Riwaya: Bring back our girls

Riwaya: Bring back our girls

BRING BACK OUR GIRLS
SEHEMU YA 26
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Kwa mara nyingine tena ,nchi yetu imepewa heshima kubwa kuandaa mkutano huu mkubwa.Ni nchi nyingi zingetaka kupewa ziandae mkutano huu lakini sisi tumeonekana tunafaa kupewa nafasi hii adimu.Ni heshima kubwa sana kwetu.Hii ni fursa nzuri kwetu kuitangaza nchi yetu,kutangaza maliasili zetu,bidhaa zetu ,ikiwa ni pamoja na wafanya biashara wetu kutanua wigo wa biashara zao kimataifa.Nashukuru kwamba katika maadalizi yenu mmeyazingatia hayo yote.” Waziri mkuu akatulia na kwa mara nyingine tena ukumbi ukapiga makofi ya kushangilia.
“Ndugu zangu sihitaji kusema mengi kwa sababu bado tuna ziara ndefu ya kuzungukia sehemu mbali mbali kukagua maandalizi yanavyokwenda.Ni matumaini yangu kwamba ndani ya muda mfupi ujao yale mambo yote ambayo yalikuwa hayajakamilika ,yatakamilishwa ili tujiridhishe kwamba hakuna tatizo lolote kubwa litakalojitokeza zaidi ya changamoto ndogo ndogo zitakazojitokeza wakati wa mkutano.Narudia tena kuwapa hongera kwa kazi nzuri mliyoifanya na ninawatakieni mafanikio katika kumalizia yale mamboyote ambayo bado hayajakamilika.” Waziri mkuu akasema na kukaa chini huku akisindikizwa na makofi ya kushangilia.Baada ya shughuli ile iliyompeleka pale kumalizika mheshimiwa waziri mkuu akaondoka na kwenda kuendelea na ziara yake ya kukagua maandalizi mengine yanayohusiana na mkutano ule.

ENDELEA…………………………………………

UWANGWA PRISON – KIGAMBONI DAR ES SALAAM

Gereza la Uwangwa lilikuwa ni gereza kubwa na la kisasa kabisa kuwahi kujengwa nchini Tanzania.Gereza hili lililojengwa Kigamboni jijini Dar es salaam lilikuwa ni maalum kwa ajili ya kuwahifadhi wafungwa wenye makosa makubwa kama ya mauaji,wafungwa wanaosubiri kunyongwa na pia wafungwa wa kisiasa.Gereza hili pia limekuwa likihifadhi watuhumiwa wa makosa mbali mbali mbali ya kivita ambao kesi zao zinaendelea kusikilizwa katika mahakama kuu ya makosa ya jinai ya Afrika iliyojengwa jijini Arusha.
Baada ya kufanikisha kukamatwa tena kwa Abdool bin sahel mtu aliyeratibu milipuko ya mabomu katika balozi za marekani jijini Dar es salaam na Nairobi aliyekuwa ametoroshwa na mtandao wa alqaeda,Tonny alikuwa amewekwa kizuizini katika gereza hili kubwa .Miaka miwili imekwisha pita sasa tangu awekwe kizuizini na hakuwa akijua ni lini atakuwa huru.Tonny amekuwa ni mtu mwenye kuishi kwa uchungu mwingi na hakuwa akitaka kuonana na mtu yeyote yule..
Haikuwa siku ya kutazama wafungwa na mahabudu lakini nje ya ofisi ya mkuu wa gereza la Uwanga mwanadada mrembo aliyevalia suruali ya jeans ya bluu na fulana nyeupe akiwa na nywele ndefu zilizosukwa kwa ustadi mkubwa,alikuwa akisubiri mkuu wa gereza amalize mkutano wake na wageni waliokuwamo mle ofisini.Toka saa tatu asubuhi mwanadada huyu mrembo kupindukia alikuwa hapa akisubiri kuonana na mkuu wa gereza.
Saa sita za mchana ndipo mkuu wa gereza alipomaliza kikao chake na wale wageni.Baada ya wageni wale kuondoka katibu muhtasi wa mkuu wa gereza akamwita yule dada na kumkaribisha kuonana na Bw.Salvatory mpimwe mkuu wa gereza la uwanga.Baada ya kuingia mle ofisini dada yule alijitambulisha kama Slish McBenard akitokea jijini Washington Dc marekani.
“Karibu sana Slish.Naitwa Salvatory Mpimwe,mkuu wa gereza hili” akajitambulisha bw Salvatory.
“Mr Salvatory nimekuja toka Marekani kwa lengo moja tu la kuonana na rafiki yangu aitwaye Tonny mkisa ambaye nimeelekezwa kwamba anashikiliwa katika gereza hili.Tonny amekuwa rafiki yangu mkubwa kwa muda mrefu .Baada ya kuona kimya kimekuwa kingi na hakuna mawasiliano baina yetu niliamua nije nimtazame ili nijue ni kitu gani kimemsibu.Baada ya kufika hapa nikaambiwa kwamba anashikiliwa katika gereza hili.Kwa hiyo Mr salvatory nimekuja hapa ili niombe nipatiwe nafasi ya kuonana na Tonny walau hata kwa dakika kumi kwa sababu natakiwa kurudi Marekani leo jioni.”
Slish akasema huku akitoa baadhi ya nyaraka zake za kuthibitisha kile alichokuwa akikisema .Salvatory akazipitia nyaraka zile ikiwa ni pamoja na tiketi ya ndege inayoonyesha kwamba anatakiwa kuondoka na ndege ya saa kumi na mbili za jioni kurejea nchini Marekani.Baada ya kumaliza kuzipitia nyaraka zile akamwangalia Slish usoni kwa makini halafu akasema
“Slish ,ni kweli Tonny anashikiliwa katika gereza hili kwa muda sasa .hatuwezi kusema kwamba amefungwa lakini amezuiliwa hapa kwa kwa ajili ya uchunguzi wa mambo Fulani ya kiserikali.Uchunguzi huo bado unaendelea.Pamoja na safari ndefu ya kutoka Marekani mpaka hapa kwa lengo moja tu la kumuona rafiki yako Tonny ,napenda kukutaarifu kwamba siku ya leo si maalum kwa ajili ya kutazama wafungwa na mahabusu.Ili kuonana na rafiki yako unatakiwa kufika hapa katika siku iliyotengwa maalum kwa ajili hiyo.Ili kukusaidia itanilazimu kuvunja taratibu za gereza na kukuruhusu uonane na Tonny kwa siku ya leo.Ni kinyume cha utaratibu kufanya hivi lakini kutokana na kwamba hutaweza kusubiri hadi siku hiyo ifike kwa kuwa unatakiwa kuondoka leo nitakupeleka ukaonane na Tonny. Ila kwa tahadhari ni kwamba kwa siku za karibuni Tonny amekuwa ni mtu asiyetaka kuonana na mtu yeyote.Kwa mujibu wa madaktari wetu ni kwamba Tonny anasumbuliwa na tatizo la kisaikolojia.Kuwa mwangalifu sana wakati ukiongea naye.”
Mkuu wa gereza akainuka akamwambia Slish amfuate.
“Umefahamiana na Tonny lini? “ Bw Salvatory akamuuliza Slish wakati wakitembea kuelekea katika chumba ambacho wafungwa hukitumia kukutana na ndugu na jamaa zao
“Tonny nimefahamiana naye miaka kama saba iliyopita alipokuja Marekani kusoma.Toka wakati huo tumekuwa marafiki wakubwa” Slish akajibu kwa ufupi.Salvatory hakuuliza tena swali lingine.
Mwendo wa kama dakika kumi na mbili hivi,wakawasili katika chumba kimoja kikubwa kilichokuwa na meza kadhaa.Salvatry akamwelekeza Slish akae katika meza moja asubiri pale wakati akienda kumchukua Tonny.
Pamoja na kwamba kila kitu katika gereza lile kilikuwa kikiongozwa na mitambo maalum ya usalama,lakini bado chumba cha Tonny kiliendelea kulindwa na askari wawili wenye silaha kwa saa ishirini na nne.Tonny alifahamika kwa jinsi alivyokuwa mtu hatari hivyo hawakutaka kumpa nafasi hata ndogo ya kutoroka gerezani.
Salvatory akasalimiwa kijeshi na askari magereza wale waliokuwa wakilinda chumba cha Tonny ,akaitikia salamu ile halafu akachukua redio call toka kwa mmoja wa wale askari akaomba afunguliwe chumba namba 22D,.Sekunde chache baadae lango likafunguka akaingia ndani. Tonny alikuwa amejilaza kitandani,akageuza shingo na kumuona aliyeingia mle chumbani kuwa ni mkuu wa gereza ,hakumjali akaendelea kujilaza.
“Habari yako Tonny? Bw Salvatory akasema
Tonny hakujibu kitu wala hakusumbuka kumuangalia
“Tonny ,nafahamu hutaki kuonana na mtu yeyote kwa sasa,lakini nimekuja mwenyewe na ninaomba unisikilze.” Akasema Salvatory huku akimsogelea Tonny ambaye alionekana mawazo yake yalikuwa mbali sana na wala hakuwa na muda wa kumsikiliza.
“Tonny nimekuletea taarifa.Kuna rafiki yako anaitwa Slish amekuja kutoka Marekani kwa ajili ya kukujulia hali.Siku ya leo si siku maalum ya kutazama wafungwa na mahabusu lakini nimeamua kuvunja taratibu za gereza na kumruhusu aje akuone kwa sababu natakiwa leo hii hii aondoke kurudi zake Marekani.Yuko katika chumba cha maongezi akikusubiri.tafadhali Tonny nakuomba kubali kuonana naye,ametoka mbali kwa ajili ya kuja kukuona wewe” Salvatory akasema lakini bado Tonny hakuonekana kumjali wala kumtazama.Mkuu wa gereza akamtazama Tonny kwa sekunde kadhaa na kuita
“Tonny…” tonny hakujibu kitu.
Salvatory hakutaka kuendelea tena kumsisitiza Tonny kuonana na Slish akageuka na kuanza kuondoka zake.Wakati amefika mlangoni Tonny akainuka na kusema
“Wait !!…Salvatory akasimama akageuka na kumtazama Tonny ambaye sasa alikuwa amekaa kitandani.
“Nakwenda kumuona” Tonny akainuka pale kitandani huku akitembea kwa mwendo wa uchovu kuonyesha ni jinsi gani alivyochoshwa na maisha yale ya gerezani.Mkuu wa gereza akiongozana na wale askari wawili wenye silaha wakamuongoza Tonny hadi katika ukumbi wa maongezi ambako Slish alikuwa amekaa akimsubiri Tonny.Mara tu Tonny alipotokeza Slish akasimama huku akionyesha dhahiri kupatwa na mshangao mkubwa kwa kuiona hali ya Tonny.Machozi yalikuwa yakimlenga.Tonny alikuwa amechoka sana.Salvatory akamuongoza Tonny hadi katika meza ile aliyokuwa amekaa Slish .
“Slish rafiki yako huyu hapa.Una dakika ishirini za kuongea naye” Akasema Salvatory huku akiondoka na kuwaacha wale askari wakiwalinda
“Excuse me officers,Could you give us some privacy ?? Slish akawaomba wale askari magereza ambao walimwelewa wakajisogeza pemBeni na kuwaacha Slish na Tonny peke yao mezani. Tonny akamkazia macho Slish halafu akasema
“sina kumbu kumbu kama tumewahi kuonana” Tonny akasema
“Shhhhhh….” Slish akasema huku akiweka kidole mdomoni mwake kumuashiria Tonny anyamaze.
“Nina dakika ishirini tu za kuongea nawe.Naomba niongelee moja kwa moja suala lililonileta hapa.” Slish akasema na kumtazama Tonny usoni.
“Monica amenituma “ Slish akasema na kukaa kimya.
“Monica !!!! Tonny akauliza kwa mstuko.
“ndiyo Monica” Slish akajibu
“Ouh Monica I miss her so much.Anaendeleaje?
“Monica anaendelea vizuri .Pamoja na mambo aliyonituma kwako ,ameniomba nikufikishie salamu nyingi sana .Anasema kwamba hataweza kukusahau katika maisha yake na hatachoka kukusubiri hadi pale utakapokuwa umetoka gerezani” Slish akasema na kumtazama Tonny ambaye alizama ghafla katika mawazo mengi.Ni wazi alikuwa amekumbuka mbali mno.
“Amekutuma nini ? Tonny akauliza
“Amenituma nikupe miwani hii” Slish akasema huku akiitoa miwani Fulani mikubwa katika pochi lake iliyoonekana kama miwani ya jua akamkabidhi Tonny ambaye moja kwa moja alijua miwani ile ilimaanisha nini.Aliitazama miwani ile akaikunjua na kuivaa.

USIKOSE SEHEMU IJAYO..........................................
 
BRING BACK OUR GIRLS

SEHEMUYA 27

ENDELEA.............................................

Sekunde ile ile alipoivaa akaanza kuisikia sauti ya Monica
“Hello Tonny,habari yako.napenda kwanza nikupe pole nyingi kwa kuwepo gerezani hadi leo hii.Nafahamu mateso unayoyapata gerezani.Nafahamu bila mimi yasingekupata haya yaliyokupata.Lakini yote namwachia Mungu kwani yeye ndiye anayepanga kila kitu kitokee.Ningependa nije mimi mwenyewe lakini siwezi kuruhusiwa kuingia nchini Tanzania kwani serikali yenu ilinipiga marufuku kuingia nchini Tanzania tena .Badala yangu nimemtuma Slish akuletee ujumbe huu muhimu.Tonny kwa sasa nimerudi katika makao makuu ya CIA hapa Marekani.Siku chache zilizopita,nilipata taarifa kwamba kwamba kuna uwezekano wa kutokea matukio ya kigaidi katika mkutano wa Sulivan unaotarajia kufanyika siku chache zijazo jijini Arusha linalotarajiwa kufanyw ana kikundi icha Alshabaab.Pamoja na kwamba uko gerezani lakini unaweza ukatafuta njia ya kuzuia shambulio lolote lisitokee.Mtu anayeratibu shambulio hilo anasemekana kwamba ni Abdulkhareem Al Iman raia wa Somalia .Tafadhali Tonny fanya kila uwezalo ili kulizuia shambulio lolote lisitokee kwani watu wengi watapoteza maisha .Mwisho nakuomba ukifanikiwa kutoka gerezani njoo marekani ,nitakusubiri siku zote ili tuwe pamoja.Bado ninakupenda na siku zote utabaki kuwa mwanaume wa maisha yangu” taarifa ile ikamalizika.Tonny akaivua miwani ile na kumrudishia Slish.
“Nenda kamwambie Monica kwamba nashukuru kama bado anaendelea kunikumbuka ,kunipenda na kuniombea ili siku moja tuwe pamoja,lakini kwa hili analotaka nilifanye sintaweza kamwe.Mwambie sitaki na siwezi tena kufanya jambo lolote kwa ajili ya nchi hii.I sacrificed my life for this country and look where I am now? For two years I’m locked in here,dying in jail for no reason.So why should I do anything for this country? I hate this country.Maisha yangu yote nimekuwa nikifanya kazi za nchi hii kiasi kwamba nimejisahau hata mimi mwenyewe,hapa nilipo sina mke sina mtoto sina raha yoyote katika hii dunia.Mwambie Monica nimekwisha achana na kazi hizi.nataka kuishi maisha mapya.Ahsante kwa kunitembelea.” Tonny akasema huku uso wake ukionyesha hasira za wazi .Akainuka na kuwaita wale askari wawili.
“Nirudisheni katika chumba changu,nimeshamalizana na huyu dada” Askari wale walimuongoza Tonny kurudi katika chumba chake huku Slish akiwa haamini kilichotokea.Baada ya kutembea hatua kadhaa Tony akasimama ,akageuka na kumtazama Slish.
“Slish.! tell Monica I love her” Akasema Tonny halafu akaondoka na hakugeuka tena.
Tonny akarudishwa katika chumba chake akaenda kukaa kitandani.Akainama huku akishika kichwa chake kwa mikono yake miwili.Alizama katika lindi la mawazo
“ Lolote litakalotokea,na litokee tu.Sitaki kujihusisha tena na kitu chochote kuhusiana na usalama wa nchi hii.Nimefanya mambo mengi makubwa ,nimehatarisha maisha yangu mara nyingi lakini hakuna faida yoyote niliyopata na leo hii ninaozea gerezani kwa kosa ambalo silifahamu.” Tonny akawaza halafu akajilaza tena kitandani.Dakika tano baadae akainuka na kukaa.Akasimama na kuzunguka zunguka mle chumbani

“Siku chache zilizopita,nilipata taarifa kwamba kwamba kuna uwezekano wa kutokea matukio ya kigaidi katika mkutano wa Sulivan unaotarajia kufanyika siku chache zijazo jijini Arusha linalotarajiwa kufanyw ana kikundi icha Alshabaab.Pamoja na kwamba uko gerezani lakini unaweza ukatafuta njia ya kuzuia shambulio lolote lisitokee.Mtu anayeratibu shambulio hilo anasemekana kwamba ni Abdulkhareem Al Iman raia wa Somalia “

Maneno haya ya Monica yakajiruida tena katika kichwa chake.akainama na kutafakari kwa kina

“No ! No ! Not this time.Monica haelewi ni mateso gani ninayapata humu gerezani.Nilipambana kufa na kupona kwa ajili ya nchi yangu lakini hakuna mtu yeyote anayenithamini.Leo nimefungwa na sijulikani tena.Ni bora niendelee kukaa gerezani kuliko kuyatoa maisha yangu kwa watu wasiothamini mchango wangu.” Akawaza Tonny akalichukua gazeti akatazama picha ya jengo utakamofanyika mkutano huo wa Sullivan
“ Jengo kubwa ,zuri na la kupendeza lakini siku chache zijazo hakuna kitakachosalia.Nawafahamu alqaeda kama wamepanga shambulio ni lazima watalitimiza.” Tonny akalirudisha gazeti mahala alikolitoa.
“Nilifanya kazi kubwa sana kumkamata Abdool nchini Sudan,niliwakomboa maafisa walioshikiliwa mateka na waasi wa Uganda,nimefanya kazi nyingi za kuhatarisha maisha yangu lakini hakuna anayekumbuka mchango wangu.Monica nasikitika sana kwa kukataa ombi lako.Sina kwa sasa nguvu za kuzuia shambulio lolote lisitokee.” Tonny akasema taratibu halafu akaketi kitandani
Sura ya Monica ikamjia akilini.Akakumbuka siku ya kwanza walipokutana katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro,akakumbuka jinsi alivyomukoa katika shambulio lililotokea katika klabu ya usiku kule Arusha ,akakukmbuka jinsi walivyofika Moshi na kujificha katika nyumba ya jasusi mwenzake.Picha ya mwanamke mrembo,mweupe na mwenye uzuri usioelezeka ikamjia .Monica akiwa mtupu wakifanya mapenzi .
“Ouh ! siwezi kuisahau siku hii.I love you Monica” Tonny akasema huku akifumba macho na kujishika kifuani mahala unapokaa moyo na kwa mara ya kwanza akatabasamu
“Natamani nikuone tena Monica lakini siwezi.Ninaozea gerezani” Tonny akasema na kwa mbali machozi yakamlenga

“Mwisho nakuomba siku ukitoka gerezani njoo marekani ,nitakusubiri siku zote ili tuwe pamoja”

maneno ya mwisho katika ujumbe ule wa Monica yakamjia kichwani.
“Monica bado ananipenda na anahitaji kuishi na mimi.Ninampenda Monica.Sijawahi kukutana na mwanamke niliyempenda kama yeye.Sijui kama nitaweza kumuona tena kwa sababu sijui lini nitafanikiwa kutoka katika kuta za gereza hili.” Tonny akawaza akiwa katika hali ya kukata tamaa.
“Kuna wazo linanijia.Pengine labda suala hili linaweza likanisaidia kutoka gerezani.Iwapo nitawataarifu kwamba kuna tetesi za kuwapo kwa shambulio la kigaidi ninaweza nikapata nafasi ya kutoka humu gerezani.Nimewekwa humu kizuizini kwa kosa la kufahamu mpango wenye kuhatarisha usalama wa nchi na nikashindwa kuvitaarifu vyombo vya usalama.Hiki ndicho kitu kinaniweka gerezani hadi leo hii nikituhumiwa kuhatarisha usalama wa nchi.Leo hii nina taarifa za mpango mwingine wa magaidi,je nikiwataarifu watanielewa na kunifikiria kunitoa gerezani? Ngoja nijaribu .Hii inaweza ikawa ni njia ya kunitoa humu gerezani.” Tonny akawaza huku akiuendea mlango akabonyeza kitufe na mara dirisha dogo likafunguliwa na askari aliyekuwa akilinda pale mlangoni.
“Unataka nini Tonny” askari yule ambaye kiumri hakupishana sana na Tonny akauliza
“Afande nina shida.”
“Shida gani?
“Sikiliza afande nimekuwa humu gerezani kwa miaka miwili kwa kosa ambalo silifahamu.Hakuna mtu yeyote anayenijali wala kuuthamini mchango wangu kwa nchi hii.Nimefanya mambo mengi kwa usalama wa nchi yangu lakini leo hii ninaozea gerezani.Kwa kuwa nimesahaulika na hakuna mtu yeyote anayeonyesha kunijali nimeamua kutafuta mimi mwenyewe mbinu za kunitoa gerezani.” Tonny akasema huku askari yule akimuangalia kwa macho ya wasi wasi kwani walikwisha taarifiwa kwamba Tonny ni mtu hatari .
“Afande ninaposema kwamba natafuta namna ya kujisaidia mimi mwenyewe ili nitoke humu gerezani sina maana ya kuvunja au kutoroka gerezani.Natafuta msaada wa watu wenye nguvu ya kuweza kunitoa humu gerezani.Ili kuwafikia watu hao ninaomba msaada wako “
“Msaada upi Tonny? “ askari yule akauliza kwa wasi wasi.
“naomba unipatie kalamu na karatasi.Nitaandika barua na nitakuomba utakapotoka mchana wa leo uipeleke mahala nitakapokuelekeza na umpe muhusika nitakayekutajia. Ukifanya hivyo utakuwa umenisaidia sana na ninaweza kupata msaada wa kunitoa gerezani.” Tonny akasema na kumtazama askari yule ambaye alikuwa na wasi wasi mwingi.Baada ya kufikiri kwa dakika kama tatu hivi akachana karatasi katika kitabu walichokitumia kukabidhiana lindo akampa Tonny ambaye alishukuru na kuanza kuandika .Aliandika maandishi ya kijasusi ambayo si rahisi kwa mtu wa kawaida kuyaelewa.Kwa lugha rahisi aliandika hivi:-

Pamoja na kuwekwa kizuizini kwa kosa la kutokutoa taarifa mapema juu ya mpango uliohatarisha usalama wa nchi,bado ninaendelea kusisitiza kwamba sikuwa na nia mbaya kwa nchi yangu.Kwa kuthibitisha kwamba nina mapenzi makubwa kwa nchi yangu nawataarifu tena kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kutokea kwa shambulio la kigaidi katika mkutano wa Sullivan utakaofanyika siku chache zijazo jijini Arusha.Ninawapa tahadhari hii ili mchukue tahadhari ya mapema.kwa taarifa zaidi onaneni na mimi gerezani
Visto 01

Tonny akarudia tena kuusoma ujumbe ule akaridhika kwamba ni mzuri akaikunja vizuri ile karatasi na kumpatia yule askari magereza na kumuelekeza aipeleke katika ofisi zao na ahakikishe amempatia mkurugenzi.Alimuelekeza kila kitu ili kuweza kumfikia mkurugenzi.

*********************

Slish alitoka mle gerezani akiwa na mawazo mengi.Kitendo cha Tonny kukataa kushughulikia taarifa alilopewa na Monica kuhusu kutokea kwa shambulio la kigaidi katika mkutano wa Sullivan ,lilimuumiza kichwa.Akarudi katika gari lililompeleka pale gerezani akatoa kompyuta yake ndogo akampigia simu Monica.Hakutaka kutumia njia za kawaida kuwasiliana na Monica ili kuepusha mawasiliano yao kunaswa .
“Hello Slish umefanikiwa kuonana na Tonny? Monica akauliza baada ya kupokea simu
“Nimeonana naye dakika chache zilizopita” Slish akajibu
“Vipi hali yake? Monica akauliza kwa haraka
“Amedhoofu sana na inaonekana suala la kuwekwa gerezani limemuathiri kisaikolojia.”Slish akasema na kumfanya Monica avute pumzi ndefu
“Masikini Tonny..Ulimwambia kwamba bado ninampenda na ninamsubiri atoke gerezani? Monica akauliza
“Ndiyo Monica.Nilimwambia na alifurahi sana kusikia hivyo.Alifarijika mno”
“Nafurahi kusikia hivyo.Vipi kuhusu kazi niliyokutuma amekubali kuifanya?
Slish akanyamaza kidogo na kisha akasema
“Monica hapa kuna tatizo.Tonny amekataa kata kata kuifanya kazi ile.Bado ana hasira nyingi kwa kuwekwa gerezani.Tonny anasikitika sana kwa sababu hakuna mtu anayeutambua mchango na thamani yake kwa nchi yake.Amesema kwamba lolote litakalotokea na litokee yeye hatajali tena kwani kwa sasa anachokitaka ni kuishi maisha mapya kabisa na kuachana na kazi hizi .Kwa jinsi nilivyomuona hakuwa na hata chembe ya utani katika matamshi yake.Alimaanisha kila kitu alichokisema.Ila mwisho kabisa alisema nikwambie kwamba anakupenda sana..Kwa hiyo tutafanya nini Monica?
Sekunde kadhaa zikapita halafu Monica akasema
“Hakuna tatizo Slish.kazi yako imekwisha hapo Tanzania.Subiri upande ndege urejee marekani.Ninamfahamu vizuri Tonny nina uhakika lazima atatafuta namna ya kufanya.Hawezi kukubali tukio kama hili litokee.” Monica akasema kwa kujiamini
“Monica kwa hali ilivyo na mahala alipohifadhiwa Tonny ni vigumu sana hata kupata mawasiliano na watu wa nje.hata mimi mwenyewe nimemuona kwa huruma ya mkuu wa gereza” Slish akasema
“Slish namfahamu vizuri Tonny.He is a smart guy.Nina uhakika atafanya nilivyomwambia.Usiwe na hofu” Monica akasema

************************

Mourine Kyaso mkurugenzi mpya wa idara ya ujasusi nchini alikuwa ni mtu wa mwisho kuwasili ikulu katika kikao cha dharura kilichoitishwa na rais kwa ajili ya kutathmini hali halisi ya usalama kabla na wakati wa mkutano wa Sullivan.Baada ya kuwasili katika ukumbi wa mikutano akasalimiana na baadhi ya wakuu wa vyombo mbali mbali vya usalama nchini na kuketi.Dakika tatu baadae rais akajitokeza ,wajumbe wote wakasimama kama heshima kwa mheshimiwa rais ambaye aliwasalimu na kuwaomba waketi
“Jamani nimewaita hapa kwa dharura ili tupeane taarifa kuhusu hali ya usalama wa nchi .Nimepokea taarifa toka Ikulu ya Marekani kwamba mke wa Rais wa marekani Bi Gwen pring akiwa na binti yake Theresa atahudhuria mkutano wa Sullivan.Huu ni ugeni mkubwa sana.Ikulu ya Marekani imenitaarifu mapema ili tuweze kuchukua hatua zipasazo kiusalama.Kama mnavyofahamu marekani ina maadui wengi sana kwa hiyo inatubidi tuwe na ulinzi wenye uhakika mno.Inatubidi tuwe na uhakika kwamba hakuna tatizo lolote la kiusalama litakalotokea kabla na wakati wa mkutano.Pamoja na kwamba mke huyu wa rais atakuwa na ulinzi wake binafsi lakini tuna kila sababu ya kuimarisha ulinzi wetu wa ndani .Pamoja na mke wa rais wa marekani ,tunawategemea vile vile marais saba toka nchi mbalimbali za afrika ,pamoja na wawakilishi wa marais toka nchi mbali mbali.Ninaweza kusema kwamba afrika itahamia Arusha .Ugeni huu ni mkubwa na mzito sana na tunakila sababu ya kuhakikisha kwamba ulinzi unakuwepo wa kutosha.Hebu kila mmoja anieleze katika idara yake amejipanga vipi kuhakikisha kwamba usalama unakuwa wa kutosha kabla na baada ya mkutano huu”
Wa kwanza kusimama na kuwasilisha taarifa ya kiusalama alikuwa ni mkuu wa majeshi ya Tanzania ambaye alimuhakikishia mheshimiwa rais kwamba ulinzi umeimarishwa katika mipaka yote ya nchi na hakuna hofu ya uvamizi wowote kutokea. .Mkuu wa jeshi la polisi naye akasimama na kuwasilisha taarifa yake mbele ya kikao kile ambaye alimuhakikishia mheshimiwa rais kwamba jeshi la polisi limejizatiti vya kutosha kukabiliana na tatizo lolote.Ulinzi ulikuwa umeimairishwa katika viwanja vya ndege na katika sehemu zote za mipakani, katika sehemu zote ambazo wageni walitegemea kufikia,sehemu watakazotembelea na katika sehemu zote zitakamofanyikia mikutano midogo midogo ya kibiashara baina ya wafanya biashara wa kutoka marekani na wale wa Afrika.Baada ya mkuu wa jeshi la polisi kuwasilisha taarifa yake alifuata mkuu wa usalama wa taifa na baadhi ya wakuu wa vitengo vya usalama wa ndani vinavyojitegemea .Mtu wa mwisho kutoa taarifa yake alikuwa ni Bi Mourine Kyaso mkuu mpya wa idara ya ujasusi nchini ambaye alimuhakikishia mheshimiwa rais kwamba idara yake iko macho na mpaka sasa bado hakukuwa na tishio lolote la mashambuio ya kigaidi.Aliwatoa wasi wasi wajumbe wa kikao kile kwamba idara yake inashirikiana kwa ukaribu sana na mashirika mbali mbali ya ujasusi duniani na kwa pamoja bado hawajaweza kupata taarifa zozote za kuwepo kwa shambulio lolote la kigaidi nchini Tanzania
Baada ya kupokea taarifa zile toka kwa wakuu wa vyombo mbali mbali vya usalama na namna walivyojipanga katika kuhakikisha kwamba mkutano wa Sullivan unafanyika kwa amani bila tatizo lolote mheshimiwa rais akafunga kikao kile cha dharura na kwenda kuendelea na majukumu mengine.

USIKOSE SEHEMU IJAYO....................
 
SEHEMU YA 28
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Baada ya mkuu wa jeshi la polisi kuwasilisha taarifa yake alifuata mkuu wa usalama wa taifa na baadhi ya wakuu wa vitengo vya usalama wa ndani vinavyojitegemea .Mtu wa mwisho kutoa taarifa yake alikuwa ni Bi Mourine Kyaso mkuu mpya wa idara ya ujasusi nchini ambaye alimuhakikishia mheshimiwa rais kwamba idara yake iko macho na mpaka sasa bado hakukuwa na tishio lolote la mashambuio ya kigaidi.Aliwatoa wasi wasi wajumbe wa kikao kile kwamba idara yake inashirikiana kwa ukaribu sana na mashirika mbali mbali ya ujasusi duniani na kwa pamoja bado hawajaweza kupata taarifa zozote za kuwepo kwa shambulio lolote la kigaidi nchini Tanzania
Baada ya kupokea taarifa zile toka kwa wakuu wa vyombo mbali mbali vya usalama na namna walivyojipanga katika kuhakikisha kwamba mkutano wa Sullivan unafanyika kwa amani bila tatizo lolote mheshimiwa rais akafunga kikao kile cha dharura na kwenda kuendelea na majukumu mengine.

ENDELEA.........................................

Toka ikulu Bi Mourine akaelekea moja kwa moja ofisini kwake.Kwa wiki nzima sasa amekuwa na shughuli nyingi ,yote hii ni katika kuhakikisha kwamba mkutano wa Sullivan unafanyika kwa amani kama ilivyokusudiwa.Baada ya kushuka garini moja kwa moja akaelekea ofisini kwake.
“Anna kuna taarifa yoyote mpya? Akauliza Bi Mourine wakati akipita katika ofisi ya katibu muhtasi wake.
“Ndiyo mkurugenzi.Kuna mtu amefika hapa akajitambilisha kwamba yeye ni askari magereza na ana ujumbe muhimu toka kwa mtu anayeitwa Tonny ambaye anashikiliwa gerezani anayedai kwamba aliwahi kufanya kazi hapa” Bi Mourine akasimama na kumtazama katibu muhtasi wake na kuuliza
“Uko wapi ujumbe huo?
“Nimekuwekea mezani mkurugenzi” Anna akajibu.
Bi Mourine akaingia ofisini kwake na kutupa jicho mezani akakutana na bahasha mpya kwa haraka akaichukua na kuifungua.Akausoma ujumbe ule na kuurudia tena kwa mara ya pili na ya tatu.Akaegemea meza huku akitazama juu akafikiri kwa takribani dakika tano ,mwishowe akabonyeza kitufe kidogo katika meza yake na katibu muhtasi wake akaingia mara moja.
“Anna naomba unitafutie faili la huyu mtu anayejiita Visto 01 mara moja”
Anna akatoka na kwenda kulitafuta faili la Tonny
“Nakumbuka wakati ananikabidhi ofisi Mr Meshack Jumbo alinipa taarifa kwamba kuna mtu mmoja ambaye alikuwa mfanya kazi wa idara hii , anashikiliwa gerezani kwa ajili ya uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.Muda mrefu umepita sasa sijapata taarifa zozote kuhusiana na maendeleo ya uchunguzi wa makosa yake.” Akawaza Bi Mourine na mlango ukaunguliwa akaingia Anna .
“Bosi tayari nimekutumia “ Akasema Anna na Bi Mourine akaiendea kompyuta yake akaanza kulipitia faili la Tonny.Alipomaliza kulipitia faili lile akabaki mdomo wazi.
“Sikuwa nimelisoma faili la mtu huyu.Kumbe nchi hii tuna mtu mwenye uwezo mkubwa kama huyu.Lakini pamoja na uwezo wake wote sina sababu ya kuamini kile anachokisema.Huko gerezani aliko hana uwezo wowote wa kupata taarifa kubwa kama hii anayoisema.Idara yangu inashirikiana na CIA na mpaka sasa hatuna taarifa zozote za kuwepo kwa shambulio lolote la kigaidi katika mkutano huu.Kama alikuwa na mpango wa kutumia nafasi hii kutolewa gerezani ,amejidanganya.Huu ni utawala mwingine kabisa na tunafanya kazi zetu kisayansi na si kwa hisia za mtu mmoja.” Akawaza Bi Mourine na kuichukua karatasi ile yenye ujumbe wa Tonny akaichana vipande vipande na kuitupa katika sehemu ya kutupia takataka.

*********************************************

Ndege ya shirika la ndege la Kenya airways inawasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro.Baada ya kusimama abiria wakaanza kushuka.Miongoni mwa abiria walioshuka katika ndege hii ni wanaume watatu waliokuwa wamevalia mavazi ya kikasisi ambao wote kwa pamoja hati zao za kusafiria zilizonyesha ni mapadre toka katika shirika la damu takatifu ya Yesu nchini Nigeria.
“karibuni sana Arusha “ Muhudumu wa sehemu ya uhamiaji akamwambia Fr.Felician oguku ambaye ndiye aliyekuwa kiongozi wa msafara ule.Huku akitabasamu Fr Felician akajibu
“Tunashukuru sana.Tunafurahi kufika Tanzania nchi ya amani na watu wakarimu “
“ Nafurahi kuona hata watu wa kidini kama ninyi mnahudhuria mkutano huu mkubwa wa Sullivan” Dada yule wa mapokezi akawaambia watumishi wale wa Mungu wakati akiendelea na zoezi la kugonga mihuri katika nyaraka zao za kuwaruhusu kuingia nchini.
“Pamoja na kufanya kazi ya kueneza injili ya bwana,lakini tunatengezeza pia bidhaa mbali mbali kwa ajili ya kuuza na kutusaidia katika kuiendeleza kazi hii ya kuhubiri neno la Mungu.Tunajitahidi kujitegemeza wenyewe bila kutegemea misaada ya wahisani.Kwa hiyo tunataka kuitumia fursa hii ya mkutano huu wa Sullivan kuzitangaza bidhaa zetu na kuzitafutia masoko zaidi” Akajibu Fr Felician
“Nawatakia kila la kheri” akasema dada yule mcheshi wakati akiwarudishia nyaraka zao za kusafiria.
Baada ya kukamilisha taratibu zote zinazotakiwa ili kuruhusiwa kuingia nchini,hatimaye watumishi wale wa Mungu wakaruhusiwa rasmi kuingia na wakatokeza nje ya uwanja ambako walilakiwa na watu wawili mmoja akiwa amevalia mavazi ya kikasisi ,wote wakaingia katika basi dogo lililokuwa na nembo ya shirika la damu takatifu ya yesu katika ubavu wake,wakaondoka pale uwanjani.
“hamkupata taabu zozote pale uwanjani? Ivan ambaye ndiye aliyekuwa dereva wa gari lile akawauliza
“Hapana.hatukupata taabu zozote zile.Tumevuka bila vikwazo vyovyote .Tanzania inaheshimu sana watumishi wa Mungu” Felician akajibu
“Imekuwa vizuri mmewahi kufika kwa sababu kuanzia kesho wageni kutoka Marekani wataanza kuwasili kitu kitakachopelekea ulinzi uimarishwe sana .” Ivan akasema
“Vipi kila kitu kimekwenda kama kilivyopangwa?
“Ndiyo Fr.Felician,kila kitu kinakwenda kama kilivyopangwa.”
“Ivan tafadhali nimechoshwa kuitwa jina hilo la Felician.naomba kuanzia sasa achana na jina hilo.” Felician akasema akionyesha dhahiri kukerwa na jina lile.
“Nimekuelewa Muhsin.majina haya ya bandia yana kero zake.”Ivan akasema
“Vipi umeongea na Abdulkhareem ? Muhsin akauliza
“Alimpigia simu Sultan saa mbili asubuhi akiwa jijini Nairobi.Yeye ataingia kutokea Kenya .Ataingia kama mgonjwa toka nchi za kiarabu aendaye kuonana na mchungaji anayetoa dawa huko maeneo ya Loliondo ambako bado watu wanaendelea kumiminika kwenda kupata dawa hiyo.Watu wengi wenye asili ya kiarabu wamekuwa wakitokea nchini Kenya na kwenda kwa huyo babu kwa hiyo hakuna mtu yeyote atakayemshuku kwa lolote.” Ivan akasema
“Vizuri sana.Nafikiri mpaka saa mbili usiku atakuwa amewasili .Tunamuhitaji sana kabla ya saa tatu usiku wa leo ili kazi ianze mara moja.” Muhsin akasema.
Safari iliendelea kimya kimya hadi walipofika eneo la Tengeru wakakata kona na kushika njia ya vumbi.Wakavuka nyumba za chuo cha mifugo na kuingia katika kitongoji cha Nambala wakavuka reli na kufuata njia iliyopandisha mlima.Nyuma ya mlima mdogo kulikuwa na jumba moja kubwa ambalo lilimilikiwa na mmoja kati ya matajiri wakubwa wa madini aitwaye Sultan ,mwenye asili ya kiarabu.Geti la jumba hili kubwa likafunguliwa na basi lile dogo likaingia na kwa haraka geti likafungwa.Gari likasimama na wageni wale wakashuka na kuingia ndani.Kila mmoja alikuwa akiustaajabia uzuri wa jumba lile,lililokuwa liking’aa kama kasri la kifalme.
“Karibuni sana” Mtu mmoja mfupi mwenye ndevu nyingi akajitokeza na kuwasalimu akina Muhsin.
“Naitwa Sultan ” akajitambulisha huku akishikana mikono na Muhsin
“Muhsin oguku” Muhsin akajitambulisha huku akishikana mkono na Sultan na kisha akaendelea kusalimia na kutambulishana na watu wengine waliokuwa wameambatana na Muhsin.
“Ndugu zanguni karibuni sana na mpumzike hadi jioni wakati tukimsubiri Abdulkhareem afike jioni ya leo ili ipango ya kazi ianze bila kuchelewa.” Sultan akawaambia wageni wale na kisha kila mmoja akapelekwa katika chumba chake kwa ajili ya mapumziko .

********************

Baada ya muda mrefu wa kumtafuta ,hatimaye serikali ya Somalia ilifanikiwa kumtia nguvuni Khaleed Aljameer ,kiongozi wa kikundi hatari cha Alshabaab kinachoendesha mapambano dhidi ya serikali ya Somalia .Baada ya muda mrefu wa mapambano dhidi ya serikali,hatimaye Khaleed akafanikiwa kukamatwa na moja kwa moja akaletwa nchini Tanzania katika mahakama kuu ya Afrika ya makosa ya jinai iliyoko jijini Arusha ili ahukumiwe kwa makosa ya mauaji aliyoyasababisha.
Kukamatwa kwa khaleed lilikuwa ni pigo kubwa kwa kikundi hiki chenye msimamo mkali.Kwa kulipiza kisasi Alshabaab wamekuwa wakiendesha mashambulizi kila kukicha katika kushinikiza kuachiwa huru kwa kiongozi wao anayeshikiliwa kizuizini nchini Tanzania lakini bila mafanikio.Baada ya kuona jitihada zote walizozifanya zinagonga mwamba hatimaye wakaamua kubuni mpango kabambe wa kuweza kumpata Khaleed
Taarifa za kufanyika kwa mkutano wa Sullivan nchini Tanzania zilikuwa njema sana kwa kikundi hiki kwani ingekuwa ni fursa nzuri kwao ya kuweza kufanikisha mpango wa kumpata kiongozi wao.Miezi sita kabla ya kufanyika kwa mkutano huo,Boko haram wakaanza kujenga mtandao mkubwa nchini Tanzania ili kufanikisha lengo lao.
Kufanyika kwa mkutano wa Sullivan jijini Arusha Tanzania kulipokelewa kwa mikono miwili na Alshabaab na hivyo kikundi hiki kilianza kwa siri kubwa kufanya maandalizi ya shambulio kubwa dhidi ya raia wa Marekani kwa lengo la kuishinikiza seriakli ya Tanzania kumuachia huru kiongozi wao.Mipango yote ilikuwa ikiratibiwa na Abdulkhareem raia wa Somalia ambaye ni mwanafizikia na mtaalamu wa mabomu..Jitihada za kikundi hiki za kuandaa shambulio zilipelekea kuunganisha nguvu na kikundi kingine cha kigaidi cha Boko Haram cha nchini Nigeria ambacho nacho kilikuwa na hasira na serikali ya Marekabni baada ya kiongozi wake kuuawa na vikosi vya marekani.
Wawakilishi wa makundi haya yaliyoungana katika kutekeleza mpango huu wakatumwa nchini Tanzania ili kuanza kazi mara moja.Nchini Tanzania mwenyeji wao alikuwa ni Sultan tajiri mkubwa anayefanya biashara ya madini.Wafuasi wa makundi haya mawili walikuwa wakiingia nchini kwa namna mbali mbali wakipitia katika kila pembe ya nchi.Wengine waliingia nchini wakitokea afrika kusini,wengine wakaingia nchini kwa kupitia Zanzibar,wengine walipita Kenya na katika nchi zote zinazoizunguka Tanzania.Kundi la mwisho kuwasili lilikuwa ni la akina Muhsin waliongia nchini kama makasisi kundi ambalo lilikuja kwa lengo moja tu kumaliza kazi waliyoianza.
********************
Uwanja wa maonyesho ya kilimo ya nane nane yanakofanyikia maonyesho ya bidhaa mbali mbali za wajasiriamali wakiwemo wale wa kutoka Kenya lilikuwa ndilo lengo kuu la kundi la kigaidi la Alshabaab kufanya shambulio lake kwa raia wa Kenya waliokuja kuhudhuria mkutano wa Sullivan na kuonyesha bidhaa mbali mbali.Muktar mmoja wa wawakilishi wa Alshabab ambaye alijulikana kama raia wa Kenya atokaye eneo la Turkana na amekuja kushiriki maonyesho ya bidhaa mbali mbali za wajasiriamali ndiye aliyekuwa mratibu wa shambulio hilo.Toka maonyesho haya yameanza amekuwa akifanya kazi moja tu ya kuandaa shambulio kubwa dhidi ya raia wa Kenya waliofika kwa ajili ya maonyesho haya.Mipango yote ilikwisha kamilika na haikuwa na ugumu kwani wajasiriamali wa Kenya walikuwa wamekusanyika katika banda moja wakionyesha bidhaa zao.Muktar naye alikuwa ni mmoja wao akionyesha bidhaa zake ambazo ni taa za kutumia nishati ya jua.Hakuna mfanyabiashara yeyote aliyegundua kama mtu waliyekuwa wakifanya naye biashara alikuwa ni mtu hatari sana na ambaye alikuwa na lengo la kuwamaliza wote .
**********************

Kama ilivyokuwa imetarajiwa saa mbili za usiku Abdulkhareem akawasili katika jumba hili la kifahari la Sultan .Kila mmoja alionyesha uso wa furaha sana baada ya kuwasili kwake.Huyu ndiye aliyekuwa kiongozi wa shughuli nzima.Alikuwa ameongozana na mwanamke mmoja aliyevaa miwani .Baada ya kupokelewa moja kwa moja akapelekwa katika chumba alichokuwa ameandaliwa .Kilikuwa ni chumba kikubwa kilichojitosheleza kila kitu.Abdul akajimwagia maji na alipomaliza kujiweka safi akatoka mle chumbani.Nje ya mlango alikuwepo mtu akimsubiri ambaye alimuongoza moja kwa moja hadi katika msikiti mdogo uliokuwamo ndani ya jumba lile ambamo alifanya ibada na kisha kurejea sebuleni ambako alikutana na Sultani wakaongea kidogo kisha wakaelekea katika ukumbi wa chakula .Katika ukumbi huu walikuwapo watu watatu tu ,Sultani ,Abdulkhareem pamoja na mwanamke aliyekuja naye.
“Hukupata usumbufu wowote njiani? Akauliza Sultani wakati wakipata chakula.
“Hapana sikupata usumbufu wowote.Haikuwa rahisi kunishuku kwa lolote baada ya kueleza kwamba nilikuwa naelekea kuonana na yule mchungaji anayetoa dawa kule Loliondo.Unajua kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la watu kutoka uarabuni kuja kupata dawa ya mchungaji huyo kwa hiyo haikuwapa watu wa mpakani shida yoyote .Vipi habari za hapa? Mambo yote yanakwenda vizuri?
“Huku hakuna shida yoyote Abdu.mambo yanakwenda vizuri kama tulivyoyanga.hakuna kitu kilichoharibika.”akasema Sultani
“Muhsin na wenzake wamekwishafika? Abdul akauliza
“wamefika muda mrefu sana na wako katika chumba cha mikutano.Uliyekuwa ukisubiriwa ni wewe pekee.”
“ Usalama ukoje mpaka sasa hivi ? kuna dalili zozote za kutiliwa shaka mpango wetu? Abdul akauliza
“kwa mujibu wa vyanzo vyetu ndani ya idara za usalama na serikalini mpaka sasa hakuna taarifa wala tetesi zozote zinazoonyesha kugunduliwa kwa mpango wetu.Hali bado iko shwari ingawa ulinzi umeimarishwa sana hasa baada ya kuwa na uhakika kwamba mke wa rais wa Marekani naye atakuwa miongoni mwa wahudhuriaji wa mkutano huu.Nilipata taarifa kutoka kwa wakala wetu aliyeko katika Idara ya ndani ya ujasusi akisema kwamba kuna mtu mmoja aliyefika pale ofisini kwao mchana wa leo na kujitambulisha kwamba yeye ni askari magereza na alikuwa na ujumbe muhimu aliotumwa na mmoja kati ya majasusi hatari ambaye yuko kizuizini katika gereza la uwangwa.Jasusi huyo aitwaye Tonny ndiye alifanikisha kukamatwa kwa Abdool nchini Sudan na kisha kumkabidhi kwa serikali ya Marekani.Vile vile ni huyu huyu Tonny ndiye aliyefanikisha tena kukamatwa kwa Abdool baada ya kuanikiwa kwa zoezi la kumtorosha miaka miwili iliyopita . Kwa taarifa nilizonazo ni kwamba Tonny amewekwa kizuizini kwa kosa la kuhatarisha usalama wa nchi kwa kuufahamu mpango ule wa kumtorosha Abdool bila kuitaarifu serikali.Kwa mujibu wa wakala wetu ndani ya idara hiyo ni kwamba askari huyo magereza alitumwa na Tonny aupeleke ujumbe muhimu kwa mkurugenzi wa Idara ile.Hakufahamu ujumbe huo ulikuwa ni ujumbe gani lakini baada ya kufanya uchunguzi kwa undani hakugundua kama ujumbe huo ulikuwa ukihusiana na sisi kwani katika kikao walichokaa jioni ya leo hakuna suala lolote la kuhusiana na sisi liliongelewa.Hii inatupa uhakika kwamba mpaka sasa hivi hakuna chochote kilichogunduliwa” Sultan akasema na kumtazama Abdul usoni.
“Kazi nzuri sana Sultan.Tunachokwenda kukifanya kitabaki katika historia ya Marekani na dunia kwa vizazi vingi vijavyo.” Abdul akasema

TUKUTANE SEHEMU IJAYO…………………………
 
BRING BACK OUR GIRLS
SEHEMU YA 29
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPIOTA
Kwa taarifa nilizonazo ni kwamba Tonny amewekwa kizuizini kwa kosa la kuhatarisha usalama wa nchi kwa kuufahamu mpango ule wa kumtorosha Abdool bila kuitaarifu serikali.Kwa mujibu wa wakala wetu ndani ya idara hiyo ni kwamba askari huyo magereza alitumwa na Tonny aupeleke ujumbe muhimu kwa mkurugenzi wa Idara ile.Hakufahamu ujumbe huo ulikuwa ni ujumbe gani lakini baada ya kufanya uchunguzi kwa undani hakugundua kama ujumbe huo ulikuwa ukihusiana na sisi kwani katika kikao walichokaa jioni ya leo hakuna suala lolote la kuhusiana na sisi liliongelewa.Hii inatupa uhakika kwamba mpaka sasa hivi hakuna chochote kilichogunduliwa” Sultan akasema na kumtazama Abdul usoni.
“Kazi nzuri sana Sultan.Tunachokwenda kukifanya kitabaki katika historia ya Marekani na dunia kwa vizazi vingi vijavyo.” Abdul akasema

ENDELEA………………..

“Inshallah “ Sultan akaitika kisha Abdul akasema
“Sultan pamoja na uhakika ulionao kwamba mpaka sasa bado mpango wetu haujagundulika,bado nina mashaka kidogo na huyu jasusi uliyesema yuko gerezani.Wasi wasi ni kwamba alituma ujumbe gani kwa mkurugenzi wake? Ninapatwa na wasi wasi kwa sababu kwa nini ujumbe huo autume katika kipindi hiki? Nadhani kuna ulazima wa kufuatilia jambo hili.Ongea na wakala huyo wakala wetu ,kwanza afanye juu chini ili tupate kilichoandikwa katika ujumbe ule na pili amtafute huyo askari aliyetumwa aupeleke ujumbe huo anaitwa nani na anaishi wapi na kisha uwatume vijana wetu wamtafute ili wafahamu na kufahamu aliambiwa nini na Tonny na baada ya kumuhoji auawe na kupotea kabisa.Ninassema hivyo kwa sababu kuna uwezekano hyo askari magereza akawa amepewa ujumbe wa maneno na Patrick .Tunahitaji kufahamu kama kuna kitu chochote aliambia kuhusiana na mpango huu” Abdul akaelekeza
“Ok Abdul usijali.Nitalifanya hilo haraka iwezekanavyo.Kuna kila ulazima wa kuchukua tahadhari mapema.” Sultan akajibu.
Dakika zipatazo arobaini walizitumia katika chakula na maongezi na baada ya kula wote wakainuka na kuelekea moja kwa moja katika ukumbi uliokuwa ukitumika kwa mikutano.Jumba hili ambalo waweza kuliita kasri lilikuwa limejitosheleza kwa kila kitu.Jumba hili lilijengwa mahsusi kama sehemu maalum ya kuratibu shughuli za mtandao wa Alqaeda katika ukanda wa afrika mashariki Ni kutokana na umuhimu wake ndiyo maana jumba hili lilijengwa na mkandarasi toka uarabuni lengo likiwa ni kuficha siri iliyo nyuma yake.
Chumba cha mikutano kilikuwa na watu kama ishirini waliokuwa wamekaa wametulia wakimsubiri mkuu wa operesheni ile ambaye ni Abdul. Sultan na Abdul wakaingia katika chumba cha mikutano na bila kupoteza muda Sultan akafungua kikao.
“Ndugu zanguni kwanza nawaomba samahani kwa kuchelewa kuanza kikao chetu.Hii nikutokana na kumsubiri mkuu wetu Abdul ambaye ilimlazimu kuingia hapa nchini kupitia Nairobi na kisha akapitia Loliondo na baadae amefika hapa.Ni safari ndefu na tunamshukuru Mungu kwani amefika salama salimini.Kwa wale wote msiomfahamu huyu ndiye Abdulkhareem.” Akasema Sultan huku akimnyooshea mkono Abdul ili watu wamfahamu.Huku akitabasamu Abdul akainuka na kuinama kidogo kisha akaketi.
“katika safari yake hii ameongozana na mwenzake ambaye anaitwa Safia Alwadhir” Safia mwanamke aliyekuwa ameongozana na Abdul akasimama na kuwasalimu watu wote mle chumbani kisha akaketi.Baada ya hapo likafanyika zoezi la kuwatambulisha mtu mmoja baada ya mwingine na kisha Sultan akasema.
“Kwa muda mrefu tuliokuwa tunafanya maandalizi ya mpango huu tumekuwa tukifanya kwa kufuata maagizo na maelekezo ya ndugu Abdul akiwa lakini leo hii tuko naye hapa na amekuja kwa kazi moja tu ya kuukamilisha mpango huu na kuandika historia mpya katika vitabu vya kumbu kumbu vya historia ya Marekani.” Sultan akanyamaza na kuwatazama wajumbe waliokuwa kimya kabisa wakimsikiliza kisha akaendelea.
“Kikao hiki ni cha kufanya majumuisho ya kazi nzima tuliyoifanya kabla ya utekelezaji wake hapo kesho kutwa.Kwa hiyo tuwe makini katika kufuatilia namna mpango mzima utakavyokuwa.” Sultani akasema kisha akaketi na kumkaribisha kiongozi wa operesheni ile ndugu Abdul ili aweze kuendelea kutoa maelekezo.
Wakati Sultani akikaa kumpisha Abdul atoe maelekezo yake simu yake ikatetema ,akaitoa mfukoni na kutazama mpigaji.Alikuwa ni Maya ambaye ndiye wakala wao katika idara ya ujasusi Tanzania.Akatoka nje ya chumba kile na kuipokea ile simu
“hallo Maya” Sultan akasema
“hallo Sultan.Muda mfupi uliopita tulikuwa katika kikao cha dharura hivyo ikanibidi niizime simu yangu.Nimeiwasha sasa hivi na kukutana na ujumbe wako ukitakana niwasiliane nawe mara moja.Kuna nini?
“Maya hebu kwanza nipe habari.Kuna taarifa zozote mbaya katika kikao mlichotoka kukaa?
“hapana Sultan mpaka sasa hakuna taarifa yoyote ya wasi wasi wa jambo lolote lile” maya akajibu
“Vizuri.Sasa maya kuna kazi ambayo tunahitaji uifanye haraka iwezekanavyo.”
“kazi gani hiyo Sultani? Maya akauliza
“Tunataka kufahamu kilichoandikwa katika ujumbe uliotoka kwa Tonny.Vile vile tunataka umfahamu askari aliyepewa ujumbe ule na Tonny aulete hapo ofisini kwenu..Unaweza ukayafanya mambo hayo kwa haraka?
Maya akafikiri kidogo kisha akasema.
“Nipe dakika ishirini hivi.Mkurugenzi wetu bado yupo na haonyeshi dalili zozote za kuondoka hapa ofisini.Ngoja nijaribu kutafuta namna nitakavyoweza kuingia ofisini kwake.Nitakupigia baadae.” Maya akasema na kukata simu.
Kisha maliza kuongea na simu Sultan akarejea ukumbini na kikao kikaendelea.
“Samahani ndugu wajumbe nilikuwa na simu ya muhimu sana .Tuendelee na kikao na kwa sasa namkaribisha ndugu Abdulkhareemambaye ndiye kiongozi wa operesheni hii ili aweze kutupa mwongozo.” Sultan akasema na kumkaribisha Abdul akasimama na kuwasalimia wajumbe kisha akasema
“Ndugu wajumbe,nafurahi kusimama mbele yenu leo hii na kutoa maelekezo ya mwisho ya mpango huu ambao utaistua dunia na kuandikwa katika vitabu vya historia ya Marekani.Kama mnavyofahamu mpango huu umeandaliwa muda mrefu toka tulipopata taarifa kwamba mkutano wa mwaka huu wa Sullivan utafanyika nchini Tanzania.Mpango huu umeunganisha nguvu toka kundi la Alshabaab na kundi la Boko haram la Nigeria.Boko haram ni washirika wetu na wamekuwa na sisi muda mrefu na hata walipokuja na kutaka kuungana nasi hatukusita kushirikiana nao kwa sababu tunauhusiano nao wa muda mrefu.Mpango huu una malengo makuu yafuatayo.Moja ni kuendeleza vita dhidi ya Marekani na washirika wake .Vita hivi havitakoma na vitaendelea milele na milele,vizazi kwa vizazi.Tutawashambulia raia wa Marekani kokote waliko duniani.Lengo lingine kubwa la mpango huu ni kumkomboa ndugu yetu Khaleed Aljameer , kiongozi wa Alshbaab aliyekamatwa na kuletwa hapa Tanzania kwa ajili ya kuhukumiwa katika mahakama kuu ya Afrika ya makosa ya jinai.Tumekuja kumchukua kiongozi wetu na kumrudisha katika mapambano.Ndugu zangu hayo ndiyo malengo makuu ya mpango huu ambayo yote yanatekelezwa kwa pamoja.”
Abdul akanyamaza na kuwatazama wajumbe waliokuwa kimya wakimsikiliza halafu akaendelea
“Kabla ya kuendelea kuuchambua zaidi mpango mzima,ninapenda kuwataarifu kwamba nimekuja na mwanasayansi anayeshughulika na mambo ya silaha za kibaolojia ambaye ni huyu hapa Safia Alwadhir..Amefuatana na mimi ili kuja kushirikaina nasi katika kulipiza kisasi cha mauaji ya mumewe na familia yake ,mauaji yaliyofanywa na majeshi ya Israel nchi ambayo ni mshirika mkubwa wa Marekani.Amekuja kutengeneza aina ya virusi ambavyo tutavitumia katika aina nyingine ya shambulio letu.Virusi hivi vinaitwa H65 virus.Ni moja kati ya virusi hatari sana .Ningependa nimpe nafasi ili aweze kutufafanulia kwa kirefu zaidi kuhusiana na virusi hivyo” Abdul akamkaribisha Safia Alwadhir ambaye bila kupoteza muda akaanza kutoa maelezo.
“Kwa muda mrefu nimekuwa nikifanya tafiti mbali mbali kuhusiana na virusi ambavyo vinaweza vikatumika kama silaha pale inapobidi.Nimekuwa nikijaribu kutengeneza aina mbali mbali za virusi ambavyo vingeweza kutumika kama silaha katika mapambano yanayoendelea lakini mara nyingi kila nigunduapo kirusi cha aina fulani basi wenzetu wamekuwa wakipata tiba yake mapema sana.Kwa siku za karibuni nimeweza kutengeneza kirusi cha H65 ambacho naweza kusema ndicho kirusi hatari kwa sasa duniani.Kirusi hiki ambacho bado hakijapatiwa kinga yake ,kinasambazwa kwa njia ya hewa.Mtu akishavuta hewa yenye kirusi hiki,humwingia mwilini na mara tu kirusi hiki kinapoingia mwilini mwa binadamu na kukutana na joto la mwili ,huweza kujizalisha na kuwa mamilioni ya virusi kwa muda mfupi sana.Kirusi hiki huanza kwa kushambulia mfumo wa upumuaji na kuharibu kabisa mapafu na kisha huingia katika damu na kuifanya damu igande ndani ya muda mfupi .Vile vile hushambulia sehemu za ubongo na uti wa mgongo hivyo kukata kabisa mawasiliano kati ya sehemu hizi muhimu na sehemu nyingine za mwili.Baada ya H65 kuingia mwilini mwa mtu,humchukua muda wa dakika thelathini kuanza kuonyesha dalili za maambukizi.Dalili ya kwanza ni mtu kupumua kwa shida na kuhisi maumivu makali sana kifuani .Pili mgonjwa hupata maumivu makali ya kichwa na uti wa mgongo na viungo vyote vya mwili huwa kama vinaungua moto .Baada ya dalili hizi ambazo huchukua kama dakika arobaini hivi mgonjwa hufariki dunia.Kwa taarifa yenu ni kwamba mara tu mtu anapokuwa ameambikizwa virusi hivi ,basi hakuna tena tiba wala dawa inayoweza kumponya zaidi ya kifo.Ndiyo maana ni kirusi hatari sana kwa sasa duniani kinachoweza kuua kwa muda mfupi Kwa kuwa bado hakina tiba na huua kwa muda mfupi na usambaaji wake ni kwa njia ya hewa hivyo iwapo kirusi hiki kitaachiwa katika hewa ,ndani ya muda mfupi idadi kubwa ya watu itakuwa imeambukizwa na ambao kila watakokuwa wakienda watakuwa wakiwaambukiza wenzao.Kwa mara ya kwanza katika historia ya dunia kirusi hiki kitatumika hapa Tanzania na kuandika historia mpya.” Safia akamaliza kutoa maelezo yake na kurudi kitini.Wajumbe wote waliokuwao katika kikao kile jasho lilikuwa likiwatoka.Abdul akasimama na kuendelea na maelekezo mengine .
“Tumemsikia Safia ambaye ametufafanulia kwa undani kabisa kuhusiana na kirusi hiki hatari ambacho tutakitumia katika shambulio letu.” Akasema Abdul kisha akawatazama wajumbe ambao wote walikuwa kimya wakimsikiliza halafu akaendelea.
“Kesho wageni wanaanza kuwasili kwa ajili ya mkutano wa Sullivan.Ndege ya kwanza itawasili saa sita za mchana ,ndege ya pili itawasili saa tisa na ya tatu itawasili saa kumi na moja.Kwa mujibu wa taarifa tulizonazo ni kwamba ndege ya mwisho kushusha wageni itawasili saa mbili za usiku.Hawa wote ni wageni kutoka nchini Marekani.Wageni wa mataifa mengine wao watakuja na ndege za mashirika mbali mbali ya ndege duniani lakini hao sisi hatuna haja nao sana,lengo letu sisi ni raia wa Marekani pekee.Kwa mujibu wa takwimu tulizonazo ni kwamba kutoka Marekani pekee watawasili watu takribani elfu moja na mia nne.Tayari tuna orodha nzima ya wageni wote wa kutoka marekani na sehemu zote watakazofikia na kutembelea.Vijana wetu wamefanya kazi nzuri sana ya kupata takwimu zenye uhakika.Mtandao wetu hapa nchini Tanzania umekuwa mkubwa na unaonyesha kufanya kazi kwa kujituma sana.” Abdul akatabasamu kisha akaendelea.
“Hoteli ya Arusha green valley peke yake itachukua wageni wapatao mia tisa wa kutoka marekani.Wageni wengine watafikia katika mahoteli mengine mbali mbali ambamo watachanganyika na wageni wa mataifa mengine.Kwa maana hiyo hoteli hii nayo imo katika lengo letu ingawa si kwa kiasi kikubwa lakini watu wetu tayari wako pale tayari kabisa kufanya kazi yoyote tutakayowatuma kufanya.Kesho kutwa saa tano asubuhi mke wa rais wa Marekani akiambatana na binti yake ,watatua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro na pale uwanjani atapokelewa na mke wa rais wa Tanzania ambaye ndiye atakuwa mwenyeji wake.Baadae atakuwa na maongezi na rais wa Tanzania na kisha ataelekea katika hoteli ya Tandala international hotel ambayo ina hadhi ya kimataifa na ambayo mke huyu wa rais wa marekani atalala kwa siku atakazokuwa hapa Arusha kwa mkutano.Jioni ya siku hiyo mkutano wa Sullivan utafunguliwa rasmi na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.Saa sita za usiku mkutano utaahirishwa hadi kesho yake saa nne asubuhi.Hii ndiyo itakuwa siku yetu ya shughuli,siku ya kuibadili historia ya Marekani.” Abdul akawatazama wajumbe ambao walikuwa kimya kabisa wakimsikiliza.

USIKOSE SEHEMU IJAYO..
 
BRING BACKOUR GIRLS
SEHEMUYA 30

Baada ya kumaliza kuongea na Sultani ,Maya akaelekea katika ofisi yake akiwaza ni jinsi gani angeweza kuifanya kazi ile aliyopewa ya kutafuta ni kitu gani kilikuwa kimeandikwa katika ujumbe ule uliotumwa na Tonny.Alitupa macho katika ofisi ya mkurugenzi wake na kumuona akiongea na simu.
“Sioni dalili kama mkurugenzi ataondoka usiku huu.Natakiwa nitumie akili kuingia ofisini kwake na kuutafuta huo ujumbe wa Tonny” Akawaza Maya huku akiinamia kompyuta yake .Maya ndiye mtu pekee anayeaminika kuufahamu vyema mfumo mzima wa mawasiliano wa idara hii.Amekuwa mfanyakazi wa idara hii kwa muda mrefu.Kwa dakika kama mbili hivi akabonyeza kompyuta yake na kisha akatabasamu
“Lazima ataniita ofisini kwake muda si mrefu” akawaza Maya.
Kama alivyokuwa ametarajia,simu yake ya mezani ikalia akaichukua haraka
“Maya kuna shida ofisini kwangu.Njoo mara moja” Alikuwa ni mkurugenzi wake
Kwa haraka Maya akaeleka ofisini kwa mkurugenzi wake.
“Maya kuna tatizo limetokea ghafla.Sielewi nini kimetokea lakini kompyuta yangu hii imejifunga na sielewi tatizo ni nini” Akasema mkurugenzi wake.
Maya akaketi kitini na kuanza jitihada za kuifungua huu moyoni akitabasamu kwani ni yeye ndiye aliyefanya vile.Dakika tano zilikatika bila kompyuta ile kufunguka ,na mara mkurugenzi akapigiwa simu akatoka mle ofisini.Hii ndiyo nafasi ambayo Maya alikuwa akiitafuta.kwa kasi ya ajabu akaanza kuutafuta ujumbe huo wa Tonny pale mezani bila mafanikio.Akasimama na kushika kidevu chake akiwaza.
“Atakuwa ameuficha wapi ujumbe huo” Akawaza na ghafla akatizama katika chombo cha kutupia takataka za karatasi akaiona bahasha moja ,akainama na kuichukua.Haikuwa na kitu ndani.Akachukua karatasi kadhaa zilizokuwamo katika chombo kile akazipitia na mara akatabasamu kwa furaha baada ya kuipata karatasi ile ambayo aliamini ilitoka kwa Tonny.Ilikuwa imeandikwa kwa maandishi ya kijasusi ambayo hakujua kimeandikwa nini .Haraka haraka akatoka mle ofisini na kuelekea katika ofisi yake kisha akaifungua ile kompyuta ya mkurugenzi.Akarudi tena ofisini kwa mkurugenzi na kuhakikisha imefunguka ,akatoka.Wakati akitoka akakutana na katibu muhtasi wa mkurugenzi.
“Kompyuta ya Mkurugenzi ilikuwa na shida ,lakini kwa sasa iko safi.” Akasema Maya
“Sawa Maya nitamtaarifu” akasema Anna
Ghafla Maya akajifanya amekumbuka kitu akamuuliza Anna.
“Anna leo mchana nilipata taarifa toka getini kwamba kuna mtu mmoja ambaye anadai ni askari magereza na anamtafuta mkurugenzi.Je ulipata taarifa zake?
“Ndiyo Maya ,alikuwa na ujumbe wa mkurugenzi”
“Ok anna.Unaweza ukakumbuka jina lake?
Anna akainua kichwa akakumbuka na kusema
“nakumbuka alisema anaitwa Ithan.sikumbuki jina lake la pili”
“Ok Ahsante Anna,nilikuwa nikihitaji kuweka kumbu kumbu sawa” akasema Maya huku akitoka na kueleka katika kompyuta yake,.Bila kupoteza muda akaingia katika kumbukumu za wizara ya mambo ya ndani na kuanza kutafuta majina ya watumishi wa idara hiyo.Watumishi wa wizara ya mambo ya ndani wenye majina ya Ithan walikuwa mia moja na ishirini.Katika kundi hilo alilolipata akatafuta Ithan ambaye anafanya kazi katika gereza la Uwangwa.Baada ya sekunde kadhaa akatabasamu .Tayari alikuwa na taarifa alizokuwa akitakiwa kuziwasilisha .
“ Ithan masanja mzaliwa wa mkoa wa Mwanza,mwenye urefu wa futi 5.6 alijiunga na jeshi la magereza miaka 6 iliyopita.Toka alipohitimu mafunzo yake katika chuo cha Magereza Mbeya amekuwa akifanya kazi katika gereza la Uwangwa.Ana mke na mtoto mmoja.” Haya ni maelezo mafupi ambayo Maya aliyapata toka katika taarifa za Ithan baada ya kuzitafuta katika kumbukumbu za wizara ya mambo ya ndani.Maelezo haya aliyaambatanisha na picha ya Ithan pamoja na ule ujumbe alioandikwa kijasusi ambao aliamini ulitoka kwa Tonny na kwa pamoja akavituma kwa Sultan Kisha tuma akainuka kitini na kuelekea katika vyoo vya wanawake na kutoa simu yake akazitafuta namba za Sultan akapiga
“Hallo Maya umeshafanikisha ile kazi niliyokutuma.? Sultan akauliza
“ Ndiyo Sultani nimeshafanikisha kuupata ule ujumbe wa Tonny pamoja na zile taarifa kuhusu yule askari aliyetumwa na Tonny alete ule ujumbe.Ujumbe ule wa Tonny umeandikwa katika lugha ambayo mimi siwezi kuisoma.Ina mana bado haujapata?”
“ Sijaupata kwa sababu bado niko katika chumba cha mikutano pamoja na Abdulkhareem na wajumbe wengine.Nitawasiliana nawe baadae”
“Sultan naomba usinipigie tena simu kwa usiku huu kwa sababu watu wote bado wapo na hapa haturuhusiwi kutumia simu zetu za kawaida.Tafadhali kama kuna suala lolote lile unalohitaji msaada wangu wasiliana nami siku ya kesho.Kwa usiku huu hali si shwari hapa ofisini”Maya akasema
“Maya ,wewe ndiye wakala wetu na tunakulipa fedha nyingi sana kwa ajili hiyo.Kipindi hiki tunakuhitaji sana kupita nyakati nyingine zote.Tuko katika mpango mzito na tunahtaji kila namna ya ushirikiano kutoka kwa kila wakala wetu .K wa hiyo usijaribu kuizima simu yako.Muda wowote tutakaokuhitaji nitakupigia simu .Jambo lingine endelea kuwa makini kama kuna jambo lolote utalisikia ututaarifu mara moja.Tumeelewana Maya? Sultan akauliza kwa sauti ya juu.
Maya akafikiri kidogo na kusema
“Nimekuelewa”
“ Good” Sultan akasema na kukata simu.
“Kazi hii inaanza kuwa ngumu.Kitendo nilichokifanya muda mfupi uliopita ni cha hatari na kama ningegundulika kingeweza kunitia matatani.Bahati nzuri mimi ni mtu makini na mwenye akili za haraka haraka.Itanibidi kuwa makini sana kwa sababu katika kipindi hiki wanaweza wakanilazimisha niwafanyie kazi ambazo ni za hatari .tatizo ni kwamba siwezi kukataa kwa sababu pindi nikikataa kufanya kazi zao wataniua mara moja..” Maya akawaza wakati akielekea mezani kwake.
Mara tu alipomaliza kuwasiliana na Maya ,katika chumba cha mikutano walichokuwamo akaingia Salum kijana ambaye anashughulika na masuala yote ya mawasilino.Alikuwa ameshika karatasi mkononi na moja kwa moja akaenda kumkabidhi Sultani ambaye akazichukua na kuanza kuzipitia.Karatasi ya kwanza ambayo ilikuwa na kivuli cha ujumbe wa Tonny hakuweza kuilewa kutokana na lugha iliyotumika,akaiweka pemBeni na kuishika karatasi nyingine ambayo ilikuwa na maelezo ya Ithan askari magereza ambaye Tonny alimpa ujumbe aupeleke kwa mkurugenzi wa idara ya ujasusi.
“Ndugu wajumbe kuna taarifa ambazo nimezipata sasa hivi” Sultani akawaambia wenzake.
“Kuna mtu mmoja anaitwa Tonny.Huyu ni mtu hatari sana .Ni jasusi wa hali ya juu mno haa nchini.Kwa sasa Tonny yuko kizuizini akishikiliwa kwa makosa ya kuhatarisha usalama wa nchi.Huyu Tonny ndiye aliyefanikisha kukamatwa kwa Abdool nchini Sudan na ni huyu huyu ambaye aliuzima mpango wa kumtorosha Abdool toka mahala alikohifadhiwa.Tulipokea taarifa toka kwa wakala wetu kwamba kuna mtu ambaye alitumwa na Tonny kupeleka ujumbe kwa mkurugenzi wa idara ya ujasusi.Hatukufahamu ujumbe alioutuma Tonny ulihusu nini lakini tulikuwa na mashaka kwamba kwa nini atume ujumbe katika idara yao katika kipindi hiki? Tulitaka kufahamu zaidi nini kilichokuwamo ndani ya ujumbe huo na kwa kumtumia wakala wetu tumefanikiwa kuupata ujumbe huo ambao ni huu hapa” Sultani akasema huku akiinua juu karatasi ile yenye ujumbe uliotoka kwa Tonny.
“Ujumbe huu umeandikwa kwa maandishi ya kijasusi kwa hiyo tutautuma kwa watu wetu wautafsiri katika lugha nyepesi ili tuweze kufahamu nini kilichomo ndani yake.Kwa sasa hatutaki kizingiti chochote hata kiwe kidogo namna gani.Tutapambana kuhakikisha kwamba hakuna kitu chochote kile kinachotuwekea aina yoyote ya kizingiti.” Sultani akasema.
“Pamoja na kuupata ujumbe huu ,lakini tuna uhakika gani kwamba Tonny hakumpa ujumbe wa mdomo huyo askari? Nina wasi wasi pengine Tonny alimpa ujumbe wa maandishi na ujumbe wa mdomo.na kama alipewa ujumbe wa mdomo tunahitaji kufahamu alimwambia nini? Hatuwezi kupuuzia suala kama hili.Huyu Tonny sijawahi kumuona kwa macho lakini nasikia ni mtu hatari sana.Sultani kuna vijana ambao umeweka jijini Dar es salaam? Abdul akauliza
“ Ndiyo Yupo Alrahman akiongoza watu wetu thelathini amabao wamewekwa tayari kwa ajili ya chochote kinachoweza kutokea.”
“Vizuri.Mtumie taarifa Alrahman atume timu ya watu sita waanze mara moja kumfuatilia huyo askari magereza wafahamu mahala anakoishi lakini wasifanye lolote lile hadi watakapopata taarifa toka kwetu tukiwataarifu nini cha kufanya.Kwa sasa tusubiri jibu la tafsiri ya ujumbe huu toka kwa watu wetu na tukishafahamu nini kimeandikwa katika ujumbe huu tutajua nini kifuate” abdulkhareem akasema.

***************

Toka alipompatia ujumbe Ithan aupeleke kwa mkurugenzi wa idara yao,Tonny hakuwa amepokea mrejesho wowote toka katika ofisi yao.Hii ilimuumiza kichwa sana.alitegemea baada ya ujumbe ule kupokelewa basi angetafutwa ili kutoa ufafanuzi na hili ndilo alilokuwa akilitaka kwani aliamini hii ingeweza kuwa moja ya njia ya kumtoa kizuizini.Mpaka giza linaingia hakukuwa na mtu yeyote kutoka idara ya ujasusi ambaye alikuja kumtembelea.
“Nashindwa kuelewa kama Ithan aliufikisha sehemu husika ule ujumbe niliompatia.Na kama aliufikisha ujumbe mahala husika kwa nini mpaka sasa hivi hakuna mrejesho wowote? Mkurugenzi wetu ninamfahamu vizuri si mtu wa kupuuzia taarifa yoyote ya kiintelijensia hasa toka kwa mtu kama mimi.Alikuwa akiniamini kupita kiasi.Nini basi kimetokea? Tonny alikuwa akizunguka zunguka chumbani kwake akiwaza.Hakuwa na habari kama mkurugenzi wake wa zamani Mr Meshack Jumbo alikwisha staafu kazi na sasa idara ya ujasusi ilikuwa ikiongozwa na mkurugenzi mpya mwanamama Mourine Kyaso.Tonny alikuwa ametelekezwa na kusahaulika gerezani.
“Kama watakuwa wameupata ujumbe ule na wakaamua kukaa kimya nina hisi pengine tayari watakuwa wamekwisha zipata taarifa hizo toka katika vyanzo vingine kwa hiyo taarifa yangu ikaonekana haina nguvu tena.Mungu wangu nitatoka lini katika gereza hili? Baada ya yote niliyoyafanya katika nchi hii lakini leo ninatelekezwa na kuachwa niozee gerezani. Nasikitika sana kwa jambo nililofanyiwa.Sikupaswa hata kidogo kutendwa namna hii.” Tonny aliwaza akiwa amekaa juu ya kitanda chake.
“ Japokuwa matumaini ya kutoka humu gerezani yanaanza kupotea taratibu,bado naamini kwamba Mungu yupo na siku moja atanijaalia nitatoka humu gerezani.Nikifanikiwa kutoka sitaki tena kujihusisha na masuala yoyote yanayohusiana na usalama.Niliyoyafanya kwa taifa hili yanatosha.Nataka nibadili maisha yangu .Nafikiria nikitoka hapa nifanye mpango wa kuhama kabisa nchi hii na kwenda kuishi mbali na hapa.Nataka nisahau mateso na machungu yote ninayoyapata gerezani kwa kosa ambalo mpaka leo hii silifahamu..” Akawaza kwa uchungu Tonny na mara sura ya Monica ikamjia akatabasamu
" I love you Monica" akasema Tonny.

USIKOSE SEHEMU IJAYO...........
 
Kwa hiyo mkuu ndio umemaliza kabisa?
Turushie hata vipande vingine viwili mkuu
Kwa spidi hii imenivutia baadae itabidi nianze ep 1

ila mkuu hiyo prifile pic imenishtua nikajua mkuu[color/darkblue]ibra 87amerudi.
 
BRING BACK OUR GIRLS

SEHEMU YA 31

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“Kama watakuwa wameupata ujumbe ule na wakaamua kukaa kimya nina hisi pengine tayari watakuwa wamekwisha zipata taarifa hizo toka katika vyanzo vingine kwa hiyo taarifa yangu ikaonekana haina nguvu tena.Mungu wangu nitatoka lini katika gereza hili? Baada ya yote niliyoyafanya katika nchi hii lakini leo ninatelekezwa na kuachwa niozee gerezani. Nasikitika sana kwa jambo nililofanyiwa.Sikupaswa hata kidogo kutendwa namna hii.” Tonny aliwaza akiwa amekaa juu ya kitanda chake.
“ Japokuwa matumaini ya kutoka humu gerezani yanaanza kupotea taratibu,bado naamini kwamba Mungu yupo na siku moja atanijaalia nitatoka humu gerezani.Nikifanikiwa kutoka sitaki tena kujihusisha na masuala yoyote yanayohusiana na usalama.Niliyoyafanya kwa taifa hili yanatosha.Nataka nibadili maisha yangu .Nafikiria nikitoka hapa nifanye mpango wa kuhama kabisa nchi hii na kwenda kuishi mbali na hapa.Nataka nisahau mateso na machungu yote ninayoyapata gerezani kwa kosa ambalo mpaka leo hii silifahamu..” Akawaza kwa uchungu Tonny na mara sura ya Monica ikamjia akatabasamu
" I love you Monica" akasema Tonny.

ENDELEA........................................................

Saa tano na dakika arobaini Salum kijana anayeshughulika na mambo yote ya mawasiliano katika operesheni hii akarejea tena katika chumba kile ambacho walikuwamo akina Sultani akiwa na karatasi mkononi na kumkabidhi Sultan,ambaye akaisoma na kumkabidhi Abdul khareem.Sultan akavua kofia yake na kujifuta jasho lililokuwa likimtoka katika kipara chake.Watu wote mle chumbani wakapatwa na wasi wasi kwamba karatasi ile haikuwa na ujumbe mzuri.Abdulkhareem akaisoma karatasi ile na kuirudia tena kwa mara ya pili na ya tatu kisha akasimama na kusema
“nadhani mnakumbuka kwamba Sultani aliwatangazia kuhusiana na ujumbe ule tuliotumiwa na wakala wetu ,uliotoka kwa jasusi aitwaye Tonny kwenda kwa mkurugenzi wa idara ya ujasusi Tanzania.Ujumbe ule ulikuwa umeandikwa kwa lugha ya kijasusi ambayo si rahisi kusomeka hivyo ikatulazimu kuutuma ujumbe ule kwa watu wetu ambao wameutafsiri na wameturudishia majibu ya nini kiliandikwa katika ujumbe huo.Ujumbe huo unasomeka kama ifuatavyo.

“Pamoja na kuwekwa kizuizini kwa kosa la kutokutoa taarifa mapema juu ya mpango uliohatarisha usalama wa nchi,bado ninaendelea kusisitiza kwamba sikuwa na nia mbaya kwa nchi yangu.Kwa kuthibitisha kwamba nina mapenzi makubwa kwa nchi yangu nawataarifu tena kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kutokea kwa shambulio la kigaidi katika mkutano wa Sullivan utakaofanyika siku chache zijazo jijini Arusha.Ninawapa tahadhari hii ili mchukue tahadhari ya mapema.kwa taarifa zaidi onaneni na mimi gerezani
Visto 01

Adulkhareem akamaliza kuusoma ujumbe ule na kuwatazama watu waliokuwamo mle ukumbini
“Hivi ndivyo Tonny alimuandikia mkurugenzi wake.” Abdulkhareem akasema
“Inaonekana tayari Tonny amekwisha nusa kitu Fulani .Toka mwanzo nilikuwa na mashaka makubwa kwamba kwa Tonny kuutuma ujumbe ule kwa kipindi kama hiki haikuwa bure.Ni lazima kuna kitu atakuwa amehisi.Tayari kuna fununu atakuwa ameshazipata.Ninaanza kuihisi hatari.Pamoja na kwamba yuko gerezani lakini huyu Tonny anaonekana bado ni hatari sana kwa upande wetu.Sielewi ni kwa nini baada ya kuupokea ujumbe huu mkurugenzi wake ameupuuzia na hajachukua hatua zozote.Hii ni faida kwetu na tunatakiwa tuitumie nafasi hii ipasavyo kwa sababu hata baada ya kupata ujumbe toka kwa Tonny ukiwataarifu kwamba kuna tetesi za kuwapo kwa shambulio Arusha bado hawajazipa uzito wowote.Pengine labda wameamua kupuuzia ujumbe ule wa Tony kwa kuzingatia kwamba Tonny amefungwa gerezani chini ya ulinzi mkali taarifa hizi atakuwa amezipata wapi? Je kuna watu ambao anawasiliana nao kwa siri na kupata taarifa hizi? Kama wapo ni akina nani? Nina hakika haya ni baadhi ya maswali yaliyopelekea hadi idara hii kuupuuza ujumbe wa Tonny.Pamoja na kupuuzwa huko na kutupwa kapuni kwa ujumbe ule muhimu tunatakiwa tufahamu kwamba Something is wrong here.. “ Abdul akasema huku akitoa sigara yake na kuiwasha.Akavuta mikupuo kadhaa halafu akasema.
“Sultani umepokea taarifa zozote toka kwa Alrahman kuhusu wale vijana niliokwambia awaandae?
“Ndiyo Abdul.Alrahmani amenitumia ujumbe wa maandishi muda mfupi uliopita na kunitaarifu kwamba vijana wako tayari na wamekwisha fahamu yule askari magereza Ithan anaishi wapi.Wanasubiri maelekezo toka kwetu nini wafanye”
“Good. Kinachotakiwa kufanyika hapa ni kumuua Tonny” Abdul akasema na kuwatazama watu waliokuwa wakimsikiliza kwa makini.Akavuta sigara na kutoa moshi mwingi
“Tonny anatakiwa auawe haraka sana kwa sababu kuna kitu amekwisha gundua.Kuna mtu ambaye atakuwa amempelekea taarifa hii .Mtu huyo aliyempa tarifa hizi ni wazi atakuwa amekwisha fahamu nini kinaendelea.Mtu huyo aliyetoa taarifa hizi kwa Tonny ambaye yuko gerezani inaonekana hakuwa na mtu mwingine wa kumpa taarifa hizi au Tonny ndiye mtu pekee anayemuamini.Tonny amejaribu kutoa onyo kwa idara ya ujasusi lakini wameonyesha kupuuzia onyo lake kwa maana hiyo anaweza akatafuta namna nyingine ya kuweza kuingilia kati operesheni hii.Kwa maana hiyo basi tunatakiwa tumuwahi kabla hajabuni njia mpya ya kuweza kuizima operesheni hii.Iwapo ataendelea kuwa hai basi tufahamu kwamba opersheni hii itaingiwa na mdudu kitu ambacho ni hatari kubwa kwa upande wetu.Muelekeze Alrahman awaelekeze vijana kwamba wavamie nyumba ya Ithan wamteke yeye na familia yake na kisha kesho asubuhi Ithan atakapokwenda kazini ampelekee Tonny kinywaji chenye sumu ambacho akinywa atafariki ndani ya muda mfupi.Ili than aifanye kazi hiyo inabidi apewe onyo kwamba asipoifanya hiyo kazi familia yake itaangamizwa.Asubuhi atakapokwenda kazini apewe chombo maalum ambacho atakiunganisha katika mitambo ya kamera za pale gerezani ambacho kitaweza kuunganisha mfumo mzima wa kamera za pale gerezani na kompyuta zetu na hivyo tutakuwa na uwezo wa kuangalia na kudhibiti kamera zote za ulinzi katika gereza lile.Lengo hapa ni kutaka kuhakikisha kwamba Ithan anafanya kile tutakachomuamuru afanye na si vinginevyo.Baada ya hapo atakwenda kumpatia Tonny chakula au kinywaji ambacho kitakuwa na sumu na ambacho kitamuua Tonny kwa muda mfupi.Ninaamini Ithan hatathubutu kufanya vinginevyo au kutoa siri hii kwa sababu kwanza atakuwa akitazamwa kila anachokifanya kupitia kamera na pili atakuwa akihofia familia yake ambayo itakuwa imeshikiliwa mateka kwa hiyo atafanya kila atakachoelekezwa kufanya. Akishamaliza kazi hiyo ili kuondoa kabisa ushahidi Ithan na familia yake yote nao wanatakiwa wauawe.Narudia tena kwamba katika operesheni hii hatutaki kabisa kuona kizingiti chochote hata kama ni kidogo namna gani .Operesheni hii imeandaliwa kwa muda mrefu na kwa gharama kubwa mno kwa hiyo kikwazo chochote hakihitajiki.Wote tulioko hapa tayari tumekwishajitoa kufa ilimradi kufanikisha lengo la operesheni hii.Tumeelewana? Abdul akawauliza wajumbe
“Tumeelewana” wote wakajibu
“Nafurahi kusikia hivyo.Sultani mtaarifu Alrahman kwamba nataka kazi hiyo ifanyike kwa umakini wa hali ya juu mno.Sitaki kusikia aina yoyote ya samahani .Nataka mpaka kufika kesho saa nne asubuhi Tonny awe amekufa.Nataka taarifa ya kila kinachoendelea kila baada ya dakka kumi na tano.Wengine mnaweza kwenda kupumzika kwani wengi wenu mnaonekana mmechoka kwa safari.Jiwekeni tayari kwa ajili ya siku ya keshoMimi na safia tunakwenda kuendelea na kuweka sawa H5 virus ambayo itatumika vile vile katika operesheni hii..
Abdul akasema kisha kila mmoja akainuka na kuelekea chumbani kwake.

*****************

Muda mupi baada ya kupokea maagizo toka kwa Sultan,Rahim akawaamuru vijana wake aliokuwa amewatuma kumfuatilia Ithan warejee nyumbani kwake mara moja.
“Nimewaiteni mrejee mara moja baada ya kupata maelekezo toka kwa viongozi wetu walioko Arusha.” Akasema Alrahman kiongozi wa kikundi kidogo cha watu 16 waliowekwa jijini Dar es salaam maalum kwa kufanya shughuli watakayoelekezwa kuifanya ambayo ingeonekana kuleta mushkeri katika kufanikisha mpango mkubwa uliopangwa kutekelezwa na Alqaeda wakishirikiana na kikundi cha Boko haram toka Nigeria.
“Viongozi wetu wa Arusha walituelekeza kwamba tutafute mahala anapoishi askari Magereza aitwaye Ithan halafu tusubiri maelekezo mengine.Nafurahi kwamba zoezi hilo limekwenda vizuri na tayari Ithan mmekwisha fahamu Ithan anaishi wapi.” Akasema Alrahman ambaye wenzake hupenda kumuita Rahman lakini yeye hupenda sana kujiita Rahim.
“Kazi tuliyopewa kuifanya usiku huu ni kuvamia nyumba ya Ithan na kumchukua yeye na familia yake na kisha waletwe hapa. Kuna kazi ya muhimu sana ambayo Ithan anapaswa kuifanya kesho asubuhi na itakamilika tu iwapo tutaishikilia familia yake na kutishia kuiteketeza iwapo hatafanya kazi tunayoitaka.Nahitaji zoezi hilo lifanyike kwa ustadi mkubwa sana na sitaki kusikia kosa lolote limefanyika.Nataka kazi hii ifanyike kiasi kwamba hakuna mtu yeyote anayeweza kuwa na udadisi wa aina yoyote ile.Mathias utaongoza wenzako katika shughuli hii.Kumbukeni kwamba Ithan ni mtu muhimu sana kwetu .Tuna mshuku kuwa ana taarifa muhimu zinazoweza kuhatarisha shughuli nzima inayoendelea hivi sasa huko Arusha.Kwa maana hiyo msithubutu kuingia ndani ya nyumba yake na kuvamia bila kuwa na uhakika kama Ithan yuko ndani .Narudia tena kwamba msivamie nyumba ya Ithan bila kuwa na uhakika kama Ithan yupo ndani.Kwa kufanya hivyo kunaweza mfanya akatoweka moja kwa moja na tusimuone tena jambo ambalo litakuwa baya sana kwa upande wetu.Kitu kingine msijaribu kutumia aina yoyote ya nguvu .Nawahitaji hapa baada ya saa moja.” Rahim akawaambia vijana wake ambao hawakupoteza muda wakachukua vifaa wanavyovihitajikwa ajili ya kazi ile ,wakaingia garini na kuelekea nyumbani kwa Ithan.
“Nyumba anayoishi Ithan imezungukwa na uzio wa michongoma .Noel , Sadiq na Shafii mtakuwa wa kwanza kuingia ndani.Kwa uchunguzi tuliokuwa tumeufanya hapo kabla, njia rahisi ya kuingia ndani ni kupitia dirisha la chooni .Mlango mkuu wa kuingilia ndani ni wa chuma hivyo hatutaweza kuufungua kwa urahisi.Mimi na Ayoub tutakuwa tukilinda usalama nje.Hivyo ndivyo operesheni nzima itakavyokuwa.Kuna yeyote mwenye swali? Mathias akawauliza vijana wake huku gari likiwa katika mwendo mkali.
“Iwapo tutaingia ndani na kuikuta familia peke yake bila Ithan tutafanya nini? Sadiq akauliza
“Ikitokea hivyo hatutakuwa na namna nyingine ya kufanya ,tutawachukua mateka mke na mtoto wa Ithan na kumsubiri hadi atakaporejea.lakini nina imani Ithan atakuwepo ndani” Mathias akasema.

******************

Mita mia moja toka nyumba anayoishi Ithan gari walilopanda Mathias na kundi lake likasimama Sixmund pekee ndiye aliyabaki garini .Kwa mwendo wa tahadhari wakaelekea ilipo nyumba ya Ithan.Si mbali sana na eneo lile ulisikika mziki mkubwa kutoka katika klabu moja ya usiku.Mida hiyo ilipata saa nane kasorobo za usiku.
Kwa kutumia mkasi mdogo wakatengeneza tundu katika uzio wa michongoma ulioizunguka nyumba ile ,tundu ambalo liliwawezesha kupenya na kuingia ndani.Mathias ndiye aliyekuwa wa kwanza kupenya na kuingia ndani.Akahakiki usalama na kisha kuwapa ruhusa wenzake waingie.Haraka haraka akawafanyia ishara akina sadiq na wenzake waelekee upande wa nyuma kulikokuwa na vyoo.Shafii akapiga magoti chini na Sadiq akapanda juu yake,akalifungua begi lake alilokuwa amelivaa mgongoni akatoa kifaa Fulani kidogo akaanza kukwaruza katika kioo kile cha dirisha taratibu na kisha akakivuta kipande kikubwa cha dirisha alichokuwa amekikata akaingiza mkono na kulifungua dirisha.Akalivua begi lake na taratibu akaanza kupenya katika dirisha lile dogo lakini lenye uwezo wa kumpitisha mtu mwenye umbo la kawaida.Alipopitisha kichwa na mabega akalishika bomba la maji na kuingia ndani.Noel akafuatia na wa mwisho akawa Shafii.Taratibu wakaufungua mlango wa bafuni na kutoka na kwa kunyata wakaufuata ujia uliokuwa ukielekea vyumbani.Nyumba ile ilikuwa na vyumba vitatu vya kulala vilivyokuwa vimeelekeana.Taratibu Sadiq akakiminya kitasa cha mlango wa chumba cha kwanza na kumkuta mtoto amelala.Akainua kidole kimoja juu kuonyesha kwamba kuna mtu mmoja.Chumba cha pili hakikuwa na mtu yeyote .Kilibaki chumba kimoja ambacho wote waliamini kwamba ni chumba cha Ithan.Bastora ikiwa mkononi Noel akakiminya kitasa cha mlango lakini mlango ulikuwa umefungwa kwa funguo.Akakiminya kitasa kile mara tatu mfululizo na kukiachia.na mara akasikia sauti kutoka ndani.
“Vanessa ? Unataka nini? Ilikuwa ni sauti ya Ithan akidhani kitasa kile kiliminywa na mwanae Vanesa aliyekuwa amelala chumba cha karibu. Noel akawafanyia ishara wenzake kwamba Ithan yuko mle chumbani.Akakiminya tena kitasa .
“Vanessa?? Ithan akaita na kwa mbali zikasikika hatua za mtu akielekea pale mlangoni na mlango ukafunguliwa.Ithan alitaka kupasuka moyo baada ya kukutana na watu waliokuwa wamezificha nyuso zao huku bastora mbili zikimelekea.
“Shhhhhhhhhhhhhhhh !! Usijaribu kupiga kelele hata kidogo la sivyo tutakuua wewe na familia yako yote” Noel akasema kwa ukali na kumsukumia Ithan chumbani.Mke wa Ithan aliyekuwa amelala kitandani akastuka na kutaka kupiga kelele lakini Shafii akamuwahi na kumuelekezea bastora.
“Usijaribu kupiga kelele….” Rebeka mke wa Ithan akaogopa na kubaki akitetemeka.Na mara Sadiq akaingia akiwa amembeba Vanessa mtoto wa Ithan.
“tafadhali naomba msimdhuru mwanangu.Nitawapa kiasi chochote cha pesa mnachokihitaji.” Ithan akaomba
“Ithan usiwe na wasi wasi hatukuja kukudhuru wewe au familia yako lakini tunaweza tukafanya hivyo kama utakwenda kinyume na tunavyotaka sisi.Kwanza tueleze nani mwingine anaishi ndani ya nyumba hii? Huku jasho likimtoka Ithan akajibu
“Kwa sasa ni mimi ,mke wangu na mtoto wetu huyu mmoja.Tuna msichana wa kazi lakini yeye kwa sasa amekwenda likizo”
Noel akainama katika bega lake la kulia ambako kulikuwa na chombo maalumm cha mawasiliano akawapa taarifa wenzake.
“Tayari tumempata Ithan .Narudia tena Ithan tumempata ”
“kazi nzuri Noel.msipoteze muda wachukueni haraka tuondoke humu ndani” akasema Mathias ambaye aikuwa nje akihakiki usalama.
“Shafii zunguka katika vyumba vyote na uhakikishe hakuna mtu yeyote aliyebaki” Noel akasema
“Ithan inuka na uchukue nguo zako za kazi haraka” Noel akamuamuru Ithan ambaye akainuka na kufungua kabati akatoa nguo zake za kazini.Noel akamfanyia ishara Sadiq na mara akatoa vitambaa na kuwafunga usoni na midomoni Ithan na mke wake kisha wakawatoa nje.Sixmund aliyekuwa amebaki ndani ya gari akalisogeza kari karibu wakaingia garini na kuondoka eneo lile kwa kasi ya ajabu.Ithan alikuwa ametekwa .

USIKOSE SEHEMU IJAYO……..
 
Back
Top Bottom