Riwaya: ANGAMIZO

iddy eba

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
573
1,171
RIWAYA.............ANGAMIZO
MWANDISHI.....HALFANI A. SUDY
SIMU..................0757 633010
SEHEMU YA KWANZA
...
Ilikuwa jumatatu tulivu sana katika mitaa ya
Arusha nchini Tanzania.
Siku iliyoanza kwa manyunyu ya mvua na radi
kidogo katika Jiji la Arusha. Kutokana na
manyunyu hayo ya mvua, hali ya ubaridi
iliongezeka katika jiji la Arusha. Baridi
iliyowafanya watu wengi kuyakumbuka makoti
yao na kuyatia mwilini.
Siku hiyo ilikuwa ya furaha sana kwa Abdul
Washiro, ilikuwa siku ambayo alikuwa anatimiza
ndoto kubwa sana katika maisha yake.
Alichaguliwa kujiunga na chuo cha Udaktari wa
Binadamu Jijini Arusha. Na jumatatu hiyo ndio
Ilikuwa siku yake ya kuripoti pale chuoni.
Abdul alikuwa na furaha sana. Hata ile hali ya
baridi haikumchukiza kabisa. Hakuwa anaihisi
baridi kabisa. Mawazo yake yote yalikuwa juu ya
kutimiza ndoto hii kubwa sana katika maisha
yake.
Wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza
walikusanyika katika ukumbi wa Chuo kwa ajiri
ya usajiri. Walikuwa wanafunzi wengi sana. Toka
mikoa mbali mbali Tanzania, waliokwenda jijini
Arusha kuisaka elimu.
Baada ya maelezo ya awali ya utambulisho toka
uongozi wa chuo, pale ukumbini, sasa ulifika
muda wa kupanga foleni ili usajiri uanze.
Kila mtu alikuwa anagombea nafasi ya kukaa
mbele ili angalau asisote sana kwenye foleni.
Ilikuwa ni fujo sana !
Abdul alikaa kwenye kiti cha plastiki akiangalia
vurugu zile. Hakuwa na wasiwasi wowote, alijua
maadamu amechaguliwa kujiunga na Chuo kile,
basi atasajiriwa tu.
Baada ya fujo kutulia, Abdul naye alienda
kujiunga kwenye foleni. Alikuwa mtu wa mwisho
katika foleni ile ya usajiri.
Alikaa kwenye foleni huku akiwaza safari yake ya
elimu ilipotokea.
*************
Abdul aliwaza jinsi alivyosoma kwa shida shule
ya Sekondari Bagamoyo. Wazazi wake hawakuwa
na uwezo wa kumsomesha. Hivyo alipata shida
sana kupata mtu mwenye moyo wa
kumsomesha. Ilibidi mchana asome sana, ili jioni
afanye biashara ndogondogo ya kuuza karanga ili
aweze kupata hela ya mahitaji madogomadogo
ya shule.
Baba yake Abdul alikuwa mvuvi . Lakini pesa
akizopata kutokana na kazi yake ya uvuvi
zilitosha kuilisha familia yake tu. Hii ilitokana na
Mzee Washiro kuwa na familia kubwa ya watoto
saba.
Mama yake hakuwa na kazi zaidi ya kuchuuza
samaki mtaani, samaki wa mumewe. Inamaana
ilikuwa sawa na kusema, baba na mama yake
Abdul walikuwa wanafanya biashara moja. Baba
anavua samaki, tena kwa zana dhaifu za uvuvi na
mama anawauza kwa kuwachuuza mtaani.
Katika watoto wote saba wa baba na mama
Abdul. Abdul pekee ndio alikuwa anasoma shule.
Wengine wote hawakutaka hata kusikia neno
shule. Hawakuona umuhimu wa shule. Waliona
kaka yao akivyoteseka kwa ajiri ya kusoma.
Kupata sare, madaftari na michango
midogomidogo ilikuwa shida.
Nduguze Abdul wote walikuwa wanashinda pwani
wakijitafutia ridhiki. Hata hivyo hawakuwa
wanapata ridhiki ya kutosha.
Pamoja na shida zote hizo, Abdul alijitahidi sana
katika masomo ili afanikiwe, na kuisaidia familia
yake iliyotopea katika dimbwi la umaskini.
Ukweli alikuwa anafanya vizuri sana darasani.
Siku zote alikuwa anaamini elimu ndio mkombozi
wake. Elimu ndio silaha pekee ya kuishika kwa
maskini kama yeye.
Na aliishika kweli elimu.
Mungu hamtupi mja wake ! Alifanikiwa kumaliza
kidato cha nne pale shule ya Sekondari
Bagamoyo, na kufaulu vizuri sana.
Abdul alichaguliwa kujiunga na masomo ya kidato
cha tano katika shule ya Sekondari Ndanda.
Pamoja na kuijua thamani ya elimu, lakini
alipofaulu, Abdul pia aliitambua thamani ya pesa.
Alijua kwamba kumbe pesa na elimu vilikuwa
vinaenda sambamba.
Abdul hakuwa na pesa kabisa ya kuweza
kumpeleka shule.
Kwanza nauli kutoka Bagamoyo hadi Mtwara,
mkoa iliyopo shule hiyo Ilikuwa mtihani.
Hapo hujajumuisha pesa ya ada pamoja na vitu
vingine vya shule.
Ndoto yake ya kusoma Abdul ilikomea hapo.
Alihisi hawezi tena kuendelea na kusoma.
Hata wazazi wake walimwambia hivyo!
Baba yake alikuwa na jukumu zito la kuhakikisha
familia inakula, familia inatibiwa, familia inavaa
pia . Hakuwa na kipato cha kutosha
kumuwezesha Abdul kwenda Mtwara kusoma.
Abdul alikuwa na akiba ya shilingi elfu kumi
iliyotokana na biashara zake za kuuza karanga
jioni.
Kumbuka Abdul ndiye alikuwa mkubwa katika
familia hii. Alikuwa na ndugu sita nyuma yake,
wote wakimwangalia yeye.
Aliamua kuzifuta kabisa fikra za kukata tamaa.
Aliamini kukata tamaa ni dhambi kubwa sana
katika maisha.
Aliyakumbuka vizuri maneno ya Mwalimu wake
wa Kiswahili wakati anasoma pale Bagamoyo
sekondari.
"Usipende kukata tamaa ukiwa bado unaishi,
pambana hadi pumzi yako ya mwisho, hakuna
linaloshindakana chini ya jua".
Maneno hayo ya mwalimu wake yalijirudia katika
kichwa chake.
Aliapa lazima asome kwa njia yoyote ile.
Alikuwa anajiona mwenye wajibu wa baadae
kuwasaidia wazazi wake. Kusaidia ndugu zake
pia.
"Lazima nisome !"
**********
Alihisi maneno hayo anayesema polepole maneno
hayo. Haikuwa hivyo, yalisikiwa na mtu aliyekuwa
mbele yake katika foleni ile ndefu ya usajiri.
"Unaonekana una mawazo sana kaka" Sauti
nyororo ya dada aliyekuwa mbele ya Abdul
ilipenya kwenye masikio yake.
"Hapana, sina mawazo dada"
"Mbona unaongea peke yako sasa ?"
Hakujibu.
"Naitwa Mayasa"
"Naitwa Abdul"
"Tunaweza kuonana baadae sehemu tofauti na
hapa?"
"Bila shaka"
Walibadirishana namba zao za simu palepale
kwenye foleni.
Zoezi la usajiri lilichukuwa saa zipatazo tano.
Hatimaye Abdul akasajiriwa kama mwanafunzi
wa udaktari katika chuo cha udaktari Arusha.
Kuwa Daktari ilikuwa ndoto yake ya siku nyingi
sana. Alikuwa anajua masomo ya msingi ili awe
Daktari.
Alikazana sana katika masomo hayo. Alijitahidi
sana katika somo la Kemia. Alijitahidi sana katika
somo la Fizikia, na alijitahidi pia katika somo la
Baiolojia.
Alifanikiwa kupata A katika masomo hayo matatu
pale Bagamoyo Sekondari.
Alikuwa anapenda awe daktari ili aje kusaidia
wananchi maskini wanaoteseka kwa kukosa pesa
za matibabu.
Siku zote alikuwa anajisemea mwenyewe. "Mimi
ndiye daktari pekee nitakayekuwa mkombozi kwa
maskini wote wanaoteseka kwa maradhi mbali
mbali kwa kukosa pesa za matibabu"
Baada ya kusajiriwa, Abdul alienda katika Hosteli
za chuo kupumzika.
Alijilaza kitandani huku akikumbuka misukosuko
ya safari yake ya elimu. Alikumbuka alivyoteseka
kipindi kile anatafuta hela ya ada pamoja na ya
matumizi ili aende kusoma shule ya Sekondari
Ndanda.
Alienda kuomba serikalini lakini hawakumuelewa.
Alienda kuomba kwa Mbunge wake naye
hakumuelewa . Hakupata hela ya ada, hakupata
hela ya nauli.
Bado alikuwa na elfu kumi ndani, chini ya mto
wake wa kulalia.
Ilikuwa bado wiki moja ili shule ifunguliwe. Na
Abdul akaanze kidato cha tano. Sasa ndoto yake
ilikuwa inaanza kuyeyuka. Hakuwa na njia ya
mkato ya kumpeleka shule.
" Si ruhusa kukata tamaa katika maisha ukiwa
bado unaishi.."
Kauli ya mwalimu wake ilijirudia tena katika
kichwa chake.
"Sasa kwanini mimi naruhusu kukata tamaa
nikiwa bado ninaishi. Tena na afya tele.
Haiwezekani !
Lazima niende Mtwara nikasome "
Usiku wa siku ile alipata wazo. Wazo ambalo
lilipewa baraka na kichwa chake.
Aliamua kwenda Mtwara kwa miguu! Alikuwa
ameamua hivyo!
Usiku ule ule aliweka vitu vyake vyote sawa.
Tayari kwa safari.
Asubuhi aliwaambia wazazi wake.
"Baba na Mama mimi leo naenda shule "
"Umepata ada mwanangu ?" Mama yake
alimuuliza kwa sauti yake ya upole.
" Hapana"
"Sasa utaenda vipi shule ?" Baba yake alimuuliiza
nae.
" Kwa miguu"
"Miguu ?"
"Ndio wazazi wangu. Lazima niende Mtwara
kusoma. Na nimeamua kwenda Mtwara kwa
miguu !"
Alisema akiwa anajiamini sana.
"Hivi Abdul unaujua umbali wa Mtwara kutoka
hapa ?"
"Siujui, lakini nitafika !"
"Ni mbali sana Mtwara, huwezi kwenda kwa
miguu Abdul !" Mama yake alimwambia kwa sauti
yake ya upole.
"Nimeshafunga kila kitu changu. Ilibaki kuwaaga
nyinyi na ndugu zangu. Nakubali Mtwara ni mbali.
Lakini bila elimu safari yetu ya kuelekea kwenye
mafanikio inazidi kuwa mbali. Bora niumie kwa
kutembea kwa miguu kuisaka elimu. Kuliko
kuumia kwa umaskini huu uliotukuka!.
Umaskini umeweka kambi nyumbani kwetu.
Hautaki kutuacha hata kidogo. Na kitu pekee
kinachoweza kuufukuza umaskini huu kipo
Mtwara.
Lazima niende Mtwara ! "
"Tufanye utaenda Mtwara kwa miguu. Je hela ya
ada utaitoa wapi?" Baba alimtupia swali zito.
Alifikiria kidogo akajibu.
"Nitajua huko huko Mtwara. Lakini lazima nifike
Mtwara kwanza. Mambo mengine yatajijibu huko
huko."
Wazazi wake hawakuwa na jinsi. Walimruhusu
aende Mtwara !
Mama yake alikuwa analia machozi kwa
kumuonea huruma Abdul. Baba yake alikuwa
anamhurumia pia.
Abdul alikuwa jasiri na imara katika msimamo
wake. Alidhamiria kwenda kusoma Mtwara kwa
njia yoyote ile !
Baba aliwaita ndugu zake wote. Akawaambia juu
ya safari ya Abdul ya kwenda shuleni Mtwara,
tena kwa miguu !
Ndugu zake wote walisikitika sana. Kila mmoja
aliingia ndani na kutoa akiba aliyojiwekea na
kumpa.
Abdul alianza safari yake ya kutoka Bagamoyo
kwenda Mtwara akiwa na elfu ishirini tu.
Familia nzima aliiacha kwenye majonzi makuu.
Hakujari !
Hakusikitika !
Alidhamiria kwenda kusoma. Alidhamiria kweli
kwenda Mtwara kwa miguu !
*****************
Abdul alikuwa katikati ya mawazo, simu yake
iliita.
Aliangalia kwenye kioo cha simu yake, alikuwa
Mayasa !
Aliipokea na kuanza kumsikiliza.
"Hallo"
"Mambo Abdul "
"Safi Mayasa, nambie"
"Nipo tu, nilikuwa na ombi moja Abdul "
"Nakusikiliza"
"Naomba nikualike chakula cha usiku leo"
"Haina shida, wapi ?"
"Tukutane Tengeru hoteli saa mbili usiku"
"Sawa Mayasa "
"Sawa baadae"
Simu ikakatwa.
Alipoambiwa habari ya chakula cha usiku.
Alikumbuka kitu.
Alimkumbuka Raiya.
Mwanamke aliyesoma nae shule ya Msingi kule
Bagamoyo, na kuja kukutana nae kama bahati
jijini Dar es salaam. Alikutana nae kama bahati
siku ile anatembea kutoka Bagamoyo kuelekea
Mtwara kwa miguu.
Siku ile alitembea kweli kwa miguu kutoka
Bagamoyo hadi Dar es salaam. Alipofika Mwenge
ndipo alipokutana na Raiya akiwa anauza duka la
simu pale Mwenge.
Ni Raiya ndiye aliyemuona na kumwita Abdul.
"Mambo Abdul?"
"Safi Raiya, za siku ?"
"Nzuri, vipi mbona na begi mkononi, unaenda
wapi ?"
"Mtwara "
"Mtwara utapata gari sahivi. Saa saba hii
Abdul ?"
"Naenda kwa miguu "
"Miguu ?!!!"
"Ndiyo Raiya"
Abdul alimsimulia kila kitu Raiya kuhusu maisha
yake.
Alivyofika mwisho aliukuta uso wa Raiya
hautamaniki.
Umelowa kwa machozi. Alimuonea huruma, na
kuahidi kumsaidia.
"Ngoja nikupe hela hii ukapumzike Hotelini.
Halafu kesho nitakusafirisha Mtwara. Na pesa ya
ada nitakupa"
"Ahsante sana Raiya yaani sijui nikushukuru vipi
dada yangu."
"Jioni nikifunga hapa nitakupigia simu tukapate
chakula cha usiku sehemu"
"Sina simu Raiya"
Raiya alitoa simu moja iliyokuwa kwenye droo
pale dukani na kumkabidhi. Kwa siku ile alimuona
Raiya Mungu mtu. Alienda kutafuta chumba cha
kupumzika. Kebby hoteli lilikuwa jibu lake.
Akaingia ndani na kukaa kitandani. Aliitoa ile
simu aliyopewa na Raiya na kuichaji
Kebby hotel ilikuwa hoteli nzuri ya kisasa yenye
gharama nafuu iliyokuwa Kijitonyama. Ilikuwa na
kila kitu ndani. Kwa Abdul Ilikuwa ni mara yake
ya kwanza kulala kwenye hoteli kubwa kama ile.
Siku ile ilikuwa ni moja ya siku aliyokuwa na
furaha sana. Ndoto yake ya kusoma ilikuwa
inaenda kutimia. Tena inatimizwa na mtu
ambaye hakutegemea kabisa. Kweli usimdharau
mtu yeyote duniani. Ingawa yeye na Raiya
hawakuwa marafiki kipindi wanasoma, lakini
walikuwa wanaheshimiana sana. Heshima ile bila
shaka ilimpa moyo Raiya wa kumsaidia leo hii.
Saa moja kamili walikutana na Raiya pale Kebby
hoteli. Kulikuwa na mgahawa mzuri wa kisasa
mbele ya hoteli ile. Walikaa na kupata chakula
cha usiku.
Wakati wanakula waliongea mambo mengi sana
na Raiya.
Raiya alimsimulia mambo mengi sana Abdul
kuhusu maisha yake. Kumbe kwa sasa Raiya
alikuwa mke wa mtu. Alimsimulia mateso
aliyokuwa anayapata toka kwa mumewe.
Mumewe hakuwa anampa vizuri haki yake ya
ndoa .
" Sasa Abdul mimi nitakupa hela"
"Nitashukuru sana yaani dada yangu"
"Lakini kwa sharti moja tu"
"Nipo tayari kufuata sharti lolote Raiya"
"Kweli ?"
"Kweli nakwambia"
"Nitakupa shilingi laki tano leo. Na nitakuwa
nakutumia matumizi kila utakapohitaji. Lakini
naomba twende chumbani ukaniridhishe Abdul.
Ukaupe nafuu moyo wangu.
Ukanipe vile nilivyovikosa tangu niolewe na
mume wangu."
Na tutakuwa tunafanya hivyo kila nitakapokuwa
nahitaji !
Abdul alipigwa na butwaa. Kwanza hakutegemea
kupata msaada mkubwa kama ule kutoka kwa
Raiya. Ulikuwa msaada mkubwa uliokuja wakati
akiouhitaji sana.
Kwa Abdul, laki tano Ilikuwa ni zaidi ya msaada.
Tatizo lilikuja katika sharti lake. Raiya alikuwa
anataka kufanya mapenzi na Abdul. Lilikuwa
sharti gumu sana kwa Abdul. Pesa alikuwa
anazitaka sana lakini kufanya mapenzi Na Raiya
tena mke wa mtu alikuwa hataki kabisa !
"Umenielewa Abdul ? "
" Nimekuelewa Raiya, lakini wewe mke wa mtu"
"Kwahiyo ? "
"Utakuwa humtendei haki mumeo"
"Hizi laki tano ninazotaka kukupa wewe
nimemuibia yeye. Je kumuibia hela zake ni
kumtendea haki ?" Raiya aliongea huku
akimuonesha burungutu kubwa la pesa.
"Kama hutaki pesa nenda kwa miguu Mtwara !"
Abdul alikuwa katika wakati mgumu sana wa
kufanya maamuzi katika maisha yake. Alijikuta
anakubari kufanya mapenzi na Raiya, siyo kwa
kumpenda ila kwa kupenda kusoma.
Aliamua kuutumia mwili wake kwa manufaa ya
maisha yake ya baadae. Walivunja amri ya sita
ndani ya Kebby hoteli !
*****************
ITAENDELEA BAADAE
 
SEHEMU YA PILI
Tatizo lilikuja katika sharti lake. Raiya alikuwa
anataka kufanya mapenzi na Abdul. Lilikuwa
sharti gumu sana kwa Abdul. Pesa alikuwa
anazitaka sana lakini kufanya mapenzi Na Raiya
tena mke wa mtu alikuwa hataki kabisa !
"Umenielewa Abdul ? "
" Nimekuelewa Raiya, lakini wewe mke wa mtu"
"Kwahiyo ? "
"Utakuwa humtendei haki mumeo"
"Hizi laki tano ninazotaka kukupa wewe
nimemuibia yeye. Je kumuibia hela zake ni
kumtendea haki ?" Raiya aliongea huku
akimuonesha burungutu kubwa la pesa.
"Kama hutaki pesa nenda kwa miguu Mtwara !"
Abdul alikuwa katika wakati mgumu sana wa
kufanya maamuzi katika maisha yake. Alijikuta
anakubari kufanya mapenzi na Raiya, siyo kwa
kumpenda ila kwa kupenda kusoma.
Aliamua kuutumia mwili wake kwa manufaa ya
maisha yake ya baadae. Walivunja amri ya sita
ndani ya Kebby hoteli !
*****************
Abdul alistuka na kuangalia saa yake ya mkononi.
Akakumbuka alikuwa na ahadi na Mayasa saa
mbili usiku Tengeru.
Na sasa Ilikuwa saa moja kamili. Alijiandaa kwa
ajiri ya kwenda kutekeleza ahadi hiyo.
Alioga.
Akavaa suruali yake nzuri ya jeans pamoja na T-
shirt nyeupe iliyoandikwa maneno kwa rangi
nyeupe 'Napenda Riwaya". Chini alivaa raba
nyeupe, zenye nembo ya Ocafona. Alijupulizia
pafyumu. alikuwa ananukia vizuri sana.
Akaenda Tengeru hoteli.
Alifika hotelini saa mbili na dakika mbili usiku.
Alimkuta Mayasa ameshawasiri tayari. Mayasa
alimlaki kwa furaha kubwa sana.
Walikaa na Mayasa na kuongea mambo
mbalimbali hadi saa nne usiku.
Ndipo Mayasa alipotaka kujua sababu ya Abdul
kuwa na mawazo na kuongea peke yake.
"Abdul"
"Naam"
"Kwanini unaonekana mtu mwenye mawazo
sana ?"
"Niko sawa Mayasa"
"Hauko sawa Abdul,unafikia hatua ya kuongea
peke yako Abdul "
"Kweli nina matatizo Mayasa, ila tutafute sehemu
iliyotulia zaidi ya hapa nitakueleza.
Wewe ushakuwa rafiki yangu sasa sina budi
kukwambia kila kitu kinachonisibu "
"Nitafurahi sana, sehemu gani unadhani itakuwa
nzuri kwako "
"Popote patakapokuwa pametulia zaidi ya hapa"
"Sawa kesho jioni nitakupigia. Tutaenda Moshi.
Kule kuna bustani moja nzuri sana kwa
maongezi"
"Sawa Mayasa"
Walikodi teksi pale Tengeru liyowarudisha hadi
Arusha mjini. Mayasa alimuacha Abdul hosteli za
Chuo, na yeye kuelekea nyumbani kwao.
Kesho yake jioni, Abdul na Mayasa walienda
Moshi, Paradise garden ndipo alipompeleka.
Ilikuwa sehemu tulivu. Yenye maua mazuri na
majani machache yaliyopandwa kwa ustadi
mkubwa. Kulikuwa na meza zilizokaa mbali
mbali.
Walichagua meza moja . Walikaa na Mayasa na
alianza kumsimulia historia ya maisha yake.
Alimsimulia Mayasa historia yake kuanzia
Bagamoyo. Magumu yote aliyopitia katika
kusoma. Alimsimulia jinsi alivyokutana na Raiya.
Na mkataba wa ngono alioingia na Raiya.
Sasa alikuwa mtumwa wa ngono wa Raiya.
Kumpa penzi Raiya kila atakapojisikia, naye
kumhudumia katika matatizo yake yote.
"Ukweli sikuwa nampenda Raiya. Sikuwa napenda
mkataba ule wa ngono. Niliuchukia sana. Lakini
sikuwa na jinsi Mayasa. Nilikuwa napenda
kusoma. Ilibidi nifanye akivyotaka Raiya.
Naamini Raiya nae hakuwa ananipenda.
Alinipenda mimi kwa ajili ya ngono tu, alinifanya
'sex toy. Nilimaliza kidato cha sita kwa
kusomeshwa na Raiya chini ya mkataba ule wa
ngono.
Matokeo ya kidato cha sita yalipotoka nilifaulu
vizuri . A ya baiolojia B ya fizikia na B ya Kemia.
Nilichaguliwa kusomea udaktari. Katika Chuo cha
udaktari hapa Arusha. Ambapo ndipo jana
nilikutana na wewe."
"Daah pole sana Abdul. Hakika umepitia makuu.
Umekuwa mtumwa wa mapenzi. Sasa una
mpango gani Abdul ?"
"Natamani kujitoa katika utumwa huo. Lakini sina
jinsi Mayasa. Elimu yangu inamtegemea Raiya.
Maisha yangu yanamtegemea Raiya.
Nitakapomaliza Chuo na kupata kazi hapo ndipo
nitakuwa nimejivua utumwa. Utumwa wa
mapenzi kama ulivyouita ".
" Nataka nikusaidie Abdul bila sharti lolote.
Dhamira yangu ya ndani nimeamua kukusaidia.
Nimependa harakati zako za kuitafuta elimu.
Unaonesha unapenda kusoma, na una akili sana."
"Nashukuru sana Mayasa. Wewe ni mwanamke
mwenye moyo wa ajabu sana."
Walimaliza kuongea na Mayasa saa nne usiku.
Walikodi gari iliyowarejesha Arusha mjini.
Sasa Abdul alihamia himaya mpya. Himaya ya
Mayasa, alimkabidhi kila kitu Mayasa kuhusu
maisha yake, kasoro moyo tu. Alipunguza
mawasiliano na Raiya na kuongeza mawasiliano
na Mayasa.
****************
Ilikuwa siku ya jumatano jioni ya wiki ya pili
tangu waanze chuo.
Abdul alikuwa na Mayasa wanajisomea darasani
muda wa jioni.
Simu ya Abdul iliita.
Alikuwa Raiya anapiga.
" Wewe unajifanya kiburi. Mimi nimekusomesha
umefika Chuo unajifanya mjanja. Sasa kesho
nakuja huko huko Arusha nione kinachokuzuzua.
Ole wako nisikie una mwanamke. Ole wako !"
Bila salamu Raiya aliwaka kwenye simu.
Hakumjibu.
Alikata simu na kuizima kabisa !
Hamu ya kusoma ilimuisha. Mayasa alisikia kila
kitu alichosema Raiya. Raiya alikuwa alimkaripia
kama mtoto Abdul na kwa nguvu.Halafu walikuwa
karibu na Mayasa .Alimuonea sana huruma.
Hamu ya kusoma ilimuisha.Alimuaga Mayasa na
kurudi hosteli.
Alifika kitandani na kulala chali. Alifikiria
mustahabari wa maisha yake. Alijiona ni mtu
mwenye mikosi.
Aliulaumu umaskini wake. Aliulaumu umaskini wa
wazazi wake. Machozi yalitoka yenyewe taratibu.
Akauhisi mkono laini ukimfuta machozi.
Alifumbua macho yakevna kuangalia. Alikuwa
Mayasa..!
"Acha kulia Abdul. Nimejitoa kukusaidia kwa
lolote kaka yangu. Naamini tutaushinda mtihani
huu.Tutamshinda Raiya. Sitokubali ulie tena."
Mayasa alimbembeleza sana Abdul. Mwishowe
akamwelewa.
Akanyamaza.
Ilipita wiki moja tangu Raiya ampe vitisho vyake
Abdul. Hakutokea Arusha wala hakumpigia simu.
Akajua labda amekata tamaa. Akawa anaishi
maisha yake kama kawaida. Furaha ikarejea
tena.Huku akimtegemea Mayasa kwa kila kitu.
Naye hakuchoka.Alimsaidia Abdul.
Upande wa darasani alikuwa anafanya vizuri sana
katika masomo. Alikuwa na uwelewa mkubwa
sana. Mayasa hakuwa mzuri sana darasani.
Alijitahidi kumsaidia kila alipopata nafasi.
Alielewana sana na Mayasa.
Walifatana muda wote. Walijisomea pamoja.
Walikuwa mithili ya chanda na pete.
Kila mwishoni mwa wiki walikuwa wanatoka nje
ya jiji la Arusha kutembea na Mayasa.
Siku moja jumamosi Abdul na Mayasa iliwakuta
Same. Sasa walikuwa marafiki walioshibana.
Abdul alikuwa anafahamu sasa baadhi ya vitu
vya Mayasa. Kumbe baba yake Mayasa alikuwa,
Ally Hamisi. Makamu wa raisi wa Zanzibar. Baba
yake alikuwa mtu mkubwa sana Serikalini lakini
hakuna hata siku moja aliyemtamkia mdomoni
Abdul. Alisikia tu kutoka kwa watu wa pembeni.
Siku waliyoenda Same, walirudi chuoni saa kumi
na mbili jioni kutoka.
Same Ilikuwa mbali kidogo na Jiji la Arusha.
Mayasa alimrudisha kwanza Abdul hosteli ili na
yeye arudi kwao. Walienda Same na gari
Mayasa.
Walipofika karibu na chumba cha Abdul, nje
walikutana na Justus. Kijana aliyekuwa wanakaa
chumba kimoja pale hosteli.
"Daah afadhali umerudi Abdul, kuna mgeni wako
ndani"
"Nani ?"
"Simfahamu, ila amefika zamani sana"
"Sawa kaka"
Waliingia ndani na Mayasa. Wakiwa hawana
wasiwasi hata kidogo. Walipofungua mlango na
kuingia ndani walimwona msichana amelala
kitandani kwa Abdul.
Wote walistuka sana!
Walipomwangalia kwa makini, Abdul alimgundua
msichana yule.
Alikuwa Raiya !
"Naitwa Raiya Mohamedi" Aliongea huku
akimwangalia Mayasa usoni.
"Naitwa Mayasa Ally" Mayasa nae alijibu kwa
kujiamini.
"Wewe ndiye unajifanya unajua kutembea na
wanaume wa watu ?"
"Sema kilichokuleta "
"Kilichonileta ndio hiki ninachoongea "
"Usione vyaelea dada......"
"Sina muda wa kuongea na wewe"
"Abdul ?" Raiya aliita.
Hakuitika
"Umenisaliti kwa sababu ya hiki kikaragosi ?"
Abdul alikaa kimya anamwangalia tu.
" Kumbuka nilipokutoa Abdul, Kumbuka Siku ile
pale Mwenge, ningekuacha ungekutana na hiki
kikaragosi leo ? "
Raiya aliongea maneno yaliyomuingia kidogo
Abdul.
Pamoja na madhaifu yake kadhaa lakini Raiya
alikuwa na mchango mkubwa sana katika maisha
ya Abdul hadi alipofikia sasa.
"Sasa chagua moja Abdul. Utakuwa na mimi au
huyu ?" Raiya aliongea kwa jazba.
Abdul alibaki njia panda. Raiya na Mayasa wote
walikuwa na mchango mkubwa katika maisha
yake. Na wote walimwangalia yeye kusubiri jibu
langu.
" Mayasa siyo mpenzi wangu" Alijua ametamka
kwa sauti kumbe sauti haikutoka nje. Mdomo
ulikuwa unatetemeka tu.
"Chagua Abdul"
"Achague nini, mimi Abdul siyo mpenzi wangu "
"Ni nani yako sasa ?"
"Rafiki yangu tu "
"Hahaha siku zote mapenzi yanaanzia kwenye
urafiki,
"OK marafiki. Basi mimi ni mke wa Abdul.
Nasema naomba muvuunje kabisa huo urafiki
wenu. Siutaki, siutaki, siutaki hata kuusikia.
Mkewe nimesema !"
"Raiya wewe ni mke wa Abdul ?"
"Hilo jibu uliza swali "
"Una hakika Raiya ?"
"Ndio"
"Na Salehe je, unamwitaje Raiya ?"
Swali hilo allouliza Mayasa lili mstua sana Raiya !
Hali sasa ilibadirika mle ndani !
"Mimi ni Mayasa Ally Hamisi, unanikumbuka ?"
Mumeo Salehe ni kaka yangu. Mtoto wa mama
mdogo Fatma. Au nimpigie Salehe nimuulize
kama kakuacha ?"
Mayasa aliongea huku akitafuta namba za Salehe
katika simu yake.
Raiya sasa alikuwa amechoka hoi. Hajui lipi
aseme, lipi aache. Alikosa kauli kabisa. Ghafla
alitoka nje ya hostel kwa ghadhabu mithili ya
roketi, bila ya kuaga !
Abdul aligundua kitu kimoja kuhusu Mayasa.
Mayasa alikuwa msichana msiri sana. Alimficha
cheo cha baba yake hadi sasa.
Pia kumbe alikuwa anamficha kama Raiya ni wifi
yake, hakumwambia kabla. Alianza kumwangalia
Mayasa kwa jicho la kumuogopa sasa.
" Usijari Abdul. Raiya ni wifi yangu lakini yeye
hakuwa ananijua. Tulionana na Raiya siku moja
tu. Tena siku ya harusi yake na kaka Salehe.
Hata wewe ulivyonisimulia historia ya maisha
yako. Ulipotaja jina la Raiya sikujua kama Raiya
wifi yangu, sikufikiria kabisa.
Leo nilivyomwona hapa ndio nimemkumbuka ".
Mayasa alinijibu kitu ambacho nilikuwa
nakifikiria.
"Sawa Mayasa nimekuelewa"
Walitoka nje ili kumwangalia Raiya ameenda
wapi ?
Hawakumuona.Hawakujua ameelekea wapi ?
Aliyeyuka mithili ya upepo !
Baadae Mayasa aliaga na kuondoka kwao huku
Abdul akibaki na wingi wa mawazo.
Abdul alisinzia akiwa na mawazo mengi. Lakini
kutokana na uchovu wa kutoka Same na
ukijumlisha mawazo aliyomletea Raiya ndio
yalimchosha kabisa, alilala fofofo.
Saa kumi usiku simu yake ilitoa mlio wa sauti
alioutega Kwa ajiri ya mwitikio wa ujumbe mfupi.
Ikimaanisha kuna meseji mpya iliingia.
'Umeuchokoza moto. Niliacha zamani ukatili.
Wewe unajitahidi kunirudisha huko. Nilikuwa katili
sana zamani. Kama hupendi nirudie tabia zangu
za zamani nakuomba achana na kikaragosi.
Nitakuuwa, nitamuuwa pia !.Nakupa siku tatu za
kufikiria juu ya suala hili. Mimi bado nipo Arusha.
Namaanisha!"
Abdul alikaa kitandani na kuurudia kuusoma
ujumbe ule mara tano. Jasho lilikuwa linamtiririka
kama maji. Akamtumia ule ujumbe na Mayasa.
Hakuujibu !
Hajaujibu mpaka leo !
Asubuhi na mapema watu wanne walienda katika
chumba cha Abdul. Walikuwa wamefuatana na
kiongozi wa hosteli, Mshauri wa wanafunzi, na
Raisi wa Chuo. Walimuita pembeni na
kumwambia.
"Sisi ni askari wa kituo kikuu cha Polisi Arusha.
Unahitajika kituo cha Polisi kwa mahojiano
kidogo "
"Nimefanya nini jamani ?"
"Utajua hukohuko kituoni !
Askari mmoja alimnyanyua kwa nyuma suruali
yake na kupelekwa kituoni. Alikuwa anatembelea
vidole sasa. Wanafunzi wenzie walimuonea
huruma pale chuoni .
Hakujua amefanya nini?
Hawakujua amefanya nini?
Baada ya kufika kituoni ndipo alipoambiwa kosa
lake.
Eti alituhumiwa kwa kumuua Mayasa !
Na ujumbe wake wa vitisho kutoka kwanye simu
yake yake ulikutwa katika simu yake.
Na ulitumika kama ushahidi !
Alihemewa sana !
Alilia sana !
Aliuona mwisho wa ndoto zake umetimia. Akajua
ataozea jela. Aliwekwa selo akisubiri ushahidi
ukamilike.
Akiwa ndani ya selo Abdul aliwaza mambo mengi
sana. Moja kwa moja alijua kama kweli Mayasa
ameuwawa basi Raiya ndiye mhusika mkuu wa
kifo cha Mayasa. Lakini ujumbe ule aliomtumia
Mayasa ulikuwa unamweka mashakani. Alikuwa
analia mithili ya kichanga.
Afande aliyekuwa anaitwa John ndiye alipewa
jukumu la kupeleleza kesi ya kifo cha mtoto wa
Makamu wa Raisi wa Zanzibar, Mayasa. Huku
wapelelezi mahiri Tanzania wakiletwa Arusha
kufumbua chanzo cha kifo hiki kisichoeleweka.
Afande John alianza kumhoji Abdul kwanza.
Mtuhumiwa wa kwanza wa mauaji yale.
" Unaitwa nani ? "
"Abdul "
"Majina matatu !!"
"Abdul Ramadhani Washiro"
"Kabila "
"Msukuma "
"Nambie uhusiano wako na Mayasa ?"
"Alikuwa mwanafunzi mwenzangu"
"Hamkuwa na uhusiano wa kimapenzi ?"
"Hapana,alikuwa ni rafiki yangu wa kawaida "
"Sasa kwanini uliamua kumuua rafiki yako ?"
"Sijamuua mimi afande "
"Soma huu ujumbe "
"Alinitumia Raiya, mimi nilimfowadia tu Mayasa."
"Raiya ndio nani ?"
ITAENDELEA!!!!
 
SEHEMU YA TATU
...
Afande John alianza kumhoji Abdul kwanza.
Mtuhumiwa wa kwanza wa mauaji yale.
" Unaitwa nani ? "
"Abdul "
"Majina matatu !!"
"Abdul Ramadhani Washiro"
"Kabila "
"Msukuma "
"Nambie uhusiano wako na Mayasa ?"
"Alikuwa mwanafunzi mwenzangu"
"Hamkuwa na uhusiano wa kimapenzi ?"
"Hapana,alikuwa ni rafiki yangu wa kawaida "
"Sasa kwanini uliamua kumuua rafiki yako ?"
"Sijamuua mimi afande "
"Soma huu ujumbe "
"Alinitumia Raiya, mimi nilimfowadia tu Mayasa."
"Raiya ndio nani ?"
Alimsimulia afande John kila kitu kuhusu ugomvi
wao na Raiya. Alirudishwa selo na afande John
alikwenda kwa kina Raiya kumhoji. Hakuwa
anapajua , na wala Abdul alikuwa hapajui.
Ila alisema atapajua tu !
Afande john alifanikiwa kufika nyumbani kwa
dada yake Raiya.
Baada ya kumuonesha kitambulisho cha Polisi,
Raiya alishangaa sana.
"Jamani, wewe ni askari wa tatu kuja kunihoji
leo !"
"Walikuja maaskari wengine hapa ?!"
" Ndio na mmoja katoka nusu saa iliyopita"
"Walikuwa na vitambulisho ?"
"Ndio walinionesha"
"Unayakumbuka majina yao"
"Nayakumbuka sana kwa kuwa majina yao wote
yanafanana"
"Wanaitwaje?"
"Wote wanaitwa John"
Afande John alisikia kizunguzungu na mivumo
isiyoeleweka masikioni mwake Ilikuwa taarifa ya
kushangaza sana !
"Itabidi nikakuhoji kituoni "
Afande John aliona pale siyo mahali salama pa
kufanyia mahojiano.
Walifuatana na Raiya kuelekea kituoni..!
Hapakuwa na umbali mkubwa sana toka nyumba
aliyokuwa anakaa Raiya hadi kituo kikuu cha
Polisi Arusha. Raiya alikuwa anakaa katika
nyumba ya dada yake aliyokuja kukaa kwa muda
mahsusi ili kutekeleza aliyoyakusudia,
kutenganisha penzi la Abdul na Mayasa kama
akivyoamini yeye kuwa walikuwa wapenzi.
"Raiya hebu nambie vizuri kuhusu hao askari
waliokuja kukuhoji kwako."
" Ndiyo kama nilivyokwambia Afande. Walikuja
askari wawili kunihoji. Mmoja alikuja asubuhi na
mwingine alikuja muda mfupi kabla hujaja wewe.
Na wote walitaka maelezo yangu kuhusu kifo cha
Mayasa na uhusiano wangu na Mayasa na Abdul
."
"Wewe uliwajibu nini?"
"Yule wa kwanza sikumjibu kitu. Maana aliniacha
kwenye mstuko mkubwa sana baada ya
kunambia Mayasa amefariki. Sikuamini kama
Mayasa amefariki..nilikuwa nalia tu kila
alichokuwa ananiuliza . Askari yule alifanya kazi
ya kunibembeleza tu, akaondoka"
"Askari wa pili je ?"
"Yule alinikuta nimetulia sasa. Nilimueleza kila
kitu kuhusu ugomvi wetu mimi, Mayasa na
Abdul."
"Alisemaje baada ya maelezo yako ?"
"Aliandika kwenye kitabu chake na kuondoka"
Afande John alishusha pumzi ndefu .Akajua
ngoma sasa imekuwa nzito !
Akamfungia Raiya selo na kutoka nje kwenda
kutafakari. Alikaa chini ya mwembe mrefu
uliokuwepo pale nje ya kituo. Akiwaza na
kuwazua.
Simu yake ikawa inaita. Namba ilikuwa ngeni.
Zilitokea namba tu. Akaipokea na kuiweka
sikioni.
"Hallo"
"Hallo nani mwenzangu ?"
"Huna haja ya kulijua jina langu. Cha muhimu
acha kuifatilia hiyo kesi utauwawa bure. Au
unahamu ya kumuweka eda mkeo ?"
"Usinitishe kijana "
"Nitakuuwa !"
"Huna jeuri hiyo"
"Unajifanya kiburi"
"Nitawakamata wote wauaji waoga!'
" utaenda kutukamata kuzimu.."
Afande John alihisi amerukiwa na kitu kama maji
maji utosini. Aligusa kwa mkono wake wa kulia.
Aligusa yale maji. Sauti ya kwenye simu ilianza
kucheka.
Ghafla ngozi ya afande John ilianza kuvuka.
Afande John alitupa simu chini, alisikia maumivu
makali sana. Alikufa taratibu kwa maumivu
makali sana!
Alikufa aina ya kifo sawa na alichokufa Mayasa !
Sasa ilikuwa mshikemshike. Mauaji ya Polisi
kuuwawa nje ya kituo. Ilizua mambo mengi.
Mauaji haya ya pili yaliwafanya Polisi wafikirie
nje ya boksi. Watuhumiwa wawili wapo ndani,
lakini Afande John kauwawa akiwa nje. Bila
shaka na wauaji walewale waliomuuwa Mayasa.
Mauaji ya hayo yalilitikisa Jiji la Arusha. Arusha
iligeuzwa nje ndani kumtafuta muuaji au wauaji.
Hawakupata fununu zozote. Polisi walibaki
gizani.
Giza totoro !
Mayasa alikuwa Mtoto wa mkubwa Serikalini.
Serikali ilituma wapelelezi mahiri watatu. Kwenda
Arusha kumsaka muuaji !
Walienda wapelelezi watatu. Lakini kila mmoja
alivuliwa ngozi kwa siku yake. Waliuwawa kwa
maji yaleyale yaliyomuua Mayasa. Maji yaleyale
yaliyomuuwa afande John !
Mmoja alikutwa amekufa hotelini kwake, akiwa
amelala.Ngozi ikiwa imejitenga na mwili wake !
Wapili alikutwa amekufa akiwa kwenye gari lake.
Aina ileile ya kifo alichouwawa mwenzake.
Wa mwisho aliuwawa mgahawani. Akiwa anakula
chakula cha usiku.
Hali sasa ilitisha !
"Ndani ya selo hali Abdul Ilikuwa mbaya sana.
Polisi hawakuwa wamempiga hata kidogo . Lakini
alikuwa amechoka taabani. Alichoka kimwili.
Alichoka kimawazo.
Kifo cha Mayasa kilimuumiza sana kichwa. Akilini
mwake alijua Raiya anahusika kwa asilimia zote.
Aliukumbuka sana wema wa Mayasa. Mayasa
alikuwa kama malaika kwa Abdul. Mayasa
alikuwa mwanamke mwenye roho ya kipekee
sana.Alimsaidia bila ya sharti lolote.
Alimkumbuka kila dakika mle selo.
Sasa alimchukia sana Raiya. Chuki kwa Raiya
ilianza taratibu.
Lakini sasa ilikuwa imeota mizizi. Alimwona ni
adui yake namba moja duniani. Adui kwa kumuua
Mayasa. Rafiki mwenye upendo wa kweli kwake.
Wazazi wake hawakuwa wanajua kama yuko jela.
Na wala hakutaka kuwaambia, maana hata
angewaambia isingesaidia lolote, maana hakuna
atakayeenda Arusha. Wasingekuwa na nauli ya
kwenda Arusha. Alikuwa anaijua hali ya uchumi
ya nyumbani kwao. Aliacha kuwaambia akihofia
kuwapa presha za bure.
Wakati akiwa anawaza hayo, mlango wa selo
ulifunguliwa. Aliingia askari mmoja wa kike.
Alikuwa na sura ya huzuni. Alikuja kumpa taarifa
mbaya ya kifo. Taarifa ya kifo cha Afande John !
"Inamaana Raiya kamuua na Afande John ?"
" Sidhani kama Raiya anahusika. Afande John
amefariki wakati Raiya yuko selo"
"Unasema !"
"Ndio hivyo Abdul, hebu tuambie mtu mwengine
unayehisi anaweza kuwa nyuma ya mauaji haya
Abdul ?"
"Hakuna nilijualo Afande kweli sijui kitu afande"
Alisema huku machozi yanamtoka .
Alirudishwa selo baada ya mahojiano mafupi na
askari yule wa kike.
Sasa akaona uzito na ugumu wa kesi hii
iliyokuwa inamkabiri. Akaamua kuwaeleza wazazi
wake Bagamoyo kwa simu. Hakuwa na jinsi sasa.
Alikuwa anahitaji hekima za wakubwa. Alikuwa
anahitaji sana majaliwa ya Mungu. Kutoka katika
mkasa huu mzito...!
Aliwaomba askari wampe simu ili awapigie
wazazi wake. Awataarifu juu ya kukamatwa
kwake.
Walimruhusu.
Alimueleza baba yake mzazi, Mzee Washiro juu
ya kukamatwa kwake na Polisi na tuhuma za
mauaji zinazomkabiri. Alisikitika sana baba yake.
Kwa mara ya kwanza alimsikia baba yake akilia
kwenye simu. Alipatwa na uchungu sana.
Abdul alikuwa mtoto wake wa kwanza kati ya
watoto saba. Alikuwa ndiye tumaini hai la familia
yake. Mtoto aliyesoma zaidi ya wote katika
familia yake.
Habari ya kutuhumiwa kwake kwa kesi ya mauaji,
kwa baba yake ilikuwa mithili ya kuzimika ghafla
kwa mshumaa pekee akioutegemea gizani.
Pamoja na yote alimuahidi kitu. Alim-ahidi lazima
aende Arusha punde atakapopata pesa.
Abdul alijua baba yake hatokukwenda Arusha
karibuni. Na pengine hatokwenda kabisa. Na
anaweza kuozea jela Arusha bila kumuona ndugu
yake yeyote. Walikuwa mafukara sana nyumbani
kwao. Lakini kidogo alipata imani. Kwakuwa
nyumbani kwao walikuwa wanafahamu sasa
kuwa mtoto wao yupo katika matatizo makubwa
ugenini.
Kwa upande wa Polisi wa Arusha Ilikuwa
hekaheka ndani ya Jiji. Walitafuta wachuna ngozi
wale wasio na huruma bila mafanikio.
Walimkamata kila waliyemuhisi, lakini
hawakufanikiwa kumkamata muuaji halisi. Ilikuwa
kama ametoweka ghafla Arusha. Jiji lilibaki
likisubiri Muuaji yule katili ataibukia wapi ?
Baada ya wiki mbili yalitokea mauaji !. Safari hii
katika Jiji la Mwanza .
Mauaji ya aina ileile kama yaliyotokea Arusha.
Katika Chuo kikuu cha St Augustine cha huko
jijini Mwanza kuna mwanafunzi aliuwawa kikatili.
Alikuwa anatoka kujisomea usiku akielelekea
Hosteli. Alinyang'anywa njiani roho yake !
Maiti yake iliokotwa asubuhi katika uwanja wa
mpira wa chuo ikiwa haitamaniki !
Ngozi iliokotwa upande wa goli la kaskazini.
Kiwiliwili kisicho na ngozi kiliokotwa karibu na
goli la kusini.
Yalikuwa mauaji ya kinyama sana ! Yaliowaacha
na uwoga mkubwa sana wanafunzi wa Chuo hiko
kikubwa jijini Mwanza.
Mwanafunzi huyo alikuwa ni mtoto wa waziri wa
ujenzi, Mheshimiwa Karimu Nduguga. Polisi wa
Mwanza nao wakalipata hekaheka kama
ilivyokuwa kwa wenzao wa Arusha, wa kumsaka
muuaji huyo asiye na huruma !
Lakini hawakumpata na wala hawakukaribia
kumpata.!
Ndipo hali ya hatari ikatangazwa nchi nzima, na
Waziri wa wa mambo ya Ndani ya nchi,
Mheshimiwa Frank Chali. Ilitolewa tahadhari hasa
kwa watoto wa viongozi wakuu wa chama na
Serikali.
Watoto wa vigogo wakawa wanalindwa hasa.
Huku doria za Polisi zikishamiri Tanzania mzima.
Abdul na Raiya waliendelea kusota selo. Sasa
walihamishiwa Gereza kuu Arusha.Ilikuwa kwa
usalama wao kama Polisi walivyosema.Wiki mbili
zilipita maisha yao yakiwa selo.
Ilikuwa siku ya jumatatu asubuhi. Ya wiki ya tatu
tangu wahamishiwe Magereza. Abdul alitolewa
selo na kupelekwa katika chumba cha mahojiano
cha Gereza lile. Siku hii alihojiwa na mtu mpya.
Hakuwa wa gereza la Arusha. Maana wengi
ailikuwa anawafahamu sasa.
"Unaitwa nani ?"
"Naitwa Abdul Ramadhani "
"Niambie kwa kifupi unavyolielewa sakata hili ?"
Alimsimulia kila kitu tangu safari yangu ya kutoka
Bagamoyo hadi nilivyofika Arusha.
"Unajua Kwa nini umewekwa ndani ? "
"Ndio"
"Kwanini ?"
"Kwa ajiri ya usalama wangu."
"Sasa mimi nataka nikutoe nje Abdul "
"Ati !"
"Ndio nataka uisaidie Polisi ukiwa nje"
"Nahofia usalama wangu, wataniua vibaya "
"Usiwe na shaka. Utakuwa na mimi kila hatua
utakayopiga,
mimi naitwa Daniel Mwaseba !!"
Alistuka sana kusikia jina hilo. Hakuna Mtanzania
ambaye alikuwa halijui jina la Daniel Mwaseba .
Alikuwa mpelelezi namba moja Tanzania. Alikuwa
mtu hatari kuliko hatari yenyewe. Alishawahi
kuliokoa Taifa hili katika matatizo makubwa
sana. Aliliokoa kutoka katika hila mbaya za
maadui zetu. Alikuwa kijana makini, mpiganaji,
mzalendo wa kweli kwa nchi yake.
Kuja kwa Daniel Mwaseba kwenye kesi hii Abdul
akajua mambo yamefikia pagumu. Mbele ya
Daniel alikuwa radhi atolewe. Aliamini atakuwa
salama. Alikubali. Walitoka Gerezani wakiwa
wamefuatana na Daniel Mwaseba.
Alijisikia fahari kufuatana na Daniel. Njiani
nilikuwa anamuuliza hili na lile. Yeye alikuwa
anajibu kwa mkato tu. Daniel alikuwa
anampekeka Kijenge juu. Kwenye nyumba
aliyopangiwa na jeshi la Polisi kuishi kwa muda.
Hosteli haikuwa sehemu salama kwake tena.
Walishuka kwenye gari ya Daniel wakiwa
sambamba. Walikuwa wanakatisha barabara ili
waingie katika nyumba aliyopangiwa.
Wakati wakiwa katikati ya barabara gari dogo
aina ya Noah nyeusi ilikuja kwa kasi kwa lengo la
kutaka kuwagonga. Abdul aliliona lakini hakuwa
na jinsi ya kufanya. Liliwakaribia sana. Kwa kasi
ile Abdul alijua lazima wagongwe. Lazima wafe
yeye na Daniel Mwaseba.
Kilikuwa kifo dhahiri usoni mwao !
Ghafla Abdul alijikuta amerudi nyuma kwa haraka
sana !
Gari lilipita sentimita chache sana na pale
waliposimama na Daniel.
Kilikuwa ni kitendo cha haraka sana !
Abdul hakuelewa amerudi vipi nyuma kwa kasi
ile. Akamwangalia Daniel Mwaseba alikuwa
anatabasamu, hana wasiwasi wowote. Huwezi
jua kama kiliwakosa kifo sikunde chache
zilizopita .
"Mwanzo mzuri" Abdul alimsikia Daniel
akinong'ona mwenyewe.
"Hivi limetukosaje lile Gari ? Halafu alidhamiria
kutugonga kwa makusudi !."
"Nilikuvuta mkono"
Daniel alijibu jibu fupi na kumshika mkono Abdul,
wakarejea kwenye gari yake.Kwa hakika Daniel
Mwaseba Alikuwa mtu wa ajabu sana !
Kwenye gari hakuongea neno. Alikuwa kimya,
makini na usukani huku akipiga mluzi. Akiimba
wimbo usioeleweka. Lakini akiangalia kwenye
vioo vya pembeni vya gari kila mara.
"Hivi kitu gani cha siri alichowahi kukwambia
Mayasa?" Ghafla Daniel alimuuliza swali Abdul
huku akiwa anaangalia mbele.
"Hakuna kitu cha siri alichowahi nambia Mayasa"
"Una uhakika Abdul ?. Nakuuliza hili kwa ajiri ya
maisha yako. Kuficha hakukusaidii kitu "
"Kweli kaka Daniel. Hakuna siri yoyote aliyowahi
nambia Mayasa."
Safari yao ilishia kituo kikuu cha Polisi Arusha.
Walikaa kaunta pamoja na Daniel na askari
mwengine.
Mara simu ya mezani ya pale kaunta ikaita.
"Hallo "
"Napiga toka Magereza Arusha"
"Ehh nambie Afande"
"Kuna tatizo hapa Magereza"
"Tatizo gani Afande ?"
"Yule mwanamke aliyewekwa mahabusu kwa ajiri
ya usalama wake amefariki!!!"
"Nani ?"
"Raiya"
"Unasemaa !"
"Ameuwawa Afande"
"Natuma askari sasa hivi"
"Sawa"
Yule askari aliwaambia taarifa ya kifo
aliyoipokea. Ilikuwa ni taarifa ya kifo cha Raiya,
iliwastua sana. Lilikuwa pigo la ghafla na la
kushangaza sana.
Mtu kufariki akiwa mikononi mwa askari siyo
tatizo sana. Lakini mtu kuuwawa mikononi wa
askari ilikuwa ni tatizo kubwa sana. Tena ndani
ya Gereza lenye ulinzi mkali kama la Arusha.
Yalikuwa maajabu !
ITAENDELEA!!!
 
SEHEMU YA NNE
Yule askari aliwaambia taarifa ya kifo
aliyoipokea. Ilikuwa ni taarifa ya kifo cha Raiya,
iliwastua sana. Lilikuwa pigo la ghafla na la
kushangaza sana.
Mtu kufariki akiwa mikononi mwa askari siyo
tatizo sana. Lakini mtu kuuwawa mikononi wa
askari ilikuwa ni tatizo kubwa sana. Tena ndani
ya Gereza lenye ulinzi mkali kama la Arusha.
Yalikuwa maajabu !
Walifuatana Abdul na Daniel kuelekea Magereza.
Daniel hakutaka kumuacha Abdul hata sekunde
moja. Alijua lazima wauaji watataka kumuua.
Kwa vyovyote walikuwa wanataka kupoteza
ushahidi kwa kuuwa.
Daniel aliamini kwa kumtumia Abdul ndipo
atakapowatia mkononi kwa urahisi wauaji.
Alimtumia kama chambo. Alijua kwa vyovyote
atakuwa anawindwa auwawe !
Waliwasiri Magereza majira ya saa nne asubuhi.
Walikuta hali ya gereza ikiwa shwari na vikundi
vidogovidogo vya askari wakijadiriana. Walienda
moja kwa moja kwa mkuu wa Gereza.
Baada ya salamu walianza kuongea.
"Ilikuwaje mkuu"
"Mnamo mida ya saa tatu asubuhi alikuja mtu.
Alidai yeye ni ndugu na Raiya. Baada ya
kumkagua askari walimruhusu aingie. Hakuwa na
kitu chochote cha hatari. Baada ya kama dakika
nne aliaga anaondoka, na marehemu alirudi selo.
Lakini baadae askari walipoenda kwenye selo
yake walimkuta ameuwawa kikatili sana !."
"Marehemu alipomuona huyo mtu alionesha dalili
yoyote ya kumtambua?"
"Siwezi kujibia hilo ngoja tumwite askari
aliyekuwa zamu"
Mkuu wa Gereza alimpigia Simu huyo askari.
Baada ya kumaliza wakaendelea na maongezi
yao
"Kwanini mnahisi huyo mgeni ndiye anahusika
Katika mauaji ?"
"Marehemu hakuongea na mtu mwengine yeyote
baada ya yule mgeni kuondoka"
Baada ya maelezo hayo yule askari aliyepigiwa
simu na mkuu wa Gereza alikuwa ameshafika.
Yeye alisema hakuwa makini kuchunguza kama
mgeni na marehemu walikuwa wanajuana ama
lah. Yeye aliwakutanisha tu na kuondoka. Bila
kutafiti chochote !
Waliongazana na mkuu wa magereza pamoja na
Daniel kwenda kuuangalia mwili wa marehemu
Raiya. Ilikuwa ni picha mbaya sana ambayo
haitafutika kichwani kwa Abdul hadi leo. Picha
mbaya ilioje kumkuta binadamu unayemfahamu
kachunwa ngozi mithili ya Ng'ombe !
Abdul alikuwa anamchukia sana Raiya lakini siku
ile alitoa machozi kwa ajili ya yake. Alimuonea
huruma sana.
Alijua kapitia maumivu makali sana akiwa
anaipigania roho yake.
Mwili usio na ngozi uliwekwa hapa. Na ngozi
iliyokusanywa iliwekwa pale...!
Hali ilikuwa ya kutisha sana. Hakuna aliyeongea
kwa zile dakika tano walizokaa katika chumba.
Abdul alimwangalia Daniel usoni. Alikuwa
anatabasamu bila wasiwasi wowote..!
Walirudi ofisini kwa mkuu wa Gereza. Sasa Abdul
aligundua tabia moja ya Daniel. Huwa
anatabasamu kila mambo yanapokuwa magumu.
Alimwona
Daniel anatabasamu mbele ya maiti ya Raiya
iliyouwawa kinyama.
"Nimemuona mkuu. Ni aina ya mauaji sawa na
ya Mayasa. Sawa na ya mtoto wa waziri
aliyeuwawa kule Mwanza. Itakuwa ni kundi moja
kama siyo muuaji mmoja. Lakini awe mtu kiwe
kikundi nitahakikisha hafanyi mauaji mengine ya
raia wema !"
Alisema kwa uchungu mkubwa Daniel.
Waliondoka pale Magereza wakiacha mwili wa
marehemu Raiya ukipakiwa kwenye gari
kupelekwa hospitali.
Abdul alikuwa mwenye majonzi sana. Watu wawili
waliojitolea kumsaidia kwa hali na mali walikuwa
wamefariki kwa tofauti ya masaa machache
sana.
Ni mkosi gani huu !
Njiani alimuona Daniel Mwaseba akitabasamu.
Akajua kuna kitu cha kakiona. Tena bila shaka
cha hatari !
"Tunafuatwa"
Alimsikia akisema kwa sauti ndogo.
"Ama zetu, ama zao ! "
Waliifuata njia iliyokuwa inaelekea Moshi mjini
kutokea Arusha. Abdul roho inamdunda sana.
Daniel alikuwa hana wasiwasi hata kidogo.
Akiendelea na mluzi wake usioeleweka. Abdul
aliangalia kwenye kioo cha pembeni naye aliona.
Gari tatu nyeusi aina ya Noah zilikuwa
zinawafuata kwa kasi kubwa sana !.
Daniel alikuwa makini na usukani. Alipofika
Tengeru alikata kulia. Wakawa wanaelekea
barabara ya vumbi iliyokuwa inaelekea katika
Chuo cha Maendeleo ya jamii, Tengeru. Zilikuwa
mbio kali sana kwenye barabara ya vumbi.
Jamaa walianza kurusha risasi. Daniel alikuwa
dereva makini. Alihakikisha hawadhuriki na risasi
zile.
Na hawakudhurika !
Daniel aliingiza gari ndani ya Chuo cha Tengeru.
Hakutegemea kama ataiingiiza gari Chuoni kwa
kasi ile. Abdul alidhani atakata kulia njia
inayoelekwa chuo cha Sayansi cha Nelson
Mandela. Haikuwa hivyo lakini.
Sasa Ilikuwa patashika ndani ya Chuo cha
Tengeru.
Walikuta wanachuo wengi wapo nje. Baada ya
kufunga breki kali ! Walishuka haraka haraka na
kujichanganya na kundi la wanachuo waliokuwa
wanaelekea kunywa chai mgahawani. Waliziona
zile Noah tatu nazo zikifunga breki kali . Vumbi
lilitimka. Baadhi ya wanafunzi wa kike wakipiga
kelele za uwoga, wa kiume walikuwa
wanashangilia. Bila kujua nini kinatokea .
Walishuka jumla ya watu kumi na tano toka
katika Noah zile tatu. Wote na bunduki mkononi.
Abdul na Daniel walikuwa washaingia
Mgahawani. Lakini waliona kila kilichokuwa
kinafanyika kule nje karibu na geti ya kuingilia
Chuoni. Wanafunzi walianza kukimbia hovyo.
Jamaa moja alipiga risasi tatu hewani. Sasa
lilikuwa vurumai. Wanafunzi walikimbia hovyo
huku wakipiga kelele za taharuki. Wakajigawa
wale majamaa. Watano walielekea madarasani.
Wawili walienda maktaba. Watatu walienda
uelekeo wa ofisi za walimu, na watatu wengine
walielekea vimbwetani na wawili walikuwa
wanaenda Mgahawani walipokuwa kina Daniel !
Daniel aliinuka pale kwenye meza akaenda
kujificha nyuma ya mlango wa Mgahawa ule.
Abdul alibaki palepale mezani pamoja na wale
wanafunzi. Hali ya hofu ilitawala ndani ya
Mgahawa.Wote waliwashuhudia watu wale wawili
wakija Mgahawani na silaha zao mkononi.
Wanafunzi walikuwa na hofu kubwa, walikuwa
wanalia kimya kimya.
Wale watu waliingia Mgahawani kwa umakini
mkubwa sana. Abdul alikuwa anasubiri hatua
atakayoichukua Daniel kule nyuma ya mlango.
Alikuwa na imani nae sana. Akaingia wa kwanza.
Akaingia wa pili.Wote wakiwa na bunduki zao
mkononi, aina ya SMG.
Ghafla yule jamaa mmoja alidondoka chini. Watu
wote walistuka mule Mgahawani.
Abdul akamwangalia Daniel kule nyuma ya
mlango alikojificha.
Aliiona mdomo wa bastola yake ukiwa unafuka
moshi. Akajua bastola ya Daniel imetumika. Na
ilikuwa imefungwa kiwambo cha kuzuia sauti. Na
bila shaka risasi ilitua mgongoni kwa yule jamaa.
Yule jamaa mwengine alibabaika sana. Hakujua
nini kimempata mwenzie ?.
Mgahawa sasa ulikuwa kimya. Kila mtu alitulia
kusubiri hatma ya roho yake.Yule jambazi
mwengine aligeuka nyuma kuangalia kule
mlangoni. Alikutana nayo!. Alipigwa risasi ya
utosini. Damu chache ziliwarukia baadhi ya
wanafunzi waliokuwa karibu naye. Nae alielekea
kuzimu bila ya kuaga.
Sasa Daniel alitoka kule mlangoni. Akazivuta zile
maiti mbili na kwenda kuzificha nyuma ya
mlango. Hakuwa na wasiwasi kabisa !
Alikuwa kama anavuta magunia ya mkaa tu.
"Wanafunzi wote laleni chini haraka.
Atakayejifanya mjuaji tu shauri yake !!"
Daniel alisema huku na yeye akilala chini.
Tulitulia shwari.
Baada ya kama dakika kumi sauti za mlango
zilisikika tena. Aliingia jambazi aliyevaa sawa na
wale wenzake. Suti nzuri nyeusi na shati jeupe
ndani. Na bunduki iliyotayari kuuwa wakati
wowote itakapoamrishwa.
Huyu aliingia bila umakini wowote. Bila shaka
alitegemea Uwepo wa wenzake mule ndani.
Hivyo yeye hakuwa makini sana.
" Chugaaa" alianza kuita.
"Naam" Aliitikiwa.
Daniel aliitikia ule wito huku akinyanyuka
alipokuwa amelala. Jamaa aliashangaa sana.
Akiwa Kwenye mshangao Daniel aliachia risasi
iliyozama katika tumbo la yule jamaa.
Alikufa na mshangao wake usoni !
Daniel aliivuta ile maiti tena na kwenda kuiweka
nyuma ya mlango nayo. Ulikuwa ni mchezo hatari
sana lakini Daniel aliucheza bila uwoga wowote !
Kosa moja tu lingesababisha kifo !
Wanafunzi wengi walikuwa wameshajikojolea
pale sakafuni kwa uwoga. Abdul sasa kidogo
alianza kuwa mzoefu. Mzoefu wa kuona maiti.
Mzoefu wa kuona watu wakiuwawa.
Alianza kuupenda pia mchezo wa kifo !.
Watu wote walikuwa wameikumbatia sakafu
kasoro Daniel pekee. Alikuwa amesimama
akiangalia kule nje.
Simu moja ya wale marehemu ilikuwa inaita kule
nyuma ya mlango. Daniel alienda kuipokea.
" Chuga hapa "
"Yah, waje wawili "
Daniel alijitambulisha kuwa yeye ni Chuga. Na
kuomba watu wawili waje mgahawani.
Hawakuchelewa!
Walikuja haraka sana. Wakati Daniel akiwa bado
yupo kulekule nyuma ya mlango. Alikoenda
kupokea simu.
Wauaji waliingia ndani huku wakimwacha Daniel
kule nyuma ya mlango. Hawakufikiria kabisa
kama kuna hatari !
Abdul jicho lake lilikuwa linaangalia nyuma ya
mlango, kwa Daniel kuona atafanya nini ?.
Alimuona akijishika kiuno. Alitoka na visu viwili.
Kimoja amekishika kwa mkono wa kulia na
kingine mkono wa kushoto.
Alivirusha vyote kwa mpigo na kwa nguvu visu
vile kuelekea kwa wale majamaa. Vyote vilitua
shingoni. Kila mmoja na chake. Walienda chini
kama mizoga.
Nilimuona Daniel akitabasamu.
Majambazi watano sasa alikuwa kawamaliza
kimya kimya mule Mgahawani .
Mara kundi la majambazi wote kumi waliobaki
kule nje lilikuwa linakuja Mgahawani wakiwa
wanakimbia. Bila shaka walihisi kuna kitu cha
hatari !
Sasa ilikuwa hatari zaidi. Abdul nae alianza
kutetemeka mwili mzima kwa hofu. Alimwangalia
Daniel kule nyuma ya mlango, alimshangaa
hakuwa na hofu kabisa mwanaume yule !. Kwa
hakika Daniel hakuwa binadamu wa kawaida. Kila
hatari inavyomkaribia yeye anazidi kuwa mtulivu
na tabasamu lisiloisha usoni mwake.
Wale jamaa waliingia ndani ya Mgahawa. Pale
nyuma ya mlango sasa Daniel Alikuwa ameshika
bastola mbili mkononi. Ndani ya nusu dakika
watu wote kumi walikuwa chini.
Wote walikuwa wameuwawa na Daniel !
Wanafunzi wote walisimama na kumpa mkono wa
pongezi Daniel.
Alikuwa shujaa kwao.
Alikuwa shujaa zaidi kwa Abdul.
Walimhusudu sana Daniel.
Abdul alimhusudu zaidi Daniel !
Walitoka eneo la Chuo huku Daniel akiwapigia
simu Polisi waje kutoa maiti zile. Wao walielekea
moja Kwa moja kituo cha Polisi Arusha.
**************
Katika nyumba moja iliyopo mtaa wa Mikocheni,
Dar es salaam. Kulikuwa na kikao. Kikao
kilihusisha watu watano. Wanajeshi wanne wenye
vyeo vikubwa jeshini na raia mmoja wa kawaida.
Wanajeshi wale walikuwa wana vyeo vikubwa
sana jeshini. Walikuwa wanajadiri mpango wao
walioupa jina la Angamizo. Lengo la awali la
mpango huo ni kuwaangamiza watoto wote wa
viongozi wa Tanzania. Ili kusafisha njia kwa
Mpango wa Angamizo !
Katika kikao kile mtu mmoja tu ndiye ambaye
hakuwa mwanajeshi. Mumewe Raiya. Salehe,
yeye ndiye aliyesababisha siri za mpango huu
zivuje Kwa mtu asiyehusika. Kwa bahati mbaya
lakini siri za mpango huu wa Angamizo zilimfikia
Raiya.
Ilikuwa siku ya ijumaa. Mumewe Raiya
alichelewa kurudi nyumbani. Raiya alijisikia
mchomvu sana. Alichukua laptop ya mumewe ili
apoteze mawazo . Kipindi hicho Raiya alikuwa na
wakati ngumu sana katika maisha ya ndoa yake.
Mumewe alikuwa bize sana. Vikao visivyoisha
hadi saa tisa ya usiku. Kutokana na ubize huo
Raiya akahisi anasalitiwa kwa kutopewa haki
yake ya ndoa. Kumbe hakuwa anasalitiwa.
Mumewe alikuwa bize na Mpango haramu
ulioitwa Angamizo !
Hakuwa anampa haki yake ya ndoa mkewe.
Alibadirika kabisa. Muda mwingi alikaa peke yake
kuipanga sawa mipango yake.
Siku moja hiyo akiwa anachezea laptop ya
mumewe. Ndani ya laptop ya mumewe Raiya
aliliona faili liliandikwa Siri. Akalifungua bila
wasiwasi wowote. Ndani ya faili hilo ndimo
alikuta mambo yaliyomtisha sana.
Mpango wa Angamizo ulipangwa utekelezwe
baada ya miaka miwili. Ulikuwa Mpango hatari
ulioratibiwa na watu hatari sana !
Siku alipoliona faili lile lenye siri toka Kwenye
laptop ya mumewe kesho yake ndipo alipokutana
na Abdul. Akiwa anatoka Bagamoyo, na
kuanzisha uhusiano haramu.
Ulikuwa uhusiano haramu lakini ulioleta faida
kubwa kwa Taifa baadae.
Siku zilivyosonga mbele Salehe alihisi mabadiliko
toka kwa mkewe. Akahisi huenda anatoka nje ya
ndoa yao. Anamsaliti!
Siku zote alikuwa anamlalamikia kuhusu suala la
unyumba. Lakini Sasa alikuwa halalamiki tena.
Akaanza kumchunguza. Na zaidi Raiya akaanza
kumuogopa sana mumewe. Salehe akachunguza.
Akagundua kila walichokuwa wanafanya na
Abdul.
Mbaya zaidi Salehe aligundua pia kuwa Raiya
amegundua mpango wao wa Angamizo!
Na akajua kwa vyovyote Raiya lazima
atamsimulia mtu wake wa karibu. Ambaye ni
Abdul !
Sasa Salehe alianza kumfatilia Raiya kwa kila
hatua aliyopiga. Siku Aliyomuaga kuwa
anakwenda Arusha alimkubaria lakini
hakumwacha peke yake.
Alimfatilia!
Ndipo alipogundua kwa kina kila kitu kuhusu
uhusiano wao na kuamua kuwaangamiza wote
kwa sumu kali na hatari iitwayo Proxine !
Ndani ya kikao kile ilikuwa ni kutupiana lawama.
Wanajeshi wote wanne walikuwa wanamtupia
lawama Salehe. Kwa kuweka rehani Mpango wao
hatari !.
Salehe alijitetea sana.Lakini hakueleweka kabisa.
Wakati wanaendelea na mazungumzo yao, simu
ya Salehe iliita.
"Halo"
"Bon, Arusha"
"Nambie Bon"
'Mambo mabaya sana"
"Kuna nini tena ?"
"Tumepoteza wapiganaji kumi na tano leo"
"Unasema !!!"
"Ndio hivyo Salehe, kumi na tano wameuwawa "
"Sisi tumefanikiwa lakini !
"Hatujafanikiwa "
"Kwanini Bon..hadi sasa anapumua?"
"Ni msumbufu sana kaka"
"Inamaana ni Abdul ndiye aliyewauwa wapiganaji
wetu kumi na tano"
"Ndio Abdul, ila yuko na mwenzie. Ni watu hatari
sana"
"Nakuja na Avira na Avast kwa ndege ya jioni,
kummaliza"
"Itakuwa poa kaka"
Hali ilikuwa tete ndani ya kundi hili lenye Mpango
wa Angamizo.
*******************
ITAENDELEA!!!
 
SEHEMU YA TANO
"Nakuja na Avira na Avast kwa ndege ya jioni,
kummaliza"
"Itakuwa poa kaka"
Hali ilikuwa tete ndani ya kundi hili lenye Mpango
wa Angamizo.
*******************
Jioni ya siku ile Salehe akiongozana na Avast na
Avira walikuwa wanaelekea jijini Arusha.Kwa kazi
moja tu. Kuhakikisha Abdul anauwawa !
Avast na Avira walikuwa wauaji hatari. Wauaji
wanaojua aina zote za mauaji. Walikuwa
makomandoo toka Nigeria walioletwa kwa ajili ya
kuleta Angamizo nchini Tanzania.
Ni hawa wauaji wanaotumia sumu hatari ya
Proxine kuwaua watu kinyama. Asubuhi ya leo
walikuwa Arusha kutekeleza kifo cha Raiya akiwa
gerezani.Na sasa wanarudi tena Arusha
kukatisha maisha ya Abdul. Hawakuwahi
kushindwa wanapoamua kuuwa mtu.Walikuwa
makini sana na kazi yao.
Walitua jijini Arusha saa moja kamili usiku.
Walipanga asubuhi ndio waanze kazi yao ya
kumsaka Abdul. Hawakuwa na wasiwasi hata
kidogo. Walikuwa na uhakika hata kama askari
wote Arusha watakaa nje ya kituo cha Polisi
alikokuwemo Abdul, waliamini lazima
watamuuwa. Walikuwa na mbinu na hila zote za
kijasusi.Waliamini watamuua tu!
Walijiamini.
Waliaminiwa pia!
Daniel Mwaseba alimwacha Abdul amemfungia
katika chumba cha siri pale Polisi. Chumba
kilichojulikana na baadhi tu ya Polisi. Kilikuwa
chumba kinachotumiwa kwa nadra sana. Tena
kwa sababu maalumu.
Daniel alienda kufanya kazi. Aliyanasa maongezi
ya Kwenye simu kati ya Bon na Salehe kutoka
Kwa rafiki yake aliyekuwa anafanya kazi katika
kampuni ya simu waliyotumia Bon na Salehe
kuwasiliana. Alihisi kuna kitu kutoka kwa
mumewe Raiya. Hivyo aliongea na rafiki yake
anase na kurekodi simu zote za Salehe kwa kifaa
kiitwacho telemax. Hivyo alisikia simu zote
zilizoingia na kutoka katika simu ya Salehe.
Ikiwemo simu aliyopiga Bon kwenda kwa Salehe.
Na Daniel sasa alikuwa uwanja wa ndege wa
Arusha akiwasubiri wageni wake..!
Daniel aliiona ndege waliyopanda Salehe, Avast
na Avira ikitua pale uwanja wa ndege wa Arusha.
Aliwaona watu wale watatu wakishuka kwa
kujiamini sana. Macho ya Daniel yalikuwa makini
sana na wale majamaa mawili, Avast na Avira.
Macho yake yalimwambia hawakuwa watu wa
kawaida !
Aliwaona walivyoshuka kwenye ndege na
kupanda kwenye gari aina ya Noah nyeusi. Sawa
na zile alizofukuzana nazo asubuhi. Aliifuata
nyuma Noah ile akiwa na pikipiki yake.
Avast na Avira hawakuwa watu wa kawaida.
Huwa wanaweka tahadhari kabla ya jambo
halijatokea. Leo walivyoshuka tu kwenye gari
walihisi watafuatwa.
Walikuwa makini sana!
Wakati Daniel akiwafata akina Avast na Avira
kutoka uwanja wa ndege, kina Avast walikuwa
makini sana na magari yaliyokuwa nyuma yao.
Baadae kidogo waliitilia shaka pikipiki iliyokuwa
inawafata nyuma. Wakawa wanasubiri muda
muafaka wamtie mikononi mfuatiliaji. Wakawa
wanaendesha gari taratibu wakiipigia hesabu ile
pikipiki.
Walikuwa na sumu yao hatari ya Proxine.Tayari
kwa kuitumia muda wowote itakapobidi. Msafara
uliwafikisha kwenye mzunguko wa Azimio la
Arusha wakielekea stendi kuu Arusha. Walipofika
mbele kidogo Daniel alibadili njia.
Hakuwafata tena.
Wakati wao wakinyoosha yeye alikata kulia njia
iliyokuwa inaelekea uwanja wa mpira wa Shekhe
Amri Abeid. Alipofika usawa wa geti la uwanja
akasimama.
Mle ndani ya gari walishangaa ile pikipiki
wakiyoitilia shaka imepotea ghafla. Wakawa
wanaangaza huku na huko hawakuiona ile
pikipiki.
Walipofika mbele kidogo walisimamisha gari yao.
Daniel sasa alikuwa anatembea kwa miguu.
Aliwaona jinsi maadui zake walivyobabaika.
Akagundua walishajua kuwa wanafuatwa.Akaj
ipongeza kwa uamuzi wake wa kuchepuka.
Kina Avast walijifanya kutengeneza gari yao.
Salehe aliingia uvunguni wakati Avast Na Avira
walikuwa wanaangazaangaza huku na kule
kumtafuta mwendesha pikipiki. Dereva alikuwa
ametulia tuli kwenye usukani, alikuwa ni Bon.
Mbinu wakizozitumia kina Avast, Daniel alikuwa
ndio Mwalimu wa mbinu hizo. Alijificha kwenye
mti mmoja akisubiri wafanye kosa lolote.
Awaadhibu !
Alikaa robo saa. Kosa halikutokea. Avast na Avira
hawakuwa watu wa kufanya makosa kizembe.
Walikuwa watu wanaoijua kazi yao. Baada ya
robo saa walipanda kwenye Gari yao na
kuondoka.
Daniel aliachana nao.
Akijua ipo siku watakutana tu !
Alirudi nyumbani kwake mtaa wa maji ya chai
kwa kutumia pikipiki yake. Usiku nzima hakulala.
Alikuwa anafikiria ni kitu gani wanachotaka
kufanya watu wale.
Hakupata jibu.
Asubuhi na mapema alienda kituoni. Alimkuta
askari mmoja yupo kaunta.Alikaa na kuongea nae
pale kaunta.
Saa moja na nusu asubuhi alikuja mgeni
alijitambulisha kama ndugu wa Abdul.
Daniel kumuona tu mtu yule alimtambua. Alikuwa
mmoja ya watu watatu aliowafatilia usiku wa
jana yake usiku. Daniel alitabasamu !
"Habari Afande"
"Nzuri vipi hali yako?"
"Kwema, kuna ndugu yangu nimekuja
kumwangalia"
"Anaitwa nani ?"
"Abdul"
"Unatokea wapi ?"
"Bagamoyo"
"Sawa"
Jamaa alionesha tabasamu la matumaini kwa
mbali.
Aliyekuwa anaongea na na yule polisi ni Avira.
Komandoo toka Nigeria. Daniel akiwa pembeni
alikuwa anamwangalia huku anatabasamu.
Alimkumbuka vizuri sana!
Daniel aliomba kuongozana na yule mtu
kumpeleka kwa Abdul. Sasa Daniel aliongozana
na Avira kwenda kumwangalia Abdul.
Abdul alikuwa amefungiwa kwenye chumba cha
siri. Kilikuwa chumba chenye kila kitu ndani yake.
Alipewa na msichana mmoja aliyekuwa
anamsaidia kazi ndogo ndogo mle ndani.
Aliona mlango ukifunguliwa. Ilikuwa saa mbili
asubuhi. Walikuwa wanakuja kama marafiki wa
kawaida. Yule mtu alinyoosha mkono ili
wasalimiane na Abdul. Daniel alipiga ukelele
mkali, akimkataza Abdul kushikana mkono na
yule mtu . Abdul alirudisha mkono wake kwa
haraka wakati yule mtu akizidi kuupeleka kwake.
Daniel Mwaseba alirusha teke lililoupiga mkono
wa yule jamaa.
Ukaanza mpambano sasa !
Yule jamaa alirusha ngumi mbili zilizopanguliwa
na Daniel kwa ustadi mkubwa. Akarusha teke
moja maridadi lililompata Daniel kwenye mbavu.
Alikuwa anataka kutoa kitu mfukoni Daniel
alimzuia kwa kungfu kali ya mkononi !
Jamaa kwa ghadhabu alirusha kichwa
kilichokwepwa na Daniel. Hadi hapo Daniel
hakufanya shambulio lolote zaidi ya lile la kuzuia
mkono wa yule jamaa usigusane na wa Abdul.
Na lakuzuia asitoe kitu mfukoni yule jamaa.
Jamaa alirusha ngumi mbili zilizompata Daniel
usoni. Daniel alijishika uso. Jamaa alitaka kutoa
kitu mfukoni Daniel alimzuia kwa teke kali
lililompata barabara mkononi.
Jamaa Sasa alikuwa na hofu. Alisimama na
kurusha kofi la nguvu Daniel , Daniel alikwepa.
Jamaa alirusha Kofi lengine Daniel akakwepa
tena.
Sasa Ulikuwa mwendo wa makofi kutoka kwa
yule Jamaa na Daniel alifanikiwa kuyakwepa
yote. Sasa jamaa akaanza kulia. Alijaribu
kuingiza mkono mfukoni Daniel alimzuia kwa
kumpiga ngumi kali ya uso !
Jamaa alisimama. Ghafla akaanza kuumuka !.
Abdul macho yalimtoka pima!. Ngozi ya yule
jamaa ilikuwa inavuka !. Lilikuwa tukio la
kusikitisha sana. Tukio la kuogofya sana. Jamaa
ngozi yake ilikuwa inashuka chini taratibu. Alikufa
kifo kinachofanana na cha Mayasa !. Alikufa kifo
kinachofanana na cha Raiya ! . alikufa kifo
kinachofanaa na cha afande John.
Yule jamaa nae alivuka ngozi !
Kumbe yule jamaa alishika ile dawa inayoitwa
Proxine pale alipotaka kumsalimia Abdul kwa
mkono. Na alivyokuwa anataka kutoa kitu
mfukoni alikuwa anataka kutoa dawa nyingine ili
ajipake dawa kuzuia madhara ya ile dawa. Lakini
alichelewa.
Daniel alikuwa anamzuia kwa pigo kila alipotaka
kuitoa ile dawa hiyo.
Alijua atakufa !
Ndomana alianza kulia kabla.
Siku zote mshahara wa dhambi ni mauti !
***E Bwana we!
 
SEHEMU YA SITA
Daniel alimsogelea taratibu na kuanza kumuuliza
Abdul kwa upole.
"Kuna kitu wanahisi unacho. Wanataka kukuua ili
kisitoke nje. Ni kitu gani unahisi Abdul ?"
"Mimi sina kitu kaka Daniel. Sijui hata
wananitakia nini ?"
"Kipo kitu Abdul"
"Kitu gani sasa kaka Daniel ?"
"Mayasa alishawahi kukupa kitu chochote enzi za
uhai wake ?"
"Amewahi kunipa vitu vingi lakini siyo vya
kudumu"
"Raiya alikupa nini cha kudumu ?"
"Hamna zaidi ya hii simu "
"Hebu ilete "
Akampa.
Daniel aliiangalia ile simu kwa makini. Aliigeuza
nyuma. Aliifungua ile simu kule nyuma. Kule
inakokaa betri ilidondoka chini karatasi ndogo.
Abdul alishangaa sana. Hakuwa ameweka
karatasi yoyote kwa kuwa hakuwahi kuifungua
simu ile tangu alivyopewa na Raiya.
Daniel akaisoma kwa sauti ndogo ile karatasi.
"Kwenye laptop ya mme wangu kuna faili la
limeandikwa Siri. Linahusu mpango wa
kuangamiza watoto wa viongozi wa nchi hii na
mambo mengine mengi ya siri sana . Abdul jaribu
kulifikisha suala hili kunapohusika ili kuliokoa
Taifa hili "
Abdul alishangaa sana. Sasa alimhusudu sana
Raiya. Alimuona ni mtu mwenye akili kuliko mtu
yeyote duniani.
Raiya kumbe alikufa na siri kubwa sana. Ambayo
siri hiyo aliifikisha kwa Abdul kwa siri pia.
Abdul alimhusudu zaidi Daniel. Aligundua kitu
alichokaa nacho miaka miwili bila kutambua .
Alikiri Daniel hakuwa mtu wa karne hii.
Alikuwa na akili na uwezo wa ziada.
Daniel alitoka nje na kile kikaratasi.
Baada ya dakika kumi na tano waliingia askari
wawili kuutoa mwili wa yule jamaa.
Daniel alitoka nje kwa nia moja tu. Kumtafuta
mume wa Raiya popote alipo. Ilikuwa lazima
ampate popote atakapokuwa !
****************
Upande wa kina Avast ilikuwa ni patashika na
taharuki kubwa. Ilikuwa yapata saa saba ya
mchana sasa, Avira hajarudi. Ilikuwa ajabu. Avira
hakuwahi kufanya kazi muda mrefu namna hii.
Avira hufanya mambo kwa haraka na kwa
uhakika. Hiyo ndio sifa kuu ya Avira. Alitekeleza
kazi ya kumuua Raiya robo saa tu alivyoenda
magereza.
Leo masaa zaidi ya matano alikuwa hajarudi.
Walimsubiri.
Walimsubiri sana.
Hakurudi.
Na hajarudi mpaka leo !.
Daniel alivyotoka palepale moja kwa moja alienda
kwa dada yake Raiya. Alienda na kumuulizia
mtaa na namba ya nyumba akiyokaa Raiya huko
Dar es salaam ilipo.
Baada ya kuelekezwa Daniel aliweka 'booking' ya
ndege ya kwenda Dar es salaam kesho yake
asubuhi.
Aliipata.
Usiku ule ulikuwa mgumu sana kwa Avast na
Salehe. Wakaanza kuhisi huenda Avira
amekamatwa. Wakawa wanahofia endapo Avira
atakuwa kakamatwa anaweza kutoa siri. Siri
pekee ambayo hawakutaka itoke ilikuwa kwenye
laptop, nyumbani kwa Salehe, Dar es salaam.
Wakapanga kesho Avast aende Dar es salaam
kuichukua ile laptop. Ili siri isifike mikononi kwa
adui !
Hawakujua kama atakutana na nini huko Dar es
salaam !
Avast anaenda Dar es salaam kesho kuifata
laptop yenye siri nzito.
Daniel anaenda Dar es salam kesho kuifata
laptop hiyo hiyo yenye siri nzito !
Wasakana !
Watakutana Dar es salaam !
*****************
Daniel Mwaseba ndiye alikuwa wa kwanza kufika
nyumbani Kwa Salehe Mikocheni.
Hakupata shida sana kuingia ndani ya nyumba ya
Salehe. Hakukuwa na ulinzi wowote kwenye
nyumba ile.
Aliruka ukuta na kuingia ndani. Aliitafuta laptop
ndani ya chumba cha Daniel.
Chumba hakikuwa na vitu vingi sana.
Kulikuwa na kitanda kikubwa, meza ya
kujirembea na kabati kubwa la nguo.
Robo saa ilitosha kukipata alichokuwa
anakitafuta ndani ya nyumba ile kubwa. Aliikuta
laptop ndani ya kabati la nguo chumbani katika
chumba cha kulala cha Salehe.
Aliiweka laptop yenye siri nzito kwenye begi na
kuanza kutoka. Hakutaka kuifungua mle ndani.
Aliona ile siyo sehemu salama.
Alipita sebuleni akafungua mlango wa sebule wa
kutokea nje.
Sasa akawa anatembea katika uwanja mpana
kulielekea geti la nyumba ile. Alilikaribia kabisa
geti. Zilibaki hatua kama tano ili Daniel atoke nje
ya nyumba ile.
Ghafla! Geti lilianza kufunguka lenyewe !
Aliingia mtu mrefu, mweusi, mkakamavu.
Alikuwa ni Mnigeria.
Kwa jina alikuwa anaitwa Avast !
Pacha wa Avira aliyemuuwa kwa mateso
makubwa jana, kule Arusha.
Sasa Daniel Alikuwa anatazamana macho kwa
macho na Avast. Wote wakiwa Na bastola
mkononi !
Avast alikuwa anauangalia sana mfuko alioubeba
Daniel.
Akajua ndani ya mfuko ule kipo alichokifuata.
Laptop yenye siri nzito !
"Wanaume wanaojiamini hawapambani kwa
silaha. Tuweke silaha chini na tuoneshane
ubabe" Avast aliongea kwa sauti yake mzito na
ya kujiamini yenye lafudhi ya kinigeria. Aliongea
kwa majigambo sana.
Daniel alitii, kwa sababu nae alijiamini. Alitaka
kumuonesha Avast jinsi Wanaume wa kweli
wanavyopigana !
Wote waliweka bastola chini.
Sasa ulikuwa mpambano wa nguvu. Mshindi
alitakiwa kuondoka na laptop ile yenye siri nzito !
Ndani ya sekunde thelathini walikuwa
wanaangaliana tu . Kila mmoja akifikiria jinsi ya
kumuingilia mwenzie. Avast ndiye alitangulia
kushambulia.
Avast aliruka juu na kumuelekezea Daniel mateke
mawili ya nguvu kuelekea kifuani mwa Daniel.
Daniel hakujiandaa vizuri . Mateke yale yalitua
sawia kwenye kifua chake. Nguvu ya mateke
yale yalimfanya Daniel adondoke chini. Huku
mfuko wenye laptop nao ukidondoka chini!.
Daniel alinyanyuka kivivu. Avast alirusha teke la
kulia lililokuwa linaenda mbavuni kwa Daniel.
Alijaribu kulipangua lakini alizidiwa nguvu na
uzito wa teke lile. Lilimpata kidogo Kwenye
mbavu. Aligumia kwa maumivu !
Avast alirusha ngumi na wakati uleule Daniel
alirusha ngumi. Ngumi zile zilikutana katikati. Ila
Daniel ndiye aliyepata madhara. Ngumi ya Avast
ilikuwa na nguvu zaidi. Daniel aliumia mkono.
Sasa Daniel akajua akitumia nguvu atapigwa.
Yule jamaa alikuwa hatari sana.
Sasa aliona ulikuwa wakati wa kutumia zaidi akili
.
Avast alirusha mateke mawili kwa mpigo. Kwa
miguu miwili tofauti.
Moja lilimpata Daniel kwenye mbavu ya kushoto
na lengine mbavu za kulia. Daniel alidondoka
chini kwa nguvu. Alikuwa ameumia mbavu vibaya
sana.
Avast hakuwa mtu wa mchezo kabisa!
Avast alitoa kichupa kidogo cha dawa ya Proxine
, akapaka kwenye kiganja chake na kumsogelea
ili ampake Daniel pale chini alipokuwa amelala !
Ile anataka kumgusa Daniel alijisogeza kwa
nguvu na kwa haraka.
Avast aligusa sakafu !
Daniel alinyanyuka sasa. Akawa makini zaidi.
Akijua kosa moja tu linaondoka na maisha yake.
Alisimama imara sasa !
Avast nae alikuwa anataka kufanya haraka ili ile
sumu ya Proxine isimdhuru mwenyewe. Ilikuwa
na uwezo wa kukaa kiganjani kwa dakika kumi tu
.Baada ya hapo ingemdhuru yeye mwenyewe.
Daniel akajua hiyo ni nafasi pekee ya kumshinda
Avast. Avast alirusha teke lililompata Daniel
kwenye shingo. Teke lile lilimpeleka Daniel chini
bila kutaka. Avast akawa anamsogelea tena
ampake Proxine. Hakumgusa, alikutana na ngumi
takatifu ya pua, damu zikaanza kumtoka. Avast
hakujigusa pua. Kujigusa pua Ilikuwa
inamaanisha kujivua ngozi. Kujiua mwenyewe
kwa sumu kali ya Proxine !
Wote walikuwa wamesimama, wanaangaliana
kama majogoo. Avast alirusha kofi kwa kutumia
ule mkono wake wa kulia wenye sumu ya
Proxine . Daniel aliliona kofi lile. Alinesa kidogo
likapita jumla. Daniel alipata nafasi. Kwa kutumia
mkono wake wa kushoto alipiga ngumi ya nguvu
kwenye mbavu za Avast. Avast aligumia kwa
maumivu makali. Alitamani kujishika mbavu lakini
hakuruhusiwa na Proxine. Proxine sasa ikawa
zuio kwake mwenyewe !
Sasa Avast mbavu zilikuwa zinamuuma huku
damu zinachuruzika puani. Alikosa umakini,
hakuweka kinga usoni. Daniel aliitumia vizuri hiyo
nafasi. Alipiga ngumi mbili za haraka usoni kwa
Avast. Avast Akawa anaona nyotanyota !
Avast aliyumba kutokana na uzito wa zile ngumi,
lakini hakuanguka. Daniel alirusha teke kali
lililompata Avast kwenye goti lake. Alienda chini
taratibu.
Kama Avira, Avast alikuwa analia naye. Alikiona
kifo kwa mbali kikimsogelea. Proxine ilianza
kuleta mrejesho.
Alijaribu kutoa dawa ya kuiondoa ile sumu ya
Proxine, akaishika mkononi. Akitaka kufungua kile
kichupa ili aondoe ile sumu hatari. Alichelewa,
teke kali la Daniel liliupiga ule mkono ulioishika
ile dawa. Chupa ilidondoka sakafuni na
kuvunjika !
Avast sasa alilia kwa sauti kama mtoto mdogo.
Alilia Kwa sauti kali! Daniel alikuwa anacheka
kimoyomoyo.
Auwae kwa upanga siku zote huuwawa kwa
upanga !
Daniel aliruka "double kick". Miguu yake yote
miwili ilitua kwenye kifua cha Avast. Avast
alitapika damu.
Huku akitapika damu ngozi yake ilianza kuvuka
taratibu.
Daniel hakusubiri. Alichukua lile begi lenye laptop
na kutoka nalo nje akiwa anakimbia.
Akitafuta hotel salama na kujifungia ndani peke
yake.Tayari kuifungua ile laptop yenye siri nzito.
Moyo wake ulikuwa unamwenda kasi alipoliona
faili lililiandikwa Siri ! Akabofyabofya kidogo.
Sasa akatulia na kuanza kulisoma.
Ghafla mlango ulifunguka kwa kasi! Ulikuwa
umevunjwa kwa teke zito !. Waliingia wazee
wawili wakiwa wamevaa suti nzuri nyeupe.
"Hatujaja kuua. Tumefata laptop tu !" Mzee
mmoja alisema.
"Hamuwezi kuipata laptop mpaka mniuwe
kwanza" Daniel nae alijibu.
Wale wazee walicheka kwa sauti kwa pamoja.
Walijiamini sana !
Wazee wale walitoa bastola .Midomo miwili ya
bastola ilikuwa inamuangalia Daniel ! Hakuihofia.
Yeye alitabasamu tu.
Wale wazee wawili Walikuwa wamenuna
hasa.Tabasamu lile la Daniel waliliona kama
dhihaka toka kwa Daniel. Wakawa wanamsogelea
taratibu pale kitandani alipokaa. Daniel aliacha
kuwaangaalia. Akawa anaitazama ile laptop.
Ikifanya alichoiagiza.
Ilikubali !
Kichwani alifikiria cha kufanya.
Jamaa walimkaribia sasa. Zilibaki hatua kama
tano wamfikie kabisa.
walikuwa makini. Walikuwa wanamtambua
Daniel. Walijua kosa moja tu lingewagharimu
maisha yao yote !
"Simama juu !" Mmoja aliamrisha.
Daniel alisimama taratibu.
"Mikono juu!" Yule yule wa mwanzo alitoa amri
nyingine
Daniel alinyoosha mikono yake juu.
Yule aliyetoa amri alimsogelea huku yule
mwengine akiwa amebaki palepale.
Akimnyooshea bastola yake.
Jamaa alimpekua Daniel harakaharaka. Alipata
visu viwili na bastola moja. Hivyo viliwekwa
sehemu ya kawaida.
Silaha alizoweka sirini hakuzipata. Zilihitaji mtu
anayejua kupekua hasa.
Akaishika ile laptop. Bila kuitazama akaifunga.
Wakawa wanarudi kinyumenyume sasa.
"Naitwa kaspersky " yule aliyempekua Daniel
alisema.
"Naitwa Zwangendaba" Na yule aliyekuwa kimya
muda wote alisema.
Wakatokomea na laptop mbio !
"Tutakutana tu " Daniel alisema kimoyomoyo,
huku akitabasamu.
Akatoka nje taratibu. Kwa utulivu mkubwa.
Kama hajatizamwa na midomo miwili ya bastola
dakika chache zilizopita.
Alitembea kwa madaha. Kwa mwendo wa
kujiamini. Huku akijiuliza kwanini wale jamaa
walimwacha akipumua.
Akawacheka ujinga. Hawakujua kuwa walifanya
kosa la karne. Daniel Mwaseba alikuwa zaidi ya
wanavyomfahamu !
Akarandaranda mitaa ya Mikocheni bila uelekeo
maalumu. Aliranda makusudi. Alikuwa
anachunguza kama kuna mtu anamfatilia.
Hakumwona mtu !
Akaingia kwenye "internet cafe" moja. Akalipia
masaa mawili. Akaifungua email yake.
Aliikuta akichokitaka !
Daniel aliikuta email iliyotumwa muda mfupi
uliopita.
Aliwapongeza wamiliki wa hoteli ile aliyokuwa
mwanzo kwa kuweka "wireless internet'.
Aliikuta email aliyojitumia yeye mwenyewe muda
mfupi uliopita alivyokuwa kule hotelini. Kabla ya
wale jamaa hawajamvamia.
Kichwa cha email kilisomeka
"SIRI ".
Daniel akatabasamu tena !
Sasa alianza kuisoma.
Alianza kuisoma ile email yenye siri nzito!
**********
ITAENDELEA
 
SEHEMU YA SABA
Kichwa cha email kilisomeka
"SIRI ".
Daniel akatabasamu tena !
Sasa alianza kuisoma.
Alianza kuisoma ile email yenye siri nzito!
**********
"Hili ni Angamizo !. Macho yasiyohusika
hayapaswi kabisa kuona maandishi haya....
Ghafla Daniel alihisi anapapaswa bega. Daniel
aligeuka. Alikuwa anatazamana uso kwa uso na
Zwangendaba !.
" Sasa nimekuja kuichukua roho yako rafiki yangu
" Alimnong'oneza Kwa sauti ndogo iliyopenya
vizuri katika sikio la kushoto la Daniel.
Kwa mara ya kwanza mapigo ya moyo yalimpiga
Daniel !.
Hakutegemea kabisa watu wale kuwa mahali
pale muda ule. Hakutegemea kabisa kukamatwa
kirahisi namna ile.
Alihisi
Kutekenywa na kitu kigumu mbavuni. Akaelewa.
Alikuwa ameguswa na bastola kwenye mbavu
zake !
"Simama juu" Zwangendaba alinong'ona tena.
Daniel alisimama.
Watu wote ndani ya 'internet cafe' hawakuelewa
nini kinaendelea. Kila mtu alikuwa anatazamana
na kompyuta yake. Daniel alikuwa anatekwa
kimya kimya !
Kaspersky naye aliingia ndani ya internet cafe.
Akaisogelea ile kompyuta akiyoitumia Daniel.
Akaifuta ile email ya siri. Akarudi nje wakapanda
kwenye Noah yao nyeusi.
Safari ya kwenda kusikojulikana iliaanza !
Ndani ya gari ilikuwa kimya. Hakuna aliyeongea.
Wale majamaa wawili walikuwa wanavuta bangi
kwa fujo ndani ya gari.
Gari yote ilitapakaa moshi wa bangi.
Yalikuwa mateso kwa Daniel. Hakuwa mvutaji
hata wa sigara. Lakini hakuruhusu hata kukohoa.
Alijua kukohoa tu ataonekana dhaifu mbele ya
watu wale.
Safari isiyojulikana ilifika mwisho. Ilikuwa nje
kidogo ya Jiji la Dar es salaam. Kulikuwa na
kibanda kidogo porini. Kibanda kilichojitenga na
nyumba za watu. Walimuweka kwenye kibanda
hicho.
Daniel alishuhudia migongo ya Kerspersky na
Zwangendaba ikitokomea. Daniel walimfungia
kwenye kibanda hicho !
Kilikuwa kibanda kidogo chenye mlango mmoja
tu. Hakukuwa na madirisha wala sehemu yoyote
ya kutolea au kuingiza hewa.
Walimfungia kinjenje. Alisikia muungurumo wa
gari, jamaa walitoweka kwa kasi kwa gari yao.
Kwenda kumalizia mpango wao hatari wa
Angamizo !.
Hawakutaka kumuua Daniel. Nia yao Daniel
ashuhudie Angamizo litakaloikumba Serikali yake.
Walimuacha hai ili ateseke kwa kuona Angamizo
hilo !
**************
Abdul aliendelea kukaa kule kwenye chumba cha
siri cha Polisi Arusha. Alikuwa ameshachoka
sasa. Alikuwa anautamani sana uhuru wake.
Hakumuona Daniel ndani ya siku tatu. Alikuwa
anatamani kumuona Daniel. Maana yeye ndio
alikuwa tumaini lake pekee la kuurudisha Uhuru
wake tena. Alianza kukonda kwa mawazo."
Upande wa Polisi nao ulichanganyikiwa sana.
Kutoonekana kwa Daniel kwa siku tatu bila
mawasiliano lilikuwa jambo la kushangaza sana.
Wakahisi huenda Daniel yuko katika matatizo
makubwa. Walimtafuta kila sehemu waliyoifikiria
bila mafanikio yoyote.
******** *****
Ndani ya kibanda kile Daniel aliteseka sana.
Kulikuwa na joto kupita kiasi. Ukijumlisha na njaa
pamoja na kiu kikali alichokuwa nacho, yalikuwa
mateso makubwa sana !
Alivyoachwa tu Daniel siku ileile alitafuta njia ya
kujiokoa bila mafanikio.
Mlango ulikuwa ni geti gumu la chuma. Ukuta wa
tofali ulikuwa mrefu wa kunyooka mgumu
kuupanda. Kwa juu ziliezekwa bati za udongo.
Ndani kulikuwa na giza kiasi cha kutotambua
usiku au mchana. Hakukuwa na madirisha kabisa
katika kibanda kile.
Dakika ya kwanza tu aliyowekwa Daniel alianza
kutafuta namna ya kujiokoa.
Hadi leo siku ya tatu hakuipata. Na wala hakuwa
na dalili ya kuipata.Alidhohofika sana kwa
mawazo.
Alidhohofika sana kwa njaa.
Sasa alilala chini akiwa amekata tamaa. Alikuwa
anakisubiri kifo .
Huku akisikitika siyo tu kwa kutozitimiza harakati
alizozianzisha duniani. Hapana, alisikitika kwa
kutofanikiwa angalau kujua watu wale walikuwa
na siri gani wakiyoilinda namna ile.
Alikuwa amelala chini huku akikoroma sasa.
Hakuwa na nguvu sasa.
Ndipo likamjia tumaini. Akakumbuka kitu pekee
kinachoweza kumuokoa mahali pale.
Mungu !.
Daniel alipiga magoti kwa shida na kuanza
kumuomba Mungu.
Hakuwa mhudhuriaji kabisa wa nyumba za ibada.
Lakini leo alikwama kweli. Alimuomba Mungu
kitu kimoja tu.
Amuokoe katika mdomo wa mauti ili akaitetee
nchi yake.
Aliomba ndani ya nusu saa. Hakikutokea kitu.
Sasa aliamua kulala akiwa amekosa matumaini
kabisa. Daniel alimuona malaika mtoa roho
akimsogelea !
Alikata mawasiliano na dunia.
Alilala usingizi mbaya huku akikoroma !
*************
Ni siku ya tatu leo mke wazee Washiro hakwenda
kuchuuza samaki mtaani. Alikuwa anamhudumia
mtu aliyemuokota mumewe, Mzee Washiro.
Katika mizunguko yake ya kutafuta matunda ya
mabungo porini ili akayauze sokoni Bagamoyo
apate pesa ya nauli ili aende Arusha
kumwangalia mwanae aliyekuwa mikononi mwa
Polisi. Mzee Washiro alikutana na kitu cha ajabu.
Ni mwezi sasa tangu mwanae Abdul alipompigia
simu na kumueleza kuwa amepatwa na matatizo
Arusha.
Mwanawe alikamatwa Kwa kosa la kumuua
mtoto wa makamu wa Raisi wa Zanzibar,
Mayasa Ally.
Siku ya tatu baada ya kuacha kazi yake ya uvuvi
ambayo aliona inamuingizia pesa pole pole
aliamua kuingia msituni kutafuta matunda hayo
ya porini na kwenda kuyauza sokoni. Sasa
alikuwa na akiba ya elfu kumi na tano ndani.
Siku ya nne aliyoenda msituni kutafuta mabungo,
hakurudi na mabungo. Alirudi na mwili wa mtu
aliyepoteza fahamu !
Siku hiyo alikiona kibanda kidogo kilichokuwepo
katikati ya msitu. Mzee Washiro alikisogelea kwa
tahadhari. Alisikia mtu akikoroma ndani ya
kibanda hiko. Bila shaka alikuwa katika matatizo
makubwa. Alivunja kufuli ya kibanda kile kwa
kutumia jiwe kubwa , alimkuta mtu aliyekuwa
akiyekoroma ndani yake. Alimchukua na
kumpeleka nyumbani kwake.
Tangu siki hiyo Daniel alikuwa anahudumiwa na
mama Washiro. Mama yake mzazi na Abdul.
Hawakuwa na uwezo wa kumpeleka hospital.
Daniel alihudumiwa kwa dawa za kienyeji. Siku
ya pili leo fahamu za Daniel hazikuwa zimerejea.
Siku ya tatu alfajiri walisikia makelele katika
chumba cha mgonjwa wao. Daniel alikuwa analia
usingizini.
Mzee Washiro alienda chumbani na kumkuta
Daniel akigaragara kitandani. Alikuwa anataja
neno moja tu.
Siri !
Siri !
Siri !
Mzee Washiro hakuelewa Maana ya maneno
hayo.
Lakini alijawa na furaha moyoni kuona mgonjwa
wao amepata nafuu.
Siku hiyo ndio ilikuwa mwanzo wa Daniel kurejea
duniani. Ilihitajika lishe bora tu ili Daniel arudi
katika hali yake ya kwaida. Maana hakuwa na
jeraha lolote mwilini.
"Nashukuru sana mzee kwa msaada wako" Daniel
alisema siku moja.
"Usijari kijana"
"Umenisaidia sana. Umenitoa kwenye ufu na
kunirudisha duniani. Mungu akubariki sana!
" Amina"
"Sasa mzee naomba uniazime simu yako
niwajulishe ndugu zangu hali yangu"
Mzee Washiro alimpa simu Daniel Mwaseba.
Simu aliyopiga Daniel ilizua chereko upande wa
pili.
Daniel alipiga simu kwa Inspekta Jenerali wa
Polisi, IJP John Rondo alifurahi sana. Kwani
alihisi Daniel ameuwawa. Nusu saa baadae
helkopta ya kijeshi ilitua ndani ya mji wa
Bagamoyo na kumbeba Daniel na kumpeleka Dar
es salam kwa uangalizi maalumu.
Daniel alimuahidi Mzee Washiro ipo siku atarudi
tena kulipa fadhila kwa aliyomfanyia..!
Daniel alienda Dar es salaam kwa lengo Moja tu,
kupata lishe bora ili kurejesha siha yake. Arudi
katika mapambano haya mazito !
Kutokana na matunzo na vyakula akivyokula Dar
es salaam, baada ya wiki moja hali ya Daniel
ilirudi kama zamani.
Baada ya kupona Daniel kabisa alisimuliwa na
IJP Rondo madhara waliyoyafanya wauaji kipindi
chote alichokuwa kuzimu. Walishaua watoto wa
vigogo wengine watano. Toka katika mikoa
tofauti .Walishaua wapelelezi kumi na moja na
raia wema ishirini. Wote waliwauwa kwa mtindo
uleule. Wa kutumia sumu kali ya Proxine !
"Nchi sasa ipo katika hali ya hatari sana.
Tegemeo pekee ni wewe Daniel. Najua ulishapiga
hatua flani katika upelelezi wako. Nchi
inakutegemea sana. Raisi anakutegemea sana.
Watanzania wanakutegemea sana. Hebu nenda
kaumalizie upelelezi wako." IJP John Rondo
alikuwa anaongea kwa sauti ndogo na yenye
hisia.
"Usijari mkuu. Nakuahidi ndani ya siku tatu
nitakuwa nishawaonesha hawa mahayawani mimi
ni nani ? Hii ni ahadi mkuu"
"Nakuamini na kukutegemea sana Daniel"
Daniel sasa aliingia kazini kwa kasi mpya.
Alibeba dhima ya Taifa. Nyuma yake kulikuwa na
Watanzania zaidi ya milioni arobaini
wakimtegemea yeye. Wakimtumaini yeye pekee !
***Twende kazi, Daniel!!
ITAENDELEA...
 
SEHEMU YA NANE
Daniel sasa aliingia kazini kwa kasi mpya.
Alibeba dhima ya Taifa. Nyuma yake kulikuwa na
Watanzania zaidi ya milioni arobaini
wakimtegemea yeye. Wakimtumaini yeye pekee !
*************
Daniel alienda Arusha. Pamoja na mauaji
kusambaa Tanzania nzima. Lakini Daniel alienda
Arusha.
Aliamini ndio kitovu cha mauaji haya ya kikatili !.
Mida ya saa kumi jioni ilimkuta yupo jijini Arusha.
Kitu cha kwanza alienda moja kwa moja kituo
cha Polisi Arusha. Kuongea na Abdul. Hadi hapo
hakuwa anajua kama Mzee aliyemuokoa msituni
ndiye Baba yake Abdul.
"Habari za siku Abdul"
"Safi. Vipi ulifanikiwa kaka Daniel "
"Tunaelekea katika ushindi sasa "
"Daah nashukuru sana kaka Daniel"
"Hivi ulishawahi kumuona mumewe Raiya kwa
sura ?"
"Hapana"
"Unajua chochote kuhusu yeye ?'
"Mmmmmm yah nimekumbuka, Mayasa alisema
ni mtoto wa baba yake mdogo"
"Safi sana. Ndani ya siku tatu tutajua mbivu na
mbichi. Umenipa pa kwenda kumalizia sakata
hili"
"Mimi nakuombea kila la heri"
Waliagana.
Daniel alitoka katika chumba kile cha siri akiwa
na pakuanzia. Aliamua kwenda Zanzibar.
Nyumbani kwa wazazi wa Salehe aliamini
angeyajua mengi. Alijipongeza kwa kitendo chake
cha kwenda kuongea na Abdul kwanza.
*****************
Ndege ya alhamisi asubuhi ilimchukua Daniel.
Kumpeleka Zanzibar.
Ndege ilimfikisha hadi kiwanja cha ndege cha
Zanzibar. Sasa alijiona anaukaribia ukweli wa
sakata hili.
Alianza kuulizia nyumba ya kina Salehe. Daniel
alishangazwa sana na umaarufu wa Salehe. Cha
ajabu yeye hakuwahi kumsikia kabisa kabla ya
sakata hili.
"Unaelekea wapi ?"
"Nyumbani kwa Mzee Makame"
"Makame yupi ?"
"Yule ndugu na makamu wa Raisi"
"Ahaa Makame Abdullah, ni elfu tano nauli"
'Haina shida"
Dakika ishirini baadae Daniel aliteremshwa
barazani mwa Nyumba ya mzee Makame. Roho
ilikuwa inamdunda. Nywele zilikuwa
zinamsisimka. Hakujua kwanini ?
Alipapasa bastola yake ilikuwa sehemu sahihi.
Alipiga hatua kuelekea kwenye nyumba ile
iliyomtia shaka sana Daniel .
Alipiga hodi mara tatu. Alisikia mlio wa miguu
mtu akija kufungua mlango. Mlango ulifunguliwa
na kijana mmoja aliyekuwa na asili ya kiarabu.
Walitazamana na Daniel !
Macho ya yule kijana yalikuwa ya kawaida kwa
mtu wa kawaida. Lakini kwa Daniel hayakuwa
macho ya kawaida. Macho ya kijana yule
yalikuwa na woga na wasiwasi ndani yake .
"Anaogopa nini ?" Daniel alijiuliza mwenyewe.
"Habari kijana ?"
"Nzuri"
"Samahani namhitaji Mzee Makame"
"Una miadi nae ?"
"Hapana"
"Nimwambie mgeni anaitwa nani ?"
"Njemba "Daniel alidanganya.
"Sawa"
Kijana hakuruhusu Daniel aingie ndani. Alimuacha
palepale mlangoni. Kwa utamaduni wa watu wa
Zanzibar haikuwa kawaida.
"Kuna kitu" Daniel alijisemea tena.
Baada ya dakika tatu mlango ulifunguliwa tena
na kijana yuleyule.
"Karibu ndani"
"Ahsante"
Walifika sebuleni. Daniel alichagua sofa
moja.Akakaa.
"Naenda kumwita mzee"
"Sawa"
Yule kijana alipotoka. Daniel alizungusha macho
yake mle sebuleni kwa harakaharaka. Hakuona la
ajabu.
Akatulia sofani.
Alitokea Mzee mwenye umri kati ya miaka sitini
na sitini na tano. Daniel akajua huyo ndiye mzee
Makame.
Walisalimiana kwa kupeana mikono. Mzee
makame alikaa kwenye sofa likilotazamana na
Daniel.
"Eeh nakusikiliza kijana"
"Naona mnakaribia kufanikiwa" Daniel alisema
akiwa anamtazama Mzee Makame.
"Sijakuelewa kijana"
"Nazungumzia mpango wenu wa Angamizo"
"Mzee alistuka kidogo.
" hahaha nilijua tu, wewe ni Daniel Mwaseba.
Umekifata kifo chako !"
"Sijakuelewa Mzee"
"Utanielewa baada ya dakika chache "
Kumbe Mzee makame Alimuona Daniel tangu
anashuka kwenye teksi. Alikuwa anamtambua
Daniel. Alichokifanya ni kukimbilia chumbani
wakati yule kijana akimchelewesha Daniel kwa
makusudi pale mlangoni.
Alipaka sumu hatari ya Proxine mkononi Halafu
alivyoingia walisalimiana na Daniel kwa mikono.
Alikuwa anategemea Daniel atakufa muda
wowote !
Daniel atavuka ngozi !
"Nisalimie kuzimu Daniel" Mzee Makame alisema
kwa kebehi.
Daniel alikaa kimya!
Mzee Makame alikuwa anaongea huku anatoa
dawa ya kutoa madhara ya Proxine mfukoni
kwake. Ili ajipake kujinusuru yeye.
Daniel alisimama..!
Daniel Mwaseba alikuwa ana akili kuliko Mzee
Makame alivyokuwa anafikiria.
Daniel alisimama, akaanza kumfuata Mzee
Makame pale aliposimama.
Mzee Makame alikuwa anajishughulisha kutoa ile
dawa mfukoni kwa haraka. Alibabaika sana.
Hakufanikiwa!
Daniel alimkaribia zaidi, alimpiga karate kali
katika mkono aliokuwa anatolea dawa. Mzee
Makame na uzee wake karate ilimuingia hasa
mkononi.
Mzee Makame alibaki na mshangao usoni huku
akiugulia maumivu. Alikuwa anashangaa kwanini
Daniel yuko imara. Pamoja na kumpaka sumu ile
Kali ya Proxine !.
Yeye alianza kuisikia ile sumu kwa mbali. Ilikuwa
inaanza kumdhuru taratibu. Wakati Daniel
Alikuwa ngangari !
Yule kijana aliyemfungulia mlango Daniel alikuja
ukumbini. Alishangaa kumkuta Mzee Makame
yupo katika hali mbaya kidogo. Huku Daniel akiwa
imara. Alitia mkono mfukoni kutaka kutoa
akichotaka kutoa.
Hakuwahi!
Naye alipigwa kareti moja ya kiume ya shingo.
Hakuweza kustahamili uzito wa karate ile kwa
sehemu aliyopigwa.
Alienda kuzimu taratibu !
Mzee Makame alianza kuvuka ngozi sasa. Kwa
mara nyingine Daniel alijipongeza kwa hatua yake
ya kwenda kumhoji Abdul kwanza Arusha. Na
kwenda Zanzibar kufatilia sakata lile.
Daniel sasa alivua ngozi laini aliyovaa
mkononi.Ilikuwa ngozi ya plastiki inayofanana na
ngozi ya kiganja chake. Alikuwa amevaa kama
'gloves'
Akavua mikono yote miwili. Akajisachi mfukoni
akatoa ngozi zingine mpya. Akazivaa .
Akaanza kuipekua nyumba ile ya Mzee Makame.
Alipekua nyumba mzima hakupata kitu. Alikata
tamaa.
Mwishoni aliamua kupanda juu ya dari .
Akayakuta maboksi kumi makubwa. Ya rangi ya
nyekundu.
Daniel akatabasamu !
Akiwa kule kule darini alijaribu kulifungua boksi
moja.
Alikuta vichupa vidogovidogo vingi. Vimeandikwa
Proxine !.
"Hawa jamaa wana nia gani lakini ?"
Alijiuliza mwenyewe. Hakukuwa na wa kumjibu.
Akayashusha yale maboksi yote kumi.
Akawa anafikiri ayafanye nini ?
Alikumbuka.
Alipiga simu kwa IGP Rondo.
Ndani ya dakika kumi gari ya Polisi waliokuwa
doria waliwasiri. Waliyabeba maboksi yote ya
sumu. Pamoja na miili ya marehemu.
Wakati Polisi wanaenda kituoni. Daniel alipanda
boti kuelekea Dar es salaam. Bado aliendelea na
kazi.
Ndani ya masaa matatu alikuwa feri.
Alishuka kama abiria wengine. Hakuna aliyekuwa
anajua kama Daniel ametoka kufanya jambo
kubwa sana Kisiwani Zanzibar muda mfupi
uliopita. Vichupa vile visingekamatwa
vingesababisha watanzamia wengi sana
wauwawe. Daniel alijiona shujaa. Na kweli
alikuwa shujaa !
Safari yake ilimpeleka moja kwa moja kwenye
nyumba ya Salehe, Mikocheni. Alipokaribia aliona
jinsi walivyoimarisha ulinzi. Kulikuwa na walinzi
wanne getini .
Aliamua kuingia nyumba ile mchana uleule.
Hakuwa na muda wa kupoteza.
Alidhamiria kulimaliza suala lile ndani ya siku
tatu tu.
Alienda pale getini kulikuwa na walinzi watatu.
"Tukusaidie nini Bosi ?"
"Namuulizia kaka Salehe"
"Hayupo"
"Kaenda wapi ?"
"Kaenda Zanzibar,kuna matatizo"
"Ameenda kwa usafiri gani ?"
"Ndege"
"Sawa"
Walinzi wale walionesha hawakuwa wanajua
ubaya wa Bosi wao. Wao walikuwa wameletwa
tu na kampuni moja ya ulinzi kulinda usalama wa
nyumba ile. Walikuwa na nidhamu ya kazi nzuri.
Daniel alimpigia simu IGP Rondo. Atume askari
wa kutosha uwanja wa ndege wa Zanzibar.
Kuhakikisha Salehe anakamatwa hapohapo
uwanjani.
****************
Muda huo Salehe alikuwa ndani ya ndege ndogo
ya Coastal. Alikuwa amechanganyikiwa sana.
Hakuamini alipoambiwa kuwa baba yake mzazi
amefariki. Baba yake Alikuwa anajua mbinu za
kijasusi. Ingawa siyo kwa kiwango kikubwa sana.
Lakini hakuwa mtu wa kufa kama kondoo.
Alishangaa sana .
Na aliuwawa vipi wakati Proxine zilikuwa ndani.
Kwanini hakuzitumia alipoona hatari inamkaribia?
Mbaya zaidi kikichomuumiza kichwa Salehe ni
maboksi kumi ya Proxine yaliyopo darini.
Kati ya maboksi kumi na tano yaliyoingia nchini
kumi waliyahifadhi kwa Mzee Makame.
Alikuwa anajiuliza ni nani aliyeikaribia ngome
yake kiasi kile. Hakumfikiria kabisa Daniel
Mwaseba. Alijua Daniel kashajifia zamani huko
Bagamoyo porini.
Ndege aliyopanda Salehe ilikuwa inatua uwanja
wa ndege wa Zanzibar .
Askari wakiwa makini.
Salehe akiwa hana hili wala lile. Hakujua kama
kuna kundi la askari lilikuwa linamsubiri kumlaki
nje ya uwanja.
Wakati huohuo Daniel alikuwa ndani ya boti
anarudi Zanzibar tena. Alikuwa anataka kumhoji
mwenyewe Salehe atakapokamatwa ili aujue
kiundani mpango wao wa Angamizo..!
Wakati Ilipokuwa inatua ndege Salehe alihisi kitu.
Alihisi kuna hali ya hatari uwanjani. Ni machale
tu yalimcheza. Akawa tayari kwa lolote.
Tayari kuua!
Tayari kufa !
***Doh! Itakuwaje sasa?
ITAENDELEA...
 
SEHEMU YA TISA
Wakati Ilipokuwa inatua ndege Salehe alihisi kitu.
Alihisi kuna hali ya hatari uwanjani. Ni machale
tu yalimcheza. Akawa tayari kwa lolote.
Tayari kuua!
Tayari kufa !
Kaspersky na Zwangendaba walikuwa ndani ya
Noah ndogo nyeusi iliyopaki pale uwanja wa
ndege. Walikuwa wanamsubiri Bosi wao Salehe
wampeleke nyumbani kwake. Wao walitangulia
kufika. Wakiwa na laptop yenye siri nzito !
Hawakuzielewa elewa kabisa sura walizoziona
uwanja wa ndege. Waliona sura nyingi za
kiaskari wakiwa kama wanamsubiri mtu.
Hawakuwa askari wa kawaida wa uwanja wa
ndege.
Ingawa walivaa nguo za kiraia ila haikuwapa
shida kwa kina Kerspesky.
Umakini wao uliongezeka huku wakifikira njia ya
kumtoa Salehe kwenye mtego ule mujarabu..!
Wakati ndege inatua kaspersky alimpigia simu
Salehe.
"Hallo Kerspersky, ndio natua hapa"
"Kuwa makini Bosi. Hali si shwari nje huku"
"Usijari, nishastuka, nitawaachia manyoya tu !"
"Nakuamini"
Simu ilikatwa.
Ndege ilitua salama katika uwanja wa ndege wa
Arusha.
Huku Salehe akisubiriwa kwa hamu kupokelewa
na askari Polisi makini zaidi ya thelathini wenye
silaha za kila aina, ashuke wamtie mbaroni.!
*************
Ndege ilitua salama katika uwanja wa ndege wa
Zanzibar. Askari wote walikuwa makini na watu
wote waliokuwa wanashuka ndani ya ndege ile.
Ilikuwa ni ndege ndogo ya watu 6 ya kampuni ya
Auric.
Alishuka abiria wa kwanza alikuwa mama wa
makamo akiwa kabeba mtoto mdogo mgongoni.
Alishuka abiria wa pili, alikuwa kijana wa
makamo wa kizungu, aliyekuwa kabeba begi
kubwa mgongoni.
Alishuka abiria watatu, alikuwa kijana wa miaka
18 wa kike, mwenye asili ya kiasia.
Abiria wa nne alikuwa ni mama wa makamo
mjamzito.
Abiria watano nae alishuka, alikuwa ni mzee wa
kiarabu mwenye ndevu nyingi. Abiria wa mwisho
katika ndege ile ndogo alishuka, yeye alikuwa
kijana wa kichina.
Kila abiria alipokuwa anashuka askari thelathini
walikuwa makini kuangalia picha ya Salehe
iliyokuwa mkononi kwa kila mmoja.
Lakini taswira ya mtu waliyekuwa na picha yake
hakushuka !
Salehe alipotea mithili ya upepo !
Askari waliduwaa na picha zao mikononi. Askari
watano waliingia ndani ya ndege kuona kama
labda Salehe alijificha mle ndani. Walitafuta kila
kona ndani ya ndege ile.
Salehe hawakumwona !
Wakati huo Salehe alikuwa mbali na uwanja wa
ndege. Alikuwa ndani ya Noah nyeusi akikaribia
nyumbani kwa baba yake, Mzee makame.
Nani angejua kama yule mama mjamzito
waliyemuona akishuka kwenye ile ndege alikuwa
ndiye Salehe ?
Alitumia dakika tatu tu kujibadiri pale pale
kwenye siti kwa usiri mkubwa. Alivaa sura ya
bandia, alivaa mwili wa bandia, begi lake
liligeuka mimba ya bandia.
Dar es salaam alipanda ndege Salehe, Zanzibar
alishuka kwenye ndege mama mjamzito !
Ndani ya gari alijibadirisha tena. Sasa alikuwa na
taswira halisi ya Salehe .
Walifika nyumbani kwa baba yake Salehe baada
ya muda mfupi. Walishuka ndani ya gari na
kutembea kwa mwendo wa tahadhari. Walijua
chochote kinaweza kutokea ndani ya nyumba ile.
Walikuta nyumba tupu.Tupu kabisa. Hakuna mtu.
Hakuna dalili ya uhai.
Waliingia ndani.
Salehe alipanda darini. Alichoka kabisa !
Hakukuwa na maboksi ya sumu ya Proxine hata
moja. Ilikuwa hasara kubwa sana. Kulikuwa na
boksi kumi za Proxine. Na kila boksi moja ilikuwa
vinakaa vyupa elfu moja vya sumu ile hatari.
Kuibiwa kwa boksi kumi, ilimaanisha vyupa elfu
kumi vya sumu ya Proxine viliibiwa.
Hasara ilioje ?.
"Sumu zote zimechukuliwa.
Sasa wametangaza vita !
Hivi ni vita vikuu vya tatu vya Dunia ! Nitauwa
kila kiumbe anayepumua katika nchi hii.
Nitaua,
nitaua,
nitaua !
Baada ya kufanya mauaji ya kutisha na
kutosheka, ndipo nitafanya kitu kitakachowaacha
watanzania na Serikali yao midomo wazi ! "
Salehe alisema kwa jazba kule darini. Hakuweza
kuyazuia machozi, Salehe alilia !
Salehe, Zwangendaba na Kerspersky walitoka
ndani ya nyumba ile vichwa waliinamisha chini.
Ama hakika waliwezwa sana.
Walitokomea kusikojulikana.
Sasa waliapa kuuwa, na walienda kuuwa kweli !
****************
Daniel alikuwa anashuka kutoka katika ndege,
uwanja wa ndege wa Zanzibar. Alishapewa
taarifa za Polisi kuachwa kwenye mataa kwa
Polisi katika uwanja wa ndege wa Zanzibar.
Hakuwalaumu Polisi, alizijua mbinu za watu
wale. Aliujua umahiri wa watu wale.
Alipofika Zanzibar, moja kwa moja alielekea
nyumbani kwa Mzee Makame. Kwa tahadhari
kubwa sana aliingia ndani ya nyumba ya Mzee
Makame.
Alikuwa amechelewa, wakina Salehe walikuwa
wameshaondoka.
Daniel alipanda darini na kutoa kidudu kidogo
mfano wa kigoroli.
Kilikuwa kinasa sauti !
Alichokiweka kabla hajaondoka kwenda Dar es
Salaam. Alikitega makusudi nia ni kusikia mstuko
atakaoupata Salehe baada ya kugundua mabox
ya Proxine yametoweka.
Alishuka chini na kuweka kile kigoroli kwenye
simu yake. Daniel hakusikia tu mshtuko. Alisikia
pia maneno ya jazba na hasira kutoka kwa
Salehe.
"Sumu zote zimechukuliwa. Sasa wametangaza
vita. Hivi ni vita vikuu vya tatu vya Dunia.
Nitauwa kila kiumbe anayepumua katika nchi hii.
Nitaua,
nitaua,
nitaua !
Baada ya kufanya mauaji ya kutisha, na
kutosheka, ndipo nitafanya Kitu kitakachowaacha
watanzania watakaobaki midomo wazi ! "
Daniel alitabasamu.
Daniel alitoka nyumbani kwa Mzee Makame
akiwa hana uelekeo maalumu. Hakujua Salehe
atakuwa ameelekea wapi ?
Alikuwa anatembea tu mitaani. Labda atakutana
na chochote kitakachomsaidia katika kutatua
mkasa huu mzito !
Hakukutana na chochote.
Aliamua kutafuta hoteli iliyotulia na kupumzisha
mwili na akili .
Alilala.
*************
Ndani ya hoteli ya Green view iliyopo mtaa wa
Uzunguni jijini Mbeya, kulikuwa na kikao cha Siri.
Kikao kilichokutanisha watu watano muhimu sana
katika mpango huu.
Angamizo !
Walikuwa ni walewale wanajeshi wanne na
Salehe Makame. Walikuwa wanajadiri maendeleo
ya mpango wao kabla ya kuuhitimisha. Zilikuwa
zimebaki siku mbili kuhitimisha mpango huo.
Mpango wenye nia mbaya kwa Serikali ya
Tanzania.
Mpango wenye Kuleta hofu na kuteteresha hali
ya usalama kwa wananchi na viongozi wa nchi
ya Tanzania.
Mpango uliopangwa kwa kuanza kufanya mauaji
ya kikatili kwa watoto wa vigogo, ili kupunguza
umakini kwa Polisi. Nia ya kuuwa watoto wa
vigogo ni kuwapoteza lengo Polisi. Walitaka Polisi
nchi nzima wawe bize kutafuta muuaji wa watoto
wa vigogo vyuoni. Ili wao wautumie kwa urahisi
mpaka wa Tunduma, kutoka Tanzania kwenda
Zambia Kutorosha silaha..!
***************
Mpango wa Angamizo ulikuwa hivi.
Mkoani Iringa, Katika kijiji cha Makete kulikuwa
na ghala kubwa sana la silaha. Lilikuwa ni ghala
la silaha kubwa katika nchi ya Tanzania.
Mpango wa watu hawa ulikuwa ni kuiba na
kutorosha nje ya nchi silaha zote katika ghala
lile. Walikuwa wameongea biashara na kikundi
kimoja cha kigaidi cha huko Somalia. Walipanga
kupita kwa siri katika mpaka wa Tunduma. Kwa
kutumia rushwa Ili kupita Tunduma kuelekea
Zambia. Halafu kutokea Zambia silaha hizo
zisafirishwe kwa njia ya ndege kwenda Somalia.
Hawakutaka kuzipandisha ndege silaha hizo
kutokea Tanzania. Hali ya usalama Tanzania
ilikuwa nzuri zaidi ya Zambia.
Ulikuwa ni mpango uliopangwa na vigogo watatu
wakubwa wa Serikali. Huku ukiratibiwa na
watendaji wakuu watano. Waliokutana leo ndani
ya Green view hotel.
"Salehe tuna jumla ya malori saba. Lazima
tuzijaze silaha na tuzipitishe mpakani leo usiku.
Najua sahivi macho ya vyombo vya ulinzi vyote
vipo Arusha, Mwanza na Zanzibar. Sisi usiku wa
leo tutaenda kuiba silaha hizo katika ghala kuu la
Serikali Makete, kesho usiku lazima tuzisafirishe.
Lazima tuwe makini sana katika hatua hii. Tena
ili kulichanganya zaidi jeshi la Polisi inabidi leo
mtu auwawe Dar es salaam. Tena awe mtoto wa
kigogo, maana akifa mtu wa kawaida Serikali
inadharau." Meja Badi Bwino aliyekuwa
mwenyekiti wa kikao kile alitoa maelekezo.
"Sawa nimekuelewa. Naamini Mpango wetu
utafanikiwa.
Lakini wewe umeshauri tuuwe mtu mmoja Dar es
salaam. Lakini ili tuwachanganye vizuri inabidi
watu watatu wafe leo !. Dar es salaam, Mara na
Kigoma. Hapo tutawaweza. Kwa kuwa ghala kuu
lipo Iringa mauaji yakitokea Mara, Dar es salaam
na Kigoma, askari wengi watapelekwa sehemu
hizo. Kwa hiyo itatupa uraisi kuziiba silaha hizo
".
Salehe nae alitoa wazo lake.
"Sawa Salehe. Wazo zuri sana" Meja Badi Bwino
alikubaliana na mpango wa Salehe.
Kikao kilifungwa.
**************
Salehe alienda uwanja wa ndege wa Songwe
uliopo nje kidogo ya mji wa Mbeya, kutafuta tiketi
tatu za kwenda mikoa tofauti. Alibahatika kupata
tiketi mbili za kwenda Kigoma na Mara. Ndege
ya kwenda Dar es salaam Ilikuwa imejaa.
Alifikiria yule mtu wa Dar es salaam. Aliongea na
mtu wake wa Zanzibar. Ndege ilipatikana. Salehe
akakata tiketi ya kutoka Mbeya hadi Zanzibar, ili
atakayeenda Dar es salaam ataenda kwanza
Zanzibar, halafu atatafuta ndege ya kwenda Dar
es salaam .
Daniel alikuwa amelala vya kutosha pale hotelini.
Aliamka, alioga na kuagiza chakula palepale
hotelini. Baada ya kula alipiga simu kwa rafiki
yake mmoja wa wafanyakazi katika uwanja wa
ndege wa Zanzibar, akajibiwa kuna ndege ya saa
kumi inayoenda Dar es salaam. Akamuomba
amkatie tiketi moja.
Daniel aliamua kurejea Dar es salaam tena !
***Go, Daniel, Go!
ITAENDELEA
 
Back
Top Bottom