Riwaya: Bring back our girls

Riwaya: Bring back our girls

BRING BACK OUR GIRLS
SEHEMUYA 11
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Wakati mlipuko ule unatokea nilijitupa chini na baada ya dakika mbili hivi nikasikia nimeguswa na kitu cha baridi shingoni ambacho moja kwa moja nilitambua kuwa ulikuwa ni mtutu wa bunduki.Mwili ukaingiwa na baridi.Nikajua kama mimi ndiye niliyekuwa mlengwa wa mashambulio yale basi tayari nimepatikana.Unapowekewa kitu kama hiki kichwani hutakiwi kufanya lolote lile kwa pupa .Inakubidi utii kila utakachoambiwa na mtu aliyekulenga na bunduki au bastora.Mtu anapokuwa amekuelekezea bunduki au bastora tayari anakuwa na moyo wa kuua na ukienda kinyume na matakwa yake basi dakika yoyote anaweza akakutoa uhai.Sikutikisika wala kuinua mkono wangu uliokuwa na bastora.
“Put your gun down and get up slowly”

ENDELEA……………………………

Nikaamriwa na sauti ya ukakamavu ya mwanamke.Sauti ile haikuwa ngeni masikioni mwangu.Nilijiuliza nimeisikia wapi?
Taratibu nikaweka bastora zangu chini na kusimama nikiwa nimenyoosha mikono yangu juu.Kwa sauti ya ukali akaniamuru nimgeukie ,nikageuka. Kwa sekunde kadhaa nilihisi ni kama nimeona mzimu.Kuna hadithi zile tulizokuwa tukihadithiwa zamani na babu zetu kuwa mashetani hupenda sana kutumia miili ya watu na kuishi nasi katika jamii.Niliamini hata mtu aliyeko mbele yangu hakuwa mtu wa kawaida bali ni kiumbe wa kiroho aliyevaa mwili wa binadamu.Nilibaki nimepigwa na bumbuwazi.Mwili ulikuwa ukitetemeka kwa baridi ya ghafla niliyoisikia.Midomo ikanicheza nikataka kusema neno lakini nikashindwa.Mwili uliendelea kunitetemeka kwa kile nilichokiona mbele yangu ,kitu ambacho hata leo hii huwa ninasisimka ninapohadithia mkasa huu.
Kiumbe aliyeko mbele yangu akiwa na bunduki aina ya SMG alikuwa ni Rosa msichana mrembo ambaye nimekutana naye mchana katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro na kujenga urafiki ambao kwa muda mfupi tuliweza kuzoeana na kutufanya tuonekane kama vile ni marafiki wa muda mrefu mno..Rosa msichana mpole mwenye kuongea kwa bashasha sikuweza kufikiri kama katika maisha yake amewahi kushika silaha ya namna yoyote achilia mbali kuzijua kwa majina,lakini sasa hivi yuko mbele yangu na silaha kali.
“Follow me” Akaniamuru huku akikimbia kuelekea katika geti la kuingilia klabuni hapo.Sikuwa mbishi nikaokota bastora zangu na kuanza kumfuata nyuma.Taharuki ilitanda na watu walikuwa wakikimbia hovyo.Magari yalikuwa yakiwaka moto.Kila mtu alikuwa akijaribu kuyaokoa maisha yake.Karibu na lango la kuingilia tulikuta gari dogo aina ya Toyota Vista iliyokuwa ikiunguruma na milango yake ilikuwa wazi.Nafikiri mmiliki wake aliamua kuliacha ili kuinusuru nafsi yake kwa kile alichokiona kikitokea hapo.Rosa akaingia ndani ya gari lile upande wa dereva akaniamuru na mimi niingie.Kabla sijafunga mlango getini likatokea gari ambalo lilingia kwa kasi ya ajabu na kuwagonga watu waliokuwa wakijaribu kutoka nje.Gari lile lilikosa kuligonga gari tulimokuwamo .Kwa kasi ya ajabu gari lile likaenda kugonga jengo la klabu na hapo kikatokea kitu ambacho mpaka leo hii nikikumbuka huwa nafumba macho kwa uchungu.Mlipuko mkubwa ukatokea na kulitikisa eneo lote la klabu ile.Rosa akanipigia ukelele niruke nami kufumba na kufumbua nilikuwa nje tukaanza kukimbia kuondoka eneo hilo ambalo kwa muda huo lilionekana kama jehanamu ya duniani.Moto mkubwa ulikuwa ukiwaka na vilio vya watu wakiteketea kwa moto vikasikika.Nilikuwa nikikimbia huku machozi ya uchungu yakinitoka na hasa nilipowakumbuka rafiki zangu Ben na Irene.Kwa jinsi hali ilivyokuwa pale klabuni sikuwa na tegemeo la kuwaona tena wale rafiki zangu.
“Are you ok Tonny ?” Akaniuliza Rosa wakati tukikimbia na kwa sasa tulikuwa tumefika katika nyumba za shirika la nyumba la taifa eneo la Soweto.Sikuamini macho yangu kwa jinsi Rosa alivyokuwa akizifahamu njia na vichochoro vya jiji hili la Arusha.Alionekana ni kama mtu aliyeishi Arusha kwa muda mrefu na ambaye analifahamu jiji hili vizuri sana.
“I’m ok.” Nikajibu kwa ufupi huku nikiwa katika tahadhari kubwa.
“Ok keep following me.” Akasema Rosa
Tuliendelea kukimbia huku ving’ora vya gari za polisi vikisikika katika kila kona.Jiji la Arusha lilikuwa katika taharuki kubwa.
" Dont look back " akaniambia Rosa.
Pamoja na kuendelea kumfuata Rosa bado nilikuwa katika fikara nzito kumuhusu yeye.Rosa ni nani? kwa nini ameniokoa toka kwa wale watu ambao nina hakika walilenga kuniua ? Katumwa na nani aniokoe? Sijawahi kumuona katika majasusi wa Tanzania je ni jasusi toka wapi? Kuna kitu gani kinachoendelea nyuma ya pazia? Siri aliyoibeba Rosa ni kubwa na inayohihusu mimi.Hata hivyo nilimshukuru kwa sababu yeye ndiye aliyeyaokoa maisha yangu katika shambulio la leo.Ni wazi shambulio lile lilinilenga mimi.Lakini nini dhana ya mashambulio yale? Ni kwa nini nikalengwa mimi? Sikuwa na jibu la maswali haya ,nikaendelea kumfuata Rosa ambaye ndiye aliyekuwa na majibu ya maswali yangu.
Tuliendelea kukimbia kwa kasi ,Rosa akiwa mbele mimi nikimfuata nyuma.Tulikuwa tukikimbia kimya kimya ,hakuna aliyethubutu kumsemesha mwenzake.Jasho lilikuwa linanitiririka.Nashukur kwa kuwa miminimtu wa mazoezi.
“How do you feel Tonny? Akaniuliza Rosa wakati tumefika katika mzunguko wa kijenge.
“I’m ok” Nikajibu.
Rosa akanitazama kwa macho makali halafu akasema.
“Pole sana kwa yaliyotokea” sikumjibu kitu nikaendelea kumtazama usoni.
“Ok listen to me Tonny.Mpaka hapa tulipo bado tunakabiliwa na hatari kubwa .Tunachotakiwa kukifanya kwa sasa ni kuondoka Arusha haraka iwezekanavyo.”
Akaikunjua karatasi iliyokuwa na ramani ya mji wa Arusha.Kwa kutumia kurunzi ndogo akanionyesha njia tunayotakiwa kupita.Sikuwa naifahamu njia hiyo.
“Njia hii ndiyo yenye usalama kwetu.Tukiifuata njia hii tunakwenda kutokea maeneo ya Usa river na pale tutakamata barabara kuu hadi Moshi.Tukiwa Moshi tutajua nini cha kufanya lakini yatubidi tufike huko kabla hakujapambazuka.”
Akaikunja ile karatasi ,tukaanza tena kukimbia tukiifuata bara bara iliyoelekezwa katika ramani .Rosa bado aliendelea kunipa mawazo mengi.Nilitamani kumfahamu yeye ni nani na nani amemtuma aniokoe? Kwa mambo aliyokuwa akiyafanya nilijua lazima atakuwa ni jasusi wa kiwango cha juu sana.Toka nimeanza kazi hii ya ujasusi sijawahi kukutana na mwanamke mahiri kama huyu.Ana uwezo mkubwa wa kutumia silaha,ni mwepesi na akili yake inafanya kazi haraka haraka sana. Mambo niliyoyaona akiyafanya usiku wa leo hayafanani kabisa na mwonekano wake.
Tulikuwa tunakimbia kimya kimya na wakati mwingine tulisimama na kutembea kwa mwendo wa kasi halafu tukaanza tena kukimbia.Nilikuwa nikimfuata Rosa lakini kwa upande fulani nilikuwa namuogopa sana.Sikujua alikuwa ananipeleka wapi.Sikutaka kuwa mbishi ,nilijua lazima kuna jambo zito lililotokea .Kuna jambo ambalo sikuwa ninalifahamu na ilinilazimu kuendelea kumfuatilia Rosa ili nilifahamu.Pamoja na kukimbia taratibu kwa umbali ule mrefu Rosa hakuonyesha dalili zozote za kuchoka.Nilizidi kumstaajabu mwanamke huyu kwa uhodari wake.Nilihisi kuchoka lakini hakunipa muda wa kupumzika.Kila mara alikuwa anaiangalia saa yake.Mara kwa mbali nikaziona taa za gari likija kwa kasi sana nyuma yetu..
“Rosa kuna gari linakuja”
Rosa akasimama na kugeuka kulitazama gari le.
“Tujifiche haraka” Akaamuru.Tukaenda kujificha pembeni ya bara bara kwenye kichaka cha miiba.Jasho likitutiririka.
" Weka silaha zako tayari.Nahisi tayari tunafuatiliwa. Ufanye kile tu nitakachokwambia ufanye.." akasema Rosa nikamuitikia japo kwa shingo upande kwani sikuzoea kupewa amri ya nini cha kufanya bali mimi ndiye huwa mtoa amri. Gari lile lilizidi kuja kwa kasi ya ajabu na kukaribia sana sehemu tuliyokuwa tumejificha.
" Get ready " akasema Rosa nikashika bastora zangu mikononi tayari kukabiliana na lolote litakalojitokeza.Pembeni ya pale tulipokuwa tumejificha ,kulikuwa na jiwe kubwa.Nikapata wazo la kuliweka jiwe lile barabarani ili gari lile litakapofika pale lisimame na hapo tungeweza kupata nafasi nzuri ya kuliteka na hivyo kulitumia kutoroka.Rosa akakubaliana na mawazo yangu haraka haraka tukalisukuma jiwe lile na kuliweka kati kati ya bara bara,tukarudi tena kujificha katika kichaka.Mawazoni mwangu nilikuwa na uhakika mkubwa kuwa gari lile lingeweza kuwa la polisi.Nikajiweka tayari kwa mapambano makali kwa sababu nilielewa kama ni polisi na wanatufuatilia sisi basi ni lazima wangekuwa wamejiandaa kikamilifu.
Dakika kama kumi na tano hivi tangu tujifiche pale kichakani ,lile gari likafika na taratibu likapunguza mwendo baada ya kuliona jiwe lile tuliloliweka barabarani.Lilikuwa ni gari kubwa aina ya Fuso lililokuwa limesheheni mzigo.Nikamshukuru Mungu kwani nilitegemea lingekuwa ni gari la polisi.Baada ya kama dakika mbili hivi wakashuka watu wawili kwa dhumuni la kuliondoa jiwe lile.Milango ilikuwa wazi hivyo toka mahala tulipokuwa tumejificha nikapata nafasi ya kuchunguza ndani,sikuona mtu yeyote mwingine aliyebaki garini.Nikampa ishara Rosa ya kuimaliza kazi haraka.Kwa kasi ya aina yake tukatoka mafichoni na kuwakabili wale jamaa.
“Hey ! mikono juu” Nikawastua wale watu ambao walipatwa na mstuko mkubwa.Ni kitendo ambacho hakuna aliyekuwa amekitarajia.Ghafla mmoja wao akaanza kutokwa na haja ndogo,huku akitetemeka mwili mzima kwa hofu na ghafla akaanguka na kupoteza fahamu.
“Mnaelekea wapi? Nikauliza kwa sauti kali
“Tafadhali msituue jamani.Hii ni gari ya kampuni ya kulima maharage na hapa tunao mzigo tunaupeleka uwanja wa ndege wa Kilimanjaro kwa ajili ya kusafirishwa nje ya nchi.Tafadhali jamani msituue hapa tuna hela kidogo tu…” akasema yule jamaa huku kijasho kikimtoka.Sikuhitaji maelezo mengi wala pesa zake kwa sababu tulichokuwa tunakihitaji muda huu ni gari la kutufikisha mjini Moshi.Nikampa ishara Rosa naye kwa kasi ya ajabu akampiga pigo moja linalompoteza fahamu mtu yule.Tukawavuta na kuwaweka pembeni ya barabara ,tukajitoma garini na kuondoka kwa kasi ya ajabu .Mimi ndiye niliyekuwa dereva.Rosa yeye alikuwa akiisoma ramani aliyokuwa nayo na kunipa maelekezo.
“Hapa tumefika Usa river ,tutaingia katika bara bara kuu ambayo itatupeleka hadi mjini Moshi.”akasema Rosa huku akiendelea kuisoma ramani ile.Tuliendelea kuchanja mbuga kuelekea Moshi kwa kasi ya ajabu huku nikimuomba Mungu atuepushe na hatari zozote za njiani.
*********************************
Joel Temba au Joe kama tulivyozoea kumwita ni mmoja kati ya vijana wapya kabisa katika idara yetu ya ujasusi wa taifa.Ni hivi majuzi tu amemaliza mafunzo yake ya ujasusi nchini Ujerumani na tayari ameonyesha umahiri mkubwa na hivyo kuwashawishi wakuu wa idara yetu kumweka katika nafasi za juu . Nakumbuka Joe aliniaga kwamba anakwenda mapumzikoni Moshi hivyo nikafarijika kwamba tayari tuna sehemu ya uhakika ya kwenda kupumzika wakati tukiangalia tena nini kinachofuata.Nilikuwa na hamu sana ya kutaka kumfahamu Rosa na nini kilichokuwa kinaendelea nyuma ya pazia.
Saa kumi na dakika kadhaa kwa mujibu wa saa yangu ya mkononi tuliwasili mjini Moshi.Tukalitelekeza gari lile maeneo ya stendi tukaanza kutembea kwa miguu kuelekea eneo la majengo ambako ndiko nyumba ya Joe ilikuwapo.Sikuwa na simu wakati huo simu yangu ilipotea katika purukushani ile ya Arusha na hata ningekuwa nayo nisingeweza kuitumia kwa sababu za kiusalama.Alfajiri hiyo kulikuwa na kiubaridi kikali.Baada ya kutembea kitambo tukafika katika nyumba ile ya Joe.Nilitabasamu baada ya kuikumbuka.Tulihakiki kwanza usalama halafu tukaelekea getini.Nikamwambia Rosa abonyeze kitufe cha kengele ya getini .Alibonyeza mara kadhaa bila kusikia hata nyayo za mtu akija kule getini.Nikaanza kupatwa na wasi wasi labda yawezekana Joe hayupo .Dakika kama tano toka tumesimama pale getini taa kubwa iliyokuwapo juu ya paa la geti ikawaka.Naifahamu taa hii ni taa ya usalama.
Haukupita muda mrefu nikasika vishindo vya mtu akija na mlango mdogo wa geti ukafunguliwa.Alikuwa ni Joe
“ Tonny !!“ akanisalimu Joe akiwa katika hali ya mshangao.
“ Joe”Nikajibu.
“Nimestuka sana nilipokuona.Mbona hukunitaarifu kama unakuja Moshi kwa Krismass?Akauliza Joe
“Joe tutaongea baadae.Tutachohitaji kwa sasa hebu tupe nafasi ya kulala na kupumzika.”
Joe alifahamu kuwa muda huo sikuwa nahitaji maongezi mengi
“Ok Tonny ,jisikie uko nyumbani.” Akajibu Joe.
“ouh Joe nilisahau kukutambulisha.Huyu anaitwa Rosa ni rafiki yangu..Rosa huyu ni raiki yangu anaitwa Joe Temba” Wakashikana mikono halafu Joe akatuongoza katika chumba ambacho tungekitumia kupumzikia.Joe katika mawazo yake alijua moja kwa moja Rosa alikuwa ni mpenzi wangu hivyo hakusita kutupatia chumba kimoja.Vyumba vyote vya kulala katika nyumba hii ni self contained yaani vinavyojitosheleza kwa kila kitu ndani.Chumba kilikuwa kisafi na kilichotandikwa mashuka mazuri.Nafikiri alikiweka katika tahadhari kwa ajili ya ugeni wowote ambao angeupata katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka kwani wengi watu watokao katika mkoa huu hupenda kurejea nyumbani katika kipindi hiki cha mwaka.Niliufunga mlango kwa ufunguo.Nilipogeuka nikamkuta Rosa amejilaza kitandani.Macho yetu yakakutana ,nikapumua kwa nguvu.Kwa mara nyingine tena nikaushuhudia uzuri wa binti huyu .Moyo ukaanza kunienda mbio baada ya kumuona akiinuka na kufungua blauzi yake.
“Nadhani tunahitaji kuoga kwanza ili kuondoa uchovu wa usiku huu kabla ya kulala” Akasema .Hakuwa na aibu ile ya kike mbele ya mwanaume.Nikazishuhudia chuchu changa kifuani kwake nikahisi damu ikinichemka.Rosa akavua nguo zote mbele yangu na kujifunga taulo.Akageuka na kunikuta bado nimesimama nikimtolea macho.Sikuamini kama niko katika chumba kimoja na binti malaika yule.
“Ok Tonny mi natangulia kuoga.Utanikuta bafuni.” Akafungua mlango na kuingia bafuni.Sikutaka kuitumia vibaya nafasi hii adimu niliyoipata.Licha ya kuwa na maswali mengi juu ya binti huyu lakini napenda nikiri wazi kuwa tayari nilikuwa na hisia juu yake toka tulipokutana jana pale uwanja wa ndege wa Kilimanjaro.Rosa alikuwa na mvuto wa ajabu mno.Nikavua nguo haraka haraka na kujifunga taulo nami nikaingia bafuni.Nilipoufungua tu mlango wa bafuni nikastukia nimemwagiwa maji ya baridi tumboni.Nikastuka na kuruka kwa hasira.Rosa alikuwa akicheka ikanibidi nami nicheke.
“Kumbe unayaogopa maji namna hiyo? Akasema Rosa huku akicheka.Akanikaribia taratibu na kunitoa taulo nililokuwa nimejifunga,akanivutia kwake na kunipa busu moja zito ambalo linanifanya damu ichemke zaidi.Nikamvuta karibu na kumpiga busu maridadi la mdomo linalomfanya anivute kwake zaidi na kunikumbatia kwa nguvu.Nikauinua mkono wangu wa kulia na kuushusha hadi katika maeneo ya kiunoni mwake na taratibu nikasikia akitoa mguno na kuanza kuhema kwa kasi.Mdadi ukanipanda na kujikuta nikianza kuongeza ufundi zaidi na kumfanya Rosa aendelee kulalama kwa miguno ya kimahaba kwa kila utundu niliomfanyia.Kwa dakika hizi chache tuliweka kando mambo yote yaliyotokea na kujikuta tukiwa katika ulimwengu wa kimahaba.Naomba nikiri binti huyu alikuwa mjuvi wa mambo.Aliyafahamu mapenzi.Nilipagawa kwa mambo aliyonifanyia.Sikutaka kuachwa nyuma kwani hata mimi mambo haya ninayweza hivyo nami nilimdhihirishia kwamba nina kiwango cha juu si katika mambo ya ujasusi tu bali hata katika mambo ya mahaba.Ilikuwa ni asubuhi ya aina yake.Tulitoka bafuni tukiwa tumechoka na kujitupa kitandani.
TUKUTANE SEHEMU IJAYO………………
 
BRING BACKOUR GIRLS
SEHEMU YA 12
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“Kumbe unayaogopa maji namna hiyo? Akasema Rosa huku akicheka.Akanikaribia taratibu na kunitoa taulo nililokuwa nimejifunga,akanivutia kwake na kunipa busu moja zito ambalo linanifanya damu ichemke zaidi.Nikamvuta karibu na kumpiga busu maridadi la mdomo linalomfanya anivute kwake zaidi na kunikumbatia kwa nguvu.Nikauinua mkono wangu wa kulia na kuushusha hadi katika maeneo ya kiunoni mwake na taratibu nikasikia akitoa mguno na kuanza kuhema kwa kasi.Mdadi ukanipanda na kujikuta nikianza kuongeza ufundi zaidi na kumfanya Rosa aendelee kulalama kwa miguno ya kimahaba kwa kila utundu niliomfanyia.Kwa dakika hizi chache tuliweka kando mambo yote yaliyotokea na kujikuta tukiwa katika ulimwengu wa kimahaba.Naomba nikiri binti huyu alikuwa mjuvi wa mambo.Aliyafahamu mapenzi.Nilipagawa kwa mambo aliyonifanyia.Sikutaka kuachwa nyuma kwani hata mimi mambo haya ninayweza hivyo nami nilimdhihirishia kwamba nina kiwango cha juu si katika mambo ya ujasusi tu bali hata katika mambo ya mahaba.Ilikuwa ni asubuhi ya aina yake.Tulitoka bafuni tukiwa tumechoka na kujitupa kitandani.

ENDELEA………………………….

“Wake up Tonny its Christmass day” alinistua Rosa toka katika usingizi mzito.
“Merry christmass” Nikasema kwa sauti ya uchovu
“Merry christmass Tonny” akajibu Rosa
Nikajizoa zoa hapo kitandani na kukaa.
“Joe ametoka kidogo ila amesema atarudi muda si mrefu.” Akasema Rosa
Niliitupia jicho saa ya ukutani ilipata saa tatu na ushee hivi.Rosa akaniletea kikombe cha kahawa,nikanywa na kufanya mazoezi mepesi ya mwili halafu nikaoga na kurudi tena kitandani.Rosa alikuja na kuketi karibu yangu,akanyoosha mikono yake na kuyashika mashavu yangu ,akakigeuza kichwa changu upande wake na kunipa busu safi linaloamsha tena hisia kali nilizokuwa nazo kwa binti huyu adimu kupatikana duniani.
“Unajisikiaje Tonny? Akaniuliza
“ Najisikia vizuri sana Rosa.” Nikajibu.Rosa akaniangalia kwa sekunde kadhaa usoni na kusema
“Pole sana Tonny kwa yote yaliyotokea jana.”akasema Rosa kwa sauti laini iliyojaa upendo ndani yake.
“Ahsante sana Rosa.ahsante sana kwa kuniokoa jana .Bila wewe kuniokoa jana muda huu tungekuwa tunaongea mambo mengine.Pamoja na yote yaliyotokea lakini bado niko kizani kuhusu nini kinachoendelea nyuma ya pazia. Ningependa Rosa unieleze kwa undani wewe ni nani na ninaimani unafahamu juu ya tukio lile.” Nikasema huku nikimtazama machoni.
Kumbukumbu ya tukio la usiku ikarudi tena kichwani mwangu na kuwakumbuka rafiki zangu Ben na Irene.Roho ikaniuma sana sikuwa na uhakika kama walikuwa wamesalimika na dhahama ile.
Rosa akaniangalia kwa sekunde kadhaa kana kwamba ananisaili akatabasamu kidogo.
“Tonny nadhani ingekuwa vizuri kama ungeanza kunifahamu mimi kwanza.” Akasema na kunyamaza kwa sekunde kadhaa halafu akaendelea
“Jina langu halisi naitwa Monica Stevens.Mimi ni raia wa Marekani.ninatokea katika jiji la New York.Umri wangu ni miaka ishirini na sita.Kwa ufupi ninafanya kazi na shirika la ujasusi la Marekani CIA.Kwa sasa niko katika operesheni ya kupambana na ugaidi katika eneo la afrika mashariki na kati. Vikundi vikubwa vya kigaidi duniani kama Alqaeda,Alshabaab,Boko haramu na vinginevyo vinalitumia eneo hili la kusini mwa jangwa la Sahara kujiimarisha,kuwafundisha wafuasi wao ugaidi na kufanya mashambulio.Kwa sababu hiyo basi serikali ya Marekani imeamua kuanzisha operesheni maalum ya kupambana na vikundi hivi. Operesheni hii ni ya siri ili kuweza kubaini nguvu na uwezo wa vikundi hivi na vile vile kuwafahamu viongozi wao na mahala walipo.Hatushirikiani na serikali yoyote katika eneo hili kwa sababu imebainika katika baadhi ya serikali kuna wafuasi wa vikundi hivi na wengine ni viongozi wakubwa kwa hiyo taarifa zozote za muhimu zinaweza kuvuja na kuwafikia walengwa na hivyo kuharibu dhana nzima ya operesheni hii ”
Monica aliongea kwa pozi za aina yake nikatulia kwa makini nikimsikiliza.Kwa uwezo aliouonyesha usiku wa jana niliamini maneno aliyokuwa akiniambia.Sikuhitaji kuthibitisha kuwa ni kweli anatoka katika shirika kubwa kabisa la ujasusi la CIA.Kazi aliyonionyesha ilikuwa ni kitambulisho tosha.
“Tonny” Akaendelea
“Mwaka 1998 nchi za Tanzania na Kenya zilionja adha ya ugaidi baada ya balozi za Marekani jijini Dar eas salaam na Nairobi kulipuliwa kwa mabomu,tukio lililosababisha vifo vya watu wengi na kusababisha majeruhi na hata ulemavu wa kudumu kwa baadhi ya watu.Waliokufa katika mashambulio yale yenye shabaha ya kupambana na marekani,walikuwa ni wazawa wa nchi hizi mbili ambao wengi walikuwa ni wafanyakazi au watu waliokuwa wamekwenda kufuatilia mambo mbali mbali katika ofisi hizo.Baada ya shambulio hilo ulianza msako mkubwa wa kuwatafuta na kuwatia nguvuni wote waliohusika .Wewe ukiwa kama jasusi wa juu kabisa katika ukanda huu wa afrika mashariki uliongoza timu maalum iliyoundwa na mlifanikiwa kumkamata gaidi mkuu aliyehusika na kupanga na kutekeleza mashambulio hayo Abdool bin Sahel bin abdool tariq akiwa mafichoni nchini Sudan.Abdool ni mmoja kati ya magaidi wa juu kabisa wa kundi la Alqaeda ambaye alikuwa akitafutwa siku nyingi na serikali ya marekani.”
Monica akatulia tena akarekebisha koo lake.Alinikumbusha mbali sana.Ni kweli niliongoza timu ya majasusi kwenda kumkamata Gaid Abdool nchini Sudan alikokuwa amejificha baada ya mashambulio ya mabomu katika balozi za Marekani jijini Dar es salaam na Nairobi.Kusema ukweli haikuwa kazi rahisi lakini kwa kutumia uzoefu wangu tuliweza kufanikiwa kumkamata gaidi yule hatari na kulifanya jina langu kuandikwa katika orodha ya majasusi hatari duniani.Monica akanitazama halafu akaendelea.
“Wiki mbili zilizopita uligunduliwa mpango kabambe wa kumtorosha gaidi Abdool ambaye bado anashikiliwa na serikali ya Tanzania akisubiri kukabidhiwa kwa serikali ya Marekani ili akasomewe mashtaka ya ugaidi.Mpango huo wa siri ulionaswa na makachero wetu ulianza kwa kukulenga zaidi wewe.Waliamini kuwa mpaka ukafanikiwa kumkamata Abdool basi ni wazi utakuwa unataarifa nyingi na za kutosha za mtandao huo wa Alqaeda na kwa hiyo ukaonekana kama mtu hatari sana kwao. lengo la kwanza lilikuwa kukuua.Lakini kabla ya kukuua walihitaji kwanza kukukamata ili uwaelekeze mahala pa siri alipofichwa Abdool na kasha wakuue.Kitu cha pili walichokuwa wamepanga ni kufanya shambulio kubwa ambalo litaistua nchi na kuvifanya vyombo vyote vya usalama viweze kuelekeza macho na nguvu zao huko katika shambulio kubwa na hivyo kuwapa wao nafasi nzuri ya kuweza kutekeleza mpango wao wa kumchukua Abdool bila matatizo makubwa.Hapo ndipo unaweza ukaona nini dhana ya shambulio la jana kule Arusha..CIA walinituma mimi ili mosi nikuokoe katika mikono ya magaidi na pili kushirikiana nawe kuhakikisha kuwa tunafanikiwa kuuvuruga mpango huo wa kumtorosha gaidi Abdool.Mpango huu ni wa siri kubwa na inabidi utekelezwe kwa usiri mkubwa.Serikali yetu haijaitaarifu chochote serikali ya Tanzania mpaka hapo tutakapokuwa tumefanikiwa kuuzima kabisa mpango huu.Tunachoogopa ni kwamba katika serikali nyingi kwa sasa duniani kuna vibaraka wa mitandao hii ya kigaidi na ambao huvujisha habari na kujipatia fedha nyingi toka mitandao hii.Niliingia nchini Tanzania kwa siri wiki moja iliyopita nikijulikana kama Rosa Monix raia wa Kenya na mafanyabishara wa bidhaa za urembo mwenye kusafiri sana kati ya dar es salaam na Nairobi.Kwa kuwa nimekaa katika eneo hili la afrika mashariki kwa miaka minne sasa nimeweza kujifunza kiswahili na kufanikiwa kukiongea vizuri .Au we unaonaje ? si ninaonekana kama mtanzania halisi? Akasema Monica wote tukacheka halafu akaendelea.
“Toka nimefika nimekuwa nikikufuatilia kwa siri na katika hilo kuna mambo nimefanikiwa kugundua.ambayo yanaweza yakatusaidia katika kazi hii .Kwanzainaonekana magaidi hawa tayari walikuwa na taarifa zako nyingi na walifahamu kila sehemu unayokwenda na kila kitu unachokifanya.Waliweza kufuatilia maongezi yako ya simu na kufahamu hata watu wote uliokuwa ukiwasiliana nao.Katika uchunguzi wetu tumegundua kwamba haya yote yalifanikiwa kwa msaada wa mtu mmoja aitwaye Rachel alphonse ambaye anafanya kazi katika ofisi zenu.Huyu amerubuniwa kwa kupewa fedha nyingi sana na magaidi ili aweze kuwapa taarifa muhimu za idra ya ujasusi Tanzania kila pale watakapozihitaji ”
Nilistuka mno kwa kulisia jina lile likitajwa katika orodha ya watu wanaoshukiwa kushirikiana na mtandao wa alqaeda.Kwa upande fulani niliweza kuamini maneno ya Monica kwa sababu kwa ghafla sana Rachel amekuwa na mafaniko makubwa kiasi cha kuwashangaza wengi.Mshahara wa Rachel ulikuwa wa kawaida lakini aliweza kumiliki jumba kubwa la kifahari,,magari ya kifahari mno,pamoja na vitega uchumi kadha wa kadha.Monica akaendelea.
“Kama nilivyosema awali kuwa,“magaidi waliweza kuyanasa maongezi yako uliyoongea na rafikiyo Ben hivyo ikawa rahisi kwa wao kuelewa kwamba ulikuwa ukielekea mapumzikoni mjini Arusha na ndiyo maana ikawa rahisi kwao kukufuatilia na hatimaye kutekeleza sehemu ya pili ya mpango wao yaani kufanya shambulio la kushtusha na kuipotezea serikali mwelekeo.Nilifahamu kila kilichokuwa kimepangwa kifanyike usiku wa jana kwa hiyo hadi tunaingia ukumbini nilijua nini kitakachotokea na tayari nilikwisha jiandaa kukabiliana nao.Usishangae nimefahamu vipi mipango yote ya magaidi,kwa ufupi ni kwamba tunavyo vyanzo vyetu vya taarifa hata ndani ya mtandao huu wa alqaeda na mitandao mingine ya kigaidi .Tukiwa pale ukumbini ukaniambia simu yako inaita nikajua tayari kazi imeanza.Ulipotoka kwenda nje huku hujui chochote kinachoendelea nilikufuata kwa nyuma bila wewe kujua.Ulipokuwa ukielekea maeneo ya maegesho ya magari niliwaona watu wanne wakishuka ndani ya gari moja dogo.Wakapeana ishara ya kukuzunguka.Akili yangu ikafanya kazi haraka haraka nikanyata mpaka karibu kabisa na ile gari walimotoka wale jamaa,nikaangalia ndani kwa tahadhari nikaona kuna mtu mmoja .Nilimnyemelea toka kwa nyuma na kummaliza kimya kimya kwa bastora yenye kiwambo cha kuzuia sauti halafu nikaingia ndani ya ile gari na kuikuta bunduki tatu aina ya SMG pamoja na silaha nyingine,nikaichukua moja.Nilitoka ndani ya ile gari nikakuona bado ukiendelea kuongea na simu nikawaona wale jamaa wakikunyemelea na ndipo nilipoanza kuwamaliza mmoja baadaya mwingine.Nilikuwa nimekaa katika sehemu ambayo haikuwa rahisi kwa wao kuniona na niliweza kuona kwa uzuri yote yaliyokuwa yakiendelea.Wale walinzi wawili wa magari niliwaona wakija upande wako nikajua lazima wataleta shida hivyo nikaamua kuwamaliza haraka kwa kutumia ile SMG kwani bastora yangu iliisha risasi na kama utakumbuka milio ile ya risasi ndiyo iliyoamsha kizaa zaa chote pale klabuni..Jamaa wale walikuwa wamejipanga kisawa sawa na walikuwa na mawasilano muda wote,hivyo walipoona mawasiliano na wenzao yamekatika,ghafla ikaingia gari nyingine toka nje iliyokuwa ikielekea kule mahala ulikokuwa.Nilitambua kwamba gari ile nayo ilikuwa ni ya wale jamaa kwa sababu nilimuona mtu mmoja akiruka toka ndani ya ile gari akiwa na bastora ndipo nilipoamua kulitupia bomu la mkono gari lile na kulilipua.Baada ya hapo ninaamini unafahamu kila kitu kilichoendelea hadi tumefika hapa.Hiyo ndiyo hali halisi namna ilivyokuwa na nadhani tayari una picha halisi ya kitu kinachoendelea hivi sasa hapa nchini.”
Monica akanyamaza akaniangalia usoni.Nilikuwa nimelowa jasho.
Pamoja na kutokwa na jasho usoni na mwilini ,nilihisi kuna ubaridi wa woga unaniingia ..Alqaeda !!!. si kundi la kufanyia mchezo hata kidogo.Huu ni mtandao mkubwa kabisa wa kigaidi duniani.Mambo niliyoyashuhudia Arusha yalikuwa ni picha tosha kuwa kundi hili tayari lilikwisha jizatiti vya kutosha hapa nchini.Kupambana nao inataka ujasiri mkubwa Lakini kwa vile wameingia nchini kwetu na wana lengo la kufanya kitu ambacho hatuko tayari kuona kikifanyika katika ardhi yetu basi sina budi kuingia katika mapambano na kundi hili hatari.Picha ya mabomu yaliyolipuka Arusha ikanijia kichwani,nikawakumbuka rafiki zangu Ben na Irene roho ikaniuma nikauma meno kwa hasira.Picha ya Abdool ikaja tena usoni kwangu,nikakumbuka ugumu tulioupata mpaka tukamkamata,..Haiwezekani wakaja kumchukua mtu huyu.Kwa Mauaji aliyoyafanya ni lazima afikishwe katika vyombo vya sheria na kujibu mashtaka dhidi yake.
“Tonny “ Monica akanistua.
“Najua utakuwa na wasi wasi mwingi kuhusiana na kazi hii lakini napenda kukuhakikishia kuwa serikali ya Marekani na shirika letu la CIA wako nyuma yetu.Wanashirikiana nasi bega kwa bega ili kuhakikisha kuwa tunafanikiwa katika kulizima jaribio hili la kumtorosha Abdool.”
“Monica” Nikasema
“Narudia tena kukushukuru kwa kuniokoa jana.Najua ulihatarisha maisha yako ili kuhakikisha ninakuwa salama.Sikuwa naelewa chochote hapo kabla na kwa sasa ninaelewa kuwa tuko vitani na mtandao mkubwa wa kigaidi duniani.Mimi siko tayari kuona Abdool anachukuliwa kutoka ardhi hii ya Tanzania na kurudishwa mikononi mwa alqaeda.Nitapambana kufa na kupona kuhakikisha suala hilo halifanikiwi.Nitapigana hadi tone la mwisho la damu yangu na Mungu anisaidie.”nikasema kwa hasira
“Jaribio lao la kwanza la kuniteka mimi ili wapate taarifa za mahala alipo abdool limegonga mwamba lakini wamefanikiwa kupoteza roho za watu wasio kuwa na hatia.Kwa sasa macho yote ya serikali yamehamia Arusha na hivyo kuwapa nafasi wao kutekeleza mpango wao.Nina hakika baada ya kunikosa mimi lazima watatafuta namna nyingine ya kuweza kumpata Abdool.Ninawafahamu vizuri watu hawa na namna wanavyofanya kazi.Siku zote huwa wanampango zaidi ya mmoja hivyo baada ya mpango wao wa kwanza kushindwa watatumia ule wa akiba.Hatutakiwi tuwape nafasi hiyo.Monica itatubidi kesho tuanze safari ya kuelekea Dar kwa sababu kule ndiko tutakapoifanyia kazi yetu.Abdool amefichwa sehemu ya siri jijini Dar na hivyo mpango mzima utatekelezwa kule.Picha yote inaenda kuchezwa jijini Dar.Natamani tuondoke hata sasa hivi”
Monica akatabasamu akaniangalia na kusema
“Tonny ninapokuwa nawe kamwe sihofu kitu chochote.Natumai tutafankiwa kulizima jaribio hilo…” Kabla hajamalizia sentensi yake mlango ukagongwa na kutufanya tukatishe maongezi yetu.Kwa tahadhari Monica akaenda kuufungua ,alikuwa ni Joe.
“Merry Christmass guys” akatusabahi
“Merry christmass Joe “Tukajibu kwa pamoja.
Joe akaniomba tukaongee faragha.Tukaelekea bustanini.Alionekana ni mtu mwenye wasi wasi mwingi.
“ Tonny,umepata taarifa yoyote toka ofisini? Akauliza Joe
“ hapana Joe sijapata taarifa zozote.Kuna taarifa gani?
“ Ina maana hujapigiwa simu na mkurugenzi? Joe akashangaa
“ Simu yangu niliiacha Dar.sikutaka mawasiliano yoyote ya kiofisi katika wakati huu wa mapumziko.Kwani kuna nini? Nikadanganya na Joe akaonyesha kuniamini.
“ Nimepigiwa simu sasa hivi na Vicky akinitaarifu kwamba watu wote tulioko nje ya dare s salaam tunatakiwa turudi ofisini mara moja.Hakunieleza kuna tatizo gani lakini nina hakika ni kutokana na tukio la jana jijini Arusha.”
“ Tukio la Arusha? !! Nikashangaa na kujifanya sielewi chochote
“ Kwani hujasikia kilichotokea Arusha?
“ Hapana Joe.Sifahamu chochote kilichotokea Arusha.Kumetokea nini?
‘ Kumetokea shambulio linalosemekana ni la kigaidi jana usiku.Klabu moja maarufu ya burudani imelipuliwa kwqa mabomu na idaid kubwa ya watu inasemekana wamepoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa.Bado hakuna taarifa rasmi zilizotolewa lakini vikosi vya ulinzi na usalama viko mahala hapo kuchunguza nini kilitokea.Nadhani ndiyo maana wote tumeitwa ofisini.” Akasema Joe
“Dah ! basi hii ni kazi kubwa.Kama ni hivyo basi hatuna budi kujiandaa kurejea dare s salaam.Ulikua na gari lako?
“ Ndiyo Tonny nilikuja na gari langu”
“ Good.Basi hilo ndiloo tutalitumia sote kurejea dare s salaam kesho.Leo lazima tupumzike tule sikukuu.Kristu amezaliwa leo kwa hiyo tukae tusheherekee na kesho turejee kazini”
“ Ok Tonny hakuna shaka” akajibu Joe.
Monica akaungana nasi pale bustanini maongezi yakakolea sana huku tukipata vinywaji.Baada ya maongezi marefu Joe akatuomba kama tunaweza kutoka na kwenda kuungana na ndugu zake katika kusherehekea sikukuu hii ya krismas.Tulimkatalia na kumuomba atuache tuendelee kupumzika ,bado tulihisi uchovu.
Joe akatuacha bila wasi wasi kwa sababu kulikuwa na kila aina ya chakula na vinywaji.Alipoondoka ,tukabaki wawili tu ndani ya jumba lile kubwa.
“ Sasa tuko huru” nikasema
“ Kwa nini unasema hivyo Tonny? Monica akauliza
“ Tuko huru kufanya mambo yetu.Dunia nzima wako katika kusheherekea kuzaliwa kwa masihi na hata sisi hatuna budi kusheherekea pia”
Monica akatabasamu na kusema
“ Unapenda kufanya nini Tonny”
“ Nataka tuifanye siku hii iwe ya furaha kwetu sote.Tuko katika kipindi kigumu na tuna kazi kubwa iliyoko mbele yetu lakini hii si sababu ya kutuzuia kufurahi.Monica naomba kwa saa hizi chache tuweke pembeni kila kitu na tuelekeze akili zetu katika kitu kimoja tu,kuifanya siku ya leo kuwa ya furaha kwetu.Naomba nikiri Monica wewe ni msichana mrembo ambaye siwezi kukufananisha na yeyote.Mambo uliyonifanyia kamwe sijawahi kufanyiwa na mwanamke yeyote chini ya jua.Si utani umenifanya nipagawe na kutaka kuwa nawe muda wote” Nikasema na kumfanya Monica acheke kicheko kikubwa.
“ Tonny wewe ndiye mjuvi wa mambo.Umenipa mambo ambayo sijawahi kufanyiwa.Wewe ni mahiri mno kitandani.Nafurahi kukutana nawe.Natamani baada ya sakata hili kumalizika niende nawe Marekani.Natamani kama ungekuwa ni mwanaume wa maisha yangu,niishi nawe hadi tufikie uzee.Huu si utani Tonny,umeziteka fikra zangu ghafla sana.”
Nikacheka kidogo halafu Monica akasema.
“ Tonny utakuwa tayari kuongozana nami kwenda Marekani baada ya kazi hii kumalizika? Tunaweza tukaacha kazi zetu hizi za hatari na kuishi maisha ya amani na starehe.Tutatafuta kazi nyingine za kufanya au hata kufanya biashara.Uko tayari kwa hilo Tonny? Akauliza Monica.Nilimtazama machoni na kugundua kwamba alimaanisha kile alichokiongea.
Nikatabasamu na kujibu
“Monica nashindwa nikujibu nini.Bado tuna mambo mengi ya kufanya mbele yetu na hatujui nini kitatokea.Ni mapema mno kukupa jibu lenye uhakika.Lakini usijali baada ya kazi hii kumalizika tutaona ninii kitafuata”

TUKUTANE SEHEMU IJAYO…………………….
 
BRING BACK OUR GIRLS
SEHEMU YA 13
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Nikacheka kidogo halafu Monica akasema.
“ Tonny utakuwa tayari kuongozana nami kwenda Marekani baada ya kazi hii kumalizika? Tunaweza tukaacha kazi zetu hizi za hatari na kuishi maisha ya amani na starehe.Tutatafuta kazi nyingine za kufanya au hata kufanya biashara.Uko tayari kwa hilo Tonny? Akauliza Monica.Nilimtazama machoni na kugundua kwamba alimaanisha kile alichokiongea.
Nikatabasamu na kujibu
“Monica nashindwa nikujibu nini.Bado tuna mambo mengi ya kufanya mbele yetu na hatujui nini kitatokea.Ni mapema mno kukupa jibu lenye uhakika.Lakini usijali baada ya kazi hii kumalizika tutaona ninii kitafuata”

ENDELEA……………………….

Ni siku ambayo naweza kusema kwamba ilikuwa ya kipekee sana kwangu.Nilishinda na binti malaika Monica tukipeana kila aina ya raha.Saa tatu za usiku tukiwa sebuleni tukiangalia runinga ambayo kwa asilimia kubwa matangazo yake yalitawaliwa na tukio la Arusha ,mara matangazo yakakatishwa na wimbo wa taifa ukapigwa ishara kwamba kuna jambo la kitaifa.Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania akajitokeza na kuligutubia taifa
“Ndugu wananchi” akaanza rais wa Tanzania kulihutubia taifa..
“Si kawaida yangu kuzungumza nanyi siku kama ya leo kutokana na utaratibu niliojiwekea,lakini kwa leo imenibidi nifanye hivyo.”
“Ndugu zangu,leo taifa la Tanzania limepatwa na msiba mkubwa ambao kilio chake hakielezeki.Usiku wa kuamkia siku ya leo ni usiku ambao hautaweza kusahaulika katika historia ya nchi yetu.Ndugu zetu wapatao 56 wamepoteza maisha katika mlipuko unaosadikiwa ni bomu uliotokea katika klabu ya burudani ya La fame jijini Arusha.Ni tukio la kustusha na kuhuzunisha mno
Ndugu wananchi,baada ya kupata taarifa hizo za kusikitisha,tumeanza uchunguzi mara moja ili kubaini chanzo cha tukio hilo .Nimevielekeza vikosi vya ulinzi na usalama vianze uchunguzi haraka sana vikiwatumia wataalamu wetu wa milipuko na mara uchunguzi utakapokamilika basi mtataarifiwa nini kilitokea na kusababisha maafa yale makubwa.
Pamoja na msiba huo mkubwa uliotupata ,tunaombwa tuendelee kuwa watulivu na wastahimilivu katika kipindi hiki kigumu.Kamwe tusijenge chuki na uhasama baina yetu kwa misingi ya dini,rangi ,kabila au utaifa.Tukumbuke siku zote kuwa watanzania ni wamoja na hata pale linapotokea jambo la kuhuzunisha namna gani bado sifa ya watanzania ni kushikamana na si kuvurugana.
Tukio hili limeitia doa amani yetu na kuwafanya hata wale waliokuwa na mipango ya kuja kutembea hapa nchini waahirishe au wasitishe kabisa mipango na safari zao.Napenda kuwahakikishia kuwa mipaka yetu ni salama,vyombo vyetu vya ulinzi na usalama viko macho muda wote na ulinzi umedhibitiwa katika sehemu zote za jiji la Arusha na nchi yote kwa ujumla wake.Napenda pia kuihakikishia jumuia ya kimataifa kuwa Tanzania bado ni nchi salama na hivyo wageni wote waliopanga kuitembelea nchi yetu wasisite kufanya hivyo.Tunawahakikishia ulinzi na usalama wao.
Kwa niaba yangu na serikali ,napenda kuchukua nafasi hii kutoa salamu zangu za rambi rambi kwa familia zote zilizopoteza wapendwa wao na ninawaombea wale wote waliopata majeraha uponaji wa haraka.Tuko pamoja nanyi katika kipindi hiki kigumu kwani huu ni msiba wetu sote.Napenda nizifikishe kwenu salamu za rambi rambi toka kwa watanzania wenzenu na wapenda amani kote duniani.Nimefarijika sana baada ya kupokea salamu nyingi za rambi rambi toka mataifa mbali mbali na wote wakiahidi kusaidiana nasi kwa hali na mali katika wakati huu mgumu.Ili kushirikiana na wafiwa wote katika kipindi hiki kigumu,serikali inatangaza siku tatu za maombolezo na kuahidi kuwazika wote waliopoteza maisha katika tukio hilo kwa heshima zote .
Tunaomba kila mtanzania kwa imani yake afanye maombi ya kuwakumbuka marehemu hawa na kuombea amani na utulivu a nchi yetu.Narudia kuwaambia tena kuwa uchunguzi wa tukio hili bado unaendelea tukishirikiana na vyombo vya usalama vya nje ya nchi na pindi uchunguzi ukikamilika basi mtataarifiwa ..
Mungu ibariki Afrika ,Mungu ibariki tanzania
Ahsanteni kwa kunisikiliza.
Rais wa Tanzania akamaliza hotuba yake fupi.Hatukuwa na muda mwingi wa kuongea tukainuka na kuelekea chumbani kujipumzisha kwa ajili ya safari ya kesho yake.

***************************************

Saa tisa na nusu za mchana siku iliyofuata tuliwasili jijini Dar.Tulitoka Mjini Moshi mishale ya saa kumi za alfajiri.Nashukuru Mungu hatukupata matatizo yoyote njiani licha ya kuwepo kwa vizuizi vingi vya askari polisi.
Joe alitaka tuelekee moja kwa moja ofisini lakini nikakataa na kumuomba anipeleke kwanza nyumbani kwangu halafu nitaelekea ofisini baadae.Niwapo safarini huwa naikabidhi nyumba yangu kwa kampuni binafsi ya ulinzi hadi hapo nitakaporudi.Pale nyumbani alikuwapo mlinzi mmoja kijana toka kampuni hiyo.Tulishuka garini tukaagana na Joel akaenda zake.Mlinzi akaja akatusalimu kwa adabu.Baada ya kusalimiana na kujuliana hali ikiwa ni pamoja na taarifa ya usalama wa nyumba mlinzi yule akanikabidhi bahasha iliyokuwa na ujumbe ndani yake.Nikaitazama bahasha ile ambayo haikuwa imeandikwa chochote juu yake.
“nani kaileta bahasha hii” Nikauliza
“Kuna jamaa alikuja hapa na gari leo asubuhi , hakunitajia jina lake.Alikuwa na gari yeupe na kwa bahati mbaya sikuweza hata kukariri namba zake.Aliuliza kama mwenye nyumba yupo,nikamjibu hayupo ,akanipa bahasha hii ili ukija nikupatie”
Nikaitazama tena bahasha ile ambayo haikuwa imeandikwa kitu chochote juu yake.Nikamshukuru mlinzi yule kwa kazi nzuri ya ulinzi wa nyumba yangu.Nikaingiza mkono mfukoni na kumuhesabia kiasi cha shilingi elfu hamsini nikampatia.Aliniangalia kwa jicho la mshangao mkubwa,lililoonyesha kunishukuru mara elfu.
“Mkuu nashukuru sana Mungu akubariki” Akasema jamaa yule ambaye kwa jina alikuwa akiitwa Hamisi.Ingawa nilikuwa nikiilipa kampuni yao kwa kunilindia nyumba sikuona tatizo kumpa kifuta jasho na yeye pia kwa kazi nzuri.
Nilimwacha hapo nje mlinzi yule akishangaa shangaa huku akikusanya vifaa vyake tayari kwa kuondoka kwa sababu sikuwa nahitaji tena mtu wa kunilindia nyumba.Nikamshika mkono Monica tukaingia ndani.Nikamwacha Monica sebuleni akiendelea kupata kinywaji mimi nikafanya zoezi la kuikagua nyumba yote.Nilipohakikisha kila kitu kiko salama salimini nikarudi sebuleni na kujimiminia mvinyo halafu nikaenda kuketi sofani.Nikaifungua bahasha ile na kukuta kijikaratasi kidogo chenye ujumbe mfupi
“Ofisini haraka”.
Sikustuka sana kwani tayari nilikwisha elewa kila kinachoendelea. “Monica kazi imeanza.Nimeitwa ofisini” Nikamwambia Monica
“ Nadhani mwito huu unahusiana na tukio la Arusha”
Monica akafikiri kidogo kisha akasema.
“Iwapo watakuwa wanataka kukupa kazi ya kufanya kuhusiana na tukio la Arusha tutakeleza vipi mpango wetu? Ninauliza hivyo kwa sababu mpango huu ni wa siri kubwa na haitakiwi mtu yeyote afahamu kama niilivyokwisha kueleza ".
“Usijali Monica.Ngoja nikawasikilize wananiitia kitu gani halafu nitajua nini cha kufanya baada ya hapo.Kama itakuwa ni kazi inayohusiana na tukio lile ninajua ni jinsi gani nitafanya ili tusiweze kuchanganya mambo.” Nikajibu na kumpa Moyo Monica.
Nilimpeleka Monica katika chumba changu cha siri ninachohifadhi nyaraka na vitu vyangu vya kazi.Monica alitaka kuwasiliana na ofisi yao. Katika chumba hiki ndimo nimehifadhi mambo yangu mengi ya siri ikiwa ni pamoja na silaha zangu.Sikuwa na wasi wasi wowote wa kumuacha Monica peke yake kwa sababu tayari nilikwisha muamini sana.Niliitoa gari yangu gereji ,nikaongeza mafuta na kuondoka kuelekea ofisini.


******************************************

Niliwasili ofisini nikaegesha gari na kwa haraka nikapanda lifti mpaka ghorofa ya nne iliko ofisi ya mkurugenzi wetu.Niliingia ofisini kwa mkurugenzi na kupokelewa na Vick.
‘aaah !! Tonny..umerudi? mambo vipi? Akanisalimu Vick kwa furaha iliyochanganyika na wasiwasi mwingi.
“mambo poa Vick habari yako? Krismass ilikuaje? Nikauliza.
“Krismass mbaya Tonny.Sikukuu yote hii nimekuwa hapa kazini,sikupata hata wasaa wa kujumuika na rafiki zangu kufurahi.
“Pole sana,ndiyo kazi zetu zilivyo.Vipi mkurugenzi nimemkuta?
“Ndiyo,Mkurugenzi yuko ndani alisema ukifika pita moja kwa moja” akasema Vicky huku akionyesha wasi wasi Fulani.Vick alionyesha kutaka kuongea na mimi kitu lakini hakupata nafasi kwani tayari nilikwisha kinyonga kitasa cha mkurugenzi na kujitoma ndani.Nilipoingia tu nikajikuta nikitazama na mkurugenzi wetu Mzee Meshack Jumbo pande la mtu akiwa amekalia kiti chake cha kuzunguka huku akionekana mchovu na mwenye hasira.Kipara chake kilikuwa kikitoa jasho licha ya ofisi yake kuwa na kipoza hewa na kuifanya hewa ya ofisini humo kuwa ya ubaridi mwingi.Pembeni kabisa ya ofisi kulikuwa na watu wawili ambao mmoja wao niliweza kumfahamu.Alikuwa akifanya kazi katika idara ya usalama wa taifa.Nyuma ya watu hao wawili kulikuwa na askari sita wote wakiwa na bunduki aina ya SMG .Kengele ya hatari ikagonga kichwani ,nikajua hapo liko jambo.
Nikamsalimu Mkurugenzi naye bila kunijibu ,akanipa ishara niketi katika kiti kitupu kilichokuwa mbele ya meza yake.Nilijilaumu sana kwa kutoongea na Vick kabla sijaingia humu ofisini.Ni wazi Vick alikuwa akitaka kunifahamisha jambo Fulani.
Mkurugenzi alikuwa akinitazama kwa hasira,akinikagua toka juu hadi chini.Akatoa kitambaa na kufuta jasho lililokuwa likimtoka usoni kama mtu aliyemaliza mbio za kilometa elfu kumi.
“Nashukuru umefika Tonny.Tumekutafuta sana katika simu yako bila mafanikio.Kwa nini ukaamua kuizima simu yako wakati ukifahamu kwamba wewe ndiye tegemeo hapa ofisini na muda wowote tunaweza kukhitaji?.Joe alinitaarifu kwamba uko naye na mnarejea Dar es salaam na ndiyo maana tukakutumia ujumbe ule nyumbani kwako.Nashukuru baada ya kuupata umeitika wito na kuja mara moja.Siku nyingine unapokuwa nje ya jiji kwa jambo lolote,kikazi au si kikazi basi usithubutu kuizima simu yako.” Akasema mkurugenzi.
“Tuachane na hayo” Akasema mkurugenzi.
“Kabla hatujaendelea ,ningependa kwanza kufanya utambulisho mdogo.Walioko mbele yako ni maafisa waandamizi toka katika idara ya usalama wa Taifa.Yule mrefu mwenye suti ya kijivu anaitwa martin Mchupa na yule mwenzake mwenye suti nyeusi anaitwa Sylvester Mkole.Wale waheshimiwa kule nyuma ni mafiasa wa polisi,.Kuanzia kushoto ni Sajenti Adam,Sajenti Krispin,PC ayoub,Koplo Alphonse, PC Fidelis na Meja Ally.”
Aliwatambulisha kwangu wale jamaa halafu akwageukia
“Jamani huyu ndiye Tonny”
Mkurugenzi akamaliza utambulisho wake mdogo.Akatulia kidogo halafu akaendelea.
“Nafikiri sote hapa tunafahamu nini kimetokea Arusha katika usiku wa kuamkia siku kuu ya krismas.Kilichotokea Arusha kimeistua sana serikali yetu na dunia kwa ujumla.Baada ya tukio hilo tulianza kufanya uchunguzi wetu mara moja tukishirikana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.Katika uchunguzi wetu wa awali tumeweza kugundua mambo kadhaa ikiwamo mmoja wa vijana wetu kuhusishwa na tukio hilo.”
Mkurugenzi akanyamaza kidogo na kunitazama kasha akaendelea.
“ Tonny ,kutokana na uchunguzi uliofanyika ,imeonekana una kitu cha kueleza kuhusiana na tukio hili.” Nywele zikanisimama baada ya kauli ile ya mkurugenzi.
“ Imeonekana unaweza ukasaidia kufahamu kiini cha tukio hili la Arusha kwa sababu kutokana na mazingira yalivyokuwa inaonekana wazi kwamba kuna kitu kinachoendelea ambacho unakifahamu.Wewe ni mtu unayefahamu mambomengi na si kila jambo unalolifahamu unalifikisha mahala husika kwa maana hiyo basi endapo kuna jambo unalolifahamu kuhusiana na tukio hili naomba uliweke wazi ili liweze kufanyiwa kazi.Taifa letu linpitia kipindi kigumu sana kiusalama kwa sasa kwa hiyo tunafanya kila kinachowezekana ili kuhakikisha tunaendelea kuilinda amani ya nchi yetu.” Akanyamaza kidogo akaniangalia kwa makini na kusema.
“ Maelekezo niliyopewa ni kwamba kuanzia sasa Tonny utakuwa chini ya ulinzi na utapelekwa katika kambi ya kijeshi ambako utashikiliwa na kuhojiwa kuhusiana na tukio hili ili kufahamu uhusika wako.Ikithibitika kwamba uhusiki kwa namna yoyote ile na tukio lile basi utaachiwa huru na kurejea kazini.Kwa maana hiyo nakuomba utoe ushirikiano wa kutosha.Kwa sasa nakukabidhi rasmi kwa wanausalama ambao watakupelekea katika sehemu utakapowekwa kwa muda” akasema mkurugenzi.Sura yake ilionyesha simanzi kubwa kwani aliniamini mno mzee huyu.
Nilivuta pumzi ndefu.Sikuwa na ujanja nilikuwa nimenasa .Tayari walikwisha fahamu kwamba ninahusika katika tukio lile baya.Nilitamani nimweleze ukweli mkurugenzi lakini nikayakumbuka maneno ya Monica kwamba jambo hili ni la siri kubwa na hatakiwi mtu yeyote ndani ya serikali kulifahamu.
Askari wale waliweka tayari silaha zao zote kunielekea miminadhani walikwisha taarifiwa kwamba mimi si mtu wa kufanyia mchezo.
Ujanja wowote ule wa ambao ningejaribu kuufanya mbele ya silaha zile ungeweza kunigharimu maisha yangu kwa kuchakazwa vibaya kwa risasi kitu ambacho sikuwa tayari kitokee hasa kutokana na kazi kubwa inayonikabili ya kuzuia mpango wa magaidi kumtorosha gaidi Abdool .
Kitu ninachomshukuru Mungu mpaka leo ni kunipa uwezo wa kufikiri na kufanya maamuzi sahihi nay a haraka.Mara nyingi nimekuwa nikijikuta katika sehemu hatari ambayo si rahisi kwa mtu kuweza kujiokoa ,lakini kwa kutumia uwezo wangu wa kufikiri na kuamua kwa haraka ukichangia na uzoefu wangu niliweza kujiokoa.
TUKUTANE SEHEMU IJAYO…………………
 
BRING BACK OUR GIRLS

SEHEMU YA 14

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA

Nilivuta pumzi ndefu.Sikuwa na ujanja nilikuwa nimenasa .Tayari walikwisha fahamu kwamba ninahusika katika tukio lile baya.Nilitamani nimweleze ukweli mkurugenzi lakini nikayakumbuka maneno ya Monica kwamba jambo hili ni la siri kubwa na hatakiwi mtu yeyote ndani ya serikali kulifahamu.Askari wale waliweka tayari silaha zao zote kunielekea miminadhani walikwisha taarifiwa kwamba mimi si mtu wa kufanyia mchezo. Ujanja wowote ule wa ambao ningejaribu kuufanya mbele ya silaha zile ungeweza kunigharimu maisha yangu kwa kuchakazwa vibaya kwa risasi kitu ambacho sikuwa tayari kitokee hasa kutokana na kazi kubwa inayonikabili ya kuzuia mpango wa magaidi kumtorosha gaidi Abdool . Kitu ninachomshukuru Mungu mpaka leo ni kunipa uwezo wa kufikiri na kufanya maamuzi sahihi nay a haraka.Mara nyingi nimekuwa nikijikuta katika sehemu hatari ambayo si rahisi kwa mtu kuweza kujiokoa ,lakini kwa kutumia uwezo wangu wa kufikiri na kuamua kwa haraka ukichangia na uzoefu wangu niliweza kujiokoa.

ENDELEA………………………

“ Siwezi kukubali kuchukuliwa na hawa askari.Lazima niwatoke” nikawaza.Nilitazama upande wa kushoto kwangu nikamuona Martini Mchupa akiinuka na kuwapa ishara wale askari wajongee wanifunge pingu.Askari wawili walinijongelea kwa dhumuni la kunikamata.Wakiwa hatua zipatazo tatu toka mahala nilipokuwa nimesimama,nilifanya kitu ambacho hakuna mmoja kati yao aliyekuwa amekitegemea.Kufumba na kufumbua niliinuka katika kiti nilichokuwa nimekalia,nikakipiga teke kali la nyuma ,kikaruka kuwalekea wale askari wawili ambao walistuka na kujaribu kukikwepa.Ni fursa hiyo ndiyo nilikuwa naihitaji.Walipokuwa katika harakati za kukikwepa kiti,niliruka na kutua nyuma ya mkurugenzi wetu ambaye naye kwa wakati huo alikuwa amesimama amepigwa na butwaa.Nilimkaba kabali shingoni kwa mkono wangu wa kushoto na kwa kutumia mkono wangu wa kulia nikaishika bastora na kumwelekezea mkurugenzi kichwani.Ni kitendo cha sekunde chache kilichowaacha watu wote mle ndani midomo wazi. “Wekeni silaha zenu chini haraka” Nikasema kwa ukali.Kitendo cha kuwaamuru askari wale waweke silaha chini kilionekana kuwa kigumu mno kwao.Lakini papo hapo waliogopa kufanya kitendo chochote cha ufyatuaji risasi kwa sababu tayari mzee meshack Jumbo nilikwisha muweka ngao yangu “Nasema wekeni silaha zenu chini!!!” Nikarudia tena kwa hasira baada ya kuona wanasita kufanya nilivyo waamuru.Bado niliendelea kumkaba mzee Jumbo kabali nzito na kumfanya aanze kupumua kwa shida.Nilimuonea huruma mzee yule lakini sikuwa na jinsi nyingine ya kufanya ili kujiokoa Mzee Jumbo ananifahamu vizuri kuwa nikiwa kazini huwa sina masihara hata kidogo.Kwa sauti ya kukwaruza kutokana na kabali niliyomkaba akasema, “we…….weke….ni…sil..aa.ha…chhh…ii.ni” Alitamka kwa taabu mkurugenzi wetu. Askari wale bado walionekana kutokukubaliana na jambo lile.Sikuwa na muda wa kupoteza nikailenga kwa risasi taa kubwa iliyokuwa humo ofisini ambayo ilitoa mlio wa kustusha.Risasi ile ikaleta kizaa zaa mle ndani.Watu wote wakalala chini.Mkurugenzi machozi yalikuwa yakimtoka.Sikutegemea kama iko siku nitamuona mzee huyu niliyekuwa nikimuona jasiri sana akitoa machozi. ‘Simameni wote na wekeni mikono yenu juu ” Nikawaamuru,na safari hii wakatii,wakainuka huku wakiwa mikono juu.Nadhani walikwisha ng’amua kuwa sikuwa na utani hata kidogo. “wote geukeni ukutani” Nikawaamuru tena.
“Wewe mwenye suti nyeusi,zisukume hizo bunduki zote kwa mguu kuja kwangu.” Yule jamaa ambaye kwa dakika hizi chache alikuwa amesawajika vibaya akazisukuma bunduki zile haraka haraka.Niligundua kuwa kila askari alikuwa na pingu .Nikapata wazo.
“Haraka sana chukua pingu hizo za kila mmoja umfunge mikono kwa nyuma kwa pingu yake.” Alitaka kuongea kitu lakini alipoyakutanisha macho yangu na yake akaogopa na kufanya nilivyomuamuru.Nafikiri aliona Israili ndani ya machor yangu.Huwa sina masihara kazini. Alipomaliza kuwafunga wenzake,nikamuamuru naye achukue pingu na kujifunga mikono halafu taratibu nikaanza kurudi nyuma huku nikiwa bado nimemkaba kabali mzee Jumbo. “Yeyote atakayejaribu kugeuza uso wake namfumua kwa risasi” Nikaendelea kuwaambia kwa hasira. Nikalikaribia dirisha kubwa nikalifungua na kuangalia nje.Nisingeweza kuruka toka ghorofa ya nne.Ghorofa ya tatu nikaona kulikuwa na kiambaza kidogo na pemBeni yake kulikuwa na bomba la maji machafu.Nikawageukia tena wale watu mle ofisini na kuwakuta wote bado wamegeukia ukutani na mikono yao imefungwa kwa nyuma kwa pingu.Ili kuwastua zaidi nikaachia risasi moja iliyoilenga saa kubwa ya ukutani iliyotoa mlio wa kuogopesha.Wote wakalala chini kwa hofu.,nikapanda dirishani na kuruka hadi katika ghorofa ya tatu.Nikatua salama katika ghorofa ya tatu nikaangaza pande zote na hakukuwa na mtu yeyote anayenifuatilia,,nikakimbia hadi kwenye boma la maji machafu nikalikwea na kuanza kuteleza nalo kuelekea chini.Mita kadhaa kabla sijatua chini nikawaona askari walinzi watatu wanaolinda geti la kuingilia ofisini kwetu wakija upande ule kwa kasi ya ajabu wakiwa na bunduki zao mikononi.Nikajua tayari mkurugenzi atakuwa amewapigia simu.Nikajilamumu sana kwa kumuacha akiwa mzima. Nikajiachia toka katika lile bomba na kutua chini ,halafu nikaanza kukimbia kuelekea zilipo ofisi za shirika la misaada la Marekani.Nikaufikia ukuta uliozitenganisha ofisi zetu na ofisi hizo za shirika la misaada la marekai,nikageuka kuwaona wale walinzi waliokuwa wakinifukuzia,,bado walikuwa wakija kwa kasi.Nikarudi nyuma hatua kadhaa na kuurukia ukuta.Nikiwa juu ya ukuta nikaiskia mivumo miwili ya risasi sentimeta chache toka kichwa changu,nikajua jamaa wameamua kunipiga risasi baada ya kuona tayari ninawatoroka.Nikajirusha ndani ya wigo wa ofisi za shirika la misaada la Marekani,nikaanza kukimbia kuelekea yalipo mabohari yanayotumika kuhifadhia vifaa mbali mbali.Mara nyingi katika majengo ya shirika hili hakuna walinzi kwa sababu wao hutumia mitambo maalum ya ulinzi.Nikakimbia mpaka nyuma ya bohari la tatu na kuuparamia ukuta ili niruke kuelekea upande mwingine.Nilipata taabu sana kupenya katika seng’e nge zilizokuwa juu ya ukuta huo.Nikafanikiwa kupanda nikajirusha upande mwingine ambao kulikuwa na kiuchochoro kilielekea katika hoteli ya kitalii ya Sunlight motel.Nikaruka uzio na kuingia katika maegesho ya magari ambako hupaki teksi nyingi.Nikaangaza angaza eneo hili na kuhakikisha liko shwari,nikaingia katika teksi moja nyeupe yenye vioo vyeusi nikamuomba dereva aniondoe pale haraka na kunipeleka sehemu niliyomuelekeza.Ingawa alionyesha wasi wasi Fulani,lakini baada ya kujishauri kwa sekunde kadhaa akaondoa gari.

********************

“Pole sana ndugu yangu” Ilikuwa ni sauti ya dereva wa ile gari niliyopanda.alinistua toka mawazoni nikageuka na kumtazama usoni.Alikuwa ni kijana wa makamo,na mtanashati .Dereva yule alikuwa ameukazia macho mkono wangu wa kulia .Sikujua ni kitu gani alichokuwa akikiangalia ikanibidi niiname kuuangalia mkono wangu.Nilikuwa na jeraha kubwa lililokuwa likivuja damu.Niliumia katika heka heka za kukumbia.Kitu cha ajabu ni kwamaba sikuwa nikihisi maumivu yoyote licha ya ukubwa wa jeraha
“Pole sana brother” Akasema tena
“Ahsante” Nikajibu kwa ufupi.Nikatulia na kumeza mate.Kutokana na jeraha kuendelea kuvuja damu nikaamua kuvua fulana yangu na kuifunga katika jeraha.
“kaka unaonaje kama ningekupitisha hospitali kwanza ukatibiwe hilo jeraha Akasema tena yule dereva. ”nashukuru sana ,ila kwa sasa sihitaji kwenda katika hospitali yoyote zaidi ya ile iliyoko kazini kwangu.Pale nitatibiwa kama mfanyakazi.Nikienda katika hospitali nyingine nitaambiwa niende kuchukua kibali cha polisi,kwa sababu jeraha hili ni kubwa.”
“Usijali kuhusu hiyo PF3 kaka yangu.Mimi ninaye rafiki yangu ana hospitali yake,naweza nikakupeleka akakutibu bila kudai kibali tena bure kabisa.”
“kaka nashukuru tena kwa kuamua kunisaidia ,lakini naomba tu uniache nikatibiwe kazini kwangu ili nipate mapumziko..” “Kwani unafanya kazi wapi kaka” akauliza
“Mimi nafanya kazi katika kampuni moja iitwayo The Taquet agencies co.Ltd iko Upanga.” Nikadanganya.Kampuni hiyo niliifahamu kutokana na rafiki yangu mmoja aliyekuwa akifanya kazi hapo. ‘naifahamu kampuni hiyo.Si ile ya kuuza magari? Akasema “Exactly….ndiyo hiyo…” nIkajibu huku nikijilazimisha kutabasamu.Lengo lilikuwa kumpoteza kijana huyu katika udadisi wake.
“kwa hiyo kwa sasa unalekea kazini? Akauliza tena
“hapana nelekea nyumbani” Nikajibu
********************

KIKAO CHA DHARURA IKULU DAR ES SALAAM

Ni mtu mmoja tu aliyekuwa akisubiriwa katika kikao hiki kizito cha dharura kilichowakutanisha viongozi wote wa juu serkalini na viongozi wote wa vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi.Aliyekuwa akisubiriwa ni mkurugenzi wa Secret Internal security ” Mr Meshack Jumbo .Mpaka muda huo ni yeye tu aliyekuwa hajatokea licha ya kupewa taarifa ya kutakiwa kuwepo katika kikao kile cha dharura. Chumba chote kilikuwa kimya ,kila mjumbe alikuwa akijaribu kupitia mafaili yake.Ni wajumbe wachache tu waliokuwa wakinong’ona.wengine walikuwa walikuwa wakijipepea kwa makaratasi kupunguza joto walilolisikia.Hii iliashiria uzito wa kikao hiki kilichoitishwa na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ili kujadili hali ya usalama wa nchi inavyokwenda hasa baada ya kutokea milipuko ya Arusha iliyosababisha vifo vya watu wengi.

TUKUTANE SEHEMU IJAYO………………….
 
BRING BACK OUR GIRLS

SEHEMU YA 15

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Ni mtu mmoja tu aliyekuwa akisubiriwa katika kikao hiki kizito cha dharura kilichowakutanisha viongozi wote wa juu serkalini na viongozi wote wa vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi.Aliyekuwa akisubiriwa ni mkurugenzi wa Secret Internal security ” Mr Meshack Jumbo .Mpaka muda huo ni yeye tu aliyekuwa hajatokea licha ya kupewa taarifa ya kutakiwa kuwepo katika kikao kile cha dharura.
Chumba chote kilikuwa kimya ,kila mjumbe alikuwa akijaribu kupitia mafaili yake.Ni wajumbe wachache tu waliokuwa wakinong’ona.wengine walikuwa walikuwa wakijipepea kwa makaratasi kupunguza joto walilolisikia.Hii iliashiria uzito wa kikao hiki kilichoitishwa na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ili kujadili hali ya usalama wa nchi inavyokwenda hasa baada ya kutokea milipuko ya Arusha iliyosababisha vifo vya watu wengi

ENDELEA.................................................

Saa tisa na dakika thelathini na nane Mr Meshack Jumbo akaingia ukumbini akiwa ameongozana na walinzi wawili huku sura yake ikionyesha uchovu na kusawajika.Akaelekezwa sehemu yake ya kukaa na bila kuongea na mtu yeyote akaketi.
Dakika zipatazo kumi toka Mr Jumbo awasili mle ukumbini ,mheshimiwa Rais akaingia.wajumbe wote wakasimama kumpa rais heshima yake hadi alipoketi kitini.Akanong’onezana machache na mkuu wa usalama wa taifa Mr Kessy abraham ambaye alikuwa akijifuta jasho mara kwa mara ,akaiangalia saa yake na kukohoa kidogo kwa dhumuni la kuwaweka sawa wajumbe halafu akafungua kikao.
“Mheshimiwa waziri mkuu,waheshimiwa mawaziri wa wizara mbali mbali pamoja na manaibu wao,Mheshimiwa mkuu wa majeshi, na wakuu wa vyombo vyote vya usalama nchini,awali ya yote napenda kuwashukuru kwa kuitika mwito huu wa dharura.Nafahamu mlikuwa katika majukumu mazito ya taifa letu lakini nafurahi kuwa nyote mmeacha shughuli zenu na mko hapa sasa hivi”
akatulia kidogo ,halafu akaendelea
“Ndugu wajumbe, nimeitisha kikao hiki nikiwa kama kiongozi wa nchi ili kujadili kwa kina hali ya usalama wa nchi yetu na kujadili hatua stahili za kuchukua.Nyote mnafahamu tukio la hivi karibuni lililotokea Arusha.Ni moja kati ya tukio baya kabisa kuwahi kutokea katika nchi yetu.Ingawa uchunguzi bado unaendelea ningeomba Mr Augustino mayowa ambaye ndiye kiongozi wa uchunguzi wa tukio hilo uweze kutupa nini mmefanikiwa kugundua hadi hivi sasa”
Mr Augustino Mayowa kutoka idara ya usalama wa taifa ambaye alikabidhiwa kuongoza timu ya uchunguzi wa tukio la Arusha akasimama na kulifungua faili lake,akarekebisha tai yake na kusema.
“Mheshimiwa rais,na wajumbe wote mliohuduhuria kikao hiki cha dharura,napenda nichukue fursa hii kuwashukuru wakuu wa vyombo vyote vya usalama kwa namna walivyoonyesha ushirikiano mkubwa katika tukio hili.Ripoti ya awali ya kiuchunguzi inasema kwamba usiku wa kuamkia siku kuu ya krismasi,katika ukumbi wa burudani wa La fame unaokadiriwa ulikuwa na watu zaidi ya 500 kulitokea mapigano kati ya makundi mawili ambayo yalipelekea tukio la kutupiana risasi na hatimaye silaha nzito za kivita kama vile mabomu kutumika.Mapigano haya yaliyosababisha milipuko miwili mikubwa amabyo bado tunaifanyia uchunguzi ili kugundua kama ni mabomu,yamesababisha vifo vya watu 67 mpaka sasa hivi na wengine 200 wakijeruhiwa kati yao 47 vibaya sana.Majeruhi wengine walio katika hali mbaya wamehamishiwa katika hospitali ya KCMC mjini Moshi na wengine watano wamesafirishwa hadi katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.Ripoti ya awali a uchunguzi imemtaja kijana wetu toka katika idara ya ujasusi Tonny Malick kuwa mmoja kati ya washukiwa wa kuhusika na tukio hilo.Sina hakika bado kama tayari amekwishatiwa nguvuni au la.Kwa vile mkurugenzi wake yuko hapa basi tutapata mengi toka kwake.Pamoja na kushukiwa huko lakini bado uhusika wake unabaki kuwa nyeti kwa sababu hatujui bado anavaa sehemu gani ya uhusika hadi hapo tutakapokuwa tumemtia mikononi na kufanya mahojiano naye.Mheshimiwa rais hiyo ndiyoripoti fupi ya awali iliyopatikana hadi hivi sasa” Akamaliza kuwasilisha ripoti yake Mr Augustino akakaa.Mheshimiwa Rais aliyekuwa akisikiliza kwa makini akasema.
“Kazi nzuri mr Augustino.Lakini naomba vijana waongeze bidii na kasi ya kufanya uchunguzi ili tuipate ripoti kamili haraka iwezekanavyo .Mr Jumbo ,nadhani tayari una taarifa juu ya mmoja wa vijana wako kuhusishwa na tukio hilo,je mmefikia wapi mpaka sasa hivi? Tayari amekwisha kamatwa?
Mr meshack Jumbo akasimama na kusema
“Mheshimiwa rais kwa sasa bado hatujafanikiwa kumtia Tonny mikononi mwetu”
“kwa nini Mr Jumbo? Kuna tatizo gani la kuweza kumkamata mkisaidiana na maafisa wa polisi? Wewe ndiye mkurugenzi wake na unayejua ni wapi alipo kwa sasa.Ugumu uko wapi? Akauliza mheshimiwa Rais.
“Mheshimiwa rais ,ni kweli tulipata taarifa toka idara ya usalama wa taifa kuhusu kuhusishwa kwa mmoja wa vijana wetu katika mauaji ya Arusha.taarifa hiyo ilimweka Tonny kama mshukiwa namba moja.Kwa mujibu wa taarifa ya uchunguzi nikwamba kabla ya tukio halijatokea,Tonny alikuwa na wenzake ambao majina yao yametambulika kuwa ni Ben Mwaipopo,Irene machuwa pamoja na msichana mwingine aliyefahamika kwa jina moja tu la happy.Msichana huyu happy amekuwa na Tonny tangu amewasili jijini Arusha .Bado uhusiano wao haujajulikana wazi lakini inaonekana kuna uhusiano wa kimapenzi kati yao.Ben ambaye ni rafiki yake na Tonny na ambaye alimpokea uwanja wa ndege wa Kilimanjaro akiwa na Happy,amenukuliwa akisema kuwa kabla ya tukio kutokea Tonny na happy walikuwa wakicheza mziki,halafu ghafla tonny akatoka na baada ya muda mfupi happy naye akatoka.Akizungumza kwa taabu katika hospitali ya Maount Meru alikolazwa yeye na Irene kutokana na majeraha waliyoyapata ,anasema aliandikisha jina katika watu waliopotelewa na ndugu zao.Jina la Tonny liliorodheshwa na Ben katika orodha ya watu waliopotea na ndilo hilo liliwafanya wachunguzi kumtafuta Ben na kumuhoji .Uchunguzi uliendelea ili kubaini kama Tonny ni mmoja wa watu waliopoteza maisha au la..wakati uchunguzi ukiendelea zikafika taarifa toka kwa watu wawili waliodai kuporwa gari na watu wawili mwanamke na mwanaume waliokuwa na silaha.Gari hilo ni mali ya kampuni ya kulima na kusafirisha maharage nje ya nchi na siku wanatekwa walikuwa wakipeleka mzigo wa maharage uwanja wa ndege wa kimataifa wa kilimanjaro kwa ajili ya kuyasfirisha nje ya nchi.Muda uliotajwa kutumiwa na watu hao kuliteka gari hilo ni kama dakika arobaini tangu tukio litokee.Wasifu ulioelezwa nanmmoja wa watu hao ,ulishabihiana kabisa vilivyo na wasifu wa Tonny.Siku iliyofuata gari hilo lilikutwa limetelekezwa mijini Moshi.Tulipopata taarifa hizo tukawasiliana na mmoja wa kijana wetu aishiye mjini Moshi kama amefanikiwa kuonana naTonny.Kwa bahati nzuri Joe akakiri kuwa Tonny akiwa na mpenzi wake aliyejulikana kama Monica waliwasili hapo kwake alfajiri ya sikukuu ya krismasi na wakashinda hapo kwake,na siku iliyofuata akawatafutia usafiri katika gari dogo la rafiki yake aliyekuwa akielekea Dar es salaam.Tulipopata uhakika kuwa Tonny anakuja Dar tukaweka mtego ili afike mwenyewe ofisini kwani hakuwa na taarifa kuwa anatafutwa.Alifika ofisini na kuwekwa chini ya ulinzi lakini kwa namna ya ajabu kabisa ameweza kutoroka na kukimbia na mpaka sasa bado hatujapata taarifa yoyote kuhusiana naye lakini Jeshi la Polisi linaendelea na msako mkali na nina uhakika muda si mrefu atapatikana.Hapo ndipi tulipofikia mheshimiwa rais”
Meshack Jumbo akamliza kutoa ripoti yake akakaa.Mheshimiwa rais akasema
“Ndugu wajumbe ,nadhani nyote mmemsikia vizuri Mr Jumbo.Kijana huyu anaonekana ni hatari mno na kuendelea kumuacha mtu hatari kama huyu awe huru kunahatarisha zaidi usalama wa taifa.Nataka nguvu zote kwa sasa zielekezqwe katika kumtafuta Tonny.Mkuu wa jeshi la polisi ninyi mmejipanga vipi katika hili?
Wilfred Senke Inspekta jenerali wa polisi, akasimama na kujibu.
“Mheshimiwa rais,kwa sasa tumewatawanya vijana wetu katika kila sehemu ambayo tunadhania kuwa Tonny anaweza akawepo.Tumeweka vizuizi katika njia zote zinazoingia na kutoka Dar es salaam na hivyo kufanya suala la kutoroka Dar kuwa gumu.Tunafanya msako pia katika nyumba zote za kulala wageni na tunaendelea na zoezi la kuchapisha picha zake ili kuzitawanya nchi nzima ikiwa ni pamoja na kutangaza zawadi nono kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwake.Zoezi hili la picha bado halijakamilika lakini nimetaarifiwa kuwa maendeleo yake ni mazuri.Ukiacha hilo la huyu kijana Tonny,jeshi la polisi bado linaendela na uchunguzi,tumekuwa tukiwahoi watu mbali mbali na zoezi hilo bado linaendela.Litakapokamilika tutatoa ripoti.”
Akamaliza Alfred senke mkuu wa jeshi la polisi.Kikao kikaendelea mpaka saa mbili za usiku na baada ya majadiliano marefu ikaonekana kuna kila ulazima wa kuongeza nguvu katika kumtafuta Tonny.

OFISI KUU ZA IDARA YA UJASUSI SAA TATU NA NUSU USIKU

Baada ya kumalizika kwa kikao na rais,Mr Meshack akamwamuru dereva wake aendeshe gari na kurejea tena ofisini.Safari ikawa ni ya kimya kimya.Hakuna aliyekuwa akiongea kitu.Mr Jumbo alikuwa amejawa na mawazo mengi juu ya kazi ngumu inayomkabili.Alikuwa akijaribu kutegua kitendawili cha jinsi Tonny anavyohusika na tukio lile,lakini akajikuta bado ndani ya fumbo kubwa.
Gari la Mr Jumbo likasimamishwa mita chache toka lilipo geti la kuingila katika ofisi hizo na askari wenye silaha waliokuwa wakifanya doria katika eneo hilo..Ulinzi ulikuwa mkali.Baada ya kujitambulisha akaruhusiwa kupita na kuingia ndani.Bado katika baadhi ya vyumba vya ofisi kulikuwa kukiwaka taa hivyo kuashiria kuwa bado watu walikuwa kazini.
Mzee Jumbo akapanda moja kwa moja kuelekea ofisni kwake.Vick katibu muhtasi wake bado alikuwa ofisini akiendelea na kazi.Mzee Jumbo alipoingia ofisini Vick akastuka kidogo kwa sababu alikuwa akisinzia .
“Vick! Bado uko ofisini mpaka saa hizi? Akasema Mr Jumbo
“Ndiyo mkurugenzi.Nimeamua nikusubiri hadi utakaporudi ili nijue kama kuna kazi yoyote ya kufanya kwa usiku huu” Vick akajibu kwa sauti ya uchovu.
“Vizuri sana Vick.Kuna habari yoyote mpya?
“Hakuna mkurugenzi” Vick akajibu
“Ok. Naomba watafute Catherine na David .nawahitaji haraka sana kabla ya saa tano za usiku wawe wamekwisha ripoti hapa.Kuna kazi muhimu wanatakiwa wafanye.

***************************************

Sikutaka dereva yule anifikishe nyumbani kwangu kabisa.Kwa sasa hivi sikuwa naamini mtu yeyote yule.Kutoroka kwangu kungelifanya idara yetu kutumia kila aina ya mbinu kunitafuta,na kunitia nguvuni,.Nikamuamuru dereva yule aniache mtaa wa pili toka nyumbani kwangu.akafanya kama nilivyomuamuru,akaniaga na kutokomea zake.
Nikaanza kutembea huku nikiwa katika tahadhari kubwa kueleka nyumbani kwangu.Watu niliokutana nao njiani walikuwa wakinishangaa kwa jinsi mkono ulivyokuwa umeloa damu.sikuwajali nikaongeza mwendo hadi kwangu.Moyo ukastuka baada ya kuliona geti liko wazi.Huwa si kawaida yangu kuliacha geti wazi namna ile.wakati naondoka nilikuwa nimelifunga.”Nani kalifungua na kuliacha hivi? Nikajiuliza. Geti hili ndugu msomaji huwa linafunguka kwa mtambo maalum .Yawezekana Monica alkalifungua halafu akashindwa kulifunga?.wazo la Monica kulifungua geti lile likafutika mara moja kwa sababu kwanza ni mgeni na hajui jinsi yoyote ile ya kulifungua.Nikajishika mfukoni na kuikuta bastora yangu bado ipo.Sijui ni kwa nini kila ninapohis jambo ambalo si la kawaida basi kitu cha kwanza kukiangalia huwa ni bastora yangu.Hii ndiyo ngao yangu na kinga yangu kwenye hatari yoyote.
Taratibu na kwa tahadhari ya aina yake nikajitoma ndani.Nikaangaza pande zote lakini sikuona dalili zozote za kuwepo mtu hapo nje.Mlango mkubwa wa kuingilia ndani nao ulikuwa wazi.Kwa kawaida huwa sina kawaida ya kuacha mlango wangu wowote wazi.Hii ikazidi kunipa wasi wasi .Nikaingia sebuleni na kwa sekunde kadhaa nikahisi kama vile niko ndotoni kwa mambo niliyoyakuta hapo .Vitu vilikuwa vimetupwa hovyo ,kila kitu kilikuwa kimepanguliwa.hakuna kitu ambacho hakikuwa kimeguswa.Nikatoa bastora yangu kwa haraka kwa sababu nilikwisha hisi mambo hayakuwa sawa.
“Monica”nikaita mara ya kwanza lakini hakuna aliyenijibu.Nikaita tena mara ya pili na ya tatu lakini sikujibiwa
“something is wrong here” Nikasema.
Kwa hatua za kunyata na kwa tahadhari kubwa nikaanza kuelekea katika chumba kile nilikomuacha Monica akifanya mawasiliano na ofisi zao.Nikakinyonga kitasa na kuufungua mlango.Ndani hakukuwa na mtu .Monica hakuwepo.Kijasho kikanitoka.Nusura nirukwe na akili baada ya kugundua kuwa Monica alikuwa ametoweka.Kwa hali ilivyoonyesha ilionekana kulifanyika upekuzi mkali mno katika chumba kile kwa sababu karibu kila kitu kilikuwa kimetupwa chini.Mezani kompyuta yangu ilikuwa imewashwa.Mapigo ya moyo yakastuka kwa sababu katika kompyuta ile ndimo nimehifadhi mambo yangu mengi ya kikazi.Nikajivuta na kuielekea. Niliomba Mungu ardhi ipasuke niingie ndani baada ya kukuta faili lenye kumbu kumbu zote za Abdool likiwa wazi.Lilikuwa limesomwa.Mwili ukaanza kunitetemeka .

USIKOSE SEHEMU IJAYO.........................
 
BRING BACK OUR GIRLS
SEHEMU YA 16
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Kwa hatua za kunyata na kwa tahadhari kubwa nikaanza kuelekea katika chumba kile nilikomuacha Monica akifanya mawasiliano na ofisi zao.Nikakinyonga kitasa na kuufungua mlango.Ndani hakukuwa na mtu .Monica hakuwepo.Kijasho kikanitoka.Nusura nirukwe na akili baada ya kugundua kuwa Monica alikuwa ametoweka.Kwa hali ilivyoonyesha ilionekana kulifanyika upekuzi mkali mno katika chumba kile kwa sababu karibu kila kitu kilikuwa kimetupwa chini.Mezani kompyuta yangu ilikuwa imewashwa.Mapigo ya moyo yakastuka kwa sababu katika kompyuta ile ndimo nimehifadhi mambo yangu mengi ya kikazi.Nikajivuta na kuielekea. Niliomba Mungu ardhi ipasuke niingie ndani baada ya kukuta faili lenye kumbu kumbu zote za Abdool likiwa wazi.Lilikuwa limesomwa.Mwili ukaanza kunitetemeka .

ENDELEA.................................

“My God” Ndilo neno pekee nililoweza kulitamka kwa wakati huo.Sikuwa nimetegemea kabisa kama iko siku kuna mtu anaweza akanifanyia kitu cha namna ile .Nilikuwa ni mtu niliyejiamini mno na mwenye uwezo wa juu lakini leo nilikuwa nimezidiwa akili.Mtu aliyefungua faili lile ni wazi alikuwa na utaalamu wa juu mno katika masuala ya mawasiliano ya kompyuta.Dakika kama tatu hivi zikapita nikiwa nimepigwa na bumbuwazi.Baadae akili yangu ikaanza kurudi na kunifanya nikubaliane na kilichokuwa kimetokea.
“Monica!! Nikasema
“Monica did this” Nikapiga meza kwa hasira.
“Why could I be so stupid and trust that woman? Nikajilaumu.
“Monica aliniokoa kule Arusha kumbe alikuwa na sababu zake.She only wanted this file.Alitaka tu kufahamu wapi alipo abdool.”
Hasira zikanipanda kupita kiasi.
“I will find you Monica.Iwill find you before you do anything” nIkasema
“Ni lazima nifanye kila linalowezekana ili kulizima jaribio hili la kumtorosha Abdool.I must fight hard” Nikasema huku nikiiendea friji na kutoa chupa ya mvinyo,nikamimina katika glasi na kuigugumia yote.Jeraha langu mkononi liliendelea kutoa damu .Nikarudi tena kule chumbani na kwa haraka nikachukua silaha na baadhi ya vitu vingine vidogo vidogo ambavyo niliona vingekuwa na msaada kwangu nikafunga milango ya nyumba na kuwapigia kampuni ya ulinzi simu kuwa watume walinzi wao kuja kunilindia nyumba yangu hadi hapo nitakapokuwa nimerudi.
“Today will be a very long day” Nikasema huku nikiingia gereji kwangu na kuungia katika gari jipya kabisa amabo nilikuwa nimepanga kumtumia mdogo wangu Lisa aliyehitimu shahada yake ya kwanza hivi karibuni.Sikutaka kutumia gari langu la kwaida kwa kuogoa kuwa linafahamika na kwa sasa hivi niwazi nitakuwa nikitafutwa .kwa mwendo wa kasi nikaondoka hapo nyumbani.
“I must find you Monica.Lazima nikuonyeshe kazi.Nitakupata tu ukiwa mzima au maiti” Nikasema kwa hasira.Mpaka hapa nilikwisha amini kuwa Monica alikuwa na ajenda ya siri ya kuwa karibu nami kwa lengo moja tu la kujua alipo gaidi abdool.Niliendelea kujilaumu kwa kumuamini Monica kiasi kile kiasi cha kumuacha katika chumba changui cha siri ambacho kwa kawaida huwa haingii mtu yeyote.Mawazoni nikajua kuwa Monica ameamua kufanya vile ili CIA wawahi kumchukua Abdool kabla magaidi wa alqaeda hawajafanya hivyo.
“No hawawezi fanya hivyo,huu si utaratibu na ni lazima nisimamishe mpango wao” nikajisemea mwenyewe.
Nilikuwa nikielekea nyumbani kwa rafiki angu mmoja wa kike aitwaye Rose.Huyu amekuwa ni rafiki yangu wa siku nyingi .Rose aliwahi kuwa mpenzi wangu siku za nyuma lakini baadae alikuja kupata mchuma wa kizungu aishiye nje ya nchi na akaachana nami.Baada ya kurejea nchini toka Ulaya tukarudisha uhusiano wetu japokuwa wote tunafahamu kuwa yupo katika mahusiano na mtu mwingine.Mara nyingi niwapo katika kazi zangu nimekuwa nikipata maficho kwake.Rose yeye ni muuguzi na ana zahanati yake biafsi si mbali sana na mahala anapoishi.
Safari iliendelea huku bado nikijaribu kutafakari kwa kina tukio zima lililotokea.Bado sikuwa na jbu la uhakika nini kusudio la Monica.Kilichonila akili ni jinsi kazi yangu itakavyokuwa ngumu kwa sababu tayari serikali inajua kuwa mimi ninahusika katika mauaji ya arusha.Kutoroka kwangu mchana wa leo kumewapa uhakika kuwa ni kweli kuna kitu kinachoendelea.Hii itawafanya waelekeze nguvu nyingi katika kunitafuta na hivyo kuifanya kazi yangu kuwa ngumu sana.lakini vyovyote itakavyokuwa ni lazima niuzime mpango wowote wa kumteka Abdool.
Sura ya Monica ikanijia tena akilini.Nikajiuliza tena aliko binti huyu mwenye uzuri wa kimalaika.Nikavuta picha ya matukio yote kuanzia tuko arusha mpaka tunafika Dar.Monica ameniokoa katka shambulio la Arusha na ndiye aliyenipa kwa undani siri ya mpango mzima wa magaidi.Iweje leo aigeuke wakati tumeianza kazi pamoja? Lakini kama hajanisaliti yuko wapi? Kila nikifika hapa nashinwa kupata jibu.Yawezekana akwa ametekwa nyara na magaidi?Taratibu nikaanza kuunganisha picha niliyoiona mle ndani kwangu na kupata picha halisi.Kuanzia kukuta geti liko wazi,vitu kupanguliwa hovyo nyumba nzima,.Yawezekana ikawa kuna watu walivamia nyumba yangu na kufanya kitendo kile.Na kama ni hivyo basi ni wazi ni watu toka katika ofisi yetu.kwa sababu nimeingia hapa dar kwa siri kubwa na waliokuwa wakijua kuwa niko hapa Dar ni ofisi yetu pekee.”Yah ! sasa naanza kupata picha.Ni lazima watakuwa wamemchukua Monica..


****************

Vivian Mdogo wake Rose ndiye aliyefungua geti.Kwa kuwa gari nilimokuwamo lilikuwa na vioo vyeusi Vivi hakuweza kunitambua mara moja hadi niliposhuka.Alipigwa na butwaa kwa kuniona jinsi nilivyosawajika.Haraka haraka akakimbia ndani na kumuita dada yake.Rose alipopata taarifa ya ujio wangu naye akatoka ndani mbio.
“What happened dear?akaniuliza Rose kwa mshangao huku machozi yakimlenga lenga
“Nini kimetokea dear? Akauliza tena Rose huku akinishika mkono na kuongoza ndani.Bil akupoteza muda akanipeleka bafuni akanitoa nguo na kuanza kunisafisha jereha langu la mkononi na sehemu zote nilizokuwa nimechubuka..Kisha oga akachukua kalabrasha la dawa na kuniganga halafu akanichoma sindano na kunilaza kitandani,akanifunika shuka na kunitaka nilale.Rose alinionyesha mapenzi makubwa siku hii ya leo.Kwa dakika kadhaa nikajaribu kutafakari kazi inayonikabili,mara nikahisi macho yanakuwa mazito nikalala.

*********************

Niliamka toka usingizini saa tatu za usiku.Rose alikuwa pemBeni yangu akisoma kitabu.
“:How do you feel dear? Akaniuliza
“I’m ok” Nikajibu huku nikijinyoosha,nikajiinua na kuketi kitandani..Rose akanikaribia na kunibusu shavuni.
“You’ll be ok my love” akanong’ona
Rose akanishika mkono na kunikalisha katika sofa lililokuwamo humo chumbani kisha akafunua kawa lililokuwa mezani na kunikaribisha chakula .Sikuwa na hamu ya kula chakula chochote nafikiri hata Rose alilitambua hilo ,akachukua jukumu la kunilisha .Nilipomaliza kula Rose akanirudisha tena kitandani kupumzika.Nilijilaza chali nikaanza kutafakari jinsi nitakavyoianza kazi iliyoko mbele yangu.Bado nilikuwa gizani,sikujua ningeanza vipi kazi ile bila msaada ambao sikujua ningeupata vipi kwa sababu mpaka sasa hivi nilikuwa natafutwa kwa udi na uvumba.Monica ambaye alionekana kuwa msaada kwangu ametoroka akiwa na siri zangu nyingi.
“Pamoja na hayo yote nahitaji kujua kinachoendelea ofisini kwetu.nahitaji kufahamu kila hatua inayofikiwa katika kunitafuta.Ni kwa njia hiyo pekee nitaweza kuvikwepa vizingiti vyote vinavyowekwa.Lakini ni nani pale ofisini ambaye anaweza kushirikiana nami katika kazi hii? Nikajiuliza bila kupata jibu..Nikamfikiria Vick katibu muhtasi wa mkurugenzi lakini nikaogopa kumshirikisha mtoto kama yule katika operesheni hii kwani kwa kufanya hivyo ningekuwa nahataraisha maisha yake.Mara ikaja sura ya David,kijana ambaye ni mtiifu na mchapa kazi hodari.Ni hivi majuzi amenza kazi katika idara yetu na mimi ndiye niliyekuwa namfundisha jinsi ya kufanya kazi.
“Nitamtumia David.He’s very royal to me.He wont fail me”
Nikatabasamu .
*******************

Catherine na David ni baadhi tu ya vijana wapya walioanza kazi katika idara yetu amhivi karibuni na ambao wameonyesha uwezo mkubwa katika kazi.
Catherine Bhoke msichana mrefu ,mwenye umbo la kuvutia lililosanifiwa na rangi nyeusi inayong’ara alizaliwa mkoani Mara miaka ishirini na tisa iliyopita akiwa ni mtoto wa mwisho katika familia yao ya watoto wanne.Alipata elimu ya msingi mkoani Mara na baadae akajiunga na shule ya ya sekondari ya wasichana Tabora na baada ya hapo akaendelea na elimu ya sekondari katika shule ya sekondari Msalato na baadae akajiunga na chuo kikuu cha Dar es laam kitivo cha sheria..Baada ya kuhitimu shahada yake ya kwanza ya sheria ,Catherine akachaguliwa kujiunga na jeshi la wananchi kwa mafunzo ya kijeshi wakati akiandaliwa kwenda kuchukua mafunzo ya awali ya ujasusi.Baada ya kuhitimu mafunzo ya kijehsi ,bila kupoteza wakati akajiunga na mafunzo ya ujasusi nchini China halafu akaenda tena nchini Isarel na akamalizia mafunzo yake nchini marekani.Kisha maliza mafunzo yake akarejea nchini na kuanza kazi katika idara yetu.Kwa muda mfupi aliokaa ameonyesha ukomavu wa hali ya juu kiasi cha kuaminiwa.
Davidi chitende mzaliwa wa Mwanza alikuwa na umri wa miaka thelathini na moja.David kijana mkakamavu na mwenye umbo lililojengeka vyema alihitimu elimu ya sekondari kidato cha sita katika sule ya sekondari Tosamaganga Iringa na kujiunga na chuo kikuu cha makerere Uganda kwa masomo ya sayansi ya siasa.Kisha maliza akaendelea masomo ya saikolojia nchni Ubelgiji na halafu akajiunga na mafunzo ya awali ya ujasusi ambayo aliyapata katika nchi ya Ujerumani na baadae nchini China ambako alihitimu vyema.Ukomavu wa david ulidhihirika pale alipofanikiwa kuwadhibiti watekaji nyara sita waliokuwa wameiteka ndege ya shirika la ndege la afrika kusini ambayo David alikuwamo ndani yake.David alifanikiwa kuwadhibiti watekaji hao hali akiwa hana silaha yoyote.Hii ilimjrngeaa umaarufu na kumfanya we ni mmoja kati ya watu wa juu kabisa idarani kwetu.

************************

“Ahsanteni sana vijana kwa kuitikia wito huu wa haraka” alianza mazungumzo mkurugenzi wa S.I.S Mr meshack Jumbo baada ya Catherine na David kuwasili ofisini kwake usiku huo.
“sipendi kupoteza muda ,naomba moja kwa moja nijielekeze katika kile nilichowaitia usiku huu”
“nafikiri nyote mnafahamu kitu kinachoendelea hvi sasa hapa nchini.kwa kuongezea tu ni kwamba uchunguzi wa tukio lillotokea arusha siku mbili zilizopita unaonyesha kuwa Visto 01 au Tonny,mmoja kati ya wafanyakazi wa idara yetu anahusika kwa kiasi kikubwa katika tukio hilo.Bado haijajulikana anahusika vipi lakini mpaka sasa yeye ndiye mtu pekee ambaye anashukiwa na vyombo vya usalama kuhusika katika shambulio lile.Leo mchana tulipata taarifa kuwa alikuwa akirejea jijini Dar akitokea Moshi.Tulituma ujumbe wa kumtaka akifika hapa dar aripoti ofisini haraka iwezekanavyo ambako tulikuwa tayari tuimeandaa mteg owa kumtia nguvuni.Kwa bahati mbaya hatukuweza kufanikiwa zoezi hilo kwani Tonny alifanikiwa kutoroka kwa namna ya ajabu kabisa.Kijana yule ni hatari .Kumuacha aendelee kuwa huru ni kuhatarisha usalama wa taifa letu.Mpaka sasa bado hatujapata taarifa zozote zinazoweza kutupa mwanga wapi alipo Tonny.Ili kutegua kitendawili cha nani alifanya na nini kusudio la mashambulio yale ya mabomu arusha yatubidi tumpate Tonny kwa jinsi yoyote ile akiwa hai.Ulinzi umeimarishwa kila kona na msako mkali unaendelea jijini dar ambako bado inasadikiwa Tonny amejificha.Serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetupa sisi jukumu zito la kuhakikisha ndani ya muda mfupi ujao Tonny anatiwa nguvuni.Kwa mantiki hiyo basi nimewaita usiku huu ili kuwapa kazi ya kumtafuta Tonny na kumkamata akiwa hai.”
Catherine na David wakaonyesha mstuko wa dhahiri kwa jukumu lile walilopewa.Wote walimfahamu Tonny ni mtu wa nanma gani na hivyo kuambiwa kuwa wakamsake na kumkamata ni kujipeleka wenyewe katika mdomo wa mamba.
“Kumtafuta mtu kama Tonny ni kazi ngumu naelewa lakini hamtakuwa peke yenu.Kebby na Robin watarejea kesho toka Zimbabwe na kesho kutwa mtakuwa nao.Isitoshe Moris na Joe pia wataungana nanyi baada ya siku mbili.Vile vile naomba mfahamu kuwa tuna ushirikiano mkubwa sana na jeshi la polisi na vyombo vingine vyote vya usalama wa nchi..Wenzetu wa polisi nao wanaendelea na operesheni kama hii na mtakuwa mkishirikiana na kupeana taarifa.muda wowote mtakaohitaji msaada wowote wa jeshi la polisi basi msisite kusema na mtapewa.Nadhani mpaka hapo nyote mmekwisha elewa nini mnachotakiwa kufanya.Nikitoka hapa nitakuwa nyumbani kwangu na ninataka kupata ripoti kila baada ya masaa matatu.Kuna yeyote mwenye duku duku au swali?
Kimya cha sekunde kadhaa kikapita na David akauliza swali.
”Mkurugenzi ,je hakuna taarifa zozote za kiintelijensia zinazoweza kutupa japo mwanga wowote kuhusu mahala pa kuanzia?
“Mpaka hivi sasa hakuna taarifa yoyote inayoonesha ni wapi Tonny anaweza kuwa amejificha.Nyumbani kwake kumekutwa walinzi wa kampuni binafsi ya ulinzi wanalinda na kwa mujibu wa maelezo waliyoyatoa ni kwamba wamepewa taarifa na wakubwa zao kuwa waende wakailinde ile nyumba.Polisi walifanikiwa kuingia ndani ya nyumba yake ili kuangalia kama kuna chochote kinachoweza kuwasaidia kupata walau fununu za mahala anakoweza kuwa amejificha Tonny lakini hawakuweza kupata kitu chochote.Nyumba yote ilikuwa imevurugwa hovyo hovyo.Lakini bado tuna matumaini makubwa kuwa bado Tonny yuko jijini Dar”
“Ok tumekuelewa mkurugenzi na tuko tayari kulitekeleza jukumu hili zito la kumtafuta Tonny.na tutakuwa tukikupa taarifa ya kila hatua tunayoifikia.”
David akasema kisha wakaagana na mkurugenzi wakatoka kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa jukumu la kumtafuta Tonny.


TUKUTANE TENA SEHEMU IJAYO……………………….
 
BRING BACKOUR GIRLS
SEHEMU YA 17
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Kimya cha sekunde kadhaa kikapita na David akauliza swali.
”Mkurugenzi ,je hakuna taarifa zozote za kiintelijensia zinazoweza kutupa japo mwanga wowote kuhusu mahala pa kuanzia?
“Mpaka hivi sasa hakuna taarifa yoyote inayoonesha ni wapi Tonny anaweza kuwa amejificha.Nyumbani kwake kumekutwa walinzi wa kampuni binafsi ya ulinzi wanalinda na kwa mujibu wa maelezo waliyoyatoa ni kwamba wamepewa taarifa na wakubwa zao kuwa waende wakailinde ile nyumba.Polisi walifanikiwa kuingia ndani ya nyumba yake ili kuangalia kama kuna chochote kinachoweza kuwasaidia kupata walau fununu za mahala anakoweza kuwa amejificha Tonny lakini hawakuweza kupata kitu chochote.Nyumba yote ilikuwa imevurugwa hovyo hovyo.Lakini bado tuna matumaini makubwa kuwa bado Tonny yuko jijini Dar”
“Ok tumekuelewa mkurugenzi na tuko tayari kulitekeleza jukumu hili zito la kumtafuta Tonny.na tutakuwa tukikupa taarifa ya kila hatua tunayoifikia.”
David akasema kisha wakaagana na mkurugenzi wakatoka kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa jukumu la kumtafuta Tonny.

ENDELEA………………………..

Nilistuka toka usingizini na kuangalia saa.Ilikuwa ni saa sita na dakika kumi na nane.Nilijaribu kuinua kichwa lakini kilikuwa kizito mno isitoshe nilihisi maumivu makali sana .Niliutazama mshale wa saa ulivyokuwa ukijisogeza taratibu,na sasa ilikuwa ni saa sita na dakika ishirini na sita.Nilijikaza nikainuka na kuchukua simu ya Rose iliyokuwa karibu.Rose alikuwa katika usingizi mzito.Nazifahamu namba za simu za David nikaziandika na kupiga.Simu ikaita kwa sekunde chache halafu ikapokelewa.
“hallow” Ilikuwa ni sauti ya upande wa pili ambayo niliitambua kuwa ilikuwa ya David.
“hallow David,Tonny anaongea hapa”
Kimya kidogo kikatanda ,nahisi David alistuka baada ya kusikia kuwa anayeongea simuni ni mimi.Hakuwa ametegemea kama ningeweza kumpigia simu kwa muda kama ule.
“Tonny ,uko wapi kaka? Pole sana kwa matatizo” akasema David kwa sauti ambayo niliweza kung’amua mara mja kuwa ilibadilika ghafla na kuwa ya wasi wasi mwingi.
“Nimerudi Dar toka jana .Nilipatwa na matatizo kidogo.”Nikasema
“nilisikia ulipatwa na matatizo Tonny.Pole sana.”
“ahsante sana David.Uko wapi kwa sasa?
“kwa sasa ninaelekea nyumbani kwangu”
“ david ninaomba tuonane usiku huu nina shida na wewe kubwa sana.Kwa sasa ni saa sita na nusu naomba kabla ya saa saba kamili tuwe tumeonana.fanya juu chini tukutane Afrique Casino kaunta C”
“Sawa Tony,naelekea huko sasa hivi” akajibu kwa sauti iliyojaa uoga.Nikakata simu na nilipogeuka nikamkuta Rose ameamka ananiangalia kwa macho makali.
“mwanaume usiye na haya wewe! Hiyo ni mikutano gani tena ya saa saba za usiku wakati hali yako unaiona si nzuri? Akasema Rose kwa ukali
“Usiogope Rose ni masuala ya kikazi tu”
“kazi gani hizo za usiku wa manane?Wakati watu wamelala nyie mnafanya kazi,kazi gani hizo? Mnawanga? Sitaki kusikia upuuzi wako Tonny.Kwanza nitaaminije kuwa ni masuala ya kikazi na si miadi na hao wanawake wako walio kila pande za jiji?
Rose akasema kwa hasira
Sikumlaumu Rose kwa sababu hakujua kitu gani kilichokuwa kikiendelea.Zaidi ya yote hakujua kama mimi ninafanya kazi katika idara ya ujasusi
Sikumjibu kitu kwa sababu tayari alikwisha kasirika na hivyo kumjibu lolote kungemuongezea hasira mara dufu kitu ambacho sikutaka kitokee.Taratibu nikaamka na kufungua kabati.Nikachukua suruali ya Jeans na fulana nikavaa,.Rose akainuka na kunifuata.
“Sorry baby,I have to go”Nikasema
“You wont go Tonny.Please stay”
“Please Rose .nakuahidi baada ya kazi hii kuisha nitakuja kwako na kukaa mwezi au miwili au hata mwaka ukitaka lakini tonight let me go please.I have to do this.”
Rose machozi yalikuwa yakimdondoka,sikumjali nikachukua kibegi changu kidogo cha kazi klichokuwa na zana mbali mbali nikafungua mlango na kuondoka.


********************
Afrique casino ni moja kati ya kasino mpya kabisa na za kisasa kuwahi kutokea jijini Dar.Kasino hii ilikuwa imejengwa kati kati kabisa ya jiji .Kwa muda wa masaa ishirini na manne kasino hili lilikuwa limesheheni watu lukuki.Hiki ndio kitovu cha burudani za aina zote,hakukuwa na starehe ambayo ungeikosa ndani ya jumba hili ambalo wenyewe wapenda starehe waliliita kama Africa paradise wakiwa na maana ya bustani nzuri na ya kupendeza .Ukiwa ndani ya jumba hili hutatamani kuondoka kwa sababu kuna kila kitu unachokihitaji,.Mara nyingi huwa napenda kuja hapa kutuliza mawazo na kukutana na watu mbali mbali.Pamoja na starehe zote kuwamo humu lakini pia kulikuwa na uchafu wa kila aina.Biashara ya ngono ,dawa za kulevya vilikuwa ni vitu vya kawaida..
Nilipaki gari maegesho na kutazama pande zote kuhakiki usalama wangu na kisha nikaingia ndani ya jumba hili.Kwa jinsi watu walivyokuwa wengi ndani ya jumba hili ni vigumu sana kubainika hata kama unatafutwa .Nilifululiza moja kwa moja mpaka sehemu ambayo nilipanga nikutane na David,.nikakaa katika kona ya kaunta sehemu iliyokuwa na mwanga hafifu ili niweze kumuona kila ajaye upande ule.Niliitupia macho saa kubwa iliyokuwa pale kaunta ilionyesha ni saa saba na na dakika ishirini na mbili.
Niliendelea kumsubiri David huku nikipitisha macho kwa warembo kadhaa waliokuwa karibu yangu wakiwa wamevaa nusu utupu.Mara moja sura ya Monica ikanijia tena kichwani,nikasikia uchungu mwingi kwa kitendo alichonifanyia binti huyu.Kwa mbali nikamwona David akiangaza angaza,nikamfanyia Ishara,akaniona.Akaja kule nilikokuwa kwa haraka.Tulisalimiana ,nikamwagizia kinywaji.Tukakaa kimya kwa sekunde kadhaa kisha david akasema
“Ndiyo Tonny leta habari”
“habari si nzuri david kama ulivyosikia.Pamoja na hayo napenda kwanza nikushukuru kwa kukubali kuonana nami usiku huu..Ni kutokana na habari hizo kuwa mbaya ndio maana nimekuita kwa ajili ya kuongea mawili matatu .”
Nilivuta pumzi nikanywa funda la mvinyo .David akanitazama kisha akasema
“ Tonny hata mimi nilistuka sana niliposikia mambo yaliyokupata.Nimefurahi sana kwa kuniamini na kuona ninafaa kwa kipindi kama hiki kukaa na kujadili nawe mambo mawili matatu.Pili kabla hujanieleza kile ulichoniitia,nimeng’amua unaweza kuwa na jambo zito na la maana kubwa, na kwa mantiki hiyo sidhani kama hapa panafaa kuongelea suala lolote la kikazi.Nadhani ingekuwa vizuri kama tungeenda kuongelea katika gari langu hapo nje au sehemu yoyote nyingine.”
Akasema david huku akiangaza angaza pande zote kana kwamba kuna mtu alikuwa akimtafuta.Kwa jinsi nilivyomsoma kwa haraka haraka alionekana ni mtu mwenye wasi wasi mwingi.Sikumtilia maanani sana,nikamfanyia ishara tukainuka na kutoka nje kuelekea mahala alikopaki gari lake.
Tulipolifikia gari lake akanifungulia mlango wa mbele nikajitoma ndani naye akaingia akaliwasha na taratibu tukaanza kuondoka maeneo hayo ya afrique casino.Nilishangaa kwa kitendo kile cha kuliwasha gari na kuliondoa hapo kasino kwa sababu hatukuwa tumeelewana kuwa tuende mahalikokote kwingine.Mwazoni nikafikiri kuwa labda ameona ni busara kama tungetoka kabisa nje ya jingo hili.Tukiwa katika mzunguko wa kuondokea hapo kasino taratibu nikaiskia kitu cha baridi kinanigusa shingo.Nilitaka kugeuka lakini nikasikia sauti kali ya mwanamke ikiniamuru
“Hivyohivyo ulivyo,usijaribu kugeuka”
Nywele zikanisimama.Sikutaka kuumiza kichwa kung’amua kuwa nilikuwa nimekamatwa.Kumbe David alikuwa ameweka mtego.
“Damn you David” Nikasema moyoni kwa hasira.
Kama vile mtu aliyeamriwa David akakanyaga mafuta na gari ikaondoka mithili ya ndege inayotaka kupaa.Hii ilitosha kabisa kunidhihirishia kuwa huu ulikuwa ni mpango uliosukwa na David ili kunikamata.Kukamatwa kirahisi namna hii kulinipa shida sana.Kama kawaida akili yangu ikaanza kufanya kazi haraka haraka ni jinsi gani ningeweza kujitoa mikononi mwa david na huyo mwenzake.Sikuamini kama David anaweza akanifanyia kitendio kama kile kutokana na jinsi nilivyokuwa nikimuamini.Kwa upande mwingine sikumlaumu sana David kwa sababu alikuwa kazini na ninajua alifanya kitendo kwa kutekeleza amri ya wakuu wake.wa kazi.
Sauti iliyokuwa nyuma yangu haikuwa ngeni sana masikioni mwangu.ni sauti ambayo nimewahi kusikia ,ni sauiti ambayo niliifananisha na sauti ya mtu Fulani ambaye si mgeni kwangu.”Lakini hii inaweza kuwa sauti ya nani? Nilibaki nikijiuliza bila kupata jibu.Tofauti na sauti ile niliyoizoea hii ilikuwa nzito kidogo na yenye mkwaruzo.
“Mpaka hapa hakuna mtu yeyote ninayepaswa kumuamini kwa sasa..Hakuna mtu yeyiote anayeweza kunisaidia.Watu wote wameamini kuwa ninahusika na milipuko ya Arusha na kila mmoja anajitahidi anitie nguvuni.Isiwe taabu,I’ll fight on my own” Nikajisemea moyoni huku nikijaribu kuangalia kama ninaweza kupata mwanya wowote wa kuweza kujiokoa.
Bastora mbili zilikuwa kichwani kwangu.Sikutakiwa hata kugeuza shingo yangu,kwa sababu kitendo hicho kingenisbabaishia matatizo makubwa.Siku zote mtu akikuelekezea bastora ni lazima uwe mpole na mtii kwa sababu tayari dhamira ya kuua iko moyoni mwake hivyo ukimletea shida anaweza akakuua muda wowote ule.
Gari lilikuwa likenda kwa kasi ya ajabu.Sikujua walikuwa wakielekea wapi.Sikuamini kama David angeweza kuwa dereva mzuri kiasi kile.Dakika kama ishirini baadae toka tuondoke pale afrique kasino ,gari likakata kulia na kuanza kuelekea kituo cha kati cha polisi.Akili yangu ikafanya kazi haraka haraka nikang’gamua kuwa walikuwa wakinipeleka kituoni.Kufikishwa polisi kungeharibu na kutibua mpango mzima.Sikutaka jambo kama hilo linitokee na hapo nikafanya jambo ambalo hakuna aliyelitegemea.
Kama umeme nikainua mkono wangu wa kushoto na kumpiga David ngumi kali sana ya uso inayomfanya aone nyota na kupoteza uelekeo.Akiwa bado katika taharuki ,kufumba na kumbua nikageuka na kumpiga yule mtu wa nnyuma aliyekuwa ameniwekea bastora kichwani ngumi nzito inayomfanya aanguke katika kiti.kwa haraka nikamkusanya shati lake,nikamvutia kwangu na kumpiga kichwa kizito kinachompoteza fahamu.gari ilikuwa ikiserereka kuelekea pemBeni kutokana na mwendo mkali lililokuwa likienda.Bado David alikuwa akicheza na usukani ili kuliepusha gari lisiweze kugonga miti iliyokuwa pemBeni ya barabara.Lengo lake lilikuwa ni kuwahi kufika pale polisi.Sikumkawiza nikampa kichwa kizito sana kinachomfanya aachie usukani na kutoa yowe la uchungu.Nikaushika usukani halafu nikaupenyeza mguu na kukanyaga pedeli ya breki na gari ikasimama huku matairi yakilalama kwa ukelele mkubwa.Kwa kasi ya ajabu nikaufungua mlango na kumpiga David teke kali la mbavu linalomtoa nje .Sikuwa na imani kama mbavu zake zilikuwa salama kutokana na uzito wa teke lile.Nikaukalia usukani na kuligeuza gari ,nikaliweka kati kati ya barabara na kuondoka kwa mwendo mkali .Kwa mara nyingine tena nilikuwa nimefanikiwa kulizima shambulio la kunikamata.
Nikiwa katika mwendo mkali ,pamoja na mateka wangu nyuma ya gari nilikuwa nikigeuka mara kwa mara na kuangalia kama nilikuwa nikifuatiliwa.Kitendo nilichokifanya pale mbele ya kituo cha polisi ni lazima kingezua udadisi na kuwafanya waanze kunifuatilia.
Kwa wakati huu nilihitaji kupata mahala ambako ningefanya ofisi ya muda kwa sababu sikuwa na sehemu yoyote yenye usalama ambayo ingeniwezesha kufanya kazi zangu kwa amani bila kuwa na wasi wowote wa kufuatiliwa na vyombo vya usalama.Mateka wangu niliyekuwa naye ndani ya gari nilitegemea ni lazima angenisaidia kupata taarifa muhimu nilizozihitaji kwa maaana hiyo nilihitaji kupata sehemu nzuri yenye utulivu ambayo ningeitumia kumuhifadhi na kumuhoji.Nilifikiria kwenda tena kwa Rose lakini nikalifuta wazo hilo haraka.Wanawake si watu wa kuwaamini hata kidogo katika shughuli hatari kama hizi.Nimekwisha jifunza toka kwa Monica.Ningeweza kwenda nyumbani kwangu lakini kwa sasa hapaingiliki na nina imani lazima ofisi yetu na jeshi la polisi watakuwa wameweka ulinzi ili nikijitokeza tu wanikamate.Sikupendelea vile vile kwenda katika nyumba za kulala wageni kwa sababu si sehemu muafaka kwa kazi hii na isitoshe kwa hivi sasa kutakuwa na msako mkali sana wa kunitafuta katika nyumba zote za wageni.Nilichekecha akili na hatimaye nikapata jibu.Afrique Casino.Nitaweka makazi ya muda pale.Sehemu ili ni sehemu yenye umati wa watu kwa masaa ishirini na manne na ni sehemu ya starehe na hivyo hawawezi kamwe kufikiri kuwa ninaweza kwenda kujificha pale.Katika kasino hii kulikuwa na vyumba vya kulala ambavyo gharama yake ilikuwa ya juu mno.Katika kibegi changu kidogo kilichokuwa na zana zangu za kazi kulikuwa na kiasi cha shilingi laki saba nlizozichukua nyumbani kwa ajili ya kunisaidia pale itakapobidi.Kadhia kama hizi mara nyingi huwa zinahitaji pesa ya kutosha.
Haikunichukua muda mrefu kufika Afrique Casino.Nilipaki gari maegesho na kumgeukia mateka wangu ambaye bado alikuwa hajapata fahamu.Nikainama ili kumtazama vizuri na kujua hali yake.Lo ! Nikakapatwa na mshangao mkubwa.Mateka wangu alikuwa ni Catherine Bhoke.Nilitabasamu huku nikimhurumia binti yule kwa kitendo alichokifanya kwa sababu kilihatarisha maisha yake.Ningeweza hata kumuua mwenzangu bila kujua.Pamoja na kumhurumia nilimsifu vile vile kwa kuwa na ujasiri wa kuamua kupambana na mimi..
Niliziokota bastora zake mbili zilizoanguka pemBeni yake nikazifutika kiunoni nikambeba na kuingia naye ndani.Nilisimama sehemu ya mapokezi na mateka wangu akiwa begani,Hapo mapokezi kulikuwa na mwanadada mmoja aliyeonyesha kuwa alikuwa akisinzia.Nilikodisha chumba kikubwa ambacho thamani yake ilikuwa dola mia moja kwa usiku mmoja.Chumba hiki kilikuwa ghorofa ya juu kabisa.Mimi na mateka wangu begani tukapanda lifti hadi ghorofa ya juu kilipo chumba nilichokodisha.Kila niliyekutana naye aliamini kuwa binti yule alikuwa amezidiwa na kilevi.haikunichukua muda mrefu kukipata chumba kile namba 364 R.Niifungua mlango na kujitoma ndani.Nilipapasa ukutani na kuwasha taa.Chumba kilikuwa kikubwa na kizuri.Kulikuwa na kitanda cha futi sita,sofa nzuri,televisheni,friji n.k.Nilimlaza Catherine katika sofa na kuanza kukikagua chumba chote..Niliporidhika na usalama wa chumba kile nikawasha kiyoyozi ili kuipooza hali ya hewa mle chumbani.Dakika kama saba hivi toka tuingie mle chumbani Catherine akafumbua macho taratibu.Akazungusha macho ili kutambua mahala alipo.
“Hallo Catherine” Nikasema huku nikitabasamu.
Hakunijibu kitu badala yake akakunja uso kwa hasira.
Tulibaki tumetazamana na Catherine kwa takribani dakika kumi hivi,nikahisi Catherine ameanza kuogopa.Niliinuka pale nilipokuwa nimekaa ,nikatoa bastora zile mbili za Catherine na kumpatia.
“bastora zako hizo Cathe.Mimi sizihitaji.Wakati mwingine ukitumwa kazi unatakiwa uwe makini sana.” Nilisema huku Catherine akiniangalia kwa mshangao mkubwa wa kutokuamini.
Nilimwangalia Catherine kwa macho makali halafu nikamwambia
“Sikiliza kate.Nataka unipe ukweli.Ni ukweli huo tu ninaoutaka ndio utakaotuweka wewe na mimi salama.Iwapo utanidanganya au kutokunipa ushirikiano wa kutosha basi mambo yatakuwa magumu na nitakulaumu sana katika maisha yangu yote”
Cathe akanitazama kwa makini na kwa mara ya kwanza toka amefika mle chumbani akasema
‘” Ni mambo gani unataka kujua na kwa nini useme mimi na wewe tuko hatarini?
“Vizuri Catherine.usiwe na haraka utafahamu kila kitu ,muhimu naomba ushirikiano wako wa dhati kabisa.Kitu cha kwanza ninachotaka kufahamu nini lilikuwa kusudio la kutumwa mnikamate?
Catherine akaniangalia kwa macho yake makubwa halafu akasema
“Sikiliza Tonny,usinidanganye kuwa hujui ni kwa nini unatafutwa .Serikali na Umma wote wa Tanzania wanafahamu kuwa wewe ndiye mtuhumiwa namba moja wa mauaji ya Arusha.Serikali inakutafuta kwa nguvu zote.Na wala usijidanganye kuwa huwezi kupatikana.Nina uhakika siku ya leo haitaweza kuisha kabla haujatiwa nguvuni.”
Catherine akasema kwa kujiamini.Alikuwa akijiamini kupita kiasi .
“naelewa hilo Catherine.Je mna taarifa zozote ni jinsi gani ninahusika na mlipuko wa Arusha? Nikauliza tena.
“Si kazi yangu mimi kujua ni jinsi gani unahusika na tukio la arusha.Kazi yangu mimi ni kuhakikisha unatiwa nguvuni haraka iwezekanavyo.” Cathe akasema kwa ukali.Sikutaka kuendelea kumuuliza kitu chochote nikasubiri hadi hasira zake zipungue.
TUKUTANE SEHEMU IJAYO…………..
 
BRING BACK OUR GIRLS

SEHEMU YA 18

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“Vizuri Catherine.usiwe na haraka utafahamu kila kitu ,muhimu naomba ushirikiano wako wa dhati kabisa.Kitu cha kwanza ninachotaka kufahamu nini lilikuwa kusudio la kutumwa mnikamate?
Catherine akaniangalia kwa macho yake makubwa halafu akasema
“Sikiliza Tonny,usinidanganye kuwa hujui ni kwa nini unatafutwa .Serikali na Umma wote wa Tanzania wanafahamu kuwa wewe ndiye mtuhumiwa namba moja wa mauaji ya Arusha.Serikali inakutafuta kwa nguvu zote.Na wala usijidanganye kuwa huwezi kupatikana.Nina uhakika siku ya leo haitaweza kuisha kabla haujatiwa nguvuni.”
Catherine akasema kwa kujiamini.Alikuwa akijiamini kupita kiasi .
“naelewa hilo Catherine.Je mna taarifa zozote ni jinsi gani ninahusika na mlipuko wa Arusha? Nikauliza tena.
“Si kazi yangu mimi kujua ni jinsi gani unahusika na tukio la arusha.Kazi yangu mimi ni kuhakikisha unatiwa nguvuni haraka iwezekanavyo.” Cathe akasema kwa ukali.Sikutaka kuendelea kumuuliza kitu chochote nikasubiri hadi hasira zake zipungue.

ENDELEA………………………..
“Catherine nimekuelewa vizuri ,sasa naomba unisikilize kwa makini.”
Nikamtazama Cathe na kumuona amekaa akinisikiliza kwa makini.
“Ni kweli ninahusika na tukio lililotokea arusha.Katika tukio lile mimi ndiye nilikuwa mlengwa mkubwa.Nilikuwa nikitafutwa na mtandao wa Alqaeda.Nilikuwa nikifuatiliwa toka Dar es salaam hadi nikiwa arusha.Kwa kutumia teknolojia za hali ya juu waliweza kujua kila nilichokuwa nikikifanya na hivyo walitambua uwepo wangu pale katika ile klabu iliyolipuliwa na bomu.” Nikatulia na kumuangalia Catherine
“alqaeda? “ akauliza kwa mshangao
“Yes alqaeda” Nikajibu.
“Hawa ndio waliofanya shambulio lile la Arusha.Shambulio lile lilikuwa na lengo la kuvipoteza mwelekeo vyombo vyote vya ulinzi na usalama ,ili vielekeze nguvu zao zote kule Arusha na hivyo kuwapa wao muda mzuri wa kuweza kuutekeleza mpango wao mkubwa .” Nikatulia na kumeza mate
“mpango mkubwa ? mbona sikuelewi Tonny? “ Catherine akauliza
“Nafikiri unakumbuka juu ya mashambulio ya kigaidi yaliyofanywa katika balozi za marekani jijini Dar es salaam na Nairobi mwaka 1998.Mtandao wa Alqaeda ulidai kutekeleza mashambulio hayo mawili yaliyosababisha vifo vya watu wengi.Baada ya mashambulio yale,uchunguzi mkali ukaanza ukishirikisha vyombo vya ndani na nje ya nchi na hatimaye ikagundulika kuwa kinara wa kupanga mashambulio yale alikuwa mmoja kati ya wanachama wa mtandao huo wa kigaidia aitwaye Abdool bin sahel Abdool.Iligundulika pia kuwa Abdool alikuwa amejificha nchini Sudan.Mimi ndiye niliyepewa jukumu la kuiongoza timu ya majasusi ya kwenda kumteka Abdool toka katika maficho yake.Operesheni hii ilikuwa ya siri sana bila ya nchi ya Sudani kufahamu.Abdool alitakiwa akabidhiwe kwa seikali ya Marekani kwa ajili ya kwenda kusomewa mashtaka ya kulipua balozi zake na kusababaisha vifo vya watu wengi.Operesheni ile ikafanikiwa na tukamleta Abdool hapa Tanzania kabla ya kumkabidhi kwa serikali ya marekani.Ni hivi Majuzi tu ,makachero wa marekani wamegundua mpango kabambe wa mtandao wa Alqaeda wa kumtorosha gaidi Abdool toka katika mahala alikohifadhiwa kwa siri akisubiri kupelekwa Marekani .Katika mpango huo wa alqaeda, mimi ndiye nilikuwa mlengwa mkubwa kwa sababu wanaufahamu uwezo wangu na pili walijua kuwa ni lazima ninafahamu mahala pa siri alipohifadhiwa Abdool.Kunipata mimi kungefanya kazi ya kumtorosha mtu wao kuwa rahisi.Kwa kuwatumia mawakala wao waliweza kupata habari zangu nyingi na hata kufanikiwa kufahamu kila nifanyacho.Baada ya kuunasa mpango ule CIA hawakutaka kuitaarifu mara moja serikali ya Tanzania kwa kuogopa kuwa hata ndani ya serikali zetu bado kuna watu wasio waaadilifu wanaoweza kurubuniwa kwa fedha na kuvujisha siri.Kwa hiyo wakaamua kufanya operesheni ya siri ya kulizima kabisa jaribio hilo la Magaidi.Kitu walichokifanya ni kumtuma mmoja wa makachero wao anayefanya kazi katika eneo la afrika mashariki na kati chini ya operesheni ya kuzuia ugaidi kwa sababu kwa sasa mtandao huu wa Alqaeda umeanza kupenyeza mizizi yake upande huu.Jasusi huyu aliitwa Monica na alitumwa kuja kushirikiana nami katika kazi hiyo ya kulizima jaribio la alqaeda kumtorosha mtuhumiwa wa milipuko ya mabomu.Siku moja kabla ya Krismas nilipata mapumziko na nikaamua kwenda Arusha.Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro ndiko nilikokutana na Monica bila mimi kufahamu kuwa ni jasusi toka CIA.Alijitambulisha kwangu kuwa alikuwa akielekea Arusha na hakuwa na mwenyeji.Kwa kuwa na mimi nilikuwa nikielekea huko huko Arusha nikakubali kuwa mwenyeji wake.Wote tulifikia hoteli moja.Usiku wa kuamkia siku kuu ya krismas tukaenda katika onyesho la muziki na huko ndiko yakatokea mliyoyasikia yametokea.Tukiwa ndani ya ukumbi simu yangu ikatetema nikatoka nje ili niipokee lakini kabla sijafanya hivyo mtu akaanguka karibu yangu alikuwa amepigwa risasi,kutahamaki akanguka tena mwingine.Baadae alijitokeza Monica akiwa na SMG mkononi .Usiku huo huo tukaondoka Arusha na kwenda Moshi kwa Joe kwa kutumia gari tuliloliteka njiani.Tuliondoka pale Moshi na kurudi Dar na baada tu ya kufika nyumbani kwangu nikakutana na ujumbe ulionitaka kuripoti ofisini haraka sana.Nilifanya hivyo na nilipofika nikawekwa chini ya ulinzi.Kwa kuwa kazi niliyokuwa nayo ni kubwa sikuwa na sababu ya kukubali kukamatwa na kuwekwa kizuizini kwani kwa kufanya vile ni wazi magaidi wangeweza kuutekeleza mpango wao kitu ambacho sikutaka kitokee.Nilitumia ujanja kidogo nikafanikiwa kutoroka.Niliporudi nyumbani nilikomuacha Monica sikumkuta.Nilikuta nyumba yote imevurugwa vibaya sana.Kitu kilichonistua ni kuikuta kompyuta yangu imewashwa na faili nilimohifadhi kumbu kumbu zangu za kazi zikiwamo zinazomuhusu Abdool lilikuwa limefunguliwa.Kwa taarifa tu ni kwamba tayari taarifa za mahala aliko Abdool wamekwisha zipata.Monica naye sijui mpaka sasa hivi atakuwa wapi,sielwei kama alitekwa nyara au amepotea katika mazingira gani..Nilimpigia simu David ili tusaidiane katika suala hili kwa sababu siwezi kufanya peke yangu.nadhani mpaka hapo umekwisha fahamu kwa undani nini kilitokea na kinachoendelea..Je bado una wasi wasi na mimi?
Nikamuangalia Catherine ambaye alikuwa akinitazama kwa makini bila kusema kitu.Nikaendelea.
“Kitu ninachokiomba toka kwako ni ushirikiano wako wa dhati ili kwa pamoja tuweze kuuzima mpango huu.Msaidizi wangu alikuwa Monica lakini baada ya yeye kupotea katika mazingira yenye kutatanisha naomba uichukue nafasi yake na ukubali kushirikiana nami.Muda uliobaki ni mchache sana kwa magaidi hawa kuutekeleza mpango wao.Je uko tayari kushirikiana nami? Nikamuuliza .
Kimya kizito kikatanda mle ndani.Catherine alikuwa katika tafakari nzito.Mimi nilikuwa natafakari kitu cha kufanya iwapo Catherine angekataa kushirikiana nami.
Baada ya kimya cha kama dakika kumi hivi Catherine akainua kichwa na kusema
“Pole sana Tonny”
“Pole sana Tonny kwa mkasa mzito uliokupata.Vile vile naomba samahani kwa yale yaliyotokea kwani nilitenda bila kufahamu siri iliyojificha nyuma ya pazia.Laiti kama ningefahamu toka mwanzo nini kinaendelea naamini ningekuwa msaada mkubwa sana kwako na ningekuwa nawe bega kwa bega katika kuuzima mpango huu wa magaidi..Yaliyotokea yameshapita kilichobaki tuangalie yajayo..Kuanzia sasa nitashirikiana nawe katika kazi hii ngumu.Bado tuna muda wa kutosha kuweza kuuzima mpango wa magaidi.I’m your body guard,nitume kazi yoyote ile nitaifanya Tonny” Akasema Catherine kwa utulivu mkubwa.Furaha niliyoipata kwa kauli ile ilikuwa haielezeki.kwa kauli ile ya kukubali kushirikiana nami tayari nilikwisha uona ushindi mbele yetu.Sikuwa na shaka kuwa labda alikubali kushirikiana nami kwa ajili ya kunilainisha na kuniweka mtegoni.Nilikuwa nimemsoma vya kutosha na kuamini kuwa hakuwa akinidanganya.
“Catherine Ahsante sana kwa kunielewa na kukubali kushirikiana nami.Kwa wakati kama huu nilikuwa nikihitaji sana msaada kama huu.Ni wazi siwezi kuifanya kazi hii peke yangu.Catherine kabla sijakupa picha kamili ya wapi tutaanzia kuifanya kazi yetu naomba kwanza nikupe japo kwa muhtasari ni wapi nimefikia kiuchunguzi hadi sasa.Mpaka sasa hivi kuna sehemu moja tu ambayo nina imani inaweza ikatupa majibu ya maswali yetu na kutupa mwanga zaidi.Kwa mujibu wa taarifa niliyoipata toka kwa Monica ni kwamba kuna baadhi ya watu ambao wanashirikiana kwa karibu sana na mtandano huu wa kigaidi na na wanalipwa mamilioni ya fedha kwa kuvujisha siri za serikali na kiusalama kwa mtandao huu.Katika idara yetu pia kuna mtu anayetumiwa katika kuwapa taarifa mbali mbali za kijasusi.Mtu huyu ambaye mpaka sasa amekwisha thibitika kuhusiana na mtandao huu ni Rachel alphonse.Sishangai kwa Rachel kuwa wakala wa mtandao huu wa kigaidi kwa sababu hili ni jambo la kawaida katika mashirika ya kijasusi duniani.Hata sisi tuna mawakala kadhaa katika mashirika mengine ya kijasusi duniani kwa ajili ya kupata taarifa mbali mbali za kijasusi.Kwa kumtumia Rachel waliweza kufahamu kila kilichokuwa kikiendelea kuhusiana na mimi.Waliweza kufuatilia na kusikiliza kila simu niliyopiga na kupigiwa.Hii iliwasaidia kuelewa kila nilichokuwa nakifanya au natarajia kukifanya.Kwa hiyo basi Rachel ndiye mshukiwa wetu wa kwanza na ambaye atatupa majibu ya maswali yetu na mwanga zaidi kuhusiana na kazi hii.”
Catherine bila kupoteza muda akajibu
“nakubaliana nawe Tonny.Tukimpata Rachel tayari tutakuwa tumepata mwanga wa nini kinaendelea.Tonny tusipoteze muda zaidi.Inatakiwa tuwahi kumkamata Rachel kabla hakujapamabazuka”
Catherine aliongea kwa ufupi huu akinitazama.Nikainua chupa ya maji safi ya kunywa nikaigugumia yote.Nikarekebisha koo langu na kusema
“Ok naelewa jinsi gani Rachel alivyo na umuhimu kwetu.Lakini kabla hatujapiga hatua kwenda kwa Rachel kuna mambo ambayo tunatakiwa tuyafanye.Kwanza kabisa naomba ufahamu kuwa katika operesheni hii wewe unatakiwa uwe upande wa serikali.Haitakiwi kufahamika kuwa unashirikiana na mimi kwa namna yoyote ile.Mpaka sasa hivi watakuwa wakifahamu kuwa mimi nimekuteka nyara .Hili litawafanya waongeze bidii katika kunitafuta kitu kinachoweza kukwamisha kuifanya kazi hii kwa ufanisi.Kwa maana hiyo unatakiwa kuonyesha kuwa uko upande wao ili kasi ya kunitafuta ipungue kidogo kwani kwa sasa na wewe pia unatafutwa ili wajue usalama wako.Kitu unachotakiwa kukifanya ni kumpigia simu Mr Meshack Jumbo na umtaarifu kuwa uko salama licha ya kuumia kidogo katika mapambano baina yako na mimi.Mdanganye kwamba ulifanikiwa kunidhibiti lakini nikatoroka katika mazingira ambayo hata wewe huyafahamu.Mhakikishie kuwa uko salama na wasihangaike kukutafuta.Ukisha malizana na Mr Jumbo piga simu kwa mkuu wa polisi na umweleze kama ulivyomweleza Mr Jumbo.naye hali kadhalika mhakikishie kuwa uko huru na salama. Halafu mwambie akupe msaada wa vijana kama sita hivi kwa ajili ya kukusaidia kufanya uchunguzi sehemu Fulani .Vijana hawa tutawatumia katika kumchunguza Rachel.Vijana hawa awatume asubuhi na mapema na wote uwakute karibu na kibanda cha simu pale Aqua snacks ambako si mbali sana na mahala hapa.Vijana hawa ambao watakuwa na kazi ya kumfuatilia Rachel na wengine kuichunguza nyumba yake watakuwa na jukumu la kutupa taarifa zote za Rachel,mahala alipo,anafanya nini,anaongea na nani na hata aina ya watu wanaoingia kwake ,ikiwezekana tupate walau picha za watu wanaoingia kwa Rachel au hata namba za magari ili tuweze kuyafanyia uchunguzi haraka iwezekanavyo.”
Kabla sijaendelea zaidi Catherine akadakia.
“samahani Tonny nina wazo moja.kwa nini kazi hii wasipewe vijana wa idara yetu.Nina imani kuna vijana mahiri wanaoweza kuifanya kazi hii kwa umakini mkubwa na ufanisi.Wana uzoefu na shughuli kama hizi ambazo zinatakiwa kufanywa kitaalamu mno na watu wenye utaalamu na ujuzi wa hali ya juu katika kumchunguza na kumfuatilia mtu.”Catherine alionyesha wasi wasi fulani
“Catherine usihofu kitu.Nalifahamu hilo lakini kwa sasa nisingependa kuhusisha watu wa idara yetu katika operesheni hii.Nina imani kama watu wa idara yetu watahusishwa watagundua kuwa nyuma ya operesheni hii nipo mimi,na mtu wanayemfanyia uchunguzi yaani Rachel ni mfanyakazi mwenzao inaweza ikawapunguzia morali ya kuifanya kazi.Hebu fikiria labda katika harakati za kiuchunguzi Rachel akamtambua mmoja wa vijana wale unafikiri itakuwaje? Ni wazi zoezi zima litakuwa limeharibika..Kwa hiyo basi ni bora tukatumia vijana toka idara ya upelelezi ya jeshi la polisi ambao hawamjui kabisa Rachel”
Catherine akatingisha kichwa ishara ya kukubaliana nami halafu nikaendelea.
“Kitu kingine unachotakiwa ukifahamu ni kwamba hatutatumia magari yetu ya kawaida yaliyozoeleka.Tunatakiwa tupate gari moja au mawili .Nataka yawe yenye vioo vyeusi na uwezo mkubwa wa kukimbia.Nataka zoezi hili la magari litimie kabla ya saa mbili za asubuhi.Gari moja tutalitumia na gari lingine tutaliweka hapa hapa kasino kwa ajili ya dharura.Unajua katika kadhia kama hizi kunakuwa na mambo mengi sana ya dharura.Nadhani suala hili ungeongea na mzee Jumbo ili alishughulikie haraka kwani yeye kuyapata magari hayo ni rahisi.Vile vile mwambie Mr Jumbo kwamba aongee na mkuu wa polisi ili atoe amri kwamba gari hizo mbili tutakazotumia zisikaguliwe au kusimamishwa katika kizuizi chochote kile cha polisi.Hii itatuepushia usumbufu na vile vile itanisaidia mimi kutokuonekana.Iwapo itatokea bahati mbaya nikaonekana basi shughuli nzima itakuwa imeharibika.” Nikasema na kumtazama Catherine
“Nimekuelewa Tonny na yote uliyoyaagiza nitayatekeleza ipasavyuo.Ila ninaomba kuuliza swali moja.”
“Uliza tu Catherine usihofu kitu”
“Je kuna umuhimu wowote wa mimi kufika ofisini kwetu na kuonana na mkurugenzi wetu ili aamni kuwa ni kweli niko huru na salama?
“ Hapana Catherine hutakiwi kabisa kuonana na mkurugenzi .Unatakiwa kuwasiliana naye kwa simu tu.Jaribu kila uwezavyo kumshawishi ili akuelewe kuwa uko huru na salama..Mwambie kuwa uko katika mpango kabambe wa kunikamata Mweleze kwamba utakuwa ukimpa taarifa kila baada ya saa moja kuhusiana na huo mpango wako wa kunikamata.Mshawishi naye awe akikupa taarifa juu ya wapi wamefikia katika operesheni ya kunitafuta.Hii itatusaidia kukwepa vizingiti na kutufanya tuifanye kazi yetu kwa kutulia.”
“Nimekuelewa vizuri Tonny.Naona tusipoteze muda mimi ngoja nimpigie simu mkurugenzi niongee naye sasa hivi “
“Ok Catherine mpigie simu.” Nikajibu na kuegemeza kichwa sofani nikamuachia nafasi Catherine aweze kuongea na mkurugenzi .
“kazi imekwisha” Akasema Catherine baada ya kumaliza kuongea na simu.
Huku nikitabasamu nikataka kujua kilichojiri katika maongezi yake na mkurugenzi.
“Nashukuru Mungu mambo yamekwenda vizuri nimefanikiwa kuwapata wote katika simu yaani Mkurugenzi na mkuu wa polisi.Kila kitu kimeenda kama tulivyopanga isipokuwa David ndio amelazwa hospitali amevunjika mbavu.Kuhusu magari nimegiza gari moja nipelekewe nyumbani kwangu na lingine liwekwe hapa.Wale vijana sita uliowaomba nao pia nimeahidiwa kupewa na watakuwa tayari kabla ya saa kumi na mbili za asubuhi.Vile vile suala la kutokuzuiliwa katika vizuizi vya polisi nalo pia limekubaliwa na nimeelekezwa na mkuu wa polisi kuwa magari hayo niliyoyaomba yakishapatikana basi namba zake zitumwe haraka sana kwake ili aweze kusambaza taarifa katika vituo vyote vya ukaguzi ili tusisumbuliwe.”
“kazi nzuri sana Catherine.Mkurugenzi hakuonesha dalili zozote za wasi wasi?”
“Hapana Tonny.Hakukuwa na hata chembe ya wasi wasi toka kwa mkurugenzi au hata mkuu wa polisi.Wote walifurahi kusikia kuwa niko hai na niko katika mpango kabambe wa kukutafuta.Hawakuwa na matumaini kama ningeweza kuwa hai kwani kwa sasa wanakuogopa sana.walijua ni lazima ungenidhuru.Ingawa alitaka sana tuonane lakini nilimkatalia kwa kigezo cha kutokuwa na muda wa kutosha.Mkuu wa polisi yeye alitaka kuniongezea idadi ya watu ili kunisaidia kazi nikakataa pia na kumhakikishia kuwa hao niliowaomba wanatosha na iwapo nitahitaji watu zaidi nitaomba tena.Kwa ufupi mambo ndio hivyo yalivyokuwa.”
Ok kazi nzuri sana Catherine.Kinachofuata ni wewe kwenda pale Aqua snacks kuwasubiri hao vijana watakaotumwa na mkuu wa polisi kisha uwaelekeze wakaanze kazi mara moja ya kumchunguza Rachel kabla hajatoka nyumbani kwake asubuhi hii. Na watupe ripoti kila baada ya dakika kumi na tano.”
“sawa Tonny kwa kuwa hivi sasa ni saa kumi na moja na dakika ishirini alfajiri ngoja niwahi nikawasubiri wale vijana halafu nitakwenda nyumbani kisha nitarejea hapa kwa ajili ya kuanza kazi.”
Nikamruhusu Catherine akachukua mkoba wake na kuanza kutoka.Kabla hajafungua mlango nikakumbuka kitu nikamwita,akageuka na kunitazama
“take this.This is the death message.Give it to anyone who want it.Today you are a death messenger”
Nikamrushia bastora akaidaka na kunitazama usoni kisha akatabasamu na kuondoka.
Baada ya Catherine kuondoka,nikahisi uchovu mwingi ,nikavua nguo na kuingia bafuni kuoga.Kisha oga nikapanda kitandani na kujilaza chali.Nilihisi usingizi mwingi kwani sikuwa nimelala kwa usiku mzima.Niliamua kuitumia nafasi hiyo kulala na kupuzisha akili japo kwa dakika chache kabla ya kazi kuanza .

USIKOSE SEHEMU IJAYO
 
BRING BACK OUR GIRLS
SEHEMU YA 19
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“sawa Tonny kwa kuwa hivi sasa ni saa kumi na moja na dakika ishirini alfajiri ngoja niwahi nikawasubiri wale vijana halafu nitakwenda nyumbani kisha nitarejea hapa kwa ajili ya kuanza kazi.”
Nikamruhusu Catherine akachukua mkoba wake na kuanza kutoka.Kabla hajafungua mlango nikakumbuka kitu nikamwita,akageuka na kunitazama
“take this.This is the death message.Give it to anyone in need.Today you are a death messenger”
Nikamrushia bastora akaidaka na kunitazama usoni kisha akatabasamu na kuondoka.
Baada ya Catherine kuondoka,nikahisi uchovu mwingi ,nikavua nguo na kuingia bafuni kuoga.Kisha oga nikapanda kitandani na kujilaza chali.Nilihisi usingizi mwingi kwani sikuwa nimelala kwa usiku mzima.Niliamua kuitumia nafasi hiyo kulala na kupuzisha akili japo kwa dakika chache kabla ya kazi kuanza .

ENDELEA............................................

Nilistuka toka usingizini saa kumi na mbili kasoro dakika tano.Muda niliolala ulitosha sana kukiweka sawa kichwa changu.Nilijizoa zoa hapo kitandani na kuiendea simu,nikapiga hotelini waniletee kahawa.
Kwa kawaidia mimi huwa mtazamaji mzuri sana wa televisheni.Mara zote huwa ni mfuatiliaji wa mambo yanayotokea ulimwenguni.Kwa kuwa humo ndani ya chumba kulikuwa na televisheni nikaiwasha kwa madhumuni ya kutazama taarifa ya habari toka televisheni ya Taifa.Nazipenda taarifa zinazotangazwa na kituo hiki cha televisheni kwa sababu mara zote huwa ni za ukweli na za kina.Kabla sijaingia katika kazi hii ya ujasusi nilikuwa na ndoto za kuwa mtangazaji wa televisheni na nilikuwa na ndoto za kufanya kazi siku moja katika shirika hili.
Saa kumi na mbili kamili taarifa ya habari ikaanza .habari ya kwanza ilikuwa ni habari ambayo mpala leo hii huwa sipendi kuikumbuka kwa sababu almanusura nipandwe na uchizi.Taarifa hiyo ilisema kwamba “LIMETOKEA SHAMBILIO BAYA NCHINI ,AMBAPO INASEMEKANA POLISI KUMI NA WANNE WAMEUAWA NA WATU WASIOJULIKANA NA KUFANIKIWA KUMTOROSHA MTUHUMIWA MKUU WA MILIPUKO YA MABOMU ILIYOTOKEA KATIKA BALOZI ZA MAREKANI JIJINI DAR ES SALAAM NA NAIROBI MWAKA 1998.ABDOOL BIN SAHEL BIN ABDOOL ALIKAMATWA NCHINI SUDAN NA ALIKUWA AMEHIFADHIWA MAHALA PA SIRI KABLA HAJAKABIDHIWA KWA SERIKALI YA MAREKANI KWA AJILI YA KUFUNGULIWA MASHITAKA YA MAUAJI NCHINI MAREKANI.SERIKALI YA TANZANIA BADO HAIJASEMA LOLOTE KUHUSIANA NA TUKIO HILO”
Nilihisi nguvu zikiniishia na kuketi sofani.
“No ! haiwezekani…” Nikasema kwa hamaki.na ghafla nikarukia mezani na kuinyakua bastora yangu.Sikumbuki nilitaka kufanya kitu gani lakini nilihisi nimechanganyikiwa ghafla.
“No..No! he cant go away…I must find him” Nikasema kwa hasira.huku machozi yakinilenga.Nikainyakua fulana yangu iliyokuwa sofani nikaivaa nikachukua na viatu vyangu nikavaa halafu nikakimbilia mlangoni.Pale mlangoni nikasimama kwa sekunde kadhaa nikitafakari.Sikumbuki ni wapi nilikuwa nafikiria kwenda.
Nilikuwa nikihema kwa nguvu.Mapigo yangu ya moyo yalikuwa yakienda kwa kasi ya ajabu.Nikarudi tena sofani nikakaa na kuinama nikitafakari.
“Ama zao ama zangu.Ni lazima nipambane nao kufa ama kupona.Ni lazima Abdool apatikane kwa jinsi yoyote ile.” Nilisema kwa sauti huku nikigonganisha viganja vya mikono kwa hasira.Nilijilaumu kwa kutoliweka suala hili wazi ili lifanyiwe kazi mapema .Lakini kwa sasa nimekwisha chelewa.yeyote nitakayemwambia hatanielewa.Kwa vyovyote vile lazima itajulikana kuwa ni mimi ndiye niliyefanikisha mpango ule.
Mawazo yangu yakakatishwa na kengele ya mlangoni.haraka haraka na kwa tahadhari kubwa nikainuka nikalekea mlangoni.Bastora yangu ilikuwa mkononi tayari kabisa kwa rabsha ya namna yoyote ile.Nikakishika kitasa cha mlango kwa mkono wa kushoto halafu mkono wa kulia uliokuwa na bastora nikauficha nyuma ya mgongo.taratibu nikaufungua mlango.Alikuwa ni muhudumu wa hoteli aliyekuwa amebeba sinia la kahawa.Nilikuwa nimesahau kama niliagiza kahawa.Nilimtazama kwa macho makali mpaka akaogopa.
“mzee uliagiza kahawa” akasema muhudumu yule kwa uoga.
“ndiyo niliagiza kahawa lakini ahsante unaweza ukairudisha.sihitaji tena.” Nikasema Nikaufunga mlango na kumuacha muhudumu ameduwaa akishangaa.Kabla sijapiga hata hatua nne kengele ya mlangoni inalia tena ,nikarudi kwa haraka kufungua mlango na kukutana na muhudumu yule yule.
“Kijana nimekwambia sihitaji kahawa tena..” Nikasema kwa ukali.nikaufunga mlango na kurudi chumbani.Nikasimama mbele ya runinga ambayo kwa sasa ilikuwa ikonyesha habari nyingine za ulimwengu.Nilihitaji kuisikia tena habari ile lakini ilikuwa imeshapita.
Nikaketi sofani na taratibu nikaanza kutuliza akili lakini bado mwili ulikuwa ukinitetemeka kwa hasira.Hali niliyokuwa nayo hata mimi mwenyewe ilinitisha.
Mara moja nikaanza kumhusisha Monica na magaidi hawa.Nikahisi alitumiwa na magaidi na kujifanya ni jasusi toka CIA ili niweze kumuamini halafu aitumie nafasi hiyo kupata taarifa za mahali alipofichwa Abdool.Nilijilaumu sana kwa kumuamini Monica kiasi kile na kumuacha akazijua siri zangu ambazo leo hii zinaigharimu nchi.Nilipaswa kulaumiwa kwa kilichotokea.Nilipaswa kuitaarifu serikali juu ya mpango ule mapema.
“Nina hatia mimi.Nimeiuza nchi yangu ,ninastahili kubeba lawama zote kuhusu jambo hili.Ninastahili hukumu.Lakini kabla sijahukumiwa ni lazima niwe nimemrejesha Abdool mikononi mwa serikali.” Nikasema kwa uchungu .Wakati nikiendelea kutafakari mara kengele ya mlango inagongwa nikainuka na kwenda kuufungua kwa tahadhari kubwa.Alikuwa ni Catherine akiwa katika sura iliyosawajika sana.Kwa kuitazama sura ile nikahisi tayari atakuwa amezipata taarifa za tukio lililotokea.Sikumsemesha kitu zaidi ya kumpa ishara aketi sofani.Catherine akalitupa begi alilokuja nalo sofani akaketi na kuvuta pumzi ndefu.Wote tukajikuta tukitazamana bila kuongea kitu.
“Tonny nimekuja na taarifa mbaya na za kustusha” Akasema Catherine
“Labda kama una taarifa nyingine ,lakini kama ni taarifa za kutoroshwa Abdool tayari nimekwisha zipata.” Nikasema
“Umezipata wapi taarifa hizi wewe? Akauliza kwa mshangao
“Nimetazama katika taarifa ya habari ya asubuhi hii.Hapa nilipo nimechanganyikiwa,sijielewi,naona kama kichwa changu hakifanyi kazi vizuri”
“usijali Tonny,bado hatujachelewa.Tunayo bado nafasi ya kumtafuta abdool na kumtia tena nguvuni.”
“nakubaliana nawe Catherine.bado tunayo nafasi japokuwa si kubwa sana lakini tukiitumia vyema tunaweza kumkamata tena Abdool.Kila kitu kimekwenda vizuri kama tulivyopanga?
“Ndiyo Tonny kila kitu kimeenda kama vile tulivyopanga.”
“Safi sana.Kwa sasa hakuna kupoteza muda .Tujiandae kwa ajili ya kazi.Leo hii jiji la dar ni lazima litikisike.Damu nyingi itamwagika .” Nikasema huku nikiifungua bastora yangu tayari kwa kuijaza risasi.

MSHIKE MSHIKE DAR

Saa moja kasorobo za asubuhi tuliwasili katika jumba la kifahari la Rachel.Jumba hili zuri na la kifahari lilikuwa limezungukwa na uzio mkubwa wa matofali ambao juu yake kulikuwa na nyaya zilizozunguka kwa ajili ya usalama.Eneo lote lilikuwa kimya kabisa,nadhani watu bado walikuwa hawajaamka.Ni milio ya ndege ndio iliyokuwa imetawala.Tulisimamisha gari letu mita kadhaa toka lilipo jumba la Rachel halafu tukashuka.Nilitupa macho kuzunguka eneo lote ili kuangalia kama vijana wale aliowapanga Catherine walikuwapo maeneo ya karibu lakini sikuweza kumuona hata mmoja wao.
“kazi nzuri.Vijana wanajua kufanya kazi” Nikajisema kimoyo moyo.
Catherine akawapigia simu vijana wake na kuwataarifu kwamba tumekwisha fika katika jumba hilo na kwa sasa tulikuwa tukijiandaa kuingia ndani hivyo walitakiwa wawepo karibu ili kutoa msaada endapo kutatokea dharura yoyote.Bila kuchelewa tukaelekea katika geti kubwa lililokuwa na rangi ya kijani huku tukiwa katika tahadhari kubwa.Kwa Catherine kushirikiana na magaidi hawa wa Alqaeda ilitupa picha kwamba eneo hilo katu si salama hivyo muda wote ni lazima tuwe katika tahadhari kubwa sana.Tulipolifikia geti nikampa ishara Catherine aangalie usalama wakatio nikigonga geti.Nilibonyeza kitufe cha kengele ya mlangoni na baada ya sekunde kadhaa geti likafunguliwa,nikajikuta nikitazamana uso kwa uso na jitu moja la miraba minne lililojazia kisawa sawa na ambalo lilikuwa na macho yenye kuashiria shari muda wote.Jitu hili lilikuwa limevaa kofia pana ya mduara iliyokishika vyema kichwa chake ,halafu akavaa na koti kubwa jeusi lililomfika magotini.Kifuani alikuwa amening’iniza mkufu wa dhahabu ambao kwa kuuangalia kwa haraka haraka ulikuwa ni wa thamani kubwa sana.
“Nikusaidie nini? Aliuliza yule jamaa mwenye sauti nzito inayokwaruza.Mara moja nikapata picha kwamba yule jamaa ni mlinzi wa nyumba ile.
“nahitaji kuonana na Rachel” Nikajibu kwa nidhamu huku nikijitahidi kuonyesha hali fulani ya uoga
“Ninyi ni akina nani? Akauliza tena huku amenikazia macho
“Sisi ni ndugu zake.Mimi naitwa Nick na yule pale anaitwa Sara tumetokea Morogoro,tumekuja hapa kwa shughuli zetu maalum na kwa kuwa tunaondoka asubuhi hii tumeona ni vyema kama tutapita hapa mara moja kumjulia hali dada yetu halafu tuendelee na safari yetu” Nilidanganya.
Kauli ile inamfanya jamaa yule aniangalie kwa makini sana halafu akainama na kiufukiri kwa sekunde kadhaa .Nilikwisha andaa ngumi nzito tayari kabisa kumtandika usoni,ngumi ambayo niliamini ingempeleka chini na kumpoteza fahamu.bahati yake malaika wake alikuwa makini kabla sijatekeleza azma yangu akainua kichwa chake na kusema.
“Subirini hapa hapa msiondoke.”
Kama utakumbuka mpenzi msomaji niliwahi kuwaleza kwamba wakati Rachel anaanza kazi pale ofisini kwetu mimi ndiye niliyekuwa rafiki yake mkubwa na kiasi kwamba niliweza kumfahamu kiundani hadi chimbuko lake.majina hayo niliyoyataja ni kweli yalikuwa majina ya ndugu zake wa damu waishio Morogoro.
Kosa kubwa alilolifanya jamaa yule ni kuuacha mlango wa geti wazi.nafikiri hata huko aliko analijutia sana kosa hili.Kwa kupitia ufa mdogo niliweza kumuona yule jamaa akiingia katika kibanda kidogo kilichokuwa pemBeni kidogo ya geti.Ndani ya kibanda kile kulikuwa na runinga kubwa .Mara moja nikagundua kwamba runinga ile ilikuwa ni maalum kwa ajili ya usalama.Akili ya haraka haraka ikanijia kwamba kama Rachel atatazama katika runinga na kugundua kwamba sisi si ndugu zake tayari tutakuwa tumempoteza.Sikutaka hilo litokee na papo hapo nikapata akili ya haraka haraka.Nilitazama juu ya geti ili nibaini kifaa ambacho kuilikuwa kikifanya kazi ya kuchukua picha lakini sikuona kitu chochote zaidi ya taa mbili kubwa .Nikatabasamu baada ya kugundua kitu.
Nikamfanyia ishara Catherine asogee halafu nikamwambia azivunje zile taa mbili kisha mimi nikajitoma ndani kwa tahadhari nikijikinga katika mitungi mikubwa ya maua.Niliangaza angaza pande zote lakini sikuona mtu yoyote zaidi ya yule jamaa ambaye kwa sasa alikuwa akiongea na simu huku akitazama juu .Mbele ya jumba lile kulipaki magari matatu ya kifahari sana kitu kilichonipa moyo kwamba Rachel atakuwamo mle ndani.
Kwa tahadhari kubwa nikaambaa ambaa kwa kunyata kuufuata ule ujia uliokuwa ukielekea katika kile kibanda.Kabla sijakifikia kile kibada ile runinga kubwa iliyokuwamo mle kibadani ikazima ghafla,nikatabasamu baada ya kugundua kwamba tayari Catherine alikwisha zivunja zile taa nilizomwambia avunje.Taa zile zilivunjwa kitaalamu sana .taa zile zilikuwa zikifanya kazi mbili yaani kumulika na papo hapo zilikuwa zikichukua picha za usalama.
Kitendo kile cha kuzima mitambo ile ya usalama kilimpa hamaki yule jamaa na kabla hajafanya lolote tayari nilikwisha fika .Akageuka na kunikuta nikimtazama ,akataka kuwahi kutoa bastora yake lakini nililitambua hilo na kwa kasi ya aina yake nikampiga ngumi nzito ya usoni inayomfanya apepesuke na kuanguka mezani.Kufumba na kufumbua nikampiga mateke mawili makali yaliyompata sawa sawa kichwani na kumpeleka chini.Bastora yake ikaanguka mita chache toka alipokuwa ameangukia.Niliinama kwa minajili ya kuiokota bastora ile lakini kabla sijaiokota jamaa akainuka mzima mzima na kuruka juu ili aweze kunikanyaga mgongoni.bahati yake ilikuwa mbaya kwa sababu nililing’amua hilo mapema na kumkwepa kitendo kilichopelekea ajibamize ukutani kwa kishindo.Nilistaajau sana kwa wepesi wa jitu lile.Akiwa bado ameegemea ukuta akigugumia kwa maumivu ,nikamrukia tena teke kali sana la shingo linalomrusha mita kadhaa.Sikuwa na imani kama ataamka tena kwa pigo lile.Nilisimama na kumwangalia yule jamaa aliyekuwa amelala kimya pale chini .Nilikuwa nikihema kwa nguvu.Nikamuendea pale chini kwa tahadhari na kumchunguza.Tayari alikwisha kata roho kitambo kwani teke lile lilikata kabisa mwasiliano baina ya kichwa na sehemu nyingine za mwili.Nilimsachi na kumkuta na bastora mbili,kete kadhaa za bangi ,shilingi elfu sabini na mbili na kitambulisho cha kazi.Kitambulisho kile kilionyesha kuwa alikuwa akitwa Danford Chemba,alikuwa mwajiriwa wa kampuni ya ulinzi ya Chem chem. Security agency kama mlinzi wa kawaida.Niliweka kadi ile mfukoni na zile fedha nikazirudisha katika mfuko wake.Nilipogeuka nikakuta Catherine amesimama akinitazama.
“Good job” Akasema .sikujibu kitu nikasimama na kuangaza angaza mle katika kile chumba kama kuna chochote kinachoweza kutusaidia lakini hakukuwa na kitu chochote ambacho kingeweza kutusadia kwa wakati ule.
“Catherine ni hivi,tutaingia ndani kwa kutumia mlango mkubwa wa mbele.Nilimwambia huku nikimfanyia ishara apite upande wa kushoto kwa kuambaa ambaa na miti ya maua halafu ajibanze sehemu wakati mimi nikiingia ndani.”
Kwa tahadhari ya aina yake nikaelekea katika mlango wa mbele .Nilipanda ngazi tatu za kibaraza halafu nikageuka na kumuona Catherine amejibanza katika pembe Fulani siyo mbali sana na pale mlangoni.
Nilijaribu kutafuta japo upenyo ili niweze kuchungulia ndani lakini sikuweza kwa sababu ndani kulikuwa kumefunikwa na mapazia mazito.Taratibu nikakinyonga kitasa ili nione kama mlango uko wazi lakini mlango uilikuwa umefungwa.Bila kupoteza muda nikaitoa funguo yangu ya bandia na nikaichomeka mlangoni na kisha taratibu sana nikakinyonga kitasa na mlango ukafunguka
“hivyo hivyo mlivyo ,mikono juu” Nilisema kwa sauti kali baada ya kujitoma sebuleni na kuikuta mibaba mitatu iliyoshiba iliyokuwa imekaa katika masofa .Pamoja nao alikuwepo pia Rachel.Katika meza ya kioo waliyokuwa wameizunguka kulikuwa na mabunda ya noti nyekundu zilizokuwa zimejaa meza.
Wote wakanitumbulia macho wasiamini kile walichokuwa wakikiona.Mijibaba ile ilikuwa na macho makali ya ukatili uliokithiri.Mezani pale palikuwa pia na bastora mbili ambazo nikajua ni za wale jamaa.
“Tonny unafanya nini hapa……………………………” Rachela akauliza kwa ukali huku akihema kwa hasira
“Shut up Rachel…” nikasema kwa ukali
Ghafla nikajikuta nikiguswa na kitu cha baridi shingoni.
“Dondosha bastora yako chini taratibu”
Niliamriwa na sauti nzito ya mtu toka nyuma yangu.Kijasho chembamba kikanitoka.Taratibu nikaiweka bastora yangu chini.
“Ipige teke bastora yako ije huku kwangu” nikaamriwa tena na mtu yule aliyekuwa nyuma yangu.Bila ubishi nikaipiga teke na kuisukuma kwa nyuma bastora yangu..Nilikuwa nimekamatwa.

USIKOSE SEHEMU IJAYO
 
BRING BACK OUR GIRLS
SEHEMU YA 20
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“hivyo hivyo mlivyo ,mikono juu” Nilisema kwa sauti kali baada ya kujitoma sebuleni na kuikuta mibaba mitatu iliyoshiba iliyokuwa imekaa katika masofa .Pamoja nao alikuwepo pia Rachel.Katika meza ya kioo waliyokuwa wameizunguka kulikuwa na mabunda ya noti nyekundu zilizokuwa zimejaa meza.
Wote wakanitumbulia macho wasiamini kile walichokuwa wakikiona.Mijibaba ile ilikuwa na macho makali ya ukatili uliokithiri.Mezani pale palikuwa pia na bastora mbili ambazo nikajua ni za wale jamaa.
“Tonny unafanya nini hapa……………………………” Rachela akauliza kwa ukali huku akihema kwa hasira
“Shut up Rachel…” nikasema kwa ukali
Ghafla nikajikuta nikiguswa na kitu cha baridi shingoni.
“Dondosha bastora yako chini taratibu”
Niliamriwa na sauti nzito ya mtu toka nyuma yangu.Kijasho chembamba kikanitoka.Taratibu nikaiweka bastora yangu chini.
“Ipige teke bastora yako ije huku kwangu” nikaamriwa tena na mtu yule aliyekuwa nyuma yangu.Bila ubishi nikaipiga teke na kuisukuma kwa nyuma bastora yangu..Nilikuwa nimekamatwa.

ENDELEA.......................................

" I’m sorry Tonny kwa kitu kitakachokutokea.Lakini haya yote umeyataka wewe mwenyewe kwa kupenda kufuatilia mambo yasiyokuhusu.Nasikitika sana kwa kijana mdogo kama wewe kufa kifo kibaya kama utakachokufa “
Rachel alibwatuka kwa hasira.Niliwatazama wale jamaa ambao hawakuwa na wasi wasi hata chembe.Bado waliendelea kunywa mvinyo na kuvuta sigara kwa fujo.Mtu yule aliyekuwa nyuma yangu akatoa pingu na kunifunga mikono yangu kwa nyuma.Sikuwa na ujanja wowote wa kuweza kujiokoa tena baada ya mikono yangu kufungwa.Kwa sasa tumaini langu lilibaki kwa Catherine.Nilijua kwa muda ule ni lazima Catherine atakuwa akijiandaa kuingia ndani hivyo nikaamua kuendelea kuvuta muda kwa kumuongelesha Rachel ambaye alionekana ndiye mkuu wa kikao kile na mwenye amri.
“Rachel tambua kwamba umelisaliti taifa lako.Umeiuza nchi yako kwa magaidi.Umesababisha maisha ya watu wengi wasio na hatia kupotea bure.Damu za watu hao zisizo na hatia zinakulilia toka udongoni.Hivi ni kitu gani kimekufanya ubadilike namna hii Rachel? Ni hizo fedha? Nikasema .
Rachel akainuka pale sofani alipokuwa ameketi akanikaribia. Pamoja na kwamba nilikuwa nimefungwa mikono kwa nyuma lakini Rachel hakuweza kunikaribia karibu zaidi kwa sababu ananifahamu vizuri.huku akiwa na uso uliojaa hasira akasema kwa ukali
“Usiwe mjinga Tonny.Hizi kazi tunafanya kwa sababu tunatafuta maisha mazuri.Sasa kama fursa imekuja ambayo itakufanya uishi maisha mazuri kwa nini usiitumie? Watu wanaimba Tanzania tunakupenda lakini hakuna mtu anayeipenda Tanzania Wote wanaimba midomoni lakini moyoni wanajua wanachokifanya.Wewe kwa kujifanya unaipenda sana Tanzania umepata nini mpaka leo hii? Tazama maisha yako yalivyo,huna mke ,huna familia,unaishi maisha kama swala porini wakati hao wakubwa zako wanaishi kama wako peponi wao na familia zao.nakusikitikia Tonny kwa sababu kama ungefumbuka macho mapema basi ningekufanya uwe na maisha mazuri sana,lakini kwa sasa umekwisha chelewa.nafasi hiyo huna kwa sababu si muda mrefu utakuwa umekufa.Pamoja na umahiri wako ,na sifa zako zote lakini leo umekamatika kijinga sana tena bila vurugu yoyote.hahahahaha ….na hili litakuwa fundisho kwa wale wote wenye tabia kama yako ya kufuatilia maisha ya watu ” rachel akasema huku akinitazama na kucheka kwa dharau.
“najua nitakufa Rachel ,lakini kabla sijafa lazima nihakikishe kwanza nimewafutilia mbali wewe na genge lote la maharamia na kumtia tena Abdool mikononi “
Kauli ile inamghadhabisha Rachel na kumfanya asogee karibu zaidi na mimi na kuninasa kibao kikali cha kike.Sikusikia maumivu yoyote yale,kwani ilikuwa ni kama ameligusa tu shavu langu.
“Frank,namfahamu vizuri sana mtu huyu,huwa hayuko peke yake.Ni lazima atakuwa na wenzake.hebu nenda nje jaribu kuchunguza kama kuna mtu yeyote amekuja naye.” Rachel akaamuru.
Ghafla bila kutegemea mtu aliyekuwa nyuma yangu akaanguka kwa kishindo huku akitoa yowe la uchungu.Wote mle ndani tukapigwa na butwaa kwa kitendo kile,lakini kabla hawajang’amua nini kinaendelea niliona mijibaba miwili iliyokuwa imekaa katika sofa lililokuwa pemBeni ya Rachel ikianguka kwa kupigwa risasi .Muuaji alitumia bastora yenye kiwambo cha kuzuia sauti.Kwa kasi ya aina yake nikalala chini na kuanza kuzisogelea bastora mbili zilizokuwa mezani.Nilikuwa nikitambaa kwa tumbo kwa sababu mikono yangu ilikuwa uimefungwa kwa nyuma.Bila kutegemea jamaa aliyekuwa amebakia aliruka juu na ghafla nilijikuta nikipigwa teke kali la tumbo linalonirusha mbali na ile meza.Nilisikia maumivu makali kupita kiasi kwa sababu teke lile lilikuwa ni kali mno.kama ingekuwa ni kwa mtu lege lege sidhani kama angeweza kuamka kwa pigo lile linalonifanya nione kiza kwa sekunde kadhaa.Nilikuwa nikigugumia kwa mauimivu makali. Jitu lile lililonipiga teke liliviringika tena hewani na kutua karibu kabisa na mlango mdogo kisha likageuka kwa kasi na kutoa bastora yake ,na mara ikasikika milio ya risasi,nikafumba macho.
Nilipofumbua macho sikuamini macho yangu baada ya kumuona Rachel akiwa amelala chini akivuja damu kifuani.Jamaa yule aliamua kumpiga risasi Rachel na kummaliza kabisa na tayari alikuwa amekwisha tokomea zake.Kwa mara nyingine tena nikaamini kwamba watu ninaopambana nao ni hatari sana.Nikiwa nimekaa pale chini mara mlango ukafunguliwa na Cathrine akasimama mlangoni akiwa na bastora inayofuka moshi nikajua ni yeye ndiye aliyefanya kazi ile nzuri .
“Amefanikiwa kutoroka mshenzi yule” Akasema catherine
Haraka haraka akamsachi yule mtu aliyenifunga ile pingu na kuzipata funguo za ile pingu akanifungua.
“amekimbia.mshenzi yule .Wataarifu vijana wetu waizunguke nyumba na wasiruhusu mtu yeyote kutoka nje.Wewe zunguka vyumba vyote uangalie kama kuna mtu yeyote bado yuko humu”” Nikasema huku nikimuendea Rachel pale alipokuwa amelala huku akivuja damu nyingi kifuani.Nilimgeuza geuza ili niangalie kama anaweza akaongea lolote lakini tayari alikwisha fariki kitambo.Nilimtazama kwa uchungu binti yule mrembo mwenye umbo la kuvutia akiwa amelala ndani ya dimbwi la damu pale sakafuni.
“haya ndiyo malipo yako Rachel.Binti mrembo kama wewe hukustahili kabisa kufa kifo kibaya kama hiki” Nilisema kwa kunong’ona.Nilimsachi mfukoni na kumkuta na simu ,nikaichukua na kuiweka mfukoni.Nilitazama hapo sebuleni kama nitaweza kupata chochote kinachoweza kutusaidia lakini muda ulikuwa ukienda kwa kasi na sikuwa na muda wa kuanza kuchunguza kila kitu.Nikapata wazo la kuwasachi wale jamaa watatu waliokuwa na Rachel.Sikuwakuta na kitu chochote cha maana cha kuweza kunisaida.Catherine akaingia tena sebuleni.Alikuwa amekwenda vyumbani kuhakiki kama hakuna mtu mwingine tena.
“Hakuna mtu mwingine yeyote.Inavyoonekana jamaa yule ameshakimbia kwa sababu mlango wa nyuma uko wazi.Inaonekana aliutumia mlango huo kutorokea.Vipi kuna lolote umeligundua hapa?
“hapana Catherine.Sijapata chochote cha kuweza kutusaidia zaidi ya kitambulisho cha kazi cha yule jamaa tuliyemuua kule getini na simu ya Catherine..Hatuna muda wa kupoteza hapa.Wapigie simu polisi waambie waje wazichukue maiti hizi na kuzihifadhi hospitali hadi hapo uchunguzi utakapokamilika.Wataarifu kwamba katika nyumba hii asiruhusiwe mtu yeyote kuingia hadi kwa ruhusa maalum kwa sababu bado tunahitaji kuifanyia uchunguzi wa kutosha.Ni lazima kuna mambo mengi yatakuwa yamefichwa humu.Halafu wataarifu vijana wako watatu waingie garini na watufuate kwa nyuma baada ya sisi kutoka hapa.” Nikamwambia Catherine ambaye alitekeleza maagizo yake haraka.Alipomaliza akanigeukia halafu tukatoka.
Wakati tukitoka nilipiga jicho mezani na kuyaona mabunda ya noti yakiwa yamepangwa yamejaa meza na mengine yakiwa yameanguka chini kutokana na zile purukushani.Niliyamezea mate lakini sikuwa na uwezo wa kuchukua hata bunda moja kutokana na maadili ya kazi.Tulipanda gari tukaondoka na kuliacha jumba lile ambalo lilikuwa limejaa harufu ya damu.
“Catherine hebu waulize vijana wako kama wakati tuko mle ndani kuna mtu yeyote aliotoka mle ndani ili tusije ondoka kumbe yule jamaa bado amejificha ndani”
Catherine akapiga simu na kuongea na vijana wake na baada ya kumaliza akanigeukia.
“ Tonny,vijana wanasema ni kweli kuna mtu alitoka mle ndani na kutokomea zake.Hawakuweza kumfuatilia bila kupata amri toka kwetu kwa sababu waliambiwa wasifanye lolote bila amri yetu.” Catherine akasema,nikaitika kwa kichwa na kuongeza mwendo wa gari.Mishale ya saa ilikuwa ikisonga kwa kasi ya ajabu na kuifanya akili yangu isitulie .
“Catherine kwa sasa tunaelekea Chem chem. Security agency.Kitambiulisho tulichokipata toka kwa yule jamaa wa getini, kinaonyesha kwamba ni mwajiriwa wa kampuni ile ya ulinzi.Ni lazima tuichunguze kampuni hii vizuri kwa sababu nimeanza kupatwa na wasi wasi kidogo.”Nikamwambia Catherine
“Nakubaliana nawe Tonny.Inavyoonekana kampuni hii inafanya kazi ya kuwaajiri vijana na kuwapatia mafunzo na kuwatumia katika shughuli zao mbali mbali.Ninahisi hata magaidi wanaweza wakaitumia kampuni hii kwa ajili ya kupitishia silaha na vitu vingine vinavyowasaidia katika kutekeleza shughuli zao.”
“Uko sahihi Catherine.Tunatakiwa tumfahamu mmiliki wa kampuni hii na jinsi inavyofanya kazi” Nikasema
Kimya cha dakika mbili kikapita halafu nikasema
“Unajua Catherine hawa jamaa wanafanya mambo yao kwa umakini mkubwa.Yule jama aliyetoroka alikwisha ona kwamba tayari walikwisha zidiwa nguvu na aliamua kumpiga risasi na kummaliza kabisa Rachel ili asiweze kubanwa na hatimaye kutoa siri za muhimu zitakazopelekea kuvurugika kwa mipango yao.Nina imani kwamba mabunda yale ya pesa yaliyokuwa mezani aidha ulikuwa ni ujira kwa Rachel au alikuwa akiwalipa wale jamaa,au walikuwa wanagawana baada ya kazi ya kumtorosha Abdool kufanikiwa alfajiri ya leo.Nasikitika kumpoteza Rachel,she was so young and pretty” Nikasema huku Catherine akinitazama.


*************************************************************

saa tatu na dakika ishirini na tatu tukawasili katika jengo ziliko ofisi za kampuni ya ulinzi ya Chem chem. Security agency,moja kati ya kampuni kubwa na ya kisasa ya ulinzi nchini Tanzania.Nje ya jengo hili kubwa tukakutana na mitambo ya kisasa kabisa ya ulinzi.Kwa kweli kampuni hii ilikuwa na mitambo ya hali ya juu mno ya usalama.
Tulisimamishwa getini na mlinzi aliyetaka tuandike majina yetu katika kitabu maalum cha wageni.Baada ya kuorodhesha majina yetu katika kitabu kile tukaruhusiwa kuingia ndani.Mlinzi yule akatuonyesha mahala pa kuegesha gari na ofisi tunazotakiwa kwenda kwa ajili ya kupatiwa msaada wa kile tunachokihitaji. Tuliegesha gari na kutoma ndani kama tulivyokuwa tumeelekezwa.Kama kawaida yetu sehemu yoyote ile ambayo huwa hatuna imani nayo huwa hatuongozani kama kumbi kumbi.Mimi nilitangulia mbele na Catherine akabaki hatua kadhaa nyuma yangu kwa ajili ya kuhaikisha usalama wetu..Katika mlango wa kuingilia ofisini tukamkuta tena mlinzi mwingine aliyekuwa na silaha na kumwonyesha kijikadi tulichopewa getini Kijikadi kile kiliandikwa AS14.Alipokiangalia tu akatuongoza mpaka katika mtambo uliokuwepo pemBeni ya mlango ,akaniambia niweke kiganja changu cha mkono juu ya kioo kidogo halafu lango likajifungua tukajikuta tukitazama na ofisi kubwa na nzuri.Tulipiga hatua kuelekea mahala kibao kilichoelekeza sehemu ya mapokezi ambako tukamkuta dada mrmbo ,mwembamba aliyezitengeneza nywele zake vizuri ameinamia kompyuta yake.
“habari zenu? Akatusabahi huku akitabasamu.
“nzuri ,habari yako” Tukajibu kwa pamoja
“sijui niwasaidie nini? Akauliza tena kwa adabu
“Tunahitaji kuonana na mkurugenzi mkuu wa kampuni” Nikasema na kumfanya dada yule astuke kwa ndani,ingawa alijitahidi kuuficha mstuko wake.
“Mna miadi naye leo? Akauliza tena
“hapana hatuna miadi naye ila tunashida ya dharura na ya maana sana ya kuonana naye leo hii” Nikasisitiza
“Nimekuelewa kaka yangu lakini mkurugenzi mkuu hayupo kwa sasa.Yuko nje ya nchi kikazi na hategemei kurudi hivi karibuni” akasema dada yule huku akiuma uma kalamu yake.
“ nani yuko badala yake? Nikauliza tena
“Msaidizi wake naye hayupo kwa sasa” Akajibu tena
“ Kwa hiyo nani yupo badala yao? Nikauliza
“Wapo maafisa wadogo wadogo wanaoshughulika na masuala madogo ya kawaida.kama kuna masuala makubwa huwa tunawasiliana naye huko huko aliko”
Nilitulia kidogo,nikafikiri halafu nikauliza tena
“toka wameondoka wana muda gani?
“Ni wiki ya tatu sasa” akajibu
Yule dada alionekana kutofurahia kuendelea kuulizwa maswali ,akachukua kitabu kikubwa na kutuangalia
“ naomBeni majina yenu na namba zenu za simu ili atakaporudi mkurugenzi tuwataarifu kwamba amesharudi” akasema dada yule huku akijiandaa kuandika
“dada ,tatizo letu ni la leo hii hii .Kama ungeweza kutusaidia kumpata mtu wa juu ambaye angeweza kutusaidia lingekuwa ni jambo la kufaa sana.” Nikasema
“kwani mlikuwa na shida gani? Akauliza yule dada
“Shida yetu ni kwamba tulikuwa tukihitaji kupata ulinzi katika kampuni yetu iliyoko mkoani Kilimanjaro.” Nikadanganya
Dada yule akafikiri halafu akasema
“kaka , mtu anayeshughulikia masuala hayo ni mkurugenzi mwenyewe au msaidizi wake na wote hawapo kwa sasa.Itawabidi muache majina yenu na namba za simu ili atakaporudi mmoja wao tuwataarifu.” akasema yule dada
Sikutaka kuendelea kubishana naye,nikaamua kuandika majina ya uongo katika kitabu kile. Niliutupia macho ukurasa ule na kukutana na orodha ndefu ya majina .Nikaandikisha majina ya uongo na na kumrudishia yule dada daftari lake halafu nikatoa kitambulisho cha yule mlinzi ambaye jina lake liliandikwa Danford Chemba na kumuonyesha yule dada
“dada mtu huyu mnamfahamu? Nikauliza
Yule dada akakichukua kile kitambulisho ,akakiangalia kwa makini na kunirudishia.Akachukua kijikaratasi kidogo akaandika halafu akanipatia
“”Habari za mtu huyu sisi hapa hatuna ,labda uende katika ofisi za usajili ukamuulizie manake kule ndiko wana kumbukumbu zote za wafanyakazi wote wa kampuni.Hapa sisi tuhahusika na mambo ya kiufundi zaidi.”Akasema dada yule huu akinikabidhi kile kijikaratasi kilichoandikwa namba za ofisi ,jina la mtu na namba za simu za mtu yule ambaye tulitakiwa kwenda kumuona kwa ajili ya kupata maelezo ya yule Danford.Kwa uzoefu wangu nilikwisha msoma yule dada ,alikuwa amestuka sana kiasi cha kutetemeka hata wakati akiongea.Sikutaka kupoteza muda zaidi hapo,tukamuaga na kuondoka zetu.Tulipofika mlangoni,milango ikajifungua yenyewe na tukatoka nje.Nilifurahishwa na ulinzi uliokuwep mahala hapa.Niliamini mpaka sasa hivi watu hawa tayari watakuwa na mashaka na sisi na tayari picha zetu wanazo kwa sababu kuna kamera za ulinzi katika kila kona ya jengo hili.Sikulijali sana hilo.

USIKOS E SEHEMU IJAYO……………
 
BRING BACK OUR GIRLS
SEHEMU YA 21
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPTA
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“dada mtu huyu mnamfahamu? Nikauliza
Yule dada akakichukua kile kitambulisho ,akakiangalia kwa makini na kunirudishia.Akachukua kijikaratasi kidogo akaandika halafu akanipatia
“”Habari za mtu huyu sisi hapa hatuna ,labda uende katika ofisi za usajili ukamuulizie manake kule ndiko wana kumbukumbu zote za wafanyakazi wote wa kampuni.Hapa sisi tuhahusika na mambo ya kiufundi zaidi.”Akasema dada yule huu akinikabidhi kile kijikaratasi kilichoandikwa namba za ofisi ,jina la mtu na namba za simu za mtu yule ambaye tulitakiwa kwenda kumuona kwa ajili ya kupata maelezo ya yule Danford.Kwa uzoefu wangu nilikwisha msoma yule dada ,alikuwa amestuka sana kiasi cha kutetemeka hata wakati akiongea.Sikutaka kupoteza muda zaidi hapo,tukamuaga na kuondoka zetu.Tulipofika mlangoni,milango ikajifungua yenyewe na tukatoka nje.Nilifurahishwa na ulinzi uliokuwep mahala hapa.Niliamini mpaka sasa hivi watu hawa tayari watakuwa na mashaka na sisi na tayari picha zetu wanazo kwa sababu kuna kamera za ulinzi katika kila kona ya jengo hili.Sikulijali sana hilo.

ENDELEA……………………………………………

“Catherine kuna chochote umeweza kukigundua pale ndani? Nikauliza huku nikikata kona kuingia barabara kuu
“Hawa jamaa wako juu katika teknolojia ya ulinzi.Kikubwa nilichokigundua hapa ni kauli zenye kubabaika za yule dada.Kutokana na jinsi alivyokuwa akijibu inaonekana kuna kitu anakificha” Akajibu Catherine
“nakubaliana nawe kate kuna kitu yule dada anakificha.Pamoja na hayo nadhani kampuni hii ina mtu mkubwa ambaye hafahamiki.Yaelekea kampuni hii inaongozwa kama lilivyokuwa kundi la MAFIA huko Italia kisha likasambaa duniani kote na watu wakafanya nalo kazi lakini bila kumfahamu mkubwa wake ni nani.Tunahitaji kumfahamu mmiliki wa kampuni hii.Kuna mambo ambayo yamejificha ambayo ni lazima tuyafichue.Baada ya kutoka katika ofisi hizi tunazokwenda sasa hivi kutafuta majibu ya huyu Danford ni nani ,tutatelekea katika ofisi ya msajili wa makampuni ili kuweza kuifahamu kampuni hii vizuri zaidi pamoja na wamiliki wake.”

*******************************************************

Ofisi ndogo za Chem chem. Security agency zilikuwa katika ghorofa ya tano ya jengo jipya kabisa la ghorofa tisa.Tulipanda ngazi za kuelekea ghorofa ya tano haraka haraka kwa kuwa lifti ilikuwa imeharibika.hatukutaka kupoteza hata sekunde moja kuisubiri lifti hivyo tukaamua kupanda kwa miguu.Haikuwa shida kubwa kwetu kwa sababu sisi ni watu wa amzoezi.
Tuligonga mlango wa chumba namba 703 ,tukaruhusiwa kuingia na sauti nzito toka ndani.Ofisi hiyo haikuwa kubwa sana .Kulikuwa na meza nne na katika meza mojawapo alikaa mtu mmoja ,pande la baba,mweusi aliyejaa mwili.Sijui kwa nini kampuni hii ilipenda kuajiri mijitu ya namna hii.
“habari yako mzee” Tukamsalimu jamaa yule aliyekuwa ametuna pale kitini
“habari nzuri.karibuni vijana.Niwasaidie nini?akauliza jamaa yule mwenye lafudhi ya watu wa kutoka koa wa mara
“mzee sisi tuna shida ndogo.Tunahitaji kufahamu kama Danford Chemba ni mwajiriwa wa kampuni yenu”
Yule mzee hakuonyesha dalili zozote za kustuka .Akatuangalia kwa makini halafu akasema
“ Danford Chemba ni mwajiriwa wa kampuni yetu.” Akajibu kwa ufupi
“Toka lini” Nikauliza tena kwa ufupi pia
“Huu ni mwezi wa nne sasa toka tumemuajiri”
“Ni vigezo vipi mnaviangalia katika kuajiri mtu? Nikauliza swali ambalo nilijua lingeweza kumuudhi yule jamaa.
“Kijana ,vigezo tunavyoangalia ni vingi.kwanza awe raia wa Tanzania,elimu yake,ufahamu wake.Mtu yeyote mwenye akili timamu na elimu isyopungua kidato cha nne anaweza kuajiriwa “
“Danford ameoa? Nikauliza
“Siwezi kufahamu kijana.Mtu huyu aliletwa hapa na dada mmoja anaitwa Sesi .yeye amekuwa ni kama wakala wetu wa kututafutia vijana ambao tunawafundisha mafunzo mafupi ya ulinzi na kuwapatia ajira.Ajira zetu sisi huwa hatuzitangazi kwa sababu huwa tunatoa ajira kutegemea na mahitaji ya wateja wanaokuja hapa kutafuta walinzi.Nina maana kwama ,kama kuna kampuni inahitaji watu wawili basi sisi huwatafuta vijana hao wawili tukawafundisha na kuwaajiri” akasema yule baba.huku akiangalia saa yake
“Samahani vijana nahitaji kutoka .Kuna mahala ninahitajika sasa hivi.Kama mkihitaji bahari za huyu Danford mtafuteni Sesi yeye ndiye anafahamu mahala alikomtoa.” Mzee yule akatuandikia namba za simu za Sesi halafu tukamuaga na kuanza kushuka chini.Tulishuka kimya kimya na kuelekea mahali tulikoegesha gari letu.Kama kawaida yetu mimi ndiye niliyekuwa nimetangulia mbele na Catherine akinifuata kwa nyuma.Nikaufungua mlango na kutaka kuingia ndani.lakini kabla sijaingia ndani nikasikia ukelele mkuwa .Ilikuwa ni sauti ya Catherine
“Tonny !!!!!!!!………….”
Niligeuka na macho yangu yakakutana na mtutu wa bunduki toka katika gari iliyokuwa imeegeshwa si mbali sana na pale tulipoegesha gari yetu.
Kama kima nikaruka juu huku milio ya risasi ikisikika na kuwafanya watu waliokuwapo pale nje wakumbwe na taharuki na kuanza kukimbia hovyo kuokoa maisha yao.Nilijibanza nyuma ya gari iliyokuwa karibu na gari yetu .Nadhani jamaa wale waliniona kwa sababu gari lile liliendelea kumiminiwa risasi na kuvunja vunja vioo.Hali ya hapa kwa sasa ilikuwa ni ya hatari kubwa.Risasi ziliendelea kuvurumishwa katika lile gari nililokuwa nimejibanza nyuma yake na kuliharibu vibaya.Kwa sasa risasi zilikuwa zikisikika kila upande na kunifanya niendelee kujibanza pale nyuma ya ile gari ndogo huku bastora yangu ikiwa mkononi .Baada ya kama dakika tano za mivumo ile ya risasi kutawala eneo lile,mara milio ile ikakoma ghafla.
“Tonny..tonny !!!!..” Nilisikia sauti ya Catherine ikiita.Nikanyanyua kichwa na kutazama kwa umakini nikamkuta Catherine akiwa amesimama katika ile gari waliyokuwa wanaitumia wale jamaa waliotaka kutumaliza huku bastora yake ikifuka moshi.PemBeni yake alikuwa amezungukwa na wale vijana wetu waliokuwa wakitufuatilia.Nilitabasamu baada ya kugundua kazi nzuri iliyofanywa na vijana wale hodari.Wale majahili wote walikuwa wameteketezwa.Nilisimama na kutembea kwa tahadhari kubwa kuelekea katika gari lile.Eneo hili kwa sasa lilikuwa halitazamiki kutokana na vioo vya magari kuvunjwa kwa risasi na magari kuharibiwa hovyo hasa lile nililokuwa nimejibanza nyuma yake.Watu wanne walikuwa wamelala chini wamekufa huku damu nyingi zikiwatoka.Walikuwa wameharibiwa vibaya sana kwa risasi.
“Catherine are you ok” Nikamuuliza Catherine aliyekuwa amejaa vumbi mwili mzima
“I’m ok Tonny.are you ok?
“yes I’m ok.Nashukuru Mungu kwa kunusurika kwa sababu jamaa walikuwa wamejipanga vilivyo” Nilisema baada ya kuziona bunduki walizokuwa wanazitumia wale jamaa.Zilikuwa ni bunduki za hali ya juu za kijeshi zenye nguvu sana.
Kijasho kilikuwa kikinitiririka.Ghafla nikagundua sikuwa na kiatu cha mguu mmoja.Kijana mmoja kati ya wale vijana wa Catherine akatoa viatu vyake na kunipatia.Nilimshukuru nikavaa.
“kazi nzuri sana vijana.hakuna hata mmoja wao aliyefanikiwa kutoroka? Nikauliza.
“hapana mkuu ,tumefanikiwa kuwadhibiti na kuwaua wote.Hakuna hata mmoja aliyefanikiwa kutoroka.” Akasema mmoja wa vijana wale
“Good job.Hebu nielezeni ilikuwaje mpaka mkawabaini? Nikauliza huku nikiinamia miili ya watu wale na kuwachunguza ili nione kama kuna kitu kinaweza kikatusaidia.
“Wakati ninyi mko ndani ,ilikuja hii gari Toyota Hilux kwa kasi na watu watatu wakashuka na kuelekea mlipokuwa mmeegesha gari lenu,wakajaribu kufungua milango lakini kwa bahati mbaya kwao milango yote ilikuwa imefungwa.Wakasimama na kujadiliana kwa muda kidogo halafu wakarudi tena katika gari lao.Wakalisogeza gari lao karibu kabisa na gari lenu.Sisi tayari tukawa na mashaka nao.Tulijua lazima kuna jambo ambalo si zuri litakuwa linaendelea.Tulifanya kama tunapita karibu na gari la wale jamaa kumbe tulikuwa tukiwachunguza na ndipo tulipoweza kugundua kuwa mle ndani ya gari wale jamaa walikuwa na bunduki nzito.Tulitaka tuwafuate tuwataarifu lakini hatukujua mlikuwa mmeelekea ofisi gani hivyo tukaamua kukaa tayari kwa mapambano kama yatatokea.Mlipotokea tu,wale jama walikwishajiweka tayari na ndipo hapo tulipopambana nao na kuwaua wote”
“kazi nzuri sana vijana.Endeleeni kutufuatilia” Nikasema baada ya kumaliza kuwakagua wale jamaa bila kupata chochote cha kuweza kunisaidia.Niwazi vijana wale walistahili pongezi kwa kazi nzuri waliyokuwa wameifanya.kama si wao wakati huu tungekwisha uawa .Niliazimia baada ya suala hili kumalizika ningeongea na wakuu wao wa kazi ili waweze kuangalia namna bora ya kuwatuza vijana wale kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa taifa lao.Kwa sasa hali ilikuwa imetulia na watu walianza kusogelea mahala tulipokuwa tumesimama ili kuishuhudia miili ya watu wale waliouawa kwa risasi.kwa mbali tukasikia ving’ora vya gari za polisi zikija.Nadhani walikwisha pata taarifa.
“Tuondokeni mahala hapa,tuwapishe polisi wafanye kazi yao.Catherine mpigie simu mkuu wa polisi na umtaarifu kwamba unahusika na tukio hili” Nikasema baada ya kuliona gari la polisi likiingia pale kwa kasi kubwa.Sikutaka kuonekana na polisi ,tukaingia katika gari letu na kuondoka.
USIKOSE SEHEMU IJAYO..
 
Back
Top Bottom