Bravo Mr Rocky Sayari yetu hii, PESA imeshika katikati ya ufahamu wa mwanadamu,sasa inasakwa kwa njia halali au haramu.
^^
Mkuu Himidini nilimuona mmoja alianzisha lake mahali tena kwenye bustani zile za jiji hana waumini akaanza kuhubiria wale wanaokuja kupumzika kwenye zile bustani mara kapata watu wawili watatu akatafuta sehem kwa mtu akakodisha akaweza hema mara waumini wakaongezeka akaongeza eneo na kuanza kujenga kwa mbao nyumba ya ibada
Miaka miwili iliyofuata mama ana V8 mpya tatu na ana kanisa kubwa na kile kiwanja kashanunua
Mwingine kaanzisha la kwake nyumbani waumini wanawahi asubuhi kwake kumfanyia usafi wa nyumba yake na kulisha mifugo yake na kuhakikisha nyumba ya mama mtumishi iko safi
Mtumishi anatakiwa asiishiwe sukari wala mafuta wala mchele so waumini ni kujichanga kununua sukari, mchele, mafuta, unga, sabuni mtumishi asiteseke
Sasa hao waumini sasa badala ya kufanya biashara waendeleze kwao wao wanakazana kumpelekea mtumishi ambaye bado na sadaka anawakamua pia
Na wewe muumini ambaye saa moja uko kwa mtumishi ni muda gani utafanya kazi za kwako
Tumeingilia thread ya watu mkuu Himidini
Last edited by a moderator: