Riwaya: Bring back our girls

Riwaya: Bring back our girls

Story ilikuwa ya Peniela bana Monika mwenyewe haingii:hizi zingine mbwembwe tu.
 
Story ilikuwa ya Peniela bana Monika mwenyewe haingii:hizi zingine mbwembwe tu.

Hahahaaaaaa Mkuy Hujamsoma tu Huyu Mwandishi Ana Vitu Unaweza Kaa chini usijue ipi ni ipi
Sema tu Vigezo na Mashart vinazingatiwa la sivyo Tunge vishusha vyote humu
 
Natamani Mpate ninavyo vipata ila Hakuna Jins vigezo na Mashart vinazingatiwa

Niko na Kurasa Kumi hapa ndo nazianza

fab86dc53a5a73c32946178d81af7a35.jpg
 
BRING BACK OUR GIRLS
SEHEMU YA 38
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Siku ya kesho tutaachia kirusi chetu hatari katika hospitali ya Mount Meru na katika hospitali ya Serian sina hakika kama nimetamka sahihi jina hili majina ya kitanzani ni magumu sana lakini tutaachia kirusi pia katika soko kuu la mji wa arusha.Hizi ni sehemu zenye mikusayiko mikubwa ya watu.Hili litakuwa ni shambulio letu la kwanza kabisa ambalo litaamsha taharuki miongoni mwa jamii na kuilazimisha serikali kuhamaki na kuelekeza nguvu nyingi katika kutaka kuokoa maisha ya watu watakaokuwa wakiangamia ndani ya muda mfupi.Hakuna dawa ya haraka ya kuweza kukizuia kirusi hiki ambacho husambaa kwa njia ya hewa.Baada ya nguvu zote za serikali kuelekezwa katika maeneo haya basi sisi tutapata nafasi nzuri ya kuweza kutekeleza mipango yetu mingine bila ya kukabiliwa na nguvu kubwa.

ENDELEA……………………..

Tonny alikuwa akitiririkwa na maji mwilini.Alikuwa ametoka kuoga.Akachukua taulo lake na kuanza kujifuta maji.Siku hii ya leo kichwa chake kilikuwa na mawazo mengi sana .Mawazo kuhusiana na shambulio la kigaidi linalokwenda kutokea jijini Arusha yalimpa wakati mgumu sana.
" Leo ndiyo siku ya ufunguzi wa mkutano wa Sullivan.Lolote linaweza likatokea katika siku ya leo kwani ni siku ambayo Alshabaab wamepanga kufanya shambulio.Nasikitika sana kwa ofisi zetu kupuuza taarifa nilizowapa kuhusiana na shambulio hili.laiti kama wangeichukua taarifa ile na kuifanyia kazi wangeweza kufanikiwa kulizima shambulio hilo.Japokuwa nimefungwa humu gerezani bila kufahamu kosa langu lakini kwa mara nyingine tena ninajikuta nikipatwa na moyo wa kutaka kusaidia kulizuia shambulio hilo lisitokee lakini sina namna ya kufanya tena kwani ujumbe wangu umepuuzwa na hakuna mtu yeyote anayetaka kuniamini.Mamia ya watu wasio na hatia watatateketea kwa sababu ya uzembe wa watu wachache.Ninamlaumu sana mkurugenzi mpya wa ofisi yetu kwa kupuuzia taarifa ya onyo niliyompa.." Tonny alikuwa akiwaza akiwa amesimama kati kati ya chumba chake.
" Anyway..sina namna nyingine ya kufanya ili kuweza kulizuia shambulio hili..iliyobaki ni mimi kukaa kimya na kuelekeza masikio Arusha kusikia kitu kitakachotokea." Tonny akaendelea kujifuta maji mwilini halafu akavaa nguo na kukaa kitandani.
" Monica atasikitika sana baada ya kusikia kwamba shambulio hili limeshindwa kuzuilika hata baada ya kufanya jitihada za kunitumia taarifa ya kuwepo kwa shambulio mapema sana.." Tonny akainama na kujishika kichwa.Akazama katika mawazo mazito.
Akiwa bado amekaa kitandani kwake akiwaza mlango ukafunguliwa na askari wanne wenye silaha toka jeshi la polisi wakiambatana na askari watatu wa magereza pamoja na Salvatory mpimwe mkuu wa gereza wakaingia .Ujio ule ukamstua Tonny akahisi kuna kitu kinakwenda kutokea.
" Habari za asubuhi Tonny" akasalimu salvatory.
" Habari nzuri mkuu..vipi mbona ujio wa ghafla asubuhi asubuhi? akauliza Tonny.
" Tonny tunakuhamisha na kukupeleka katika seli nyingine."akasema Salvatory
" Mnanihamisha !!....Tonny akashangaa
" Ndiyo Tonny tunakuhamisha tunakupeleka katika seli nyingine yenye ulinzi wa juu zaidi.Tunataka kuzuia jambo lolote kama lililotokea jana lisijirudie tena..." akasema Salvatory.
Tonny akavuta pumzi ndefu akamtazama Salvatory na kisha akawatazama wale askari wenye silaha ambao wote walikuwa wakimuangalia kwa macho makali kwani walikwisha pewa angalizo kwamba Tonny si mtu wa kufanyia mchezo.
" Ouh My God ! kazi imeanza..." akasema Tonny kwa sauti ndogo huku akiinuka pale kitandani na muda huo huo vyuma vikasikika katika bunduki za wale askari walikuwa wakijiweka sawa kwani waliogopa pengine Tonny angeweza kufanya jambo lolote lisilo la kawaida.Tonny akawatazama akacheka na kusema
" Msiogope ndugu zangu..mimi niko kifungoni na sintaweza kufanya jambo lolote lile la kuhatarisha usalama wenu.kama ningetaka kuondoka humu gerezani ningekwisha ondoka muda mrefu sana lakini sitaki kufanya hivyo ninasubiri hadi wale walionileta humu waje wanitoe wenyewe.Nawaomba muwe na amani mioyoni mwenu." akasema Tonny huku akicheka halafu akanyoosha mikono yake ili aweze kufungwa pingu kisha akatolewa ndani ya chumba kile na kupelekwa sehemu nyingine iliyokuwa chini ya ardhi.
" taarifa imekuja nihamishwe..right? Tonny akamuuliza Salvatory ambaye hakujibu kitu
" Mr Savatory naomba unijibu..ni kweli umetumiwa taarifa unihamishe seli? taarifa imetoka kwa vigogo .right?..
Salvatory akakosa jibu la kutoa akaendelea kutembea kwa kasi.
" Ukimya wako ni jibu kwangu kwamba ni kweli wakubwa wamekutumia taarifa ya kunihamisha seli..I know how these people works..Salvatory fumbua macho yako natumiwa bila kujijua..They are using you to lock me up...hakuna shaka lakini siku inakuja ambayo utajutia uamuzi wako..." Tonny akasema huku akicheka kicheko cha chini chini.
" Please shut up Tonny and mind you own business..I'm just following orders" akasema mkuu wa gereza Tonny hakutaka tena kumsumbua kwa maswali zaidi kwani alifahamu fika zile zlikuwa ni njama za Alqaeda .
Seli aliyohamishiwa Tonny ilikuwa ni moja kati ya zile seli ambazo huwa wanawekwa watu muhimu sana ambao hawatakiwi kuonana na mtu yeyote yule.Ni moja kati ya seli hizi ndiko alikohifadhiwa Khaleed Aljameer kiongozi wa kundi hatari la Boko Haram nchini Nigeria.
" kwa kutumia nguvu ya pesa Alqaeda wamefanikiwa kuwaweka mikononi baadhi ya viongozi wa juu wa serikali na ndiyo maana wameamua kunihamisha chumba na kunileta huku .Hawakuwa na haja ya kufanya hivi kwa sababu hata kama wasingenileta huku nisingeweza kufanya jambo lolote lile..nitakaa kimya na kuangalia namna jiji zuri la Arusha litakavyotapakaa damu ndani ya kipindi kifupi kijacho." akawaza Tonny

*****************************

Eneo lote la kuuzunguka uwanja wa ndege kimataifa wa Kilimanjaro lilizungukwa na askari wengi waliokuwa wakilinda usalama.Magari ya doria yaliyojaza askari yalikuwa yanazunguka zunguka huku na huko ili kuhakikisha kwamha hali ya kiusalama uwanjani hapo inakuwa ya uhakika.Bado wageni mbali mbali waliendelea kuwasili kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Sullivan unaofanyika kwa mara ya pili jijini Arusha.Licha ya kuwepo kwa ulinzi mkali sana toka katika idara mbali mbali za usalama za ndani ya nchi,walikuwepo pia makachero toka nchini Marekani ambao nao kazi yao kubwa ilikuwa kuhakikisha usalama kwa raia na mke wa rais wa Marekani aliyetarajiwa kuwasili mida ya saa nne za asubuhi kwa ajili ya kuhudhuria mkutano huu muhimu kwa bara la Afrika..Kikosi hiki maalum kilikuwepo hapa nchini kwa muda wa takribani miezi mitatu sasa kuratibu shughuli zote za kiusalama kwa ajili ya ujio huu.
Saa tatu na nusu msafara wa mke wa rais wa Tanzania ,uliiacha barabara ya Arusha – Moshi na kukata kulia kushika barabara iliyokuwa ikielekea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro.,Hatimaye msafara ukawasili uwanjani na mke wa rais akashuka na kupokewa na waziri wa mambo ya nje ya nchi ambaye alikuwepo hapo uwanjani kuanzia asubuhi akiwapolkea wageni mbali mbali na viongozi waliokuwa wakiendelea kuwasili kwa ajili ya kuhudhuria mkutano huu.Pamoja naye alikuwepo pia mkuu wa mkoa wa Arusha na viongozi wengine kadhaa wa serikali na taasisi waliokuja kumpokea mke wa rais wa Marekani .Vikundi mbali mbali vya ngoma vilivyokuwa hapo uwanjani kwa ajili ya kutumbuiza wageni viliendelea kutoa burudani kwa watu waliojitokeza kumpokea mke wa rais huyu wa Marekani.Waandishi wa habari wa vyombo mbalI mbali vya habari vya ndani na nje ya nchi waliokuja kwa ajili ya kuandika na kuripoti kuhusu mkutano huu mkubwa walikuwepo kwa wingi uwanjani hapo kwa ajili ya kuchukua matukio yaliyokuwa yakiendelea kutokea uwanjani hapo kwani bado viongozi mbali mbali waliendela kuwasili .
Muda ulikaribia na viongozi wote wakaelekea ndani ya uwanja ambako walijipanga tayari kabisa kumpokea mke wa rais wa Marekani.
Makachero toka katika vikosi vya ulinzi vya marekani walikuwa macho na makini mno wakisaidiana na wanausalama wa ndani ya nchi kuhakikisha kwamba hali ya kiusalama inaboreshwa uwanjani hapo.Saa nne na dakika saba ndege aina ya Boeing 757 iliyombeba mke wa rais wa marekani ikaonekana angani.Taratibu ikaanza kushuka na hatimaye ikagusa ardhi ya Tanzania na kisha ikatembea kwa kasi juu ya bara bara na taratibu mwendo ukaanza kupungua ,ikageza na kuanza kurejea kwa mwendo wa taratibu sana na mwishowe ikasimama.Baada ya kama dakika kumi hivi toka iliposimama mlango ukafunguliwa na wakashuka maafisa wa usalama wakasalimiana na wanausalama waliokuwepo pale uwanjani halafu wakarejea tena ndegeni na baada ya dakika chache mke wa rais wa kwanza mweusi wa Marekani akashuka ndegeni na kupunga mikono akiwasalimu watu waliokuwepo pale uwanjani kumpokea.Uso wake ulipambwa na tabasamu pana sana .PemBeni yake alikuwepo binti yake Theresa ,binti ambaye majarida kadhaa ya urembo nchini marekani yamekuwa yakimuandika kwamba ni mmoja kati ya mabinti wenye uzuri wa kipekee kabisa.Kama ilivyokuwa kwa mama yake ,naye uso wake ulikuwa na tabasamu zito na kuyafanya mashavu yake yabonyee na kutengeza vishimo.Walishuka ngazi kwa taratibu huku wakitabasamu .Burudani toka kwa vikundi mbali mbali vya ngoma za kiasili zilipamba moto hapo uwanjani.
Mara tu baada ya kushuka mke wa rais wa marekani akakumbatiana na mwenyeji wake mke wa rais wa Tanzania Bi Fenera,halafu akasalimiana na waziri wa mambo ya nje ya nchi na viongozi wengine waliokuwepo pale uwanjani.Pamoja naye ndegeni alikuwepo pia waziri mdogo wa serikali ya Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika Bi Lisah Damison.Alikuwepo pia mchungaji Albert stalks mmoja kati ya watu mashuhuri toka jamii ya weusi nchini Marekani.Wote walisalimiana na viongozi waliokuwepo uwanajani pale kuwapokea halafu wakaelekea katika burudani za ngoma.Kulikuwepo na vikundi mbali mbali vya ngoma vilivyokuwa vikitumbuiza na kuwafanya wageni wote waliokuja kutabasamu na kufurahi sana..Baada ya kushuhudia burudani zile zilizowakonga nyoyo wakaingia katika magari na msafara ukaondoka pale uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro kuelekea jijni arusha.Kote msafara ulikopita kulikuwa na idadi kubwa ya watu mabarabarani waliotaka kumshuhudia mwanamama huyu mke wa rais wa kwanza mweusi wa marekani.
Toka uwanja wa ndege wa KIA,msafara ulilekea moja kwa moja katika ikulu ndogo ya raisi jijini Arusha ambako mke huyu wa rais wa Marekani alitazamiwa kuwa na mazungumzo na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania..Alipokewa na rais na kukaribishwa ikulu ambako walikuwa na maongezi kidogo na baadae yeye na ujumbe wake wakaelekea Tandala International Hotel ambako ndiko angelala kwa muda wote atakaokuwepo jijini Arusha.Kulizunguka hoteli hili kubwa na la aina yake afrika Mashariki,kulikuwa na ulinzi mkali sana wa vikosi vya usalama vya ndani wakisaidiana na makachero wa marekani.
Ukumbi unamofanyika mkutano wa Sullivan ,ulifurika watu waliokuwa wakisubiri ufunguzi rasmi wa mkutano.Saa moja za jioni mgeni rasmi ambaye ni rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania akawasili ukumbini.watu wote wakasimama kwa heshima yake na akaenda kuchukua nafasi yake.Baada ya watangulizi wawili kuhutubia ikafuata zamu ya mheshimiwa rais wa Tanzania kuufungua rasmi mkutano wa Sullivan.
“ Ndugu Hope masters,rais wa taasisi ya Leo Sullivan na gavana wa mkutano huu,
Mr Jacob strise na Mr Peter brosaw wenyeviti wenza wa mkutano huu,
Mheshimiwa Lisa damis waziri mdogo wa Afrika katika serikali ya Marekani
Viongozi mbali mbali wa mataifa
“ wageni waalikwa mabibi na mabwana
Ninasimama mbele yenu kwa heshima na taadhima kwa niaba ya watanzania wote kuwakaribisha katika mkutano huu wa Sullivan unaofanyika kwa mara ya pili katika jiji hili la Arusha.Mwaka 2008 mkutano kama huu ulifanyika hapa hapa Arusha na kwa mara nyingine tena nchi ya Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano huu mkubwa na muhimu kwa bara la Afrika.
Ninawashukuru viongozi wa mataifa ya Afrka na wawakilishi wao kwa kukubali mwaliko wetu..Nawashukuru vile vile wageni wote kutoka Marekani,Karibean,Afrika na kwingineko kote duniani kwa kufika nchini kwetu.
Ninamshukuru kwa namna ya pekee kabisa mke wa rais wa Marekani Bi Gwen pring kwa kuja kutuunga mkono katika mkutano huu.Ninawashukuru pia viongozi mbali mbali waliokuja kuungana nasi kutoka katika serikali ya Marekani.Tunamshukuru raisi wa marekani kwa kuwatuma kuja kuungana nasi hapa.”
Hivi ndivyo alivyoianza hotuba yake mheshimiwa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania akiwakaribisha viongozi wa mataifa na wageni mbali mbali waliohudhuria mkutano huu mkubwa wa Sullivan

TUKUTANE SEHEMU IJAYO………………………..
 
Back
Top Bottom