Ripoti ya ESCROW yawasha moto

Ripoti ya ESCROW yawasha moto

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
1,016
Reaction score
2,195
kafulila.jpg

Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulilla

Dodoma. Ripoti ya uchunguzi katika akaunti ya escrow imeonekana kuipasua kichwa Serikali baada ya wabunge kuibana wakitaka ripoti hiyo iwasilishwe bungeni na kuwekwa wazi.

Hali hiyo ambayo imelifanya Bunge kupanga suala hilo lijadiliwe katika Kamati ya Uongozi, ilizua malumbano bungeni baada ya Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila kuomba mwongozo wa Spika.

Kafulila alisema ripoti hiyo ni ya haraka baada ya uchunguzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kukamilika.

Baada ya Kafulila kutoa hoja hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alisimama na kusema: "Ni kweli Waziri Mkuu alitoa maelekezo kwa Takukuru na CAG kufanya uchunguzi huo na kukabidhi ripoti kwake ili atoe taarifa bungeni."

Lukuvi alisema ukaguzi wa CAG bado unaendelea na utakamilika muda si mrefu kwa kuwa unahusisha mambo mengi.

Alisema itakapokabidhiwa, Waziri Mkuu ataiwasilisha kwa Spika kwa ajili ya utekelezaji. Waziri huyo alisema taarifa hizo mbili hazijakabidhiwa kwa Waziri Mkuu na akadokeza kuwa Takukuru ikimaliza uchunguzi wake inaweza kuchukua hatua yenyewe na taarifa inayosubiriwa na Bunge kwa sasa ni ya CAG.

Majibu hayo ya Lukuvi yalimnyanyua Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali akitumia Kanuni ya 68(1) na 64(1)(a) akidai kuwa taarifa inaliyotolewa na Waziri Lukuvi haina ukweli. "Nashangaa waziri anasimama na kusema hapa bungeni kwamba hii hoja si ya haraka wakati kuna matatizo mengi yanayohitaji fedha hapa nchini. Haiwezekani waziri anaongea blah blah hapa," alisema Machali.

Baada ya kauli hiyo, Lukuvi alinyanyuka tena na kusema: "Mimi hapa ndiye ninayetoa maneno ya Serikali hapa ndani, kama mbunge anasema ni blah blah basi anapingana na Serikali, kama nyie mnayo hiyo ripoti ileteni hapa tuijadili."

Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba naye alisimama na kusema ni lazima Bunge lifanye uamuzi. "Nakubali kuwa bado Serikali inachunguza na inaweza kuendelea kuchunguza kwa muda mrefu tu, lakini kupitia Bunge hili, lazima ifikie mahali sasa tuunde tume kuchunguza hili jambo ili liishe."

Baada ya mvutano huo, Ndugai alisema: "Suala la Kafulila tutalishughulikia kwenye Kamati ya Uongozi kwa kuwa kiti hiki hakina mamlaka."

Chanzo: Gazeti MWANANCHI
 
Hapo tumeshaliwa tena kama kawaida yamafisadi,huku Kafulila akipambana kwa kujitoa mhanga kwa taifa hili wananchi nao tupo kama hayatuhusu!
 
Kwa kasi yenu ya kufyatua viuzi inatupa mashaka sana kila sekunde kiuzi kinazaliwa humu jf kuhusu escrow na ripoti. Mmejipanga vizuri kuupotosha umma lakini ukweli utasimama milele fedha za escrow toka escrow inaanzishwa mpaka kufungwa kwake hazijawahi kuwa fedha za umma.
 
Hivi Lukuvi hajui kuwa kazi ya Mbunge ni kupingana na serikali pale anapoona kuna haja ya kufanya hivyo?

“Mimi hapa ndiye ninayetoa maneno ya Serikali hapa ndani, kama mbunge anasema ni blah blah basi anapingana na Serikali..."
 
tatizo la nchi hii ni sisi wananchi, hatuna umoja pale 2napoibiwa, hatuwez hata kushinikiza jambo serikali itekeleze,ha2wez kuweka tofauti ze2 za kisiasa pembeni ili kulifanyia kazi suala la kitaifa! hatuna uzalendo tena!! natamani angekuwepo nyerere na sera zake za kijamaa! zaman wakati nasoma historia ya tz nilikuwa nahisi mababu ze2 walikuwa wajinga kunyanyaswa na wakoloni ndani ya ardhi yao, kumbe sisi ndo wajinga tena wajinga zaidi 2naibiwa na watanzania wenzetu ndani ya nchi ye2, tumebaki kujadili ndani ya mitandao! wajukuu ze2 wata2dharau sana tena sana! WAJINGA wakubwa sisi.....(asha kum si matusi, mnisamehe)
 
Kwa kasi yenu ya kufyatua viuzi inatupa mashaka sana kila sekunde kiuzi kinazaliwa humu jf kuhusu escrow na ripoti. Mmejipanga vizuri kuupotosha umma lakini ukweli utasimama milele fedha za escrow toka escrow inaanzishwa mpaka kufungwa kwake hazijawahi kuwa fedha za umma.

kwanin mtu kama huyu alizaliwa tanzania?Kweli mtanzania unaweza kutoa kauli kama hiyo?una uhakika gani kama hyo charges zilikuwa halali?huoni kuwa suala hili kupigwa danadana kuna walakini ndani yake?kwa tuliyoyashuhudia ni ki2 gani kinashindikana nchi hii?ni kweli suala hilo halina uharaka?The government z trying 2 cover its own ass!
Inasikitisha wazalendo wanapopigania nchi and we r standing stl!
 
Ni kweli sio za umma, na nyie ambao mmekua mkitetea huu ujambazi hapa ni sehemu ya huo ujambazi kwahiyo wala hatuwashangai. Stupid MOFO!
 
We mbw@ wa tumbili, kama kutofautiana na tumbili kuna nifanya nisiwe mtanzania basi bora hivyo. We unauhakika gani kuwa charge hazikuwa sahihi? kwa uthibitusho gani ulionao wewe? Mwaka 2001 kesi ya IPTL na TANESCO kuhusu capacity charge ilikwisha ICSID na viwango vya capacity charge kushushwa kutoka $ 4.2 mil mpaka $ 2.6 mil na IPTL hata juzi wameendelea kusisitiza kuwa hawana kesi na TANESCO popote duniani.
Waacheni wataalam watengeneneze ripoti kwa utaalam wao siyo kwa kulazimisha kwenu, mkiona inachelewa tengenezeni ya kwenu mkaisome kwenye bunge lenu.
Watu washachoka na uzushi huu ndio maana hakuna anayestushwa na uzushi wenu msifanye wananchi hawana akili nyie wajinga.
 
Ni kweli sio za umma, na nyie ambao mmekua mkitetea huu ujambazi hapa ni sehemu ya huo ujambazi kwahiyo wala hatuwashangai. Stupid MOFO!

Mku@&ndu unajua ---- siyo za umma sasa unaharish@ nini? Ujambazi gani sasa, toka lini mtu akijiibia fedha zake? fedha za IPTL/PAP sasa imekuwaje wameziiba
 
Kuwatandikia wageni zuria jekundu na kuwapa viti vya mbele badala ya wazawa kwaa kisingizio cha uwekezaji plus 10% ni sawa na kunywea pombe vikombe vya hekaruni.Hole wenu siku watanzania watakapochoka.
 
Uchunguzi utaendelea hadi January 2016
 
mi naona hzo hela kuleni tu na nyingine mkaprint t-shirt, kofia, vtenge na kanga manake uchaguz umekarbia. mamburura wenu wataendelea kuwachagua. ila nicseme mburura manake wapo watu vyuo vikuu bado wanavaa kijan na wanakubaliana na madudu yao. they actually think by use their ........as....
 
Hapo tumeshaliwa tena kama kawaida yamafisadi,huku Kafulila akipambana kwa kujitoa mhanga kwa taifa hili wananchi nao tupo kama hayatuhusu!
Wanaotuwakilisha bungeni ndio waje juu mimi na wewe na yule ambao tuko nje ya bunge we can not do anyting. Ila moto inabidi uwake bungeni mpaka kieleweke,
 
INAWAPASUA VICHWA NYINYI TU MANDONDOCHA SERIKALI IMESHASEMA RIPOTI BADO, NYINYI NDIO MNAHAHA KUTWA KUCHWA KUBADILISHA VIUZI HUMU JF. SUBIRINI RIPOTI VILAZA NYIE.

attachment.php

attachment.php
 
Kwa kasi yenu ya kufyatua viuzi inatupa mashaka sana kila sekunde kiuzi kinazaliwa humu jf kuhusu escrow na ripoti. Mmejipanga vizuri kuupotosha umma lakini ukweli utasimama milele fedha za escrow toka escrow inaanzishwa mpaka kufungwa kwake hazijawahi kuwa fedha za umma.

Naomba unifafanulie Mkuu, maana naona labda hili jambo sijalielewa vizuri. Hivi kama hizo pesa si za umma kwa nini serikali, CAG wanahusishwa na kwa nini limepewa nafasi ya kujadiliwa Bungeni? Na kwa nini nchi wafadhili wamesitisha msaada wa bajeti mpaka jambo hili litolewe ufafanuzi?
 
Back
Top Bottom