Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,054
- 463,937
Atapanda alichovunaHahahaa... Inasemwa "zubaa uzikwe"...
Atapanda alichovunaHahahaa... Inasemwa "zubaa uzikwe"...
Mama tafadhari punguza ku quote uzi mzima,unatupa taabu tunaotumia simuMhariri kampiga bao walari
Gereza la Kifo - 18
Mtunzi - HAMISI KIBARI
ILIPOISHIA
"Yote unayosema ni kweli kabisa, bosi, kwamba mambo hayo yanahitaji ushahidi mkubwa. Lakini mimi naona ushahidi wote ninao kama kuna mtu atapingana na tulichoandika. Kama nilivyokueleza kwa njia ya simu kila kitu kipo," akasema Walari.
Baada ya kusema vile Walari alitoa kile kimtambo cha kunasia sauti na kumfungulia bosi wake ili asikie mazungumzo yake na mahabusu akiwa gerezani.
Tiririka nayo...
"Licha ya mimi mwenyewe kushuhudia baada ya kuingia gerezani na hawa niliyowarekodi, mmoja wa mtu ambaye alikaa mahabusu muda mrefu na ndiye wa kwanza kunipa habari hizi naweza kumpata na ninaamini, hata kama tutafikishwa wapi atasema hali halisi anayoifahamu na ndiyo tutakayokuwa tumeandika. Mchungaji Alex Kabongo ambaye tuliingia naye gerezani pia ni shahidi na yeyé nilimrekodi na utasikia sauti yake. Mkuu, hii ndiyo hali halisi ya gereza la Magamaga. Hali ni mbaya sana," alisema Walari na kuongeza kuwa kuna uwezekano wa kupata hata watu 10 waliofungwa katika gereza hilo na kutoa ushahidi wa hali halisi. Kadhalika alimwonyesha baadhi ya picha alizozipiga kwenye simu, picha ambazo alimtumia pia ingawa hazikuwa na ubora.
Mhariri alisikiliza kanda ile kidogo lakini baada ya sentensi mbili tatu za mfungwa mmoja, akaonekana hana hamu zaidi ya kusikiliza na kumwambia Walari auzime, inatosha.
Walari alitoa kitabu chake kidogo na kumtajia baadhi ya majina ya wafungwa waliokufa katika kipindi cha miezi sita pamoja na namba zao.
"Kama nilivyokwambia kwa njia ya simu, mkuu, nilitaka tutaje idadi tu na ikitokea mtu anapinga ndipo tunachapisha hii orodha ya majina pamoja na namba zao za jela."
Mhariri aliangalia yale majina juu juu kisha akasema kwamba tatizo kubwa la habari yao hiyo linabaki katika kipengele cha kumtuhumu zaidi mkuu wa gereza, hivyo ilitakiwa kumhoji kwa kina zaidi na kumsikiliza namna anavyojibu tuhuma hizo.
"Pia lazima tujue kwamba gereza hili ni dogo sana lakini wanajitahidi kutunza wafungwa wengi kuliko uwezo wa gereza... Lazima tulifikirie na hilo pia, ukiachilia mbali kuwa na ushahidi.”
"Lakini mkuu," akaanza Walari, "Kama umeisoma habari yote nimefanya mahojiano na mkuu wa gereza na kila alichosema nimeandika."
"Sawa, nimeona. Hata mimi nilitaka nimhoji kidogo maswali kwa sababu tuhuma nyingine, kama hili la kuwa na duka la dawa na kwamba dawa za wafungwa pengine anapeleka humo, linahitaji ushahidi zaidi."
"Mimi nilidhani umeshaonana naye, bosi?" Akauliza Walari.
"Bado sijaonana naye. Nimekwenda ofisini kwake sijamkuta. Nimeacha maagizo tuonane jioni hii."
"Yaani tuseme hamjafanya mahojiano tu ama hamjaonana kabisa?" Akauliza tena Walari.
"Hatujaonana kabisa. Toka nimewasili hatujaonana," akajibu mhariri huyo, jibu ambalo lilimshangaza sana Walari, kwani mchana ule pale uwanja wa ndege aliwaona kwa macho yake wakipanda katika gari moja. Tena gari hiyohiyo ya mkuu wa gereza ndiyo ilikuwa tena imemleta mhariri huyo pale ofisini kwake na bila shaka ilikuwa ikimsubiri.
Walari alitamani kumuumbua lakini akasita.
Akamgeukia tena, "Kwa hiyo tuseme bosi ukimaliza uchunguzi wako ndipo habari hii itachapwa, na hii nadhani itakuwa wiki ijayo, siyo?"
"Kwanza lazima niseme ninakupongeza sana kwa hatua uliyofikia. Pili, kama ulivyosema, tutaichapa hii habari tukiona sasa inafaa kuitoa na haitatuletea matatizo yoyote. Na pia lazima niseme, kama tutaona itatuletea matatizo, heri tuachane nayo na kushughulikia habari nyingine."
“Tuachane nayo! Kwa nini bosi?”
“Kwani habari ni ya gereza tu. Zipo habari nyingi za kuandika zihusuzo wananchi. Ni lazima kama chombo cha habari tuangalie pia usalama wa waandishi wetu,” akajibu Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Upekuzi, Sam Odoyo.
********************
Kama alivyolala akiwa mnyonge, Walari aliamka asubuhi, siku ya Jumapili akiwa mnyonge pia.
Sentensi ya mhariri wake kwamba, "lazima niseme, kama tutaona (habari hii) itatuletea matatizo heri tuachane nayo...." ilikuwa inamhuzunisha sana kila akiikumbuka.
Yeye bado aliamini kuwa habari ile aliyokuwa ameichunguza kwa kina sana na bado alikuwa akiendelea kuichunguza kuhusu gereza la Magamaga ilikuwa haina matatizo yoyote, na kama isingechapishwa gazetini jamii kubwa pamoja na wakubwa wa serikali huko makao makuu ya nchi wasingefahamu chochote kuhusu namna maisha ya wafungwa na mahabusu yalivyo katika hatari kubwa kwenye gereza hilo.
Pia kitendo cha mhariri kumwambia kwamba alikuwa hajakutana na mkuu wa gereza wakati si kweli, kilimshangaza na asijue nini hasa lengo lake. Kwa kiwango fulani alianza kupata hisia alizokuwa nazo rafiki yake Nurdin kwamba kama habari hii haikutoka wiki iliyopita, pengine mhariri wake alishaahidiwa hongo na mkuu wa gereza.
Lakini kwa jinsi alivyokuwa akimheshimu na kumwamini mhariri, Sam Odoyo, hakutaka aamini kwamba kitu kama hicho kinaweza kutokea.
Kwanza mhariri alikuwa na shida gani? Ingawa naye alikuwa kaajiriwa na taasisi iliyokuwa inamiliki gazeti lao hilo ya Sauti ya Wanyonge Foundation iliyokuwa pia ikiendesha gazeti lingine la uchunguzi kwa lugha ya Kingereza la The Friday Observer, lakini alikuwa amejitosheleza kwa vitu vingi.
Walari alikuwa na habari kwamba mhariri wao, licha ya gari la kampuni alilokuwa anatembelea, yeye mwenyewe anamiliki magari mawili binafsi, alikuwa na ng'ombe kama sita hivi wa kisasa, shamba la mazao mbalimbali nje ya jiji la Bandaria na kubwa alikuwa na nyumba nzuri. Isitoshe mkewe pia alikuwa akimiliki duka zuri la vipodozi na nguo za kike na mara kadhaa akisafiri kwenda China na Dubai kununua bidhaa.
Toka jana yake Zuhura alikuwa ameshagundua mabadiliko ya mumewe na alimuuliza mara mbili kama anaumwa lakini Walari akawa anajibu kwamba hana tatizo lolote.
Hata hivyo, mwanamke huyo alikuwa anahisi sababu ya mumewe kuwa katika hali ile. Ni habari ya gereza kutotoka gazetini. Mara mbili alitaka kumuuliza kwa nini habari haikutoka lakini akasita, akihisi angezidi kumchanganya zaidi mumewe.
Kwa vile ni siku ya Jumapili ambayo huwa anapumzika baada ya mumewe kumaliza kilichokuwa kinampeleka kanisani, ilipofika saa tatu kasorobo ndipo Walari alikuwa anajinyanyua kitandani tayari kwa kuoga.
Alipomaliza kujimwagia maji, alikwenda kwenye sebule yake ndogo kusubiri chai. Hiyo ilikuwa ni siku ambayo mama yake mzazi alikuwa anatarajia kuondoka kurudi kijijini.
Akiwa pale sebuleni akiongea na mama yake, mtu mmoja akapiga hodi. Alikuwa muuza duka ambalo liko jirani na ofisi yake ambamo huwa anapokelea simu.
Alimkaribisha kijana huyo muuza duka ambaye kwa bahati walikuwa wakiishi jirani katika eneo hilo la uswahilini.
Alimkaribisha chai, lakini yule kijana aitwaye Abdul alijibu kwamba asingekaa.
"Nimekuletea taarifa tu halafu ninarudi kazini," akasema huku amesimama karibu na mlango wa kutokea nje.
"Unasemaje Abdul?" akauliza Walari.
"Kuna mtu mmoja anaitwa Sam Odoyo, anahitaji kuongea nawe. Amesema ni muhimu sana na anapiga simu yako ya mkononi hakupati."
"Yeah! Ni bosi wangu toka makao makuu. Na simu ndo nimeamka na kuiweka kwenye chaji... Yuko wapi?"
"Kapiga simu hapo dukani kwangu, akaniambia uwashe simu yako ya mkononi atakupigia kwani ni muhimu sana. Kanikodia usafiri wa pikipiki kukuona"
"Sawa... Ngoja niwashe simu. Kwa vile hii simu ni ya kwangu binafsi na si ya ofisi hawezi kunilaumu kwa kuizima," alisema. Walari aliangalia saa yake. Ilikuwa saa nne kasorobo, asubuhi.
Alinyanyuka ili kumsindikiza yule kijana aliyekataa kunywa chai na kuacha kikombe chake cha chai mezani kikifuka mvuke huku pembeni mwa kikombe hicho kukiwa na vitumbua vitatu vilivyonunuliwa na mkewe asubuhi hiyo kwa jirani yao. Pia kulikuwa na mihogo aliyochemsha mkewe asubuhi hiyo kuongezea kitafunio.
Kabla hajarejea ndani, mara akaja mgeni mwingine ambaye aliegesha pikipiki yake upenuni mwa nyumba hiyo aliyokuwa amepanga Walari, nyumba ya kizamani iliyokuwa na wapangaji wawili. Mwenye nyumba alikuwa akiishi shamba.
Mgeni huyo alikuwa rafiki yake mkubwa, Nurdin. Walari alimkaribisha huku akijiandaa kupambana kwa maneno ya rafiki yake huyo baada ya habari yake kutotoka gazetini.
Wakati Nurdin akishuka kwenye pikipiki huku Walari akiwa bado kasimama mlangoni akimtazama, alimuona akichomoa gazeti alilokuwa amelikunja na kulibana kwa mpira katika kiti cha nyuma cha pikipiki yake, kisha akajongea mlangoni huku akitabasamu.
Walari alimkaribisha ndani na alijua kwamba gazeti alilokuwa ameshikilia ni Upekuzi.
"Tuseme hii habari yako ya gereza la Magamaga imetupwa au kumetokea nini tena?" Akauliza Nurdin akiketi kabla ya salamu. Shemeji yake alimkaribisha chai.
"Shemeji nashukuru," akajibu Nurdin, "Nimeshatoka huko. Kilichonileta hapa ni hili gazeti. Jana nikashangaa nanunua gazeti sioni habari ya mumeo."
Walari alibaki kimya bila kujadili chochote. Nurdin aliuliza tena akitaka kujua ni vipi habari ya gereza haikutoka, na hiyo ni mara ya pili?
"Kama nilivyosema juzi," Walari akalazimika kujibu. "Habari hiyo ni nzito. Bado mhariri anaifanyia kazi."
Hata hivyo, Walari alisita kueleza kwamba mhariri huyo yuko mjini hapo na keshamweleza sababu za kutoichapisha habari hiyo.
Itaendelea...
Update app yako mkuuMama tafadhari punguza ku quote uzi mzima,unatupa taabu tunaotumia simu
Sent using Jamii Forums mobile app
TumefikaKama kawa, mzigo mpya unaingia asubuhi hii, karibuni mtiririke, wakuu Tater, moneytalk, marybaby, nipo2, ram, kisukari, the_legend, Smart911, Madame S, carbamazepine, Astelia, culture girl, Prisoner of hope, Mine eyes, kuku mweus, Thad, hearly, Shunie, moneytalk,Tumosa, hearly, nipo2, Katavi , Mine eyes, Kudo, swahiba92, ludist, Toyota escudo, Clkey, macson3, Thad, boga la kiangazi, macson3, LEGE, Smart911, Richard irakunda, skfull...
Pole walari na familia yakoGereza la Kifo - 21
Mtunzi - HAMISI KIBARI
ILIPOISHIA
Nilikwenda kumuona Jumatatu, siku hiyohiyo akawasiliana na wakubwa wake London, na leo ndiyo wameleta taarifa. Kesho naanza kazi rasmi na kesho hiyohiyo ninatuma habari yangu ya gereza. Jioni itasikika dunia nzima. Yule mwakilishi wao kaipenda sana hii habari ya gereza. Ingawa miye nilikuwa sipendi kufanya kazi na redio lakini hata hivyo, nashukuru kwamba habari hii itajulisha dunia nzima hali ya gereza la Bulibuli kuliko hata gazeti ambalo linasomwa nchi chache tu, sana sana ni mbili tu, hapa kwetu na majirani zetu wa kaskazini."
Zuhura hakutaka kujadili zaidi kuhusu suala hilo kwa sababu alikuwa anahisi usingizi. Alipanga kuendelea kumhoji mumewe kuhusu uamuzi wa kuacha kazi Upekuzi na kwenda EBC kesho yake.
"Samahani mpenzi, mimi nasikia usingizi sana. Nalala," alisema akijirusha kitandani na kuvuta shuka juu ya nguo yake ya kulalia aliyokuwa kavaa usiku huo.
Endelea...
"Sawa. Wewe lala. Ngoja miye nisome magazeti. Unajua leo sijapata kabisa muda wa kusoma haya magazeti. Nimesoma juujuu tu vichwa vya habari."
Mwandishi huyo alivuta magazeti matatu yaliyokuwa juu ya meza na kuanza kusoma moja wapo huku akiwa kajilaza kitandani.
Baadaye alisikia mwanae akilia kuashiria kwamba alitaka kujisaidia. Mkewe pia alishtuka kwa kilio hicho, lakini Walari akamtaka aendelee kulala.
Alinyanyuka na kwenda kwenye kitanda cha mtoto. Akamshusha chini na kumsogezea dubwasha la kukojolea. Mtoto alijisaidia kisha Walari akambeba mwanaye huyo na kumlaza kwenye kitanda chake huku akimpiga busu.
Kisha alirudi kuendelea na usomaji wa magazeti. Hata hivyo, baada ya kupitia magazeti mawili alihisi usingizi. Wakati huo mkewe alikuwa anakoroma.
Ilikuwa ni kawaida yake anapopanda kitandani kuchukua kati ya saa moja na mbili akisoma magazeti, hali ambayo mkewe alikuwa ameshaizowea japo ilikuwa inamuudhi, lakini siku hiyo Walari alisikia usingizi mapema kidogo.
Aliangalia saa yake na kugundua kwamba ilikuwa inaelekea saa tano na nusu usiku.
Alinyoosha mkono kupunguza sauti ya redio, kisha akazima taa, akijitupa kitandani pembeni mwa mkewe na kuvuta shuka.
Wakati mwandishi huyo ameshalala usingizi alishituka na kwa sekunde kadhaa hakujua nini kilichomshitua usingizini. Baadaye alisikia kama mchakato au mtu kupita nje ya dirisha la chumba chake.
Alisikiliza kwa makini lakini ule mchakato ukatulia.
Wakati akiwa kaanza tena kusinzia, alisikia kishindo kikubwa ambacho kilimshtua sana. Kishindo hicho kilifuatiwa na kingine na kingine na mara akagundua kwamba mlango wa kuingia kwenye sebule yake ndogo ulikuwa unavunjwa. Mtu akishaingia sebuleni ni rahisi kuvunja mlango wa chumba chake ambao ulikuwa si imara sana.
Mkewe naye alikuwa keshashtuka na kukaa juu ya kitanda. Mara wakasikia mlio wa risasi huko nje. Wakaingiwa uoga zaidi.
"Tupige kelele mume wangu, tumevamiwa," akanong'ona Zuhura karibu na sikio la Walari huku akitetemeka kwa uoga.
Walari alilipuka kwa makelele lakini sekunde ileile mlango wa chumba chao ulikuwa unavunjwa.
Walari na mkewe waliendelea kupiga makelele ya kuomba msaada ambayo inaonekana yalipokelewa vyema kwani kwa mbali walisikia kama milango ya nyumba za majirani nazo zikifunguliwa.
Ghafla mlio wa risasi ukasikika chumbani mwao, na Walari kama umeme akaruka na kulala chini huku akimvuta mkewe.
Mkewe naye alimfuata chini. Risasi ambazo sasa waligundua kwamba zilikuwa zinatokea dirishani zikaanza kumiminika mle chumbani uelekeo wa kitanda chao. Baada ya risasi kusikika, vurugu za kuvunja mlango wao zikakoma lakini bunduki ya dirishani ikaendelea kufyatua risasi mle chumbani kuelekea kwenye kitanda chao ambacho hakikuwa na mtu wakati huo na nyingine zikigonga ukuta.
Mtoto wao alipiga makelele pale kitandani na Zuhura akataka kunyanyuka ili amchukuwe na kulala naye pale chini, lakini Walari akamvuta mkono ili asinyanyuke. Hata hivyo, mwanamke yule akafanya nguvu na kufanikiwa kumponyoka na kunyanyuka.
Sekunde chache baada ya mkewe kunyanyuka, Walari alisikia mlio wa risasi kutoka dirishani na muda huo huo akasikia mkewe anapiga makelele ya kuomba msaada.
Mkewe na mtoto walimwangukia pale chini. Akamsikia mkewe akiugulia kwa maumivu, mwanaye pia, akiwa pale chini alikuwa akiangua kilio kikali.
Risasi ambazo nyingi zilikuwa zikipiga kitandani au kugonga ukuta zilikoma.
Mkewe aliendelea kuugulia kwa maumivu pale chini, pembeni mwa kitanda na yule mtoto sauti ilikuwa imemkauka kwa kulia.
Yeye Walari alikuwa anajiamini kwamba bado yuko salama lakini alikuwa na mashaka na mkewe pamoja na mwanae.
Alipata hali ngumu aliposikia mkewe ananyamaza kimya pamoja na mtoto, muda mfupi baada ya kusikia mlio mwingine wa risasi.
Alihisi mkewe na mwanae wamekufa, akatamani ajitokeze naye auawae.
Aliona hakuna haja ya yeye kusalimika kama mkewe na mtoto watakuwa wameuawa.
Kwa mbali alisikia vishindo vya watu wanaokimbia. Zilipita dakika kama tatu hivi bila kusikia mlio mwingine wa risasi wala kishindo chochote, iwe mle chumbani au nje ya dirisha ambako alihisi majambazi hao walikuweko zaidi ya mmoja.
Alinyanyuka, sasa akiwa tayari kukabiliana na kifo kwani aliamini mkewe na mtoto wameshakufa.
"Niueni nyiye watu. Kwa nini mniulie familia yangu? Kama mngetaka kila changu ningewapa. Si mngechukuwa TV na chochote mnachotaka kuliko kuniulia familia yangu," alisema kwa ukali akinyanyuka na kusimama pembeni mwa mwili wa mke wake katika chumba hicho kilichokuwa giza.
Alisikiliza kidogo na kugundua kwamba hali ilikuwa shwari na bila shaka majambazi hao walikuwa wameshakimbia. Alishangaa kwamba hadi muda huo kulikuwa hakuna jirani yeyote aliyejitokeza.
Walari aliwasha taa ya chumbani baada ya hali ya ukimya kuendelea kutawala. Aligundua kwamba mlango wa chumbani kwake ulikuwa umevunjwa, lakini kulikuwa hakuna dalili kwamba majambazi yale yaliingia chumbani mwake. Akahisi kuwa makelele yao yalisadia wasiingie chumbani na ndipo wakaamua kufyatua risasi kupitia dirishani.
Aliangalia chini na kumuona mkewe akiwa amelala katikati ya dimbwi la damu.
Mwanae mpendwa, Ashraf, naye alikuwa kalala katika dimbwi jingine la damu.
Wakati akijongea kuangalia hali zao, majirani sasa ndipo walikuwa wamepata ujasiri wa kufika nyumbani kwake.
Baadhi walisimama dirishani na wengi wakaingia ndani na kumkuta Walari akiwa kainama pembeni mwa mkewe. Alimgusa na kugundua kwamba alikuwa kazirai lakini bado mzima.
Alimshika pia mwanae kifuani na kugundua kwamba hata yeye alikuwa kapoteza fahamu tu.
Walari aliomba msaada wa haraka. Wale majirani wakafanya haraka kumsaidia na baaada ya dakika chache, gari ikaletwa na majeruhi hao wakakimbizwa hospitali. Gari hiyo ilikuwa ya jirani yao mmoja aliyeonekana kuwa tajiri mkubwa pale mtaani kwao uswahilini.
Walari akiwa na majirani watatu, mmoja akiwa mpangaji mwenzake, ndani ya gari hilo pamoja na dereva, walikumbuka kwamba kule hospitali wasingepata tiba yoyote kama wasingepitia polisi kwanza kuandika maelezo na kupewa hati maalumu ya kwenda nayo hospitali.
"Jamani, mimi ninajua utaratibu ndiyo huo, lakini hamuoni tutawapoteza hawa watu kama tutapoteza muda kwenda huko?" Akashauri Walari akitaka waende hospitali kwanza ambako wangejitahidi kuwashawishi madaktari na wauguzi hadi waelewe hali ilivyo na kutibu majeruhi wao.
"Tiba kwanza, mambo ya polisi baadaye," akawa anasisitiza mwandishi huyo wa habari aliyekuwa na mashaka makubwa juu ya hali ya mkewe na mtoto.
Hata hivyo, majirani wale waling'ang'ania kwamba itakuwa ni kazi bure kwenda hospitali kama hawana hati ya polisi kwani isingelikuwa rahisi wao kupokelewa na kupewa tiba.
Walari hatimaye alisalimu amri baada ya kuona hata dereva aliyekuwa akiendesha gari hilo akisisitiza kwamba, kwa tukio kama hilo, ilikuwa ni kupoteza muda na kuharibu bure mafuta kwenda hospitali bila kupitia polisi kwanza.
Saa nane kasorobo, usiku, Walari na wale wasamaria wema walikuwa wanawasili katika kituo kidogo cha polisi. Kwa eneo hilo, kituo hicho ndicho kilionekana kuwa karibu, japo ilikuwa mbali kidogo kutoka kwa Walari na bila shaka hata milio ya zile risasi ilikuwa ni vigumu kusikia na kama zilisikika basi ni kwa mbali sana.
Pale kituoni walimkuta askari mmoja tu akiandika maelezo ya watu walioaminika kuwa wazururaji ambao baadaye akina Walari waliambiwa kwamba walikamatwa na askari waliokuwa doria, askari ambao baada ya kuwakamata watu hao na kuwaleta kituoni walirudi tena na kumuacha huyo mwenzao mmoja kituoni.
Walishangaa sana kugundua hilo na wakajiuliza kama wale walioko doria hawakusikia milio ya risasi, pengine wangekurupusha majambazi yaliyokuwa yamemvamia Walari. Yule askari wa kituoni naye alijibu kwamba hajasikia mlio wowote wa risasi na akajibu kwamba inaonekana askari waliokuwa doria usiku huo walipita njia tofauti.
Walari na wenzake walimweleza askari yule kuhusu wagonjwa waliokuwa nao mle kwenye gari, lakini askari huyo asiye na cheo, aliyeonakana hana haraka, akawataka wasubiri.
Huku wao wakiwa wamesimama nyuma ya kaunta fupi ya kituo hicho kidogo, askari yule aliendelea kuwahoji wale watuhumiwa wa uzembe na uzururaji taratibu sana huku akiendelea kuandika maelezo ya watuhumiwa hao waliokuwa wameketi sakafuni.
Kila mtu alimshangaa askari huyo kwa kutoonekana kujali taarifa kwamba kikundi kile cha watu kilikuwa na wagonjwa mahututi. Ikabidi tena Walari amjie juu, tena kwa sauti ya hasira.
"Ndugu askari. Tumekwambia tuna wagonjwa mahututi, vipi?"
"Kama mngekuwa na haraka mngekuja jana. First in, first out. Nyiye si mmewakuta hawa, subirini. Kama mgonjwa ni wa kufa atakufa tu."
Itaendelea...
Dah, uko fasta! Hongera sana...Pole walari na familia yako
Asante Bishop nilikuwa online ndio maanaDah, uko fasta! Hongera sana...
Gereza la Kifo - 22
Mtunzi - HAMISI KIBARI
ILIPOISHIA
Walari na wenzake walimweleza askari yule kuhusu wagonjwa waliokuwa nao mle kwenye gari, lakini askari huyo asiye na cheo, aliyeonakana hana haraka, akawataka wasubiri.
Huku wao wakiwa wamesimama nyuma ya kaunta fupi ya kituo hicho kidogo, askari yule aliendelea kuwahoji wale watuhumiwa wa uzembe na uzururaji taratibu sana huku akiendelea kuandika maelezo ya watuhumiwa hao waliokuwa wameketi sakafuni.
Kila mtu alimshangaa askari huyo kwa kutoonekana kujali taarifa kwamba kikundi kile cha watu kilikuwa na wagonjwa mahututi. Ikabidi tena Walari amjie juu, tena kwa sauti ya hasira.
"Ndugu askari. Tumekwambia tuna wagonjwa mahututi, vipi?"
"Kama mngekuwa na haraka mngekuja jana. First in, first out. Nyiye si mmewakuta hawa, subirini. Kama mgonjwa ni wa kufa atakufa tu."
Endelea...
"Jamani tuachane na huyu mtu, twen'zetuni Central (Kituo cha polisi cha kati)" alishauri dereva wa gari walilokuwa nalo.
Walirudi kwenye gari, Mama Ashraf bado alikuwa hajitambui, lakini sasa damu zilikuwa zimekoma kumvuja sehemu ya jeraha baada ya kumpa huduma ya kwanza.
Lakini yule mtoto alikuwa ana fahamu zake, isipokuwa alikuwa analia muda wote kutokana na maumivu.
Walipofika kwenye kituo cha polisi Kati, ambako Walari alienda kwa shingo upande baada ya wenziye kumkatalia tena nia yake ya kwenda moja kwa moja hospitali, walisikilizwa haraka na kupatiwa huduma.
Baadaye wakaondoka kasi kuwahi hospitali ya mkoa. Huko nako, baada ya kuwasili, iliwachukuwa zaidi ya dakika 20 kabla wagonjwa hao hawajaanza kuhudumiwa.
Wakati mkewe anaanza kuhudumiwa wodini ilikuwa ni saa kumi na ushee usiku, zaidi ya masaa mawili toka mwanamke huyo apigwe risasi.
Walari alikuwa na mashaka makubwa kama mkewe atasalimika kifo kwani hata wakati wauguzi wanampokea pale mapokezi walionesha hali ya kukata tamaa. Iligundulika kwamba mkewe alikuwa amepigwa risasi kiunoni na alikuwa ametokwa damu nyingi sana. Kitu kingine kilichomsikitisha Walari ni maelezo kwamba hata kama akipona, kiuno kinaweza kisifanye kazi au miguu kupooza na hivyo akawa ni mtu wa kukaa muda wote mithili ya kiwete.
Daktari aliyewapokea alisema ilitakiwa mwanamke huyo aongezewe damu haraka, lakini benki ya damu ya hospitali hiyo ilikuwa haina hata tone.
Walari na wale majirani wawili pamoja na dereva walijitolea kutoa damu.
"Hata hivyo, itachukuwa muda kumwekea mgonjwa wenu damu. Si mnajua siku hizi damu haziaminiki? Mpaka zichunguzwe sana," akasema daktari huyo baada ya Walari kuona muda unakwenda bila mkewe kuwekewa damu. Wakati huo ilikuwa inaelekea saa 12 alfajiri.
Mtoto Ashraf yeye alikuwa amepata jeraha kwenye bega, kwa kile kilichoonekana kwamba alikwaruzwa na risasi. Tayari mtoto huyo alikuwa ameshashughulikiwa kwa kusafishwa jeraha na kuwekewa dawa na sasa alikuwa kalala chumba cha mapumziko akiwa ametundukiwa dripu ya maji.
Wasiwasi ulizidi kumwandama Walari kuhusu hali ya mkewe. Hata hivyo, daktari aliyekuwa akimhudumia aliwaambia warudi nyumbani na kuja kuangalia hali ya mgonjwa baadaye.
"Mbona kumeshakucha, tuje asubuhi gani tena?" Akauliza Walari akiangalia saa yake.
Lakini jirani mmoja akamkumbusha kwamba walitakiwa kuondoka kwenda polisi kituo cha Kikuu kuwachukua askari kwenda eneo la tukio mapema.
Wakiwa njiani kurudi polisi, pamoja na mtoto Ashraf ambaye alikuwa kalala, jirani mmoja alisema kwamba wakati majambazi yale yanavunja mlango wao walisikia na hadi akina Walari walipokuwa wanapiga makelele wao walikuwa nje na silaha zao duni, lakini waliogopa baada ya kugundua kwamba majambazi hayo yalikuwa mengi pamoja na bunduki zaidi ya moja.
"Sisi tulianza kuja lakini wakafyatua risasi kuelekea upande wetu, ikabidi tukimbie. Walikuwa kama majambazi sita hivi," akasema jirani mmoja, mtu wa makamo, ambaye nyumba yake inapakana na ile aliyopanga Walari.
Mfanyabiashara aliyepanga nyumba moja na Walari yeye alisema kwamba inaonekana majambazi yale yalimpania Walari peke yake, kwani yalipofika yalifunga mlango wa chumba chake na wa sebule yake kwa nje na hilo aliligundua wakati alipojaribu kufungua akidhani labda nyumba iliyokuwa inavunjwa ni ya jirani.
Alisema alipong'amua kwamba majambazi yale yako kwenye nyumba yao, hasa baada ya kusikia milio ya risasi, akalazimika yeye na mkewe kujificha nyuma ya kabati chumbani mwao.
"Hata chumba cha watoto nako walikuwa wamefungiwa kwa nje," alisema mpangaji mwenzake huyo, Ibrahim Nyamsha, ambaye katika nyumba hiyo yenye wapangaji wawili, alikuwa na vyumba viwili na sebule. Akasema baada ya hali kuwa shwari majirani waliofika kwenye tukio ndio waliowafungulia mlango uliokuwa umefungwa kwa nje kwa komeo.
"Kuna haja ya kuweka vitasa vya kisasa ambavyo haviruhusu mtu kukufungia kwa nje," akasema Nyamsha.
Nyamsha ndiye aliyekuwa na sebule kubwa na vitu vingi na mtu yeyote angefikiria kwamba kutokana na kuwa na vitu vingi, angekuwa kivutio kikubwa cha majambazi kumvamia kulinganisha na Walari.
Walifika kituoni na kuondoka na askari wawili hadi nyumbani kwa Walari kufanya uchunguzi wa tukio hilo.
Walipofika nyumbani, majirani kadhaa walikuja asubuhi hiyo, na ndipo mmoja akasema alifanikiwa kumchoma mkuki jambazi mmoja, ingawa ana hakika hakumuua. Hata hivyo akasema nusura na yeye apigwe kwa risasi lakini hawakufanikiwa kumuona na kilichosadia zaidi ni kwamba walikuwa wanakimbia kutoka katika eneo la tukio na mkuki huo ulisaidia kuwakimbiza zaidi kwenye gari lao.
"Mimi nilikuwa nimejibanza mahala na mkuki wangu na wao wakati wanakimbia kurukia kwenye gari aina ya pick-up waliokuwa wameiegesha uchochoroni, mimi nilikuwa nimejificha kwenye banda moja na ndipo nikampiga mkuki mgongoni mmoja wao aliyekuwa mwisho," akasema jirani yule.
Jirani huyo, ambaye alizoeleka kwa jina la Mzee Matata, jina ambalo Walari hajui lilitokana na nini kwani si jina lake halisi, akasema baadaye ule mkuki aliukuta katika eneo la tukio lakini ana hakika ulimpata huyo mtu kwani yeye na watu wengine walishuhudia asubuhi hiyo damu nyingi katika eneo hilo na mkuki wenyewe ulikuwa na damu pia. Akasema inaonyesha mkuki ulimwingia jambazi huyo kiasi cha nchi nne hivi.
"Sijui kaumia kiasi gani na ana bahati mkuki hauna sumu. Ningemuua yule," akasema na kuongeza kuwa ana hakika mtu huyo kama hakumpiga sehemu mbaya inayoweza kusababisha kifo chake basi lazima atapelekwa hospitali kutibiwa na hivyo kuwepo na urahisi wa kumkamata.
"Tatizo nilikuwa mbali kidogo. Kama ningekuwa karibu yule mtu lazima angekwenda chini na asingenyanyuka hata kama mkuki hauna sumu," akasema mzee huyo ambaye zamani alikuwa mwindaji wa kutumia zana za jadi.
Askari waliokuwa wakisikiliza maelezo ya mzee huyo kabla ya kufanya upekuzi ndani ya nyumba ya Walari, waliahidi kufanyia kazi maelezo ya Mzee Matata.
Askari walifanya uchunguzi huku wakimhoji maswali haya na yale Walari pamoja na yule mpangaji mwenziye, wakagundua kwamba hakuna kitu kilichoibiwa mule ndani zaidi ya kamera yake aliyokuwa ameiacha sebuleni juu ya meza wakati anaingia kulala.
Karibu vitu vyote vya maana, kama vile redio kubwa, televisheni na deck vilikuwa mahala pake. Walari pia alishukuru kwamba vifaa vyake vilivyo na habari kuhusu gereza, kama vile mikanda aliyorekodi na kitabu kidogo alichokuwa amenakili majina ya wafungwa waliokufa kwa kipindi cha miezi sita, vilikuwa salama.
Hisia zilianza kujengeka kwamba majambazi yale bila shaka hayakuwa na lengo la wizi, bali kufanya hujuma, na hasa kuua mtu, na bila shaka yalidhamiria kumuua yeye Walari.
Sababu za kutuhumu namna hiyo zilikuwa nyingi kwa polisi waliofanya uchunguzi. Na hata majirani pamoja na Walari mwenyewe alituhumu hivyo.
Moja, ilikuwa hali hiyo ya majambazi yaliyosadikika kuja kwa gari, kuondoka bila kuchukua kitu chochote cha maana zaidi ya ile kamera ambayo ilionekana kwamba pengine watu wale waliichukuwa kama kudanganyia tu au walitaka asitumie tena kifaa hicho, kama siyo kuhisi kwamba kulikuwa na picha wasizopenda zichapishwe gazetini.
Sababu nyingine ni majambazi hayo kulenga zaidi risasi zao kitandani ambako inaonekana yaliamini Walari alikuwapo na kwa vile chumba kilikuwa giza, bila shaka yalikuwa yamefanya utafiti na kugundua mahala kitanda kinapokaa chumbani kwake.
Sababu nyingine ilikuwa ni kumvamia Walari ambaye hakuwa na mali nyingi kulinganisha na mpangaji mwenzake ambaye alikuwa na vitu vingi vya thamani na bila shaka alikuwa hakosi akiba ya kutosha chumbani mwake kulinganisha na Walari.
Akiwa anaelekea kumaliza ujenzi wa nyumba yake si mbali sana na Gereza Kuu la Magamaga mpangaji mwenza huyo wa Walari alikuwa anamiliki duka kubwa la vipodozi stendi na vitu vingi vyenye thamani sebuleni kwake kama redio kubwa na televisheni kubwa bapa ya kisasa.
Mara kadhaa mpangaji huyo alikuwa hafungui muziki kwa sauti kubwa kwa hofu ya kuvutia wezi, hasa kwa kuzingatia kuwa nyumba hiyo ya kizamani waliokuwa wakiishi haikuwa imara sana kwenye milango na madirisha na wala haikuwa na ua.
Pia mpangaji huyo alikuwa na vitu vingi vya kisasa kama vile mafriji, majiko ya gesi, mitambo ya umeme ya kufulia nguo, kompyuta mbili mpakato, yake na ya mkewe na kadhalika.
Walari, katika kusaka mtu anayeweza kuhusika katika tukio hilo, kama si majambazi, moja kwa moja alielekeza tuhuma zake kwa Masunju kwa vile aliahidi kupambana naye.
Alikumbuka maneno aliyoyasema Masunju siku alipomvamia ofisini kwake: "Lakini pamoja na hayo lazima pia nikuonye kitu kimoja. Kama utakataa hii offer yangu na kuendelea na mpango wako utakuwa hutaki urafiki nami, badala yake utakuwa umetangaza vita na mimi. Kwa hali hiyo lazima nami nitajihami na hapo tutalazimika kupimana ubavu. Tafadhali usiseme hivi ni vitisho bali ni ukweli mtupu.... Najua kuna watu wanakutumia ili uniharibie jina kwa malengo yao. Mimi nina maadui wengi sana wasiotaka maendeleo yangu, lakini pia nina marafiki wengi ambao najua watanisaidia kama utaamua kuendelea na vita dhidi yangu."
Itaendelea...