Sehemu ya 12*
Wakati vikosi vya askari polisi vikizidi kuweka ulinzi sehemu mbalimbali ili kuhakikisha Zedi Wimba anaingia mikononi mwao,ni wakati huhuo Zedi alikuwa kawapiga chenga ya akili na mwili,.
Baada ya kuchepuka na kuwatoroka askari lengo lake lilifanikiwa na akajikuta yupo Dodoma mjini,pasipo kusubiri akapaki gari lake kwenye gereji ya champion kisha akachukua daladala hadi uwanja wa ndege wa Dodoma,hapo akajitbulisha kwa jina la Zamoyoni akaomba ndege binafsi,akalipia pesa iliohitajika na baada ya utaratibu kukamilika akapaa mwewe kwenda Dar kufanya alioyajua.
*****
Kikao kilikaliwa eneo tofauti na lile la mwanzo,huku mwenyekiti wa kikao kile akiwa mwingi wa wasiwasi na sura ya kupungua morali,akawatazama tena kisha akanena.
"Zedi kaingia zoezini"akaiacha kauli yake ikiambaa kwa wajumbe wake kisha akaendelea
"Zedi hayuko peke yake,na kuna mtu atakuwa kamtuma kufanya jambo hili na bila Shaka ni mwalimu wake kijeshi"
Mjumbe mwingine akadakia
"Meja Salim Komba? inawezekanaje hii? Akatoa swali kwenda kwa wenzie na bila kumwemwesa mkuu wa kikao kile akatoa ufafanuzi,
"kepteni Shayo alikuwa ni mtu wa karibu na Meja Salim,mbali ya kuwa rafiki yake pia alikua ni mwanafunzi wake katika medani ya vita,kubwa zaidi Zedi ni ni rafiki wa wote japo Zedi aliasi jeshi lakini bado anatumia taaluma yake kwa malipo sehemu mbalimbali za Dunia hii."
Akaendela baada ya kupisha ukimya ndani ya dakika moja.
"kilichonifanya niwaite hapa ni kwa sababu mwakilishi wetu Ikulu amenipa taarifa ya kuwa hata Rais anahisi hili jambo la kuuawa wanajeshi wake lina jambo nyuma yake,na ndo maana akatumwa Sajini Mina kuanza upelelezi,sasa sijui tufanyeje ili mambo yaende sawa." akamaliza kuongea bwana yule.
Baada ya ukimya mfupi akakohoa mjumbe mmoja na macho yote yakaelekezwa kwake kumsikiliza
"Mpango Tikisa lazima uitikise Tanzania kisha baada ya raia kutikiswa bungeni nitapeleka hoja ya kumpinga rais ikishindikana nyinyi mtapindua nchi,Ibra mbaya anaendelea kuwafua vijana msituni,lakini hatutaweza kufanya yote hayo kama Zedi atakuwa duniani na Meja Salum ashughulikiwe....
****
Wakati kikao kikiendelea Zedi Wimba alikuwa anatoka maabara ya silaha ya usalama wa taifa Mbezi mwisho.
Huko alikutana na mpenzi wake ambae kimsingi ndie alikuwa mtalam wa silaha.
Alikuwa na jibu la ganda la risasi alilolichukua kutoka Chaya alikofia kepten Shayo.
Jambo moja lilimchanganya ile risasi ilikuwa ina kipenyo cha 18mm na hii ni risasi kubwa sana na inauwezo wa kutembea nusu kilomita au mita hamsini kwa sekunde moja,na inatumika na bunduki ya kudungulia aina ya magnum rifle slig hii ilikuwa ni silaha mpya na hapa kwetu hatukua nayo na wagunduzi wa silaha hii ni wafaransa.
Zedi akaihisi hatari katika nchi hii,.
Wakati akitafakari hayo alikuwa anaikaribia ubungo stendi ya mabasi lengo lake ni kwenda kitunda kulikokuwa na msiba wa kepteni shayo,alipanga kwenda kule akiamini atapata jambo la kumtatulia kitendawili cha matukio haya.
Ni wakati alipokuwa akikunja kona kuifuata barabara ya Tazara,akakumbuka kitu siku anamwokoa Mina alimwibia kijitabu kidogo kilichokuwa kipo kwenye kifua cha mwanadada yule.
Akatafuta maegesho akasimamisha gari aliloazima kwa mpenzi wake.
Akakitafuta kijitabu kile katika mfuko mdogo wa kuhifadhia vitu vyake muhimu,
Hakukawia akakipata,alipokitoa tu kwenye mfuko,akakutana na damu iliokuwa imeganda juu kwenye kijitabu kile cha kumbukumbu,hapo akatafakari kidogo yawezekana hiki kijitabu kilipokonywa mikononi mwa mtu aliekuwa yupo hoi akipigania uhai wake.
Akakifunua na neno la kwanza kukutana nalo juu kabisa ya kijitabu kile ni "MEGA 09" akajua hiyo ilikuwa ni namba ya utambulisho ya kepteni Shayo katika medani za kimkakati vitani.
Akazidi kukifunua akakutana na mambo mengi ya kumbukumbu za maisha ya kepteni shayo.
Punde akakutana na ukurasa mmoja uliokuwa umeandikwa lugha ya fumbo
"Usimwambie mtu kifo"
Kisha akakuta jingine
"Kivu kongo (Goba)"
"saa tatu usiku ngerengere"
"Fire team"
Kisha kukafuatia orodha ya namba zikianza na neno Mega,hii ikimaanisha zilikuwa ni namba utambulisho wa makomando
"Mega 01,G2,Z4,K3"
Kisha kukafuatia na alama ya kuuliza na hakukua na neno lingine zaidi ikabaki ni tafakuri ya nini alichomaanisha kepteni Shayo,hakuona kama ni wakati sahihi wa kutafakari jambo hilo akawahi kwenda Kitunda kwenye mazishi ya rafiki yake Shayo.
Watu wengi walihudhuria msiba ule, Zedi akiwa yupo tofauti kimwenekano alikuwa ni mmoja ya watu waliohudhuria msiba ule.
Alikuwa makini na kila hatua ya mtu msibani pale lengo lilikuwa ni kumtafuta mtu aliemwona kwenye viwanja vya jeshi kambi ya ngerengere siku ya kuaga mwili wa Kepteni Shayo na luteni Koba na dereva private Zedekiah.
Katika pitapita za macho yake akakutanisha macho na mwanamke mmoja aliekuwa kavalia hijabu,walipokutanisha macho Zedi akagundua kariba ya mwanamke yule akatabasamu maana alijua kapata msindikizaji wa nyendo zake.
Baada ya kuuzika mwili wa kepteni shayo kukafuatia heshima ya kijeshi kupiga saluti na mizinga.
Kisha Zedi hakutaka kusubiri zaidi akaenda ilipo gari yake na kuitafuta barabara.
Ni wakati akiwa anaikaribia ukonga akagundua nyuma kuna gari inayomfuata akatabasamu kisha akapanga la kufanya ili akutane na msindikizaji wake...
Asalaam kudo