Ripoti ya Mauaji ya Mwangosi yatoboa siri

Ripoti ya Mauaji ya Mwangosi yatoboa siri

Kichwa habari na maudhui yake ni irrelevant! Nilitegemea kuwa siri imeelezwa ndani ya habari, badala yake ni porojo tu kuwa ripoti imekebidhiwa kwa waziri! Hii ndio siri?

ndio habari za pale mtaa wa manhattan,kinondoni manyanya, tunawaambia kila siku hawa jamaa wamepoteza mwelekeo wamebaki na taarifa za kuokoteza na za kupandikiza chuki.haya ndio habari zao hizi.
 
Gazeti letu la tz daima hili ndio limetufikisha hapa.mwenye akili atatafakari na kupata jibu ni habari ngapi amedanganywa.
 
Nimesoma hii post na kurudia mara tatu sijaona hiyo SIRI iliyotobolewa,,, labda wenzangu mnisaidie.

Hadi niione hiyo ripoti ndo nitaamini maana hawa magamba kwa manipulation ndio mabingwa, anything can be manipulated kwao achilia mbali ripoti ya Mwangosi
Nimesoma kutafuta hiyo SIRI iliyofichuliwa sikuiona.
 
Nyie kamati halali kwenu ni inayoundwa na Chadema tumieni akili msiendekeze mambo ya siasa kwenye kila kitu.
We ndo unatakiwa utumie akili aliyepanga mauaji na mwenye dhamana na wizara iliyoua anaunda Kamati na anapelekewa repoti hivi kwa akili yako hiyo ripoti itatoa majibu gani usiwe unakurupuka tu kuleta ushabiki jitahidi kuushughulisha ubongo wako.
 
Je unajitahidi kuuza gazeti lisilonunulika?

Habari haina siri yeyote iliyotobolewa bali siri iliyoendelea kufungiwa!!
 
I wish ripoti ituambie utumbo wa Mwangosi uliopelekwa MR Hotel ulipelekwa wapi
 
Best ripoti hii itachakachuliwa na hakuna yeyote atakayewajibishwa kwa mauaji ya Mwangosi. Utakuwa ni usanii kama ambavyo tulivyozoea toka kwa hii Serikali DHAIFU

Kamati haiwezi kupendekeza Nchimbi ajiuzulua, chezeiya per diems wewe. Kwanza ukiwa kwenye hizo kamati kila unachoongea na kuandika kinakuwa monitored. Ndo maana hata siku moja hutasikia mtu radical anawekwa kwenye kamati, na hata ukiingia kwa mafuriko bahati mbaya usishangae kuwepo ripoti mbili tofauti. Hii ndo bongo zaidi ya uijuavyo, hakuna mupya.
 
Back
Top Bottom