japo kwa mbali na mazungumzo yao yakawa,

"Nani mmliki wa gari hili"

"Kimbu Zibora"

"Nani kimbu kati yenu"

"Hakuna kati yetu"

"Afu nyinyi sio wakongo!"

Akasita kujibu koplo Ziga,akamtazama koplo makame,Koplo Makame akampa ishara ambayo haikuonwa na sajenti yule kutoka jeshi la Kongo.

'Ndio sisi sio wakongo"

"passport?!"

"Aah tumezisahau kwa mwenyeji wetu"

Sajenti akawatazama kwa muda kisha akatoa ishara kwenda kwa watu wake,punde lile gari likawa limezingukwa na wanajeshi wale huku waliondani wakiamuliwa washuke.

Makoplo wale wakateremka,baada ya kuteremka askari mmoja akawakagua kisha akarudi kwa mkuu wake na kutoa taarifa hajapata kitu toka kwao na hata gari yao haikuwa na kitu pia.

Sajenti yule akawafuata tena makoplo wale kisha kwa upole akawaambia

"Samahani kwa usumbufu ila ni mambo ya kiusalama tu maana silaha zinapita hapa kila siku,kifupi tu karibuni Kongo,naitwa Sajenti Zebyirimana"

Akageuka na kwenda zake huku makomando wale wakiondoka eneo lile kwenda wanakokujua.
****
Papaa Deo Mukamba aligurugwa na taarifa alioipata ya kuwa vijana wake wawili wameuwa na mtu waliemtilia shaka baada ya kuonekana akiikagua nyumba yake.
Hakuwa anajua huyo mtu katokea wapi na kwanini anaichunguza nyumba yake,na kama anaichunguza inamaana anamjua yeye.
Akanyanyua simu na kupiga simu mahali fulani huko akatoa maagizo mji mzima wa Goma upekuliwe na kila mgeni anaeingia na kutoka apate taarifa zao,ila hakujua wageni wake hawakuwa na urafiki na makazi ya watu wa mjini.
****
Kilikuwa kama kichaka kikihama upande mmoja kwenda mwingine huku nyuma kikifuata kichaka kingine kikipita kwa hatua zile zile za kile cha kwanza.
Alikuwa ni Komando Makame na Komando Ziga na hapa ni baada ya kutoka goma kufanya harakati za kujua ni wapi wataanzia ili waeze pata taarifa muhimu walizozihitaji,na sasa walikuwa karibu na Kambi ya AGFT na silaha pekee ni visu vya kikomando vilivyokuwa mikononi mwao na bastola mbili kila mmoja walizokuwa wamezipachika viunoni mwao
Nia ni kuitafuta ramani halisi ya kambi ile yote na wajue jinsi ya kumwokoa 01 ambae hawakuwa na hakika kama yuko hai hadi muda huo.
........

Asalaam Kudo (Bahati Mwamba)
 
Sehemu ya 15*

Zedi alipokea taarifa kutoka kwa Meja Salim komba ya kuwa hizo code ni utambulisho wa makomando wanne wanaotoka vikosi tofauti vya jeshi kuna anaetoka Makutopora Dodoma,unguja,Msata na orojolo Arusha.

Ila katika hao wote taarifa zinasema walichukua likizo tarehe 30 ina maana wote walichukua likizo siku moja japo wanatoka vikosi tofauti isipokua huyo kepten Zegera yeye alipewa ruhusa ya dharura tarehe hiyo hiyo ila hadi sasa anaripoti kazini hapo hapo msata.

Meja Salim aliendelea kueleza kuwa siku ya tarehe hiyo hiyo alifuatwa na kepteni Zegera akiwa na barua ya kuomba dharura ana shida nyumbani kwake mabibo dar es laam.
Baada ya siku mbili alirudi na kimsingi ndo dharura yake ilikuwa inaisha.

Zedi akahitimisha maelezo yake mbele ya wenzie Afsa na Mina.wakapanga mkakati pangua maana waliiuta pangua kwa sababu waliamini wenzao watakua wanapanga jambo wasilolijua na wao hapo walipo wanapanga kupangua wasichokijua.

Zedi alijipa jukumu la kumtafuta Zegera kwa kuamini kuna jambo analijua katika mpango wa mauji ya wanajeshi na kukosekana kwa baadhi ya makomando na taarifa zilizokinyume cha utaratibu na kutia mashaka.

Sajini Mina alijipa jukumu la kufuatilia kifo cha waziri wa afya bwana Makaya Changulu.Ambapo kimsingi kifo chake kuwa na taarifa ya kudunguliwa kwa bunduki ya kudungulia au sniper rifle.

Afsa yeye akajipa jukuma la kutoa Msaada wa dharura kila panapohitajika.

****
Kepteni Zegera alitoka mapema kazini kwake kwa sababu alikuwa na jukumu moja tu kuhakikisha silaha zilizoagizwa zinaingia bandarini na kutolewa salama bila kuwa na kizuizi na kwa kuwa silaha zile zilikuwa zinaingia nchini kwa kibali cha serikali hakuwa na shaka kuwa atapata usumbufu wowote kazi yake ilikuwa ni kuhakikisha silaha zile zinatua mikononi mwa Mbaya ili ziwafikie vijana waliokuwa kambini wakijiandaa kwa ajili ya mpango Tikisa.

Alifika mabibo akiwa amepoteza saa mbili za kuwa safarini kwa kutumia gari yake ndogo.
Alipofika nyumbani kwake akapokelewa na vijana watatu waliotoka kwa Ibra Mbaya akiwemo Deepaklipa.
Ukafanyika mgawanyo wa kazi,Deepaklipa yeye alipangiwa kuhudhuria mkutano wa waziri wa viwanda bwana Zakayo kuzigwa lengo ni kummaliza akiwa mkutanoni na waandishi wa habari.
Zegera alikuwa na jukumu la kukutana mkurugenzi wa bandari ili kuhakikisha kunakuwepo na uangalizi siku ya kufika mzigo wa silaha ambazo mkurugenzi yule alijua kazi yake.

Kepteni Zegera hakuwa sawa kifikira kuna kitu kilimsumbua ila hakujua kinachosumbua akili yake.Baada ya kufikiria kidogo akachukua simu na kupiga na punde ikapokelewa upande wa pili

"Zagamba hapa"

"Naomba ufike kwangu na mbwa wako natoka"

"Nimekupata"

Akakata simu na kujipaki kisha akaondoka eneo lile yeye wenzie wakipanga kukutana tena baada ya saa kadhaa na hiyo ilikuwa ni saa kumi na moja jioni.
*****
Zedi alikuwa kavaa nguo nyeusi juu mpaka chini alitembea kwa mguu kutoka KKT Mabibo alipokuwa kaipaki gari yake,akaifikia paraise bar napo akapapita,kisha akafika zilipo ofisi za Ale kampani hapo akasimama na kuangalia mbele hatua kadhaa kabla hajaifikia nyumba ya kepteni zegera,akajipa utulivu katika akili yake,akazidi kusogea na kuipita nyumba ile akakunja kushoto na kuiacha nyumba ile ikiwa nyuma yake,hakufika mbali akageuza na kuambaa na vivuli vya mti kisha kwa wepesi usioufikiria akadandia ukuta mmoja na kudondokea ndani bila kutoa kishindo.
Haikuwa tageti yake nyumba ile ila aliruka kuingia pale maana ukuta wa nyumba zile ulikuwa umeungana kwa hiyo ili uingie nyumbani kwa zegera kwa njia za panya ilikupasa upitie ukuta ule na ndivyo alivyofanya.
Akatazama kushoto na kulia hakuona wenyeji wa nyumba ile hapo akapiga hatua kadhaa na kuutathimini ukuta ule akauparamia akadondokea kwenye uwanja mpana wa nyumba ya kepteni Zegera ila hakujua kuna macho ya mtu yalikuwa yakimtazama kila alichofanya ikabaki ni mwindano pale ndani.


....Asalaam Kudo(Bahati Mwamba)
.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom