mkude kibwana
JF-Expert Member
- Oct 9, 2014
- 348
- 27
Naomba unifafanulie Mkuu, maana naona labda hili jambo sijalielewa vizuri. Hivi kama hizo pesa si za umma kwa nini serikali, CAG wanahusishwa na kwa nini limepewa nafasi ya kujadiliwa Bungeni? Na kwa nini nchi wafadhili wamesitisha msaada wa bajeti mpaka jambo hili litolewe ufafanuzi?
Usinchoshe mie weye! Toka mmemezeshwa huo ----- majibu mengi mshapewa lakini mmetia pamba masiko yenu hata mkieleweshwa hamuwezi kuelewa, sasa kwanini nirudie. Soma humu kwenye vinyuzi mnavyofatua kila sekunde utapata majibu.
Nawewe kama pesa ni za umma kwanini Mkurugenzi wa IPTL Bahruden Majida husishwe kwenye utiaji saini wa mkataba wa escrow??
Mwakani kuna tetesi kuwa Donors wanajiandaa kusitisha misaada ya kibajeti mpaka tuwape kijana mmoja awape mgongo! Kwenye hili sina wasiwasi maana najua mkuu utajitolea ili kuokoa jahazi.