Ripoti ya Sky News kuhusu Magufuli na COVID-19

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,212
113,501
Hiki ni kipande cha ripoti ya Sky News, moja ya shirika la habari la binafsi huko Uingereza.

Ni kipande kilichorushwa tarehe 8 mwezi Juni mwaka huu.

Ni kipande kinachozungumzia jinsi ambavyo Rais Magufuli na serikali yake ilivyoamua kukabiliana na huo ugonjwa wa Coronavirus.

Ni karibu miezi miwili sasa tokea Sky News wairushe hiyo ripoti yao.

Sky News waliirejea hofu ya shirika la afya duniani [WHO] kwamba Tanzania iko juu kwenye orodha ya nchi ambazo shirika hilo la afya lilikuwa na hofu nazo sana.

Miezi miwili kasoro juma moja, maisha bado yanaendelea tu kama kawaida!

Maiti hazijatapakaa mabarabarani. Hakuna makaburi ya halaiki. Spitali hazijajaa wagonjwa. Nikijizungumzia mimi binafsi, hakuna ndugu, jamaa, jirani, wala rafiki ambaye nimempoteza kutokana na hiyo Corona.

Kwa muktadha wa kinachoendelea sasa hivi baina ya Tanzania na Kenya, nadhani kuna kitu ambacho Wakenya wanaweza kujifunza kutoka Tanzania ya Magufuli.

Wameamua kukata sijui ndege toka Tanzania. Kuna kipindi sijui walifunga mpaka na Tanzania, na mengineyo.

Ninachokiona toka huko Kenya ni [1] uoga wa viongozi wao na [2] ukosefu wa uthabiti katika maamuzi yao.

Ni kama vile Kenya inaiga mataifa ya Ulaya na Marekani, kwa jinsi ilivyoamua kukabiliana na hiyo Coronavirus.

Tokea dunia ikumbwe na hilo janga, ni karibu miezi 6 sasa au hata na zaidi.

Kama yangekuwepo madhara makubwa sana basi yasingeweza kufichika kabisa.

Haiwezekani kuficha vifo na maradhi. Watanzania tulio wengi hatujaathirika na hiyo Corona. Maisha yetu yanaenda kama kawaida.

Hofu ya WHO haijatimizika. Natamani hao Sky News warudi tena Tanzania baada ya miezi miwili tokea warushe hicho kipande cha habari yao. Natamani warudi waje kufanya ‘follow-up’.

Sijui wakirudi watasemaje tu!!?

NB: Baadhi ya tafsiri zao za watu walioongea Kiswahili katika hii video yao Naona ni kama hazipo sahihi.....

 
Hawawezi kurudi tena kuongelea swala hili.

Mabeberu hao hawatutakii mema hata siku moja.

Mshambulizi wetu kaucheza na bao kalifunga... majirani zetu wamebaki kutafuta mpira na mpaka sasa hawauoni
 
Nikijizungumzia mimi binafsi, hakuna ndugu, jamaa, jirani, wala rafiki ambaye nimempoteza kutokana na hiyo Corona.
Afadhali umejizungumzia wewe, ok, sasa wewe mwenyewe uko kwa mabeberu, utapatia wapi ndugu? ndugu zako wanadedi kimya kimya, unadhani wakivuta kuna Wa kunyanyua domo lake kua kavuta na hio kitu? Thubutu yake!

ataambiwa au kuandikiwa kua ni kwa changamoto za upumuaji, jifanye unajitangazia hio kitu ndio utawajua hao unaowapamba!

Nikwambie tu watu tunaishi kwa kudra za god basi!
 
afadhali umejizungumzia wewe, ok, sasa wewe mwenyewe uko kwa mabeberu, utapatia wapi ndugu? ndugu zako wanadedi kimya kimya, unadhani wakivuta kuna Wa kunyanyua domo lake kua kavuta na hio kitu? thubutu yake!
ataambiwa au kuandikiwa kua ni kwa changamoto za upumuaji, jifanye unajitangazia hio kitu ndio utawajua hao unaowapamba!
nikwambie tu watu tunaishi kwa kudra za god basi!
We mbona hujafa?
 
afadhali umejizungumzia wewe, ok, sasa wewe mwenyewe uko kwa mabeberu, utapatia wapi ndugu? ndugu zako wanadedi kimya kimya, unadhani wakivuta kuna Wa kunyanyua domo lake kua kavuta na hio kitu? thubutu yake!
ataambiwa au kuandikiwa kua ni kwa changamoto za upumuaji, jifanye unajitangazia hio kitu ndio utawajua hao unaowapamba!
nikwambie tu watu tunaishi kwa kudra za god basi!
Labda wewe na ukoo wako!!
 
Jana tu hapa jirani Kuna mtu kaanguka na kufa.Hivi mzee wa uwazi alilazwa kwa siku ngapi vile?
 
Hawawezi kurudi tena kuongelea swala hili......
Mabeberu hao hawatutakii mema hata siku moja.......
Mshambulizi wetu kaucheza na bao kalifunga.......majirani zetu wamebaki kutafuta mpira na mpaka sasa hawauoni......
it nice to see you Preta
(hatufahamiani)
 
Back
Top Bottom