RIWAYA: Kikosi cha Pili

RIWAYA: Kikosi cha Pili

Sehemu ya 6*

"Hampaswi kujiuliza mara nyingi,labda niwaambie hatupendezwi na unyanyasaji wa watu eneo hili,tunautaka uhuru wetu,dakika chache zilizopita nadhani mmeona vifo vya wakazi wa kijiji kile,wale ni waasi lakini hawapiganii haki ya raia,wanapigana kwa kutumika tu na faida ya matumbo yao,sisi ndio tunapigana kwa haki za wanyonge hapa Goma.Lakini hatuna silaha na hatuna ujuzi wa kutosha kutoka kwa maaskari wetu,pia ni wachache sisi, basi kama hamtojali tunaomba muungane na sisi katika ukombozi wa watu wetu,"
Kiongozi yule akawatazama tena mateka wake,kisha bila kusema neno akasimama na kutaka kuondoka,Koplo Makame akamzuia kisha akamuuliza alijuaje kuwa mwenzao bado yu hai ilihali wao waliona kifo chake machoni mwao,"

Kiongozi yule akageuka na kuwatazama makomando wale kisha akawaambia,yeye anaitwa Kimbu alikuwa ni mpiganaji wa kikundi cha AGFT,lakini hakupendezwa na yanayoendelea kule,kuua watu badala ya kutetea,pia wamekuwa ni watekaji wa migodi mikubwa na kisafarisha madini wanayoyapata kwa watu wa magharibi,hapo ndipo aliamua kuwa muasi ndani ya jeshi la waasi,Kimbu akaamua kutengeneza kikosi chake cha La people Front(LPF),ila muda wote hajawahi kupigana na was so wale AGFT kwa sababu ya nguvu ndogo walizonazo,pia akawaambia wakubaliane nae yeah yeye atajua jinsi ya kuwasafirisha kurudi Tanzania,pia aliwaahidi kuwapa siri nzito kuhusu matukio yalionyuma ya mpango wa kumkomboa Ibra Mbaya aliekuwa mpiganji wa Loraa Nkunda huku akiwa ndie mlinzi mkuu wa muasi yule alieigana na kujipatia umaarufu miaka ya tisini kwenye mipaka ya Kongo,Rwanda,Burundi hadi uganda.
Na hapo makoplo wale ndipo waliona walivyokuwa gizani kwenda kumkomboa muasi yule kumpeleka nchini mwao,
Wakaona kuna tatizo Tanzania,wanapaswa kufanya wawezalo kukomesha yajayo wasio yajua,na watazuia vipi ikiwa wako nchi ya watu,lakini swali kubwa lilibaki kwanini wakubwa wao waliwatuma kumkomboa Ibrahim Mbaya,na kwanini waliopelekwa kwenye mpango huo walitolewa sehemu tofauti tofauti huku wakipewa oda Hakuna kutambuana majina wala vikosi walivyotoka,si Koplo Ziga au Koplo Makame aliekuwa na imani na jeshi la nchini Tanzania,japo waliamini mpango si wa wote,ni wachache miongoni mwao,hawakuwa na namna ilibidi wakubali kutumika ili wajue watatokaje nchini Congo ili waje kukabiliana na Ibrahim Mbaya.

*********

Alipotoka nyumbani kwa Dr kije alikata shauri kwenda mkoani singida,eneo yalipotokea mauji ya kepteni Shayo na Luteni Koba,alipita Gapco petro station akajaza mafuta gari lake,kisha akaianza safari huku akiamini adui zake walioanza kuihisi harufu yake wametega njia ya Dar es laam ili wamnase,hapo akaikumbuka sura ya Deepaklpa akatabasamu huku akijiambia Duniani kuna watu wabaya hata Harmorapa yuko sura nzuri,akakoleza mafuta wakati akizidi kuuacha mji kasoro bahari ukiomboleza kifo cha Dr Kije.

Wakati Zedi akitimka kuelekea Singida Deepaklipa yeye alikuwa kawekwa kitimoto na kundi la watu zaidi ya sita wakiwa wanamlaum uzembe aliofanya kumwacha adui yake akiwa hai,.

Kiongozi wa lawama zile hakuwa mwingine zaidi ya Ibra Mbaya,hakuishia tu kulaumu isipokuwa kutoa onyo kwa vijana wote aliokabidhiwa katika mpango huo uliopewa jina mpango Tikisa.
Hakuna kurudi nyuma ukifeli ni bora ufe kuliko kurudi kwenye timu Tikisa,.

Baada ya kupeana vitisho vya hapa na pale Ibra akatoa majina ya watu watatu wanao stahili kufa maana wao ndio kikwazo,iwapo wasipowazima mapema,walikuwa wanne ila tayari mmoja tayari ashauwawa kisomi na Zegera,.
Vijana walisamabaratika huku wakielekeza nguvu kumtafuta Zedi ambae waliamini ashanusa harufu ya yajayo,.

********
Nchi nzima ilizizima kwa kifo cha waziri wa Afya bwana Makaya Changulu alieuwa kwa kupigwa risasi ya kichwa,akiwa katikati ya mkutano wa ufunguzi wa Zahanati ya Mbezi,vyombo vya usalama viliahidi kufuatilia hatua kwa hatua juu ya hilo na wahusika watafikishwa kwenye vyombo vya sheria,

Taarifa hii Zedi aliisikia akiwa anaukaribia mji wa Dodoma,kilichomvutia katika taarifa hii ni kule kusikia alishambuliwa na mtu inaesadikika ni mdunguaji,hakutaka kujipa maswali,akatia gari moto na kuinusa Dodoma.

Alipofika Dodoma,akaamua kuvuta muda kwa kupita kwenye mgahawa wa Chef Asili ili kujipatia staftahi.
Mgahawa huu ulijaa watu jioni hiyo,nae akajiunga nao akatafuta meza iliokuwa haina watu akakaa hapo punde mhudumu alievalia nadhifu akajongea mahali pale na kumsikiliza,alipokwisha kusikilizwa akaona huu ndio wasaa wa kukipitia kitabu kile cha Dr Kije,.
Alioyakuta humo yakampa mwanga angalau wa kilichotokea siku hiyo.....

Ndimi Kudo(Bahati Mwamba )
 
Usijee ukatuleweshaa then ukatuaachaa hewani... Shikiliaa ahad yako mkuu
 
Sehemu ya 7*

Alisoma tena maelezo ya kitabibu yaliokuwa yameandikwa kwenye kijitabu kile cha Dr Kije,ambapo yalieleza ugunduzi katika miili ile,

Alifunua kurasa kadhaa kwenye kijitabu kile,akavutiwa na kurasa moja iliokuwa imeandikwa kwa kirefu zaidi,ilijiieleza kuwa,dereva wa gari lile la kijeshi alishambuliwa na mtu aliekuwa amesimama mbele au alijibanza mahali ambapo ilikuwa rahisi kuwaona wakati wakija.
Kwenye mabano paliwekwa neno(mdunguaji).
Kijitabu kile kiliaendelea kueleza kuwa,kulingana na vipimo kutoka kwenye mwili wa dereva yule,risasi ilitoka kwenye bunduki iliokuwa umbali wa mita sabini au sitini ndio maana mgandamizo ulikuwa mkubwa wakati risasi ikitokea upande wa nyuma,pia Kepteni shayo kifo kimemkuta akiwa nje ya gari maana hakuwa na majeraha makubwa ya kuunguzwa na moto uliolipuwa lile gari lao,lakini hata risasi zilizompata zilipigwa na mtu aliekuwa hatua mbili au moja kutoka usawa wa mwili wake.

Zedi alikifunga kijitabu kile,kisha akasimama na kuondoka eneo lile la Chefu Asili na kuikamata barabara ya Singida.

Mida ya saa kumi na mbili jioni ilimkuta eneo la pori yalipotokea mauji yale ya wanajeshi,kisha kama yeye ndie mlengwa akageuza gari likawa kama linatoka Tabora kwenda Manyoni akasimama eneo lililoonesha ulipo mchoro wa polisi kuonesha ndipo tukio lilipotokea,kisha akatazama mbele hatua hamsini akauona mti mrefu kiasi,akapitisha shauri ndo mti alipokaa mdunguaji,
Akajiuliza kwanini alitumika mdunguaji,ilihali walikuwa na RPG?
Akafikiri kidogo kisha jibu likaja ilikuwa ni kurahisisha kazi ili dereva asiweze ona aliposimama mtu alilipuwa lile gari,kwa kuwa ni mwanajeshi kama Angeliona alikuwa na uwezo wa kutumia maarifa kukwepa na hapo walengwa wangejiokoa.

Akiwa bado ndani ya gari akatafakari kama aliepigwa risasi ni dereva gali lilikosa uelekeo,nae akawasha gari na kuyumbisha kidogo kisha akasimama,hapo akatazama mbele,kushoto akakadiria alipokuwa kasimama alieshika RPG,

Akashuka akapiga hatua Hulu akizihesabu,akafika hadi eneo lenye makisio,akatazama juu akaona uwezekano wa mtu kukaa hapo,akalikagua eneo hilo vizuri kabisa,kwa mbali akaona ganda la risasi,akaliokota na kulitia mfukoni,akaangaza angaza tena eneo hilo,hakuona cha maana akapiga hatua kwenda eneo lile alilohisi mshika RPG alikuwa amesimama,alipofika hapo akapachunguza kwa makini akauona mburuzo kama kumepitika na watu,akaufuata mburuzo ule.

Mburuzo ukampeleka hadi eneo kulikokuwa na makazi ya watu,nyumba nzuri japo zilionesha zimekosa matunzo kwa muda mrefu,.Haikumchukua muda kugundua yalikuwa ni makazi ya wachina wakati wa ukarabati barabara ile,huku macho yake yakiangaza kama paka mwizi hakukawia kuona kivuli cha mtu kikijaribu kumtazama kutoka moja ya nyumba zile,hapo Mwili wake ukasisimka,akahisi kuna jambo hapo,akazidi kujongea kwenye nyumba zile,punde akajikuta akitazamana na milango kadhaa huku hali ikionesha ni makazi yalioachwa muda mrefu bila wakazi,.

Aliuendea mlango mmoja na kuusukuma kisha akaingia ndani ajabu alikutana mandhari safi kuashiria kunaishi watu au mtu,na chini palikuwa na vipisi vya sigara kuashiria palikaliwa na mtu anaependa kuvuta sigara.

Akageuka ili atoke akakutana na mitutu miwili ya bastola ikimtazama huku walioshika wakionekana hawana masihara Kia ujanja wowote ambao angelijaribu kuufanya.

Mmoja kati ya watu wale alimuamuru Zedi atoke nje nae akafuata kabla hata hajapiga hatua tatu akajikuta yuko chini na kiza kikitanda usoni pake......


Ndimi kudo(Bahati Mwamba)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom