Riwaya : Kichaa

Madame S

Madame S

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2015
Messages
15,035
Points
2,000
Madame S

Madame S

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2015
15,035 2,000
RIWAYA: KICHAA.

Na: ZUBER R. MAVUGO.

N0. 01.

Njaa, iliendelea kulisumbua tumbo lake na kumpelekea kuanza kujipitisha maeneo ya ma'ntilie, huku akiamini kuwa shibe yake ipo mikononi mwao.

"mmh, mmh, mmh, puu. Lalalalala. Toka! Hebu tutolee kichefu chefu hapa," Ni baada ya mtu huyo kufika kwenye moja kati ya migahawa ipatikanayo maeneo ya Igoma ndani ya jiji la Mwanza, sauti moja ya mwanamama muuza mgahawa ndio iliyatoa maneno hayo yenye kuonesha kukereka kwa uwepo wa mtu fulani maeneo yale.

"Bado hunisikii. Eti, eee," Alibwata tena, huku mate yake yakishindwa kujizuia kubakia mdomoni na kujikuta yaki mwaga cheche zilizokuwa zikimfuata kijana ambae maneno hayo yalimuhusu yeye. Kijana yule ni kama hakuwa mwenye kusikia maneno yale, si.. Kwamba hana masikio. Laa! Hasha, bali pindi yalipomfikia yalipita sikio moja na kuelekea jingine.

"We.. Kichaa, unajifanya hausikii, si,ndio? Mnatoka huko makwenu mmefanya uchawi au kuiba mmelogwa halafu mnakuja mjini kuwa kero kwetu. Hebu toka, kabla sijakufanyia kitu kibaya." Mama yule aliendelea kumfukuza yule kijana kwa maneno lakini ndio kwanza kijana yule aliendelea kutabasamu huku meno yake machafu yakipata ruksa ya kuonekana maeneo yale.

"Anhaa! Kumbe unanicheka eti ee! Kwahiyo hapa nafanya upuuzi. Ngoja nikuoneshe," Aliongea mama yule huku miko yake akiwa ameiweka kwenye kiuno chake ambacho amekipiga kanga nzuri yenye maandishi ya bezo.

"Asia?," Aliita mama yule na baada ya yule muitwaji kuitika. Akasema, "Niletee hilo sufuria lenye maji ya moto hapa. Nataka ni muoneshe huyu mbwa," Asia, alitii amri na kuleta sufuria hilo. Kwa kuwa lilikuwa la moto, alishindwa kulibeba bila kuweka kitu cha kuzuia hali ile. Aliamua kuchana boksi na kulitengeneza vizuri kisha akalishikamanisha na sufuria lile, baada ya hapo akaliinua na kumpelekea Mama yule.

"Mwanaharamu mkubwa wewe. Unataka kuleta gundu mida hii.. Mbwa wewe." Alitamka maneno yale, kisha akayasindikiza maneno yake na maji ya moto yaliyompata vilivyo kijana yule.

Masikini, kijana yule, aliangua kilio kama cha mbwa mwizi. Sasa alishindwa kustahimili maumivu aliyonayo na kujikuta akikimbia hovyo mfano wa mbwa aliepigwa jiwe la kichwa.

"Hicho ndicho chakula chako. Mbwa mkubwa we... Na bado, allaaa!! Ukichaa peleka milembe, mjini kila mtu yupo timamu bwana." Maneno yale ya bila huruma ya ubinadamu yaliendelea kutoka mdomoni kwa mama yule bila hata haya. Aliendelea kujisifu kwa kuhisi amemkomesha binadamu mwenzake na kusema.

"Hatorudia tena. Wewe mbwa mwenyewe ukimwagia maji kiasi hicho, harudi tena. Ije yeye binadamu? Na akirudi basi atakuwa na roho ya paka. Halo, halo. Analeta ujiwe mbele ya nyundo. He,he,he,he. Ndo.. Basi tena." Baada ya kutamba kwa maneno yake pamoja na vidole vyake alivyovichezesha huku mkono mmoja akiwa kauweka kiunoni. Alirudi na sufuria lake ndani ya mgahawa huo, kisha akateka maji ya mengine na kuyachemsha.

"Mamaaa! Mammaaa! Nakufa! Nakufaaa. Yalaaaa!" Kijana yule alipiga kelele za uchungu wa maumivu huku akiendelea kukimbia hovyo bila kujielewa. Ingawa alikuwa na minywele mingi iliyochakaa, ngozi yenye ukurutu uliokomaa nakuwa kama machacha, ngozi hiyo ilifunikwa na madaso ambayo zamani yalikuwa nguo. Madaso hayo, yalichanika kila mahali, kwa harakaharaka usingeshindwa kumuita kichaa mtu yule, maana hata usowake, ulipambwa na poda ya jalala aina ya majivu, pamoja na mafuta ya oil.

Naam, alikuwa ni kichaa. Nadhani hata mama yule aliempa adhabu hiyo ya maji ya moto. Alimpa kwa sababu alijua kijana yule ni kichaa. Akashtaki wapi wakati Mahakama yake ni jalala? Akamlilie nani wakati wazazi wake ni mbwa wapatikanao mtaani? Nani wakumsaidia kijana huyo ambae hata hatathamani.

Ni njaa pekee ndiyo iliyompelekea kufanyiwa hivyo. Wakati wewe ukisikia njaa unakimbia mapema nyumbani kwako na kupata chakula, au unaenda mgahawani. Kumbe kuna wengine wanapata adhabu ya kuunguzwa na kutengenezewa majiraha kisa njaa zao.

Masikini, kijana yule aliendelea kukimbia huku maji yale yakiwa yameachia hatamu ya umoto na kusababisha maumivu yasiyo mithilika. Hapohapo jiraha kubwa lililoambatana na uvimbe kutokana na kuunguzwa kwa maji lilijijenga kuanzia, mkono wakushoto, ubavuni hadi mguuni. Aliendelea kukimbia hivyohivyo huku akiita neno 'MAMAA' na wala mama yake asije.

Wengi waliomuöna barabarani walimzomea wengine wa kimcheka na kumthihaki, huku wachache wakimtumia kwenye mada zao. Hakuna hata mmoja aliemsaidia kichaa yule japokuwa alikuwa akiomba msaada.

Alikimbia na kwenda kujitupa jalalani. Hakuwa na mahala pengine pakujisitili zaidi ya jalalani. Huko akakutana na watoto ambao nao walivalia madaso kama yeye huku wakiokota vyuma chakavu, pamoja na kina mama waliochafuka kwa kutafuta chakula ambacho hutupwa jalalani hapo. Watu wale masikini ndio walikuwa msaada wake, walimfuata na kumbeba, ingawa kila walipomvuta nguo, waliishia kubakiwa na kipande cha nguo hiyo kutokana na kuisha kwake. Lakini hilo halikuwafanya waache kumbeba na kumsogeza pembezoni mwa jalala lile.

Walipomsogeza pembeni, mapema tu wakaanza kumpatia huduma ya kwanza ya kishamba. Bora wangekuwa na asali ilikumpaka huenda ingesaidia, hawakuwa na dawa yeyote zaidi ya mchanga uliopatikana maeneo yale ya jalala. Walimpakaa mchanga ule wenye chembechembe za uchafu kisha wakamuhitaji apumzike iliasiendelee kuyahisi zaidi maumivu.

"Mpumzishe kwa lazima." Aliongea mama mmoja aliekuwa amesimama huku akiendelea kukiadhibu kichwa chake kwa kukikuta kutokana na muwasho aliokuwa akiupata;muwasho wa mmba pamoja na chawa katili.

"Sawa, maana inabidi apumzike tu." Alijibu mama mwingine ambae yeye alikuwa bize na kufukuza inzi maeneo ya kidonda. Kisha mama yule akaiacha kazi ile kwa nukta, na kupeleka mkono wake hadi kwa maeneo ya shingoni mwa kichaa yule ambae sasa alikuwa akipiga mikono yake chini pamoja na paji lake ilikupolea maumivu kama alivyodhani. Mama yule, aliigusa gusu shingo ya kichaa yule iliyojaaliwa ukurutu mgumu, na nikama alikuwa akitafuta mshipa fulani. Hata alipoupata aliuzimisha kiustadi wa hali ya juu na palepale kichaa yule alipoteza fahamu.

Ingawa njia ile ina madhara, lakini ndio njia pekee iliyopatikana kwao. Hawakuweza kumpeleka mgonjwa hosipitali akachomwe sindano ya ganzi iliasihisi uchungu au sindano ya usingizi kutokana na kutokuwa na pesa. Walilitambua hilo na walijua wazi hata kama wangempeleka hospitali, asingepata msaada wa aina yoyote ile zaidi ya kuangaliwa kwenye benchi kwa kebehi kama inzi mla mavi. Kwao, waliona njia pekee ya kutuliza maumivu ni kumfanya mgonjwa azimie kwa muda. Kumbe wakati wewe unapopata jiraha na kupigwa ganzi, au sindano ya usingizi. Kuna wengine ambao hata hiyo sindano hawaipati badala yake wanapata nyenzo za hatari.

"...we mama, leta hiyo siso kabla sijakuharibia hapa." Ni sauti ya ukali iliyotoka kinywani mwa mtoto mwenye umri wa miaka kumi na nne, maeneo ya jalala hilo. Sauti hiyo isiyojali utofauti wa miaka iliendelea kukoroma. Mama alieambiwa atoe chuma chakavu, alionesha kama kutosikia sauti ile ya dharau tena ukizingatia mtoaji wa sauti ile ni mtoto ambae anauwezo mkubwa sana wa kumzaa. Alifikiria endapo atampa chuma kile chakavu basi ataikosa pesa il-hali nae anashida chungu nzima, hivyo aliona uamuzi wa yeye kuwa nunda ndio pekee utamsaidia mbele ya mtoto yule.

"..we maza nunda sio? Nakwambia leta hapa hiyo siso." Aliendelea kutoa amri mtoto yule utadhani anaongea na mtoto mwenzake kumbe ni mama mzima. Mtoto yule alikuwa ana ngozi chafu iliyojaa ukurutu;ngozi ambayo hakuivika shati kutokana na ukosekanaji wa mashati juu ya hali duni aliyonayo. Huku chini akiwa amevaa kaptula iliyotoboka na kupelekea makalio yake yaliyopauka na kupata sugu kutokana na kukaliwa bila heshima yaonekane vilivyo pasina uficho.

"We... Mtoto wa mbwa, hebu kuwa na adabu pamoja na heshma. Wakubwa husalimiwa mjinga wewe, na sio kutolewa amri za siso tu." Aliongea mama yule kauli iliyohifadhi hasira za wazi juu ya kuchukia amri za mtoto yule mdogo ambae kwa kumuangalia tu. Anashindwa hata kumfananisha na watoto wake kutokana na umri mdogo alionao.

"Afu.. We, maza takuharibia sasa hivi. We sema kama hutaki kunipa hiyo siso uone kama siichukui kwa nguvu. Heshima unaijua wewe? Kama ungekuwa na heshima ungekuja huku jalalani? Acha ujinga. Wenye heshima na adabu wapo majumbani kwao wakipikia waume zao na kuosha watoto wao. Wewe upo huku jalalani halafu unaitaji heshima, sijui adabu. Hebu lete hiyo siso, mpuuzi mkubwa."

Mtoto yule alimkwapua mama kile chuma chakavu, kwa kuwa mama yule hakukubaliana na ile hali ya kunyakuliwa kirahisi chuma ambacho angekiuza na kupata pesa. Ndipo alipoamua kumvaa mtoto yule na kumng'ata vilivyo maeneo ya tumboni kwa kutumia meno yake yasioujua mswaki badala yake yanakijua chakula chajalala. Chakula ambacho kina bakteria waliojificha na wanaoonekana bila hata hadubini.

"Unaning'ata. Ayaah! Niachie mbwa wewe." Alibwata mtoto yule baada ya meno ya mama kuzama vilivyo kwenye ngozi yatumbo lake. Mama yule alisikia kilio cha mtoto yule, lakini hakini hakuhtaji kumuachia mpaka hapo atakapo hakikisha karejeshewa chuma chake iliakauze na kupata pesa.
Hapo mtoto yule akajihami kwa kumpiga mama yule na kile chuma kichwani. Kitendo kile kilimpelekea yule mama kuanguka chini huku damu nyingi zikimtoka na palepale alipoteza maisha.

Hakuna aliebaki maeneo ya jalala lile. Si, wakinamama waliokuwa wakimsaidia kichaa pembezoni mwa jalala, wala machokoraa waliokuwa wakijitafutia riziki. Wote walikimbia ilikuepuka kubambikiziwa kesi na maafande. Hata yule mtoto nae alitimka. Hapo ulibaki mwili wa mama yule. Pamoja na kichaa aliekuwa pembezoni.

Masaa kadhaa yalipita, hatimae yule kichaa alizinduka, kumbe muda huo ndio maafande walikuwa wanafika kwenye eneo la tukio. Walimbeba mama yule na kumbwaga kwenye gari kisha wakamchukua yule kichaa yule na kumsukumia ndani ya gari bila kujali jeraha lake.

"Afande, huyu mjinga ndio tuna mbebesha kesi ya mauaji." Aliongea afande mmoja.

"Huyu lazma itaijibu serikali, kwanini ameua." Alipokeza afande mwingine. Kisha maafande hao wakaingia wote kwa pamoja ndani ya gari.

Yule kichaa alisikilizia maumivu maradufu ya alivyo yapata kabla, kusukumwa na maafande wale kulimpelekea yeye kutonesha jeraha lake na kuyahisi maumivu makali yasiyo na ganzi. Alipiga ukelele kila maumivu yalivyozidi kuongezeka.
 
Madame S

Madame S

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2015
Messages
15,035
Points
2,000
Madame S

Madame S

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2015
15,035 2,000
RIWAYA: KICHAA.

Na: ZUBER R. MAVUGO.

N0. 02.

ILIPOISHIA.

Masaa kadhaa yalipita, hatimae yule kichaa alizinduka, kumbe muda huo ndio maafande walikuwa wanafika kwenye eneo la tukio. Walimbeba mama yule na kumbwaga kwenye gari kisha wakamchukua yule kichaa yule na kumsukumia ndani ya gari bila kujali jeraha lake.

"Afande, huyu mjinga ndio tuna mbebesha kesi ya mauaji." Aliongea afande mmoja.

"Huyu lazma itaijibu serikali, kwanini ameua." Alipokeza afande mwingine. Kisha maafande hao wakaingia wote kwa pamoja ndani ya gari.

Yule kichaa alisikilizia maumivu maradufu ya alivyo yapata kabla, kusukumwa na maafande wale kulimpelekea yeye kutonesha jeraha lake na kuyahisi maumivu makali yasiyo na ganzi. Alipiga ukelele kila maumivu yalivyozidi kuongezeka.

ENDELEA.

Maafande wale walipata kero kutokana na makelele ya kichaa yule kufuatia maumivu aliyokuwa akiyapata. Hakuna kati yao aliyoyajali maumivu yake pamoja na ndonda ambalolilianza kutoa majimaji na damu, bali waliishia kukereka na sauti ya maumivu ya kichaa yule.

"Kimya! Allaaa! Nani unaemuimbia huo wimbo wako?" ni sauti kutoka kwa afande. Sauti iliyoambatana na rungu kali lililotua kwenye ugoko wa kichaa yule. Hakika aliyahisi maumivu mengine ambayo hakuwahi kuyawazia.

Badala apunguze kilio, hapo aliongeza na kupigwa rungu la kwenye goti, alipolia tena alishushiwa moja la kichwa na hapohapo akazimia.

Maafande wale wasio na huruma walianza kujipongeza kwa kazi ya kudhibiti ukelele wa kichaa kwa kumpiga hadi akazimia. Kisha kwa mbwembwe wakawasha gari lao na kuianza safari ya kuelekea kituoni.

Ni barabara ya buzuruga. Gari moja kubwa la mizigo lilionekana kukatiza eneo lile, kutoka maeneo ya mabatini na kuelekea maeneo ya igoma. Maafande wale ambao hawakuwa makini katika uendeshaji wao waliweza kukumbana nalo mbele hatua kadhaa. Kabla hawajagongana dereva wa maafande alilipiga kona gari lake na kulielekeza upande wa raia waliotembea kwa miguu, ileanatafuta breki kabla hata hajapiga alimgonga mpita njia mmoja na kumsababishia kifo palepale. Breki zilikubali huku damu za mpita njia huyo zikikipamba kioo cha gari la maafande.

Raia wenye hasira kali waliifuata gari hiyo na kuiadhibu kwa mawe. Huku wakihitaji kuwashusha maafande waliokuwamo ndani ya gari lile.

Walifanikiwa kuwatoa maafande wale na kuwaadhibu huku nyuma nako walimvuta yule kichaa na kumjumuisha kwenye mkumbo huo wa kipigo. Hazikupita hata dakika tano gari jingine la maafande lilifika maeneo yale na walioshuka walitawanya raia kwa kupiga risasi juu. Kisha kuwaokoa waliokuwa wakipigwa na raia wenye hasira kali.

Walimchukua tena kichaa yule nakumpeleka hosipitali pamoja na wale maafande wengine kufuatia kipigo cha raia.

"Hakikisheni mnafanya juhudi zenu zote ili huyo kichaa apone."

"Usijali, tupo kwa ajili hiyo. Chamsingi ni nyie kutulia tu."

"yaani, dokta hakikisha unatumia uwezo wa hali ya juu maana serikali ina muhitaji sana huyo, na ndio mtuhumiwa wa kesi ya mauaji ya watu wawili."

"Usijali."

walikaa kusubiria hali ya kichaa yule ilivyoendelea na hiyo ni baada ya maiti ya yule mama pamoja na yule aliegongwa gari na maafande kupelekwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti kwa ajili ya upelelezi. Waliendelea kusubiri huku wakiomba kichaa yule apone.

"Huyu, inabidi tujitahidi hata kuhonga iliatibiwe kwa taaluma ya juu maana akifa tu. Hakuna muda wa kuanza kupeleleza wahalifu, chamsingi huyu tunampa kesi za mauaji ya watu wawili." aliongea afande kipara huku akisikilizwa kwa umakini na wenzake watatu.
Palepale maafande wale walihamaki, na hiyo nibaada ya mlango aliyomo kichaa yule kufunguliwa na kutoka daktari.

"Dokta, anaendel..."

"Njooni ofisini."

walimfuata huku pumzi zao zikiwa juu juu na mapigo ya moyo kuwaenda kasi utadhani wamepewa taarifa za msiba.

Dokta aliwaambia kuwa mgonjwa wao, hali yake bado tete na mpaka muda huo hakuwa amezinduka. Akawapa ruhusa wakaendelee na kazi kisha watarudi jioni.

Waliafiki kisha wakarejea kituoni kwao pamoja na wale maafande ambao walipata majiraha lakini hawakuumia kufuatia hasira za wananchi.

Walipofika tu. Cha kwanza walifungua faili la kesi ya mauaji.

"Huyo mpuuzi lazma ashughulikie kesi zote. Chamuhimu ni yeye kupona tu. Sisi ndio maasikari wa nchi hii. Naipenda nchi yangu kwa sababu inanipa uhuru wa kukaa juu ya sheria hata kama na makosa. Sawa nyie ndio mmegonga hadi mkaua ila kesi lazma imuangukie huyo mjinga, hata yule sijui mama aliekufa kwa jalala, mjinga huyu ndie atatueleza kwanini amemuua. Lazma akubali labda kama sina kofia ya uafande nja gwanda la uafande." Aliongea afande kipara huku akimsimamia yule mwenye jukumu la kuandika faili la kesi.

"Mtu mwenyewe hana muelekeo wa kimaisha. Bora tumuokoe kwa kwenda kunyongwa au kufungwa kifungo cha maisha. Ale bure alale bure, avae bure, tena bila kufanya kazi ngumu. Huoni kama tumemuokoa na maisha ya jalalani." Aliongea afande Dani na kuwafanya wenzake kuangua kicheko.

Raia waliishia kunong'ona juu ya uonevu waliofanyiwa na kulalamikia jeshi la polisi lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa zaidi ya jambo hilo kuongelewa rediöni tena mara moja tu.

Ilipofika majira ya saa moja usiku. Wale maafande walirudi hosipitali kwa ajili ya kujua hali ya mtuhumiwa.

kama hakuna uthibitisho basi yule aliekamatwa huitwa mshukiwa. Lakini maafande hawa walimpa jina la mtuhumiwa.

Walionana na daktari kisha akawapatia maendeleo ya mgonjwa wao na kuwahitaji waendelee kuwa na subra. Hawakuwa na jinsi maafande wale zaidi ya kuondoka, lakini walimsihi daktari ajitahidi kuhakikisha mgonjwa anapona kwa gharama yeyote ile.

Walirudi mpaka kwenye kituo chao, baadhi yao walilala humohumo. Huku wengine wakiendelea kuburudika na vileo pasina kujali kofia na mikanda ya jamuhuri.

"Afande.. Afande.. Naombeni msaada. Wanamuua mdogo wangu." Ni sauti ya binti mmoja mwenye umri wa miaka kumi na sita, sauti hiyo iliambatana na nukta za mihemo kutokana na mbio alizotoka nazo binti yule. Ukimuangalia, hutotamani kurudia tena kutokana na uchafu uliomjaa kwanzia usoni hadi kwenye mafundo ya miguu. Kuachilia mbali nguo zake ambazo zilitia kinyaa kutokana na kuanguka mara kadhaa kwenye mitaro ya maji machafu na kuzalisha harufu kali,lililoshindwa kustahimili pua za maafande. Vilevile, binti yule alinuka jasho pamoja na uchafu wa kike kutokana na kushindwa kujitunza. Si kwasababu hapendi, bali ni kutokana na kukosa matunzo. Kama usipoisikia sauti yake basi lazma uwe na mashaka usijue huyo binti ni msichana au mvulana.

"Wewe chokoraa! Hebu kuwa naadabu."

"Hapana, afande. Mdogo wangu wanamuua tafadhali naombeni msaada." Aliongea binti yule kwa sauti kavu, ambayo hata kutoka ilitoka kwa shida. Maafande wale kwao waliona ni kama kero kwani walikuwa bize na mambo yao. Halafu ukizingatia binti yule alikuwa ni chokoraa.

Binti yule hakuchoka aliendelea kuomba. Sasa alishuka hadi chini na kupiga magoti huku akiishikiria yunifomu ya afande kipara na kumuomba.

"Hebu toa uchafu hapaa! Mwanaharamu mkubwa. Nenda kamshike mama ako mavazi yake nasio kunichafulia gwanda langu la jamuhuri kwa harufu yako." Alifoka afande kipara huku kauli yake akiisindikiza na msukumo wa mguu uliomtoa binti yule na kumtupa pembeni.

Masikini, binti yule chokoraa, alivyosukumwa kumbe alijibamiza. Tayari damu zikawa zinamchuruzika. Alianza kulia na kukata tamaa. Lakini alipokumbuka kuwa msaada pekee ni mapolisi. Hakuishia hapo, aliendelea kuwaomba hivyohivyo. Sasa afande kipara alichukia zaidi na kufungua mkanda wake kisha akamsogelea binti yule. Palepale akautua maungoni mwa binti yule. Kujigaragaza na kutoa ukelele wa majonzi ndivyo vilivyoashiria maumivu ya binti yule. Hapo kipara akamvutashati binti yule nakujikuta akibakiwa na kipande cha daso kutokana na kuisha kwa nguo ya yule binti.

"Haa! Kumbe wewe ni wakike?" Alishangaa kwa swali kichaa yule. Nahiyo nibaada ya shati labinti kuchanika na kuzifanya chuchu zake zilizosimama kuonekana machoni mwa kipara. Hapo yule binti akaona aibu nakuanza kuficha maeneo ya maungo yake, lakini tayari alichelewa kwani maafande wote tayari walishayaona maungo yake mazuri na yenye kupendeza.

"Yaani. Mie, nihangaike usiku kutoa pesa kwa malaya wakati nyie wa bure mpo! Tena mnafaa kuliko hata wale malaya." Aliongea afande kipara. Bila hata aibu kwa binti yule ambae asingeshindwa kumtofautisha na mwanae, huku wenzake wakimpongeza na kumpa hongera kwa mbuzi kufia buchani.

Alitoa, amri binti yule abebwe na kuingizwa sero kisha akamfuata humo humo na kumuingilia binti yule bila hata kujali picha ya raisi wa jamuhuri ambayo ilikuwa juu ya ukuta wa kituo. Alimtoa ubikira binti yule, na kumfanyia yale yote ilhali anajua wazi kuwa yeye ni muathirika wa virusi vya ukimwi. Ambavyo alivipata miaka kadhaa iliyopita.

Binti yule alishindwa kuvumilia aibu ile, alishindwa afiche damu, afiche sura, au chuchu zake iliaendelee kujenga mjengo waheshima. Kutokana na kuingiliwa bila ridhaa yake alijikuta akiumia sana na kichwa kilimgonga hadi kuzimia. Maafande wale walimchukua na kumuweka kwenye gari lao ambalo wamelipewa na serikali kutokana na makato ya mishahara ya wananchi walipiao kodi. Bila kujali hilo, waliyatumia mafuta ya gari lile, mafuta ambayo ukiyatathmini ni pesa za wananchi wa kipato cha chini, na kisha wakaenda kumtupa binti yule pembezoni mwa mto wa mchafu kuoga. Masikini binti yule, alifanyiwa yale kutokana na kudhani haki ipo kituoni. Sasa hakujua kama mdogo wake atakuwa hai au ameshauawa.

Maafande wale, walimuacha yule binti maeneo ya hatari kama yale, kisha moja kwa moja wakarejea kituoni kwao na kuendeleza mambo yao. Wakasahau hitaji la binti yule, wakasahau shtaka lake, na maumivu aliyokuja nayo.

Kipara alianza kuwahadithia wenzake utamu alioupata, kipindi anafanya ufirauni wake na wenzake walicheka kila alipoweka nukta. Waliendelea kujadili juu ya upuuzi wao mbele ya picha kubwa iliyokuwa maeneo yale. Picha ya rais wa Tanzania.

Huku nako binti yule waliomtupa, alipatafahamu na kuhtaji kuinuka kwenda kumsaidia ndugu yake lakini alijishangaa baada ya kukabiliwa na maumivu ya kichwa, aliendelea kujikaza kila alipokumbuka adha aipatayo mdogo wake. Lakini alikumbana na mkinzano wa maumivu makali sehemu zote za mwili wake hasa sehemu zake za siri. Ndipo aliporudisha kumbukumbu kuwa alikuwa amebakwa.

Binti yule, hakuwa na uwezo wa kuamka kutokana na maumivu aliyo yapata. Alitamani apate msaada wa kwake, lakini hakuna aliemjali. Kila alipomkumbuka mdogo wake, akakumbuka unyama wa mapolisi. Aliishia kuendelea kulia.

Nyanyuka nenda kapambane, hata ukikaa na kulia hakuna msaada utakaokuijia. Jikaze wewe ni mwanamke wa shoka. Ni sauti iliyomuijia binti yule ndani ya nafsi yake na kumpa ujasiri wa hali ya juu. Aliinuka kwa kujipepesua hivyohivyo, taratibu akajisogeza kwenye mto ule ujulikanao kama mchafu kuoga. Mto upatikanao maeneo ya buzuruga. Akanawa uso wake, na akavua madaso yake kisha akaoga maji yale machafu, ilikuondoa damu zilizomuenea kisha akayafua madaso yake na kuyavaa kwa mara nyingine.
 
Madame S

Madame S

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2015
Messages
15,035
Points
2,000
Madame S

Madame S

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2015
15,035 2,000
RIWAYA: KICHAA.

Na: ZUBER R. MAVUGO.

N0. 03.

ILIPOISHIA.

Binti yule, hakuwa na uwezo wa kuamka kutokana na maumivu aliyo yapata. Alitamani apate msaada wa kwake, lakini hakuna aliemjali. Kila alipomkumbuka mdogo wake, akakumbuka unyama wa mapolisi. Aliishia kuendelea kulia.

Nyanyuka nenda kapambane, hata ukikaa na kulia hakuna msaada utakaokuijia. Jikaze wewe ni mwanamke wa shoka. Ni sauti iliyomuijia binti yule ndani ya nafsi yake na kumpa ujasiri wa hali ya juu. Aliinuka kwa kujipepesua hivyohivyo, taratibu akajisogeza kwenye mto ule ujulikanao kama mchafu kuoga. Mto upatikanao maeneo ya buzuruga. Akanawa uso wake, na akavua madaso yake kisha akaoga maji yale machafu, ilikuondoa damu zilizomuenea kisha akayafua madaso yake na kuyavaa kwa mara nyingine.

ENDELEA.

. Hapo sasa akaanza kutembea kutokea buzuruga mpaka maeneo ya mabatini kwa ndani ndani. Ndipo alipokatiza sehemu na kukuta watu wamejaa. Nywele zilimsisimka na kuingiwa na uoga. Aliamua kwenda kutazama nini kilichowajaza watu wale. Hakuyaamini macho yake baada ya kukuta mwili wa mtoto umefunikwa shuka jeupe na kuachiwa maeneo ya kichwani kwa ajili ya kutambuliwa.

Aliangua kilio cha hasira lakini hakuwa na jinsi mdogo wake tayari alikuwa amekwisha fariki. Wananchi walimsaidia na kwapamoja wakazika.

Upande wa hosipitali mgonjwa aliendelea vizuri na hata zilipopita wiki mbili. Hapo maafande walipatiwa mtuhumiwa wao na kumpeleka moja kwa moja, mahabusu.

Masikini, walimuadhibu kichaa yule pasina kujali hali aliyokuwa nayo. Walichukuwa plaizi na kumfinya sehemu mbalimbali za mwili wake huku wakimng'ang'aniza akili kufanya mauaji.
Kichaa yule alishindwa kuvumilia maumivu makali kama yale. Aliamua kukubali kuwa yeye ndie aliemuua yule mama kule jalalani, na yeye ndie aliemgonga yule mtu na gari, hali yakuwa ukweli unajulikana kuwa mapolisi ndio walimgonga na gari yule mtu.

Alipokubali kukili ndipo wakamrudisha mahabusu ilikusubiria siku ya kesi mahakamani.

Upande wa yule binti, hali yake ilizidi kuwa dhoofu. Kila alipopita hakuwa na msaada na wala hakutamani kuomba msaada. Upungufu wa damu katika hospitali ya bugando ndio ulimfanya nae akajitolee damu iliangalau apate kuokoa maisha ya watu kutokana na kushindwa kuokoa ya ndugu yake. Hakuiona thamani yake katika hii dunia, alitamani ardhi ipasuke na aingie ndani yake lakini kwa muda huo ardhi haikufanya alichohtaji.

"Samahani dada. Damu yako inaonesha wazi kuwa wewe ni muathirika wa virusi vya ukimwi. Hivyo haiwezekani kuwekwa katika mwili wa binadamu mwenzako." Ni maneno ya daktari aliewachukuwa vipimo wote walioenda kujitolea kwa hiyari damu zao.

Binti, alichoka. Palepale alianguka chini na kuzimia. Alikaa masaa kadhaa ndipo alipozinduka.

Aliwakumbuka wazazi wake walivyo mpenda yeye na mdogo wake, akaikumbuka ajali ya M.V, bukoba iliyowatenganisha wao na wazazi wao. Akakumbuka jinsi walivyolifakamia jiji la mwanza kama watoto wa mtaani kutokana na kukosa msaada. Akakumbuka siku ambayo alivamiwa na watoto wa wakoma na kuhtaji kumuingilia kwa lazma. Siku hiyo inamuuma sana maana ndiyo iliyomfanya ampoteze mdogo wake wapekee pale mdogo wake alipoingilia ilikumkinga dada yake asibakwe. Watoto wa wakoma walimuacha kwanza dada mtu na kumfuata mdogo mtu na kuanza kumshushia kipigo pamoja na kumshambulia kwa nyembe zao.

Akakumbuka pia pale alipopata akili ya kwenda kutafuta msaada kituoni. Palepale alinyanyuka kwa hasira. Ingawa alikuwa na maumivu, lakini alitembea utadhani hana maumivu. Alipita sehemu na kukutana na muuzaji wa genge. Aliazima kisu kisha akaenda moja kwa moja hadi kituoni.

Alimkuta afande kipara peke yake. Pamoja na yule mtu asiejielewa(Kichaa). Alipofika, alipokelewa kwa dharau na maneno ya kashfa. Kitendo bila kupoteza muda alimchoma kisu Afande kipara. Alimtoboa toboa mara kadhaa, kiasi cha yeye kujawa na damu. Maeneo yote ya mwili.

"Dada, umeua?" Ni sauti ya kichaa yule.

"Ndio, nimeua naninahitaji kufia gerezani. Sioni haja ya kukaa na mateso ambayo hayana hukumu. Bora nikahukumiwe huko na nife kifo kizuri cha kunyongwa. Nahitaji kufa, nifunge pingu na uniweke mahabusu, usihofu. Mahakamani nitakili ufanyaji wa tukio hili na wewe sitokufanya chochote bali utakuwa shahidi wa kesi hii ya mauaji." Aliongea binti yule maneno ya ukali. Huku akidhihirisha wazi kutokuogopa lolote litakalomkuta.

"Una umri mdogo sana. Hufai kufungwa. Nenda kimbia kabisa wala usiwahi onekana machoni mwangu. Bado unahitaji kukamilisha ndoto zako. Usinione kichaa ukadhani sipo timamu. Leta hicho kisu kisha utoweke maeneo haya kabla haujakutwa hapa." Aliongea kichaa yule, maneno yaliyomfanya hadi binti yule ashangae sana.

"Hapana, nilipouhitaji msaada, haukuja. Leo, siuhitaji ndio ujilete. Kaka umechelewa kunisaidia, nimedharirika, nimenyanyasika. Hadi nimeambukizwa virusi vya ukimwi. Ndugu yangu amefariki kisa haki yangu, mimi nimeharibiwa maisha kisa kutafuta haki. Sioni haja ya kuishi bora nikanyongwe iliniende huko haki ilipo. Sitaki nikuingize kwenye matatizo kaka yangu." Aliongea binti yule.

Binti yule aliendelea kulalamika na alichohtaji kwa mda huo ni kunyongwa tu.

"Dada yangu, hii dunia imebeba mengi na yenyekujificha machoni mwa watoto wa dogo. Kadri unavyozidi kukuwa ndivyo unavyozidi kuyaona. Huna haja ya kuamua maamuzi ya mbali wakati hauyajui hata ya kesho. Bado unahaja ya kuyaona ya duniani iliupate kujifunza, nakuomba nipatie hicho kisu kisha utoweke hapa." Aliongea kichaa huku akipeleka mkono wake kupokea kisu ambacho kimeng'ang'aniwa na dada yule.

"Kaka, yadunia yanaumiza sana. Yameshanichosha. Bora nife, dunia gani hii iliyojivika ngozi ya simba, dunia inayomuwinda masikini utadhani swala porini. Hata kama nikiendelea kuishi nitaenda wapi mimi? Hakuna! Hakuna! Mama, baba, mdogo wangu wamesha tangulia kule haki ilipo. Na uhakika wameniandalia makazi mema na sasa wako wananisubiri."

"Usiwe mdhaifu hali yakuwa wewe ni msichana. Wanawake huvumilia magumu na mepesi, mengi na machache. Na wako radhi wavuke mabonde na milima ya shida. Hautokuwa mwanamke jasiri kama unaogopa yaliyomo kwenye hii dunia. Naitwa MAVUGO." Aliongea maneno yale yaliyomfanya yule binti akose nguvu za kukishikiria kisu na hapo ndipo kichaa yule alipokinyakua.

"Nashukuru sana kwa kuniokoa. Nitakukumbuka milele, sitoacha kulitaja jina lako. Mimi naitwa.. Aisha Mapuya. Nashukuru sana kaka yangu." Aliongea binti yule huku machozi yakimtoka.

"Milima inatabia ya kukaa sehemu moja, lakini binadamu hana tabia hiyo. Ndio maana wanasema 'Milima haikutani binadamu huk..."Kabla hata hajamalizia kauli yake, ving'ora vilisikika kwa mbali na wakagundua wazi kuwa maafande wanakuja.

"Kimbia.. Pita huku.. Mungu akuongoze." Ni sauti ya kichaa yule aliejitambulisha kwa jina la Mavugo.

Binti yule, alimuangalia sana kichaa yule na alikalili alama kutoka kwa kichaa yule kisha akamuaga na kutimka.

Ile ameondoka tu. Palepale maafande wakawa wamefika. Hawakuamini baada ya kumkuta mkubwa wao amelala chini huku majiraha yaliyoonekana vizuri kwenye mwili wake. Yakiwachekea na kuwadhihaki. Walipo tupa macho yao pembeni walimuona kichaa ameshikiria kisu chenye damu.

Walijiuliza maswali mengi ya siyo na majibu kuhusu kichaa yule alipopatia kisu kile, na alitokaje mahabusu hadi kuua.

Alipoona wamemkodolea sana macho, alikitupa kisu kile na kunyoosha mikono juu kamaishara ya kujisalimisha mbele ya maafande wale.

Walimpokea, na kumdunda vilivyoutadhani hukumu imeshatolewa mahakamani.

Hapo sasa kichaa yule akawa na kesi tatu za mauaji. Alipelekwa mahakamani na kesi yake ilikuwa ngumu sana. Alipopewa muda wa kujitetea hakuna alichosema zaidi ya kuihtaji hukumu yake.

"Hakimu, ndio nimeua. Hili swala halihtaji ushahidi wowote, nimekili mwenyewe na ninahitaji hukumu. Naombeni msipoteze muda nihukumuni." Ni kauli alizotoa pale alipopewa fursa ya kujitetea. Hakika alishangaza sana mtuhumiwa huyo asieogopa hukumu kali itayomfuata.

"Kiukweli mtukufu hakimu. Hakuna sababu iliyonifanya niue. Lakini niliamua kuua kwasababu nilijisikia kuua tu. Nilimuua yule mama kule jalalani, nikamgonga na gari yule kijana njiani, na mimi huyohuyo nilimchoma visu yule Afande tena ndani ya kituo chake. Naombeni hukumu kabla sijajisikia tena kuua. Tafadhali." Kichaa yule alizidi kuitikisa mahakama ile kwa majibu yakujiamini kiasi kile.
Kesi ile ilikuwa na mashahidi wa kugushi, ambao walisisitiza kuwa wao walishuhudia mauaji ya Kichaa yule.

Mwisho wa siku kichaa alihukumiwa kifungo cha maisha jela, hakupewa adhabu ya kazi ngumu kama wengine kutokana sijui na kifungu gani cha sheria alichokidokeza hakimu mahakamani pale.

"Hakimu.. Nataka hukumu ya kunyongwa! Mbona hujanipa hukumu, badala yake umenipa raha? Hata huko gerezani nikijisikia kuua nitaua tu." Alibwata kichaa yule. Kipindi anatolewa kwa ajili ya kwenda kutumikia hukumu yake. Hakimu alibaki ameduwaa na hapo ndipo akaanza kuwa na wasiwasi na akili za mtu yule. Lakini hakuwa na jinsi kwakuwa tayari hukumu imeshapita.

+ + + + +

Aisha mapuya, alijiegesha chini ya mti mmoja huku akitafakari jinsi ambavyo ameokolewa kwenye kesi ya mauaji tena na mtu asiyemjua. Alikumbuka jinsi mtu yule alivyokuwa akimsihi kutokukata tamaa. Lakini alibakiwa na mawazo mengi sana yaliyoendelea kutembea kichwani mwake. Akiwa katika mawazo yale, kichefuchefu kilimuijia ghafla na kujihisi kutapika.

Mmh! Mbona sina ugonjwa?, au mimba? Lakini kama mimba..! Mbona sijatembea na mwanamume yeyote. Hii itakuwa malaria tu, au uchovu. Alijiuliza na kujijibu maswali mfululizo aliyoyatengeneza kichwani mwenyewe.

Kichefu chefu kile kiliambatana na kizunguzungu kilichomfanya aione dunia jinsi ambavyo hutumia masaa ishirini na nne kukamilisha mzunguko wake. Alikishika kichwa lakini hiyo haikuwa msaada kwake. Hapo akapatahamu ya kutapika na kabla hata ya kuhitaji matapishi yakatoka kwa makusudi. Alilala chini ya mti ule na baada ya kuamka ndipo alipogundua maumivu ya kichwa aliyonayo. Alifikiria kwa nukta kadhaa, kilichomfanya aumie kichwa namna ile nakung'amua kizunguzungu alichokuwa nacho masaa kadhaa. Alipokumbuka kichefuchefu na kutapika ndipo alamu ya hatari ikagonga kichwani mwake na kuanza kumwambia kuwa, zile dalili alizozisoma kipindi kile anasoma shule za kuhusu mimba ndizo alizo nazo. Lakini aliendelea kuidharau alamu ile kwa jikosoa nakujiona kuwa hajawahi kufanya mapenzi kwa hiyari bali alifanya kwa lazma hivyo asingeweza kudhurika. Alihisi huenda atakuwa na malaria maana pia hizo ni dalili za malaria.

Baada ya kufikiri kwa muda kadhaa, akajinyanyua na kusimama kwa ajili ya kuondoka maeneo yale. Aliposimama akili ilikosa pakumpeleka, kila alipopawazia aliona hakutakuwa na msaada kwake. Bila hiyari yake alijikuta akichukuliwa na miguu moja kwa moja ikaanza kumuongoza maeneo ya Igoma, alipofika. Wazo la kuomba kazi lilimwijia nakuona nibora akaombe kazi tu tena za ndani.

Alifika nyumba moja na kufunguliwa na mlinda geti la nyumba hiyo.

"Unashida gani?"

"shikamoo..."

"Sina shida nayo. Kuwa nawewe utazipata nyingi tu hadi utazichoka baada ya kugundua zinasumbua akili bila faida. ...we sema shida yako tu."

"Samahani kaka yangu kama nimekukwaza. Mimi ninaomba kazi."

"Kwa mimi naajili msichana wa kukaa nami muda wote katika geti hili, msichana wa kunitengea maji yakuoga, msichana wa kunipikia chakula na msichana wakuni... Wakuni..." Akasita kidogo baada ya kuona bosi wake akijongea maeneo yale kutoka ndani. Kishaakaendelea. "tuachane na hayo. Pia bosi wangu nae anatoa ajira muda huo huo. Anaajiri mfanyakazi wa kuosha vyombo, kusafisha ndani, kufuanguo zake na za mmewe, na mengineyo. Sasa chaguo ni lako kati ya kuajiriwa na mimi au na bosi wangu."

ITAENDELEA.
 
Madame S

Madame S

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2015
Messages
15,035
Points
2,000
Madame S

Madame S

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2015
15,035 2,000
RIWAYA: KICHAA.

Na: ZUBER R. MAVUGO.

N0. 04.

ILIPOISHIA.

Alifika nyumba moja na kufunguliwa na mlinda geti la nyumba hiyo.

"Unashida gani?"

"shikamoo..."

"Sina shida nayo. Kuwa nawewe utazipata nyingi tu hadi utazichoka baada ya kugundua zinasumbua akili bila faida. ...we sema shida yako tu."

"Samahani kaka yangu kama nimekukwaza. Mimi ninaomba kazi."

"Kwa mimi naajili msichana wa kukaa nami muda wote katika geti hili, msichana wa kunitengea maji yakuoga, msichana wa kunipikia chakula na msichana wakuni... Wakuni..." Akasita kidogo baada ya kuona bosi wake akijongea maeneo yale kutoka ndani. Kishaakaendelea. "tuachane na hayo. Pia bosi wangu nae anatoa ajira muda huo huo. Anaajiri mfanyakazi wa kuosha vyombo, kusafisha ndani, kufuanguo zake na za mmewe, na mengineyo. Sasa chaguo ni lako kati ya kuajiriwa na mimi au na bosi wangu."

ENDELEA.

Hapo, Aisha akatabasamu, kidogo baada ya kugundua vituko vya mlinda geti yule. Muda huohuo akafika yule bosi.

"Shikamoo dada.."

"Marahaba. Unashida gani?" Aliuliza baada tu yakuitikia salamu. Huku kwa muda huo mlinzi wa geti akiwa amenywea na kuendelea kuliadhibu rungu lake, kwa uoga wa bosi.

Sijui ni mwambie nahitaji kazi au nimuombe msaada tu. Mmmh! Nikimuomba msaada hauwezi kunisaidia, hata hii kazi kweli nitaifanya kwa hali hii?.

"We binti ni kiziwi?" Aliuliza yule bosi na hapo ndipo Aisha akagutuka kutoka mawazoni ghafla bila kufikiria akaropoka.

"Hapana. Mi sijaua." Jibu lake lilikuwa na maana iliyojificha japo aliropoka kutokana na mawazo tu. Alimpelekea bosi amuhisi binti aliyerukwa na akili. Huku mlinzi wageti akipatia upenyo wa kucheka hadi akaanguka chini.

"Nawe.. Kibakuli, uo wehu utakuisha lini? Hilo jibu limekuchekesha kiasi hicho. Badala hata ungehuzunika. Punguza wehu. Mdogo wangu hebu nifate tukaongee vizuri unaonekana hauko sawa kiakili wewe." Aliongea ma'mwenye nyumba kisha wakafatana hadi ndani. Walipofika wakaketi kwenye masofa na yule mama akaomba aelezwe shida ya binti yule.

"Dada, nimekuja hapa kwako kwa ajili ya kuomba kazi. Naomba unisaidie dada yangu." Aliongea shida yake kiufupi. Ma'yule alimuuliza maswali kadhaa. Nakumpa tahadhali lakini pia aligusia suala la machokoraa jinsi walivyo na tabia mbovu. Kisha akamuomba historia ya maisha yake na anapotokea ilihatakama likitokea tatizo wajue jinsi yakulitatua mapema. Alitoa historia japo ilikuwa ya uongo. Dada yule alimkaribisha na kumpeleka pahala kwa ajili ya kuoga kisha akamuonesha chumba cha kupumzikia.

Ilikuwa ni zaidi ya furaha kwa Aisha. Alishukuru sana Mungu, huku akimuombea kichaa yule apumzishwe huko alipo.

* * * *

Mavugo baada ya kupelekwa gerezani. Ndipo alipogundua kumbe ingawa gereza ni pahala pakufundishia adabu vilevile nisehemu pakufundishia uharifu.

Siku ya kwanza tu anaingia hivi. Alikaribishwa yeye nawenzie watatu ambao waliingia wote kwa pamoja siku hiyo. Wale waliowakaribisha walikuwa na maneno yasiyo na heshma hata kidogo.

"Wakezetu.. Karibuni. Tutawaoa.. Karibuni." Ni maneno baadhi katika wimbo wa kuwakaribisha. Wimbo uliofanana na kwaya lakini ulitumia mikono kama kifaa pekee cha muziki maeneo yale. Wimbo ule ambao ulikosa kwaya masta pekee uliendelea kuimbwa ndani ya gereza. Huku wafungwa wale wapya wakiipelekwa sehemu na maaskali jela waliowapokea.

Hapo.. Matumbo yawafungwa wale wapya yakaanza kupata joto kutokana na wimbo ule uliokuwa na maneno makali na yenye lugha chafu. Sijui mtunzi wa nyimbo ile kipindi yupo uraiani alikuwa akiimba nyimbo za aina gani au labda aliwaza nini mpaka akatunga wimbo wa kukaribisha wafungwa. Tena wenye vitisho namna ile.

Wafungwa wale wapya waliendelea kuusikia wimbo huo bila kificho. Walifikishwa mpaka kwenye vyumba vyao maalumu kulingana na namba zao.

Ingizo jipya alikuwemo Mavugo, mwenye kesi ya mauaji ya watu watatu. Alikuwemo Moshi. Kesi yake ilikuwa ni yakuua mtu mmoja. Huku Salmini yeye akikabiliwa na kesi ya kumuua mke wake pamoja na mtoto wake.

Kwakuwa waliingia pamoja hivyo muda wa chakula walitafutana haraka na kuonana, kisha wakaenda kupanga foleni kama maagizo yanavyosema.

Mavugo, aliendelea kushangaa baada yakugundua kuwa kumbe hata wapishi nao ni wafungwa. Alijiuliza jinsi wanavyopata malipo yao lakini hakupata jibu. Ilipofika zamu yake kwenye foleni. Alienda na kupatiwa chakula kichache tofauti na waliomtangulia. Hata marafiki zake walipata hivyohivyo.

Hawakuwa na jinsi waliamua kwenda kukaa kwa ajili ya kula na ndipo alipokuja jamaa mmoja aliepanda hewani. Huku nyama za mwili wake zikiwa zimejikata mapingili na kukomaa kila mahali. Jamaa yule alifanana na wanyanyua vyuma wazoefu.

"Wapuuzi nyie. Mnakulakula tu. Mmelipia hapa?" Aliongea jamaa yule na hiyo nibaada ya kuipiga meza waliyokuwa wamewekea chakula wafungwa wale. Hapo, hakuna alieongea kila mmoja alinywea na hapohapo jamaa yule bila hata uoga wa nyampala aliyekuwa maeneo yale. Akaamrisha. Ati wachukuliwe wafungwa wale iliwaende kukaribishwa na hata kama wakila chakula, wawe wanakula kiuhalali. Sio kula bila kukilipia. Hapohapo alichukuliwa Salmin na kwenda kulawitiwa na wafuasi wa jamaa yule ajulikanae kwa jina la Tripple B. Kisha wakamchukuwa Moshi japo alipambana lakini walimshinda na kumfanyia yale waliyoyafanya kwa Salmin. Hapo wakamchukuwa Mavugo kwa ajili ya kumfanyia vile. Walianza kumtolea nguo zake alizokuwa amezivaa. Wakiwa kwenye harakati za kumfanyia ujinga wao huku akijitetea bila mafanikio. Hapo ndipo alipoingilia mtu mmoja nakutoa msaada kwa kuwatembezea judo wote walioonesha kuwashambulia wafungwa wale.

Mtu huyo alimchukua Mavugo na kumpeleka moja kwa moja pahali pazuri. Huku wale wafuasi wa Tripple pamoja na Tripple wote wakinywea kutokana na kutembezewa kichapo cha adabu.

"Kwa majina naitwa. Emanueli Zakayo. Nimeagizwa na serikali kwa ajili yako. Ingawa umepewa hukumu ya kifungo cha maisha lakini ushahidi haukuweza kuridhisha na hata kuwa namashaka na akili zako kutokana na maneno uliyokuwa ukiyaongea. Najua, utakuwa na sababu ya kuhitaji kunyongwa na ndiomaana ulitamani kunyongwa sana. Sasa labda ningependa kujua kwanini unahitaji kifo kuliko hata kuishi?" Aliongea mtu yule aliejitambulisha kwajina la Emanuel.

"Mnanichunguza ee. Hivi nyie wapelelezi!! Mara ngapi nimeshawambia kuwa. Mimi sijui nilipotoka, yaani hata jina langu silijui. Au mnashida gani tofauti na hiyo. Kama shida ni kunipeleleza. Basi mniache, msidhani kisa mimi kichaa ndio mnaweza kujanipeleleza nakuwasaidia chochote. Kwanza achaneni na mimi. Au nawewe unataka kufa? Sema! Msipende kuwa wambea namna hiyo." Aliongea Mavugo na kumfanya Emma abadilishe pozi lake.

"Mavugo. Tunashida na historia yako. Natunaihitaji zaidi ilikuhakikishatunaamua uamuzi sahihi. Unajua mpaka leo wanaendelea kuishi nawe unaendelea kuteseka. Je, unajisikia furaha kila siku kujitumbukiza kwenye matatizo huku ukijipa kauli mbiu ya Maumivu ndio haki yako. Hivi. Wewe niwakujifanya kichaa na kukubali kuangamia kisa vitu vya nyuma. Hebu angalia wapitumetoka. Shida yangu mimi nikukusaidia wewe na si vinginevyo. Nakuomba tafadhali elezea nami nitaichukua kama ushahidi. Ushahidi utakaokuweka huru na haya uliyoyafakamia bila kufikiri. Tafadhali usikubali kupotea hivihivi. Yaani, haki uloitafuta mwenyewe. Leo nd'0 imekufanyia hivi?" Aliongea Ema. Nakimaneno tu. Alionesha kumjua zaidi na kuwa na ukaribu fulani na anamfahamu sana Mavugo.

"Ema, ukitaka niongee. Mlete mke wangu, mlete mtoto wangu pia. Hapo ndipo nitaongea. Lakini kama wao wamekosa haki, basi mimi sioni haja yakuitafuta hiyo haki ambayo imewaondoa wao." Aliongea Mavugo kwa ghadhabu kisha akaongeza. "Maisha ya ukichaa. Hayakuhusu. Bora uniache naukichaa wangu nami naufurahia kwasababu napata muda wa kuyaepuka ya dunia kwa kuwa mjinga." Aliongea. Kwa upole huku akiwa kama ni mwenye kumnong'oneza Ema. Wala hakushangaa kuiona sura ya Ema ndani ya gereza.
Baada ya mavugo kumnong'oneza Ema. Aliamua kuondoka na moja kwa moja kurudi hadi kwenye chumba chao. Alipofika, aliwaza sana na kuwazua. Kisha alifunua mchago na kuchukua picha moja kati ya tatu alizokuwa amezihifadhi chini ya mchago huo.

Aliziangalia mara kadhaa, kiasi chakutokwa na machozi.
Ni picha ya muhimu sana kwake. Kwenye picha hiyo kulikuwa na sura ya Mwanamke mmoja ambae ukimuangalia kwa wasiwasi wawezadhani ni mwarabu kumbe ni kutokana na uzuri wake wa asili. Mwanamke huyo alionesha tabasamu lililomfanya awe mzuri zaidi, alikuwa kushoto mwa picha hiyo huku katikati akionekana mtoto ambae ukimkadilia ni chini ya miaka kumi. Kuanzia sura, hadi mavazi basi usingeshindwa kugundua kuwa mtoto huyo ni wakiume. Kulia kwa mtoto huyo alionekana mwanamume ambae nae kama wengine aliashiria tabasamu. Huku mbele ya wote watatu hao kukipambwa na keki iliyokuwa kwenye meza maalumu kabisa. Na kwa muda huo ungegundua kuwa ni muda wa kuzima mishumaa yakeki hiyo kutokana na mtoto yule kuonesha ishara ya kupuliza mishumaa iliyokuwa ikiwaka.

Mke wangu, nakupenda sana. Najua kuwa nawe unanipenda. Hata huko uliko huwa unaniombea na kutamani angalauuungane nami. Lakini inakuwa ngumu.
Natambuwa wazi kuwa haupotena kwenye hii dunia. Lakini roho yako ipo pamoja nami.. Na unasikia kila ninachoongea kwa muda huu. Hakika umeondoka kwa kudhalilika sana. Naomba utambue kuwa, mimi kama mume bora nilipata pigo kubwa sana na sitokaa nisahau kamwe. Alijisemea Mavugo huku akiwa amekaza jicho lake upande wa mwanamke wa kwenye picha ile aliyokuwa akiiangalia. Kisha akayachukuwa macho yake kwa hali ya unyonge usio mithilika na kuyabwaga kwa mtoto aliyeonekana kwenye picha ile.

Kumbukumbu zikamrudisha miaka kadhaa nyuma..

* * * *

"Mwanao Sufiani anapenda sana kusoma magazeti. Sijui naye anataka akikuwa awe Muandishi kama wewe Baba yake?" Ni sauti nyororo kutoka kwa Bi. Chiku au Ma. Sufiani kutokana nakujaaliwa mtoto wa kiume mwenye jina hilo. Sauti hiyo ilikuwa imeambatana na mikono ambayoiliendelea kupapasa,papasa maeneo ya uso wa mumewe huku mume wake nae akiipokeza kwa kuishika kuizuia isiendelee kumtekenya tekenya.

"Eee, mtoto wa kiume lazma amrithi baba yake. We unataka mwanangu apende kuwa daktari iliakahangaike na vidonda huko, kama wewe Mama yake. Mwanangu ni Muandishi wa habari, na atafichua siri za uovu pamoja na kuwasaidia watu kwakufikisha matatizo yao mbele ya uongozi. Mwanangu hatokula rushwa ya kutoa Mimba, mwanangu hatoangalia watu wakifia hospitali na kuwafunikia kisha kuwaingiza mochwari. Bali mwanangu atawaanika madaktari wanao kula rushwa, atawafanya madaktari waingie gerezani kwa kosa la kusababisha vifo kisa uzembe. Hayo yote atayafanya kupitia Magazeti atakayoandika huko mbeleni. Na ndiomaana anapenda sana kusoma magazeti na sio kuuguza vidonda kama ufanyavyo wewe mama yake."

"Umeanza tayari mambo yako. Mimi kila siku nakwambia Baba Sufiani. Bila mimi kumzalisha Mama yako wewe usingekuwepo hadi leo. Usimdharau daktari yeyote, sawa mimi ni mkeo lakini ukiugua nakutibu tu."

ITAENDELEA
 
Madame S

Madame S

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2015
Messages
15,035
Points
2,000
Madame S

Madame S

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2015
15,035 2,000
RIWAYA: KICHAA.

Na: ZUBER R. MAVUGO.

N0. 05.

ILIPOISHIA.

"Eee, mtoto wa kiume lazma amrithi baba yake. We unataka mwanangu apende kuwa daktari iliakahangaike na vidonda huko, kama wewe Mama yake. Mwanangu ni Muandishi wa habari, na atafichua siri za uovu pamoja na kuwasaidia watu kwakufikisha matatizo yao mbele ya uongozi. Mwanangu hatokula rushwa ya kutoa Mimba, mwanangu hatoangalia watu wakifia hospitali na kuwafunikia kisha kuwaingiza mochwari. Bali mwanangu atawaanika madaktari wanao kula rushwa, atawafanya madaktari waingie gerezani kwa kosa la kusababisha vifo kisa uzembe. Hayo yote atayafanya kupitia Magazeti atakayoandika huko mbeleni. Na ndiomaana anapenda sana kusoma magazeti na sio kuuguza vidonda kama ufanyavyo wewe mama yake."

"Umeanza tayari mambo yako. Mimi kila siku nakwambia Baba Sufiani. Bila mimi kumzalisha Mama yako wewe usingekuwepo hadi leo. Usimdharau daktari yeyote, sawa mimi ni mkeo lakini ukiugua nakutibu tu."

ENDELEA.

" Astaghafirullah.. we mwanamke wewe... Acha uongo. Utapata dhambi bure. Nani aliyekudanganya. Mama Mavugo alimzaa Mavugo hospitali. Mimi sikuwa mzembe kiasi hicho. Nimezaliwa zangu nyumbani swaafi. Na sio huko hosipitali. Halafu ukome kumfunza mwanangu hayo ma microscope yako hayo. Sijui ma silinji. Sitaki mwanangu umuambukize udaktari. Dume langu lazma lifichue maovu na kuiandikia jamii mambo yaliyo jificha bwana. Alaaa!"

Waliendelea na mjadala wao na mwisho wa siku waka kosa maelewano ikabidi wa muite mwana wao na wamuulizie anachopenda kati ya udaktari au Uandishi.

"Baba.." aliita mtoto.

"Naam, mwanangu" aliitikia Mavugo. Kisha mtoto akamuangalia mama yake na kumuita. Hivyohivyo kama kwa baba yake aliitika Mama. Kisha mtoto akaongea..

"Ikiwa kama kunaulazima wa mimi kuiandikia jamii. Basi kushika kalamu ni jukumu langu. Lakini pia kama jamii itaugua basi nitashika sindano yenye dawa na kumchoma mgonjwa hadi apone ndipo niikamate tena kalamu." Majibu yale ya mwanawao huyo mdogo ambae alikuwa na umri wa miaka nane pekee. Yaliwafurahisha sana wazazi wake.

* * * *

Kengele ya kuwaamrisha wafungwa wote kulala. Ndiyo iliyakata mawazo yote ya Mavugo, na harakaharaka akafuta machozi. Kishaakairejesha picha ile mchagoni ilikufanya wafungwa wenzie wasiione.

"Amka uoge kisha twende shoping kwa ajili ya kuchukuwa mavazi yako ya kuvaa maana huna kabisa nguo" Ni sauti ya Bosi wa Aisha aliyekuwa akimuamsha Aisha mara kadhaa hapo kabla.

"Sawa dada." Aliamka Aisha. Nakuoga kisha akavaa nguo za dada yule ambazo zilimfanya aonekane wa tofauti kidogo.

Wakachukuwana hadi kwenye gari iliyokuwa sehemu ya kuhifadhia magari kwenye uwanja wa dada yule. Kisha wakapanda moja kati ya magari manne yaliyokuwepo pale.

Mlio wa honi ndio ulio muamsha Kibakuli. Nakwenda kufungua geti kisha bosi wake pamoja na Aisha wakaondoka.

Wakiwa ndani ya gari Aisha na bosi wake. Hawakuwa hivi hivi bali walizungumza mawili matatu huku gari hilo likienda.

"Mmmh! Hapana Aisha, mie sipo hivyo. Kwanza samahani nilisahau kukujuza kuwa. Nimeolewa, na lakini kwa sasa mume wangu yupo dar-es-laam kuna mambo kaenda kufanya."

"Waoo. Hongera sana bosi wangu."

"Aisha. Nimekukataza mara ngapi kuhusu hilo jina la kuniita bosi. Wewe niite dada tu, sawa?"

"Samahani dada yangu. Nimazoea tu."

" usijali mdogo wangu."

Hayo ni baadhi ya maongezi waliyokuwa wakiyaongea njiani. Hatimae walifika kwenye maduka ya nguo kisha wakachagua nguo nzuri na zakisasa kabisa. Umbo zuri alilojaaliwa Aisha ndilo lilizifanya nguo nyingi kumpendeza. Karibu kila kizuri cha dukani kwake kilifaa. Walinunua nguo na kuamua kurudi nyumbani kwao. Kama ilivyo kawaida walifunguliwa geti na kuingia ndani.

Walipofika hatua ya kwanza ilikuwa ni kuoga kutokana na uchovu kisha Aisha akaelekea jikoni kwa ajili ya mapishi, huku Dada yake yeye akitazama moja kati ya seasöns za kikorea.

Dada yule alijulikana kwa jina la Aneth. Aneth akiwa anaendelea kutazama Seasön mara ghafla simu yake ya mkononi iliita. Alipoiangalia kwenye kioo ilisomeka 'My husband'. Akaipokea na kuiweka sikioni.

"Hello sweety" Ni sauti kutoka upande wa pili. Sauti ngumu iliyoonesha kujilazimisha kulainika.

"Hello, darling" Ni sauti ya majibu kutoka kwa Aneth. Sauti nyororo yenye kutia hamu kuisikia tena pindi upatapo nafasi ya kuongea nayo.

"Baby. Nimepata taarifa kuwa Mama amezidiwa na ule ugonjwa wake wa Moyo. Si unajua mimi nipo mbali? Nakuagiza wewe uende kahama kwa ajili ya kumuangalia si unajua huko nyumbani hakuna wa kumuangalia." Aliongea Wilson. Mume wa Aneth.

"Haa! Masikini... Ameanza lini?" Aliuliza aneth. Kisha mumewe akamjibu kwa haraka.

"Basi sawa mme wangu. Leo najiandaa kesho asubuhi nitaenda huko." Baada ya kupeana taarifa za hapa na pale simu ilikatwa na aneth akaendelea kuangalia video.

Mmhmh! Hapa lazma ni mwambie dada kuhusu hii Mimba. Lakini.. Akiniuliza juu ya nilipoitolea nitamjibu nini?.. Je, nimwambie ukweli kuwa nilibakwa na maafande?. Hapana, siwezi. Nikimwambia hivyo tayari nitakuwa nimejiharibia kwa sababu historia ya maisha yangu nilompa haitoendana na mwisho ataniona muongo. Sasa nifanye nini wakati hali inazidi kuniwia ngumu. Au niitoe tu. Ndio, hapa chamuhimu nikuitoa ilinisipoteze kazi. Lakini...! Kutoa mimba ni dhambi kubwa na huleta madhara! Mimi kesho kutwa lazma ni mwambie dada najua atanisaidia anaonekana ni mwenye huruma. Ni mawazo yaliyokuwa yakimzunguka kichwani mwake Aisha pindi yupo jikoni na hiyo ni baada ya kupatwa na kichefuchefu cha ghafla.

Hatimae muda wa chakula ulifika na wote kwa pamoja wakakutana mezani na kupata chakula. Kisha wakaongea machache, lakini Aisha hakugusia swala lake la mimba kwakuwa alipanga kumjuza dada yake swala hilo kesho kutwa.

Haya, hatimae usiku uliingia na muda wa chakula chausiku ulipofika. Ndipo Aneth alipomuachia Aisha majukumu na kumpatia matumizi kisha akamjuza kuhusu safari ya yeye kwenda kahama kumuuguza mama mkwe. Hapo Aisha akapumua nakujua kuwa itakuwa ngumu sana kwa Aneth kuelewa kuwa yeye anamimba. Hivyo akaamua kuweka siri moyoni kama kawaida.

Siku ya pili yake ilipofika. Aneth aliondoka na kwenda hadi kahama. Alipofika, alimkuta mama mkwe wake kwenye hosipitali ya goverment pale wilayani kahama, kishaakaanza kumuuguza.

Huku nyuma Aisha alijiona yupo huru, na hakupata uoga tena kila alipobanwa kutapika alikimbia na kutapika. Tumbo lilipomuuma alitumia dawa. Kila alipomaliza kazi za nyumbani na kuwa huru. Alipenda sana kutoka nje na kuzurura zurura, lakini alifanya hivyo kwa tahadhali sana.

Siku ziliendelea kusonga hatimae ikapita wiki nzima na hapo akawa ameizoea kabisa nyumba ile. Mimba nayoiliendelea kumsumbua ingawa bado ilikuwa haijaanza kujifichua. Hapo akawa mvivu kupika, kufanya usafi hata kusababisha migogoro kila siku kati yake na mfungua geti.

Huwezi juwa lililomo moyoni mwa mtu. Siku moja mfungua geti aliingia ndani na kumkuta Aisha kajilaza kwenye masofa kutokana na uchovu. Alipofika ndani mule yeye moja kwa moja akahitaji kumjua Aisha kwa nguvu, japo kuwa Aisha alipinga. Lakini hakuwa na ubavu wa kukinzana na getimani yule, hivyo akafanikiwa kumjua Aisha.

"Sasa, ulikuwa unanibania nini. We mwenyewe umefaudu utamu. Kaone, ulikuwa unajikatisha raha bure!" Ni baadhi ya maneno aliyoyatoa getimani yule. Huku akimfuta machozi Aisha ambae kwa muda huo alikuwa akitoa machozi.

Masikini Aisha alikuwa akilia kwa kumuhurumia kijana wa watu ambae amejisababishia ukimwi bila kujua. Lakini hakutaka kumwambia maana alijua endapo atamwambia basi atamfanya kijana wa watu asiishi kwa amani. Lakini pia aliona kijana yule ameumia kutokana na tamaa zake.

Hakuwa na jinsi na hapo akaamua kuliamisha penzi lake kwa geti mani. Kila siku usiku wakawa wanavunja amri ya sita, ndani ya nyumb ya bosi wao Aneth.

Siku zilienda hatimae Mimba ya Aisha ikajidhìhirisha machoni mwa getimani.

"sawa, minimekubaliana na hiyo mimba. Lakini nakuomba tunza siri." Masikini getimani alijikuta akikubali mzigo usio kuwa wake. Na hakuwa na kipingamizi kwa sababu yeye ndie mwanaume pekee wa Aisha. Hapo Aisha akawa amepata wa kumbambikizia mimba na ukimwi juu. Waliendelea na mapenzi yao hadi aliporudi Aneth na kukuta Aisha tayari ana mimba. Kwakuwa Aisha alimficha, Aneth toka mwanzo. Hivyo aneth alijua huo utakuwa ni umalaya wa Aisha na kuwaza kuwa huenda kipindi ambacho yeye hayupo ndicho Aisha alichokitumia kufanyia umalaya wake.

"Aisha, ulikuja kuomba kazi nami nikakupa. Hakuna nilichokunyima kwanzia chakula, mavazi, na hata malazi. Nilikupa uhuru na kukuchukulia kama mdogo wangu. Lakini wewe leo umepoteza heshima. Hivi, we unadhani nani ana muda na kulea hiyo mimba yako humu ndani. Kiukweli sina msaada kwako, chamuhimu ni wewe kwenda kwa mahawala zako waliyokupa hiyo mimba." Hata Aisha alipojaribu kujitetea, hakuna kilichobadilika. Alipewa usiku mmoja tu wa siku hiyo kwa ajili ya hifadhi na kutakapo kucha aondoke ndani ya nyumba ile.

Alichoka, kila akiukumbuka mtaa, akikumbuka shida za mtaa, akikumbuka uovu wa mtaa. Kisha akiwianisha jinsi alivyopokelewa na Aneth na kuanza kuishi pale. Pasina kusema kuwa anamimba na mimba yenyewe hakuipata hivihivi bali alibakwa tu bila ridhaa yake. Alibaki kujilaumu na kuwaza huenda angemtaarifu Aneth mapema kuwa alikuwa na mimba. Yote hayo yasingetokea. Alijiinamia kwa muda huku akiendelea kuwaza mawazo yasiyo wazuka.

Alilaani kitendo cha kumpatia geti mani mwili wake na kumsababishia ukimwi. Pia alikumbuka kuwa yeye ndie aliyesababisha getimani amfuate kufuatia mitego aliyompa, lengo lake ilikuwa si. Kumuambukiza Ukimwi bali kumbambikizia kesi ya mimba kwa kudhani huenda kupitia getimani yeye asingefukuzwa. Masikini, Aisha anaishia kukinzana na migogoro ya nafsi na kuishia kujiona mwenye makosa. Soni ilimjaa, na hata kushindwa kuinua uso wake japo alikuwa ndani ya chumba alichopewa kwa ajili ya kupumzikia lakini alijionea aibu mwenyewe.

Tumbo limemjaa, Aisha ameharibika. Ukimuangalia uso wake wakutisha huwezi tamani kurudia tena. Ingawa alikuwa akitumia vidonge vya kuongeza siku lakini hakuweza kukabiliana na mimba aliyokuwa nayo.

Alitamani kujiua lakini kila alipoangaza vifaa vya kutolea uhai wake hakuona hata kimoja, alitamani atoke nje na kwenda kununua sumu dukani lakini hakuwa na pesa. Bora hata angekuwa na kanga huenda angeifunga juu ya paa nakujining'iniza lakini nguo zote alizokuwanazo alinyang'anywa na Aneth kwa sababu alinunuliwa na sio kwamba alijinunulia yeye. Labda nguo alizobakiziwa ni zile alizokuwa amezivaa kwa siku hiyo.

Ingawa alipewa hifadhi ya kulala kwa siku hiyo lakini hakuweza kuvumilia kulala kwenye nyumba hiyo iliyojaza aibu yake. Taratibu bila hata kuaga aliichukuliwa na miguu yake na kupelekwa hadi getini. Alipofika alifunguliwa geti na mpenzi wake kibakuli au geti mani kwa jina la nyadhifa yake. Waliagana kwa majonzi na kwa muda wote huo getimani hakuwa ameanza kuadhirika zaidi na virusi vya ukimwi hiyo ilibaki kuwa siri ya Aisha pekee.

Masikini, hapo sasa Aisha akaanza kutangatanga mtaani mida ile ya usiku huku baridi kali likiendelea kumuadhibu na kile kinguo chake cha mikono wazi kilichoishia juu kidogo ya magoti. Baridi hilo liliendelea kumpiga na kumfanya ayaadhibu meno yake kwa kuyagonganisha muda wote.

ITAENDELEA.
 
The Icebreaker

The Icebreaker

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2018
Messages
4,085
Points
2,000
The Icebreaker

The Icebreaker

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2018
4,085 2,000
Nitarudi kuisoma ngoja nikachukue maji ya kunywa kwanza.
 
Madame S

Madame S

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2015
Messages
15,035
Points
2,000
Madame S

Madame S

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2015
15,035 2,000
RIWAYA: KICHAA.

Na: ZUBER R. MAVUGO.

N0. 06.

ILIPOISHIA.

Ingawa alipewa hifadhi ya kulala kwa siku hiyo lakini hakuweza kuvumilia kulala kwenye nyumba hiyo iliyojaza aibu yake. Taratibu bila hata kuaga aliichukuliwa na miguu yake na kupelekwa hadi getini. Alipofika alifunguliwa geti na mpenzi wake kibakuli au geti mani kwa jina la nyadhifa yake. Waliagana kwa majonzi na kwa muda wote huo getimani hakuwa ameanza kuadhirika zaidi na virusi vya ukimwi hiyo ilibaki kuwa siri ya Aisha pekee.

Masikini, hapo sasa Aisha akaanza kutangatanga mtaani mida ile ya usiku huku baridi kali likiendelea kumuadhibu na kile kinguo chake cha mikono wazi kilichoishia juu kidogo ya magoti. Baridi hilo liliendelea kumpiga na kumfanya ayaadhibu meno yake kwa kuyagonganisha muda wote.

ENDELEA

Alipita kwenye vichochoro vya igoma utadhani yeye ni jasiri sana kumbe kutafuta pa kulala tu. Alifika sehemu yenye duka na kuchukua maboksi kisha akayachana kiustadi na kujitengenezea sehemu ya kulalia. Alipomaliza aliuweka mwili wake juu ya maboksi yale hakuwa na shuka hivyo alijifunika ngumi.

"Oyaa. Mwanangu leo mie sijapata hata mtu wa kupiga ngeta. Daah! Bisu langu halijafanya kazi kabisa." Ni sauti ya Vijana wawili wa mtaani. Vijana ambao ukiwaona tu utawafananisha na vibaka waliyoshindikana kutokana na makovu yaliyowaenea.

"Bora, wewe... Mimi mwenzio hapa. Nilipitia mitaa ya makoroboi, nikapitwa wembe na wale watoto wakule. Yaani hata sijafanya kazi." Aliongea kijana yule wa pili kwa sauti ya unyonge.

"weeweeee! Acha basi. Kwahiyo jemedari unataka kusema wale watoto wa mama wa huko kati nd'o wamekupita wembe wako."

"Nd'o hivyo mwanangu. Ila nimewakalili." Aliongea kijana yule aliyekuwa akilalamika. Safari ya vijana wale wawili. Iligota pale walipofika maeneo ya kibaraza cha duka ambapo ndipo alipokuwa amelala Aisha.

Walinong'onezana kwa sauti. Kishawakamkurupua Aisha ambae kwa muda huo hakuwa anajielewa kama yupo macho au amelala.

"oyaa. We manzi unazingua. Nani kakwambia ulale sehemu yangu." Aliongea mmoja kati ya vijana wale. Aisha nae alikuwa mgumu kuelewa. Aliendelea kujibizana na vijana wale. Ndipo walipochukuwa jukumu la kumpiga palepale mateke ya tumbo bila kujali mimba aliyokuwa nayo kisha wakamkimbia.

Ilikuwa ni zaidi ya maumivu kwa binti Aisha, tena kwa bahati nzuri au mbaya mimba yake ilikuwa imefikisha miezi tisa timilifu hakuna ilichosubiria zaidi ya uchungu tu. Kama uchungu basi hapo aliupata tena wakutosha kiasi kwamba akawa hajielewi kabisa kutokana na maumivu. Hapohapo nje ya duka hilo mida hiyohiyo ya usiku.

"Jikaze.. Jikaze.. Haya sukuma.. Sukumaa.." Ni sauti ya mama mmoja msamalia mwema. Mama ambae nae kama Aisha ni mlala nje. Alikuwa amelala na kina mama wengine kwenye kibaraza cha jirani lakini alienda kumsaidia Aisha baada ya kugundua kuwa anamimba. Muda wote huo Aisha aliendelea kujikema kwa nguvu utadhani ni mwenye kutoa haja kubwa. Zoezi hilo lilichukuwa muda kidogo mpaka kukamirika.

Yule mama aliyekuwa amevalia mifuko ya nailoni kutokana na kukosa vifaa maalumu kwa ajili ya zoezi lile. Nikama aliongozwa na Mungu pale alipokata na kufunga kwa upesi kitovu cha mtoto yule wa kiume ambae ndio kwanza amezaliwa na kwa bahati alichapwa makofi kadhaa akaanza kulia.

Naam. Inawezekana na hilo halina ubishi hata wanasayansi wa kale na wasasa wote wanakubali kuwa. Mtoto anaweza kuzaliwa bila virusi vya ukimwi ilhali mzazi wake anavyo. Najua utakuwa na maswali mengi lakini hiyo ni siri ya Mwenyezi Mungu pekee. Unaambiwa pale kwenye kumkata ule mrija unaemuunganisha Mama na mtoto. Basi hapo ndipo panaweza kumfanya mtoto akapata na virusi au asipate. Aisee., tumuacheni Mungu aitwe Mungu tu. Wala tusijadili zaidi uwezo wake maana tutajikuta wenye kukufuru pasipo kutarajia.

"ng'aaaa... ng'aaaa...ng'aaaa...." Ni sauti ya mtoto yule ambae ndio kwanza ameingia duniani. Kwa muda huo Aisha alikuwa amezimia kutokana na shughuli pevu aliyoimaliza. Hapo Mama yule mwenye huruma akambeba mtoto yule na kwenda hadi maeneo ya mto kishaakachukuwa maji na kumsafisha. Maji mengine aliyoyabeba kwenye madumu ya dasani aliyatumia kumsafishia Aisha huku mikono yake akiwa ameifunga kiustadi.

"Mwanangu. Hakuna maji yakukukandia. Hakuna dawa ya kutuliza maumivu. Ila nimekuchumia dawa ya kukata damu japo kidogo. Lakini yote kwa yote naomba umshukuru Mungu kwa kukujaalia neema ya kupata mtoto katika kipindi hiki kigumu ulichonacho. Ni wachache sana wapatao neema hizi, hii ni baraka mwenyezi ameamua kukuruzuku. Huwezi juwa labda kupitia mtoto huyu, wewe utapata kivuli na kuondokana na jua hili la utosini ulilonalo. Hapa chamuhimu wewe ondoka. Najua unamaumivu lakini haina jinsi hapa simahala pazuri kwako. Toka maana ukikutwa umezalia hapa kwenye duka la watu, wao hawatoelewa shida zako bali watajua ni wewe kuwapelekea nuksi." Aliongea mama yule mwenye huruma. Mama ambae ukimtazama waweza kumdharau kutokana na uchakavu wa nguo zake unaopelekea aonekane hana thamani lakini miaka ya nyuma mama huyo alikuwa daktari mzuri tu. Ila ni historia ndefu iliyompelekea kuwa maeneo yale.

Labda kwa ufupi... Huko nyuma kabla ya kuujua mtaa. Aliitwa beatrice wanyika. Beatrice alikuwa mrefu kidogo, mwembamba kiasi. Sura iliyopambwa na macho maregevu huku kope zake zikiashiria kuhitaji kusinzia muda wote. Nyusi za asili ambazo hazihitaji haja ya wanja, huku shavu dodo lenye kuruhusu machozi ya furaha na huzuni yapite bila mkwaruzo wowote. Hivyo na vingine ndivyo vilivyompelekea Beatrice kuwa mzuri zaidi na hata kufatwa na wanamume. Lakini mara zote aliwakataa, kutokana na kutohitaji kujihusisha na maswala ya mapenzi. Hakika alikuwa na msimamo, kuachilia mbali kazi yake ya udaktari vilevile kwao walikuwa na uwezo hivyo hakuna kilichomshinda. Baada ya wazazi wake kufariki kwa ajali, na yeye kunusurika. Ndipo mjomba pamoja na ndugu kadhaa walipowahi mali za wazazi wake na kumzulumu. Kwakuwa alikuwa na haki ndipo alipoamua kufungua kesi mahakamani lakini sheria ni upanga na sio msumeno. Ilikata upande mmoja na yeye kuswekwa gerezani ati kwa kesi ya kuwaua wazazi wake. Wakati ni wazi kuwa wazazi wake walikufa kwa ajali ambayo haijatengenezwa na binadamu. Aliingia ndani na ndipo alipogundua kumbe hata kwenye magereza huwa kuna ubabe. Kwanza alipofika, alikutana na mfugwa mmoja kwa jina la Annastazia. Yeye alikuwa ni mfungwa aliyehukumiwa maisha yote gerezani na kwa muda huo Anna alikuwa na miaka ishirini toka aingie gerezani mule. Alikuwa katili kuliko hata wanamume, alikuwa jasiri na kila mfungwa mpya. Yeyme alimchukulia kama mke wake kwa hiyo hata alipofika kule Beatrice naye aliolewa na mwanamama huyo. Hayo ni mafupi kati ya mengi yaliyompata beatrice ambae kwa sasa ni mama anae ishi mtaani. Alitoka gerezani kufuatia msamaha wa rais. Hakuwa na pa kwenda zaidi ya mtaani tu.

Haya tuendelee..

"Nashukuru sana Mama angu kwa msaada wako. Sina chakukulipa ila nakuombea kwa Mungu akulinde. Hakika wewe umeokoa maisha yangu na maisha ya mwanangu. Kwakuwa umesema mtoto huyu nimemzaa katika kipindi kigumu ila kwa neema za Mungu ameingia duniani," Aliongea Aisha kisha akakohowa kidogo kikohozi kigumu na kuendelea.

"Angekuwa mtoto wa kiume basi ningemuita Baraka. Kutokana na misukosuko pamoja na changamoto hasi na chanya alizozipitia kipindi yuko tumboni. Lakini kwakuwa ni wakike acha na muita rehema. Hakika hii ni rehma ya Mungu pekee. Nakushukuru sana kwakunisaidia." Aliongea Aisha na kuanza kumuaga Mama yule kwa heshma zote kisha akaondoka maeneo yale. Aisha aliendelea kuzurura usiku ule yeye mtoto pamoja na maumivu yaliyotokana na taabu ya kujifungua. Kwakweli alipata taabu sana usiku huo.
Alipita sehemu kwenye kiuchochoro kichafu na kuamua kujituliza hapo ilikupumzisha mwili wake ambao kwa muda huo ulikuwa taabani.

" Mimi nalewa, nitaendelea kulewa hadi siku ya mwisho. Labda tuitwe walevi wote duniani na kuzuiwa, hapo sasa ndipo nitakapo anzakujifunza kuzoea. Lakini wewe pombe, nakupenda, nakujali, na ninakuhtaji sana maisha yangu yote. Hakika wewe ndio mke wangu wa maisha, sitokuacha hata kama wakikupiga vita kiasi gani. Nafurahi unanitoa mawazo, nazisahau shida niwapo na wewe. Mwaah! Nakupenda sana pombe." Ni sauti ya mlevi mmoja aliyekuwa akipita maeneo yale mkabala kabisa na Aisha, alikuwa akiongea maneno yake huku mkononi ameshikiria chupa ya bia. Alipofika kwenye kichochoro alifungua zipu kisha akaanza kukujoa pasina kuangalia mbele kutokana na ulevi aliyonao.

Laahaullah.. Kumbe mkojo wake wa kilevi aliokuwa akiumwaga maeneo yale uliwamwagikia kina Aisha. Hapo sasa aisha akashindwa kuvumilia.

"Kaka.. Usitufanyie hivyo. Mbona unatukojolea." Ni sauti iliyomtoka Aisha katika hali ya unyonge zaidi. Mlevi yule alipatwa na mshituko ghafla na kuhisi huenda maajabu yameamua kumpata. Lakini akajitutumua kilevi na kuendelea kukojoa tena.

Sauti nyingine ya lawama ndiyo iliyomfanya mlevi yule agundue kumbe kuna mtu na mtoto maeneo yale. Na hiyo ni baada ya kichocheo cha kilio cha mtoto yule mchanga kwa jina la rehema.

Ingawa mtu yule alikuwa mlevi, lakini hakunyimwa roho ya huruma. Alimchukuwa Aisha kisha akampeleka nyumbani kwake.

Ni chumba chakupanga. Chumba ambacho hakiujui umeme, iwe mchana au usiku. Chumba hicho ndicho kilikuwa sebure na mahali pakulalia. Buibui, na wadudu wengine watambaao pamoja na baadhi warukao walijisweka ndani ya nyumba ile na kuishi kana kwamba wao ndio wapangaji. Naam. Kulikuwa kuna godoro dogo, kitanda kidogo na kilichotumika miaka mingi kabla, waweza sema ni cha urithi. Hakika ungefanikisha kutupa jicho ndani ya chumba hicho. Basi usingeshindwa kupaita stoo kwa jinsi ambavyo makolokolo yamejazana ndani mule.

Ingawa chumba kile hakikuwa kisafi lakini aisha alionesha kukifurahia na moja kwa moja alikaribishwa kwenye kitanda kile na mlevi kisha aisha akalala yeye pamoja na mtoto wake. Lakini mlevi kwa heshma alichukuwa shuka na kulala chini.

Japokuwa kitanda kile kilijawa na kunguni, lakini Aisha hakuonesha kuathirika na chochote mara zote yeye alifurahia tu na kumshukuru Mungu.

Mlevi hawezi kulala bila kuisifia pombe. Vivyo hivyo kwa mlevi yule, aliimba nyimbo kadhaa alizozitunga palepale na kisha akapitiwa na usingizi.

Pilikapilika za wakazi wa jiji la Mwanza pamoja na makelele ya hapa na pale huku jua likianza kupenyeza ndani ya nyumba ile kufuatia matundu makubwa makumbwa yaliyomo ndani, ndivyo vilivyo muamsha mlevi yule na kuanza kujiandaa kwa kuoga na kupiga mswaki, baada ya hapo aliingiza mkono ndani ya suruali yake na kutoa shilingi elfu mbili na mia tatu. Akamuamsha Aisha na kumpatia pesa hiyo kisha akaondoka na kumwambia kuwa wataongea baadae kiundani zaidi.

... ... ... ....

ITENDELEA.
 
Madame S

Madame S

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2015
Messages
15,035
Points
2,000
Madame S

Madame S

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2015
15,035 2,000
RIWAYA: KICHAA.

Na: ZUBER R. MAVUGO.

N0. 07.

ILIPOISHIA.

Japokuwa kitanda kile kilijawa na kunguni, lakini Aisha hakuonesha kuathirika na chochote mara zote yeye alifurahia tu na kumshukuru Mungu.

Mlevi hawezi kulala bila kuisifia pombe. Vivyo hivyo kwa mlevi yule, aliimba nyimbo kadhaa alizozitunga palepale na kisha akapitiwa na usingizi.

Pilikapilika za wakazi wa jiji la Mwanza pamoja na makelele ya hapa na pale huku jua likianza kupenyeza ndani ya nyumba ile kufuatia matundu makubwa makumbwa yaliyomo ndani, ndivyo vilivyo muamsha mlevi yule na kuanza kujiandaa kwa kuoga na kupiga mswaki, baada ya hapo aliingiza mkono ndani ya suruali yake na kutoa shilingi elfu mbili na mia tatu. Akamuamsha Aisha na kumpatia pesa hiyo kisha akaondoka na kumwambia kuwa wataongea baadae kiundani zaidi.

... ... ... ....

ENDELEA.

Siku ziliendelea kwenda na hata kupita zaidi. Huku Mavugo akiwa ndani ya gereza. Alipazoea sasa na alipata marafiki kadhaa ingawa akili zake zilikuwa zikija na kupotea kwa muda. Ukimuona Mavugo huwezi kushindwa mfananisha na kichaa. Kuna masaa aliongea kama mtu mwenye akili lakini pia kuna masaa aliongea kama mtu asiye na akili. Hiyo ilipelekea asiaminiwe kwa kila alilolisema na aliitwa kichaa muda wote.

Naam.. Nikweli kabisa kuwa, Mavugo alikuwa akirejewa na akili zake kwa dakika chache kisha akili hizo kutoweka kwa muda mrefu na kumfanya aonekane kichaa. Aliongea maneno ambayo wenzie yaliwa hakikishia kuwa mfungwa mwenzao ni kichaa. Ingawa yeye alijiona yupo sahihi. Kuna siri kubwa sana iliyojificha, ina muhusu yeye. Lakini hakuna alichokijua kutokana na kulukwa na akili. Kila alipoijiwa na akili, alikumbuka mambo ya ajabu ambayo yalimliza muda wote. Lakini punde tu. Akili zinapomtoka huurudia ukichaa wake. Taarifa za ugonjwa wa ukichaa ziliwapata wakuu wa gereza na wao kuzifikisha mahali husika. Walipomchunguza waligundua ni kweli kabisa Mavugo anaugonjwa wa akili na sio utani kama walivyodhani wao.

Ati, walihukumu kichaa. Mtu ambae alifaa awe mirembe hosiptal, au bugando hosipil. Wao wakamuweka gerezani. Waligundua kuwa kwenye kitabu cha hukumu hakuna msitali hata mmoja unaomfunga kichaa. Hivyo waliamua kumpeleka tu. Kwenye hosipitali ya vichaa.

Walimchukuwa na kumpeleka hospitali ya vichaa nae akaanza kuishi huko pamoja na vichaa.

Ndugu msomaji ule msemo usemao kwamba, 'ukistaajabu ya mussa utayaona ya fir'auni' haukuwa na maana ya kuchekesha wala kudanganya bali ulikuwa na ukweli ndani yake.

Binadamu muache aitwe binadamu pindi awapo na akili timamu. Hebu kwanza kabla hujaendelea kusoma mshukuru Mungu kwa kukufanya kuwa na akili timamu mpaka muda huu... Kule alipopelekwa Mavugo, alikutana na watu wa aina mbalimbali. Kuna wale muda wote wanacheka tu tena bila hata kufurahishwa. Kuna wale ambao muda wote wanazunguka utadhani wamepewa kazi ya kuweka usalama wa bosi fulani. Ati kuna wale ambao wao wanavua samaki hadi kwenye mabakuli.

"Habari yako" Ni sauti ya Mavugo iliyokuwa ikimjulia hali kichaa mmoja ambae toka asubuhi yeye alishinda anakimbia tu mpaka muda ule jasho lilikuwa limemtoka lakini hakuahirisha. Alivyosikia sauti ya Mavugo akasimama kisha akamjibu,"Njema tu." Hapo sasa Mavugo akahisi huenda amepata rafiki maana alijua kuwa huko wote ni vichaa tu.

"Vipi rafiki yangu. Mbona tangu jua lichomoze wewe unakimbia tu. Tena upohapahapa mpaka muda huu. Hauchoki?" Akairejea kazi yake ya uandishi wa habari kwa muda.

"Nichoke!? Ohøoo.. Shauri yako, mwenzio kila siku nakimbia mpaka sasa nimeshafika dar-es-salaam. Lazma nitoroke Tanzania. Nataka kwenda somalia huko vitani, kwahiyo usinibughudhi kabisaaa! Wewe endelea kukaa hapo. Sie wenzio wanajeshi. Allaaa!!" Hapo Mavugo akashindwa kuelewa.

Ati, yupo Dar-es-salaam. Ati, anatoroka aende somalia akapigane vita.. Mmmh! Mbona naona yupo palepale toka asubuhi. Hivi hata hiyo safari ya Somalia ataifika kwa hali hii kweli. Hebu achanimuulize tena. Aliwaza Mavugo kisha akamsemesha tena.

"Rafiki, naonaga watu wakipanda magari na kwenda Dar, kisha wanachukuwa ndege na kwenda somalia. Tena huwa wanatumia muda mrefu sana kufika. Je, wewe hiyo safari yako ina muda gani hadi leo. Yaani kutokea hapa mpaka huko Dar ambapo umefika kwa sasa kama usemavyo."

"hahahahaha! Rafiki una maswali ya utani wewe... Ok, nina miaka Saba toka nianze kusafiri. Nimepita mikoa mingi sana na nimeishi sana mahali mbalimbali lakini kila siku huwa naanzia safari yangu kituo hiki hiki na kuhusu hao wa mandege mie nikifika vitani nitayapanda tu. Usijali hebu kwanza niache kuna gari nashindana nalo hapa lisije kunipita bure." Alijibu kichaa yule na Mavugo akaanza kujiona yeye ukichaa wake unauafadhari.

Akamuacha na kumfuata kichaa mwingine ambae yeye alikuwa bize huku mkononi akiwa ameshikiria iliyofungwa kamba ya ndoano, huku kichaa yule akiwa ameweka fimbo hiyo ndani ya bakuri dogo lenye maji. Mavugo alipomfikia kichaa yule akampa salamu. Lakini kichaa yule alimuonesha ishara ya kumtaka akae kimya ili samaki wasije wakatoroka.

Bakuri? Samaki? Mmmh! Híi kali.. Alijisemea Mavugo kisha akaondoka maeneo yale na kuona bora tu akakaepeke yake. Aliiona sehemu moja yeye utulivu akaifuata kwa ajili ya kukaa. Alipofika nako huko akakutana na kichaa mmoja ambae yeye alikuwa amenuna. Mavugo aliamua kumsemesha iliajue nini kilichomsibu chakushangaza kichaa yule akaondoa hali yake ya kununa na kuanza kucheka. Alicheka kwa muda mrefu sana bila kupumzika. Hapo tena Mavugo akapaona hapamfai. Akaondoka na kwenda sehemu nyingine huko akatulia hadi usiku ulipofika.

* * * *

Mume wa Aneth alirejea kutoka dar-es-salaam na wakaendelea na Maisha yao. Aneth alimu hadithia mumewe juu ya yeye kumfukuza Aisha mwaka mmoja uliyopita. Ndipo mumewe alipomtafutia mfanyakazi mwingine na Maisha yakaendelea. Kama kawaida ya geti mani alimtaka mfanyakazi yule mpya wa ndani. Japokuwa mfanyakazi alikataa mwanzoni lakini mwishoni alijikuta amemkubalia. Wakaanzisha mapenzi. Kwakuwa mabosi wao walishinda kazini. Wao waliutumia mwanya huo kudumisha penzi lao. Mfanyakazi huyo binti aitwaye Pendo aliamua kumpenda geti mani na hata getimani aitwaye kibakuli naye pia aliamua kumpenda pendo. Getimani hakujijua kuwa tayari alikuwa ameathirika kutokana na damu yake ya grupu o.

.... ... ... ....

Mlevi na Aisha walizoeana, lakini hawakuwahi kufanya mapenzi wala kuwa wapenzi. Aisha alimuheshimu yule mlevi kwa jina la David, halikadhalika devid alimuheshimu Aisha kama Dada yake na alimchukulia mtoto wa aisha(Rehema) kama mpwa wake ingawa wote waliishi ndani ya nyumba moja.

Aisee.. Wanasema mapenzi ni hisia zitokazo moyoni. Hisia hizo huwa hazitokei hivi hivi bali huanza taratibu na mwisho wake kudhihirika. Ile devi kumjali Aisha, kumkirimu yeye pamoja na mwanae pasina kudai malipo ilimpelekea Aisha kutumbukia kwenye dibwi la mapenzi. Alijikuta anampenda sana Devi(Kaka wa hiyari) lakini aliogopa kumwambia kama anampenda. Hiyo ilichangiwa na Devi kupenda ulevi. Yaani asubuhi anaenda kazini halafu jioni anarudi akiwa amelewa. Bahati nzuri kupombeka kwake hakukumuathiri sana kiasi cha kuwa mbogo ndani ya nyumba. Bali kulimuathiri kimaendeleo ya maisha pamoja na kuidhoofisha afya pekee.

Aisha alijisikia aibu sana kuishi kwa aliyemsaidia bila fadhira zozote. Kila alipofikiria alitamani amlipe japo fadhira lakini hakuwa na chakumpatia kama fadhira. Kila akifikiria aliishia kumuhurumia kaka yake yule wa hiyari.

Mmmh! Namimi hata sina aibu.. Analala chini. Ananiacha mimi na mwanangu kitandani ilhali hata hatufahamiani. Mimi sijiongezi, mpaka sasa umepita mwaka toka anisaidie. Ananiachia pesa za matumizi, nakula mimi na mwanangu. Yeye akirudi jioni anarudi kalewa na kujibwaga chini kisha analala. Hakuna.. Hakuna.. Inabidi nimlipeangalau hata fadhira, sina pesa, sina mali, bali nina mwili na mtoto pekee. Alaaa! Nimpe mtoto? Hapana mtoto si.. Damu yake. Inabidi nimpe mwili wangu kama fadhira. Lakinii... Lakini mimi ni muathirika. Nikisema nimpe mwili... Mmmh! Achani muache. Masikini, lakini Moyo wangu umeshampenda tayari. Najua tu ananivumilia kwa kujua kwamba ipo siku nitajiongeza. Lakini mimi namuhurumia. Sihtaji ni muambukize. Eeeh. Mungu nipe moyo wa uvumilivu. Nilinde na haya yanayoenda kunikabili. Hakika hadhaririki uliye mfanya rafiki. Ni maneno aliyowaza Aisha au Mama Rehema.

Alitoka kwenye mawazo na kuchukuwa pesa ya matumizi. Moja kwa moja hadi sokoni yeye na mtoto wake mgongoni. Alinunua mahitaji kishaakaenda nyumbani kwa ajili ya mapishi. Alipika kisha akala. Alipomaliza kula kama kawaida alienda kwa jirani yao. Mama. Suzan. Kwasiku hiyo alienda kwa ajili ya kuomba ushauri.

Alimuelezea yote yaliyomsibu katika maisha yake. Kisha shoga yake huyo akamshauri kuwa amwambie tu david kwamba yeye ni muathirika na hata hapo alipoanatumia madawa. Kasoro mwanae ambae yeye si muathirika na hata maziwa anayotumia ni yale ya kwenye chuchu za plastik.

Aisha aliupokea ushauri ule na usiku ulipofika aliamua kuwa mkweli kwa david. David hakuonesha kukereka bali alimuhurumia Aisha na kumuhurumia mtoto wake Rehema. Kisha akamlalamikia kwa kutokumuambia toka mwanzo lakini Aisha alimpa sababu za kuridhisha mwisho wa siku wakaendlea kuishi kwa heshma hivyohivyo kama kaka na dada japokuwa Aisha alikuwa tayari ameshampenda sana devid.

Siku zilienda siku zikapita. Ni siku moja iliyokuwa imetulia, siku hiyo Devid alirudi nyumbani mapema sana na hakuwa amelewa lakini alikuwa ameshikiria kilevi. Siku hiyo devid alikula chakula na kujipumzisha. Aisha alijua wazi kuwa Devi atakuwa anaumwa sana. Hata alipomfuata nakumuulizia juu ya kuwahi kuja nyumbani kwa siku hiyo. Yeye alijibu kuwa ni mawazo tu.

"Hivi kaka! Wewe kwanini sijawahi hata kukusikia ukimuongelea wifi yangu hata siku moja?" Ni swali lenye mtindo wa kichokozi kutoka kwa Aisha.

Devi alicheka sana kisha akainuka na kushikiria chupa ya bia na kuibusu, "Aisha mke wangu mimi ni pombe ambae wewe unamuita wifi." Ni majibu yaliyosisimua nywele za Aisha. Hapo akajawa na shauku ya kutaka kujua kwanini Devi amemjibu hivyo. Alitega sikio lakini devi muda huo alikuwa kimya. Ukimya ulipozidi ndipo Aisha akaamua aulize swali la kuchombeza iliajuzwe zaidi.

"Kaka, mbona upo kimya. Hebu niambie kwanini unasema kwamba wewe mke wako ni pombe?." aliuliza kisha akakaa mkao wa kula iliapate majibu. Lakini chakushangaza Devid alifungua kifuniko chabia kisha akapiga funda kama tatu hivi halafu aka hema kwa kwa nguvu na kusema.."Dada yangu. Mwanamke, ukiwanae atakupa mawazo lakini kamwe mke wangu pombe huwa hanipi mawazo. Mwanamke atakusaliti lakini kamwe mke wangu pombe hajawahi kunisaliti. Pombe hunipa starehe ya nafsi na moyo lakini mwanamke ataiumiza nafsi na kuuchakaza moyo wangu kwa maumivu muda wote. Naipenda sana pombe." Aliposema maneno yale hapohapo akafatia kwa kulibusu chupa la bia.

"Hapo kaka nakupinga. Hivi we.. Unaona ni bora ukauwe figo bandama sijui mapafu na hata utumbo kupitia kilevi kisa unaogopa kuumizwa. Aaah! Hapo umepotea." Aliongea Aisha huku akimtoa mtoto mgongoni na kuchukuwa chuchu iliyokuwa na maziwa kisha kuanza kumnywesha.

"Aisha.." Aliita Devid kisha aisha akaitika kiupole huku akiendlea kumbembeleza rehema ambae kwa muda huo alikuwa hataki chochote zaidi ya maziwa tu.

ITAENDELEA.
 
Madame S

Madame S

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2015
Messages
15,035
Points
2,000
Madame S

Madame S

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2015
15,035 2,000
RIWAYA: KICHAA.

Na: ZUBER R. MAVUGO.

N0. 08.

ILIPOISHIA.

"Hapo kaka nakupinga. Hivi we.. Unaona ni bora ukauwe figo bandama sijui mapafu na hata utumbo kupitia kilevi kisa unaogopa kuumizwa. Aaah! Hapo umepotea." Aliongea Aisha huku akimtoa mtoto mgongoni na kuchukuwa chuchu iliyokuwa na maziwa kisha kuanza kumnywesha.

"Aisha.." Aliita Devid kisha aisha akaitika kiupole huku akiendlea kumbembeleza rehema ambae kwa muda huo alikuwa hataki chochote zaidi ya maziwa tu.

ENDELEA.

"Najua itakuchukuwa muda sana kunielewa lakini yaliyonikuta katika maisha yangu. Ndio yaliyonipelekea kuipenda sana pombe," Alitulia kidogo Devid kishaakainamisha kichwa chake chini alitumia sekunde kadhaa kisha akainuka. Uso mzima tayari ukawa umelowa kwa machozi. Hapo Aisha akagundua kuwa huenda maneno yake yamemkumbusha mbali sana, hakutaka kuongea akamuacha Devid akiendelea na machozi yake.

"Aisha.. Ndani ya hii dunia kuna mambo mengi sana ambayo yamejificha na hayaonekani mbele ya wengi. Huwatokea wachache tu na kutengeneza historia ngumu za maisha yao. Yote hayo ni mapito tu.

Mimi leo ninaishi kwenye haka kajumba kabovu na kachafu lakini jana sikuwa hivi. Kila nikiikumbuka jana yangu hapo ndipo naona ni bora nilewe tu. Labda kuna kitu hujui Aisha.. Mimi zamani sikuwa nakunywa pombe, sikuwa najenga nyumba kama kibarua bali nilikuwa kijana mtanashati tena mstaarabu lakini. Dah! Hebu ngoja nikusimulie ili unielewe vizuri...." Palepale Devid akaanza kusimulia.

** ** **

"Mwanangu... Mimi ma'yako umri umenitupa mkono na hitaji nicheze na wajukuu wangu. Lakini wewe kila nikwambiapo swala la kuoa unabadilika na kuwa mkali. Kwanini lakini mwanangu?" Ni sauti ya Ma'Devi ambae sasa alionesha kuchoshwa na tabia ya mwanae. Ni mwanae wapekee hakuwa na mtoto mwingine zaidi yake hivyo alikuwa anahitaji angalau mjukuu kwakuwa umri wa Mama huyo tayari ulikuwa umekwenda. Devid ambae kwa muda huo alikuwa mwalimu kwenye moja kati ya shule huko Chato mkoani Kagera. Yeye hakupenda kabisa kusikia habari za wanawake na wala hakuhitaji mwanamke kwa kipindi kile kutokana na kiapo alichojiapisha cha kutokupenda tena. Ni matatizo ya kimapenzi yaliyomfanya asihitaji tena mwanamke. Kila akikumbuka kipindi bado yupo mwanafunzi katika shule ya sekondari Buselesele aliishia kupinga kauli ya mama yake iliyomtaka aoe.

"Mama. Mie sijapanga kuoa kwa muda huu. Labda miaka kadhaa ijayo. Pia nadhani unajua suala lakuoa sio la kukurupukia mama yangu. Inabidi nitulie ilinitazame yupi atakae nifaa."

"Wewe mtoto ni mjinga sana. Nimeshakwambia nahitaji mjukuu. Hivi unadhani hiyo miaka yako kadhaa inaweza kukabiliana na uzee niliyonao? Tambua wewe ni mwanangu wapekee. Kama mama nahitaji nipate wajukuu ambao watanifanya nipate furaha na kusuuzika nafsi. Hebu niletee wajukuu hapa. Sitakikukuelewa kabisa," Alitulia kidogo mama yule kisha akavuta pumzi nakuendelea.

"Hebu fikiria. Kama wanawake nimeshakuletea wengi sana. Si kwasababu mimi ni Mama nisiye na adabu. Laa.. Bali nikukutaka wewe mwanangu uoe. Mpaka imefikia kipindi mimi nimechoka sasa. Sitaki kusikia upuuzi wako nachohitaji kusikia ni sauti ya mjukuu wangu. We mwanamume gani usiyependa mtoto wewe.. Sasa nakupa wiki moja, nenda kajitafutie mke wa kuoa kwasababu kipindi na kubembeleza hadi kukuletea wanawake ulikuwa ukiwakataa. Na ikipita hiyo wiki moja bila wewe kutambulisha mwanamke hapa.. Mtafute Mama yako mwingine unaemsikia nasio mimi." Aliongea Mama Devid kisha akawa anaondoka sebureni na kuelekea jikoni.

"Lakini mamaa..."

"Eee.ee. Sihitaji mjadala na mtoto niliyomnya mwenyewe. Nimemaliza." Aliongea Mama devid kisha akaingia jikoni na kwenda kuendelea na Mapishi.

Devid alibakia pale sebureni huku ameshikiria remote. Nguvu zilimuisha kufuatia maneno makali kutoka kwa Mama yake. Palepale akajibwaga kwenye sofa. Mara wazo likamuijia akaona ni bora atazame video. Kila chanel aliyobonyeza aliona kama haina maana hapo akaamua kuitupa remote pembezoni mwa sofa na yeye akainuka moja kwa moja mpaka chumbani mwake. Alipofika alijitupia kitandani bila heshima ya kitanda kile kisha akaanza kuutafuta usingizi. Alimaliza nusu saa nzima bila kupata hata lepe la usingizi bali mawazo yaliyomjaa. Hapo tena akaona kitanda hakina maana akajiinua na kwenda hadi kwenye maktaba yake ya vitabu kishaakaanza kupekuwa vitabu vya kusoma. Alianza na riwaya ya Joram kiango 'NAJISIKIA KUUA TENA' amesomasoma akaona nayoinazidi kumchanganya kutokana na maudhui yaliyomo ndani yake. Hapo akakirejesha kitabu kile na kukiendea kitabu cha NYONGO MKALIA INI. Hicho hata kukielewa hakukielewa kabisa. Hakuwa na hamu ya kusoma. Taratibu miguu ikamchukua na kumpeleka hadi nje ya nyumba yao. Alipotoka nje, aliwaza wapi aelekee.. Aliona ni bora aende sehemu yenye miti mingi huenda akapata ufumbuzi watatizo lake. Taratibu akaita tax na kuelekea eneo moja alilopenda kwenda kwa ajili ya kutatua matatizo yake ya kiakili. Alipofika alisogea kwenye moja kati ya miti iliyokuwa maeneo yale na moja kwa moja akaanza kupitiwa na upepo mzuri wa maeneo yale. Ghafla mawazo yakamtwaa na kumkumbusha mambo yaliyomtokea kipindi cha nyuma alipokuwa mwanafunzi huko shule ya sekondari buselesele iliyoko Chato...

Mawazo yalimpeleka hadi siku aliyoenda kuripoti shuleni hapo. Akakumbuka jinsi alivyopokelewa na kupelekwa moja kwa moja hadi kwenye darasa alilopangiwa.

"How are you students?" Ni sauti ya mwalimu wa darasa la kidato cha kwanza ambae kwa muda huo aliingia yeye pamoja na devid ambaye ni mgeni kabisa. Mwalimu huyo aliongea maneno ya kiingereza yaliyokuwa na maana ya kuwajulia hali wanafunzi wale wa kidato cha kwanza.

"We are fine.. How about you?" walimjibu kuwa hawajambo kisha wakamuulizia juu ya hali yake.

"Am fine too" aliwajibu kuwa naye yupo sawa.

"Ok, students. Am here inorder to introduce ur new friend. As you see here. This is ur friend his name is Devid Damson. Ok" Aliongea Mwalimu wa darasa kwa lugha ya kigeni ikiwa inamaanisha utambulisho wa mwanafunzi huyo mpya.

Baada ya utambulisho huo mfupi David alipewa siti ya ukutani na kukaa. Kwakuwa alikuwa mgeni, hakuwa na wakuongea nae wala hakutaka kujishughulisha na wanafunzi wenzie darasani humo. Alichukuwa kalamu yake na kuanza kuandika majina ya wachezaji mbalimbali wa mpira. Alikaa na upweke mpaka ulipofika muda wa mapumziko. Hakupenda kwenda kantine hivyo alibaki darasani.

" Sista nd'o huyu aliyekushika mkono oya.. Wewe ndo Unajifanya unajua sana sindio... Hebu sogea hapa. Unapenda sana kushobokea madada za watu ngoja tukuoneshe boya wewe." Ni sauti ya kibabe iliyokuwa ikitoka nje ya darasa alilokuwemo David kwa muda huo. David aliisikia sauti hiyo lakini alíipuuzia na kuendelea na mambo yake.

"Nd'o huyo. Eti kimenikuta niko na maria kikaanza kunishika mkono. Nilipokiuliza eti kikanambia kinanipenda" Ni sauti nyororo yenye dhihaka ambayo ilipendeza masikioni mwa yeyote. Ingawa muongeaji aliitoa kwa dhihaka lakini ndio kwanza sauti yake iliendelea kuwa nzuri. Anaitwa Irene ni msichana mrefu kidogo modo, mwenye sauti ndogo halafu iliyo nyororo haina mikwaruzo hata pale alipolia iliongezeka na kuwa nyororo zaidi. Macho yake ya aibu ambayo hayakuwa na uwezo wa kuhimili kuangaliwa kwa sana pasina kuzileta kope zake ndefu kuyafumba, ndiyo yalikuwa kivutio kizuri zaidi na kuwapelekea vijana wengi kumdai moyo wao. Naam, ingawa ni modo lakini nyonga zake zilitanuka vizuri na kuwakilisha umbile la kibantu lililosimama, alikuwa na weusi uliyokolea vilivyo na kumfanya aonekane mrembo zaidi kulingana na umbile lake.

"Ayaaah!... Jamani sirudii.. Yaishe tu. Tafadhali Irene naomba uniombee msamaha kwa makaka zako wataniua bure mtoto wa watu." Ni kipigo alichopewa Martin mpaka akaanza kuomba msamaha.

Kaka wa Irene waliendelea kumshushia kisago Martin. Ukelele ulipozidi ilibidi David ambae alikuwa darasani, ainuke na kuchungulia dirishani. Alimuona Martin akiendelea kupata kisago kutoka kwa vijana Wanne ambao kwakuwa kadiria aligundua watakuwa wa kisoma vidato vya mbele. Lakini alipogeuza jicho lake pembeni kidogo nipo macho yake yakagongana na macho ya Irene ambae nae kwa muda huo aliangalia dirishani na hiyo ni baada ya kusikia dirisha limefunguliwa.

Wanasema macho huongea tena kwa lugha yake, lugha ambayo wewe huwezi kuisikia ila moyo pekee ndio husikia lugha hiyo. Moyo wa Irene ulimruka baada ya kumuona kijana mtanashati, maji yakunde mwenye kifua chakukamata shati huku mwili wake wa mazoezi ukionekana. Sura nzuri iliyomvutia Irene, labda naweza sema na nywele za David ziliweza kuchangia maana alikuwa na nywele utadhani alidhuru uarabuni., naam.. Mapigo ya moyo yalimuenda kasi sana. Kumbe siyeye tu. Hata David naye alipatwa na kitu moyoni mwake, palepale alirejea na kukaa kwenye kiti kwa sababu David hakupenda ugomvi. Aliwachukia sana wale kaka zake na Irene ambao waliendelea kumpiga martin.

Ni kama Irene aligundua jambo lile palepale aliwakataza kaka zake wasimpige jamaa yule. Kisha akatoka pale huku anakimbia moja kwa moja hadi kwenye darasa analosomea. Alipofika alikikimbilia kiti chake na kujilaza moja kwa moja huku mawazo yakile alichokiona yakiwa yamemjaa.

Siamini... Bado sina uhakika kama kuna binadamu mzuri kiasi kile. Mmmh! Kweli kila shetani ana mbuyu wake. Alijisemea maneno yale huku fikra zake zikimrejesha pale alipokutanisha macho yake na macho ya David kisha hapohapo Moyo ukamdunda.

Mmmh! Nimepatwa nanini leo. Mbona moyo wangu umekuwa hivi? Na mbona macho yangu yanatamani kuendelea kumuona yule kijana? Mungu wangu. Hadi mikono yangu inatamani kumpapasa kijana yule. Mh! Mh! Mh! Sijui uonjwa gani umenipata. Alijisemea tena Irene huku akiweka taswira ya David pamoja na jinsi anavyojisikia.

Labda kwakuwa Irene hajawahi kupenda ndio maana hakugundua kuwa kwa muda huo alisumbuliwa na mapenzi. Au labda kwakuwa hajawahi kuwa na mpenzi ndio maana hakujua nini kilichompata...

Ulifika muda wa darasani wanafunzi wote walirejea kwenye madarasa yao. Irene alisoma Kidato cha kwanza pia lakini mkondo ulikuwa tofauti na ule wa David. Aliingia mwalimu wa kiingereza darasani mwa kina Irene. Siku hiyo Irene hakuonesha uhusika mzuri darasani kama ilivyo kawaida yake. Alikuwa mtulivu na muda mwingi alijiinamia tu. Masomo hayakupanda kabisa mpaka wanafunzi wenzake ambao wamemzoea kama kina maria wakahisi huenda Irene akawa na matatizo.

"Irene leo wewe ukoje? Unaumwa! Mbona umepooza hivyo." Ni swali kutoka kwa rafiki yake Maria.

"Mmmh! Maria.. Nahisi kuna kitu kimeingia mwilini mwangu. Yaani.. Hata sijielewi. Kiufupi siko sawa Mary."

"Mhhh! Pole sana. Basi twende nikusindikize ukaombe ruhusa iliuende nyumbani kupumzika."

"bora.. Maana sijisikii kufanya chochote. Hebu nisindikize tukaombe ruhusa." walichukuwana kisha wakaenda moja kwa moja hadi ofisini na kuomba ruhusa. Mwalimu wa darasa alitoa ruhusa kisha akampatia kibari Maria iliaweze kumsindikiza mwenzie kwa baiskeli maana kutokea shuleni hadi mjini kuna kaumbali kidogo.

ITENDELEA.
 
Madame S

Madame S

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2015
Messages
15,035
Points
2,000
Madame S

Madame S

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2015
15,035 2,000
RIWAYA: KICHAA.

Na: ZUBER R. MAVUGO.

N0. 09.

ILIPOISHIA.

"Irene leo wewe ukoje? Unaumwa! Mbona umepooza hivyo." Ni swali kutoka kwa rafiki yake Maria.

"Mmmh! Maria.. Nahisi kuna kitu kimeingia mwilini mwangu. Yaani.. Hata sijielewi. Kiufupi siko sawa Mary."

"Mhhh! Pole sana. Basi twende nikusindikize ukaombe ruhusa iliuende nyumbani kupumzika."

"bora.. Maana sijisikii kufanya chochote. Hebu nisindikize tukaombe ruhusa." walichukuwana kisha wakaenda moja kwa moja hadi ofisini na kuomba ruhusa. Mwalimu wa darasa alitoa ruhusa kisha akampatia kibari Maria iliaweze kumsindikiza mwenzie kwa baiskeli maana kutokea shuleni hadi mjini kuna kaumbali kidogo.

ENDELEA.

Walifika nyumbani kwa kina Irene kisha Maria akarudi shule kwa ajili ya kuwahi vipindi vya mchana. Huku nyuma Irene alijibwaga kitandani kwake baada ya kuwasalimia wakubwa zake waliyokuwa nje.

"Vipi mbona umerudi mida hii. Au umeburuzwa mboko huko shuleni eti."

"Hapana dada. Sikofresh tu. Nimeona bora nije kupumzika nyumbani tu.

"Mhhh! Haya mdogo wangu pole. Lakini... Nini hasa kinachokusumbua?"

"Kichwa dada."

"Kichwaa!? Kimesababishwa nani hicho kichwa"

"mmmh! Mi ata selewi. Nimeshangaa tu kinaanza kugonga." Akatoka dada yake chumbani mwao na kuelekea sebureni kufuata dawa. Ile anarudi akashangaa kumuona mdogo wake anafurahi na kujitwika matabasamu hadi anaushika moyo wake huku akiongea maneno ya chinichini ya kumsifia yule kijana aliyemuona kule shuleni.

"Irene.. Umependa! Wewe utakuwa umeangukia kwenye mapenzi mgonjwa wa kichwa hayupo hivyo mdogo wangu. Achakunidanganya. Sema tu ukweli umependa?" Kauli ile kutoka kwa dada yake ndiyo ilimgutua kwenye furaha yake na kumfanya agundue kumbe tayari dada yake alikwisha ingia ndani mule."

"Ndio..! Hap..hap.. Hapana...!! Si... Sij.. Sijui.. Hapana dada sijapenda" Oooh. Irene alishindwa hata kujitetea na kubaki akijiumauma na kuzalisha vigugumizi visivyokuwa na faida. Kwa hali ile dada yake alikuwa tayari ameshagundua kuwa Irene anasumbuliwa na ugonjwa wa mapenzi. Alimpa ushauri na kumsii mambo kadha wakadha, kisha akamjaza sumu zakuwachukia wanamume na kumfunza jinsi ya kuwaona kama picha.

Ni kama alikuwa anachukua maji na kuyamimina ndani ya kinu kisha anachukuwa mchi na kuyatwanga. Tayari Irene ameshapenda. Hakuna alichosikia wala kuweka akilini. Si kwanguvu zake bali kwa nguvu za mapenzi.

Siku baada ya siku Irene alianzisha na kukomaza mazoea na David. Kwakuwa mapenzi hayana siri. Walijikuta wakizaa penzi tamu lenye mazoea. Kaka zake na Irene walipiga hadi wakachoka lakini David aliwaambia hawezi kumuacha Irene hata wakimuua.

Walishawahi kumtoa mpaka alama za kudumu lakini hakukata tamaa. Walimuacha. Miaka ikasonga hadi walipofika kidato channe, alikuja mwalimu mgeni. Mvaa mavazi ya kisasa. Mwanzoni alipoanza kumtongoza Irene. Basi irene alimwambia mpenzi wake David. Lakini mwishoni Irene alishindwa kuviepuka vishawishi vya teacher na kujikuta anamsaliti David. Sasa penzi likawa kizaazaa. Irene akaanza kuzoea maneno ya David na kwakuwa mazoea nimabaya basi akajikuta hapati athari na kuanza kutamani ladha. Alianza kujitongozesha kwa wanamume huku usiku akienda kusoma kwa teacher. Tabia ile iliendelea mpaka siku moja David akaja kumkutaniza Irene getokwa mshikaji wake. Na hata alipomuuliza. Irene akawa mbogo na kumkana David ambae kwa muda huo alikuwa ameshapenda. Hapo sasa ndipo davi alipoyapata Maumivu. Aliporomoka kimasomo, mwili ulimkonda huku akiendlea kumuomba Irene msamaha utadhani yeye ndiyo mkosaji. Mara ya mwisho davi alipewa ushauri na Rafiki kisha akajazwa sumu na kujikuta anawachukia wanawake. Akaweka wanawake pembeni na kukaza. Alianza kupanda kimasomo na hata mtihani wa kidato channe ulipofika alifanya mtihani vizuri. Matokeo yalitoka na kuruhusiwa kuendelea. Huku Irene matokeo yake yakawa mazuri lakini alishindwa kuendelea kutokana na kujazwa mimba. Aliondoka zake na asionekane tena. Na kwanzia hapo David hakutaka maswala ya kuwa na msichana tena.

...... ........

Kumbukumbu zile zilimtoka na akaanza kuyafikiria kauli ya Mama yake. Kauli ya Amri iliyomuamrisha aoe. Alichoka na kukunja ngumi kisha akakipiga kichwa chake mara kadhaa.

"Kweli.. Kama maisha yapo mazuri. Kuishi na mke ninaweza. Kulea mtoto ninaweza. Kazi ninayo tena ya ualimu. Sasa kwanini nisioe. Eti.. Kisa Irene. Aaaaah! Nisiwe mjinga kiasi hiki! Aliyenitenda ni mmoja kwanini niichukie dunia nzima? Huenda alinitenda kwakuwa sikuwa na kazi. Je, leo nitatendwa? Hapana.. Haijalishi niliapa nini.. Inabidi nimletee Mama "wajukuu watakao mfanya mama yangu asiujutie uzee bali afurahie kwa kutaniana nao. Ndio.. Nimeamua kuoa. Lakini!... Nitamuoa nani?" alijisemea Dev kishaakaendelea kutafakari zaidi juu ya mwanamke wa kuoa.

Mpaka jua linazama devi alikuwa bado hajapata jibu sahihi la kuhusu mwanamke atakae muoa. Aliamua kurudi nyumbani kwakuwa giza lilianza kuingia. Alivyofika ndani alimkuta mama yake amenuna. Naye akajifanya hajui kinachoendelea, akachukua chakula na kula hiyo ni baada ya kuoga. Alipomaliza yote hayo alienda kupumzika. Akiwa kitandani amelala mara ghafla simu yake ikaita. Akaichukuwa alipoiangalia kwenye kioo ilisomeka namba ambayo haikuwa na jina kisha akaipokea.

"Hello" sauti ya upande wa pili iliongea hvyo.

"Ndio. Samahani sijui nani mwenzangu?" Hiyo ni sauti ya Devid na hiyo ni baada ya kusikia sauti iliyomvutia zaidi kutoka upande wa pili.

"Naitwa Rose. Ni dada wa katalina anaesomea shule unayofundishia wewe."

"oooh.. Katalina. Nimempata. Enhee! Ulikuwa unashida gani dada yangu?"

"Mmmmh! Nilikuwa nashida ya kuonana nawe iliunipe maendeleo ya Katalina kwa hapo shuleni. Siunajua tena hawa watoto wanahitaji uangalizi sana."

"Ok. Mr.Rose, kwakuwa leo ni jumapili. Hebu jitahidi kesho ufike shuleni ilinikupatie maelekezo vizuri."

"Sawa teacher.. Nitashukuru sana."

"ok.. Nakutakia usiku mwema."

"Nawe pia"

Rose akakata simu kishaakaiweka kitandani. Huku nae Devid akaitoa simu sikioni na kubaki anaitathmini namba ile. Aliiangalia kwa muda kidogo mpaka akajikuta ameikariri kisha akalala.

Asubuhi ilipofika alijiandaa na alipomaliza alikunywa chai na kumuaga mama yake na kwenda moja kwa moja shuleni. Alipofika akasaini kishaakaanza majukumu yake. Vipindi vilipoanza yeye alienda madarasani nakufundisha. Hata ulipofika muda wa mapumziko alitoka hadi ofisini na kuchukua kiti huku pembeni mwa meza yake kukiwa na chakula. Alikichukuwa na kukiweka mezani kisha akakianzishia mashambulizi. Akiwa kwenye shughuli hiyo pevu ya ulaji alisikia simu yake inaita na hata alipoangalia namba aliigundua hapohapo akaiweka sikioni baada ya kuipokea.

"Teacher. Mie nimefika."

"ok.. Nimo ofisini tayari. Wewe ulizia tu ofisi ya taaluma kisha uingie."

"Sawa teacher"

Rose akakata simu kisha akaulizia ofisi ya taaluma kwenye kundi la wanafunzi kadhaa waliyokuwa wakipata vitamin d.

Alipata maelekezo na moja kwa moja akaingia ofisini. Alimkuta teacher Devid ingawa teacher devid alikuwa hamjui Rose lakini hakushindwa kumuhisi pindi tu alipoingia ndani ya ofisi.

Macho ya walimu wote wa kiume yaliyokuwa bize na madaftari. Yalitupa miale mwilini mwa Irene ambae alikuwa amevaa mavazi ya kisasa yaliyomkaa vilivyo. Umbo lake lilijichonga utadhani namba nane, hakuonesha kununa bali tabasamu lililopambwa na lipstick iliyomfanya aonekane mrembo zaidi. Walimu walijikuta wakishindwa kuandika wala kuandaa hints za kufundishia vipindi vya mchana kwa muda huo wakabaki kuushanga uzuri na urembo wa rose aliyepambika kwanzia sauti hadi mavazi.

"Mr. Devid?" aliita Irene na kumgutua mwalimu devi ambae ni kama alikuwa mbali kimawazo pindi alipomuona tu dada yule.

Mawazo ya kichwa chake yalimuijia kuwa. Ati, ameshamtongoza Irene na wakakubaliana kuoana kisha akaenda kumtambulisha nyumbani na ndoa ikapita. Baada ya ndoa walikaa mwezi mmoja na Rose tayari akawa na mimba yake miezi tisa ilifika nao wakapata mtoto wa kiume ikawa nifuraha. Akiwa katika mawazo hayo ndipo aliposhtushwa na sauti nzuri ya Rose.

" Yes. Ndio mi...mimi." alijibu teacher Devid bila kuamini kama ni kweli amuonae mbele yake ndio yule msichana wa kwenye simu. Alikoswa pozi lakini akajitutumua kiume iliasioneshe paniki ambayo tayari alikwisha ipata. "bila shaka. Wewe ndio Rose. Dada wa Katalina?" kwa tabasamu Rose akajibu huku mkono wake mmoja akiushikisha kwenye meza ya mwalimu huyo ilikutengenza pozi. "Ndio mwenyewe wala haujakosea."

"Ok, karibu sana. Jisikie amani. Mmmmh! Nipe dakika mbili nichukuwe viti nipeleke pale kwenye mti ilituweze kuongelea huko." Aliongea Devid. Rose hakuwa nakipingamizi alikubali.

Devid alichukuwa viti viwili na kuwaomba radhi walimu wenzake kishaakaenda kuvitua karibu na mti ule uliokuwa na kivuli pamoja na upepo mwanana.

"Mrs. Rose.. Nilikuwa nikijaribu kupitia baadhi ya mitihani ya nyuma inayomuhusu katalina, pamoja na kukagua madaftari yake na vitu kadha wa kadha. Takwimu inaonesha kuwa maendeleo ya Katalina yanaridhisha naam. Sio mabaya. Lakini mtoto huyu anasumbuliwa sana na utundu wa hapa na pale. Mara utasikia kachana daftari la mwenzie mara kajichafua na wino, mara ameumia.. Ilimradi tu utundu utundu basi. Ila kitaaluma anajitahidi sana. Chamuhimu mie ninawashauri mumpeleke awe anasoma masomo ya ziada kwa ajili ya kuifanya akili yake iwe imara na bora zaidi, aidha.. Kumkanya apunguze utundu wake." Aliongea mwalimu Devi huku akipatapata shida ya kulikwepa tabasamu zuri la Rose iliasiharibu kazi. Lakini mara kadhaa alishindwa kuliepuka.

"Sawa Mwalimu mafanikio ya katalina yapo mikononi mwenu kama walimu wake. Kama walezi tunashukuru sana kuona mnavyotusaidia jukumu hili zito la kusimamia taaluma mpaka nidhamu. Kuhusu masomo ya ziada usijali swala hilo. Pia usijali kuhusu utundu utundu wake. Tutajitahidi kumkanya tu na nina imani kwa kushirikiana nanyi. Katalina atakuwa mwanafunzi mpole na mwema asiyependa makuu. Otherwise thank you." Aliongea Rose na mwisho wa kaulizake akapiga lugha ya magharibi ikimaanisha shukurani tu.

"Usijali Rose huo nd'o wajibu wa kazi yetu. Kuhakikisha mwanafunzi anakuwa sawa." Aliongea Devid huku akiyasumbua macho yake mara ayatupie kwenye sura ya Rose, mara kwenye kifua, mara kwenye umbo la ujumla ilimradi tu apate taabu. Kila Rose kwa kutumia mapozi ya kichokozi nae hakuwa nyuma katika kuhakikisha anamteka Devid kimawazo.

Ni fulu utamu wa aibu machoni mwa Devi. Alijitahidi kuyazuia macho yake yasiangalie mapaja mazuri ya Mrs. Rose ambayo yalikuwa yamejiweka kihasara. Lakini alishindwa kukabiliana na sumaku ya mapaja yale. Mara ghafla mwili wote wa Devi ukamsisimka. Mawazo yakamchukuwa na kumpeleka mbali sana.

"Baby... Hakika wewe ndio kila kitu kwangu. Wewe ndio Asali wa moyo wangu. Hivyo nakuomba ufanye moyo wangu upate tiba kupitia wewe. Usije hata siku moja kuutupa kwani utaufanya utapetape bure na mwisho kupotea kabisa. Tafadhali endelea kuvaa vazi hilo la uaminifu na usije kulitupa." Ni sauti ya Rose siku ambayo alikuwa yupo kwenye kifua cha Devid. Na hiyo ni baada ya kutalii utalii wa ndani kwenye maeneo kadhaa ya mwili wa devi.

ITAENDELEA.
 
Madame S

Madame S

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2015
Messages
15,035
Points
2,000
Madame S

Madame S

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2015
15,035 2,000
RIWAYA: KICHAA.

Na: ZUBER R. MAVUGO.

N0. 10.

ILIPOISHIA.

Ni fulu utamu wa aibu machoni mwa Devi. Alijitahidi kuyazuia macho yake yasiangalie mapaja mazuri ya Mrs. Rose ambayo yalikuwa yamejiweka kihasara. Lakini alishindwa kukabiliana na sumaku ya mapaja yale. Mara ghafla mwili wote wa Devi ukamsisimka. Mawazo yakamchukuwa na kumpeleka mbali sana.

"Baby... Hakika wewe ndio kila kitu kwangu. Wewe ndio Asali wa moyo wangu. Hivyo nakuomba ufanye moyo wangu upate tiba kupitia wewe. Usije hata siku moja kuutupa kwani utaufanya utapetape bure na mwisho kupotea kabisa. Tafadhali endelea kuvaa vazi hilo la uaminifu na usije kulitupa." Ni sauti ya Rose siku ambayo alikuwa yupo kwenye kifua cha Devid. Na hiyo ni baada ya kutalii utalii wa ndani kwenye maeneo kadhaa ya mwili wa devi.

ENDELEA.

"Furaha yangu ipo ndani yako. Sina chakusema zaidi ya kuyatunza uliyoniambia. Najua unanipenda tena sana tu. Nami sitotumia upendo wako kama gereza la mateso balinitaendelea kuutumia upendo wako kama nchi ya furaha kila siku iitwayo leo." Aliongea maneno yale Devid huku akitalii kwenye mashavu ya Rose.

Mawazo yaliendelea kumsumbua na kumpeleka mbali zaidi. Muda wote huo Rose alikuwa akimuita Devid bila mafanikio. Alichokiona usoni devid ni tabasamu pekee. Alivyochoka kumuita hapo akajitoa kwenye pozi lake na kuchukuliwa na mkono wake kisha akautuwa begani mwa devid kishaakaanza kumuita huku akisaidizana na mkono. Ndipo Devid aliposhtuka na kushangaa kuiona sura iliyokuwa ikimliwaza muda kidogo ipo mbele yake. Bila hiyana wala uoga aliamua kuongea palepale.

"Mrs. Rose. Kwakweli toka nikuone. Ni kama kuna kitu kimeukumba moyo wangu na kituhicho ni upendo. Hakika umeyatwaa mawazo yangu na kila uongeapo, uniangaliapo hata ugeuzapo pozi mbele yangu mwenzio na kosa raha. Nakuomba uwe wangu haijalishi kwa sharti lolote lile hata kama litahusika kuuweka rehani uhai wangu mimi nitafanya hivyo bila kipingamizi. Uzuri wako utatoshakabisa kutambua kwanini nakupenda hivyo sitegemei swali la namna hiyo. Tafadhali naomba unipokee." Kumbe Devid ni kama alimuwahi Rose maana naye alihitaji kuyanena yaleyale lakini aliona aibu tu. Na ndio maana alitumia sana vishawishi ilikujaribu kama angalau angeweza kumteka kimapenzi. Bila ajizi alisema kuwa, lengo lake kubwa mpaka kuja hapo shuleni sikwa ajili ya katalina bali ni kwa ajili yake. Na akaiongelea mara ya kwanza kuonana na Devi. Ilikuwa ni siku ambayo Katalina alikuwa anaumwa hivyo Rose akaenda kumuombea ruhusa hata alipoulizia mwalimu wa darasa ndipo alipoambiwa yupo bize. Ni kweli alikuwa bize lakini ubize wake haukumfanya Rose asimuone japo yeye hakumuona. Kwakuwa alikuwa na haraka aliamua kuomba namba za mwalimu yule kwa waalimu wenzie waliyokuwa nje ndipo walipompa. Lakini anasema kuwa alipomuona tu. Palepale alimpenda na ndio maana amefanya njama mpaka akapata kuonana naye. Devid alitumbua mimacho kama mjuzi aliyebanwa na mlango kwa kushangaa mambo yale. Palepale alianzisha penzi jingine kati yake na Rose. Mara kadhaa alitoa tahadhari huku akiichukuwa historia yake ya nyuma ya mapenzi ya usaliti kati yake yeye na Irene kama rejea ya tahadhari. Penzi lao lilichanua na ndani ya siku tano. Devid alienda kumtambulisha mpenzi wake nyumbani kwao. Mama yake alifurahi sana na kumsii mwanae aoe kama kweli huyo ndiye chaguo lake.

Naam.. Mwezi uliyofuata watu walikula pilau na nyama huku wakisherehekea ndoa ya Mr. And mrs. Devid. Walikula kiapo cha kutokuachana mpaka Mungu atakapozichukuwa roho zao. Watu waliyohudhuria ndoa ile walikenua meno yao mara kwa mara kutokana na shamlashamla za hapa na pale. Vijana wa kisasa wanasema ati fulu shangwe tu. Na ndivyo ilivyokuwa siku hiyo.

Naam.. Rose na Devid wakawa mke na mume. Wakaanza kuishi maisha yao rasmi. Maisha yalikuwa mazuri ndani ya mwezi mmoja ila yalianza kuingia doa baada ya mwezi huo kupita.

"Chanzo cha mabadiliko hayo yasiyopendeza ni mkewangu kipenzi. Hakika alitenda mambo mazito ambayo sitoyasahau katika maisha yangu. Mambo ambayo yalinifanya mie niwaone wanawake hawana maana na kuamua kuioa pombe." Aliongea Devid huku uchungu ukiwa umemjaa kwa muda huo. Aisha alikuwa na shauku ya kutaka kujua nini Devd alichotendewa haswa.

"Rose, nyie wanawake ni kama maua. Hunyauka tu hata kama mlianza kwa kupamba vipi. Nakumbuka kipindi hicho mke wangu alianza..."
* * *

Mke wa devid ambae ni Rose. Alianza kufura kwa hasira kila siku bila sababu za msingi. Akawa ni kama anamchukia mumewake. "Wewe mwanamume. Njoo uoshe vyombo. Mimi nataka kupumzika."

"Lakini mke wangu... Hapa siumenipa kazi ya kudeki? Mbona hivyo baby?"

"We mwanamume mbona mvivu sana. Hivi unategemea chai utapika muda gani kama tu kudeki unachelewa. Haya, hayo mavyombovyombo utaosha sangapi. Bwege wewe.."

"Mmmh! Basi mpenzi. Usikasilike nitafanya yote kwa haraka zaidi. Basi eti."

"aah! Hebu niache huko. Nani unamshika na mamikono yako hayo mabaya."

"Lakini mke wangu. Kwani mie kukushika kuna tatizo gani?"

Naam.. Hayo ndiyo maisha ya Devid baada ya mwezi mmoja wa ndoa. Hapo sasa akawa anachelewa kazini kutokana na kuchoka, akirudi nyumbani kutoka kazini. Mara afue, mara apige deki, mara aoshe vyombo, amtengee mkewe maji ya kuoga. Huku mke wake akibadili mapozi kwenye televisheni. Sio tu sebureni na nje. Bali hata chumbani mchezo wa ubabe uliendelea.

"Hebu niache...! Unanishika nini..? Kwahiyo kama mkeo?"

"Lakini mke wangu Rose. Hilo jambo sini haki yangu kama mumeo mbona unanifanyia hivyo jamani... Hebu tazama. Ni miezi mitatu sasa imepita bila wewe kunipa haki yangu. Huoni huo ni uonevu." Aliongea Devid huku akijisogeza na kujaribu tena kulifakamia umbile la mke wake.

"Haki haipo kwako. Bwege mkubwa wewe. Muone kwanza. Wewe humu ndani nimfanya kazi. Hujaoa wewe allaaah. Shika adabu yako juha wewe." Aliongea Rose tena bila hiyana. Hakuishia hapo akasema tena. "hebu kwanza shuka chini utandike hapo maana unanitia kinyaa. Sitaki hata kukugusa. Shuka chini!! Mbweha wewe.." Nae Devid hakuwa na jinsi zaidi ya kushuka chini kisha akalala. Na huo ndio ukawa mwanzo wa Devid kulala chini.

Siku hadi siku zilipita hatimae mtafaruku huo ulifika hadi miezi nane. Devid aliendelea kufanya kazi za nyumbani huku mkewake akiendelea kutumbulia macho televisheni. Usiku Devi alishindwa kuvumilia. Kama utaniakauanza mchezo wa kujichua uume wake. Kwa lugha ya magharibi wanaita 'masterburtion' ila kwetu sisi hutumia lugha ngumu kidogo. Kumradhi sitoitaja lugha hiyo. Lakini ndohivyo. Kujichua uume wake ukawa ndio mchezo wake kila usiku aliingia bafuni na mafuta kishaanavuta hisia na kuanza kufanya mapenzi na mkono wake huku akiiangalia picha ya mke wake. Mara kadhaa mkewe alishamkuta Devid akihangaishwa na penzi hilo. Lakini hakuna msaada aliyompatia zaidi ya kumcheka tu.

Masikini Devid aliuzoea sana mchezo ule na akaupenda sana. Hapo sasa akawa kila muda anapoenda kuoga lazma ajichue. Akimuona tu mke wake hisia zinampanda kuyafakamia mafuta. Mke wake aliendelea kumuona mume wake akitaabika.

Mama ndio kila kitu kwa mtoto. Mtoto hakui kwa mama hata siku moja. Kwakuwa mtu pekee wa karibu kwa devid alikuwa ni Mama yake hivyoaliamua kufunga safari na kwenda kumwambia mama yake. Mama alimpa ushauri wa kuvumilia kishaakamsihi kwamba amtegemee Mungu maana yeye ndie muweza wa kila jambo. Liwe kubwa liwe dogo hata lawastani.

"Sawa mama nimekuelewa" Aliongea Devid. Lakini katu hakuuongelea ule mchezo wake wa kujichua mbele ya mama yake.

"Hivi wewe Rose.... Mbona mumeo anakupenda, anakujali, anakuheshimu. Hakuna unachotaka ukakosa. Sasa iweje wewe humpatii haki yake na huu na ni miezi kadhaa sasa tangu uanze kumsumbua." Rose alikuwa ameinama muda wote. Kisha akajiinua huku amelowa uso wake na machozi.

"Mama.. Mimi nampenda mme wangu. Lakini yeye hanipendi. Mara zote amekuwa akinipiga, akinitesa kwakuninyanyapaa. Hata sasa halali na mimi. Yeye sikuhizi analala chini tu. Nikimuuliza kwanini. Ananijibu majibu ya chooni. Lakini sikweli kwamba mimi namtesa mume wangu Devid. Nampenda sana na ndio maana nimeamua kuolewa nae. Mamaa namp... " Ni kama alishindwa kuendelea kuongea kutokana na kilio kile kilichozaa kwikwi hadi Mama devid akamuhurumia mwinga wake huyo ambae alionesha kabisa dhahiri kuwa Mumewe ndio anaemtesa. Kwakuwa kilikuwa ni kikao. Basi devid nae alikuwepo. Lakini muda wote alikaa kimya kwani hakuwa na sauti mbele ya mke wake.

Ukimya wake ulitafsiriwa kuwa.. Ameumbuka, au amedharau maongezi yale. Na mwisho wa kikao yeye akawa na makosa.

Alionywa kutokumpiga mke wake. Kikao kile kilichobeba wazazi wa pande mbili kiliisha kwa mawaidha. Kisha waliondoka wazazi na kuwaacha wana ndoa wale.

"We mwanamume juha wewe.. Hivi kwa akili yako ulidhani kuwa utanishinda mimi eti! Sasa nakwambia hivi hiyo sijui haki yako hupati. Na mwendo wa kufua tu. Hapa bwege wewe... Allaaa." Aliongea mke wa Devid na hiyo ni baada ya kuyafuta machozi ya kinafki.

Devid.. Mawazo yakamjaa. Alijiona kama mtuhumiwa. Hakuwa na msaada kwenye kesi ile ngumu ya kuhujumu maisha yake. Akaanza kukonda kutokana na mawazo. Hata shuleni alijaza barua za ruhusa ndani ya ofisi ya headmaster.

Devid hakuiacha ile kazi yake ya utumwa. Kila siku aliosha vyombo, alifua nguo za kwake pamoja na za mke wake, halafu kama kawaida usiku hakulala kitandani bali alitandika chini iliasimuudhi mke wake.

" Eee Mola wangu. Ulisema hutomdhalilisha uliyomfanya rafiki. Na wala hautompa pumziko uliyemlaani. Pia niwewe huyohuyo ambae ulisema kuwa tuombe nawe utatupa. Basi mie nakuomba mbadilishe mke wangu mpendwa na umuongoze. Mpe utambuzi wakujua kwamba atendacho si sahihi na wala hakifai. Mfanye atambue kuwa mimi ni mmewe. Kumfulia nguo, kumpikia, na hata kupiga deki hizo si kazi zangu. Mke wangu kawa mkali zaidi ya mbwa wa polisi. Siwezi kumkanya kwasababu naogopa asijekuniacha ilhali bado na muhitaji. Nakutegemea wewe mwenyezi-Mungu. Naomba umfungulie njia mke wangu na umfanye aelewe kuwa atendacho si sahihi kwangu. Aamin." Ni kawaida ya Devid kumuombea mke wake kabla ya kulala. Muda huo Devi amuombeapo mke wake kumbe nae mke wake huomba kwa Mungu huyo huyo..

"Najua Mungu unanisikia. Sina kimbilio zaidi yako, nakuomba kwa neema zako niondolee huu mzigo. Nimeshafanya kila njia ilikumfanya mwanamume huyu aniondoke, mambo mengine ni magumu. Kila siku namfulisha nguo, nampigisha deki kwakudhani kuwa huenda atanisikia lakini nd'o kwanza anafanya yote nimwambiayo. Ee mola wangu. Nafsi yangu inaniuma mimi.. Japo nafanya mambo utadhani napenda lakini... Sikweli kwamba mie napenda kulala kitandani peke yangu kisha kumlaza mwenye kitanda chini. Laa. Nafanya hivyo ilikumchokoza iliakasirike na kunifukuza lakini ndio kwanza. Hata mawazo anaonekana hana. Kiukweli mimi simpendi mume wangu. Ila niliamua kuolewa nae baada tu ya kupewa pesa na Mama mkwe. Ni maradhi yapesa: upendo wangu ulikuwa kwenye pesa za Mama yake. Lakini yeye hakuwa moyoni hata kidogo. Nami nahitaji furaha yangu. Nimempata ninaempenda hivyo najitahidi kufanya visa ilianiache lakini ndio kwanza hata hanieldwi. Tafadhali nakuomba niondoe kwenye mateso haya mie nilihadaika na pesa tu. Lakini sikuwa na mapenzi kwake. Nakuomba mfanye atambue kuwa simtaki. Aaamin." Ni maombi ya Rose kabla hajalala.

ITAENDELEA.
 
Madame S

Madame S

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2015
Messages
15,035
Points
2,000
Madame S

Madame S

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2015
15,035 2,000
RIWAYA: KICHAA.

Na: ZUBER R. MAVUGO.

N0. 11.

ILIPOISHIA.

"Najua Mungu unanisikia. Sina kimbilio zaidi yako, nakuomba kwa neema zako niondolee huu mzigo. Nimeshafanya kila njia ilikumfanya mwanamume huyu aniondoke, mambo mengine ni magumu. Kila siku namfulisha nguo, nampigisha deki kwakudhani kuwa huenda atanisikia lakini nd'o kwanza anafanya yote nimwambiayo. Ee mola wangu. Nafsi yangu inaniuma mimi.. Japo nafanya mambo utadhani napenda lakini... Sikweli kwamba mie napenda kulala kitandani peke yangu kisha kumlaza mwenye kitanda chini. Laa. Nafanya hivyo ilikumchokoza iliakasirike na kunifukuza lakini ndio kwanza. Hata mawazo anaonekana hana. Kiukweli mimi simpendi mume wangu. Ila niliamua kuolewa nae baada tu ya kupewa pesa na Mama mkwe. Ni maradhi yapesa: upendo wangu ulikuwa kwenye pesa za Mama yake. Lakini yeye hakuwa moyoni hata kidogo. Nami nahitaji furaha yangu. Nimempata ninaempenda hivyo najitahidi kufanya visa ilianiache lakini ndio kwanza hata hanieldwi. Tafadhali nakuomba niondoe kwenye mateso haya mie nilihadaika na pesa tu. Lakini sikuwa na mapenzi kwake. Nakuomba mfanye atambue kuwa simtaki. Aaamin." Ni maombi ya Rose kabla hajalala.

ENDELEA.

Wote kwa pamoja hulala baada yakuwa wameomba hivyo.

Mke wa Devid akaanza tabia ya kwenda disko na kurejea usiku wa manane lakini devid alimfungulia hivyo hivyo bila kuonesha chuki ingawa nafsi haikupenda mambo yale. Lakini aliogopa kumkanya mke wake kwa kuhofu kuharibu ndoa.

Mke wa devid alipoona kuwa devid hana hata dalili ya kumuacha. Hapo sasa akaamua akodi mwanamume mwenye miraba minne kisha akamleta nyumbani na kumuingiza chumbani anapolala yeye na mumewe. Akaona kumuingiza haitoshi akaamua kumruhusu mwanamume yule auingilie mwili wake. Wakafanya ufuska wao juu ya kitanda alichonunua devid kwa mshahara wake aupatao kutokana na kazi yake ya ualimu. Kama hiyo haitoshi wakasinzia palepale huku wamewekeana mikono. Devid alipotoka kazini alishangaa kukuta mlango upo wazi halafu mke wake hayupo kwenye televisheni. Kwakuwa alikuwa amechoka aliona asijali sana na moja kwa moja alichukuliwa na miguu yake hadi chumbani.

Devid.. Alishindwa kuyaamini macho yake baada ya kuona jitu lenye miraba minne limemkumbatia mke wake. Tena kwenye kitanda alichonunua kwa pesa yake mwenyewe. Alikuwa ameshikiria kisanduku chake kidogo lakini mikono yake ilikosa nguvu nakujikuta amekiachia hadi chini. Hapo akili yake ikamtuma awavagae wawili wale na awape adhabu ilinganayo na maumivu aliyonayo.

"Nyie wapuuzi. Mmekosa gesti. Mpaka mmeamua kufanya ujinga huu ndani ya nyumba yangu tena kwenye kitanda changu. Halafu wewe mgoni wangu.. Hukujua kuwa huyu ni mke wangu?"

Hapo devidi akachukuwa pombe yake akanywa tena kisha akamfunulia Aisha shati na kumuonesha upande wa kushoto wa kifua chake. "Aisha... Hili kovu unaloliona. Si kwamba nilienda vitani kupigania nchi yangu. Hapana.. Ndio maana nilikwambia kuwa. Bora mke wangu pombe yeye hunipa raha na katu hanisaliti." Kisha akaendelea na historia ile...

* * * *

Lile janaume laana kabisa lile.. "Ndio ni mke wako. Lakini mimi huyu ni mpenzi wangu. Na kuhusu suala la kulala... Aliamua tu kunileta hapa nyumbani kwake kwakuwa alilalamika kuwa wewe huwezi kukitendea haki kitanda chako. Mie nipo hapa kwa ajili ya kukirudisha kwenye hadhi..." Akadakia mke wangu Rose. Huku akimtomasa mgöni wangu tena mbele yangu pasina kuhisi aibu.

"Majuha.. Huona kila watende walo nisahihi. Na hujifanya watii wa kila jambo. Kama kukwambia nimeshakwambia hadi mdomo ukachoka. Kama kukufanya uondoke nimeshajaribu sana. Lakini umeonesha ujuha wako. Sasa kama kusikia hukusikia inamaana hata vitendo hauvioni?" Aliongea huku akinibetulia midomo yake na kunifanya nikasirike zaidi. Hapo nikawa simjanja tena wa kuzizuia hasira zangu. Mkono ukaniponyoka na kuzalishakofi lililomfuata vilivyo mke wangu. Lilimpata kiukweli ukweli hadi akaenda chini na hiyo ndio mara yangu ya kwanza kumpiga mke wangu toka nianze kuishi nae.

Mke wangu alianza kulia utadhani nimemuonea sana..

Akiwa kwenye kilio kile mimi nilijiona mkosaji sana kwa muda huo. Mara nikashtuka baada ya kujikuta nipo chini huku damu zikinitoka puani na masikioni. Nilipojiuliza kilicho sababisha mimi kuwa vile. Ndipo nilipomuona mgoni wangu ambae kwa muda ule alikuwa ameikunja sura. Nilijaribu kusimama huku nikijipepesua lakini nilisukumwa na teke lililotua vilivyotumboni mwangu na kuniweka ukutani. Nilicheua damu nyingi na kuanzia hapo nikama nililala usingizi kwani sikusikia wala kuota. Zaidi ni yale maneno ya mwisho mwisho ambayo niliyasikia kwa taabu pindi mke wangu alivyokuwa akimwambia mgoni wangu kuwa.. Imetosha wasinipige zaidi.

Nilikuja kushtuka nipo hosipitali huku pamba zikiwa masikioni pamoja na jiraha la kisu upande wa kushoto mwa kifua changu. Nilijiuliza marambilimbili sababu ya mimi kulazwa pale ndipo nilipokumbuka kile kipigo nilichopokea baada ya kumuwasha kofi mke wangu. Nilipandwa na hasira baada ya kupapasa macho na kuona mke wangu yupo pale tena karibu kabisa na kitanda nilicholazwa huku akionesha huzuni kana kwamba siyeye aliyesababisha mie nilazwe pale. Nilijitahidi kunyanyuka kitandani pale ilinimuoneshe hasira zangu, lakini sikuweza kutokana na maumivu niliyokuwa nayo. Hapo ndipo nilipougundua udhaifu wangu mwingine kuwa sina nguvu hata za kunyanyuka pale.

"Wewe muuaji unalia nini? Hebu futa machozi ya kinafki na sitaki nikuone mbele ya macho yangu. Toka hapa.. Toka.." nilijikuta nikionge. Lakini chakushangaza daktari, nesi, mama, na rafiki zangu pamoja na mke wangu huyo ambae amesababisha nikawa kwenye hali ile. Walinishangaa na daktari akasema kuwa huenda akili yangu haipo sawa zaidi akamwambia nesi ati alete sindano ya usingizi. "Hapana dokta.. Mie nipo sawa kabisa. Tafadhali nitoleeni huyu mwanamke. Sitaki kumuona." Niropoka kwa uchungu huku akili yangu ikiendelea kukumbuka jinsi mke wangu alivyokuwa akimpa raha mwanamume mwingine tena mbele ya macho yangu. Zaidi ni pale nilipokumbuka kuwa yeye ndie alikuwa akimuamrisha mjinga yule anipige mimi. Nilipandwa na hasira nikaanza kujifukutua kwenye kitanda kile huku nikiyotoa madripu lakini sikufanikiwa kujitoa hata kitandani pale ila niliishia kujitonesha vidonda tu.

Nesi alileta dawa ya usingizi kishawakanichoma hapo nikapatwa na usingizi mzito ulio nichukuwa kama masaa ishirini na nne hivi. Niliposhituka nilikuwa peke yangu nilipotupa jicho upande wa pili ndipo nikamuona mke wangu. Nae aliponiona akainuka na kurudishia mlango wa wodi ile kishaakaniambia kuwa, yeye hakunipenda mimi bali alikuwa na shida na pesa tu. Akanipa hadithi kuwa, siku moja Baba yake alikuwa mgonjwa sana na yeye hakuwa na pesa ya kumtibia kwani hospitali walisema kuwa hawawezi waka mtibu baba yake bila kuleta pesa hiyo. Akiwa anatoka hospitali huku kichwa chake kimechanganyikiwa. Ndipo alipokutana na mama yangu na alipomuelezea tatizo. Mama akamwambia kuwa atumie usichana wake kunishawishi mimi kimapenzi mpaka nikubali kuolewa naye ili aweze kumsaidia pesa ile iliyokuwa ikihitajika hospitali iliaokoe maisha ya baba yake. Kwakuwa alikuwa na shida ndipo alipoamua kukubali iliaweze kusaidiwa na mama. Ni kweli mama alimsaidia na matibabu kwa baba yake yakaanza. Hapo mimi nikiwa sina hili wala lile nilijikuta na angukia kwenye mapenzi ya Rose na kwakuwa mama yangu alihitaji mke ndipo nilipoamua kumpatia furaha yake kwa kumuoa rose pasina kujua kuwa kuna siri nzito kati ya mama yangu pamoja na Rose. Mapenzi yalinoga ndani ya mwezi mmoja. Kumbe baba yake na rose ugonjwa wake ulizidi na kupoteza maisha. Hapo ndipo rose alipoanza kunitesa mimi kwakuwa sikuwa chaguo la moyo wake. Alifanya kila njia lakini zilishindikana ndipo alipoamua kuniadhibu kwa mtindo ule.

Alimaliza maneno yake na kuondoka hapohapo huku akiniambia kuwa nyumba yangu na vitu vyangu tayari ameuza kwahiyo nikipona nisitegemee chochote.

Kiukweli Aisha niliumia sana. Sikuwa na lakufanya zaidi ya kuchanganyikiwa tu. Nilimchukia mama yangu na kuona kuwa yeye ndio chanzo cha yote yale. Pia nilimchukia mke wangu kwakiapo cha kinafki mbele ya kanisa. Halafu nikaanza kufikiria kuwa nyumba yangu imeuzwa kwahiyo sina kwangu tena. Nilipiga moyo konde nikavumilia hospitali mule bila ruhusa nilitoroka. Nilienda kwa rafiki yangu mmoja lakini siku taka kwenda kwa mama yangu kwakuwa nilimchukia sana. Huko nilikaa hadi nilipopata nafuu na huko ndipo nilipoianza pombe kwani rafiki yangu yule alinishauri kuwa muondoaji wa mawazo ni pombe, na nilipoanza kunywa pombe nikaamua kuipa maisha yangu. Pombe akawa baba yangu, pia mama yangu na mke wangu pia. Kwakuwa kazi yangu iliota nyasi kutokana na kuja wakaguzi ambao walikagua shuleni nami nikaonekana simuhudhuriaji wa vipindi na nimeisababishia shule kushuka kitaaluma kutokana na mimi kuwa mwalimu wa taaluma. Ndipo nilipopoteza kazi yangu na sikuwa na laziada zaidi ya kutoka huko chato na kuamua kuja huku mwanza kwa ajili ya kumtafuta rafiki yangu mmoja ambae nilisomanae shule ya msingi...

Kwa mara ya kwanza nikatua ndani ya jiji hili la mwanza. Namshukuru Mungu nilipokelewa salama na rafiki yangu huyo. Tulicheka na hata tulipofika kwake mkewe alitupokea vizuri tukala na kunywa yaani fulu raha. Kwakuwa yeye ni maarufu kwa ufanyabiashara, aliona ni vyema tushilikiane. Hapo nikapata kazi kwa rafiki yangu huyo.

Niliendelea kunywa pombe huku nikiamini kuwa hiyo ndiyo starehe yangu pekee. Siku zilienda hatimae nilimaliza mwaka mzima kwa rafiki yangu yule. Kwakuwa nami kwa kipindi hicho nilikuwa nimejipanga. Niliamua kujenga nyumba na baada ya miezi sita nikahamia nyumbani kwangu maisha mapya nikayaanza. Huku mikono ya shukurani nikiendelea kuinyanyua kwa rafiki yangu yule aliyenifadhili.

Siku moja nikiwa nimetoka kupata moja moto moja baridi kama ilivyokawaida yangu. Nikiwa kwenye gari yangu mara ghafla nikamuona mtu mbele ya barabara. Nilivyomtizama kiumakini nikama nilimfahamu. Lakini alikuwa tofauti na nilivyomzoea. Nilipomkaribia nilimuita kwa jina lake.

"Rose..!" Akageuka na kunitazama. Akanigundua masikini. Nilimuonea huruma jinsi alivyokuwa amechoka na kuchakaa, mwili wake uliyounda umbo lake la mwanzo, haukuwepo tena. Ule uzuri wake wa awali ulikuwa umepotea na kuzalisha sura kavu yenye tabasamu la kuogofya. Roho ya huruma ilinijaa nikamuuliza wapi anakwenda nae akanijibu kuwa anakwenda kutafuta pakulala. Nilishangaa sana. Nikambeba kwenye gari langu kwakuwa nilimuhurumia sana.

Nilimchukua hadi kwangu na kumuuliza kipi kisa na mkasa mpaka akawa kwenye hali ile wakati mie nakumbuka aliniacha huku ameuza nyumba yangu. Swali langu ni kama liliyazalisha machozi yaliyokuwa yamejificha machoni mwa Rose.. Nilimuhurumia zaidi kwakuwa nilimpenda. Hapo akaniomba msamaha na kunihadithia kuwa, baada ya yeye kuondoka na kuniacha hospitali huku akiwa ameuza nyumba yangu na mali zangu. Aliamua kuondoka chato yeye pamoja na yule mwanamume ambae alihisi kuwa ni chaguo lake. Waliondoka na kuja huku Mwanza walipofika walifikia hotelini na kukaa huko huku wakifurahia maisha. Kwakuwa alimuamini yule mwanamume wake hakuona kama kuna haja ya kumnyima pesa. Akachukuwa pesa zote na kumkabidhi huku wakiwa na mawazo ya kununua nyumba pamoja na kufanya mambo mengine mengi. Hapo ndipo mwanamume yule alipoamua kumudhulumu pesa zote na kumuacha ndani ya hotel kwa siku tatu bila kuonekana. Bili ya hotel ilipoisha alifatwa na wahudumu kishaakaambiwa alipie bili nyingine aliomba muda nakuendelea kukaa kwa deni hotelini mule huku akimsubiria mumewake ambae kwa muda huo hakuwa anapatikana kwenye simu.

ITAENDELEA
 
Madame S

Madame S

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2015
Messages
15,035
Points
2,000
Madame S

Madame S

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2015
15,035 2,000
RIWAYA: KICHAA.

Na: ZUBER R. MAVUGO.

N0. 12.

ILIPOISHIA.

Nilimchukua hadi kwangu na kumuuliza kipi kisa na mkasa mpaka akawa kwenye hali ile wakati mie nakumbuka aliniacha huku ameuza nyumba yangu. Swali langu ni kama liliyazalisha machozi yaliyokuwa yamejificha machoni mwa Rose.. Nilimuhurumia zaidi kwakuwa nilimpenda. Hapo akaniomba msamaha na kunihadithia kuwa, baada ya yeye kuondoka na kuniacha hospitali huku akiwa ameuza nyumba yangu na mali zangu. Aliamua kuondoka chato yeye pamoja na yule mwanamume ambae alihisi kuwa ni chaguo lake. Waliondoka na kuja huku Mwanza walipofika walifikia hotelini na kukaa huko huku wakifurahia maisha. Kwakuwa alimuamini yule mwanamume wake hakuona kama kuna haja ya kumnyima pesa. Akachukuwa pesa zote na kumkabidhi huku wakiwa na mawazo ya kununua nyumba pamoja na kufanya mambo mengine mengi. Hapo ndipo mwanamume yule alipoamua kumudhulumu pesa zote na kumuacha ndani ya hotel kwa siku tatu bila kuonekana. Bili ya hotel ilipoisha alifatwa na wahudumu kishaakaambiwa alipie bili nyingine aliomba muda nakuendelea kukaa kwa deni hotelini mule huku akimsubiria mumewake ambae kwa muda huo hakuwa anapatikana kwenye simu.

ENDELEA.

. Ndipo rose alipokuja kushituka na kugundua kuwa ameibiwa. Masikini Rose akanyanganywa nguo, simu, pamoja na mali nyingine alizokuwa nazo ilikulipia fidia ya hoteli hiyo. Na hapo ndipo alipoanza kuishi kwa kutangatanga. Bila kula na alikoswakoswa kubakwa mara kadhaa na wahuni wapatikanao hata siku niliyokutana nae ilikuwa kama bahati maana alikuwa anahofu kutokana na kusakwa na wahuni wale aliowakimbia. Na hadithi yake ikaishia hapo.

Huwezi amini nilimuhurumia sana Rose, na nikajisemea kuwa atakuwa amejifunza, nikaona sina haja yakumtimua au kulipa kisasi chochote kile kwasababu tayari dunia imemfunza. Kwakuwa nilimpenda. Nikaamua kumsamehe na kurudi kuishi nae tena. Tumekaa miezi kama sita hivi. Mara siku moja nikiwa kazini nilishangaa napigiwa simu ati nyumba yangu imeuzwa, nilipofatilia nikaambiwa mke wangu Rose ndie ameiuza. Sikuamini, hapo ramani za maisha zikavurugika nikaanza kukopa kila siku hatimae madeni yaka nizidi. Nikajikuta naanza kuuza mali zangu hadi nguo. Nikakosa muelekeo wa maisha. Siku moja nikiwa natangatanga mtaani nilishangaa sana kukutana na Rose huku akiwa na yuleyule mwanamume wake. Hapo bila haya wala aibu usoni. Akaniambia kuwa huo ulikuwa ni mpango waliyoupanga kunifanya nipate taabu. Kisha Rose akaongeza kwakunambia kuwa mjini ni shule.

Niliumia sana, hapo sikuwa na jinsi. Nilijiona mjinga wa wajinga. Nilitamani kujiua lakini kila nilipofikiria nafsi iliniuma. Nikatamani kurudi kwetu lakini nisiwe na nauli. Hapo mtoto wa kiume nikafuta machozi na kuanza kuchakalika kwenye vibarua. Nilianza kwa kuokota taka taka, baada ya mwezi nikaingia kwenye ufundi seremala. Huko ndipo nilipopatia hutu tuvyombo na kununua kitanda cha urithi wa mtu aliyefiwa na babu yake. Nilitokwa na hamu na wanawake nikaiweka hamu hiyo kwenye pombe. Nikaona bora pombe aniibe pesa kuliko mwanamke. Nikaona bora pombe anipatie maumivu ya mapafu na kuchoma utumbo kuliko mwanamke. Kwanzia hapo nikawa nikitoka kazini napita kwenye pombe kisha nakuja nyumbani kulala. Na hiyo ndio historia ya mimi na pombe. Sitaki kuoa wala hakuna wakunishawishi kuoa katika hii dunia nimeshafunga pingu za maisha na pombe tu." Mlevi yule ajulikanae kwa jina la Devid. Alimaliza historia yake kishaakaendelea kunywa pombe yake. Hapo Aisha mapuya. Macho yaka mtoka na kwa muda huo alisahau kumnywesha maziwa mtoto wake Neema.

"Aisee.. Pole sana kaka yangu. Kwa jinsi ulivyoumia sidhani kama utakuwa unawapenda wanawake. Lakini kaka, si wote wapo hivyo. Tunatofautiana, kuna wale ambao wameiweka mioyo yao kwenye tamaa za mali lakini pia wapo ambao wanahitaji mapenzi na hawaongei wala kuwaza chochote kuhusu mali. Tafadhali kaka punguza hasira najua ni vigumu sana wewe kukubali kuishi na mwanamke tena, lakini hebu jiulize. Je, hiyo pombe itakupa mtoto ambae atakuwa mrithi wako? Je, hiyo pombe itakupa utajili au kukufanya uwe chini kila siku? Haya maisha tu kaka yangu na hizi ndizo changamoto za maisha. Kuitwa mwanamume siyo kujua kuranda mbao, au kujua kunywa kuliko wenzio huko baa. Wala kuitwa mwanamume siyo kulalamika hovyo. Bali ni kukabiliana na changamoto zote nasiyo kuzikimbia kaka yangu. Bado unanafasi nyingine katika maisha yako ya kuishi na mtu, hivyo nakuomba tafuta anaekufaa wewe oa. Kumbuka nawe una moyo sasa iweje ujifanye mgumu kama jiwe wakati moyo wako unanyama na unaruhusu maumivu? Pole sana kwa yaliyokusibu. Lakini yote tunayaita maisha." Aisha alitoa hotuba na mawaidha kwa pamoja. Kiukweli, mawazo ya Aisha yalibadilika roho ya huruma ilimuijia na kumthamini Mlevi Devid. Nadhani hakuwaza kama devid angekuwa ni mwenye kupitia mapito hayo. Yeye alikuwa akijua huenda Devid ni mtoto aliyezaliwa kwenye familiya ya hohehahe. Wasiyo na mbele wala nyuma. Alibakiwa na maswali ambayo aliweza kujijibu.

Maneno ya Aisha yalipita vilivyo kwenye masikio ya Devid lakini hayakuweza kuathiri chochote badala yake Devid alitoa majibu kuwa.. Mke wake yeye ni pombe. Mtoto wake ni pombe. Na kila kitu cha thamani kwake ni pombe.

Ni kweli kabisa Aisha asingeweza kuupingua msimamo mkali kutoka kwa devid. Hapo ndipo alipoamini kuwa kuna watu kwenye hii dunia wanamisimamo. Alifananisha tatizo lake kisha akafananisha na la Devid akajicheka na kujisemea kuwa,

"Nilikuwa nadhani mimi ndio mwenye matatizo makubwa. Kumbe wapo waliyoumia zaidi yangu." Devid, aliongeza jambo jipya kwa kusema,"Mama Neema. Mie niko radhi kumlea mwanao Neema kwa gharama yeyote ile. Na ninakuomba endelea kuishi namimi kama kaka na dada. Tumlee Neema wote kwa pamoja na siri hii iwe kati yetu. Tusiruhusu mtu ajue kuwa mimi na wewe ni mtu na dada yake. Fanya hivyo nakuomba." Neema alipata faraja na akaamini kweli kuna watu wema. Yaani hajazaa nae, wala si mpenzi wake lakini ameomba amlee mwanae tena waishi kama kaka na dada. Nasi.. Mtu na mume au mke wake. Alijikuta akiangua kilio cha furaha kwani hakuwahi kuamini kama kwenye hii dunia kuna mwanamume mwenye wema kama yule.

Miaka ilisonga hatimae Devid akafungua kijiwe chake mwenyewe cha ufundi seremala na kazi yake ikawa na heri. Mtoto neema alikuwa hadi akafikisha miaka nane. Shule alipelekwa ile ya serikali, huko nae hakuwa msumbufu ni kama alijua yupo shule kwa sababu gani. Alikuwa na kipaji cha kucheza mpira. Kipaji hicho kilianza kujionesha kwanzia nyumbani alipokuwa akicheza mipira ya kupondana hadi hapo alipokwenda shule ambapo aliwatesa wenzake na zaidi alikuwa mbaya pale alipoanza kuutumikia mpira wa pete. Wanafunzi na hata waalimu wake waliuona uwezo wa mtoto huyo mdogo aliye pigana vikumbo na madada zake kwenye mechi mbalimbali. Hakika uwezo wake ulikuwa wa kutatanisha sana. Kila mtu shuleni alimjua mtoto yule, walimu walimpenda na kutamani kuongea nae muda wote atokapo darasani. Kulingana na uwezo wa ajabu aliyokuwa nao mtoto yule. Kamati ya shule ilibidi iwaite wazazi wake na kuwaambia wazazi wa Neema kuwa kuna wazamini wamejitokeza na wamehitaji wa msomeshe Neema. Wazazi walipolipata jambo lile Mama wa neema aitwae Aisha yeye alimshauri Kaka yake wa hiyari ambae ni mlezi mwenzie ajulikanae kwa jina la Devid, kuwa ni bora wakubali kusaidiwa. Lakini Devid alikataa katakata. Nakusema kuwa.. Aliahidi kumlea Neema kwa jasho lake hivyo hakuhitaji usaidizi wowote.

"Baba, leo tumecheza mpira na timu ngumu!" aliongea Neema baada ya kumlaki Devid aliyekuwa amelewa kama ilivyo kawaida yake atokapo kazini. Ulevi wa devid haukumuathiri yeyote kwenye familia hiyo na ndio maana hata Neema alikuwa na uhuru wa kumkumbata Baba yake pasina kujali kuwa amelewa au la.

"Mwaa.. Mwaanangu. Wewe ni mwamba. Popote unatimba. Bila kuremba. Hebu njoo kwanza ndani mwanangu." Alimsifia kisha akaingia ndani alipofika alikaa kwenye kochi na Neema alikaa pembeni. Kisha Baba Neema akasema. "Kumbuka wewe ni mwamba. Popote unatimba. Tena bila kuremb. Kwahiyo sidhani kama uliremba kwenye hiyo mechi. Vipi, walihimili mikikimikiki ya Mwamba? Au walishindwa?" Aliuliza Baba Neema.

"Mmmh!! Baba.. Nadhani unanijua huwa sitanii kabisa kwenye anga zangu. Walijifanya wagumu lakini.. Mpaka sasa hawaamini kama ni mimi na udogo wangu." alijibu kwa majigambo Neema. Kama alivyozoea kumjibu baba yake huyo kipenzi.

"Nakujua mwanangu.. Hebu kwanza niitie huyo Mama yako." Akatoka Neema kisha akarejea. "Umemuacha wapi?" aliuliza kisha akajijibu baada ya kumuona Mama Neema.

"Mpenzi.. Kumbe umefika. Nilikuwa sijakusikia, si unajua namie ni kiwa bize na upishi. Enhee nambie kwema huko? Maana mwanao alivyonifuata!." Aliongea Mama Neema baada ya kufika sebuleni alipo Devid.

"Wewe mama Neema wewe... Ina bidi leo nikufumue haswa haswa."Alisema Devid.

"Jamaani.. Kwa kosa gani tena mume wangu?" Aliuliza Mama Neema kwa sauti ya upole.

"Neema!" Aliita baba Neema. Neema akaitika kisha baba Neema akaendelea. "Mwanangu. Nimpige mama yako? Au nisimpige.." Devid aliuliza kwa sauti ya upole huku akitingisha kichwa chake kilevi levi.

"Msamehe tu Baba yangu. Si unajua tena Mama mwenyewe hana hata pakupiga, ukimpiga utajitafutia kesi bure!" Aliongea Neema kisha Mama Neema akamsukuma Neema kichwa chake kwa kutumia kidole cha shahada kumaanisha kuwa hajapendezwa na kauli ya mwanae.

"e..eeeh. Una msonkola mwanangu. Wakati anakutetea." Alipanda juu Baba Neema.

"Kwani. Mume wangu nimekosa nini?"

"Eti.. Kwani mume wangu nimekosa nini?" aliigiza Maneno kwa Kubana pua kisha akasema. "Inamaana unataka kunambia kuwa hujui kama Mwanangu.. Hujampatia grucose ya kutosha. Hivi nimenunua grucose yote hiyo halafu mwanangu anachoka uwanjani. Kweli? Kama siyo hila za kumfanya superstar wangu ashindwe kufikia ndoto zake. We unadhani ninini ha..." kabla hata hajamalizia mkewe akadakia. "Jamaani.. Nilisahau kumpatia grucose lakini mbona hakunambia mimi. Eti wewe Neema mbona hukunambia mimi ukamwambia baba yako."

"e. Eeeh.. Usimtuhumu mwanangu kiasi hicho. Kwakuwa umekili kosa wewe nenda kapike halafu utuache tuendelèe na yetu. Au siyo Mwamba?"

"ndiyo.. Dady."

"Mama. Akikuchanganya unakuja kunambia. Wewe ni Mwamba popote unatimba. Oohoo."

Mama Neema alitoka na kwenda jikoni huku Neema na Baba yake wao wakiendelea kutaniana.

Chakula kilitengwa na wote kwa pamoja wakala. Huku wakitaniana na kudumisha amani yao. Kama ilivyo ada. Neema hulala na Mama yake, pia Baba Neema hulala kivyake. Ndivyo walivyofanya. Ilipofika asubuhi, Neema aliamshwa na Mama yake kisha akaoga na kuvaa nguo za shule, baada ya hapo alikunywa chai nzito kisha akaenda shule.

Maisha yaliendelea vilevile hadi hapo Neema alipofika darasa la sita ndipo rafiki yake wa kiume ajulikanae kwa jina la Mussa alipomletea barua ya kimapenzi. Siku hiyo Neema alichukia sana ingawa barua ile iliambatanishwa naombi la kutokumjuza yeyote lakini Neema alilipeleka swala lile hadi ofisini.

ITAENDELEA.
 
Madame S

Madame S

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2015
Messages
15,035
Points
2,000
Madame S

Madame S

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2015
15,035 2,000
RIWAYA: KICHAA.

Na: ZUBER R. MAVUGO.

N0. 13.

ILIPOISHIA.

"e. Eeeh.. Usimtuhumu mwanangu kiasi hicho. Kwakuwa umekili kosa wewe nenda kapike halafu utuache tuendelèe na yetu. Au siyo Mwamba?"

"ndiyo.. Dady."

"Mama. Akikuchanganya unakuja kunambia. Wewe ni Mwamba popote unatimba. Oohoo."

Mama Neema alitoka na kwenda jikoni huku Neema na Baba yake wao wakiendelea kutaniana.

Chakula kilitengwa na wote kwa pamoja wakala. Huku wakitaniana na kudumisha amani yao. Kama ilivyo ada. Neema hulala na Mama yake, pia Baba Neema hulala kivyake. Ndivyo walivyofanya. Ilipofika asubuhi, Neema aliamshwa na Mama yake kisha akaoga na kuvaa nguo za shule, baada ya hapo alikunywa chai nzito kisha akaenda shule.

Maisha yaliendelea vilevile hadi hapo Neema alipofika darasa la sita ndipo rafiki yake wa kiume ajulikanae kwa jina la Mussa alipomletea barua ya kimapenzi. Siku hiyo Neema alichukia sana ingawa barua ile iliambatanishwa naombi la kutokumjuza yeyote lakini Neema alilipeleka swala lile hadi ofisini.

ENDELEA.

"Unalia nini Neema." Ni sauti ya Madam Ana, aliyekuwa amesimama mlangoni mwa ofisi.

"Si.. Huyu Mussa. Eti ameniletea barua yenye tabia mbaya.." Alijibu Neema kisha akaulizwa ilichosema. Akajibu,"Mi sijui hata. Yeye ameandika eti ananipenda.. Mi nimeamua kuja kumsemea." alishtaki Neema huku akiendelea kulia.

"Basii.. Futa machozi. Hebu nenda kamuite hapa." Akatoka anakimbia. Kisha akaenda kumuita.

Mussa huwa anamuonea aibu sana Neema japo alimpenda lakini alishndwa kumwambia kwa kuogopa huenda angesemwa kwa mwalimu kwasababu Neema huwa anasuluhisha kesi zake stafu.

"Ni..ni..ni..nini tena. Ne..ne.. Neema?" aliuliza Musa kwa sauti ya uoga.

"Kwani hujui Musa? Hujui?.."

"Ni..ni..ni..nini. Tena mbona hivyo. Au tatizo ile barua." Aliuliza kwa upole Musa huku akimtuliza Neema ambae sasa alianza kupaza sauti hadi darasa zima wakasikia, wote kwa pamoja wakawageukia kina Neema na kuwashangaa.

"Inamaana. Hujui kuwa wewe uliniandikia barua ya tabia mbaya eti unanipenda. Sasa nimeenda kukusema kwa mwalimu.. Twende, ukafundishwe adabu." Hapo Musa akakosa nguvu na kuanza kulia kabla hata hajavuka mlango wa darasa. Wakati huo Neema alikuwa ameshaanza kuongoza njia ya kwenda kwa mwalimu. Darasa zima lilimuhurumia Musa kutokana na kesi ile ya mapenzi. Lakini halikuwa na lakufanya. Kwa upole Musa akaanza kujivuta hadi ofisini.

"Wewe.. Musa, hizi tabia mbaya mbaya za kuwatumia wenzio barua umeanza lini. Na ninani kakufunza?" Aliuliza madam Ana.

Musa kimya.

"Inamaana hunisikii au kiburi" Hapo Musa akazungusha kichwa chake mashariki na magharibi kwa kumaanisha kukataa.

"Unavyozungusha kichwaa inamaana unamaanisha huwezi kuongea au?"

"Hapana mwalimu. Naomba msamaha." Ni jibu alilotoa Musa huku akiwa amepiga magoti. Kwapembeni yake alikuwepo Neema ambae alionekana kulia kwa kosa la kupendwa.

Maadamu alimuuliza Neema, kuhusu adhabu ya kumpa Musa. "madamu.. Mimi sijui, ila nilikuja kumsema tu kwasababu sipendi tabia mbaya." Alijibu Neema. Hapohapo Neema aliagizwa viboko kisha waalimu kadhaa wakamzunguka Musa huku wanafunzi wanne wenye nguvu na maumbo makubwa wakimshika mikono na miguu kwa wakati huo tayari Musa alikwisha vuliwa unifomu zake za kushule na kubakizwa pensi iliyochanika chanika ovyo. Masikini Musa alichapwa viboko tena kwa zamu. Akichoka mwalimu huyu anaingia yule. Akichoka yule anaingia huyu. Mpaka anakuja kuachwa, tayari alikuwa amevimba kwanzia makalio, mapaja, mgongo, hadi mikono. Alilia bila machozi ilikujikaza mbele ya Neema. Lakini alikuwa tayari ameshapata aibu kutokana na kuvuliwa.

Musa alipomaliza kupokea adhabu yake alivaa uniform zake za shule na akaamua kuongeza kosa jingine la kutoroka shuleni. Aliona ni bora kutoroka kuliko aibu ile aliyoipata.

"Mamaaa! Ayaa... Pole pol.. Ayaa mama.."

"Hebu tulia nikukande vizuri."

"Mama, sasa mie sitaki maana wewe unanikanda utadhani unahasira namimi. Aya, bora uniache na maumivu yangu."

"sawa mwanangu achanikukande taratibu. Lakini siunajua tena dawa huwa chungu. Ila nawewe mwanangu punguza utundu. Ona leo umechapwa hivi. Kesho siutakuja hauna hata huu mwili."

Huo ulikuwa ni muda wa usiku pindi Mama Musa alipokuwa akiangaika kushughulikia majiraha ya Musa aliyoyapata shuleni. Musa alipoulizwa na mama yake juu ya kosa alilochapiwa. Alidanganya nakusema kuwa niuchelewaji tu wanamba.

Hatimae Musa alimaliza kukandwa na hakuwa na la ziada zaidi ya kwenda kufakamia kitanda chake.

"Mmmh! Ila namimi kwenye siku zote leo ndio nimeaibishwa. Yaani darasani wanafunzi sijui watanitazama vipi tu. Haya nikikutana na walimu sijui uso wangu nitauhifadhi wapi iliwasiuone. Mamamamama.. Bora hao, sasa vipi kwa Neema. Aliniona kipindi nachapwa ndani ya kaboka. Dah! Sijui hajawambia darasani wakaanza kunitania. Yaani.. Leo namimi nimepatikana, kama nyumbani kungekuwa na uwezo. Mimi ninge hama tu shule." Aliendelea kujisemea Musa peke yake huku akiwaza nini afanye ilikuepukana na ile adha.

"Au nimuache Neema. Lakini... Nikimuacha neema sind'o tajiongezea mawazo sana. Mimi neema simuachi hata nifanywe nini. Bora waniue tu." kwa muda huo Musa akiendelea kukizungusha kichwa chake ndani ya mji wa mawazo. Huku nako Neema nae alipata muda wa kupumzika vivyohivyo kama Musa nae alikuwa mawazoni., "Eti, Neema nakupenda sana.. Yaani tena anabahati leo angechapwa fimbo nyingi. Kumbe mimi kumuheshimu kama dada yake, yeye akaona alete mambo yakijinga jinga. Ngoja na nikimuona lazma nimchambe. Anabahati jana alijiwahi kutoroka tu. Ngoja nilale kesho nisijekuchelewa bure. Nataka nikamuoneshe chamtemakuni." Alijiwazia Neema kisha akayafumba macho yake. Haikumchukuwa muda sana usingizi ukawa umeshampitia.

Kama ilivyo ada Mama yake alimuamsha nakwenda shule, huku nae Musa aliamka na kwenda shule. Sikuhiyo Musa hakuwa na amani kabisa hata darasani alikuwa amejiinamia muda wote. Neema na kundi lake wakamfuata kwa ajili ya kwenda kumshushua.

"Enhee.. Wewe... Eti nakupenda. Yaani nilikuwa nakuheshimu lakini heshima yote imeshuka. Nakuona kama kinyago. Lione ukomtoto unakimbilia mambo makubwa. Unalooo! Hata kama nikitaka kupendwa mtu kama wewe mimi nikupeleke wapi sasa. Tena nikwambie, kwanzia leo.. Sitaki mazoea, nenda hukohuko na tabia zako zisizo na kichwa wala miguu. Allaaa. Hebu twendeni nadhani taarifa ameipata." Neema alimshushua huku marafiki zake kama kina jeska wakimsonkola kichwani Musa ambae muda wote aliinamia chini si kwasababu ya usingizi mzito. Bali kwasababu ya kuuhifadhi uso wake. Aliona ni bora viungo vingine viaibike lakini sio uso. Hakuwa na pamba masikioni japo alihitaji kuwa nazo iliasisikie alichokuwa akiambiwa. Walipoondoka kina Neema haukupita muda sana kengele ya mapumziko ikagongwa. Wanafunzi wote walitoka nje, isipokuwa Musa ambae aliendelea kujilaza kwenye dawati huku uso wake ukiwa umelowa machozi.

"Unamtafuta Musa? Daa.. Mwanangu Mkali wako leo kaaibishwa na kale kaneema."

"Weewee. Usinambie.. Nini tena?"

"Sijui alikatumia barua ya mapenzi jana. Sasa kakafura kichizi, siunajua kale huwa kesi zake zinatatuliwa kwa waalimu? Kaka mpeleka. Mchizi akadundwa ile mbaya. Aliona aibu na kwenda home, sasa kumbe kale kadem kalipanga na marafiki zake kuja kumchamba mkali Musa. Leo sasa.. Muda wa free, wakamvagaa mwana. Da, wakamchamba ileile. Halafu mwana ameinama tu, siunajua tena hakuwa na chakufanya. Ila pigo kama zile hazifai.. Sasa hivi sisi tumeshakuwa wakubwa maswala ya kusemana hayana inshu"

"Dah! Masikini.. Kwahiyo mkali Musa yuko wapi?"

"Sasa hivi. Yumo class amelala tu."

"Poa beka. Acha mie nikamcheki. Halafu huyo dem anaejiona anakunya keki mie nitadili nae."

"Poa Side. Achamie nikaombe ombe misuba huku. Siunajua madogo wa darasa la nne wengi wanapujapuja sana. Kwahiyo mie watanigeia tu."

Hayo yalikuwa ni maongezi kati ya Saidi ambae ni rafiki mkubwa wa Musa, pamoja na Bakari ambae nae ni rafiki wa Musa. Waliagana kisha Saidi akaenda hadi darasani kwa kina Musa na kumkuta rafiki yake kajiinamia. Alimuita lakini hakuitika, akamsogelea kisha akamuinua kichwa. Ndipo aliposhuhudia machozi ambayo sasa yalikauka kutokana na kulia sana kwa rafiki yake huyo. Alimuhurumia na kumuuliza kilichotokea, Musa alimuelezea kila kitu Side.. "Pole, ila we jikaze kiume.. Huyo demu anajifanya mzuri. Ngoja nitamuonyesha tu. Hawezi kukuzingua hivi mwanangu."

"Musa, achananae tu. Hajui analolitenda. Hajui kuwa mimi siwezi kula kama amenikasirikia, siwezi kulala kama amenizingua. Ipo siku atajua. Mie bado nampenda ukimzingua. Mwisho aache kunipa hata salamu halafu nikawa naumia zaidi."

"da.. Poa mwana usiongee sana mie nimekuelewa. Lakini lazma nimwambie kuwa alichofanya sio. " Aliongea Side.

"Nitashukuru kama hautomzingua. Nakujua wewe sekunde moja na kofi. Usimpige please. Siunajua japo naumia kwa yeye kunidhalilisha lakini bado nampenda?"

"poa. Usijali, achamie nirudi darasani kuandika,andika notes za kingereza. Siunajua jana sikuja skul, nilikuwa namishemishe home. Sasa teacher akikuta hujaandika Notes yeye hatakikujua."

"poa side. Achamie niendelee kuvumilia."

Waliagana marafiki wale. Side akaenda kuandika notes huku Musa akiendelea kubaki darasani. Haukupita muda kengele ya kurejea madarasani ikagongwa. Wanafunzi wote wakaanza kukimbizana kuyawahi madarasa. Wale waliyokuwa wakinunua misuba, walikimbia huku wengine wakiacha chenji zao kwa mama muuza. Ungepata muda wakuwaona, nadhani hapo ndipo ungeamini jinsi wanafunzi wanavyojua kuheshimu kengele. Wale waliyochelewa walipigishwa magoti na viöngozi wao. Kwakuwa hata viongozi wa wanafunzi hupokea rushwa hivyo mwenye shilingi mia au miambili yeye aliachwa na kwenda darasani huku wale wasio na pesa wakirukishwa vichura kupelekwa ofisini kwa ajili ya kupata adhabu.

Mwalimu kibalaghashia alikuwa na kipindi baada ya mapumziko kwenye darasa la kina Musa. Hivyo alichukuwa kitabu chake cha hesabu huku mkono mwingine ameshikiria fimbo na kwenda moja kwa moja hadi darasani mwa kina Musa.

"Motto" Aliropoka mmoja kati ya wanafunzi wa darasa lile. Kisha wanafunzi wote wakakaa kimya huku wale waliyokuwa wamekaa vibaya wakijirekebisha haraka na macho yao yote wakayaelekeza maeneo ya mlangoni. Wote kwa pamoja wakasimama..

"Elimu ni ufunguo wa maisha. Shikamoo mwalimu." Walisalimu na kutulia kimya utadhani maji mtungini.

"Mar-habaa. Hamjamboo?" Aliitikia salamu ya wanafunzi kisha akawauliza hali zao.

"Hatujambo.." Waliitikia wote kwa pamoja. Hata Musa nae aliitika ilhali alikuwa ni mgonjwa wa mawazo.

"OK, kama ilivyokawaida yetu. Atakaejibu swali ndie atakae kaa sawa?" wakaitikia wanafunzi baadhi. Huku wale wagonjwa wa hesabu wakikasirika na kuzidisha chuki kwa mwalimu wao.

Mwalimu aliuliza maswali na wote waliyojibu wakakaa. Kicha akafundisha na alivyomaliza alitoa zoezi kishaakaondoka.

Wakati wote huo Musa alikuwa akikumbuka viboko vingi alivyochapwa na walimu wake, kishaakawa akiyaangalia majiraha ambayo bado hayajapona. Hakuona haja ya kukaa darasani akaona bora atoroke maana shuleni paliendelea kumboa.

Alitoroka na kwenda kwa rafiki yake mchoraji ajulikanae kwajina la Macho.

"Oy, macho niaje."

"Shwari Musa. Vipi mbona mapema? Au umekuja kunivunja goti la chai. Nini"

"Aaaah! Hapana Macho. Mie nimekuja kusikilizia. Siunajua tena huko skul. Miyeyusho sana. Nimeona bora kuja huku kibandani kwako."

Kwakuwa Macho. Alikuwa ni mmoja kati ya wale ambao swala la Elimu lilisha wapita kushoto. Alifurahia uwepo wa Musa muda ule ambao musa angefaa kuwa darasani.
 
Madame S

Madame S

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2015
Messages
15,035
Points
2,000
Madame S

Madame S

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2015
15,035 2,000
RIWAYA: KICHAA.

Na: ZUBER R. MAVUGO.

N0. 14.

ILIPOISHIA.

"OK, kama ilivyokawaida yetu. Atakaejibu swali ndie atakae kaa sawa?" wakaitikia wanafunzi baadhi. Huku wale wagonjwa wa hesabu wakikasirika na kuzidisha chuki kwa mwalimu wao.

Mwalimu aliuliza maswali na wote waliyojibu wakakaa. Kicha akafundisha na alivyomaliza alitoa zoezi kishaakaondoka.

Wakati wote huo Musa alikuwa akikumbuka viboko vingi alivyochapwa na walimu wake, kishaakawa akiyaangalia majiraha ambayo bado hayajapona. Hakuona haja ya kukaa darasani akaona bora atoroke maana shuleni paliendelea kumboa.

Alitoroka na kwenda kwa rafiki yake mchoraji ajulikanae kwajina la Macho.

"Oy, macho niaje."

"Shwari Musa. Vipi mbona mapema? Au umekuja kunivunja goti la chai. Nini"

"Aaaah! Hapana Macho. Mie nimekuja kusikilizia. Siunajua tena huko skul. Miyeyusho sana. Nimeona bora kuja huku kibandani kwako."

Kwakuwa Macho. Alikuwa ni mmoja kati ya wale ambao swala la Elimu lilisha wapita kushoto. Alifurahia uwepo wa Musa muda ule ambao musa angefaa kuwa darasani.

ENDELEA.

Usihangaike kumjua macho.. Labda kiufupi... Macho ni mtoto wa Mzee Sadick, kabila la baba yake ni msukuma. Macho hakuwa na Mama kwasababu Mama yake alifariki kipindi Macho anazaliwa. Hivyo alilazimika kulelewa kigumu na baba yake. Kipaji cha kuchora kilijionesha pindi tu. Macho alivyojua kushikilia kalamu. Baba yake alimpeleka shule, lakini macho hakupenda shule. Aliwahi kurudia Darasa la nne kwa muda wa miaka minne. Kwakuwa alijua kumjumlisha na kutoa, pamoja na kuandika na kusoma vizuri. Hivyo aliona ni bora aachane na shule kishaakamuomba baba yake amfungulie kijiwe iliaanze kazi kupitia fani aliyonayo. Baba alimuelewa na kumfungulia. Mpaka muda huo Macho anamiaka saba kwenye kazi ile. Nailikuwa ikimlipa kama kawaida. Na hiyo ndio historia fupi ya Macho.

Mudi alimuelezea matatizo yake rafiki yake huyo. Nakwakuwa marafiki hao walipendana. Macho alimuhurumia sana Musa kwakuwa anayajua mapenzi kutokana na yeye kupitia hukohuko. Hakuona ajabu kumshauri rafiki yake huyo ambae alimzidi miaka tisa nyuma ya kuzaliwa.

"Hapa chamsingi ni kwenda kwa mganga ilikumfanya. Neema ajilete mwenyewe." Alishauri Macho.

"Hee! Wewe Macho. Waganga kazi yao sikutibu wagonjwa na kuwapa dawa. Sasa kwani mimi ni mgonjwa?" Alishangaa Musa.

"Ndio, wewe ni mgonjwa. Tena mgonjwa wa mapenzi.. Hivyo ni vyema kwenda kwa mganga iliakatupatie dawa za mapenzi."

"Inamaana unataka kunambia kuwa kuna dawa za mapenzi"

"Haa! We utajulia wapi mtoto wa juzi wewe... Kama kuna dawa ya malaria, ugonjwa unaoua. Ije Mapenzi tu," Akacheka Macho kisha akaendelea kusema, "Tena huyo msichana. Atajileta mwenyewe.. Hata kama alikuwa anakuchukia."

"weewee..! Macho tafadhali nipeleke sasa hivi. Siunajua tena. Na hamu yakuwa nae."

"Wewe usijali. Ngoja nimalizie hapa kazi za watu. Halafu nitakupeleka. Chamuhimu wewe nenda hom kabadili nguo. Kishaugeuze halafu twende sasa kwa mganga mahili asiyeshindwa hata siku moja."

palepale, Musa akaaga na kwenda kwao kubadili nguo. Alipofika alimsalimu mama yake na kupata chakula.

Alipomaliza kula, hapohapo akatoka mbio na kwenda moja kwa moja hadi kwa rafiki yake Macho. Alipofika akamkuta macho bado anafanyakazi. Akaendelea kumsubiri.

* * * *

Saa tisa na dakika ishirini ndio muda ambao hugongwa kengele ya mapumziko kabla ya kugongwa ile ya kutanyishwa. Ilivyogongwa kengele hiyo kila mwanafunzi alijiandaa, wale wana michezo wao waliwaza kwenda kushindana, wale walioanzisha dhambi ya mahusiano wao pia waliwaza kukutana, hata watorokaji pia hawakuwa nyuma huku wasiyopenda kusoma wakiona hicho ndicho kipindi bora kwao na zaidi walikuwa wakiomba kila siku wasisome bali wacheze tu.

"Neema twende tuwahi. Siunajua leo hatuna mazoezi bali tunacheza tu."

"ndio najua. Nyie fanyeni kutangulia mie namalizia kuweka madaftari yangu kwenye mfuko halafu nakuja huko."

"poa. Acha sie tutangulie."

Hayo yalikuwa ni majibizano kati ya Neema na marafiki zake. Neema aliachwa akiweka madaftari kwenye mfuko wake kisha wenzie wakatangulia. Alipomaliza akatoka nje na kuanza kuitafuta njia ya kwenda uwanjani.

Akiwa anaendelea kutembea huku akiwahi, mara akasikia anaitwa. Kugeuka nyuma, akamuona Side rafiki yake na Musa. Kwakuwa alimjua, hivyo hakuwa na haja ya kuendelea na safari bali alimsubiri.

"Mambo, Side?"

"Mabaya"

"mmh! Kwanini?"

"Inamaana unajifanya hujui kuwa kuna mtu ameumia, mwili na moyo kwa ajili yako? Unajifanya hujui kuwa kuna mtu mpaka sasa anaona aibu kutokana na wewe kumdhalilisha. Hebu fikiria, akitembea anahisi yupo uchi, anapopita watu wanamsontesheana mikono halafu eti unanishangaa kukwambia Mambo mabaya."

"Mbona sikuelewi Side. Kwani ninani huyo ambae nimemfanyia hivyo jamani?" hapo Neema akaanza kupata hamu ya kudadisi zaidi.

"Nani mwingine zaidi ya Musa.."

"Haa! Kumbe Musa. Huyo hatasinahuruma nae. Kwanza nilikuwa na muheshimu sana ila alichonifanyia.. Sihitaji hatakumuona."

"Kipi hicho alichokufanyia hadi usihitaji kumuona? Kipi Neema. Au kukwambia Anakupenda?"

"Kumbe, jibu unalo. Pigia msitari. Yaani bila hata aibu ananiletea barua. Mara, ooh nikilala nakuota, mara ooh, naomba ukubali kuwa namimi. Hivi kweli hata kama niwewe ungefanya nini. Kwakuwa alijifanya anajua kudhalilisha watu.. Nami nikaamua kumsema kwa mwalimu, halafu zaidi nikamchamba iliaelewe kuwa sikupenda."

"Kwahiyo Neema. Kosa la Musa hapo ninini?"

"Side, usitake kujifanya hujui kosa hapo. Mbona lipo wazi. Kosa ni kunitumia hiyo sijui barua yake ya ujingaujinga" Akajibu Neema huku akibetua mdomo wake ilikukazia kauli yake.

"Kwahiyo. Kukutumia barua ndio kosa, sindio?" akauliza Side.

"Pigia msitari" Akajibu Neema kwa ufupi.

"Anhaa! Je, angekufuata mwenyewe bila barua?" Akauliza tena swali jingine.

"Angenifata. Ili...?" alibwata Neema.

"Iliakwambie kile alichokuwa amekiandika."

"Usinichekeshe.. Ina maana wewe huoni kama hayo maneno, ni yakijingajinga. Sasa ananipenda, kwani nani kamwambia anipende." Aliongea Neema, huku akijihami iliasijiweke kwenye kosa.

"Neema. Hujajibu swali, bali umeelezea tu jambo ambalo hata halina maana. Ok, hebu nijibu inamaana unataka kunambia kuwa mtu akisema anakupenda wewe unahisi nikosa eti?" Aliuliza Side.

"Ndio.. Ni kosa."Alijibu Neema. Alipohisi maelezo yake haya ridhishi hapo akaongeza, "Kwani we Side. Unataka kunambia hujui kama Neno hilo hutumiwa na wakubwa. Au unauliza nini hasa." Side alicheka kidogo kicheko chadharau, kisha akasema; "kwani Neema. Wewe haumpendi mama yako? Au baba yako? Je, ukiwaambia kuwa unawapenda nikosa? Hebu acha utoto..." Side ni kama alimchokonoa Neema. Neema hapendi kuambiwa kuwa afanyacho ni utoto. Hapo akafura kwa hasira, sura yake ikabadilika, macho yakawakilisha kuwa amani imetoweka.

"Vipi mrembo! Umechukia kuambiwa uache utoto?. Ndio.. Acha utoto, we unadhani mtu mkubwa na akili zake timamu anaweza kumdhalilisha mwenzie eti kisa amemwambia anampenda. Mimi nilikuwa nakuona umekuwa kumbe bado unamambo ya kitoto. Hebu angalia umefaidika nini. Kumtukana Mtu eti kisa kakwambia anakupenda, öna umemfanya apigwe kisa anakupenda. Je unajua majiraha amekandwa nanani? Au ulikuwa tu unamsababishia majiraha eti. Haya umeona haitoshi sasa umemtangaza kila sehemu. We huoni huo ni utoto?" Maneno ya Side yalimuingia vilivyo Neema. Palepale akajiona mwenye makosa sana. Akaondoka bila hata kuaga huku akikimbia, aliusahau tena uwanja. Na hapo akaanza kushika njia ya kuelekea kwao. Njiani hakutaka kusemeshana na mtu.

"Vipi mwanangu mböna unakataa kula." Aliuliza mama Neema.

"Hapana mama. Sijisikii tu. Kula." Alijibu Neema huku akijitoa kwenye sofa na kuanza kuelekea chumbani.

"Au.. Unaumwa?" Aliuliza tena Mama Neema.

"Hapana. Siumwi wala nini mama."

Akaingia chumbani kisha akajifunika shuka gubigubi na kuendelea kujionea aibu. Alihisi dunia nzima imemuona kuwa yeye ni mtesaji wa viumbe. Aliumia sana kila alipofikiria jinsi alivyokuwa akimshushua Musa. Alijiona ni mwenye makosa sana.

Mawazo yakaanza kumuadhibu, huruma ikaanza kuumiza moyo.

Yaani nimemsema kwa mwalimu! Mtoto wa watu ameadhibiwa! Kadhalilishwa kwa kuvuliwa uniform zake mbele yangu!! Nimemfanya ashindwe kusoma.. Nimemtangaza kwa watu. Pia nimemfuata na kumuaibisha..! Haa!. Masikini naona aibu mie. Sijui nitaanzaje kumuomba msamaha. Ni baadhi ya mawazo yaliyoendelea kukisumbua kichwa chake.

Mama Neema alishindwa kuelewa kwasababu haikuwa kawaida kwa mwanae kurudi shule majira ya saa tisa tena hataki kula. Amefikia ndani na kujifungia. Aliwaza sana lakini hakutaka kumfatilia sana mwanae. Alihisi huenda wamepishana kauli huko shuleni.

..... ..... ... ....
"Karibuni.. Karibuni.. Najua mmekuja na matatizo sana. Semeni matatizo yenu ilimtatuliwe mbele ya mganga Ngulu.. Mganga wa waganga.. Hahahahaha...hahahahaha.." Ni sauti ya kuogfya iliyomtoka mganga Ngulu baada ya kuwakaribisha kina Musa ndani ya kijumba chake kidogo kilicho zungushiwa majani kwanzia juu hadi chini. Huku ndani ya kijumba hicho kukiwa na makolokolo mbalimbali. Vibuyu vidogo vidogo vilienea juu ya shuka jekundi lililotandikwa chini huku vichupa mbalimbali vikiwa vimejaa dawa zisizoeleweka. Si tu sauti ya mganga ngulu au mganga wa waganga iliyoogofya. Vilevile kitambaa cheusi alichojifunga mfungo wa lubega, huku akipitisha chekundu ilikuwianisha na kutengeneza vazi pamoja na kile kitambaa cheupe alichokifunga kichwani huku uso wake akiwa ameuchafua chafua kwa ungaunga wa madawa yake ndivyo vilimfanya aonekane kwenye muonekano wa kutisha na kuogofya zaidi.

Alichukuwa kibuyu chake kidogo kisha akakisogeza puani na kukinusa. "Chchaaa! Chchaaa! Chaaa!" Alipiga chafia tatu mfululizo kisha akasema, "Naitwa Makata, nimetoka pande za mashariki maghalibi, kusini kaskazini mwa saudiarabia. Nimekuja hapa kwasababu nimeitwa na wanadamu wenye shida. Tafadhali ongeeni shida zenu wala msiogope nami nitawatatulia." Ni sauti ya tofauti na ile ya kwanza aliyokuwa akiitoa mganga Ngulu. Sauti hii ya sasa ilimfanya Musa aogope zaidi na kujikuta akitetemeka tu lakini Macho yeye hakuwa kwenye uoga kwani ni mzoefu na kwa imani yake aliamini kuwa yule waliyokuwa wakimsikia si, mganga Ngulu bali ni jini lamganga ngulu.

"Sisi, tunashida.. Mlimwengu huyu anateseka sana. Kuna binti ametokea kumpenda sana. Kama unavyomuona Mlimwengu amefanya kila njia lakini ameshndwa ndio maana tumeamua kuja kwako iliangalau utusaidie." Alieleza matatizo Macho.

"Ni sikia matatizo yake. Mlimwengu hebu nipatie mkono wako." Akaambiwa Musa kisha Musa akamshika mkono mganga yule japo alikuwa anamuogopa. Baada ya mganga kushikana mkon na Musa akamwambia kuwa kila jambo atalosema sharti Musa aseme 'tawile' kama lipo sahihi.

"Je, unahitaji awe anakuwazia muda wote?"

"Tawile"

"Ha.ha.ha.ha. Sasa mlimwengu hapa umefika. Ha.ha.ha.ha.ha. Nakupa dawa. Dawa hii uwende ukajifukize. Kadri moshi utavyotoka ndivyo wewe unatakiwa utaje jina la huyo binti. Ha.ha.ha.ha.ha. Lakini dawa hii inamasharti. Masharti yenyewe, hautakiwi uiweke kwenye mkaa bali kwenye ukuni ilimoto unapofuka ufuke na ule wa ukuni."

"Tawile."

"Haya mie naondoka. Chamuhimu wewe fuata masharti. Lakini pia usiache kutoa Elfu tano kwa ajili ya kiti."

"Tawile."

Hapo mganga akajigeuza geuza shingo kwa nguvu kisha akajibwaga chini kwa dakika moja halafu baada ya hapo akawa kama fahamu zimemuijia na kuonesha kuwa hakuwa anajua chochote kilichokuwa kikiendelea maeneo yale.

Walitoa pesa na wakaaga kisha wakaondoka. Wakiwa njiani Musa hakusita kuulizia juu ya maajabu aliyoyaona kule kwa mganga na pia aliielezea hali yake ya uoga ambayo ilimpata. Yote kwa yote, Macho alimsihi Musa kuwa atimize masharti ilidawa ifanye kazi. Hatimae walifika sehemu na kuachana. Macho akaelekea kwao na Musa akaelekea kwao. Alipofika akachoma ile dawa kwenye ukuni kisha akaanza kujifukiza moshi huku akilitaja zaidi jina la Neema. Nakumuita. Ati Neema ndio amfuate Musa. Kitendo ambacho si rahisi.
 
Madame S

Madame S

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2015
Messages
15,035
Points
2,000
Madame S

Madame S

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2015
15,035 2,000
RIWAYA: KICHAA.

Na: ZUBER R. MAVUGO.

N0. 15.

ILIPOISHIA.

"Ha.ha.ha.ha. Sasa mlimwengu hapa umefika. Ha.ha.ha.ha.ha. Nakupa dawa. Dawa hii uwende ukajifukize. Kadri moshi utavyotoka ndivyo wewe unatakiwa utaje jina la huyo binti. Ha.ha.ha.ha.ha. Lakini dawa hii inamasharti. Masharti yenyewe, hautakiwi uiweke kwenye mkaa bali kwenye ukuni ilimoto unapofuka ufuke na ule wa ukuni."

"Tawile."

"Haya mie naondoka. Chamuhimu wewe fuata masharti. Lakini pia usiache kutoa Elfu tano kwa ajili ya kiti."

"Tawile."

Hapo mganga akajigeuza geuza shingo kwa nguvu kisha akajibwaga chini kwa dakika moja halafu baada ya hapo akawa kama fahamu zimemuijia na kuonesha kuwa hakuwa anajua chochote kilichokuwa kikiendelea maeneo yale.

Walitoa pesa na wakaaga kisha wakaondoka. Wakiwa njiani Musa hakusita kuulizia juu ya maajabu aliyoyaona kule kwa mganga na pia aliielezea hali yake ya uoga ambayo ilimpata. Yote kwa yote, Macho alimsihi Musa kuwa atimize masharti ilidawa ifanye kazi. Hatimae walifika sehemu na kuachana. Macho akaelekea kwao na Musa akaelekea kwao. Alipofika akachoma ile dawa kwenye ukuni kisha akaanza kujifukiza moshi huku akilitaja zaidi jina la Neema. Nakumuita. Ati Neema ndio amfuate Musa. Kitendo ambacho si rahisi.

ENDELEA.

Ilikuwa majira ya saa kumi na mbili jioni. Musa alikuwa chumbani mwake akijisomeasomea huku Mama Musa yeye akihangaika nje na kuwasha Moto kwa ajili ya maandalizi ya mapishi ya usiku. Muda huo, anaonekana Neema akiwa amevalia viatu vyenye uwezo wa kugonga nyoka, huku mwili wake ukiwa umefunikwa na gauni refu lililooana na kitambaa cheusi alichojitanda pamoja na mawani meusi. Neema safari yake ilikomea pale nje kwa kina Musa. Akasalimia kisha akauliza kama Musa yupo. Mama Musa alimjibu kuwa yumo na kumuelekeza chumba cha Musa.

"Hodi.." Aliongea baada ya kugonga mlango mara tatu kwa kutumia mkono wake wakulia. Ilikuwa ajabu sana kwa Musa kusikia sauti ya kike ambyo haifanani na ile ya Ma.yake. Alishazoea kusikia sauti ya rafiki zake wa kiume kama kina Side. Lakini siku hiyo alishangaa sana kusikia sauti yakike.

"Karibu.. Pita ndani" Aliongea Musa huku akijitengeneza kwa ajili ya kumpokea mgeni huyo asiye mjua.

"Ahsante." Aliitikia Nèema kisha akaanza kufungua mikanda ya viatu vyake na kuvivua.

Neema alipomaliza kuvua viatu vyake aliingia moja kwa moja hadi ndani. Alipoingia tu, aibu ikamjaa akashindwa hata kumtazama Musa.

Kimoyomoyo, Musa alifurahi na kuamini kuwa huenda dawa ya mganga itakuwa imefanya kazi. Hapo akatabasamu rohoni huku uso wake ameukunja kuashiria kuchukizwa na jambo alilotendewa na Neema.

"Enhee! Nambie umefuata nini nyumbani kwetu? Au nd'o umekuja kuniua kabisa eti?" Aliongea Musa.

"Hapana Musa usiseme hivyo.." kabla hata Neema hajamalizia maneno yake. Musa akadakia.

"Kumbe nisemeje.. Neema. Umenidhalilisha kisa na kupenda, umenifanya niadhibiwe pia. Halafu unakuja eti unanambia nisiseme hivyo. Tafadhali toka kwetu usije kuniua bure!" Akatulia kidogo. Hapo alipotulia ndipo Neema alipopatumia.

"Nia yangu sio kukuua wala kukuumiza. Bali nikukuomba msamaha. Samahani sana kwakukuumiza. Najua umeumia sana na mpaka sasa huna amani kisa mimi. Najua unashindwa hata kusoma kwa raha kisa mimi. Tafadhali naomba unisamehe mie sikujua kama kutatokea mambo yote hayo." Aliongea Neema huku machozi yakimchuruzika.

"Eti, Tafadhali naomba unisamehe mie sikujua kama yatatokea mambo hayo." Musa akanukuu kwa dharau maneno ya Neema kisha akaendelea. "Inamaana unataka kunambia, kipindi unaichukua hiyo miguu yako na kuipeleka stafu. Hukujua kama ukinisema nitaadhibiwa? Au unataka kunambia kuwa hukusoma mwisho wa barua pale nilipokuomba kuwa iwe siri yako? Sasa haukujua kama kitatokea kitu gani. Au umekuja kunikashfu eti?" Hapo Neema akaongeza kilio chake cha kwikwi huku moko wake wa kushoto akiutumia kujifutia machozi yaliyokuwa yakimtoka. Hakuwa na jinsi, akashuka hadi chini na kuishikiria miguu ya Musa huku yeye akiwa amepiga magoti kisha akaendelea kuomba msamaha, "Ni kweli.. Ni kweli kabisa Musa. Nilikufanyia yote hayo. Nimekusema kwa mwalimu ukaadhibiwa tena mbele ya macho yangu kwa udhalilishaji wa hali ya juu. Lakini mpaka sasa nimetambua kosa. Na sitorudia tena kufanya hivyo. Naomba unisamehe nipochini ya miguu yako." Hapo Musa alikuwa si mwenye kujali maombi ya Neema bali aliendelea kufurahia ile hali ya kunyenyekewa na msichana anaempenda. Aliendelea kufurahi moyoni huku akijiaminisha kuwa, ile dawa ya mganga ndio iliyomuita Neema. Kwakuwa lengo lake ni kukubaliwa nasio kuombwa msamaha. Hapo sasa akaanza kutumia sayansi ya ulimi ilikuvumbua upendo wake uliyojificha moyoni mwa Neema.

Alijitahidi sana kutupa maneno yenye uwezo wa kumdhoofisha Neema. Lakini Neema alionesha kupinga vikali tena kwa mifano bayana.

"Mi, siwezi kuwa na mpenzi. Bado mdogo sana. Umri wangu haujafikia kiwango chakumiliki mvulana. Halafu labda nikupe ushauri kaka yangu... Wewe bado upo mdogo. Yanini uyawahi? Mapenzi yapo tu. Subiri umri wako utafika utayapitia hadi utayachoka. Hebu tusome acha hizo tabia mbaya. Mie sipendi rafiki mwenye tabia mbaya." Hayo ni baadhi tu ya maneno yaliyomtoka Neema baada tu yakuachiwa upenyo wa kuongea. Ni kama Musa alifanya kosa kumsamehe Neema kwani hapo alikutana na ushauri hadi akaanza kuona aibu. Mwisho wa siku waliachana bila kufikia muafaka. Neema alikumbatia msimamo wake huku Musa akimuomba akajaribu kufikiria tena.

Usiku wa siku hiyo Musa alimtembelea rafiki yake macho na kumueleza mafanikio ya ile dawa waliyopewa na mganga. Macho alifurahi na kumsihi rafiki yake kuwa asikate tamaa kwani mwanzo huwa ni mgumu.

Walipomaliza maongezi yao, Musa akaaga kishaakaenda kwao kula. Siku hiyo alikuwa na furaha hadi mama yake akamshangaa.

Alipomaliza kula akamuaga mama yake kishaakaenda kwa rafiki yake Side usiku huohuo.

Alimkuta side ameshaanza kuupata usingizi. Lakini hakukubali maneno yake yalale. Akamuamsha kishaakaanza kumpa stori. "Unajua Side, mi nauhakika ile dawa ya mganga niliyojifukiza ndiyo iliyosababisha yote yale. Maana huwezi amini mtoto mwenyewe akajileta. Minilidhani labda amekuja kuniharibia hadi kwa mama. Ila chakushangaza mtoto akaanza kuomba msamaha. Hadi machozi yakamtoka. Mimi nikasema Yes! Dawa inafanya kazi.. Hapo nikaanza kujishaua shaua. Mara nikatae mara nafsi ikubali. Mtoto akashndwa kuvumilia. Mwennyewe akashuka chini. Ooh, nisamehe, sijui sikutegemea kufanya hivyo. Basi mie nikamkazia utadhani nimekasirika kweli. Ila mwisho wa siku nikamsamehe kwakudhani huenda labda.. Labda mwenyewe amenikubali. Chakushangaza nilipoanza kumuingzia swaga za mapenzi. Dogo akazingua kinyama. Halafu akajifanya mama ushauri yaani.. Leo nimepewa ushauri we acha tu."

"We unauhakika gani kama huyo mganga ndio kakusaidia? Afu acha inshu zako nawewe. Mie dogo nimemuita skul nikampa mabango hadi akaona aibu. Amekuja kukuomba msamaha kisa mimi na siyo madawa ya mganga wako. Halafu huenda angekubali kuwa nawe sema ujinga wako tu. Wakutumia madawa ndio umekuharibia bwege wewe." Akasema Side na kumfanya Musa abakikwenye mshangao.

"Ku..ku..kumbe ni wewe uliyeøngea nae?" Aliuliza Musa huku akiwa amejawa na kigugumizi mdomoni kwani hakutaraji habari ile kutoka kwa Side.

"Kumbe ulijua ni hayo madawa ya mganga wako. Afu nilikuwa nakukaushia tu kipindi unamsifia,sifia huyo mganga wako. Lakini poa tu kwasababu we ni mkali wangu ila angekuwa mwingine tungezenguana mie inshu za kuamini waganga sifagilii. Mwanamume hatongozei wanawake kwa dawa. Bali hutumia maneno matamu yenye ladha isiyomithilika."

"Poa Side nashukuru sana kunisaidia. Lakini... Kwa jinsi ni mjuavyo Neema si mrahisi namna ile. Nadhani hata wewe nishahidi. Neema alishawahi kunipiga shiti mbele ya darasa, ila mwanangu.. Wewe ni noma. Hebu namimi nipe kanuni uliyotumia hadi kumkokotoa mtoto anaejifanya mgumu kama swali la hesabu." Aliongea Musa kisha akajiweka sawa kusikiliza. Huku kwa muda huo rafiki yake Side akitoa kicheko cha kebehi.

"Sikia mwanangu. Hawa mademu huwa hawana kanuni ila hushindwa kulingana na maneno yao.

Unajua hakuna kiumbe dhaifu kama mwanamke. Yaani ni waoga, wapole, watu wanaopenda amani siku zote. Ila hujifanya wakali, hawaogopi, eti wanashushua wanaume mbele ya watu. Kiukweli wanawake wote ni waoga. Ukiwa kama mwanamume. Unanjia nyingi za kumfanya msichana akuelewe. Labda utake tu mwenyewe." Akakohoa kidogo side kishaakaendelea, "Hakuna kanuni ya mwanamke hata ukijaribu kumtafutia kanuni utaishia kuumia. Wewe njia ya kukuokoa mbele yao ni kuutumia udhaifu wao ilikuwapata. Kwamfano, Mwanamke akiwa anajifanya anajua kuongea sana ujue huo ndio udhaifu wake. Sasa kujua hivyo tayari utamshinda kwani utakuwa umeingia vitani huku umemsoma adui wako. Pia kuna wale wanawake wenye dharau.. Yaani unaweza ukamuita akakutukana, au ukamuomba kuongea nae yeye akawa anajifanya hana muda. Sasa hao nao pia huo ndio udhaifu wao sasa nijukumu lako wewe kuutumia udhaifu wao iliuwashinde. Amini wanawake ni waoga kama unabisha hebu chukua hata kadudu halafu kaweke kwenye shati au kichwa au sehemu yeyote kwa msichana unaehisi huyo ni jasiri kisha muoneshe uone jinsi atakavyohangaika kwa uoga na makelele. Sasa ule ukelele ndio tofauti ya wewe na yeye hivyo wanawake ni waoga. Tena nikupe siri nyingine. Hujifanya hawana huruma kumbe wao ndio wenye huruma kuliko chochote dunia hii. Sasa huruma ni udhaifu, tumia huruma yao kuwateka akili na mioyo yao. Ni maneno, na vitendo pamoja na hisia pekee ndivyo vitu vitavyokufanya uweze kupata utakacho kwa Neema wala siyo Imani. Imani haina msaada kwako pindi utongozapo tena usilete maongezi ya imani maana utajiharibia kumbuka, kutongoza ni sayansi au sanaa ya ushawishi. Mshawishi yeyote hutegemea lugha ilikufanikiwa. Lugha ndio kiungo pekee kitakachokufanya ufanikiwe. Ukitumia lugha ya chooni Neema atakufananisha na choo, ukitumia lugha ya sokoni Neema atakufananisha na Soko lakini ukitumia lugha ya kiume lazma ufananishwe na mwanamume. Mimi nilitumia lugha ya kiume ndio maana Neema alinielewa na kujakukuomba msamaha." Aliongea Side maneno ambayo kwa Musa yalikuwa ni zaidi ya elimu kwani hakuwahi kuyajua hapo kabla. Musa alimshukuru sana rafiki yake na kumuahidi kuwa ataachana na masuala ya waganga. Kwakuwa usiku ulikuwa umezidi, hakuwa na laziada hapo alimuaga rafiki yake na kurudi kwao kulala.

.... ... ...

Ilikuwa ni majira ya saa saba usiku kama ilivyosoma saa iliyokuwa ukutani mwa chumba anacholala Neema. Muda huo mama Neema alikuwa akikoroma tu. Upande mwingine wakitanda huku upande aliyopo Neema akiendelea kushindana na mawazo yaliyomsumbua kichwani. Alilazimisha kulala lakini mawazo yaliendelea kumlazimisha asilale. Kila akifumba macho ilikuzalisha usingizi. Utasa wa macho yake ulijionesha na usingizi wake ni kama ulipeperuka na kwenda asipopajua. Alibaki amefumbua macho huku akilazimishwa na mawazo kumuwaza kijana aliyemfanyia matukio ya ajabu.

"Wewe Moyo wangu. Hebu usiniumbue mwenzio. Nakuomba usimuweke mtu, tafadhali nakusihi. Mama alisema mapenzi ndio muharibifu wa maisha, sasa mbona wewe Moyo unaishara za kupenda? Nakuuliza wewe.. Unajifanya hunisikii eti? Kwani sio wewe uliyeshauriana na akili huko nyuma na kuahidi kupenda masomo? Sasa mbona najihisi mapenzi,mapenzi tu. Aaah! Usijifanye huijui ilekauli ya baba. Mimi ni mwamba, popote na timba tu." Ni baadhi tu ya mashtaka aliyoyatoa Neema kuupatia Moyo wake. Alijilaumu kujikuta amependa lakini pia alifurahia jinsi mapenzi yalivyompeleka.

Kesho yake alienda shule baada ya kufanya mazoezi kwenye chumba chake cha mazoezi.
 

Forum statistics

Threads 1,336,205
Members 512,562
Posts 32,530,421
Top