Riwaya - Balaa

Riwaya - Balaa

Hard copy tuu. Soft copy hapana

Mkuu mapengo junior vp tena mbona mnazungumzia mambo ya hard copy na soft copy? Vipi riwaya ndo imeisha nini? Au umepata mfadhili wa ku print kitabu? If yes niambie tutakipata wapi na kwa kiasi gani.
 
Nipo mkoani kwa sasa,je hicho kitabu nitakipataje? Nina operation kusanya riwaya pelelezi zote.

MAWAKALA WA KITABU CHA PENZI CHUNGU.

Wakala wa Kariakoo
Jina : Abrassa
0773985828 mkunguni na livingstone

DODOMA WAKALA
JINA KAVISHE
ST Mwanza avenue karibu na TRA
Phone 0654 070 744

KILWA MASOKO
JINA HADIJA
Swanaha. Com..karibu na By night
Simu; 0652283663

Musoma wakala.
Jina Novanus Amiani
Barabara ya mkendo kubwa jengo la Embassy Hotel
Phone 0754 468 964

Moshi Wakala
Jina Osca Mmasy
Yupo jengo la seven eleven , barabara ya chagga
Phone 0769 483 595

Wakala Lindi
Jina Said Watanga
Yupo Stand ya mabasi inatizamana na NMB BANK
Simu 0718 689 619

Wakala Zanzibar
Jina Walid Salim
Yupo mbweni
Contact: 0789369601
0778828989.

Wakala Arusha
Jina Goodluck Mariki
Yupo barabara ya makongoro inatizamana na jengo la CCM mkoa.
Phone 0756 296 443

Wakala Kigoma
Jina Michael
Yupo Kigoma mjini opposite na EXIM bank
Phone 0755 823 527

Wakala Upanga
Jina Fahad Said
Yupo Gold Fashion
Contact: 0686821502

Manzese wakala
Kambangwa
Yupo opposite na JM hotel
O784508250/0763218019

Wakala Iringa
Jina Abel Kisimba
Yupo Uhuru road ,nyuma ya ukumbi wa Highland Hall

Mwanza wakala
Jina Mpombo
Yupo lwempisi house , mtaa wa Liberty
Phone 0756 348 074

Temeke wakala
Jina Hashimu mapengo
Tandika magorofani
Simu- 0714526379

Mbagala, Vikindu, Mwandege na Mkuranga
Simu; 0687 028898

Wakala wa mbeya
Jina zuberi marijani
Mobile 0763218014

Wakala morogoro
Faisal Nassoro
Mobile 0715 978 711
0779780355
 
SIMULIZI; BALAA
MWANDISHI; HALFANI SUDY
SIMU; 0757 633010

SEHEMU YA HAMSINI NA SABA

Kwa bahati nzuri mtu aliyewekwa na Zaidi Kilumba alifika pale wodini wakati Dokta Yusha akiwa ameenda kutafuta gari kwa ajiri ya kuwapakia wagonjwa wake na kuwatoa katika hospitali ile, iliyogeuka kuwa hatari sana sasa, au wakala wa kifo kama alivyoiita Mzee Mpaukha.

Baada ya nusu saa Dokta Yusha alirejea, akiwa na gari aina ya Costa kwa ajiri ya kuwapakia wagonjwa wake. Dokta Yusha alishuka garini, kwa mwendo wa kasi alielekea wodini. Alitembea kwa kasi kwa kuwa alijua hatari ya kukaa pale hospitali kwa muda mrefu. Uharaka wake lakini haukupunguza umakini wake, Dokta Yusha alikuwa makini pia. Alikuwa anamwangalia kila mtu , ili angalau ajue kama hatari ikiwa inamkaribia.

Ghafla! Akiwa njiani Dokta Yusha alishikwa bega na mtu.
Alistuka sana!
Aligeuka kwa kasi na tahadhari kubwa sana. Tayari kwa lolote!
Alikuwa Mwanasheria mlevi!

"Mbona faster Dokta"
"Nataka nihamishe wagonjwa wangu Mwanasheria"
"Nimetoroka Polisi kuja kukwambia hiko kitu kaka"
"Umetoroka Polisi?"
"Hatuna muda wa kuongea hapa, wewe ni hatari zaidi kuonekana hapa, rudi garini nakuletea wagonjwa wako wote garini"
"Unajua Nasra alipo Mwanasheria, basi twende wote"
"Rudi garini!" Mwanasheria mlevi alisema kwa hasira. Hakuongeza neno, aliondoka kuelekea wodini, akimwacha Dokta Yusha amehemewa!
Hakuwa na jinsi, alirejea kwenye gari huku akishangaa akili za Mwanasheria mlevi. Sasa Dokta Yusha alianza kumuhusudu Mwanasheria mlevi. Alimwamini yule mlevi akiyemdharau sana kabla ya kisanga hiki.

Mwanasheria mlevi aliingia wodini akiwa anaangaliwa na yule kijana, mlinzi aliyewekwa na kina Don Genge. Moja kwa moja alienda katika kitanda cha Mzee Mpaukha. Aliteta nae kidogo kisha akatoka nje.

Mwanasheria mlevi alienda nyuma ya wodi ile, sehemu ambako kulikuwa na choo pia.

"Mamaaa nakufaaaaaaa!"

Mwanasheria mlevi alipiga makelele yasiyo na mfano kule nyuma ya wodi. Watu walichanganyikiwa. Na baadhi ya watu walikimbilia kule nyuma. Yule kijana aliyewekwa na Dokta Kilumba nae alivutwa na ukelele wa Mwanasheria. Naye alielekea kule nyuma ya wodi. Wakati yule kijana akikimbilia kwa kupita upande wa mashariki kuelekea nyuma ya wodi, Mwanasheria mlevi alipita upande wa magharibi kurudi mbele ya wodi..

ITAENDELEA MUNGU AKIPENDA
 
SIMULIZI; BALAA
MWANDISHI; HALFANI SUDY
SIMU; 0757 633010

SEHEMU YA HAMSINI NA NANE

Yule kijana umbea ulimponza, watu wengi waliendelea kukusanyika kule nyuma ya wodi bila kuelewa kilitokea nini.
Mwanasheria mlevi aliingia wodini harakaharaka, kwa kushirikiana na mzee Mpaukha wakamweka Hasina katika kiti chenye magurudumu manne, na kuanza kuondoka nae kwa kasi kuelekea garini, Mwanasheria mlevi ndiye aliyekuwa akisukuma kiti kile huku akifuatwa kwa nyuma na Mzee Mpaukha, aliyekuwa akifuata kwa mwendo wa taratibu.
Walifika ilikopaki ile gari, kwa kushirikiana na Dokta Yusha walimuingiza Hasina garini.
Mwanasheria mlevi alishuka katika gari harakaharaka ili akamchukue na Nasra, mkewe Dokta Yusha.

"Unaenda wapi tena Mwanasheria?"
"Kumchukua Nasra"
"Nishamchukua tayari, ingia kwenye gari tuondoke"
"Safi sana comrade" Mwanasheria mlevi alisema huku akimwangalia Nasra aliyekuwa amelala katika siti ndefu za nyuma ya ile gari.
Safari ya kukimbia katika hospitali ile ya wilaya, ambayo sasa ilikuwa ni sawa na wakala wa kifo wa wilaya ilianza.

Kule nyuma ya wodi watu walitafutafuta sana bila kumuona mtu aliyepiga kelele. Hawakuona kitu, watu walianza kuondoka kidogo kidogo, huku wakionesha kukereka kwa kiasi kikubwa, na yule kijana nae alirejea katika lindo lake. Alikaa palepale kwenye kiti akimsubiri Dokta Yusha afike pale, ili awape taarifa mabosi wake waliomtuma.
Laiti angejuaaaaa...
Alikuwa amechelewa sana. Hakujua kwamba Mwanasheria mlevi alimuona pale muda mwingi sana, na alimtilia shaka yule kijana pale kitini. Ndio akaamua kuucheza ule mchezo wa makelele. Mchezo uliomuokoa awali Dokta Yusha bila kujua kipindi anaelekea katika chumba cha kuhifadhia maiti alipokuwa amejificha Tano, na sasa mchezo uleule wa makelele unaookoa watu wengi zaidi lakini safari hii ukichezwa kwa kukusudia..

ITAENDELEA MUNGU AKIPENDA
 
SIMULIZI; BALAA
MWANDISHI; HALFANI SUDY
SIMU; 0757 633010

SEHEMU YA HAMSINI NA TISA

Don Genge alibaki masikio wazi kusubiri taarifa katika simu yake. Lakini simu haikupigwa!

Baada ya kukaa kwa muda mrefu kidogo, Don Genge alinyanyuka pale sofani na kwenda katika chumba wanacholala Six killers, aliwaamsha kwa upole na kuanza kuongea.

"Six Killers, mmelala vya kutosha vijana, nina maana yangu kuwaruhusu mje kulala wakati kama ambao hamkupaswa kulala kabisa. Kuanzia sasa hamtalala tena, mpaka mtakapomleta Dokta Yusha hapa! Kule wodini kuna kijana tumemweka endapo kama Dokta Yusha atawasiri atujurishe kupitia kwa Dokta Kilumba. Lakini hadi sasa hakuna taarifa yoyote. Inamaana yule mwanaharamu hajafika pale hospitali. Sasa wote mnaenda wodini kumchukua yule mzee na yule dada na mtaenda kule ICU kumchukua yule mfu. Leo ndio siku yao ya kufa!. Vifo vibaya sana, ambavyo havijawahi kushuhudiwa na Dunia. Hakikisheni hamfanyi kosa lolote vijana "

"Sawa Bosi" Six Killers waliitikia kwa pamoja.

Safari ya kuelekea hospitali Kilwa Kivinje ilianza. Six killers wakiwa na hasira sana na Dokta Yusha. Mtu ambaye anataka kuwakosesha usingizi. Wakati wao wanaelekea Kilwa Kivinje hospitali, Dokta Yusha akiwa na Mwanasheria mlevi na wagonjwa wao walikuwa nd'o wanakipita kijiji cha Mandawa wakielekea mkoani Lindi. Nia yao ni kuwapeleka wagonjwa wao katika hospitali misheni ya ndanda.

Six killers walienda moja kwa moja katika wodi waliolazwa Mzee Mpaukha na Hasina. Waliingia kwa mbwembwe kubwa sana. Lengo ni kuwabeba wale wagonjwa na kwenda kuwauwa vibaya sana, na kuwatoa moyo kule katika chumba cha kuhifadhia maiti.
Walikuta wodi ipo tupu!.
Hakukuwa na mgonjwa wowote pale wodini.

Moja alichukua simu yake na kumpigia Don Genge kumtaarifu habari hizo mbaya kabisa, habari ambazo ni chungu kutoka katika mdomo wa Moja, chungu kusikiwa na sikio la Don Genge.

"Bosi hakuna mtu humu wodini" Moja alisema kwa fadhaha bila hata kumsalimia Bosi wake.
"Unasemaje wewe!" Don Genge aliuliza kwa ghadhabu.
"Hakuna mtu Bosi hapa wodini, jamaa itakuwa katuwahi" Moja aliongea kwa utulivu sasa.
"Huyo kijana aliyepewa kazi ya kulinda hapo yupo?"
"Tunae hapa"
"Afe yeye leo, na moyo wake utolewe, afe kifo sawa na tulichopanga kuwauwa wale mbwa!" Don Genge aling'aka simuni.

ITAENDELEA MUNGU AKIPENDA
 
SIMULIZI; BALAA
MWANDISHI; HALFANI SUDY
SIMU; 0757 633010

SEHEMU YA SITINI

Yule kijana alianza kutetemeka. Muda uleule six killers walimgeukia. Hawakuwa na mas'hara hata kidogo. Walimsukasuka kwa nguvu, safari kuelekea katika chumba cha kuhifadhia maiti ilianza.
Walikuwa wanaenda kumuua yule kijana!
Siku zote mshahara wa dhambi ni mauti. Kijana aliponzwa na Mwanasheria mlevi, mlevi anayetumia akili sana katika mambo yake, mlevi ambaye watu wengi wanamdharau, bila kujua uwezo wake wa juu wa akili aliokuwa nao. Kijana aliingia katika kesi asiyoijua mwanzo wala mwisho. Hakuwekea uzito maagizo aliyopewa na Dokta Zaidi Kilumba, hakujua kama kosa lolote la aina yoyote ile lingegharimu maisha yake. Hakupewa tahadhari hiyo na Dokta Kilumba, labda angepewa hiyo tahadhari angekuwa makini zaidi. Au labda angeikataa kabisa ile kazi ya kifo. Lakini ilikuwa bahati mbaya sana kwake, hakutahadharishwa awali pia hakupewa muda wa kujitetea, ili kuelezea kitu gani kilitokea, kwanza kundi la Six killers hawakuwa na muda huo, muda wa kumuhoji yule kijana dhaifu, walikuwa na haraka isiyo na kifani. Ilikuwa lazima wamtafute Dokta Yusha, ilikuwa lazima wapate mioyo kumi na tano kila siku. Kumbuka walibaki wanne sasa, ukiondoa wale madaktari vibaraka. Tano alikuwa mgonjwa, Sita alienda kusikojulikana. Walikuwa lazima wajigawe vizuri ili kufanikisha mipango yao..ilikuwa lazima wawepo wa kuhakikisha zoezi la utoaji moyo linaendelea kama kawaida, pia wawepo wa kuhakikisha zoezi ambalo lilikuwa gumu sana kwa sasa, zoezi la kumtafuta Dokta Yusha linafanikiwa.
Yule kijana asiyekuwa makini, na kuzidiwa akili na mlevi, aliuwawa kwa kunyongwa shingo na Moja wa Six Killets, na kutolewa moyo na Dokta Sharifa Juma...

ITAENDELEA KESHO MUNGU AKIPENDA😀
 
Dah hapo ndipo ninakupendea mapengo junior
Ahsante sana kwa kukata kiu yangu tena!
 
SIMULIZI; BALAA
MWANDISHI; HALFANI SUDY

SEHEMU YA SITINI NA MOJA

Tatu na Nne walibaki pale hospitali, kulinda usalama wa pale, Moja na mbili ndio walienda kuwasaka wakina Dokta Yusha, kuwasaka mahala pasipojulikana.

Ghafla, simu ya Don Genge iliita.
Aliangalia katika kioo cha simu yake, kilisomeka..... Kifo!
Don Genge alipokea ile simu huku akiwa na hofu kuu.

"Hallo Bosi" Don Genge aliita simuni kwa sauti yake yenye hofu.
"Nipe maendeleo ya project yetu Don Genge"
"Mambo yako sawa Boss, ingawa kuna kidudu mtu katuingilia kidogo katika mipango yetu"
"Ni nani huyo Don Genge? na kaiingilia vipi hiyo project?"
"Anaitwa Dokta Yusha, amegundua kila kitu tunachokifanya huyo jamaa ni mjanja sana aisee"
"Na na bado anaendelea kupumua mpaka sasahivi?"
"Ndio Bosi anapumua, ingawa naamini anamalizia pumzi zake za mwisho"
"Six killers wanasemaji?"
"Wanajaribu kupambana vijana, ila bado hali haijakaa sawa mpaka sasa, mmoja ni missing in action, na mmoja ni majeruhi"
"Nani aliyepata majeruhi, na nani missing in action?"
"Majeruhi Tano, missing in action Sita"
"Lazima ufanye kitu Don, usiache hali ikawa namna hiyo, vipi kuhusu mzigo?"
"Mzigo uko wa kutosha, tutausafirisha kesho asubuhi"
"Fanya hivyo Don, mzigo umepungua sana huku, na tuna oda nyingi sana"
"Nitafanya hivyo"
"Sawa jamaa, huyo jamaa sijui Dokta nani anastahili kifo kabla hajatoa taarifa kwa jeshi la polisi au mahala popote ambako itakuwa si salama kwetu"
"Nimekuelewa Bosi, nitahakikisha tunamziba mdomo"
Simu ikakatwa.

Kifo, alikuwa ndio Mkurugenzi mkuu wa mradi huu kitaifa. Mradi wa kutoa mioyo ya maiti. Mioyo ambayo ilikuwa inatumika katika utengenezaji wa sumu kali zaidi duniani, Sumu ya Proxine!

Sumu ambayo, ukiigusa bila ya kuwa na kizuizi chochote kinachofuata ni kifo! Kifo baada ya dakika thelathini. Sumu ambayo ilikuwa inatengenezwa nchini Ujerumani, lakini malighafi za kutengeneza sumu hiyo zilikuwa zinatoka Tanzania. Sumu ya Proxine, sumu hatari iliyopigwa marufuku kutumika dunia mzima.
Hiyo ndio kazi ya mioyo hii ikiyochukuliwa na kundi la Six killers likiongozwa na jasusi Don Genge. Unaweza ukasema utoaji wa mioyo haukuwa na madhara sana kama asemavyo Don Genge, lakini je hivyo ndivyo wanavyopaswa kufanyiwa maiti, na je matumizi ya sumu ya Proxine, yalikuwa hayadhuru watu wasio na hatia?

Dokta Yusha na msafara wake uliingia katika hospitali ya Ndanda, wote wakiwa hoi kwa uchovu wa safari. Moja kwa moja walienda kwenye hospitali hiyo kubwa ya misheni. Wagonjwa walichangamkiwa walipofika nje tu ya hospitali hiyo. Manesi wenye vitoroli waliwapokea haraka haraka na kuwapeleka wodini. Kwa umakini na kasi walipewa huduma zinazojitajika. Huduma zilizomridhisha sana Dokta Yusha. Alikuwa na furaha usoni, ingawa furaha yake ilisinyaa akikumbuka madhila ya watu wale wabaya aliowaacha huko Kilwa.

Ndani ya wiki Moja, Mzee Mpaukha alikuwa mzima kabisa. Nasra na Hasina waliendelea kuwa wafu kitandani. Huku Hasina akifumba na kufumbua macho yake bila ya kuongea lolote. Akiba aliyokuwa anaweka Dokta Yusha ilimsaidia sana katika kipindi kile kigumu kilichohitaji awe na pesa za kutosha...

ITAENDELEA MUNGU AKIPENDA.
 
SIMULIZI; BALAA
MWANDISHI; HALFANI SUDY
SIMU; 0757 633010

SEHEMU YA SITINI NA TATU

Huko Kilwa Masoko, kundi la six killers lilikuwa katika hali ngumu sana. Wiki nzima walimsaka Dokta Yusha bila mafanikio yoyote. Six killers walianza kuingiwa na hofu labda Dokta Yusha amefichwa sehemu fulani baada ya kwenda kutoa taarifa Polisi na muda wowote watakuja kukamatwa na mipango yao kuwa hadharani, pamoja na kuwa na fikra hizo lakini hawakusumbuliwa kabisa na Polisi. Hali iliyowaaminisha kwamba askari Polisi hawakuwa wanajua lolote. Six killers waliendelea kufanya kazi zao, lakini wakiwa na wasiwasi mkubwa sana. Dokta Yusha aliichukua furaha yao na kwenda kuificha mahali kusikojulikana.

Upande wa Tano wa kundi la Six killers hali yake iliendelea vizuri. Sasa alianza kufanya mazoezi madogo madogo ishara kwamba goti lake lilianza kupata nafuu. Aliendelea kutibiwa kwa siri kwenye ile nyumba yao iliyopo kule porini Ngome. Sita wa Six killers walimtafuta sana, lakini hawakuweza kupata, na wala hawakupata fununu wapi amekwenda. Hawakuwa na hisia kabisa kwamba kiti cha kifo ndiyo sababu ya kifo cha Sita.

Kutoweka kwa Dokta Yusha kuliongeza hofu kwa kundi la Six killers. Sasa wakawa hawafanyi kazi kwa uhuru tena kama zamani. Iliwapasa kuhamisha mahala pa kufanyia operesheni zao zile za kikatiri, sasa wakawa wanaiba maiti na kwenda kuzitoa moyo huko kambini kwao, kisha kuzitelekeza porini ngome. Kubadilisha mahali pa kufanyia mauaji kukazua jambo jipya katika hospitali ya wilaya ya Kilwa, zilianza kupotea maiti kumi na tano kila jua lilipokuwa linazama. Kupotea maiti kumi na tano kila siku nako kukazua jambo kuu.
Tanzania nzima sasa ikapata habari juu ya upotevu huo wa maiti huko Kilwa. Wananchi wa Kilwa wakawa wanaishi kwa woga na wasiwasi mkubwa sana. Hakuna aliyekuwa anajua maiti za wapendwa wao zinapotea vipi. Wananchi wenye imani dhaifu wakahusianisha na imani za ushirikina. Wananchi wa Kilwa walijaribu kila njia kuzuia wizi wa maiti lakini hawakufanikiwa.

Upotevu huo wa maiti ukawasogeza karibu wapelelezi mbalimbali nchini Tanzania na waandishi wengi kwenda Kilwa kufatilia sakata hilo. Kazi ilikuwa ngumu sana kwa wapelelezi hao, hii kazi ya kuiba maiti ilifanywa na watu makini, tena wakishirikiana na madaktari makini pia. Wapelelezi walipeleleza kwa siri sana lakini hawakupiga hatua yoyote..

ITAENDELEA KESHO MUNGU AKIPENDA
 
SIMULIZI; BALAA
MWANDISHI; HALFANI SUDY
SIMU; 0757 633010

SEHEMU YA SITINI NA NNE

Laiti wangejua wapelelezi hao wangemfata Dokta Yusha ama Mwanasheria mlevi, hao ndio walikuwa wanajua kila kitu juu ya sakata hili.

Mmoja wa waandishi wa habari aliyekuja kuchunguza sakata hii alikuwa anaitwa Gabriel Rondo. Mwandishi wa habari mahiri toka gazeti la Chokochoko. Gabriel Rondo alikuwa Mwandishi wa habari mdadisi sana, mara nyingi akifatilia jambo hufatilia kwa undani kabisa, na huja na habari yenye kumridhisha kila msomaji wa gazeti la Chokochoko.

Asubuhi moja Mwandishi wa habari Gabriel Rondo ilimkuta akiwa mlangoni kwa Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya Kilwa. Nia na madhumuni ni kwenda kupata maono ya Mganga huyo wa wilaya juu ya kupotea maiti maiti kumi na tano kila siku katika hospitali yake. Gabriel Rondo alifika katika ofisi ile mnamo saa mbili asubuhi, lakini mganga mkuu Dokta Zaidi Kilumba hakuwa amefika. Dokta Kilumba aliwasiri ofisini kwake saa sita mchana, akiwa ananuka harufu mbaya ya pombe. Alifika ofisini kwake na kukuta msururu wa mkubwa watu ukimsubiri yeye, Dokta Zaidi Kilumba aliwapita watu wale kwa dharau kama hakukuwa na watu pale, Dokta Zaidi Kilumba hakuwajari, hakuwasalimia wala kuwaangalia usoni watu wale. Alijiinamia chini na kuingia ofisini kwake akiambatana na harufu yake ya pombe.

Watu pale nje walianza minong'ono, minong'ono iliyotoka katika midomo ya wasemaji na kutua moja kwa moja katika masikio yote mawili ya Mwandishi wa habari Gabriel Rondo.

Baada ya Dokta Zaidi Kilumba kuingia ofisini kwake, wateja waliokuwa katika foleni pale nje walianza kuingia ofisini kwa Dokta Kilumba, kulingana na foleni yao. Watu waliingia ofisini mpaka zamu ya Mwandishi wa habari, Gabriel Rondo ilifika.

"Naitwa Gabriel Rondo, Mwandishi wa habari wa gazeti la Chokochoko" Gabriel Rondo alijitambulisha baada ya salamu.
"Naitwa Dokta Kilumba, mganga mkuu hapa" Dokta Kilumba nae alijitambulisha.
"Nina masuala machache ambayo nataka ufafanuzi toka kwako Dokta"
"Sawa nakusiliza Ndugu Gabriel Rondo"
"Hivi ni muda gani sahihi kwa mtumishi kufika kazini?"
"Ni saa moja na nusu, ila leo nilikuwa na dharura kidogo" Dokta Kilumba alijibu swali la Mwandishi Gabriel Rondo huku akijibu swali asiloulizwa.
"Jana ulifika kama leo, juzi ulifika kama jana, ulikuwa na dharura pia?" Mwandishi Gabriel aliuliza swali lililotokana na minong'ono aliyoisikia kule nje....

ITAENDELEA KESHO MUNGU AKIPENDA
 
Shukrani mkuu,weekend yetu sasa ni nzuri sio kama kule kwenye uchu. Watu wanajifanya ma-Godfather wa jf
 
Back
Top Bottom