Riwaya: 'hofu'

Riwaya: 'hofu'

duh sasa kuna tofauti ya kidi kudi na willy gamba? au unaandika na kujijibu mkuu? hata hivyo nashukuru mnatukumbusha ya zamani
 
duh sasa kuna tofauti ya kidi kudi na willy gamba? au unaandika na kujijibu mkuu? hata hivyo nashukuru mnatukumbusha ya zamani

Mkuu mimi nipo namfuatilia Willy Gamba 1 kimya kimya. Naona jamaa ameniwahi kuileta hii riwaya, namfuatilia akifeli ntakuwa tayari kumsaidia ikibidi.
 
Last edited by a moderator:
tofauti na wewe, yeye haagi. anasepa mazima. ulikuwa unatujuza tukutane muda gani. yeye anashtukiza
 
Mkuu mimi nipo namfuatilia Willy Gamba 1 kimya kimya. Naona jamaa ameniwahi kuileta hii riwaya, namfuatilia akifeli ntakuwa tayari kumsaidia ikibidi.

Mkuu kama hadi usiku atakuwa bado nadhani utupie tu
 
Last edited by a moderator:
Mtaniwia radhi,nashindwa kuweka timetable ya kuweka hii kitu niko mzigoni kwa hiyo nikipata upenyo kama hivi nitawaleteeni. Mnivumilie kwa hilo. Kama yupo mwenye kuweza kuendeleza pale ninapokwama/kuchelewa ruksa tu alimradi tuburudike sote
 
HOFU
SEHEMU YA TANO

DAR ES SALAAM
III

Wakati Willy alipokuwa anaelekea kwake alianza kuwafikiria akina Bon na Rocky. Kule kuwafikiria kulimfanya apate nguvu rohoni mwake. Hii ilitokana na kwamba Willy aliwafahamu fika hao wenzake na zaidi ya hayo aliwaamini. Alifikiri sana juu ya kazi iliyokuwa mbele yake. Ni kweli kwamba kazi hiyo ilikuwa imewekewa uzito wa hali ya juu kama ilibidi kuwatuma watu wote hawa watatu katika operesheni moja. Mchukue Bon. Kwa mara kwanza Bon kufahamiana na Willy ilikuwa huko Japan ambako wote wawili walikuwa wanachukua mafunzo ya Ninja. Willy alikuwa amehitimu mapema na kumwacha Bon ambaye alikuwa amejiunga na chuo hicho nyuma yake. Willy alikuwa amemsaidia sana Bon katika masomo yake na alijuwa fika kwamba Bon nae angehitimu tu.

Bon alimchukulia Willy kama kaka yake na wote wawili walipendana sana. Baada ya mafunzo yake Bon alirudi Zimbabwe ambako alikuwa anakaa. Wakati huo Kamati ya Ukombozi ya nchi huru za Afrika iliwatuma kazi muhimu ambayo waliifanya kwa mafanikio makubwa. Kazi hiyo ilifanyika ndani ya Afrika Kusini na mpaka leo makaburu hawaamini kwamba kazi hiyo ilifanyika na watu wawili. Kisa hiki kukieleza kingechukua siku nzima, hivyo naachia hapa. Bali tu niseme kuwa safari yao huko Afrika Kusini iliwafanya wafahamiane vizuri na kila mmoja kudhibiti ujuzi na uwezo wa mwenzake. Kwa hiyo Willy, alipojuwa kuwa angekuwa na Bon katika kufanya kazi hii, basi wasiwasi ulitoka.

"Ninja wawili kutumwa Arusha. Kwani huko kuna nini?, labda makaburu watume jeshi zima", Willy alijisemea kimoyomoyo. Alimfikiria Rocky pia. Ingawa ni mara yake ya kwanza kufanyakazi nae, umaarufu wake ulijulikana Afrika kote. Walikuwa wameonana mara mbili. Lakini ilijulikana Rocky alishatumwa kazi ambazo zilifanana sana na kujituma mikononi mwa kifo. Pamoja na hali hiyo, Rocky alikuwa amefanyakazi hizo na kurudi salama. Kuweza kufanyakazi kama hizo kulimdhihilishia Willy kuwa Rocky alikuwa mtu jasiri sana. Willy aliamini kuwa yeye na vijana hao wawili walikuwa na uwezo wa kuwazuia makaburu kusababisha maafa katika mkutano huo muhimu wa wapigania uhuru.

Kulikuwapo habari za kipelelezi kuwa baada ya mkutano huo, mapambano ya kupigania uhuru yangeahamia ndani ya Afrika Kusini. Kwa hiyo kama makaburu walikuwa na fununu juu ya habari hizi, ilikuwa ni dhahiri kwamba wangejitahidi kuvuruga mkutano huo, kinyume cha kufanya hivyo ilikuwa kufungua mlango ili wapigania uhuru waiangishe serikali ya makaburu. Makaburu walijuwa fika kuwa mkutano huo ulikuwa hatua ya kwanza muhimu katika safari ya kuuangusha utawala wao bila kujali safari hiyo ilikuwa ndefu kiasi gani. Kuzuia hatua hiyo ilikuwa lazima kwao.

Alipofika nyumbani Willy alikwenda bafuni na kuoga. baadae alifungua sanduku lake ambamo alikuwa anatunza zana zake muhimu za kufanyia kazi. Alizichukua na kuziweka kwenye mkoba wake, alipiga simu kwa Sammy ambaye alimwarifu kuwa alikuwa anasafiri kwenda Arusha na kuwa habari zaidi angezipata ofisini. Vile vile aliomba atumwe mtu uwanja wa ndege kwa ajili ya kurudisha gari lake. Sammy alikuwa chini ya Willy kikazi lakini walikuwa marafiki wakubwa sana na mara nyingi walifanyakazi pamoja. Baada ya kupiga simu aliondoka kuelekea Mwenge ili kumwaga Mwana.

Alifika nyumbani kwa Mwana mnamo saa moja usiku. Tiketi yake ilikuwa inaonyesha kuwa safari yake ilikuwa saa tatu na nusu usiku. Hivyo Willy alikuwa bado na muda kuzungumza machache na mpenzi wake. Alipofika alibisha hodi na kufunguliwa mlango. Alikaribishwa ndani. Mwana alikuwa amejinyoosha na huku amejifunga kanga tu.

"Afadhali umekuja, nilikuwa na wasiwasi! vua ulale", Mwana alimwambia Willy.

"Nimekuja kukuaga", alijibu Willy.

Mwana aliinuka na kanga aliyokuwa amejifunga ikadondoka. Willy alitupa macho yake na kuona mwili wa mtoto huyu ambaye ubichi wake ulisisimua na kuchangamsha roho. Matiti yalisimama kwenye kifua chake kilichokuwa kinatweta utafikiri ni mapera yaliyoiba. Mwana alimrukia Willy aliyekuwa amekaa kwenye tendegu la kitanda na kumkumbatia. Joto la msichana huyu lilimwingia willy kama kisu kinavyotoka na kuingia ndani ya siagi. Ilihitaji mtu mwenye roho ngumu kama Willy kushinda jaribu hili.

"Mwana tafadhari niache niende", Willy alimsihi.

Mwana ambaye sasa alikuwa anatokwa na machozi alisema kwa uchungu, "Willy, kwanini unanitesa? kama hunitani si heri unieleze tu. Kama huna hamu na mimi kwanini ulinidanganya tangu siku ya kwanza. Kwanini usingeniambia ukweli kuliko kunitesa hivi, ooh! mungu wangu nimekosa nini mie".

Mara Mwana alijitupa kitandani na kuanza kulia; machozi yakimtililika kama mtoto mdogo.

"Mwana tafadhali, kuna kazi imetokea ghafra. Nilipotoka tu hospitali kumpeleka mzee nilikuta tiketi na ujumbe kutoka kwa mkubwa wetu wa kazi kuwa lazima niende Arusha. Kama ujuavyo sisi wafanyabiashara safari zetu ni za ghafra ghafra tu. Wewe unafikiri ni kijana gani ambaye anaweza kumwacha msichana mbichi kama wewe kwa siku na saa kama hii, na hasa baada ya raha ya leo mchana? Huyo huenda siyo mwanaume kamili", Willy alijibu kwa uchungu pia kwani hata yeye alikuwa amesisimka.

"Basi lala angalau kidogo. Dakika tano tu", Mwana alimwomba Willy.

"Mwana mambo haya hayaendi namna hiyo. mimi nitarudi baada ya siku mbili au tatu. Baada ya hapo wewe mwenyewe utajua kuwa nina hamu kiasi gani mimi na wewe," Willy alijibu.

"Haya nenda. Nakuruhusu," MWana alisema kwa uchungu.

Willy aliinama na kumbusu. Alisikia lile joto tena. Bila kusita aliinuka, akafunga mlango nyuma yake na kwa maudhi alijisemea, "Kwa kweli kazi nyingine......!".

Alipoingia ndani ya gari aliweka nyuma mawazo kuhusu Mwana. Wakati akiendesha gari, alifikiria safari iliyokuwa mbele yake.

Alifika uwanja wa ndege saa mbili usiku. Aliweka gari lake kwenye maegesho. Kisha alitoa swichi kwenye funguo zake na kuiweka mahali pa hifadhi ya swichi za magari. Hivyo ingemwezesha kijana ambaye angekuja kurudisha gari lake kuichukua hapo. Alifunga milango mitatu na kuacha mmoja umerudishiwa. Kisha kuchukua mkoba wake na kuelekea kwenye jengo la uwanja wa ndege.

"Tiketi yake tafadhari", aliomba Afisa Usalama hapo uwanjani.

Wakati anatoa tiketi yake alikuwa akiangaza huku na kule katika jengo zima.

"Haya endelea", alisema Afisa Usalama huku akimrudishia Willy tiketi yake.

Alielekea ndani. Kwenye kaunta alimkuta msichana aliyemfahamu.

"Willy, safari tena?", msichana aliuliza.

"Ndio", alijibu Willy.

"Wapi".

"Arusha".

"ZIko ndege mbili usiku huu. Wameongeza nyingine kwa sababu wageni wengi wanakwenda Arusha kwenye mkutano", msichana yule alimweleza Willy.

"Alaaa, sasa mimi niko ndege ipi?", Willy aliuliza.

"Chaguo lako. Sema unataka ipi. Iko ya saa tatu na nusu na pia ile ya saa nne na nusu", mischana alijibu.

"Subiri kwanza, ile ndege kutoka Harare imefika?".

"Ndio. Imefika saa moja".

"Kulikuwamo wageni wangu wanaopitiliza kwenda Arusha", Willy alisema.

"Majina yao tafadhari", msichana aliomba huku akimsogeza Willy pembeni ili watu wengine wasiweze kusikia. Halafu alimtaka aendelee.

"Sipele na Malele".

Msichana yule aliangalia kwenye orodha ya majina ya wasafiri kisha akainuka.

"Ya, wote wapo. Sasa hivi wanakula kwenye mghahawa hapo juu. Wataondoka kwa ndege ya saa nne na nusu", msichana alieleza.

"Oke, mimi niweke kwenye ndege ya saa tatu na nusu", Willy alisema.

Jina lake liliwekwa katika orodha.

Halafu alisema, "Hebu nikawaangalie hapo juu".

Alipopanda kwenye baa na mghahawa alikuta watu wamejaa ndii. Huku akisalimiana na watu huku na pale, Willy alijipenyeza kupita kwenye baa mpaka kwenye mghahawa. Mara aliwaona Bon na Rocky wamekaa kwenye kona wakila na kuzungumza. Aliwaendea polepole na Rocky ndiye alikuwa wa kwanza kumuona Willy.

"Bon, Willy yule".

"Aaaa mzee!", Bon alisema kwa furaha huku akiinuka na kumkumbatia Willy.

"Usinipakazia uzee, Bon, au huoni humu ndani kuna watoto. Unataka kuniharibia soko, vipi?", Willy alisema kwa mzaha.

"Hujaacha matani yako tu?", Bon aliuliza huku wakipeana mikono.

"Keti, bwana", Rocky alimvutia kiti.

"Ehee, leteni habari", Willy alisema.

"Mambo safi", Rocky alijibu.

"Safari, je".

"Safi kabisa", alijibu tena Rocky.

"Tulipata habari kuwa tungeungana hapa", alisema.

"Mimi nimeambiwa leo mchana", Willy alijibu.

"Kila mara huyo mzee wako anapenda kukushtusha", Bon alitania.

"Wazee wengine kama ujuavyo...", alisema Willy.

"Chakula vipi", Rocky alimuuliza willy.

"Mimi ndiye napaswa kuwauliza swali hilo kwa kuwa mko nyumbani kwangu", alisema Willy.

"Tumwisha jikaribisha", Bon alijibu.

"Vipi mzee wako kakupasha kidogo?", Rocky alimuuliza Willy kwa sauti ya chini.

"Kanipasha", Willy alijibu.

"Je, tutasafiri katika ndege moja".

"Hapana, mimi sina budi nitangulie na ile ya tatu na nusu, kama ujuavyo wote hatuwezi kusafiri katika ndege moja, ikianguka, je", aliuliza Willy.

"Willy hubadiliki", Rocky aliuliza.

"Siku nikibadilika ndio siku nitakapoacha kazi hii", Willy alijibu.

"Ni kweli, maana waati huo itakuwa ni hatari kwa maisha yako", Bon aliongeza.

Waliendelea kuzungumza huku wakiangalia kwa chati; kila kona ili kuona kama kuna watu waliowatia maanani. Lakini kufuatana na hali ya mambo ilionekana kila mtu alikuwa anashughulika na mambo yake.

"Tukutane hotelini kwangu mnamo saa sana usiku", Rocky alieleza.

"Wewe uko hoteli gani?", Willy aliuliza.

"Mimi niko Equator Hoteli kwa leo halafu nitahamia Maunt Meru hapo kesho, Bon alitaka Safari Hoteli", Rocky alimjibu.

"Basi mimi naona tukutane kesho asubuhi, mpate kupumzika leo kwani huenda kukawa na kazi kali baadaye. Mimi nitafikia New Arusha Hoteli", Willy alieleza.

"Mimi nafikiri maneno yako ni sahihi Willy", Bon alijibu.

"Oke, tuonane wapi na saa ngapi".

"Njooni hotelini kwangu saa tatu asubuhi", alijibu Willy.

"Oke, ahadi........", Rocky alijibu.

Mara walisikia tangazo;

Shirika la ndege Tanzania: Ndege namba 1001 iendayo Arusha, niko tarari kuondoka, abiria wote wanaosafiri na ndege hii wanaombwa kuelekea kwenye ndege hiyo sasa hivi.

"Jamani eeh, kwaherini. Tutaonana kesho", Willy aliwaaga wenzake na kukimbia akitelemka chini.

Alipofika kwenye kaunta alimkuta tena yule msichana.

"Siku nyingine utaachwa wewe".

"Niko macho", Willy alijibu.

"Utaniletea nini ukirudi?".

"Vitunguu".

"Nitafurahi sana. Haya safiri salama", yule msichana alimwaga.

"Ndipo Willy alikumbuka kuwa alikuwa hajakata tiketi ya malipo ya kiwanja. Hivyo alifanya karaka na kukata tiketi hiyo. Halafu alirudi na kwenda kwenye chumba cha kuondokea. Hapo chumbani Willy alikuta msururu bado mrefu sana.

"Lo! Leo pana jua nini iko. Watu hapana panda", Mhindi mmoja alilalamika.

Huenda kuna mtu anayo bastola. Labda wanaogopa kutekwa nyara maana hapo ndani wanakagua sana", Kijana mmoja alijibu.

Msururu huo ulikwenda pole pole, lakini hatimaye wote walipekuliwa. Kisha waliruhusiwa kuingia ndani ya ndege. Willy alikuwa ameridhishwa na upekuzi ule kwani ulikuwa upekuzi kweli kweli.

Willy alikaa nyuma kiti cha mwisho kama kawaida yake. Alifunga mkanda na kisha na kisha akakaa akisubiri matangazo ambayo alishayasikia mara elfu kidogo. Hayo yalikuwa matangazo ya IATA yahusuyo usalama wa usafiri wa anga. Baada ya matangazo hayo, ndege yao aina ya Boing 737 ilirushwa na vijana hawa wa Kitanzania.

Willy aliinamisha kiti chake kikakaa sawa. Akaanza kufikiri juu ya yale yote aliyokuwa akiambiwa na Chifu. Alichambua kipengele kimoja baada ya kingine na namna ya utekelezaji wa kazi nzima.

"Patakuwa na kazi", Willy alisema moyoni kwake.

ITAENDELEA
 
HOFU
SURA YA SITA

MAMBO

Ilikuwa sikukuu ya Idd. Siku ile Willy na Chifu walipozungumzia mipango kujidhatiti kiulinzi ili kuzuia uwezekano wa majasusi wa makaburu kuingia nchini bila kujulikana na kuvuruga mkutano wa wapigania uhuru. Wakati huo huo majasusi tayari wameshaingia mjini Arusha na tayari walikuwa wanapumzika nyumbani kwa F.K wakiwa tayari kuanza kazi. Hiyo ilikuwa na maana kwamba usiku wa jana yake F.K na Tondo kwa upande wa Tanzania na Peter kwa upande wa Kenya walikuwa wameweza kuwaingiza nchini kwa siri. Zaidi ya hayo, majasusi wa Makaburu walikuwa wameingiza mizigo yao yote. Asilimia mia tisini ya mizigo hiyo zilikuwa ni silaha za aina mbali mbali na vyombo vya kisasa vya kufanyia ujasusi.

Kwa kuwa gari la F.K lilikuwa halipekuliwi, safari yao kutoka mpakani hadi Arusha haikuwa na kisanga chochote. Pamoja na ulinzi mkali uliowekwa kwenye vizuizi njiani, watu hao waliweza kupita. Kila alipofika kwenye kizuizi F.K alitoa kichwa chake nje tu na maafisa wa polisi kimzaha walimpigia saluti na kumwashilia aendelee. Hivyo sifa za kinafiki za F.K ziliweza kusaidia majasusi wa makaburi wa Afrika Kusini kuingia Tanzania tayari kutoa kipigo dhidi ya wapigania uhuru wa Afrika huru kwa ujumla.

Baada ya kuvuka mpakani, Peter alirudi Nairobi akiwa ameridhika kuwa nusu ya kazi yake ilikuwa imefanyika tayari.

Mchana wote wakati majasusi walipokuwa nyumbani kwa F.K walikuwa wanajitayarisha walisafisha silaha zao, na wale Ninja wawili walifanya mazoezi madogo madogo. F.K alikuwa amewapeleka likizo wafanyakazi wake wote hivyo aliacha nyumba yake nzima itumike na majasusi. Walikuwa wakijipikia na kujifanyia mambo kadhaa. Kama nilivyoeleza hapo awali, nyumba ya F.K ilikuwa imejengwa kwa madhumuni kama hayo. Hata mtu angefika kwa F.K asingeweza kugundua kuwepo kwa majasusi kwani walikuwa wanatumia vyumba vya siri.

Ilikuwa yapata saa za jioni wakati F.K alipowakusanya majasusi ili kuwapasha habari.

"Sasa hivi nimepata habari kupitia kwenye chombo cha kupashana habari kilicho chumbani kwangu", F.K alisema "Wakubwa wetu wamepata habari kuwa mpelelezi mashuhuri wa wapigania uhuru, Bon Sipele na mpelelezi mwingine mashuhuri kutoka Zimbabwe, Rocky Malele, wameondoka leo mchana mjini Harare na Ndege ya shirika la ndege la Tanzania wakiwa njiani kuelekea Arusha. Taarifa niliyonayo inasema kwamba watu hawa ni hatari sana. Hivyo ni lazima wauawe, la sivyo watatia dosari katika mipango yetu. Vile vile nimeelezwa kuwa Paul na Fouche wanawafahamu watu hawa".

Nyumbani kwa F.K kulikuwa na chombo kupashana habari cha hali ya juu sana. Chombo hicho kilikuwa kinapokea habari kutoka kwenye Setelaiti. Setelaiti hiyo iliwekwa angani na Makaburu wa Afrika Kusini wakisaidiwa na Marekani. Kazi yake kubwa ilikuwa kupashana habari za kijasusi. Hivyo mawasiliano kati ya F.K na mabwana zake yalikuwa hayapitii njia za kawaida. Ndiyo sababu aliweza kupashana habari na hao bwana zake bila kugunduliwa na vyombo vya upelelezi vya Tanzania.

"Ndio, tunawafahamu vizuri sana", Paul alijibu.

"Kama kweli hawa watu wanakuja", Fouche alieleza "ni lazima kujiweka tayari. Hao mimi nawajuwa siyo mchezo. Kama maagizo yanasema wauawe mara moja ni sahihi kabisa. Wakisha fahamu na kuwa na wasiwasi wanaweza kufanya kazi yetu iwe ngumu. Ujuzi na uwezo wao ni mkubwa. Mimi naamini kuwa hata kama wanatutilia wasiwasi, bado hawajui kama tayari tumeingia. Wao wanatarajia sisi tuingie kwa ndege. Hivyo watajishughulisha na kuchunga viwanja vya ndege vya Dar es Salaam na Kilimanjaro".

"Kama wameweza kutuma wapelelezi mashuhuri kama hao", John aliasa "Ina maana hata serikali hizi zinahisi kitu".

"Lazima. Lazima mjue nchi hizi sasa hivi siyo mchezo", F.K alionya "nchi hizi zina uwezo mkubwa wa kipelelezi. Hivyo mfahamu kuwa mmekuja kupambana na watu wenye ujuzi kama wenu hivyo msifanye mchezo".

"Watafika saa ngapi watu hawa", Geoger aliuliza. Yeye ndiye alikuwa mkubwa wa kikosi hiki na pia mmoja wa wale ninja wawili. Yeye na Dave walikuwa na uwezo mkubwa kuliko wale wenzao.

"Ndege hiyo inatarajiwa kufika hapa saa tatu na nusu", F.K alieleza "Lakini nimepata habari sasa hivi kutoka kwa watu wangu walioko uwanja wa ndege kwamba kutokana na wingi wa wageni kutakuwa na ndege mbili. Kama mnavyojuwa mpaka sasa wageni wengi wameshaingia. Hadi kufikia kesho kila mjumbe anatakiwa awe hapa kwa ajili ya ufunguzi wa mkutano hapo kesho kutwa. Hii ina maana kwamba lazima tufunge kazi takatifu mnamo muda wa masaa sabini na mbili yajayo".

"Hiyo kazi itafungwa katika muda huo wala usiwe na shaka", George alijibu.

"Sasa umeamua nini juu ya watu hawa wawili Dave, ambaye wenzake wanamwita Devil, yaani shetani, aliuliza.

"Watu hawa lazima wauawe usiku huu huu". George alijibu "Kitendo hicho kitawafanya adui wapagawe. na hivyo kutupa sisi nafasi nzuri zaidi kufanya kazi yetu".

"Hali ya ulinzi huko uwanja wa ndege ikoje", aliuliza.

"Ilinzi mkali sana", F.K alijibu. "Na siyo tu kwenye uwanja wa ndege, hali katika mji mzima, wameletwa askari polisi wageni kabisa kutoka mikoa mingine kulinda mkutano. Hivyo ulinzi ni mkali sana.


"Waacheni waonge ulinzi. Jambo hilo lisiwafanye tumbo moto. Ikiwezekana F.K uiambie serikali ya Tanzania ilete jeshi lake zima hapa Arusha na bado cha mtema kuni watakiona tu", Dave alijigamba.

"Paul na Fouche, hiyo ni kazi yenu sitaki Bon na Rocky walione jua litakalochomoza kesho. Mipango yote mnaijua ni kama kawaida", George alisema.

"Hesabu kwamba hiyo kazi imefanyika", Paul alijibu.

"F.K. Nataka unipatie majina ya viongozi wote wa vyama vya wapigania uhuru ambao wameshaingia. Vile vile nataka unipatie majina ya hoteli na vyumba wanakolala. Habari hizi nazitaka leo hii", George alimwagiza F.K.

"Utapata bila matatizo", alijibu F.K.

"Wengine mliobaki nitawaeleza baadaye nini cha kufanya kwa usiku wa leo", George alisema huku akigeuka upande mwingine. Na nyie Paul, Fouche na F.K nataka utekelezaji sahihi kutoka kwenu.

ITAENDELEA
 
HOFU
SURA YA SITA

MAMBO

II

Siku hiyo ilikuwa sikukuu ya Idd-elftri. Mjini Nairobi mchana ule Mike alikuwa ofisini akipokea ripoti kutoka kwa Mwaura.

"Tangu jana mimi na vijana ulionipa tulikuwa tunachunga nyumba hii kwa zamu", Mwaura alisema. "Hata hivyo, hatujagundua kitu chochote. Hakuna mtu hata mmoja ambaye ametoka nje ya nyumba ile. Ila kuna kitu kimoja kinashangaza. Ni kwamba jioni hatumwona Peter akirudi nyumbani. Na Onyango ameniletea habari kuwa amemwona akirudi sasa hivi tunahisi kwamba Peter hakulala nyumbani".

"Unayo hakika hakurudi na kutoka?", Mike aliuliza.

"Labda hiyo iwe wakati tulipokuwa hatujaanza doria wakati wa mchana".

"Hivyo una maana wale watu bado wako ndani?".

"Bila shaka. Labda tu ule muda ambao nilikuja hapa kuwasiliana nawe. Maana kama nilivyokwambia jana, kwa muda ule wa masaa manne hapakuwa na ulinzi", Mwaura alijibu.

"Mike Maina alifikiri sana na kisha akasema. "Sidhani, lakini lazima tuwe na uhakika mtu anaweza kufanya hivyo kama amehisi kuwa tunamfuata".

"Sidhani kama alikuwa ameniona", Mwaura alieleza, "Mimi naelewa kuwa mtu ambaye huchukua tahadhari na mwenye ujuzi kama Peter hawezi kuwa katika hali ile kama alihisi kufuatwa na watu. Bali Onyango aliniambia alipokuwa anarudi leo mchana alionekana kama mtu mwenye wasiwasi kuwa anafuatwa".

"Ndio. Hapa kuna kitu kinanitia wasiwasi sijui ni nini! Mwaura jiweke tayari mnamo saa sita usiku nipitie nyumbani kwangu. Tutakwenda kwa Peter kwani lazima tuhakikishe kuwa mambo gani yanaendelea ndani ya nyumba yake. Waache wale vijana waendelee kufanya kazi", Mike aliagiza.

"Sawa mzee", Mwaura alijibu.

ITAENDELEA
 
HOFU
SURA YA SITA

MAMBO

III

Mnamo saa nne na nusu ndege namba TC 1001 iliwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro. Willy Gamba alikuwa mmoja wa abiria walioteremka. Alijichanganya na kundi la abiria wenzake mpaka akafaulu kutoka nje ya uwanja bila mtu yeyote kumtambua. F.K, Paul na Fouche walikuwa kwenye kundi la wapokeaji wakichunguza watu kwa makini. F.K hakuweza kumtambua Willy. Mawazo ya Paul na Fouche yalikuwa juu ya Bon na Rocky na hata chembe hawakumfikiria Willy, mbali ya kumtambua.

Alipofika nje ya jumba, Willy alikuta madereva taksi wakigombania abiria. Ingawa taksi za kawaida huwa haziruhusiwi uwanjani hapo, siku ile zilijaa tele. Ziliruhusiwa kwa vibali maalum kutokana na haja ya kuhudumia wageni ambao walikuwa ni wengi sana.

"Oh, mzee njoo huku", teksi dereva mmoja aliyemfahamu Willy alimwita huku madereva wengine wakimwandama na kumsihi apande magari yao.

"Oh, Omari, habari za siku nyingia?", Willy alimsalimia.

"Nzuri tu, mzee, ila wewe tu umepotea", Omari alijibu huku akipokea mkoba wa Willy na kuelekea kwenye gari.

"Sababu ya biashara, bwana. Siku hizi imekuwa ngumu", Willy alijibu.

Wakati walipokuwa karibu kuondoka Willy alisita kidogo.

"Hebu subiri kidogo, kuna kitu nimekumbuka", Willy alisema.

Omari ambaye alikuwa ameliwasha, gari alilizima.

Ilikuwa jambo la kawaida kwa Willy kulitumia gari la Omari. Mara nyingine Omari alimwachia gari Willy aendelee yeye mwenyewe kwa malipo fulani.

Baada ya kupanga na kupangana Willy aliamua kuwangojea wenzake ambao wangekuja kwa ndege ya pili.

"Omari, samahani nitakusumbua, kuna mahali ambapo nataka niende lakini nataka niende peke yangu. Je, sijui kama utaniachia gari yako ili nifanye shughuli yangu? wewe unaweza kupanda gari nyingine", Willy alisema "Mambo mengine kama kawaida yetu".

Bila kusita Omari alikubali ombi la Willy, alijua fika kwamba Willy alikuwa kizito na kila alipochukua gari lake kwa shughuli zake kwa muda mfupi, aliweza kulipwa kiasi ambacho angeweza kukifanyia kazi kwa zaidi ya mwezi mzima.
"Bila shaka", Omari alijibu kwa furaha, Petrol imejaa mzee na gari kama kawaida halina matatizo. Ukisha maliza kazi utanipigia simu kunijulisha hata kama ni baada ya juma zima.


"Ahsante", Willy alijibu huku akichukua swichi ya gari.

Omari alimwaga Willy na kuambaa zake.

Omari aliachana na Willy kwenye maegesho ya magari uwanja wa ndege. Katika gari la sita katika safu kutoka alipokuwa Willy. F.K. pamoja na wenzake walikuwa wamekaa ndani. Walifanya hivyo ili kusubiri maadui zao ambao wangefika kwa ndege ya pili.

"Mimi nafikiri niwaache maana hakuna usalama tukionekana pamoja. Nisingependa mambo yetu yagundulike kabla hata kazi yetu hatujaianza", F.K. aliwashauri wenzake.

"Wewe nenda, kazi hii sisi ni saizi yetu, mambo yote tuliyotaka umefanya. Kazi yako umemaliza", Paul alimruhusu.

"Nawatakia bahati njema", F.K aliwaambia huku akiondoka kuelekea kwenye gari lake jingine ambamo Tondo alikuwa anamsubiri.

"Ahsante", PAul alijibu.

Bila kujua, Willy. Paul na Fouche walikuwa wakisubiri wageni wale wale, lakini kwa nia na madhumuni tofauti.

Ndege iliwasili mapema kuliko ilivyotarajiwa. Ilifika saa tano kasoro dakika kumi.

"Ndege hii imewahi kuondoka Dar", Willy alijisemea moyoni huku akiwa tayari kwenda kuwapokea wenzake.

Paul na Fouche walitoka kwenya gari lao mara moja na kwenda kujichanganya tena na wapokeaji wengine waliofika kuwalaki wenzao.

Ndege ilisimama na abiria wakatelemka kama kawaida.

Willy aalikuwa tayari amejigeuza kimawazo na kimazingira kutokana na ujuzi pamoja na uzoefu wa muda mrefu katika kazi hii. Alijibanza katikati ya nguzo moja kama asiyekuwa na hili wala lile. Hata hivyo aliweza kumwona kila mtu aliyetoka nje ya jumba la uwanja kutoka pale aliposimama. Paul na Fouche pia, wakitumia ujuzi wao walijitosa kwenye vurugu la wapokeaji kiasi kwamba hakuna mtu ambaye angewahisi chochote. Hii ilitokana na kwamba wao hawakuwa wazungu peke yao hapo uwanjani. Watu waliotoka kwanza ni wale waliokuwa wanasafiri bila mzigo mikubwa.

Hatmaye Rocky Malele alitokea. Paul alimgonga Fouche begani na wote wakamtambua Rocky. Willy nae alimwona Rocky lakini akaendelea kubana. Rocky aliangaza huku na kule kisha akaamua kupanda Kombi ya shirika la Taifa la Huduma za Kitalii.

"Wakati kama huu wa usiku ni vizuri kupanda gari la watu wengi kwa tahadhari na usalama", Rocky alijisemea.

Kulikuwa na watu wengine ndani ya gari hili lakini lilikuwa bado kujaa. Hivyo iliwabidi kusubiri abiria wengine zaidi. Paul, Fouche na Willy Gamba walimwona Rocky akipanda gari hilo. Ingawa Paul na Fouche hawakujuana na Willy. Wote waliendelea kumsubiri Bon atokee.

Lakini jambo la kushangaza ni kwamba Bon hakutokea. Pande zote mbili zilitarajia kuwa angefika kwa ndege hii. Lakini kwa mshangao mkubwa Bon hakuonekana kamwe.

Willy ambaye alikuwa anachunguza nyendo za hapa kwa makini, aliona wazungu hawa wawili wanaondoka na kuelekea kwenye gari lao. Katika akili yake Willy alifikiri kitu fulani kilichojitokeza kama hakieleweki. Ilikuwa kwamba Willy aliwaona wakati anafika. Na sasa alikuwa amewaona tena Wazungu wale wale. Ilionekana kama kwamba nao pia walikuwa wanasubiri mgeni ambaye hakuwasili kwani wao pia walikuwa wa mwisho.

Pamoja na hayo, Willy alijisemea, "Lakini inawezekana walikuwa wamekuja kuwapokea wageni wao halafu wakakuta hawakuwasili. Hii inawezekana na haina ubaya wowote".

Hata hivyo Willy aliamua kufuatilia nyendo za Wazungu hao. Aliwaangalia wakiingia kwenye gari naye pia aliamua kuingia ndani ya gari lake. Mara gari alilokuwemo Rocky liliondoka.

"Tulifuate gari hilo", Paul alimwambia Fouche ambaye alikuwa anaendesha.

"Itakuwa vigumu kulishambulia gari hili; ingekuwa vizuri kama angekuwa amechukua teksi yeye peke yake", Fouche alieleza.

"Kuna wakati atabaki peke yake. Usiwe na wasiwasi kwani tunayo siku nzima ya kufanya kazi hii", Paul alijibu.

Gari la akina Rocky lilifuatwa na gari moja, halafu lilifuatwa na gari la akina Paul na Fouche. Willy alisubiri gari lingine lifuate ndio naye aweze kujiunga na msafara. Alipotaka kuondoka aligundua kuwa tairi mbili za nyuma hazina upepo!

"Shenzi", Willy alilaani.

ITAENDELEA
 
HOFU
SURA YA SITA

MAMBO

IV

Wakati F.K anawaaga Paul na Fouche ili aende kwenye gari alilokuwa ameegesha Chris Tondo, Chris Tondo alikuwa amemwona Willy Gamba akitoka nje ya uwanja na kumtambua. Vile vile wakati Chris Tondo alipokuwa ofisa wa polisi aliwahi kumfahamu Willy kikazi na kimaisha. Kwa upande mwingine, Willy hakumweka Chris Tondo maanani. Hivyo alikuwa hawezi kumkumbuka.

"Nimemwona Willy Gamba", Tondo alimwambia F.K.

Aliposikia hivyo F.K alishituka kwani alimfahamu Willy kutokana na umaarufu wake kama nilivyokwisha kusimulia.

"Oh, yuko wapi?", liuliza F.K kwa mshangao mkubwa.

"Namwona anangojea ndani ya teksi ile".

"Basi, bila shaka na yeye anawasubiri", F.K alisema.

"Anawasubiri akina nani?", Tondo aliuliza.

Pamoja na mambo yote ambayo Tondo alikuwa anayafanya kwa wizi nzima, F.K alikuwa hajamweleza kinagaubaga operesheni hii ilikuwa ya namna gani. Baada ya kufikiri kwa muda aliona ni vyena amweleze habari zote kwani kumficha Tondo kungeweza kusababisha makosa ambayo yangeweza kuleta hatari kubwa, hasa kwa wakati kama huu.

"Unajua Tondo, wewe nakuchukulia kama ndugu yangu. Ni mtu ambaye nakuamini katika maisha yangu. Hivyo wakati umefika na mimi kukueleza kinaganaga juu ya shughuli yote hii", F.K alimwambia Tondo na kisha akamweleza juu ya operesheni hii kuanzia mwanzo mpaka mwisho, kisha alisema. "Hivyo umefika wakati wa kulipa kisasi dhidi ya serikali ya Tanzania kama ulivyowahi kuahidi. Bila shaka utakuwa upande wetu".

"F.K wewe ni ndugu yangu. Mimi niko pamoja nawe. Naahidi kuwa nitatumia ujuzi wangu wa kipolisi kikamilifu ili nilipize kisasi changu cha kunionea na kunifedhehesha ", Tondo aliahidi.

Hivyo F.K na Tondo walibaki ndani ya gari lao wakimchunguza Willy alikuwa anafanya nini. Wakati ndege ilipwasili na Willy akatoka kuelekea mahali alipojibanza ili kuwaangalia akina Riocky. Tondo aliteleza gizani mpaka kwenye gari la Willy. Hapo hapo alitoa upepo kwenye matairi mawili ya nyuma.

"Nimemweza", Tondo alijigamba huku akirudi kwenye gari.

"Kazi hii itakuwa kubwa", F.K alisema. "Itakuwa ni vita vya kutafutana. Vita kwa akili na ujuzi kwani wapelelezi mashuhuri wa Afrika naona wako hapa. Heri sisi tutangulie tuwape habari wenzetu halafu tujitayaruishe kwa ajili ya mapambano makali. Hapa tulipo hatuna hata silaha yoyote. Kama tunapenda kuiona kesho tumkwepe Willy. Kazi tuliyofanya inatosha kwa leo. Willy anaweza kusubiri mpaka kesho. Waache Paul na Fouche nao wafanye kazi yao. Kesho tutakuwa tayari kumumaliza Willy. Hata yeye mwenyewe ataingiwa na woga baada ya kusikia wenzake wameuawa".

"Nafikiri tungoje tuone kama Willy alikuwa anawasubiri wenzake", Tondo alisema. "Ikiwa ni hivyo itakuwa rahisi kwa Paul na Fouche kuwamaliza wote kwa wakati mmoja".

"Sidhani, hawawezi kusafiri wote pamoja, Tondo", F.K alipinga usemi. "Mimi ni jasusi na mchezo huu naufahamu. Paul na Fouche wanajua sana mchezo huu pia. Hivyo wao waachie, wewe ni mchezaji wa ridhaa. Katika shughuli hii ya kijasusi vizuri kuwaachia wajuzi. Achana na Willy huyo atakuwa nyama yetu kesho".

Tondo aliwasha gari na kujipenyeza kwenye msururu na kuondoka.

Wakati Tondo anatoa upepo kwenye tairi za nyuma za gari la Willy. Lyimo alikuwa sehemu ile. Lyimoa alikuwa mwizi mkubwa. Wizi wake alifanya wa kuvunja magari yaliyoegeshwa na kuiba vitu vilivyomo ndani. Siku ile alikuwa katika pilika zake hapo uwanja wa ndege wa Kilimanjaro, baada ya kusikia magari mengi yangekuwa hapo. Wakati huo Lyimo alikuwa hajabahatisha kitu chochote. Alikuwa amejibanza kwenye gari karibu na lile la Willy. Ndani ya gari lile Lyimoa alikuwa ameona mkoba ambao alikuwa anaunyemelea. Alikuwa anajaribu kufungua mlango wa nyuma. Mara alisikia mtu anasogea karibu na gari lililokuwa jirani. Aliinuka kidogo na kuchungulia. Alimwona mtu anakuja kwa kunyata. Kwanza kabisa Lyimo alifikiri yule alikuwa mwizi mwenzie. Lakini sura yake pamoja na jinsi alivyokuwa ilionyesha kinyume. Aliona huyo mtu anatoa upepo kwenye gari halafu kunyata na kuondoka.

Lyimo aligundua kwamba gari lile lilikuwa teksi ya Omari ambaye anamfahamu sana. Ili kuchunguza vizuri kisa hiki Lyimo alimfuatilia yule mtu na kuona gari alimoingia. Alichukua kalamu yake na kuandika namba za gari hilo kwenye kiganja chake cha mkono. Akitarajia kumweleza Omari kana angetokea. Mara nyingine Omari alikuwa akimsaidia. Safari hii aliona amepata nafasi ya kulipa ukarimu wake angalau kwa ishara hiyo ndogo.

"Mimi ni mwizi", Lyimo alijisemea moyoni. "Ninaiba ili nipate fedha za kunifanya niishi. Lakini watu wengine ni waharibifu tu. Kwa mfano mtu huyu amemsumbua mwenzake bure. Afadhali mara mia angekuwa na nia ya kuiba kitu".

Mshangao wake ulizidi alipoona lile gari linaondoka kuelekea mjini.

ITAENDELEA
 
HOFU
SURA YA SITA

MAMBO

V

Wakati Willy alipokuwa anaangalia matairi, Lyimo alitokea."Habari gani, mzee", Lyimo alimsalimia Willy kwa heshima.

"Nzuri", Willy alijibu huku akimwangalia Lyimo kwa makini. Kisha aliendelea, "Ngoja kidogo".

Willy alisogea mbele na kuandika namba za gari la Wazungu lililokuwa linapita mbele yake halafu akarudi.

"Eh, unasemaje?", Willy alimsaili Lyimo."Mwenye gari hii ni rafiki yangu. Siyo gati la Omarui hili", Lyimo aliuliza.

"Ndio, na mimi ni rafiki yangu. Ameniachia gari hili. Lakini ajabu nimekuta limepata pancha mbili sasa hivi", Willy alijibu.

"Nimeona mtu anatoa upepo ndani ya matairi haya", Lyimo alieleza.

Mara Willy alisikia kengele zinalia kichwani mwake.

"Eh, mtu wa namna gani?", Willy aliuliza kwa shauku kubwa.

"Mtu mmoja nadhifu sana. Mwanzo nilifikiri ni mwizi. Lakini hakuonyesha dalili ya wizi. Aliinama, akatoa upepo na kuondoka. Aliingia kwenye gari ambalo lilikuwa na mtu mwingine ndani halafu wakaondoka zao. Hata hivyo, mimi nilichukua nambari za gari hilo ambayo ni ARKK 567", Lyimo alimwambia Willy huku akisoma kwenye kiganja chake.

Willy alikariri nambari hiyo na kushangaa, kwa kujiona alikuwa na bahati iliyoje.

"Wewe unaitwa nani?", Willy aliuliza

"Naitwa Lyimo".

"Na wewe ni dereva wa teksi?".

"Hapana, mimi ni shanta".

"Shanta maana yake nini?".

"Mimi huwa nawasaidia madereva kama wanao usingizi. Huwa naendesha halafu wao huwa wananilipa chochote", Lyimo aliongopa.

Wakati huo akili ya Willy ilikuwa inafanya kazi haraka haraka. Mara alipata jawabu.

"Ninaweza kupata gari nyingine hapa?".

"Subiri niangalie", Lyimo alijibu na kuondoka.

Punde si punde Lyimo alirudi na kijana mmoja.

"Huyu anaitwa Tarimo, ni rafiki yangu vile vile, hata Omari ni rafiki yake pia", Lyimo aliwajulisha.

"Aah, mimi naitwa Willy. Omari ni rafiki yangu. Kiniachia gari lakini nimepata mkasa".

"Sasa unataka tukusaidie vipi?", Tarimo aliuliza.

"Unayo pampu?".

"Ndio", Tarimo alijibu.

"Nafikiri kama utakubali utanipatia gari lako, mimi nitakulipa shilingi elfu tatu. Weka upepo kwenye gari la Omari halafu tuonane kesho asubuhi huko New Arusha Hoteli. Gari lako utalikuta hapo".

Bila kuchelewa Willy alianza kutoa fedha na kumhesabia Tarimo. Tarimo aliona kama ameangukiwa na ngekewa. Alichukua fedha na huku Lyimo akibeba mizigo ya Willy, wakielekea kwenye gari.

"Lyimo umenisaidia sana. Chukua hizi shilingi tano ukanywe angalau bia moja", Willy alimwambia Lyimo.

"Lo! ahsante sana. Leo siku nzima nilikuwa sijapata kitu. Mungu akuongezee.

"Amina", Willy alijibu huku akifikiria namna Lyimo alivyokuwa amemsaidia bila kujua.

"Kesho asubuhi", Tarimo alisema.

"Kesho asubuhi", Willy alijibu na kuondoka.

"Sasa ni lazima niyakamate yale magari", Willy alijisemea moyoni.

Gari la Tarimo lilikuwa aina ya Peugeot 404 lenye umri kidogo. Lakini lilikuwa na nguvu ya kutosha. Tangu yale magari yaondoke ilishapita muda wa dakika kumi na tano. Willy alilipamba moto na kuendesha kwa mwendo mkali sana. Wakati akiendesha Willy alifikiri mambo yote haya. Na ajabu zaidi, Willy alimfikilia Bon Sipele ambaye alikuwa hakuonekana hapo uwanja wa ndege.

ITAENDELEA
 
HOFU
MAMBO

VI

Karibu na mpakani, katikati ya sehemu ya Tengeru, nje ya mji wa Arusha. Willy aliyafikia magari yaliyokuwa yametangulia. Alilipita gari moja ndipo akaliona lile lililokuwa linaendeshwa na wazungu. Vile vile aliona ile Kombi iliyombeba Rocky. Hivyo aliamua kubana nyuma ya magari hayo.

Kituo cha kwanza cha ile kombi kilikuwa Saba Saba Hoteli. Rocky alikuwa amemwambia Willy kuwa angefikia Equator Hoteli. Alipofika Sabasaba Hoteli na kuona ile kombi pamoja na gari la wazungu vikiongoza kwenda hoteli hiyo, yeye Willy aliamua kwenda moja kwa moja akabane Equator Hoteli. Alifanya hivyo ili akaone kama alivyofikiri ilikuwa kweli. Akiliwa ameegesha gari katikati ya magari mengine karibu na Safari Hoteli, aliona ile kombi inasimama pale Equator Hoteli. Watu watatu wakiwa na mizigo walitelemka. Rocky alikuwa mmoja wapo punde si punde, Willy aliona gari lile la wazungu linaegeshwa karibu na Hoteli hiyo hiyo. Lakini kwa upande mwingine wa barabara.

Mzungu mmoja aliondoka na kuelekea huko Hotelini. Willy alisubiri. Baada ya kama dakika kumi hivi, yule Mzungu alirudi na kuingia ndani ya gari. Willy aliendelea kusubiri. Alipoangalia saa yake ilisema saa sita usiku.

Ilipofika saa saba usiku Paul alimwambia Fouche, "Sasa twende, mimi nitapita kwa nje wewe utapita kwa ndani. Kama nilivyokueleza, chumba chake kiko kwenye pembe ya kulia. Huwezi kukikosa kwani ni moja kwa moja. Mimi nitaingilia dirisha la bafuni ambalo ni kubwa la kutosha. Bila shaka atakuwa amelala".

Waliondoka ndani ya gari na kutokomea gizani, Willy naye aliondoka kwenye gari baada ya kuwaona wanafanya hivyo. Alifanya hima kuelekea kwenye kijumba cha simu kando ya barabara. Alipiga simu Equator Hoteli kwani aliyokuwa anatuhumu yajidhihirisha kuwa ni kweli.

"Hallo, Equator Hotel?", simu iliitika.

"Nipe mapokezi", Willy aliomba.

"Mapokezi hapa", Willy alijibiwa baada ya muda kitambo.

"Rocky Malele yupo chumba gani?", Willy aliuliza.

"205".

"Nipe nizungumze naye".

Baada ya muda kidogo, sauti ya Rocky ilisikika.

"Hallo, Rocky hapa".

"Willy hapa", Willy aliitika na kisha aliendelea, "Chunga tai wawili wanataka kula nyama yako sasa hivi".

"Chunga", Rocky aliitikia huku akiweka simu chini.

Aliamka haraka kutoka kitandani na kuchukua bastola yake kutoka chini ya mto. Aliikagua.

Willy naye alitoka kwenye kibanda cha simu, akaigusa kwa chati bastola yake huku akimwemwesa.

ITAENDELEA
 
HOFU

MAMBO

VII

Ilikuwa saa saba za usiku. Mjini Nairobi Maina na Mwaura walipanda ua na kuingia ndani ya uwanja wa jumba hili la kifahari la Peter Gerrit. Waliangaza na kumwona mlinzi aliyekuwa bado amekaa kwenye kijumba chake huku akisinzia sinzia. Walizunguka nyumba kwa uangalifu mkubwa ili waweze kupata mahali pazuri pa kuingilia.

"Wewe zungukia kulia na mimi nizungukie kushoto, kisha tukutane mbele", Maina alimweleza Mwaura. "Jaribu kuangalia mahali pazuri pa kuingilia".

"Sawa, Mzee".

Walipokutana, Mwaura alimwambia Maina. "Kuna mlango pembeni. Nafikiri unatokea jikoni. Unaonaje tukiingilia huko?".

"Funguo zako unazo?".

"Ndio".

"Na! kufuli ni la aina gani?".

"Ni la kawaida. Nitafungua, hamna taabu", alijibu Mwaura.

Huku kila mtu akiwa ameweka bastola yake tayari, walifungua mlango huo. Mara walijikuta wako jikoni. Wafungua na kujikuta kwenye chumba kikubwa. Walihisi hicho kilikuwa chumba cha chakula. Kwani humo ndani kulikuwemo meza kubwa iliyozungukwa na viti visivyopungua kumi na nane. Wakifanya tahadhali kubwa, walisonga mbele . Walikwenda wakiangalia chumba hadi chumba. Jumba lenyewe lilikuwa kubwa kiasi cha mtu kuweza kupotea.

"Shiii!", Maina alimtahadhalisha Mwaura.

Alifanya hivyo kwa sababu alikuwa amesikia kitu kama mashine ya teleksi inalia kutoka kwenye chumba alichokuwa amekitazama. Huku akimuonyesha ishara abaki nyuma ili aweze kumsaidia iwapo ingetokea shida yoyote, Maina alifungua mlango ule. Mle chumbani hakukuwa na kitu, lakini bado alisikia mlio wa mashine ukizidi. Aliangaza huku na kule ndipo, kutokana na uzoefu wa kazi yake wa siku nyingi, alipouona mlango aliokuwa akiutafuta. Alibonyeza kifungo hapo ukutani na mlango ule ukafunguka. Mwaura alichungulia huku moyo wake ukipiga haraka haraka. Mara alimwona Maina anamuonyesha ishara ya kumfuata baada ya muda mfupi. Aliingia ndani na kuurudisha mlango.

Alikuta ngazi zinazoelekea chini ambazo alizifuata. Sasa alikuwa na hakika kabisa ndani ya jumba hili kulikuwamo makubwa. Alichunguza bastola yake ya kawaida na ile ya akiba. akajiweka tayari wakati akizidi kutelemka chini.

Aliufikia mlango mwingine. Huku ameweka bastola yake tayari, aliufungua. Hapo alijikuta kwenye ukumbi mkubwa uliomuonyesha kuwa alikuwa kwenye sehemu za maofisi. Alitega tena masikio yake vizuri. Ndipo alipogundua ni chumba gani ambacho mlio wa mashine ulikuwa ukitokea.

Aliangaza huku na kule na kusikia kimya, alianza kufungua ule mlango. Kwanza alifungua kidogo kiasi cha kuweza kuangalia ndani. Aliona Wazungu watatu wakiangalia mashine kubwa ya komputa ikileta habari. Wawili walikuwa wamesimama na yule aliyekaa Maina alimtambua kuwa ni Peter Gerrit. Aliweza kumtambua kwani waliwahi kuonana wakati wa upelelezi kuhusu mauaji yaliyotokea katika Visiwa vya Shelisheli.

Alirudisha mlango kidogo, akafikiri, halafu akaufungua ghafla na kwa nguvu.

"Hapo hapo mlipo!", Maina aliamru kwa sauti kali. "Mtu akileta ushenzi amekufa!. Mikono juu!.

Waligeuka na bila kubisha wakainua mikono juu. Bila kupoteza wakati. Maina alisoma maandishi yaliyokuwa kwenye ile mashine:

"LAZIMA UTUONGEZEE WATU MAANA HATUTAKI KUSHINDWA IKIWA HATA HUYU GAMBA YUKO HAPA HAPA JIBU".

Ghafla maandishi yalifutika.

"Peter, jibu", Maina alimwambia Peter.

"Nijibu nini".

Wakati huo Maina alikuwa tayari amewafikia na kuwapekuwa ili kuhakikisha kama walikuwa na silaha. Alikuta wale Wazungu wengine wanazo bastola ambazo aliwanyang'anya na kuzitupa kando.

"Maina mbona unanifuata fuata. Kazi inaitaka ama huitaki".

"Naitaka Peter, na safari hii huwezi kunipo...".

Ghafla chumba kikawa giza Maina alijirusha kutoka aliposimama na kuanguka kando. Wakati huo huo risasi zikamiminika pale alipokuwa amesimama. Naye alijibu mapigo huku akijiviringisha chini.

"Oh, nakufa", sauti ya mtu ilisikika.

Watu waliobaki walifungua mlango na kukimbia nje. Huko alisikia risasi zinalia na akajua Mwaura alikuwa kazini.

Aliinuka haraka na kufungua mlango wa ukumbini alikuta maiti nyingine mbili. Aliamua kuelekea sehemu aliyosikia mlio wa risasi. Mwaura alikuwa amefanya kazi kubwa. Mara aliona maiti nyingine moja. Mambo yalikuwa yanakwenda haraka. Kumbe sehemu hiyo pia kulikuwa na ngazi nyingine. Maina alizifuata ngazi hizo. Mwisho wa ngazi chini alimkuta Mwaura ameanguka chini baada ya kupigwa risasi ya kifua.

"Bosi, wamebaki wawili tu, wawahi, Mwaura alisema kwa maumivu.

"Mwaura! Mwaura!", Maina aliita kwa uchungu. Mwaura aligeuza macho na kumtazama Maina, kiasi akakata roho.

Machozi yakamtililika Maina.

"Umekufa kishujaa, Mwaura, mimi nitakulipizia kisasi. Natoa ahadi.

Kwa haraka alikimbia kumfuata Peter lakini alikuwa amechelewa. Kwani alisikia gari linawashwa na kuondoka. Kwa kasi.

Alirudi ukumbini ambamo kuliwa na simu. Alimpigia Mkurugenzi wa Upelelezi nyumbani kwake.

"Ni nani...?", Mkurugenzi aliuliza kwa sauti ya kulalamika. Lakini maelezo ya Maina yalifuta mawazo yake.

"Peter amekimbia. Mwaura ameuawa katika mapambano. Majasusi sita wameuawa. Maiti zote ziko hapa nyumbani. Naomba Polisi wafike haraka ili waweze kuchukua ushahidi ambao ni mkubwa na wa uwazi. Vile vile viwekwe vizuizi kwenye barabara zinazotoka mjini hapa. Wasiliana na wenzako huko Tanzania. Nataka kujua Willy Gamba yuko wapi".

"Sawasawa. Tuonane ofisini saa kumu na mbili. Nafikiri hapa kuna kazi kubwa", Mkurugenzi alijibu.

"Kwaheri, mzee", Maina alijibu halafu akaweka simu chini na kuondoka.


ITAENDELEA
 
HOFU
MAMBO

VIII

Fouche alikwenda katika sehemu ya mapokezi ya Equator Hoteli. Mhudumu wa mapokezi alikuwa akisinzia sinzia pale kwenye kiti.

Aliangalia kwenye bodi ya funguo na bila kusita akamwambia mhudumu. "Chumba mia mbili na ishirini".

Yule kijana bila hata kugutuka alichukua funguo. akampatia na kuendelea kustambari.

Fouche alipanda mpaka ghorofa ya pili na kwa tahadhali kubwa alielekea chumba namba 205.

Paul alizunguka na kuuangalia ukuta. Alivaa mifuko yake ya mikono. Mifuko hiyo ilikuwa ya aina yake, kwani iliweza kushika ukutani kama sumaku. Hivyo ilimwezesha kupanda ukuta bila matatizo. Aliangalia saa yake halafu akaanza kukwea.

Baada ya Rocky kupata simu ya Willy, aliyomtahadharisha, alitengeneza kitanda chake vizuri. Alikunja Blanketi na kuifunika na shuka mpaka ikaonekana kama mtu aliyelala. Baada ya kufanya hivyo, alibana mahali na kusubiri.

Akiwa katika hali ya kunyata. Willy alijipenyeza kwenye njia kati ya Equator Hoteli na Jengo la posta kwa upande wa kulia. Kwa haraka akamuoana mtu anaelekea kwenye ukuta. Mara akahisi ni nani. Aliendelea kunyata haraka haraka mpaka akafikia usawa wa mtu yule ambaye sasa alikuwa amekaribia kushika dirisha.

"Shiii", Willy alitoa sauti ya kustua mtu.

Paul aligeuka kumtazama mtu aliyetoa sauti hiyo. Kutokana na mwanga wa mbalamwezi. Paul alijikuta anatama kwenye mdomo wa bastola.

Willy alimwamru atelemke. Vinginevyo angemkita risasi ya matako. Kufumba na kufumbua, Paul alifyatuka kama risasi na kumwangukia Willy. Willy alipiga risasi ambayo ilimkosa Paul na wote wakaanguka chini. Bastola ya Willy ilidondoka umbali wa kama futi sita kutoka mahali walipokuwa. Hapo ndipo vita vya ana kwa ana vilipoanza. Willy alitaka kupiga mbio kuelekea kwenye bastola. Lakini Paul aliwahi kumrukia kwa pale pale chini. Hata hivyo, Willy alimpiga teke-farasi na Paul akaanguka upande mwingine lakini akaamuka mara. Hapo ndipo walipogundua kuwa walikuwa wamekutana wajuzi watupu.

Hapo mwanzo Paul alikuwa amefikiri huyu alikuwa askari wa kawaida, lakini sasa alikuwa na mawazo tofauti. Kupambana naye bila kutumia silaha isingewezekan. Alijaribu kutoa bastola yake iliyokuwa kwenye mkoba wake chini ya kwapa. Lakini Willy aligundua janja yake. Alimwahi kipigo cha karate kilichomfanya Paul aone nyota. Pale pale Paul alitoa mapigo manne ya karate haraka haraka. Lakini Willy aliyaona. Willy alimgeuzia Paul na kumpiga teke la kinena lililomwangusha chini. Alimrukia ili amumalize kabisa. Lakini Paul alijiviringisha kando na Willy akamkosa.

Lakini alijiviringisha tena kabla ya kutua na kumwahi Paul ambaye wakati huo alikuwa amechomoa bastola. Aliipiga teke ile bastola nayo ikafyatuka wakati ikitoka mikononi mwa Paul. Teke lile lile lilikuwa limevunja mkono wa Paul wa kulia. Paul aliamka ili akimbie, lakini Willy alimwahi kwa kumpiga ngwara. Alipoanguka chini Willy alimpiga Paul teke ambalo lilimvunja mbavu kama tatu hivi za upande wa kulia na hapo hapo moto ukamwishia. Akabaki kugwaya.

"Nyinyi ni nani?", Willy alimwuliza Paul, huku amembana pale chini asiweze kufurukuta.

"Sisi ni Wazungu", Paul alijibu kwa jeuri maana alijua huo ndio mwisho wa maisha yake, haraka sana alifikiri jinsi alivyokwisha waweka watu wengine katika hali kama aliyokuwemo kwa sasa hivi. Kwa mara ya kwanza kati maisha yake alijiwa na woga na hali ya kuogopa kifo. Hata hivyo alijuwa huo ndio ulikuwa mwisho wake kwani hapakuwa na ujanja wa kuokoka.

"Wenzako wako wapi?", Willy aliuliza kana kwamba alikuwa akijua.

"Niko peke yangu tu", Paul alijibu huku akisikia maumivu makali kutoka mbavuni.

"Aah, kumbe bado unafanya mchezo", Willy alitishia.

"Kama ni kuniua si uniue tu?, unataka nini zaidi", Paul alimuuliza Willy.

"Kwanza ujibu maswali yangu, vinginevyo bado unayo safari ndefu ya kwenda ".

"Hutapata jibu hata chembe, unapoteza muda wako".

"Basi, kama wewe ni Kaburu leo umefika kwa wazalendo wa Afrika. Utakiona cha mtema kuni. Kama hutaki kifo chako kisiwe cha maumivu makali bora uanze kusema", Willy alimwambia huku akigandamiza mbavu za Paul zilizovunjika.

Paul alisikia maumivu makali ambayo alikuwa hajawahi kusikia. Lakini pamoja na uchungu wote ilikuwa ni sheria ya 'KULFUT' kwamba hakuna askari wake kutoa siri bali kutafuta njia ya kujiua ili kupunguza muda wa mateso.

"Sema wenzako wako wapi, Kaburi wee", Willy alimuuliza huku akizidi kumbana mbavu kwa kukandamiza mkono wake.

Mara alishitukia Paul anatoa ulimi wake nje ghafla halafu akaukata kwa meno yake kama mkasi.

"Shenzi mkubwa we!", Willy alitukana.

Kaburu alikuwa ameamua kujiua kwa njia ya ajabu sana.

"Kweli tunayo kazi maana Majasusi hawa wa Makaburu siyo watu wa kawaida", Willy alijisemea moyoni.

Fouche aliendelea kuziparamia ngazi kana kwamba naye alikuwa mgeni aliyefikia chumba namba 205, aliangaza huku na kule, halafu akatoa bastola yake na kujiweka tayari. Kama ilivyo desturi, bastola yake ilikuwa na kizibo cha kuzuia sauti. Alichukua funguo zake malaya akafungua kufuri la mlango.

Rocky, ambaye alikuwa ndani amezima taa lakini akiwa amevuta pazia kuacha mwanga wa mbalamwezi uingie kidogo, alisikia kwa mbali kufuli likifunguliwa. Hivyo alijiweka tayari.

Fouche alikuwa amelidhika kwamba kufuri halikupiga kelele. Hivyo alishika komeo. Kwa kasi ya umeme. Fouche alifungua mlango na moja kwa moja akamimina risasi kama kumi pale kitandani. Halafu aliingia chumbani na kuwasha taa huku akiangaza kitandani.

"Umefanya kazi nzuri", Rocky alisema kwa sauti ya kebehi.

Fouche aligeukia kule sauti ilikokuwa inatokea na pale pale akawa amegundua jinsi alivyokuwa amedanganywa. Alijuwa mambo yamekuwa mambo. Hivyo alifyatua risasi lakini Rocky alikuwa tayari amekaa imara. Alimpiga Fouche risasi moja ya kifua akaanguka chini. Alipomkaribia alimkuta kawa maiti tayari.

"Mara Rocky akasikia kitu kinadondoka bafuni. Aliruka ili azime taa. Hapo hapo mlango wa bafuni ukafunguliwa kama radi kabla hajazima taa. Huku bastola zikiwa zimeelekezana. Alishangaa kumwona Willy.

"Chunga sana. Willy", Rocky alisema. "Siku nyingine unaweza kuumia.

"Mimi nafikiri wewe chunga zaidi; ongeza kasi", Willy alijibu.

Wote wakacheka.

"Umempiga sachi ?", Willy aliuliza huku akiangalia maiti ya Fouche.

"Zaidi ya hii bastola yake", Rocky alijibu. "Hana kitu kingine".

"Hata yule wa nje hana kitu", Willy aliongeza Rocky alielewa mara moja.

"Hivi ulijuaje nia ya watu hawa?", "Kama si wewe Willy, mimi ningekuwa maiti hivi sasa.

"Hiyo ndio faida ya kuwa wengi", Willy alisema. "Hebu chukua vitu vyako tuondoke hapa. Nitakueleza zaidi huko njiani".

Waliondoka chumbani humo kwa kupitia dirishani.

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA SABA

ARUSHA

Ilikuwa saa moja asubuhi wakati F.K alipoegesha gari lake. Huku nusu akitembea nusu akikimbia , aliingia nyumbani. Majasusi wote walikuwa wanamsubiri kwa hamu.

"Eh imekuwaje?", George aliuliza.

"Paul na Fouche wameuawa!", F.K alijibu.

"Nini?", Dave aliuliza kwa ghadhabu.

"Wamekufa", F.K alieleza. "Polisi wanasema maiti zao zimekutwa Equator Hotel. Sasa hivi Polisi wanafanya upelelezi kwani watu hawa hawana rekodi kuhusu kuwa kwao nchini. Zaidi ya hayo, hakuna jibu lolote kutoka kwa Peter Gerrit, sijui kumetokea nini!".

"Mungu wangu, maana hata Peter ameuawa?", Dave aliuliza.

"Sijui, lakini hakuna jibu. Hivyo wanahisi kuna kitu kimetokea".

"Oke, sasa kazi imeanza. Katika mchezo huu mambo kama haya sharti yatokee. Hivi Bon na wenzake wametupiku. Sasa ni zamu yetu kufunga kazi; F.K kazi yetu ya usiku wameisha izungumzia? George aliuliza.

"Kati ya wale watu wawili ni ofisa mmoja wa wapigania uhuru ambaye ameuawa. Yule wa sabasaba Hoteli alikuwa mfanyabiashara. Kwa hiyo hicho chumba kimekosewa", F.K alijibu kwa sauti ya uwoga.

"Nafikiri ni lazima uifanye kazi yako vizuri, F.K sharti ulete habari sahihi maana kazi kubwa iko leo usiku. Kusema kweli kama mtafanya mchezo mtateketea nyote. nyinyi wenyewe mmeona jinsi Paul na Fouche walivyoangamia. Inatubidi kujidhatiti na kufunga kazi haraka. Jambo moja lazima niwahakikishie; hakuna kushindwa, sawa?", George alisema kwa ukali.

"Sawa", wote walijibu kwa pamoja.

"Oke, tuendelee na maelezo kuhusu mipango ya mashambulizi ya siku nzima", George alishauri.

Wote walisogea ili kila mmoja wao ajue kazi yake na jinsi ya kuitekeleza.

ITAENDELEA
 
HOFU
ARUSHA
II

Saa tatu juu ya alama Bon Sipele alibisha hodi kwenye chumba cha Willy, huko New Arusha Hotel, kama walivyokuwa wamepanga jana yake.

"Hakllo vipi", Bon alimsalimia. Rocky alikuwa amejilaza kitandani.

"Wewe ni mchawi nini?, ulipotelea wapi?", Willy aliuliza.

"Wewe mwenyewe unajuwa kwamba kujibadilisha kama kinyonga na kuwapotea watu ndio mchezo wangu", Bon alijibu kwa mzaha.

"Hivi ulipita pale pale? Sidhani. Hata mimi nisikutambue?", Willy aliuliza kwa mshangao.

"Mimi nilikuona umejibanza kwenye nguzo. Nikakurushia busu la uzima halafu nikawahi kwenda kulala ili leo niamke safi", Bon alijibu.

"Si kitu. SItaki kujua ulitoka vipi", Willy alisema. "Inatosha kukuona mzima kwani tulikuwa na wasiwasi huenda umetekwa nyara. Huo ukinyonga wako uweke iwe siri yako, kwani huenda utakufaa baadaye. Maana kusema kweli ulitupotea kishenzi. Hapo hata mimi nimevua kofia".

"Eh, vipi, mbona kama kwamba nyinyi nyote mmelala humu maana naliona sanduku la Rocky Equator Hoteli ilijaa", Bon aliuliza.

"Ilijaa?", Rocky alidakia, "Hebu Willy mpashe kabla hajauliza mengi".

"Sisi bado hatujalala kama wewe. Mpaka sasa lazima ujuwe kwamba majasusi wameshaingia hapa. Zaidi ya hayo, jana usiku tumepambana nao!", Willy alianza kumweleza yote yaliyotokea usiku ule.

Bon alisikiliza kwa mshangao mkubwa.

ITAENDELEA
 
Back
Top Bottom