Bishop Hiluka
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 7,147
- 14,711
- Thread starter
- #101
Itaendelea...
Hahaha! Yupo bize na kazi...Haki at times namchukia walari my foot jitu halijaseto vizuri kichompeleka kiwandani nini?! Bnaee asiniumize moyo acha waliue hes so mean n selfish ameacha kwenda kuona mtoto wala kaburi mbio kiwandani ana roho kubwa na akome sitamuhurumia tena na amkome sam odoyo
Gereza la Kifo - 35
Mtunzi - HAMISI KIBARI
ILIPOISHIA
Kulikuwa na harufu mbaya na nzito katika chumba hicho kidogo kiasi kwamba kichwa kilianza kumuuma sana Walari huku akipiga chafya kila baada ya muda mfupi. Kulikuwa na harufu ya haja ndogo na kubwa pia na Walari alishindwa kujua kama kuna mtu alikuwa kajiharishia humo ndani ya selo, ingawa kila wakati aliona mahabusu wakipiga makelele kuita askari awasindikize kwenda kujisaidia pale wanapobanwa na haja nje ya selo hiyo ingawa pia kulikuwa na mtondoo kwa ajili ya haja ndogo.
Baadaye alisikia mahabusu mmoja aliyekuwa akitazama nje kwenye dirisha dogo la selo hiyo akiuliza kama kulikuwa na mwandishi wa habari mule ndani.
Walari alinyanyuka na kwenda pale dirishani na kusababisha mahabusu wengi kumtumbulia macho.
Endelea...
Pale kwenye dirisha hilo lililosilibwa kwa nondo alikuta mwanamke mmoja kasimama na alipomwangalia vizuri akakumbuka kwamba ni yule mwanamke mfanyakazi wa Halmashauri ya Manispaa, aliyemfuata kuongea naye siku alivyopigwa na wafanyakazi wa Halmashauri hiyo wanaofanyakazi ya kuzika maiti zisizotambuliwa na ndugu.
"Kaka habari ya leo," akamsalimu yule mwanamke.
"Nzuri dada, habari za siku nyingi."
"Nzuri tu... Pole. Nilisikia kwenye vyombo vya habari kwamba ulivamiwa na majambazi, kisha nikasikia baadaye mkeo alifariki dunia kutokana na hilo tukio. Pole sana."
"Asante sana, ndiyo hali ya dunia."
"Mbona uko humu kaka? Unajua miye nilikuwa hapo nje nikashangaa kuona umefungwa pingu na polisi kisha unaingizwa humu. Nimekaa nikitafakari kwa muda mrefu hadi nikaamua kuja kukuona nijue kulikoni."
"Haya yote yanatokana na mambo ya kazi kama wale jamaa wa Manispaa walivyonipiga," akaanza Walari na kuendelea kumweleza mwanamke yule kwamba kuna kitu alikuwa anafuatilia katika kiwanda cha sabuni na mafuta kilichoko kusini mwa Bulibuli na ndiko akakamatwa na sasa kabambikwa hadi kesi ya bangi.
Yule mwanamke alimsikitikia sana mwandishi huyo kwa masahibu hayo yaliyomkuta. Walari alimuomba amdhamini mwanamke huyo aliyemfahamisha kwamba naye yuko mahakamani pale kwa ajili ya kesi ya madai ya talaka.
Alimweleza harakaharaka kwamba mumewe amekuwa akimnyanyasa sana hasa baada ya kupata nyumba ndogo.
"Ugomvi wetu mkubwa ni kwamba amepata mwanamke mmoja baamedi ambaye amekuwa akimfundisha mapenzi ya ajabu ambayo anayaleta hadi kwangu... Miezi sita sasa hajanipa unyumba," akasema mwanamke huyo pale dirishani bila kujali kwamba mahabusu wengine nao walikuwa wanasikiliza.
Mwanamke huyo alikubali kumdhamini kwani kwa bahati alikuwa na kitambulisho cha kazini kwake ambacho kinakubalika.
"Lakini wanaweza kutaka wadhamini wawili. Itakuwaje sasa?" Akauliza mwanamke huyo.
"Kijikesi chenyewe hiki sidhani kama watahitaji wadhamini zaidi ya mmoja."
"Hata hivyo, usihofu. Kuna dada mmoja hapa tunafanya naye kazi nitamuomba tukudhamini, najua atakubali. Mimi kesi yangu imeshaahirishwa hadi wiki tatu zijazo."
"Kwa kweli nitashukuru sana dada kwani suala hili la dhamana lilikuwa linaniumiza kichwa. Kwa kweli ninakushukuru sana kwa sababu hakuna ndugu yangu anayejua kama nimekamatwa na niko huku."
Baadaye askari mmoja alikuja kuchukuwa mahabusu wawili na kumuondoa huyo mwanamke.
Saa sita na nusu mchana kesi ya Walari iliitwa kwa hakimu na yeye akatolewa mahabusu chini ya ulinzi wa polisi mmoja.
Kesi yake iliyofanyikia chumbani kwa hakimu, ilishuhudiwa na watu wachache tu akiwemo yule mwanamke aliyeahidi kumdhamini akiwa pamoja na mwenzake mmoja ambaye sura yake ilikuwa ngeni kwake.
Walari alihisi kwamba huyo ndiye aliyetajiwa na mwanamke huyo wa Manispaa kwamba angemuomba amdhamini Walari kama wangetakiwa wadhamini wawili.
Walari alisimama kizimbani tayari kwa kusomewa shitaka, akapepesa macho huku na huko lakini hakuona mwandishi yeyote pale mahakamani. Alikuwa anaamini kwamba aliwajua karibu waandishi wote wa Bulibuli.
Lakini kwa vile alikuwa na uhakika wa mtu wa kumdhamini hakuhofu sana kukosekana kwa mwandishi.
Karani wa mahakama alisoma jarida la kesi mbele ya hakimu, kisha askari mmoja wa kike mwenye cheo cha Inspekta Msaidizi wa Polisi akaanza kumsomea shitaka Walari.
Yule mwendesha mashitaka alimwambia Walari kwamba anakabiliwa na makosa manne. Kosa la kwanza ni kuingia kwa jinai katika eneo la jeshi kwa lengo la kutenda uhalifu. Akataja kosa la pili kwamba ni kukutwa na bangi na kosa la tatu ikiwa ni kuuza dawa za kulevya aina ya bangi katika eneo la jeshi. Kosa la nne alilosemewa Walari ni kuongea na mfungwa bila kibali cha mamlaka husika, kinyume cha sheria.
Walari alikanusha mashitaka yote.
Baada ya Walari kukana mashtaka, hakimu alisema dhamana ya mshtakiwa huyo iko wazi lakini akauliza upande wa mashtaka kama ulikuwa na pingamizi lolote.
Mwendesha mashitaka, Inspekta Msaidizi wa polisi, alinyoosha mkono, akasema ana kitu cha kuiomba mahakama. Akadai kwamba upande wake ulikuwa unapinga dhamana kutokana na waraka ambao alidai umetoka kwa ofisa Upelelezi wa Mkoa (RCO) huku ukiwa na saini yake ambao ulidai kwamba mshtakiwa ni mtu hatari kwa sababu alipokamatwa katika eneo la jeshi alisema maneno yenye kuvunja amani na kwamba akiwa nje anaweza pia kuvuruga ushahidi ambao ulikuwa umekamilika.
"Hata hivyo tunaomba wiki moja tu, mheshimiwa, ili kesi hii ije kwa kusikilizwa na hivyo tungeomba mshtakiwa awe ndani kwa kipindi hiki kifupi sana kwani tunaamini akiwa nje atasababisha kuvunjika kwa amani," akasema yule mwendesha mashtaka baada ya kusoma waraka aliodai unatoka kwa RCO.
Walari alinyoosha mkono haraka na hakimu akampa nafasi ya kusema. Mwandishi huyo alipinga hoja ya mwendesha mashitaka kwa sababu ilikuwa ya kipuuzi.
"Kwa kweli mheshimiwa hakimu, nashindwa kuelewa hoja kwamba nitaharibu ushahidi nikipewa dhamana. Haingii akilini kwamba kwa kesi kama hii nitaharibu ushahidi kwa namna gani, tena ushahidi ambao upande wa mashitaka umesema umeshakamilika. Naomba mheshimiwa utupilie mbali hoja ya upande wa mashtaka na kunipa dhamana ambayo ni haki yangu ya kikatiba. Haya si makosa ambayo hayana dhamana."
Walari, akiongea haraka haraka, pia alimwambia hakimu kuhusu mateso na manyanyaso ya kinyama aliyopewa na askari wa magereza wakati alipokamatwa kwa uonevu na baadaye polisi.
Hakimu aliinama kwenye meza na kuandika mambo fulani kwa sekunde kadhaa, kisha akamuuliza Walari kama atakuwa na shahidi katika kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa wiki moja ijayo.
Walari alimjibu kwamba hategemei kuwa na shahidi. Kisha hakimu huyo akaandika maneno mawili matatu katika jarida lililokuwa mbele yake.
Huku chumba cha mahakama hiyo kikawa kimetulia tuli, hakimu alinyanyua kichwa chake, akapepesa macho huku na huko, kisha akasema: "Ombi la upande wa mashtaka limekubaliwa. Mshitakiwa utakaa mahabusu kwa wiki moja hadi kesi hii itakapokuja hapa mahakamani kwa kusikilizwa."
Wakati Walari akishangaa pamoja na wanawake wale wawili waliokuwa tayari kumdhamini, sekunde haikupita kabla askari polisi wawili waliokuwa katika chumba hicho cha mahakama hawajamfuata pale alipokuwa kasimama kizimbani haraka. Walimkwida suruali na kumpeleka tena kwenye mahabusu ya gereza hilo kusubiri karandinga la kumpeleka katika gereza la Bulibuli ambako ndiko mahabusu wengi walikuwa wakipelekwa. Hii ilitokana na sababu za mji wa Bulibuli kutokuwa na gereza kwa ajili ya mahabusu, hivyo gereza la rufaa, ambalo lilikuwa limejazana kuliko kawaida lilitumika tena kama mahabusu.
Mwandishi huyo wahabari, huku akiwapungia mikono wanawake wale wawili waliokuwa wakimwangalia kwa huruma, alikokotwa mpaka kwenye kijichumba kile kidogo na kuungana na mahabusu wengine ambao walikuwa wakisubiri karandinga kupelekwa katika makazi ya kifungoni.
Walari alibaki akiwaza, huku kichwa kikimuuma namna alivyonyimwa dhamana kwa kile ambacho yeye aliona ni kuonewa tu. Pia alilaumu namna polisi walivyokataa hata kumpa nafasi ya kuongea na wale wanawake, pengine angepata mwanya wa kuwaelekeza kwa rafiki yake, Nurdin, wakamweleze matatizo yaliyomfika.
Saa 11 na nusu, jioni, karandinga lililokuwa limejazana sana mahabusu kiasi cha kutopata nafasi ya kujigeuza huku wengi wakiwa wananuka kwa uchafu, lilikuwa ‘linawatapika’ watu hao katika gereza la Bulibuli.
Ni kiasi cha miezi minne na ushei iliyokuwa imepita, toka Walari alipoingia kwa mara ya kwanza katika gereza hilo kubwa kwa umbo lakini lisilotosha kulingana na idadi ya wafungwa na mahabusu. Wakati safari hiyo ya kwanza aliingia kwa ujanja wake kama mwinjilisti, sasa aliingia humo kama mahabusu.
Alipatwa na mshituko mkubwa na moyo ulikuwa ukimwenda mbio sana. Hali hiyo, kuchanganya na hasira pamoja na njaa, alijisikia kama mtu anayetaka kuzirai. Kichwa pia kilikuwa kikimuuma sana mwandishi huyo wa habari na kuwa katika hali ya kutoamini macho yake. Kwamba anaingia gerezani kama mahabusu alikuwa kama vile anaota.
Alikumbuka kwamba anaingia katika himaya ya mtu ambaye alikuwa amejaribu mara mbili kutaka kumuua, lakini ikawa inashindikana. Hii ni himaya ya mtu ambaye aliamini kwamba katika majaribio ya kumuua alisababisha kifo cha mkewe na sasa mwanae alikuwa hoi hospitali.
Walari alikuwa haamini kwamba anaingia katika gereza alilokuwa amepania kutumia kalamu yake kujaribu kuufumbua macho umma ufahamu fika namna hali ilivyo mbaya ndani ya kuta ndefu za gereza hilo kubwa. Alirudia kumlaumu sana aliyekuwa mhariri wake, Sam Odoyo kwa kumsababishia madhila hayo.
Usikose kufuatilia mkasa huu wa kusikitisha na kusisimua...
Haki at times namchukia walari my foot jitu halijaseto vizuri kichompeleka kiwandani nini?! Bnaee asiniumize moyo acha waliue hes so mean n selfish ameacha kwenda kuona mtoto wala kaburi mbio kiwandani ana roho kubwa na akome sitamuhurumia tena na amkome sam odoyo
Wakuu, Tater, moneytalk, marybaby, nipo2, ram, kisukari, the_legend, Smart911, Madame S, carbamazepine, Astelia, culture girl, Prisoner of hope, Mine eyes, kuku mweus, Thad, hearly, Shunie, moneytalk,Tumosa, hearly, nipo2, Katavi , Mine eyes, Kudo, swahiba92, ludist, Toyota escudo, Clkey, macson3, Thad, boga la kiangazi, macson3, LEGE, Smart911, Richard irakunda, skfull, mzigo ndiyo huo, mshindwe wenyewe...
Kaz gani akwende zake huko yani simpendi na asisumbue wenzie asubiri hukumu afungwe stori yake iishe anajua watu tunaumizwa na mangapi af nalo lije kutuletea uzwazwa wakeHahaha! Yupo bize na kazi...
Haya ndio mambo BishopSasa leo nazimwaga 'kama loote' mhangaike nazzo hadi Jumatatu...
Walari kwa nini unaendelea kumfatilia masunju atakuuaGereza la Kifo - 31
Mtunzi - HAMISI KIBARI
ILIPOISHIA
Mwandishi huyo aliendelea kukaa kwenye gogo moja la mwembe ambalo bila shaka lilitumika kama meza ya wateja wanaotaka kulia chakula nje ya kibanda cha mama lishe hao bila kuona mfungwa mwingine akitoka nje. Badala yake aliona watu waliovaa kiraia wakiingia na kutoka. Kuna walioingia kwa miguu na kutoka wakiwa mikono mitupu ama vifurushi na kuna waliongia na magari na wengine kwa baiskeli.
Endelea...
Baadaye alisogea karibu na binti mmoja aliyekuwa akasaidiana na mama mmoja wa makamo kugawa chakula kwenye banda hilo. Akainama na kumuuliza binti yule kama ilikuwa rahisi kuongea na mfungwa katika kile kiwanda au hata kuingia ndani kama huna shughuli yoyote inayoeleweka.
"Mule ndani kuna wafungwa na vibarua wengine raia. Kama unataka kuingia wewe nenda tu."
"Mh! Yule askari mlangoni ataniruhusu kweli kuingia?"
"Kama shida yako ni kuingia tu kuona wafungwa ndani, wewe jifanye kama vile unakwenda kununua mafuta. Si mule wanauza mafuta hata galoni moja moja! Nenda kama unaulizia bei kisha utaona wafungwa," akasema huyo msichana.
Walari alimshukuru msichana huyo, akavaa ujasiri wake wa siku zote na kuanza kujongea geti kubwa la chuma la kuingia katika kiwanda hicho ambacho sehemu moja ilikuwa inatengeneza sabuni za kufulia na kuogea na nyingine ikitengeneza mafuta ya kula. Alikumbuka ahadi moja ya Masunju wakati akimtaka asiandike habari kuhusu gereza lake ilikuwa ni ya kumpa sabuni na mafuta ya bure kila wiki.
Alifika getini na kumweleza askari magereza aliyekuwa akilinda hapo kwamba alikuwa na shida kiwandani humo. Askari yule alimruhusu kuingia baada ya kusikia kwamba Walari alitaka kununua mafuta, na hasa kujua bei, na pia kuona kama atapunguziwa kidogo bei ili akamjulishe bosi wake aliyemtuma.
Walari alipopita kwenye mlango mdogo wa kuingilia waenda kwa miguu ndani ya kiwanda hicho baada ya kuruhusiwa akaona wafungwa wawili wakifyeka mbele yake, umbali wa kama mita 40 kutoka pale getini.
Bila shaka wafungwa hao walikaribia kumaliza vifungo vyao kwani hawakuwa na ulinzi wowote na sehemu moja ya ukuta wa kiwanda hicho, si mbali sana kutoka pale getini, ilikuwa fupi sana kiasi cha kutoweza kumzuwia mtu kuruka, hata kama ni mtoto mdogo, na kwenda zake.
Walari alimsalimia mmoja wao ambaye alikuwa jirani na barabara alikokuwa anapita. Yule mfungwa aliitikia salamu, kisha akasimama.
"Samahani 'braza', nisaidie hela ya sigara," akaomba yule mfungwa.
Walari alijipapasa mifukoni kisha akatoa noti ya Sh 2000. Yule mfungwa akaifuata akiwa bado kashikilia kwanja mkononi mwake.
"Vipi bwana mzee, naona wewe nguo yako bado nzuri kabisa tofauti na wafungwa wengine. Niliwahi kuona wengine nguo zao zimechanikachanika," akamsemesha Walari.
"Huu uzi (nguo) nimeupata kwa ujanja wangu tu, lakini kwa kweli, braza, hali kule gerezani ni mbaya sana. Wafungwa hawana nguo na wengi wanalazimika kubaki kwenye selo bila kutoka nje kwa sababu hawana nguo."
"Hivi hiki kiwanda ni cha magereza?" akazidi kumuuliza yule mfungwa.
"Kilikuwa cha magereza halafu kikabinafsishwa. Mimi nasikia magereza ina hisa ndogo sana sasa hivi. Walijiuzia wenyewe mabosi wa magereza, yaani hao hao waliokiua pamoja na polisi. Siku hizi kinashamiri," akajibu yule mfungwa.
"Hivi wafungwa mnaruhusiwa kuvuta sigara?"
"Waruhusu, wasiruhusu sisi tunavuta tu. Wewe hujui kule gerezani maafande ndiyo wanatuuziaga sigara, bangi hadi madawa ya kulevya?"
"Wewe. Unasema kweli? Yaani madawa ya kulevya na bangi vinauzwa gerezani?"
"Kibao tu, na askari ndiyo biashara zao."
"Samahani, tunaweza kuendelea kuongea au maaskari hawaruhusu?" akauliza Walari.
"Hakuna matatizo hata kidogo. Wewe zoza (sema) tu, maaskari wote hapa washikaji tu hawana noma (matatizo). Miye sichungwi. Mwezi ujao namaliza kifungo."
"Nasikia hapa kuna sehemu kuna kemikali zinawaunguza sana watu, ni kweli."
"Tena kuna mshikaji majuzi aliteleza na kutumbukia kwenye kemikali akaungua hadi viungo vya uzazi. Bahati nzuri alikuwa kabakiza wiki moja tu kumaliza kifungo, huenda huko aliko anatibiwa, lakini sidhani kama atakuwa ana uwezo tena wa kushiriki tendo la ndoa. Na angekuwa gerezani yule, wiki hii angezikwa," akajibu mfungwa yule.
Wakati akitaka kuhoji zaidi kuhusu tukio hilo, Walari alisikia gari ambayo muda mfupi ilikuwa ikifunguliwa geti na yeye kudhani ni moja ya magari yaliyokuwa yanaingia kiwandani humo kuchukua bidhaa na kutoka, ikisimama nyuma yake.
Aligeuka na kugundua kwamba ilikuwa ni gari alilokuwa anatumia Mkuu wa Jeshi la Magereza. Alishtuka na uoga kumwingia alipomuona Masunju akiteremka. Roho ilizidi kumdunda kutokana na mtu huyo ambaye yeye alimtuhumu kujaribu mara mbili kutaka kumuua kumkuta katika himaya yake. Hata hivyo, alijikaza na kutulia bila kuonesha kwamba alikuwa akitetemeka kwa ndani kusibiri litakalotokea.
Masunju ambaye kwenye gari hilo alikuwa na askari wawili, mmoja akiendesha gari na mwingine akiwa ameketi kiti cha nyuma kama mlinzi wake, alimtuma yule aliyekuwa kiti cha nyuma kumwita askari aliyekuwa mlangoni.
Mkuu huyo wa gereza akaanza kumfokea askari aliyekuwa getini kwa nini kamruhusu Walari kuingia ndani na kisha kumruhusu kuongea na mfungwa.
Askari huyo alijitetea kwamba alimruhusu raia huyo kuingia kiwandani baada ya kujitambulisha kwake kama mteja aliyetaka kununua mafuta.
"Kwa nini sasa unaruhusu raia kuongea na mfungwa," akazidi kufoka Masunju ambaye povu la hasira lilikuwa likimtoka mdomoni wakati anaongea.
Askari huyo alibaki kimya kwani alimuona Walari akiongea na mfungwa huyo aliyekuwa anakaribia kumaliza kifungo chake lakini akajua wanaombana sigara tu, kitu ambacho ilikuwa ni kawaida kwa raia kupiga soga na wafungwa wa aina hiyo.
Afande Masunju aligomba hadi kufikia kumnasa kibao askari huyo, kitendo ambacho kilimsikitisha sana Walari.
"Haya, kamata huyu mshenzi tutafute gari tumpeleke anakostahili, amezidi kunifuatafuata," akatoa amri afande Masunju.
"Nimekosa nini, afande?" akauliza Walari.
"Mshenzi mkubwa. Hujui kosa lako. Nasema kamata huyu mtu. Mweke hapo getini kisha tukamfunze adabu."
Askari mmoja aliyekuja na Masunju alimfuata Walari na kumkwida suruali kwa nyuma, lakini Walari akahoji tena kisa cha kukamatwa huku akiisukuma mbali mikono ya askari huyo. "Nina kosa gani miye?"
Kitendo kile kiliwatia hasira zaidi askari magereza hao na ndipo dereva na yule ofisa mlinzi wa afande Masunju, wakamvamia.
Wakampiga ngwala hadi akaanguka chini na alipojaribu kunyanyuka akajikuta katikati ya mvua ya kwenzi, makofi ya mgongoni na mateke pamoja na kitako cha bunduki aliyokuwa nayo askari wa getini. Hali hiyo ilimfanya mwandishi huyo wa habari aendelee kubaki chini.
Masunju aliagiza askari aliyekuwa getini afunge geti na asifungulie mtu na kisha akaagiza askari wake wamfunze adabu Walari.
Askari wale, mmoja alirudi kwenye gari na kuchomoa kirungu na kuungana na wenziye waliokuwa wakiendelea kumpiga.
Mwandishi huyo wa habari alisimamishwa, akakalishwa chini akarushwa kichura chura na kupigwa virungu mikononi hadi akawa hoi. Kirungu au mateke vilikuwa havichagui mahala pa kutua. Alipigwa kichwani, mgongoni, kwenye mikono, kwenye pua na hata sehemu za siri.
Baadaye, huku Walari akiwa hawezi kusimama tena kutokana na kipigo, alimsikia afande Masunju ambaye alikuwa kasimama pembeni akipiga simu ya mkononi na maongezi yakaonyesha kwamba alikuwa anaongea na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Bulibuli.
Walari, ambaye alikuwa anaendelea kugaragazwa chini kwa mateke, makofi na kwenzi, akasikia Masunju akisema
"huyu mshenzi tunamleta sasa hivi. Tungemtupa uwani kwetu lakini anaweza kuwa kawaaga washenzi wenzake."
Sasa Masunju alitoa amri ya kumweka Walari ndani ya gari waliokuwanayo na kama nyuki askari wale watatu wakamkamata, wakambeba msobemsobe na kumtupa kwenye gari ile ya kisasa aina ya Landrover, mithili ya mzigo wa mihogo. Askari na mkuu wao waligeuza gari haraka haraka, kumaanisha kwamba safari ya kiwandani hapo ilikufa na kuanza safari mpya ya kuelekea sehemu ambayo, kwa mujibu wa maongezi ya simu, Walari alihisi ni polisi.
Ingawa alijua anaonewa, sasa alianza kuhisi kitu kibaya zaidi. Hasira za Masunju zilikuwa si za kawaida, na sasa alipata hisia kwamba Masunju anaweza kutumia hatua hiyo kumuondoa duniani baada ya majaribio mawili ya kumuua kushindikana.
“Heri nife tu kuliko kukaa kimya nikiona mtu huyu anatumia madaraka yake kujinufaisha na kuumiza wananchi wenzangu. Damu yangu ninaamini haitapotea bure. Katika kupigania haki lazima watu wa kujitoa mhanga kama mimi wawepo,” alijisemea Walari.
Itaendelea...
Haki at times namchukia walari my foot jitu halijaseto vizuri kichompeleka kiwandani nini?! Bnaee asiniumize moyo acha waliue hes so mean n selfish ameacha kwenda kuona mtoto wala kaburi mbio kiwandani ana roho kubwa na akome sitamuhurumia tena na amkome sam odoyo





