RIWAYA: KICHAA.
Na: ZUBER R. MAVUGO.
N0. 32.
ENDELEA.
''Oy, We mwanasheria amka tupige pindi.'' Nilizoea kumuamsha hivyo kila ilipofika mida yetu ya kujisomea, sikwamba hakuwa na jina anaitwa Maganga Mazezere Maluvya yeye alipenda kujiita Trriple M, tofauti na mimi ambae nilipenda sana kumuita mwanasheria.
'' Aisee, Mavugo, nitakufunga mimi. Hujui una muamsha jaji wa baadae, sasa unapaswa uwe makini sana sio ukijiskia tu kunisukumasukuma basi unafanya.'' Nikawaida yake kabisa kunijibu hivyo, kwahiyo sikuwa nikipatwa na mshangao wa aina yoyote kwani nillisha mzoea kabisa. ''Acha zako, inamaana hata hao majaji ndo huwa wanaamshwa kama mayai!!!Hebu nawa huko tupige pindi.''
''Takufunga? Sipendi dharau, hata kidogo. Wewe ni muandishi halafu mimi ni jaji hivi unadhani utaniweza wewe???? Kwanza hebu leta hilo daftari la Histori hapa nianze kwanza mimi kusoma lasivyo, Ibara ya hamsini na mbili kifungu namba moja hadi mbili kitatumika hapa.'' Alikuwa akipenda kunionea kwa vifungu vyake nisivyovielewa, lakini yote kwa yote tulikuwa tukichukulia kila maneno tuliyo kuwa tukiyaongea kama sehemu yetu ya utani tu. Baada ya maneno yetu basi wote hukaza msuli kwani tulikuwa tukisoma mchepuo wa aina moja.
Yeye ndie aliye nifunza kuuheshimu muda kwani hapo kabla sikuwahi kuuheshimu muda hata kidogo. Nilikuwa radhi muda unipite nami nikajiona niko sawa tu.
'' We Mavugo, ngoja nikwambie kitu, hivi unajua kila kitu kifanywacho na binadamu kwa siku, hutegemea muda.'' Kwakuwa nilipenda ubishi basi sikuwa nikisita kumbishia,''Umeanza uanasheria sasa, naona unaniona mwehu, ina maana hata kuongea tunategemea muda!!! aaaaah!!! hahahaha we jamaa wewe muongo kinoma.'' Nilimjibu vile huku tukielekea kwenye kijimgahawa kilichopo shuleni kwetu, kwakuwa anaujua ubishi nilobarikiwa basi alikuwa akiniacha na kuanzisha mada nyingine tofauti na ile kisha baadae hunielewesha.
Shule yetu ilikuwa ni mchanganyiko hivyo hatukuwa na uwezo wa kuepuka mabinti ambao tulishindanao darasani kutwa nzima tofauti ni kwamba hatukupewa uhuru wa kulala pamoja nao kwani shule yetu ilikuwa na mabweni yawasichana na yale ya wavulana.
Mimi katika maisha yangu sikuwahi kujua wala kutegemea kujua kitu kinachoitwa Mapenzi, nilikuwa nikishuhudia tu toka nipo mdogo watu wakipendana na hata kwa macho ya barehe yangu changa niliweza kutamani tu wasichana lakini sikuwakaribia kutokana na aibu niliyokuwa nayo, nadhani hata wewe ni shahidi Mwambe kwani o-level tulisoma wote. Nilikuwa sipendi kumuongelea msichana na hata nilipo muona mtu akilia kwa ajili ya sichana nilikuwa sisiti kuangua kicheko cha dharau mbele yake hadi hapo atakapo nichukia. Bila shaka niliwaona wote waliyokuwa wakiumia kwa ajili ya mapenzi ni kama mapunguwani, nilikuwa nikijisemea, ''Mwanamume huwa analililia daftari lake bwana nasi kumlilia mwanamke ambae haleti hata maarifa.'' Rafiki zangu walikuwa wakinicheka ukiwemo na wewe Mwambe, na kuniambia kwamba , ''Mavugo unaongea tu, huyajui mapenzi wewe.'' Nadhani nawe nishahidi kwa jinsi nilivyokuwa nikiwaangulia kicheko kilichokuwa kikiwafanya muendelee na shughuli zenu na kuniacha mimi kivyangu.
Ilikuwa mara ya kwanza katika maisha yangu kuona msichana aliyeridhiwa na moyo pamoja na nafsi yangu kwa ujumla. Siku hiyo ilikuwa ni jumapili au siku ya wali kama tulivyoipachika jina. Muda huo nilikuwa nimekaa mazingira ya uwanjani kama ilivyokuwa kawaida yangu toka shule ya awali. Hapo ndipo alipopita mrembo yule ambae macho yangu yalimpatia vigezo vyote vya urembo wa dunia na kumpa kura ya ushindi wa urembo huo endapo kama angeshiriki. Katika maisha yangu sijawahi kuklubali niyakodoe macho yangu kwa ajili ya kumuangalia msichana lakini siku hiyo ndio mara yangu ya kwanza, nilimuangalia sana binti yule kisha nikaanza kupekuwa ndani ya kichwa changu huku nikijaribu kuufananisha urembo wake na urembo wowote ambao nilishawahi kuuona lakini sikupata, nilifikiria mara ya pili ndpo nilipoamua kumfananisha urembo wake na urembo wa wale wanaosifiwa kwenye vitabu vya dini kuwa huwa ni wazuri, watiifu, na hufuata amri za Mungu tu. Hawajawahi kumkosea wala kukaribia kufanya hivyo. ''Ewaaa!!!! Huyu ni maraika kweli.'' kupitia mapigo ya moyo wangu, chapisho la maneno hayo liliweza kuonekana kifira huku sjui nimuite, sjui niacha zikiendelea kunisumbua akilini mwangu. Nafsi ilitamani kumshika binti yule walau hata mkono tu, lakini kila ilipoiamrisha miguu kitete kilinijaa na kushindwa kumsogelea. Nilisahau kabisa kama binti yule aliye nishugulisha mwili mzima kasoro kivuri ndani ya dakika moja tu, alikuwa akiondoka na kuniacha nikipata fursa ya kumuangalia maungo yake ya nyuma, sikuwa na dini wala sikupenda mambo ya dini lakini nilijikuta nikiropoka ''Astaghafirullah'' Labda pengine kwa kuwa malaika yule alikuwa amevaa mavazi ya kiisilamu tu. Hapo hapo fikra zina nichukuwa na kujikuta nawaza nipo katika ndoa huku shekh akifungisha ndoa.
''Hivi!!! Mavugo, sikuhizi unavuta bangi???'' Alinihoji Maganga baada ya kunikuta nipo nikichekacheka peke yangu. Hakika hakujua mwenzie nilipokuwa kifikra. Nilikasirika sana baada yakukatishwa mawazo yangu kwani nilijua kabisa tayari nimeshaoa, nilijaribu kufumba macho na kukumbuka mawazo yale, lakini malaika wanguu hakuja tena.
Kwakuwa ni raiki yangu mkubwa basi siku sita kumwambia jambo lile.
''Sheria ya Mapenzi kifungu namba tatu kilichoandikwa na wapendanao wa kwanza walisema kuwa, Mapenzi huanza kama chemchem ndogo ndani ya moyo lakini chemchem hiyo huzaa bahari kubwa na kuujaa moyo kadri mpendaji anavyo zidi kujiathiri kimawazo kwa kumuwazia yule aaehisi kuwa anampenda. Ikumbukwe kwenye tahadhari ya wapendanao wa awamu ya pili wao waliwahi kusema kuwa ile ladha ya uchungu ambayo hupelekea mapigo ya moyo na baada ya hapo kuhisi raha, ndio hiyohiyo ambayo hupelekea maumivu pindi yule unaehisi unampenda atakapo kuacha na makovu. Kwahiyo sasa tuna pata jibu kuwa asilimia za upendo ndani ya mapenzi ndizo hugeuka kuwa za maumivu baada ya kutendwa. Karibu sana kwenye uwanja wa dhambi kwani huku kwetu kulizana ni sunna kabisa.'' Huweziamini moyo ulikuwa ukikimbia kadri Maganga alipokuwa akiongea maneno yake, nami nilikuwa niki yanukuu kwenye kidaftari changu kidogo kwani nilipenda sana kukusanya habari na sikuwa mtu wa kurdhika habari inipite kwakuwa nilipenda sana uandishi wa habari.
''Kwahiyo nipe anuani nikusaidie kukuunganishia.'' Aliongea, Maganga huku akitazama na kulichanua lile tabasamu lake la kuoneshea ushirikiano.
'' Wewe, kwani ukimpenda mtu hadi ajue bwana... Achana nae, mistaki'' Nilikaidi kinamna ile.
''Acha mambo yako wewe, muandishi gani anaekub ali kupitwa na habari?''
''Habari??? Ipi hiyo nikaandike.''
''Jione ulivyo bwege,'' Huku akiigiza maneno yangu kwa kubana pua na kunifanya nijionee aibu, '' Eti, Habari, ipi hiyo nikaandike,'' Kisha akaendelea, '' Ujuwe, juha si yule mfalme tu wa kwenye vitabu, bali hata kuwa mtu wa aina yako ni ujuha tosha.'' Hapo aliniacha hoi kwa hasira za ghafla kwani kila nilipokuwa nikilifikiria lile neno Juha nilikuwa nikichukia sana. Kwa hasira nikamvagaa kimaneno, ''Usiniletee, umeona nani juha hapa. alafu usidhani kukaa kimya muda wote ndio nakuogopa, sasa umependa wewe au mimi!!! Mbona unataka kuniwekea masharti kwenye moyo wangu? Kwani we hauna limoyo? Sasa siuliite juha lakwako nasi kuniita mimi, tena kwa taarifa yako juha mwenyewe.'' Nilimjibu huku kwa akili yangu nikijua ataniacha kumbe nitofauti na nilivyodhania.
Huku akicheka, ''Aisee!!! sijawahi kuona muoga kama wewe, huo ni uoga tu unakusumbua. Eti unajiita muandishi!! Muandishi gani unaogopa hadi madem, natuone sjui utafika wapi boya wewe.'' Labda niseme tu ukweli kuwa maneno yake yali ni choma sana, ni dhahiri kabisa alikuwa amenipatia kwani nilikuwa nikiogopa wasichana na sikuwa na lakuongea mbele yao. Nikaanza kusaka jibu kichwani mwangu la kuifanya kauli yake ione kane ya uongo....
Sikila anaechanua tabasamu anamaanisha kudhihirisha furaha, wengine hutumia njia hiyo kuyafuta yale yawaumizayo. Hakika uso umehifadhi mengi sana ya siri kutoka moyoni na kamwe hauwezi kuyaelezea pasina vigezo muafaka. Ndivyo ilivyokuwa kwangu, nilipokosa jibu la kumjibu rafiki yangu Maganga nilijifanya ninafuraha ilhali moyo wangu una aibu isiyo mithilika. Hakika aliniweza, nilitamani iwepo jokofu iliangalau nikapoze joto la aibu ile lakini hapakuwa na kitu hicho. Nilitamani sana kumwambia rafiki yangu angalau akanisaidie kuongea na mrembo yule lakini nafsi ilikataa huku ikinisihi kuwa niende mwenyewe kwani si adabu mwanamume kuzielezea hisia zake mbele ya mwanamume mwenzake ilhali anakila kitu cha kumfuata mwenyewe ampendae ''Staki kutongozewa.'' Nikauli iliyotoka moja kwa moja moyoni, baada ya kuisikiliza kauli ile palepale ni kamwambia Maganga kuwa lazma nimtafute mrembo yule na niyaelezee ya moyoni mwangu.
Kama wafanyavyo vijana walika letu, tulijipongeza huku Maganga akiniambia kuwa huo ndio uanaume nami nikafurahia huku nikimpiga ngumi za begani. Tulichukuana na kuelekea, bwenini kwa ajili ya kujadili jinsi gani nitaweza kuongeanae.
''Sio, hivyo. Tatizo lako wewe bado mshamba sana, mrembo huwa hafatwi kwa style hiyo.'' Alinikosoa Maganga kipindi tupo bwenini tukifanya majaribio mbalimbali ya jinsi nitakavyomfuata mrembo yule kwani kiukweli sikuwa nikifahamu chochote kuhusu msichana.
''Kumbe vipi?'' Nilimuhoji huku nikisogea karibu na sanduku la nguo na kumuacha yeye ilianielekeze.
''Kwanza unapomfuata unatakiwa uhakikishe kuwa uko safi, usikubali kabisa akusome hata kidogo kwani akikusoma tu, tayari ataanza kukudharau.......'' Aliendelea kunielezea mambo kadha wa kadha huku nami nikiandika baadhi japo si yote.
''......aisha yangu yapo mikononi mwako, uzuri wako haunitoki machoni mwangu, kwamara yakwanza tu kukuona nilihisi moyo wangu ukikufuata, nilijitahidi kuuzuia lakini katu haukukubali, sikuwa najua kilicho nipata lakini baada ya kuitazama sura yako kwa umakini ndipo nilipogundua kuwa nusu ya moyo wangu ipo kwako na hicho ndicho chanzo cha kugundua kuwa nakupenda. Kila jina ninalojaribu kukupatia nahisi halito sadifu uzuri wako mrembo, kabla ya kuja hapa nimejaribu kupekuwa majina mazuri mazuri ni yajuayo lakini hakuna hata moja ambalo linawianna na uzuri wako, kama mimi tu nimepata shida kukutungia jina basi sipati picha hao waliyokuzaa sijui walikupa jina gani? Acha niseme tu ukweli, sina uhakika kama wewe ni mtanzania halisi, nahisi utakuwa chotara tena chotara wa huko umalaikani......'' Hiyo ni baadhi tu ya mistari aliyokuwa akinipatia Maganga huku nami nikiinukuu kwenye daftari langu ilinisisahau. Maganga alikuwa anakipaji cha saikolojia ingawa saikolojia si kipaji, hakika sikuwa nikimuelewa rafiki yangu yule kwani mambo yake niliyafananisha kabisa na yale ya watu waliyobarikiwa.