ElPuto Jefe
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 5,286
- 19,463
Mambo yanazidi kupamba moto....!!
Asante BishopWakuu, Tater, moneytalk, marybaby, nipo2, ram, kisukari, the_legend, Smart911, Madame S, carbamazepine, Astelia, culture gal , Prisoner of hope, Mine eyes, kuku mweus, Thad, hearly, Shunie, moneytalk,Tumosa, Katavi , Mine eyes, Kudo, swahiba92, ludist, Toyota escudo, Clkey, macson3, Thad, boga la kiangazi, macson3, LEGE, Smart911, Richard irakunda, skfull, popie, Krizy Beat, hearly SUPER EMILY, WISDOM SEEDS nipo2 na wengineo, karibuni muendelee. Nawatakia Jumapili njema...
😀😀😀mi nkajua utaanza kusoma kwa sautii mkuutoka nimeanza kusoma nilikua nasoma kimya kimya. sasa nimefika mlipo fika asantee mwndishiiiii
Sent using Jamii Forums mobile app
nikisoma kwa kelele itakua fujo humu😀😀😀mi nkajua utaanza kusoma kwa sautii mkuu
Hahaa...NYAMAGWILA FANIKISHA MPANGO HUU... Nikutoe kwenye kazi ya mochwari nikupeleke uwe msimamizi wa kuruhusu ndege ziluke terminal 3(three)
Sent using Jamii Forums mobile app
Asubuhi murua kabisa na kifungua kinywa cha ukweliGereza la Kifo - 51
Mtunzi - HAMISI KIBARI
ILIPOISHIA
"Sasa mimi naita teksi uende zako. Kuna maiti hapa isiyotambuliwa, ina wajihi kama wako. Hii ndiyo nitakayoivisha nguo zako na nitabandika jina la Walari kwa sababu maofisa wa magereza kuna wakati huwa wanafuatilia, hasa kujua maiti zao ambazo zimetambuliwa na wenyewe," akasema Nyamagwila.
"Sasa nguo nitapata wapi za kiraia?"
"Mimi sina jinsi. Itabidi nikupe maguo fulani ya maiti wasiotambuliwa ambayo huwa yanabaki humu. Mengine mimi huwa nawauzia wauza mitumba".
"Kwani hao wauza mitumba wako mbali sana? Kwa nini usiende kuninunulia haraka haraka shati na suruali ili nivae hizo?"
"Wazo zuri. Lete pesa nikimbilie."
"Pesa nitoe wapi, si ndizo nilikupa zote?"
Endelea...
"Wewe pesa zenyewe ulizonipa hazitoshi na nitakudai zingine, sasa kama ni hivyo, hela ya teksi utatoa wapi?"
"Mimi nilidhani tulikubaliana pia kuhusu hilo kwamba wewe utanilipia hela ya teksi... Waswahili wanasema, nifae la jua nami pengine kuna siku nitakufaa la mvua. Umeshakula ng’ombe mzima tafadhali malizia mkia."
"Mbona sasa rafiki yangu unaniangusha wakati pesa yenyewe ulionipa kidogo sana?"
"Sikiliza Nyamagwila. Umefanya kitu kikubwa sana cha kuniokoa na kifo. Wewe toa pesa, kaninunulie nguo za mitumba na utanilipia teksi. Hizo pesa nitazilipa. Na subiri tu hela ya asante yako nitakuletea pia siku moja."
Nyamagwila alisema hakukua na haja ya kununua nguo za mitumba wakati alikuwa nazo humo. Alifungua kabati moja na kutoa nguo, suruali na shati.
"Haya, nguo hizi hapa. Vua hizo za jela kisha niivalishe hiyo maiti isiyotambulika. Fanya haraka wakati ninaita teski. Umesema ukitoka hapa utakwenda kujificha wapi?"
"Nakwenda kule kule Magamaga kwa rafiki yangu Nurdin," alisema Walari akinusa zile nguo. Kweli shida haina adabu kwa sababu Walari hakuota kwamba kuna siku atavaa nguo zilizotoka kwa maiti bila hata kufuliwa.
"Kumbe mbali hivyo. Hela yote itaishia kwenye teksi... Vaa haraka."
"Usijali rafiki yangu. Mambo yakiwa sawa nitakutembelea tena na kukufariji. Suala la pesa lisikusumbue sasa."
"Sawa rafiki yangu, lakini ujitahidi kujificha sana na ikiwezekana uhame huu mji hata kwa miaka minne. Ukigundulika kwamba hukufa, mimi na yule muuguzi tutapata matatizo sana."
"Suala la mimi kukamatwa au kutokamatwa pia lisikutiea presha. Cha msingi na muhimu ilikuwa ni mimi kuokoka kifo. Ninakuhakikishia hata kama nitakuja kujulikana niko hai na wananchi kujua ulichokifanya, utapongezwa na si vinginevyo. Nina hakika na hilo."
"Wewe mtoto, unataka kusema utanitaja.... Eh, unataka nijute kukusaidia?”
“Ninakuhakikisha, Nyamagwila, hakuna litakaloharibika kwa sababu umefanya jambo jema lakini nitajitahidi kuficha hii siri kwa muda mrefu kadri itakavyowezekana.
Walari alivua nguo za kifungwa na kuvaa alizopewa. Hazikuwa zinamtosha kwa jinsi alivyokonda lakini ghafla alibadilika. Nyamagwila aliangalia ofisini kwake akatoa kofia moja kubwa akampa, kisha akampa miwani ya jua avae. Nyamagwila alionekana na wasi wasi kwamba Walari anaweza kugundulika, lakini kwa mavazi yale, kofia pana na ile miwani myeusi isingekuwa rahisi.
"Unaona umeniachia tena kazi ya kuvalisha maiti nguo zako za jela. Hii pia lazima unilipe. Ni kazi ngumu sana."
"Usijali rafiki. Tuombe uzima," alisema Walari wakitoka kwenye chumba cha maiti. Kwa bahati kulikuwa na teksi ikipita karibu ambayo bila shaka ilikuwa imemleta mgonjwa hospitalini hapo. Waliisimamisha, wakauliza nauli ya kwenda Magamaga, eneo la Majengo Mapya. Dereva akataja Sh 20,000. Nyamagwila akamuomba afanye sh. 15,000. Akakubali na Nyamagwila akalipa hiyo pesa. Walari akaingia, teksi ikaondoka huku Nyamagwila akipunga mkono.
Wakati wanaondoka pale kwenye chumba cha maiti ilikuwa inaelekea saa tisa na nusu alasiri.
Dereva yule aliondoka kwa kasi na baada ya muda wa dakika 40 walikuwa wamefika Magamaga, eneo la Majengo.
Walari alimwelekeza yule dereva njia ya kupita ya kuelekea kwa Nurdin, ambayo ni kama uchochoro ambao gari hupishana kwa taabu sana na pia njia ina mashimo mashimo.
Yule dereva ambaye alikuwa ameshalipwa hela zake na Nyamagwila alionekana kulalamika kuhusu njia ile akitaka aongezewe pesa, lakini baadaye alikubali kwenda kwa shingo upande.
Walari hakutaka ile teksi imfikishe kabisa kwenye nyumba alikokuwa anakwenda kwani hakutaka dereva teksi huyo apaone. Akashuka umbali wa mitaa mitatu kutoka kwa Nurdin. Baada ya mwendo wa taratibu wa takriban dakika nne, alikuwa anajongea nyumba ya Nurdin, nyumba ndogo yenye vyumba vitatu na sebule. Nyumba hiyo ilikuwa inabeba familia ya watu wanne tu, yeye Nurdin, mkewe, mtoto wao Hadija, na msichana wa kuwasaidia kazi za ndani.
Huku akijiandaa kumshitua na kumshangaza Nurdin au mkewe kama watakuwepo muda ule, Walari aligonga hodi.
Alikuja kufungua mlango msichana wa kazi aitwaye Mariam. Kwa jinsi Walari alivyochongeka kwa kukonda, yule msichana alimwangalia kama anayemfananisha kupita matundu ya geti la chuma na kidogo asite kufungua kwa sababu ilikuwa marufuku kumfungulia mtu asiyemtambua. Kama si kujitambulisha kwamba yeye ni Walari aliyekuwa jela baada ya kugundua kilichokuwa kinamsumbua yule msichana, pengine Mariamu asingemfungulia kabisa mlango.
"Mariam, umenisahau. Kumbe basi ninatisha. Mimi ni baba Ashraf," akamwambia yule msichana wakati akiingia ndani.
Yule msichana mdogo alimkaribisha kiti na haraka haraka akamletea juisi ya nanasi kutoka kwenye friji.
"Baba Hadija na mama Hadija hawapo?" Akauliza Walari.
Mariamu akamjibu kwamba bado wako shughuli zao, Baba Hadija akiwa kazini kwake benki na mkewe kwenye biashara zake za kutengeneza nguo aina ya batiki.
"Tena nimesikia asubuhi wakisema watapitia hospitali jioni hii kutazama mgonjwa. Mimi nilidhani wanayepita kumwangalia ni wewe. Wewe hukua hospitali?"
"Nidyo nilikuwa hospitali lakini nemetoka," akajibu Walari ambaye alikuwa amefunga kuharisha na kujihisi amefanikiwa kupona ule ugonjwa mbaya huku akishusha tumboni kwa kasi ile juisi tamu ya nanasi iliyochanganywa na parachichi kwa mbali.
Baadaye Mariam akaendelea na shughuli zake uani akimwacha Walari akipitisha macho kwenye magazeti yaliyokuwa chini ya meza ndogo iliyoko kwenye sebule nadhifu ya Nurdin.
Ingawa magazeti mengi yalionekana ni ya nyuma kidogo lakini Walari alifurahi kuyasoma kwa sababu muda mrefu alikuwa hajatia gazeti machoni na alikuwa hajui vizuri mambo mengi yaliyokuwa yametokea nchini mwake katika kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja alichokuwa jela.
Nusu saa baadaye Mariam alikuwa keshamaliza kutayarisha chakula, ugali kwa samaki wa kukaanga na kumtengea Walari mezani.
Mwandishi huyo alikula sana chakula hicho kitamu, ambacho alikuwa hajawahi kukila toka ahukumiwe kifungo.
Baada ya chakula kile, Walari alihisi usingizi na kumuomba yule msichana amfungulie chumba cha wageni ili ajipumzishe.
Saa moja kasorobo jioni, Walari alikuwa anashituka usingizini. Alihisi kwamba bila shaka mama Hadija na mumewe walikuwa wamesharejea kutoka kwenye shughuli zao hata kama walikuwa wamepitia hospitali kumtazama ambako alihisi bila shaka waliambiwa kafa.
Alitoka nje ya chumba hicho kuelekea sebuleni ambako yule binti, Mariamu, alimjulisha kwamba baba na mama Hadija walikuwa hawajarejea.
Aliketi kwenye sofa ndefu pale sebuleni na kuendelea kusoma magazeti yaliyokuwa chini ya meza ndogo. Akiwa anaendelea kusoma magazeti yale ya nyuma, ghafla mawazo yake yalihamia kwa mwanae mchanga ambaye kwa sasa alikuwa akilelewa na mama yake Walari kule kijijini kwao baada ya kuchukuliwa kutoka kituo cha kulelea watoto wasio na wazazi ambako alipelekwa na wauguzi wa hospitali ya Bulibuli.
Alijikuta akitamani kumuona mwanae huyo mdogo haraka. Sasa akajipangia kwamba ikiwezekana kesho yake aende kijijini kwao kumuona mwanaye huyo mchanga ambaye wakati akikamatwa na hadi kufungwa, alikuwa hajamtia machoni.
Wakati akiwa katika lindi kali la mawazo, Walari alishituka pale aliposikia mtu anagonga mlango.
Itaendelea...

Nimeshushia na cocacola baridi kabisaaa asubuhi asubuhiiGereza la Kifo - 52
Mtunzi - HAMISI KIBARI
ILIPOISHIA
Aliketi kwenye sofa ndefu pale sebuleni na kuendelea kusoma magazeti yaliyokuwa chini ya meza ndogo. Akiwa anaendelea kusoma magazeti yale ya nyuma, ghafla mawazo yake yalihamia kwa mwanae mchanga ambaye kwa sasa alikuwa akilelewa na mama yake Walari kule kijijini kwao baada ya kuchukuliwa kutoka kituo cha kulelea watoto wasio na wazazi ambako alipelekwa na wauguzi wa hospitali ya Bulibuli.
Alijikuta akitamani kumuona mwanae huyo mdogo haraka. Sasa akajipangia kwamba ikiwezekana kesho yake aende kijijini kwao kumuona mwanaye huyo mchanga ambaye wakati akikamatwa na hadi kufungwa, alikuwa hajamtia machoni.
Wakati akiwa katika lindi kali la mawazo, Walari alishituka pale aliposikia mtu anagonga mlango.
Endelea...
Wakati huo ilikuwa saa moja na kitu usiku. Giza lilikuwa limeshatanda kila sehemu.
Mariamu, alitoka kasi kuelekea mlangoni kufungua. Sekunde chache baadaye, watu waliokuwa wanagonga hodi waliingia. Alikuwa Nurdin na mkewe, mama Hadija.
Wote walipatwa na bumbuazi walipofika sebuleni na kumkuta Walari akiwa maeketi huku akitabasamu baada ya kuwaona.
Tena mama Hadija alitaka kupiga kelele akidhani ameona mzimu kama siyo msukule.
"Vipi, mbona mmeshikwa na mshangao.
"Ni wewe kweli, Walari, au tunaota," akauliza Nurdin akiwa bado kasimama katikati ya sebule huku bodo uso wake ukionyesha mshangao mkubwa.
"Ni mimi jamani. Ketini tuongee. Ni hadithi ndefu."
Ukiona miujiza ndiyo hii. Ni wewe kweli Walari?" Mama Hadija naye akauliza akiwa bado anatetemeka. Inaonekana dhahhiri alipatwana mshtuko mkubwa.
"Jamani kaeni chini tuongee. Mlipitia hospitali, siyo?"
"Ndiko tunakotoka na..."
"Najua mmeambiwa nimekufa, siyo?" Akadakia Walari akimkata kauli Nurdin.
"Ndiyo, tuliambiwa umekufa. Tumekwenda hadi chumba cha kuhifadhia maiti kuthibitisha, tukakuta jina lako kwenye kitabu cha watu waliokufa. Hivi sasa tulikuwa tunapanga namna tutakavyoshughulikia mazishi yako, na hasa tulikuwa hatujui taratibu za kuzika mtu aliyefia jela. Je, gereza litatupa tumzike wenyewe ama inakuwaje," akasema Nurdin akiwa anaketi kwenye kochi moja mkabala na lile alilokuwa ameketi Walari huku sasa uso wake ukichangamka.
Baada ya wanandoa hao kuketi, huku mama Hadija akionekana bado ana utando wa mkanganyiko kwenye uso wake, Walari alianza kusimulia kilichotokea.
Alielezea namna alivyofuatwa na mfanyakazi wa Masunju, ambaye pia ni hawara yake na kumweleza mpango aliousikia wa kumuua. Akawaeleza namna msichana huyo alivyomsikitikia hadi akaamua kwenda kumweleza ili kama anaweza kufanya lolote kujinasua na kifo afanye hivyo.
Akawasimulia namna alivyohangaika hadi alipoonana na mhudumu wa chumba cha maiti na kufanikisha mpango wa kumtorosha wodini baada ya kufanya udanganyifu kwamba kafa.
"Tena ilikuwa bahati Nyamagwila kuwahi kidogo, kwani dakika chache baada ya kunipiga sindano ya usingizi na kuonekana nimekufa, wale watu wa magereza wakawa wamefika. Walipoambiwa nimekufa wakaamini. Niamshukuru saa Mwenyezi Mungu," akasema Walari.
Nurdin na mkewe sasa walimwelewa Walari na nyoyo zao zikatulia, lakini swali sasa likawa namna Walari atakavyoishi katika hali hiyo.
"Sasa utajificha wapi ili isifahamike kwamba hujafa? Kwa sababu inatakiwa upotee angalau kwa miaka miwili hivi," akahoji Nurdin.
"Cha msingi ilikuwa kuokoka kifo. Hilo tutalipanga baadaye," akajibu Walari.
*************************************
Hatimaye kulikucha Walari akiwa nje ya gereza kwa kutoroka. Hiyo ilikuwa ni siku ya Jumatatu, siku ambayo rufaa ya Walari ilikuwa inakuja kwa hukumu.
Ingawa alikuwa na uhakiwa wa asilimia nyingi za ushindi, lakini ilikuwa inawezekana pia kushindwa rufaa yake. Swali, alilokuwa akijiuliza ni endapo akishindwa rufaa yake huku akiwa ametoroka gerezani angeishije?
“Lakini la msingi ni hili lilitokea, la kujiokoa na kifo. Hayo mengine nitayakabili kadri yatakavyokuja,” alijisemea.
Asubuhi hiyo, Madenge Marare, ambaye tayari alikuwa ameshaelezwa na Nurdin kuhusu Walari kutoroka wodini, alipitia nyumbani hapo ili waandamane kwenda mahakamani, na pia alikuwa na hamu ya kuongea mawili matatu na Walari.
Mama yake Walari, yeye walipanga kukutana naye huko huko mahakamani.
Mwanamke huyo ambaye alikuwa amelazimika kuuza baadhi ya mashamba yake ili kugharimia rufani ya Walari, huku Madenge na Nurdini wakimpiga jeki, alikuwa hana habari yoyote kuhusu Walari kutoroka jela. Hata hivyo, Mama Walari alijikuta akibaki na sehemu kubwa ya fedha hizo baada ya Wakili kusema angelimtetea Walari bure kabisa.
Alfajiri siku hiyo ya Jumatatu, Walari alikuwa ametaka kwenda kijijini kwao, ili kuwaeleza wazazi wake kilichotokea na kumuona mwanae mchanga, lakini Nurdin na mkewe wakamzuia kwanza.
Wakamwambia kwamba ilitakiwa kwanza ajifiche sana, wakati wakitazama upepo unavyokwenda kwani anaweza kuonekana na kushitakiwa kwa kosa la kutoroka gerezani, hasa ikizingatiwa hawakujua hukumu ingekuwaje.
Madenge Marare alipowasili kwa Nurdin asubuhi, yeye alikuwa na mawazo mchanganyiko. Alipongeza hatua ya Walari kujinasua na kifo lakini akaonya asionekane kwani inaweza ikafahamika na hata kuandikwa kwenye vyombo vya habari, hali inayoweza kusababisha ajikute na kesi nyingine.
"Kama zingefanyika juhudi za wewe kuepuka kifo lakini ukawa bado hospitali au hata gerezani ingekuwa kitu kizuri sana kwa sababu leo naamini kwa asilimia 100 utashinda rufaa na kuwa mtu huru... Lakini hakuna neno, hata kilichotokea si kibaya kwa vile kilikuwa lazima kifanyike kuokoa uhai wako," akasema Marare.
Baadaye Marare na Nurdin waliondoka kwenda mahakamani kusikiliza rufani ya Walari kwa kutumia pikipiki. Walari alibaki nyumbani hapo akisikilizia kitakachotokea huko mahakamani.
Saa nane na nusu mchana, Walari alikuwa akitoka kwenye chumba cha wageni ambako alikwenda kujipumzisha baada ya kuhisi usingizi. Haukupita muda, mama yake aliingia akiwa ameandamana na Madenge Marare.
Uso wa mama yake ambao ulikuwa unaonyesha furaha wakati wanafunguliwa mlango na Mariamu, ulisinyaa kidogo baada ya mama huyo kumtia mwanae machoni. Hii ni kutokana na afya mbaya aliyokuwa nayo bado. Lakini mwalimu huyo mstaafu alijikuta akumkumbatia mwanae kutokana na kuhakikisha kwamba yule aliyekuwa mbele yake ni mwanae ambaye kuna wakati aliamini ni mtu atakayefia jela.
Baadaye Marare alimpa mkono Walari na kumpongeza wakati mama yake akiwa ameshindwa cha kuongea kutokana na furaha. Nurdin alikuwa amepitia kazini kwake baada ya hukumu.
"Hongera sana ndugu yangu. Ingawa taarifa za mahakama zimeonyesha umekufa, lakini hakimu aliendelea kutoa hukumu ya rufaa yako na kukupa ushindi. Umeshinda rufaa yako, kwa hiyo, ingawa wewe unajulikana kama mfu lakini uko huru," akasema Marare.
"Hakimu amesema nini wakati akisoma hukumu?"
"Amesema mwenzie wa mahakama ya mwanzo alikosea sana katika hukumu yake, kwa sababu kwa jinsi alivyopitia mwenendo wa kesi ulivyokuwa, kulikuwa hakuna ushahidi wa kukutia hatiani kwa makosa ulioshitakiwa nayo. Isitoshe hakimu pia ameshangaa adhabu uliyopewa kwamba ilikuwa kubwa sana, kwani yalikuwa ni makosa madogo tu yenye adhabu ya kifungo kisichozidi mwaka mmoja, kulipa faini ama vyote kwa pamoja," akajibu Marare.
"Asubuhi nilisikitikia kitendo chako cha kutoroka ukiwa bado uko jela," akaanza kusimulia Marare," lakini pia nimeona manufaa yake. Kuna kila dalili kwamba Masunju angekata rufaa kupinga hukumu ya leo kama kusingekuwa na taarifa kwamba umekufa."
"Ndugu yangu Marare, kwa kweli wewe pamoja na Nurdin, na mama yangu, ninawashukuru sana kwa jinsi mlivyopigana kiume hadi kuniokoa na kifungo cha uonevu. Isingekuwa juhudi zenu ningefia jela. Kwa kweli sina maneno mazuri ya kuelezea namna ninavyowashukuru," akasema Walari.
"Wala usijali. Hili lilikuwa jukumu letu na kwa kweli kama tusingelitekeleza tusingekwepa lawama. Sisi sote tuna furaha kuona tumefanikisha kitu tulichokipigania," akajibu Marare.
"Vipi, waandishi wa habari hawakuwepo mahakamani. Wasije kesho wakaandika kwamba nimekufa," akauliza Walari.
"Niliona waandishi wawili pale mahakamani, lakini hawajui kama kulikuwa na hii kesi ya rufaa, kwa hiyo tumejitahidi kuwakwepa. Hakuna mwandishi aliyeingia kwenye chumba cha mheshimiwa hakimu wakati wa hukumu," akajibu Marare.
"Vipi, Masunju alifika kortini kusikiliza hukumu?"
"Alikuwepo ofisa mmoja wa magereza ambaye ndiye nilimsikia nje akiongea na wakili wao kwamba kulikuwa hakuna haja ya kumkatia rufaa mtu ambaye keshakufa," akajibu Marare.
"Nina mashaka, Masunju anaweza akawaambia jamaa wa gazeti la Upekuzi kwamba nimekufa."
"Ngoja tusubiri Juma