mtugani wa wapi huyo
JF-Expert Member
- Dec 5, 2012
- 1,239
- 1,477
- Thread starter
- #41
BRING BACK OUR GIRLS
SEHEMU YA 22
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“kazi nzuri sana vijana.Endeleeni kutufuatilia” Nikasema baada ya kumaliza kuwakagua wale jamaa bila kupata chochote cha kuweza kunisaidia.Niwazi vijana wale walistahili pongezi kwa kazi nzuri waliyokuwa wameifanya.kama si wao wakati huu tungekwisha uawa .Niliazimia baada ya suala hili kumalizika ningeongea na wakuu wao wa kazi ili waweze kuangalia namna bora ya kuwatuza vijana wale kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa taifa lao.Kwa sasa hali ilikuwa imetulia na watu walianza kusogelea mahala tulipokuwa tumesimama ili kuishuhudia miili ya watu wale waliouawa kwa risasi.kwa mbali tukasikia ving’ora vya gari za polisi zikija.Nadhani walikwisha pata taarifa.
“Tuondokeni mahala hapa,tuwapishe polisi wafanye kazi yao.Catherine mpigie simu mkuu wa polisi na umtaarifu kwamba unahusika na tukio hili” Nikasema baada ya kuliona gari la polisi likiingia pale kwa kasi kubwa.Sikutaka kuonekana na polisi ,tukaingia katika gari letu na kuondoka
ENDELEA……………………………………..
“Tonny, ninaona kama muujiza kwa jinsi tulivyonusurika kuuawa.Watu hawa tunaopambana nao ni watu hatari sana” Catherine akasema huku akifuta vumbi lililokuwa limemjaa mwilini.Nilimuonea huruma binti yule kwa sababu toka ameanza kazi hakuwahi kukumbana na kadhia ya hatari kama hii.Nikatabasamu na kusema
“Pole sana Catherine.Hapa ndipo kazi hii inapokuwa ngumu.Kifo kinaweza kutokea dakika yoyote ile.Pamoja na yote yaliyotokea , kuna kitu nimekigundua.Kampuni ile ya Chem chem. Sequrity ni wakala wa mtandao wa kigaidi hapa nchini na kwa kupitia kampuni hii wameweza kuingiza silaha ,zana na watu wao katika mpango mzima wa kumtorosha Abdool.Nimepata uhakika huu mkubwa kwa sababu baada ya sisi kuondoka katika ofisi kuu za Chem chem. Sequrity waliamua kutufuatilia kwa vile walijua wazi kwamba tunaelekea katika ofisi zao ndogo ili kuweza kuujua undani wa mtu wao tuliyemuua kule kwa Rachel.Nadhani walikwisha tung’aza sisi ni akina nani na hivyo lengo lao lilikuwa kutumaliza haraka iwezekanavyo.Baada ya kufanikiwa kuwaua watu wao kwa hivi sasa mapambano yatakuwa makali sana.Kitu muhimu kwa sasa ni kumuwahi huyu dada aitwaye Sesi ambaye ndiye anayesemwa kumpeleka Danford katika kampuni ile.Huyu Sesi ni lazima atakuwa anafahamu mambo Fulani Fulani kuhusiana na kampuni hii.iwapo tutampata huyu Sesi anaweza akatusaidia kutupa mwanga Fulani.Kama kuna kitu anakifahamu kuhusiana na kampuni hii basi naye atakuwa katika orodha ya watu wanaotakiwa kuuawa kwa haraka sana.Tunatakiwa tumuwahi” Nikasema
“hata mimi nafikiri hivyo Tonny.Hawa jamaa ni lazima watakuwa wanafahamu kwamba tunaelekea kwa Sesi hivyo watajitahidi kumuwahi Sesi kabla hatujamfikia.Mimi naona ingekuwa vizuri kama ungewasiliana naye ili tujue yuko wapi kwa sasa.” Nilikubaliana na mawazo ya Catherine nikachukua simu na kuzipiga namba za sesi.
“hallow “ Ikaita sauti ya upande wa pili wa simu
“Hallow naongea na nani? Niliuliza
“Sesi hapa anaongea ,nani mwenzangu?
“Mimi ni binamu yake na Danford ,kuna ujumbe amenipa ili nije nikuone ,uko wapi kwa sasa?
“ Kwa sasa niko nyumbani Sinza”
“Sipafahamu nyumbani kwako,naomba unielekeze tafadhali ” Sesi bila hiyana akanielekeza nyumbani kwake..Nikamwambia asitoke anisubiri.
************************
Nilisimamisha gari nje ya nyumba ya Sesi maeneo ya Sinza kama alivyokuwa amenielekeza.Sikuwa na shaka kwamba tumepotea kwani nilifuata maelekezo yote aliyokuwa ametupatia.Nyumba hii haikuwa na uzio wowote ,nje kulikuwa na mitungi minne ya maua.
Baada ya kuhakikisha usalama upo,tukauendea mlango wa mbele na kuugonga.Mlango ukafunguliwa na dada mmoja mnene mfupi
“karibuni” akasema dada yule mwenye macho mazuri.
“Ahsante sana ,habari yako” tukasema kwa pamoja.
“Nzuri karibuni ndani” Alitukaribisha ndani ,tukaingia katika sebule ile kubwa na nzuri.Dada yule alikuwa akituangalia kwa macho yaliyojaa wasi wasi mwingi.nafikiri ni kwa sababu ya kutowahi kutuona hapo kabla.Sikuweza kujua kama huyu ndiye Sesi mwenyewe au siye.
“Tunahitaji kuonana na Sesi,” Nikasema bila kupoteza wakati.
“Sesi ametoka kidogo ameenda hapo nyumba ya jirani.Ila ameacha maagizo kwamba wageni wake wakifika nimpigie simu.Ninyi ndio wageni aliokuwa anawasubiri?” akasema dada yule huku akichukua simu yake.
“Nadhani ni sisi kwa sababu tuliongea naye kwa simu muda si mrefu na akasema kwamba yuko nyumbani.”
Yule dada akaongea na Sesi katika simu halafu akatugeukia.
“Amesema mumsubiri atakuja muda si mrefui” Akasema mwanadada yule huku akilifungua friji na kutupatia juice.Mimi nilikuwa nimekaa katika sofa lililoelekea dirishani.Toka pale nilipokuwa nimekaa niliweza kuona kila aliyekuwa akipita nje ya nyumba.Dakika kumi zikakatika bila ya Sesi kutokea hivyo yule dada akainuka na kwenda kusimama mlangoni kwa lengo la kumfuata dada yake.
“anakuja” akasema yule dada huku akirudi ndani baada ya kumuona dada yake akija .Ghafla lilitokea tukio moja ambalo lilitokea kwa haraka sana .Gari moja dogo jeupe likatokea kwa kasi kubwa sana likielekea katika nyumba ile ya Sesi na mara ikasikika milio ya risasi hatua chache toka ile nyumba ya Sesi Kama umeme nikatoa bastora yangu kwani tayari nilikwisha inusa hatari,nikamfanyia ishara Catherine tukatoka kwa tahadhari kwenda nje.Mita chache toka nyumba ile ya sesi nililiona gari moja likiondoka kwa kasi ya ajabu
“My God” Nilijikuta nikitamka maneno yale huku nikiuma meno kwa hasira
Hatua chache mbele yetu dada mmoja alikuwa amelala katika dimbwi la damu Kwa haraka na kwa tahadhari kubwa nikamuendea na kumchunguza.hakuwa na uhai ,alikuwa amekwisha fariki.Alipigwa risasi nyingi kifuani.Machozi yalikaribia kunitoka baada ya kumsikia yule msichana tuliyemkuta ndani mwa Sesi akipiga yowe la uchungu kuwa yule aliyekuwa amepigwa risasi pale nje ndiye Sesi dada yake .. Sesi alikuwa amelala katika dimbwi la damu.tayari alikuwa amekwisha fariki kitambo.Alikuwa amechakazwa kwa risasi nyingi kifuani.Roho iliniuma sana kwa msichana mrembo kama yule kufa kikatili namna ile.Nikiwa bado nimeinama nikimuangalaia Sesi huku umati wa watu ukianza kujikusanya eneo lile Catherine akaingia katika gari letu lakini nikahisi miguu inaishiwa nguvu baada ya kugundua kwamba tairi za gari letu hazikuwa na upepo,zilikuwa zimepigwa risasi na hivyo gari lisingeweza kutembea tena.Kwa mara nyingine tena walikuwa wametuzidi ujanja.Nywele zikanisimama.Mwili ukachemka kwa hasira.Muda ulizidi kuyoyoma lakini bado hatukuwa na mwanga wowote wapi alipokuwa Abdool.Iwe isiwe Gaidi huyu alitakiwa apatikane siku ya leo
Nilichekecha akili tutafanya nini ili tuweze kuondoka .Watu walikuwa wakija kwa wingi eneo lile nikaanza kuingiwa na wasi wasi pengine wangedhani kwamba sisi ndio tuliohusika na mauaji yale kisha wakaanza kutushambulia.Wakati nimesimama nikijaribu kuchekecha akili mara nikamuona Catherine amechomoka kwa kasi akaelekea katika gari moja lililokuwa limesimama pale karibu na nyumba ya Sesi.Dereva wake alikuwa ameshusha kioo cha gari akishangaa kitu gani kilichokuwa kimetokea pale.Kwa kasi ya aina yake Catherine akamnyooshea bastora na kumuamuru ashuke chini.Bila ubishi dereva yule akashuka ndani ya lile gari. “Tonny twende tuondoke .” Akasema Cathe kwa sauti kubwa.Nilimuacha Sesi pale chini nikaingia katika lile gari alilokuwa ameliteka Sesi.Idadi ya raia ilizidi kuongezeka.Kama nilivyokuwa nimehisi ndivyo ilivyokuwa imetokea,raia wale walikuwa wakija na silaha pamoja na mawe.Ili kupata nafasi ya kuondoka eneo lile salama nilipiga risasi tatu hewani na ndani ya sekunde kadhaa eneo lote likawa jeupe.Kila mmoja alikimbia na kwenda kujificha kujinusuru.Kwa kasi ya ajabu Catherine akaiondoa gari tukaanza kuifukuzia ile gari ya wale watu waliokuwa wamempiga risasi Sesi. .
Moyo ulikuwa ukinienda mbio kwa hofu iliyokuwa imechanganyika na hasira kubwa.Mapambano yalianza kuwa makali sana kwa kadiri dakika zinavyosonga mbele.Kila tunavyojitahidi kupiga hatua moja wao walikuwa wanaturudisha nyuma hatua mbili.Hii ilionyesha ni jinsi gani jamaa walivyokuwa wamejipanga kikamilifu.Hawakutaka kutupatia hata chembe ya nafasi ambayo ingeweza kutupatia mwanga wa wapi alipo Abdool .Muda ulizidi kusonga mbele na bado hatukuwa na mwanga wowote wa wapi alipo gaidi huyu hatari aliyetoroshwa alfajiri ya leo.Inawezekana Sesi alikuwa na taarifa muhimu kuhusiana na wao ndiyo maana wameamua kumuwahi kabla hatujaonana naye.Walifahamu fika kwamba ni lazima tungeonana na Sesi ambaye angeweza kutupatia taarifa muhimu ambazo zingetusaidia kufahamu kuhusiaa na mtandao huu.Kwa kumuua Sesi walikuwa wameturudisha nyuma mno.Kwa sasa hatukuwa tena na chanzo kingine ambacho kingeweza kutupatia taarifa za magaidi hawa.Hali ilikuwa ikiogopesha.Niliamini jamaa lazima wangekuwa wakituwinda na sisi ili watumalize kabisa kwa sababu tayari tumekwisha onekana ni kizingiti kwao.
Wakati nawaza haya Catherine alikuwa akiyapita magari ili kuifukuzia gari la wale jamaa.Niliustaajabia uhodari wake katika kuendesha gari.
“wale pale” akasema Catherine na kunionesha gari aina ya Vitara nyeupe ambayo ilikuwa magari mawili mbele yetu.
*********************
Tuliendelea kuwafuatilia wale jamaa kwa ufundi mkubwa bila ya wao kutambua kwamba walikuwa wakifuatiliwa.Catherine alinifurahisha sana kwa jinsi alivyotumia mbinu za hali ya juu za kijasusi katika kuwafuatilia wale jamaa.Mara gari ya wale jamaa iliwasha taa kuashiria kwamba ilikuwa ikikata kona na kuingia katika mgahawa maarufu ulioko katikati ya jiji.Jamaa wale walipaki gari na kushuka .Toka ndani ya gari lile wakashuka jamaa watatu.Tukiwa ndani ya gari yetu niliweza kuwatazama wale jamaa wakiingia mgahawani.Mmoja ambaye ndiye aliyekuwa dereva wa gari ile alikuwa mweupe mwenye nywele fupi zilizosokotwa kwa mtindo wa rasta.Aliyefuatia alikuwa na asili ya kiarabu ,alikuwa amevaa suti nyeusi iliyomkaa vyema ,macho yake yalifunikwa na miwani myeusi.Wa mwisho alivaa suti ya kijivu na huyu alikuwa mrefu kiasi ,mwembamba na macho yake yalionyesha kuwa hakuwa mtu wa masihara.
Taratibu waliingia ndani ya mgahawa kisha nasi tukashuka toka ndani ya gari.Tulihakiki usalama wetu kwanza halafu kwa tahadhari kubwa tukaingia ndani ya mgahawa.Tulikaribishwa na wahudumu wenye uchangamfu mkubwa.Tukakaa katika meza moja ya pemBeni kabisa.Watu walikuwa si wengi sana.Toka pale tulipokaa tuliweza kuwaona wale jamaa wakiwa wamekaa katika meza moja ambayo haikuwa mbali sana na mlango wa kuingilia pale mgahawani.Tuliagiza vinywaji na kuendelea kunywa taratibu huku tukiendelea kuwachunguza wale jamaa .
“Catherine una uhakika gari uliyokuwa ukiifuatilia ni ya wale watu waliomuua Sesi? Nikamuuliza Cathe baada ya kuona muda unazidi kusonga mbele na wale jamaa wakiwa wametulia bila kuwa na wasiwasi wa aina yoyote.
‘NdiyoTonny.Wakati wewe umeinama pale ukimtazama Sesi mimi niliitazama vizuri gari ile ya wale jamaa japokuwa ilikuwa mbali kidogo.Nina uhakika mkubwa kwamba gari tuliyokuwa tukiifuatilia ni ya wale jamaa.”
“Ok kama ni wao basi lazima watakuwa wanahusika moja kwa moja na mtandao huu na ndio watakaotupatia majibu ni wapi alipo abdool.” Nikasema huku nikiendelea kuwatazama wakinywa mvinyo huku wakiongea.Muda ule ule yule jamaa mwenye asili ya kiarabu na suti nyeusi aliinuka na kuufuata ujia uliokuwa ukielekea maliwatoni.Sikupoteza hata sekunde nami nikainuka.
“cathe ninamfuata yule jamaa anayeelekea chooni.Wakati naelekea chooni wachunguze hawa jamaa waliokaa pale mezani kama wataonyesha dalili zozote za kunitilia shaka.Iwapo wataonyesha wasi wasi wowote basi nitaarifu haraka kwa kubeep simu yangu mara mbili haraka haraka.” Nikamwambia Catherine naye akatikisa kichwa huku akiwa na uso wenye wasi wasi.Hakuwa amekutana na kadhia ya hatari kama hii toka alipoanza kazi.
Nilitembea kwa tahadhari huku nikijaribu kuwachunguza wale jamaa waliokuwa wamebaki pale mezani kama wamenitilia shaka au vipi.Lakini jamaa bado walikuwa wakiendelea na kupata mvinyo na hawakuwa na habari yoyote na mimi.Nilipohakikisha kwamba hawakuwa na mashaka na mimi niliushika ujia uliokuwa ukielekea maliwato .Nilimuomba Mungu watu wasije upande ule kwa dakika chache ili niweze kuimaliza kazi iliyonipeleka kule.Mlango wa vyoo vya wanaume ulikuwa umefungwa.Nikachungulia katika kioo kizito kilichokuwa mlangoni pale nikaiona taswira ya mtu akiwa mle ndani.Nikaishika bastora yangu na kuiweka tayari kisha nikakinyonga kitasa na mlango ukafunguka nikaingia ndani.Mle maliwato alikuwemo yule jamaa peke yake akijisaidia haja ndogo.Nilienda kusimama pemBeni yake na kuanza kufungua zipu ya suruali .Nikampiga chabo yule jamaa na kumuona akimalizia kuifunga zipu ya suruali yake.Sikutaka kupoteza hata sekunde moja .Kwa kasi ya aina yake nikatoa bastora yangu na kumuwekea kichwani .
“Tulia hivyo hivyo ulivyo.Usijaribu kufanya lolote” Nikasema kwa sauti kali.Jamaa hakuamini macho yake .Aliona ni kama njozi .
USIKOSE SEHEMU IJAYO……………….