Ripoti ya Uchunguzi vifo vya watoto Tabora | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ripoti ya Uchunguzi vifo vya watoto Tabora

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Invisible, Oct 19, 2008.

 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  Oct 19, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  MUHTASARI WA TAARIFA YA TUME YA MKUU WA MKOA WA TABORA YA KUCHUNGUZA TUKIO LA VIFO VYA WATOTO 19 KATIKA KUMBI ZA MUZIKI ZA BUBBLES CLUB NA NSSF (110 DISCO THEQUE)

  Mnamo tarehe 1/10/2008 kati ya 9.00 alasiri na saa 11.30 jioni katika la NSSF Plot Na. 3, Kata ya Kanyenye kati ya Mtaa wa Shule na Jamhuri katika manispaa ya Tabora kwenye kumbi mbili za ‘Bubbles Club’ na NSSF (110 Disco) kulikuwa na Disco kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Eid el Fitri. Wakati muzziki wa Disco unaendelea katika kumbi hizo zilipatikana taarifa za watoto kuzimia kwa ukosefu wa hewa safi.

  Kutokana na taarifa hiyo, askari polisi (traffic) waliokuwa kazini katka eneo hilo pamoja na baadhi ya wananchi walisaidiana kuwaokoa watoto waliozimia na kuwapeleka Hospitali ya mkoa kitete (Kalunde OPD), ambako iligundulika kuwa watoto 19 waliofikishwa hospitali tayari walikuwa wamefariki na 16 majeruhi.

  Kutokana na hali hiyo uliitisha kikao cha dharura cha kamati ya ulinzi na Usalama ya Mkoa na baadaye uliunda Tume kuchunguza chanzo cha tukio hilo. Tume ilianza kazi tarehe 03/10/2008.

  Uchunguzi uliofanywa na tume kwa kuzingatia hadidu za rejea, na kubaini yafuatayo:-

  • Upigaji muziki katika ukumbi wa ‘Bubbles Club’ haukuwa halali. Muziki kwa watoto ulipigwa ndani ya eneo kunako uzwa vileo na biashara ya vileo ilikuwa inaendelea. Aidha ‘Bubbles Club’ haikuwa na kibali cha kupiga “Disco toto”.

  • ‘Bubbles Club’ haikuwa na usajili hai wa BASATA hivyo haikustahili kupewa kibali chochote cha kuendesha shughuli za sanaa.

  • ‘110 Disco Theque’ haina usajili wa BASATA hivyo haikustahili kupewa kibali cha kkuendesha shughuli za sanaa.

  • Ofisi ya Afisa Utamaduni Manispaa ambayo ina mamlaka ya kutoa vibali vya kuendesha shughuli za sanaa haizingatii taratibu za utoaji vibali na ndani ya ofisi hiyo upo uholela mkubwa katika utekelezaji wa jukumu hilo. Mbali na vibali kusainiwa na wasiostahili (makarani na wahudumu), vinatolewa bila kuwa na saini ya mwombaji au muidhinishaji na vingine kutolewa kwa wasiostahili.

  • Usimamizi mbovu wa shughuli za sanaa umesababisha Halmashauri ya manispaa ya Tabora kupoteza mapato mengi yatokanayo na shughuli hizo. Ada za vibali zinazotozwa ni ndogo kuliko zinazotakiwa na wanaopewa vibali bya muda mrefu wamekuwa wakilipa china ya robo ya kiwango cha fedha kinachotakiwa kulipwa.

  • Ofisi ya Afisa utamaduni wa Manispaa imekuwa haifanyi ukaguzi katika ukumbi nyingi zinazoendesha shughuli za sanaa kujiridhisha endapo masharti ya vibali yanafuatwa na imekuwa haizingatii kanuni ya vibali inayoelekeza maombi yawasilishwe siku kumi na nne kabla ya siku ya onyesho ili kuipatia ofisi yake muda wa kufanya ukaguzi.

  • Matumizi yliokusudiwa na mmiliki wa jingo la NSSF kwa kumbi za ‘110 Disco Theque’ na ‘Bubbles Club’ ni kwa mikutano na sherehe za kiofisi (Functional Hall/Meeting). Mkataba hai wa upangaji kati ya NSSF na Manji L. Patel(Bubbles Club) ni kwa matumizi ya ofisi. Hata hivyo uongozi wa NSSF unakiri kuwa ulifahamu kuwa Manji L. Patel aliomba ukumbi huo kwa lengo la kupiga Disco na kwamba kosa lililofanyika ni katika kujaza mkataba (Typographical error).

  • Uongozi wa NSSF ulifahamu na ulitoa kibali cha mabadiliko yaliyofanywa na mmiliki wa ‘Bubbles Club’ya kuziba madirisha na sehemu nyingine za kupitisha hewa ya asili pamoja na hatua ya kuufanya ukumbi huo upitishe sauti (sound proof). Pamoja na jambo hilo, hawakumtaka mpangaji huyu kuwapatia michoro ya marekebisho hayo ili waiwasilishe kwa mhandisi wa Manispaa kuomba kibali cha ujenzi. Kutokana na kutozingatiwa kwa taratibu, mmilkki wa ‘Bubbles Club’ alifanya mabadiliko ambayo hayakuzingatia ushauri wa kitaalamu na tahadhari za kiusalama kama vile kuwa na milango zaidi ya dharura (escape routes) na vifaa vya kugundua moto (smoke and heat detectors)

  • Uuzaji tiketi umeonyesha kasoro kubwa. Siku ya tarehe 01/10/2008. Uuzaji tiketi ulifanywa nje ya jingo la NSSF badala ya kufanywa katika milango ya kuingilia kwenye kumbi hizo. Waendeshaji wa Disco kwenye kumbi hizo ambao ni Mkurugenzi wa ‘Bubbles Club – SHASHKANI PATEL na mmiliki wa ‘110 Disco Theque’ PROJESTUS FIDELIS waliotoa vitabu vingi vya tiketi kwa mawakala waliowapatia jukumu la kukatisha tiketi ambalo walilitekeleza jukumu hilo nje ya jingo NSSF upande wa Mtaa wa Shule. Mawakala hao walikuwa wakiendesha zoezi hilo mithili ya wapiga debe kwa kuhangaika walinzi katika milango ya kuingilia kumbini (Mabaunsa) kwa lengo la kudhibiti uingiaji ndani ya kumbi. Mazingira hayo yanadhihirisha kuwepo kwa kipaumbele cha kujaza kumbi na kupuuzwa kwa tahadhari za kutozidisha watoto katika kumbi na kuupuzwa kwa suala la usalama ndani a kumbi na nje katika ngazi za kuelekea katika kukmbi hizo. Tume inaamini kuwa ingekuwepo mipango thabiti ya kuangalia usalama madhara haya yaliyotokea yangeweza kuepukika

  • Kutokana na mahojiano na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dr. LESLIE MHINA, Tume imebaini kuwa watoto waliofikishwa hospitali ya kitete ni 35. Kati yao 19 walikuwa wamefariki kabla ya kufikishwa hospitali.
  Orodha ya watoto hao ni kama ifuatavyo:-

  S/NO JINA KAMILI UMRI JINSIA ANAKOTOKA
  1. Veronica Maningu 7 F KANYENYE
  2. Beatrice Makelele 14 F MWINYI
  3. Jacob Cerad 12 M TAMBUKARELI
  4. Salim Hamisi 12 F TAMBUKARELI
  5. Hadija Waziri 12 F GONGONI
  6. Rehema Frugensimoyo 13 F SIKONGE ROAD
  7. Selemani Idd 11 M NG’AMBO
  8. Mrisho Seleman 9 M ISEVYA
  9. Abdallah Rehani 14 M MWANZA ROAD
  10. Agatha Maningu 12 F KANYENYE
  11. Paulina Emmanuel 11 F MWINYI
  12. Mohamed Kapaya 15 M IPULI
  13. Ramla Yenga 15 F CHEYO
  14. Habiba Shabani 14 F MWINYI
  15. Donald Galus Kasela 12 M MIRAMBO BARACKS
  16. Mwanahamisi Waziri 11 F GONGONI
  17. Philipo Haule M IPULI
  18. Ashura Jabal 12 F MWINYI
  19. Yasin Rashid 11 M B/MZINGA

  Watoto 16 majeruhi walifikishwa hospitali, wane walitibiwa na kuruhisiwa siku hiyo hiyo. Watoto 12 walilazwa, watoto 11waliruhisiwa kwa nyakati tofauti. Mgonjwa mmoja JUMANNE MASHAKA amehamishiwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi. Hadi Tume inakamilisha kazi yake hali ya mgonjwa ilikuwa haijabadilika.

  Watoto waliolazwa ni hawa wafuatao:-

  S/NO JINA KAMILI UMRI JINSIA ANAKOTOKA
  1. SAKINA ALLY 10 F KIZIGO PR. S NGB
  2. DAVID CHARE 18 M MWINYI
  3. KULWA IDDI 12 F KIZIGO PRE. S. NGB
  4. JOSEPHINA JULIUS 13 F FILTER (COMPLETED STD VII
  5. THERESIANA JERAZI 12 F MWINYI PRIS STD VI
  6. NAOMI JOSEPH 13 F NGB. STD. VI
  7. AGNESS KASELE 13 F MWINYI COMP. STD VII
  8. TATU HAMADI 15 F MWANZA ROAD COMP. STD VII
  9. SHUFAA HASSANI 12 F KANYENYE PR. STD. III
  10. MSIMU REHANI 15 F
  11. JUMANNE MASHAKA 11 M MWINYI STD III
  12. MWAMI MASUMBUKO 10 M

  Kwa ujumla taarifa ya uchunguzi wa kitaalam imeonyesha kuwa watoto hao walifariki kwa kukosa hewa safi (Suffocation Tazama T. 24). Tume imebaini kuwa hatua zilizochukuliwa na uongozi wa hospitali ya Mkoa Kitete kuwahudumia wahanga na wale waliofariki zilikuwa za haraka na za kitaalamu. Imebainika kuwa watoto walifikishwa hospital ya kitete (Kalunde OPD) kati ya saa 11.30 – 12.30 jioni. Watoto 19 walifikishwa wakiwa wamefariki. Watoto 16 walikuwa majeruhi katika hatua mbalimbali. Aidha vifaa vya matibabu kwa huduma za awali vilikuwa vinatosha na hakuna mtoto aliyefariki mikononi mwa Madaktari ambao walikuwa wanatosha kutoa huduma kwa wahanga hao.
  Changamoto iliyojitokeza kwa hospitali katika tukio hili ni upungufu wa magali ya kubeba majeruhi (Ambulance), upungufu wa machela (stretcher) na kupokea majeruhi wengi kwa wakati mmoja pasipo kuwa na taarifa za awali.

  Siku ya tarehe 01/10/2008 kumbi za ‘Bubbles Club’ na NSSF (110 Disco Theque) zilijaza watu wengi kupita uwezo wake kwa lengo la kupata mapato zaidi. Ulikuwepo mbanano mkubwa ndani ya kumbi hizo, joto kali na haikuwepo nafasi ya kutoshaya kucheza mziki. Joto kali ndani ya ukumbi wa Bubbles Club’ ilisababishwa na msongamano mkubwa wa watu,kushindwa kufanya kazi kwa viyoyozi, kukosekana kwa mzunguko wa hewa safi, uvutaji sigara ndani ya ukumbi, unywaji pombe na rangi iliyokuwa imepakwa siku chache kabla ya siku hiyo kulisababisha watoke jasho, wasikie kiu, harufu mbaya na kukosa hewa safi hali iliyowafanya watoto kutafuta njia ya kutoka ndani ya ukumbi. Kutokana na hali hiyo watoto watatu walifariki ndani ya ukumbi wa ‘Bubbles Club’. Aidha katika arakati za kujiokoa, baadhi ya watoto waliamua kutoka nje ya kumbi zote mbili huku uuzaji wa tiketi na uingiaji wa wateja ukiendelea.Watoto walijazana katika ngazi na kusababisha msogamano mkubwa ambapo baaadhi ya watoto walianguka, kulaliana, kukanyagwa na kuzimia kwa kukosa hewa katika eneo lililoanzia mbele (linding) ya mlango wa ukumbi wa NSSF (110 Disco) hadi kwenye ngazi zinazoelekea nje ya jingo hilo upande wa mtaa wa shule.Hali hiyo ndiyo ilisababisha kelele za watoto zilizoleta mshtuko kwa waliokuwa nje na msingi ndio mwanzo wa vifo zaidi vya watoto kwa kukosa hewa.Ingawa maelezo ya ‘bubbles Club’ yanaonyesha ukumbi wake unauwezo wa kuinga watoto 300.Uchambuzi wa kitaalamu umebaini kuwa uwezo wake ni watoto mia moja na hamsini tu (150).Endapo utatumiwa na watu wazima, uwezo wake ni watu 97 tu. Wakati PROJESTUS FIDELIS ameonyesha kuwa ukumbi wa NSSF (110 Disco) una uwezo wa kuingiza watoto 450, uchambuzi wa kitaalamu unaonyesha kuwa uwezo wake ni watu wazima 240 na 332 tu.Baadhi ya vitabu vya risiti vilivyowaeilishwa mbele ya tume vimeonyesha kuwa ukumbi wa ‘bubbles club’ peke yake uliingiza watoto 632 na NSSF (110 Disco) kwa mujibu wa mwenye disco hilo ni zaidi ya watoto 450 walikuwa wameingia. Hali hii inaonyesha wazi kuwa watoto walioingizwa katika kumbi zote mbili walikuwa wengi zaidi kuzidi uwezo wa kumbi zenyewe.

  Halmashauli ya Manispaa ya Tabora ilikuwa na taarifa za kasoro za ukumbi wa Bubbles Club tangu mwaka 2007 kupitia taarifa ya kikao maalumu kilichofanyika tarehe 12/5/2007 (Tazama T.18),ukagizi wa maafisa Afya kata ya kanyenye wa tarehe 16/09/2006 na barua ya Afisa utamaduni wa Manispaa ya Tabora kwa mmiliki wa ‘Bubbles Club’ (Tazama T,19-kumb. Na.TMC/E/UM/69/111/211 ya tarehe 16/06/2007). Pamoja na taarifa hiyo hakuna hatua thabiti zilizochukuliwa. Endapo hatua zingechukuliwa , tunaamini kuwa vifo vya tarehe 01/10/2008 visingetokea.

  Ingawa waendeshaji wa kumbi za Bubbles Club na NSSF (110 Disco) wanadai kuwa walikuwa wanaendesha disco la watoto, ndani ya kumbi hizo kulikuwa na vijana wenye umri wa miaka 18-21. Hali hiyo watoto walichanganywa na watu wazima kiasi cha kuhatarisha usalama wao. Vijana hawa wenye umri mkubwa walichania kwa kiasi Fulani vifo vya watoto kwa kuwakanyaga katika harakati za kujiokoa.

  Usanifu wa ngazi la jingo la NSSF ulizingatia maumizi ya kiofisi na si kwa kupitisha watu wengi kwa wakati mmoja.Mapungufu hayo ya ngazi yalikwamisha kupitia watu wengi kwa wakati mmoja hivyo kuchangia tukio la vifo vya watoto19.

  Ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Tabora hakuna maeneo salama na yaliyoendelezwa kwa ajili ya burudani za watoto.Hali hiyo inachangia kujaa kwa watoto siku za sikukuu katika kumbi zisizo salama na kusababisha msongamano mkubwa.

  Baadhi ya watoto waliokuwa wamekwenda katika kumbi za burudani za ‘Bubbles Club’ na NSSF (110 Disco) hawakuwa na ruhusa ya wazazi/walezi wao hadi wazazi /walezi walipopata taarifa ya tukio hilo. Tume inaamini kuwa ipo haja ya wazazi/walezi kusimamia maadili kwa watoto wao.

  MAONI NA MAPENDEKEZO YA TUME

  MAONI YA TUME
  Jengo la NSSF Tabora lilikuwa limesanifiwa kwa matumizi ya kiofisi na kumbi za mikutano; azama kiambisho T.01 (permanent office building). Hivyo tume ina maoni kuwa mabadiliko yoyote ya matumizi ya jingo hilo ambayo NSSF waliridhia yafanyike (tazama kiambisho T.07) yaliakiwa yamshilikishe msanifu wa jingo husika na wataalamu wa manispaa waliotoka kibali cha ujenzi. Tume ina maoni kuwa uongozi wa NSSF kuridhia kumbi zilizokusudiwa na shughuli za kiofisi kutumika kwa shughuli za Disco na Bar pasipo kmshilikisha msanifu wa jingo na mtaalamu wa manispaa waliotoa kibali cha ujenzi, kumechangia kwa tatizo lililotokea tarehe 1/10/2008 la vifo vya watoto 19

  Jukumu la kusimamia shughuli za sanaa katika manispaa ya Tabora ni la idara ya utamaduni Manispaa. Ni maoni ya tume kuwa kushindwa kwa Afisa utamaduni Manispaa kufanya ukaguzi katika shughuli za sanaa, kumbi za disco, kutoa vibali holela vya kupiga muziki na disco kinyume cha sheria na kanuni za BASATA kwa kiasi kikubwa kumechangia vifo vya watoto 19 katika jengo la NSSF tarehe 1/10/2008.

  Kwa mujiu wa sheria za BASATA namba 23 ya 1984, na kanuni za BASATA, Afisa utamaduni Manispaa ni msajili Msaidizi wa vikundi vya sanaa na ni katibu wa kamati ya sanaa mkoa. Tume inamaoni kuwa afisa utamaduni Manispaa ameshingwa kukusanya ipasavyo mapato yatokanayo na utoaji wa vibali vya sanaa/disco kama iliyotekelezwa katika sheria ndogo ya manispaa (fees & charges) ya 2003 na hivyo kuikosesha Manispaa mapato.

  • Mapungufu katika Ukimbi wa BUBBLES CLUB yalikwishabainika mapema kabla ya tukio la tarehe 1/10/2008, katika kikao cha Halmashauri cha Kamati maalum ya kujadili maombi ya Club ya Royal na Bubbles Club’ cha tarehe 12/05/2007. Tazama kiambatisho T. 17, na kikao cha tarehe 16/05/2008 – Tazama kiambatisho T. 18. Tume ina maoni kwamba kwa mapungufu haya ya ukimbi wa ‘Bubbles Club’ ambao yalikwishabainika mapema, ukumbi huu ulistahili kufungiwa mapema ili mapungufu yaliyobainishwa yarekebishwe lakini hakuna hatua aliyochukuliwa na Manispaa kuchukua hatua za kuufungia ukumbi huu licha ya mapungufu yaliyobainishwa mapema kumechangia kutokea tukio la tarehe 1/10/2008 la vifo vya watoto 19.
  • Jukumu la usimamizi wa shughuli za upigaji wa Disco, uuzaji wa tiketi, kuzingatia masharti ya vibali na taratibu za uendeshaji wa ukumbi. Tume ina maoni kwamba utaratibu ulitumiwa na wamiliki wa kumbi wa kutoa kuuza tiketi nje ya jengo tofauti na sehemu walizotenga badala yake kuruhusu wauzaji wa tiketi kugombania wateja nje a jengo ni utaratibu mbovu ulisababisha kuuzwa kwa tiketi nyingi bila kuzingatia uwezo wa kumbi watoto/vijana wengi kwenye kumbi za ‘Bubbles Club’ na one disco na pia watoto wengine wakiwa na tiketi kusimama kwenye ngazi wakitaka kuingia kwenye disco na kusababisha vifo vya watoto 19 tarehe 01/10/2008. Tume ina maoni kuwa kuuza tiketi ambazo hazijazwi tarehe ni ukiukaji wa taratibu na mwanya wa kuruhusu idadi kubwa ya watu/watoto kuingia katika kumbi za muziki/Disco.
  • Jukumu la kuchukua hatua, kuzifanyia kazi taarifa za ukaguzi zinazowasilishwa manispaa na maafisa Afya wa kata ni la afisa Afya wa manispaa. Tum ina maoni kuwa kitendo cha afisa Afya wa kufumbia macho mapunguu yaliyoainishwa na Afisa Afya wa kata ya kanyenye katika taarifa ya ukaguzi wake katika ukumbi wa Bubbles Club tarehe 19/09/2006, uliwza kutoa mwanya wa kumbi hizi kuendesha shughuli za upigaji Disco hadi kufikia kusababisha maafa yaliyotokea tarehe 01/10/2008.
  • Ni jukumu la Afisa biashara kuhakikisha kuwa kabla hajatoa leseni ya vileo, sehemu amboyo vileo hivyo vitauzwa imekaguliwa na vyombo husika ambayo ni Afisa Afya, Afisa mipango miji, Afisa polisi wilaya kwa lengo la kuhakikisha eneo lililokusudiwa linakighi matakwa ya sheria. Tume inamaoni kuwa kwa Afisa biashara kutozingatia matakwa hayo ya biashara alitoa alitoa leseni ya vileo kwa Bubbles Club tarehe 19/9/2006, uliweza kutoa mwanya wa kumbi hizi kuendesha shughuli za upigaji Disco hadi kufikia kusababisha maafa yaliyotokea tarehe 01/10/2008.
  • Ni Jukumu la Afisa Biashara kuhakikisha kuwa kabla hajatoa leseni ya vileo, sehemu ambayo vileo hivyo vitauzwa imekaguliwa na vyombo husika ambavyo ni Afisa Afya, Afisa Mipango Miji, Afisa wa Polisi Wilaya kwa lengo la kuhakikisha eneo lililokusudiwa linakidhi matakwa ya sheria. Tume ina maoni kuwa kwa Afisa Biashara kutozingatia matakwa hayo ya biashara alitoa leseni ya vileo kwa Bubbles Club na matokeo yake watoto walioingia disko 1/10/2008 katika ukumbi wa Bubbles Club waliuziwa pombe, na pia kutofanya ukaguzi kulisababisha watoto wa chini ya miaka 16 kuingia katika ukumbi unaouzwa pombe kinyume cha sheria ya vileo.
  • Jukumu la kutenga maeneo ya kuchezea watoto ni la Halmashauri ya Manispaa. Tume ina maoni kuwa, Manispaa haijahamisha jamii vya kutosha kuwekeza katika biashara ya kuendeleza maeneo ya wazi ili yatumike pia kama sehemu za kuchezea watoto.
  • Katika uchunguzi wake, Tume imegundua kuwa wakati wa sikukuu mbalimbali hususan za kidini, baadhi ya wazazi huwaachia watoto wao kwenda kwenye maeneo ya starehe kumbi za disko, bila uangalizi wa wazazi au walezi. Tume in maoni kuwa wazazi wazingatie maadili mema katika malezi ya watoto. Wazazi wanapaswa kutoa uangalizi kwa watoto kuepusha matukio ya aina hii kwa siku za baadaye.

  MAPENDEKEZO YA TUME
  1. Tume inapendekeza kwamba marekebisho yote yaliyofanyika katika ukumbi wa Bubbles club pasipo kushirikisha mamlaka husika yaondolewe na sehemu hiyo itumike kwa matumizi ya awali ambayo ni ya ofisi na mikutano.

  2. Tume inapendekeza mwenye jengo la NSSF Mkoa awajibishwe kutokana na yeye mwenyewe kuridhia mabadiliko hayo bila kuwashirikisha wasanifu wa jengo hilo na wataalamu wa Manispaa.

  3. Tume inapendekeza ofisi ya Afisa Utamaduni Manispaa kuwe na viongozi waadilifu na wenye uwezo wa kuweza kusimamia shughuli hizo za sanaa katika manispaa ya Tabora, ili kuepusha tukio kama hilo lisitokee tena.

  4. Tume inapendekeza kuwa uongozi wa manispaa Tabora uwe unayafanyia kazi mapendekezo yanayotolewa na kupitishwa na vikao vyao halali vya kiutendaji.

  5. Tume inapendekeza kuwa kumbi zote za burudani zilizosajiliwa na ambazo ziko hai zioneshe idadi kamili ya watu wanaoruhusiwa kuingia ndani na tiketi ziuzwe kulingana na idadi hiyo na pawepo sehemu maalum ya kuuzia tiketi.

  6. Tume inapendekeza kuwa kumbi au maeneo kwa ajili ya maonyesho au disko la watoto zisiwe na leseni za kuuza vileo.

  7. Tume inapendekeza kuwa baadhi ya sehemu za jengo la NSSF zikiwemo kumbi za one Ten Disco na Bubbles Club hazina vifaa vya usalama vya kujiokoa na majanga mmiliki wa jengo (NSSF) ni lazima aweke vifaa vyote muhimu vya kuzimia moto, vifaa vya kugundua moto (fire detectors) na kuweka milango ya dhararu ya kujiokolea pindi janga la moto au msongamano wa watu unapojitokeza. Milango ya dharura iliyozibwa yote irudishwe katika hali yake ya zamani kwa ajili ya usalama.

  8. Tume inapendekeza kuwa idara ya Afya Manispaa iwajibishwe kwa kushindwa kutekeleza majukumu ipasavyo, mathalani kwa kushindwa kuchukua hatua kwa ukumbi wa ‘Bubbles Club’ baada ya kugundua kuwa unamapungufu ya usafi.

  9. Tume inapendekeza kuwa Afisa Utamaduni wa Manispaa awajibishwe kwa kushindwa kusimamia shughuli za sanaa ipasavyo na kutoa vibali kiholela, kutoa vibali kwa vikundi ambavyo havijasajiliwa na pia kutoa vibali kwa vikundi ambavyo usajili wake sio hai na vile vile kutofuatilia ua kukagua waendeshaji wa disco kuona kama wanatekeleza masharti ya vibali walivyopewa, hadi kuchangia kutokea tukio la vifo vya watoto 19.

  10. Tume inapendekeza Halmashauri ya Manispaa itenge maeneo ya wazi kwa ajili ya burudani ya watoto. Vile vile watu binafsi wahamsishwe kuwekeza katika maeneo ya burudani kwa ajili ya kuchezea watoto.

  11. Tume inapendekeza vibali vya disko la watoto vitolewe kwa maeneo maalumu yaliyoandaliwa kwa ajili ya watoto . vile vile vibali hivyo vitaje umri wa watoto wanauruhusiwa kuwepo maeneo hayo.

  12. Tume inapendekeza kuwa ili kuhakikisha usalama wa watoto ambalo ni jukumu la msingi la kila mzazi/mlezi, wazazi wahakikishe suala la maadili ya mtoto linazingatiwa. Watoto wasiruhusiwe kwenda kwenye maeneo ya disko pasipo uangalizi.

  13. Tume inapenekeza kuwa mamlaka zinazohusika na utoaji wa leseni za vileo zifanye shughuli zao kwa kushirikiana na idara ya Afya, polisi wa mipango Miji, kufanya ukaguzi mara kwa mara kwa lengo la kubaini wanaokiuka taratibu na masharti yanayotakiwa kwenye biashara husika.

  14. Tume inapendekeza kuwa ili kutoa ulinzi katika sehemu za burudani jeshi la Polisi litaarifiwe kuhusu shughuli hizo ili wafuatilie usalama wa maeneo hayo.

  15. Tume inapendekeza kuwa mmiliki/mwendeshaji wa Bubbles Club achukuliwe hatua za kisheria kwa kufanya biashara ya Disco kinyume cha sheria na kanuni za BASATA, na kusababisha vifo vya watoto 19.

  16. Tume inapendekeza kuwa mmiliki/mwendeshaji wa Bubbles Club achukuliwe hatua za kisheri kwa kuvunja sheria ya vileo inayokataza kuingiza watoto sehemu zinazouzwa vileo kirahisi wakati wowote ule janga lolote linapotokea ndani ya kumbi.

  17. Tume inapendekeza kuwa Jeshi la Polisi liwatafute walinzi (Mabaunsa) na wakatisha tiketi wote waliohusika katika tukio la tarehe 1/10/2008 wachukuliwe hatua za kisheria.


  Natumaini inasomeka vema...
   
 2. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2008
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 428
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Date::10/18/2008
  Vifo vya watoto Tabora vilichangiwa na sigara, pombe holini
  Victor Kinambile, Tabora

  TUME iliyoundwa kuchunguza chanzo cha vifo vya watoto 19 vilivyotokea katika kumbi za disco siku ya Idd mosi mjini hapa imekamilisha kazi hiyo na kueleza kuwa vifo hivyo vilitokana na kukosa hewa, kuchanganywa na wakubwa, kuvuta sigara, kunywa pombe na harufu ya rangi iliyokuwa imepakwa siku moja kabla tukio.


  Akikabidhi ripoti hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Abed Mwnyimsa, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Emson Mmari ambaye pia ni Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, alisema tume hiyo imebaini kasoro nyingi kwenye kumbi hizo, ambazo zinasadikika kuwa ni chanzo cha watoto hao kukosa hewa na kisha kufariki dunia.


  Alisema wamiliki walikuwa wakiuzia watoto pombe kinyume na sheria za vileo,watoto walichanganywa na watu wazima ambao walisababisha kukanyana kwa kuwazidi watoto hao nguvu.


  Alisema tume imebaini kwamba baadhi ya sehemuza jengo hilo linalomiliuwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii nchini (NSSF) na hasa kwenye kumbi hazina vifaa vya usalama hivyo kumtaka mmilikiwa wake kuweka vifaa vyote muhimu.


  Mmari amezitaja kasoro hizo kuwa, ni wamiliki wa kumbi hizo kukatisha

  tiketi kupita kiasi na kuruhusu watoto wengi zaidi kuingia ukumbini, milango

  ya dharula siku hiyo kuwa imefungwa, na hasa katika ukumbi Bubbles, ambako ingekuwa wazi huenda maafa hayo yasingetokea.  Kufuatia hali hiyo tume, imependekeza kwamba wamiliki wa kumbi hizo

  wachukuliwe hatua kali za kisheria kwa kufanya biashara ya disico na

  kuwauzia watoto pombe kinyume cha sheria na kusababisha vifi vya watu 19.


  Tume hiyo pia imependekeza kuwa mmiliki mwendeshaji wa Bubbles night Club

  achukuliwe hatua za kisheria kwa kuvunja sheria ya vileo inayomkataza

  kuingiza watoto sehemu zinazouza vileo.


  Pia imependekeza kuwa Mmiliki wa na mwendeshaji wa Bubbles achukuliwe hatua, kwa kuingiza idadi kubwa ya watoto bila kujali uwezo wa ukumbi na hivyo kusababisha msongamano mkubwa na hatimaye vifo vya watoto 19.


  Pia tume hiyo imependekeza kuwa mmiliki wa jengo hilo (NSSF) awajibishwe kutokana na yeye mwenyewe kuridhia mabadiliko ya jengo kuwa kumbi za disco bila kushirikisha msanifu wa jengo hilo na wataalamu wa Manispaa.

  Adha tume hiyo imependekeza kuwa Afisa Utamaduni Manisapaa ya Tabora pamoja na Idara ya Afya wawajibishwe kwa kushindwa kuchukua hatua kwa ukumbi wa Bubbles Club baada ya kugundua kuwa siyo salama kiafya.

  Source: Mwananchi

  Karibuni tujadili kujua mbivu na mbichi kwenye hili suala na hii "snapshot" ya ripoti ya tume iliyoteuliwa na mkuu wa mkoa kuchunguza hii ajali.
   
 3. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2008
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Bora waongezewe ili wakija na new report iwaguse na wenyeviti wa usalama wa mkoa huo akiwamo RC na DC wake maana hii ya sasa haijakaa vizuri bila ya hao wawili Riport hiyo itakuwa unfair.
   
 4. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #4
  Oct 19, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Hiki ndicho nilichokiofia. Msanifu wa majengo yeyote anayetambulika kisheria angeweza kufanya kazi hiyo. Si lazima awe yule aliyelisanifu jengo awali. Huku ni kuingiza biashara pasipo takiwa.

  Wataalamu wa manispaa sehemu yao ni kupitia mapendekezo ya mabadiliko na kutoa kibali au la. Kinachoshangaza ni kama haya mabadiliko yaliishafanyika kitambo walikuwa, kitu gani kiliwazuia manispaa kutoa stop order hadi hapo taratibu zitakapokamilika? Kutokana na udogo wa mji wa Tabora ni lazima walijua kibali hakijatolewa kwa mmiliki kufanya mabadiliko hayo! Hii biashara ya kungoja waletewe na kuogopa wakubwa ndiyo iliyochangia maafa haya.
   
 5. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #5
  Oct 19, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Niliwaomba wananchi hapa kua tusubiri matokeo ya uchunguzi wa tume, na haya ndiyo matokeo yenyewe, kwangu hapa case closed!
   
 6. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #6
  Oct 19, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Vipi kama "msanifu wa jengo hilo" hakuwepo kwenye hiyo trade ya usanifu any longer ? (aliistaafu, alimaliza mkataba au ana bifu na NSSF, alipoteza leseni , na alihamia nje ya nchi.)

  Inawezekana kabisa ni kutafutiana ulaji, kama Fundi Mchundo anavyosema (kama nimekuelewa vibaya nisahihishe FM). Mimi nadhani hii ni incompetence ya Tume. Kipande hicho kimenifanya ni doubt hii tume. Halafu kuna sehemu Tume inaripotiwa kusema "imebaini kasoro nyingi kwenye kumbi hizo, ambazo zinasadikika kuwa ni chanzo cha watoto hao kukosa hewa..."

  Huwezi kushauri watu washitakiwe mahakamani based on "kusadikika." Kwenye criminal case unatakiwa uthibitishe kila kipengele cha mashitaka (ikiwemo chanzo cha watoto kukosa hewa, au kwa hapa inaweza kuwa "causation") uthibitishe "beyond reasonable doubt." Tume ilipoongelea kusadikika inaweza ikawa imewapa defense attorneys kitu cha kusema mahakamani.
   
 7. O

  Ogah JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Kutokuwepo kwa msanifu wa jengo hilo hakuzuii.........wasanifu wengine qualified kufanya kazi inayotakiwa..........kwa kutumia .....as built drawings zinakuwa produced......baada ya mradi kuisha
   
 8. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #8
  Oct 19, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ndio maana nimesema na doubt uwezo wa hii Tume kwa sababu ndio imetuambia kwamba ilibidi NSSF irudi kwa yule yule msanifu wa mwanzo!!!
   
 9. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #9
  Oct 19, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Wakuu hii tume ni level ya mkoa tu, na matokeo yake ni ya kimkoa mkoa, and they did their best as mkoa.

  Sasa lets respect matokeo ya mkoa!
   
 10. O

  Ogah JF-Expert Member

  #10
  Oct 19, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  ......hapana......reference inapoangaliwa back to yule msanifu wa jengo ni kwa sababu kuna kitu kinaitwa design liability.............kwa hiyo wasingeweza kukurupuka tu na kusema.......bila ku-consult any qualified......unaanzia kwenye chimbuko kwanza.......then kunafuata kwingine........with the support of agreement with the next consultant.........which should also take into consideration the intended use of the original design........i.e. without jeopardizing it!!!......au sio Fundi Mchundo!

  Ingawa sijaisoma ripoti kamili ya tume..........nafikiri kwa point hiyo (to consult the original designer) nawapa credit tume husika.............
   
 11. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #11
  Oct 19, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ogah,

  Unajichanganyachanganya. Na manukta nukta katika ya sentensi zako ndio yanafanya unazidi kuwa completely incoherent. Mwanzo umesema hivi: "Kutokuwepo kwa msanifu wa jengo hilo hakuzuii.........wasanifu wengine qualified kufanya kazi inayotakiwa....."

  Sasa kama ulisema mwanzoni kwamba msanifu yoyote qualified angeweza kuendewa kwa nini sasa hivi unaitetea Tume inayoikosoa NSSF kwa kushindwa kumwendea msanifu yule yule wa mwanzo ?

  Field Marshall ES

  Hicho kitu hicho cha kusema tuheshimu na tusiswalishe tunayoambiwa na Serikali ni hoodwinking, brainwashing, upumbazwaji ulioanzia toka utotoni wakati tunafundishwa kutamka A E I O U, hizi ni herufi kuu. Ni tyranny ya Serikali on the minds of men. Ni kutufanya wagonjwa wa vichwa. Sitaki!!!!

  Uwezo wa Tume unatia mashaka kwa wao kusema NSSF ilibidi imwendee msanifu yule yule wa mwanzo. Na pia ni screw up kwa tume "kusadiki" chanzo cha vifo. Kama huna uhakika huwezi kupendekeza hatua za jinai, kwa sababu inabidi Jamhuri iweze kuthibitisha kila kipengele cha mashitaka "beyond reasonable doubt." Lugha ya Tume ya "kusadiki" inaweza kutumiwa na defense attorneys mahakamani.
   
 12. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #12
  Oct 19, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Unajua upumbavu wa mwananchi huonyeshwa kwa njia nyingi sana kwa hiyo mkuu usidhani kwamba kwa kurusha maneno yako kama haya kwamba unajiweka mbali na upumbavu inategemea ni nani anayekusoma, mimi nimesoma shule zote za bongo kama wewe nevr before nimewahi kupumbazwa wala kua brainwashed, siku zote nimepitia kila kitu cha bongo nikiwa na akili zangu intact, sasa labda tukupe pole mkuu kwa kuruhusu kupumbazwa,

  Binafsi ninasema kua bado ninaheshimu haya matokeo ya level ya mkoa, siwezi kuwa mgonjwa wa kichwa kwa kulazimisha matokeo ya mkoa ambayo yametengenezwa kwenye mazingara ambayo ni very limited in resources yalingane ya Ken Star wa US, huo utakua ndio ugonjwa wenyewe wa kichwa au upumbavu! Kama sio idiocy!
   
 13. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #13
  Oct 19, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo unakubali kwamba Tume ikifanya kazi famba na ikatoa ripoti inayoweza kutumiwa kama vielelezo vya kufunga watu jela hiyo ni sawa kwa vile Tume haikuwa na resources ? Kwa mawazo yako wewe yenye umahiri hicho kitu ni sawa na tukiheshimu ?

  Na ni wapi umeambiwa "Tume ya Mkoa" haikuwa na resources za uchunguzi ? Au una habari za ndani ? (Ndio hizi habari za ndani zilizokwambia kwamba Mwinyi alimrithi marehemu Karume kama Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kama ulivyojibu hapa https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/19392-naomba-kuuliza-2.html#post305588 ?
   
 14. O

  Ogah JF-Expert Member

  #14
  Oct 19, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  ............Kuhani tatizo lako ni kuwa........you don't think!..........unachukua kitu kizima kizima ....na kumeza..........sorry....im not here to baby sit any..........kwi kwi kwi kwi..................kusema kwangu "msanifu yeyote qualified angeweza kuwa consulted"..........haimaanishi taratibu husika zirukwe......nilichofanya ni kuongezea pale nilipoishia kuwa.........huwezi kukurupuka na ku-consult any qualified person........mambo kama hayo hayatakiwi kwenda kienyeji enyeji......and thats my point.........sasa kigumu kwako kuelewa ni kipi.........

  ...don't just jump onto my "nuktas".........na kumeza kitu kizima kizima......kwi kwi kwi kwi
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Oct 19, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hakuna sababu ya kumwajibisha mtu mwingine yeyote. Watoto wameshakufa imetoka hiyo. Waliokwisha kamatwa waadhibiwe yaishe.
   
 16. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #16
  Oct 19, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  1.
  1. Haya ni mawazo yako mgando, ya kila ishu kulinganisha bongo na Ulaya, unalilia neno "beyond reasonable doubt" ambalo mwananchi yoyote mwenye akili timamu anatakiwa kujua kuwa halihusiki hapa kabisa kwa sababu hii kamati haikuwa ya Federal Criminal Investigation, au kamati teule ya bunge ambayo ilikuwa na power of ku-waita wahusika kisheria.

  2. Halafu unashindwa ku-aknowledge kwamba matokeo ya kamati hii hayawezi kuwa na nguvu yoyote kisheria kwa sababu hakuna mjumbe yoyote wa kamati aliyeapishwa na anybody under oath, na kwamba ahkuitwa mtu yoyote kutoa ushahidi under oath, uchunguzi wa kisiasa wa state level wewe unataka utoe matokeo ambayo yatakuwa legally accepted na taifa, sasa exactly unataka niite mawazo yako haya kwa jina gani zaidi ya idiocy?

  3. Umahiri wa mawazo huonyeshwa kwa hoja, ambayo inazingatia mazingara ya ishu at hand, all the facts and opinions, na mwisho kutoa conclusion. Lakini umahiri wa mawazo hayawezi kulazimishwa kwa kutumia maneno ya chooni as of your tendecy, na kwenye this haya matokeo ya uchunguzi you are way out of the line na ukweli
  .

  More foolishness, timu ya mkoa wa Tabora wenye madakitari bingwa wawili tu uinaweza kuwa na what reources za ku-prove beyond any reasonable doubt legally kwamba nani ashiatkiwe na nani asishitakiwe on this ishu? Hivi ninahitaji kuwa na habari za ndani kuelewa hili? Are you serious au ndio ile ile kawaida yako na hoja za chooni?

  Karume has nothing to do na ishu ya watoto 19 kufariki Tabora, lakini nitaigusa anyways ingawa sikutaka kabisa kuigusa kule kwa sababu ni chini ya level yangu ni way too low, siwezi kukusaidia iwapo huelewi kwamba rais Karume alipouliwa ni Mwinyi ndiye aliteuliwa na baraza la mapinduzi kushika nafasi yake, na kwamba rais wa baraza la mapinduzi huko visiwani automatically ndiye mkuu wa baraza la mapinduzi kwa sababu ndiye rais wake period, au labda naomba unifundishe ni kiongozi gani wa Zanizbar toka ipate uhuru aliyewahi kuwa mwenyekiti wa baraz la mapinduzi bila kuwa rais wa huko?

  Umejaribu kila njia ndani ya hii forum ku-despute dataz na habari za ndani zinazotolewa humu, lakini kila mtu anajuaa jinsi ambavyo umeshindwa vibaya sana, tena ni aibu kubwa sana, halafu ukajaribu kujifanya bingwa wa uchunguzi wa Dr. Masau na hata ukatishia a law suit yamekushinda vibaya sana na ni aibu ambayo haijawahi kumpata anybody humu ndani zaidi yako wewe tu, umejaribu kuiviruga hii forum na matusi kwa kutumia majina yako napo umeshindwa vibaya sana, umejaribu kupigania uhuru hapa forum nayo yamekushinda maana wote tunajua kwua hapa tuko huru kutoa mawazo yetu bila kutishiwa na mtu hata awe nani,

  Sasa unahangaika, huna goal wala misssion zaidi tu ya kuharibu mijadala, ulitegemea utatishia watu hapa wasitoe dataz, lakini si unaona tunamwaga dataz as usual, sisi tuko hapa kuhabarishana na kuelimishana na kama tungekua tunajua kila kitu kama wewe mwenzetu basi hakuna haja ya kuwepo hapa JF, ukiamua kuwepo hapa ni ku-get down with a program tu huna jinsi bro!

  You are nothing but an idiot and confused creature of God, haya nitukane sasa, again you are an-idiot!
   
 17. M

  Mama JF-Expert Member

  #17
  Oct 19, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  matusi ya nini
   
 18. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #18
  Oct 19, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Haya sio matusi ila ni maneno yanayokubalika hapa JF, upumbazwaji unaweza kufanyika pale tu mlengwa anapokuwa mpumbavu, au idiot,

  Sasa siamini kuwa ulikuwa unajitukana mwenyewe ulipotumia neno Upumbwazaji, au?
   
 19. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #19
  Oct 19, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Jamani huyu ndio tried and trusted source of data zinazoletwa na kujadiliwa hapa Jamii Forums!

  Unatuambia - umerudia matundiko matatu - kwamba Mwinyi ndio aliteuliwa kuwa Rais wa Zanzibar Karume alipokufa mwaka 1972 ?

  Shocking, outandish and bizzare!!

  Yani wewe ndio the heralded conduit of information to Jamii Forums!!!!!

  Only in Tanzania!!! Amazing!!!
   
 20. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #20
  Oct 19, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Mkuu ni kosa ambalo hata siwezi kuli-aknowledge kwa sababu kila mwenye akili mwananchi m-Tanzania, anajua kuwa hili ni kosa dogo sana, lakini ukweli uko pale pale kwamba huna hoja, kuanzia kwenye matokeo ya kamati ya Tabora, wala ishu ya Mwinyi, mimi nilifikiri kwamba una something serious kumbe ni ujinga na nonesense kama kawaida!
   
Loading...