Bishop Hiluka
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 7,147
- 14,709
- Thread starter
- #141
Itaendelea...
Ahsante sana mkuu kwa kunikumbuka ktk ufalme wako..Wakuu, Tater, moneytalk, marybaby, nipo2, ram, kisukari, the_legend, Smart911, Madame S, carbamazepine, Astelia, culture girl, Prisoner of hope, Mine eyes, kuku mweus, Thad, hearly, Shunie, moneytalk,Tumosa,@hearly, nipo2, Katavi , Mine eyes, Kudo, swahiba92, ludist, Toyota escudo, Clkey, macson3, Thad, boga la kiangazi, macson3, LEGE, Smart911, Richard irakunda, skfull, popie, @Krizy Beat mzigo ndiyo huo...
Haha, anaona mnafaidi.
Achana naye, anaonekana dish limeyumba kidogoWaswahili mna kazi sana. Kwa hiyo sina majukumu mengine ya kufanya, muda wote nionekane Jamii Forums ili kukufurahisha? Upuuzi ulioje...
Ovyoo! Kwani akiuza wewe unakuhusu nini, au umelazimishwa kusoma? Mfyuuuu!
Wakuu, Tater, moneytalk, marybaby, nipo2, ram, kisukari, the_legend, Smart911, Madame S, carbamazepine, Astelia, culture girl, Prisoner of hope, Mine eyes, kuku mweus, Thad, hearly, Shunie, moneytalk,Tumosa,@hearly, nipo2, Katavi , Mine eyes, Kudo, swahiba92, ludist, Toyota escudo, Clkey, macson3, Thad, boga la kiangazi, macson3, LEGE, Smart911, Richard irakunda, skfull, popie, @Krizy Beat mzigo ndiyo huo...
Gereza la Kifo - 39
Mtunzi - HAMISI KIBARI
ILIPOISHIA
Mahakama, ikiwa imetulia tuli, mithili ya maji mtungini, hakimu wa kesi hiyo, Mheshimiwa Karwana Mayogu, alianza kusoma hukumu kwa kutalii kwa ufupi namna ushahidi wa kesi hiyo ulivyotolewa mbele yake na pande zote mbili. Wakati huo moyo wa Walari ulikuwa ukidunda pa, pa, pa. Hakuwa na ule ujasiri wake wa kawaida.
Hakimu Mayogu akasema kwamba upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha shitaka la kwanza dhidi ya mshitakiwa. Shitaka hilo lilikuwa ni la kumuuzia bangi mfungwa.
Pia akasema mahakama yake ilikuwa haioni kama upande wa mashitaka umefanikiwa kuishawishi mahakama yake kuamini kwamba alikuwa amekutwa na bangi.
"Hata hivyo, mahakama hii," akasema hakimu huyo akimtazama mshitakiwa kupitia juu ya miwani yake ya kusomea aliyokuwa ameilegeza kwenye pua yake ndefu, "inakutia hatiani kwa makosa mawili; kuingia katika eneo la jeshi kwa lengo la kutaka kufanya uhalifu na kosa la kuongea na mfungwa kinyume cha sheria."
Je, nini kitampata Walari? Endelea...
Baada ya kusema vile hakimu aliupa upande wa mashitaka kusema chochote kabla mahakama haijatamka adhabu. Wakati huo wazazi wa Walari pamoja na marafiki zake walionesha sura za kukanganyikiwa, kila mmoja akimwangalia mwenzake kama ameelewa hakimu alichokisema ama amesikia vibaya. Walioelewa alichokisema Hakimu waliangaliana kama watu ambao wangeomba hukumu ile ibatilishwe muda ule ule au wanaoamini kuwa hakimu kateleza tu katika matamshi yake.
Mwendesha mashitaka, Inspekta wa Jeshi la Polisi, Sam Manure, alisimama na kuomba mahakama impe adhabu kali sana mshitakiwa huyo ili kukomesha tabia ya watu kuingia katika maeneo ya jeshi na yasiyoruhusiwa kwa lengo la kufanya uhalifu.
"Na kuna tabia mbaya kabisa inakua kila siku ya watu kuongea na wafungwa holela. Naomba mahakama hii tukufu itoe adhabu kali sana kwa mshitakiwa ili liwe fundisho kwa watu wenye tabia mbaya kama ya mshitakiwa," akamaliza kusema mwendesha mashitaka aliyekuwa kavalia magwanda ya kipolisi, akaketi kwenye kiti chake, mbele ya hakimu.
Baadaye hakimu alimgeukia Walari na kumuuliza kama alikuwa na chochote cha kuomba kabla hajatamka adhabu dhidi yake atakayokwenda kuitumia jela.
Walari alipopata nafasi hiyo alimwambia hakimu kwamba haelewi ni kwa nini mahakama yake inamtia hatiani kwa kosa ambalo hajafanya.
"Muda wa kujitetea ulishakwisha, omba shufaa kama unataka na kama huna chochote cha kuomba nyamaza," akasema hakimu kwa hasira.
"Mheshimiwa hakimu, siwezi kuomba shufaa ya hatia ambayo mimi binafsi sina, na bila shaka lazima niseme kesi hii ina influence (msukumo) ya kitu, si bure."
"Mshitakiwa unaonekana una dalili za kutaka kudharau mahakama. Unaweza kujikuta ukishitakiwa kwa kosa jingine sasa hivi," akasema hakimu akionyesha hasira zaidi na huku sauti yake sasa ikiwa imepanda juu kuliko pale mwanzo.
Kikapita kimya kifupi wakati hakimu yule akiwa ameinama akiandika kwenye makaratasi meupe yaliyokuwa ndani ya jalada la kesi hiyo mbele yake. Akaendelea:
"Mshitakiwa, kwa kosa la kuingia kwa jinai utatumikia kifungo cha miaka miwili jela, na kosa la kuongea na mfungwa utakwenda jela miezi sita. (Jumla umefungwa miaka miwili na nusu lakini) Makosa haya yanakwenda pamoja (kwa hiyo utatumikia kifungo cha miaka miwili). Nafasi ya kukata rufaa iko wazi."
Zilipita sekunde kama 30 watu wote mahakamani humo wakawa wameshikwa na bumbuazi na mara vilio vikaanza kusikika. Aliyeanza kulia alikuwa ni mama yake, akafuatia mke wa Nurdin. Nurdin mwenyewe pamoja na Jamila, yaani yule mwanamke wa Halmashauri ya Manispaa nao walijikuta wakifuta machozi. Hata Janeth ambaye Walari hakumuona kwenye msiba wa mkewe zaidi ya mama yake naye akanza kulia.
Mama yake Walari alianguka chini na kuzirai karibu na mlango wa kutokea kwenye chumba cha mahakama. Baada ya kupewa huduma ya kwanza, mwalimu huyo mstaafu aliyeonekana dhahiri amechanganyikiwa alitoka na kujirusha mbele ya gari iliyokuwa inapita kwenye barabara, mbele ya mahakama hiyo, kwa lengo la kujiua.
Hata hivyo, gari hiyo aina ya Landrover iliyokuwa inakuja kasi ilimkwepa, akaanguka chini na kuzirai tena. Watu wakatoka kwenda kumchukua mwanamke huyo na kumpa huduma ya kwanza.
Walari baada ya kuiambia mahakama kwamba lazima atakata rufaa, alizolewa na askari polisi kutoka kizimbani na kwa mbali akaona watu wakimhudumia mama yake chini ya kivuli cha mti mkubwa ulioko upenuni mwa mahakama hiyo ya wazi.
Baadaye Nurdin alimfuata Walari wakati akikokotwa na yule askari na kumwambia kwamba lazima wakate rufaa.
"Lazima tukate rufaa. Kuna askari mmoja pale anajua sheria nimemsikia akidai kwamba adhabu ya makosa kama haya ni haidi kifungo cha mwaka mmoja. Lazima tukate rufaa na amini usiamini hakimu kahongwa hela nyingi na Masunju ili akukomoe. Inanisikitisha," akawa anasema Nurdin macho yake yakiwa yamejaa machozi, lakini yule askari aliyekuwa kamkwida Walari akimkokota akamtimua na kutishia kumweka ndani.
*************
Wiki ilikuwa imekatika toka Walari awe katika gereza la Magamaga kama mfungwa.
Huko nje, Nurdin pamoja na yule mwandishi wa EBC, Madenge Marare, walikuwa wameungana kutafuta namna ya kukata rufaa dhidi ya hukumu iliyomuona Walari akiwa na hatia ya makosa mawili na kumfunga kifungo cha miaka miwili jela. Akina Nurdin pia walikuwa wameomba Walari apewe dhamana wakati anashughulikia rufaa yake, lakini hakimu Karwana Mayogu alikuwa amekataa.
Katika wiki hiyo moja aliyokuwa katika gereza hilo, roho ilikuwa ikimuuma sana na alijua juhudi za Masunju zilikuwa zimezaa matunda. Wasiwasi wake mkubwa ulikuwa ni kuuawa akiwa gerezani humo katika kipindi hicho ambacho ndugu zake walikuwa wanashughulikia rufaa yake.
Kutokana na wasiwasi wa kuuawa kupitia chakula, pengine kwa kuwekewa sumu, Walari alikuwa makini sana na chakula, na muda mwingi alikuwa akishinda na njaa, au kuomba chakula cha wafungwa wenzake ambacho aliamini ni salama. Muda mwingi alikuwa akilala kwa kunywa maji tu.
Hata hivyo, kwa muda wa wiki hiyo moja aliyokua amenza kutumikia kifungo, Walari alikuwa hajaona hila au kitendo chochote cha makusudi cha kutaka kuhujumu uhai wake. Lakini wiki hiyo moja aliiona kama mwaka, wakati miaka miwili ya kukaa jela ilikuwa ikimsubiri!
Siku ya Jumapili ya wiki hiyo ya kwanza akiwa gerezani, Marare alikuja kumjulia hali na kumjulisha kwamba walikuwa wanakwamishwa kukamilisha taratibu za rufaa kutokana na hakimu aliyemfunga kuwapiga chenga katika kuwapa nakala ya hukumu ili waitumie katika kukata rufaa. Akasema hata makarani wa mahakama walikuwa wanaonekana kuwapiga chenga kila wanapofuatilia nakala ya hukumu hiyo.
Hata hivyo, Marare alimjulisha Walari habari nyingine iliyomkosesha raha. Alimwambia kwamba baada ya uongozi wa EBC kupata habari kuwa amefungwa, ulikuwa umesitisha taratibu za kumwajiri na hivyo sasa walikuwa wanatafuta mwandishi mwingine.
Marare ambaye aliwekewa mizengwe na kuchunguzwa sana kabla ya kumuona Walari, hata hivyo, alisema: "Lakini hilo la EBC lisikuhuzunishe sana, ndugu yangu. Cha msingi ni wewe kutoka katika hiki kifungo cha uonevu."
Marare pia alimweleza kwamba, licha ya waandishi wote kuonyesha mshikamano kwa kutoripoti vibaya kuhusu kifungo cha mwenzao, gazeti la Upekuzi, ambalo lilikuwa halina mwandishi kwa wakati huo mjini Bulibuli, liliripoti kama vile linashangalia kufungwa kwake.
Alimjulisha kwamba gazeti hilo liliandika kwamba Walari amepatikana na hatia ya kuuzia wafungwa dawa za kulevya, kitu ambacho si kweli kwa sababu mahakama ilikuwa imempata na hatia ya makosa ya kuingia katika eneo la jeshi kwa kutaka kufanya uhalifu pamoja na kuongea na mfungwa aliyeko gerezani kinyume cha sheria.
"Ninaamini mabosi wamelisoma gazeti la Upekuzi London kupitia kwenye mtandao wa kompyuta, kwa sababu inaonekana maelezo yao ambayo nimeyapata kwa faksi asubuhi hii, yanaonyesha wamesoma gazeti hili lilipotoka jana. Pengine wameona kwamba kama gazeti ulilokuwa ukiliandikia linakulalamikia kama mwandishi unayetia aibu taaluma basi utakuwa hufai," alisema Marare akionesha masikitiko.
Marare pia alimjulisha kwamba mwanaye njiti alikuwa kachukuliwa na ustawi wa jamii baada ya watu wa hospitali kupata habari kwamba baba yake kafungwa na mama yake kafariki dunia.
Kuhusu mwanae mwingine, Ashraf, Marare alimjulisha kwamba amepata habari kupitia kwa Nurdin kwamba bado yuko hospitali na hali yake ambayo ilikuwa inatoa matumaini, sasa imebadilika na kuwa mbaya.
"Nahisi Nurdin kakosa nafasi ilikuwa akuletee habari sahihi leo kwa sababu aliwasiliana na mama yako. Lakini usiwe na wasi wasi. Nadhani hali yake itakuwa nzuri na Mungu atamsaidia huyu mtoto."
Baadaye Marare alifukuzwa na askari mmoja, kati ya wawili waliokuwa wanaangalia watu waliokuwa wanaongea na ndugu zao pale getini. Kama kawaida kulikuwa na zogo kubwa sana pale mlangoni, hata kuwasiliana kwao ilikuwa inamlazimu wapigiane makelele sana.
Walari alikuwa haelewi ni kwa nini siku ya raia kutembelea mahabusu na wafungwa, kundi kubwa la watu lilikuwa linafunguliwa kuwaona wafungwa kwa mara moja badala ya kufanya utaratibu wa kuruhusu idadi ndogo na nyingine kusubiri ili watu wanaowaona ndugu zao wafungwa au mahabusu wawe wachache na kuweza kusikilizana.
Jumapili nyingine ilimkuta Walari akiwa bado yuko mahabusu. Lakini siku hiyo akaletewa habari mbaya sana. Habari hizo zilisema kwamba mwanae Ashraf ambaye alikuwa amezidiwa tena, alifariki dunia.
Akajulishwa kwamba pengine Ashraf angeweza kuokoka kama ingepatikana gari ya kumkimbiza mapema katika hospitali ya Rufaa ya Bulibuli kutokana na matatizo yaliyompata.
Habari hizo mbaya ambazo pia zilipelekwa kwa uongozi wa gereza, zilimchoma moyo na kumfanya azirai mara kwa mara.
Hata hivyo, katika hali hiyo ya kuzirai hakuwa anapewa huduma yoyote ya maana, na askari wale kama kawaida waliomba hata afe ili kupunguza msongamano wa wafungwa ambao kila mara walidai kwamba unawakera sana.
Baada ya kupata taarifa hiyo ya kifo cha mwanae Walari alikuwa amechanganyikiwa na akawa anaongea mambo yasiyoeleweka mithili ya mtu ambaye malaria imempanda kichwani.
Itaendelea...
Tuvumiliane wakuu mnapoona kimya, sometimes majukumu yanabana sana, ndiyo maana ninapopata nafasi tu namwaga mzigo chap' chap'. Kwa leo mzigo unatosha...