Sehemu ya 17*
Kama ungeliingia ukumbi ule wa mkutano usingelichelea kuona milango ya kuingilia vyooni upande wa kulia wa mlango wa kuingilia ukumbini pale,na kama ungeliingia moja kwa moja vyooni kule ungekutana na sehemu ya kutenganisha korido mbili ya kike na kiume,lakini katika uwazi huo wa kutenganisha kulikuwa na mlango upande wa pembeni kidogo sehemu ya kuingilia wanawake,mlango ule ulikuwa ni mlango wa dharura ndogondogo kwa jinsia zote,moja ikiwa ni kupata hewa safi,kuzungumza na simu,n.k.
Sajini Mina aliona toafauti kwa mtu aliekuwa anafuatilia nyendo zake,mtu yule alievaa suti hakuwa mwingine ni Deepaklipa.
Sajini Mina alifuata kila hatua anayopiga Deepaklipa ukumbini pale,hata wakati Deepaklipa alipokuwa akiingia chooni yeye aliona na kuvuta subira.
Waziri wa viwanda aliingia ukumbini na kukaribishwa na msoma ratiba,ni wakati alipokuwa akisimama kuiendea kinasa sauti au maiki,ndipo Koplo Mina akaona jambo upande wa pembeni kidogo kulipokuwa na mapazia mapana ya kuziba madirisha,mapazia kadhaa yalikuwa yamekunjwa hivyo kuruhusu vioo vya madirisha yale kuonekana hivyo alipotizama kwenye moja ya vioo vile akaona kitu mfano mdomo wa bastola,akafikiria vioo vile vingeweza kuakisi kitu kutoka wapi,hakukawia kugundua ni nyuma ya ukumbi usawa wa mlango wa vyoo alipotizama hakuona kitu,akatulia na kujipa umakini akamtazama Deepaklipa napo akagundua jipya,sikioni alikuwa na kicheep kidogo na alikuwa akimwemwesa midomo na mkononi alishika kamera kubwa,
Mina akaona hakuna mawasiliano ya kamera ile na chip ile kuna jambo.
Akasimama akapiga hatua kuvifuata vyoo vile.
Akafika mlangoni akatazama usawa aliohis kumetokea mtutu ule hapo akaona uwazi wa kioo kilichomwezesha mtumiaji wa vyumba vile kuona upande wa ukumbi,akafanya hima kuingia kule vyooni,akazama ndani hapo akaona upande wa vyoo vya kike milango ile ya vyumba vya dharura ila akakutana na neno closed,ikimaanisha hapatumiki kwanini wakati ukumbi ulikuwa unafanya kazi,akachomoa bastola yake akasogea hadi ulipo mlango ule akaujaribu nao ukaitikia kwa utaratibu sana wa hatua za kutokupiga kelele,akaingia ndani ila akakuta kuko kimya akatazamana na viti kadhaa,hapo akachukua jukumu la kutazama alipohisi aliona kitu.
Ilikuwa ni sniper rifle Gt 91 new model ilikuwa imesimama mdomo wake ukichungulia dirishani,ajabu mmliki wake hakuwepo Mina akageuka ili atazame ni wapi mmliki alikuwa hapo akakutana na kitu ambacho hakukitarajia mtutu wa bastola ukimtizama.
Sajini Mina akapokonywa silaha yake,na akaaamuliwa kugeuka nyuma,punde mlango ukasukumwa alikuwa ni Deepaklipa aliengia baada ya kuambiwa kuna tatizo upande wa ndani,akaingia akiwa amefura kwa hasira maana muda ulizidi kwenda na hajafanya lilowapeleka,akamtazama Mina akamchapa kofi lililopelekea aone nyotanyota,kisha wakashauriana kumfunga kamba koplo Mina.
Deepaklipa akaangaza mle akaikosa kamba akainama kufungua kamba ya kiatu chake.
Sajini Mina alikuwa akipiga hesabu zake namna ya kufanya ili ajiokoe lakini hakuona upenyo maana jamaa aliemshikia bastola hakumpa hata dakika ya kupepesa macho,hata wakati Deepa akiinama kufungua kamba bwana yule hakutikisika alijua anachokifanya.
Afsa pia alikuwa ni miongoni mwa wahudhuriaji wa mkutano ule,alikua akiona kila kitu alichokuwa anakifanya Sajini Mina,hata alipoingia kule vyooni aliona,na alipoingia Deepaklipa aliona pia hapo akapata Shaka nae bila kujiuliza akapiga hatua kadhaa kuingia kule,alipoingia akakutana na watu kadhaa wakiwa wanaingia na kutoka macho yake yakatua mlango wa vyumba vya dharura akakutana na neno Closed.
Akasogea mlangoni pale baada ya watu kupungua mle vyooni,akatazma kushoto na kulia hakuona mtu,akapanga kuingia mle ndani kwa njia ya kustukiza,ila kabla ya kuingia akachungulia kupitia upenyo wa maandishi yale hapo akafanikiwa kuona Mina alivyotaitiwa na alikuwa anafungwa kamba,akapiga hesabu,
Vile walivyokuwa wamesimama aliamini kama akiwastua kwa kufanya lolote Mina atajinasua hapo akanyanyua bastola yake akapiga kioo cha mlango ule nao ukagawanyika na kwa kasi ya ajabu mwanamke yule wa shoka akazama ndani,na kama alivyotarajia akamkuta Mina ameshaingia mchezoni nae hakuwa na budi kujiunga.
Deepaklipa alikuwa na Safari mgumu wa kuyapangua mapigo maridadi yaliotoka kwa koplo Mina huku Afsa yeye akiwa anajitahidi kumkwepa msaidizi wa Deepaklipa,
Afsa alimtazama adui yake vile alivyokuwa akitumia nguvu nyingi na hii ilimpa picha Afsa ya kuwa adui yake alikuwa na plani za kumshambulia haraka ili amalize mchezo,hivyo yeye akataka kwenda kinyume awe na kazi ya kupangua tu bila shambulizi.
Haukupita muda adui wa Afsa akaanza kuhema baada kutumia nguvu nyingi na hapa ndipo alipopahitaji Afsa kwa weledi wa hali ya juu akaanza kutupia mapigo ya kuvunja,akatupa ngumi ya kike yenye ujazo wa lita tano za mafuta ya taa,ngumi ile ikaondoka na mbavu za mtu,akatupa teke la uzani wa Kilo nne likampata adui kwenye shingo,akaenda chini na hakunyuka tena.
Sajini Mina akawa anapata tabu kidogo kushambulia hasa alipogundua uwezo wa Deepaklipa akaona kosa moja litamgarimu akawa anavizia,punde akapata usaidizi wa Afsa wakawa wawili kwa mmoja.
Katika wakati mgumu katika maisha yake,huu ni wakati ambao Deepaklipa alikiri amepigika vibaya na hadi muda huo alikuwa hoi kwa kichapo cha madada wawili wanaujua kupiga kwa mitindo ya ajabu kabisa,hapo akakumbuka mbinu zake za kujiokoa hasa kwa kukimbia na pia alikiri yeye hajawahi kufaulu mara nyingi huwa anachezea kichapo hevi.
Bila kutarajia akajikuta akipokea teke maridhawa kutoka kwa Sajini Mina,teke lile likampeleka hadi mlangoni,akaona mungu ampe nini zaidi ya kuokoa kiroho chake,akajizoa zoa ili anyanyuke akamshudia Afsa akiwa katika ubora wake akimfuata kwa kasi ya kimbunga,Deepa klipa akaona usinitanie wewe kwa upenyo wa mpasuko wa vioo mlangoni akajitupa nje na kuanza kutimka huko akakutana na kundi kubwa la watu waliokuwa wameanza kujisogeza kule vyooni baada ya mmoja wa walioenda kujisaidia kusikia mtafaruku akarudi kutoa taarifa,waandishi wa habari na kamera zao wakaanza kwenda kule.
Afsa na sajini Mina baada ya kukimbiwa na mtu yule mbaya wa sura wakaona wasiuze nyago magazetini wakatumia milango ya dharura walioikuta kule wakatokomea zao huku wakiiacha maiti na mtutu wa bunduki dirishani,waziri wa viwanda nae akiwa mbali eneo lile kwa ulinzi wa maaskari...
*******
A
Asalaam kudo(Bahati Mwamba)
Nb:niwengi wanafuatilia hivi sasa na washukuru kwa hilo lakini nawakumbusha tu ya kuwa bado nahitaji uungaji mkono wenu kwa chochote kitu ili nifanikiwe kutoa kopi za vitabu viwili ninavyoshugulikia hivi sasa.
.Pia unaesoma like na koment ili twende sawa msisubiri pale arosto inapozidi ndo mnajitokeza huo utakuwa ni unafiki wa wazi.
Nawashukuru mnao like na kutoa maoni hadi sasa na huwa nawatag kila nikitoa kipande hapa.