iddy eba
JF-Expert Member
- Aug 28, 2015
- 573
- 1,174
- Thread starter
- #21
SEHEMU YA KUMI
Daniel alikuwa amelala vya kutosha pale hotelini.
Aliamka, alioga na kuagiza chakula palepale
hotelini. Baada ya kula alipiga simu kwa rafiki
yake mmoja wa wafanyakazi katika uwanja wa
ndege wa Zanzibar, akajibiwa kuna ndege ya saa
kumi inayoenda Dar es salaam. Akamuomba
amkatie tiketi moja.
Daniel aliamua kurejea Dar es salaam tena !
*****************
Ndege ya saa kumi jioni kwenda Dar es salaam
ilijikuta imepandwa na maadui wawili. Daniel
Mwaseba na Kerspersky . Hakuna aliyekuwa
kamuona mwenzie.
Daniel ndiye alikuwa wa kwanza kuingia kwenye
ndege. Alikwenda uwanja wa ndege mapema
zaidi. Alikosa cha kufanya kule hotelini. Aliona
bora awahi kwenda uwanjani. Saa nane kamili
ilimkuta ndani ya uwanja wa ndege wa Zanzibar.
Akisubiri muda wa kuondoka ndege ufike.
Arudi Dar es salaam.
Kerspersky yeye alifika baadae pale uwanjani.
Alifika Zanzibar saa tisa na nusu akitokea Mbeya.
Baada ya kumaliza utaratibu wa pale uwanjani,
Kerspersky aliingia ndani ya ndege.
Daniel alikuwa amekaa katika siti ya nyuma
kabisa ya ndege ile. Akiwa amezongwa na
mawazo tele. Hakutegemea kama kazi ya
kuwafichua wauaji wale ingekuwa ngumu kiasi
kile. Sasa aliona siku tatu ni chache sana.
Kutokana na kuelemewa na mawazo mengi
aliamua kuyapunguza kwa kusoma riwaya.
Alifungua kibegi chake kidogo na kutoa kitabu
cha riwaya ya Mdunguaji, riwaya iliyotungwa na
Gwiji wa riwaya Tanzania, Hussein I Tuwa.
Alikifunua taratibu na kuanza kukisoma. Mambo
ya Badi katika riwaya ile yalimsahaulisha kidogo
Daniel adha za Dunia.
Alielea katika dunia nyingine kabisa.
Wakati Daniel anasoma kitabu ndipo Kerspersky
aliingia ndani ya ndege ile. Alikaa siti za mbele
kabisa. Kerspersky hakuwa makini kuwachunguza
watu waliokuwepo katika ndege ile. Alitulia
shwari katika siti yake. Akiiwazia kwa kina kazi
iliyopo mbele yake.
Kerspersky alipanga kwenda katika chuo cha
usimamizi wa fedha IFM kutekeleza adhma yake.
Chuo alichokuwa anasoma mtoto wa waziri wa
kilimo na chakula, Mheshimiwa Nyongo Daudi.
Alidhamiria kwenda kumuua Janeth Nyongo.
Mtoto wa waziri wa kilimo na chakula.
Saa kumi kamili ndege ile iliiacha ardhi ya kisiwa
cha Zanzibar, kuelekea Dar es salaam.
Baada ya muda mchache ndege iliwasiri katika
uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere, Jijini la Dar
es salaam.
Abiria mmojammoja walianza kushuka kwenye
ndege ile. Daniel alikuwa abiria wa mwisho
kushuka katika ndege ile. Akitanguliwa
Kerspersky na abiria wengine.
Daniel alikuwa makini sana. Alikuwa anaifata kila
hatua akiyopiga Kerspersky . Jamaa hakujua
kabisa kama anafuatwa.
Alichukua teksi pale nje ya uwanja wa ndege wa
Mwalimu Julius Nyerere, na kuelekea Posta,
maeneo kilipo chuo cha IFM.
Daniel nae alifata kwa kutumia teksi. Ulikuwa
mfuatano wa kimya kimya.
Kerspersky hakuwa makini kabisa. Hakuwa na
wasiwasi kabisa. Alifika posta, akashuka.
Sasa akawa anaelekea IFM kwa miguu, Daniel
akiwa nyuma yake !
Kerspersky alifika chuoni IFM. Kerspersky
akapita katika geti la chuo bila wasiwasi wowote.
Hakuwa na hofu yoyote, na wala hakuna
aliyemtilia shaka.
Alianza kuwauliza wanafunzi. Mwanafunzi wa
kwanza hakuwa anajua Janeth anakaa chumba
gani, mwanafunzi wa pili bila kujua dhamira ya
jamaa yule alimuelekeza Kerspersky chumba
alichokuwa anakaa mtoto wa waziri wa kilimo na
chakula, Janeth.
Taratibu Kerspersky akawa anaelekea huko
alikoelekezwa.
Kerspesky alikuwa anaelekea hosteli huku
akigeuka nyuma mara kwa mara. Lakini
hakumwona mtu wa kumtilia shaka.
Alipanda ngazi za kuelekea hosteli kwa mwendo
wa haraka sana.
Sasa damu ilikuwa inamchemka mwilini mwake,
alikuwa amedhamiria kuuwa !
Akafika chumba namba 33. Chumba
alichoelekezwa kuwa ndicho anachokaa Janeth.
Aligonga hodi kwa kutumia mpini wa kisu chake
kirefu, lakini mlango haukufunguliwa.
Akarudia kugonga tena.
Sasa taratibu mlango ulikuwa unafunguliwa .
Aliangaliana na bastola !
Alikuwa Daniel Mwaseba!
Kumbe Kerspersky alivyokuwa anamuuliza
mwanafunzi wa kwanza na kumfata wa pili.
Daniel alimfata yule wa mwanafunzi wa kwanza.
Baada ya kumuuliza alimwambia yule jamaa
alikuwa anamuulizia Janeth, Daniel alipiga hatua
moja mbele. Kwa haraka akaenda kumuuliza
mwanafunzi mwengine.
Alielekezwa chumba cha alichokuwa anakaa
Janeth. Alitangulia yeye chumba namba 33. Kwa
bahati nzuri kilikuwa kimefungwa. Alifungua kwa
kutumia funguo wake malaya, alifanikiwa.
Alitulia kitandani akimsubiri mgeni wake.
Kerspersky alipigwa na butwaa. Hakutegemea
kumkuta Daniel pale. Pia hakutegemea
kukaribishwa kwa mtindo ule.
"Karibu sana"
Kerspersky hakujibu.
Daniel alitabasamu.
"Najua hukutegemea kukaribishwa na mimi.Ila
imekukuta bahati mbaya "
Jamaa kimya.
"Natakaa uongee ukimya haukusaidii ! " Daniel
alisema kwa ukali.
Hakujibu.
Daniel alikasirika. Alimpiga kwa kutumia kiwiko
cha mkono kwenye mdomo. Kerspersky alianza
kutokwa na damu.
"Utaongea huongei?"
Jamaa aligeuka bubu.
Alimchukua na kwenda kumhifadhi kituo cha
Polisi Posta.
Daniel alitoka nje ya kituo kile akiwa hajui
anaelekea wapi ? Alikuwa na mawazo mengi
sana. Hajui aelekee wapi ? Hajui afanye nini?
Baada ya masaa mawili kuzunguka mtaani alirudi
tena kituo cha Polisi Posta.
"Naomba unitolee yule Mhalifu"
Kerspersky akaitwa.
Akakaa mbele ya Daniel.
"Utaongea sasa hivi" Daniel akasema kwa upole.
Kerspersky akawa anamwangalia tu.
"Usinilazimishe kufanya ninachotaka kukufanya"
"Nifanye chochote sikwambii chochote "
Daniel akaisikia sauti ya Kerspersky kwa mara ya
kwanza.
Daniel alinyanyuka. Akaenda pale kwenye kabati
la pale kaunta . Akafungua droo moja ya kabati.
Akachukua mkanda mdogo, ulikuwa kama saa ya
mkononi ndogo.
Akamvesha ule mkanda mkononi kwa Kerspersky.
Ulimkaa vizuri sana.
Akamfunga mkono mwengine kwa pingu
akiunganisha na kile kiti cha chuma alichokalia
Kerspersky .
Baada ya muda mfupi ule mkanda ukaanza
kumbana Kerspersky. Ulianza kumbana taratibu,
baadae kasi ya kubana ule mkono iliongezeka.
Ukazidi kubana ule mkanda !
Kerspersky alianza kusikia maumivu yakizidi.
Maumivu yakazidi sasa.
Ule mkanda ukaanza kupita kwenye nyama za
mkono wa Kerspersky.
Machozi yalianza kumdondoka
Damu zikaanza kumwagika Kerspersky !.
Kerspersky alianza kulia kwa sauti. Maumivu
hayakuwa na mfano sasa !.
"Nitasemaa.. ! "
Daniel alijifanya kama hamsikii.
Hali ilikuwa ngumu sana kwa Kerspersky.
Mkono wa Kerspersky ulikuwa unaelekea
kukatika. Sasa ule mkanda ulifika kwenye mfupa
wa mkono !
Daniel alikuwa mtu katili sana. Hakumuonea
huruma. Alikuwa anamwangalia tu Jamaa.
Sasa Daniel alitosheka. Akamfungua ule mkanda
Kerspersky.
"Utaongea" Alimuuliza huku anaangalia pembeni.
"Ndio kaka" Alijibu kwa sauti ya huruma.
"Unaitwa Nani?"
" Abednego "
"Nani anayekutuma kuua ?"
"Salehe"
"Yuko wapi sasa hivi ?"
"Mbeya"
"Amefata nini Mbeya"
Kerspersky huku analia alieleza kila kitu kuhusu
Mpango wao wa Angamizo.
Alieleza pia kuhusu watu waliotuma Kigoma na
Mara.
Daniel aliwapigia simu wakuu wa Polisi wa
Kigoma na Mara. Kuhakikisha wale watu
wamakamatwa.
Na mwenyewe alijiandaa kwenda Iringa
kusimamisha Mpango huo haramu.
Aliwachukua askari kumi pale kituo cha Polisi
Posta. Kwa ajili ya kwenda kuuangamiza Mpango
wa Angamizo.
***Ahsante, Daniel!!
ITAENDELEA