Riwaya: Barua Kutoka Jela

Riwaya: Barua Kutoka Jela

loading.......................
msishangae,najaribu kuload next episode.
 
Uhhhhhhhh nimejtahid mpka nimefika hapaaaa sijafanya kazi leo najitahidi kuisoma hii riwaya
 
Hii riwaya haijafika mwisho katika pitia yangu nitajitahidi kuleta ntakachokipata wakuu.
 
RIWAYA; BARUA KUTOKA JELA
MTUNZI; IBRAHIM GAMA
SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE
SIMU/WHATSAPP 0718603654 / 0688039464

“Jeradi Mwaipopo, hakufata taratibu za kazi tangu wakati yupo kazini, anaposema chochote wakati huu, kinakuwa hakina maana sana! Yeye anazifahamu ngazi husika, kama alionewa, alipaswa kupanda ngazi za juu ili kutoa taarifa ifanyiwe kazi, kama alikaa nayo taarifa yake, kwa muda huu, ninaipokea kama changamoto!”
IGP baada ya kusema hayo, akachukua gilasi ya maji akanywa, kisha akaendelea.
“JM na Shankara, na mke wa marehemu Dokta Masawe, siyo muda mrefu, watafikishwa mahakamani, mara baada ya Shankara kupata nafuu majeraha ya risasi, na Jm kifua chake kimepata matatizo, nae yupo hospitali, wote wakipata nafuu, watafikishwa katika vyombo vya sheria, ili wakajibu mashitaka yao!”
IGP alinyamaza kimya ili kutoa nafasi kama kuna swali, alipoona kimya, akaendelea.
“Kuanzia kesho mmepata likizo, ya mwezi mmoja, leo hii mtapata pesa yenu ya likizo, na kesho nitakuwa na Mwaduga Dingo, ili nimpe majukumu mapya.”
IGP aliposema maneno yale kabla hajaagana na vijana wake, kupitia simu yake ya upepo, ilisikika taarifa iliyowafanya waume meno kwa ghazabu. Taarifa ile ilisema hivi.
“Jambazi sugu, Jeradi Mwaipopo, ametoroka katika ulinzi wa polisi, pingu alizofungwa, zimekutwa chini ya uvungu wa kitanda, na askari wawili waliokuwa wakimlinda, wamekutwa wamezirai”!

“Kuanzia sasa, kila kitu kimevurugika, Likizo nimeifuta na mtarudi tena kazini, mpaka huyu Jeradi Mwaipopo, tuwe nae mikononi!”
IGP alisema maneno hayo huku akiwa amekasirika vibaya sana.
Na wote askari wale,Inspekta Jamila, na Sajenti Kubuta kwa pamoja wakasema.
“Sawa afande!”
IGP akawataka askari wake aende nao Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ili akajionee mwenyewe, kilichotokea.
Bila kuchelewa, safari ya Hospitali ya Muhimbili ikaanza!
IGP Kupitia kifaa chake cha mawasiliano, akatoa amri kwa wakuu wa polisi wa kanda zote za Dar es salaam, wahakikishe, vituo vya mabasi, uwanja wa ndege, bandari ya kwenda Zanzibar, vyote vinakuwa na ulinzi mara moja, ili kumzuia Jeradi Mwaipopo, asitoroke nje ya Mkoa huu!
Picha za Jeradi Mwaipopo zikasambazwa katika vyombo vya habari, ikiwemo magazeti na Luninga, kuwa anatafutwa na Polisi, na mtu yeyote atakae fanikisha kukamatwa kwake, Donge nono limeandaliwa kwa ajili yake!

IGP, pamoja na vijana wake wakaelekea katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, na wakajionea hali halisi ilivyokuwa!
Askari wawili walikuwa wapo hoi, hawajitambui kwa usingizi! Lakini pia povu jeupe likiwa katika vinywa vyao! Ulimi ukiwa umetoka nje kwa kiasi kikubwa sana!
Walikuwa wakipumua kwa tabu, mithili ya mtu aliekuwa katika ‘Sakalatilmauti’Yaani hatua za mwisho anazozipitia mwanaadam, kabla hajafikwa na umauti.

Pingu zilikuwa chini ya kitanda sakafuni, zikiwa zimefunguliwa!
IGP, alitikisa kichwa kwa masikitiko, nakuwataka askari aliokwenda nao pale hospitali, kuhakikisha kwa gharama yoyote, Jeradi Mwaipopo, anatiwa katika mkono wa sheria, tena haraka iwezekanavyo!
Inspekta Jamila na Sajenti Kubuta, waliitikia “Sawa Afande.” Huku wakisaluti
Inspekta Jamila, alivaa glovu na kuanza kuikagua miili ya askari wale,waliokuwa hawana fahamu.
Akagundua walikuwa hawana simu zao za mikononi, akashangaa!
Akakikagua chumba kizima kwa umakini mkubwa, hatimae macho yake yakakutana na mfuko laini mweusi wa plastiki, uliokuwa pembeni ya chumba kile.
Akauwendea ule mfuko, na alipoufikia akachuchumaa na kuutazama kwa makini. Ule mfuko ulikuwa haukufungwa juu yake, hivyo uliweza kuonesha kitu kilichokuwamo ndani yake!
Inspekta Jamila akiwa pale alipo, aliushuhudia mfuko ule ndani yake, kulikuwa kuna mabaki ya chakula.
Viazi vilivyokaangwa pamoja na mayai, maarufu huitwa chipsi, nyama ya kuku wa kukaanga na mifupa ya kuku iliyokwishaliwa tayari!
Inspekta Jamila, aliuchukua ule mfuko kwa umakini mkubwa, kisha akamgeukia bosi wake na kumwambia. “Afande nahisi hiki chakula watakuwa wamekula askari wetu, na bila shaka kinaweza kikawa ndiyo sababu ya haya matokeo tunayoyaona!” Alisimama kuzungumza Inspekta Jamila, na IGP kwa haraka akadakia.
“Kwa nini unahisi hivyo Inspekta!”
Inspekta jamila huku akiwaoneshea vidole wale askari waliokuwa mahututi, alimjibu kiongozi wake kwa unyenyekevu mkubwa.”Afande, hao askari mikono yao inaonesha walikula chakula hiki na hawakunawa baada ya kula! kwani mafuta yapo katika vidole vya mikono yao na mabaki ya tomato !”
“Inspekta unamaanisha chakula hicho kinaweza kikawa na sumu?!” IGP aliuliza kwa mshangao kisha akaendelea “Itabidi haraka kikapimwe ili tujiridhishe, na kama itathibitika ni kweli, swali hili litahitaji majibu, nani alieiweka sumu hiyo, na atakuwa ametumwa na nani?!”
Tafakari na ukimya ulitanda kwa muda, kisha Inspekta Jamila akasema kumwambia IGP.
“Afande mie naona, hawa askari tufanye kila tuwezalo, ili kuokoa maisha yao, kwani wao pekee kwa sasa ndiyo watakaokuwa na majibu sahihi, ya waliponunua au mtu aliewaletea chakula hiki, au chochote kilichopelekea kikaingia humu ndani chakula hiki!”
Mara moja aliitwa mganga mkuu pale hospitali, na kutakiwa kuzipima zile chipsi zilizosalia kama zipo salama, huku askari wale baada, ya kuwafanyia uchunguzi wa kina askari wenzao, waliokumbwa na masahibu yale, wakakabidhiwa madakitari ili kujaribu kuokoa maisha yao.
Na dakika arubaini baadae, Mganga mkuu aliwapa ripoti ya chakula kile!
“Vipimo vimeonesha kuwa, chakula hiki kimewekwa dawa za usingizi kwa kiasi kikubwa aina ya LAGACTIL, dawa tunazozitumia kuwapa wagonjwa wa akili, ili kupata usingizi! Kama mwendawazimu amezapo dawa hizi hupata usingizi, basi alapo mtu asiekuwa mgonjwa wa fahamu, anaweza kupata madhara makubwa sana katika ubongo wake, kama kulala kwa muda mrefu zaidi, kulewa, kutokwa na ulimi kama mbwa,na hata kufa, ikiwa atakuwa amekula au kulishwa dawa hizo kwa kiasi kikubwa.”
Alihitimisha mganga mkuu taarifa yake kwa askari wale, na wao wakawa wanamaswali mengi yaliokosa majibu sahihi, nani alieweka dawa zile katika chakula kile?! Na je mtandao wa genge la uhalifu lakina JM bado halijamalizika?! Fadhaa, hasira, chuki na sintofahamu, ikawakumba askari wale na kiongozi wao mkuu kabisa!

*******

Jeradi Mwaipopo, akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi wawili, katika chumba maalum pale hospitali ya taifa ya Muhimbili, alikuwa amefungwa pingu za miguu, na pia pingu za mikono! Ingawa katika mikono, alifungwa pingu mkono mmoja, na sehemu nyingine ya pingu ile, ilikuwa imefungwa katika kitanda cha chuma alichokuwa amelazwa.
Jeradi mwaipopo alikuwa katika maumivu makali, lakini akiwa katika fahamu zake kamili!
Alijizoazoa katika kitanda kile na kutaka kukaa kitako,akashindwa. Akawaambia askari wale. “Ndugu zangu nataka kwenda chooni.”
Askari aliekuwa na funguo za pingu, alizofungwa nazo JM, akamsogelea na kumfungua pingu za miguu zenye nyororo ndefu kiasi, kisha akamfungua pingu ya mkononi, ili waende nae chooni.
Jeradi Mwaipopo au kifupi JM, akawatazama askari wale, kisha akawaambia huku akiwatazama usoni moja kwa moja! “Ndugu zangu mnajuwa kuwa mie ni mwenzenu? Mbona mnanifanyia hivi?!”
Askari aliemfungua pingu akamjibu. “JM wewe ulikuwa askari, ila sasa siyo askari, lakini hata kama bado ungalikuwa ni askari, sie tunatekeleza wajibu wetu.”
JM, alitafakari kidogo, kisha akainuka na kuelekea katika choo, huku akifatwa kwa karibu na askari wale.
JM, aliingia chooni akiwa anatembea kwa kuburuza miguu yake, kutokana na pingu alizokuwa amefungwa nazo miguuni mwake muda mrefu, na kukazwa kumpa maumivu.
Alijisaidia haja kubwa na ndogo, huku akiwa akili yake ikifanya kazi kwa haraka na kubawabu hiki na kile, hadi alipomaliza haja zake, akawa amekwisha pata maarifa yakufanya! Akajisafisha na kurudi kitandani kwake, katika mwendo kama ule wa awali. Akakaa kitandani, na kunyoosha mikono yake, ili afungwe pingu kama awali, naam alifanyiwa huduma hiyo, iliyokuwa imemstahili kwa wakati ule, huku askari mwingine akimfunga zile pingu za miguu, JM sasa akiwa amelala chali, akasema kuwaambia askari wale.
“Ngugu zangu, naomba msaada mmoja kwenu, nina ndugu yangu anaishi jirani na hapa, naomba mnifanyie huduma ya simu, kumwambia kama nipo hapa, ili aniletee chakula, lakini pia nitamwambia awawekee vocha simu zenu, tafadhalini sana.”
Wale askari wakatizamana, kisha mmoja akamjibu JM kwa kumwambia. “Huo siyo utaratibu wa kazi yetu JM, wewe upo chini ya ulinzi, hivyo kukuitia watu ni kuhatarisha usalama wako na wetu, hilo halitowezekana, labda isubiri zamu itakayokuja, sie hapana JM!”
JM akiwa ametoa macho kwa jibu lile, akamjibu askari Yule, kwa kumwambia.
“Hiyo ni haki yangu ya msingi askari, sheria inaniruhusu kufanya hivyo! Kisha mie sijahukumiwa bado, bali ninatuhumiwa tu, hivyo nina haki ya msingi kwa mujibu wa sheria, kumbuka mie pia ni askari hivyo ninatambua haki zangu za kimsingi. Pia hiyo zamu ijayo sidhani kama haifanyi kazi kwa mujibu wa sheria. Naomba bwana nisaidie, au kama unataka nikulipe kwa jambo hilo, basi nitajie kima!”
Sasa ikawa zamu ya wale askari kufikiri, huku JM akiombea akubaliwe ili atimize azma yake, aliyoikusudia wakati ule!
“Unataka msaada JM, burebure tu, watu tupo kazini bwana, kama unaweza kutupa elfu hamsini, mie nitakupa simu yangu umpigie huyo jamaa yako, kama huna pesa, basi endelea kuugulia maumivu yako!”
Alisema askari mmoja aliekuwa na funguo za pingu za JM, ambae ndiye aliekuwa kiongozi.
JM,alitabasamu huku akichezesha kichwa chake kushoto kulia, kisha akasema. “Mie kama mnionavyo hapa nilipo, sina pesa hata kidogo, ila huyo ndugu yangu, naweza kuzungumza nae, akawaletea pesa hata elfu hamsini kila mmoja, wachilia mbali wewe kutaka elfu hamsini mgawane, mie natambua kuwa, mbuzi anakula kwa urefu wa kamba yake!”
Naam mjadala ule ukapata muafaka kuwa, JM azungumze na ndugu yake.
Jeradi Mwaipopo, alipewa simu, akabonyeza namba kadhaa kwa ule mkono wake mmoja uliokuwa huru, kwani mkono mmoja wa kulia, ulikuwa umefungwa pingu, pamoja na kitanda! Mkono wa shoto, uliwachwa kusudi, ili aweze kujikuna na kumpa huduma zingine!
JM alizipiga namba zile, na upande wa pili, ikawa inaita simu ile. Ama kweli, penye udhia, penyeza rupia.
“Halow…” JM alisema baada ya kupokelewa ile simu upande wa pili, na kuendelea. “…JM hapa, nipo hospitali ya muhimbili, huku karibu na Moi,nikiwa chini ya ulinzi. Hii simu ya askari nimeiomba hapa ili niwasiliane na wewe uje kunifaa nduguyo, naomba uje na Shilingi laki moja ili niwape viongozi wangu bwana, hawa ni watu muhimu sana kwangu, nakaa nao vizuri tu, kisha niletee……” JM akasimama kuzungumza na simu, akawauliwa wale askari.
“Mtakula nini awaletee, semeheni tu, kwani mchana unaingia!”
Wale askari walitazamana kisha mmoja akatabasamu, akasema .
“Mwambie atuletee chipi yai, na kuku aweke pilipili nyingi.”
JM huku akishusha pumzi ndefu akarejea katika simu na kumwambia mtu aliemuita ndugu yake. “……niletee chipsi mayai, na kuku sahani mbili, weka pilipili nyingi, watengenezee vizuri sana. Mie niletee maziwa fresh yananitosha, ukiniletea na pesa kidogo, utakuwa umenifaa sana!”
Baada ya kusema hayo, JM alikata simu, kisha akaifuta ile namba aliyoipigia, na kuirudisha simu kwa mwenyewe huku akiwa anatabasamu.

***NINI KILIENDELEA,
 
RIWAYA; BARUA KUTOKA JELA
MTUNZI; IBRAHIM GAMA
SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO
SIMU/WHATSAPP 0718603654 / 0688039464
JM alizipiga namba zile, na upande wa pili, ikawa
inaita simu ile. Ama kweli, penye udhia, penyeza
rupia.
“Halow…” JM alisema baada ya kupokelewa ile
simu upande wa pili, na kuendelea. “…JM hapa,
nipo hospitali ya muhimbili, huku karibu na
Moi,nikiwa chini ya ulinzi. Hii simu ya askari
nimeiomba hapa ili niwasiliane na wewe uje
kunifaa nduguyo, naomba uje na Shilingi laki moja
ili niwape viongozi wangu bwana, hawa ni watu
muhimu sana kwangu, nakaa nao vizuri tu, kisha
niletee……” JM akasimama kuzungumza na simu,
akawauliwa wale askari.
“Mtakula nini awaletee, semeheni tu, kwani
mchana unaingia!”
Wale askari walitazamana kisha mmoja
akatabasamu, akasema .
“Mwambie atuletee chipi yai, na kuku aweke pilipili
nyingi.”
JM huku akishusha pumzi ndefu akarejea katika
simu na kumwambia mtu aliemuita ndugu yake.
“……niletee chipsi mayai, na kuku sahani mbili,
weka pilipili nyingi, watengenezee vizuri sana. Mie
niletee maziwa fresh yananitosha, ukiniletea na
pesa kidogo, utakuwa umenifaa sana!”
Baada ya kusema hayo, JM alikata simu, kisha
akaifuta ile namba aliyoipigia, na kuirudisha simu
kwa mwenyewe huku akiwa anatabasamu.
Dakika arubaini baadae simu ya Yule askari, iliita
na alipoitazama ile namba, ilikuwa ngeni machoni
mwake, akaipokea. “Halow, ndiyo hii, ehee, sawa
njoo hadi hapa Moi, mie nakufata hapo nje,
umevaa nguo rangi gani?, Haya basi sogea
nakuja!”
Yule askari alikuwa akizungumza na ndugu wa
Mwaipopo, kisha akakata simu na kutoka nje,
akimuacha mwenzake akiwa anamdhibiti JM.
Kijana mmoja mrefu wa wastani, mweusi tii,
aliekuwa amevalia nguo za kubana mwilini
mwake,aliingia katika chumba kile, baada ya
dakika zisizozidi saba, akiwa pamoja na askari
aliemfata, alikuwa amebeba mfuko laini mweusi wa
plastiki, akautoa mfuko wa ndani, na kuwakabidha
wale askari. Kisha paketi mbili kubwa za maziwa
ya Tanga fresh, akimkabidhi Jeradi Mwaipopo,
huku akimwambia. “Pole ndugu yangu, nimekuja
kukufaa!”
Aliyasema maneno hayo, huku akiwa amewapa
mgongo maaskari wale. JM akamwambia ndugu
yake, ”Umeniletea pesa nilizokuambia?!” Yule
ndugu yake akajibu kwa vitendo, aliingiza mkono
mfukoni, na kutoa burungutu la pesa, akazihesabu
shilingi laki mbili, nyingine akazirudisha mfukoni.
Akataka kumkabidhi JM, lakini JM akamwambia.
“Laki moja wape askari, laki moja nipe mwenyewe.
Yule ndugu yake JM, akafanya hivyo.
Wale askari walizipokea zile pesa wakagawana
palepale huku wakitabasamu, kisha wakanawa
mikono katika bomba lililokuwa chooni mle kwa
zamu, wakiwa na pesa mfukoni, wakaanza kula
chipsi mayai na kuku, kwa fujo!
Hawakufanikiwa kuzimaliza zile chipsi, walianza
kunyong’onyea miili yao, nguvu zikawatupa mkono,
wakataka kusema jambo midomo ikawa mizito,
mikono yao haikuweza kuhimili uzito hafifu wa
chakula walichokuwa nacho mikononi mwao,
mifuko ile iliwadondoka! Walipotaka kupiga hatua,
miguu yao ikakataa kutii, wakaanguka chini kama
mizigo, wakaingia katika usingizi mzito!
Geradi Mwaipopo, akamwambia ndugu yake,
“Chukua funguo anazo huyo alielala kushoto
kwako.”
Yule bwana hakuchukua funguo peke yake, bali
alichukua funguo za pingu, pamoja na pesa zake
walizogawana askari wale,na simu zao, kisha
akamfungua pingu za miguuni kisha akamfungua
pingu ya pili ile iliyofungwa kitandani, ikafunguka
na kuningg’inia kipande chake cha pili katika
mkono wa kulia wa JM. Nae JM aliimalizia
mwenyewe kuifungua,pingu ile akaitupa pingu ile
chini ya uvungu wa kitanda!
Yule ndugu yake JM alichukua zile chipsi mayai,
akaziweka katika mfuko mmoja, akitaka kuondoka
nazo, JM akamwambia. “Wacha kubeba mizigo ya
bure!” Na yule bwana akauwacha mfuko ule,
ambao sasa ulikuwa katika mfuko mmoja!
Akakumbatiana na Jeradi Mwaipopo, kisha
wakatoka katika chumba kile, wakatoka katika
jengo la hospitali ya taifa ya Muhimbili, na
kutokomea kusikojulikana!
*******
Askari waliokuwa wanaingia zamu mchana,
kuwatowa wenzao walioingia asubuhi, walipigwa
na butwaa ya mwaka, baada yakuwakuta wenzao,
wakiwa wamelala chini hawana fahamu, na Jeradi
Mwaipopo, akiwa ametoweka! Kupitia simu zao za
mikononi, walitoa taarifa kwa mkuu wao wakituo,
na mkuu wa kituo alirusha hewani taarifa ile kwa
simu ya upepo, ‘Radio call’
na ikasambaa kwa kila radio iliyokuwa wazi katika
Jiji la Dar es salaam. Na haikushangaza kuwafikia
taarifa ile Inspekta Jamila, na Sajenti Kubuta,
wakiwa katika kikao na bosi wao IGP.
11
Inpekta Jamila, akiwa na Sajenti kubuta, baada ya
kutoka Hospitali ya taifa ya Muhimbili, alikuwa
anawaza mengi, akiwazuwa, hatimae akamwambia
Sajenji Kubuta. “Inawezekana huu mtandao wa
uhalifu wa kina JM bado upo, tena ni mkubwa
sana! Sasa hivi inabidi twende katika mtandao wa
simu, ili tukaone na huko kama tunaweza kupata
lolote la maana, ingawa mie nahisi, huko
kutatufanya tuwe karibu na JM, kwa namna moja
au nyingine!”
Aliwasilisha ujumbe wake kwa Sajenti Kubuta, na
wakawafikiana lazima wafike huko.
Sajenti Kubuta, akamuuliza kiongozi wake.
“Tunakwenda kampuni gani ya simu Afande?!”
Inspekta Jamila alimtazama Sajenti Kubuta kwa
jicho la udadisi, kisha akampa kikaratasi kidogo
kilichokuwa kina namba mbili za mitandao tofauti!
Huku namba zile mojawapo ilikuwa imewekewa
alama ya nyota mbele yake. Na inspekta Jamila
akamwambia Sajenti Kubuta “Tunaanza na
kampuni ya simu iliyowekewa alama ya nyota!”
Dakika tano baadae, wakawa barabarani,
wakielekea Maeneo ya Moroco katika makutano ya
barabara ya Ally Hassan Mwinyi, na Kawawa.
Wakaingia kushoto katika jengo moja lililojengwa
mithili ya meli, wakaegesha gari yao na kuteremka,
wakajichoma ndani ya jengo lile.
Wakiwa ndani ya jengo lile, walifika mapokezi na
kujitambulisha mapokezi, kisha wakataka kuonana
na meneja wa kampuni ile ya simu, na baada ya
mawasiliano haya na yale, wakakaribishwa katika
ofisi ya meneja wa kampuni ile ya simu.
“Karibuni ofisini kwetu, niwasaidie nini jamani?”
Alisema meneja yule akiwa katika sura ya
kutabasamu.
“Asante meneja, kama ulivyotambulishwa na katibu
muhutasi, sie ni askari polisi kutoka makao makuu.
Tumekuja hapa tunahitaji tupate msaada wako, ili
kuweza kufanikisha upelelezi wetu.”
Inspekta Jamila alimwambia yule meneja wa
kampuni ya simu, huku akitoa kitambulisho chake
na kumuonesha.
“Sawa Inspekta, nikusaidieni nini?”
Aliwajibu meneja yule, baada ya kukitazama
kitambulisho kile, huku akiwa katika hali ya utulivu
mkubwa.
“Askari mwenzetu, ni mteja wenu, na hivi
tuongeavyo, anakaribia kufa kwa hicho
alichofanywa, sasa tulitaka kufahamu, na tupate
‘PRINT OUT’ ili tuone simu alizowasiliana nazo leo
hadi saa sita mchana!” Inspekta Jamila
alihitimisha huku akimtazama moja kwa moja
usoni, meneja yule.
“Ahaa hilo halina neno, ila tunautaratibu itabidi
muufate, kwani siri ya mteja wetu, hatupaswi
kumpa mtu mwingine! Hivyo mtasaini kitabu hapo,
na kueleza kuwa, mnataka taarifa zipi na kwa nini,
kisha mwanasheria wetu, atasaini na hatimae
mtapata hayo mnayoyataka!”
Inspekta Jamila, akafanya kama alivyoelekezwa, na
nusu saa baadae, ilichapishwa taarifa ya simu
zilizowasiliana na namba ile aliyowapa yeye, ikiwa
inasomeka ujumbe, simu zilizobeep, zilizobeepiwa,
simu zilizopigwa, na simu zilizo ipigia!
Inspekta Jamila, aliiweka karatasi ile juu ya meza,
akiwa anakusudia na Sajenti Kubuta, aione kwa
umakini, taarifa ile.
Inspekta Jamila, alitoa kalamu na kuanza
kuipitisha juu ya karatasi ile kwa umakini mkubwa
sana, mara baada yakuimaliza kuipitia, akapiga
mstari katika namba ya mwisho, ambayo ilisomeka
simu ya yule askari iliipigia, na simu ile dakika
arubaini baadae iliipigia simu ya yule askari!
Inspekta Jamila, alitabasamu, pale alipoiona
namba iliyofanya mawasiliano na simu ya yule
askari mwenzao, pia ilikuwa ni simu ya kampuni ile
waliyokuwa katika ofisi zake!
“Meneja tunashukuru kwa msaada wa kwanza, ila
bado tunahitaji msaada wako, tunaomba pia
‘PRINT OUT’ za namba ya mwisho kuwasiliana na
simu ya askari mwenzetu, ikibidi ianzwe kuchapwa
mawasiliano iliyofanya wiki moja nyuma!” Inspekta
Jamila, alimwambia yule meneja, huku akionesha
msisitizo!
Yule meneja akafanya kama alivyoelezwa, na
dakika tano baadae zikaletwa karatasi zilizokuwa
na kila kitu walichokihitaji. Wakaagana na meneja
wakiwa wanatabasamu, wakarejea ofisini kwao,
wakiwa na matumaini mapya!
Inspekta Jamila, na Sajenti Kubuta, walihamia
katika chumba cha compyuta kwa muda, wakiwa
na wahka ile mbaya!
Koplo Dihenga, mtaalam wa IT,(Imformation
Technology) wa jeshi la polisi, aliwapokea na
kuwasikiliza shida yao.
“Koplo, hebu tutafutie picha za mtu huyu, na data
zake, kadiri utakavyoweza. ”Inspekta Jamila,
alimwambia Koplo Dihenga, huku akimkabidhi
karatasi waliyotoka nayo kule katika kampuni ya
simu.
Koplo Dihenga, aliekuwa amezungukwa na
kompyuta kadhaa! Aliipokea ile karatasi na kuilisha
data compyuta iliyokuwa mbele yake, kisha akawa
anaisubiri, kompyuta ile ikitafuta mambo
iliyotakiwa itoe taarifa zake!
Baada ya dakika takribani tano, kompyuta ile,
ilinyambua data zifuatazo! Mwenye namba ya
simu, anaeulizwa anaitwa Mwakyembe Anthony.
Line ya simu yake, inatumiwa katika simu aina ya
Blackbery yenye imei:256436-03-020155-7.
Imeongea ikitumia mnara wa kampuni ya simu ya
Airtel, uliokuwa upanga mashariki, katika wilaya ya
Ilala, mkoa wa Dar es salaa, Tanzania. Simu yake
ilikuwa katika mnara wa Muhimbili, saa tano
zilizopita! Muda huu namba ya simu hiyo
imei,inasomeka katika mnara wa Kongowe ya
Mbagala! Ikiwa ipo katika nyumba ya kumi na
mbili upande wa kusini, kutoka katika mnara!
Koplo Dihenga, aliiprint taarifa ile, na kumkabidhi
Inspekta Jamila.
Inspekta Jamila, akampongeza Koplo Dihenga, na
kumwambia. “Hatuna muda wa kupoteza,
tunaelekea Kongowe, kadiri simu hiyo itapohama
eneo,utatupa taarifa!”
“Timamu Afande” Coplo Dihenga alimwambia
Inspekta Jamila, huku akiwa katika ukakamavu,
kuonesha heshima kwa mkubwa wake.
Inspekta Jamila, alipanga timu yake, dakika ishirini
na tano baadae, gari mbili za kiraia, aina ya
TOYOTA NOAH zikiwa na askari nane, wenye silaha
za kivita smg, walikuwa wamezipakata katika
miguu yao, huku Inspekta Jamila, na Sagenti
Kubuta, wakiwa katika gari ndogo Toyota Soluna,
ikikamilisha idadi ya gari tatu, zinazoelekea eneo la
Kongowe,katika wilaya ya Temeke.
*******
Jeradi Mwaipopo akiwa na mtu aliemwita nduguye,
anaeitwa Mwakyembe Anthony, baada ya kutoka
katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, wakitumia
usafiri wa Mwakyembe, pikipiki aina Boxer kutoka
India.Ikiendeshwa na Mwakyembe, walivaa
elementi wakawa wanaonekana kama abiria
amepanda Bodaboda!
Safari yao, ilielekea Maeneo ya wilaya ya
Temeke,katika eneo liitwalo Kongowe, kama
unaelekea Mkuranga, nyumbani kwake
Mwakyembe.
Walipofika waliingiza pikipiki ndani, wakafunga geti
na kukumbatiana upya, kama watu waliokuwa
hawajaonana muda mrefu nyuma.
“Asante sana ndugu yangu, kumbe bado
unakumbuka maagizo yangu kuwa, nikikwita na
kukwambia njoo unifae, namaanisha nini?!”
ITAENDELEA..
 
RIWAYA; BARUA KUTOKA JELA
MTUNZI; IBRAHIM GAMA
SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA
SIMU/WHATSAPP 0718603654 / 0688039464
“Timamu Afande” Coplo Dihenga alimwambia
Inspekta Jamila, huku akiwa katika ukakamavu,
kuonesha heshima kwa mkubwa wake.
Inspekta Jamila, alipanga timu yake, dakika ishirini
na tano baadae, gari mbili za kiraia, aina ya
TOYOTA NOAH zikiwa na askari nane, wenye silaha
za kivita smg, walikuwa wamezipakata katika
miguu yao, huku Inspekta Jamila, na Sagenti
Kubuta, wakiwa katika gari ndogo Toyota Soluna,
ikikamilisha idadi ya gari tatu, zinazoelekea eneo la
Kongowe,katika wilaya ya Temeke.
*******
Jeradi Mwaipopo akiwa na mtu aliemwita nduguye,
anaeitwa Mwakyembe Anthony, baada ya kutoka
katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, wakitumia
usafiri wa Mwakyembe, pikipiki aina Boxer kutoka
India.Ikiendeshwa na Mwakyembe, walivaa
elementi wakawa wanaonekana kama abiria
amepanda Bodaboda!
Safari yao, ilielekea Maeneo ya wilaya ya
Temeke,katika eneo liitwalo Kongowe, kama
unaelekea Mkuranga, nyumbani kwake
Mwakyembe.
Walipofika waliingiza pikipiki ndani, wakafunga geti
na kukumbatiana upya, kama watu waliokuwa
hawajaonana muda mrefu nyuma.
“Asante sana ndugu yangu, kumbe bado
unakumbuka maagizo yangu kuwa, nikikwita na
kukwambia njoo unifae, namaanisha nini?!”
Jeradi Mwaipopo alimwambia mtu aliependa
kumwita ndugu yake, kwa sababu wote walikuwa
wanatoka katika mkoa mmoja wa Mbeya.
“Naam nakumbuka sana, kwani natambuwa kama
umeshakamatwa, kwani nilikuwa nafatilia kwa
karibu sana. Ndiyo maana uliponiambia nije
nikufae, upo muhimbili,kisha ukanitaka nije na
chakula kwa ajili ya wale askari, nikatambuwa
natakiwa nifanye nini! Nilipita duka la dawa pale
muhimbili, nikanunua zile ‘Njunja’(LAGACTIL)
nikimwambia muuzaji, ndugu yangu anasumbuwa
mwenye ugonjwa wa akili akiwa hospitali, na
manesi wa pale muhimbili, wamenielekeza nije
kununua dawa zao za usingizi hapa! Naomba
nisaidie dada yangu. Basi Yule muuzaji wa duka la
dawa Muhimu. Alinipa dozi kabisa, nami nikampa
elfu ishirini, nikimwambia chenji aendelee nayo!
Nikaenda pale karibu na Geti lakuingilia, upande
wa kushoto, nikanunua maziwa paketi mbili,
nikanunua na chipsi mayai, na kuku, nikasaga zile
dawa za wehu za usingizi, nikazinyunyizia katika
kile chakula, nikamtafuta Yule askari katika namba
yake, akanielekeza ndiyo nikaja kukufaa! Nilidhani
wangenambia nionje kile chakula, basi ningeonja
kisha ningekunywa yale maziwa pakiti moja
kuondosha ile sumu ya zile dawa, nabado balaa
lingekuwa upande wao!”
Mwakyembe alihitimisha taarifa yake, kwa JM
huku akiwa na wingi wa furaha. “Asante sana
ndugu yangu kwa kunifaa, kwani nilikuwa sina mtu
mwengine zaidi yako, ambae ni shababi na
anaeweza kucheza mchezo ulioufanya leo! Sasa
kuanzia sasa, jeshi la polisi litakuwa linakutafuta
wewe pamoja na mimi, hivyo umakini unahitajika
sana! Nakupongeza kwa kuchukua simu za wale
askari, kwani wangebaki nazo, ile simu uliyoipigia
namba yako ingebaki, na wangekusumbua, ila kwa
kuwa umeichukuwa, umefanya jambo la maana
sana!”
JM alimwambia Mwakyembe huku akimtizama
kama alikuwa na neno la ziada, alipomuona
hakuwa na neno, aliendelea. “Itabidi mie niondoke
sasa hivi nielekee nyumbani kwangu Vingunguti,
kwani kule ndiyo kuna hazina, na nikiwa kule
hujihisi nipo pahala salama zaidi.” Jm alisema
maneno yale na kutulia huku akijinyoosha viungo
vyake!
*******
“Nipe taarifa tafadhali, amebadilisha eneo?”
Inspekta Jamila alikuwa akiwasiliana na Koplo
Dihenga kutoka makao makuu.
“Hapana Afande, inaonekana bado yupo hapohapo,
kwani Imei inasomeka bado katika mnara huohuo,
akiwa katika usawa uleule wa nyumba ya kumi na
mbili,upande wa kusini, kutoka katika mnara.”
Alijibu Koplo Dihenga, huku akiwa anaangalia
katika kompyuta iliyokuwa mbele ya macho yake!
“Sawa Koplo umesomeka, nipo Mbagala Kizuiani
nasonga eneo la tukio, tafadhali hakikisha hupotezi
lada!” Alihitimisha Inspekta Jamila, kisha akakata
simu. Akawa anaangalia mbele huku akiwa kimya
na mawazo tele!
Sagenti Kubuta, alikuwa anaendesha gari
akiongoza msafara ule, huku akiombea wahusika
wanaowafata, wawakute ili wamalizane nao!
Wakiwa njiani eneo la Mbagala rangi tatu, simu ya
Inspekta Jamila iliita, nae kwa papara akaitwaa
simu yake, nakuitazama namba inayopiga, na hata
alipoiona akaipokea simu ile chapu kwa haraka!
“Unasomeka nipe taarifa!” Ilikuwa ni simu ya Koplo
Dihenga kwa Inspekta Jamila. “Afande simu ya
Konstebo Iddy Gebo, imewashwa katika mnara
huohuo, ila imetolewa line iliyosajiliwa simu hiyo,
na sasa imewekwa line nyingine! Hapa inasoma
imei yake katika mnara, umenisoma mpaka hapo?”
Alimaliza taarifa yake Koplo Dihenga kwa swali. Na
Inspekta Jamila kwa wahaka mkubwa alimjibu.
“Nimekusoma Koplo, hiyo inaonesha mtu
mwengine yupo na Mwakyembe, anaweza kuwa ni
JM, au Mwakyembe ameamua aitumie pia simu
yapili! Endelea kunijuza tafadhali,nakaribia eneo la
tukio nipo Tanita mpakani mwa Mbagala na
Kongowe!” Alijibu Inspekta Jamila na Koplo
Dihenga akakata simu.Dakika kumi baadae,
wakawa eneo la Kongowe,wakiikaribia nyumba
husika, Inspekta Jamila akampigia Koplo Dihenga,
na kumwambia “Nipo eneo la tukio, je kupo vilevile,
au kuna badiliko?!” Koplo Dihenga aliangalia
komptuta yake akamwambia. “Afande simu ya
Constebo Iddy Gebo, imezimwa kama dakika tano
hivi, ila simu ya Mwakyembe bado taa ya mnara
inasomeka yupo hapohapo!” Alisema Koplo Dihenga
na Inspekta Jamila,akamwambia “Labda itakuwa
imezimika chaji, ngoja tufanye ambushi tutajuwa
hapo hapo ndani, je hapa tumeshahesabu nyumba
ya kumi na mbili, kutoka katika mnara wa simu,
unaoonekana mbele yetu, kwa upande wa kusini,
upo sahihi na data?”
“Hapo sahihi kabisa mkuu, hakuna shaka na data,
endelea na kazi mkuu!”
Koplo Dihenga, alimjibu mkubwa wake akiwa
anajiamini na majibu yake!
Inspekta Jamila, alikata simu, nakupanga timu
yake kuzunguka nyumba ile, kisha yeye akaenda
mlangoni nakulijaribu geti la nyumba ile, akaliona
limefungwa nganganga! Akamtizama Sajenti
Kubuta, kama aliekuwa anataka msaada, Sajenti
Kubuta, akamwambia kiongozi wake. “Plani B plus
mkuu!”
Na hata alipokwisha kusema maneno yale,
Inspekta Jamila akamjibu “Plani B, Sajenti!”
Kufumba na kufumbua askari wale waliparamia
ukuta wa nyumba ile, huku baadhi ya raia
wakishangaa kwa kitendo kile, lakini kwa kuwa
wao walikuwa kazini, wala hawakutaka kuwajali,
waliendelea na hamsini zao. Askari wanne
walikuwa juu ya ukuta, na wanne walibaki
chini.Wale askari waliokuwa chini, kila mmoja
alikuwa na silaha, aina ya SMG,akiwa ameikamata
barabara, akiwa doria katika pembe ya nyumba ile,
akihakikisha kwamba hakuna mtu, asiyekuwa wao
ataeruka kupitia ukuta wa pembe aliyokuwepo!
Inspekta Jamila, Sajenti Kubuta, na askari wawili,
wataalam wa mapambano ya mikono, wote kwa
pamoja waliparamia ukuta wa nyumba ile uliokuwa
na ruva nyingi, kwa ajili ya kuruhusu hewa
kuingiza kwa wingi ndani ya nyumba ile. Kwa
ustadi mkubwa waliparamia na kufika juu kabisa
ya ukuta ule usiopungua futi nane urefu wake,
wakachuchumaa huku mikono yao, ikiwa imezama
viunoni mwao, ilipokuja ibuka ilikuwa imekamata
silaha ndogo ya Bastola mikononi mwao! Vitendo
vyote hivyo vilikuwa vikifanyika kwa pamoja tena
bila kelele! Wote wakiwa pale juu ya ukuta na
bastola mikononi mwao, waliruka pamoja hadi
chini ndani ya uwa wa nyumba ile, wakibimbilika
walipofika chini na kulalia tumbo huku silaha zao,
zikielekezwa mbele tayari kwa matumizi! Walilala
pale chini kwa sekunde kadhaa, walipoona kimya
hakuna rabsha yoyote iliyotokea, walitambaa kwa
matumbo,na viwiko vya mikono, wakiufata mlango
mkubwa wa kuingilia ndani, huku wakichelea
kuonekana kama wangelisimama kupitia dirisha
lililokuwa pana mbele yao! Na hata walipoufikia
mlango, waliukuta mlango ule umefungwa kwa
funguo, nyumba ikiwa kimya kabisa!
Sasa wakainuka huku wakijigawa wawili kila
pande, waliegemea ukuta, huku silaha zao sasa
zikikamatwa kwa mikono miwili, zikiwa
zimeelekezwa juu!
Inspekta Jamila, alitoa ishara kwa wenzake, na
kitendo bila kuchelewa, Sajenti Kubuta alirudi
nyuma, kisha akapiga hatua kubwa na kupitia bega
lake, aliukumba ule mlango kwa kishindo kimoja
kikubwa, na ule mlango bila khiyana, ukafungukia
kwa ndani kwa kasi na kujipigiza ukutani!
Askari wale wote wakalala chini kifudifudi kwa kasi
ya ajabu,na kutulia pale chini huku sasa wakiwa
wanaitazama korido ikiwa tupu haina mtu! Pia
wakijikinga kama adui akiwa na silaha,basi kama
angefyatua risasi, risasi ile ingepita juu, na wao
wangekuwa salama. Askari wale waliinuka kwa
ghafla wawili wakiwa upande wa kulia, na wengine
wawili wakiwa upande wa kushoto. Wakatembea
na ukuta huku wakiwa makini, safari hii wakiwa
katika mwendo wa kunyata, askari mmoja wakila
upande wa mbele alikuwa ameielekeza silaha yake
mbele, na aliekuwa nyuma yake, aliielekeza silaha
yake nyuma! Kifupi ilikuwa kila mmoja alikuwa
akimlinda mwenzake, huku wakisonga mbele!
Walipofika usawa wa iliyoonekana kama mwanzo
wa sebule, walisimama huku wakiegemea ukuta, na
Inspekta Jamila kupitia mkono mmoja, alikuwa
anatowa ishara, ilihali mkono mwingine, alikuwa
amekamata silaha yake sawasawa. Askari wale
kila mmoja alitikisa kichwa kuwashiria kuwa
ameelewa maelekezo aliyokuwa anayatowa
kiongozi wao.Inspekta Jamila na vijana wake,
walivamia wakiwa katika mstari mmoja bastola
zikilenga mbele, tayari kwa kutumika, naam
wakafika katika sebule lakini wasiyaamini macho
yao! Wote walipigwa na mzubao wa mwaka, huku
wakiongeza umakini mara dufu, walipiga goti,
wakawa wanageuka kila upande tayari kwa
mashambulizi, lakini bado ulikuwa kama kucheza
na kivuli chake mtu, huwa hakina madhara yoyote!
Inspekta Jamila huku akiwa ametaharuki kwa hali
anayoishuhudia, alitowa ishara ya kusachi
vyumbani, katika nyumba ile iliyokuwa mpya
kabisa, ikiwa haina samani nyingi ndani yake, pia
kulikuwa bado milango ya vyumbani, ilikuwa
haijawekwa katika nyumba ile! Hivyo haikuwa
shida kufika vyumbani, lakini hadi kinafikiwa
chumba cha nne na cha mwisho katika nyumba ile,
hakukuwa na majibu yaliyopatikana, yaliyotofautian
a na ya vyumba vingine, vilikuwa hakuna
mwanaadamu aliekuwa katika vyumba vile, sasa
wakiwa wameshusha silaha zao chini, wote
walijongea pale sebuleni, wakiwa bado hawaamini
kitu wanachokiona kwa macho yao!
Mwakyembe Anthony, alikuwa amelala chali macho
yamemtoka pima yakiwa hayaoni yanachotazama!
Mwili wake ukiwa na matundu ya risasi usawa wa
moyo wake, damu nyingi zilikuwa zimetapakaa
sebuleni pale,na zilianza kuganda kuonesha kiasi
ya kama dakika kumi na tano hivi, ndiyo roho
imeacha mwili wa Mwakyembe Anthony, Lakini
Jeradi Mwaipopo, akiwa hajulikani alipo wala
hakuwamo katika nyumba ile! simu ya marehemu
Mwakyembe, aina ya Blackbery, ilikuwa ipo juu ya
stuli ikiwa ipo on! Inspekta Jamila alitikisa kichwa
kwa masikitiko, safari hii akimkosa Jeradi
Mwaipopo,au JM kwa dakika chache sana!
*******
Jeradi Mwaipopo, alikuwa anajinyoosha viungo
vyake,Mwakyembe alitowa simu yake pamoja na
simu za wale askari,akawa anazithaminisha, ndipo
JM alipoiona ile simu ya Blackbery ya Mwakyembe,
na mara moja moyo wake ukapiga paah!
Akakumbuka simu hii ndiyo aliyowasiliana na yule
askari, akipigiwa na yeye kupiga, JM anatambuwa
tangu akiwa askari, madhara ya simu za Blackbery
kwani zinaweza kukuonesha kila ulipo, na yeye
mwenyewe alishawahi kuwakamata wahalifu
waliokuwa wameziiba simu za aina hiyo, kwani
hata kama ungebadilisha laini, lakini bado
ingeweza kusomwa mahala ulipo, akahisi matatizo
mbele yake,yakimjia kwa haraka!
“Akamwambia Mwakyembe, una kitu gani cha
kutulinda humu ndani, ikitokezea mahasimu wetu,
wakitujia hapa?!” Mwakyembe huku akitabasamu,
alimwambia JM. “Ondoa shaka juu ya hilo,hapa
nina Bastola inayobeba risasi kumi na nane, tena
ikiwa imejaa risasi, lakini kama haitoshi jana tu
ndiyo nimepata kiwambo chake cha kuzuia sauti!”
Mwakyembe alisema maneno hayo, huku
akikigeuza kiti cha kukaa mtu mmoja, aina ya sofa,
juu chini na kuibua bastola peke yake ikiwa
imevishwa magazini yake, na kiwambo cha kuzuia
sauti kikiwa pembeni yake. Akamkabidhi JM kwa
maana ya kumuonesha! JM aliipokea ile silaha
huku akitabasamu, akakivesha kiwambo cha kuzuia
sauti, akapandisha risasi chemba, akiwa kama
anaeijaribu ile silaha kama inafanya kazi
sawasawa, huku akiwa ameielekeza juu silaha ile,
na risasi ikapanda juu, ikisubiri amri ya kutumwa
iende wapi, naam JM akiwa anatizamana uso kwa
uso na Mwakyembe, aliishusha ile silaha kwa kasi
ikamlenga Mwakyembe, usawa wa moyo, na JM
huku akifumba macho, aliziruhusu risasi mbili,
kutoka katika silaha ile, naam nazo zikajibu kama
zilivyotumwa, zikafumua moyo wa Mwakyembe,
kila moja ikipiga katika moyo na kufumua nyama
kubwa kwa nyuma!Kwa kuwa Mwakyembe alikuwa
karibu kama futi tatu kutoka alipokuwa JM, risasi
zile zilimrusha nyuma kama mita nzima na
kumtupa chali chini kama mzigo alitupa mikono
kidogo akatulia tulii kama maji mtungini, akawa
amebadilishwa jina na kuwa marehemu
Mwakyembe! JM aliibusu ile silaha aliekuwa
anaihitaji kuliko kitu chochote kile kwa wakati ule,
kisha akafunga usalama wa silaha ile automatic,
huku risasi nyingine, ikiwa tayari ipo chemba,
ikisubiri safari! Jm aliziendea zile simu zilizokuwa
zimewekwa katika stuli na marehemu Mwakyembe,
akaichukua simu moja iliyouwa inahadhi na
heshima kidogo, mali halali ya Konstebo Iddy Gebo,
akatowa line iliyokuwemo mle ndani, akatoa line
nyingine ya simu, kutoka katika sehemu ya kuvalia
mkanda kwa nje, aliibinjua suruali yake, na sehemu
iliyokuwa imekatwa, akasogeza kwa vidole vyake,
akatowa line ya kampuni ya simu ya Airtel, na
kuipachika katika simu ile akaiwasha, na simu
ikakubali kuwaka! Baada ya kujiridhisha kuwa
ameshapata simu, silaha kwa ajili ya kujilinda,
akaichukua na ile simu ya yule askari mwingine,
nokia ya toch, akaziweka mfukoni mwa suruwali
yake, mara ile simu aliyoweka line yake, ikatoa
mlio wa betri kukosa chaji ya kutosha, na JM
akaizima kabisa. Akatoka nje akifunga mlango kwa
nje, akaiendea ile pikipiki ya marehemu, akatoka
nayo hadi nje, akalifunga lile geti kwa funguo na
kuondoka na ufunguo wa nyumba na wa geti,
pamoja na ile silaha akatokomea zake, akielekea
Vinguguti kwa fida Hussein!
12.
WADAU WETU, KITABU CHA BARUA KUTOKA JELA
KIPO MITAANI, KUPATA KHATMA YA JM
TAFADHALI PATA NAKALA YAKO SASA ILI
KUMUUNGISHA MWANDISHI. ASANTENI SANA
KWA KUWA SOTE TANGU MWANZO HADI HAPA.
 
Wakuu nimejitahidi kuchimbachimba na hapo ndipo nilipofikia..
 
Wakuu nimejitahidi kuchimbachimba na hapo ndipo nilipofikia..

Kwa hapa Dar hivyo kitabu kinapatikana wapi? Na bei ni kiasi gani? Mkuu pia niambie kama kuna riwaya zingine za kipelelezi na kijasusi,nipe orodha yake na bei zake ili nijipange. On Wednesday 7-1 nije kuvichukua
 
Sijasoma toka mwanzo lakini sehemu hii ya 25 ina mapungufu. Majambazi wote huzitupa simu zao punde mara baada ya mawasiliano. Rejea tamthilia ya prison break season 2, michael scofield alikuwa na lundo la simu ambapo kila akiwasiliana na watu huitupa simu husika. Inaonekana mwandishi bado yupo mwaka 47.
 
Sijasoma toka mwanzo lakini sehemu hii ya 25 ina mapungufu. Majambazi wote huzitupa simu zao punde mara baada ya mawasiliano. Rejea tamthilia ya prison break season 2, michael scofield alikuwa na lundo la simu ambapo kila akiwasiliana na watu huitupa simu husika. Inaonekana mwandishi bado yupo mwaka 47.

Hayo Ni mawazo yako mkuu

Hebu jaribu kutengeneza story yako ya Hiyo format afu tuone itakaa vipii
 
Hayo Ni mawazo yako mkuu

Hebu jaribu kutengeneza story yako ya Hiyo format afu tuone itakaa vipii

Watu wote duniani hatuwezi kufanya kazi moja lakini kila mmoja anatakiwa kufanya kazi yake kwa weledi na kiubunifu zaidi. Kazi iliyofanywa kiuweledi huwezi kuikosoa kwa haraka na hovyohovyo hasa ktk 'technical issues'. Wahasibu, wanasheria, wanahabari n.k. kila mmoja awe makini ktk kazi zake.
Pamoja na yote, kazi yako ikikosolewa ni wazi kuwa watu wameikubali na wanataka uiboreshe zaidi.
Shida yetu waafrika, kuanzia ngazi ya mtu mmojammoja, familia, ukoo, mpaka serikalini, hatutaki kukosolewa. Mtu adui ni yule anaekosoa hata kama ni kwa technical issues.
 
Back
Top Bottom