Riwaya: Barua Kutoka Jela

Riwaya: Barua Kutoka Jela

RIWAYA: BARUA KUTOKA JELA
MTUNZI: IBRAHIM GAMA


SEHEMU YA MWISHOOO!!!!

Mara kikasikika kishindo kikubwa chumbani mle, na Inspekta Jamila alipotazama kule kilipotokea kishindo kile, alikuwa akitazamaza na Sajenti Kubuta Aliekuwa na silaha mkononi mwake. Na kabla hajasema kitu,akaingia Koplo Magane, na wakaingia askari wengine watatu, wote wakiwa wamekamata bunduki mikononi mwao aina ya SMG. "Sajenti KUbuta umechelewa sana bwana, ningekuwa marehemu sasa hivi, nilikwambia tangu jana ofisini katika mikakati yetu, kuwa uwe ukinifatilia kutokana na kuwindwa kwangu, ila kwa kuwa umefika na nipo salama, basi halijaharibika neno, niambie hapa ni sehemu gani tulipo, kwani mie sijui kabisa nipo wapi!"
"Samahani Afande, kama mikakati ilivyokuwa ikisema mimi nilikuwa pale uwanja wa ndege, nikakusindikiza hadi pale hotelini, nilipotaka kuondoka nikashuhudia jambo ambalo sikulitarajia. Yule jamaa wa kithethe alikupiga Karate shingoni, wakakubeba haraka na kukupandisha ndani ya ya gari yao, mimi ningeweza kupambana nao, ila nilitaka nifike ambapo nilidhani, ndiyo yangekuwa masikani yao, ili tuwatie mbaroni wote, kwa kuwa nilikuwa peke yangu, ilibidi niongeze nguvu kutoka kituoni pale magomeni, kwani hapa tupo Maeneo ya Kawe" Baada ya kusema maneno yale Sagenti Kubuta alitoa pingu, ili amfunge JM, ambae sasa alikuwa amelala huku akitweta kwa maumivu makali. "No Sagenti Kubuta, huyo nilichukua ahadi kuwa nitamfunga pingu kwa mikono yangu mwenyewe, hivyo inabidi nitimize ahadi yangu." Inspekta Jamila alimfunga pingu JM, akamuendea mzee wa Kithethe, akaichukua simu iliyokuwa mfukoni mwake, akaiangalia simu iliyokuwa ikiwasiliana na bwana Yule, namba ya simu ile iliyokuwa imewasiliana na mzee wa Kithethe, ilimtia fadhaa kubwa sana, ikamtoa machozi, akakata shauri mara moja akiwa na ile simu mkononi mwake
.........
Inspekta Jamila, aliingia hotelini kwa nguvu, akakutana uso kwa uso na Mpenzi wake, akiwa amekaa akiegemea mto, huku akiwa amepatwa na mshituko mkubwa! "Karibu sweety, vipi mbona hivyo?" Hatimae Shany alifunguka kwa kutoa kauli.
Inspekta Jamila, alimtazama mpenzi wake, kwa jicho la husda!
"Mimi siyo sweety wako tena kuanzia sasa, wewe ni mshenzi, na muuaji mkubwa!" Inspekta Jamila baada ya kusema maneno hayo alikwenda kwa kasi ili amvamie Shany, lakini alipiga hatua mbili tu, hakuweza kuipata hatua ya tatu, Shany aliinua mkono wake na Bastola ikawa inaonekana waziwazi ikimlenga Inspekta Jamila!
"Hatua moja mbele, nikusaini kifo! Mimi ninakujua kuliko unavyojijua wewe!" Shany alisema maneno hayo huku akisimama kutoka kitandani, na kumkabili Inspekta Jamila.
Huku akiwa amesimama, kwa taharuki, Inspekta Jamila, alisema kwa fadhaa. "Hata nawe pia?! Mtu niliekuthamini, kukupenda, kukuheshimu na kukupa mapenzi ya dhati, leo umekuwa nyoka wanigeukia?! Kwa lipi lakini baya, nililokutendea?!"
"Siku mbili zijazo, nitakuwa katika orodha ya matajiri wanaotajika duniani, kwani mpango wangu ukishafanikiwa, nitapata pesa nyingi sana, Jamila wewe ni kikwazo kikubwa, katika kufikia malengo yangu, samahani sana, kwani bila ya hivi, siwezi kutimiza malengo yangu!"
Shany alimwambia Inspekta Jamila, akiwa amemuoneshea mtutu wa bunduki, usoni mwake.
Mara baada ya kusema hayo, inspekta Jamila alilia kwa huzuni kubwa, na mara Shani akakipeleka kidole husika, katika kiwambo cha kufyatulia risasi, ili amalize kazi yake! Mara risasi ikalia na Inspekta Jamila, akalala chini! Alipokuja kuinua uso wake, alimuona Shany anavuja Damu mkononi, huku silaha yake, ikiwa ipo chini! Kabla hajatahamaki, alimuona mtu akitokea chini ya kitanda, na Inspekta Jamila alipomuona mtu Yule, macho yalimtoka pima,fadhaa ikamjaa, taharuki na Wahka ukachukua nafasi!
"Naitwa Jongo Janga, ukipenda niite JJ, natoka makao makuu ya usalama wa taifa, kitengo kisichokuwa na mipaka!"
Ilikuwa ni sauti ya ukakamavu, kutoka kwa Yule mtu alietoka uvunguni mwa kitanda kile, ambae Inspekta Jamila, alimtambua kama muokota chupa za plastiki, na vyuma chakavu!Alisema maneno yale, na kuonesha kitambulisho chake juu, katika namna ya kutoa nafasi ya kusomwa!
"Lakini, usalama wa taifa unahusika vipi na kesi hii, lakini pia umeingiaje humu chumbani bila kuonekanwa?!" Inspekta Jamila, alimuuliza Jongo Janga, huku akiwa amepatwa na mshangao mkuu!!!
"Bastola ile ya kimada, wa bosi Serikalini, anaeitwa Hamida, kauwawa Mikocheni!" Jongo Janga, alikuwa anasoma moja kati ya beti za BARUA KUTOKA JELA. Kisha akaendelea kusema huku akimuelekezea mtutu wa Bunduki Shany, aliekuwa amesimama akishikilia mkono wake uliokuwa unavuja damu! "Shany Karama Rashidi, A,K,A SHANKARA, nyoosha mikono yako juu!" Inspekta Jamila moyo wake ulipiga sarakasi, kwa mshituko alipolisikia jina lile lililokuwa katika waraka, likihusishwa na aliekuwa mpenzi wake, ama kweli usilolijua, litakusumbua! Shany alitii amri na kunyoosha mikono juu, Jongo Janga, akapiga hatua kubwa na kuisogeza ile silaha ya Shany, kwa mguu. "Lakini nataka kujua, wewe umeingiaje humu ndani?!" Inspekta Jamila, alikuwa na dukuduku la kutaka kujua namna Jongo Janga, alivyoingia mle ndani. "Mara baada ya wewe kutekwa, nilikuwa nashuhudia! Na baada ya dakika zisizozidi tatu, Huyu bwana alikwenda nje, ili kumalizia mzigo wake uliokuwa ndani ya gari,kwani alikuwa akifahamu mtego aliouandaa! nami kwa mwanya huo nikaingia chumbani humu, ingawa alikuwa amefunga na funguo, kwani sisi tunapotaka kuingia mahala popote, huwa tuna uwezo wa kufanya hivyo kwa funguo zetu zenye uwezo wa kufungua mlango na kufuli lolote!" Jongo Janga, aliondosha shaka ya Inspekta Jamila, na akatoa pingu, mfukoni mwake, akamrushia Inspekta Jamila, ili amfunge Shany Karama Rashidi, au kwa kifupi Shankara! Inspekta Jamila, huku akimfunga pingu aliekuwa mpenzi wake, akajisemea moyoni mwake, "Ama kwa hakika, huu ni mtego wa panya!" Shany muda wote alikuwa ameinamisha uso wake chini, kwa jinsi alivyoaibika na kufadhaika.
"Shankara, huwezi tena kwa sasa, kulipua chochote ndani ya nchi hii, waambie hao waliokutuma, serikali ya Tanzania, ipo makini, na ina usalama wa kutosha! Tunazo taarifa kuwa kesho ilikuwa ulipue bomu, katika benki kuu ya Tanzania, na mitambo yako ambayo ingeingia kesho hapa nchini kwa njia ya Bahari, hivi ninavyoongea na wewe, tayari tupo nayo katika himaya yetu!"Jonga Janga, alizizima ndoto za Shany katika moyo wake. "Yaani wewe Shany, umekuwa na roho ya tamaa namna hiyo? Unadiriki hata kuuw......!!!
"...Kuuwa huyo ndiyo kazi yake inayompa pesa! Huyu, ndiyo kiongozi wa genge la uhalifu nchini. Amekuwa akifadhili sana vitendo hivyo, na huyu Shany, ndiye aliekuwa akifatwa na kina Jeradi Mwaipopo, pale kwa macheni!" JJ alimkatisha na kuingilia mazungumzo yale.Inspekta Jamila, alimchukia Shany, kama mtu ambae, hakuwahi kuwa mpenzi wake! Kwa mikono yake alimfunga pingu mikononi, akazikaza pingu zile hadi namba ya mwisho,zikambana Shankara, akalalamika zilegezwe, lakini hakuna mtu, aliemsikiliza! Shany akiwa mbele ya Inspekta Jamila, huku Jongo Janga, akiwa anapekua mizigo yake, akawashangaza askari wale. Alizunguka na pigo moja aina ya ORAKEN, likatua katika shingo ya Inspekta Jamila,likampeleka chini kama mzigo, akadondokea kichwa, akanyooka pale chini, akiwa hatikisiki, yaani alikuwa kama gogo! Shany haraka akatimua mbio, kuuwahi mlango, lakini hakufika, Jongo Janga alifyatua risasi mbili, kila moja ikawa imepigwa mguu wake, na Shankara akadondoka, huku akipigiza uso wake, katika sakafu,akatoa yowe kubwa na kutupatupa miguu yake!(ORAKEN, NI PIGO LINALOPIGWA NA MPIGAJI, AKIWA AMEMPA ADUI MGONGO,HUZUNGUKA NA KUPIGIA NYUMA YA KIGANJA, NA LIPIGE SHINGONI KWA ADUI)
Mara Sagenti Kubuta, aliwasili mahala pale, na timu yake, baada ya kumuhifadhi Jambazi, mkorofi Jeradi Mwaipopo katika kituo cha Polisi cha kati. Na gari nyingine ikiwapeleka wale maiti, katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.


*****
Inspekta Jamila, alipokuja kupata fahamu, alijikuta katika chumba kimoja tulivu, kikiwa na watu watano wakiwa wanamtazama. Alipotazama vizuri, akaiona sura moja ngeni machoni mwake, Dokta Zahara,akasogea karibu yake, na kumwambia,"Pole sana shoga yangu, lakini unaendelea vizuri" Inspekta Jamila, alitaka kusema jambo, lakini alishindwa, machozi yakawa yanamtiririka, kisha akageuza sura yake, akakutana na Jongo Janga, akiwa anamtazama kwa upole. Inspekta Jamila, alimkazia macho, na hatimae akazungumza katika sauti ya kwikwi, "Yupo wapi Shankara?!" Yule mtu aliekuwa mgeni katika macho ya Inspekta Jamila, akasogea karibu, na kusema, "Pumzika Kwanza, ili upate nguvu sawasawa, kwani ubongo wako, umepata maumivu makubwa, ingeweza kukulelea Busting chuma,ingepasua mishipa ya fahamu. Hivyo unatakiwa upumzike, ili urudi katika hali yako ya kawaida!" Alikuwa ni Dokta Rehema Kanyela, aliekuwa akimtibia kwa karibu, yeye pamoja na Dokta Zahara. "Inspekta, pumzika umefanya kazi kubwa sana, unahitaji pongezi kwa kweli. Nimekuja kukuona mara baada ya kuruhusiwa kutoka kwa madaktari wanaokutibu, ambao tumeona awepo shoga yako, lakini pia yupo mtu wetu hapo ambae ni Dokta, na ni Inspekta mwenzio, kwa ajili ya usalama ambae ni Inspekta Rehema Kanyela. Shankara na Jeradi Mwaipopo, wapo chini ya ulinzi mkali, tunaendelea kuwahoji, hivyo tulia, kila kitu kipo sawa umenisoma Inspekta?!" Ilikuwa ni sauti ya IGP aliemwambia kijana wake kinachoendelea, na kumaliza kwa swali.
"Nimekuelewa Afande, ila kuna kitu kinanichanganya kidogo, ile BARUA KUTOKA JELA, imewapataje watu wa usalama wa Taifa?"
"Unatakiwa kutii Inspekta, siyo kuuliza tena, kumbuka barua zote zinazotolewa nje kutoka gerezani, huwa zinapitiwa na afisa usalama,nae ndiyo anatoa idhini kama zichapishwe pale gerezani na kutolewa nje, au zikachapishwe nje na kutumwa sehemu husika. Hata Mwaduga Dingo, alipopeleka barua yake ikachapishwe na kuruhusiwa kutolewa nje, amini ilishapita kwa watu wa usalama! Hivyo kwa nukta hiyo, sidhani kama utakuwa na mashaka yoyote katika nafsi yako!" IGP alihitimisha maneno yake, kwa kijana wake, na Inspekta jamila, hakuinua tena mdomo wake, kuuliza au kusema chochote kile.
Siku tatu baadae, Inspekta Jamila, alikuwa katika kikao na IGP, yeye na Sagenti Kubuta, na IGP alikuwa akiongoza kikao kile kama kawaida, akawa anawaeleza vijana wake. "Inspekta Jamila, kupitia watu wa usalama, tumepata uthibitisho mkubwa kuwa kwenye gari yako, kulifungwa kifaa maalum, na Shankara, ambacho kila ulipokuwa na gari ile, ulikuwa unaonekana katika GPS. Na gari hiyo uliyonunuliwa na Shankara, ilikuwa imewekwa mitambo ile toka Japan, ilipotoka gari ile." IGP alikuwa akizungumza huku akiwatazama vijana wake, walivyokuwa wamepigwa na butwaa, kisha akaendelea kutoa habari. "Hivyo kila ulipokuwa ukizungumza, iwe kwa simu, au na yeyote, kulikuwa na chombo maalum, kilichokuwa kinatoa taarifa, kila kilipotakiwa kufanya hivyo, kwa mantiki hiyo, mambo yako mengi, yalikuwa yanajulikana na watu wale, katika namna ambayo, ingesumbua kufahamu katika hali ya kawaida!" Inspekta Jamila, alikuwa akitingisha kichwa kwa kuelewa taarifa ile nyeti sana. "Shankara ni wakala wa ugaidi, alipokuwa huko ng'ambo, alipewa mafunzo ya ulipuaji mabomu, na kupitia Interpol, tumeweza kupata taarifa, na usalama wa Taifa, wameshadhibiti kila jambo, vinginevyo Taifa lingepata zahma kubwa sana!" IGP alihitimisha taarifa yake, na kuwataka vijana wake kama wana maswali.
"Nimekuelewa Afande, vipi kuhusu Jeradi Mwaipopo, alipohojiwa alikuwa na lipi jipya?!" Inspekta Jamila, alitaka kufahamu. "Jeradi Mwaipopo, hakufata taratibu za kazi tangu wakati yupo kazini, anaposema chochote wakati huu, kinakuwa hakina maana sana! Yeye anazifahamu ngazi husika, kama alionewa, alipaswa kupanda ngazi za juu ili kutoa taarifa ifanyiwe kazi, kama alikaa nayo taarifa yake, kwa muda huu, ninaipokea kama changamoto!" IGP baada ya kusema hayo, akachukua gilasi ya maji akanywa, kisha akaendelea. JM na Shankara, na mke wa marehemu Dokta Masawe, siyo muda mrefu, watafikishwa mahakamani, mara baada ya Shankara kupata nafuu majeraha ya risasi, na Jm kifua chake kimepata matatizo, nae yupo hospitali, wote wakipata nafuu, watafikishwa katika vyombo vya sheria, ili wakajibu mashitaka yao!" IGP alinyamaza kimya ili kutoa nafasi kama kuna swali, alipoona kimya, akaendelea. "Kuanzia kesho mmepata likizo, ya mwezi mmoja, leo hii mtapata pesa yenu ya likizo, na kesho nitakuwa na Mwaduga Dingo, ili nimpe majukumu mapya." IGP aliposema maneno yale kabla hajaagana na vijana wake, kupitia simu yake ya upepo, ilisikika taarifa iliyowafanya waume meno kwa ghazabu. Taarifa ile ilisema hivi, "Jambazi sugu, Jeradi Mwaipopo, ametoroka katika ulinzi wa polisi, pingu alizofungwa, zimekutwa chini ya uvungu wa kitanda, na askari wawili waliokuwa wakimlinda, wamekutwa wamezirai"!


Jagarld Jullie Z Sangomwile Khantwe Mr Rocky Gunda66 Himidini VAN HEIST BPM ABUBAKAR SHEKAUNYIROmamsapkhan born again pagan princetx Ennie mcubic jonnie_vincy slim5 MAVUNO mp anoldamoneyazan
 
Da!! Haiwezekani casuit !! Itaendeleaaa
^^
 
Last edited by a moderator:
Jambazi kuu nahisi kama ametoroka sijui inakuwaje hapa?. Poa itaeleweka tu wakati ukifika.
 
Back
Top Bottom