Riwaya: Chaguo la Neema ... Ng'ombe wa Mahari

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
32,933
2,000
Pamoja na kwamba alikuwa ameanza mwaka wa kwanza Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam Deo Tegeule alikuwa hakosi starehe kila mwisho wa juma. Alikuwa na kundi la marafiki zake wawili – Timothy Haule na Jumanne Mamba ambao pamoja walitengeneza timu ya wanaopenda kusoma pamoja na kujirusha pamoja. Wenyewe walikuwa wanajiona wajanja sana kwani licha ya kuwa walikuwa wanapasua darasani – waliitwa vipanga -walikuwa pia ni kivutio cha wasichana wengi pale chuoni na katika hilo walikuwa hawajivungi. Walisifika pale campus kati ya wanafunzi walioingia mwaka ule kwa jinsi ambavyo waliweza kubadilisha wasichana kama kubadilisha picha za kwenye facebook.

Walikuwa ni watanashati wa kupindukia. Vijana wengine wakiume walikuwa wanawaita masupa modo wa ubishoo. Hakuna wakati wowote ambapo vijana hao watatu walikuwa wamevaa varuvaru. Wote watatu walikuwa wanatoka familia maarufu nchini. Deo akiwa ni mtoto wa Jaji wa Mahakama Kuu, Tim mtoto wa Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Polisi na Jumanne mtoto wa Waziri wa Nchi ofisi ya Rais (Utawala Bora). Pamoja na ujiko wa uzuri na ucheshi wao walikuwa na ujiko wa nafasi za wazazi wao. Walisomeshwa kwa pesa za wazazi wao na hawakuchukua hata tone moja la mkopo toka Bodi ya Mikopo – ambayo ilikuwa haijapungukiwa kashfa za ufisadi.


Jumamosi moja Deo na wenzake waliamua kwenda kusherehekea siku kuu ya kuzaliwa kwake. Walipanga kwenda Club Bilicanas kujirusha kwani waliamini pale palikuwa na uhuru wa aina yake kujichanganya na watu wa sehemu mbalimbali. Pamoja na kuwa na uchaguzi mkubwa wa lundo la wanawake ambao angeweza kwenda kujirusha nao alikuwepo msichana mmoja tu ambaye Deo alikuwa amepanga kumwomba watoke naye kwa siku hiyo. Alishamtongoza vya kutosha tangu walipoanana kwa mara ya kwanza pale Maktaba ya Chuo Kikuu. Binti yule alikuwa akimtolea nje mara kwa mara hasa kwa vile alikuwa miaka miwili mbele ya Deo pale chuoni na haikuwa fasheni kutoka na kijana wa mwaka wa kwanza. Lakini Deo alikuwa hajui kushindwa; kwa kadiri Lina – yule msichana - alivyomtolea nje ndivyo Deo naye alivyozidi kumbembeleza na kumwimbisha kila akipata nafasi.

Asubuhi ya siku ile ya kuzaliwa Deo alibembeleza zaidi. Alimtumia ujumbe wa simu Lina.

Hi Baby, umefikiria ombi langu? We mbona king’ang’anizi hivyo; miye niache kufikiria mambo ya maana nikufikirie wewe; sifikirii. Aliweka alama ya picha ya uso wenye huzuni.
Acha hivyo Lina, hata kwa birthday yangu? Birthday yako lini? Leo Kimya kikapita kidogo. Deo aliamua kuandika tena. Hata kuniwish happy birthday hutaki? I’m sorry, happy birthday
Mbona kavu hivyo?
Unataka ije na maji?
Naomba basi tutoke wote jioni mara hii tu Lina please?
Hivi wewe hukati tamaa eh?
Kukata tamaa ndio nini lol
Nikikubali safari hii utaacha kunisumbua?
Kabisa nitashukuru sana.
Wapi unaenda kusherehekea?
Bilicanas
Ok. Nitakukuta huko
Are you serious?
Niulize tena uone kama sibadili mawazo.
Thanks hautajuta.


PATA NAKALA YAKO BURE HAPA:
CHAGUO LA NEEMA - NG'OMBE WA MAHARI
 

Attachments

snochet

JF-Expert Member
Mar 31, 2011
1,283
2,000
safi sana,tuonjeshe page chache basi kama ile ya karatu,,,,,,,napenda sana story zako,,kama bado huja-publish,please consider kuweka a more attractive cover,huyo mama na mtoto wametokelezea,lakini hivyo vingine,jaribu kuweka kitu kingine,tafuta mtu wa graphix mzuri,,,itavutia zaidi
 
Top Bottom