Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,280
- 15,717
Mkutano huo umeanza kwa kikao cha ngazi ya Wataalamu kitakachofanyika kuanzia Mei 29 hadi Juni 1, 2026, nakufuatiwa na Makatibu Wakuu kinachotarajiwa kufanyika Juni 2 hadi 3, 2026, kabla ya kuhitimishwa na Mkutano wa Mawaziri utakaofanyika Juni 4, 2026.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Mkurugenzi wa Forodha katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bi. Flavia Busingye, amewataka wataalamu hao kujikita katika majadiliano yatakayotoa suluhisho la kudumu kwa changamoto zinazoathiri ukuaji wa biashara ndani ya Jumuiya.
Kupitia mkutano huo wa SCTIFI, Jumuiya inalenga kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi, kuimarisha mazingira ya uwekezaji, kukuza biashara ya mipakani, kuondoa vikwazo vya biashara na kuchochea maendeleo ya viwanda katika Nchi Wanachama.
Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo ngazi ya Wataalamu unaongozwa na Mkurugenzi wa Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Benjamini Mwesiga, akiwa ameambata na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mikakati na Siasa za Ulimwengu katika Wizara hiyo, Balozi Thobias Makoba, pamoja na maafisa wengine waandamizi wa Serikali.