Riwaya : Kichaa

Riwaya : Kichaa

RIWAYA: KICHAA.

Na: ZUBER R. MAVUGO.

N0. 16.

ENDELEA.

"Wewe Moyo wangu. Hebu usiniumbue mwenzio. Nakuomba usimuweke mtu, tafadhali nakusihi. Mama alisema mapenzi ndio muharibifu wa maisha, sasa mbona wewe Moyo unaishara za kupenda? Nakuuliza wewe.. Unajifanya hunisikii eti? Kwani sio wewe uliyeshauriana na akili huko nyuma na kuahidi kupenda masomo? Sasa mbona najihisi mapenzi,mapenzi tu. Aaah! Usijifanye huijui ilekauli ya baba. Mimi ni mwamba, popote na timba tu." Ni baadhi tu ya mashtaka aliyoyatoa Neema kuupatia Moyo wake. Alijilaumu kujikuta amependa lakini pia alifurahia jinsi mapenzi yalivyompeleka.

Kesho yake alienda shule baada ya kufanya mazoezi kwenye chumba chake cha mazoezi.

... .. ...

Siku hiyo Mama Neema aliamka vizuri na kufanya usafi kama kawaida. Alipomaliza kazi aliamua kwenda kwa rafiki yake kwa ajili ya kupiga stori maana hakuwa na kazi ya kufanya kwa muda huo. Huko kwa rafiki yake waliteta wakiwa kwenye maongezi yao mara ghafla alipita Kichaa mmoja aliyekuwa ameshikilia mfuniko wa ndoo huku mdomo wake akiutumia kama sauti ya gari. Alipiga sauti za honi kwa mdomo huku akitumia mfuniko kama usukani wa gari yake. Alifika hadi maeneo waliyokuwepo kina Mama Neema.

"Wewe.. Mwehu wewe. Hebu toka hapa nyie ndio waleta nuksi." Ni sauti ya rafiki yake na Mama Neema iliyofoka.

"Jamaniii... Sio vizuri hivyo dada Suzi..." Alidakia Mama Neema baada ya kumsikia shoga yake akiendelea kumfokea yule kichaa.

"Kumbe vizuri niaje Mama Neema!.. We unadhani hiyo harufu ya jalala anayonuka nani wa kuivumilia." Alidakia shoga yake mama Neema ajulikanae kwa jina la Suzi.

"Ni kweli, ananuka.. Lakini ungemwambia tu vizuri. Nasiyo kumfokea kama hivyo."

"Ma. Neema.. Mimi siyokuwafokea tu. Hata maji ya moto huwa nawamwagia kabisa. Hawana adabu wala heshima. Hebu lione hapo nimelitukana ilabado linajichekelesha. Licheki na miudende yake inalitoka tu mdomoni hadi kinyaa." Akatema mate chini kisha akafoka, "We mwehu inamaana bado husikii eti?" Akachukua kikombe cha maji kilichokuwa karibu na mguu wa Ma'Neema. Akampondea mwehu yule.

"Jamaani... Mungu hapendi hivyo da'Suzi. Hebu jiulize hata kama ungekuwa wewe au ndugu yako anafanyiwa hivyo ungejisikiaje. Sio vi..."

"E..eee.. Ma'Neema usinichefue... Kama unatetea wehu kivyako. Mimi siwezi hurumia mwehu tena niache tusije tukakosana. Ohooo, kwanza toka.. Sitaki kukuona hata hapa kwangu." Suzi alisema maneno yale baada ya kudakia kauli ya mama Neema. Hapo akajiinua kwenye mkeka alipokuwa ameyatunza makaliyo yake. Kisha akavaa viatu na kujiingiza ndani mwake huku amefura.

Mama Neema. Alibaki pale nje akimshuhudia Mwehu yule ambae kwa muda huo alikuwa akiendesha gari lake la mfuniko wa ndoo. Alimuhurumia sana lakini asimsaidie.

Hakuwa najinsi zaidi ya kuchukuliwa na miguu yake kwa hiyari na kupelekwa moja kwa moja hadi ndani ya nyumbani kwake alipofika alijibwaga kwenye sofa huku akili yake akiirudisha kwa Suzi ambae alionekana kutokuwa na huruma hata kidogo. Kitendo kile kilimfanya akumbuke kesi ambayo ingemfanya aingize shingo yake kwenye kitanzi au ahukumiwe kifungo cha maisha. Alimkumbuka sana yule mtu aliyemsaidia kuepuka kesi ile. Mtu aliyeonekana kama kichaa. Akakumbuka ushauri wa kichaa yule kipindi anamnyanganya kile kisu alichokitumia kuuchomoa uhai wa Afande Kipara. Akakumbuka kuwa, Kichaa yule aliyemuokoa na kesi ya mauaji ndie aliyemfanya awaheshimu watu wote wanaotembea jalalani na mitaani huku miili yao wameivika madaso yaliyooza, midomo yao muda wote ikiropoka pasina kujali muktadha. Hapo tena akamfikilia huyo shoga yake suzi ambae bila haya alimtukana Mwehu kwa kosa tu lakupita pembezoni mwa mkeka waliyokuwa wamewekea makalio na miguu yao.

"Eee Mungu.. Najua yule kichaa wa watu aliejitolea kifo kwa ajili ya kunihurumia. Kwa sasa atakuwa yupo mbele ya haki. Nakuomba msamehe madhambi yake na umpatie uzima na faraja ya roho huko aliko." Alijitamkia Mama Neema huku akimkumbuka kichaa yule aliyejitambulisha kwa jina la Mavugo, huku akiamini kabisa.. Kichaa yule hatokuwa duniani kwa muda ule kwani ni miaka mingi imeshapita toka waachane siku ile ambayo mama Neema hatoisahau ingawa kwa kipindi kile hakuwa anaitwa Mama Neema bali Aisha Mapuya. Alipitiwa na usingizi palepale kwenye sofa.

.... ...

Siku hiyo Neema hakuwa na raha kabisa hasa kila alipotupa jicho upande wa nyuma kule kwenye madawati ya mwisho na kuiona sura ya upole aliyoivaa Musa. Muda wote Neema alijihisi aibu. Musa na Neema waliendelea kukatana macho kwa mavizio ya zamu. Mwalimu akigeuka kuandika Neema aligeuza shingo yake na kuyatupa macho yake usoni mwa Musa ambae kwa muda huo yeye aliyatupa chini ya dawati ilikuyasitili. Kwa upande wa Musa yeye aliyatupa Macho yake mwilini mwa neema pindi ambapo mwalimu alikuwa bize kwenye maongezi. Waliendelea na kamchezo kao kakutupiana macho na wakati mwingine walipata ajali za kugongana uso kwa uso lakini wote kwa pamoja walijishtukia na kuyainamisha chini macho yao ilimradi tu aibu aibu.

Ulipoisha muda wa vipindi, Neema alienda kwenye dawati la Musa na kuwaomba wale marafiki wa musa wa mpishe kidogo kwani alikuwa na maongezi kidogo na Musa.

Rafiki wa Musa pamoja na wanafunzi wengine walishangazwa sana na kitendo kile maana wanajua wazi kuwa Neema na Musa si marafiki kwani walitukanana na kupelekana hadi kwa walimu. Wale wanafunzi wenye midomo walianza minong'ong'ono ya chini,chini. Huku vichwa vya habari vyao vikiwa ni Neema na Musa.

"vipi Musa bado umenikasirikia?" Aliuliza Neema baada ya kujuliana hali na kupeana salamu.

"Hapana Neema. Mbona nipo fresh tu."

"Anhaa.. Poa."

"Ok. Usijali."

Ukazuka ukimya wa muda kati yao. Huku wote wawili wakipatwa nauoga uliopelekea hata sauti zao kujawa na mitetemiko ya hapa na pale.

Musa akajitutumua na kuuliza,"Vipi.. Unamishe yeyote mbona backbench?" hapo Neema akaanza kujing'atang'ata kutafuta maneno. Huku jasho likianza kumtoka kwapani.

"Nn..nili...nilii.. Hapana. Nilitaka tu kukuomba unifunze alichofundisha mwalimu maana sikumuelewa kabisa." Alijibu Neema huku akiikanyagakanyaga miguu yake.

"Kwanini hujamuelewa mwalimu? Au haukuwa makini, e?" Alihoji Musa.

"Hapana nilikuwa makini lakini sijamuelewa. Ufundishaji wake sijui haukuwa mzuri?" Alijitetea Neema.

"Mmmh! Mbona ameeleweka tu. Ok, na mbona alipotoa ruhusa ya wanafunzi ambao hawajaelewa kunyoosha mkono. Wewe hauku nyoosha wakati haukuelewa." Musa aliendelea kutengeneza hoja mbalimbali ilikumfanya Neema azidi kujitetea zaidi.

Mwisho wa siku Musa aliamua kumuelekeza yale aliyofundisha mwalimu. Alimsihi kuwa awe makini sana pindi mwalimu awamo darasani na kumwambia kuwa kuna mambo ambayo huwa ni ya siri sana yamtokayo mwalimu pindi afundishapo jambo fulani hivyo nijukumu lake kuwa msikivu na mtulivu. Neema aliinua kichwa chake kuonesha amekubali yaliyosemwa na Musa.

Siku hiyo Neema alikuwa muda wote yupo na Musa kwanzia ndani na hata nje ya darasa jambo lililopelekea walimu na wanafunzi hasa wanaofahamu ugomvi wa wawili hao kupata hofu.

"Neema... Umenisindikiza hadi huku halafu ushindwe kuingia home. Kweli?"

"Usijali, acha niende nyumbani kwanza huwa sipendi kupitia kwenye nyumba yeyote kabla ya kupitia kwetu."

"Kwanini, hupendi? Au ukipita huwa unakaukiwa damu?" Alipohoji swali lile Musa ni kama alimtekenya Neema. Hapo akaanza kucheka. Kishaakasema," Yaani wewe unavituko." Akawa makini kidogo na kuendelea, "Hapana.. Hapana hayo ni maisha yangu na sheria zangu binafsi." Maneno yake yaka sababisha mshangao wa hiari kutoka kwa Musa.

"Kumbe sheria tu!! Mi nilidhani labda una sababu ile yamsingi au labda ushachanjiwa dawa kumbe sheria tu. Twende bana.. Sheria zinatenguliwaga tu. Siunajua sheria si, Msahafu eti hazitotenguliwa. Fanya hivyo." Akamaliza maneno yake na kumshika mkono Neema. Neema hakutaka kuelewa somo hata kidogo. Akaendelea kugoma mpaka Musa akaishiwa maneno ya kuongea..

"Sawa.. Umeshinda. Hebu tuachane na hayo. Vipi, ulilikiria kwa mara ya pili ombi langu?" Aliuliza huku nafsi yake ikivuka ujasiri na kuanza kuleta uoga.

"Hivi, Musa.. Ina maana tuseme wewe huwa kichwa ngumu eti! Yaani mimi niache kufanya mambo yangu nianze kukufikilia wewe sindio?" Neema alibadilika na kuongea sauti ya juu. Tena ile ya kuogofya, sauti ile ikazidisha uoga kwa Musa na kuhisi huenda akizidisha king'ang'anizi hata uo urafiki utakufa akose yote.

"Basi... Yaishe, lakini sio vizuri hivyo."

"Kumbe, vizuri niaje Musa. Acha mie niende." Akaondoka. Musa ile furaha yake ya siku nzima ikaisha ghafla. Alipofika nyumbani kwake kitandani hapo akaanza kutalii ndani ya bahari lile la mawazo. Mawazo yalimshinda na kuamua angalau amtafute rafiki yake amshauri.

.... ...

"Afya.. Eee. E.e. Afya ni kitu bora. Ya kwanza mchicha ya pili mayai. Na maharage pia.." Ni sauti ya Baba Neema. Alikuwa akiimba moja kati ya nyimbo azipendazo pindi awapo kwenye akili ya pombe.

"We.. Neema? Wewe Mwanangu." Aliita huku akigonga mlango kwa hodi. Neema aliisikia sauti ya Baba yake kipenzi na kwenda kufungua mlango.

"Karibu baba."Alimkaribisha Baada ya kumsalimu na kumjulia hali.

"Ahsante sana mwamba, popote unatimba.. Eee nakutegemea wewe. Uje urithi hadi pombe sawa mwanangu." Neema alimuitikia Baba yake kwa kila alichosema kwakuwa anamjua baba yake pindi anukiapo pombe kinywani huwaje.

Mzee alimpigisha mwanae hadithi mbili tatu kishaakakaribishwa chakula na mke wake. Alienda na kula chakula kile. Waliagana na kila mmoja akaenda kulala.

Upande wa Musa. Yeye alikuwa kwa rafiki yake akipata ushauri.

"Unajua wewe Musa. Uache ushamba wako. Elimika, oohooo. We jifanye domo zege. Labda ni kwambie kitu. Mwanamke kama nilivyokwisha kwambia, huwa anatabia ya kujifanya anamaamuzi ya mdomo. Wewe kama mwanamume unachotakiwa sio kushughulika na utatuzi wa maamuzi yake ya mdomo bali shughulika na moyo wake tu." Aliongea Side na kumfanya Musa aendelee kujenga maswali mengi kichwani.

"Sawa nimekusikia mzee wa mipango. Samahani natakaniulize ila usinicheke.. Umesema kuwa mwanamke akiongea mimi nisijali maneno ya mdomo wake bali niongee na Moyo wake." akaitikia Side kumaanisha kuwa alitamka jambo lile. Kisha Musa akaendelea, "Sasa ndugu yangu.. Hebu nielekeze jinsi ya kuongea na Moyo wa mwanamke. Maana labda hilo ndilo kosa langu kubwa." Aliomba msaada wa elimu kwa rafiki yake.
 
RIWAYA: KICHAA.

Na: ZUBER R. MAVUGO.

N0. 17.

ENDELEA.

"Usijali, wewe ni rafiki yangu kwahiyo mambo kama haya ni muhimu na unapaswa kuyatambua. Unajua binadamu ni kama gari na mwili wake nio ulitumika kama mfano wa gari. Kwakuwa gari huwa na gia boksi basi binadamu huwa na ubongo kama gia boksi. Basi kwenye gari kuna kitu cha muhimu sana kinaitwa injini, nadhani unafahamu umuhimu wa injini na kazi kubwa ya injini. Nako pia kwa binadamu kuna kiungo kinaitwa Moyo. Kiungo hicho hufanya kazi za muhimu sana ndani ya mwili. Sina muda wa kukuelezea kazi zote ila natumai ukirejea kwenye kitabu cha Sayansi darasani utazipata. Huo moyo ndio umebeba kitu cha muhimu sana kiitwacho hisia na hiyo ndio siri ya moyo kuona hata kama macho yako hayana nuru, kusikia hata kama masikio yako hayaruhusu kupenya kwa sauti. Moyo unauwezo wa kufanya kazi zote za milango yafahamu pasina kuihusisha na hiyo yote inatokana na uwepo wa hisia. Unajua kuwa moyo ukichafuka na kutoa hamu ya chakula, binadamu hawezi kula hata kama ana midomo mingi? Je, unajua kuwa hisia za moyo zikikupeleka sehemu fulani lazma uende hata kama pana ogopesha na kutisha? Je, unajua kuwa hisia zina uwezo wa kuagiza chozi na kulitoa kupitia macho? Je, unajua kuwa hisia ndio huufanya mwili wa binadamu usisimke na kuhisi jambo pindi uguswapo?. Basi tangu leo elewa hisia ndio sababu ya yote. Mdomo hupenda kuongopea yaliyomo moyoni kwasababu unajua kabisa hisia ni mbaya, hata macho hupenda kuongopea yaliyomo kwenye hisia. Sasa wewe kama mtafutaji unajikuta unakatishwa tamaa kwa kusikiliza maneno ya kinywa bila kutambua maneno ya Moyo. Kuna njia ya kuteka hisia. Njia hizo ni mbili tu. Yaani njia ya Maneno na njia ya matendo. Ninaposema maneno yaani nikuyatamka yali yasemwayo na moyo wako pasina uoga au uongezaji chumvi kwani lugha ya moyo huwa tamu sana. Huleta chozi, huleta tabasamu, huleta maumivu pia.. Usije ukadanganywa na mdomo. Siku zote mdomo huwa kinyume na moyo. Pindi akutukanapo wewe usidhani Moyo ndio umetukana. Moyo huwa unaheshma tu. Unachopaswa kufanya sio kubishana na mdomo wake bali moyo wake kupitia maneno au vitendo vyako, lengo ni kuteka hisia zake tu. Mtu yeyote hata kama mfalme au rais, ukimteka hisia tu. Unauwezo wa kumfanya akafanya chochote kwa ajili yako. Mi nakusihi fanya hayo." Alimaliza kutoa elimu kisha akaruhusu swali. Hapo Musa hakuwa na swali bali kushangaa na kutoamini elimu aliyoipata.

"Labda na swali la uzushi."

"Ha.ha.ha.ha. Uliza tu."

"Hivi... Yote hayo wewe uliyajulia wapi?"

"Mimi hayo yote nilijifunza kwa marehemu babu yangu. Alikuwa akinifunza mengi sana mpaka alipofariki."

"Haa! Hivi kumbe hata tuzee tunayajua mapenzi?"

"Babu alikuwa akiniambia kuwa vijana wa siku hizi hatujui mapenzi. Sasa wewe Musa.. Hebu fanya tuchonge kesho maana hapa nimechoka ile mbaya."

"poa mwana.."

Wakaagana kisha Musa akaondoka na kurudi kwao.

Upande wa Neema yeye alibaki akiulaumu mdomo wake kwa utoaji wa maneno ambayo hayapo hata Moyoni.

"Lakini.. Mimi niliongea vile sikwamba sikutaka kwenda kwa kina Musa. Bali nilikuwa nahtaji aendelee kunibembeleza kwa maneno matamu. Siwezi kukubali hata siku moja kuamrishwa na maneno yasiyo na ladha. Mie hadi nipate ladha hapo ndipo utaniona na nyanyuka na kumtumikia mtu fulani. Kwa hilo naomba Moyo unisamehe maana ni kazi yangu kuongea nikiwa kama mdomo." Hayo ni baadhi ya majibu yaliyojibiwa na mdomo wa Neema pindi alipokuwa akiulizwa na kulaumiwa na Moyo.

Ndugu msomaji, kumbe hata viungo vya mwili navyopia hukoseana, hulaumiana, na husameheana. Amini usiamini ndivyo ilivyo na ndio maana unaweza kujikuta unadhulika pasina kutarajia, kwa mfano; Mokono unaweza taka kushika moto, halafu ngozi ikakataa, au akili ikakataa kutokana na kuyajua madhara ya Moto, ila mkono ukawa mbishi na kushika Moto. Hapo madhara yanaweza kutokea na lawama zitapelekwa kwa Mkono. Kwahiyo kumbe tunapoteua viongozi wa nchi tusisahau na kuteua viongozi wa miili yetu ilikuhakikisha usalama.

Siku hiyo ilipita, siku iliyofuata ndio siku ambayo Musa alijiapisha kuwa lazma akaongee ya moyoni na siyo ya mdomoni pasina kujali mahali watakapo kuwa.

Huku Neema nae akiwaza jinsi ya kumzungusha Musa kwa maneno.

Siku hiyo Musa alichelewa shule, hivyo aliadhibiwa na walimu kisha akapewa adhabu ya kuchimba shimo dogo la kutupia taka kabla hazijachomwa.

Neema hakuwa na raha kumkosa Musa darasani, hakuwa na jinsi aliamua kutoka kinyonge na kuelekea chooni na hiyo ni baada ya kuomba ruhusa kwa mwalimu aliyekuwa akifundisha. Ukweli Neema hakuwa anaenda chooni kwa ajili ya haja. Bali kuwaza tu.

Akiwa nyuma ya madarasa na kukiendea choo. Pembezoni mwa miti mingi mingi alimuona kijana mmoja ambae kwa muda huo alikuwa amevua shati na kubakiza flana. Kijana yule alikuwa bize na uchimbaji. Neema aliumaliza muda wake kumuangalia kijana yule mpaka hapo alipogundua kuwa kijana yule amevaa sura kama ya Musa usoni mwake. Aliamua kuahirisha safari ya chooni na kuelekea maeneo aliyokuwapo kijana yule.

Hakuna lugha ngumu kama ile iongelewayo na macho. Macho hupata tabu sana kuuaminisha moyo kuwa, chaguo sahihi ndilo ulitazamalo. Kwa lugha ya mdomo inayotegemea sana muktadha, yenyewe huongea tu hata kama yatokayo kinywani haya husiani na yaonekanayo machoni.

Naam, alipofika akamuona Musa akiwa bize na uchimbaji wa shimo lile la taka. Hakusita kumuita, walisalimiana kwa furaha huku wote kwa pamoja wakizisahau karaha walizokuwa nazo muda mfupi.

"Masikini.. Vipi, mbona umepewa adhabu ngumu hivi?" Aliuliza Neema kwa roho ya huruma.

Musa, huku akicheka kidogo utadhani haumizwi na kazi ile., "Kawaida tu Neema. Siunajua tena masuala ya uchelewaji. We usijali au sio?"

"Lazma, nijali. Hebu tazama walivyokuchosha, jasho linakumwagika tu. Ona.. Ona.. Pote hapa umechimba wewe tu. Hapana Musa huu ni uonevu." Aliongea Neema huku akipatwa na huzuni.

"Sasa unadhani utafanyanini? Hapa shuleni mwanafunzi asiye na cheo yeye huruhusiwa kuyaonja maumivu makali, endapo tu hana chenji. Lakini yule mwenye chochote mfukoni yeye huheshimiwa na ahongapo huachishwa kazi yake na kupewa mwingine. Kwahiyo tumeshazoea we usijali." Neema aliendelea kuumia zaidi. Hapo akaomba jembe na yeye kujichanganya iliangalau atumikie adhabu ile wakiwa pamoja.

Walifanya kazi ile pasina kujali wanafunzi wenzao waliyowapita wala walimu waliowatazama na kuwahoji maswali ya hapa na pale. Hatimae majira ya saa nane, walimaliza kabisa kazi ile na kupeleka taarifa.

Wakiwa njiani wakielekea kwenye moja kati ya miti mizuri ya shuleni pale. Mara Neema akapandiliwa na jani. Kwa uoga aliruka na kumvaa Musa iliampatie msaada. Kwakuwa Musa hakuwa na taarifa ya ujio wa mwili wa Neema. Hapo akapitiwa na kuanguka chini. Kwa bahati nzuri alianguka vizuri, huku Neema akiwa juu ya kifua chake. Wote kwa pamoja hawakuamini kama kweli wapo chini tena wamelaliana. Naam, ni chuchu ambazo zilikuwa ndio kwanza zinaanza kulitafuta jua la adhuhuri. Wanaziita chuchu saa sita, ndizo zilizomchoma vilivyo Musa na kumpelekea asiikumbuke ajali waliyoipata na kuanza kuzalisha wazo jingine. Aliwaza kuwa amemuoa Neema na hapo wapo kwenye fungate ya harusi yao. Musa alikuja kukurupushwa na kibao kilichotoka mkononi mwa Neema na ndipo alipokumbuka kuwa, kumbe alikuwa ameanza kumtomasa kwenye maeneo ya faragha pasina idhini.

Naam, wanasema kibao cha mpenzi hakiumizi.. Ndivyo ilivyokuwa kwa Musa ambae aligeuza shavu jingine na kuomba azidishiwe vibao.

"Samahani sana Neema kwakukushika bila ridhaa yako. Labda nakuomba usitoe hukumu yako mbele ya mwili wangu, kumbuka sikufanya hivyo kwa kupenda bali nilikuwa mawazoni. Nakuomba usinichukie tafadhali. Rudi basi." Alibaki akiongea peke yake huku Neema akikimbia na kwenda hadi maeneo ya vyoo vya kike huku akilia. Neema hakuhtaji kusikia chochote kutoka kwa Musa alichojua ni kuondoka eneo lile.

"Mimi ni mjinga sana. Hivi nilishindwa kujizuia hadi nikaanza kumshika Neema? Ona sasa, nimeshindwa kuvuta subira sasa nimevuta majanga. Sidhani kama Neema atanisamehe Side. Yaani alitoka amechukia halafu kama hajielewi hivi? Mi sikufichi hapa nimeshamkosa Neema wangu kwa ujinga." Alikuwa akijilaumu mbele ya rafiki yake Side ambae walitafutana muda wa saa tina, ule muda wa michezo. Musa hakukomea hapo... Aliendelea kujilaumu, zaidi na zaidi mbele ya rafiki yake huyo.

"Musa? Umefanya vizuri sana. Na hapo umeongea na moyo wa mtu kwa vitendo pasina wewe kujijua. Neema alikunasa kibao ilikutetea jinsi yake tu natumai ni baada ya kukumbuka maneno ya mama yake juu ya wanamume. Neema kama kweli angekuwa hakupendi, basi angekukabili palepale. Ila alionesha udhaifu wa uoga wa mapenzi tu, na jambo hilo hufanya wengi waliopenda bila kutamani kwa mara ya kwanza. Hawezi kukufikiria uwapo mbele yake na ndio maana akakuondokea iliakakufikirie zaidi. Hakuna mtu anaechukia kukumbatiwa, wala hakuna anaechukiwa kuambiwa anapendwa. Nina uhakika asilimia zote Neema ameangukia kwenye mapenzi. Na aliyemuangukia ni wewe tu." kupitia maneno yenye ukweli wa utatuzi kutoka kwa Side, yaliweza kumfumbua Musa na kuirejesha theluthi ya furaha yake ambayo ilikuwa imepotea. Hapo Musa akakili wazi kuwa anajivunia kupata rafiki kama Side.

... ....

"Unajua huyu kichaa Mavugo. Yupo tofauti sana na wenzake. Sawa yeye hajielewi lakini hufikia muda akili zake hurudi kwa dakika kadhaa tena hutoweka, tumejaribu kila njia ya kurejesha kumbukumbu. Kwani tatizolimsumbualo ni kutojielewa. Lakini tumeishia kufeli tu. Kama shoti tumeshampiga sana ila nikama tunamuumiza tu na hakuna kumbukumbu yoyote inayomrejea. Ila ni kichaa mzuri, anatambua hatari na kuzikwepa, hapa labda tufanye uchunguzi zaidi juu yake."

"Ni kweli kabisa dokta Endrew.. Lakini pia Mavugo anaonekana kuwa na mengi sana kichwani mwake. Ukichaa wake si..wa bure. Nahisi ni msomi. Ngoja tufanye uchunguzi kwanza. Enhee, hivi unamuonaje huyu mgonjwa aliyeletwa leo. Anavituko sana."

"Ha.ha.ha. Kumbe huyo anaelilia kunyonya?"

"hapana si,huyo."

"Kama si, huyo. Kumbe ni yupi docta izack." Alihoji docta Endrew huku akichezea kalamu yake kwenye meza.
 
RIWAYA: KICHAA.

Na: ZUBER R. MAVUGO.

N0. 18.

ENDELEA.

"Unajua huyu kichaa Mavugo. Yupo tofauti sana na wenzake. Sawa yeye hajielewi lakini hufikia muda akili zake hurudi kwa dakika kadhaa tena hutoweka, tumejaribu kila njia ya kurejesha kumbukumbu. Kwani tatizolimsumbualo ni kutojielewa. Lakini tumeishia kufeli tu. Kama shoti tumeshampiga sana ila nikama tunamuumiza tu na hakuna kumbukumbu yoyote inayomrejea. Ila ni kichaa mzuri, anatambua hatari na kuzikwepa, hapa labda tufanye uchunguzi zaidi juu yake."

"Ni kweli kabisa dokta Endrew.. Lakini pia Mavugo anaonekana kuwa na mengi sana kichwani mwake. Ukichaa wake si..wa bure. Nahisi ni msomi. Ngoja tufanye uchunguzi kwanza. Enhee, hivi unamuonaje huyu mgonjwa aliyeletwa leo. Anavituko sana."

"Ha.ha.ha. Kumbe huyo anaelilia kunyonya?"

"hapana si,huyo."

"Kama si, huyo. Kumbe ni yupi docta izack." Alihoji docta Endrew huku akichezea kalamu yake kwenye meza.

"Ni yule aliyekuwa analilia apelekwe studio akatoe albamu." Aliongea dokta Izak huku akijibadili mkao wake kwenye kiti.

Docta Endrew alikumbuka kishaakajikuta akicheka kila alipokumbuka vituko vya kichaa yule mpya. "Sasa... Docta, achamie nikuache kidogo. Weendelea na kazi." Aliongea docta Endrew kisha akajitoa kitini.

"wapi sasa?" Aliuliza docta Izack huku akipekuapekua makaratasi kadhaa mezani pale.

"Naenda kumchoma sindano ya usingizi yule kichaa anaekula nyama yake mwenyewe. Nahisi atakuwa ameshaamka, ngoja nimuwahi asije kujibebena mwili mzima."

"anhaa.. Upo sahihi. Wewe nenda kamshughulikie." Akatoka docta Endrew kishaakaelekea kwenye chumba ambacho wamemuhifadhi kichaa yule ambae yeye maisha yake kila leo hujiadhibu tu. Alipofika alimkuta bado amelala akamkadiria muda kishaakatoka. Docta Endrew aliona bora ajipitishe angalau kwenye uwanja waliyopo vichaa.

Kuna kichaa mmoja yeye ni wamakamu lakini muda wote amuonapo mtu hupenda kupiga goti na kusalimia. Kichaa huyo ni msumbufu lakini si mkorofi. Kwakuwa docta endrew anawafahamu vichaa wale jambo hilo halikuwa tabu alimuitikia na kuendelea na safari yake.

Kufika sehemu akakuta vichaa kadhaa wamesimama na kutulia kimya. Huku mmoja wao akiwa mbele na vile vitabu vya watoto ambavyo huchorwa midoli, "Hili andiko linasema, mama mwenye nyumba hulipwa deni lake kila adaipo. Vilevile tukifungua hukumu za kisasa aya ya kwanza msitari wa pili hadi watatu unasema; Tuwaheshimu wazee wetu kwa kuwa shika videvu vyao na tuwatii kwakusikiliza hadithi zao japo ni zauongo." Ni kichaa mmoja aliyekuwa bize huku akiwahubiria wenzake mambo ambayo ni kama waliyaelewa wenyewe tu. Hapo docta Endrew akacheka sana baada ya kutazama umakini wa vichaa wale wengine waliyo kaa kama wasikilizaji, akawakejeli kimoyomoyo huku akisogea mahali walipo.

"Mwalimu... Umesema kuwa, wototo wadogo wanapaswa wapelekwe shule wakiwa migongoni mwa mama zao. Je, watu wazima wapelekwe shule wakiwa wapi?" Ni swali kutoka kwa mmoja kati ya vichaa wasikilizaji. Kichaa yule aliyeongoza mahubiri akanuna kidogo kishaakafungua kitabu chake na kutoa majibu. Docta Endrew aliona kuendlea kukaa pale ni kama kupoteza muda, akajivuta na kuondoka taratibu. Akiwa njiani alifanikiwa kumtazama kichaa mmoja aliyekuwa bize kuandikaandika chini. Aliamua kumsogelea na hapo ndipo alipomkuta kichaa ambae kwake anamthamini na kumtofautisha na vichaa wengine. Kichaa huyo ana umri kati ya miaka arobaini na moja hadi arobaini na nne. Aliletwa hospitali hapo miaka kumi na tano iliyopita baada ya kubainika kuwa anaugonjwa wa akili hivyo gereza si haki yake. Naam, ndio yuleyule aliyefungwa kwa kesi ya mauaji ya watu watatu kwenye mazingira tofauti anaitwa, Mavugo. Docta alimsogelea na kwenda kukaa nae kwani anampenda sana.

.... ... ...

Neema alitumia muda wake mwingi kumuwazia Musa. Zaidi alikuwa akijipa picha ya kumbukumbu jinsi yeye na Musa walivyoanguka kwa pamoja. Alitamani angalau wangechukuliwa hadi picha iliawe analitazama pozi tamu alilokuwa ameliweka mwilini mwa Musa. Kila akikumbuka jinsi Musa alivyomkosea adabu anacheka kimoyomoyo baada ya kubaini kuwa alimuadhibu kwa kofi. Hisia za utamu zilimjaa na kumpatia raha muda wote. Alijicheka na kujinunisha muda huohuo huku akizikebehi zile hasira zake za kinafki.

Side na rafiki yake Musa, wao walikuwa wameshakwenda kucheza mpira maana walikuwa wanamechi za mikondo.

Timu ya Musa ilikuwa ni tofauti na ile ya Side kwakuwa mikondo yao haikuwa sawa. Musa hucheza kama kiungo mchezeshaji ndani ya timu yake ya mkondo huku kwenye timu ya shule akiwa kama kiraka. Yaani yeye niwakupachika namba yeyote ile anacheza. Upande wa Side yeye ni namba tisa mzuri tu. Mechi hiyoilikuwa tamu sana si tu kwa waliyobahatika kuitazama bali hadi kwa wachezaji wenyewe. Hawa kucheza kwa kuzimiliki dakika tisini bali waliishia robo yake kutokana na kulia kwa kengele ya kutawanywa.

Wanafunzi wote waliposikia kengele hiyo ya kutawanywa waliichukuwa miguu yao huku wakiwa wamevuta vyema pumzi zao na kukimbia vilivyo hadi paredi kwa ajili ya kusikiliza matangazo.

Walipomaliza kutangaziwa, walitawanyishwa na kila mmoja kwenda kwao.

"Musa..! Musa..!" Ni sauti ya Neema aliyoita jina hilo huku mwenye jina akiambiwa na ubongo wake uliopata taarifa kutoka kwenye sikio kuwa ageuke. Akageuka kuja kuhamaki. Uso kwa uso na Neema. Hakuyaamini macho yake akayafumba na kuyafumbua lakini aliendlea kumuona Neema. Hapo akaanza kuvuta picha jinsi walivyozinguana muda mchache uliyopita, akaendelea kutokujiamini. Akahisi macho yana muongopea. Akaamua kutumia sauti yake kumuita huyo Neema iliaamini kupitia masikio.

"Neema.. Kumbe niwewe?" Aliita Musa na hapo ndipo alipoamini kwamba kumbe aliyemuwazia ndie. Alimfuata kwa kasi, akamshika mkono na kumtoa kwenye msongamano ule wa wanafunzi wenzao. Kisha wakajibakiza nyuma na kuanza kuongea. Neema aliomba msamaha kwa kosa la kumuadhibu Musa kwa kibao, kwakuwa Musa alitambua wazi kuwa ile ilikuwa ni haki ya Neema kufanya vile. Akajifanya kumsamehe wakati hata moyoni mwake hakuwa amekosewa. Hatimai hayo yakaisha wakaendelea kupiga soga za hapa na pale. Neema alipoishiwa maneno alileta umbea na kwapamoja wakashirikiana kuteta.

"Neema. Hebu tuachane na hayo. Hayatuhusu, siunajua tena." Aliongea Musa huku akimpiga Neema ngumi isiyoumiza begani.

"kumbe tupige stori zipi?" alihoji.

"Zozote," Alijibu, alipomuona Neema yupo kimya. Alijua huenda hajaridhika na jibu lake ikabidi aseme tena, "Hata za movie, au za nyumbani, za maisha, hata za mapenzi kama zipo." Neema alipopangiwa listi hiyo akajichekelesha kidogo. Hakukurupuka kwenye uteuzi japo alikuwa na moja ambayo alishaiteua.

"ok, minimeonelea tupige stori za nyumbani." Ni kinyume na matarajio ya Musa kwani yeye aliiweka mada ile kwenye listi kwa kudhani huenda haitotajwa.

Neema akaanza kumsimulia Musa vituko vya baba yake. Kiukweli vilikuwa vinafurahisha lakini Musa hakutoa walau tabasamu hata moja. Muda wote alijawa na hasira alikuwa amebadilika sura na kutengeneza uso wake wa kukasirikia lakini alijitahidi sana kuung'ang'aniza uwe na furaha ya lazma.

"Oy, Neema eee. Nimechoka na maneno maneno yako ambayo hayana kichwa wala miguu. Mimi nakupenda na wewe hilo unalijua, sasa swala lililopo ni wewe kuniambia jibu ulilofikiria na sio kuchengesha mada hapa." Ni matokeo ya Musa kushindwa uvumilivu ndipo alipojikuta akiropoka maneno yale ya hasira pasina kuyazuia. Palepale Neema nae akajikasirisha na hasira zisije, akauchukua mkono wake na kuingiza ndani ya begi lake la shule, alipoutoa ukatoka na kikaratasi kidogo alichokifunga na kamba.

"Shika.." Alisema huku akimpatia kikaratasi kile. Alipochukua, Neema akaongeza, "Nakuomba usifungue hadi mimi nitokomee" Musa akakubali japokuwa alikuwa na maswali mengi ambayo alijua majibu yake yatakuja muda mfupi.

Neema alitokomea na kumuacha Musa aliyekuwa akingoja kusoma kikaratasi kile. Alipoona Neema ametokomea, akaanza kufungua kamba ile kwa ajili ya kutazama kilichomo ndani. Alikuta kikaratasi kingine kidogo zaidi ya kile chajuu. Kikaratasi kile kilikuwa na neno moja tu. Musa alidhani huenda maneno yangekuwa mengi lakini alipoishika karatasi ilionesha neno moja. Akalisoma, kwanza hakuamini, ikabidi amshirikishe mtu mmoja aliyepita maeneo yale kwa uhakika zaidi kwani alidhani huenda kisomo chake kimemdanganya.

"Imeandikwa 'NAKUPENDA'" alisoma mtu yule.

Furaha isiyokifani ilimpata Musa aliamua akimbie hadi kwao iliakaipatie haki furaha yake.
.... ... ....

"Bwana Mavugo.. Shikamoo...." Alisalimu Docta Endrew baada ya kumfikia kichaa yule aliyekuwa bize na kuandika andika.

"Hivi, wewe Endrew? Nani kakwambia anashida na kunyenyekewa. Hebu nitolee salamu za dhalimu mkubwa mbele ya masikio yangu." Hapo Endrew akatabasamu kiaina kwa kujua lazma ajifunze kitu kupitia kwa kichaa yule aliyejawa na mengi. Akajiulizisha iliapate kujua jambo.

"Waliotutawala pasina ridhaa yetu karne kadhaa zilizopita. Ndio waliyoleta salamu hii ya utumwa. Walifanya hivyo nia na madhumuni ni kutufanya tuwanyenyekee wao utadhani ndio waliyoiumba dunia. Salamu hiyo haikutolewa kama udhaniavyo wewe bali wenzetu walipga magoti na kunyenyekea kisha wakaitoa." Endrew akabisha kishaakasema. "Kama ni kweli, hebu niambie salamu sahihi ni ipi?"

"Safi sana Endrew.. Najua umetumia miaka yako mingi masomoni iliangalau uweze kupunguza ujinga. Lakini nasikitika umeambulia kuishi na vichaa tu. Labda nikuulize jambo. Hivi.. Unaweza kuniambia neno, Shikamoo linatafsiriwa vipi katika lugha yeyote ile ya kigeni au hata ya kibantu," docta Endrew akaishia kukuna kichwa lakini asipate maana. "Sio unakunakuna kichwa tu. Sema usaidiwe." alisema Kichaa Mavugo. Kwa aibu docta endrew akakubali kuomba msaada kwa kichaa. Hapo Mavugo akajikuna kidogo kidevuni kwa mbwembwe kisha akasema..

"Unajua sisi binadamu matendo yetu yanategemea majira, hivyo hata salamu zetu hutoka kwa kufuata mfumo huo wa muda. Hebu funguka kifikra wewe, waingereza husalimiana kwa majira, waarabu, hata wa bantu, si hivyo tu, dunia nzima inategemea majira. Lengo la salamu ni kutakiana amani baada ya kujuliana hali nasi kunyenyekeana kana kwamba kuna muumba kati yetu. Mimi kwakuwa nafuata majira, asubuhi nitakujulia hali, mchana na hata usiku. Rudi shule Endrew, ukajifunze salamu na sio kukurupuka tu."

Endrew huku akicheka akasema "Unajua Mavugo wewe huwa nakushangaa sana. Sijui mwenzangu unayatolea wapi yote haya. Hapo kidogo umeniacha, naomba kuuliza. Hivi hili neno salamu kwanza linamaana gani? Manake mie sijui, huwa nawambia tu watoto wanisalimie tu lakini kiukweli wakinihoji maana yake sijui. Nisaidie bwana Mavugo." Alitega sikio tena ilikusikiliza majibu kutoka kwa Mavugo.
 
RIWAYA: KICHAA.

Na: ZUBER R. MAVUGO.

N0. 19.

ENDELEA.

"Unajua sisi binadamu matendo yetu yanategemea majira, hivyo hata salamu zetu hutoka kwa kufuata mfumo huo wa muda. Hebu funguka kifikra wewe, waingereza husalimiana kwa majira, waarabu, hata wa bantu, si hivyo tu, dunia nzima inategemea majira. Lengo la salamu ni kutakiana amani baada ya kujuliana hali nasi kunyenyekeana kana kwamba kuna muumba kati yetu. Mimi kwakuwa nafuata majira, asubuhi nitakujulia hali, mchana na hata usiku. Rudi shule Endrew, ukajifunze salamu na sio kukurupuka tu."

Endrew huku akicheka akasema "Unajua Mavugo wewe huwa nakushangaa sana. Sijui mwenzangu unayatolea wapi yote haya. Hapo kidogo umeniacha, naomba kuuliza. Hivi hili neno salamu kwanza linamaana gani? Manake mie sijui, huwa nawambia tu watoto wanisalimie tu lakini kiukweli wakinihoji maana yake sijui. Nisaidie bwana Mavugo." Alitega sikio tena ilikusikiliza majibu kutoka kwa Mavugo.

"Sikia docta Endrew, wajinga huachwa na ujinga wao. Ingetosha nikakuacha lakini kwakuwa wewe ni rafiki yangu, hebu achanikuambie jambo. Penda kuishi kwa kujifunza iliuwe mwanafunzi bora.

Ok, neno 'Salamu' chimbuko lake sio kiswahili bali nineno la kiarabu. Neno hili linatumiwa tu kwakiswahili kwasababu lilitoholewa kutoka lugha ya kiarabu hadi kiswahili. Lakini sikwamba walilitohowa neno hilo kwakukosa msamiati wake la, hasha! Msamiati wake upo. Nao ni 'Amani' hivyo Salamu kwa kiswahili ni Amani. Kumbe sasa huwa tunasalimiana kwalengo lakutakiana Amani na sio kunyenyekeana. Nadhani umenipata." Mavugo akaendelea kuandika.

"Mmmh! Hapo nimekupata. Wala sina swali. Labda tu nikuulize, hivi unaweza niambia labda kabla hujapatwa na hali hii ya ukichaa ulikuwa na kazi gani?"

"Mbona Endrew huwa hunielewi? Mimi sio kichaa. Ebo! Vichaa ni wale kule wanachezacheza kichizi. Tena usitake kunikera hapa."

"Sawa bwana Mavugo. Samahani sana, labda nimekosea kukuuliza tu. Lakini lengo langu halikuwa baya. Nauliza tu zamani ulikuwa na kazi gani?"

"Swala la kazi mie sijui hata kidogo. Kwanza hata mie mwenyewe sijielewi mbona nyie madocta wasumbufu ah! Kwanza naomba unipishe niladhani umeanza kupata akili kumbe bado hazimo."

Docta Endrew alipofukuzwa na Mavugo ndipo alipokumbuka ile kazi yake ya kwenda kumchoma sindano ya usingizi yule kichaa aliyekuwa akifanyakazi yakujitafuna mwenyewe. Akatoka kishaakaenda kumchoma baada ya kumkuta macho, alipomaliza akarudi kwa docta mwenzie kishaakamuhadithia yote kwa pamoja wakacheka, huku Mavugo yeye akiendelea kuandika mambo yasiyofahamika.

"Unajua nimejaribu kupitiapitia hapa habari za Mavugo inaonesha aliletwa hapa miaka kumi na tano iliyopita na..."

"Kumbe ni wakitambo humu!!" Alidakia docta Endrew hata kabla mwenzie hajamaliza.

"Lakini pia nimegundua, kumbe huyu Mavugo hata kama tukisema tumpige shoti vipi haitosaidia. Kumbe anatatizo kubwa sana, na hakuna njia yeyote ile ya kumrejesha kwenye hali yake ya kawaida ila atarejea endapo atamuona mtu aliyewahi kuishinae au kuwa rafiki yake kabla ya hayo matatizo hapo ndipo kumbukumbu zitamkaa sawa na akili yake itatulia. Si unajua huwa anauwezo wa kukumbuka kidogo na hata anapokumbuka anapata kazi sana kwani huumia kichwa tu wala asielewe kama akikumbukacho ndicho." docta Endrew huruma ikazidi kumjaa baada yakung'amua jambo juu ya hali ya Mavugo.
Atapona vipi na kurudi timamu wakati yupo hospitali? Atawaona vipi hao wataomkumbusha? Au nd'o ataishi hivyohivyo milele?. Hayo ni baadhi kati ya maswali aliyoendlea kujiuliza docta yule ambae ingawa anamiezi miwili na robo toka ahamishiwe Bugando hosipatal. Lakini alikuwa ametengeneza urafiki na kuvutiwa sana na mambo ya Kichaa Mavugo, zaidi aliamini kuwa huenda Mavugo aliwahi kuwa na cheo fulani katika nchi hii lakini alikuwa akilikebehi wazo lake baada ya kugundua kuwa mtu yeyote mwenye cheo asingeachanizwa namna ile.

Lazma nijue nini hatma ya Mavugo. Alijisemea huku akizungushwa na kiti cha ofisini mwake.

..... .... .....

"Utaniumiza mwanangu... Mama yako nimeshajiishia hapa." Aliongea Mama Musa baada ya Musa kumkwapua na kumbeba juujuu kwa furaha.

"Mama leo nina furaha sana?" Aliongea Musa huku akimtua Mama yake ambae sasa alianza kulalamika kwa kubebwa juujuu.

"Furaha gani tena Mwanangu? Halafu mbona michirizi ya jasho na nguo inauchafu wa udongo. Umepigana?"

"Hapana mama.. Sema leo tulikuwa na kijikazi shuleni ndio maana unaona hivi"

"sawa, nambie namimi nijue unachofurahia mwanangu manake leo upo tofauti sana."

Musa akaona aibu,

"Hapana mama.. Nafurahia tu kumuelewa mwalimu."

"haa! Hicho ndicho kimekufanya uje kunisumbua hivyo. Mmmh! Haya bhana, jitahidi mwanangu siunajua mimi nakutegemea wewe."

"Natambua hilo mama."

Musa akatoka kishaakakimbilia chumbani mwake, alipofika akajitupia kitandani hivyohivyo na nguo zake za shule. Akakitoa kile kikaratasi na taratibu akaanza kukipitia utadhani anajisomea.

Musa akiwa kitandani pale huku akiendelea kutabasamu, mawazo yalimvaa na kumrudisha nyuma akaanza kukumbuka kipindi anamuhangaikia Neema, mpaka anafikia hadi kuadhibiwa kisa yeye, baada ya kumbukumbu hiyo iliyoambatana na machozi ya furaha. Alibadili nguo na palepale alijiinua moja kwa moja hadi kwa rafiki yake Side.

"Aiseeee!! Side umenisaidia sana." Aliongea kabla hata ya salamu. Kwa muda huo rafiki yake alikuwa bize na kuchota maji. Lakini alipomuona Side, akaamua kuahirisha kazi yake nakusikiliza ujio wa rafiki yake.

"Unamaanisha nini kusema hivyo. Halafu kwanza tuheshimiane sawa?" Aliongea Side huku akisontesha kidole chake kwenye paji la uso wa Musa.

"Kwani hatuheshmiani? Au umeanza talalila zako hapa." Alijibu Musa huku uso wake ukionesha furaha na kuendelea tanguliza utani mbele.

"Mi najua kuwa sina hadhi ya mbwa. Mbona unakuja na kufurahi bila salamu. Hivi unajua umuhimu wa salamu wewe? Huijui hali yangu? Unakuja tu namifuraha yako hapa hujui tupoje. Pengine labda tupo kwenye huzuni. Sasa we unadhani utajuaje. Waafrika tumefunzwa kutoa salamu. Allaaaa! Sio kufika nakuelezeana tu raha wala karaha zetu. Kwani utajua vipi kama mie sinafuraha bila kunijulia hali. Acha pigo zako kijana." Alilalamika Side huku akikemea vilivyo tabia ya rafiki yake.

"Ok, ni kweli... Nisamehe mkali, vipi, mambo yanasemaje?"

"dah! Mdogomdogo tu. Sijui huko kwenu."

"Huku sisi tunamshukuru Mungu tu."

"ndio, hicho ndicho chamsingi. Siunajua hata hapa akapenda anazichukua pumzi zake alizotuazima. Lakini ameziacha tu. Hivyo, hatuna budi kumshukuru. Yeye ndie kila kitu. Enhee! Leta stori"

"Mwana... Basi si tumetawanishwa skuli. Nikiwa naenda hom, mara nikasikia naitwa. Nikajiuliza, nani tena anaeniita. Kugeuka nikakutana na malaika..." Hapo Side akashangaa kidogo kusikia neno malaika.

"Ha! Sasa mbona unashangaa hivyo. Simaanishi malaika wa mbiguni. Mi namuongelea mtoto Neema. Yule ambae, akitoka Mama anaingia yeye. Hapo mtoto akanipa salamu, siunajua kuna kaugomvi kati yangu nayeye? Nikamwambia hayo yaishe, nae akasema kashapotezea, nikajisemea 'Yes, game over' namimi nikasema lazma nimtupie maswaga niliyopewa na Side. Mwanangu nikaanza kutupa maneno matamu hadi mwenyewe nayatamani. Nimemuimbisha wee hadi akatoa kikaratasi. Kuja kukisoma, mtoto amekubali. Nilipata shangwe, nikakimbia hadi home. Siunajua bimkubwa alivyo na kaunene ka aina? Sasa mie nilimbebelea juujuu. Huwezi amini kwafuraha tu. Hadi nilijikuta nataka kuropoka mbele ya bimkubwa. Ila nikavunga kiana" Aliongea Musa huku furaha ikiendelea kumjaa vilivyo mwilini na moyoni mwake.

"ok, hatua nzuri. Sasa hapa chamsingi ni wewe kumvizia nyumbani kwao. Siunajua tena huyo dogo bado kabisa. Sasa anaweza kufikiria mara yapili na sumu yako akaifyonza yote. Tena nenda muda huuhuu. Kaongeze max. Siunajua huu ndio mtihani wa somo la mapenzi. Nenda kaufanye poa." Kitendo bila kuchelewa, Musa aliamua kuondoka na kwenda moja kwa moja hadi kwa kina Neema, alipofika. Hakuna aliyemkuta zaidi ya Neema pekee. Siku hiyo waliongea mengi na wakafungua rasmi ukurasa wa penzi lao."

* ** *

Jijini dar-es-salaam. Maeneo ya masaki. Moja kati ya nyumba zilizojengeka vilivyo kwa uimara na uzuri. Muheshimiwa, Pita Mwambe, anaendelea kufurahia na mke wake pamoja na watoto wake wawili ambao mmoja kati yao ni wakiume kwa jina la John, huku wapili akiwa ni wakike kwa jina la Esta. Mheshimiwa Pita, yeye alikuwa na maisha ya furaha siku zote. Alikuwa na kitambi laini kilichodhihirisha shibe yake. Huku, nguo nyadhifu zikiendelea kuwafanya watu wasiomfahamu. Kumuita tajiri, au kumvika cheo chochote kiendanacho na mavazi yake. Akiwa anaendelea kupiga soga kwa kukejeliana huku wakichekeshana na familia yake. Mara ghafla, alipigiwa simu. Kwa manjonjo na jeuri ya pesa, aliichukuwa simu yake na kuisoma kwenye kioo. Aliitambua kisha akaiweka sikioni.

"Hello, Muheshimiwa!" Iliongea sauti ya upande wa pili wa simu yake.

"Enhee! Nakusikia?."

"Muheshimiwa.. Mimi ndio yule, mlezi wa watoto yatima kwenye kile kituo ulichotembelea jana. Nilikuwa tu. Nakukumbusha kuhusu ile ahadi yako, ya vyakula ulivyoahidi. Vipi? Maana bado hatujavipata."

"Kuhusu jambo hilo, usijali.. Nilikuwa nimesahau tu. Ila muda si,mrefu vitakuwa hapo. Ngoja niongee na vijana wangu ili wavilete." Akashukuru, kisha simu ikakatwa. Nikawaida yake kuwasaidia wananchi wake pasina kujali matabaka. Ingawa amefunikwa na shuka zito tena jeusi la utajili, lakini hiyo haikumfanya yeye asiwaone masikini. Kila leo alitoa msaada na nikipenzi cha watu sana. Hakuna anae mchukia.
Alimuita Sam, kijana mwenye mwili uliyotengemaa kwa kuzoea mazoezi magumu afanyayo kila siku. Alipomuita akamuagiza kupeleka chakula kwenye kituo cha kulelea watoto yatima. Alipomaliza kutoa maagizo hapohapo Sam akachukuwa vijana kadhaa na kupanda nao kwenye gari moja kwa moja hadi super market wakanunua mahtaji kisha wakayaweka garini na moja kwa moja wakaelekea kwenye kituo kile cha kulelea watoto yatima. Walipofika wakaonana na uongozi wa kituo kile kisha wakatoa msaada.
"Napenda kuchukua nafasi hii kutoa shukurani za dhati kwa niaba ya wahusika wa kituo hichi. Hatuna chakuwalipa bali maombi pekee ndio malipo yetu. Mwenyezi awabariki, azidishe kipato chenu na awaongezee umri mrefu ilimuendelee kutoa msaada kwa wenye shida. Hatuna ziada zaidi ya kuwaomba tu muendelee kuwa na moyo huohuo." Alitoa shukurani, Mlezi wa watoto wale ajulikanae kwa jina la Magrena. Ni mama wa makamu, mpole, mstaarabu, na mengineyo mengi yanayofanana na hayo.

Kushukuriwa kwa Kundi hilo la Muheshimiwa pita Mwambe, kwao ilikuwa ni kawaida. Hata sifa sasa walikuwa wameshazizoea hivyo walipomaliza kupewa shukurani, hawa kubweteka pale. Walirudi kwenye usafiri wao na kujirejesha moja kwa moja hadi maskani kwao. Walipofika walishuka huku wote kwa pamoja wakiwa wamevalia suti nyeusi, viatu, mpaka kofia. Walirejea katika sehemu zao na kuendelea kuweka ulinzi ndani ya nyumba hiyo kubwa na yenye kuvutia.

Sam, alirejesha taarifa kwa Muheshimiwa baada ya haponae pia alienda kufanya ulinzi.

Muheshimiwa Mwambe alikuwa akiendelea kufurahi na wanae huku akiwa sihi wasome kwa bidii. Hakika ni ukimuona utajua moja kwa moja kuwa ni mpenda maendeleo na mtu mwenyekupenda kusaidia wenzake.
 
RIWAYA: KICHAA.

Na: ZUBER R. MAVUGO.

N0. 20.

ENDELEA.

Sam, alirejesha taarifa kwa Muheshimiwa baada ya haponae pia alienda kufanya ulinzi.

Muheshimiwa Mwambe alikuwa akiendelea kufurahi na wanae huku akiwa sihi wasome kwa bidii. Hakika ni ukimuona utajua moja kwa moja kuwa ni mpenda maendeleo na mtu mwenyekupenda kusaidia wenzake.

..... .... ... ...

Kila kichaa hutembelewa na ndugu rafiki pamoja na jamaa kila ifikapo siku ya kutembelewa isipokuwa Mavugo ambae nikama hakuwa na ndugu wala jamaa, nae hakuwa hata na muda wa kuhtaji kutembelewa. Kila siku za kutembelewa, yeye huwa bize na mambo yake. Hata maafande waliokuwa wa kimtembelea zamani. Waliacha baada ya kubaini umakini wa ugonjwa aliyonao mfungwa wao. Kwa mujibu wa sheria, walimuacha huru kwani waliamini uwezekano wa yeye kupona ni mdogo sana.

"Mammaaa... Nipelekeni nyumbani.. Huku hakuna hata matope ya kuchezea. Kila siku sivui samaki japo nina tega kwenye bakuli langu. Mistaki kuchomwa sindano... Nirudisheni tuu" Ni kawaida ya vichaa kutoa visingizio vyao kwa ndugu zao ilimradi tu, waombe kutolewa pale na hiyo ilikuwa ni sauti ya kichaa mmoja aliyekuwa akijitetea mbele ya Mama yake.

Kichaa mwingine yeye kila ndugu zake walipomuongelesha, hakuwajibu zaidi ya kuwacheka tu, huku mwingine akileta fujo na kuharibu haribu zawadi kitendo kinachopelekea achomwe sindano za usingizi tu. Kuna wale vichaa ambao kazi yao kubwa ni kutoa mate midomoni mwao muda wote pasina kujali kuwa robo tatu ya mwili wa binadamu ni maji.

Ndugu msomaji, kama unampenda ndugu yako hebu tafuta tiba kwa hali na mali iliapone nasio kumpeleka kwenye hospitali ya vichaa. Hakika kule ni kumuongezea ukichaa tu. Nasio kumpatia tiba kuna kila aina ya vichaa na ukimpeleka nduguyo lazma uamini hilo hakika chozi halitosita kukutoka kama hauwezi kuvumilia mateso wayapatayo binadamu wenzako ambao wamerukwa na akili.

"Mavugo, mbona umejiinamia tu. Unawaza nini?" Aliongea docta Endrew huku akimshika kichwa Kichaa Mavugo.

"Najaribu kuwaza tu. Hivi, hii dunia kwanini kila inavyojizungusha ndivyo binadamu wanazidi kuchanganyikiwa. Hebu mtazame yule pale binadamu." Akasontesha mkono mbele ya Kichaa moja ambae yeye alikuwa anajiwasha makofi yanguvu muda wote huku akilia kutokana na maumivu aliyokuwa akiyapata, na pindi aliposhikwa mikono na nduguze waliyokuja kumuona. Alikuwa akikasirika na kujibadilishia adhabu. Kutoka kwenye kujiwasha makofi hadi kujibamiza kwenye meza. Hakika ni mateso makubwa aliyoendelea kujipa, si kwamba haumii. La. Bali anashindwa kujizuia na adhabu ile ya kujipa mwenyewe.

Docta Endrew, alipotazama adhabu ile aliyoendelea kujipa kichaa yule, aliumia sana na kuchukua sindano ya usingizi iliakamchome na kumuondoa kwenye mateso yale kwa muda. Lakini Mavugo alimzuia na kumwambia kuwa, "Huwezi kukuwa bila kutazama matatizo." Hapo docta Endrew akapinga.

"Lakini Mavugo, matatizo mengine hayavumiliki. Hebu ona anavyojiumiza. Dah! Mpaka nauhisi moyo wangu unaruka."

"Docta.... Kila kifanyikapo ndani ya hii dunia. Nifunzo tosha... Usimchome sindano angali bado anatamani kuongea na ndugu zake. Sindano yako haina uwezo wa kuunda akili bali inamdhoofisha tu. Jaribu kufikilia hata kama ni wewe ungekuwa ukikubali kuchomwa sindano nyingi kiasi kile kwa siku? Basi muache, huenda ni somo bora la kitisho kwa ndugu zake. Na hapo ndipo Mungu anaonesha ufahari mbele ya waja wake."

Docta Endrew huwa anamuheshimu kichaa Mavugo. Lakini si kila aongealo hulifuata. Hapo akatoka na kwenda kumchoma sindano za usingizi Kichaa yule aliyeendelea kujipa mateso.

Alipomchoma sindano akasinzia moja kwa moja wakambeba na kumpeleka wodini. Alipotoka huko akarejea moja kwa moja hadi alipomuacha Mavugo. Alimkuta, wakacheka kwa pamoja kutokana na vituko ndani ya maongezi yao. Docta Endrew alijitahidi kumpeleleza Mavugo juu ya anachokumbuka maishani mwake lakini ni wazi kuwa Mavugo nikama alikuwa hakumbuki chochote zaidi alikuwa akiishikilia ile picha aliyopiga yeye, mtoto mmoja, mwanamke pamoja na keki tu.

Kichaa mmoja aliwaita wenzake na kuwataka watoroke kwa siri kwani hawakupenda kukaa hospitali mule. Wenzake walimsikia na kufuata alichosema huku Mavugo yeye akiwapinga vilivyo walipogoma na kuhtaji waliloamua liwe ndipo akachukua chaki kishaaka chora mlango ubaoni,

"Anhaa! Anatufungia mlango eti? Basi tunaubomoa huohuo." Aliongea kiongozi wavichaa wale wenye mpango wa kutoroka. Wote kwa pamoja wakajipanga na akili zao zikawa zinawatuma waendelee kubomoa ule mlango. Ungewaona walivyohangaika, mara kusukuma ubao ule uliochorwa mlango, mara kuupiga vichwa kwakuzani kuwa huenda wakaufungua mlango ule. Walihangaika huku Mavugo akiwaacha na kujua kuwa tayari amewakomesha.

"Naona muda huu tumechoka. Hii inatokana na mlango kuwa mgumu sana kufunguka. Hivyo tunahitajika kwenda kupumzika na kesho mapema tuwahi na nguvu mpya kisha tuubomoe tena ilitutoroke. Tumechoka na manyanyaso." Alipomaliza kuongea mkubwa wao, wote walirudi na kujilaza.

Hayo ndio maisha aliyoishi Mavugo hospitali hapo.

Kila usiku ulipofika yeye alikuwa ni mtu wa kuingalia picha yake na kukumbuka tu ahadi za mwanae pindi alipokuwa akitoa ahadi ya uandishi wa habari. Hakuna kingine alichokumbuka, ingawa alikumbuka jambo hilo. Lakini nalo halikuweza kumsaidia kujitambua hata kidogo. Kila siku alilala kwa mateso makali ya kukumbuka jambo fulani maishani mwake.

"Hivi docta Izack, we unadhani huyu Mavugo itakuwa rahisi kumponyesha?" Aliongea docta Endrew.

"Kiukweli hapo sijui. Lakini kama vipimo vilivyosema, anahtajika kumuona mtu atakaemfanya akumbuke mambo yote na hapo ndipo akili zitakapomrejea. Lakini kinyume na hivyo. Hapo hakuna msaada wa aina yeyote. Kama unavyojua, kwa hapa hospital sivirahisi kumpata mtu ambae ni ndugu yake mwenye uwezo wa kurejesha kumbukumbu zote za Mavugo. Labda miningetoa wazo. Itafaa zaidi, endapo tukiiiba ile picha yake na kwenda kuitangaza kwenye media mbalimbali, huenda waliopo kwenye hiyo picha wakajitokeza na huo ndo ukawa msaada wakumsaidia yeye." Aliongea docta Izack.

Wazo la docta Izack, lilichambuliwa na kuonekana lipo sawa. Wakakubaliana kuhusu kuiba picha ya Mavugo, lakini pia wakapinga suala la kutangaza picha ile kwenye media kwakuhofia usalama wa Mavugo.

.... .... ....

Siku zilipita, miezi, hatimae miaka kadhaa. Neema na Musa penzi lao lilinoga sana, na kwa wakati huo Musa alikuwa akijihusisha na kazi za mtaani kutokana na kushindwa kuendelea na kidato cha tano. Si kwamba alifeli, hapana. Bali ni majukumu tu, yalimbana. Mama yake kwa wakati huo hakuwa mwenye kujiweza hivyo ilimbidi yeye ayachukue majukumu yote ya familia akiwa na umri wa miaka ishirini kwa kipindi hicho, suala la Musa kuishia njiani, halikumfanya Neema amchukie wala asimjali. Zaidi aliongeza upendo, ingawa alikuwa akisoma kwenye moja kati ya shule za bweni hapo Mwanza lakini hakuacha kumuwaza mpenzi wake hata kidogo. Kila ilipofika likizo alienda kumtembelea Mama yake na Musa, na kumsaidia kazi ndogo ndogo. Mama Neema alilijua penzi la Musa na mwanae lakini alilistahi na kumsihi mwanae kuwa awe makini sana. Mawaidha ya Ma. Neema, ndio ukombozi wake kwani aliyasikiliza na kuyapa nafasi ya kumuathiri moyoni mwake, jambo lililopelekea kujihadhari na kufanya mapenzi na Mavugo, ahadi wakaweka kwamba. Watafanya tendo baada ya kuwa mke na mume. Hakuna kati yao aliepinga Musa aliendelea kujishughulisha mtaani huku Neema shuleni ilimradi tu mwisho wa siku wajenge familia njema.

Hicho kidogo alichokipata mtaani, ndicho alichokula na mama yake nyumbani. Hali ya Mama Musa iliendelea kuwa mbaya kutokana na maisha magumu. Kwakuwa hakukuwa na pesa za kutosha kwa ajili ya kumpeleka hospitali iliatibu magonjwa yaliyoendelea kumtokea, aliamua kukaa nyumbani kana kwamba haumwi. Musa yeye ndio baba, pia ndio mama huku kazi anayoitegemea ni ya uoshaji magari wa kujitegemea. Yaani anasubiria gari lipack sehemu, akitoka mwenye gari, hapo Musa anajikimbiza na ndoo yake kwa haraka anachukua tambala na sabuni kisha anaosha, kazi hiyo ilikuwa na changamoto nyingi sana ikiwemo kufanyakazi bila malipo kwani hakukuwa na makubaliano baina ya muoshewa gari na muosha gari.

Huku nako kwa Neema, alikiheshimu kitabu. Kilipoanguka, alikiokota na kukibusu, kisha akachukuwa kisomo. Miguu yake alikuwa akiiweka ndani ya karai lake dogo lenye maji iliajisomee na kuuepuka usingizi. Darasani alifanya vizuri huku kwenye upande wa michezo akifanya vizuri pia.

Kiufupi Neema hakuujua usingizi kivile kwani ratiba yake ya masomo iliubana sana usingizi wake. Siku nzima aliimaliza darasani huku usiku wa siku hiyo akiumalizia kwenye kujisomea mwenyewe, ni zaidi ya adhabu aliyoamua kujipa huku akiamini kuwa lazma angekuja achana nayo.
Wanafunzi wengi wa kiume walivutiwa na sura yake huku wengine wakivutiwa na maungo yake ambayo yalitanuka vilivyo. Kila walipomfuata waliishia kujilaumu tu kwani Neema ni kama hakuwa na muda wa kuwa na mvulana. Yeye zake ni masomo tu.

"Hivi, Anna... We unadhani kweli, Neema atakuwa hana mshikaji kweli." Aliuliza mvulana mmoja kwa jina la brian. Kaka mkuu wa shule ile, pia ni mmoja kati ya wavulana ambao walishamfuata Neema lakini wasikubaliwe.

"Nikweli, Neema hana mvulana mbona huamini? Kwani vipi. Na wewe umetolewa nje?" Alijibu Anna ambae ni rafiki wa karibu wa Neema.

Brian huku akitoa misonyo ambayo haieleweki kama ni yakujilaumu au yakujidharau au yanini. Alijibu huku akikikuna kichwa chake kana kwamba kimejaa wadudu chungu. "Yaani Anna huwezi amini. Amenitolea nje pasina kuangalia skafu wala tai niloivaa. Minashangaa mpaka sasa, inamaana kuna mtanashati kama mimi kwenye shule hii anaemzuzua au ile amri ya kuwaruhusu wavulana wote wavaemashati ya mikono mirefu ndio imepelekea kila mtu awe kambale eti! Sasa we ngoja, siananichomolea mimi kilagia. Achanimuoneshe kwamba mimi ndio mwenye cheo kikubwa shuleni hapa. Yaani, naenda kuongea na kiongozi wa toi, nikitoka hapo naenda kwa stoo kipa, nikitokahapo naenda kwa dispilini prifekti. Huko kote naenda kumchafulia tu. Ilikila siku hapa shuleni aione chungu. Na kwa taarifa yako, lazma ajilete tena kwa kuomba msamaha. Allaaah! Mimi ndio brian mwingine toleo feki" Alipomaliza akanyanyuka darasani na kwenda kutekeleza yale aliyoongea mbele ya Anna.

Neema alianza kupatiwa adhabu sikubaada ya siku huku akiambiwa kama akitaka kusamehewa basi amkubali kaka mkuu. Maskini Neema kila siku anadeki vyoo, anapanga vifaa store, anapewa makosa yakinidhamu na kupata adhabu. Afanye nini wakati hana cheo shuleni, amlalamikie kiongozi gani matatizo yake ilhali kiongozi mkubwa ndie atoaye amri ya mateso apewayo. Aliona bora apewe adhabu kulikokufungua ukurasa mwingine wa mapenzi ambao hata hakuwa na shidanao.
 
RIWAYA: KICHAA.

Na: ZUBER R. MAVUGO.

N0. 21.

ENDELEA.

Brian huku akitoa misonyo ambayo haieleweki kama ni yakujilaumu au yakujidharau au yanini. Alijibu huku akikikuna kichwa chake kana kwamba kimejaa wadudu chungu. "Yaani Anna huwezi amini. Amenitolea nje pasina kuangalia skafu wala tai niloivaa. Minashangaa mpaka sasa, inamaana kuna mtanashati kama mimi kwenye shule hii anaemzuzua au ile amri ya kuwaruhusu wavulana wote wavaemashati ya mikono mirefu ndio imepelekea kila mtu awe kambale eti! Sasa we ngoja, siananichomolea mimi kilagia. Achanimuoneshe kwamba mimi ndio mwenye cheo kikubwa shuleni hapa. Yaani, naenda kuongea na kiongozi wa toi, nikitoka hapo naenda kwa stoo kipa, nikitokahapo naenda kwa dispilini prifekti. Huko kote naenda kumchafulia tu. Ilikila siku hapa shuleni aione chungu. Na kwa taarifa yako, lazma ajilete tena kwa kuomba msamaha. Allaaah! Mimi ndio brian mwingine toleo feki" Alipomaliza akanyanyuka darasani na kwenda kutekeleza yale aliyoongea mbele ya Anna.

Neema alianza kupatiwa adhabu sikubaada ya siku huku akiambiwa kama akitaka kusamehewa basi amkubali kaka mkuu. Maskini Neema kila siku anadeki vyoo, anapanga vifaa store, anapewa makosa yakinidhamu na kupata adhabu. Afanye nini wakati hana cheo shuleni, amlalamikie kiongozi gani matatizo yake ilhali kiongozi mkubwa ndie atoaye amri ya mateso apewayo. Aliona bora apewe adhabu kulikokufungua ukurasa mwingine wa mapenzi ambao hata hakuwa na shidanao.

Upande wa Musa, yeye aliendelea kuhangaika hivyohivyo kiume.

Siku zote hakupata, hata siku alizolala njaa yeye, hakuweza kukubali na mama yake alale njaa. Alijipiga na hata kukopa ilimradi tu, mama ale.

Hakuwahi kumjua, baba yake wala kufahamu chochote kuhusu baba yake. Yeye alichojua ni mama yake tu. Hakuwa na ndugu zaidi ya huyo. Alipouliza juu ya baba yake, mama aliishia kutoa chozi jambo lililomuumiza sana Musa. Alijiapiza kutomuuliza tena mama yake maswali ya kuita machozi ya mama yake.

Kila likizo, Musa na Neema walikutana na kujadili maisha yao matarajiwa.

.... ... .... ....

Docta Endrew na docta Izack, walishafanikisha kupora picha ya Mavugo japo iliwachukua sana muda kupora picha hiyo. Wakaaitoa kopi kisha kila mmoja akawa na ya kwake wote kwa pamoja wakaanza kutembea mtaani kwa ajili ya kuwatafuta wale walioonekana kwenye picha ile. Hakuna walichopata wala kuambulia zaidi ya kupigwa na jua kali. Walifanyakazi hiyo bila mafanikio ya aina yoyote. Walitafuta hadi wakasema kuwa wamechoka. Wakaamua kuirejesha tu. Picha ile kwa Mavugo ambae anaamini aliipoteza kwa muda mrefu.

.... ... .... ....

Pita Mwambe, aliendelea kushukuriwa na wananchi kila siku kutokana na misaada aliyowapatia. Hakuwa anachagua, alitoa kwa masikini, watoto yatima, watoto wanaoishi mazingira hatarishi, alitoa pembe jeo kwa wakulima mbalimbali, barabara zilitengenezwa jimboni kwake. Sasa kwanini wananchi wa mchukie? Alitoa saidia mamia na maelfu ya watu pasina kujali matabaka yao. Hakuna mbuge aliejaribu kugombea kwenye jimbo la pita Mwambe nae akapita. Ni wazi kuwa wananchi walikuwa wameshamkabidhi kura zao kutokana na jinsi alivyowajali. Vyombo vya habari vyote vilimsifia huku vikiendelea kukuza jina lake kwa kutaja misaada mbalimbali aliyoendelea kutoa. Licha ya moyo wake, vilevile kule bungeni, mawaziri walipata tabu sana kwani hakuwa mtu wa kutania katika ujengaji hoja na hakuogopa yeyote yule.

Baba Neema aliendelea kuchakalika kila siku kwa ajili ya familia yake. Alihakikisha kuwa, familia yake haikosi hata sumni.

Kama kawaida ya Baba Neema, yeye kila siku atokapo kazini huwa anatabia ya kwenda kupombeka kisha anarejea nyumbani majira ya usiku.

"Muhudumu... Mimi nimesema leta bia, wewe unanizuia. Hivi hela nizakwako auuu zaa kwangu. Nitamwambia bosi wako akufukuze kazi sasa hivi. We unajua mimi ni nani. Mimi ndio Devi. Allaaa, natumia pesa zangu nasio zako." Ni sauti ya kilevi iliyomtoka Baba Neema kwenye moja kati ya pub aliyoipenda sana. Sikwamba hakuwa akiudumiwa, bali nikawaida yake kuchangamka na kuleta utani pindi atoshekapo. Kama humjui unaweza kumuongeza bia, wengi wameshakula losi kwa kuyaamini maneno yake. Akiwa na rafiki yake ajulikanae kwa jina la Amos, walianza kujadili mambo yao ambayo kwao wanayathamini sana.

"Hivi, Amosii... Unajua kuwa Mwamba, anaetimba popote hata kwenye miamba. Sasa amerudi." Aliongea Baba Neema.

"Unamaanisha, Mwanao Neema au nini?" Aliongea Amosi.

"aaah! Amosi,.. Usitake niambia huto tuchupa twa bia ulitokunywa tena kwa hela yangu ndio tuna kupelekea wewe uniulize upuuzi. Inamaana ni kisema Mwamba hunielewi. Hadi ulete maswali yasiyo na kichwa wala miguu hapa." Aliongea Baba Neema huku akiendelea kunywa.

"Tatizo lako wewe ndio hilo, yaani ukininunulia pombe, mpaka uninyanyase.. Uninyanyase.. Weee.. Kwani mimi kuuliza nikosa?" Aliongea Amosi rafiki wa Baba Neema.

Waliendelea kupiga soga za hapa na pale. Lakini zaidi wakuwa wakiisifia pombe tu. Walipomaliza walinyanyuka na wakaagana kila mmoja akaenda kwake. Baba Neema akiwa njiani, aliendelea kusindikizwa na nyimbo mbalimbali ambazo huzitunga pindi alewapo. Hatimae alifika kwake, kama kawaida hupokelewa vizuri na kupewa mahtaji yote ikiwemo chakula, maji ya kuoga na kadhalika. Siku hiyo ni ndani ya masiku ambayo Neema alikuwa likizo, na kwakuwa kwa muda huo alikuwa ni kama ameshakuwa. Aliona achukuwe nafasi ile kuuliza swali linalomtatanisha miaka yote toka yupo mdogo.

"Baba.. Unampenda mama?" alijibu baba yake kuwa anampenda sana. Kisha Neema akageuza macho yake kwa mama yake. Nako akauliza hivyohivyo. Mama yake pia akajibu kuwa anampenda baba yake.

"Nashukuru kusikia mnapendana kiasi hicho. Lakini... Mie kuna suala moja ambalo linanitatiza. Hivi ni kwanini toka nipo mdogo, baba huwa analala chumba chake na mama huwa analala chumba chake. Wakati nyie ni mume na mke?" Aliuliza Neema swali lililomfanya baba yake ahisi kama pombe imekata kichwani na sasa anaulizwa swali ambalo hanauwezo wa kulijibu pasina kulewa. Mama yake nae, alijikuta akipaliwa na maji aliyokuwa akiyanywa. Wakaangaliana wawili wale kwa nukta kadhaa huku alama za mshangao zikijichora usoni mwao. Neema alishuhudia jambo lile, lakini kwakuwa hakuwepo pale kwa ajili ya kushangaa. Alitulia ilikusikiliza atakachoambiwa na wazazi wake. Baba alikosa jibu, kisabuni mama akajikaza.

"Haya ni mambo ya wakubwa. Hayakuhusu, tena usijikuze kiasi cha kudadisi vilivyo nje ya umri wako. Unanisikia wewe mtoto? Shika adabu yako. Nisisikie tena unahoji swali hilo." Alifoka Mama kisha akatoka hapohapo na kwenda hadi chumbani mwake, huku baba akifuatia nae pia alienda chumbani mwake na kwenye meza. Wakamuacha Neema pekee.

Neema aliwaza sana akiwa mezani pale peke yake. Mwisho wa siku alijiona huenda yeye ndie mwenye makosa. Aliamua kwenda chumbani kwa mama yake bila hodi. Ile anaingia tu. Akamkuta mama yake anameza vidonge ambavyo nikama anavifahamu. Alipochunguza kwa umakini aligundua kuwa ni vidonge vya kuongeza siku. Alikumbwa na bumbuwazi la ghafla, hakutegemea jambo lile mama nae alipohisi kama kuna mtu ameingia ndani mwake akataka kuvificha lakini alipoangalia mbele tayari alikuwa amechelewa kwani mwanae tayari alisha viona.

"Mama.. Unataka kunambia kuwa.. Kuwa... Huwa unaishi kwa kuongeza siku?" Aliuliza Neema.

.... .... .....

"Nimelikumbuka jalala. Nahtaji kwenda kukaa karibu yake, ninuse harufu nzuri itokayo jalalani. Huku nikiwaona watoto waliyoachwa na wazazi wao wanavyojituma kulisaka tonge jalalani huko. Nimekumbuka kuona vurugu za kugombania mabombonya na vyuma chakavu. Nahtaji kuwaona wanawake waliyofukuzwa makwao na kuwekwa wengine kisa walikosea kusuuza sahani. Wanawake majasiri wasioogopa ukali wa jua utuao utosini mwao.. Wanawake wanaoweza kuhimili kuishi na uchafu pasina kuugua, wanaoweza kula chakula ambacho kimelambwa na mbwa. Nimeukumbuka sana mtaa. Mtaa uliyona mafunzo tele juu ya maisha. Mtaa usio na huruma mbele ya watoto waliyozaliwa na wanawake. Nahtaji kurudi mtaani iliniendelee kujifunza somo zuri la maisha. Hakika mimi bado mwanafunzi. Vipi wewe Endrew ambae ndio kwanza hata robo tatu ya ujana haujaifikia ni vipi uniambie umeshasoma sana. Kama wewe ni msomi je, unaijua njaa... Ushawahi kumwagiwa maji ya moto na kuachiwa alama ya maisha? Je, ushawahi kuua kwa maneno?" Aliuliza Mavugo. Maswali yaliyozidi kumchanganya docta Endrew.

Alibaki akimtumbulia macho Mavugo. Hakujibu wala kuongea chochote kwa dakika zaidi ya mbili. Docta Endrew alibaki kujiuliza maswali mengi sana juu ya Mavugo.

Kama kweli ni kichaa.. Mbona anajua mengi? Ni yapi hayo yaliyomkuta au aliyoyashuhudia mtaani? Mbona faili lake linaeleza kinyume na maneno yake?. Hayo ni baadhi ya maswali yaliyojijenga kichwani mwa docta Endrew, alihisi kama maswali menyewe yanakiwasha kichwa ndipo akaanza kukikuna.

"Docta, vipi, mbona unakuna kichwa? Una mvi, chawa, kunguni, au sungusungu wamehamia kichwani?" Aliuliza Mavugo na kumpelekea Docta Endrew ajishtukie kisha akasema."Hapana Bwana Mavugo, najaribu tu kukuna akili. Siunajua tena.."

"Docta, unajua mie natatizo moja." Alidakia Mavugo.

"Tatizo? Lipi tena hilo Mavugo" Alihoji kwa mshangao docta Endrew.

"Tatizo langu ni kuwaona nyie na minguo yenu ya hospitali. Siipendi sana. Kingine ni juu ya hawa machizi ninaoishinao. Kutwa hawawazi maendeleo wenyewe wakilala na kuamka, akili zao zinafanya ya jana tu. Sasa kunisaidia, nilikuwa naomba angalau unitoroshe hapa. Au uwe unanipeleka mtaani kisha jioni na rudi kupumzika maana sioni ninachofanya tafadhali nisaidie kwa hilo." Mavugo alipoweka nukta ya maneno yake. Huku Docta Endrew tayari tumbo lilianza kumsumbua huku akitetemeka kwa uoga wa maneno ya Mavugo.

"We Mavugo wewe. Hivi kwa akili yako unadhani kuna ruhsa ya kumtoa kichaa akachanganyikane na raia? Aisee hapo mie siwezi. Japo wewe ni rafiki yangu." Alijibu Docta Endrew huku akimshika bega Mavugo.

"Docta... Nadhani hutambui maana ya urafiki wewe. Hivi unadhani kuongea nami pekee kunaweza fanya niamini kuwa wewe ni rafiki yangu? Labda nikwambie kitu. Unaweza kunitoa hapa kama ukitaka, na hauwezi kunitoa kama hutaki.

Kumbuka, kichaa huletwa hapa baada ya kukosa matunzo au tiba au labda usumbufu wake ulikuwa mkubwa huko uraiani. Nadhani unajua mie nipo hapa kwakuwa nimekosa matunzo tu. Sasa naomba unichukue na unitunze kama kweli wewe ni rafiki yangu wa damu. Kama kweli ulivyokuwa ukisema kuwa upo tayari kunisaidia ulisema ukweli basi nisaidie. Nahtaji nianze maisha mapya kupitia wema wako kwani hapa nilipo sina hata chembe yanijuacho kuhusu maisha yangu. Simjui baba, simjui mama. Sijui nimetoka wapi wala naelekea wapi nijuacho ni hapa nilipo labda na mambo niliyoyafanya baada ya kuharibika kwa kumbukumbu zangu za zamani. Tafadhali, nisaidie kunitoa hapa mie nitakubali kulelewa nawe. Sitokusumbua kama nifanyavyo kwa wengine kwakuwa wewe ni rafiki bora kwangu. Huu muda mfupi niliyokaa nawewe hapa hospitali umetosha kuniaminisha kuwa wewe ni kijana mwema na mtu anaependa kujifunza. Tafadhali ninahtaji kutoka humu nitoe." Ni maneno makali sana aliyoongea Mavugo. Kwanini chozi lisimtoke Docta Endrew? Hakika sikuchoka pekee bali moyo pia ulimuuma na kutengeneza huruma isiyo kifani. Alijifikiria juu ya tabia ya Mavugo, akafikiria juu ya maisha anayoishi na kujipajibu kuwa hayaendani hata kidogo na yeye. Akatupa jicho kiuwezo japo simkubwa lakini sihaba mpaka ashindwe kumsaidia bwana Mavugo. Aliendelea kuisumbua akili yake huku ukimya ukitawala si kwa Endrew pekee bali hata kwa Mavugo pia.
 
RIWAYA: KICHAA.

Na: ZUBER R. MAVUGO.

N0. 22.

ENDELEA.

Kumbuka, kichaa huletwa hapa baada ya kukosa matunzo au tiba au labda usumbufu wake ulikuwa mkubwa huko uraiani. Nadhani unajua mie nipo hapa kwakuwa nimekosa matunzo tu. Sasa naomba unichukue na unitunze kama kweli wewe ni rafiki yangu wa damu. Kama kweli ulivyokuwa ukisema kuwa upo tayari kunisaidia ulisema ukweli basi nisaidie. Nahtaji nianze maisha mapya kupitia wema wako kwani hapa nilipo sina hata chembe yanijuacho kuhusu maisha yangu. Simjui baba, simjui mama. Sijui nimetoka wapi wala naelekea wapi nijuacho ni hapa nilipo labda na mambo niliyoyafanya baada ya kuharibika kwa kumbukumbu zangu za zamani. Tafadhali, nisaidie kunitoa hapa mie nitakubali kulelewa nawe. Sitokusumbua kama nifanyavyo kwa wengine kwakuwa wewe ni rafiki bora kwangu. Huu muda mfupi niliyokaa nawewe hapa hospitali umetosha kuniaminisha kuwa wewe ni kijana mwema na mtu anaependa kujifunza. Tafadhali ninahtaji kutoka humu nitoe." Ni maneno makali sana aliyoongea Mavugo. Kwanini chozi lisimtoke Docta Endrew? Hakika sikuchoka pekee bali moyo pia ulimuuma na kutengeneza huruma isiyo kifani. Alijifikiria juu ya tabia ya Mavugo, akafikiria juu ya maisha anayoishi na kujipajibu kuwa hayaendani hata kidogo na yeye. Akatupa jicho kiuwezo japo simkubwa lakini sihaba mpaka ashindwe kumsaidia bwana Mavugo. Aliendelea kuisumbua akili yake huku ukimya ukitawala si kwa Endrew pekee bali hata kwa Mavugo pia.

"Lakini.. Japo kesi ilishakatwa ila naomba unipe ukweli ili hata kama nikikusaidia nijue jinsi ya kufanya. Sijui unaweza kuniruhusu nikuulize swali."

"Uliza tu Docta. Toa shaka." Alikubali Mavugo.

"Inasemekana miaka kumi na mitano iliyopita. Wewe ulifanya mauaji ya watu watatu na ukahukumiwa japo huku jitetea zaidi ulionesha kiburi lakini mwisho wasiku ndipo walipobaini kuwa wewe ni mgonjwa wa akili. Je, ni kweli wale watu uliwaua wewe. Tafadhali naomba jibu fasaha." Alihoji Docta Endrew na kutega sikio ilikupata mkanda mzima wa majibu.

..... ... ... ... ...

Mama Neema alikosa la kumjibu mwanae akabaki kimya tu huku uso wake ameuweka chini.

"Mamaa! Sinaongea nawewe... Inamaana hunisikii au?" Akauliza Neema kwa ghadhabu huku akiviendea vidonge vile ndipo alipohakikisha kuwa, Mama yake anatumia A.R.V. Neema alilia sana huku akimvutavuta mama yake kwa machungu.

Aliwaza mengi sana Neema. Lakini alijikuta akizimia ghafla baada ya kukumbuka kuwa alishawahi kufanya mapenzi na Musa.

Alizinduka baada ya kumwagiwa maji ya baridi, huku mbele ya macho yake akimuona Mama yake akimlilia. Akamuangalia kwa hasira sana na kuhisi kuwa huenda Mama yake anajiliza kinafki. Kilichokuwa kikimuumiza sana ni juu ya Mama yake kuutambua uhusiano kati ya yeye na Musa na mara kadhaa alishawapatia baraka lakini hakuwahi kumwambia hata siku moja kuwa yeye ni muathirika. Neema aliamini kuwa kama mama yake nimuathirika basi nae lazma atakuwa ameathirika. Na kwaharakaharaka alihisi kuwa ndio maana Baba yake hulala chumba tofauti na Mama yake.

"Niache.!!! Usinishike. Kama unanipenda mbona ulinificha mpaka nimegundua mwenyewe. Ona nimemuambukiza mtoto wa watu pasina kujua." Alilalamika sana Neema huku Mama yake akishindwa aanze vipi kumuelezea kwani hakutaka kumpa hata nafasi ya kujielezea.

Neema akiwa analia alirudisha kumbukumbu nyuma na kuikumbuka vyema ile siku ya kwanza toka wapate likizo shuleni kwao na akaukumbuka kwa umakini zaidi usiku wa siku hiyo. Ndio angekumbuka nyota za angani au chakula alichokula usikuhuo lakini hakukumbuka hayo bali alichokumbuka ni vile vishawishi vya mpenzi wake Musa pale alipoomba waitengue amri ya sita ndani ya chumba anacholalia Musa. Kumbukumbu za Neema zinamkumbusha kuwa alikataakatakata na kumsisitiza Musa kuhusu ile ahadi yao ya kutofanya mapenzi kabla ya ndoa. Lakini Musa alibembeleza vilivyo tena kwa sauti iliyosindikizwa na machozi na ndipo hapo Neema aliporuhusu nguo zake kumshuka chini na kuzitupa pembezoni mwa kitanda kisha wote kwa pamoja wakashirikiana kuvunja ahadi yao. Kumbukumbu zile ziliendelea kumtesa zaidi Neema na kumfanya asahau kama alikuwa amelishika shati la mama yake huku akimvuta kwa hasira. Alikuja kukurupushwa na kofi moja lililompeleka hadi chini.

"We mtoto huna adabu wewe... Hivi unataka mie mama yako nikubembeleze vipi iliunisikilize ninachoongea? Allaaah! Sikia ni kwambie mwanangu. Mimi sio mjinga kukuficha yote hayo bali ninamaana yangu. Nimengi yaliyonikuta mpaka leo hapa nilipo. Nakupenda sana mwanangu.. Nakupenda." Hapo Mama Neema akavuta pumzi huku kamasi na machozi yakiendelea kumtoka, akafumba macho kwa sekunde kisha akayafumbua na kuyatazamisha kwa mwanae aliyekuwa chini kwa muda huo. Sura ya Neema ilionesha chuki ya wazi dhidi ya mama yake. Lakini mama hilo hakulijali akamshika mkono mwanae na kumketisha kitandani kishaakaanza kumpa hadithi ya maisha yake kwanzia pale walipotengana na wazazi wao pindi meli ya Mv bukoba ilipozama. Mpaka walipolifakamia jiji la Mwanza. Yeye pamoja na mdogo wake. Pia hakusita kumuhadithia sababu ya kifo cha mdogo wake na kisa cha yeye kubakwa na Afande Kipara. Aliihadithia vizuri ile siku aliyoenda kutoa damu katika hospitali ya Bugando na ndiko alikokupata habari ya ugonjwa wa Ukimwi. Alihadithia kiundani zaidi na hakuna alichoficha. Mpaka jinsi alivyojifungua kwa taabu mwanae huyo Neema. Alipofika hapo akasitakidogo kishaakamwambia kuwa, yeye aliamini kuwa Neema atakuwa na V.v.u lakini vipimo vilipinga hilo. Ndipo kwa mara ya kwanza akayaona maajabu ya dunia kwani aliamini kuwa, kama mama akiwa na V.v.u basi na mtoto lazma awe navyo, alihadithia vizuri zaidi mpaka hapo alipomaliza.

Neema alijiona ni mkosaji sana kwani alimchukia mama yake bila kujua, alijikuta akifurahi huku akishangaa hapohapo, pia soni ilimjaa usoni huku akizilaumu fikra zake. Alishukuru sana kujua ukweli ambao ulijificha unaohusu maisha yake. Hapo akamfuta machozi mama yake na kumuhurumia sana pia alimsifu kwa ushupavu na kutamka wazi kuwa Mama yake ni shujaa wa kike. Mtoto na mama walifutana machozi na mpaka wote kwa pamoja walijikuta wakichukuliwa na usingizi huku wakiwa wamekumbatiana.

..... .... ......

Ulikuwa usiku wa kipekee zaidi kwa Musa, usiku ambao hakutamani apatwe na usingizi hata kidogo, japo haikuwa kawaida yake kukaa macho hadi mida ya saa tatu usiku kwani hutoka mihangaikoni akiwa amechoka sana hivyo hula, kuoga na kulala tu. Lakini siku hiyo alikuwa macho huku akifikiria sana. Hakuwa anafikiria, mbingu wala viatu bali alifikiria kiumakini zaidi ile kazi aliyoahidiwa siku ijayo kutoka kwa mfanyabiashara maarufu jijini hapo. Anakumbuka kuwa chanzo cha yeye kuahidiwa kazi ni juu ya wema mdogo aliyoufanya, wema wa kuokota picha iliyomdondoka mfanyabiashara yule na kurejeshea.

"mmmh! Yaani mtu kumuokotea picha yake tu. Tena picha iliyochakaa. Tayari anakuahidi kazi. Mmh! Hakika kila sifa anastahiki mwenyezi. Natamani kesho ifike iliaje kuongea na mama kwa ajili ya kunipatia kazi. Nitafurahi ile mbaya. Halafu watanikomaje? Ngoja tu, muda wa dharau unaelekea ukingoni. Sasa nadhani nitapajua hata dar-es-salaam live nasiokuishia kupaona kwenye tv tu." Alijisemea Musa huku akiendelea kupingana na usingizi uliyokuwa ukimnyemelea. Aliwaza lakini mwisho wa siku alipitiwa na usingizi tu.

.... .... .....

"Swali lako ni zur sana docta Endrew lakini hebu tazama saa yako. Usiku umeenda sana. Hata kama nikisema nikujibu, itachukuwa muda sana mpaka kukamilika kwa jibu. Istoshe umeshapitiliza hadi shifti. Ni usiku muda huu. We huoni hupaswi kuendelea kuwepo hapa. Hebu nakuomba nenda nyumbani kesho ukija nakuahidi jibu lako lakini unapaswa uwe makini sana maana nishakusihi kuwa mjinga huachwa na ujinga wake." Aliongea Mavugo na kumfanya docta Endrew agundue kuwa tayari muda ulishamuacha sana. Hakujutia kupoteza muda wake akiwa na Mavugo zaidi alijiona kuwa ni mwenye bahati kwani aliamini kila sentensi ya Mavugo kwake ni darasa tosha. Kwakuwa muda nikweli ulikuwa hauruhusu. Hapo docta Endrew akaondoka na kwenda kwake huku Mavugo nae akibaki hospitali hapo kama kawaida yake

Musa alikurupuka na kuiacha shuka baada ya kushindwa na miale ya jua la asubuhi iliyoingia ndani kupitia kwenye matundu yaliyokuwepo kwenye mabati ya chumba chake. Huwezi ukasema sababu ya Musa kuamka ni miale ya jua. La! Hasha. Mara ngapi Musa anachelewa kuamka ilhali jua lipo. Hapo hakuna kingine kilicho muamsha mapema namna ile zaidi ya furaha ya ahadi ya kazi. Alishukuru Mungu kuiona siku mpya, siku aliyoingoja kwa hamu na hata kuifanya ichelewe zaidi. Alienda kunawa pamoja na kupiga mswaki kisha akajirudisha tena ndani kwa akafungua kopo moja la mafuta ya kujipaka kopo dogo kabisa la bei ya chini ya kuanzia kuuza mafuta hayo kwenye duka lolote hapa nchini, akachovya kwani badala atoke na mafuta ya mgando kama yatokayo kwenye kopo la aina ile. Yeye akatoka na mafuta ya kula. Bila wasiwasi akapaka usoni huku akisahau kichwani na maeneo ya masikioni pamoja na shingoni. Akapaka mikono yote miwili huku akiishia mkabala na mabega kisha akamalizia miguuni. Naam, nisehemu ambazo huwa hazistiri kwa mavazi tu lakini sehemu kama kifua, tumbo na maeneo mengine ikiwemo yale ya faragha, menyewe hakuyapatia mafuta kisa huwa hayaonekani kwenye halaiki na hiyo ilikuwa namna moja ama nyingine ya kubana matumizi ya mafuta. Baada ya hapo aliyavua yale mavazi aliyolalanayo usiku wa siku hiyo na kuchukuwa mavazi nadhifu kabisa na kisha akayavaa.

"Mwanangu mbona umeupara hivyo utadhani Muendeshaji wa harusi? Au unaenda kwenye harusi?" Alihoji Mama Musa na hiyo ni baada ya kujuliana hali na mwanae. Musa kusikia hivyo akacheka kidogo huku akimalizia kufunga nyuzi ya vile viatu vyake ambavyo huwa anavivaa kwenye sherehe au ahadi maalumu. "Mama nawe kwa kejeli! Kwahiyo unashindwa tu kuniambia kuwa sijapendeza hadi unifananishe na wale ma mc wa kwenye harusi. Wale wasiojua kuwa mkanda huvaliwa kiunoni na situmboni, acha basi Mama." Akajidhalilisha kiutani mbele ya Mama yake.

Kama kawaida Mama yake akamsifia ilikurejesha hisia ya Mwanae nae ajihisi ni mtaalamu wa kuchagua nguo kama wafanyavyo vijana wenzake wa kileo.

"Haya wasalimie huko uendako." Aliaga Mama.

"Usijali. Badae Mama" Alipokeza Musa na moja kwa moja akaondoka. Hakuwa na baiskeli wala usafiri wowote wa haraka zaidi ya miguu yake. Mguu mosi, mguu pili kwa mwendo wa kuogopa vumbi na uchafu wa hiari, hukuakiiamini saa yake iliyosoma vyema mkononi. Aliiangalia kila baada ya dakika kadhaa. Alienda moja kwa moja hadi sehemu walipoahidiana wakutane na mfanyabiashara yule. Alipofika alisubiri kama Nusu saa tu. Baada ya hapo ilifika gari aliyoijua na kuifuata, haikumchukua muda kufikiria kuwa gari ile ndio ya yule mfanyabiashara bali ilimchukua muda kufikiria jinsi yakumuheshimu bwana yule kwa kumpa salamu ya kipekee. Kama kawaida alinyenyekea kwa dhati nae akaitikiwa. Waliongea kidogo maneno ya hapa na pale kisha Musa akaingia garini. Gari iliwashwa huku Musa akitoa maelekezo ya sehemu za kupitia na mwisho wa siku walifika nyumbani kwa kina Musa. Walipofika mfanyabiashara yule akasalimu na utambulisho mfupi ukafuata.

"Mama huyu ndo, yule niliyekwambia jana. Kuhusu ahadi yake ya kuja hapa kuniomba angalau nifanyenae kazi." Alimtambulisha mgeni kwa mama yake.
 
RIWAYA: KICHAA.

Na: ZUBER R. MAVUGO.

N0. 23.

ENDELEA.

"Usijali. Badae Mama" Alipokeza Musa na moja kwa moja akaondoka. Hakuwa na baiskeli wala usafiri wowote wa haraka zaidi ya miguu yake. Mguu mosi, mguu pili kwa mwendo wa kuogopa vumbi na uchafu wa hiari, hukuakiiamini saa yake iliyosoma vyema mkononi. Aliiangalia kila baada ya dakika kadhaa. Alienda moja kwa moja hadi sehemu walipoahidiana wakutane na mfanyabiashara yule. Alipofika alisubiri kama Nusu saa tu. Baada ya hapo ilifika gari aliyoijua na kuifuata, haikumchukua muda kufikiria kuwa gari ile ndio ya yule mfanyabiashara bali ilimchukua muda kufikiria jinsi yakumuheshimu bwana yule kwa kumpa salamu ya kipekee. Kama kawaida alinyenyekea kwa dhati nae akaitikiwa. Waliongea kidogo maneno ya hapa na pale kisha Musa akaingia garini. Gari iliwashwa huku Musa akitoa maelekezo ya sehemu za kupitia na mwisho wa siku walifika nyumbani kwa kina Musa. Walipofika mfanyabiashara yule akasalimu na utambulisho mfupi ukafuata.

"Mama huyu ndo, yule niliyekwambia jana. Kuhusu ahadi yake ya kuja hapa kuniomba angalau nifanyenae kazi." Alimtambulisha mgeni kwa mama yake.

"Anhaa... Nashukuru kukufahamu. Karibu sana hapa ndio kwa kina Musa na mimi ndio mama ya..." Alisita kidogo baada ya kugundua kuwa aliongea maneno yale kabla ya mgeni kuketi kitini. "Samahani baba.. Naomba keti kwenye kigoda ilituweze kuongea kwa utulivu. We Musa, hebu niletee hilo sandalusi langu la kukalia." Akatoka Musa na kuingia ndani, hakukawai akarejea huku ameshikiria alichoagizwa alipofika akatandika kisha Mama yake akaketi.

Maongezi mafupi ya utambuzi yaliisha ikiwa tayari walijuana hadi kabila, mpaka maeneo waliyozaliwa.

Mgeni yule alieleza kiundani zaidi juu ya shida yake ya kumuhitaji Musa kwa ajili ya kumfanya awe anasaidiana nae kazi kutokana na kupenda hulka yake pamoja na moyo mwema aliyokuwanao Musa. Hakusita pia kuelezea wema uliyomfanya yeye ampende Musa na pia akatoa mifano kadhaa ya vijana ambao ameshafanyanao kazi lakini wakamzunguka hiyo nikutokana na uaminifu ziro wa vijana wale istoshe walimtafuta wenyewe ila kishawishi kingine kilichompelekea amuhtaji Musa ni baada ya Musa kujitambulisha kwamba yeye si mtoto wa mtaani bali anakwao kabisa na hata elimu anayo tena ya kiwango kizuri tu.

Mama Musa kwakuwa anapenda maendeleo ya Mwanae. Hakuona kama kuna haja ya yeye kumzuia mwanae japo alijua kuwa ni lazma atengane nae kwani mwanae alihtajika kwenda kuuza duka kubwa la mfanyabiashara huyo lipatikanalo jijini Dar-es-salaam. Zaidi aliamini kuwa mafanikio ya Mwanae ni yake pia.

Musa alifurahi sana baada ya Mama yake kuridhia na aliahidi palepale kwamba anaenda kufanyakazi iliamsaidie Mama yake yule ambae maradhi yalimpata kila siku kutokana na virusi vya umasikini ambavyo viliruhusu kila aina ya magonjwa ya njaa.

Yule mfanyabiashara aliahidi kumuijia wiki kadhaa mbele kisha aliacha pesa ya kumfanya Mama Neema angalau apate kula na kubadili mwili wake. Kisha akaaga na kuondoka. Furaha iliyonakshiwa na machozi huku majonzi yakiipongeza kwa hiari. Hawakujua wanafurahi kwasababu ya kutengana au wanalia kwasababu ya kasi.

Neema alipopelekewa taarifa za uondokaji wa mpenzi wake, aliumia sana kwani hakuwahi kuwaza kutengana nae namna ile.

"Salio la uhai wangu umelibeba wewe... Jinsi utakavyolitunza ndivyo unavyoendelea kuokoa maisha yangu... Nipende kama unipendavyo na unilindie penzi langu... Ningekuwa nauwezo wa kutamka neno 'hapana' basi huu ungekuwa wasaa wake.. Lakini nitaanzaje kutamka ilhali ufuatacho ndicho cha muhimu. Kumbuka mimi ndio pekee kwako kisha ukumbuke kuwa huku pia umemuacha Mama halafu upige kazi kwa bidii... Nakupenda sana Musa lakini unapaswa kuniacha japo tumezoeana. Ila... Please and please hifadhi pendo langu na ulisome kama Msahafu kamwe usilibadili hata kidogo. Kama ukinicheat i swear to God takuua kwa mikono yangu dhaifu isiyoweza hata kushikiria kisu. Heshimu hisia zangu popote utakapokuwa." Aliongea Neema huku macho yake pamoja na maneno yakimtoka kwa hali ya kutisha zaidi.

"Nashukuru kwa kunikumbusha japo natambua nanijukumu langu kutambua.. Napenda kufanya rejea ya maneno ya wahenga pale waliposema kuwa 'Jasiri haachi asili'. Mpenzi mimi ni jasiri na wewe kwangu ni kama asili, basi siwezi kukuacha hata kama nitanyooshewa bunduki kinywani au kuwekewa panga shingoni. Nataka kukuona kwenye sofa nataka kumuona mwanangu akichezea toi huku pembeni televisheni ndogo kwa ajili yake ikiendelea kuonesha Muvi zakitoto. Nahitaji kulala kwenye magodolo ya wale wanaojiita matajiri na hitaji niifutilie mbali hii lugha mbaya isiyojulikana pamoja na huu msamiti wa umasikini kisha ni andike upya msamiati wa mafanikio tena kwa kalamu ya kijani anayomiliki rais tu. Nakupenda nakuheshimu nakujali pia. Sina usemi hata nikitafuta sitopata, najua unajitambua penzini. Sina shaka na pendo lako."

Waliendelea kutoleana maneno, mazito kwa mepesi. Yakuumiza na yakufurahisha lakini zaidi waliichukia dharau wapatiwayo kisa umasikini tu. Pia Musa hakusita kumuhimiza mpenzi wake kuwa anatakiwa kusoma kama hatosoma tena ilikufanikisha malengo yake.

Siku zilitimia hatimae Musa alichukuliwa na yule mfanyabiashara. Moja kwa moja hadi Dar-es-salaam. Ni kama robo ya ndoto zake ilitimia ile tu kuuona mji ule. Alifurahi sana. Walipokelewa vizuri kwenye nyumba ya heshma kwanzia getini.

"Jisikie upo nyumbani.. Hapa ni kwetu sote.. Naimani hutokuwa nauoga baada ya maneno hayo." Ni maneno ya mwisho mwisho aliyoyaongea Mfanyabiashara yule baada ya kumkaribisha Musa kwa maneno marefu kidogo. Musa alikaribia kwa heshima zote. Kwakuwa uchovu ulimtawala kwani hajawahi na wala simzoefu wa kusafiri safari ndefu. Aliomba aonyeshwe pahala pa kujipumzisha alichukuliwa na kupelekwa. Hakuwa na muda wakuongea bali wakulala tu. Hivyo alijiza na usingizi palepale ukamvaa.

..... .... ......

Docta Endrew aliendelea kusumbuliwa na maneno ya Kichaa Mavugo. Kubwa zaidi lililomfanya mpaka kujipigapiga kichwa ofisini mwake kwa mkono wake wenye kalamu yake ni juu ya ukweli alioupata kutoka kwa Mavugo.

Ina maana huyu Mavugo hakuua? Kumbe si Muuaji? Aaah! Miaka yote hiyo mahakama imemuweka ndani bila ushahidi.

"This is unfair." Akajiropokea ofisini mwake huku akipiga meza kwa nguvu wala asiyajali maumivu.

Hapo akasimama na mkono wake wa kulia akiushikisha mezani huku ule wa kushoto akiutumia kukizungusha kile kiti cha ofisini mwake. Akakereka zaidi akakiacha kiti na kuanza kukuna kichwa. Hapo napo akaona kama bado, akaanza kutembea tembea ndani ya ofisi yake Safiri isiyokuwa na mwisho.

Kama hakuua yeye, basi amesingiziwa na kama amesingiziwa basi kuna jambo limejificha hapa. Mmmh! Jambo lipi? Je, Mavugo analijua? Hapana hawezi kulitambua kutokana na kufutika kwa kumbukumbu kichwani mwake. Na vipi kuhusu kumchukua. Je, nimchukue???

Hayo ni mawazo yaliyokuwa yakiendelea kutalii kichwani mwa Docta Endrew.. Mawazo hayo tu ndio yaliyomtoa kitini na kumsimamisha mwisho wa siku kumzurulisha ofisini mule pasina kumsimamisha. Mara aende kulia mara kushoto, mara ashike kalamu mara aiweke mezani. Kumbe ni mawazo tu.

Siku hiyo Docta Endrew aliomba ruhusa mapema na kurejea nyumbani kwake. Alipofika hakuhitaji stori wala nini. Moja kwa moja alipitiliza hadi chumbani na kujipumzisha baada ya kumeza dawa za kichwa alizonazo palepale kwake.

Mke wa Docta Endrew ni mpenzi sana wa filamu hasa zile filamu ndefu zenye misimu. Hupenda kufanya hivyo kila siku amalizapo shughuli zote za pale nyumbani kwake. Haikuwa kawaida ya Mumewe kurejea mida kama ile tena huku akisahau kumjulia hali mke wake na kupitiliza hadi ndani.

Inamaana hajaniona? Audharau tu? Ata!! Huyu atakuwa natatizo. Ngoja nimfuate. Nimawazo aliyowaza mkewe.

Mke wa Docta Endrew aliingia chumbani na kumkuta mumewe amejipumzisha huku macho yake mawili akiwa ameyaangalizisha juu. Alisita kidogo baada ya kumuona mumewe ametawaliwa na huzuni. Taratibu akamsogelea na kumshika begani.

"Mume wangu... Kipi kimekusibu?" Alihoji mke wa Docta Endrew huku akiendelea kupitisha mkono wake kichwani mwa mmewe.

"Hakuna kitu mke wangu. Sema niuchovu tu." Alijibu Docta Endrew huku akijiinua kitandani na kujikalisha.

"Uchovu?? Aaah! Usinidanganye. Usiniaminishe kuwa uchovu pekee ndio umekupelekea kurudi nyumbani muda huu. Wala usiniambie eti. Hali uliyoingia nayo humu leo inauhusiano na uchovu. Mie staki ngonjera bali nahtaji kujua umepatwa nanini?" Maneno yalimtoka Mke wa Docta. Docta anajua mke wake akikazania jambo hupenda mpaka alijue ili ashiriki kwenye utatuzi. Kwakujua hilo ilibidi alete ubeberu ilikumuonyesha mkewake kuwa yeye ndie mwanamume.

"Halafu we mwanamke usiniletee usumbufu.. Tena kama umeshindwa kuangalia televisheni heli ukaoshe vyombo. Niache nilale.. Kwanza huna adabu, Mumeo anafika badala ya kumuacha apumzike we... Unamuamsha tu. Hivyo ndivyo kwenu wamekufunza eti? Nakuuliza wewe... Kwenu huwa mko hivyo? Sasa kaendelee kazi yako niliyokukuta unaifanya. Ebo!" Maneno yale yalitosha zaidi kumvunja moyo mke wa Endrew. Hapo hakuwa na usemi kwani hapendi kumuudhi mumewe. Alilitambua kosa na kunyanyuka kwa kujivuta kama asiyejiskia taratibu akaondoka na kurejea sebuleni.

Docta Endrew aliendelea kutembelewa na maswali yaliyomchekesha, mkejeli, na kumuhuzunisha. Alikaa na kufikiria siku hiyo nzima. Baada ya kufikiria kwa kina aliona ni kweli Mavugo si'wakukaa hospitalini pale bali angekuwa katika shirika fulani akifanya kazi zake. Siku hiyo iliisha huku tayari amepata jibu na siku iliyofuata akaanza taratibu za kumtoa mgonjwa yule wa akili.

Docta Endrew ingawa alikabiliwa na changamoto nyingi lakini mwisho wa siku alikubaliwa kumchukua na kumpeleka kwake. Mavugo alifurahi sana baada ya kutoka hospitali na kupelekwa kwa Docta Endrew. Alitoa shukurani kama wafanyavyo wengine.
..... ... .....

Likizo fupi ya Neema iliisha na yeye akarejea shule. Kama kawaida ya Neema yeye huwa bize na masomo huku akiamini lazma yatamtoa tu.

"Hivi we Neema? Mbona huelimiki japo we nimsomi. Sjui nini kinachokupelekea hivyo.. Au kwenu bushi nini... We mtu gani usiyekuwa na boyfriend. Kila siku unatusumbua sisi tunapoongea na watu wetu. Mara ooh! Ongeeni taratibu mie nisome. Acha hizo shtuka hapa mjini afu shule ndio sehemu ya kuwa huru. Hivi we unawezaje kukaa hivyo hivyo tu tena kwa muda mrefu. Mie siwezi duh!" Aliongea rafiki yake kwa jina la Mishi. Hiyo ni baada ya Mishi kuombwa na Neema apunguze sauti ya aliyekuwa akiongea nae kwenye simu.

"Labda mwambie nawewe shosti. Huenda akakuelewa maana. Mi kila siku lazma niseme. Lakini wallaaa hasikii. Anajifanya wakusoma sana." Aliongea Jesca ambae nae pia ni rafiki wa Neema pamoja na Mishi.

"Hivi, niwaulize swali?" Alihoji Neema baada ya kuwaangalia marafiki zake kwa jicho la ukali kidogo.

"Uliza shosti" Alijibu Jesca.

"Mmekosa kazi ya kufanya?" Aliuliza Neema na kuwapelekea rafiki zake walikutazamana kisha wakakosa majibu. Swali la Neema lilikuwa ni moja kati ya maswali ambayo kama ukiulizwa bila kutaraji basi lazma uchukie au uumie moyoni. Na ndivyo ilivyokuwa kwa washauri wale ambao waliamua tu kujilaza na kufikiria ya kwao huku ya Neema wakimuachia mwenyewe.
 
RIWAYA: KICHAA.

Na: ZUBER R. MAVUGO.

N0. 24.

ENDELEA.

"Labda mwambie nawewe shosti. Huenda akakuelewa maana. Mi kila siku lazma niseme. Lakini wallaaa hasikii. Anajifanya wakusoma sana." Aliongea Jesca ambae nae pia ni rafiki wa Neema pamoja na Mishi.

"Hivi, niwaulize swali?" Alihoji Neema baada ya kuwaangalia marafiki zake kwa jicho la ukali kidogo.

"Uliza shosti" Alijibu Jesca.

"Mmekosa kazi ya kufanya?" Aliuliza Neema na kuwapelekea rafiki zake walikutazamana kisha wakakosa majibu. Swali la Neema lilikuwa ni moja kati ya maswali ambayo kama ukiulizwa bila kutaraji basi lazma uchukie au uumie moyoni. Na ndivyo ilivyokuwa kwa washauri wale ambao waliamua tu kujilaza na kufikiria ya kwao huku ya Neema wakimuachia mwenyewe.
... ... .......

Ilikuwa ni siku moja kati ya masiku aliyopendelea kwenda sokoni Mama Neema. Siku hiyo alichukua kapu lake na kwenda kununua mahtaji ya nyumbani. Akiwa njiani kutoka sokoni alipita kona kadhaa na kutokea barabarani. Alinyoosha na kufika sehemu wanapokaa ombaomba kwakuwa ni mtu wa huruma. Alimfuata ombaomba mmoja aliyekuwa anaonesha dhahirikuwa anaugonjwa mkali sana. Ombaomba huyo alikuwa akikohoa kikohozi kigumu na kutema makohozi yaliyoambatana na chembechembe za damu. Huku mwili wake ukiwa umekonda maratatu ya wewe, macho yake yakiiacha ngozi iliyojikunja kunja kwa madonda yaliyokauka na kupona huku mengine ya kijitonesha. Nywele zake zilikuwa ni kama zimenyonyoka na kukosa rutba ya kuota kama zamani. Ndio, salawili yake ilioneshawazi kumshuka kama angesimama lakini natumai angesitahiwa na kamba ya katani aliyokuwa ameivaa kiunoni kama mkanda. Mama Neema alimtathmini mtu yule ambae kwaharaka hakujulikana kama ni mtoto alietaraji kuingia duniani au ni mzee wa miaka elfu moja na kuendelea. Mtu yule alinyenyekea zaidi mkono wa Neema uliyokuwa umeshikiria shilingi miatano na asimuangalie usoni kama wafanyavyo wengine. Haikuhitaji hadubini kuzigundua shida zilizomjaa mtu yule. Wala hakukuwa na haja ya kutumia darubini ilikutazama kubaini ugonjwa wa kisasa aliyokuwanao bwana yule. Naam, kuna waliyompita huku wakitema mate kwani alitoa harufu kutokana na kukosa matunzo, pia ombaomba wenzake walimtenga na kumuweka mbali kidogo na wao kwa kuwa kosesha wateja.

Macho ya Mama Neema yaliendelea kuuangalia mwili wa mtu yule kwa umakini zaidi huku akili ikiendelea kupekuwa kwenye mafaili yake kwa ajili ya kujaribu huenda anajulikana.

"Ki... Ki... Kiki... kibakuli?" Aliongea kwa mshangao huku akiruhusu kidole chake kisonte mwili wa mtu yule.

Mawimbi ya sauti ya Mama Neema yalipiga vilivyo kwenye ngoma ya masikio ya mtu yule ambae kama ukimuita ombaomba ndio utakuwa umetaja jina la kazi yake. Sikwamba hakuisikia sauti iliyoita. Aliisikia vizuri tu lakini hakupata muda wa kuifikiria zaidi kwani katika maisha yake hakuwa na kumbukumbu kama alishasikia sauti ya aina ile ikimshangaa.

Kwa udhaifu mkubwa akayachukuwa macho yake na kuyahamishia mwilini mwa Mama Neema.

Mtu yule hakuamini alichokiona. Alihisi huenda ni jinamizi imemuijia mchana mchana. Alijikebehi kwa mshangao lakini alijiona mpuuzi baada ya kugundua kuwa giza lilikuwa halijaingia. Kwakuwa hakuwa na imani na macho yake, aliyapikicha kisha akaangalia tena lakini aliishia kuiona sura ileile.

"Aishaaaa!!!!" Alishangaa sana ombaomba yule baada yakugundua kuwa kumbe macho yake yalimkutanisha na mwanamke anaemjua kwa jina la Aisha.

"Ndio mimi Kibakuli wangu. Vipi mbona upo kwenye hali hii?" Alihoji Mama Neema huku akiangusha kapu lake chini "Yuko wapi Dada Aneth. Umefikajefikaje hapa?" Mama Neema hakuna alichojibiwa zaidi ya kuishia kuyaona machozi ya mtu yule.

Kabla hajaongea, akakohoa kikohozi cha pumu, kisha akayameza makohozi yake kwa kujua kuwa endapo yakionekana basi na chembechembe za damu zingeonekana.

Mama Neema hakuhitaji kuhangaika kufikiri ilikutambua kuwa mtu yule hakuwa na makazi. Haraka alikodi tax na kumpeleka moja kwa moja hadi kwake. Alikaa nae mpaka muda aliporejea mume wake. Alimuelezea kiufupi na kuomba wampeleke hospitali.

Kwa ushirikiano wa Baba Neema na Mama Neema walimchukuwa mtu yule na kumpeleka hadi hospitali ya bugando. Alilazwa na matibabu yakaanza mara moja.

Docta Endrew ni mfanyakazi katika hospitali ile lakini yeye huusika na vichaa tu. Kipindi anatoka kazini alipamiana kwa bahati mbaya na Mama Neema kitendo kilichopelekea adondoshe mafaili kadhaa aliyokuwa ameyashikiria.

"Oooh! Samahani mdogo wangu." Aliongea Mama Neema baada ya kupamiana na Docta Endrew.

"Bila samahani dada. Kawaida wala usijali." Wote kwa pamoja wakaokota makaratasi machache pale chini kwakusaidiana.

"Ok, thanks.. Naitwa Endrew ni dacta na ninahusika na wagonjwa wa akili." Alishukuru Docta Endrew baada ya kukabidhiwa karatasi na Mama Neema. Kisha akajitambulisha.

"Nimefurahi kutambua jina lako. Mimi naitwa Aisha Mapuya au zaidi unaweza ukaniita Mama Neema."

"Oooh! Ok.. Bila shaka umeleta mgonjwa."

"Ndio wala hujakosea."

"Aaah! Ninani yako?"

"mhh! Kaka tu"

"Ok, kwasasa ninaharaka kidogo. Labda nikuachie business card yangu utanitafuta kwa msaada zaidi kuhusu mgonjwa."

"Kaka unadhani wenzio tumesoma? Sasa hizo sjui bibinesi dadi tunapesa ya kuzinunua basi. Ndio kwanza mgonjwa yupo hospitali kwani zinauzwa hapa hapa?"

Docta huku akitabasamu."hapana dada yangu. Business card sio dawa. Ok, basi tuachane na hayo. Una simu?" Mama Neema akatoa Simu kisha wakabadilishana namba na wakaachana.

Docta Endrew alienda mpaka kwake na kukutana na Mavugo ambae kwa muda huo alikuwa nje ya nyumba ile huku ametulia.

"Vipi mbona leo umechelewa kutoka?" Alihoji Mavugo baada ya kusalimiana na Docta Endrew.

"Kuna mdada nilipamiana nae kwa bahati mbaya kipindi nakuja sasa nadhani yeye ndie kanichelewesha. Lakini hakuna kilichoharibika kwani nimechelewa kama dakika tano pekee."

"Ok, pole kwa hilo. Lakini wakati mwingine unapaswa kuwa makini sana na muda iliusipoteze mambo yako ya muhimu. Kumbuka sekunde moja ikikupita nisawasawa na kupitwa na madili miliöni moja sasa vipi wewe upitwe na dakika tano zote halafu ulizike? Usikubali muda ukupite hata kwa dharula. Kumbuka laiti kama dunia ingekuwa haiyaheshimu masaa basi mambo yako yote yange goma. Hebu ona uaminifu wa dunia, kila siku inajizungusha katika muhimili wake kwa masaa 24 na kuzalisha usiku na mchana. Sasa kwanini wewe ukubali dharula ziingilie mipangilio yako? Usilaumu nchi jilaumu mwenyewe." Ni kawaida ya Mavugo kuchambua kila jambo liwe dogo au kubwa. Kwakuwa docta Endrew alikwisha mzoea, jambo hilo halikumsumbua sana. Alimuomba waingie ndani. Walikaribishwa kwa vizuri kama ilivyo kawaida ya mke wa Docta Endrew kumkaribisha mumewe pindi atokapo kazini.

Upande wa hospitali Docta aliwaita mama neema na baba neema.

"ok, inabidi tu mkubaliane na matokeo. Mgonjwa wenu ana Virusi vya ukimwi na inaonekana hakuwa akitumia hata A.R.V. Hivyo magonjwa mengi yamepata ruksa ya kumuingia kwa haraka zaidi na kumdhoofisha. Ina bidi abaki hapa hospital kwa muda wa wiki nzima ilituangalie hali yake itaendaje." Ni baadhi ya maneno aliyoongea Docta.

Walikubaliana na maneno yale kisha wakaaga na kwenda kwao.

Wakiwa njiani kuelekea kwao. Baba Neema alihoji maswali mengi sana ikiwa ni kuhitaji kumjua huyo waliyekuwa wakimsaidia.

"Baba Neema.. Subiri kwanza hali yamgonjwa iwe vizuri na hapo ndipo nitakapokujibu maswali yako kiusahihi zaidi." Majibu ya Mama Neema hayakuwa yakimridhisha Baba Neema hata kidogo. Kwakuwa kwa muda huo Mama Neema hakuwa sawa kiakili. Baba Neema hakuona haja ya kuendelea kumfyatulia maswali yenye majibu yasiyoridhisha.

Walifika nyumbani na zoezi la upishi kwa Mama Neema likaanza. Alipomaliza kupika walikula.

"Sasa.... Unajua leo umenitoa tu kazini kwa dharula."

"Kwahiyo?" Alihoji Mama Neema.

"Kwahiyo nini.. Sinahtaji niende zangu kwa wifi yako, pombe. Siunajua ndomida yenyewe hii." Aliongea Baba Neema huku mkono wake wa kushoto akiuangalizisha kulia na kutazama Saa yake.

"Hivi... Hata kama ndo mapenzi ya dhati na hiyo pombe! Ndo uache matatizo hapa ya wagonjwa na wewe kwenda kupombeka." Akaongea Mama Neema huku ameweka mikono yake kiunoni mwake.

Baba Neema hilo hakulijali sana akaanza safari ya kwenda kuisaka pombe. Mama Neema akajiweka mlangoni na kuziba njia ilikusudi Baba Neema au Devi asiondoke.

"Mbona unanizuia?"

"Kwasababu hutakikunielewa. We unadhani ukirudi umelewa hayo mawazo yakushauriana yatatokea wapi?" Alihoji Mama Neema. Hapo Devi ikabidi atumie utaalamu wake wa maneno. Akamlaghai Mama Neema mpaka akakubali kuiachia njia.

Devi alienda kwenye pombe kitendo kilichompelekea Mama Neema kuboeka kukaa peke yake ilhali anamawazo.

Alikumbuka jambo. Akachukuwa simu yake na kuibonyeza kana kwamba kuna kitu anatafuta. Alipopata na kujiridhisha aliiweka simu ile kwenye sikio lake. Iliita na mwisho wa siku ilipokelewa.

"Hello!" Sauti kutoka kwenye simu iliita. Mama Neema alijibu na kisha kujielezea.

"Usijali.. Hatamie ulinipatia namba zako hivyo hakuna kilichoharibika hapo. Enhee vipi mgonjwa wenu anaendeleaje?" Alihoji mtu yule wa upande wa pili. Mama Neema alimjibu na kumpatia maelezo yote waliyopatiwa na Docta.

Baada ya kupeana taarifa. Hakukuwa na ziada zaidi yakukata Simu.
Mama Neema kila akifikiria, chozi lilizidi kumtoka. Alijitamania kufa kwa kuliko kuendelea kutatua matatizo yasiyo tatulika. Alijiona kila kosa lililoendelea.. Yeye ndio chanzo cha kosa hilo. Kwanini asiangue kilio ilikuiridhisha nafsi yake juu ya kipindi kigumu alichonacho? Aliuchukia uwepo wake na alijihisi yeye yupo duniani kwa ajili ya kuwaweka watu matatizoni.

Alikumbuka ile siku aliyomuingiza matatizoni yule mtu aliejitambulisha kwa jina la Mavugo. Akakumbuka jinsi alivyo mharibia maisha Kibakuli kule kwa Aneth. Naam, yule Getiman ndio aliitwa Kibakuli. Alikumbuka zile siku zote alizoishi pale kwa Aneth akiwa kama mfanyakazi wa ndani. Alifumba macho na kuminya chozi kishalikaanguka chini.

Ni mengi aliyoyawaza mpaka akahisi yeye amebeba maovu na uwepo wake utaendelea kutangaza maovu zaidi. Akatamani kujiua. Akakiendea Kisu huku baada ya kuandika maandishi ya kutokuhusishwa katika kesi ile kwa mtu yeyote. Kishaakashikiria kisu na kukiangalizisha tumboni. Akiwa anakipeleka tumboni aliwaza mengi sana, akakumbuka alivyomuhangaikia mwanae na pia akawaza maisha ya mwanae baada ya yeye kufariki. Akauona ugumu wa mwanae ataoupitia bila Mama. Pia akamfikiria kibakuli atavyoteseka. Hapohapo yakajirudia kichwani mwake yale maneno yenye busara aliyowahi kuambiwa siku aliyofanya mauaji. Alimkumbuka vilivyo huyo mtu aliejitambulisha kwa kipindi kile kwa jina la Mavugo. Akapata picha matatizo atakayo yaacha kwa Devi pindi maafande watakapo mng'ang'ania kama mshukiwa namba moja wa mauaji. Hapohapo akafumba macho yake mawili na kukitupa kisu kile chini.

Aliamua kuichana ile karatasi na moja kwa moja akakimbilia chumbani mwake na kujibwaga kitandani huku akiendelea kulia.
 
RIWAYA: KICHAA.

Na: ZUBER R. MAVUGO.

N0. 25.

ENDELEA.

Ni mengi aliyoyawaza mpaka akahisi yeye amebeba maovu na uwepo wake utaendelea kutangaza maovu zaidi. Akatamani kujiua. Akakiendea Kisu huku baada ya kuandika maandishi ya kutokuhusishwa katika kesi ile kwa mtu yeyote. Kishaakashikiria kisu na kukiangalizisha tumboni. Akiwa anakipeleka tumboni aliwaza mengi sana, akakumbuka alivyomuhangaikia mwanae na pia akawaza maisha ya mwanae baada ya yeye kufariki. Akauona ugumu wa mwanae ataoupitia bila Mama. Pia akamfikiria kibakuli atavyoteseka. Hapohapo yakajirudia kichwani mwake yale maneno yenye busara aliyowahi kuambiwa siku aliyofanya mauaji. Alimkumbuka vilivyo huyo mtu aliejitambulisha kwa kipindi kile kwa jina la Mavugo. Akapata picha matatizo atakayo yaacha kwa Devi pindi maafande watakapo mng'ang'ania kama mshukiwa namba moja wa mauaji. Hapohapo akafumba macho yake mawili na kukitupa kisu kile chini.

Aliamua kuichana ile karatasi na moja kwa moja akakimbilia chumbani mwake na kujibwaga kitandani huku akiendelea kulia.

..... .... ......

Baada ya muda kupita, ulisikika wimbo uliyokuwa ukiimbwa kilevi. Wimbo ule ulikuwa ukiisifia bia tu na ulionekana ni mpya masikioni mwa kila aliyeusikia. Sauti ya wimbo ule ilisikika vyema sikioni mwa Mama Neema nae akaitambua sauti ile na mtunzi wa wimbo ule bila shaka alimtambua.

Muimbaji alipofika mlangoni aligonga mlango na kufunguliwa na Mama Neema. Hata alipofika alianza ucheshi wake wa hapa na pale. Baadae alijitupa kwenye sofa na kupitiwa usingizi palepale. Huku Neema kwa muda huo nae akiwa amerejea kulala.

Usiku wa siku hiyo ulipita. kulipo pambazuka Mama Neema aliamka na kwenda kufanya usafi wa mwili baada ya hapo alimuamsha Devi ambae alikuwa amelala sebuleni kutokana na pombe aliyo kunywa usiku wa kuamkia siku hiyo. Devi baada ya kuamka nae alifanya usafi wa mwili huku Mama Neema yeye akianza uwashaji jiko kwa ajili ya mapishi.

''Vipi kwani kuna haja ya mimi kwenda kumuona mgonjwa?'' Alihoji Baba Neema.

''Haina haja kwani kinachotakiwa hapa ni mimi kwenda kumpelekea chakula tu. Kwahiyo sidhani kama swala hilo lina weza kukufanya wewe uhangaike namna hiyo. Wewe nenda tu kazini, nitakupa habari'' Alijibu Mama Neema.

''Sawa haina shida achamie niende kazini manake kuna kazi za watu jana zime lala sasa naimani watakuja asubuhi kuziijia.'' Aliongea Baba Neema.

Walitaniana kidogo kisha Baba Neema akaondoka nyumbani na kuelekea kazini. Alipofika alichukuwa vifaa nakuanza kupaka rangi kabati aliyoilaza jana, alipomaliza alihamia kwenye vitanda kadhaa ambavyo aliacha kuvipiga msasa siku iliyopita. Alifanya kazi zile na kuzimaliza saa moja kabla ya wale wahusika kuanza kuja. Hata walipofika walimlipa pesa yake nae akawapatia vitu vyao.

''We Marijani... Hebu nnjoo hapa mara moja'' Aliita Baba Neema kumuita mmoja kati ya wafanya kazi wake.

''Ndio nakusikiliza mkubwa'' Aliitikia wito kwa heshma.

''Nadhani unakumbuka vizuri kuhusiana na ile inshu ya kutengeneza madwati ya shule. Vipi unayafuata saa ngapi maana naona muda unazidi kwenda tu. Wakati tuna kazi nyingi.. Au we unapenda kila kitu hadi ukumbushwe?'' Alihoji Baba Neema.Na hapo ndipo Marjani akakumbuka kuhusu swala lile.

''Lakini Boss ile inshu ya shule simpaka saa tatu au nilisikia vibaya?''

'' oooh... Shit!!!!! Hivi wewe Marijani huwa unatumia akili ya nani kufikiria?''

''Nani?? mimi??''

''Kumbe naongea nanani?"'

'' Hahahahaha... Bosi bwana. Nilidhani unamuuliza mtu mwingine. Sasa bosi inamaana watu huwa wanatumia akili za kina nani kufikiria?''

''Sipendi maswali hebu nenda kafanye kazi'' Aliongea Baba Neema na Marjani akatii.

Nikawaida ya Marjani kugombezwa na Bosi wake kwani nae nimmoja kati ya wale binadamu waliyopo kwa ajili ya masihara. Sasa mara nyingi Baba Neema si mpenzi wa masihara pindi awapo kazini. Lakini huwa ana vituko pindi tu aiwekapo pombe kinywani. Na hayo ndio maisha ya Baba Neema. Ufundi seremala ndio unamlisha yeye pamoja na familia yake, una msomesha Neema, na kupangilia mambo mengine ya kimaendeleo. Ni bora uchezee sehemu yoyote lakini si hiyo yake ya kazi.

.............................. ...............................................

Musa alianza kazi ya kuuza duka huko Dar-es-saalam. Duka lenyewe lilikuwa ni lile linalohusika na maswala ya ujenzi. Naam, lilikuwa kubwa sana kitendo kilichopelekea yeye kuongezwa pale na kuweka idadi ya wauzaji wawili maana haikuwa rahisi kwa muuzaji yule wa mwanzo kuwa ridhisha wateja wengi ambao waliyokuwa wakija pale na kununua vifaa. Wengi wao walikuwa wakikasirika na kuondoka kutokana na foleni huku wengine waki hudumiwa ilhali wana fyatua malalamiko. Naam, ujio wa Musa ulisaidia sana kwani wateja wengi walianza kupata haki zao na waliendelea kufurika kila leo kutokana na upatikanaji wa mahitaji yao kiurahisi.

Musa aifanya kazi yake kwa bidii sana huku akifikiria jinsi maisha yao yalivyo magumu. Bahati nzuri ile kazi yao hawakuifanya hadi usiku bali waliifanya hadi mida ya saa kumi na nusu na kufunga duka lao kisha kurejea pale walipoishi wote kwa pamoja.

''Dah! leo nimechoka sana, siunajua wateja walivyokuwa wengi. Yaani sasa hivi naenda kulala kabisa maana duh!!'' Aliongea Musa kipindi anafanya harakati za kufunga pale.

''pole sana jamaa.. Ila wewe kaza tu. Siunajua mwanzo mgumu.... Sema nini? nakupa bigapu. unajitahidi sana mkali wangu. Mi... nilikuwa nakuchukulia mchumba tu. Kumbe kazi unaiweza mwanangu.'' Aliongea Paul au pal kama alivyojiita na kupenda watu wa muite. pal yeye ni mzoefu na ndio mfanyakazi mwenzie na Musa. Yeye Pal sikwamba aliokotwa au kuletwa kufanya kazi kwa msaada. la. huyu pal yeye ni mtoto wa dada yake na mwenye duka kabisa, yeye kwakuwa hakupenda kusoma. Aliamua kumuomba mjomba wake kazi ya dukani nae mjomba wake akampatia bila kinyongo cha aina yoyote.

....................... .................................................

''Mavugo acha mie niende nikamuone yule dada nilokwambia kuwa ni rafiki yangu.''

''Yupi huyo? aaaaaaaah kumbe yule ambae ulinambia ana mgonjwa''

''yes.. Huyohuyo. Kuna mambo anahitaji kunieleza sasa ameomba nikamsikilize kisha ni mshauri''

'' Umshauri?'' akacheka Mavugo tena kwa kicheko cha dharau. Kisha akasema. ''Hivi wewe ndugu yangu, ushaona maji yakidanganywa hata siku moja?'' Hapo Docta Endrew nikama hakuelewa chochote ikabidi aulize.

''Sikia Endrew.. Usitake kunifanya mie mtoto sawa? unajua tokea elimu itolewe vichwani mwa watu na ikakusanywa kwenye vitabu iliwatu mjifunze. Matokeo yake mmeshinwa kujifunza na kuanza kutengeneza matabaka ya wasomi na mbumbumbu.'' Aliongea Mavugo na kumfanya Docta Endrew ajihisi vibaya.

''Aaaaaaah! Unajua Mavugo hapo unakosea sasa.. Kwani kuonana na rafiki yangu kuna uhusiano gani na elimu yangu?''

''Kijana kuwa uyaone. Mkubwa akikosea huwa haambiwi kwa namna hiyo. Kingine mimi nimekwambia hivyo kutokana na maneno yako yaliyo likosea heshima sikio langu. Huwezi kunidanganya kisa unadhani sijui.. Hivi toka lini mtu aliyepata matatizo akapatiwa ushauri? au ndio tuseme hujui hata maana ya ushauri eti?'' Aliongea Mavugo. Hapo Docta Endrew akatabasamu kidogo na kuiachia ile sura yake ya mikunjo aliyoanza kuitengeneza.

''Kweli.. Nilikuwa nimesahau ugonjwa wako. Kumbe bado unaumwa? Kwani wewe kwa akili zako unaweza kumshauri mtu wa aina gani kama unasema mwenye matatizo hashauriwi'' Alihoji Docta Endrew kwa mzaha.

'''We.. naona shule ilikuharibu na si kukufunza. Hebu kabla hujaondoka na kwenda huko. Naomba nikufunze jambo'' Aliongea Mavugo na Docta Endrew akakaa ilikusikiliza utumbo wa Mavugo kama alivyodhania.

'' Unajua ushauri huwa hautolewi baada ya tatizo bali hutolewa kabla ya tatizo lakini umetumia laghai zako tu kunidanganya kuwa unaenda kumpa ushauri mtu ambae tayari ana matatizo'' Aliongea Mavugo na kumpelekea Docta Endrew aangue kicheko chakujilazimisha ilikuibua dharau iliyo jificha moyoni mwake.
''Kweli wewe ni Kichaa.... Ina maana unatakakuniambia watu wote wanaopewa ushauri hua hawana matatizo? Hebu punguza kichaa bwana, kwani mimi ninapo kushauri wewe baada ya kukosea huo hauitwi ushauri? ahaaaa!!! acha hivyo bwana Mavugo kwanza unazidi kunilia muda wangu acha mie niende.'' Aliongea Endrew huku akianza kunza kuondoka.
''Subirii!!!'' Ilisikika sauti ya kukalipa iliyomfanya Endrew asimame, kisha Mavugo akamsogelea. ''Unajua wewe unajifanya umtaalamu sana wa mambo eti kisa umekabidhiwa kuhudumia wagonjwa wa akili. Hebu ngonja nikupe somo kabla hujaenda huko kwa huyo mtu wako.. Unajua kuna vitu viwili ambavyo umeshindwa kuvitofautisha na kujikuta ukijiona uko sawa kumbe unakosea.. Kuna kitu kina itwa ushauri na kuna kingine kinaitwa nasaha,'' Hapo Endrew akawa makini kusikiliza.
'' Ushauri wenyewe hutolewa kama tahadhari kwa ajili ya jambo linalo sadikika kutokea au kinga ya jambo hilo.Halafu pia kuna kitu kina itwa nasaha, hichi hutolewa baada ya jambo fulani kumtokea mtu. Sasa wewe kwenye nasaha unaweka ushauri na kwenye ushauri unaweka nasaha na hapo ndipo kutokuelewana kwetu kunapoingia'' Aliongea Mavugo kisha akaanza kuondoka na kurejea ndani. Docta Endrew yeye akajikuta akipatwa na bumbuwazi kwani hakutaraji kabisa kama angekuwa na makosa. Hapo kwa mara nyingine akamuomba Mavugo msamaha na zaidi akapendekeza kama Mavugo ataweza basi aendenae kule alipohtaji kwenda.
''Hapana mie sijiskii kutoka acha nibaki tu. Wewe nenda wala usijali'' Alikataa Mavugo.
''Tafadhari naomba nawe uungane nami angalau ukampatie nasaha zako yule dadanakuomba'' Aliendelea kubembeleza lakini Mavugo alikataa katakata ndipo Endrew alipoamua kuondoka yeye mwenyewe.
Alienda hadi eneo walilo ahidiana wakutane na Mama Neema, alipofika walisalimiana na maongezi ya kaanza.
''Unajua dokta mie nimekuita hapa ili uweze kunisaidia maana kuna mambo ambayo yanakisumbua sana kichwa changu'' Aliongea Mama Neema na Docta Endrew aiendelea kuonesha umakini katiika kusikiliza kile alichokuwa akihitaji kuambiwa.
'' Dokta mie unavyoniona mpaka hapa ni muathirika wa virusi vya ukimwi na ninaishi navyo kwa zaidi ya miaka kumi na tisa illiyopita......'' Alihadithia yote yaliyompata katika maisha yake na hakuficha hata moja mbele ya Docta Endrew yaani alieleza mpaka ile siri iliyopo kati yake yeye na Baba Neema kwamba yeye na Baba Neema simke na Mume bali ni kaka na dada wa hiari lakini waliweka siri tu.
Hapo Docta Endrew akapumua na kukosa hata aya yakuanzia, alibaki akilishangaa umbile dogo la mwana mama yule huku akitathmini mengi aliyo yapitia katika maisha yake alichoka. Jasho lilijikuta likimtoka ghafla bila yeye kukusudia huku akizidi kumuhurumia zaidi Mama yule.
''Ina maana unataka kuniambia ulishawahi hadi kuua?''
''Ndio Dokta''
''Sasa mbona serikali haijakuhukumu. na ilikuwaje hadi akahukumiwa mtu mwingine tena asiye na makosa wakati
 
RIWAYA: KICHAA.

Na: ZUBER R. MAVUGO.

N0. 26.

ENDELEA.

'' Dokta mie unavyoniona mpaka hapa ni muathirika wa virusi vya ukimwi na ninaishi navyo kwa zaidi ya miaka kumi na tisa illiyopita......'' Alihadithia yote yaliyompata katika maisha yake na hakuficha hata moja mbele ya Docta Endrew yaani alieleza mpaka ile siri iliyopo kati yake yeye na Baba Neema kwamba yeye na Baba Neema simke na Mume bali ni kaka na dada wa hiari lakini waliweka siri tu.
Hapo Docta Endrew akapumua na kukosa hata aya yakuanzia, alibaki akilishangaa umbile dogo la mwana mama yule huku akitathmini mengi aliyo yapitia katika maisha yake alichoka. Jasho lilijikuta likimtoka ghafla bila yeye kukusudia huku akizidi kumuhurumia zaidi Mama yule.
''Ina maana unataka kuniambia ulishawahi hadi kuua?''
''Ndio Dokta''
''Sasa mbona serikali haijakuhukumu. na ilikuwaje hadi akahukumiwa mtu mwingine tena asiye na makosa wakati

''Dokta!!! Nimesha kwambia kuwa yule aliye hukumiwa alihukumiwa kwaiaba ya kunisaidia tu. Nahakuna yeyote anaejua kuwa mimi nilishaua zaidi ya wewe niliyekuambia pamoja na Devi tu. Tafadhali nisaidie dokta kuhusu suala la huyu mbonjwa wangu muathirika ambae alisababishiwa uathirika na mimi. Nimfanmye nini maana kiukweli japo ni miaka kumi na tisa imepita lakini bado na mpenda. Istoshe mimi kwa sasa naishi na Devi toka miaka hiyo iliyopita pia nakumbuka kipindi nafukuzwa kule kwa Aneth mimi na mimba yangu. Kibakuli alihitaji kuondoka na mimi lakini nilimzuia tu, ila mpaka leo anajua kuwa ile mimba ilikuwa yake wakati, ni yayule mwana haramu aliyekufa miaka kadhaa kwa kifo alichostahili aliyeitwa afande Kipara. Tafadhali dokta nisaidie maana huyo mgonjwa akigundua kuwa mimi ndie nilyemuambukiza ukimwi basi atanichukia tena atanilaani kama nikimwambia kuwa Neema si mwanae wa kumzaa. Bora Neema ningekuwa sijampa historia ya maisha yangu lakini tayari hakuna asilolijua kuhusu mimi. Sasa we unadhani hapo mie nifanye nini. Tafadhali Dokta nisaidie, sihitaji kumpoteza kibakuli wangu''
Hapo Dokta Endrew hakuwa najibu zaidi ya kukikuna kichwa chake tu. Alijaribu kufikiria mpaka mwisho wa akili zake lakini hakuna alichoweza kukiambulia ambacho kina weza kuwa msaada kwa Mama Neema.
''Dada nimekuelewa sana. lakini swala lako linahitaji ufikiri wa hali yajuu zaidi kwani yakifanyika makosa kwenye kufikiri. Basi kutatokea tatizo kubwa sana. Hivyo nilikuwa ninaomba unipe muda wa kufikiri. Lakini kwakuwa sasa hivi mwanao Neema yupo shule, basi mi sioni kama kuna ubaya wewe ukikaa na kaka yako huyo wa hiyari kisha umueleze jambo hilo ili huyo mpenzi wako akiruusiwa kusiwepo tena na mitafaruku ya hapa na pale. Akikuuliza kuhusu mtoto, wewe usimwambie kuwa si..wake bali mwambie kuwa ni wake na kwasasa yupo shule. Siku Neema akirejea hapo nadhani tayari cha kufanya kitakuwa kimesha fahamika.'' Aliongea Endrew na wote kwa pamoja wakaagana baada ya kumaliza maongezi yao. Kwa namna fulani Mama Neema aliridhika a ushauri ule hata alipofika nyumbani alifanya mambo yake huku akimtegea Devi arudi jioni.
Siku hiyo Devi alirudi jioni huku kinywa chake kikiwa hainukii pombe, kwakuwa alijua kunauwezekano siku hiyo kukawa na kikao kati yake na Mama Neema maana hata yeye alikuwa na shida ya kufahamu mambo mengi kuhusuyule mtu waliyemsaidia kwani hakuwa akimfahamu hata kidogo.
Baada ya kupata cha kula cha jioni ukurasa wa maongezi ulifungulwa kati yao na hiyo ni baada ya Devi kutaka kumjua yule mgonjwa waliyemsaidia.

'Mhhh!! dada yangu hapo una mtihani sana maana endapo mambo haya yakijulikana zaidi. Inaweza kuwa hatari sana na hata kukugharimu. Hapa unachotakiwa kufanya nikuacha nyuma ya pazia pabaki mamefungwa na kufanya usiri tu. Haina jinsi.
Mdanganye kuwa mtoto ni wake ilikuokoa mengi, nibora atambue kuwa wewe ndie chanzo cha yeye kuwa hivyo ilhali anajua ana mtoto. Kuliko kujua ukweli. We fanya hivyo na imani mambo yataenda vyema tu na sir itaendelea kutunzwa.'' Aliongea Devi huku kwa wakati huo Aisha akizungusha mikono yake kichwani kwa kumaanisha kwamba kwa muda huo akili yake iikuwa inavuruga tu.
''Kaka usitake kuniambia kuwa kutunza siri kwa Kibakuli ndio suluhisho la matatizo,'' Aliongea Aisha kisha akavuta pumzi kidogo na kuendelea kusema.''Mpaka sasa tayari Neema anajua kuwa wewe si Baba yakke mzazi nami nilimwambia ukweli wa mimi na wewe japo sikumwambia kuwa wewe ni kama kaka yangu ila anajua kuwa wewe simzazi wake. Sasa we unadhani Neema anaweza kukubali kuishi na Baba nitae mletea na kumtambulisha kuwa ndio Baba yake? kumbuka anamchukia sana Baba yake japo sijawahi kumwambia kuwa hayupo duniani yule mwana haramu.'' Aliongea Aisha huku akionesha wazi kushindwa kuya vumilia aliyokuwa akiyaongea. Hapo Devi akashusha pumzi ya nguvu.
Ati, anamjua Baba yake? Ati anatambua kuwa mimi si Baba yake? Toka lini?. Ni maswali yaliyoendelea kukizunguka kichwa cha Devi. Maswali hayo hayakuwa haba kiasi cha kumfanya kichwa chake kisimuume. Hapo akauchukua mkono wake wa kulia na kuanza kuutembeza kichwani mwake si kwa ajili ya kusafisha nywele zake! bali ni kukikunakuna tu na asielewe nini alipaswa kukifanya.
Nikama kiti alichokalia kilikuwa na miba jinsi alivyo jitoa kwacho. Alisimama sasa na hapo akannza kutembea kwakuzunguka palepale huku paji lake la uso akiendelea kulisurubisha kwakutumia kiganja cha mkono wake ambao ulitoka punde tu kukuna kichwa chake.
''Kwahiyo unataka kunambia kuwa Neema tayari anajua kila kitu!!!!!???? kwanini ulimjuza mapema sana? kwanini??? ahhhhh!! sasa nini maana ya kutunza siri toka kipindi kile? ah! kama ulijua utafanya hivyo mbona ulikubali kutunza siri halafu kwa unafiki wako eti ukiwa nami unaniita mumeo. Sasa kumbe huwa una nifanyia unafki tu.'' Aliongea Devi huku akipiga piga ukuta baada ya kuliachia paji la uso wake. Akaona kama kuendelea kuendelea kuwa pale ni kama kero akaanza kuchukuliwa na miguu yake ilikupelekwa ndani lakini kabla hata hajavuka maeneo yale akadakwa mkono. Hapo ikabidi ajigeuze na kutazama nyuma ilikujiridhisha japo alitambua wazi kuwa aliyekuwa amemshika ni Aisha. Ndipo alipomuona aisha akiwa amemkaza mkono huku akiiruhusu miguu yake kusakiti eneo lili na kuyaruhusu magoti yake kutua chini kisha akaanza kuomba msamaha.
Aliomba msamaha wakuridhisha sana na akaongezea kwakusema kuwa Neema bado anajua kuwa mimi na wewe ni mtu na mkewe isipokuwa tu ameshajua kuwa wewe si mzazi wake. Nilimueleza ukweli siku aliyonibana sana, siku hiyo sikuwa na jinsi zaidi ya ukweli tu Lakini haikuwa dhamira yangu, naomba unisamehe'' Msamaha aliupata baada ya kujieleza kiundani zaidi mpaka Devi akaridhika.
Mama Neema alieleza mbinu aliyopewa na Docta Endrew na Devi akaridhika nayo.
''Ipo vyema.... Inafaa hiyo'' Alisema Devi baada ya kuulizwa kama waitumie au la.
Siku hiyo waliagana huku wakiwa wamekubaliana kuifuata ile mbinu ya Docta Endrew.
............................. ....................................................... .................
Musa yeye aliendelea kuangalia video usiku ule ilhali wenzake wakiwa wameondoka na kumuacha peke yake sebuleni. Naam, nikwakua vitu kama vile hakuwahi kuvipata akiwa nyumbani kwao ambapo si video tu. Bali hata umeme haukuwahi kuingia kwao.
Alikuwa ameanza kuifuatilia tamthiia moja ya kikorea ijulikanayo kwajina la Dong yi. Kwakuwa alkuwa akiifahamu lugha ya kigeni, jambo hilo halikuweza kumtatiza sana kushindwa kuelewa mpaka tafsii za maneno zilizo kuwa zikipita kila wahusika walivyo kuwa wakiongea. Hakika aliifurahia tamthilai ile iliyosheheni masuala ya utawala wa kifalme huku ikitembea na dhamira ya mapenzi. Alimpenda sana Dong yi akamchukia Lady jung kama ambavyo alivyopatiwa roho ngumu kwenye hadithi ile Zaidi nile penzi tamu na la kipekee lililochorwa kati ya mfalme na Dong yi ndilo liliweza kumvutia zaidi na kumfanya ajihisi yupo na mpenzi wake Neema. Mawazo yalikitawala kichwa chake na kuanza kuingiza amri za kumbukumbu zilizomrudisha mbali kimawazo na hata kuikumbuka ile siku aliyotamkiwa wazi na Neema kuwa lazma atamuoa kwa hali yeyote ile pasina kujali msululu wa shida zilizomo katika familia yao.
Kila alipo kumbuka bas aligundua kuwa amemkosa sana mpenzi wake yule, alitamani awe karibu nae lakini masomo ndio tatizo ila kwa upande mwingine aliona hata kama angekuwa karibu nae angemlishanini? angemlaza wapi? angempeleka wapi? Hapo ndipo hasira za kujituma katika kazi kwa bidii ziliendelea. Akalisaliti sofa na kuanza kujongea hadi chumbani kwake alipofika alifanya utaratibu wa kuchojoa mavazi ya juu na kubakiza yale ya ndani aliyoyateua kwa ajili ya kulalia akakiendea kitanda chake kilichokua hatua kadhaa mbele ya macho yake kisha akajibwaga na kuyaruhusu mawazo yamtawale kwa hiyari yake.
Alidhani huenda mawazo yange mrudisha kwenye ile fikra ya mpenzi wake Neema, badala yake yalimfanya amkumbuke Mama yake na akumbuke jinsi shida alivyo jaza utajiri nyumbani kwao. Hakika hakuipenda shida japo shida ilimng'ang'ania na hata kumvuta shati kila siku lakini alijitahidi juu chini kuikwepa na ndio maana alifanya kazi kwa bidii huku akiamini kuwa yale yaliyomo katika maisha yake kwa wakati huo yataja kuwa historia. Alipokumbuka kuwa kwa wakati ule Mama yake alikuwa na simu. Akaichukua simu na kubonyeza vitufe kadhaa kisha akaiweka sikioni. Simu iliita kama sekunde kumi tu na hapo hapo ikapokelewa, alimjulia hali Mama yake na kumuuliza juu ya upatikanaji wa chakula pamoja na mahitaji mengine muhimu. Mama yake alishukuru Mungu na kumwambia kuwa kila kitu anapata kwani mfanya biashara yule anampatia msaada wa kutosha kila aendapo Mwanza.
Baada ya maongezi yale hapo kidogo roho ya Musa ikaridhika kwani huwa anapatwa na mashaka sana kila amkumbukapo Mama yake, akaichukua shuka na kujifunika hakuchukua muda sana tayari usingizi ukawa umemchukua.
.............................. ......................................................
Asubuhi ya siku iliyofuata Neema na wanafunzi wenzake kadhaa waliofuzu mashindano ya mpira wa pete yaliyofanyika jijini mwanza na kisha yakafanyika kikanda nako pia wakafuzu. Hatimae walichaguliwa kwenda kushindana kitaifa ambapo michezo hiyo ilifanyika kibaha. Huko kulikuwa kuna kila aina ya wachezaji waliyo sheheni vipaji kedekede kuachilia mbali wachezaji wale ambao kila mmoja alikuwa na uchu wa kuwa bingwa kutokana na kujiamini. Vilevile kulikuwapo na mgeni rasmi ambae aliahidi kutoa zawadi kwa shule ya mwanafunzi atakae wakilisha vyema katika mashindano hayo. Mgeni huyo hakuwa mwingine bali ni Pita Mwambe ambae ni mbuge pia ni waziri wa michezo na utamaduni.

Kia timu ilikuwa imejipanga kuwa kabiri wapinzani. Kuna ile iliyothamini sana madawa huku timu aliyokuwemo Neema ikiamini kuwa madawa ya kuloga hayana maana uwanjani kwani mpira ni kipaji na si uchawi.
Soka lilianza huku televisheni pamoja na redio vikionesha na kutangaza soka lile bila chenga kwani lilikuwa ni soka lililosubiriwa kwa hamu zaidi hapa nchini kuanzia pale walipoanza mpaka siku hiyo ya fainali.
 
RIWAYA: KICHAA.

Na: ZUBER R. MAVUGO.

N0. 27.

ENDELEA.

Asubuhi ya siku iliyofuata Neema na wanafunzi wenzake kadhaa waliofuzu mashindano ya mpira wa pete yaliyofanyika jijini mwanza na kisha yakafanyika kikanda nako pia wakafuzu. Hatimae walichaguliwa kwenda kushindana kitaifa ambapo michezo hiyo ilifanyika kibaha. Huko kulikuwa kuna kila aina ya wachezaji waliyo sheheni vipaji kedekede kuachilia mbali wachezaji wale ambao kila mmoja alikuwa na uchu wa kuwa bingwa kutokana na kujiamini. Vilevile kulikuwapo na mgeni rasmi ambae aliahidi kutoa zawadi kwa shule ya mwanafunzi atakae wakilisha vyema katika mashindano hayo. Mgeni huyo hakuwa mwingine bali ni Pita Mwambe ambae ni mbuge pia ni waziri wa michezo na utamaduni.

Kila timu ilikuwa imejipanga kuwa kabiri wapinzani. Kuna ile iliyothamini sana madawa huku timu aliyokuwemo Neema ikiamini kuwa madawa ya kuloga hayana maana uwanjani kwani mpira ni kipaji na si uchawi.
Soka lilianza huku televisheni pamoja na redio vikionesha na kutangaza soka lile bila chenga kwani lilikuwa ni soka lililosubiriwa kwa hamu zaidi hapa nchini kuanzia pale walipoanza mpaka siku hiyo ya fainali.

. Mama Neema alikuwa karibu zaidi na televisheni yeye pamoja na Baba Neema. Docta nae alikuwa kwake ametulia yeye na mke wake pamoja na Mavugo wakitazama mpira ule wa pete, huku Musa siku hiyo akiwa mzembe zaidi kazini kutokana na akili yake yote kuiwekeza kwenye tv iliyokuwepo maeneo yale. Mama Musa nae japo hakuwa na uwezo wa kununua tv lakini alikuwa na karedio kake. Alichukuwa muda wake kukasikiliza na alifurahi kila aliposikia jina la mkwe wake likitajwa na kusifiwa na mtangazaji.
Mechi ilikuwa ngumu sana kitendo kilicho wafanya wachezaji wote kuogopana sana kutokana na kila timu kujiamini hadi kupitiliza. Neema kila alpoupata mpira uwanja mzima ulifurahia sana kwani alikuwa akifanya ukinzani na utundu usiyo na mfano. Kuna muda alijitutumua na kuruka nao mpira hewani japo hakuwa mrefu zaidi lakini alitendewa madhambi na mchezaji wa timu pinzani kitendo kilichompelekea aanguke palepale, alitolewa nje na kutoka kwake nikama kutoka kwa wachezaji wote kisha wakamuacha mchezaji mmoja. Naam, mipira kadhaa ilitupwa ndani ya goli la kina Neema huku wakijitahidi nao kushambulia kwa nguvu zao zote lakini jiti hada zao hazikuwa zikizaa matunda waliyo yataraji kutokana na kukosekana kwa kiungo wao Neema.
Kila mtu alikata tamaa watu wengine kama kina Mavugo walitoka kwenye runinga huku wakisema kuwa hawawezi kuuacha muda wao upotee ilhali washindi wameshajulikana.
Neema alijifikiria mara mbilimbili. Nikweli nimeumia. Lakini je, kuumia kwangu ndiko kuigharimu timu yangu na ishindwe fainali hii??? haiwezekani!!! Sikubali kabisa jambo hili, lazma nirejee uwanjani hata kama nikujitoa sadaka lakini sikukubali timu yangu ishindwe mbele ya macho yangu. Nitachechemea tu. Nimaneno yaliyo muingia Neema kichwani na kama yalivyo aliyatoa mbele ya kocha wake kitendo kilichopelekea kocha ashangae uzalendo wa Neema. Neema haitimae alirejea uwanjani huku wapinzani wakiamini kuwa hatoweza kuwasumbua tena nikwakuwa tu hawakumjua Neema ambae yeye hujeza kwa hasira ya ushindi tu, hapendi kurudi nyuma hata kidogo. Hapo aliwachezesha mpira wa ajabu na kusababisha magoli kadhaa kwene timu yake huku yeye akifunga mawili kwa mkono wake.
Mpaka mpira unamalizika, timu ya kina Neema ilikuwa imeibuka kidedea kwa kuizidi bao moja tu ile timu ya upinzani kwani nayo ilikuwa na mabao mengi. Waziri wa michezo alifurahia sana uchezaji wa Neema na alitoa zawadi kwa kila mchezaji kwani timu zote mbili wachezaji wake walitoka shule tofauti tofauti hivyo kila mchezaji alie wakilisha shule yake. Alizawadiwa yeye na shule aliyotokea. Mheshimiwa Pita Mwambe aliomba amsmeshe Neema mpaka atakapo maliza. Kipindi anamalizia kuongea maneno yale na kisha skilini kugeuzwa kwa Neema ndipo Mavugo aliporudi na kwa bahati nzuri au mbaya hakupata kumuona Waziri yule ambae anapendwa na kila mwananchi.

''Vipi mbona makelele tena watu tumepumzika? Alihoji Mavugo baada tu ya kurejea sebuleni.
''We siulisema ile timu itashindwa?'' Alidakia mke wa Docta Endrew.
''ipi hiyo? ile ya yule mtoto aliyekuwa akicheza vizuri?''
''Hiyo hiyo.''
''Msinitanie nyie... Ina maana mnaweza kusema kwamba ile timu ndo imeshinda? aaa!!! acheni kunitania nyie, yani yule mtoto alivyoumia tu hakuna tena kilichoendelea na ndo maana mi niliona ni bora kwenda ndani kupumzika enhee!!! ilikuwaje hadi wakashinda, usinambie hawakutumia dawa!!!'' Aliongea Mavugo.
''We ulivyoondoka tu, alirudi na kucheza tena mara ya pili.''Alijibu mke wa Endrew tena hakuishia hapo akaongeza kwakusema.''Yaani, hadi mheshimia mwenyewe akajitolea kumsomesha bure.''
''Hao waheshimiwa ndo wanafanya nchi inayumba tu. Kama walikuwa wanajua umuhimu wa msaada mbona hawakuutoa pale ulipo hitajika na wautoe leo baada ya mateso.'' Aliongea Mavugo hapo docta Endrew akataka kupinga. Lakini alipogundua kuwa msemaji alikuwa ni Mavugo. Ikabidi aulize tu na sio kupinga.
Kwanini unawasema vbaya waheshimiwa waliyopewa nyadhifa za kukaa bungeni na kutatua matatizo ya nchi yako?''
''Hahahahaha,'' Akacheka Mavugo kisha akamgeukia Endrew ambae alikuwa amekaa kwenye sofa upande wa nyuma.''Wewe Endrew wewe kumbe unaweza hata kufurahia pindi ukimuona mtu anakuibia wewe. Ok, tuachane na hayo. Ila kama kweli wanatoa msaada basi wange msomesha kwanzia elimu yake ya awali lakini tofauti na hilo hapo niuongo tu . Usitake kuniambia mtu ambae tayari yupo sjui form 6 au 5 ambae amebakiza muda mchache tu amalize masomo yake hapo ndipo mtu ajitokeze kumsaidia, huo ni upuuzi.''Aliongeas Mavugo.
''Ok, tuachane na hayo. ila naomba tuongee kidogo inshu moja.'' Aliongea Docta Endrew na palepale mke wake akaamka na kuondoka ilikuwapisha waongee kwani alijua maongezi hayo yatakuwa haya muhusu.
''Sawa nakusikiliza''Alijibu Mavugo baada yakuona kuwa wamebaki wawili tu.
Dokta Endrew akamwambia Mavugo kuwa anatamani sana amkutanishe na Mama Neema iliangalau yeye akampatie ushauri maana Endrewni kama alikuwa ameshindwa kumpatia ushauri stahiki. Mavugo aliafiki swala lile na kumtaka Docta Endrew apange muda kama itawezekana iliaweze kumshauri. Hapo wakawa wamekubaliana . kitendo bila kuchelewa Docta Endrew akampigia simu Mama Neema na kumueleza kuwa kuna mshauri mzuri amempata na anaimani kuwa mshauri huyo atamsaidia sana Mama Neema. Wakapanga kama itawezekana wiki ijayo waweze kuonana.
......................... ..........................................................
Musa alikuwa na furaha kwani hakutarajia kama mpenzi wake angeweza kufanya maajabu kiasi kile. Hakusita kujitapa kwa rafiki yake wa kazi lakini aliishia kuchekwa tu kwani hakuna aliyemdhania kama angekuwa na uwezo wa kumiliki msichana kama yule. Wakiwa katika marumbano yale mara alikuja mteja na kukatisha maongezi yao. Alipofika walimuhudumia nae akaondoka.
''Aisee mwanangu, sjui watu wengine walitelemshwa tu?''Alhoji Musa huku akimtathmini kwa umakini zaidi mdada yule kipindi anatoka dukani pale.
''Aaaaaaa!!!! wewe na wewe, mbona unatamani hadi vilivyo nje ya uwezo wako? kwa akili zako unadhani huyo dem unahadhi hata ya kuwa rafiki yake?'' Aliongea rafiki wa Musa.
''Kwanini unasema hivyo? au yeye haendi chooni nini? au huw anajisaidia matofari ya nyumba.''
''Hapana sina maana hiyo.''
''kumbe ipi? Ujue nyie watanzania bwana! huwamnanishangaza sana. Tatizo lenu mnapenda kujitoa kasoro nyingi sana hadi mnafikia kutojiamini kabisa.'' Aliongea Musa.
''Sasa kumbe we ulidhani nchi gani wajitoe kasoro kama sisi watanzaniaa tukiacha kujitoa? huo ndo utamaduni wetu bwana. Halafu usinione mimi kama mshamba sana, ujue huyo dem ni mtoto wa Waziri kabisa halafu we... unatamani tamani tu. Shauri lako utafungwa!''

''Acha zako wewe. Kwani mtoto wawaziri ndio nani? ah! usipende kuwa namna hiyo. Kama ukiendelea kujiona mdogo basi utaonwa mdogo hata na wadogo zako. Fanya, ukuwe. Hatakama angekuwa mtoto wamfalme, ila punguza uoga.''
Wakiwa katika maongezi yao mara walimuona tena dada yule akirejea kwa mara nyingine, Musa alimkaribisha tena.
'' Thanks. Samahani nimesahau simu yangu hapa, sjui mmenionea?''Aliongea yule binti mrembo.
''Simu!!!! wapi hapa??'' Aliongea Musa.
''Ndio, nakumbuka kipindi nakuja nilikuwa nayo mkononi sasa huenda niliisahau hapa ndio maana nimerudi kuitazama.'' Aliongea tena yule mrembo.
''Hivi hata hizi simu huwa hazina akili eti? inawezekana vipi simu inamilikiwa na kisura kama wewe halafu zinapotea, ok, ngoja nikusaidie kutafuta labda imeangukia kweye maboksiboksi humo.''Aliongea Musa na kuanza kutafuta tafuta. Utani na ucheshi wa hapa na pale ulimpelekea Mrembo yule avutiwe sana na Musa kwani katika maisha yake hakuwahi kukutana na kijana ambae kama ukikaanae kwa muda wa dakika moja bila kufurahi basi utakuwa unaongopa tu. Musa aliitafuta ile simu hatimae akaipata na kumpatia mrembo yule aliyembambika jina lakisura.
''Nashukuru sana kwa msaada wako.''
''Usijali, tumeumbwa tusaidiane. Yaani nikujali unijali. '' Akafuatiza kwa kicheko cha lazima huku Kisura akibaki na tabasamu.
''Ningependa nikupatie namba zangu za simu iliangalau tuwe tukichati pale upatikanapo muda.'' Aliongea Kisura.
''Ondoa shaka kwa hilo. Lakini minahisi nikichukua namba zakonitakusumbua bure maana mimi huwa sina mtu wa kuchati nae zaidi ya huyu rafiki yangu hapa. Sasa nahisi nitakuwa nakukera sana.''Alionngea Musa ikiwa ni kama kujaji jambo fulani.
''Usijali, hatamie na muda wa kuchati ndio maana nikahitaji mawasiliano nawe''
Walibadilishana namba za simukisha wakaagana kwa heri na kisura yule akawa ameondoka.
''Mwanangu wewe ni mchawi aisee'' Aliongea Rafiki yake baada ya kisura yule kupotea machoni mwao.
''Hapana, unajua kwenye hii dunia hutakiwi ujishushe hovyo, yule pale mrembo hawezi kuchomoa japo umenambia sijui ni mtoto wa mbunge.''
''Kweli, maana!!! Hivi, hicho nikipaji chako au ni mangekewa tu hayo?''
''Kawaida tu. Sema unahtajika ubunifu zaidi ilikuweza kumpata mtu .''
Waliendelea na maongezi yao na walipofika wateja waliwapatia huduma kama kawaida.
.............................. ...................................................................

''Kwahiyo na wazazi wako pia wapo hukohuko Mwanza?''
''Ndio, ndipo wanapoishi.''
''Vizuri, sasa inabidi twende wote kwa wazazi wako ili kama inawezekana nikawaombe nikuchukue niishi na wewe huku Dar-es-salaam kwani huku zipo shule nzuri naimani utafanya vizuri zaidi.''
Yalikuwa ni baadhi ya maongezi kati ya Mheshimiwa Pita Mwambe ambae kwa muda huo alikuwa kwake yeye pamoja na Neema. Alimchukua Neema baada tu yamashindano yale kuisha na kumpeleka moja kwa moja hadi kweake. Walipanga kuwa wiki itakayokuja ndio itakuwa sahihi kwao kwenda Mwanza kwa ajili ya kumumba Neema kwa wazazi wake. Aliamua aende bwana Mwambe mwenyewe
 
RIWAYA: KICHAA.

Na: ZUBER R. MAVUGO.

N0. 28.

ENDELEA.

''Kwahiyo na wazazi wako pia wapo hukohuko Mwanza?''
''Ndio, ndipo wanapoishi.''
''Vizuri, sasa inabidi twende wote kwa wazazi wako ili kama inawezekana nikawaombe nikuchukue niishi na wewe huku Dar-es-salaam kwani huku zipo shule nzuri naimani utafanya vizuri zaidi.''
Yalikuwa ni baadhi ya maongezi kati ya Mheshimiwa Pita Mwambe ambae kwa muda huo alikuwa kwake yeye pamoja na Neema. Alimchukua Neema baada tu yamashindano yale kuisha na kumpeleka moja kwa moja hadi kweake. Walipanga kuwa wiki itakayokuja ndio itakuwa sahihi kwao kwenda Mwanza kwa ajili ya kumumba Neema kwa wazazi wake. Aliamua aende bwana Mwambe mwenyewe.
....................................... ....................................

Siku iliyofuata ndio siku ambayo waliahidiwa wakamchukue Kibakuli hospitali, Aisha na Devi walishirikiana na wote kwa pamoja wakaenda kumchukua kisha wakamleta nyumbani.
''Ahsanteni sana kwa msaada mliyoweza kuutoa kwangu kwani sikuweza kutegemea tena katika maisha yangu kupata msaada lakini Mwenyezi Mungu pekee ndie aliyepanga jambo hili. Nakushukuru sana Aisha kwa kuweza nipatia msaada huu kiukweli ina chakukulipa zaidi ya kukuombea dua tu.'' Aliendelea kuongea kibakuli maneno yale.
''Kawaida, usijali. Nijukumu langu kukusaidia kwani wewe ni mtu wa muhimu sana katika maisha yangu. Huyu hapa, anaitwa Devid. Nikaka yangu wa hiari na ndie aliyenisaidia mpaka leo nipo hapa.'' Aliongea Aisha.
''Devi, Huyu hapa anaitwa Kibakuli. Ndio yule mpenzi wangu niliyekwambia, naweza sema kuwa huyu ndio Baba Neema. Kama ujuavyo, nilitengana nae baada ya mie kufukuzwa na Bosi wangu kwakosa la mimi kupewa mimba na yeye...............'' Aisha alitoa utambulisho mrefu sana huku akielezea mambo mengi yaliyomkuta katika maisha yake.
''Aisha, naomba unisamehe mpenzi wangu kwani wewe ulipoondoka tu. Aliletwa mfanyakazi mwingine nami nikaamshawishi hadi akakubali kuwa namimi. Nadhani huyo mfanya kazi ndie aliyenisababishia mimi gonjwa hili la hatari kwani nalianza kuona dalili ndipo nilipoamua kwenda kupima baada ya kupima ndpo nilipokutwa na ugonjwa huu nilipomfuata yule binti nae akanilalamikia mimi ila kwa asilimia zote, yeye ndi aliye niambukiza hivyo naomba unisamehe kwahilo mpenzi wangu.'' Aisha alilia kwa uchungu huku akimuhurumia mpenzi wake kwa kujipatia kosa ambalo halikumuhusu. Alijifanya kumpoza mpenzi wake yule.
Hata bwana Kibakuli alipomuulizia mwanae aliambiwa kuwa Mwanae yupo shule na kwa muda huo alikuwa ameshakuwa. Alifurahi sana baada ya kugundua kuwa mwanae ni msomi, alimshukuru Devi kwa kumsomeshea mwanae na kuahidi kumlipa gharama zote alizotumia pindi tu atakapo pata maisha mazuri lakini Devi yeye hakuwa na shida na malipo kwani aliamua kujitolea tu. Kumsomesha mtoto yule na kumlea.
Kwakuwa, Mama Neema alikuwa akilala peke yake, aliona hamna tatizo kama akilala na mpenzi wake tu kwenye chumba kimoja na hivyo ndiyo ilivyokuwa usiku wa siku hiyo japo hawakufanya chochote.

Usiku ule Aisha aliweza kulala na Kibakuli chumba kimoja huku wakikumbushana mambo kadha wa kadha ambayo tayari walikuwa wamesha yapitia katika maisha yao pindi walipokuwa pamoja. Ingawa Kibakuli alikuwa mgnjwa lakini hilo halikumfanya yeye asitishe masihara pamoja na vituko vyake bila shaka hicho ndicho alicho kipenda Aisha kutoka kwa Kibakuli.
''Kwahiyo unataka kunambia mtoto wetu ni mcheza mpira???''
''Ndo hivyo, tena anacheza yule!! sijui hata amefuata kwa nani maana mie mama yake mambo hayo siyajui kwannza hata shuleni sikuwahi kupata namba.''
''Huyo atakuwa amefata kwenye ukoo wa Baba yake.''
''Kivipi tena? kwani we baba yake ulikuwa ukicheza mipira ya pete?'
''aaaaah!!! umeanza. Toka lini mtoto wa kiume akacheza michezo hiyo nawe? Mimi nilikuwa professional footballer, kijiji kizima walikuwa wakinitegemea .''
''toka lini? Au ndo unanitania maana wewe nawe'' Akapiga kofi moja Aisha angani kisha akasema. ''Sikuwezi''
''Wewe naona unanisikia tu. Unajua mie spendi ubishi au kama unabisha ngoja tuje twende kijijini kwetu ukaulize, au siku yoyote ile ukipata mtu anaeenda huko mwambie akaulize jina la proessional Kibakuli kama atanikosa.''
''Haya bhana, umeshinda. Lakini mbona Neema hachezi mchezo huo wa mpira wa mguu kama kweli karithi kwako?''
''Huyo Neema atakuwa amerithi kwa shangazi yake maana yule dada yangu alikuwa ninoma kwenye mpira wa pete. Walikuwa hawawezi kucheza bila kumuita yeye. Nakumbuka alichukuliwaga na wazungu kwa ajili ya mpira akapelekwa huko. Siku hizi anasomwa tu kwenye vyombo vya habari yaani ninoma sana.'' Aisha akaguna baada ya kugundua kuwa alikuwa akidanganywa, kisha akampiga kofi dogo Kibakuli.
''Unanipiga, ngoja nikuoneshe'' Kibakuli nae akampiga Aisha kiutani ilimradi tu kudhihirisha uwepo wa pendo lao. Wapendanao hao wakaendelea na utani wao huku wa kikumbushana mengi sana yaliyo wafurahisha na kuwahuzunisha. Yaliyo wahuzunisha ni kama habari za kifo cha Mama mkwe wa Aneth, ambae alikuwa Boss wao wote wawili. Pia nijuu ya Aneth kuachika kwa mme wake baada ya mme wake kuoa mwanamke mwingine huku akilazmisha kuwepo kwa wanawake wawili. Baada ya Aneth kuondoka, utawala mpya wa mwanamke yule aliyeolewa na mume wa Aneth uliweza kupelekea Kibakuli afukuzwe kazi na kunyimwa huduma hali iliyopelekea kuzorota kiafya na kukosa muelekeo kabisa wa maisha. Machozi pia hayakusita kumtoka Aisha kla Kibakuli alipoweka nukta katika usimuliaji wake.
................................ ...................................................
''Hello'' Ni sauti iliyo sikika kutoka upande wa pili wa simu ya Musa.
''Nambie, Kisura'' Aliongea Musa huku akiendelea kuuchezea mto wake ambao kwa muda huo alikuuwa haja uweka kwa ajili ya kuuegemea bali kuubeba kifuani.
''Nikuambie nini sasa mimi zaidi tu ya kuhitaju utani wako'' Alijibu binti yule aliyesikika sauti ndani ya simu ya Musa na asionekane sura.
''wapi??? mbona mie sina utani wowote unanisingizia tu.''
''Utakosaje utani nawewe? haya leta chochote ulicho nacho ilitukifanye kama stori''
''stori!!!! mmmmhhh!!! we unapenda stori za aina gani maana hapa ndo kisiwa cha stori'' Akajibu Musa huku akijitengeneza na kujiweka sawa.
''Zozote tu ulizo nazo.'' Akajibu yule bint mwenye kusikika sauti tu bila kuonekana sura.
''We taja tu, au nikusimulie za misukule na wachawi?''
''Weweeee. Tma mate chini, Hujui mwenzio naogopa sana tena usiku huu istoshe niko peke yangu. Mistaki za kutisha tisha.''
''Kumbe unataka zipi Kisura?''
'' Nipe menu kisha nitajichagulia mwenyewe''
''Mhhh... We muoga eti?''
''Kwanini unaniita muoga.''
''Hapana wewe si muoga wala nini, nilikuwa tu nakutania''
''Mistaki.. Niambie kwanza huo uoga wangu maana huwezi ukaongea kitu sirious halafu unidanganye eti, ulikuwa unatania tu.''
''Tuachane na hayo, mwisho salio liishe bure halafu nishindwe hata kukusimulia. ok, chagua unapenda stori za Maisha, shule, za kutisha au mapenzi?''
''Ammmmmh!!! hiyo ya mwisho''
''ipi hiyo?''
''Ebwana ee.. Mie spendi, siumeitaja mwenyewe kwani hadi namie niitaje bwana?''
''Kwahiyo umekasirika Kisura''
''Hapana ile sipendi kukejeliwa.''
Musa huku akitoa kicheko cha kujilazimisha, ''Basi. Siunataka ya mapenzi?''
''Hiyohiyo'' Musa akashusha pumzi kisha akaanza kutililika maneno yake.
Naam, naweza sema Musa si mtu mshamba mdomoni, anauwezo wa kuongea vizuri na kufikiria vizuri huku mpangilio wake wa maneno ukiwa na maana moja ambayo husindikizwa na maana nyingine ndogo ndogo zenye dhamira kuu moja. Alichezesha mdomo wake kwa maneno ambayo yaliingia moja kwa moja hadi moyoni mwa Binti yule mrembo tusiye mjua jina lakini ni mtoto wa waziri au kisura kama tunavyoweza kumuita kupitia Musa amtaniavyo.
Maneno matamu, ahadi tamu, sauti tamu, ucheshi wa hali ya juu uku uongo wa kumfananisha Kisura na Malaika kwa uzuri aliyokuwanao. Kwanini Kisura asikubali? Angekuwa mehu kama asingekubali maana toka aanze kufuatwa na wanaume hajawahi kukutana na maneno matamu kama ya Musa. Vijana waleo kwa kilugha chao wanasema mtoto amesaini. Naam, ukurasa mpya wa mapenzi ukaanzishwa kati ya Musa na mtoto wa waziri. Wakapeana ahadi kemkem, za kukomboana kiuchumi huku zingine za kuoana ilimradi tu mapenzimapenzi.
Jina la Musa likamtoka Kisura na akazalisha majina mapya yaliyosoma kichwani mwake kwa muda huo. Mara amuite, baby, mara sweet, darling na majina mengine ya kiingereza ambayo yanamaanisha mapenzi mapenzi tu.
Wakiwa katika maongezi yale mara simu nyingine ikaingia kwenye simu ya Musa. Akamuomba Kisura akate mara moja ili aweze kushughulika na simu ile kwanza kisha atapiga tena.
''Hellow'' Aliongea Musa, kisha mpigaji wa simu ile akampatia taarifa iliyompelekea Musa aongee kizungu bila hiyari yake.
''What???????????, Mmeshampelka hospitali?''
''Sasa tungejuaje kama ana Kansa bila kumpeleka Hospitali???'' NisautI iliyosikika kutoka kwa mpigaji.
''ok, nakuja huko kesho'' Aliongea Musa kisha akakata simu. Alihema kwa nguvu huku kichwa kikimgonga na akili ikimuuma baada ya kupokea taarifa zile za kwenye simu. Japo kulikuwa kuna baridi lakini yeye alihisi joto kambidi aende kuoga. Alipotoka alikutana na simu zilizopigwa kuangalia akakuta namba iliyandikwa kisura, hakuijali kwani alihisi haina msaada kwake. Hapo akaishikiria simu na kuanza kutafuta namba za watu muhimu kwake kwa muda huo. Aliwapigia wote kwa ajili ya kuomba msaada wa pesa lakini hakuna hata mmoja aliye msaidia, akakuna kichwa na kutamani kufuta namba zote za kwenye simu yake lakini akasita baada ya kukutana na namba ya Bosi wake, hapo akafumba macho na kupiga iliajaribu kwani aliamini baada ya hapo hakuna msaada mwingine. Bosi wake nae akamwambia kuwa hana pesa. Hapo mchozi ukatoka kila akifikilia umakini wa jambo aliloambiwa akabaki kajiinamia ingawa ilikuwa saa tisa usiku lakini yeye alikuwa macho muda huo. Mara simu ikaita kwa mara nyingine akaitazama kwenye kioo akaigundua kisha akaipokea kivivu huku akiwa hana hata hamu ya kuongea.
''Hellow baby, mwenzio nimeshindwa kulala hadi muda huu please usinifanyie hivyo ni bora kuniambia tu kama nimekukera kuliko kuacha kupokea simu yangu.'' Bila shaka alikuwa ni Kisura ambae alikuwa akilalamika na kuomba msamaha kwa pamoja pasina kujua kosa. Hapo Musa nikama hakuwa akielewa chochote kile hata tena uzuri wa sauti ya Kisura hakuusikia tena.
''sikia mimi na matatizo niache utanitafuta kesho.'' Aliongea Musa kwa sauti ya ushari kitu ambacho ni kigeni kabisa masikioni mwa Kisura toka amjue huyo Baby wake kama alivyomuita.
'' Kipi hicho mpaka umfiche mpenzi wako? hapana sikuachi mpaka uniambie.''
''Skia Kisura wangu. Hata kama nikikwambia huwezi kunisaidia kwani shida hiyo hata mimi mwenyewe naishindwa ije wewe?'' Aliongea Musa baada ya kuhisi moyo wake ukimsuta kwa kuwa alitaka kuzimaliza hasira za kukosa msaada kwa kumkasirikia kisura wake.
 
RIWAYA: KICHAA.

Na: ZUBER R. MAVUGO.

N0. 29.

ENDELEA.

''sikia mimi na matatizo niache utanitafuta kesho.'' Aliongea Musa kwa sauti ya ushari kitu ambacho ni kigeni kabisa masikioni mwa Kisura toka amjue huyo Baby wake kama alivyomuita.
'' Kipi hicho mpaka umfiche mpenzi wako? hapana sikuachi mpaka uniambie.''
''Skia Kisura wangu. Hata kama nikikwambia huwezi kunisaidia kwani shida hiyo hata mimi mwenyewe naishindwa ije wewe?'' Aliongea Musa baada ya kuhisi moyo wake ukimsuta kwa kuwa alitaka kuzimaliza hasira za kukosa msaada kwa kumkasirikia kisura wake.
'' Baby, please dont hide your problems infront of me. I think you know my posiotion in your heart and your life so please baby tell me whats happen to you my tomorow Husband'' Aliongea Kisura kwa sauti ya upole na yenye utukivu wa hali ya juu huku kiitumia ile lugha yake ambayo huwa anaiaminia katika kubembelezea.
''Sawa achanikwambie mpenzi wangu. Muda ule nimekuomba ukate simu, kulikuwa na jambo ambalo si nzuri.” Akamuhadithia yote.

Ilifika ahsubuhi ya siku ile, nae Musa hakuwa na chakusubiri, alibeba nguo zake na moja kwa moja hadi ubungo. Alikuta agari mengi yanayoenda mikoani, hakusita kupanda kwenye moja kati ya magari yaliyomridhisha magari hayo hayakuwa yeye kuchelewa hivyo haikumchukuwa muda sana kuianza safari yake.
Wakati yupo njiani aliendelea kuongea na mpenzi wake kwa njia ya ujumbe mfupi. Walifarijiana huku wakitekenyana kupitia maneno yao matamu ya kulisifia na kulipamba pendo lao. Mawazo yakawa hayamuijii sana Musa kutokana na kutolewa shaka na mpenzi wake huyo mwingine ambae kwake anaweza sema kama nizawadi kutoka kwa Mungu kwa ajili ya kumsaidia kwenye matatizo yake, yeye anakumbuka kuwa mara yakwanza kipindi anahtaji kumtongoza yule kisura alikuwa akijaribu tu kupima nyota yake lakini hakuwa na shida na mpenzi kwani alikuwa nae mpenzi wake anaempenda na kumthamini sana japo alijua kwa muda huo atakuwa shule.
Musa alifika kwao Mwanza baada ya kulala njiani kwa siku moja kutokana na ubovu wa gari alilokuwa amelipanda. Hata alipopita alienda moja kwa moja mpaka Bugando Hospital na kumkuta Mama yake akiwa amepewa kitanda tu na asifanyiwe hata operesheni. Alipoliza kwanini Mama yake hajafanyiwa opareshen aliambiwa oparesheni itafanyika baada ya kuwepo na pesa istoshe kuna madaktari wachache tu wenye taaluma ile katika hospital hiyo hivyo alihitajika atoe pesa haraka sana. Akiwa katika kujifikiria mara ghafla simu ilipigwa na alipoangalia kwenye kioo aligundua ilitoka kwa mpenzi wake Kisura aliipokea na alifurahi baada ya kisura kusema kuwa yupo njiani kayika usafiri wa ndege hivyo muda si mwingii ataweza kutua jijini hapo.
Haikuchukuwa muda, Kisura akkafika na kutoa pesa kisha Musa akasaini Mama yake akafanyiwe opareshenimaana kansa hiyo ilizidi kuongezeka kila baada ya muda mchache tu.
................................................ .....................................................

''Mavugo, muda ndio huu, inabidi twende kwao kabisa ilitukawashauri vizuri kwani naimani mpaka sasa wapo wote. '' Aliongea Endrew baada ya kuona kama Mavugo hajali jambo lile. Hapo Mavugo akajiandaa kwa haraka zaidi.
.......................... ...........................
Upande wa kwa Mama Neema wao walikuwa hawana taarifa ya ugeni wowote kwa siku ya wiki hiyo tofauti na ugeni wa washauri ambao wataweza kusuluhisha kile kilichojulikana kama matatizo ilikueka mambo sawa hivyo kwanzia Dev, Kibakuli na hata Aisha mwenyewe wote walikuwa sebuleni kuusubili ugeni huo wa kina Docta Endrew kama walivyo ahidiana wiki iliyopita.
................................... ................................................
Wakati huo huo, Neema alikuwa ametuwa kwenye ndege baada ya kutangulizwa na Waziri kwani kwa muda huo waziri alikuwa kwenye kikao. Alifika moja kwa moja hadi kwa na ndipo aliposhangaa baada ya kuona sura ngeni, kama kawaida yake alisalimia huku akilazimishwa kuwa amsalimie mgeni yule kwa heshma kwani ndio Baba yake.
''Mwanangu kwanini ualia siku kama hii ya furaha. Siku ambayo ndo kwanza unamuona Baba yako eee?'' Alihoji Kibakuli baada ya kumuona Neema alitokwa na machozi kwa mshangao. Mara ghafla Neema akawa mkali.
'' Hebu niache!!! Mbakaji mkubwa wewe!! kama ungekuwa unampenda Mama yangu, ungethubutu kumbaka? au kama ungekuwa ukimpenda ungeweza kumuachia virusi vya ukimwi na kumsababishia mateso ya kuishi kwa kutangatanga hapa duniani. Umekuja lini hapa kwanza? na umeletwa nanini hapa? tafadhali sihitaji kukuona maana hujui jinsi gani Mama yangu kahangaika na mimba yangu huku wewe ukiendelea kufurahia na malaya zako huko......'' Neema aliendelea kuporomoka maneno mazitomazito na hakukuwa na wakumzuia kwani wote walikuwa wakiyasikiliza maneno yale. Naam, Neema alikuwa sahihi kuliko wao walivyofikiria. Mama yake neema ndie aliye mwambia Neema kuwa Baba yake alimuingilia tu bila ridhaa yake lakini hakumwamba kuwa Baba yake alisha fariki tena aliuliwa na Mama yake huyo huyo. Lawama zilizidi tena kwa aneno yaliyochoma sana mpaka ikafikia hatua Mama Neema akashindwa kuvumilia na kuhitaji kuutoa mkanda mzima palepale. Aliamua kuliko kuwaona watu wakirumbana pasina ukweli ni bora yeye ajieleze tu na hakukuwa tena a haja ya kuwepo washauri kwani tayari alianza kuuongea ukweli wote. Aliyaongea ya siri na ya wazi, mpaka akadhihirisha kuwa yeye kwa mikoo yake alimuua Baba Neema ambae alikuwa ni afande na akasema kuwa hata kipindi anakutana na kibakuli kwa mara ya kwanza alikuwa tayari anamimba pamoja na virusi vya ukimwi pia alieleza kuwa yeye ndie aliyempa kibakuli ukimwina hiyo ilisababishwa na ung'ang'anizi wa kibakuli huku Neema akijilinda pale il mwisho wa siku mimba ikionekana abambikiwe Kibakulli iliapate mlezi wa kuilea kwani mimba ile haikuwa na Baba na niwazi kuwa asingeweza kuilea yeye mweyewe tena ukizingatia na ugonjwa ule aliyokuwa nao.
''We mshenzi lazma nikuue. Kumbe weweni mnyama kiasi hicho. Ulinibambikizia mimba na kunilaghai kuwa huyo mtoto ni wangu halafu kumbe ndio wewe uliyenipatia maambukizi huku mimi nikiendelea kuwaambukiza watu wasiojua lolote. Lazma nikuue labda uanze wewe mjinga sana wewe...'' Aliongea Kibakuli huku kwa muda huo akiwa amebadilika sura na kuwa katili, ndio alidhamiria kufanya alichokisema lakini ilikuwa ngumu baada ya kukutana na ukinzano wa Devi ambae alijitahidi kumtunza maungoni mwake iliasije kumdhuru Mama Neema. Wakati yote hayo yakiendelea upande wa Neema yeye alikuwa akilia tu baada ya kugundua kuwa kumbe amemchomesha Mama yake.
wakiwa katika migogoro ile iliyo sindikizwa na ya nafsi mara mlango uligongwa, Neema ndio pekee aliyekuwa na uwezo wa kufungua kwani wengine wote walikuwa bize na kushughulikia matatizo yao.
''Haaa!!! We binti sindo ulikuwa ukicheza jana jumapili kwenye ile timu huko kibaha au mko mapacha?'' Aliongea Mavugo baada ya kufunguliwa tu mlango na Neema.
Neema hakumjali sana Mavugo kwani kwa muda ule hakuwa na muda wa kuanza kuongelea masuala ya mpira tna bai ni jinsi gani ataweza kutatua mgogoro huo.
Mama Neema alipoisikia sauti ya Mavugo ikiongea pale nje nikama kuna kitu alikumbuka, lakini kumbukumbu yake ilikuwa ikikabiliwa na tukio la mauaji huku tena akiwaza kuuliwa hapo akawa hajielewi.
Hatimae Mavugo na Docta Endrew wakapita ndani huku Neema akifuata kwa nyuma. ile wanafika tu hivi, macho ya Mama Neema yalitua vyema machoni mwa Mavugo.
''Ni wewe tena!!!!. Aisha Mapuya?'' Alihoji kwa mshangao sana Mavugo baada ya kumgundua Mama Neema.
''Haaaa!!! Ama kweli milima haikutani binadamu hukutana. Hivi unataka kuniambia kwa muda wote huo wewe bado upo tu, au nimekufananisha?'' Aliongea Aisha na kuwafanya wote waliyomo ndani mule wapatwe na mshangao wa hali ya juu sana hasa hasa Docta Endrew, docta ambae aliahidi kumfanya Mavugo arudi kwenye hali yake ya maisha ya kawaida.
''mm..m..mnafahamiana?'' Alihoji Docta Endrew huku akisindikizwa na kigugumizi chamshangao.
''Docta, wajinga ndio hupoteza muda kuuliza maswali yanayojionesha lakini waelevu hukaa kimya iliwasijikute wanaropoka mambo yatakayo wafanya wa shuke hadhi. Ndi nilibu tosha la kukufanya utambue kuwa mimi na Aisha mwana wa Mapuya tunafahamiana.'' Alijibu Mavugo na kuleta mshangao mwingine baada ya Aisha kumkimbilia na kumkumbata huku akitoa machozi.
''Nisamehe sana. Kwanza shikamooo!!! pili naomba usinielewe vibaya ukadhani labda siku ile nilikutoroka la. Mwenzio nilikimbia kujitetea na nilijua wazi kwamba sitokuona tena katika maisha yangu hata siku moja. Nilijua mahakama haitoweza kukupatia msamaha hivyo sikuona haja ya kukuona ukinyongwa kwa kosa usilohusika nalo. Niliamua kufuata maneno yako kwani ulinisihi kamwe ni sikubali kujikatia tamaa kwakuwa maisha haya katwi na mapito kisha ukaniambia kuwa mimi bado binti mdogo sana na siku stahiki kunyongwa kwa wakati ule. ahsante sana kwa moyo wa kipekee lakini vipi mbona u,mzima mpaka sasa?'' Hapo wote wakawa kimya huku Docta Endrew akiona kama ndoto zake zina kwenda kutimia.
Mavugo alijieleza kwanzia pale alipokutwa na maafande akiwa ameshikilia kisu mpaka siku hiyo yaleo. Kila mmoja kwenye ile nyumba aliishangaa sana roho ya kipekee kutoka kwa Mavugo lakini Docta Endrew hakuridhika na chochote baada ya kugundua kumbe historia ya watu wale ni baada ya Mavugo kupoteza kumbukubu nasi kabla.
Wakiwa bado kwenye mshangao ule mara ghafla mlango uligongwa kwa nje kama kawaida Neema alifungua mlango na kumuona waziri akiwa nje. Alishangaa sana kwani Waziri saa moja lililopta alikuwa Dar-es-salaam tena kwenye kikao, alimsalimia kisha akamkaribisha ndani japo alijua kuwa kwa muda huo ndani hapakuwa na maelewano. Yeye wazirri nia ya safari yake ilikuwa ni kwenda kumuomba Neema kwa ajili ya kumchukua na kwenda kumsomesha tu. Alipofika ndani alikuta nyumba nzima ipo kwenye majonzi, macho ya wote waliyokuwa ndani mule yalimuangalia kwa uoga kwani wanamjua vyema tu. Ilikuwa tofauti sana na Mavugo kwani yeye baada tu ya kuwa amemuona tu, Waziri yule alimuita jina lake kabisa na akapatwa mshituko hapo hapo kisha akaanguka chini na kuzimia.
''Mchukueni haraka na tumuwahishe hospitali tafadhali kuweni makini na mfanye haraka.'' Aliongea Peta Mwambe baada ya kumuona Mavugo ameanguka chini ghafla. Pita mwambe alikuwa na furaha sana huku woga ukimjaa hapo hapo kwani alihofia hali ya Mavugo kutokana na kuanguka kwake. Lakini alifurahi kumuona tena kwa mara nyingine Mavugo ilhali ameishi akimtafuta katika maisha yake yote.
Devi, Neema,kibakuli,Endrew,Aisha, pamoja na Pita Mwambe huku wakifuatiwa na walinzi, wote waliweza kupanda kwenye magari ya msafara wa waziri yule na moja kwa moja waka wahi, Hospitali kwa ajili ya kuwahi kuokoa maisha ya Mavugo.
 
Back
Top Bottom