Riwaya - Gereza la Kifo

Riwaya - Gereza la Kifo

Gereza la Kifo - 13

Mtunzi - HAMISI KIBARI

ILIPOISHIA

"Kwa hiyo, mimi mke wangu sijabadili dini. Nilijaribu kuchunguza utaratibu wa viongozi wetu wa Kiislamu nikagundua kwamba utaratibu wao usingeniwezesha kukutana na hadi kuongea na wafungwa ana kwa ana."
Akamwambia mkewe kwamba kwa vile shule ya sekondari aliyosoma ilikuwa inamilikiwa na kanisa, ilimsaidia kufahamu mambo mengi kuhusu dini ya Kikristu na ndiyo maana hakupata taabu alipoingia kanisani na kwenda sambamba na waumini wengine.
"Shuleni kwetu, japo kila mtu alikuwa na dini yake na anaruhusiwa kuabudu siku yake ikifika, lakini ilikuwa lazima pia kuingia kanisani. Nilipoamua kwenda kanisani nilijifunza harakaharaka sana na kwa bidii. Nikamvutia sana Mchungaji Kabongo na ndiyo maana amekuwa akinitafuta akitaka nirudi kanisani, lakini hataniona tena. Kilichonipeleka huko kimeisha," akasema.

Endelea...

Zuhura alifurahi sana kusikia habari zile, lakini akamlaumu mumewe kwa kumficha ukweli.
"Umeniweka roho juu sana katika kipindi chote hiki. Ulipaswa kuniambia. Kwa kweli sasa nilikuwa napania niende kwenye baraza la dini kujadili hatma ya ndoa yetu baada ya kuona wazazi wako ambao niliwaandikia barua toka majuzi wakiwa hawatokei."
Walari alimjulisha mkewe kwamba sehemu ya kwanza ya habari hiyo alikuwa aitume siku hiyo lakini mkuu wa gereza alikuja ofisini kwake na kumchanganya.
"Sasa nitaituma kesho na itakuwa bado imewahi," akasema.
Alimsimulia kuhusu ahadi za mkuu wa gereza na namna anavyomshangaa kwa kujaribu kumhonga ili aachane na habari hiyo.
"Huyo ofisa wa magereza mjinga sana. Yaani anaamini kuwa atatumia umaskini wangu kuniziba mdomo nisiueleze umma maovu yake. Kesho nitakwenda kumbwagia ofisini kwake hati yake ya kiwanja ambayo nimeshairudufisha, halafu nitatuma habari yangu kama kawaida. Jumamosi gazeti litakapotoka hataamini macho yake," akasema Walari na kumsimulia mkewe ahadi zote za Masunju ikiwa ni pamoja na kumpeleka mtoto wao kusoma nje ya nchi, kuanzia masomo ya chekechea na kuendelea.
Muda wote mkewe alikaa kimya akimsikiliza na Walari akaendelea: "Tena huyu ofisa atajiona mjinga sana kwa sababu mazungumzo yote tuliyofanya naye, pale aliponitisha kule ofisini kwake na ofisini kwangu wakati anabembeleza kunipa rushwa yote nimerekodi. Hana ujanja hata siku moja na hakuwa anajua kabisa kwamba nimemrekodi," akasema na kutoa kimtambo chake kidogo cha kunasia sauti mfukoni na kumfungulia sehemu kidogo mkewe, mahala anakosikika ofisa huyo akimwahidi kumjengea nyumba na kusomesha mtoto wao.
"Japo ushahidi wa kurekodi sauti wakati mwingine unakataliwa, lakini kulingana na mazingira ya tukio lenyewe ninaamini utanisaidia baadaye kumkomesha huyu mshenzi."
Baadaye, mwanamke huyo aliyekuwa kimya muda wote akisikiliza, alimgeukia mumewe na kumwambia kwamba maneno yake yanazidi kumshangaza na kumuumiza roho badala ya kumfurahisha kama pale mwanzo alipomwambia kuwa hajabadili dini.
"Mume wangu, kwanza nashukuru kwamba kumbe hajabadili dini na ninakupongeza kwa hatua uliofikia katika kufuatilia suala hili la wafungwa, lakini msimamo wako sikubaliani nao kabisa, na tena ninakushangaa sana."
"Msimamo gani huo na unanishangaa kwa kitu gani?"
"Yaani unaona hali zetu wenyewe zilivyo. Nyumba wala kiwanja hapa mjini hatuna, leo unapata bahati, mtu anakupa hati ya kiwanja kilichopimwa na serikali halafu unataka kupoteza bahati hii! Labda kama umechomwa sindano ya ujinga."
"Mimi nilidhani ninavyokuona ukisali dini imekuingia, kumbe sivyo? Unasema hatuna kiwanja na kile cha kijijini kwetu ni kitu gani?"
"Kiwanja cha kijijini utalinganisha na cha hapa mjini wewe?" Akahoji na kumgeukia tena. "Hivi una maana gani kusema ninasali lakini dini haijaniingia?"
"Kwani hujui kwamba suala hili la kupewa kiwanja, kujengewa nyumba pamoja na ahadi zingine za huyu dhalimu ni rushwa? Licha ya ukweli kwamba rushwa si kitu kizuri kabisa, lakini hata wewe unajua kwamba dini yetu inakataza kabisa kupokea na kutoa rushwa!"
"Sikiliza mume wangu, Mwenyezi Mungu anaweza kukushushia kipato kwa njia ambayo hukutegemea na ukiikataa akakususa hadi ukafa hivyohivyo. Mimi naona Mungu kakushushia kipato kupitia kwa huyu ofisa wa magereza na wale watu waliokuja kukwambia ufuatilie suala hili waliongozwa na Mungu kukuonyesha kitu cha kufanya ili kikusaidie katika maisha yako."
"Bado sikuelewi kabisa, mke wangu. Yaani unamsingizia Mwenyezi Mungu katika kutenda uovu?"
"Mimi naona ulichofanya mpaka sasa kinatosha. Huyo mkuu wa gereza sasa ataogopa kuendelea na maovu kwa sababu waandishi wapo wengi ambao watafuatilia suala hili. Halafu, nchi hii rushwa imekita mizizi kila mahala. Wewe mtu mdogo utaweza kuikomesha?” alisema huku Walari akimtazama kwa mshangao.
Akaendelea: “Usilaze damu mume wangu. Chukua kiwanja tujengewe nyumba, tutakaa nyumba za kupanga, tena za kizamani kama hii hadi lini? Ona tunaanza kuwa na watoto," akasema mwanamke huyo ambaye alikuwa na ujauzito wa pili.
"Hivi itakuwa na maana gani kweli, sisi kufaidika na hii rushwa wakati jamii inateketea kwa ufisadi unaofanywa na mkuu wa gereza? Utalala kwenye nyumba inayopatikana kwa rushwa huku ukijua fika kwamba binadamu wenzako wanakufa kila siku gerezani? Ina raha gani nyumba hiyo?”
Walari akaendelea kusema: “Hivi kweli mke wangu unashindwa kujua kwamba kama ni utajiri atatupa Mwenyezi Mungu na umaskini ni makadirio yake pia. Mke wangu unashindwa kukumbuka kwamba hapa dunia tunaishi muda mfupi sana na muda mwingi tutakuwa kaburini na kisha kufufuliwa kwa maisha ya milele? Huko tutamwambia nini Mwenyezi Mungu mlezi?"
Walari aliendelea kumkatalia mkewe na kusisitiza kwamba kulikuwa hakuna cha kumzuia kuendelea na mpango wake wa kufichua hali mbaya ya gereza la Magamaga kupitia vyombo vya habari.
Mwanamke huyo naye hakuonekana kuchoka kumshawishi mumewe: "Wewe mwenyewe huwa unasema jamii nzima imeoza. Sasa hiyo habari yako si utaishia kuandika tu na watu kusoma lakini hakuna kitachofanyika! Namaanisha watu wataiacha kama ilivyo. Utakuwa umefaidika nini?"
"Lakini unasahau kwamba mimi ni mwandishi wa habari. Kazi ya mwandishi ni kuripoti tu. Suala la kufuatilia au habari hiyo kusaidia marekebisho muhimu katika jamii ni jingine. Nikishafichua kinachoendelea gerezani, kazi yangu, kama mwandishi, itakuwa imekamilika."
"Halafu utapata nini, sifa? Kwanza nina wasiwasi utajitumbukiza katika majanga na matatizo tu. Kama mkuu wa gereza anaweza kuahidi kukupa vitu vikubwa namna hiyo, anajua ni habari mbaya kwake, kwa hiyo ukiitoa utakuwa hasimu wake mkubwa."
"Sasa hayo mke wangu ni matusi. Lini uliona nafanya kazi kwa kutaka sifa? Mimi naheshimika sana, pengine kuliko mwandishi yeyote hapa Bulibuli kutokana tu na kuheshimu kazi yangu.
Huwezi mtu kuuza utu na heshima yako kirahisi namna hii. Nimeshasema, Mwenyezi Mungu Mlezi akikupangia kupata nyumba utapata na akikupangia kukosa hupati ng'o, hata kama utapokea rushwa na rushwa."
"Hiyo heshima unayopata mbona haijakuletea nyumba?" Zuhura akazidi kuhoji.
Walari akamjibu kwamba watu wenye tabia kama ya mkuu wa gereza, akishakupa rushwa nawe ukaipokea, anaanza kukuendesha anavyotaka.
"Atakudharau, kisha atakuendesha kadri anavyotaka. Leo atakwambia andika wafungwa wa gereza la Bulibuli wamefurahia huduma muhimu wanazopata kutoka kwa maofisa wao wakati hakuna kitu kama hicho na kesho atakwambia kitu kingine. Mfano hai ni mwandishi mwenzetu hapa Bulibuli jinsi anavyowashangaza wafanyakazi wa kiwanda cha Matunda.
Amekuwa akiandika mambo ya uongo kutukuza uongozi wa kiwanda hicho wakati ukweli ni kinyume chake. Majuzi wafanyakazi wamegoma kwenda kazini ili kuulazimisha uongozi wao dhalimu kuweka mazingira bora zaidi ya kazi lakini yeye anaandika kwamba wafanyakazi wote wamesusia mgomo ulioitishwa na chama cha wafanyakazi cha tawi, na eti shughuli ziliendelea kiwandani hapo kama kawaida.
Majuzi nusura wafanyakazi wampige kwa kuandika uongo. Kila anakopita anazomewa. Unataka kunifikisha huko?" Akauliza Walari.
Wanandoa hao waliendelea kubishana hadi usiku wa manane.
Katika ubishi huo, Zuhura aliendelea kumtaka mumewe kuacha msimamo wake huo ili apate vitu alivyoviita vyenye manufaa kutoka kwa mkuu wa gereza pamoja na mtoto wao kuwa na uhakika wa kusoma shule yenye ubora wa kimataifa. Lakini Walari akasema hata mbingu zikipasuka na jua kwenda kinyume hawezi kuacha kufichua uoza katika gereza kuu la Bulibuli.
Licha ya pale mwanzo mwanamke huyo kufarijika kusikia mumewe hajabadili dini, sasa alinuna, tena hasira zilimjaa kooni akimshangaa mumewe kukataa kitu ambacho aliamini kingerahisisha maisha kwa kile alichoamini ni tabia ya mumewe kutaka sifa kwamba yeye ni mwandishi mahiri.
Hata pale Walari alipomweleza mkewe kwamba kinachofanywa na mkuu wa gereza ni unyama mkubwa sawa na unaofanya na wale watu wa Manispaa wenye jukumu la kuzika maiti wasio na ndugu, mkewe aliendelea kutomuunga mkono.
Waliamua kulala huku kila mmoja akiwa kanuna kutokana na kushangaa msimamo wa mwenziye. Walari usingizi haukuja, akaamka na kuandika hili shari ambalo alipania pia kulichapisha kwenye gazeti.

Aliniambia babu, binadamu sawa duma
Ni kitu ustaarabu, kinachompa huruma
Kinamtenga na dubu, akawa mwenye heshima
Binadamu ni mnyama, akiniambia babu.

Anapokivua hima, atatisha kwa unyama
Hutokwa chembe ya wema, kwa wanziye wanadama
Hovyo atawasukuma, bila roho kumuuma
Binadamu ni mnyama, akiniambia babu.

Binadanamu kwa asili, ni mchoyo heri kima
Anapoiona mali, inamtoka hekima
Atamuua Jamali, ili apate neema
Binadamu ni mnyama, akiniambia babu.

Babu akanisaili, niihofu jahanama
Niishi kwa maadili, nimpendeze Karima
Sikuelewa kauli, utoto ulinizama
Binadamu ni mnyama, akiniambia babu.

Mwanadamu ni hatari, leo nami ninasema
Anapenda ufahari, wenzake awale nyama
Ni chanzo cha kukuthiri, maafa katika umma
Binadamu ni mnyama, akiniambia babu.

Wasio hofu na Mungu, viongozi wenye dhima
Husababisha machungu, jamii kwenda mrama
Kila mali kwake yangu, hawakihofu Kiama
Binadamu ni mnyama, akiniambia babu.

Pesa ndio iko mbele, utu sasa umekoma
Mwenye haki tupa kule, muovu huitwa mwema
Mimi napiga kelele, sintokubali dhuluma
Binadamu ni mnyama, akiniambia babu.

Walari alirudia kusoma shauri aliloandika akilighani kwa sauti ya chini na kujisikia faraja kidogo. Akapanda kitandani na sasa alipata usingizi.

Itaendelea...
Mm mwenyewe nipo upande wa mke wa walari nani anataka kuishi maisha ya shida na fursa imetokea
 
Jamaa nimesoma hadi hapa dah upo vyema sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gereza la Kifo - 17

Mtunzi - HAMISI KIBARI

ILIPOISHIA

Sauti ya kike ya karani huyo iliyosikika upande wa pili ilimjulisha kwamba mhariri alikuwa amepata safari ya ghafla kuja Bulibuli, kwa hiyo ajiandae kukutana naye.
"Mhariri anakuja kwa ndege na hivi keshaondoka kwenda uwanja wa ndege. Kwenye saa sita hivi mchana atakuwa keshawasili hapo. Ameniambia huenda akarejea na ndege ya jioni au kesho asubuhi," ikasema sauti ile ya kike na ujumbe huo kuvuma vyema kwenye ngoma ya masikio yake.
Walari alimhoji kidogo karani yule kama anajua sababu ya safari hiyo, lakini karani huyo alimjibu kwamba hajui, na kwamba Mhariri aliipanga safari hiyo ghafla jana yake.

Endelea kutiririka nayo...

Walari pia alimdodosa huyo karani kama anaweza kuhisi sababu ya kutotumika kwa habari yake kuhusu gereza la Bulibuli.
"Sijui kwa kweli. Lakini niliona mhariri akiizungumzia mara kwa mara. Labda ngoja nikuitie mhariri wa habari," anaweza kufahamu chochote," akajibu.
Sekunde chache baadaye Walari alikuwa anaongea na mhariri wa habari, Fadhili Kalisa, na moja kwa moja akataka kujua sababu ya habari yake kuhusu gereza kutotumika.
Kalisa alimjulisha kwamba yeye aliisoma habari hiyo na kuiboresha hapa na pale na kisha kumpa mhariri mkuu, lakini hajui kwa nini haikutumika gazetini wakati haikuwa na tatizo lolote.
"Inawezekana baadaye mhariri ameiogopa hiyo habari, lakini haikuwa na matatizo. Ni habari ambayo kwa kweli ninakupongeza kwa namna ulivyofuatilia na huo ndiyo uandishi. Kama ameiogopa ninamshangaa sana kwa sababu tumeshatumia habari hatari kuliko hiyo, kwa mujibu wa kumbukumbu zangu," akasema yule Mhariri wa Habari ambaye hushikilia ofisi Mhariri Mtendaji anapokuwa hayupo.
Taarifa hiyo ilimshutua kidogo Walari, lakini alishukuru kwamba Mhariri Mtendaji alikuwa anakuja Bulibuli. Pengine alikuwa anahitaji maelekezo mawili matatu kuhusu habari yake hiyo ya uchunguzi kabla haijaenda gazetini tayari kwa kusomwa na umma.
Alipata wazo la kwenda kumpokea mhariri wake uwanja wa ndege lakini akakumbuka kwamba taarifa ya karani wake haikuonyesha kama alitakiwa kwenda kumpokea, isipokuwa ajiandae kuonana naye.
Mwandishi huyo aliendelea na shughuli zake akisubiri kutembelewa na kiongozi wake ofisini hapo, na hiyo ingekuwa mara ya pili kumtembelea.
Walari pia alipania kutumia wasaa huo kumwomba mhariri kutoa pesa za kuboresha ofisi yake pamoja na kumfungia simu ya mkononi inayolipiwa na kampuni na mashine ya faksi haraka badala ya kutegemea simu ya jirani.
Baadaye, Walari alihisi kwamba haikuwa busara kutokwenda kumpokea bosi wake. Isitoshe alikuwa na hamu ya kumsikiliza haraka iwezekanavyo kuhusu sababu za habari ya gereza kutotumika Jumamosi hiyo. Aliangalia saa yake. Ilikuwa inaelekea saa tano na nusu.
Alitoka haraka kuelekea stendi kutafuta usafiri wa basi wa kumfikisha Uwanja wa Ndege. Akiwa njiani alikumbuka kitu kingine kwamba hajui mhariri wake anakuja kwa ndege gani. Hata hivyo, alijipa moyo kwamba hiyo haikuwa hoja ya kushindwa kumpata, labda kama atakuta ndege aliyopanda imeshawasili na bosi wake huyo kuondoka uwanjani. Kitu kingine hakuwa anajua bosi huyo angefikia hoteli gani, lakini alipanga akimkosa arejee haraka ofisini kwake kumsubiri kwani, kama alivyoelezwa na karani wake, angemtembelea.
Akiwa bado kwenye basi, umbali mrefu kiasi kabla ya kufika Uwanja wa Ndege, alisikia ndege ikitua. Alihisi bila shaka itakuwa ni ndege iliyombeba bosi wake.
Kutokana na basi hilo kusimama simama sana, saa sita na dakika 10 ndipo lilikuwa linawasili uwanja wa ndege. Aliteremka haraka na kuchepuka kuelekea kwenye sehemu ya kupokelea wageni ambapo ni mbali kidogo kutoka mahala yanapoishia mabasi uwanjani hapo, umbali wa mwendo wa dakika takribani nne kwa miguu.
Walari alipiga hatua kuwahi kwenye vyumba vya kupokelea wageni isije ikawa mhariri kaja na ndege hiyo iliiyotua kwenye uwanja huo kiasi cha takribani dakika 10 zilizokuwa zimepita na kupishana naye akiondoka.
Haraka yake ilizidi baada ya kukutana na teksi zikianza kuondoka na watu wenye mabegi kuelekea katikati ya mji, hali iliyoashiria kwamba tayari watu waliokuja na ndege hiyo walishatoka nje ya vyumba vya kupokelea wageni.
Akiwa sasa amebakiza kama hatua 70 kufika kwenye mlango wa chumba wanachotokea wasafiri, alimuona mhariri, Sam Odoyo, nje ya chumba cha kupokelea wageni akiwa na mkoba mdogo mkononi.
Lakini alishituka kidogo kumuona akisalimiana na mtu mmoja mnene sana pale mlangoni. Alipomwangalia vizuri baada ya kugeuka na kutembea kwa kuongozana, aligundua kwamba mtu yule mnene alikuwa ni Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Magereza na ambaye ndiye mkuu wa gereza la Bulibuli, Josephat Masunju.
Walari alijisikia moyo ukifa ganzi na kugeuza njia ghafla huku akihakikisha kwamba wanaume wale wawili ambao sasa walikuwa jirani naye kidogo hawamuoni.
Alizidi kupiga hatua ili kuwa mbali nao, huku akijichanganya katika makundi ya watu. Baadaye alichepuka na kujibanza pembeni mwa kibanda kimoja kinachouza vinywaji baridi uwanjani hapo.
Baada ya kuhakikisha kwamba wanaume wale wawili, mmoja mnene sana na mwingine mrefu, na unene wa wastani hawamuoni, alitulia ili awaangalie wanapoelekea.
Aliwaona wakijongelea gari moja la kifahari lenye namba za kiraia, ambalo ilikuwa si mara yake ya kwanza kuliona. Hili lilikuwa gari binafsi la mkuu wa gereza ambaye Jumamosi hiyo alivaa kiraia.
Aliwaona wote wakimezwa na gari hilo na kisha dereva wake ambaye alikuwa akisubiri muda wote akawasha gari na kuondoka.
Mwandishi huyo alitamani kuwafuata ili aone wanakoelekea lakini hakuwa na usafiri wala pesa ya kukodi teksi.
Akitembea kinyonge, Walari alikwenda kwenye kituo cha daladala huku pia akihisi kuwa hakufanya jambo la busara kuwakimbia wanaume wale wawili.
"Nadhani nilitakiwa niwe jasiri zaidi na kuwakabili badala ya kuwakimbia… Hivi kwa nini nimewekwepa? " Akijihoji akiwa kainamisha kichwa chake chini.
Saa nane kasorobo mchana ilimkuta Walari akiwa ofisini mwake akimsubiri kwa hamu bosi wake, Sam Odoyo. Wakati mchana ule akisumbuka kwenye daladala, mhariri huyo bila shaka alikuwa keshawasili huko alikofikia na kupiga simu kwenye duka alilokuwa akipokelea simu, jirani na ofisi yake, lakini kwa vile hakumkuta aliacha ujumbe kwamba asitoke nyakati za saa 10 jioni, angemtembelea.
Saa 10 na robo jioni Walari alisikia kitu kama gari ikisimama mbele ya ofisi yake. Kama alivyotarajia alisikia mlango wa ofisi yake ambao alizoea kuusindika karibu muda wote ukigongwa.
Alikwenda kufungua na kukutana na mhariri akiwa kasimama mlangoni.
Alimkaribisha huku akipiga jicho haraka nje na kugundua kwamba gari ile iliyokuwa imeegeshwa karibu na ofisi yake, ambayo alihisi ndiyo imemleta, ni ile aliyoiona ikimbeba mhariri huyo kule uwanja wa ndege na dereva alikuwa yuleyule.
Walari alimkaribisha tena mhariri wake ambaye alipita moja kwa moja na kuketi kwenye lile benchi fupi, pembeni mwa meza yake. Alitamani ampishe kiti chake kwa jinsi alivyoona kama alikuwa hastahili kukaa kwenye benchi duni lile.
"Bosi, hii ndiyo ofisi yetu. Bado kazi kubwa ya kifedha inahitajika ili kuiboresha," akasema Walari na kuongeza kwamba jina lake kama mwandishi ni kubwa nchini kote lakini ofisi hiyo inamuangusha.
"Ni kweli, lakini lazima tutafute mwandishi mwingine atakayeshika nafasi yako hapa na wewe uhamie makao makuu. Hii ofisi iko pazuri sana licha ya pilika nyingi za huu mtaa. Lazima tutaiboresha," akasema mhariri huyo, Sam Odoyo ambaye mara nyingi alionekana kuheshimu sana kazi ya Walari.
"Sawa bosi. Mimi niko tayari kuhamia huko kwenu lakini maisha ya huko jijini nitayaweza kweli?"
"Mbona maisha ya hapa Bulibuli ni ghali zaidi kuliko huko tuliko. Ukija utazowea na utayapenda tu. Unapokuja kule na kukaa hoteli matumizi yanakuwa makubwa ndiyo maana unadhani maisha magumu."
"Sawa bosi," alijibu. Akameza mate na kumgeukia. "Wiki iliyopita sikuona kitu. Leo nimeangalia tena gazeti nikashangaa kukuta ile habari ambayo imenitesa sana na ambayo wewe mwenyewe ulikuwa ukiiulizia sana ikiwa haipo kwenye gazeti. Nimeshangaa sana, bosi."
"Safari yangu ya kuja huku, pamoja na mambo mengine, nilikuwa pia nimefuatilia mambo fulani kuhusu habari hiyo kabla hatujaichapa," akajibu mhariri huyo.
"Mambo gani bosi?"
"Unajua ile habari ni very sensitive (ni nyeti). Kama ina mashaka yoyote lazima yamalizike kabisa. Tunaweza kushitakiwa kwa habari ile na gazeti likafilisiwa kwa kulipa fidia au hata kufungiwa."
"Ni sawa bosi. Tuseme umegundua vitu gani vyenye mashaka au mapungufu ambavyo umeona ni vyema uvifuatilie?"
"Viko vingi, lakini kwanza ni kujiridhisha kama mambo uliyoandika kwamba yanafanyika gerezani ni sahihi na yanatokea kweli. Pia ni kuwa na ushahidi kama mtu atatutaka tuthibitishe.
Tatu, kama ni kweli watu wanakufa huko na majina uliyosema unayo ni sahihi. Pia habari hii inaonekana kumshutumu zaidi mkuu wa gereza kwa kuhujumu gereza kwa maslahi yake binafsi pamoja na uzembe wa kusababisha vifo vingi vya wafungwa na mahabusu. Hizi ni tuhuma nzito sana na lazima tuwe na ushahidi kamambe ili tuweze kuzichapisha gazetini. Kumbuka, kama ulivyonidokeza, kipande kingine cha habari hii ambacho hujatuma kitaeleza namna mkuu wa gereza anavyonufaika kwa kutumia mgongo wa gereza na kuwa tajiri wa kupindukia."
"Yote unayosema ni kweli kabisa, bosi, kwamba mambo hayo yanahitaji ushahidi mkubwa. Lakini mimi naona ushahidi wote ninao kama kuna mtu atapingana na tulichoandika. Kama nilivyokueleza kwa njia ya simu kila kitu kipo," akasema Walari.
Baada ya kusema vile Walari alitoa kile kimtambo cha kunasia sauti na kumfungulia bosi wake ili asikie mazungumzo yake na mahabusu akiwa gerezani.

Itaendelea...
Mhariri kampiga bao walari
 
Back
Top Bottom