Riwaya: Barua Kutoka Jela

Riwaya: Barua Kutoka Jela

Huyo Mwaipopo kweli ni jambazi aliekubuhu .!
 
Yaani kama naangalia movie......fast and furious
 
RIWAYA: BARUA KUTOKA JELA
MTUNZI: GAMA, Ibrahim


SEHEMU YA KUMI NA TISA

Kiasi kulikuwa hapatoshi eneo lile la Buguruni, kwani watu waliokuwa wanatokea Buguruni upande wa sokoni, na wale waliokuwa wanatokea upande wa Buguruni chama na kwa Mnyamani na kule upande wa sheli wote walikuwa wanakimbilia upande ule kulipotokea kizazaa cha pikipiki kelele zake lilipogeuzwa uelekeo, na kule kulipotokea kelele za gari alilokuwa anaendesha Inspekta Jamila.

Kwa kweli ilikuwa ni hatari tupu kukimbilia jambo kama lile.

Pikipiki ndiyo iliyowahi kufika katika maungio yale ikaingia, huku Inspekta Jamila akiwa amezuiliwa na gari iliyokuwa ikisuasua mbele yake, akaipita gari ile mkweche aina ya Datsun Nissan Old Model yakubebea mizigo, na sasa akawa yeye nyuma ya Pikipiki iliyokuwa imeibiwa na yule Ombaomba wa ajabu!

Mara Inspekta Jamila akamshuhudia yule Ombaomba akigeuza uso wake kumtazama, huku mkono wake wa kushoto ukiwa na bastola iliyofungwa kiwambo cha kuzuia sauti isisikike {Silence} akimnyooshea pale upande wake usawa wa dereva.

Mara akaona kidole kikigusa kile kifyatulio cha risasi {Trigger}

Inspekta Jamila kitendo bila kuchelewa aliipeleka gari upande mwingine wa barabara ile kule kwa watembea kwa miguu ‘Service Road' kwa haraka huku akibonyea mle ndani ya gari na kukanyaga Breki.

Na wakati huohuo ikasikika mlio wa kuvunjika kioo cha gari iliyokuwa inasuasua iliyokuwa nyuma yake! na vipande vidogovidogo vikimwagika chini kwa kuwa chenga tupu!

yule Ombaomba alirusha risasi,aliyokuwa amemkusudia Inspekta Jamila, ila kwa kitendo cha yeye kukata kona ya ghafla na kutoka barabarani, risasi ile ikaipiga ile gari mkweche kwa bahati mbaya.

Gari aliyokuwa anaendesha Inspekta Jamila ilikipanda kikuta cha barabara ya watembea kwa miguu, huku ikiwa inasota kwa sababu ya Breki za ghafla alizokanyaga, na gari iliposimama akafungua mlango haraka na kutoa bastola mgongoni mwake usawa wa kiuno.

Huku mlango ule ukiwa umefunguliwa akaipitisha mikono yake katika uwazi wa mlango pale baina ya Flem ya mlango ule na mlango wenyewe, huku akiwa ameushusha mguu mmoja nje, na kuuacha mguu wake wa kushoto ndani ya gari ile, mikono yake miwili iliyoshika bastola ya kipolisi aina ya Rivolver akalenga shabaha kwa tabu kumlenga yule Ombaomba aliekuwa anakaribia kabisa kuingia katika barabara ile ya Mandela na kufyatua risasi moja.

Mlio wa risasi ya silaha ya Inspekta Jamila ulisikika sehemu kubwa kwani bastola yake ilikuwa haina kiwambo cha kuzuia sauti.

Yule Ombaomba ilimkosa risasi ile sentimita chache na ikaenda kupiga katika chuma cha ngao ya gari ya mizigo iliyokuwa inaelekea Ubungo na kutoa cheche za moto!

Kwa ustadi mkubwa yule Ombaomba akaanza kuiendesha pikipiki ile katika mtindo wa Zigzaga na kuingia katika barabara ya Mandela, akakata kushoto kuelekea Tazara, na kumuacha Inspekta Jamila katika mataa ya Barabara ya Mandela na Uhuru!

Inspekta Jamila sasa akiwa ameshuka chini nje ya gari, alilipiga teke tairi la gari kwa hasira! Huku akilaani msongamano wa watu na magari uliyokuwa katika eneo lile, kwani ndiyo uliomfanya asiendelee kurusha risasi nyingine akihofia kuuwa au kujeruhi raia wasiokuwa na hatia, lau kungelikuwa hakuna msongamano wa watu angeliendelea kumrushia risasi yule Zabania mpaka angemdondosha chini!

Inspekta Jamila akakumbuka kwa kina Afande Kubuta, na akafikiri kuwa kwa vyovyote vile, kutakuwa kumetokea Zahma kubwa, kwani yule ombaomba alikuwa ni mtu hatari kuliko anavyoonekana!

Inspekta Jamila akaingiza mkono wake mfukoni mwa suruali yake aina ya Kadeti na kutoa simu ili ampigie Afande Kubuta kumwambia kilichoendelea, akaiona simu yake imezimika!

"Shit jana sikuichaji simu, kwani umeme ulikatika na kurudi asubuhi."

Inspector Jamila alijisemea kimoyomoyo baada ya kugundua kuwa simu yake imezimika kwa kukosa chaji ya kutosha.

Alijaribu kuiwasha na simu ikawa kama haikubonyezwa kitufe chochote, unaweza kuifananisha na ‘Toy!' akakata shauri kurudi kule alipowaacha askari wenzake wakiwa na mualifu wao Dokta Masawe ili akajue kilichotokea.

Inspekta Jamila akaingia ndani ya ile gari, na kabla hajaufunga mlango wa gari ile, alisikia sauti ya chuma aliyokuwa ameizoea masikioni mwake.

Ilikuwa ni sauti ya chuma cha Bunduki aina ya SMG ‘Sub Mashene Gun' ikikokiwa katika harakati za kupeleka risasi chemba tayari kwa kufyatuliwa wakati wowote!

Na namna kilivyolia chuma kile, wakati silaha ile ilipokuwa inavuta risasi, akatambua kuwa silaha iliyokokiwa, imekokiwa katika mfumo wa kutoa risasi mfululizo {Basta / Rapid}na sio ule mfumo wa kutoa risasi mojamoja ‘Single Systim' na mara akasikia sauti ya mtu ikimwambia

"Upo chini ya ulinzi,shuka chini na usalimishe silaha yako!"

Inspekta Jamila akashuka kutoka katika ile gari huku akitii amri ile kwa kuiweka chini silaha yake.

Aliposhuka chini akawaona askari polisi wawili, waliokuwa wapo katika sare zao za jeshi la polisi.

Askari mmoja akiwa ameshika Bunduki aina ya SMG, na askari wa pili alikuwa amekamata simu ya upepo ‘Radio call'.

Eneo lile lililotokea kizaazaa, walikuwa wamejaa watu wengi sana.
Yaani lilikuwa jambo la hatari sana sehemu iliyolia Bunduki watu badala ya kukimbia, kinyume chake wao wanakimbilia! Wakiwa hawawazi kwamba risasi inaweza kumkosa mlengwa ikampata raia asiekuwa na hatia, kwa sababu ya kiherehere na kimbelembele kilichowajaa!

Ama kweli jambo usilo lijuwa ni kama usiku wa kiza!

"Afande mimi ni askari, nilikuwa napambana na Jambazi"

Inspekta Jamila alikuwa anajitambulisha kwa wale askari, huku akiwaangalia usoni moja kwa moja.

"Wewe ni askari kutoka katika kituo gani"
Yule askari alieshika "Radio Call" alimuuliza Inspekta Jamila.

Kabla Inspekta Jamila hajajibu swali lile, Afande kubuta alitokea na alikuwa anawatambua askari wale!

"Afande Majuto huyu ni askari mwenzetu, mwenye cheo cha Inspekta, anaitwa Inspekta Jamila, kutoka makao kakuu."

Afande Kubuta aliyasema maneno yale huku akiiokota ile silaha ya Inspekta Jamila pale chini, iliyokuwa imesalimishwa na kumkabidhi Inspekta Jamila.

Wale askari wawili wakakakamaa na kutoa heshima ya utii kwa Inspekta Jamila.

Inspekta Jamila alipokea heshima ile kwa moyo mkunjufu, kutoka kwa wale askari waliokuwa katika ulinzi wa kawaida wa jeshi la polisi, katika kila kwenye makutano ya barabara kubwa na kwenye taa za kuongozea magari.

"Vipi Dokta Masawe ana hali gani huko aliko, kwani yule Ombaomba ni zaidi ya Jamba……"

"Yule ni Gaidi mkubwa!"

Afande kubuta alimkatisha kauli Inspekta Jamila, aliekuwa anataka kujuwa kilichotokea kule nyuma alipowaacha na kutaka kumuelezea yule Ombaomba.

"Yule ni Jeradi Mwaipopo au Gaidi, na Dokta Masawe hivi tunavyozungumza ni marehemu!"

Maneno ya Afande Kubuta yalimkata maini Inspekta Jamila na kumfanya kutingisha kichwa kwa masikitiko makubwa.

Inspekta Jamila sasa hakuwa na shaka kuwa Dokta Masawe ameuwawa na yule aliekuwa akimuona kama Ombaomba, kumbe ni Jeradi Mwaipopo mtu aliowafanya wawe maeneo yale kwa siku ile ili wamtie mikononi, badala yake amekuja na kuwaachia maafa, yasiyofikirika kabisa kutokea, hasa kukiwa na ulinzi kama ule!

Mara ikasikika sauti ya King'ora cha gari ya wagonjwa, ikija kwa kasi kuelekea kule kwenye Baa ya Y2K Buguruni kwenda kuchukua mwili wa Hayati Dokta Masawe.

Ilikuwa ni simu ya Afande Kubuta alipokata shauri, la kuwapigia simu pale katika Hospitali ya Amana Ilala, ili kwenda kuuchukua mwili wa Marehemu Dokta Masawe ili ukaifadhiwe katika chumba cha maiti pale Hospitalini Amana, na uchunguzi zaidi wa mwili ule, uweze kufanyika kwa kina.

Inspekta Jamila akawageukia wale askari wawili wa Doria, waliomuweka chini ya ulinzi muda mfupi uliopita, akawapa maelezo kwa harakaharaka, na alipomaliza akageukia upande wa pili wa gari ile na kupanda, huku Afande Kubuta akiingia upande wa Dereva wa gari ile na kuwasha gari na kuiingiza barabarani kuelekea katika barabara ya Mandela.

Afande Kubuta alipofika pale katika makutano ya barabara ya Uhuru na Mandela, akakata upande wa kushoto wa barabara ya Mandela, na kuelekea Tazara.

Wale askari wawili Afande Majuto na Mwenzie, walioachiwa maagizo na Inspekta Jamila, waliiendea ile gari iliyopata ajali ya kuvunjwa kioo cha mbele kwa risasi na Jambazi aliepanda cheo na kuwa Gaidi, Jerard Mwaipopo.

Gari aina ya Datsun Nissan Old Model, huku dereva wa gari ile akiwa haonekani eneo la tukio.

Wale askari walipoona kimya kila walipokuwa wanamuuliza dereva wa gari ile, yule askari aliekuwa na kifaa cha mawasiliano, Afande Majuto aliongea kupitia kifaa kile na muda wa kama dakika tano hivi gari mbili aina ya Land Rover 109, zilikuja kwa mwendo wa kasi katika eneo lile, na kuifunga mnyororo gari ile na kuivuta kuipeleka katika kituo cha polisi cha Buguruni. Pale mkabala na soko na kituo cha Basi cha Buguruni.

watu waliokuwa katika kushangaashangaa katika eneo lile, ilibidi wasambae na kuondoka kwani hakukuwa na jambo la kushangaa tena. Na kiasi ya dakika kama kumi baadae eneo lile lilirudi katika hali yake ya kawaida, kukawa kama halikutokea tukio lolote la hatari hapo kabla.

*******

Jeradi Mwaipopo aliendesha ile Pikipiki kwa kasi ya ajabu, kama aliekuwa katika mashindano ya kuendesha Pikipiki!

Alipofika katika eneo la Tazara akazikuta Taa za kuongozea magari, zimeruhusu gari za kutoka upande wa Buguruni kupita.

Hivyo akiwa bado katika mwendo kasi, alilala nayo ile Pikipiki upande wa kulia, akishika njia kuelekea upande wa uwanja wa ndege.

Kila alieiona Pikipiki ile namna ilivyolazwa pale kwenye kona ikienda sanjari na taa ya kijani iliyoruhusu vyombo vya moto kupita, alishika kichwa kwa masikitiko, kwani mwendo ule ukianguka tu, huwi majeruhi abadani ila kifo kitakutembelea!

Hususan dereva wa Pikipiki ile hakuwa na ile kofia maalum ya kuendeshea Pikipiki ‘Elementi'
lakini hata mavazi ya dereva yule, na Pikipiki ile, vilikuwa havifanani kabisa, ilikuwa tofauti kama maji na mafuta!

Lakini kila kwenye Welevu, na Wajinga hawakosi.
Wapo watu wachache waliokishangilia kitendo kile cha mwendo kasi, huku wakipayuka kuwa;

"Siku hizi wazee nao wamechoka, kwani wanaendesha Pikipiki kama hawana akili nzuri!"

Mwendo kasi aliopita nao Jeradi Mwaipopo kwenye taa zile za kuongozea magari pale Tazara, kuliwagutusha askari wa usalama Barabarani na askari wa doria wa Pikipiki waliokuwa wamebarizi pale kwenye kivuli cha mti kwenye kona ya Barabara ile.

Waliitilia mashaka pikipiki ile, wakawasiliana na askari wenzao waliokuwa doria pale katika eneo la Vingunguti, kwenye kona ya kwenda Vingunguti kiembe Mbuzi, kwa upande wa kulia na ile kona ya Bombom Kijiwe samli kwa upande wa kushoto, kwenye Njia ya Viwandani.

Huku askari wa doria wenye Pikipiki waliokuwa pale tazara, wakiifatilia Pikipiki ile kwa mwendo wa kasi vilevile.

Askari wale waliokuwa pale kwenye kona ya Vingunguti, na Viwandani walikuwa wamejiandaa na bunduki mikononi!

Lakini hadi wale askari waliokuwa wana Pikipiki waliotoka Tazara, walipofika pale kwenye ile kona ya Vingunguti na Bombom, bado waliwakuta askari wenzao, wakiwa na bunduki mikononi wakisubiri mtu aliepita na Pikipiki kwa mwendo wa kasi bila mafanikio!

Wote kwa pamoja walikuwa wamepigwa chenga ya Mwili.
Baadae wakapata taarifa zilizowafanya wakunje uso kwa ghadhabu, kwani taarifa ile kupitia Radio Call zao ilisema;

"Jambazi Sugu Geradi Mwaipopo anaetafutwa na Polisi, kwa makosa ya mauwaji na uhalifu wa kutumia silaha, amepora Pikipiki aina ya Honda 750 GL ya Ndugu Majidi Ndosho katika maeneo ya Buguruni, na kuelekea Maeneo ya Tazara.
Hivyo askari wote watakaoiona Pikipiki au mtu anaeiendesha, anaeonekana kama mtu mzima, mtu huyo, awekwe chini ya Ulinzi mara moja Ova"



***NI KIMBEMBE HIKI……….Mwaipopo anasumbua vichwa vya askari lukuki……
Jagarld Jullie Z Sangomwile Khantwe Mr Rocky Gunda66 Himidini VAN HEIST BPM ABUBAKAR SHEKAUNYIROmamsapkhan born again pagan princetx Ennie mcubic jonnie_vincy slim5 MAVUNO mp anoldamoneyazan



 
RIWAYA: BARUA TOKA JELA
MTUNZI: IBRAHIM GAMA


SEHEMU YA ISHIRINI

Lakini hadi wale askari waliokuwa wana Pikipiki waliotoka Tazara, walipofika pale kwenye ile kona ya Vingunguti na Bombom, bado waliwakuta askari wenzao, wakiwa na bunduki mikononi wakisubiri mtu aliepita na Pikipiki kwa mwendo wa kasi bila mafanikio!

Wote kwa pamoja walikuwa wamepigwa chenga ya Mwili.
Baadae wakapata taarifa zilizowafanya wakunje uso kwa ghadhabu, kwani taarifa ile kupitia Radio Call zao ilisema;

"Jambazi Sugu Geradi Mwaipopo anaetafutwa na Polisi, kwa makosa ya mauwaji na uhalifu wa kutumia silaha, amepora Pikipiki aina ya Honda 750 GL ya Ndugu Majidi Ndosho katika maeneo ya Buguruni, na kuelekea Maeneo ya Tazara.
Hivyo askari wote watakaoiona Pikipiki au mtu anaeiendesha, anaeonekana kama mtu mzima, mtu huyo, awekwe chini ya Ulinzi mara moja Ova"

Ilipomaliza taarifa ile, wale askari wakasambaa kuanza msako mkali wa kumtafuta Jambazi yule.

Eneo lote la Tazara kuanzia mchicha, hadi katika maeneo ya Viwandani, yalikuwa katika mshikemshike wa hali ya juu kabisa, akitafutwa Jeradi Mwaipopo.

Katika kona ile ya mchicha kwenda Kiwalani kabla ya kufika ile pacha ya Vingunguti na Viwandani, ilitiliwa mashaka kuwa huenda Jeradi Mwaipopo, akawa amechepukia pale, kwa kuwa Pikipiki ile haikuonekana kupita katika njia panda ya Vingunguti, Bombom!

Hivyo nguvu kubwa ikaelekezwa pale, askari wa doria kenda, pamoja na askari wa pikipiki, walilizunguka eneo lile, wakawa wanamsaka Jeradi Mwaipopo!

Wacheza kamari wa maeneo yale, hawakuwa na raha kabisa siku ile, wala walevi wa Pombe ya Gongo, kwani kila walipowaona askari Wakitayaya, wao walikuwa nusura wavunje miguu yao kwa mbio!

Msako ule uliendelea katika eneo lote la Kiwalani lakini muda ulikuwa unakwenda, Jeradi Mwaipopo alikuwa haonekani hata vumbi lake!

Wale askari waliotoka tazara wakiwa na pikipiki walifanikiwa kuziona alama za Tairi za Pikipiki ile, wakaanza kuifata taratibu.

Walifanikiwa kuzifata alama zile za Tairi kwa robo kilometa!

Lile wingu zito jeusi lilokuwa limetanda angani, likaanza kunyesha Mvua kubwa, ikaharibu mwenendo mzima wa kuzifatilia alama za tairi za Pikipiki aliyokuwa akiiendesha Jeradi Mwaipopo, kiasi wale askari walimuhusisha Jeradi Mwaipopo na kutumia pia, nguvu za Kiza!

Dakika ishirini baadae, ilipatikana taarifa kupitia Radio Call ,kwamba Pikipiki aina ya Honda 750 GL, iliyokuwa inaendeshwa na Jambazi Jeradi Mwaipopo, imekutwa imetelekezwa katika eneo la makazi ya Walemavu kule Kiwalani!

*******
Afande Kubuta, akiwa na Inspekta Jamila akaendesha gari ile huku akiwa hajui wanakwenda wapi, akamuuliza Inspekta Jamila aliekuwa ameinama kwa mawazo, yaliokuwa yanatembea kichwani mwake.

"Sasa afande tunaelekea wapi?"

Inspekta Jamila aliinua kichwa chake akatazama nje, akaona walikuwa katika Taa za kuongozea magari za Tazara, zinapokutana barabara zenye majina ya viongozi mashuhuri Barani Africa, Barabara ya Mandela, na Barabara ya Mwalimu Juliasi Kambarage Nyerere.

Inspekta Jamila akasema;
"Turudi ofisini tukajipange upya, mradi taarifa ya kutafutwa yule Gaidi tumeshaitoa askari wa doria watamtafuta."

Afande Kubuta akapinda kushoto gari ile na chombo kikawa kinatazama mjini, huku askari wale wakiwa wamelowana ndembendembe kwa namna Jambazi Jeradi Mwaipopo alivyowafanza!

Inspekta Jamila mara baada ya kufika ofisini kwao, akamwambia Afande Kubuta kwamba;

"Kuna mtu mmoja yupo Kijitonyama, tunatakiwa tumfikie na tumuhoji ili tubaini kama nae anahusika, kwa namna moja au nyingine katika kadhia hii!"

Afande Kubuta akiwa bado hajamuelewa Inspekta Jamila akamuuliza;

"Ni mtu gani huyo Afande unaemaanisha ambae kwamba, atakuwa anaweza akawa anahusika na kesi hii?!"

Inspekta Jamila alivuta mtoto wa meza yake nakutoa picha, aliyokuwa ameihifadhi mle, picha ambayo ameichukua katika Albam ya Marehemu Hamida, katika zile picha tatu ambazo mbili tayari ameshazifanyia kazi na tayari majibu yake yameshapatikana!

Ilikuwa ni Picha ya Bitozi, ambayo bado hajajuwa kama itampa jibu gani.
Akaichukua picha ile na kumpa Afande Kubuta.

Afande Kubuta aliipokea picha ile na kuitazama kwa makini, kisha akaipindua upande wa pili akaona maandishi yalioandikwa kwa mkono katika picha ile kwa kalamu ya wino yaliokuwa yakisomeka BITOZI.

Afande Kubuta alimtazama usoni Inspekta Jamila, akamuona nae anamtazama kwa makini sana! Afande Kubuta akasema;

"Huyu Predeshee namfahamu huyu mie, ni muuza magari maarufu sana, na ni mgonjwa kwa wanawake huyu!"

Inspekta Jamila huku akiwa anatabasamu akamuuliza Afande Kubuta;

"Wewe unamfahamu kivipi huyo Bitozi, au Predeshee kama ulivyomwita?"

"Nina jamaa zangu kama wawili hivi, wamenunua magari kwake na mara zote mbili nilionana nae, sidhani kama anaweza kuwa na mahusiano yoyote na Genge lile!"
Afande Kubuta alikuwa anamjibu kiongozi wake huku akiondosha kabisa Dhana kama jamaa anaweza kuwa na uhusiano na kesi ile.

Inspekta Jamila alicheka huku akionyesha mshangao kwa majibu ya Afande Kubuta, akamwambia;

"Kwani Afande unataka kuniambia kwamba, ukimtazama mtu tu unaweza kumjuwa matendo anayofanya? Hivi uliwahi kufikiri kuwa Dokta Masawe anaweza kuhusika na kesi hii?, Na akawa ndiyo chanzo cha Mauwaji yaliyotokea?!"

Afande Kubuta aligwaya kwelikweli, na Inspekta Jamila akaendelea kwa kusema;

"Mimi sijasema kama huyo Predeshee anahusika hata kidogo, bali ninachotaka kujuwa alikuwa na mahusiano gani na Marehemu Hamida, hadi akapiga nae picha! Na hakuna mtu mwingine anaeweza kutupa ukweli wa jambo hili bali ni Bitozi mwenyewe, lakini pia kuchunguza ndiyo kazi yetu!"

Afande kubuta akatikisa kichwa chini juu, kuonyesha kuwa ameelewa. Kisha akasema;
"Kwa kuwa huyu jamaa ni Mkwale, nashauri bora uwende wewe kiongozi, kwani jamaa lazima atatoa ushirikiano unaopaswa! Lakini pia Bosi wangu nasema kidhati kuwa Mungu amekupa upendeleo maalum, kiasi hata mwanaume angekuwa mgumu kiasi gani, basi kwako atakuwa laini kama Pamba!"

Inspekta Jamila alimtazama Afande Kubuta kwa macho ya aina yake kisha huku akimwemwesa akasema;

"Nashukuru kwa Mungu kunipa huo upendeleo kama upo, pia asante kwa kunisifia."
Alipokuwa anamwemwesa mashavu ya Inspekta Jamila yalikuwa yana vishimo maalum vilivyokuwa vinabonyea kwa kuingia ndani.
Mashaallah Inspekta Jamila alikuwa ni mrembo sana, kitu kilichokuwa kinampa tabu Afande Kubuta ni kule kuona kuwa, pamoja na uzuri wa sura, umbo, na tabia, lakini bado alikuwa hajaolewa!

Akawa hajuwi kama wanaume walikuwa wanamuogopa kumtokea, au mwanamke yule hana bahati ya kuolewa, au alikuwa hataki kuolewa!

Ilimradi Afande Kubuta alikuwa amehemewa kwa uchu wa mapenzi kwa bosi wake, lakini pia nayeye alikuwa anamuogopa kumwambia!

Akawa anaishia kusema kimoyomoyo, kuchukua mwanamke kama yule ni kujipa presha za bure!
Ama kweli hakuna kizuri kikakosa kasoro.

Inspekta Jamila akasema;
"Sawa sasa tuweke masihara pembeni na turudi katika kazi, hivi sasa ni saa saba za mchana, itabidi tukapate chakula cha mchana, na ikifika saa nane kamili tukutane hapa ofisini, kwa kuendelea na zoezi letu ili tuone leo tunaimaliza siku kwa jibu gani."

Alipokwisha kusema hayo Inspekta Jamila aliichukua ile picha ya Bitozi na kuirudisha ndani ya mtoto wa meza, na kutoa chaja ya simu, na kuichaji simu yake.

Afande Kubuta aliinuka nakutoka nje kwenda kupata chakula cha mchana.

Inspekta Jamila alipotaka kufunga yule mtoto wa meza, akaiona simu ya Marehemu Dokta Masawe aliyokuwa ameihifadhi mle ndani, na hapo akawa kama mtu aliekumbuka jambo fulani!

Aliitoa simu ile mle ndani nakuiwasha, na baada ya kuwaka aliibonyeza namba ya mwisho kuipiga simu ile na kuipiga.

Akasubiri kwa muda kidogo huku moyo ukimuenda mbio kama saa mbovu, na kwa mastaajabu makubwa simu ile ikawa inaita upande wa pili!

Kwani hakutarajia kuisikia simu ile ikiita katika muda ule, matarajio yake nikusikia kwamba simu ile imezimwa.

"Halow Jm mambo vipi?"

Inspekta Jamila alitamka kifupi cha jina la Jerard Mwipopo baada ya simu ile kupokelewa.

Kwa mshangao wa ajabu, alisikia upande wa pili ukimjibu tena bila ya wasiwasi wala kutetemeka!

"Muongeaji ni Inspekta Jamila, nipe habari."

Ama kwa hakika kitendo kile hakukitarajia kabisa, akajikuta anamuuliza Jeradi Mwaipopo;

"Umejuaje kama Inspekta Jamila ndiyo unaeongea nae, hali ya kuwa simu niliyoitumia kukupigia ni ya rafiki yako Dokta Masawe?!"

Kwa swali lile alisikia upande wa pili wa simu ile, Jeradi Mwaipopo akicheka sana kisha akajibu kwamba;

"Mimi ni askari Afande, hivyo kutambua jambo hilo na zaidi, ya hilo sio kitu cha kushangaza kabisa!"

Inspekta Jamila alitingisha kichwa juu chini karibu mara tatu!

Akiwafiki maneno yale ya Jeradi Mwaipopo, kisha akarudi katika hali yake ya kawida na kumwambia.

"Hapana JM, ulikuwa Askari hapo mwanzoni, ila sasa ni jambazi hatari sana wewe, na hilo ndilo lililokufanya ufukuzwe kazi katika Jeshi la polisi."

Jeradi Mwaipopo huku akiendelea kucheka, alijibu kwa kusema.

"Baadhi ya watu wengi sana wanaelewa hivyo, ulivyoelezwa wewe kuhusu mimi, ila ninachokwambia ni kwamba hizo ni taarifa za uzushi mtupu, huku sababu za kweli za kuachishwa kazi kwangu haziwekwi wazi!"

Inspekta Jamila akajilaumu kwa nini asingetumia simu yake kuongea na JM – kwani angeweza kuyarecodi mazungumzo yale, lakini simu ya Marehemu Dokta Masawe haina uwezo wa kurekodi!

Ingawa yale mazungumzo yalikuwa yanamgusa sana, kwani alikuwa anapata maelezo ya kwanini Jeradi Mwaipopo amefukuzwa kazi.

Ingawa Jeradi Mwaipopo anakana tuhuma za kufukuzwa kazi kwa sababu ya uhalifu, lakini picha yake imeonekana katika vipimo vya kitaalamu alivyowekewa machoni marehemu Kiyarwenda Mwemezi, lakini pia aliwajeruhi Askari kwa risasi siku moja nyuma pale Barakuda Bar na leo hii amemuua Dokta Masawe!

"Hapana huyu ni Jambazi anavunga tu, kwani wezi wachache sana hukubali kuwa wameiba!"

Inspekta Jamila baada ya kupita mawazo hayo kichwani mwake, akamtupia swali linguine.

"Kama wewe hukufukuzwa kazi kwa sababu za kujihusisha na uhalifu, lakini upo ushahidi wa kutosha, kuwa wewe ni muhalifu, lakini pia unashirikiana na wahalifu, ambao baadhi yao tumewakamata na wanatuthibitishia kila kitu kuwa wewe ni muhalifu!"

Jeradi Mwaipopo aliacha kucheka, na akasema;

"Acha kutumia simu ya marehemu, kwani sheria haikuruhusu kufanya hivyo, huo pia ni uhalifu!"

Inspekta Jamila alichukia, kwa maneno ya kiburi ya Jeradi Mwaipopo, akamjibu huku akimuuliza swali.

"Kwa taarifa yako, Dokta hukumuua kama ulivyokusudia! Lakini Jeradi kama wewe ni mwanaume kweli, unaejiamini, niambie upo wapi nikufate?"
"Ukiwa wewe ni askari, unatakiwa unitafute unikamate, ili utambue ukweli wa mimi kufukuzwa kwangu kazi, na tumetambua vipi kama wewe ndiyo unayefatilia kesi hii, hata siku yako ya kwanza tu ya kuanza kazi hii, tukakuachia ujumbe kule katika Hospitali ya Taifa ya Rufaa ya Muhimbili!"

Inspekta Jamila alipagawa kweli kweli kwa maelezo yale, akamwambia Jeradi Mwaipopo kwamba.

"Basi Jeradi kwa nini tusipange sehemu tukakutana na tukaongea kwa kirefu kiurafiki?!"

Jeradi Mwaipopo alitungua kicheko kama mwehu vile kisha akamjibu Inspekta Jamila.

"Hata mimi nilipokuwa upande huo, nilikuwa nawalaghai watu hivyo hivyo, na hatimaye niliwatia nguvuni. Sasa kitanda hicho nimeisha kilalia, na nawajua kunguni wake! Ila zingatia kwamba huu ni mtego wa panya Inspekta Jamila wa Ilala Mtaa wa Songea nyumba namb………!"

Simu ile ilikatika na Inspekta Jamila akaingia kiwewe akapiga ngumi katika meza yake!



***ITAENDELEA……

Jagarld Jullie Z Sangomwile Khantwe Mr Rocky Gunda66 Himidini VAN HEIST BPM ABUBAKAR SHEKAUNYIROmamsapkhan born again pagan princetx Ennie mcubic jonnie_vincy slim5 MAVUNO mp anoldamoneyazan
 
ram huku kumependeza
 
Last edited by a moderator:
RIWAYA: BARUA KUTOKA JELA
MTUNZI: GAMA IBRAHIM


SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA

Inspekta Jamila alichukia, kwa maneno ya kiburi ya Jeradi Mwaipopo, akamjibu huku akimuuliza swali.

"Kwa taarifa yako, Dokta hukumuua kama ulivyokusudia! Lakini Jeradi kama wewe ni mwanaume kweli, unaejiamini, niambie upo wapi nikufate?"
"Ukiwa wewe ni askari, unatakiwa unitafute unikamate, ili utambue ukweli wa mimi kufukuzwa kwangu kazi, na tumetambua vipi kama wewe ndiyo unayefatilia kesi hii, hata siku yako ya kwanza tu ya kuanza kazi hii, tukakuachia ujumbe kule katika Hospitali ya Taifa ya Rufaa ya Muhimbili!"

Inspekta Jamila alipagawa kweli kweli kwa maelezo yale, akamwambia Jeradi Mwaipopo kwamba.

"Basi Jeradi kwa nini tusipange sehemu tukakutana na tukaongea kwa kirefu kiurafiki?!"

Jeradi Mwaipopo alitungua kicheko kama mwehu vile kisha akamjibu Inspekta Jamila.

"Hata mimi nilipokuwa upande huo, nilikuwa nawalaghai watu hivyo hivyo, na hatimaye niliwatia nguvuni. Sasa kitanda hicho nimeisha kilalia, na nawajua kunguni wake! Ila zingatia kwamba huu ni mtego wa panya Inspekta Jamila wa Ilala Mtaa wa Songea nyumba namb………!"

Simu ile ilikatika na Inspekta Jamila akaingia kiwewe akapiga ngumi katika meza yake!

Akaipiga tena namba ile ya simu iliyokatika.
Akasikia ujumbe kutoka kwenye simu ile ya Marehemu Dokta Masawe, ikimwambia;

"Salio lako halitoshi kupiga simu hii, tafadhali ongeza pesa katika simu yako kabla hujajaribu kupiga simu nyingine!"

"Shabashi" Inspekta Jamila alisema maneno hayo huku sasa akiwa amesimama na akawa anatembea kwenye ofisi ile toka kwenye kona moja kwenda kwenye kona nyingine, huku akitafakari mazungumzo ya Jeradi Mwaipopo, kwani alimtajia hadi Mtaa anaoishi bila shaka hadi namba ya nyumba alikuwa aitaje kwani kama si kukatika kwa simu ile pengine angesikia namba ya nyumba yake ikitajwa!

Kitu kilichomtia hofu zaidi ni kwamba, watu anaowatafuta wao wanamfahamu vizuri hadi katika nyumba anayoishi, kitu ambacho ni hatari kubwa sana kwa maisha yake kwani angewezwa kuviziwa na kupigwa hata risasi na majambazi wale!

"Ama kweli huu ni mtego wa panya."

Inspekta Jamila alijikuta akitamka maneno hayo, mara kama mtu aliyegutuka, akakumbuka jambo Fulani, akaenda hadi sehemu alikochomeka simu yake kwenye chaja akaichomoa.

Akaichukua simu ya Marehemu Dokta Masawe, pamoja na simu yake, kwa mwendo wa haraka, akaelekea katika chumba cha mawasiliano ‘Computer Room.'

Akamfuata afande Dihenga na kumpa mkadima mzima.

Vyombo vikawekwa sawa na baada ya kusetiwa mitambo ile, simu ya Jeradi Mwaipopo ikapigwa, na ikasikika sauti katika simu ile;

"Simu unayopiga kwa sasa haipatikani, tafadhali jaribu tena baadae"

"Oh shit" Inspekta Jamila alitamka maneno hayo huku akikunja ngumi katika mikono yake yote miwili kwa hasira.

Walijaribu kuipiga namba ile zaidi ya mara tano, ulipatikana ujumbe ule ule kutoka kwenye simu ile, hii ikimaanisha kwamba simu waliyokuwa wanaipigia imezimwa!

Inspekta Jamila akazichukua simu zile mbili pamoja na chaja yake na kurudi navyo ofisini kwake huku akiwa hoi bin taabani kwani Jeradi Mwaipopo aliiharibu kabisa siku yake kwa maneno aliyomwambia.

Lakini akapiga moyo konde huku akisema kimoyomoyo.

"Vilima Havikutani bali wanadamu wanakutana, hivyo ipo siku nitakutana na Jeradi Mwaipopo uso kwa uso, na mimi mwenyewe nitahakikisha ninamfunga pingu!"

Kichwa cha Inspekta Jamila kilijaa mawazo lukuki, kiasi kwamba akaanza kuhisi uchovu na njaa, huku akili yake ikishindwa kabisa kufanya kazi kwa wakati ule.

Akaangalia saa yake na kuona imetimia saa nane kasorobo.
Robo saa tu ndiyo iliyosalia ili wakutane tena na Afande Kubuta wapate kuendelea na ratiba yao.

Inspekta Jamila alikuwa amechoka sana kiasi hawezi kufanya kazi kwa ufanisi.

Aliiweka simu yake katika chaja huku ikiwa inachajiwa, akampigia simu Dokta Zahala.

"Shoga nakuja nyumbani kwako mchana huu kwa mambo makuu mawili. Jambo la kwanza ni kuja kula chakula cha mchana, na la pili ni kuja kupumzika. Kwani kwako ni mahali salama kwa kazi yangu na maisha yangu kuliko nyumbani kwangu kwa hivi sasa!".

Dokta Zahala akiwa hakumuelewa vizuri shoga yake, akamuuliza.

"Mbona sikuelewi shoga, yaani leo nyumbani kwangu kuwe pahali salama kwa maisha na kazi yako kuliko nyumbani kwako ki vipi?!"

Inspekta Jamila akamwambia shoga yake

"Punguza Wahka shoga, mimi ninakuja huko huko kwako maswali mengi ya nini?"

Wote wakatungua kicheko kirefu kwani watu wale kila wanapokutana, walikuwa wanapendana kama watoto mapacha.

Baada ya muda Afande Kubuta aliingia ofisini mle, akiwa ameshikilia chupa ya maji safi iliyokuwa shinda.
Akamuona Inspekta Jamila akimaliza kuongea na simu.
Afande Kubuta alistaajabu, kwani kiongozi wake hakuonekana kama ametoka nje kwenda kula. Akamuuliza.

"Vipi kiongozi wangu mbona wewe bado hujaenda kupata chakula hadi muda huu, kumezuka jambo jipya au umeagiza viazi?!"

"Hapana sijala chochote toka wewe uondoke, wala sijaagiza kitu ila kazi zilikuwa zimenibana, sasa kwa kuwa wewe tayari umekwisha pata chakula cha mchana, itakubidi muda huu uende Kijitonyama kwa Bitozi ili ukamchukulie maelezo.
Mimi nakwenda kupata chakula cha mchana nyumbani kwangu, lakini pia ndiyo tutakuwa tumeagana, kwani nikiondoka ofisini hapa sitarajii kurudi tena hadi kesho.
Hivyo asubuhi tutakapokutana kwa majaaliwa ya mungu, tutapeana taarifa kamili na matokeao ya kazi yako huko uendako."

Afande Kubuta alipatwa na bumbuazi au mzubao kwani yeye alidhani kuwa Inspekta Jamila ndiyo angekwenda kule Kijitonyama lakini pia yeye ndiye aliyesema kwa muda ule wakapate chakula cha mchana.

Sasa iweje tena yeye asiende na kusema kwamba anakwenda kula kwake! Lakini afanye nini na kiongozi wake ndiyo kasema hivyo.

Akageuka na kutoka nje ya ofisi ile na kuelekea katika sehemu ya maegesho ya magari akachukua gari ile yenye namba za kiraia na kufungua mlango na kujipakia mle ndani.

Akawasha gari na kutoka eneo la jengo lile kuelekea Kijitonyama kwa Bwana Bitozi au Predeshee.

Inspekta Jamila akafunga mtoto wake wa meza kwa funguo baada ya kuweka vitu vyake muhimu ndani yake, pia alizima computer na kiyoyozi kilichokuwa kinafanya kazi muda wote.

Kisha akaichukua simu ya Marehemu Dokta Masawe aina ya Siemens MC 60 na simu yake aina ya NOKIA 6230i pamoja na chaja yake, akafunga ofisi na kutoka nje katika maegesho ya magari, akaiendea gari yake na kufungua mlango na kujipakia ndani kisha akawasha gari na kutoka nje ya eneo lile na kuitafuta Wilaya ya Temeke katika maeneo ya Keko Bora nyumbani kwa Dokta Zahala.

Inspekta Jamila, alishituka kutoka katika usingizi mzito,akawa bado anatafakari katika fikra zake kilichomuamsha muda ule.

Alisikia mlio wa simu, ukihanikiza katika chumba cha wageni alipokuwa amelala, pale kwa shoga yake dokta Zahara. Akatazama saa yake ya mkononi, aliyolala nayo, ilimuonesha kuwa ni saa nane za usiku!

Akanyoosha mkono wake, kivivu akachukua simu yake, akaitazama namba ya mtu aliekuwa akimpigia simu, usiku ule wa manane! Moyo wake ukawa unakwenda mbio kwa furaha, huku akiipokea ile simu na kutamka majina matatu, yalioonekana katika simu ile "SHANY KARAMA RASHIDI" Huku akiitikia kwa madaha "Halow sweety?"

Aliongea kwa mbwembwe nyigi,mizaha, na zihaka, ilitawala mazungumzo yao, huku Bwana Shany aliekuwa nje ya nchi kwa mambo yake ya biashara, akimtaka aende kumpokea katika uwanja wa ndege wakimataifa wa mwalimu Nyerere, akamwambia muda atakaotua Tanzania kutoka ughaibuni.

Inspekta Jamila, usingizi ulimpaa akaanza kufikiri mambo mengi kumuhusu Shany, tangu siku ya kwanza walipokutana, hadi kuanzisha mahusiano. Alipokuja kutoka katika mawazo, alisikia majogoo yanawika!

Aliinuka kutoka kitandani, akafanya mazoezi ya viungo kidogo, kisha akaingia bafuni, alipotoka hakujipodoa sana, alitaka kuwahi nyumbani kwake kabla hakujapambazuka, ili kukagua usalama, kisha awahi kazini, kwake kwa utendaji zaidi.
Alipotoka Sebuleni, akamkuta shoga yake Dokta Zahara, ameshaamka muda mrefu, anapata kifungua kinywa.

"Shoga hulali umekuwa kama kolokoloni?"
Inspekta jamila alimtania shoga yake, na Dokta Zahara kwa utani akamjibu.

"Mimi nakulinda wewe, siwezi kulala, kwani wewe ni mtu muhimu sana!"

Wote kwa pamoja, waliangua vicheko huku wakikutanisha, mikono yao hewani (Wakagonga) Baada ya kupata kifungua kinywa, Inspekta jamila, akaagana na Dokta Zahara, akaiendea gari yake, na safari ya nyumbani kwake, ikaanza huku akiwa na shauku, ya kutaka kujua usalama wa nyumbani kwake.

Inspekta Jamila aliendesha gari yake huku akiwa makini, hadi akawa umbali wa alipo na nyumbani kwake, ni takribani nyumba kumi hivi, akaegesha gari yake pembeni, kisha hakushuka ndani ya gari yake, akawa anatazama nyumbani kwake, kama kuna mtu anaetoka au kuingia! Lakini mtaa ule wa Songea pale Ilala, ulikuwa tulivu, na watu wengi walikuwa bado wamelala.

Inspekta jamila, alibakia mle ndani ya gari yake, kwa zaidi ya dakika kumi, lakini hakuambulia kitu cha maana, zaidi ya kumuona mtu mmoja mwembamba mrefu,akiwa katika mavazi machafu na chakavu, akiwa amebeba mfuko aina ya kiroba,kikiwa kichafu, akihangaika eneo lile, kuokota chupa za plastiki, na vyuma chakavu!

Inspekta jamila, alitazama saa yake, na kuona kuwa ilikuwa imeshatimu, saa kumi na mbili na robo, akajisemea kimoyomoyo, "Hawa mateja hawalali?" Kisha baada ya kusema hayo, aliteremka ndani ya gari yake, na kutembea hatua za taratibu, kuelekea nyumbani kwake.

Akiwa yupo karibu na nyumba yake, kwa tofauti ya nyumba mbili, akapishana na Yule muokota chupa. Inspekta Jamila alimtazama Yule bwana,akashangaa kiasi,kwani yeye alishazoea kuwaona vijana walioathirika na madawa ya kulevya, ndiyo, wanaookota chupa za plastiki na vyuma chakavu, lakini huyu jamaa anaepishana nae, hakuonekana sura yake, kama inachembe ya ujana!
Walipopishana, Inspekta Jamila aligeuka kumtizama kwa nyuma Yule bwana, lakini Yule bwana wala hakuwa kabisa na habari na yeye. Inspekta Jamila akafika nyumbani kwake,akawa makini mara dufu, na kila kitu anachokitazama. Akakijaribu kitasa cha mlango wake kama kimefungwa kama alivyo kiacha, naam kitasa kikawa salama! Akatazama katika kipande cha zulia la kufutia miguu pale mlangoni, naam hapo mapigo ya moyo, yakamuenda mbio kama saa mbovu!

Bahasha nyeupe ilikuwa imewekwa pale kwenye futio la miguu, kwa chini. Robo tatu ya bahasha ile ikiwa imefunikwa haionekani na kile kipande cha zulia, na robo ya bahasha ile ikiwa inaonekana dhahiri, shahiri.

Inspekta jamila, aliinama huku akiongeza umakini zaidi, akaiokota bahasha ile.Akatizama huku na huko,asimuone mtu yeyote mahala pale, hata Yule "mteja mtu mzima"hakuonekana eneo lile!
Akatoa funguo za mlango, akafungua akaingia ndani.Alikagua kila kitu muhimu mle ndani kwake,akaviona vimekaa, kama alivyoviweka,hakukuwa na badiliko lolote.

Inspekta Jamila,aliifungua ile bahasha, akakutana na kipande cha karatasi, kilichoandikwa kwa mkono, tena kwa maandishi mekungu, kilichoandikwa "SHANKARA!" Alikisoma tena na tena, lakini hakuelewa maana yake,sasa akawa yupo katika tafakari nzito, akazama katika dimbwi la mawazo, akagutushwa na mlio wa simu yake.

"Halow Dokta?"
Ilikuwa ni simu ya Shoga yake Dokta Zahara.
"Vipi mbona kimya hunambii kama huko ni salama? Kwani roho yangu nimeitundika hapa kama mkungu wa ndizi sina amani?!"
"Mmmmh shoga, sijui niseme salama, au nisemeje, manaake hapa nimepagawa kwelikweli, kifupi nipo salama, ila kuna jambo halipo sawa!"
"Duuuh pole sana shoga, kama huko hakuko sawa beba nguo zako, uje ukae huku, hao wanaharamu wasije kukutoa roho bure!"


"Nikifa kazini,itakuwa heshima kubwa kwangu na familia yangu, ila sitorudi nyuma Dokta, nitapambana hadi hatua ya mwisho, mimi ni askari niliepasi chuoni kwa nadharia na vitendo, sikupita kule kwa njia mkato!"

Inspekta Jamila alijibu majibu ya kishujaa, akakata simu, akabadilisha nguo na kutoka, kuelekea kazini kwake, tayari kwa majukumu, ya siku ile!

Asubuhi ile, bado foleni ilikuwa haijachanganya, hivyo ilimchukua dakika ishirini tu hadi kufika ofisini kwake.

Ilipotimu saa mbili kamili juu ya alama Afande Kubuta nae aliwasili, ofisini kwao, akiwa yupo tayari kwa maelezo ya kazi aliyokuwa ameifatilia.

"Ndiyo Afande, lete taarifa!"
Inspekta Jamila, alianzisha mazungumzo yale, huku akitaka kujua kilichojili.


"Kiongozi kama nilivyowahi kusema, Bitoz alikuwa mpenzi wake Hamida, ila hajui chochote kuhusu kesi hii, tunayoifatilia, kwani nimetumia mbinu, zote za kuhoji, lakini jamaa hakuonyesha maelezo tofauti yenye shaka hata kidogo!"


Inspekta Jamila, alimsikiliza Afande Kubuta kwa umakini, kisha akatingisha kichwa chake kukubaliana, na maelezo yale.


"Sasa leo ni Jumamosi, hivyo andaa jalada la mke wa Dokta Masawe, ili jumatatu apande kizimbani, hatuna sababu ya kukaa nae!"
Inpekta Jamila, baada ya kusema maneno yale, alitoa ule waraka alioukuta nyumbani kwake asubuhi ile, na kumpa Afande Kubuta kisha akamwambia.
"Unaelewa nini juu ya neon hilo?"


"SHANKARA?!"
Alisema Afande kubuta, kwa mfumo wa kuuliza, na kushangaa!
Inspekta Jamila, yeye alikuwa ametulia makini, akimtazama usoni msaidizi wake,katika namna ya kumsoma!
Sasa ikawa zamu ya Afande Kubuta,kuzama katika lindi la mawazo.
"Nini hii?! Na umeipata wapi?" Sasa ikawa zamu ya Afande Kubuta kuuliza.
"Huo waraka, nimeukuta leo mlangoni kwangu! Alieuweka simjui, wala una maana gani vilevile sitambui, ila lazima kuna maana, tena ni kubwa sana!"
Inspekta Jamila, alimueleza msaidizi wake kutokulala kwake ile jana, kwa simu ya Geradi Mwaipopo, hadi asubuhi alipokwenda kukagua nyumba yake, alipoukuta huo waraka, ila hakuthubutu kumweleza mahali, alipolala!


***SHANKARA nd'o nini??
 
Jamila vs Jeradi... Patamu hapa.
Asante Casuist
^^
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Casuist leo umetufungia kazi,SHANKARA bila shaka ni huyo mchumaba wake Jamila.:smash:
 
Ahaa, Krimasi inakuja vizuri tunapokuwa na masimulizi ya kusisimua kama haya.
 
Back
Top Bottom