Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,232
- 113,610
Hiki ni kipande cha ripoti ya Sky News, moja ya shirika la habari la binafsi huko Uingereza.
Ni kipande kilichorushwa tarehe 8 mwezi Juni mwaka huu.
Ni kipande kinachozungumzia jinsi ambavyo Rais Magufuli na serikali yake ilivyoamua kukabiliana na huo ugonjwa wa Coronavirus.
Ni karibu miezi miwili sasa tokea Sky News wairushe hiyo ripoti yao.
Sky News waliirejea hofu ya shirika la afya duniani [WHO] kwamba Tanzania iko juu kwenye orodha ya nchi ambazo shirika hilo la afya lilikuwa na hofu nazo sana.
Miezi miwili kasoro juma moja, maisha bado yanaendelea tu kama kawaida!
Maiti hazijatapakaa mabarabarani. Hakuna makaburi ya halaiki. Spitali hazijajaa wagonjwa. Nikijizungumzia mimi binafsi, hakuna ndugu, jamaa, jirani, wala rafiki ambaye nimempoteza kutokana na hiyo Corona.
Kwa muktadha wa kinachoendelea sasa hivi baina ya Tanzania na Kenya, nadhani kuna kitu ambacho Wakenya wanaweza kujifunza kutoka Tanzania ya Magufuli.
Wameamua kukata sijui ndege toka Tanzania. Kuna kipindi sijui walifunga mpaka na Tanzania, na mengineyo.
Ninachokiona toka huko Kenya ni [1] uoga wa viongozi wao na [2] ukosefu wa uthabiti katika maamuzi yao.
Ni kama vile Kenya inaiga mataifa ya Ulaya na Marekani, kwa jinsi ilivyoamua kukabiliana na hiyo Coronavirus.
Tokea dunia ikumbwe na hilo janga, ni karibu miezi 6 sasa au hata na zaidi.
Kama yangekuwepo madhara makubwa sana basi yasingeweza kufichika kabisa.
Haiwezekani kuficha vifo na maradhi. Watanzania tulio wengi hatujaathirika na hiyo Corona. Maisha yetu yanaenda kama kawaida.
Hofu ya WHO haijatimizika. Natamani hao Sky News warudi tena Tanzania baada ya miezi miwili tokea warushe hicho kipande cha habari yao. Natamani warudi waje kufanya ‘follow-up’.
Sijui wakirudi watasemaje tu!!?
NB: Baadhi ya tafsiri zao za watu walioongea Kiswahili katika hii video yao Naona ni kama hazipo sahihi.....