Riwaya: Barua Kutoka Jela

Riwaya: Barua Kutoka Jela

Mwacheni casuits ale x mass akimaliza atatumwagia u tamu
 
Kwan nimefanya nini ?mbona najiona Niko sawa kaka slim 5
miss nuru wala hujankosea dadangu, kuna mstari uliuandika hapo nyuma unasomeka hv:
"Jaman mbona kimnya"
Hilo neno la mwisho ndio uliangalie vzr! miss nuru xmass inaisha ht krb ya utani hamna!
 
Last edited by a moderator:
Askari wale wakapanga na kupangua, hadi saa nane mchana. Walipeana mikakati ya kufanya, ili kushinda kesi ile kwa kishindo.
"Sasa naona leo hapa tulipofika,siyo pabaya sana, itabidi tufunge kazi kwa leo, ila kama ujuavyo, askari muda wote yupo kazini!
Hivyo tunaweza kuitana muda wowote ule!"
Inpekta Jamila alimwambia msaidizi wake, kisha ule waraka akaufungia katika droo ya meza yake, akaendelea kusema.
"Leo usiku nina mgeni anaingia kutoka ughaibuni, ambae ndiye dakitari wa mwili wangu, nyonda mkalia ini wangu, kipenzi cha roho yangu!"
Inspekta Jamila alikuwa akizungumza huku akitabasamu, na kumfanya Sajenti kubuta nae kuwa katika hali ile ya kutabasamu!
"Haya sasa mie nifanyeje Afande?"
Sajenti Kubuta alisema maneno hayo huku nae akiwa anatabasamu.
"Nataka uniambie duka, wifi yangu anaponunulia Msio, kwani nataka kumsinga Bwana,najua ameyakosa mambo haya muda mrefu"
"Hahaha Afande Msio ndiyo nini? Kwani ndiyo kwanza nakusikia wewe hilo neno!"
"Heee makubwa haya, wewe hujui msio?! Tuseme huyo wifi yangu huko nyumbani kwako, hajawahi kukusinga?!"
Inspekta Jamila alimuuliza msaidizi wake, huku akimshangaa!
"Hawa wanawake wenzangu, baadhi yao wamezidi, yaani unakaa na mume au bwana, hujawahi kumsinga hata siku moja, ukamwimbia nyimbo za mahaba, ukamtuliza ndani, hakika unyago ni kitu muhimu sana kwa wanawake!"
"Basi niletee huyo wifi yangu, nikaenae walau siku tatu tu, atabadilika huyo!"
Wote wakaangua kicheko kisha wakaagana.

……………
SEHEMU YA 21 INAENDELEA
Ilikuwa saa nne za usiku, Inspekta Jamila, alikuwa anakaribia uwanja wa ndege wa kimataifa wa JULIUS KAMBARAGE NYERERE,alipokuwa akikata kona ya kuingia katika uwanja wa ndege, akiiacha ile barabara ya Pugu, mara macho yake yakamvuta kumtizama muokota chupa na vyuma chakavu, aliekuwa amesimama pale kona katika njia ya kutokea uwanjani, akiwa na kiroba na nguo chakavu!
Inpekta Jamila akasimamisha gari ili amtizame sawasawa, akasikia kelele za tairi kutoka nyuma, zilizokuwa zinasuguana kwa breki,iliyokanyagwa ghafla!
Inspekta Jamila, haraka alikanyaga mafuta gari yake, nakuokoa ajali ambayo angeisababisha yeye, kwa kusimama ghafla Barabarani.
Ile gari ya nyuma ilitanua kulia, ikasimama sawasawa na gari yake. Dereva wa ile gari alishusha kioo, akatazamana na Inspekta Jamila, huku dereva Yule akiwa amefura kwa hasira, alimuonyesha vidole vya kati vya mikono yake yote miwili, kisha akapandisha kioo akaondoa gari,kuelekea kwenye geti na kuchukua kadi maalum, akaiingiza gari yake katika maegesho akaiegesha na kushuka, akaendelea na hamsini zake!
Inpekta Jamila, pale alipo aliishuhudia ile gari dereva wake aliemtusi,ikiondoka mbele yake, akaiandika namba ya gari ile. Nae akasogeza gari yake hadi pale kwenye lile geti, akachukua kadi nakwenda kuiegesha gari yake, kisha kwa mwendo wa haraka, alitembea ili kumuwahi Yule muokota chupa na vyuma chakavu.
Inspekta Jamila, alitazama eneo lote la pale alipomuona Yule bwana muokota chupa na vyuma chakavu, alipokuwa amesimama awali, lakini hakumuona!
Akavuka barabara hadi pale kituo cha basi, chakuendea mjini, pia hakumuona, kichwa chake kikaanza kuchanganyikiwa!
Kinachanganyikiwa kwa sababu, hakuna waokota vyupa na vyuma chakavu, wanapokuwa kazini, wakapanda gari, kwani hivyo vitu wanavyookota watavipataje?
Pia hakuna waokota vyupa na vyuma chakavu, wanaofanya kazi zao usiku kama ule!
Lakini pia Muokota vyupa na vyuma chakavu huyu, aliemuona muda mfupi uliopita, ndiye aliemuona asubuhi, maeneo ya nyumbani kwake Ilala mtaa wa Songea!
Inspekta Jamila, alirudi uwanja wa ndege ili kuendelea na jambo lililompeleka pale, lakini fikira zake, zikianza kumtilia mashaka Yule bwana.
Alikwenda mpaka katika maegesho lilipokuwa gari lake, akaikagua gari yake, ikawa ipo salama kabisa.
Akaelekea pale wanapokaa watu kuwasubiri abiria, mara wakasikia tangazo kupitia vipaza sauti vilivyokuwa pale uwanjani kuwa, ndege iliyotarajiwa kufika muda ule, imefika salama, na watu wakaanza kujongea, karibu na mlango ule mkuu wa kutokea wageni, ili kuwapokea wageni wao, huku wengine wakiwa na mabango madogomadogo, yaliyoandikwa majina ya wageni wao,
Ili mgeni iwe rahisi kwake, kumtambua mwenyeji wake, hasa ikiwa hawajawahi kuonana ana kwa ana!
Inspekta Jamila, alikuwa makini na kila aliekuwa akitoka katika mlango ule, na mara, akamuona mtu wake aliekwenda kumpokea, akamkumbatia na kumbusu, kisha akamwambia.
"Karibu nyumbani mpenzi wangu."
"Asante nishakaribia mpenzi"
Alijibu mgeni Yule, Shani Karama Rashidi.
Inspekta Jamila, alisaidiana mizigo na mpenzi wake, wakaenda kwenye gari yake, akapakia mizigo ndani ya gari yake, akajipakia upande wa dereva, na Shani upande wa abiria, safari ikaanza kuelekea mjini.
Baada ya gari ya Inspekta Jamila, kuondoka eneo lile, huku nyuma gari ndogo nyeupe, ilikuwa ikimfatilia kwa mbali!
"Sweety nimekodi hotel,ya Kibodya ile ya mtaa wa Nkruma, ili tupumzike mahala pale!"
Inspekta Jamila, alimwambia mpenzi wake, huku akiwa makini katika usukani.
"Alaa kama umeamua hivyo, hakuna tatizo, kwani mfungwa hachagui gereza, nami kwako ni kama mfungwa wa mapenzi kwako!"
Walitabasamu kwa pamoja, huku wakiwa wameshafika katika taa za Tazara. Usiku ule barabara zilikuwa hazina foleni.
Hatimae wakafika Kibodya Hotel,wakateremka na mizigo baadhi, wakaingia hotelini, Inspekta Jamila, alichukua funguo mapokezi, na kwenda hadi katika chumba alichopanga, akafungua mlango huku akitamka.
"Karibu waukweli, mimi nashuka chini, kumalizia mizigo kwenye gari." Inspekta Jamila, alimbusu mdomoni mpenzi wake, akashusha ngazi, kuelekea nje ya Hotel ile.
Inpekta Jamila, alifungua mlango wa gari ili atoe mizigo iliyobakia, mara akajihisi hakuwa peke yake mahala pale!
Akageuka nyuma ili ajiridhishe fikira zake, lakini hakuweza kumaliza mzunguko wa shingo yake, kwani kitu chenye ugumu kama wa ubao, kilitua usawa wa kichogoni kwa pigo moja, lililopigwa kiufundi na mpigaji, na Inspekta Jamila, alianguka mle ndani ya gari kama mzigo, akapoteza fahamu.
Inspekta Jamila, alipokuja kutanabahi, alijikuta amefungwa kamba katika kiti cha chuma, akiwa amezingilishwa kamba kutoka mabegani hadi kiunoni, huku mikono yake ikiwa imefungwa kwa nyuma na kamba zile, bila kusahau miguu yake, ambayo pia ilitatalizwa kwa kamba zile za nyloni, huku akiwa amekalishwa katika kiti kile!
Ama kwa hakika alikuwa amepatikana khaswa.
"Thatha mkubwa,huyu dem tumalidhe, au tumtie ulemavu wa maisha, kwani huyu mpumbavu thana."
Inspekta Jamila, aliyasikia mazungumzo yale, ya Yule mtu aliekuwa akizungumza na simu, ili kupata maelekezo, kutoka kwa huyo aliekuwa akizungumza nae.
Ila kitu kilichomfanya sasa ainue kichwa chake na kumtizama Yule mtu aliekuwa akizungumza na simu,ni ile lafidhi ya Kithethe!
Alitazamana na mtu Yule, kisha akaona pia na watu wengine wawili, wakiwa mle.
Nao pia walikuwa wakimtazama, ingawa wale jamaa, wao walimtazama kwa dharau na kedi ya hali ya juu!
Inspekta Jamila, akiwa pale kitini alipofungwa kamba, aligeuza uso wake, na kutazama kulia na kushoto kwake, hakuona watu wengine zaidi ya hawa watatu, waliokuwa wamesimama mbele yake.
Alikuwa katika chumba kikubwa, ambacho hakikuwa na kitu chochote zaidi ya kile kiti cha chuma, alichofungwa nacho!
"Nimekuelewa bothi, thithi tunamalidha kabitha."
Yule bwana anaezungumza kwa kithethe, alihitimisha mazungumzo yake, akakata simu.
Akapiga hatua kubwa mbele, akamnyooshea bastola aliyokuwa ameishika mkono wake wa kulia, huku akitumbukiza simu yake mfukoni kwa mkono wake wa kushoto.
Inspekta Jamila, akawa anaswali kimoyomoyo, kumuomba mungu wake, amnusuru na mkono ule wa mauti, wa madhalimu wale, akawatazama wale jamaa wengine wawili, akawaona wote kwa pamoja, wanampungia mkono wa kwaheri! Aligeuza shingo yake, upande ili asiwaone wale jamaa wanaomdhihaki, macho yake yakatazama upande wa kulia, akauona mlango.
Akiwa katika kuutizama ule mlango,mara akasikia Yule jamaa wa kithethe, akiipandisha risasi kutoka katika megazin yake, na kuipeleka chemba tayari kwa kuiruhusu itoke, ili kufanya kazi aliyoikusudia!
Inspekta Jamila, aliuona ule mlango, kitasa chake, kikiwa kinashuka chini!
Akafumba macho huku machozi yakimtiririka mashavuni mwake.
Milio ya risasi, ilisikika ikihanikiza katika chumba kile kwa sekunde kadhaa, kisha ukimya ukatawala mle ndani, huku damu zikisambaa kwa wingi, kiasi khaswa unaweza kusema, kile kilikuwa chumba cha mauti!
*** NINI KIMEJIRI?!***
 
SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI

Akiwa katika kuutizama ule mlango,mara akasikia Yule jamaa wa kithethe, akiipandisha risasi kutoka katika megazin yake, na kuipeleka chemba tayari kwa kuiruhusu itoke, ili kufanya kazi aliyoikusudia!
Inspekta Jamila, aliuona ule mlango, kitasa chake, kikiwa kinashuka chini!
Akafumba macho huku machozi yakimtiririka mashavuni mwake.
Milio ya risasi, ilisikika ikihanikiza katika chumba kile kwa sekunde kadhaa, kisha ukimya ukatawala mle ndani, huku damu zikisambaa kwa wingi, kiasi khaswa unaweza kusema, kile kilikuwa chumba cha mauti!
Inspekta Jamila, alifumbua macho yake,akamuona mtu aliekuwa amevaa mask katika uso wake, akimfungua kamba ambazo sasa zilikuwa zinamuumiza mwilini mwake.
Akatizama pale chini, akawaona Kithethe akiwa na bastola mkononi, na wenzie wale wawili, wakiwa wamelala chini damu zikiwatoka kwa wingi mwilini mwao, wakiwa wamesambaratisha mikono na miguu, hawana dalili ya uhai!
Baada ya kufunguliwa kamba, Inspekta Jamila akasimama huku akimshukuru mungu, pia akawa anajinyoosha viungo vyake.
Hamadi?!
Inspekta Jamila, alipigwa kibao cha kelbu katika shavu lake, akahisi maumivu makubwa!
(KIBAO CHA KELBU, NI MKONO UNAOPIGIWA NYUMA YA KIGANJA)
Alipokuja kurudisha uso wake, akamuona yule mtu aliemfungua kamba,ambae ndiye aliyempiga, akiivua ile mask usoni mwake, huku akiwa amempa mgongo Inspekta Jamila,na yule bwana alipogeuka, Inspekta Jamila, akawa anatazamana uso kwa uso na Jeradi Mwaipopo au kifupi JM!
Inspekta Jamila, alitaharuki kupita maelezo, kisha kwa fadhaa akajikuta akitamka
"JM?!"
"Yes, my name!"
Jeradi Mwaipopo aliitikia kidharau, huku akimtizama usoni bila kupepesa macho!
Kisha akaendelea.
"Bila shaka leo tumekutana, Inspeka Jamila"
"Naam hakika, leo tumekutana, tena tukiwa wawili, bila shaka leo, utaweza kunieleza kwa nini upo upande huu!"
Inspekta Jamila, alimwambia Jeradi Mwaipopo, huku akiwa anachua shavu lake!
"Unajua leo ulikuwa tayari ni marehemu? Je ungewezaje kujua kwa nini nipo upande huu?!"
JM alimwambia Inspekta Jamila, huku akiwa anamtazama usoni moja kwa moja!
"Sina ubishi juu ya hilo, kuwa mungu angetaka, leo ningekuwa marehemu, ila naona ameniokoa na kifo kile cha udhalili, kupitia mikononi mwako JM!"
Inspekta Jamila, alimjibu JM, katika namna ya kuvuta muda, lakini pia kukusanya nguvu.
"Afande mimi, sijakuokoa na kifo, ila nimetaka mimi, ndiyo nikuuwe, na siyo hao marehemu wenzako, waliyokutangulia!"
JM, alikuwa akisema maneno hayo huku, kwa mkono ule uliokuwa umeshika silaha, akiinyooshea miili ya marehemu wale watatu, ambao sasa damu zilizokuwa zikiwamwagika, sasa zilianza kuganda!
Inspekta Jamila, alimtizama JM, usoni mwake, akagundua kuwa hakika alikuwa hatanii hata kidogo!
"Sasa JM, hata kama utaniuwa mimi, bado na wewe utakufa vilevile, ama utauwawa!"
Inspekta Jamila, alikuwa akimsemesha JM, ili kupoteza muda, asaakheri huwenda akapata namna ya kujinusuru, kutoka katika mikono ya mtu mbaya, kabisa alieacha zahma kubwa, katika mwenendo wa kesi ile.
"Mimi sitojali, kama nitakufa, ila nakuhakikishia umeingia kwenye mtego wa panya, na leo umenasa kisawasawa!"
JM muda wote alikuwa akimtazama usoni, Inspekta Jamila, kumsoma mawazo yake bila shaka.
"Sasa JM, sivibaya ukanieleza walau kwa ufupi, sababu khaswa zilizokupelekea, wewe kugeuka na kuwa upande mwengine?!"
Inspekta Jamila alisema maneno haya,huku akionesha utiifu, mkubwa kwa JM aliekuwa ameshikilia silaha ya moto kwa ujasiri mkubwa.
"Afande sina muda wa kupoteza hapa, naona unanikawiza kufanya azma yangu, lakini nitakwambia ili ukawaeleze huko kuzimu!"
JM alisema maneno hayo, kisha akamwemwesa kidogo, akaendelea.
"Kama nilivyokwisha kusema, katika Jeshi la Polisi, kuna baadhi ya viongozi, wameligeuza jeshi hili, kuwa kama mali yao binafsi.
Kwani wapo watu wanalitumikia jeshi, kwa miaka na miaka, lakini hawapandishwi vyeo!
Lakini pia wapo watu wanalipwa mishahara mikubwa kuliko watendaji halisi wa kazi husika!
Hao baadhi ya viongozi, wamekuwa wakijihusisha na mambo haramu, na mimi nilipokamata, nikaambiwa naingilia miradi ya watu!
Mwisho nikafanyiwa zengwe, nakusingiziwa kuwa najihusisha na uhalifu, na nikafukuzwa jeshi, na leo hii, familia yangu nimeirudisha nyumbani Mbeya, ikiwa hohehahe!"
JM aliposema maneno hayo, huzuni, hasira, na dukuduku lilimjaa moyoni mwake, akajikuta akilia kwa uchungu huku akisema.
"Nachukia kazi ya Polisi, na nawachukia Polisi, kwani hao ndiyo walionifikisha hapa leo, wao ndiyo waliotoa picha yangu katika magazeti, nakuniharibia, hadi nimekuwa siwezi kupata ajira mahala popote ndani ya nchi hii, nikikomeshwa na wakubwa, wanaojali masilahi yao binafsi, wao na familia zao, wakati wakina JM, wakitaabika kwa kuwa tu, walikuwa wakitekeleza majukumu yao sawasawa!"
Jeradi Mwaipopo alikuwa akitafuna meno yake kwa hasira, na mara akainua mkono wake uliokuwa umeshika silaha, akamuelekezea Inspekta Jamila, ili kutimiza dhamira yake ya kuua!
"No JM. Wewe mtoto wa kiume, hivyo hupaswi kumuua mwanamke kwa risasi, tumia mikono yako bwana, unakuwa dhaifu mbona?!"
Inpekta Jamila, alikuwa akimpandisha jazba JM, lakini pia akimshusha, ili tu asiweze kuuliwa na risasi.
"Kwa hiyo wewe unataka kupigana na mimi siyo?!"
JM alimuuliza Inspekta Jamila kwa dharau ya hali ya juu!
"Bila shaka JM, kwani mimi sina silaha yoyote mwilini mwangu, kwa nini wewe utumie silaha?! Kama kweli unajiamini, na unajiona ni mwanaume hasa, tupa silaha chini, tupange mtu mbili mimi na wewe!"
Inspekta Jamila, alikuwa akimtia hasira JM, ili ahamaki, na hatimae atupe silaha chini.
Naam bila wasiwasi, JM aliinama na kuiweka silaha yake shini, akawa amempa ubabu Inspekta Jamila, na aliposimama juu huku akiwa bado yupo ubavu, JM alirusha teke aina ya YOKO GELI, likatua ubavuni mwa Inspekta Jamila, na kumfanya apepesuke nusura adondoke chini. (YOKO GELI.NI TEKE LAKUSITUKIZA, LINALOPIGWA UBAVU, ADUI ANAPOKUWA AMEKAA UBAVUNI MWAKO!) Inspekta Jamila alipata maumivu kwenye mbavu zake, lau kama si kubana pumzi alipopigwa teke lile, bila shaka angevunja mbavu zake.
Baada ya kukaa sawa, akawa anatazamana uso kwa uso na JM. Ispekta Jamila, akagundua kuwa mtu anaepambana nae, siyo mtu wa mchezo hata kidogo.
Hivyo alikaa katika mkao wa kupambana na mjuzi mwezie.
JM alipomuona Inspekta Jamila, amekunja ngumi huku mguu mmoja, akiwa ameutanguliza mbele, alirusha teke linguine, safari hii, akirusha teke aina ya MAWASHI GELI. (MAWASHI GELI, NI TEKE LINALOPIGWA KUTUMIA FUNIKA, HUKU LIKIZUNGUKA, NA LINAPIGWA USAWA WA SHINGO YA ADUI.)
Inspekta Jamila, aliliona teke lile, hivyo akachanuka msamba, teke lile likawa linapita juu yake.
Inspekta Jamila, hakufanya ajizi, palepale alipokaa msamba, alipiga ngumi moja maridadi aina ya GEDAN NZUKI katika korodani za JM, na akatoa mguno mkali kwa maumivu, lakini pia akiinama na kushikilia korodani zake, huku akirukaruka mwa maumivu(GEDAN NZUKI, NI NGUMI INAYOPIGWA USAWA WA KORODANI, NA KITOVU) Inspekta Jamila, alipomuona JM amepoteza kujilinda kwa maumivu aliyompa, aliinuka pale chini haraka, akapeleka ngumi nyingine aina ya SEDAN NZUKI, Jm akapiga yowe kubwa la maumivu, huku sasa mkono mmoja, ukiwa kwenye korodani, na mkono wa pili, akishika kifua chake, usawa wa chembe.(SEDAN NZUKI, NI NGUMI INAYOPIGWA USAWA WA CHEMBE) Akawa ameuacha uso wake, alioukunja kwa maumivu ukimtazama.
Inspekta Jamila, hakuremba akapeleka ngumi ya tatu, safari hii akipiga ngumi aina ya JODAN NZUKI.
Ikawa imemlewesha JM akawa anayumbayumba.
(JODAN NZUKI, NI NGUMI INAYOPIGWA USAWA WA USO, BAINA YA PUA NA PAJI LA USO)
JM aliyumba hadi akawa karibu na ile silaha, akawa anainama kwa tabu ili aichukue silaha ile, na Inspekta Jamila, akang'amua alichokuwa anataka kukifanya JM.
Hivyo akapiga pigo moja takatifu, akitumia teke aina ya JAMPING MAIGELI, teke lile lilimsogeza JM hatua kadhaa kutoka pale ilipokuwa ile silaha, na damu za pua zikachukua nafasi yake.
(JAMPING MAIGELI, NI TEKE UNALOPIGA UKIWA UMERUKA HUKU UKIMFATA ADUI, UKIWA UNATAZAMANA NAE USO KWA USO, NA PIGO LAKE HUTUMIKA CHINI YA VIDOLE/ UNYAYO.)
Inspekta Jamila,alishalichungulia kaburi, hivyo akutaka kufanya maonyesho, alipigana na mtu ambae, muda wowote, anaweza kutoa roho ya mtu!
Mara kikasikika kishindo kikubwa chumbani mle, na Inspekta Jamila alipotazama kule kilipotokea kishindo kile, alikuwa akitazamaza na Sajenti Kubuta Aliekuwa na silaha mkononi mwake.
Na kabla hajasema kitu,akaingia Koplo Magane, na wakaingia askari wengine watatu, wote wakiwa wamekamata bunduki mikononi mwao aina ya SMG.
"Sajenti KUbuta umechelewa sana bwana, ningekuwa marehemu sasa hivi, nilikwambia tangu jana ofisini katika mikakati yetu, kuwa uwe ukinifatilia kutokana na kuwindwa kwangu, ila kwa kuwa umefika na nipo salama, basi halijaharibika neno, niambie hapa ni sehemu gani tulipo, kwani mie sijui kabisa nipo wapi!"
"Samahani Afande, kama mikakati ilivyokuwa ikisema, mimi nilikuwa pale uwanja wa ndege, nikakusindikiza hadi pale hotelini, nilipotaka kuondoka nikashuhudia jambo ambalo sikulitarajia.
Yule jamaa wa kithethe alikupiga Karate shingoni, wakakubeba haraka na kukupandisha ndani ya gari yao, mimi ningeweza kupambana nao, ila nilitaka nifike ambapo nilidhani, ndiyo yangekuwa masikani yao, ili tuwatie mbaroni wote, kwa kuwa nilikuwa peke yangu, ilibidi niongeze ngumu kutoka kituoni pale magomeni, kwani hapa tupo Maeneo ya Kawe"
Baada ya kusema maneno yale Sagenti Kubuta alitoa pingu, ili amfunge JM, ambae sasa alikuwa amelala huku akitweta kwa maumivu makali.
"No Sagenti Kubuta, huyo nilichukua ahadi kuwa nitamfunga pingu kwa mikono yangu mwenyewe, hivyo inabidi nitimize ahadi yangu."
Inspekta Jamila alimfunga pingu JM, akamuendea mzee wa Kithethe, akaichukua simu iliyokuwa mfukoni mwake, akaiangalia simu iliyokuwa ikiwasiliana na bwana Yule, namba ya simu ile iliyokuwa imewasiliana na mzee wa Kithethe, ilimtia fadhaa kubwa sana, ikamtoa machozi, akakata shauri mara moja akiwa na ile simu mkononi mwame

.........

Inspekta Jamila, aliingia hotelini kwa nguvu, akakutana uso kwa uso na Mpenzi wake, akiwa amekaa akiegemea mto, huku akiwa amepatwa na mshituko mkubwa!
"Karibu sweety, vipi mbona hivyo?"
Hatimae Shany alifunguka kwa kutoa kauli.
Inspekta Jamila, alimtazama mpenzi wake, kwa jicho la husda!
"Mimi siyo sweety wako tena kuanzia sasa, wewe ni mshenzi, na muuaji mkubwa!"
Inspekta Jamila baada ya kusema maneno hayo alikwenda kwa kasi ili amvamie Shany, lakini alipiga hatua mbili tu, hakuweza kuipata hatua ya tatu, Shany aliinua mkono wake na Bastola ikawa inaonekana waziwazi ikimlenga Inspekta Jamila!
"Hatua moja mbele, nikusaini kifo! Mimi ninakujua kuliko unavyojijua wewe!"
*** USIKOSE KESHO UONE MTU NA MCHUMBA WAKE NINI KITATOKEA***
 
ram amka, kumenoga
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom