Riwaya - Gereza la Kifo

Riwaya - Gereza la Kifo

Rip Zuhura
Gereza la Kifo - 24

Mtunzi - HAMISI KIBARI

ILIPOISHIA

"Ninapenda sana kutoa damu hata dakika hii, lakini si unajua tena siku hizi damu zetu haziaminiki? Na kusema kweli naogopa sana kupima. Majibu yakionyesha kwamba ninao (Ukimwi), si nitakufa kihoro?"
"Kwanza ninakusahihisha. Kwa vile ninakuona una afya njema, ukipima, kinachoweza kuonekana ni virusi na sio Ukimwi. Ukimwi ni ugonjwa ambao humpata mtu aliyeambukizwa virusi baada ya kupita muda. Lakini ninachojua mimi ukitoa damu, kama itakuwa chafu, ni siri ya hao waliokupima, nawe au mtu mwingine hatojua chochote, labda kama wewe mwenyewe utataka uambiwe. Na hata kukwambia, kama utapenda kujua, kama mambo si mazuri, hawakurupuki tu, mpaka wakuandae kisaikolojia kupokea majibu hayo. Hilo litafuatiwa na kukupa ushauri nasaha. Nurdin kupima afya yako ni jambo jema sana rafiki yangu."

Endelea...

"Wewe ulishapima? Mbona wayajua haya!"
"Ninapima kila mara. Hata hivi mimi na mke wangu kwa sababu ya ujauzito tulishajipanga tena kupima. Inshallah, akipona janga hili tutapima, ingawa itakuwa kama ushahidi tu kwani wote tunajiamini tuko fiti. Ninamwamini mke wangu kwa kuheshimu ndoa na mimi ninajiamini pia."
Walari aliondoka akimwacha Nurdin akienda kutoa damu.
Ilikuwa asubuhi hiyo atume habari ya gereza EBC lakini badala yake alipofika kwenye ofisi yake mpya, mwandishi mwenziye ambaye ilikuwa ahamie makao makuu ya nchi muda wowote, alilazimika kumhoji na kutuma habari kuhusu kuvamiwa na majambazi. Hata hivyo, Walari katika mahojiano na mwandishi huyo wa EBC aliepuka kumtaja Masunju kama mtuhumiwa namba moja kwa sababu bado hakuwa na ushahidi wowote, na isitoshe alikuwa bado anafuatilia vipengele fulani katika habari yake kuhusu gereza.

******************************

Saa tisa na nusu mchana, madaktari waliokuwa wakimfanyia upasuaji Zuhura walitoka chumba cha upasuaji, huku Walari, Nurdin na waandishi wenziye watatu pamoja na mpangaji mwenzake wakiwa pale nje ya chumba hicho.
Madaktari hao wakiwa na nyuso za huzuni hawakusema chochote, isipokuwa dakika ileile Walari akaona wauguzi wakipita haraka wakimsukuma mkewe kwenye kitanda cha matairi kuelekea chumba cha wagonjwa mahututi.
Hali ile ilimshtua sana Walari na wenzake aliokuwa nao. Alimfuata daktari mmoja na kutaka kujua maendeleo ya mkewe.
"Bado tunamtibu lakini tumeshamfanyia operesheni na tayari mtoto, kwa vile hajatimiza miezi yake, keshapelekwa kwenye chumba maalumu. Lakini mkeo hali yake ni mbaya sana na ndio hivi unaona tuko katika kujaribu kuokoa maisha yake. Mapigo yake ya moyo hayaendi vizuri."
"Kajifungua mtoto gani?"
"Ni mtoto wa kike. Mtoto anaonekana hana matatizo yoyote," alijibu daktari yule.
Baadaye Walari alielekea kwenye chumba cha mapokezi kuulizia kama kuna mtu alikuwa kalazwa katika hospitali hiyo baada ya kutobolewa na kitu chenye ncha kali kama vile mkuki.
Huko aliambiwa kwamba kulikuwa hakuna mtu kama huyo, na kisha akaonyeshwa kitabu cha orodha ya watu waliolazwa katika siku hizo.
Yule mtu wa mapokezi pia alimwambia kwamba kulikuwa na askari wawili ambao pia walikuja kuulizia mtu wa aina hiyo lakini hawakumpata.
"Nimesikia wanasema kuwa wanaelekea kwenye hospitali za watu binafsi labda akawa kalazwa huko," akajibu mtu yule wa mapokezi.

****************************

Saa 12:15 Asubuhi, Walari akiwa amembeba mwanaye, Ashraf, alikuwa anawasili katika hospitali ya Bulibuli.
Kwa siku tatu mfululizo hali ya mkewe ilikuwa bado mbaya. Licha ya jeraha la risasi na jeraha la mshono, matatizo ya moyo yalikuwa yakimsumbua sana na mara kadhaa alikuwa akipoteza fahamu.
Kutokana na hali hiyo, Walari alikuwa ameshindwa kufanya kazi na karibu muda wote alikuwa anashinda hospitali au polisi.
Baada ya kuomba ulinzi polisi akidai kwamba anahofia maisha yake, polisi walikuwa wamempuuza na hivyo Nurdin akawa amemshauri ahamie kwake kwa njia ya kificho, isijulikane analala wapi, kwani walihisi kwamba kama shambulio lile lilikuwa la 'kigaidi' na si ujambazi, basi wahusika wangeweza kuwa wanatafakari kumvamia tena Walari kwa lengo la kumuua. Hata safari zake za kwenda hospitali alikuwa akizifanya kwa uangalifu mkubwa. Alikuwa akivaa miwani ya jua na kofia pana.
Katika siku hizo tatu, Walari alianza kugundua kitu kingine. Polisi walionekana hawafuatilii chochote na wala walikuwa hawataki kumhoji Masunju ambaye Walari alimtaja kama mtuhumiwa namba moja.
Polisi sasa walibadili msimamo. Wakawa wanadai kwamba tukio lile wanaliona kama la ujambazi tu, na hivyo kulikuwa hakuna maelezo yoyote ya maana ya kuwafanya polisi wafikie hatua ya kumhoji ofisa wa juu wa serikali, kama Mkuu wa Gereza kwa tuhuma za eti kumfanyia ujambazi mwandishi huyo wa habari.
Polisi walimwambia kwamba kama angekuwa ana uthibitisho wowote, kama vile Masunju kudondosha kitambulisho chake cha kazi katika eneo la tukio, pengine wangefikiria kumhoji lakini hakuwa na ushahidi wa aina hiyo.
Wakamweleza kuwa hawawezi kufanya kazi kwa hisia ama kuridhisha tu matakwa yake.
Alipowaambia kuwa ana ushahidi wa maneno aliyomrekodi ofisa huyo wa magereza, polisi wale wakacheka wakasema huo hautoshi kuthibitisha kwamba yeye Masunju atakuwa kamkodia majambazi na kwamba anaweza kuiga sauti yake na kuirekodi.
Pia walimjibu kwamba hawajasikia mtu yeyote aliyelazwa hospitalini kwa kupigwa mkuki. Lakini Walari aligundua kuwa polisi walikuwa hawajazungukia mahospitali ya binafsi kama walivyoahidi siku walipokwenda hospital ya mkoa.
Wauguzi wawili walimkaribisha mwandishi huyo ambaye asubuhi hiyo hakuwa ameandamana na rafiki yake Nurdin isipokuwa shemejiye, yaani mke wa Nurdin, ambaye alikuwa kabeba kifungua kinywa kwa ajili ya mgonjwa wao.
"Leo mgonjwa wako kalala na hali mbaya zaidi," akasema muuguzi mmoja baada ya Walari kuwasili pale wodini.
"Usiku wa leo kwa kweli hakulala na pengine asubuhi hii tutamrudisha kule kwenye wodi ya wagonjwa mahututi ambako ataungwa kwenye vifaa vya kumsaidia kupumua."
Taarifa hizo za muuguzi alizisikia kama zinachoma maini yake kama upanga. Jana yake alikuwa ameona matumaini ya mkewe kupona yanarejea baada ya kuonekana ana hali njema na akiongea kidogo, tofauti na siku za nyuma, hali iliyosababisha atolewe kwenye wodi ya wagonjwa mahututi na kuletwa ile ya kawaida.
Walari alikwenda kwenye kitanda cha mkewe na kumkuta akigugumia kwa maumivu. "Nakufa. Nakufa... Nakufa bila kumbeba mwanangu mchanga," akawa analalamika mwanamke huyo Walari akiwa kainama pale kitandani.
Mwandishi huyo wa habari, akiwa na mwanae Ashraf pembeni, alimshika mkewe kifuani kisha akamwita kwa sauti ya chini.
Mkewe ambaye alikuwa akionekana mwenye maumivu makali alifumbua macho na kumtazama mumewe.
"Mume wangu, sidhani kama nitapona... Nasikia vibaya sana. Ninakuomba uwaangalie watoto. Naomba sana uchague mwanamke mwingine wa kuoa ambaye atajali watoto wetu. Usikurupuke kuoa mwanamke atakayetesa watoto. Usiache ibada. Usiache kuniombea kila unaposwali," akasema mwanamke yule kwa taabu.
"Usiseme hivyo, Zuhura, Inshallah Mwenyezi Mungu atakunusuru na kifo," alisema Walari akiwa bado kamwinamia mkewe na kuomba dua pamoja na kumsomea mkewe Qur’an ili Mwenyezi Mungu Mlezi amfanyie wepesi. Pembeni mwake akiwa kasimama mke wa Nurdin, maarufu kama mama Hadija, sasa akiwa ametua chini ule mzigo wake wa kifungua kinywa aliokuja nao kwa ajili ya mgonjwa huyo.
Zuhura alitaka kuongea kitu lakini akashindwa. Jasho likawa linamtoka kwa wingi kwenye paji la uso.
Alinyoosha mkono kwa taabu na hatimaye akafanikiwa kusema, "mwanangu Ashraf, sogea nikuage...."
Alimshika kichwani mtoto huyo ambaye alikuwa amesogea karibu na kitanda cha mama yake. Akataka kuongea maneno mengine lakini akashindwa. Akafanikiwa kusema maneno ya Kiarabu Laa ila ha-illallah (hakuna apaswaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu mmoja) Akashtuka kidogo na mara mkono wake ukalegea ukiwa bado juu ya kichwa cha mwanae.
Walari alimshika kifuani. Moyo ulikuwa umesimama kusukuma damu kuashiria kwamba uhai ulikuwa umemtoka mwanamke huyo mswalihina. Tena kifo hicho kilikuwa kimempata siku chache kabla hajaanza kufunga mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Walari hakutaka aamini kwamba Zuhura alikuwa ameshindwa kupambana na kifo. Aliamini kwamba muda wowote Mwenyezi Mungu anaweza kufanya maajabu yake mkewe akarudishiwa uhai wake.
Mwandishi huyo alibaki ameduwaa akitazama mwili wa mkewe pale juu ya kitanda huku mkono wake ukiwa bado umenyooka juu ya kichwa cha mtoto wao Ashraf.
Alijaribu kumwita. Mwanamke yule hakuitika. Akamwita huku akimtikisa lakini mwanamke yule hakuitika.
"Mpenzi Zuhura, usife tafadhali... Zuhura usife," akawa anasema Walari akiutingisha mwili wa mkewe pale kitandani. Lakini Zuhura, akiwa kama aliyelala usingizi hakuitika wala kutikisika.
Walari akaanza kulia kwa sauti. Yule mke wa Nurdin (Mama Hadija) alishajua kwamba Zuhura amekata roho. Alijua pia kwamba shemeji yake keshachanganyikiwa na haamini tukio lile lililotokea mbele yake.

Itaendelea...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole walari jamani inasikitisha watoto wadogo jamani mama kawaacha

Masikini walari roho yake bado inatafutwa
Gereza la Kifo - 27

Mtunzi - HAMISI KIBARI

ILIPOISHIA

Kikubwa kilichokuwa kinampa faraja ni habari za mwanae aliyezaliwa kabla ya muda kuendelea vizuri hospitalini huku shemeji yake, Mama Hadija, akiwa ndiye amegeuka mithili ya mama mzazi wa kichanga hicho na ilikuwa imepangwa kwamba akitoka hospitali basi Mama Hadija angeendelea kumlea.
Siku moja aliingia kulala kwenye banda lenye vyumba viwili upenuni mwa nyumba kubwa walimokuwa wakilala wazazi wake, banda alilokuwa akilala kila siku, kama kawaida.
Alipania asubuhi yake aamkie kwenye kufuatilia suala la mgogoro wa wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu na serikali.
"Hili suala la wachimbaji wadogowadogo lisinichukulie muda sana. Nikiona linahitaji muda mrefu nitaliacha kwanza na kisha nitalirudia baada ya kukamilisha kabisa habari hii ya gereza," akajisemea usiku huo wakati akisaka usingizi.

Endelea...

Akiwa kalala fofofo usiku huo na mwanae Ashraf pembeni mwake, alishituka usingizini na kugundua kuwa hali ilikuwa si ya kaiwada katika chumba hicho kidogo alichokuwa amelala.
Naam, alipepesa macho haraka na kuona dirisha na sehemu moja ya paa ikiwaka moto mkali na kugundua kwamba kumbe ndio ilikuwa kisa cha moshi ule mzito mle ndani ambao ndio uliomshitua toka usingizini.
Alikirupuka na kukimbia na mwanae mlangoni ili watoke nje lakini alipogusa mlango ukawa haufunguki na ilionekana umefungwa kwa nje. Aliutikisa tena kwa nguvu lakini haukufunguka. Akakumbuka hoja ya mpangaji mwenzake ambaye pia alifungiwa nje kwa komeo katika tukio lile la ujambazi kwamba ni heri milango ya nyumba iwe ni yenye vitasa vya kisasa ambavyo mtu huweza kufungia kwa nje.
Huku akiona moto ukiwa umeshashika mlango huo, Walari alijaribu kuupiga teke lakini haukufunguka, na kumbe, tofauti na alivyofikiria mwanzo, mlango wa mbao za kijichumba hicho ingawa ulitokana na mbao za kawaida tu aina ya mpodo lakini ulikuwa imara.
Alimrudisha mwanae kitandani na kujaribu kufungua kijidirisha kingine cha chumba hicho ambacho kilikuwa hakijashika moto lakini akagundua kwamba ilikuwa si rahisi kupenya humo kwani pia kilikuwa kimesilibwa kwa wavu mnene.
Sasa alianza kupiga kelele za kuomba msaada akirukia ule mlango wa mbao uliokuwa unaendelea kuwaka moto kwa mateke ili kuufungua. Moto pia ulikuwa unazidi kutapakaa juu ya paa huku joto kali na hewa nzito ikizidi kujaa ndani ya chuma.
Alikumbuka maelezo aliyowahi kuyapata kuhusu hatua ya kwanza kuchukua kama nyumba ulomo ndani imeshika moto kuwa ni kulala chini ambako kunakuwa na hewa kuliko juu au katikati ya chumba. Hivyo alimlaza mwanae chini ya sakafu huku yeye akiendelea kung’ang’ana kupiga teke ule mlango.
Hali hiyo ilizidi kumtisha mwandishi huyo wa habari mithili ya usiku ule aliovamiwa na majambazi.
Alifanikiwa kuubomoa huo mlango bila kuunguzwa na moto lakini alipoangalia nyuma yake akaona mbao za paa zenye moto zikamwamgukia mwanae pale chini.
Kabla mwanae hajaungua sana Walari alifanikiwa kumnyakua katikati ya moto na kukimbia naye nje.
Huko nje alikutana na kundi la watu, wakiwemo wazazi na dada zake waliokuwa wamelala kwenye nyumba kubwa ambao ndio kwanza walikuwa wanawasili eneo la tukio kujaribu kuzima moto ule. Vijana wa pale mtaani ambao walifika katika eneo la tukio kutokana na makelele ya Walari waliingia kazini kuzima moto kwa mchanga ili usiteketeze kabisa kibanda kile.
Vijana wawili wanaosoma shule waliokuwa wamelala kwenye chumba cha pili cha kibanda hicho walifanikiwa kutoka bila kuungua na kusalimisha mali zao kadhaa, hususani madaftari na vitabu. Inaonekana moto huo ambao mpaka wakati huo chanzo chake hakikujulikana ulianzia katika chumba alichokuwa amelala Walari na mwanae. Pia haikufahamika bado ni kwa vipi mlango wa chumba chake ulifungwa kwa nje.
Walari alikuwa kababuka ngozi, mikononi lakini mwanae alikuwa kaungua sehemu za mgongoni na sasa alikuwa amelazwa nje juu ya mkeka akilia kwa maumivu ya moto. Huduma ya kwanza aliofanyiwa yeye na Walari ilikuwa ni pamoja na kumwagiwa maji ya baridi katika maeneo ya majeraha, hatua iliyopunguza kidogo joto.
Hilo lilikuwa tukio la pili, katika kipindi kifupi sana kumuona mwanae akiwa na hali mbaya kiasi hicho. Machozi yalimbubujika Walari kama bomba kila alipokuwa akimwangalia mwanae.
Wanakijiji, kwa kushirikiana na baba yake walikimbia kwa mtu mmoja aliyekuwa akimiliki gari, aina ya pick-up, umbali wa mwendo wa kama dakika kumi kutoka pale kwao na kuikodi.
Baadaye Walari na mwanae walikimbizwa katika hospitali ya misheni Kurugongo na kuanza kuhudumiwa.
Walari alitibiwa na kuondoka lakini mwanae ambaye alikuwa kaungua zaidi alilazwa. Madaktari walisema pengine mtoto huyo angeweza kuhamishiwa katika hospitali ya rufaa Bulibuli kama ingebidi na hivyo alikuwa si wa kurudi nyumbani siku hiyo kutokana na kuungua karibu ngongo wote na maeneo ya shingo.
Walari alirudi nyumbani, huku bado akiuguza majeraha na kuanza kutafakari chanzo cha moto ule na hasara yake na kumwacha hospitali mama yake aliyekuwa anaendelea kumwangalia mjukuu wake.
Alipowasili nyumbani alikuta kundi la watu likiendelea kuajabia namna kibanda kilivyoungua. Wengi walisema kwamba kibanda hicho kingekuwa kimeezekwa kwa nyasi kama zilivyo baadhi ya nyumba nje kidogo ya mji mdogo wa Kurugongo hali ingekuwa mbaya zaidi na pengine asingelitoka mtu katika kibanda hicho ambacho wakati kinashika moto kulikuwa na watu wanne waliokuwa wamelala.
Walari alipowasili aliitwa na baba yake sebuleni, kwenye nyumba yao kubwa ambako mzee huyo alikuwa akiongea na watu wanne, wote wanaume.
Walari aliingia sebuleni, akawasalimu watu wale ambao pia walimpa pole na kisha baba yake, Mzee Hassan Saire, akamtaka aketi chini awasikilize akisema wale jirani zake, walikuwa wameleta habari inayotoa mwanga kidogo kuhusu tukio la moto.
"Mwanangu, hili pia ni tukio la hujuma na bila shaka bado unawindwa na wabaya wako ili uuawe," akasema Mzee Chirukile.
Wale watu walimwambia Walari kwamba moto ule ulisababishwa na kijana mmoja ambaye wanakijiji walimuona usiku huo akikimbia na dumu ambalo wanahisi kwamba alilitumia kuwekea mafuta ya taa au petroli ambayo ndiyo yaliyotumika katika kuunguza banda alilokuwa kalala Walari na mwanae huku chumba cha pili katika banda hilo kukiwa kumelala vijana wengine wawili wanaosoma shule.
Wale watu wakasema kwamba wanakijiji baadaye walimuona kijana huyo akirukia kwenye gari moja iliyokuwa imeegeshwa mbali kidogo na kisha ikaondoka kwa kasi.
"Kwa bahati nzuri kijana huyo ambaye tunamtuhumu kuunguza nyumba hii tunamfahamu na watu wanasema walimuona mitaani akiuliziaulizia kama kuna mtu kafa kwa ajali ya moto," akasema mmoja wa watu wale ambaye ni ndugu yao wa ukoo.
"Huyu mtu hatuwezi kumfuatilia na kumripoti polisi?" Akauliza Walari akionekana ni mwenye hasira nyingi.
"Ndiyo maana tumekuita. Kwa vile taarifa hii tayari iko polisi, na kwa vile hali yako inaonekana si mbaya sana sasa, ninafikiria uondoke na hawa watu waliotusaidia kupata hizi habari ili mwende polisi sasa hivi, ikiwezekana huyu mtuhumiwa akamatwe. Nitakuandikia jina la askari mmoja pale kituoni nadhani unamfahamu, Ally Sumuni, yule binamu yako, mtoto wa dada yangu binamu. Nashangaa hajafika hapa pengine hana habari kama umefiwa na mkeo. Nilimpelekea taarifa mara mbili lakini wajumbe hawakumkuta kwani alikuwa safari ya kikazi. Siku hizi kahamishiwa hapa kutoka mkoani. Yeye atatusaidia sana kama atakuwepo," akasema Mzee Saire.
Walari na wanaume wawili miongoni mwa wale wanne waliondoka kwenda kwenye kituo cha polisi cha mji mdogo wa Kurugongo ambacho kilikuwa umbali mrefu kidogo kutoka nyumbani kwao.
Baada ya mwendo wa kama dakika 45 kwa miguu walikuwa wamewasili katika kituo hicho cha polisi.
Walimuulizia Sumuni kama alikuwepo pale kaunta. Wakajibiwa kwamba askari huyo alikuwa mapumziko baada ya kumaliza siku tatu za kufanya kazi katika zamu ya usiku.
Lakini kwa vile kijana huyo anaishi kambini katika nyumba za polisi zilizoko eneo hilo la kituo, waliamua kwenda nyumbani kwake kwanza baada ya kuelekezwa, kabla ya kuripoti kwa askari wengine. Imani iliyojengeka vifuani mwao ni kwamba heri mtu siku hizi upate askari anayekufahamu anaweza kukuhudumia vizuri kuliko asiyekufahamu ambaye kumtoa kituoni tu anataka pesa. Rushwa ilikuwa inasumbua kila mahala!
Walari na kundi lake waligonga hodi katika mlango wa chumba cha askari huyo na kumkuta akiwa amejifungia. Baadaye waligundua kwamba alikuwa na msichana mmoja ambaye walihisi ni hawara yake tu, kwani kwa mujibu wa maelezo ya Mzee Saire, askari huyo alikuwa hajaoa.
Waligundua kuwepo kwa msichana huyo baada ya Sumuni kufungua mlango na msichana mmoja aliyekuwa kavaa upande mmoja wa khanga kuchungulia mlangoni kisha akarudi ndani.
Sumuni alipofungua mlango wa chumba anachoishi katika jengo hilo lenye askari ambao hawajaoa na ambao wamepewa chumba kimoja kimoja, akina Walari wakagundua kwamba walikuwa wamemkatisha askari huyo usingizi pamoja na starehe yake na hawara wake huyo.

Je, nini kitaendelea? Usikose kufuatilia mkasa huu wa kusisimua...
 
Back
Top Bottom