Riwaya - Gereza la Kifo

Riwaya - Gereza la Kifo

Asante bishop kwa tag lakini kuanzia mwanzo wa simulizi nilikua sipati notifications adi nlipoikuta humu kwa bahati tu yani kuanzia jana nmelazimika kuwakimbilia na finaly nimewakuta
Amani iwe nawe mkuu
 
Kaz gani akwende zake huko yani simpendi na asisumbue wenzie asubiri hukumu afungwe stori yake iishe anajua watu tunaumizwa na mangapi af nalo lije kutuletea uzwazwa wake
Najikuta nacheka manake mwandishi kaamua kupiga chenga yale yoote tuliyoyatarajia

Sasa badala ya wariri kuumia sisi ndio tumeumia

Kujitetea halijui halafu hata mbinu linaingilia mambo kichwa kichwa
 
Gereza la Kifo - 43

Mtunzi - HAMISI KIBARI

ILIPOISHIA

Siku ya pili yake Walari aliletewa uji kwenye saa tatu hivi, na alishangaa kuona anajisikia vizuri.
Hata alishangaa namna ambavyo aliunywa uji huo wote bila matatizo yoyote.
Ilipofika jioni, Walari alianza kujisikia vizuri zaidi na sasa akagundua kuwa dawa zile ambazo zilionekana kwamba ni za Kichina alizokunywa zilikuwa zinatibu haraka sana maleria.
Siku ya tano ilikuwa imemkutia tena kwenye chumba hicho cha mateso na kulikuwa hakuna dalili ya kutolewa katika chumba hicho. Mujora naye akawa hajaonekana.

Endelea...

Ilipofika siku ya tisa, akiwa bado kwenye chumba hicho cha mateso, sasa aliona kama wahusika wamemsahau humo na hajui wanataka nini hasa baada ya kuokoka kifo cha ugonjwa wa maleria. Kwa bahati, yale maji yalikuwa yanaelekea kuuka na kwenye kona moja alikuwa anaweza kukaa na kulala.
Walari sasa alikuwa akijiuliza wabaya wake watamuua kwa kitu gani, kwa sababu alihisi mwisho wa yote ni yeye kuuawa.
Alihisi huenda Masunju, alipanga mkakati wa kumuulia kwenye kijichumba hicho kwa njia ya mateso na malaria kutokana na kuwa na mbu wengi. Pia alikuwa haelewi kinachoendelea huko nje ya kuta za gereza kuhusu rufaa yake.

******************

Walari alitolewa kwenye kile chumba cha mateso na askari mmoja na kushukuru Mungu akiamini kwamba hatua ya kumtesa ilikuwa imemalizika. Ingawa alikuwa bado hajisikii vizuri lakini kile kitendo cha kutoka nje ya chumba hicho alijisikia faraja na kupata nguvu japo kidogo.
Askari aliyemtoa katika chumba hicho hakumweleza anakompeleka lakini aliona hampeleki selo bali katika maeneo ya ofisini. Yale matumaini yalitoweka na kuhisi labda amebadilishiwa mateso sasa anaeleka kumalizwa kabisa.
Aliingizwa katika moja ya vyumba na kuamriwa kuketi kwenye kiti kilichokuwa kimetayarishwa mahala hapo. Upande wake wa pili, kulikuwa na mtu ameketi, wakiwa wanatenganishwa yeye na mtu yule kwa wavu.
Sura ya mtu yule aliyevaa suti nyeusi haikuwa ngeni sana kwake. Alijaribu kujitahidi kumkumbuka na taratibu taswira ikaanza kumwijia. Alikuwa Dickson Mafuru, mmoja wa mawakili maarufu pale Bulibuli na hata makao makuu ya nchi, Bandaria.
“Haya ninawapa dakika zisizozidi ishirini. We’ mkorofi ongea na wakili wako,” alisema yule askari na kuondoka eneo hilo na kukaa pembeni.
“Pole sana Walari, pole sana lakini madhali umeniona hapa fahamu kila kitu kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu na juhudi zetu kitakwenda salama,” alisema Wakili Mafuru baada ya kutambulishana na kila mmoja kugundua kwamba alikuwa anamfahamu mwenziye.
Wakili alianza kwa kumjulisha kwamba alikuwa amefanikiwa kukata rufaa nje ya muda baada ya Mahakama ya Mwanzo Bulibuli kutaka kuzuia haki hiyo.
“Hilo pekee limedhihirisha kwamba hujafungwa kihalali, kwa hiyo usiwe na hofu. Mambo yatakwenda vizuri tu,” akasema Wakili Mafuru.
Pamoja na kusimuliwa kwa kifupi kesi yake na mwandishi mwenziye, Marare, lakini Wakili huyo alitaka kusikia kutoka kwake kituo kwa kituo.
Walari akaanza kumsimulia mwanzo hadi mwisho na katika hali ambayo hakurajia, wakati anamalizia masimulizi yake wakili yule alijikuta akifuta machozi kwa uchungu.
“Nchi yetu imeoza kwa rushwa na ufisadi. Ninaomba usiku na mchana ikiwezekana katika uchaguzi ujao tukapata viongozi watakaotuondolea adha hii. Kwa bahati mbaya sana, hata sisi wapiga kura tunataka kuhongwa na wagombea wa hovyo,” alisema Mafuru akiendelea kufuta machozi.
Akaendelea: “Walari, nitapigana kwa kila nitakachoweza na kwa masimulizi haya, sitahitaji hata senti moja, nitaifanya kazi hii bure,” alisema wakili huyo na hata kabla hawajamaliza mazungumzo, yule askari akamnyanyua pale Walari na kumtaka Wakili aondoke kwani muda waliopewa ulikuwa umemalizika.
Katika hali ambayo hakutarajia Walari alirejeshwa kwenye chumba cha mateso ambacho hata hivyo, maji yalikuwa karibu yamekauka yote.
Usiku wa siku hiyo ya tisa tangu afunguwe katika chumba hicho, hali ya Walari ilibadilika tena. Alianza kuhara damu na tumbo kumkata sana. Alihisi huo ni ule ugonjwa ambao, si kipindupindu, lakini ulikuwa unaua wafungwa wengi sana katika gereza hilo.
Huo ni ugonjwa ambao aliambiwa mara kwa mara kwamba mtu akiukwaa si rahisi kupona.
Wafungwa wenyewe walikuwa wakiuita ‘Ukimwi wa gereza’ kutokana na kusababisha vifo vya asilimia kubwa ya wengi waliouugua. Ugonjwa huo ambao tumbo lilikuwa likiuma sana labda sawa na lile la uzazi kwa wanawake, wengine walihisi kwamba ni wa 'kutengeneza', kwani mara nyingi ulikuwa unawapata wakorofi na watu ambao maaskari jela hawawapendi au wameshawashindwa.
Kadhalika, wengi waliokuwa wanapelekwa kwenye chumba cha mateso aghalabu walitoka humo salama bila kuugua ugonjwa huo, ambapo baadhi walifia katika jela hiyo au wengine kufia hospitalini ambako walikimbizwa wakiwa hoi. Haikueleweka kama hospitali ya Bulibuli ilikuwa haina dawa za kutibu aina hiyo ya ugonjwa wa kuhara au la na pengine walikuwa hawajatafiti ili kujua huo ni ugonjwa gani hasa.
Usiku huo tumbo liliendelea kumkata na kumfanya aharishe kwenye mtondoo mara tano hadi nguvu zikamwishia kabisa. Tena kila alipokuwa anajisaidia ndiyo alikuwa anasikia maumivu ya ajabu kwani sehemu za haja kubwa ziliuma sana utadhani zimemwagiwa pilipili kichaa iliyochemshwa na wakati huohuo tumbo likikazana kukata.
Kuna wakati alipokuwa juu ya mtondoo alijisikia maumivu makali kiasi cha kukaribia kuzirai, huku jasho jingi likimtoka.
Baada ya kuhara mara mbili, mwishoni akwa anaharisha mapovu tupu kwani tumbo lilikuwa halina kitu. Alihisi kusingekucha salama bila kufariki dunia. Alihangaika hivyo usiku hadi kukacha huku akiendelea kumtaja Mwenyezi Mungu ampokee salama na kumfutia madhambi yake.
Kutokana na ugonjwa huo wa aina yake ambao Walari alikua hajui jina lake kitaalamu, wafungwa walihisi kwamba huwenda vijidudu vyake vilikuwa vinawekwa makusudi kwenye chakula au maji anayopewa mfungwa au kundi la wafungwa ambao walitakiwa wafe ili kupunguza idadi ya wafungwa katika gereza hilo ambalo lilikuwa limejaa sana kuliko kawaida. Ingawa gereza lilikuwa na sehemu kubwa, Walari alikuwa hajui kwa nini lilikuwa halipanuliwi. Isitoshe gharama za ujenzi zilikuwa rahisi. Matofali ya kuchoma yangetayarishwa na wafungwa wenyewe wakajenga kwa kuzingatia kwamba baadhi yao wana taaluma ya wajenzi.
Walari alikumbuka tena kitabu alichowahi kusoma ambacho kilizungumzia namna Waafrika wapigania uhuru katika nchi za Namibia, Afrika Kusini, Msumbiji na Rhodesia (siku hizi Zimbabwe) walivyokuwa wakitengenezewa magonjwa makusudi.
Katika kitabu hicho, kwa mfano, inaelezwa kwamba wakati wa utawala wa Ian Smith aliyekuwa akitawala Zimbabwe kabla ya uhuru ulioletwa na wapiganaji wa Kizalendo wakiwemo akina Robert Mugabe na hayati Joshua Nkomo zaidi ya miaka 35 iliyopita, Wazungu wachache na vibaraka wao wangeweza kwenda eneo fulani la Waafrika na kumwaga vijidudu vinavyosababisha ugonjwa wa kipindupindu kwenye mto au kisima kinachotegemewa na wananchi, kisha wanapougua ugonjwa huo, hawapelekwi kutibiwa kwa makusudi ili Waafrika wapukutike kwa kufa.
Lakini katika hali ambayo Walari aliita ujinga wa Waafrika, wazalendo walikuwa tayari kumsamehe mtu kama Ian Smith kwa kuwafanyia unyama kama huo na kukataa kumsamehe Mwafrika mwenzao, kama Robert Mugabe, akifanya makosa kidogo ya kibinadamu kwenye utawala wake, kwa sababu yeye si Mzungu!
Walari pia alikumbuka kusoma katika kitabu hicho ikielezwa kwamba katika nchi hiyo ya Zimbabwe wananchi walikuwa wakiwekewa kwa makusudi unga wenye vijidudu vya ugonjwa wa kimeta kwenye nguo zao.
Alianza kumfikiria tena mwanafunzi mwenziye waliyesoma pamoja shule ya msingi, Mujora James kama atatokea tena na kumuokoa ama ndio siku zake za kukaa duniani zilikuwa zimefikia ukomo.
Wakati lishe ilikuwa duni, maleria nayo ambayo alikuwa amepona lakini ikiwa umempunguzia kilo kadhaa, sasa aliona kuharisha ndiko kutamuua. Kitu kilichoanza kumsumbua akili ni namna mazishi yake yatakavyokuwa ya hovyo kama atazikwa mithili ya mtu asiyejulikana.
Yeye angetamani azikwe katika makaburi ya Kurugongo, mjini Bulibuli alikozikwa mkewe ili awe karibu naye, lakini alijua atakufa na mwili wake kuozea katika chumba cha maiti pale katika hospitali ya Bulibuli na kwa jinsi alivyokonda, yule mhudumu wa chumba hicho, Nyamagwila, isingekuwa rahisi kumkumbuka.

Itaendelea...
Pole walari
Askofu asante sana
 
Back
Top Bottom