Riwaya: Hatia

Riwaya: Hatia

Hao watoto watarajiwa ndio kizungumkuti.
Joy ampoteze baba mtoto awe na Michael?

Michael amuache Martha na mwanae awe na Joy?

Michael yupo kati
 
duuuuhh....kila nikiwaza mwisho sielewi..nahic kama ndo inaaza...
 
RIWAYA: HATIA
MTUNZI: George Iron Mosenya

SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA


Defao alipagawa kumkuta Joyce akiwa bado ana mimba aliyompatia. Hali hiyo ikamfanya kuisahau kabisa ile pesa waliyoikuta pale ndani.
Joyce naye akasahau kisasi. Wawili hawa wakawa kitu kimoja. Defao akahamishia makazi katika chumba cha Joyce. Kile kitoto ndani ya tumbo la Joyce kikaleta pendo jipya.
Japo mimba ilipatikana kwa kitendo cha ubakaji lakini mimba ilibakia kuwa mimba.

Jiji la Mwanza halikuwa na usalama wowote kwa wawili hawa. Baada ya kuwa wamesimuliana kila mmoja nini kimemsibu sasa waliamua kwa sauti moja kutoweka katika jiji hilo. Jiji lililobadilisha historia ya kila mmoja.
Mpango ukasukwa usiku huohuo. Na kesho yake wakaongozana kuelekea stendi kukata tiketi.
Nyegezi!!! ni huku waliweza kuonwa na Michael bila wao kujua.
Michael akawa amemuona Matha.


****

John Mapulu aliiendesha gari kwa kasi sana kama inavyokuwa wakati wa matukio ya uhalifu hasahasa wa kuiba magari ama kuiba kwa kutumia silaha. Kichwani na moyoni mwake alikiri kuwa alikuwa amekufa na kuoza kwa penzi la Matha. Na alihisi kiasi fulani umuhimu wa Joyce Keto ukipungua kadri anavyozidi kumweka Matha kichwani.
Tayari alikuwa amewapa taarifa washirika wenzake. Arusha mjini alikuwa ameweka watu wawili maalum kukagua kila gari linaloingia kutokea jijini Mwanza. Naye alikuwa katika mwendo kasi kuwahi jijini Arusha, jina la Adrian lilikuwa likimtia kero kila alipofikiria. Kumuua Stallone haukuwa mwisho wa mapambano!!!

Wakati Michael anajaribu kumpigia ili kumtaarifu juu ya alichokiona tayari alikuwa eneo lisilokuwa na mtandao.
Michael akakata tamaa nakuhisi bahati ile huenda isijirudie tena.
Maamuzi binafsi!!! Michael akaamua.

Kwa jinsi yule mwanaume alivyokuwa amejiweka jirani sana na Joyce huku akiwa amemshika mkono Michael alisoma kitu fulani wa oyce.
Hofu!! Joyce alikuwa katika hofu kuu. Michael akaamini kuwa hakuwa katika mikono salama.
Nguo alizokuwa amevaa yule mwanaume waliyekuwanaye nazo zilimtia mashaka.
Mtekaji!!! Alijiwekea hisia hizo kicwani mwake.
Akachukua tahadhari katika kukabiliana na suala hili. Akawa makini Joyce asiweze kumuona. Kwani akimuona lazima atafanya tafrani ambazo zinaweza kuzua mengine ambayo hakutaka yatokee.
Wawili wale wakaifikia taksi moja wakapanda. Michael ambaye alikuwa ameanza kuiva kimbinu na ye akasubiri sekunde kadhaa akachukua teksi nyingine.
"Ifuate taksi hiyo inayokata kona." Michael alimwamuru dereva. Akatii amri.
"Hakikisha hajui kama tunamfuatilia."
Safari ikaanza!! Michael alikuwa makini kabisa, zaidi ya dereva aliyekuwa anaongoza chombo. Hakutaka kuipoteza hata kidogo ile taksi.


Mwendo wa dakika kama kumi ile teksi aliyokuwa amepanda Joyce na Defao ilisimama katika geti la hoteli. Defao alikuwa wa kwanza kushuka, kisha akamfungulia Joyce mlango naye akashuka.
Bado Joyce hakuonekana kuwa na amani. Jambo hili lilizidi kumuweka Michael ambaye muda tu naye alikuwa ameshuka katika taksi aliyokuja nayo. Michael kwa tahadhari zaidi alizidi kufuatilia nyendo za wawili hawa na sasa walichukua funguo kutoka mapokezi wakaanza kupanda ngazi kuelekea juu.
Kosa lililofanywa na muhudumu wa pale mapokezi, kuinama lilikuwa faida kwa Michael ambaye alipenya kama upepo na sasa alikuwa katika korido akiwafuatilia wawili hawa.
Chumba walichoingia Michael akakikariri vyema. Hakutaka kupoteza muda. Akatazama huku na huko kisha akaitoa bastola yake mafichoni. Na kama alivyofundishwa akaweka kiwambo cha kuzuia sauti. Sasa akakiendea kile chumba.
Bunduki mkononi!! Tayari kwa lolote.
Akaufikia mlango akaugonga? Kimya?
Kwa mbali akasikia sauti za kunong;onezana. Kisha hatua kwa hatua hatimaye zikasikika hatua zikikoma.
Kitasa kikashushwa mlango ukafunguka!!
Michael alikuwa anasubiri kitendo hicho!! Akausukuma ule mlango kwa kutumia goti lake. Aliyekuwa anauzuia akapinduka na kusalimiana na ardhi. Michael bunduki mkononi. Akamuelekezea Defao. Kimya kikatanda. Joyce hakuwepo!!
Kabla Michael hajaulizia mlango wa bafuni ulifunguliwa. Joyce Keto ana kwa ana na Michael.
"Mai....Mai..Michael.." aliita akionyesha kutoamini anachokiona.
"Huyu ----- ni nani na anataka nini kwako?." Michael alimuuliza kabla ya kuitikia.
"Ni..Defao....Defao..."
"Ni nani?." Michael alizidi kuwaka akiwa bado amemuelekezea bastola Defao. Defao alikuwa amenyanyua mikono juu.
Joyce alijielezea kwa kifupi huku akimtoa Defao hatiani. Michael akayaamini maneno ya Joyce. Mara watatu hawa wakawa kitu kimoja. Japo Michael aliweka tahadhari kubwa sana katika kila dakika. Hakutaka kumwamini Defao kwa asilimia zote.
Na mara kwa mara alimvuta Joyce pembeni na kuzungumza naye mawili matatu. Swali kubwa kichwani mwa Michael ambalo hakutaka kuliuliza ni juu ya tumbo la Joyce. Lilimtia katika hofu na wivu.
Nani amempa mimba? Hilo lilikuwa swali.
Lakini haukuwa wakati muafaka wa kuliuliza.
Jioni watatu hawa walizunguka mjini kidogo kwenda kupata chakula.
Michael akiwa ameambatana na Joyce huku Defao akiwa amebaki nyuma kidogo. Joyce na Michael hawakujua nini kinaendelea. Hadi walipojikuta kwa pamoja wanageuka nyuma kutazama umbali waliomuacha Defao.
Joyce hakuweka mashaka yoyote lakini Michael kwa sekunde kadhaa tu huku akitumia ubongo wa John Mapulu alimg'amua kuwa Defao alikuwa mikononi mwa polisi.
Akamsihi Joyce wakakaza mwendo!! Wakakifikia kiuchochoro na kujibanza huku wakishuhudia tukio la Defao akifungwa pingu.
John Mapulu ana akili sana huyu jamaa!! Michael alikiri kimoyomoyo baada ya mafunzo aliyopewa na John kufanya kazi yake ipasavyo!!!
Wakatoweka na hawakurejea tena katika hoteli ile. Michael aliendelea kuutumia ubongo wa John Mapulu.


****

Steven Marashi, alikuwa mpelelezi pekee aliyeamua kufanya kazi ya kujitolea nje ya malipo ya kiofisi. Alikuwa akiupenda sana upelelezi na ilikuwa furaha kubwa kwake akikabidhiwa kesi afanyie upelelezi.
Suala la Defao kukamatwa kwa tuhuma za mauaji kisha kuachia katika namna dhaifu kulimshangaza sana kijana huyu, japo kwa hakika Defao alionekana kuwa hana uwezo wa kufanya mauaji na hapakuwa na alama za vidole vyake katika bunduki zilizokutwa eneo la tukio. Bado Steve hakuridhika. Akaamua kufanya upelelezi wa kimya kimya. Alizifuatilia nyendo za Defao hadi siku aliyorejea pale hotelini na kuulizia chumba namba kumi na nane. Alikuwa ni Steve pia katika harakati za defao kutafuta mahali pa kuiuza simu yake kisha akarejea katika hoteli ile tena.
"Ana nini huyu bwana...anauza simu kisha anarejea kupanga katika hoteli ya bei juu kiasi hicho? Lazima kuna kitu." Marashi alijisemea huku akiufurahia upelelezi huu wa kimya kimya ambao aliamini kuwa una manufaa ama una siri nyuma yake.
Defao aliingia peke yake katika hoteli ile. Lakini siku ya pili anatoka na mtu mle ndani.
Marashi akawahi kwenda kuuliza mapokezi. Muhudumu akataka kuleta ugumu kutoa siri za wateja. Akaonyeshwa kitambulisho cha kazi ya muulizaji. Akalainika akamtaja huyo dada kuwa alikuwa chumba namba kumi nane.
"Je ni mara ya ngapi huyu mgeni kupanga katika hoteli yenu."
"Mara ya kwanza...aah!! labda kama alihudumiwa na mwenzangu siku nyingine..lakini mimi ni mara ya kwanza."
"Siku ya kwanza aliulizia chumba namba kumi na nane unakumbuka?"
"Ndio nakumbuka."
"Sasa inakuwaje unasema ni mara yake ya kwanza kupanga katika hoteli yenu?" akakoroma Marashi, muhudumu akakosa cha kujibu huku uso wake ukitawaliwa na hatia ya kutotunza kumbukumbu vizuri.
"Na je? Mmoja kati yao amewahi kupata ugeni wowote?" alihoji kwa utulivu akiwa amemkazia macho muhudumu.
"Hapana afande."
"Mpuuzi sana wewe na mbona wametoka wakiwa watatau wakati chumba walipanga wawili?" muhudumu kimyaa!!

"Ok! Anaitwa nani?" Marashi aliuliza
"Yupi huyu wa kike au mwanaume?"
"Wote!!"
Muhudumu akajikita katika uchambuzi wa majina kwa dakika chache.
"Juliana na Said Ndulla" aliyataja majina kwa utulivu.
Mshenzi anabadili majina!!! Alishtuka Marashi.
"Naomba kutembelea vyumba vyao. Utakuwa shahidi hii ni dharula kwa usalama wa wote." Muhudumu hakupinga akamwongoza Marashi hai chumba namba 25, huku hapakuwa na lolote. Lakini chumba namba 18, kilipatikana kile kilichopoteza muda wa Marashi kufuatilia. Bunduki!!
Hatia ikamuangukia Defao kuwa ndiye mmiliki na wale wenzake ni majambazi pia. Sasa hakuchukulia kama mchezo tena akaingia kazini rasmi. Akachukua kitambaa akaikamata vyema ile bastola na kuihifadhi katika kikoba chake.

"Usiwaambie lolote lile...na wakirejea nipe tarifa. Ole wako uvujishe siri!!" alichimba mkwara. Akaacha namba ya simu akatoweka. Muhudumu akabaki akiwa amekodoa macho. Hakuwahi kuiona bunduki hapo kabla

Alipotoka nje wawili wale waliokuwa wanaongozana hawakuwepo tena. Marashi akaingia ndani ya gari yake na kujaribu kufuata machale yake yalivyomtuma.
Matunda yakaonekana baada ya kuingia mjini. Hapa ndip alimuona Defao akiwa peke yake. Mnyonge kabisa.
Marashi hakutaka kuichezea bahati hii. Akamfikia Defao na kumweka chini ya uliznzi. Marashi aliamini kuwa lazima kuna hatia inamkabili bwana huyu.

Safari hii Defao alijikuta akibanwa na kumtaja Minja. Upelelezi ukahamia Singida Minja akapatikana. Alikamatwa akiwa katika maziko ya sajenti Kindo ambaye alikuwa ameaga dunia kutokana na ugonjwa uliokuwa ukimsumbua muda mrefu!!
Minja na Defao wakawa hatiani. Hatia ya kuua kwa kutumia bunduki ambayo ilikamatwa katika chumba alichokuwa anaishi Joyce na Defao.
Sheria ikachukua mkondo wake!!


****


John aliwasili Arusha akitanguliwa na basi moja tu la abiria. Mwendo alioondoka nao ulikuwa mkali sana na gari ile aina ya Pajero ilihimili mikikimikiki ya barabarani.
John hakutaka kufanya pumziko lolote lile. Aliyatembelea mawindo yake aliyoyatega mapema baada ya kuambiwa juu ya msichana anayeitwa Matha aliyesafiri kutoka Mwanza kwenda Arusha.

"Mmefanikiwa kumwona?." Aliuliza kwa utulivu bila kujibu salamu alizopewa na washirika wake hao.
"Tumemchukua na tumemuweka katika hifadhi."
"Alikuwa na nani katika safari hiyo."
"Tumemchapa makofi kadhaa anasisitiza kuwa alikuwa peke yake."
"Ahaa!! Ok!! Sawa." John alikubali huku kichwani akiwa na lake jambo.
Machale yalimcheza. Akayaheshimu. Hakutaka kuandamana na washirika wake kwenda kumtazama huyo wanayedai ni Matha. Maana hata muonekano waliomuelezea haukufanana na Matha anayemfahamu yeye. Japo hakuwaambia moja kwa moja alizuga kuna mahali anaenda kwanza kisha atarejea.
Akatumia mchezo huo, kuendelea kutega pale.
Masaa mawili yakapita, bado haukata tamaa alikuwa makini kabisa kufuatilia magari yanayowasili kutokea mikoani.
Baada ya masaa manne machale yake anayoyaheshimu yalimpatia majibu. Sasa aliweza kumwona. John Mapulu aliweza kumuona Matha. Na pia alimuona Adrian. Akajisifu kimyakimya kwa kuyaheshimu machale yake kwani sasa yalikuwa yamemwezesha kupata alichokikimbilia Arusha. Kumpata Matha.
"Wale wajinga wangenipoteza hivihivi." Aliwaza John, huku akifuatilia nyendo za Adrian na Matha.
"Huyu ----- anamtorosha malikia wangu. Namuua kwa mikono yangu." Alizungumza kwa ghadhabu. Sasa aliweza kuwashuhudia Matha na Adrian wakiingia ndani ya Teksi.
Kama kawaida akawafungia tela.
Uvumilivu ulimshinda John, wivu ukachukua nafasi kubwa. Safari ya kuwafungia tela ikaanza kumchosha na ni kama vile alikuwa anachezea shilingi katika tundu la choo. Muda wowote ule inaweza kudondoka. John akamtazama dereva wa teksi ambayo alikuwa amekodi akamwona yupo makini kufuatilia gari aliyoelekezwa aifuate. Taratibu akazama katika mkoba ,mdogo aliokuwa nao.
Alipoibuka alizua hofu na taharuki kwa dereva.
"Utafuata nitakachokueleza sawa!!" aliamuru John. Dereva akawa amekodoa jicho. Gari ikiwa imepunguza kasi yake.
"Simamisha!!.' Amri zikaanza. Mdomo wa bunduki ukiwa makini kusubiri amri ya kutema risasi iwapo itatakiwa.
Dereva akashika breki za ghafla. John kidogo apoteze muhimili wake na laiti kama yule dereva naye angekuwa masshuhuri katika mbinu za kinyang'anyi basi angeweza kumtia John mikononi mwake. Lakini yule dereva hakuwa na mbinu zozote. Gari ikasimama.
"Bila kuleta ujanja wowote fungua mlango wa gari. Hatua kwa hatua bila kugeuka nyuma utoweke eneo hili kimya kimya." Alitoa maelekezo Johnkisha akaendelea, "Ukithubutu kuleta ujanja na kuifanya gari hii ina thamani kuliko uhai wako....." hakumalizia!!!
Yule dereva akiwa katika taharuki ya hali ya juu alifuata maelekezo. Aliposhuka kiutaratibu. John akarukia katika siti ya dereva akaitia gari moto ikatoweka dereva akabaki peke yake barabarani!!!
John aliondoka kwa mwendo kasi mkubwa. Alikuwa na hasira. Baada ya dakika chache akaziona namba za gari ambayo ilikuwa imembeba Matha na John. Barabara nzima ilikuwa kimya. Magari yalipita kwa uchache sana. Muda ulikuwa umeenda.
Ugeni wa John katika jiji la Arusha ukamtia wasiwasi iwapo ataendelea kuwafuatilia akina Matha kwa muda mrefu. Aliamini watafika mahali watamuacha. Akaamua kuongeza mwendo. Gari ile ikawa kama inapepea.
Ndani ya sekunde chache akawasha taa za kuomba kupishwa njia aweze kuwa mbele. Dereva wa ile teksi akasalimu amri akakata kushoto akimwacha John ampite kulia kwake.
Likatokea tendo la ghafla. Badala ya ile gari kupita na kuendelea na safari zake. Ilipita kisha ikapinda kushoto na kuwa imeziba barabara. Dereva wa teksi akatoa yowe la hofu. Adrian aliyekuwa amelala hakujua nini kinaendelea.
Breki kali zikafungwa. Kabla hajamaliza kuhamaki katika dirisha lake ikapenya silaha ya moto. Aliyeishika akavua miwani yake. Macho yake yalikuwa yanatisha.
Dereva akapoteza fahamu!!!

Huyu alikuwa ni John Mapulu. Akaanza kutoa makaripio na maonyo kwa yeyote atakayethubutu kutingishika ndani ya gari. Kimya!!
Akatoa simu yake akawasha tochi akamulika mle ndani. Siti ya nyuma alikuwepo mwanaume peke yake akiwa hajulikani kama amesinzia ama amezimia. Matha hakuwepo!!
Shit!! Akatukana John!!
Akausogelea mlango wa nyuma akaufungua. Akatuliza kitako cha bunduki katika mguu wa Adrian. Akazinduka kutoka usingizini. Akawa anashangaa shangaa. Akamulikwa machoni. Akayafunika macho yake. Mara akashtuliwa na mkono mzito shingoni. Akatoa yowe la uoga na maumivu.
"Matha...Matha..." aliita. Akapokea teke lililotua tena katika shingo yake. Akangukia katika siti ya dirishani. Taa zikawaka ndani ya gari. Alikuwa amegusa kitufe cha kuwashia.
Ana kwa ana na John mapulu, baada ya miaka kadhaa kupita sasa alimuona tena John. Mwanaume aliyempokonya tonge mdomoni enzi hizo!!!
"John!!." Aliita. Akakutana na jicho lililojaa chuki.
Akatetereka. Huyu hakuwa yule John mpole wa kipindi hicho. Huyu alikuwa mwingine kabisa.
"Nakupa dakika moja ya kujieleza ni wapi ulikuwa unampeleka Matha, ni wapi umemuacha!!." John aliunguruma.
"Mi sijui..ni yeye mimi...sijui hata ni wapi .." hakueleweka Adrian, na asingeweza kueleweka.
"Bado dakika yako haijaisha. Ikimalizika sitakupa sekunde chache za kusali sala yako ya mwisho." John alizidi kutetemesha.
Adrian akabaki kama zezeta. Asijue nini kinaendelea. Akajiuliza Matha yuko wapi hakupata jawabu.
Sekunde zikazidi kukatika na dakika ikawa inakaribia kuchukua hatamu. John alikuwa hatanii.
Ni hapa ndipo MPAMBANO uliokuwa unasubiriwa ukaibuka!!!
Bastola ya John iliyokuwa inasubiri amri ya kumuondoa Adrian duniani ilipigwa teke ikaruka juu sana. Haikufyatuka!! Adrian alikuwa amefumba macho. Huenda alikuwa anasali ile sala ya mwisho. Jasho likimtiririka
John akatoa yowe la mshtuko. Alipogeuka akakumbana na na mguu imara wa ukasalimiana na fuvu la kichwa chake katika namna ambayo ni nzuri kutazama lakini usiwe mtendwa wewe.
Akapoteza muhimili mikono miwili ikamzuia asiweze kuisalimia ardhi.
Akageuka tena sasa bunduki isiyokuwa na masihara ilitazamana na uso wake.
Mikono ya mwanamama illikuwa imepakata silaha hiyo ya moto. Mikono hii ilionekana kujua vyema matumizi ya hii kitu.

Sekunde kadhaa zilizopita alikuwa amejirusha kutoka garini baada ya kuchezwa machale na mabadiliko ya mwendokasi wa gari iliyokuwa nyuma yao. Adrian aliyekuwa amelala hakujua lolote na hata dereva aliyekuwa ametaharuki hakushtukia tukio hili. Sasa alikuwa amerejea tena kufanya ukombozi.
"Matha!!." Aliita John. Lakini huyu hakuwa Matha aliyemtambua. Huyu alikuwa mwingine kabisa. Hakutabasamu hata kidogo.
"Ukipiga hatua mbele nasambaratisha ubongo wako." Matha naye akaunguruma. Adrian hoi akiitazama filamu hii ya kutisha.
"Matha unasema?" alifoka John. Matha naye akafoka kwa namna ya kipekee, namna ya kuachia risasi iliyochimba pembeni kidogo ya mguu wa John.
"Uwiiii." John akapiga kelele. Hakutegemea kitendo hicho kutoka kwa Matha.
Sasa akaingiwa na uoga wa kupoteza uhai. Akatii amri akatulia tuli akiwa ameinyanyua mikono yake juu. Kwa mara ya kwanza katika maisha yake anatishwa na mwanamke tofauti na mama yake aliyemzaa.
"John. Uonevu wako umezidi. Nakuheshimu sana lakini kwa kuipigania roho hii isiyokuwa na HATIA naapa heshima na iishe. Au lasivyo yawepo makubaliano ya amani. Adrian abaki huru bila kusumbuliwa. Hilo ni moja. Na pili..."
"Huwezi kunipangia amri Matha..." Aliingilia kati mazungumzo Adrian.
Risasi nyingine ikafyatuka. Ikatua palepale ilipotua ya kwanza.
"Nadhani unafahamu kuwa huwa sikosei nikiamua kulenga." Alisema Matha. John akaelewa mwanamama huyu ana maanisha nini. Alimaanisha kuwa anamkosa maksudi. Akiamua anamuua ndani ya sekunde moja.
John akawa mtulivu!!.

***NI VITA KUU HATIMAYE MATHA aliyefunzwa na JOHN MAPULU sasa anamkabili kwa kuliokoa PENZI LAKE LA UTOTONI....kwa kumuokoa ADRIAN. MATHA kiwa na bunduki mkononi...JOHN mikono mitupu!!! ADRIAN mtazamaji!!!! NANI ATAPONA NA NANI ANAONDOKA NA HATIA YAKE????

***JOYCE mikononi mwa MICHAEL TENA!!! Je wataelekea wapi????


Wazo Langu Mr Rocky NYIRO master09 Khantwe KABERWA2013 mbalu Honey Faith Sangomwile Jullie Z mugaruVAN HEIST binti kiziwi Donatila
 
daaaaaaahh...bola yawepo ya amani jamaniiiiiiiiiiiii
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom