Riwaya: Kikomo

king of zodiac

JF-Expert Member
Sep 3, 2013
311
432
Si kazi yangu kujishughulisha na makosa ya jinai. nilishangaa kidogo chifu aliponiamuru nifuatie tatizo la upungufu wa almasi.
Isingekuwa kwa sura aliyoonesha nilitaka kumwambia apeleke malalamiko yake kwa kamishna wa polisi au anipr uhamisho wa kwenda huko kama alikuwa hanihitaji katika idara yake.
Siku hiyo alivaa sura ya kutisha na sikuwa na la kufanya ila kukubali. Kulikuwa na ushahidi kwamba almasi zilizouzwa katika masoko nje ya nchi zilikuwa chache sana kulinganisha na kiasi kilichokuwa kinachimbwa kwa nini?
Idara ya upelelezi ya makosa ya jinai imejitahidi bila mafanikio. Askari polisi joel amegusa chanzo cha uhalifu akafa kayika ajali ya ndege siku chache kabla ya kufunga ndoa na mchumba wake amanda na uhalifu ukaendelea
Chifu alimtuma jack mbwile mpelelezi wa kawaida lakini maiti yake iliokotwa ikielea ziwa victoria na uzito wa jambo zima ukawa umetambuliwa. Ndipo nikatumwa mimi willy gamba

ITAENDELEA
 
85c02461711ece2fa6b74521ca9e762a.jpg
f483b0024147b0d3a1c23b1ae253550d.jpg
 
Aristablus Elvis Musiba, gwiji wa riwaya za kipelelezi.

Waandishi kama hawa sijui kwanini hawapo tena siku hizi.Musiba aliandika mpaka vitabu vyake vikapigwa marufuku na wanasiasa uchwara.Alijua kuitumia vyema kalamu yake, si hawa vijana wa sasa kazi kuandika "Kampa kampa tena".

Serikali kupitia wizara yake ya Elimu pamoja na Wizara ya Sanaa na Michezo ingekuwa serious ingefanya kuhifadhi maandishi ya waandishi hawa ili zisipotee.Lakini sasa cha kustaajabisha ni kwamba 'Ndiyo kwanza wameshusha neti na kukoroma'.Taifa makini huhifadhi maandishi ya waandishi wake hata kama maandishi hayo wangewauma wanasiasa.

Si kuwanyanyasa, kufutilia mbali kazi zao na wakati mwingine kuwatishia wasitishe uandishi wao.Huku ni kujichimbia kaburi.

Ipo haja Serikali kupitia wizara zake husika kurudisha kazi za kina Shaaban Robert, Musiba, Mtobwa, Kezilahabi, Anduru nk kwa ajili ya kizazi cha baadaye.

R.I.P All.
 
Wanan,finyango,johape,shubalozimchovunie,kibuyu180,tumosa shamac matukutuku, bess,ngoma ya ukae,malafyale guasa amboni nemesis swahiba 92 mtoro8 cmases shunie
Lutayega
Mambo ndio haya watu wana njaa na riwaya kisha wauliza jamani niwaletee chakula ?Shukran nyingi kwako ndugu yetu zodiac.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom