Risala fupi ya marehemu SSM

Zogwale

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
15,287
10,842
Wakuu nawaletea Risala fupi ya marehemu SSM kama ambavyo nilipita katika kikao kimoja cha Wazee na kusikia haya:

1. Marehemu alizaliwa 5.2.1977

2. Enzi za uhai wake marehemu alijishughulika na yafuatayo:
(i) Kuua mazao ya biashara kama pamba,tumbaku, kahawa, katani, korosho, n.k
(ii) Kuua viwanda kama Mwatex, Mutex, Kiltex, Ufi, Bora, Tanelec, Mgololo, Tanganyika Packers, Viwanda vya kusindika maziwa n,k
(iii) Kuwaleta wagenii wanaoitwa wawekezaji na kuwapa mali za Watanzania kupitia makampuni uchwara ambayo wamiliki wake ni pamoja na mafisadi wanaoifadhili

3. Marehemu ameacha wachina kariakoo, waarabu Loliondo, Makaburu Mererani, wazungu wa kila aina kwenye migodi yote ya madini, gasi na utafiti wa mafuta.

4. Marehemu ameacha mke mmoja anaitwa FUC, na watoto wawili PDU na LTP

5. Shetani amuweke pabaya motoni milele. Amina.

Wadau huu ni wasifu mfupi tu, naamini wewe unayo machache ya kuongeza kuhusu huu wasifu. Funguka. Karibu.
 
Heshima kwenu wana JF;
Zongwale umesahau kitu kimoja mkuu,marehemu ameacha watoto wawili Rushwa na Ufisadi.
 
mashimo shinyanga,mwanza,musoma na kwingineko

Mkuu nyabhingi, si huko ulikotaja tu ambako ni mbali, kama uko Dar mbona tena hakufai!!! Barabara za kuchepukia nyingi ni mahandaki!!! Na zile zilizokuwa na lami ikaisha manispaa kama za temeke wanaweka kifusi juu yake na mvu ikinyesha basi kazi msimu mwingine inaanza upya!! Wapi na wapi unaweka kifusi juu ya lami? Yet, tuna uongozi imara! Kodi wa walala hoi!!
 
Heshima kwenu wana JF;
Zongwale umesahau kitu kimoja mkuu,marehemu ameacha watoto wawili Rushwa na Ufisadi.

Mkuu maste peace, sijui nimesahauje tena hizi chawa mbili a.k.a viroboto kunguni!! Wametunyonya na tunabakia mifupa sasa!! Na zilaaniwe.
 
No.3 Wasomali Kariakoo na kwenye mbuga zetu,
pia ameacha wanyama wetu wakiwa nchi za kiarabu,
Watoto wetu wanakwenda sekondari hawajui kusoma na kuandika,
Ameacha shule za kata zisizo na waalim.
 
marehemu ameacha magofu kila kata yanayotumika kama viwanda vya kutengeneza matoto majinga
 
sifa kuu ya marehemu alidhani ataishi milele
lakini shetani amempenda zaidi.
apunzike kwa shetani...amuna.
 
jamani hajafa bado ila kalazwa ICU halafu msimwogope kihivyo kwa kufichaficha jina lake halic ambalo ni CCM/ CHAMA CHA MADALALI
 
Back
Top Bottom