Viwanda hivi alivyovijenga hayati Mwalimu Nyerere viwe chachu ya kutatua suala la ajira

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,399
Ikiwa nchi yetu ya Tanzania itarudi katika hali yake ilikuwa nayo miaka ya mwanzoni mwa 80 na mwishoni mwa miaka ya 90, suala la tatizo la ajira linaweza kuwa historia.

Hayati Mwalimu alipenda kujenga nchi ambayo ina mfumo uchumi wa kisasa ambao unaineemesha jamii ya watanzania ambayo itakuwa inafaidi matunda ya jitihada zake kwa kuweka haki, usawa na rasilimali kwa wote.

Ifuatayo ni orodha ya baadhi ya viwanda ambavyo hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipenda aivushe nchi yetu iwe na uchumi wa kujitegemea bila kuwa ombaomba.

1. TANGANYIKA PACKERS - usindikaji, upakiaji na usambazaji wa nyama ya ng'ombe. Kiwanda hiki kilikuwa kawe na kingine kule mkoni Shinganya.

2. URAFIKI, MWATEX, KILTEX,MUTEX, POLYTEX- Nguo, vitenge

3. MOROGORO CANVAS - MAGUNIA, MATURUBAI

4. MOROGORO SHOES- VIATU

5. MOROGORO TANNERIES- NGOZI

6. MWANZA TANNERIES- NGOZI

7. BORA SHOES- UTENGENEZAJI WA VIATU

8. KIBO MATCH FACTORY- Viberiti

9. NATIONAL, MATSUSHITA, PHILLIPS- Utengenezaji wa batteries, radio na radio cassete.

10. PAMBA ENGINEERING- Uchongaji wa vipuri vya mashine za uchambuaji pamba.

11. SIDO - Shirika la kuhudumia viwanda vidogo

12. Kiwanda cha kubangua Korosho Mtwara

13. Viwanda vya kusindika na kubangua , Kahawa, Alizeti, Pareto, Karanga na Miwa.

14. Kiwanda cha vipuri vya mashine cha Mang'ula

15. Kiwanda cha vipuri za mashine cha Kilimanjaro

16. Kiwanda cha malori (kuunda mabasi na malori) cha Scania

17. Kiwanda cha magari cha Nyumbu cha jeshi Kibaha

18. TANALEC- kiwanda cha kutengeneza vifaa mbalimbali vya umeme.

19. Kiwanda cha karatasi cha Mgororo Mufindi mkoani Iringa.

20. Kiwanda cha kusindika na kusambaza maziwa cha UTEGI mkoani Mara.

21. Kiwanda cha usindikaji wa nafaka cha National Milling Corporation cha Dar-es-Salaam

22. Tanga Steel Rolling Mill- vyuma, saruji na mabati.

23. Viwanda vya saruji vya Tembo Cement, Twiga Cement, Simba Cement pamoja na vile vya ALAF na GALCO.

24. Kiwanda cha zana za kilimo - UFI

25. Kiwanda cha madawa ya binadamu cha KPC - Keko Pharmaceutical Company.

26. Viwanda vya Bia vya Dar, Ndovu na Pilsner Arusha

27. Kiwanda cha Mvinyo Dodoma

27. Kiwanda cha matairi cha General Tyre kilichopo Arusha

28. Kiwanda cha katani cha Amboni mkoani Tanga.

29. TIPER - kiwanda cha kusafisha mafuta machafu, kusambaza mafuta ya dizeli, petrol na mafuta ya taa.

Hii orodha ni baadhi tu ya viwanda vingi ambavyo serikali ya hayati mwalimu ilijitahidi kuvianzisha chini ya ushirikiano na nchi marafiki kama China, Russia (iliyokuwa USSR) na India.

Licha ya jitihada za mwalimu, bado wafanyabiashara binafsi walianzisha viwanda kama vile Amboni Plastic Ltd, Tungi Ltd, Waraguru Partnership Ltd, Sumaiya Group of Companies, kiwanda cha mbolea Tanga, na vingine vingi tu visivyo idadi.

Pia licha ya utitiri huu wa viwanda hivi, hayati Mwalimu alijenga miundombinu kama barabara, njia za reli ya kati na ile ya TAZARA, bandari za Dar-es-Salaam, Tanga, Mtwara na ile ya Zanzibar.

Bila kusahau viwanja vya ndege vya JNIA, Kilimanjaro na Mwanza ni miongoni mwa viwanja vikubwa nchini mwetu.

Kuna kilio cha ajira kila kona ya nchi na soko la ndani la ajira limekuwa dogo mno lisilo na matumaini ya kusimama kwa muda mfupi.

Lakini mwalimu alipong'atuka mwaka 1985 hakuweza kuwa amemteua mtu sahihi wa kuendeleza yale aliyoyaanzisha na hali hii hatuwezi kuona ikitokea katika nchi kama ya Russia maana raisi Putin hawezi tu kukurupuka na kumteua mtu awe raisi wa nchi hiyo halafu aje kuharibu utararibu mzuri ulowekwa na serikali ya sasa ya Russia.

Sasa tumepata serikali ya awamu ya tano ambayo inajikita kwenye kutumikia wananchi na kuhakikisha ndoto za mwalimu zinatimia, yaani kuwa na Tanzania yenye viwanda.

Isiwe ni jitihada za serikali pekee katika kuboresha njia mbalimbali za kuwawezesha wananchi kujianzishia biashara na kujiajiri, bali iwe pia ni jukumu la wafanyabiashara, mabenki na wenye viwanda na hata wale wenye mawazo ya namna ya kuanzisha na kubuni bisahara na njia za ajira.

Waziri wa viwanda na biashara mheshimiwa Charles Mwijage aendeleze jitihada zake ambazo zinaonekana katika kuitafutia Tanzania kujikwamua kwenye hili eneo la ajira na viwanda, kwani bila viwanda hakuna ajira, na bila mazingira mazuri kwa wenye kutaka kuwekeza basi hakuna viwanda.

Serikali pia inayo kila sababu ya kufungua zaidi uwezo wa mabenki ambayo yatawawezesha baadhi ya watanzania wenye mawazo mazuri kufufua baadhi ya viwanda ambavo vipo kwenye orosha hapo juu na kuwezesha soko la ajira kuanza kupanuka nchini kote.

Tanzania ina kila sababu ya kujivunia jitihada hizi za mwalimu na sisi wananchi hatuna budi kuunga mkono jitihada hizi za serikali ya awamu ya tano kwa nguvu zote.
 
Baadhi yetu tunamsema Mzee Kambarage as ameua viwanda, ina maana alianzisha akijua anakwenda kung'atuko akaamua kuviua NO.

Bahati mbaya wengi wetu pia tunashindwa kuchambua uongozi na wasaidizi wa kiongozi baada ya kiongozi huyo kuondoka tunakosa malengo na nguvu kuendeleza mazuri ila tunapigana misumari kwa kuonyesha madhaifu tu.

Na bahati mbaya hao hao viongozi tunao wapiigia makofi ndiyo hao hao wakiingia kula bata pale ndani, nao wanaanzisha yao na kuachilia mbali ya aliyemtangulia utadhani ameingia nchi tofauti na aliyokuwepo mtangulizi wake.
 
Safi sana mkuu. Umeviorodhesha takribani vyote. Labda kizazi cha sasa hivi watafanyakazi tofauti na hapo mwanzo. Vingi ya hivyo viwanda vilikuwa vinaendeshwa na ruzuku ya serikali. Matokeo yake hayakuwa mazuri. Purely Eutopia.
 
Alijenga kwa pesa yake mfukoni au ni kodi za wananchi?
Viwanda Vingi hapo vilijengwa sio kwa pesa zake wala kodi ya Wananchi. Vilijengwa kwa msaada wa watu wa China, Urusi na Marekani.

Kwa mfano Mwatex, Kilitex, Urafiki na vingine vya nguo vilijengwa na Wachina kwa urafiki wao na Tanzania

General Tyre ni kwa msaada wa Marekani, nafikiri na cha kusindika nyama (Tanzania Packers)

Kwahiyo HONGERA KUBWA bado ni kwa Mwl. Nyerere kwa kujenga Urafiki na nchi hizo ambazo zimekuwa ni msaada mkubwa sana kwetu.
 
Viwanda Vingi hapo vilijengwa sio kwa pesa zake wala kodi ya Wananchi. Vilijengwa kwa msaada wa watu wa China, Urusi na Marekani.

Kwa mfano Mwatex, Kilitex, Urafiki na vingine vya nguo vilijengwa na Wachina kwa urafiki wao na Tanzania

General Tyre ni kwa msaada wa Marekani, nafikiri na cha kusindika nyama (Tanzania Packers)

Kwahiyo HONGERA KUBWA bado ni kwa Mwl. Nyerere kwa kujenga Urafiki na nchi hizo ambazo zimekuwa ni msaada mkubwa sana kwetu.
Sawa mkuu
 
Back
Top Bottom