Sehemu ya 10*
Akiwa anaiacha manyoni anaitafuta Bahi,ndipo simu yake ilipoita,akaitoa kisha akaiweka sikioni na kusikiliza maelezo ya mtu upande wa pili,kisha alipokwisha kusikia ya mpigaji akairudisha simu mfukoni mwake kisha akamgeukia mwanadada aleikuwa amekaa upande wa pili wa dereva.
Hawakuwa wamezungumza chochote tangu walipotoka Chaya,sasa ni wakati Zedi alioamua kumuuliza mwanamke aliemuokoa yeye ni nani na kwanini alitekwa,.Mwanamke yule hakumjibu Zedi alikaa kimya,Zedi akaamua kukaa kimya na yeye pasipo kuongea.Japo alihisi yule mdada aeza kuwa askari ila akaamua kukaa kimya tu pasipo kusema kitu huku akili yake ikifanya kazi mara mbili zaidi ya uwezo wake,kikubwa aliwaza taarifa aliopokea ya kuwa msako umeanza wa kumtafuta kama mtuhumiwa wa kwanza wa mauji yanayoendelea.
Waliipita Bahi,hatua kadhaa mbele Zedi akakiona kituo cha kujazia mafuta cha princess Muro na Mabasi kadhaa yakiwa yamepaki huku watu wakijipatia chakula kwenye mgahawa ulioko hapo.
Nae akakunja gari na kwenda hapo kituoni akajaza mafuta kisha akamwambia yule mwanadada ni wakati wa kusambaratika,hataki kuzungumza basi itambidi ampandishe kwenye basi mojawapo ili waachane salama.
Yule mwanamke akamtazama Zedi kisha akamwambia yeye anaitwa Sajini Mina,mengine watatambuana wakija kukutana huko mbele ya safari maana anaona wanatembelea mbuga moja,kisha pasipo kusubiri akateremka na kufuata moja ya mabasi yale,ila kabla hajafika mbali Zedi akamwita nae akarudi Zedi akatoa noti kadhaa za kitanzania na kumkabidhi kama nauli ndani ya basi.
Alifanya hivi kwa kuwa Meja Salim Komba alimpigia simu na kumueleza yanayoendelea juu yake,hivyo hakuona sababu ya kuhatarisha maisha ya mrembo yule.
Akalitia gari mafuta na kuitafuta Dodoma.
Ni wakati akiwa kilomita tano kabla hajaufikia mzani wa Nala,akaona mbele kuna magari machache yameweka foleni njiani,hakukawia kujua sasa amekamatika,punde na yeye akajikuta yupo kwenye foleni ile.huku kwa kutumia mwanga wa taa za magari ya mbele akaona maaskari polisi wakikagua gari moja baada ya jingine.
Akateremka ndani ya gari lake,kisha kama anaeenda haja akachepuka upande wa pili kulikokuwa na kipori,akaambaa nacho hadi sehemu kulipokuwa na kimlima kidogo na hapo akapata kuona magari kama matatu ya askari polisi,akafikiria cha kufanya akajipekuwa mfukoni akakutana kifaa kidogo cha kuhifadhia milipuko ya dharura ambayo lengo ni kumpoteza adui uelekeo,akainama kidogo chini akakutana na jiwe,akapiga hesabu zake pale gizani,lengo ni kuwachanganya maaskari wale ili apate njia rahisi ya kuchomoka pale,akachimba kidogo chini ya jiwe na kukitega kibomu kile akiamini ndani ya dakika mbili kitatoa mlipuko mkubwa kutokana na mkandamizo ule wa jiwe,.
Ili kuwavuruga zaidi ikabidi atoe bastola yake akaondoa kiwambo cha kuzuia sauti kisha akapiga risasi kule walipo maaskari wale,na kwa kasi ya mionzi akapotea eneo lile huku akiwaacha maaskari polisi wale wakihaha kujua risasi imetoka kwa nani na ememdhuru nani. Wakati wao wakiwaza vita ukatokea mlipuko mkubwa eneo lile polisi baadhi wakaanza kupiga hovyo risasi huku wengine wakikimbia hovyo eneo lile,si polisi tu hata madereva wa malori waliokuwa wametii kukaguliwa hawakupenda kifo aliekuwa mbele akaanzisha safari kwa kiroho,wa nyuma nae akafuata,ikawa ni mtibuano barabarani.
Zedi nae akaunga pale pale nyuma ya yale magari,polisi hawakuwa na kuzuia magari ikiwa wao hawajui hatima ya uhai wao,.
Zedi ilikuwa ni lazima afanye jambo kuwakwepa polisi au wanajeshi ambao ni lazima wangelikuwa na taarifa ya kilichotokea,kwa hiyo umakini ungehitajika kwenye upekuzi wao akaona isiwe tabu akachukua simu yake na kuwasha data kisha akaingia ilipo ramani ya kimtandao akaona eneo alipo ila upande wa magaribi yake hatua chache kuna njia inayochomoza kupita kipori flani cha makutupora,kisha atatokea mundemu na hapo atapata barabara itakayomfikisha mzakwe,kisha ataipita kambi ya jeshi makutopora inamaana atarudi Dodoma mjini na hapo atajua cha kufanya,hakutaka kungoja safari ikaanza.
***********
Katikati ya misitu ya Goma,mazoezi yaliendelea kwa weledi wa hali ya juu,vijana wapatao arobaini walikuwa wanazidi kuiva ndani ya muda mfupi,koplo Makame na Koplo Ziga walikuwa wamesaidia kuwapa ujasiri vijana wale wa kikongo,kilichokuwa kimebaki ni kutumia uchache wao kuleta mapinduzi kwa kundi lingine la waasi wa AGFT,lakini tatizo likawa silaha walikuwa nazo tano tu na hazikuwa na ubora wowote,pia walikuwa na nguvu kidogo.
Kimbu kiongozi wa LPF akatoa wazo la kuongeza nguvu kutoka kwa vijana walio kijiji cha jirani na wao,hilo likatekelezwa na vijana yapata mia moja wakaletwa mbele ya Koplo Makame na Koplo Ziga mazoezi yakaendelea,.
Waasi wa AGFT kila ilipokuwa ikifika mwisho wa mwezi ni lazima silaha ziletwe kutoka sehemu wanayoijua wao na kwa kuwa kutoka goma kwenda goba hamna barabara iliwalazimu kupokea silaha katikakati ya mji wa Goma kisha kuzisafirisha kupitia misitu ya Goma wakitumia mto Kivu kuvuka kwenda Goba ilipo kambi yao,hayo yalisemwa na Kimbu kiongozi wa Lpf.Kisha ikawekwa ramani mbele ya makomando wa kitanzania wakaisoma na wakaona mahali pa kuzichukulia silaha zile ni mto kivu kwa weledi wa mapigano ya kuvizia napo wakachagua vijana kama kumi akiwemo na Kimbu wakaanza kupewa mazoezi ya kikomando ili iwe rahisi kuwavamia waasi wake Zeso.
Papaa Deo Mukamba alikuwa na kikao na watu watatu ila mmoja kati yao alikuwa ni mzungu,kikao chao kilikaliwa nyumbani kwake Papaa.
"Tunajaribu Tanzania maana wao wanamali nyingi Sana ila hazifaidishi watu isipokuwa zinafaidisha serikali tena kwa kiasi kidogo,mipango inakwenda sawa na tayari mbabe wa mafunzo na mapambano Ibra Mbaya yupo huko na anapata sapoti kubwa kutoka kwa maafisa wa jeshi ambao wao watautumia mpango huu kumpindua rais kisha wajimilikishe wao madaraka na faida tugawane"
Hiyo ilikuwa ni hoja ya mmoja wa wajumbe katika kikao kile,akadakia mwingine
"japo tunamatumaini na kuitikisa Tanzania lakini hata majaribio ya ile sumu yafanyike huko huko ili kuwavuruga zaidi"
Hapo akadakia mzungu yule
"Silaha tayari zipo njiani kufika Tanzania zinapotia Zanzibar kisha zinatua mikononi mwa mbwa mwitu"
Papaa nae akazungumza
"yote yanafanyika lakini kuna baadhi ya vijana wao wawili wamepotelea hapa na haijulikani walipo na mmoja yupo mikononi kwa Zeso,Zeso anapenda pesa akigundua mpango wetu basi atatutisha ili apate pesa lakini kikubwa huyo komando aliemikononi mwa Zeso pia si kuamini sana anaeza..."
Papaa hakumaliza kauli yake kikao kikapata ugeni,ugeni wa dharura ugeni ambao hawakuutarajia...
Asalaam Kudo(Bahati Mwamba)
Nb:watu wa Kenya wengi wameonesha kuunga mkono juhudi zangu tofauti na hapa kwetu Tanzania,ambapo mwitikio ni mdogo sana,labda sijawafurahisha na utunzi wangu,kuweni huru kunambia nitsitisha mara moja kuiweka hewani hii kitu,nitaweka nyingine tena ili lengo langu litimie
Sipo hapa kumkwaza mtu kama mtu Toka kenya anaomba kusapoti hapa kwetu kimya inanipa picha tofauti.
Wakenya mlioomba kusapoti naandaa utaratibu wa nyie kunitumia chochote kitu na nitawatumia yote kwa njia ya soft copy pia nitakuja huko mnakoomba niziweke, JamiiForums.com. .
Bado nawaomba mnisapoti bandugu
0758573660
0658564341
0624155629