Ripoti ya siri juu ya Zitto Kabwe kwa CHADEMA

Status
Not open for further replies.

Jason Bourne

JF-Expert Member
May 11, 2011
200
438
Wakuu kutokana na ripoti hii kuwa ndefu, nitakuwa nawapa kidogokidogo mpaka iishe, kisha pimeni wenyewe.

##############
TAARIFA:
CHADEMA imeukana waraka huu na kudai umetengenezwa kwa malengo ya kisiasa na wapinzani wao
##############

RIPOTI YA SIRI JUU YA ZITTO KABWE
KWA
CHADEMA


UCHUNGUZI WA MWENENDO WA KISIASA WA ZITTO Z. KABWE NDANI NA NJE YA CHADEMA.



UTANGULIZI:
Tangu mwaka 2008 mwenendo wa kisiasa wa Zitto Zuber Kabwe ulianza kutiliwa shaka na wanachama wa CHADEMA ndani na nje ya chama, Hili lilipelekea kuibuka maneno ya chini kwa chini kuwa anakisaliti chama.

Hilo liliilazimu timu ya kijasusi ya chama kuanza kufuatilia nyendo zake kwa ukaribu zaidi usiku na mchana ili kujiridhisha pasipo kuacha chembe ya mashaka. Ifahamike kuwa chama kina idara ya ulinzi na usalama wa chama na viongozi wake yenye uwezo wa kufuatilia nyendo za majasusi wa nje na viongozi na wanachama wake popote walipo kwa masaa 24. Baada ya kujiridhisha kuwa mwenendo wake ni wa mashaka, bila kusita timu ya ujasusi ilianza kazi rasmi ya ujasusi dhidi ya nyendo zote za Zitto Zuberi Kabwe


MAMBO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI DHIDI YA ZITTO KABWE.

Kumfuatilia yeye binafsi nyendo zake.
Kufuatilia mawasiliano yake ya simu.
Kufuatilia mawasiliano yake ya barua pepe.
Kufuatilia pato lake nje ya kazi zake halali za kibunge.


SEHEMU YA KWANZA 2008

Chombo chetu cha ujasusi tulichokipandikiza kwa siri katika nyendo zote za Zitto Kabwe na ndani ya vikao vya mwanzo kabisa vya Zitto na viongozi serikalini, nahata vile vikao muhimu vya idara ya ujasusi ya chama cha mapinduzi (ccm), kinatupa fursa ya kuweka msingi wa kuimarisha chama cha CHADEMA na kutenda haki kidemokrasia kwa maslahi ya chama na Taifa kwa ujumla:

Mnamo Jumatatu ya tarehe 16/6/2008 saa 09:46 asubuhi, Mh Zitto Kabwe kupitia simu yake ya kiganjani namba +2557547...50 alipokea simu kutoka kwa xxxxxxx mwenye namba +255717...473ambaye ni afisa Usalama wa Taifa anayefanya kazi ikulu hivi sasa. Alijitambulisha kuwa yeye ni Usalama wa Taifa ametumwa na mkuu wake wa kazi aje aongee na Zitto, Maelezo ya msingi katika simu hii ilikuwa ni bwana xxxxxxx kuomba miadi ya kuonana kutokana na agizo la mkuu wake wa kazi.

Siku sita baadae yaani Jumatatu ya tarehe 23/6/2008 saa 07:52 asubuhi, Zitto alipigiwa tena simu na xxxxxxx akimkumbusha maongezi yao waliyo fanya siku 6 zilizopita na kumuomba siku hiyo jioni waonane, ingawa Zitto alionekana kusita kidogo lakini baadae alikubali, Walikubaliana wakutane Sea Cliff Hotel, ilipofika jioni ya siku hiyo Zitto akiwa na marafiki zake wawili Omar Lyasa na Abdalah Said walifika Sea Cliff Hotel wakaketi na kuagiza vinywaji, Baada ya kama dakika kumi hivi Zitto alipokea simu ikimuelekeza alipo bwana xxxxxxx kisha Zitto akawaambia marafiki zake wamsubiri kidogo, akaondoka kuelekea aliko elekezwa…..

Mashariki mwa lango kuu la kuingilia Sea Cliff Hotel mita kama tatu tu kuna mlango mdogo unaoelekea kwenye vyumba maalumu (VIP), chumba namba 8 ndicho Zitto alichokuwa anaelekezwa kwa simu kuingia, chumba hiki kina meza moja na sofa zilizo zunguka meza ile zenye uwezo wakukaliwa na watu watano hadi sita, Ndani ya chumba kile Zitto anakutana na watu watatu ambao ni Steven Wasira, xxxxxxx na Abdalla Punja.

Mazungumzo yao ndani ya chumba hiki yalianza maramoja, akianza Mr xxxxxxx kueleza sababu za wao kumuita Zitto, kikubwa ilikuwa ni “bwana Zitto, serikali (ikulu) inakutaka uache kuibana na kuishurutisha hasa kwa hili suala la Buzwagi”. Tunaomba kujua shida yako kubwa ni nini?” xxxxxxx alihoji, Katika majibu yake Zitto anajibu, “Mimi napigania haki za watanzania, nimechaguliwa na wanakigoma na watanzania wameniamini ni wawakilishe hivyo”, Lakini mashambulizi ya ushawishi yalipozidi Zitto alilegeza msimamo wake.

Katika kikao hiki kilichochukua masaa mawili, Zitto anaonekana kusita sana na anaomba apewe muda akafikirie aliyoitiwa, wote wanaafiki na kukubali ombi la Zitto na kikao kinaahirishwa.

Siku tatu tu baada ya kikao cha Hotel ya Sea Cliff, yaani tarehe 27/6/2008 Zitto anakutana na Naibu Mkurugenzi wa TISS Ndugu Jack Zoka jijini Arusha, hiki sio kikao chao maalumu bali wamekutana kwa mara ya kwanza wote wakiwa kwenye shughuli za kitaifa, Katika mazungumzo yao wanaonekana ni watu wanaofahamiana japo si kwa undani, Baada ya maongezi ya dakika kadhaa wakiwa wamesimama, Mr Zoka alimuuliza “Vipi vijana wangu walikupa ujumbe, umefikia wapi?” Zitto aliitikia kwa kucheka na kusema “yap nipo tayari, lakini nihakikishieni usalama wangu” Katika maongezi haya, Zoka anasikika akisema “Ondoa shaka” Kisha Mr Zoka anamuagiza Zitto kuwa kesho kutwa yake aende kwa Charles Kimei (Mkurugenzi CRDB Benki) pale Makao makuu, atayakuta maagizo yake huko.

Tarehe 30/6/2008 majira ya saa 12:22 za alasiri, Zitto akiwa ameongozana na kijana mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Rajabu Abdala anaingia eneo la CRDB Benki mtaa wa Azikiwe, na kwenda moja kwamoja kuonana na Bw Kimei, baada ya salamu haikuchukua muda mrefu, Zitto akapelekwa katika moja ya vyumba maalumu vya bank hiyo kwenye jengo hilohilo la Azikiwe, baada ya kufika katika chumba hicho Zitto alihamaki kuwakuta watu wawili katika chumba hicho, mmoja alikuwa ni mfanyakazi wa bank hiyo aliyetambuliwa kwa jina la Maselina K. Kombe na mwingine hakuwa mgeni machoni mwa Zitto, alikuwa ni xxxxxxx yule wa TISS waliyekuwa naye kwenye kikao cha awali kule Sea Cliff Hotel wiki chache zilizopita, Zitto alikabidhiwa Briefcase nyekundu iliyokuwa imesheheni pesa halali za kitanzania kiasi cha Shilingi milioni 250.

Wakati hayo yakitendeka yule kijana aliyekuja na Zitto alikuwa kwenye gari aina ya Toyota Mark 11 No T 134 AAB yenye rangi nyeupe na vioo vyeusi (Tinted). Baada ya makabidhiano yaliyochukua kama dakika 10 tu, Mr xxxxxxx alimwambia Zitto, “tunataka utulivu, mengi mazuri yanakuja utafurahia kijana,” Na kisha Zitto akatoka na begi lake (Briefcase) na kuingia nalo katiga gari ile na kutokomea.

Uchunguzi umeonyesha kuwa pesa ile aliyokabidhiwa ndugu Zitto, ilitoka katika akaunti Namba 0J56708968923 yenye jina la Shani Maya, ambapo inaonyesha kuwa akaunti hii ilifunguliwa CRDB tawi la azikiwe tarehe 25/6/2008 saa 10:14 asubuhi, kisha tarehe 27/6/2008 iliingizwa kiasi cha pesa za kitanzania milioni 400. Na tarehe 30/6/2008 pesa hizo zilitolewa zote na akaunti hii ilifungwa. Madhumuni ya pesa hii kutoka CRDB kwenda kwa Zitto yanathibitishwa na kikao cha 23/6/2008 pale Hotel ya Sea Cliff kuwa ni kupunguza kasi ya Zitto kuibana serikali hasa anapo kuwa bungeni. Na kweli kasi yake iliyozoeleka kwenye kuibana serikali akiwa bungeni ikapungua na kuweka msingi wa ujenzi wa mashaka juu ya mwenendo wake wa kibunge.


SEHEMU YA PILI 2009

Mnamo Jumatatu ya tarehe 30/11/2009 saa 04:30 asuhuhi wakati wa maandalizi ya uchaguzi wa mkuu wa 2010, idara ya ujasusi ya ccm ilikutana kwa siri pale Moven Pick/SERENA Hotel, ndani ya idara hii wakiwamo Jack Zoka, Wilson Mkama, Kingunge Ngombale Mwiru, Jakaya Kikwete, Nape Nnauye, Fred Kimati, Steven Wasira, xxxxxxx, Martin Palakyo, Mwigulu Nchemba, Ahamed Msangi na Abdalla Punja. Katika kikao hiki yalijadiliwa mengi sana, lakini kubwa lilikuwa nikukabiliana na vyama vya upinzani hususani CHADEMA, zilipangwa mbinu nyingi sana juu ya Chadema, Mbinu hizo ni kama ifuatavyo:

Kuwanunua wagombea ubunge na Udiwani (Mtakumbuka wagombea wetu kadhaa walikuja kununuliwa na chama kina ushahidi kwenye hili).

Kuwanunua VIONGOZI wajuu wa CHADEMA.
Kutumia TISS kutisha wagombea na wanachama wa Chadema (Hii ilikuwa ni kuwakamata au kuvuruga mikutano).
Kuwaua baadhi ya wafuasi wa Chadema, viongozi wa Chadema na wabunge.

Lakini walitilia mkazo zaidi njia ya kwanza ,ya pili na ya tatu ambapo kikao kilijiridhisha kuwa mmoja wa VIONGOZI wa Chadema ambae ni Zitto Kabwe ni mtu wao ambaye wamesha anza kumtumia, kikubwa liandaliwe fungu tu kwa ajili yakuanza mikakati yao, Waliafikiana mambo mengi kwaajili ya uchaguzi wa mwaka ambao ungefuata, na wakakubaliana mambo kadhaa ambayo walimuagiza Mr Zoka akamwambie Zitto nini cha kufanya ili kupunguza nguvu ya upinzani.

Kwa upande wake Zoka alikiambia kikao kuwa Zitto amemthibitishia kuwa yeye anawafuasi wakutosha ndani ya chama ambapo watamuunga mkono kwa lolote hivyo kikubwa ni pesa tu. Lakini kwanza kikao hicho kilimtaka Mr Zoka amwambie Zitto kuwa taarifa zote zinazoihusu Chadema na za kila vikao vya ndani vya chama zinatakiwa pia ziifikie timu hiyo ya kijasusi ya ccm, pili walitaka Zitto apunguze ushiriki katika majukwaa ya chama na shughuli nyingine za chama. Baada ya kikao sasa ulikuwa ni utekelezwaji wa maadhimio yao.

Zoezi la kikao cha tarehe 30/11/2009 linaonyesha kuzaa matunda hasa baada ya kubainika mawasiliano ya karibu sana kati ya Zitto na Jack Zoka, Kwamfano: Jumamosi ya tarehe 6/12/2009 saa 03:43 asubuhi Zoka kupitia namba yake ya simu +255756....35 alimpigia simu Zitto kupitia simu yake ya kiganjani ambayo ni +2557547...50, wakati wa mawasiliano yao haya ya simu Zitto alikuwa Tabata na maongezi yao yalihusu kikao cha 30/11/2009 na kile walichoamua timu ya kijasusi ya chama (ccm) na matakwa yao kwa Zitto. Ndani ya maongezi yao yaliyochukua dakika 68, Zitto anasema, “Mr kazi hii ni nzito, vipi mmeongeza hela? Isije kuwa kama ile ya mwaka jana.” Anajibiwa na Zoka kuwa “ondoa shaka una dili na Jamhuri, hela sio tatizo”

Lakini zaidi Zitto anamshauri bwana Zoka kuwa utaratibu wa uchukuaji wa pesa ubadilike, “Mr Jack ile staili ya uchukuaji pesa kule CRDB mwaka jana ilinitisha kidogo halafu hii isije ikabumburuka vyombo vya habari vipo makini kweli sasa hivi” Anajibiwa na Bwana Zoka kuwa “Tunazo njia nyingi sana ambazo si TAKUKURU wala polisi wanaoweza kubaini, tusikilize sisi, tutakacho kuambia ujue ni salama, Haya Mr (Zitto) wewe unayajua mazingira vizuri katika nchi moja ya Ulaya?, au unaweza kutafuta mtu unae mwamini huko ili atumiwe yeye hiyo pesa na awe wa kuaminika ili tumtumie kwa vipindi hivi vyote, kisha uifuate huko au uangalie mwenyewe njia sahihi ya kuichukua huko” Suala la kumpata mtu Ulaya lilionekana kama zito kidogo kwa Zitto, kwani aliomba wawasiliane kesho yake ili awe na jibu la uhakika.

Tarehe hiyo hiyo 6/12/2009 ya Jumamosi saaa 23:05 usiku, Zitto kupitia simu yake ya mkononi namba +255754....50, alipiga namba +49157.....853, kimaongezi walionekana ni watu wanafahamiana sana, alikuwa anaongea na mwanamke ,waliongea mengi lakini kubwa lilikuwa ni Zitto kuomba kupitisha hela yake kwenye akaunti ya huyu mtu. Mwanamke huyu alihoji kama pesa hiyo ni nyingi na haina madhara? Lakini alijbiwa sio nyingi na haina madhara kwakuwa inatoka serikalini na chama tawala, Mwanamke huyo alizidi kuhoji zaidi, “sasa vyombo vya dola vya hapa Berlin vikinihoji nitasema nimepata wapi?” Anajibiwa kuwa “Darling huniamini? Nimesoma na wewe na nimefanya kazi na wewe, lakini huniamini? Utasema umelipwa nchini Tanzania kwa kazi yako”, kisha katika maongezi ya hapa na pale dada akakubali na baada ya dakika kumi akamtumia akaunti namba 033B 33093101 Berliner Bank German.

Baada ya kuipata akaunti hii Zitto hakuchelewa, akaipeleka kwa Mr Zoka kwa njia ya ujumbe wa maandishi (sms), baada ya dakika 5, Zoka akampigia simu Zitto kupitia namba +255756...535 nae Zitto akapokea kupitia namba +255754....50, na mazungumzo yao yaliyochukua dakika 6 yakaendelea, Zoka aliuliza swali kuwa “Mwenye akaunti hiyo huko Ujerumani unamwamini na unamjua vema?” Majibu ya Zitto yalikuwa “Ondoa shaka Mr Jack nafanya kazi ya hatari na wewe , siwezi kukuangusha au kujiangamiza, huyu mtu nimesoma nae na ninamfahamu in and out” Zoka akajibu “ok”.

Jumatano ya tarehe 16/12/2009 majira ya saa 13:12 za mchana kwa Ujerumani akaunti namba 033B 33093101 Berliner Bank, ziliingizwa dola za kimarekani 266,000 pesa hizi katika uchunguzi zimebainika kuwa zilitoka Tanzania katika Benki ya NMB tawi la NMB House jiji Dar katika akaunti namba 2231604658 yenye jina la TSA, hii ni moja ya akaunti za siri za TISS, ambapo wao ndio huzisimamia akaunti zao zote kwa kutumia mawakala (TISS) walio ndani ya benki hiyo.

Kujiridhisha kuwa pesa hiyo ilifika Ujerumani, kunabainishwa na mawasiliano ya barua pepe kati ya Zitto Kabwe na yule mwanamke wa kijerumani aliyemtumia akaunti ya benki, anafahamika kwa jina la Andrea Cordes, mawasiliano yaliyofanywa tarehe 17 alhamisi saa 20:34 usiku ambapo Andrea kupitia barua pepe yake acodes@gmail.com anamwandikia Zitto kupitia barua pepe ya Zitto iitwayo zittokabwe@gmail.com , Andea anasema “Hey sweet, mzigo yako imefika, can we talk?” Ujumbe huu unajibiwa na Zitto saa 21:03 usiku huo kwakusema, “I’m so sorry my darling, nimechelewa kukujibu, I will call you soon”

Saa 23:23 Zitto Kabwe kupitia simu yake ya kiganjani namba +255754....50, alimpiga Andrea Codes kupitia namba +491573...853, akimweleza kuwa anashukuru kwa mzigo kumfikia, lakini anataka kumpa utaratibu wa kuichukua hiyo pesa, ambapo alimweleza kuwa atakuwa anaichukua kidogo kidogo kila mwezi kwa njia ya Western Union kuanzia dola 20,000 hadi dola 50,000, wakati huo Andea Codes atakula kamisheni ya dola 25,000.

Uchunguzi wa ndani umebaini pesa hiyo ilitumwa kwa Zitto ndani ya miezi 8 kwa vipindi tofauti kupitia Western Union kama alivyoomba, na alikuwa anachukulia maeneo tofauti tofauti hapa jijini Dar, vilevile uchunguzi umebaini kuwa mwanamke huyu ni Mjerumani aliyewahi kuishi Tanzania na amezaa mtoto mmoja hapa Tanzania, Mwanamke huyu anaitwa Andrea Cordes, anaishi Mechernich Ujerumani, mtaa namba 134, nyumba namba 141, anafanya kazi UN Women Nationales Komitee Deutschland e.V. Shirika ambalo shughuli zake huendeshea pia Tanzania. Katika uchunguzi zaidi imebainika kuwa akaunti aliyomtumia Zitto ni ya kwake binafsi, katika ushahidi tuliobaini kupitia benki iitwayo Berliner Bank yenye Code No Hardenbergstraße 32, 10623 iliyopo mjini Berlin nchini Ujerumani.


SEHEMU YA TATU 2010
Uhusiano usio wa kawaida na wa karibu wa Zitto na viongozi wa ccm, serikali na wale wa Usalama wa Taifa uliendelea kushamiri hasa kipindi cha kampeni na kipindi cha uchaguzi mkuu wa 2010, Mfano tarehe 7/9/2010 siku ya jumanne saa 11:21 asubuhi, Ahmed Msangi kupitia namba yake ya simu ya kiganjani +2557842....4, alimpigia Zitto kupitia simu ya kiganjani namba +255754....50 waliongea mambo mengi japo kwa muda mfupi, na jambo kubwa lilikuwa ni “vipi kuna kipya ndani ya Chadema?” Zitto alijibu “yapo mengi lakini hayana impact kwa ccm” Msangi anajibu “Ok mr nikutakie siku njema”

Lakini mawasiliano ya simu yaliyochukua mda mrefu zaidi yalikuwa kati ya Zitto na Zoka yaliyofanywa tarehe 10/9/2010 siku ya ijumaa saa 07:04 jioni na mazungumzo yao yalichukua dakika 71, Mazungumzo haya yalifanywa wakati huo Zitto akiwa katika hoteli ya Blue Pearl Ubungo, Mr Zoka alitaka kujua mambo kadhaa kuelekea Uchaguzi mkuu, kwanza alimuuliza “Mr Zitto umejiandaaje, una timu ya kazi?” Zitto akajibu “nipo fiti kiakili na kimwili na nina timu ya kutosha, ondoa shaka juu yangu, kama ipo hiyo hela tumeni tu Ujerumani kwenye ile akaunti, na ningeomba kukutana na mwenyeti wenu (rais JK)” Zoka lijibu “hilo halina tabu nitalifikisha sehemu husika bwana Zitto”,

Uchunguzi umebainisha kuwa akaunti namba 033B 33093101 Berliner Bank ya German iliendelea kuingizwa pesa kwa nyakati tofauti kutoka Tanzania kupitia NMB akaunti namba 2231604658 yenye jina la TSA ambayo ni moja ya akaunti za siri za .........

............................................

ITAENDELEA KESHO,



HUTAKI UNAACHA!!!!!


========================
KAULI YA ZITTO - Oktoba 26, 2013:
Wana JF, kuna uzi umewekwa hapa na member anajiita Jason Bourne ambao unarusha shutuma zisizo na ushahidi wowote (maneno ya kuungaunga) dhidi yangu.

Hiki kinachoitwa uchunguzi ni hekaya ya kutungwa ambayo haina kichwa wala miguu na ninashangaa ni kwanini inaweza hata kufikiriwa kuwekwa hapa JF maana sheria za JF zinahitaji mtu aje na ushahidi kwa tuhuma nzito kama hizi.

Moja, Kuonyesha kuwa hii ni hadithi wanaongea mambo ya Buzwagi Juni 2008 wakati Taarifa ya Kamati ya Bomani iliwasilishwa Bungeni mapema kabla ya hapo. Buzwagi ni suala la mwaka 2007 na hizo hadithi zote za kutungwa wala haziendani na hali halisi.

Pili, Hekaya hii inataja namba za simu ambazo wala sijawahi kuwa nazo katika maisha yangu na hata pale walipopatia baadhi ya namba wameandika mambo ya uongo kabisa. Inasikitisha wana JF hata hawahoji hili.

Tatu, hizo Benki zinazotajwa wangeweka angalau bank statements basi kama ushahidi (mimi nawaruhusu kama wanao ushahidi huo badala ya kuchafua majina ya watu kwa nia zao chafu). Katika maisha yangu yote sijawahi kuwa na account iliyofikia kiwango kinachotajwa na wala sijawahi kuwa na account kupitia kwa mtu yeyote. Waje na ushahidi ili tuweze kujadili kitu chenye tija.

Nne, Benki za Ujerumani zinazotajwa ni uwongo mtupu, maana sijawahi kuwa na account huko. Wasiishie kutaja akaunti, walete ushaidi usio wa maneno.

Tano, mbaya sana wanataja watu wasiohusika na masuala haya kwa kuwachafulia majina na taasisi wanazofanyia kazi. Huyu dada Andrea Cordes masikini ni mdada wa watu innocent anaingizwa kwenye ujinga kama huu na hata sehemu anayofanyia kazi. Hii ni mbaya sana. Naomba JF isiruhusu mambo kama haya. Maadui zangu kisiasa wapambane na mimi wasionee watu wasio na hatia!

Moderators na administrators wa JF, msiruhusu hekaya kama hizi kuharibu jukwaa. Naomba tuanzishe jukwaa la watunga hadithi ili tuwape fursa ya kuandika hadithi kama hizi!

Zitto

==========
JamiiForums imemtaka mwanzisha hoja kuthibitisha kama taarifa hii kaitoa Makao Makuu ya CHADEMA lakini hakuweza kuthibitisha; uongozi wa CHADEMA ulikana kumpa yeyote habari hii na kudai kuwa kama chama jambo lolote ambalo kinataka lifahamike kwa umma hutumia akaunti za viongozi wa chama au ya Kurugenzi ya Habari. Hivyo basi, hoja hii haitaruhusiwia kuendelea JF.
 
Hizi ni distractions ili watu wasizungumzie zile ngumi za jana na hoja za msingi kuhusu governance ndani ya chadema? Au ni kupoteza interest ya watu kuhusu ukaguzi wa vyama?
Mbona mnahangaika?
 
Mnahangaika sana kuwagombanisha viongozi wa chadema. Ninachotaka kuwaambia kuliko kupoteza muda wenu ni heli muijenge CCM yenu inayopoteza mvuto kila siku. CHADEMA imeshakabidhiwa kwa wananchi na sasa mabadiliko ndiyo wananayotamani wananchi. Viongozi wa chadema wapo makini kwa kila uzushi utaowekwa hapa jamvini. Hivi namimi nikikaa nyumbani kwenye laptop yangu nikiamua kuitumia vizuri micro soft word nakuandika kitu kama hicho halafu nikaipa jina la ripoti itajenga maana gani. Kama kweli ulikuwa unajiamini kwanini usingeweka nakala ya hiyo ripoti hapa jamvini. Magamba kweli mmechanganyikiwa!!!
 
Hii ni riwaya ya upelelezi? Can you publish the book please?
nami naiona hivyo pia lakini ukurudi nyuma na kuangalia kile Rais wa Ufaransa pamoja na Angela Markel wa Ujerumani wanachobishania na Marekani kuingilia mawasiliano yao sishangai.

 
Uwiiiiiiiii....nani wakutuvusha?,nani wa kutusaidia?,nani wa kuondoa uovu huu ktk Tanganyika yetu? nani wa tumuamini? Oooooh! I CANT CARRY IT! Nani wa kumuamini??
 
Zitto mwenyewe anaufuatilia huu uzi anajipanga jinsi ya kukwepa hii kashfa lakini hawezi kuipangua hii. Hata kama chadema wasingefanya upelelezi, kuna clue nyingi sana zinazomwonyesha zitto yuko CDM kwa kazi maalumu.

Kwanza ukaribu wake na top members wa CCM unatia shaka kubwa sana, Mungu hawezi kuwa na urafina na shetani hata kama ni democrasia.

Pili haiwezekani wanachama wote wa CCM wawe nyuma ya Zitto kumtetea kila linapotokea jambo.

Tatu haiwezekani mashambulizi yote yanayotoka kwa CCM na mamluki wao kwenda CDM yaelekezwe kwa viongozi wote wa juu wa CDM pamoja na wabunge wao kasoro ZITTO. ??????

Haiwezekani Zitto apunguze kasi yake aliyokuwa nayo bungeni tokea suala la buzwagi na sasa hata mikutano ya kampeni ya kueneza chama M4C hashiriki akidai ametingwa na majukumu ya kibunge

Haiwezekani Mgombea uraisi wa CCM mwaka 2010 azunguke Tanzania nzima katika kila jimbo akijinadi yeye na mgombea wa ubunge wa CCM kasoro jimbo la ZITTO ambako aliona picha itaungua maana itabidi ajinadi yeye na mgombea wa CDM bwana zitto

Zipo Clues nyingi sana ambazo mtu yeyote yule akizi-reason atajua Zitto ni mamluki. Kwa taarifa hii nimezidi kuipenda CHADEMA, kwa kujionyesha ni chama tofauti na vingine, inajiendesha kisasa. Kwa kuwa washabiki wa CDM hapa chuoni nilipo ni wengi na sio wote wana access ya computer, naenda kuiprint hii ripoti na kuibandika ili kila mshabiki wa CDM ajue kuwa zito sio mwenzetu. Siku akipanda jukwaani ni kupigwa mawe tu. Tamaa mbele mauti nyuma
 
Mkuu Jason bourne kwa upande wangu Zitto nilishamwondoa katika list ya watu makini siku nyingi sihitaji bandiko hili ili kuhalalisha fikra zangu dhidi ya huyu Bwana mdogo.Anatumika sana angalia anajifanya kuvalia njuga mabilioni wakati yeye akichunguzwa habaki kitu.


Mkuu wangu umewahi kujiuliza ni kwanini kampeni za mwaka 2010 Kikwete hakukanyaga jimbo lake la uchaguzi ????????? !!!!!!!.
 
Last edited by a moderator:
Hizi ni distractions ili watu wasizungumzie zile ngumi za jana na hoja za msingi kuhusu governance ndani ya chadema? Au ni kupoteza interest ya watu kuhusu ukaguzi wa vyama?
Mbona mnahangaika?
Mwali,

Ni akina nani?Wataje mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Hivi! Ngoja! Are you serious? Inawezekana kweli, mapesa mengi namna hiyo? Na Kimei- professional banker naye ni kiazi kiasi hicho? Hii Nchi imeoza kiasi hocho? Haiwezekani Bwana, weewe unaandika hadithi za kubuni. Zitto anaweza akawa mnafikikwa kipindi kirefu namna hio? Na hii repoti imetolewa lini! IMETOLEWA LINI au TUSEME CHADEMA WAMEJUA LINI NA WAMEFANYA NINI!


NIMEKASIRIKASANA.....na kwa ajili hii Zito anafahamu jinsi gani wezi wa hela zetu wanavyozipeleka Uswisi- haunted by the guilty- he is now out in the open-------pengine hadithi yako ni kweli....Mungu nisaidie nisvumilie nisimpige mtu!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom