Ripoti ya Mauaji ya Mwangosi yatoboa siri

Medical Dictionary

JF-Expert Member
Mar 12, 2012
1,060
309
KAMATI iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, kuchunguza mauaji ya mwanahabari, Daudi Mwangosi, imekamilisha kazi yake, huku ikitoa siri nzito.

Siri hiyo ambayo huenda ikasababisha baadhi ya vigogo wa polisi kupoteza kazi, itawekwa hadharani katika mkutano wa waandishi wa habari Jumanne ijayo, mbele ya kamati hiyo na Waziri Nchimbi mwenyewe.

Tayari kamati hiyo iliyofanya kazi kwa siku 30, imekabidhi ripoti yake kwa Dk. Nchimbi jana, kumpa fursa ya kuipitia kabla ya ukweli kuhusu mauaji hayo kuwekwa hadharani.

Ripoti hiyo ilikabidhiwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Theophil Makunga ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa Mwananchi Communication.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Makunga alisema kamati yake ilifanya ziara mkoani Iringa na kufanya mahojiano na wadau mbalimbali mkoani humo na jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo jana, Dk. Nchimbi kupitia taarifa iliyosambazwa kwa vyombo vya habari, ameahidi kuwa yeye pamoja na kamati hiyo, watafanya kikao na waandishi wa habari kueleza kilichobainishwa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyosainiwa na Msemaji wa Wizara hiyo, Isaac Nantanga, Nchimbi mbali na kupokea ripoti hiyo aliishukuru kamati kwa kazi waliyoifanya.

Ripoti ya kamati hiyo imekabidhiwa ikiwa ni takribani zaidi ya mwezi mmoja tangu mwanahabari huyo alipouawa kinyama na polisi Septemba 2, mwaka huu katika Kijiji cha Nyololo wilayani Mufindi wakati polisi walipovamia na kutawanya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliokuwa wakifungua tawi la chama hicho katika kijiji hicho.

Mazingira ya kifo cha Mwangosi yamesababisha uhasama mkubwa baina ya Jeshi la Polisi na wanahabari ambao katika baadhi ya mikoa wameamua kususia kazi za jeshi hilo.

Mgogoro huo ulisababisha Nchimbi afikie hatua ya kuunda kamati hiyo baada ya siku tatu tangu kutokea kwa mauaji hayo ili kubaini utata wa kifo hicho.

Kamati hiyo yenye watu watano iliwashirikisha Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu, Steven Ihema, Makunga na Ofisa wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Pili Mtambalike.

Wengine ni mtaalamu milipuko kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kanali Wema Wapo pamoja na Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Isaya Mungulu.

Dk. Nchimbi aliiagiza kamati hiyo kufanya kazi yake kwa siku 30 na kukabidhi ripoti kwake na kueleza umma chanzo cha tukio hilo.

Kamati hiyo ilipewa hadidu za rejea sita huku Nchimbi akiahidi kwamba askari watakaobainika kuhusika na tukio hilo, watachukuliwa hatua za kinidhamu.

Hadidu za rejea ni pamoja na maswali kadhaa kuhusu chanzo cha kifo cha Mwangosi.

Nyingine ni ile inayotokana na kuwepo kwa taarifa kwamba kuna uhasama kati ya Jeshi la Polisi na waandishi wa habari wa Mkoa wa Iringa na kama kuna waandishi watatu wa habari wanatafutwa na
polisi.

Hadidu nyingine ni kujibu maswali kama nguvu iliyotumika katika kukabiliana na tukio lile ilikuwa kubwa kupita kiasi na je, kuna taratibu za kukata rufaa kwa chama kinachodhani hakikutendewa haki na Jeshi la Polisi?

Pia aliiagiza kamati hiyo ichunguze kama kuna tatizo kwa vyama vya siasa kwamba, havina mahusiano mazuri na Jeshi la Polisi.

Hata baada ya kamati hiyo kuundwa, waandishi wa habari katika baadhi ya mikoa, ikiwamo Dar es Salaam waliongoza maandamano ya kulaani mauaji ya mwanahabari mwenzao.
Source:tanzania daima
 
Kamati ya Mwangosi yamaliza kazi

KAMATI iliyokuwa ikichunguza vurugu zilizotokea mkoani Iringa na kusababisha kifo cha aliyekuwa Mwandishi wa Kituo Cha Televisheni cha Channel Ten, David Mwangosi imekabidhi ripoti yake kwa Waziri wa Mambo ya Ndani Dk Emaanuel Nchimbi.

Katika vurugu hizo ambazo zilizotokea Kijiji cha Nyololo wilayani Mufindi Septemba 2 mwaka huu, kati ya Polisi na wafuasi wa Chadema waliokuwa wakifungua tawi la Chama hicho baadhi ya watu walijeruhiwa akiwemo askari wa jeshi hilo.

Taarifa iliyotolewa jana na Msemaji wa Wizara hiyo Isaac Nantanga ilisema kamati hiyo imekamilisha kazi iliyopewa na hivyo kusubibili kikao cha kamati hiyo na waziri wiki ijayo.

“Waziri ameishukuru kamati hiyo kwa kazi walioifanya na Jumanne (kesho kutwa) atafanya kikao na waandishi wa habari” alisema Nantanga.

Wakati akiitangaza kamati hiyo Dk Nchimbi aliitaka kujibu maswali sita ambayo yalikuwa hanaya majibu kutokana na tukio hilo.

“Tuna maswali sita ambayo mimi sina majibu yake. Swali la kwanza tunataka kujua nini chanzo cha kifo cha Daudi? Pili tujue ni kweli kwamba kuna uhasama kati ya polisi na waandishi Iringa?” alisema Dk Nchimbi

Aliongeza: “Tatu tujue kama ni kweli kuna orodha ya waandishi watatu wa kushughulikiwa Iringa? Nne kama nguvu zilizotumika zilistahili? Tano kama kuna utaratibu wa vyama vya siasa kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa polisi? Mwisho kujua uhusiano wa Jeshi la Polisi na vyama vya siasa ukoje?”

Dk Nchimbi alisema, sheria lazima zifuatwe kwani nchi ikiingia kwenye matatizo, Serikali haitaweza kuwaeleza wananchi kwamba ndicho kitu kinachotakiwa... “Hatutaki tuwe na vita vya wenyewe kwa wenyewe.”

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Theophil Makunga alisema kamati yake ilifanya ziara katika mikoa ya Iringa na Dar es Salaam na kufanya mahojiano na wadau mbalimbali.

Alisema wakati wa zoezi hilo walizingatia yale waliyoelezwa na Dk Nchimbi ikiwa ni kufanya kazi kwa kuweka mbele maslahi ya taifa.
“Alitutaka kufanya kazi bila kuegemea upande mmoja wa Serikali ama chama na tumejibu maswali yote yaliyokuwa katika habibu za rejea alizotupa bila kuacha hata moja,” alisema Makunga.

Aliongeza licha ya kujibu habibu hizo za rejea pia tumetoa mapendekezo ambayo kama yatatekelezwa hakutatokea tukio kama hilo.

Alipotakiwa kueleza kilichomo ndani ya ripoti hiyo alisema hawezi na kutaka kusubiri Jumanne ambapo Waziri na Kamati nzima itazungumza na waandishi wa habari.

Kamati hiyo ilikuwa watu watano ambayo ilikukuwa chini ya Mwenyekiti , Jaji mstaafu Steven Ihema, mwakilishi wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Theophil Makunga,

Wajumbe wengine walikuwa ni mwakilishi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Pili Mtambalike, mtaalamu wa milipuko kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kanali Wema Wapo na Naibu Kamishina wa Polisi (DCP), Isaya Mngulu.

MY TAKE:

Nini uhalali wa matokeo ya uchunguzi huu? Ikiwa Tume sio halali, je matokeo yatakuwa halali?
What If Kamati ikawa imependekeza Waziri ajiuzulu? Just thinking aloud
 
Jumanne Nchimbi ataweka kila kitu hadharani, tukae mkao wa kusubiri atangaze rasmi kujiuzulu uwaziri
 
Hii ni kama kamati ya harusi. Haina meno au uhalali wa kisheria.
Huu ni upuuzi wa watu kulinda vibarua vyao kwa gharama za maisha ya wananchi.

Lawama za pekee zimwendee Theophil Makunga. Yeye akiwa mhariri mwanadamizi hakupaswa kuingia katika uchunguzi wa kilaghai dhidi ya mauaji ya mwenzao. Tatizo si uhasama wa Polisi na raia, ni ukikukwaji na uvunjaji wa haki za binadamu.
Tatizo ni mauaji ya Mwangosi (R.I.P) akiwa kazini tena kwa silaha nzito.

Makunga alipaswa kuelewa kuwa hakuna uhasama wa waandishi wa habari na Polisi na kama upo kifo cha Mwangosi hakipaswi kutumiwa kama mtaji wa kisiasa au kama funiko la uchafu.

Kwa hili Makunga ameusaliti umma na taaluma ya uandishi wa habari. Haiwezekani ampelekea taarifa Nchimbi ambaye katika kesi hii akiwa waziri wa mambo ya ndani anapaswa kwanza ajiuzulu ili apishe uchunguzi halali.

Ninahakika Theophil Makunga hakuongozwa na weledi wa taaluma, pengine allowance za kuzunguka mikoani zilimvutia zaidi kuliko haki na maisha ya waandishi wa habari wa Tanzania.

Ninaipuuza taarifa hii kwasababu Nchimbi anapaswa kwanza ajiuzulu, iundwe tume yenye uhalali wa kisheria ikiwa huru.
Hata hivyo hakuna shoka linalokata bila mpini na hapa mpini ni Theophili Makunga.

Jamii ya wapenda amani na Waandishi wa habari iachane na taarifa hii na ijikite zaidi kumsuta, kumkemea, kumtenga Theophil Makunga kwa usaliti wa hali ya juu, ikiwa ni pamoja na kuidhalilisha taaluma ya habari nchini.

Theophil Makunga, wewe ni msaliti wa Mwangosi, taaluma na Watanzania.
 
Mkuu Nguruvi nakubaliana na wewe. Kitakachofanyika ni kufunika kombe na kumfanya mwanaharamu apite, sidhani kama kutakuwa na justice, aliyetoa order ya kuuawa kwa mwangosi hatafanywa kitu na huenda asitajwe, kama kuna mtu anadhani kutakuwa na justice kwenye hili basi yeye atakuwa si mtanzania.
 
Nyie kamati halali kwenu ni inayoundwa na Chadema tumieni akili msiendekeze mambo ya siasa kwenye kila kitu.
 
Nyie kamati halali kwenu ni inayoundwa na Chadema tumieni akili msiendekeze mambo ya siasa kwenye kila kitu.
Umesahau kuwa hii iliundwa kama tume halafu ikbainika haina nguvu za kisheria ndipo ikabatizwa jina la kamati. Hebu tupe uhalali na nguvu ya hii kamati kisheria. Itaoa matokeo gani unayodhani yana nguvu za kisheria.
Hapa tunajadili issue siyo politics kwahiyo tujikite huko.
 
Kamati haiwezi kupendekeza Nchimbi ajiuzulua, chezeiya per diems wewe. Kwanza ukiwa kwenye hizo kamati kila unachoongea na kuandika kinakuwa monitored. Ndo maana hata siku moja hutasikia mtu radical anawekwa kwenye kamati, na hata ukiingia kwa mafuriko bahati mbaya usishangae kuwepo ripoti mbili tofauti. Hii ndo bongo zaidi ya uijuavyo, hakuna mupya.
 
Kweli kabisa mkuu lkn binafsi huwa nachukizwa sana ninapoona mwongo anajiandaa kunidanganya anaandaa watu wakumsaidia kunidanganya anaanza kunidanganya ananilazimisha nimuamini eti kwasababu cheo chake na nafasi yake aliyeipata kwa njia isiyokua halali...Kama afanyavyo huyu nchimbi
 
Yaani nchimbi anayestahili kujiuzulu na kushitakiwa mahakamani na The Hague anakabidhibiwa report aangalie inapendekeza nini juu yake yeye na majambazi wenzake akina kamuhanda,mwema na Chagonja kisha waamue watakavyo then waendelee kuwa na uhalali wa kuiongoza hii nchi?
 
wewe unategemea nini kwenye hiyo repoti wakati mchimbi mwenyewe ni mtuhumiwa!
 
Mara ya kwanza iliitwa tume baada ya Tundu Lisu kwa niaba ya Chadema kusema haina nguvu ya kisheria na waziri hana mamlaka ya kuunda tume, ikabatizwa jina la kamati....huu ndio upuuzi wa kubebana, ilitakiwa waandishi washinikize tume huru ya kimahakama sio ujinga wa vitume vya kiuahkaji. Nchimbi kwenye hii kesi ni mtuhumiwa...halafu anapokea ripoti kweli mtaji wa ccm bado ni watu wenye uelewa mdogo na njaa.
 
Nimesoma hii post na kurudia mara tatu sijaona hiyo SIRI iliyotobolewa,,, labda wenzangu mnisaidie.

Hadi niione hiyo ripoti ndo nitaamini maana hawa magamba kwa manipulation ndio mabingwa, anything can be manipulated kwao achilia mbali ripoti ya Mwangosi
 
hata mimi nimeitafuta hiyo siri nzito bila mafanikio!
 
invisible lala aisee usidelete hizo post, zipe kama masaa sita basi na wewe......... aaaaghhhrrrrrrrr:doh::doh::doh::doh::doh::doh:
 
Nimesoma hii post na kurudia mara tatu sijaona hiyo SIRI iliyotobolewa,,, labda wenzangu mnisaidie.

Hadi niione hiyo ripoti ndo nitaamini maana hawa magamba kwa manipulation ndio mabingwa, anything can be manipulated kwao achilia mbali ripoti ya Mwangosi
ndio waandishi wetu wa habari hao
 
Back
Top Bottom