NADHARIA Nadharia mbalimbali kuhusu Covid-19 na chanjo zake

Taarifa hii ni nadharia tu, tumeitolea ufafanuzi kwa kadiri ilivyowezekana
Covid-19 ni janga ambalo lilitikisa ulimwengu kuanzia mwaka 2019. Virusi vya korona ni jamii kubwa ya virusi vinavyojulikana kusababisha magonjwa yanayoanzia homa ya kawaida hadi homa kali kama vile Homa Kali ya Upumuaji ya Mashariki ya Kati (MERS) na Homa Kali ya Mfumo wa Upumuaji (SARS). Virusi hivyo kwa mara ya kwanza viligunduliwa 2019 huko Wuhan, China.

Uzi huu utapitia baadhi ya nadharia zilizoibuka wakati huo pamoja na fafanuzi za kitalamu za nadharia hizo.

1692918200775.png
 
Tunachokijua
JamiiForums inakuwekea pamoja baadhi ya nadharia zilizoibuka wakati wa chanjo za Covid-19 ili kuweka Rejeo muhimu kwa sasa na baadaye.
***

1. Chanjo ya COVID-19 haiathiri nguvu za kiume
Kulikuwapo mawazo yaliyodai kuwa Chanjo ya Covid-19 ilikuwa ni hatari na iliathiri mfumo wa uzazi wa kiume ikiwamo kupunguza nguvu za kiume.

Ukweli ni upi?

JamiiForums ilitafuta ufafanuzi wa Wataalamu mbalimbali wa Afya ili kupata ufafanuzi ambao walieleza yafuatayo:

Wataalamu wa Afya wanaeleza kuwa nadharia zote zinazozihusisha Chanjo za #Coronavirus na kupunguza nguvu za kiume na mfumo wa uzazi kwa mwanaume sio za kweli.
Aidha kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanywa juu ya suala hili Wataalamu wanabainisha kuwa Chanjo za corona zimetengenezwa ili kujenga mfumo wa kinga mwilini wakati mfumo wa uzazi unajitegemea.
Hivyo, wataalamu wanasisitiza kuwa chnjo haiongezi wala kupunguza nguvu za kiume.

***

2. Chanjo ya Covid-19 ilitengenezwa mahususi kuwezesha teknolojia ya 5G
Kulikuwapo na uvumi kwamba janga la virusi vya corona lina uhusiano na juhudi za kusambaza teknolojia ya kisasa ya mawasiliano ya 5G. Uvumi huu ulisambaa kwenye mitandao mbalimbali na kuna baadhi ya watu mashuhuri nchini Tanzania walisimamia hoja hii. Mathalani, Askofu Gwajima katika kanisa lake alitoa mahubiri kwa namna gani Chanjo za Covid-19 ilieneza teknolojia ya 5G.

Je, ukweli ni upi kuhusu hili?
JamiiForums ilipitia ufafanuzi uliotolewa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) ambao ndicho kilikuwa chanzo kikuu kilichofafanua masuala yote yanayohusu Covid-19 na chanjo zote wakati huo. Ufafanuzi wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) kuhusu chanjo kueneza teknolojia ya 5G ulieleza:

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema Virusi vya Corona haviwezi kusafiri kwenye mawimbi ya redio/mitandao ya simu, na kwamba COVID-19 tayari inaenea katika nchi nyingi ambazo hazina mitandao ya simu ya 5G.
COVID-19 huenezwa kupitia matone ya kupumua wakati mtu aliyeambukizwa anapokohoa, kupiga chafya au kuzungumza. Watu wanaweza pia kuambukizwa kwa kugusa sehemu yenye virusi na kisha kushika macho, mdomo au pua.

***

3. Chanjo za Covid-19 huharibu mimba
Kulikikuwa na mashaka kwa watu mbalimbali wakidai Chonjo za Covid-19 zilikuwa hatari kwa mwanamke mjazito kwa sababu zilikuwa na uwezo wa kuharibu mimba.

Upi ukweli kuhusu jambo hili?
JamiiForums ilipitia utafiti uliofanywa na Kituo cha Kudhibiti Magonjwa nchini Marekani (CDC) ambao walieleza yafuatayo:

Kituo cha CDC kinahimiza wajawazito wote, wanaofikiria kuwa wajawazito na wale wanaonyonyesha kupata chanjo ili kujikinga na #COVID19. Utafiti umegundua kiwango cha kuharibika kwa mimba baada ya chanjo ya #COVID19 ni sawa na kiwango cha kuharibika kwa mimba kwa idadi ya watu kwa ujumla.
Data za CDC zilionyesha kuwa manufaa ya kupokea chanjo kwa wajawazito hushinda hatari zozote zinazojulikana au zinazoweza kutokea.

***

4. Chanjo za Covid-19 zinnathiri DNA
Kuliibuka mining'ono kuhusu chanjo za COVID-19 kuathiri DNA. Watu wenye hoja hii walisema chanjo hizo zimetengenezwa kwa lengo la kuharibu DNA ya watu weusi ili kupunguza uwezo wao kukabiliana na magonjwa.

Je, hili lina ukweli wowote?
JamiiFoums ilipitia vyanzo mbalimbali ikiwamo WHO, UNICEF na CDC ambao walitoa ufafanuzi wa kitaalamu kuhusu jambo hili kama ifuatavyo:

UNICEF inaeleza kuwa chanjo hufunza seli jinsi ya kutengeneza protini ambayo huchochea mwitikio wa kinga ndani ya mwili ili kuulinda dhidi ya virusi. mRNA ni tofauti na DNA na hukaa tu ndani ya seli kwa takriban saa 72 kabla ya kuharibika. Hata hivyo, haiingii kamwe kwenye kiini cha seli, ambapo DNA huhifadhiwa.

***

5. Chanjo za Covid-19 husababisha usumaku mwilini
Kuliibuka uvumi ulioambatana na Video mbalimbali zikionesha namna miili ya watu ikipata usumaku na kunata vitu mbalimbali vya chuma baada ya kuchanjwa chanjo za Covid-19. Baadhi video pia zilionesha namna miili ya watu waliochanjwa ikizalisha umeme na kuweza kuwasha taa.

Upi ukweli wa jambo hili?
JamiiForums ilipitia ufafanuzi uliotolewa na Kituo cha CDC ambao walisema yafuatayo:

Chanjo ya COVID19 haisababishi mwili au sehemu ya mwili iliyochomwa sindano kutengeneza nguvu ya usumaku. Chanjo hizo hazina viambata vyovyote vyenye asili ya chuma
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom