Usijali japo hamna siku uliosema ndefu....
Kumbe like maana yake ni ndefu! Usipoweka fupi!Hahahaa sio kweli....siku zingine nagongaga like kimyakimya
Kumbe like maana yake ni ndefu! Usipoweka fupi!
Ntaiweka baada ya dakika chache...
Ukiwa na mke kama Jamila, usimchokoze! Waweza kugeuzwa vipande vya mshikaki ivi ivi unajiona.
yani nimedata na hii story....yani imekuwa nikiingia humu naisaka hii tu...zingine naona hazifikii utam wa hii.Ahsante bro Casuist...tupo pamoja kam matope na maji!RIWAYA: BARUA KUTOKA JELA
MTUNZI: IBRAHIM GAMA
SEHEMU YA KUMI NA MBILIIGP alihitimisha suala la Mwaduga Dingo.
Inspekta Jamila na mkuu wake wa kazi walipanga mikakati ya namna ya kushinda kesi ile kwa ushahidi usio na chembe ya shaka, kisha wakaletewa chakula mlemle ofisini wakala, walipomaliza kula ilikuwa imeshatimu saa mbili za asiku!
Sasa wewe nenda ukapumzike kazi nzuri sana uliyoifanya katika siku ya leo, na kama ulivyopendekeza katika ripoti yako, Afande Kubuta awe ndiyo askari utakaeshirikiana nae, hilo litakamilika na usiku huu yeye ndiye atakaekwenda kumkamata Dokta Masawe nyumbani kwake.
IGP akaagana na Inspekta Jamila ambae alikuwa amechafuka na amechoka, huku yeye akiinua simu na kumtafuta Afande Kubuta na kumwita ofisini kwake usiku uleule!
Afande Kubuta alipofika alipewa mikakati yote ya kazi inayotakiwa kufanyika usiku ule, pia atafanya kazi ile akiwa chini ya Inspekta Jamila, na atatoa ripoti ya kazi yake kwa Inspekta Jamila, huku akisisitiziwa kwamba kwa kipindi hiki chote watakachokuwa wanashughulikia kesi ile, hatakiwi kujihusisha na kesi nyingine yoyote, na mkuu wake wa kituo atafahamishwa suala lile.
Inspekta Jamila alipofika nyumbani kwake alikwenda kuoga ili kupunguza uchovu, kisha akavaa kaptula na fulana nyepesi, akaisogelea Compyuta yake nakuchukua simu yake akachomeka waya kwenye simu, na upande mwingine akachomeka kwenye Compyuta.
Akawasha Compyuta na kufungua faili maalum, na baada ya muda picha za video zikawa zinaonekana.
Zilikuwa ni zile picha alizokuwa akiwarekodi Dokta Masawe na wenzake bila wao kutambua, kiasi alikuwa akionekana kama limbukeni wa simu!
Alihamisha picha zile za video kutoka kwenye simu, nakuingiza kweye Compyuta kisha hakuishia hapo, alizitoa zile picha kutoka kwenye Compyuta akazituma kwenye FLASH DISC kisha akazifuta kutoka kwenye simu yake ya mkononi.
Mara simu yake ikawa inaita alipoitazama namba ya simu ile, ilikuwa ni namba ya Dokta Zahala.
Vipi shoga upo Nyumbani?
Dokta Zahala aliuliza baada ya kupokelewa ile simu.
Ndiyo Dokta vipi una habari nyingine, manaake shoga wishi habari kama Idara ya habari maelezo!
Inspekta Jamila alianzisha utani kwa rafiki yake kipenzi.
Nitakosa wapi habari wakati mie ni Salatul Habari? Washa sasa hivi TV stesheni ya ITV uone vitu!
Inspekta Jamila akafanya kama alivyoambiwa na shoga yake, akaona taarifa ya habari ya saa nne usiku ikiendelea, ikionyesha lile gari lililoanguka baada ya Inspekta Jamila kulishambulia, katika lile tukio la pale Friends Corner Hotel.
Pia baadhi ya watu wakihojiwa tukio lilivyotokea, huku kila mtu akisema lake!
Jambo lile lilimchukiza sana Inspekta Jamila, kwani litaharibu upelelezi wa kesi hasa wale majambazi watakapoona taarifa ile au usikia.
*******
Dokta Masawe akiwa nyumbani kwake, aliangalia habari ile kwa makini, huku moyo ukimuenda mbio! Kwani hakuamini hata kidogo kama yule mwanamke aliekuwa akiongea nae ni Askari polisi.
Mimi nilikuwa mle hotelini nakunywa, yule dada alipoingia pale nilimuagiza muhudumu ampe ofa ya chupa mbili, za kinywaji alichokuwa anakunywa! Alipotoka nilikuwa namfatilia kule nje, ndiyo nikakutana na kasheshe aisee! Yule dada anapiga Karate bwa shee usisikie!
Alikuwa ni jamaa aliekuepo eneo la tukio akitoa ushuhuda kwa aliyoyaona. Na ndiye aliemfungua macho Dokta Masawe, lakini akimuudhi Inspekta Jamila!
Kwani alijua kuwa kwa vyovyote vile wale majambazi wanaweza kuona taarifa ile waka kimbia!
*******
Saa tisa kamili ya usiku, Afande Kubuta alikuwa na askari wengine saba, walikuwa katika Gari yao ya polisi aina ya Land Rover 110 Defender.
Walikuwa wameiegesha gari yao katika Baa ya Patchoto pale Kinondoni, wakiwa jirani kabisa na nyumba ya Dokta Masawe.
Wale askari wakiwa na silaha aina ya SMG walitelemka katika gari ile, na kwenda kuizingira nyumba ya Dokta Masawe!
Afande Kubuta yeye alikuwa anamuhoji mlinzi wa Baa ile, ili amtajie anapoishi, mjumbe wa Shina wa mtaa ule.
Yule mlinzi akamuelekeza katika nyumba moja ya kota iliyokarabatiwa vizuri, na Afande Kubuta bila ya kupoteza muda, alikwenda kubisha hodi katika nyumba ile.
Ndugu Mjube mimi ni Mwana Usalama, naomba utoke nje ili tuzungumze.
Afande Kubuta alijitambulisha, na baada ya muda yule mjumbe aliekuwa anatambulika kwa jina la Mohamedi Mwinyi Kheri alitoka huku akiwa na mashaka!
Vipi mbona usiku jamani! Kumetokea nini katika Mtaa wangu?
Mjumbe Bwana Mohamedi Mwinyi Kheri alimuuliza yule afande aliekuwa amevaa koti la kipolisi.
Samahani Ndugu mjumbe kwa kukusumbua saa hizi ukiwa umepumzika, ila tunakuhitaji kwani katika mtaa huu, tunataka kuingia kwenye nyumba ya Dokta Masawe ili tumpekuwe katika nyumba yake, lakini pia twende nae kituoni kwa mahojiano zaidi, hivyo nataka uwe shahidi tutapokuwa tunafanya hivyo.
Afande Kubuta alimwambia Mjumbe wa nyumba kumi Bwana Mohamed Mwinyi Kheri. Na dakika tatu baadaye wanaume wale walikuwa ndani ya nyumba ya Dokta Masawe.
Dokta Masawe hakuwemo mle ndani toka saa nne na nusu ya usiku!
Alipokwisha kuangalia taarifa ya habari, walikuja wenzie wakamfuata!
Yalikuwa ni majibu ya Mke wa Dokta Masawe ambayo yalimwacha hoi bin taabani Afande Kubuta na vijana alioongozana nao!
Je alikuaga kuwa anakwenda wapi? Afande Kubuta alimuuliza yule Mama wa kichaga mke wa Dokta Masawe.
Hapana kwa kweli Babangu, hakusema anakwenda wa..wapi kweli. Yeye alisema anatoka mara moja hatochelewa kurudi ila sisi tufunge milango, atakaporudi atatugongea!
Mke wa Dokta Masawe, alikuwa akiongea kwa lafudhi ya kichaga, alikuwa anajibu akiwa na uhakika na majibu yake.
Afande Kubuta alikuwa amehemewa! Kwani sasa mambo yote yalikuwa yameelekea kwenda kombo.
Sasa?!
Hakuna cha sasa, hapa tutamsubiri hadi asubuhi, mjumbe wewe nenda kapumzike, huyu bwana atakaporudi tutakwita!
Yalikuwa ni majibu ya Afande Kubuta alipokuwa anamjibu mke wa Dokta Masawe aliposema sasa, akiwa anataka kujua kinachoendelea!
Humu ndani ya nyumba yangu hamtosubiri peke yenu, labda awepo na mjumbe, kwani pia mtu mliyemfata hamkumkuta, hata mlipoingia vyumbani kumtazama hamkumuona sasa mtabakiaje humu?!
Mke wa Dokta Masawe alikuja juu akiwa amekasirika, asionyeshe woga hata kidogo!
Samahani jamani sio kama naingilia kazi yenu, ila huyu mkewe ampigie simu mumewe amuulize alipo nasi tutajua chakufanya!
Mjumbe alitoa rai na mke wa Dokta Masawe akajibu mara moja
Simu yangu haina Dola mzee!
Afande Kubuta akatoa simu yake akataka namba ya simu ya Dokta Masawe, Mke wa Dokta Masawe alichukua Business Card pale sebuleni walipokuwa wamekaa nakumpa Afande Kubuta.
Afande Kubuta aliipiga namba ile zaidi ya mara tano lakini ilikuwa haipatikani ilikuwa imefungwa!
Lakini kwani mume wangu amefanya nini?
Mke wa Dokta Masawe alitaka kujua, kwani mumewe haijawahi kutokea hata mara moja akafatwa na polisi namna vile, kwake kilikuwa ni kitu cha ajabu sana.
Lakini hakuna askari yeyote kati ya wale sita waliokuwa mle ndani, nadhani hata askari wa saba aliebaki kwenye gari ambae ni Dereva kama angeweza kumueleza yule mama, mumewe alichofanya!
Hata Mjumbe Bwana Mohamed Mwinyi Kheri alipoamua kubaki na wale askari nyumbani kwa jirani yake, hakuwa Dokta Masawe wala simu yake aliepatikana mpaka jua likawapambazukia.
Wana Usalama wale wakaondoka na mjumbe wa shina huku wakiwa patupu!
Siku ya jumanne saa mbili asubuhi Inspekta Jamila alikuwa yupo Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili kwa mambo mawili.
Kwanza kuchukua maelezo ya wagonjwa wake!
Pili kumkamata Dokta Masawe kwa mikono yake, baada ya Afande Kubuta kumpa taarifa kwa ufupi kupitia njia ya simu kuwa hawakufanikiwa kumtia mbaloni, kwani hakulala nyumbani kwake!
Dokta Masawe huwa ana Clinic siku ya jumanne pale muhimbili, kitengo cha MOI.
Hivyo kwa vyovyote vile angekwenda kazini tu, na yeye angemtia mikononi kiulaini!
Akaamua aanzie katika wodi ya Kibasila walipokuwa wale majeruhi wake waliolala na pingu mikononi mwao.
Jibu alilolipata huko lilimrudisha nyuma hatua hamsini kikazi!
Ninasikitika Afande tumejaribu kuokoa maisha ya hawa wagojwa bila mafanikio, kwani huyu mmoja moyo wake ulikuwa umepasuka na kumwaga damu nyingi ndani kwa ndani. Lakini hata katika kichwa chake amepata athali kubwa, kwani ubongo wake wa nyuma katika kisogo MEDULA OBLANGATA ulivurugika na damu, hivyo katika hali kama hiyo mtu hawezi kuishi; huyu alifariki dakika ishirini toka kufikishwa hapa!
Daktari aliekuwa anawatibia wale jamaa wawili alikuwa anamfahamisha Inspekta Jamila namna ya yule jamaa aliepambana nae namna alivyokuwa ameumia na kupelekea kifo chake, akalikumbuka teke lake aina ya MAIGERI, lilivyotua usawa wa kifua na jinsi yule jamaa alivyoangukia kisogo.
Mara moja akatambua Medula Oblangata pale ndipo ilipochokozwa!
Dah nimekuelewa Daktari je na yule mwenzake nae vipi?
Inspekta Jamila alitaka kujua kuhusu yule jambazi aliyepinduka na gari baada ya yeye kupiga mipira yote miwili ya nyuma ya gari ile kwa risasi na kupelekea kupinduka kwa gari ile.
Yule nae alifariki saa mbili baadae tangu alipofikishwa hapa. Yule alikuwa na tatizo la kukosa hewa kwani mbavu zake sita zilivunjika, tatu kila upande na hata kama angepona asingefanya kazi yoyote yule!
Hiyo ilikuwa ni ripoti ya Daktari aliekuwa akiwahudumia wagonjwa wale toka walipofikishwa Hospitalini pale jana yake.
Inspekta Jamila alipelekwa hadi katika chumba cha kuhifadhia maiti pale Muhimbili na kuonyeshwa maiti zile, na akawatambua na akawapiga picha katika nyuso zao!
Kiasi Roho ya Inspekta Jamila iliingia simanzi kidogo alipoiona ile maiti ya yule jamaa aliemwambia UHAI WAKO NIMEUSHIKA UPO MKONONI MWANGU
Inspekta Jamila alitoka katika wodi ya Kibasila na kuelekea Moi, ofisini kwa Dokta Masawe, alisubiri sana, sasa akiwa yupo katika benchi walilokalia wagonjwa waliokuwa wanasubiri huduma ya Dokta Masawe, lakini hadi inatimu saa nne kulikuwa hakuna dalili za Dokta Masawe bali daktari mwingine aliingia kwa dharula na kuwahudumia wagonjwa!
***USHAHIDI mkuu alioutegemea Jamila ndo huo hauna maana tena ..nini kitaendelea
Jagarld Jullie Z Sangomwile Khantwe Mr Rocky Gunda66 Himidini VAN HEIST BPM ABUBAKAR SHEKAU NYIROmamsapkhan born again pagan princetx Ennie mcubic jonnie_vincy slim5 MAVUNO mp anold amoneyazan