Mafanikio ya Utawala wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa awamu ya kwanza

Benson Mramba

Verified Member
Oct 29, 2013
606
1,000
HISTORIA
WENGI WADOGO TUKUMBUSHANE
Anaandika Profesa Mwesiga Baregu
Hayati Mwalimu alipenda kujenga nchi ambayo ina mfumo uchumi wa kisasa ambao unaineemesha jamii ya watanzania ambayo itakuwa inafaidi matunda ya jitihada zake kwa kuweka haki, usawa na rasilimali kwa wote.
Ifuatayo ni orodha ya baadhi ya Mambo ambayo hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipenda aivushe nchi yetu iwe na uchumi wa kujitegemea bila kuwa ombaomba.
1.TANGANYIKA PACKERS - usindikaji,upakiaji na usambazaji wa nyama ya ng'ombe. Kiwanda hiki kilikuwa Kawe na kingine mkoani Shinganya.
2.URAFIKI,Nguo 3.MWATEX, Nguo
4.KILTEX,Nguo
5.MUTEX, Nguo
6.POLYTEX- Nguo, vitenge
7. MOROGORO CANVAS - MAGUNIA, MATURUBAI
8. MOROGORO SHOES- VIATU
9. MOROGORO TANNERIES- NGOZI.
10.MWANZA TANNERIES- NGOZI.
11.BORA SHOES- UTENGENEZAJI WA VIATU.
12. KIBO MATCH FACTORY- Viberiti.
13. NATIONAL, MATSUSHITA, PHILLIPS- Utengenezaji wa batteries, radio na radio cassete.
14. PAMBA ENGINEERING- Uchongaji wa vipuri vya mashine za uchambuaji pamba.
15. SIDO - Shirika la kuhudumia viwanda vidogo
16. Kiwanda cha kubangua Korosho Mtwara
17.Viwanda vya kusindika na kubangua , Kahawa, Alizeti, Pareto, Karanga na Miwa.Morogogo/Kilimanjaro/Singida
18.Kiwanda cha vipuri vya mashine cha Mang'ula
19.Kiwanda cha vipuri za mashine cha Kilimanjaro
20.Kiwanda cha malori (kuunda mabasi na malori) cha Scania.
21.Kiwanda cha magari cha Nyumbu cha jeshi Kibaha.
22. TANALEC- kiwanda cha kutengeneza vifaa mbalimbali vya umeme.
23. Kiwanda cha karatasi cha Mgororo Mufindi mkoani Iringa.
24. Kiwanda cha kusindika na kusambaza maziwa cha UTEGI mkoani Mara.
25. Kiwanda cha usindikaji wa nafaka cha National Milling Corporation cha Dar-es-Salaam.
26.Tanga Steel Rolling Mill- vyuma, saruji na mabati.
27.Viwanda vya saruji vya Tembo Cement, Twiga Cement, Simba Cement pamoja na vile vya ALAF na GALCO.
28.Kiwanda cha zana za kilimo - UFI
29. Kiwanda cha madawa ya binadamu cha KPC - Keko Pharmaceutical Company.
30. Viwanda vya Bia vya Dar, Ndovu na Pilsner Arusha
31. Kiwanda cha Mvinyo Dodoma
32. Kiwanda cha matairi cha General Tyre kilichopo Arusha
33. Kiwanda cha katani cha Amboni mkoani Tanga.
34. TIPER - kiwanda cha kusafisha mafuta machafu, kusambaza mafuta ya dizeli, petrol na mafuta ya taa.
34.Bila kusahau viwanja vya ndege vya JNIA, Kilimanjaro na Mwanza ni miongoni mwa viwanja vikubwa nchini mwetu.
35.Mazingira ya Uwekezaji kwa Watu binafsi.Licha ya jitihada za mwalimu, bado wafanyabiashara binafsi walianzisha viwanda kama vile Amboni Plastic Ltd, Tungi Ltd, Waraguru Partnership Ltd, Sumaiya Group of Companies, kiwanda cha mbolea Tanga, na vingine vingi tu visivyo idadi.
36.Hayati Mwalimu alijenga miundombinu kama barabara,Njia za reli ya kati na ile ya TAZARA, bandari za Dar-es-Salaam,Tanga, Mtwara na ile ya Zanzibar. (Reli ilichanuliwa zaidi si Kama walivyoacha wakoloni)
37.Uanzishwaji wa Vyuo Vya Elimu ya Juu,UDSM, IDM, SUA, IFM,CBE.
KIVUKONI
38.Upanuzi shirika la Ndege kwa kuongeza idaid hadi ndege 14
39.Ujenzi wa Mabwawa ya Kuzalisha Umeme
40.Uanzishwaji wa Benki Kuu ya Tanzania
41.Kutoa Elimu Bure chekechea hadi Chuo kikuu, Kuongeza idadi ya shule za Elimu ya Msingi Nchi nzima, (Tofauti na alizotaifisha)
42.Kuimarisha Ulinzi kwa kuliunda Upya Jeshi la Wanachi JWTZ
43.Kiwanda Cha baskeli Cha Swala.
44.Ujenzi wa Vivuko Viwili.
45.Uanzishwaji wa Vijiji Vya Ujamaa Na Usambazaji wa huduma, Maji, Umeme Na Afya
46.Uanzishwaji wa vituo Vya Afya kila Wilaya kwa Wilaya zaidi ya 100
Hii orodha ni baadhi tu ya viwanda vingi ambavyo serikali ya hayati mwalimu ilijitahidi kuvianzisha chini ya ushirikiano na nchi marafiki kama China, Russia (iliyokuwa USSR) na India.
ONGEZA VITU VINGINE ALIVYOFANYA MWALIMU NYERERE UWASOGEZEE HABARI WATANZANIA WALIO WENGI WAJUE
 

bablai2020

Member
Sep 5, 2020
56
150
Mwalimu isingelikuwa ile vita na Uganda..nchi ingekuwa mbali sana. Tutamsema kwa madhaifu yake yoote ila Moja tu sijawahi kusikia..WIZI.

Huyu mzeee aliipenda hii nchi..kwa upendo ambao hakuna kiongozi yeyote wa vizazi vilivyomfwatia sio Tanzania pekee bali africa nzima waliwahi zipenda nchi zao..
 

Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
23,924
2,000
Ukipora Viwanda vya watu na vitega uchumi vyao kwa kigezo cha Azimio la kuondoa Unyonyaji vinakuwa kwny orodha ya Viwanda ulivyojenga?
 

Narubongo

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
2,698
2,000
Alianzisha shule za ufundi ifunda, Mbeya tech, Arusha, tanga, mazengo nahisi zilihujumiwa ili tuwe tegemezi wa teknolojia kutoka nje

Alikienzi kilimo kwa kuanzisha shule za sekondari zenye mchepuo wa kilimo, leo hii tunawaambia vijana wa dar wajiajiri kupitia kilimo baada ya kumaliza degree ya uhasibu hawajui hata aina tatu za udongo. Tulianza kusoma somo la kilimo kuanzia darasa la 3 au 4 hivi mpaka sekondari form 3 ikiwa somo la lazima, kwa waliobase masomo ya sanaa nao waliruhusiwa kusoma mpaka form 4

Vyuo vingi vya kilimo na mifugo nchi nzima

Ranchi zilikuwa na maelfu ya mifugo

Taasisi za utafiti wa kilimo TARI kila kanda na mifugo LITI

Ukimsoma vizuri mwalimu alikuwa strategist mzuri sana, tatizo aliowaachia hawakujua impact ya hivi vitu kwa miaka ya mbele
 

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
13,712
2,000
Mengi umeyasahau
Ukimaliza kidato cha nne unaenda A-level, kozi au direct employment. Ukimaliza A-level ni higher education, kozi za kati au direct employment na unasaign mkataba kutumikia umma miaka mitano nk. NVTC au FDC kwa waliotaka kujiendeleza baada ya elimu ya msingi nk.

National Institutes of Medical Research- ziko nyingi, Vyuo vya kilimo, SUA, Ukiliguru, Naliendele, etc. na MADARAJA sehemu mbalimbali.
Kiwamda Cha Chibuku Ubungo
Arusha National Milling

Uanzishwaji wa kampuni za mabasi na za biashara za Mikoa,kama vile Mabasi ya Kamata, Uda, Moretco, Coretco... n.k,Kampuni za usafirishaji wa mizigo za Mikoa kama vile Kaudo, Kaumu, Kauru..n.k,RTC kwa Mikoa yote...
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
9,938
2,000
Wewe mwenyewe kuwepo hapo ni mafanikio ya utawala wake, vinginvyo ilikuwa uondoke na surua au Pepo punda.

Kwanza wazazi wako ungewauliza wangekueleza jinsi alivyowaweka pamoja

Sasa swali la msingi nikuulize: kuna sababu yoyote iliyokusukuma kuanzisha mjadala juu yake wakati huu badala ya tunayekwenda kumzika sasa?
Kila jambo lina wakati wake.

Najua utanuna, lakini ni lazima uambiwe ukweli.
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
9,938
2,000
Hii orodha ni baadhi tu ya viwanda vingi ambavyo serikali ya hayati mwalimu ilijitahidi kuvianzisha chini ya ushirikiano na nchi marafiki kama China, Russia (iliyokuwa USSR) na India.
ONGEZA VITU VINGINE ALIVYOFANYA MWALIMU NYERERE UWASOGEZEE HABARI WATANZANIA WALIO WENGI WAJUE
Tanzania Pharmaceuticals, Arusha.

Reli, TAZARA na Barabara, Bomba la Mafuta kwenda Zambia.

Misitu ya Buhindi, Geta, Mufindi, Rubya..., ambayo hadi sasa inavunwa.

Scandinavian countries - Sweden, Norway, Denmark walikuwa ni washiriki muhimu; kama ilivyokuwa Canada

Na wakati huo huo, nchi ikiwa kwenye vita ya ukombozi wa makoloni kusini mwa Afrika - Zimbabwe, Angola, Mozambique, Namibia, Africa Kusini

Bila kusahauVisiwa vya Shelisheli na Comoro.

Alikuwa haimbi "Mabeberu" tu. Alikaa nao na kuwapa ukweli wao, wengi wao walimwelewa, hata kama iliwaumiza kukosa maslahi yao na kuanza kumpiga kampeni za kumpaka matope, baada ya kuelewa ubaya wa matendo yao kwa nchi maskini.

Wananchi walimwelewa alipowaeleza maana ya "ubeberu".

Mengi haya yalifanyika, nchi ikiwa ni maskini sana, hata kama ilijulikana kuna utajiri wa madini chini ya ardhi.

Hivi alianza na wataalam wangapi: mainjinia, madaktari......., hata makatibu mhitasi maofisini huenda walikuwa ni wa kuhesabu kwenye vidole vya mikono miwili. Na alipong'atuka je, ni nyanja gani ilikuwa bado haijaguswa!

Lakini tuache haya ya ujenzi wa mavitu pekee.

Ujenzi muhimu sana ulifanyika katika ujenzi wa umoja wetu, kama wananchi wa taifa moja.

Kijana mdogo anamaliza kidato cha nne mahali fulani Singida, anajikuta yupo Mtwara, hata hana mtu mwingine anayemfahamu tokea Singida, na anajisikia yupo nyumbani kabisa. Hakuna wa kuuliza yeye katokea wapi kwa kejeli.
 
  • Love
Reactions: BAK

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom