Riwaya: Chokoraa

Story yako ya chokoraa iko vizuri sana nmeipenda japo inahuzunisha kwa kiasi fulan, pongezi kwa mtunzi maana ameweza kucheza na akili yangu, wakati nasoma nilihisi Mwanaidi amekutana na mkombozi mwingine kumbe ni walewale walio katika mzunguko wa hadithi. Nasubiri nione mwisho wake
 
RIWAYA: CHOKORAA
MTUNZI: George Iron Mosenya




SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO




Kichwa kilikuwa kinamuuma sana Kasuku. Kifo cha mpenzi wake na mkewe mtarajiwa kilikuwa kimemchanganya sana.
Gari lilikutwa limeegeshwa katika hoteli, mwili wa marehemu ukakutwa katika mtaro mkubwa ukiwa na mpini wa kisu uliozama ipasavyo katika mgongo wake.
Kifo hiki sio kwamba kiliishia kumsisimua na kumuumiza Kasuku lakini kilimtia wazimu kabisa.
Alijiuliza maswali mengi. Hakupata jawabu.
Huzuni!! Huzuni ikawa rafiki yake.
Akachukua likizo isiyokuwa na malipo aweze kuipumzisha akili yake.


KASUKU alizoea kufuatilia matukio ya hapa na pale yasiyomuhusu, haya yalikuwa mepesi na alikuwa anafurahia kuyafuatilia kisha kuyaandika.
Matukio aliyokuwa anayafuatilia na kuyaandika yalikuwa makubwa sana. Tena ya kushangaza. Cha kushangaza tukio hili la kifo cha mkewe hakujua ni wapi ataanzia.
Gari limekutwa barabarani, mwili umekutwa mtaloni.
Ataanzia wapi kupeleleza.
Alama za vidole zilizokutwa katika mwili wa marehemu zilikuwa za mwanamke.
Usukani haukukutwa na alama zozote zile. Hii inamaanisha muuaji alikuwa makini sana na kazi yake. Hakukubali kuacha ushahidi kirahisi.
Hapa kila aliyeufuatilia mlolongo huu alichanganyikiwa na kupoteza tumaini la kumpata muuaji.
Kasuku alikumbwa na fedheha kubwa sana. Simu kutoka katika ukoo wa mwanamke kila siku kumuuliza ni wapi amefikia zilimkwaza sana lakini hakuwa na jeuri ya kukataa kupokea simu yao wala kujibu maswali yoyote watakayouliza.
Ilikuwa bahati kuwa alikuwa amejaaliwa mwili mwembamba. Hata alivyopungua haikushangaza sana tofauti kama angekuwa na mwili mkubwa.


Mwenzake aliyekuwa na mwili mkubwa alikongoroka kwa kasi kubwa sana. Kitambi kikaanza kufutika. Mali alizokuwanazo zikakosa maana. Akawa mkali katika familia yake, kila mara anamgombeza mkewe, mara apige watoto wake.
Alikuwa kama amechanganyikiwa.
Siri kubwa ilikuwa inamtesa. Atamshirikisha nani? Hakuwepo wa kumshirikisha.
Habari za upelelezi unaendelea zilikuwa zinamchanganya mzee Dembele. Kila alipozisikia jitihada hizi zinaendelea aliona namna anavyokaribia kuumbuka.
Mbaya zaidi hakuwa anafahamu ni wapi Frida na Mwanaidi pamoja na yule mama mwendawazimu ni wapi walikimbilia.
Akili ilikuwa imechoka kujiuliza ilikuwaje mkewe Kasuku akakutwa amekufa katika nyumba yake ya siri.
Alizihitaji roho zao ili kujiweka mahali salama. Ni roho hizi pekee ambazo zingetoa jawabu kwake.
Uhuru wake ulikuwa matatani. Na laiti kama ingefahamika kuwa alikuwa anajihusisha na na uuzaji wa madawa ya kulevya kwa njia ya kutoa misaada kwa yatima maisha yake yangemalizikia katika kitanzi.
Alikuwa muuaji!!
Siku zilizidi kukatika bila bwana Dembele kugusiwa lolote juu ya kuhusika kwake katika katika kifo cha mke wa Kasuku.
Wasiwasi wake haukupungua kamwe. Aliamini bado alikuwa katika wakati mgumu sana.
Hakuwa na la kufanya akaungoja wakati uzungumze!!




****


Mwanaidi hakuwa na mamilioni ya pesa kuweza kuwahifadhi watu hawa wawili. Mama George na Frida. Lakini alijitahidi kadri ya uwezo wake kuwahifadhi wawili hawa kwa kidogo alichokuwa nacho.
Pesa aliyoipata kwa kumwibia marehemu mkuu wa kituo cha watoto yatima isingeweza kudumu kamwe. Hasahasa ikiwa inatumika pasi kujizungusha. Mwanaidi aliamini kuwa akifikia uamuzi wa kumpeleka mama hospitali basi pesa itaishia hapohapo.
Baada ya siku takribani tano za mapumziko katika chumba alichokuwa amepanga Mwanaidi sasa likaibuka wazo la kutazama nini cha kufanya ili maisha yaweze kuendelea.
Mwanaidi hakutaka kurejea tena katika maisha ya uchokoraa.
Kwanza kwanini arejee?? Wakati sasa anaye mama anayemwona kama mzazi kwake?
Hapakuwa na haja ya kujiita yatima tena.
Alikuwa na dada aliyeitwa Frida na bado mwingine anayeitwa Isha na kaka anayeitwa George. Hapa alipungua mzazi wa kiume pekee kuweza kuikamilisha familia hii ya maajabu.
Mwanaidi alipofikiria na kujitoa katika uyatima akagundua kuwa amefanya ubinafsi wa hali ya juu sana. Kummiliki yule mama ilhali kuna yatima wengi mtaani.
Atakuwa mama wa wasiokuwa na mama mtaani!! Alipitisha kauli hiyo katika ubongo wake.
Kila neno lahitaji kitendo liweze kuonekana.
Mwanaidi akafikiria cha kufanya ili neno lake liweze kuishi katika matendo.


Frida na yule mama walikuwa wamelala bado.
Akawatazama kwa jicho la huruma.
Moyo wake ukakiri kuwa alikuwa anawapenda sana!!


Mwanaidi alingoja baada ya siku tatu. Sasa akawa amefikiria nini cha kufanya.
Katika hili alihitaji sana kumpata mtu mwenye taaluma kidogo anayeweza kuzungumza na msomi.
Atampata wapi? Alijiuliza. Mara akapata wazo.
"Frida!!" aliita.
"Sema kamanda." Alijibu kwa utani huku akiwa analamba kipande chake cha limao kukata kichefuchefu cha mimba.
"Ulisema kuwa unapafahamu nyumbani kwa George."
Frida akatikisa kichwa juu na chini kuashiria kukubali.
Mwanaidi akaelezea nia yake ya kutaka kuonana na George.
Frida aliposikia jina George na mpango wa kuonana naye alifadhaika sana kutokana na mzigo alioubeba tumboni.
Hakusita kumueleza ukweli Mwanaidi. Mwana akamuelewa.
Wakazungumza kuwa, kwa kuwa tumbo bado halijachungulia sana basi George hataelezwa ukweli. Mwanaidi aliongezea kumweleza Frida kuwa yule mwanamke ni mama yake George hivyo wanampelekea zawadi kwa ukarimu wote aliowahi kuwatendea.
Kwa kusikia hivyo, Frida akasahau yote yaliyopita akakubaliana na Mwanaidi.
Wakamuacha mama nyumbani.


Kisichokuwa ridhiki hakiliki!! Alipokuwa anaishi George hakuwepo tena. Na hapakuwa na taarifa yoyote ya wapi alipohamia.
Chokoraa hana makazi ya kudumu. Mwanaidi akafadhaika.
Lakini hawakuwa na jinsi wakaamua kurejea walipotokea.


****


SIASA ni mchezo mchafu. Lakini mchezo huu hauchezeki bila pesa. Pesa hunogesha mchezo huu. Na iwapo hauna pesa ni vyema usijiingize kabisa katika mchezo huu.
Cha kushangaza bwana Seba Sebastian aliingia katika mchezo huu bila pesa na akaweza kuucheza.
Wengi walijaribu kumuiga njia yake ya maneno matupu lakini hawakufanikiwa kitu zaidi ya kuangukia pua na kusahaulika.
Msimu huu wa kuelekea uchaguzi hali haikuwa kama zamani.
Mgombea wa chama alitakiwa kuteuliwa kwa kura za wajumbe wa chama.
Hapa sasa pesa haikuwa na budi kutumika.
Seba alikuwa bahili sana, hakuwa tayari kutumia pesa nyingi kununua nafasi ya uongozi.
Sasa anafanya nini kuwashawishi wajumbe wakati ukifika wamchague tena? Hili lilikuwa linamuumiza kichwa. Alitakiwa kuwa na pesa nyingi sana kuweza kumkabili mpinzani wake mtarajiwa, kwani alikuwa na pesa nyingi tena za kutisha
Mlango wa ofisi ya diwani wa kata ulipogongwa hakuusikia vyema mpaka ulipogongwa tena.
Akamruhusu aliyegonga. Akaingia.
"Shkamoo."
"Marahaba binti karibu" alijibu kiuchovu bwana huyu.
Binti akaketi. Bwana Seba kwa kumtazama yule binti akaanza kuweka ubashiri wa nini kimeletwa mbele yake. Aidha amefaulu anataka kuchangiwa ada ama ana matatizo na familia yake amekuja kutoa taarifa.
Udiwani nao una kero zake!!


"Nakusikiliza."
Binti akajiweka sawa katika kiti. Akamtazama diwani. Akakohoa kuweka koo sawa.
"Naitwa Mwanaidi." Alijitambulisha bila chembe ya wasiwasi.
"Nakusikiliza binti zungumza." Alisema kwa hasira.
"Nimekuja hapa mimi na wewe tusaidiane, iwapo tutashindwana naweza kwenda kwa mwingine japo wewe itakusaidia sana." Alianza kuzungumza chokoraa huyu aliyekuwa ngazi ya cheo cha dada mkuu kabla ya kushindwa kuendelea na shule.
Diwani akatoa miwani yake akaifuta kisha akamtazama tena yule binti.
Hakusema neno. Akaendelea kumsikiliza.
"Ni kuhusu Dembele…Mathias Dembele."
Diwani akashtuka. Binti mdogo kama huyu ana nini cha kuzungumza juu ya Dembele. Akastaajabu.
"Upo tayari." Badala ya kumruhusu diwani amalize kushangaa Mwanaidi akamtupia swali.
Diwani akaduwaa, hakujua nini cha kumuuliza yule binti. Midomo ikawa kama inataka kusema lakini inashindwa kuendelea kusema, ikawa inatetemeka.
"Umesema unaitwa nani?" akauliza bila kutarajia.
"Upo tayari tusaidiane?" Mwanaidi hakumwambia jina lake tena.
Ule uoga aliokuwanao awali ulikuwa umetoweka na hakuona maana ya kuwa na uhitaji wa msomi kuweza kufanya jambo hili.
"Nipo tayari, ni nini kwani?"
"Kuna jambo unatakiwa kujua kuhusu jamaa." Mwanaidi akazungumza kwa sauti ya chini.
"Jambo gani?"
"Ndo nahitaji tusaidiane."
"Kivipi?"
"Nataka nikwambie na wewe unilipe kidogo tu."
Diwani akakuna kichwa.
"Kwani kuniambia mpaka nikulipe?" Seba akaingiza ubahili wake wa kuzaliwa.
"Jamaa zungu la unga." Alisema huku akitabasamu.
Diwani akashtuka kusikia habari hiyo.
"Kivipi? Nani kakwambia?" aliapagawa.
"Unapenda kuuliza hupendi kulipia. Naondoka wapo wengi tu wa kuilipia siri hii." Alinung'unika Mwanaidi huku akisimama aweze kuondoka.
"Hapana sikiliza..sikia wewe niambie kisha nakulipa."
"Naomba niondoke."
"Haya bei gani."
"Mshahara wako wa mwaka mzima. Halafu faida yako wewe itakuwa mara mia. Kwanza utaupata tena udiwani, na serikali itakulipa kwa kumfichua jamaa." Mwanaidi aliongea kwa kujiamini sana, maneno hayo hakuyapanga hapo awali.
"He!! Nini, nipishe nipishe." Bahili alipagawa kusikia mshahara wa mwaka mzima uishie kumpa binti yule mdogo.
Mwanaidi akasukuma kiti nyuma akasimama. Akaufungua mlango akimuacha diwani bahili akitukana matusi yote anayojua.


Diwani alijikuta akiwa kimya ghafla. Akayakumbuka maneno ya Mwanaidi, akamfikiria na Dembele ambaye ndiye alikuwa mpinzani wake mtarajiwa.
Mbiombio akatoka nje ya ofisi. Kimya kimya hadi akamfikia Mwanaidi akamsihi warejee ofisini.
"Tunaenda kumalizana ama..sitaki maneno kuna mahali naipeleka habari hii na nitalipwa mara moja." Alikoroma sasa chokoraa.
Diwani akaubali yaishe. Alikuwa anaupenda udiwani na pesa pia alikuwa anaipenda.
Wakarejea ofisini.
Mwanaidi akauza habari. Mauaji ya mke wa Kasuku akamuuzia bwana Dembele. Kila uozo ukawa juu yake. Akampa diwani vithibitisho vyote. Wakaenda hadi katika ile nyumba ambayo bwana Dembele hufanyia maasi yake.
Wakati akizungumza haya alikuwa na milioni nyingi katika mkoba wake, pesa iliyotoka katika akiba ya diwani bahili, Mkoba ulikuwa na kisu chake iwapo kuna ujanja wowote unaoweza kufanyika.
Mwisho wa biashara!!


Mwanaidi akarejea nyumbani akiwa ndani teksi. Hakuamini kama alikuwa amefanya jambo hilo kwa wepesi kiasi kile.


Sasa alikuwa na jeuri ya kusema kuwa alikuwa na pesa ya kuweza kufanya jambo.
Nani kama Mwanaidi??


****
MCHIKICHINI almaarufu kama ‘Mchikidown'. Mwanafunzi gani wa jijini Dar es salaam mwenye nia ya kufaulu na shule anayosoma haina waalimu bora halijui eneo hili?
Hapa kuna vibanda vingi sana vinavyofundisha masomo ya ziada kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita.
Ni eneo maarufu ambalo huchangia wanafunzi wengi wasihudhurie vipindi vya kawaida shuleni na badala yake hujikita Mchikichini kwa ajili ya masomo ya ziada.
Cha kufurahisha. Mchikichini mwanafunzi unalipa kwa siku kupata huduma. Hapana masuala ya malipo kwa mwezi.


Jina George likatambaa kama upepo likafika Mchikichini.
Huduma zake zikahitajika.
Hesabu ugonjwa wa taifa. Daktari kapatikana.


George alikuwa ana utaratibu wa kurejea nyumbani mapema baada ya kumaliza vipindi vyake mahali alipoajiriwa.
Alipohitajika Mchikichini mambo yakaanza kuwa tofauti.
Pesa huenda pale penye pesa. George alivyoanza kuikamata pesa ndogo na nyingine ndogo iliongezeka na kuwa kubwa. Pesa ikazidi kutiririka.
Furaha kwa chokoraa huyu.
Thamani yake ikapanda.
Akatingwa haswa. Na akapokea pesa murua.
George hakuwasahau watoto wa mitaani. Kila mara alipopata nafasi alifanya kitu alichoweza kwao.
Kuna vitu kadhaa ambavyo humfanya mwanadamu anukie, sahau kuhusu marashi. Kuna umaarufu, kipaji, na kingine ni pesa.
Pesa ikikuzoea hukufanya unukie, ukishanukia kuna viumbe wataisikia ile harufu, wakiisikia wataanza kukumendea ili wakunuse vizuri. Ole wako wakunuse!!
George alianza kunukia.
Akinadada wakatamani kumnusa. Akawakwepa kwa jitihada zote akafanikiwa kwa awamu kadhaa.
Huo haukuwa mwisho wa mchezo.
Mwanamke ni sumu, huua pale anapotaka. Lakini hukuua kama ukishawishika. Na hakuna jambo gumu kama kuikwepa sumu hii.
Sumu iliyommaliza Adam na kujikuta akila lile tunda.


George akapokea simu kutoka mahali asipopajua.
Sauti ya mwanamke. Akajitambulisha kama mama Sakina.
Akazungumza na George kuhusu kibarua cha kumfundisha mwanaye anayejiandaa na mitihani ya kidato cha sita.
Sharti ni kwamba alitakiwa kumfundishia nyumbani.
George hakuwa ameikinai pesa. Akakikubali kibarua.


Malipo yalikuwa mazuri.
George alikuwa na muda usiku pekee. Hivyo majira ya saa mbili alikuwa anafika katika nyumba hii kutimiza wajibu baada ya malipo.
Alaaniwe binti yule aliyeubadili uelekeo wa kijana George.




***NI BINTI GANI ANAUBADILI UELEKEO WA GEORGE.
***MWANAIDI shujaa wa yatima ana pesa kibindoni…je harakati zitaendelea vp.
***DEMBELE…siri imevuja..nini hatma ya mwanaharamu huyu???


ITAENDELEA

muuza ubuyu ram culbby mbalu BPM Jullie Z Khantwe nifah
 
Last edited by a moderator:
Casuist tunashukuru sana, naomba leo uachie zingine ili tuzibe pengo la jana! kitu kizuri kweli hiki!
 
Last edited by a moderator:
dah safari za ghafla hizi!!! utamu umenipita hivi hiviii... mkuu leta mambo kwasasa nasitisha safari....
 
Tunasubiri kuona kitakachoendelea kwa chokoraa hawa
 
Kama kitabu kiko tayari aseme na kinapatikanaje ??
 
Aiseee sikujua kama kuna utam hapa.. wacha nianzie episode one na malikia miss neddy.. hand to hand!
 
Last edited by a moderator:
RIWAYA: CHOKORAA
MTUNZI: George Iron Mosenya


SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA


Mwanamke ni sumu, huua pale anapotaka. Lakini hukuua kama ukishawishika. Na hakuna jambo gumu kama kuikwepa sumu hii.
Sumu iliyommaliza Adam na kujikuta akila lile tunda.


George akapokea simu kutoka mahali asipopajua.
Sauti ya mwanamke. Akajitambulisha kama mama Sakina.
Akazungumza na George kuhusu kibarua cha kumfundisha mwanaye anayejiandaa na mitihani ya kidato cha sita.
Sharti ni kwamba alitakiwa kumfundishia nyumbani.
George hakuwa ameikinai pesa. Akakikubali kibarua.


Malipo yalikuwa mazuri.
George alikuwa na muda usiku pekee. Hivyo majira ya saa mbili alikuwa anafika katika nyumba hii kutimiza wajibu baada ya malipo.
Alaaniwe binti yule aliyeubadili uelekeo wa kijana George.


****




Nyumba nzuri ya kuvutia. Hii haikumshangaza George maana awali kabla ya kurejea katika dunia ya uchokoraa aliwahi kuishi.
Gari nzuri za kifahari. Hata hizi pia aliwahi kuishi mahali zinapobadilishwa kila siku.
Kwa bwana Emmanuel ambaye alikuwa baba yake mlezi.
Hakushangaa!! Akapokelewa ndani.
Akapelekwa mahali akajibweteka, akapewa huduma ya kinywaji alichoagiza. Baada ya kuulizwa.
Mazingira yalikuwa mazuri sana.
Wakati akiendelea kufanya utafiti na ukaguzi wa macho katika yale mazingira. Mara alikatishwa na hatua zilizojongea kwa kunyata.
Kwa jicho la kuibiaibia alianza kumtazama. Akaugundua utofauti wake. Nywele zake zilitaka kufanana na za Frida, tofauti kati yao ilikuwa ni hizi anazoziona zilikuwa zinang'ara sana.
Na hazikuwa fupi. Zilianguka hadi mgongoni.
Alitembea kwa madaha sana. Na macho yake yalikuwa yamefunikwa na vioo vya mawani aliyokuwa amevaa. Alijongea hadi akamfikia George. Akaondoa ile miwani.
"George!!..."
"Shkamoo."
"Karibu mwalimu." Alikwepa kujibu ile shkamoo.
Yule mwanamke akaketi pembeni ya George. Marashi makali yakapenya katika pua ya kijana huyu. Hayakumkera zaidi ya kumburudisha.
Mazungumzo yalipoanza George alibaini kuwa ile sauti haikuwa mara ya kwanza kuisikia. Alikuwa ni Yule mama aliyejitambulisha katika simu.
Mazungumzo ya sasa yalikuwa juu ya lini somo linaanza.
Baada ya kukubaliana kuwa lianze siku inayofuata. Sasa ikafuata zamu ya mwalimu kukutana na mwanafunzi wake.
George alikuwa na uzoefu wa kukutana na wasichana walimbwende wakati yupo chuoni na kama hii haitoshi baada ya kuingia mtaani katika zunguka zunguka za huku na kule usiku wa manane aliweza kukutana na machangudoa. Hata hawa walikuwa warembo pia.
Sasa mbele yake alikuwepo mwanadada anayefanana na wasichana hawa maarufu kwa biashara za usiku.
"Naitwa Sakina."
"Mwalimu George ndio jina langu." Alijitambulisha George.
Mwanadada akabetua midomo yake.
"We ndo umetumwa uje kunilinda."
George alishtushwa na kauli hiyo, akashindwa kujibu chochote akajichekesha.
"Nimekuuliza mbona unajichekesha ndugu." Aliongezea yule binti.
Majibu ya yule binti yalimfadhaisha George, hakujua ni kwanini anamletea dharau hivyo. Kwa sababu haikuwa mara ya kwanza kudharauliwa alipuuzia. Na kumuona huyu naye ni wale wale.
"Tutaanza na topic gani?" George aliuliza.
"Yoyote unayojua."
George alibaki kushangaa!!
Hakujua aegemee upande gani kimtazamo kuhusu binti huyu, ni jeuri ya pesa ama kuna jingine la kumfanya amjibu vile.


Baada ya binti. Mtu wa mwisho kukutana na George alikuwa ni mzee ambaye haukuhitaji maelezo yoyote kumtambua kama mwenye nyumba hiyo. George akamsalimia kwa heshima zote.
Mazungumzo yalikuwa juu ya mshahara na hatua za kulipana.


****


MKEWE alidhani mume wake huenda amerogwa kutokana na uamuzi wake wa kujiingiza katika kinyang'anyiro cha kuwania ubunge. Ama la laana ya ndugu zake inamshambulia, laana ya kudiriki kuoa mwanamke wa dini nyingine kwa ndoa ya kiserikali badala ya kuoa mwanamke wa dini na mabila yao.
Hofu ikatawala.
Hali ilikuwa tete. Mume hakamatiki wala hashikiki, ukithubutu kumshauri anabwatuka matusi mazito. Tena mbele ya watoto bila kujali lolote.
Kama hii haitoshi, baba mwenye nyumba akaibuka na mengine.
Watoto wake waliokuwa likizo, kama ilivyo kawaida hujikita katika masomo ya ziada. Wakazuiliwa kutoka nje ya geti.
Hakuna sababu yoyote waliyopewa kuwa ni chanzo cha maamuzi hayo lakini waliamrishwa wakatii.
Sakina. Binti aliyekuwa kidato cha tano alikerwa sana na kitendo hiki cha mzee wake kupiga marufuku wao kutoka nje ya uzio. Lakini angefanya nini.
Kimbilio lake likawa kwa mama. Nani kama mama? Hata tatizo liwe kubwa vipi anaaminika kuwa anaweza kulitatua.
Sakina alihitaji kusoma somo la hesabu kwani hakuwa mzuri sana katika somo hilo na alikuwa amekaribia mitihani yake.
Mama Sakina, mama wa kiarabu aliyeolewa na Dembele kwa sababu tu ana pesa akafanya aliloombwa na mwanaye. Dembele na kichaa chake cha hofu akajibu kwa hofu pia.
Akamuagiza yule mama wa kiarabu atafute mwalimu mzuri wa kuja kumfundishia Sakina nyumbani. Hilo halikuwa wazo bali amri.
Ikapitishwa.
Dembele alikuwa katika mbio za sakafuni ambazo kwa namna yoyote ile huishia ukingoni. Yeye hakuamini kuwa kuna ukingo japo matumaini yalikuwa yanapotea kwa kasi.
Kuizuia familia yake isionekane nje ya nyumba aliamini kuwa anawazuia wasiifikie siri ambayo hataki waitambue. Siri ya kuuza madawa ya kulevya.
Sasa ameagiza mwalimu aletwe. Mama sakina anapata mawasiliano ya mwalimu ambaye anasifika sana kwa kufundisha somo la hisabati.
Nani mwingine kama sio George?
George anatangaziwa dau kubwa. Anavutika!!
Baada ya kuelekezwa nyumba ilipo. Anaingia rasmi katika himaya ya bwana Mathias Dembele.
Mwanaume anayesumbuliwa na siri kubwa moyoni siri inayomtesa.
Ni mwanaume huyu aliyechanachana tumbo la mama yake mzazi George, akatia madawa ya kulevya mara nyingi awezavyo kwa manufaa yake. Akajitajirisha na sasa ile pesa chafu, anategemea kumlipa George kwa kumfundisha mwanaye, Sakina.
Sasa mwalimu George na Dembele ana kwa na wakizungumza juu ya namna ya kupeana malipo.
George anapendekeza kulipwa nusu kwanza na nusu nyingine baadaye.
Wanaafikiana.
George anaondoka, kwa makubaliano ya kuanza kazi usiku wa siku inayofuata.


****


TAA iliendelea kuwaka hadi majira ya saa nane usiku.
Haikuwa kawaida kwa kiumbe huyu kujisomea kwa muda mrefu kiasi hicho. Lakini siku hii alikuwa mzito sana kuzima taa.
Kila alipojipa moyo kuwa anamalizia ukurasa mmoja kisha anazimisha taa, alitamani tena ukurasa mwingine. Sasa ilikuwa imetimia saa nane usiku nab ado alitamani kuendelea kusoma. Hakuwa na usingizi bali alifanya kazi ya kupangusa machozi mara kwa mara.
Kuna muda alifunika daftari lile na kujilaumu kuwa yeye ni mjinga aliyepitiliza. Analia kwa maandishi!!
Maajabu na kweli!!
Akajitia ujasiri akaendelea kusoma tena. Sasa kidogo alitabasamu, alichokisoma kidogo kiilimfariji.
Ghafla giza!! Umeme ulikuwa umekatika.
Akatoa tusi zito la kiingereza akiwatukana wahusika wa Nyanja hiyo ya serikali. Kisha akajibweteka kitandani, akaanza kumjengea picha mwandishi wa simulizi ile ya ajabu.
Hakika ni mwandishi wa ajabu, maana binti huyu hakuwahi kuwa na kawaida ya kusoma makala yoyote ndefu. Aliamini kila makala ndefu ni siasa ama michezo, na hakuwahi kuvutiwa na vitu hivi.
Lakini sasa amesoma na ameburudika. Zaidi amejifunza kitu.
"Alimaanisha nini sasa UKURASA ULIOSAHAULIKA!!" Alijiuliza yule binti. Akilinukuu jina la riwaya hiyo iliyoandikwa kwa mkono moja kwa moja lakini mwandiko ulionyooka vyema.
Akiwa katika kufikiria ni kwa nini simulizi ile ambayo hajaimaliza bado ilimtoa machozi, akakumbuka kuwa kuna mistari mingi ilimshambulia moja kwa moja.
Akakumbuka majibu yake aliyoyatoa kwa mwalimu wake mtarajiwa. Akajikuta katika HATIA huku aibu ikimsindikiza.
Akazilaza nywele zake za kiarabu. Akajifunika shuka.
Sakina akasinzia huku akijiwekea ahadi ya kumwomba msamaha George siku inayofuata.


****


George alipopanda ndani ya gari aligundua kupungukiwa kitu.
Daftari lake lenye umuhimu huenda kupita yote.
Daftari analolitumia kuandika simulizi.
Licha ya kupitia magumu ya mtaani. Bado alipenda kuandika kila anachokipitia na chochote anachoona kinafaa kuandika.
Aliihangaisha sana akili yake kupata kujua ni wapi alikuwa na daftari hilo kwa mara ya mwisho. Akili iliyochoka ikagoma kutoa majibu.
George akafika nyumbani akiwa mpweke. Isha akaigundua hali hiyo.
Akamuuliza George, kwa simanzi George akajielezea.
Isha ambaye hakuona umuhimu wowote wa simulizi hizo aliishia tiu kumpa pole isiyo na msaada zaidi.
Siku ikamalizika.


****


HAKUNA somo lenye washabiki wachache kama hisabati, licha ya kuonekana kuwa gumu upande wa wasichana, lakini hata wanaume huangaika nalo.
Ukipewa talanta ya kulifahamu vyema somo hili basi nafasi yako katika jamii inakuwa kubwa na ya kuheshimika.
George alikuwa analifahamu vyema somo hili.
Wagonjwa wake wengi wakawa wasichana.
Wasichana wa vidato kuanzia cha tatu hadi cha sita, kwa mjini hawa ni wasichana wakubwa na wengine wanawatunza wazee umri wa baba zao.
George hakuwahi kukutana na dhahama hii ya usumbufu. Lakini huu ulikuwa usumbufu wa maajabu, usumbufu usiokuwa na maneno ndani yake.
Usumbufu wa vitendo.
Mara huyu avae hivi mara yule arembue jicho. Ilimradi shaghalabaghala.
Mwanaume akajikaza!!


Lakini atajikaza mara ngapi iwapo usiku ule uvumilivu ulimshinda akataka kumbaka Isha??
Hata kama hakumbaka sasa ana ujauzito.
Hata George ni mwanadamu!!


***GEORGE katika vishawishi, je? Atayashinda majaribu haya??


***DEMBELE na GEORGE ndani ya nyumba moja……ni maadui wasiofahamiana…..ITAKUWAJE??


***SAKINA navutiwa na simulizi….iliyoandikwa na GEORGE……je atavutiwa zaidi…


***Ni nani aliyeupoteza uelekeo wa GEORGE???


muuza ubuyu ram culbby mbalu BPM Jullie Z Khantwe Excel ladyfurahia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…